“Date me.” Jerry akawa bado hajampata. “Mara ya mwisho tumeachana ukiniambia mimi sina tofauti na Sandra.” “Naomba unisamehe Tuma.” “Hapana Jerry. Hukukosea. Ulisema kwa kumaanisha kwa sababu nilifanya alichokuwa akikufanyia Sandra. Hutaki kurudia kosa, na mimi ndoa kwangu si kitu cha kukimbilia tu, au sifa ya siku moja nikiwa nimevaa shela, watu washangilie, na mimi niingie kwenye orodha ya wanawake walioolewa. Hapana.”
“Nimejiapia, ni bora nibakie peke yangu kuliko kuwa na ndoa ya wazazi wangu. Tafadhali date me first. Tuanzie chini kabisa tulikokukimbia. Tuanzie mahusiano ya kusomana. Sasa hivi umesema umekuwa bora, nina uhakika hutaki kurudishwa nyuma.”
“Sitaki kuwa mwiba kwako. Na sitaki uwe mwiba kwangu. Kile kilichotokea siku ile, sitataka kije kutokea tena kwenye maisha yangu. Ulinidhalilisha vibaya sana Jerry.” “Najua.” “Hapana Jerry. Hukuwa upande wangu, hukuwa nilipokuwa nimesimama mimi, ukahangaika kufanya yale yote ukiwa mgonjwa, kwa nia ya kumfurahisha mtu, halafu kuishia kufananishwa na ex aliyekuumiza kwa kiasi hicho! Hakika hujui Jerry. Ni mbaya mno.” Jerry akapoa.
“Ndio maana nakwambia, safari hii, kama kweli bado kuna mapenzi, tuchukulie hili jambo taratibu bila pressure yeyote ile. Tusomane. Mjue Tuma anavyokuwa katika kila hali, ndipo uamue kama ni mtu ambaye unataka awe kwenye maisha yako au la! Na mimi hivyohivyo. Hutaki kuwa ukirudia kuwa na ndoa mbaya kila wakati na mimi hivyohivyo Jerry. Sitaolewa ilimradi kutimiza wajibu. Hapana.”
“Nimekuelewa Tuma. Na kazi? Naomba urudi tufanye wote kazi.” “Naomba tupate muda wa kuzungumza Jerry. Safari hii tusikurupuke.” “Sawa. Nije?” Tuma akacheka taratibu.
“Sio usiku huu. Tupange wakati mwingine. Sasahivi narudi kulala.” “Hujanimiss Tuma kweli?!” Tuma akatulia. “Eti Tuma?” “Naomba safari hii tusiongozwe na mihemko Jerry. Tafadhali. Usiku mwema.” “Naomba niwe nakupata kwa simu Tuma!” “Sawa. Nitakupa namba ninayotumia sasahivi. Hii huwa naiweka kuona kama ulinikumbuka na kuniachia hata ujumbe.” Jerry akafunga macho akijilaumu ni kwa nini hakufikiria kuwa akiacha ujumbe kila anapomkosa!
“Kwamba hukuwa ukiona missed calls zangu?!” “Hata moja. Yaani sasahivi niliiweka tena kuona kama kutakuwa na ujumbe wako. Ila siitumii tena.” “Pole Tuma. Pole sana. Nilichokuwa nikihangaika ni nikusikie sauti yako pengine ingenituliza. Swala la kuandika ujumbe lilipotea kabisa kichwani mwangu.” “Usijali. Usiku mwema Jerry.”
“Nimefurahi umepokea simu yangu. Na asante kwa nafasi ingine.” Tuma akacheka taratibu. “Naomba nije kukuuguza vichomi.” “Nitakuwa sawa Jerry. Hata hivyo nimehamia mbali sana na jiji.” “Hakuna umbali nitashindwa kuendesha Tuma.” “Pumzika tu na mimi acha nirudi kulala.” “Naomba tuonane kesho.” Akatulia.
“Umeniambia niku date. Ndio nataka kukutoa kwa chakula cha mchana.” Tuma akaanza kucheka. “Au hukumaanisha?” “Sawa. Tutaonana kesho.” “Nije kukuchukua?” “Ndio date ya kwanza tu! Wewe niambie ulipo, nitakufuata.” Wakapanga sehemu nzuri ya kukutana, kabla hajakata akamuwahi. “Tafadhali nitumie namba yako mpya Tuma.” “Nitafanya hivyo. Usiku mwema.” Akakata.
~~~~~~~~~~~
Akaenda kujisaidia. Kwa furaha ya kumsikia Jerry, na kwamba anamuhitaji, yeye akarudi kulala, akasahau kumtumia namba. Ulikuwa mkesha mbaya sana kwa Jerry. Akili ikamwambia ameshampoteza tena Tuma. Akaanza kujilaumu kwa kutomuuliza hili na lile, zaidi kama bado ana mtoto wake au alishatoa mimba. “Kwa nini hata sikung’ang’ania namba ya simu!” Akazidi kujilaumu muda unakwenda, macho yapo kwenye simu.
~~~~~~~~~~~
Kwenye majira ya saa kumi na nusu alfajiri ujumbe ukaingia. ‘Hii ni namba yangu mpya. Utanipata zaidi kwa hii. Tuma.’ Hapohapo akampigia. “Mbona hulali?” “Nilisinzia, nimeamshwa na maumivu ya vichomi tena. Na wewe mbona hulali?” “Nilikuwa nikisubiria namba.” Tuma hakuamini.
“Jerry Jamani!” “Nilipaniki Tuma. Tafadhali naomba nielewe. Uliniahidi ungetuma, kisha ukapotea kama mwanzo, unafikiri ningefikiriaje?” “Si tulipanga tunakutana mchana!?” “Tulipanga mambo mengi sana mimi na wewe Tuma, lakini ulipotea na ukaendelea na maisha bila ya kugeuka nyuma.”
“Tulifika pabaya Jerry! Yote tuliyozungumza yalipoteza maana. Uliniweka kundi moja na Sandra kwa kosa la kutaka kukufurahisha! Kweli ilikuwa nibaki ili iweje wakati hata kula uliacha kula na mimi ukawa ukila ofisini kwako?” Tuma akaendelea.
“Ulinifikisha mahali nikajiona sina tofauti na maisha yale anayoishi mama yangukwenye ile ndoa yake! Yupo kama mtu baki akichungulia maisha fulani ndani! Vilikosa maana halafu nikajigundua ni mjamzito na wewe uliniambia hutaki tena watoto au huna shida na watoto kitu kama hicho!” “Nilimaanisha wale wa Sandra! Sio wako na wangu ambao mimi mwenyewe nilikuomba Tuma!”
“Siku ile ukiongea hukufafanua. Sikujua. Ilibidi nipate muda wa kujifikiria na kujipanga upya. Niambie mwenyewe Jerry, unaletaje kiumbe kisicho na hatia katikati ya mazingira kama yale, yaliyojaa hasira, vurugu, maneno makali yasiyoisha ya wewe na exwako?” Jerry kimya akiumia kuona alisababisha mtoto wake kuuwawa.
“Ile fujo mimi mwenyewe mtu mzima ilinishinda. Ilikuwa ni ngumu kukutizama hata kwa dakika mbili jinsi ulivyokuwa umejawa hasira wakati wote. Halafu kweli ulitarajia nilete kimbe katikati ya yale mazingira, kweli!?”
“Halafu eti mwisho wa yote, hangaika yote ile na kuvumilia kote kule nikidhania ipo siku utafika mwisho. Utakumbuka Sandra si mkeo. Hana nguvu tena juu yako. Unayo maamuzi yako binafsi, hakupelekeshi, nikidhania hiyo siku itakuja fika, naishia kuitwa na mimi kama yeye! Kweli?” Jerry akavuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha taratibu.
“Hapakuwa na ahadi yeyote iliyobakia tena Jerry, maana hata wewe ulifuta zako zote ulizoahidi na kuishia kunidhalilisha vibaya sana. Nilitakiwa kurudi au kukutafuta na kuzidi kukuumiza?” Akamsikia amepandisha juu.
“Basi Tuma. Basi. Nimekosa. Naomba msamaha. Kama ulivyosema, tuanze. Naomba tuanze. Nimebadilika. Hata mambo ya Sandra nimeweza kuyakabili. Nitakwambia vizuri tutakapopata nafasi.” Tuma akaanza kutulia.
“Daktari uliyemuona, alikupa dawa yeyote?” Akajaribu kubadili mazungumzo kwa kumuonyesha anamjali. “Hapana. Kwa sababu hakuona tatizo. Ila nitakwenda jumanne kwa vipimo zaidi. Nitakuona baadaye Jerry.” “Unaishi wapi?” Kimya.
“Tuma?” “Naishi mbali sana na ulipo Jerry! Tukutane kesho.” “Tafadhali niambie Tuma. Sitaweza kulala.” Huyo Tuma hakuwa eti na umbile la ajabu sanaaa. Au sura nzuri sanaa. Kwamba useme anaweza kukuchanganya unapomtizama kama Umi. Lakini usiwahi mfungulia moyo, na yeye akakukubali. Akakaa kwenye maisha yako na kuondoka! Utajua umepungukiwa tu. Kilichompata Mbaki, ndicho kinampata Jerry mwenye pesa, na warembo waliotayari kuolewa na HB Jerry wakati wowote ule, lakini anakesha akimsubiria Tuma.
“Utanivuruga zaidi ya hivi. Nihurumie Tuma.” “Sasa kwa nini na wakati unayo namba yangu ya simu, kuwa utanipata muda na wakati wowote ule!” “Ni wapi huko mbali unakoishi?” “Magogoni.” Jerry akakunja uso akijaribu kufikiria. Kimya upande wa pili.
“Magogoni ya Kigamboni?!” “Ndiko nilipata sehemu nzuri, na kwa bei nzuri. Na hakuna joto kali kama pale Kinondoni. Madirisha mapana, mwenye nyumba hajaamia bado. Ni nyumba mpya. Amenipa kwa bei ya chini nakuwa kama namlindia. Ila ameweka na mlinzi pia, anaishi na familia yake kwenye nyumba ndogo. Sio pabaya.”
Akamsikia akishukuru na geti linafunguliwa. “Jerry? Unakwenda wapi!?” “Simu ya kwanza nakupigia nilikuwa nimekaa sebuleni na viatu mguuni nilishindwa hata kutoa. Nikajua baada ya kunitumia namba, ningeenda kuoga, nilale. Ukaacha kunitumia, nikabaki nimekaa nakusubiria huku nikijilaumu kwa nini sikukuuliza unapoishi. Nikabaki nimekaa kwenye kochi nasubiria.”
“Uliponitumia namba na kupokea simu yangu, nikahamia kwenye gari nikisubiria kujua unapoishi. Sasahivi nipo njiani nakuja.” “Wapi!? Kwa nini usisubiri mpaka…” “Unataka kusikia nimefungwa kamba nipo hospitali ya vichaa kabisa ndipo utaridhika na kuona kweli nakuhitaji?” Kimya.
“Mimi nimekuwa nikikutafuta kuanzia siku ile ya birthday uliyosema nimekudhalilisha mpaka hivi sasa. Sijalala usiku kuchwa, nasubiria namba yako ya simu. Kwamba hujanielewa au unakusudia kuniadhibu tu?” Na yeye akampandishia. Tuma akashuka.
“Nyumba ipo kupita makaburini. Ni ngumu kuelezea Jerry, na sasahivi ni usiku. Nahisi amepata hiki kiwanja kwa kuuziwa na wenye viwanja wanao mzunguka kwamba wamemkatia katikati. Nyumba yake ipo katikati kweli! Inamaana inabidi mimi nitoke, nitembee umbali mrefu ili niweze kukuongoza ufike hapa.” Jerry akafikiria kwa haraka akapata wazo.
“Mwambie mlinzi akakutafutie usafiri ukulete sehemu ambayo nirahisi, kukutana sisi.” “Kwa nini usisubiri tukakutana kama tulivyopanga! Nakuahidi sitapotea tena Jerry. Na mimi nataka kukuona.” “Basi mimi nakuja, nitaegesha gari hukohuko Magogoni, utakapoamka, unitafute, sitazima simu.” Tuma akafikiria, akaona ni bora akubali yaishe.
Ukawa usiku wa hekaheka ili kupatana hao wawili. Jerry yupo Kigamboni ila hapajui Magogoni, ni usiku kunakaribia kupambazuka hana pakuuliza. Ikabidi sasa Tuma kuhangaika kumsaka huku akijaribu kuelewa alipo, mpaka akafikia alipoegesha gari yake, amekwama.
Baada Ya Mawingu Ya Ugomvi Kutoweka, Jua La Mapenzi
Lina Dalili Ya Kuwaka Tena
Akamuona wakati anatembea akifuata gari lake. Alishangaa Jerry! Tuma alishakuwa na ujauzito unaoonekana kabisa! Alionekana na afya nzuri tu, akashuka garini kwa haraka akamsogelea kwa haraka na kumkumbatia kwa muda akishindwa kumuachia. Akajikuta machozi yakimtoka.
“Na mimi nimekumiss Jerry!” Wote wakaanza kulia. Uzuri bado palikuwa ndio panapambazuka. Wakabembelezana mpaka wakatulia.
“Pole nimekufanya ukeshe kama mimi.” “Lakini nimefurahi kukuona. Nilikumiss mwenzio.” Tuma akajilalamisha. Akambusu na kumkumbatia tena. “Twende tukalale.” “Tulikubalina unanidate kwanza Jerry!” “Nitaku date kwa maisha yako yote hapa duniani, Tuma. Usiwe na wasiwasi. Twende nikakusaidie hivyo vichomi, vikitulia ulale usingizi mzuri.” “Wapi sasa!? Kwangu hakuna A/c kama kwako Jerry! Hutapapenda.”
“Wakati nasubiria namba yako ya simu baada ya kuniambia unavichomi, nimeshapata ushauri wa nini chakufanya.” Tuma akashituka sana. “Kwa nani tena?!” “Jemimi amekuwa karibu yangu kuliko mwanzo. Huwa anawasiliana na mimi mara kwa mara. Kwa hiyo nilipokuwa nikikusubiria, na yeye akanitafuta. Si unajua ni daktari?” Tuma akabaki akimwangalia.
“Acha wasiwasi wewe! Twende. Ameniambia chakufanya. Na amefurahi nimekupata.” “Tunakwenda wapi tena Jerry, jamani!?” “Kufunga kwako na kuhamia kwangu, au kufunga kwangu, nihamie kwako. Uwamuzi ni wako. Ila hutanichanganyatena Tuma.” Akabaki akimwangalia.
“Na ule utaratibu wa mwanzo, sitafanya tena.” “Upi!?” “Ule sijui ulisema huishi na mwanaume mpaka ndoa! Nahisi hata hivyo tumeshachelewa. Huna chakuepuka tena. Twende.” Akimaanisha ashashika mimba.
Akaenda upande wa abiria na kumfungulia kabisa mlango, akabaki amesimama ameduaa. Jerry amesimama mlangoni akimsubiria. “Twende tukapumzike Tuma. Tunazidi kupoteza muda ambao hatuna tena. Tunachoendelea kufanya sasahivi nikujicheleweshazaidi, na mtoto anakuja atatukuta sisi bado tunayumba, kama tusiojielewa.” Ikabidi Tuma apande.
~~~~~~~~~~~
Wakaenda mpaka kwa Tuma. “Huku kweli kufika ingekuwa ngumu.” “Njoo ukae hapa kwanza Jerry!” Akaingia na kukaa. “Ndio inakuaje?” “Tunaanza kuishi wote.” Akajibu bila ya kumumunya maneno. “Iwe hapa au kule kwangu, tunaishi wote. Ila jua kule ile nyumba iliisha, ila haina vifaa. Niliacha tuje tufanye wote kama tulivyokuwa tumekubaliana. Ile nyumba ibebe sura yetu, kasoro chumbani, nilinunua kitanda kizuri sana. Najua utakipenda. Usipokipenda, tutakiweka chumba cha wageni, kisha tununue kingine.”
“Kwa hiyo beba vitu vya muhimu hapa, ukipata nafuu, tutajipanga zaidi. Ila sasahivi twende ukapumzike. Niambie ni nini chakuweka wapi.” Akaanza kufungasha wakaondoka kurudi Masaki palipokuwa nyumbani kwa wazazi wao.
Bado Tuma alikuwa kama kwenye bumbuazi, hajui tena, na Jerry ndiye anayeongoza mambo. Akamuingizia mizigo yake ndani, yeye amesimama ameduaa. Alipomaliza kila kitu akamfuata hapo alipokuwa amesimama sebuleni. “Twende ukaoge, nikusaidie ulale.” Akiwa bafuni, akashangaa na yeye ameingia. Akampisha majini, akaingia, akabaki pembeni akijisugua taratibu.
“Nimekumiss Tuma! Nimekumiss vile ulivyokuwa ukinishika na kunichezea, mpaka nilirukwa na akili.” Akainama mtoto wa kike na kumshugulikia vilivyo. Alipiga kelele akikojoa huyo Jerry kama mtoto wa kike.
“Mbona hujataka tuhamie kitandani?” “Ninamaumivu Jerry! Nikikaa sitamani kuamka. Na nikiamka napata maumivu makali sana.” “Basi lazima turudi kwa daktari wa wakina mama.” “Sasahivi natamani kulala tu.” “Nitakubembeleza utalala tu. Na asante. Nilikuwa na hali mbaya!” Tuma akaanza kumcheka vile alivyokuwa akipiga kelele hapo bafuni. Alikuwa akimchanganya Mbaki hivyohivyo. Alijua kuwachezea hao wanaume, nakuwafanya wawe kama wehu, wanaenda na kurudi wakimkumbuka yeye.
Kila alivyokuwa akimwangalia tena, anacheka. “Sawa Tuma!” Tuma akamaliza na kutoka.
~~~~~~~~~~~
Akaliweka taulo kwenye maji ya vuguvugu wakati akimpaka mafuta kuzunguka tumbo lake. “Jemimi anasema itakusaidia pia ujauzito usikuache na michirizi.” Akaendelea kummasaji kuzunguka tumbo zima. Ile hali tu ya kusikia mikono ya Jerry kwenye Tumbo, akaanza kupatwa hamu.
Akamuona anakaa na kuanza kumkiss, Jerry akamcheka moyoni ila akimpa ushirikiano. Ananyonya midomo yake huku mkono ukimchezea, akalegea mpaka akawa anajilaza. Hakumuachia. Wakaendelea kupeana midomo huku akilala. Akajilaza pembeni yake, ananyonya midomo yake huku akiongeza nguvu kwenye kisimi, Tuma anamwaga ute kwa hamu zote, naye Jerry akawa anapambana na ule utelezi.
Alionekana hata yeye alikuwa na hamu ya kupitiliza. Aliendelea kwa muda kumsugua na vidole viwili mpaka na yeye Tuma akamwaga, na ndipo akamuachia midomo akitafuta pumzi.
“Nina hamu na wewe Tuma! Nataka lilipate hilo joto. Na umemwaga ute wa kunitosha kabisa.” “Nyanyua miguu uendelee.” Alifurahi Jerry, hakutegemea. Akamuwahi kwa haraka sana. Akabeba miguu begani na kumvutia juu. Bwana Jerry alijifaidia! Tena taratibu. Akabaki akijifuta machozi. Kajoto kamimba! Halafu Tuma mwenyewe akawa ananogewa! Acha amsugue kwa utamu, kisha akamgeuza, akitaka kumuinamisha.
Akamvuta na mkono akaurudisha mbele kwenye kisimi. Akawa akimchezea taratibu kumpa na yeye raha, asikauke na kumuumiza zaidi, huku akiingia na kutoka. Tuma alikuwa akisikia raha anavyochezewa! Akasahau maswala la vichomi. Taratibuuuu, Jerry akigugumia raha mpaka akahitimisha. Alipomaliza tu, Tuma akajitupa pembeni.
“Nakufuta hapohapo, lala.” “Bora. Ninausingizi!” “Lala. Nakusafisha, halafu nitakuwekea na tauli la vuguvugu ili kutuliza misuli.” Mtoto akaanza kucheza. Alifurahi Jerry. Akaanza kucheza naye.
“Basi mimi sitalala Jerry, jamani! Ni nini?” Alijawa na furaha huyo na kumshangaza Tuma kwa mtoto wa tatu! Hakutegemea. Akatulia tu akimwangalia mpaka mtoto akatulia ndipo akamuwekea sasa hilo taulo. Tuma alilala asijue alipo. Na kile kiubaridi! Hakuna kujipepea! Uchovu wa mchezo mfupi lakini mtamu! Ukame ukakaushwa kwa taratibuuu! Hapo roho shwariii. Alilala nusu mfu.
~~~~~~~~~~~
Simu yake ikawatoa usingizini. Tuma akatoka kwenda kujisaidia, alikuwa JJ. “Najua upo na Tuma.” Akajua Jemimi ameshatangaza. Kaka yake akaendelea. “Lakini usisahau jioni hii tunakutana wote.” “Ni kama anavichomi! Siwezi kumuacha.” “Kama sio vibaya sana, mwambie tungependa kumuona.” “Kwamba na yeye anakaribishwa?!” “Kabisa. Na safari hii nenda umbali mrefu zaidi kumuonyesha unamaanisha. Mkaribishe nyumbani.” “Asante.” Simu ikakatwa, Jerry akabaki akifikiria na simu mkononi.
~~~~~~~~~~~
Tuma akarudi na kumkuta ametulia kama anayewaza kitu kilichomfurahisha. “Umefurahishwa na nini huko mawazoni?” Akamuuliza akirudi kujilaza. “Bro alianzisha utaratibu wa kukutana familia zote kila mwisho wa mwezi. Inakuwa siku maalumu, hakuna kukosa. Alijilaumu sana kutokujua kama uliondoka, na kuniacha peke yangu, mpaka kuugua kwa kiasi kile. Yaani anajilaumu mpaka leo.”
“Ndio ilikuwa mbaya hivyo!?” “Acha Tuma.” Akamuelezea mengi, na yeye akamwambia mengi ya tokea wanaachana. Wakabaki wametulia kitandani wakipapasana.
“Njaa inauma Jerry!” “Usiharibu njaa. Tuoge twende kwa JJ. Mkewe huwa anaandaa vitu vizuri sana. Utakula mpaka uchoke.” “Kama sipo tayari kukutana nao!” “Kwa nini!?” Akashangaa mpaka akakaa kabisa.
“Naomba sisi tuwe sawa kwanza Jerry! Tunaharakisha sana!” “Sasa hapa tulipo sasahivi, unataka tufanye nini na mtoto anakuja?” “Sijui Jerry! Naomba tutulie sisi kwanza. Ndio tumepatana tu leo!” “Tafadhali naomba nisindikize Tuma. Maana mimi nilazimaniende, na siwezi kukuacha.” Akaanza kulalamika.
“Yaani kwetu, mimi ndio ni kama nina mkosi wa mahusiano aisee! Wenzangu wanawake na familia zinazoeleweka, mimi nimekuwa kama nimekwama, au kama kijana mdogo! Sasa sijui ni mkosi au nini, hakika mimi sijielewi na sijui natakiwa kufanya nini tena.” “Mimi naomba twende Jerry. Na nia haikuwa mbaya, wala kukurudisha nyuma. Nilitaka…” Akafikiria, akasita.
~~~~~~~~~~~
Ila ukweli ni kama alikuwa akiona aibu kutokana na aliyoyasikia alivyotafutwa alipoondoka, mpaka Jerry kuugua! Halafu alishajua jinsi JJ anavyopenda wadogo zake! Akahofia na lawama pia. Alitamani kama aanze kukutana na mama J, kwanza. Angalau ajue wanaposimamia. Ajirudi taratibu sio kutokea na tumbo mbele yao! Ila vile Jerry alivyoanza kulalamika, akaona asizidi kumuumiza.
~~~~~~~~~~~
Akatoka hapo chumbani kuelekea wanapoweka nguo, Jerry akamfuata. “Usione kama nakulazimishia.” “Wewe nilazimishe tu. Mimi sina neno.” Jerry mwenyewe akaanza kucheka. Tuma akiendelea kusaka nguo.
“Unacheka nini sasa, na uvae uache kunitamanisha.” Alicheka Jerry mpaka akakaa. “Usiniambie nakutamanisha.” “Vaa bwana!” Akamsogelea karibu kusudi tu amchezee. Naye Tuma uvivu wa mapenzi, alinyimwa. Hapohapo akaanza kumchezea kwenye hicho chumba chao cha nguo. Jerry akasuuzwa roho na penzi ambalo hakutegemea.
Ndipo akaanza kujiandaa. Kila nguo aliilalamikia Jerry. “Hiyo ndio kabisa! Mpira mtupu huo Tuma.” “Basi tafuta wewe.” Akahangaika hapo kwenye mzigo wa Tuma akakwama. “Hakika hakuna chakuvaa hapa.” Tuma kimya akijua anavyothamini mavazi huyo na ndugu zake.
Akaendelea kujitengeneza akimsikiliza anavyozisema nguo zake huku akichambua. Mwishoe akachagua moja. “Ni hivyo hamna namna.” Hakumbishia wala kuongeza, akavaa, akahakikisha anapendeza tu, wakatoka kuelekea kwa JJ. Ilikuwa ni jioni hata giza halijaingia. Yaani huyo Jerry, ukimwangalia tu usoni, utajua kuna jambo jema linaloendelea nafsini mwake.
~~~~~~~~~~~
Tuma alikuwa akishangaa hapo nje kwa JJ, mpaka Jerry akamvuta. “Sasa kama hapa nje ndio unashangaa hivi, basi huko ndani utatia aibu.” Tuma akaanza kucheka. “Kwamba pazuri zaidi?!” “Nina uhakika kwa asilimia nyingi sana. Mimi niliyetembea nje na ndani ya hii nchi, hujaona mahali pazuri kama hapo ndani.”
“JJ na mkewe wanapenda vitu nadhifu sana. Na huwa hapazoeleki maana mkewe anabadili mara kwa mara mpaka rangi za ukuta na thamani zake. Sisi wenyewe kila siku tunapaona kupya. Maana unaweza kuta kochi lilipokuwa jana si leo. Ila sasa usiende ukashangaa kwa staili hii.” Tuma hana mbavu akikumbuka alivyoambiwa na mama J.
“Basi nipige picha hapa nje kwenye maua.” Akachuma kabisa ua. Jerry alishangaa, kama ameona nyoka. “Sasa unashangaa nini?” “Sijajua kama ndio unaushamba wa kiasi hicho chakupiga picha kwenye maua!” Bwana Tuma alicheka mpaka akakaa chini.
“Ushamba gani huo Tuma wewe! Acha bwana, twende ndani.” Tuma anazidi kucheka vile alivyomshangaa kwa wazi kabisa. “Na ujue hii nyumba kila kona ina kamera, hivi humo ndani watakuwa wanakuona unavyoshangaa hapa.” Tuma akasimama kwa haraka.
“Acha bwana Jerry!” “Hakika sikuongopei. Hapo washaona mpaka uchumaji wako wa maua.” Tuma akalitupa kwa nyuma. “Hata hivyo wameona.” “Acha kunitisha bwana! Nimelitupa kwa nyuma.” “Nimekwambia kila kona kuna kamera. Huna unachokifanya hapa, wasijue ndani.” “Jerry wewe mtu mbaya jamani! Umesubiri nimeingia aibu ndio unaniambia!” Jerry akaanza kumcheka alivyopoa.
“Hutaki tena picha?” “Akuu!” Akakataa kabisa na mabega. Jerry alicheka mpaka machozi, akatoa simu yake. Akaokota hilo ua kwa haraka na kuliweka kwenye pochi.
“Huo sasa wizi. Wanajua unaiba maua yao.” “Mungu wangu ni kweli!” Jerry hana mbavu. Akalitoa kwenye pochi na kumuwekea kwenye mfuko wake wa suruali. Jerry akatoa mfukoni kwake akicheka akawa anamrudishia. “Mimi nataka kukupiga picha na ua bwana!” “Acha bwana Jerry! Watu wote watajua kweli mimi mshamba.”
Mara akatoka kijana anafanana na JJ haswa. Akaanza kutaja namba ya simu ya Tuma kwa kichwa. “Nyie jamani!” Tuma akashangaa sana akimwangalia Jerry. “Hakuna kiumbe kwenye hii familia asiyejua hiyo namba.” “Ilikuwa shuguli ya ukoo mzima!” Akatoka mke wa JJ na kuongeza kwa kijana wake, na kumfanya Tuma acheke mpaka kufunika uso.
“Aibu zako mwanamke!” Alikuwa mama J. “Ni Jerry huyo!” “Aliyefanya nini?” Mama J akaendelea kumuuliza yeye akicheka nyuma ya Jerry amejificha. “Kumbe wewe mpenzi wa maua?” Alikuwa JJ na yeye ametoka. “Hana upenzi wowote, ushamba tu.” Tuma hana mbavu.
“Kwa hiyo kweli eti nyinyi humo ndani mmeniona nikichuma ua?” Wakawa na wao wanacheka. “Mshamba huyu! Eti alikuwa akitaka nimpige picha na hili ua hapa nje kwenu.” Wakazidi kucheka. “Nyie ujue ilitakiwa kuwa siri Jerry wewe! Lakini kwani eti nyinyi kwani mmeshawahi ona nyumba nzuri hivi!” Mpaka Jeremi akacheka kwa sauti.
“Sikukwambia hapa utatia aibu wewe! Ona sasa.” Mama J hana mbavu. “Tumaaa!” “Ni pazuri sana bwana!” “Kwa hiyo ukataka kupigwa picha bustanini?” Hilo swali la mama J likafanya wazidi kucheka. “Ni moja tu!” Watu hawana mbavu jinsi alivyojibu kwa upole.
“Njoo Tuma nikupige picha utakazo. Ila kwa simu yangu ili na Jemimi naye akuone, apumzike.” “Nyie jamani!” “Halikuwa jambo dogo! Mtoto unatafutwa na kila mtu!” “Mimi naona mnisamehe tu, halafu mnipige picha.” Walicheka, hawana mbavu. “Mama kakazania picha kwa watu huyu! Aibu gani hii!” “Ni hivyo mimi mgeni jamani! Mwenzenu sijawahi kufika sehemu kama hizi.” Walikuwa wakicheka hao!
Maana wao walikuwa na ustaarabu fulani hivi. Kunyamazia mambo fulanifulani, hata kama yanawashangaza. Halafu huyo JJ walikuwa wakimuheshimu sana. Utani mwingi hakuna. Sasa wakakutana na Tuma amekuja na kicheko. Akawachangamsha.
“Ngoja nimpige hiyo picha roho yake itulie.” “Ila sasa sio hapa kila mtu akiniangalia na wewe Jerry!” Wakazidi kucheka wasiamini. “Huna utakapokwenda kuzunguka hii nyumba, usionekane mama.” JJ akaongeza. “Basi baadaye.” “Kwamba ulikuwa na mapozi yako hutaki tuyaone?” Hilda akamuuliza. Akakubali kwa kichwa akicheka.
“Basi tupige ya familia. Wote. Nenda kawaite wadogo zako.” JJ akimaanisha watoto wa Jeremi. Mtoto wao huyo mkubwa akaingia ndani kuwaita. “Si umeona tutatapata picha ya ukumbusho!” “Hapana bwana, wewe umetia tu aibu.” Jerry akafanya waanze kucheka upya. “Na ua ulilotupa, ukaokota, ukalitia kwenye pochi, kisha kuliweka kwenye suruali ya Jerry pia wamekuona.” “Nyie kumbe kweli! Hii kweli aibu.” Wakapata wakati mzuri hapo nje hata hawajaingia ndani. Wakapiga picha kweli. Wakiwa kwenye ile hali ya picha akaona ajiwahi.
~~~~~~~~~~~
“Naomba mnisamehe kwa kuwasumbua. Mimi nilijua Jerry asingejali!” “Nakwambia namba yako ya simu tumeishika kwa kichwa, mpaka kina dada wa humu ndani wanaijua. Ilikuwa kazi ya kukupigia mchana na usiku.” “Poleni sana jamani. Na mnisamehe. Na mimi nilikuwa nikiiweka mara moja moja kuangalia kama angalau Jerry alinikumbuka hata akanitumia ujumbe!” Ndio kila mmoja kufunguka akili.
“Hivi ni kwa nini hakuna aliyekumbuka hilo!” Wakaanza kuulizana. “Mimi nilikuwa nataka kumsikia tu, hata ujumbe haukuwa mawazoni.” Akajibu Jerry. “Sasa na mimi nilivyokuwa nikimkosa kwenye simu, basi, nikajua kweli nilimuumiza kiasi hataki kuniona tena.” “Pole mama. Tumefurahi umerudi, naona hata sura ya Jerry imebadilika kabisa!” Kaka yake akamtania. “Jerry anacheka bwana!” Jeremi akaongeza akiendelea kumtania. “Acha hizo wewe!” Wakazidi kucheka. Wakimwangalia Jerry.
~~~~~~~~~~~
“Hongera Tuma. Naona umependeza!” Alikuwa mke wa JJ. “Asante.” Akajibu akicheka akimwangalia Jerry. “Ila Jemimi ameniambia unavichomi vinakusumbua. Umemuona daktari?” “Nilikwenda kumuona daktari wa kawaida tu, akasema hajaona tatizo, akanishauri nikamuone daktari wa wakina mama. Ndio nikaona nisubirie siku ya jumanne kwenye kliniki yangu, maana kumpata huyo ni shida!” “Unamuona nani? Alipomtaja wote wakawa wanamfahamu.
“Ni daktari mzuri sana kwa kina mama. Tutajaribu kuona kama anaweza kukuona kesho, ili usikae na maumivu muda mrefu. Umeshajua jinsia?” Kabla hajamjibu akashangaa wote wanacheka huku wakimwangalia mama J.
~~~~~~~~~~~
“Au na wewe unataka surprise?” “Surprise za Hilda bwana!” Mumewe akafanya wazidi kucheka. “Anaweza kuwatia shuguli, anajidai hataki kujua jinsia. Sasa mimi na Jemimi kila wakati huwa tunamwambia, angalia tu tujue jinsia uturahisishie manunuzi. Anakuwa mbishi weee! Mwishoe JJ anaingilia kati, tumuache. Mnanunua kila kitu cheupe, maana si hatujui jinsia!” Wakaanza kucheka vile alivyoanza kutingisha kichwa mke wa JJ kabla hajaendelea.
“Sasa acha vimcharuke. Anataka kumjua mtoto wake, na hawezi kusubiri. Hapo dada huyu analia kabisa, Jemimi akamtafutie mahali, ajue mtoto wake.” Hilda hana mbavu. “Namsaka sasa JJ aliyemuunga mkono, namwambia mwenzio amebadili mawazo anataka kujua alichobeba, hawezi kusubiri na appointment za huko nchi za watu ni za kusubiri. Kazi inabakia kwangu na Jemimi. Anatulaumu eti kwa nini mwanzo tulimsikiliza!” Hapo mpaka Tuma akaanza kucheka.
“Mama mtoto analia, anataka kumjua mtoto wake, siku aliyoipata haifiki.” “Mkafanyaje sasa?” “Ikabidi kumuita mumewe. Mke hanyamazi.” “Nyie mama J!?” “Ni zile homoni za mimba na wewe Tuma akili inakuwa haikai vizuri, unalizwa na kila jambo!” Bwana walikuwa wakicheka.
“Kwahiyo?” “Ndio mumewe akaja sasa, na mama yake maana hapo tena mimi na Jemimi tushakuwa wabaya, hatumshauri vizuri.” Wakazidi kucheka. “Halafu JJ sasa alivyo, akawa anamkwepa kabisa ili na yeye asilaumiwe, ametuachia mimi na Jemimi.”
“Na usifikiri ni mtoto wa kwanza tu, na wapili hivyohivyo. Tukamkumbusha alichotufanyia kwa mtoto wa kwanza, akajidai oooh, ule ulikuwa ugeni wa mimba, ashakuwa mzoefu, mtoto ni mtoto.” “Akaja kubadilika tena?” “Vibaya sana, ila uzuri safari hii wabaya tukawa wengi mpaka mumewe.” Bwana walikuwa wanacheka.
“Nikamwambia, akiongeza watatu, atake asitake, tutamjua jinsia. Hapo anacheka mbavu hana, kama mazuri! Sasa wewe mwenzetu ni vipi?”
~~~~~~~~~~~
“Mimi vya surprise siviwezi.” Wote wakacheka. “Halafu Eli aliyekuwa akinihangaikia mambo ya hospitalini na afya yangu alivyokuwa na kiherehere huyo! Yeye ndio akataka kujua wa kwanza! Kwa hiyo kabla ya kuondoka, mama alivyokuja tukaenda wote kumuangalia. Wakataka kumpa jina, nikawaambia namsubiria Jerry.” Ikamgusa sana Jerry.
“Nashukuru japo sikuwa hata na wazo la kukuuliza. Yaani kichwani eti najua ni mtoto tu wakiume tu. Si ndivyo?” Tuma akaanza kucheka. “Si ni wa kiume!?” Hapo akamfanya Jerry kuhamasika zaidi. “Wakike bwana.” Aisee walifurahi sana. Sana mpaka wakamshangaza Tuma.
“Huku kwetu tunauhaba wa watoto wa kike, Tuma. Ni Jemimi tu alipatikana kama kuokotwa kwa lulu, basi. Kila mtu anamdekeza Jemimi, hatutaki akue.” Alikuwa mtoto mkubwa wa JJ. Wakacheka. “Na anavyopenda kupendwa Jemimi!” Akaongeza mama J na kufanya wacheke.
“Hongera sana mama. Hongera sana. Karibu ndani.” “Aisee nimefurahi! Nampa jina la mama. Jemma.” Jerry akafanya wote wamuangalie. “Precious stone.” Kaka yao akatoa tafasiri ya hilo jina Jemma, akionekana amefurahia sana. “Asante Jerry. Nimefurahi sana. Mimi nilisema kama ningepata mtoto mwingine tena, akawa wakike, ningemuita Jemma.” Hilda akamtizama mumewe. “Mbona hukuwahi niambia?!” “Sikutaka kukuwekea pressure.Nimefurahi sana. Mungu amkuze awe mwema kama mama.” Jeremi akaonekana kuguswa haswa.
“Mama yetu alikuwa na upendo sana.” “Sana.” JJ akaongeza kwa Jeremi. “Hilo jina la mama J unaloniita mimi, basi ujue lilikuwa jina la mama yao. Alikuwa mtulivu, ametulia haswa wakati wote na tabasamu, na upendo mno. Huwezi kufika kwake asikulishe. Mpaka kaka zangu walikuwa wanapenda kuja kwao hawa.” Akaongeza Hilda. “Kwa ajili ya chakula?” Tuma akafanya wacheke.
“Nakwambia kwa mama J kulikuwa kunaliwa muda na wakati wowote ukipita. Hiyo ni moja ya sifa aliacha. Kaka zangu walikuwa wakitaniana eti wakizurula mjini, njaa zikawauma, kwetu ilikuwa mbali, kwa mama J ni hapo Masaki, basi wanaambiana wakati wanasubiria foleni, wanapita kumsalimia mama J. Kumbe kufuata msosi tu.” Wakawa wakicheka.
“Basi tumtamkie baraka mama yangu mkwe. Akiwa huko tumboni, na akizaliwa. Mema matupu ndio yamfuate. Tunafuta mabaya yote, na yale mema aliyoyakosa wajina wake, apewe yeye yote. Upendo na ukarimu vikawe sehemu yake. Tuombeni.” Yaani hapohapo wote wakashikana mikono nakufanya maombi kama alivyoshauri mke wa JJ yeye mwenyewe akiongoza.
~~~~~~~~~~~
Wakapata wakati mzuri sana. Wakamkaribisha ndani na kumkarimu Tuma vilivyo. Jemimi naye akapiga simu na kusalimiana na Tuma kama anayemfahamu. Wakapata wakati mzuri wakicheka kwa hili na lile wakizidi kufahamiana.
~~~~~~~~~~~
“Sasa Tuma, mama, naomba utuulizie taratibu za mahari.” Akashituka Tuma, hakutegemea. “Au nyinyi mlipanga nini?” Ikabidi JJ aulize akidhani amekosea. “Kuna kitu tulipanga na Jerry.” Wote wakamgeukia Jerry, akabaki akimwangalia Tuma kwa kumsuta.
“Kitu gani?” “Muulize Tuma, mwenyewe.” “Ungesema tu Jerry! Au umesahau?” “Mimi nataka ukirudie hapa, ili na wewe mwenyewe ukisikie vizuri, halafu uone kinavyosikika.” “Nyie Jerry jamani! Mbona kama nahisi unanigeuka!” “Wewe sema ule mpango wako.” Mwenyewe Tuma akaanza kucheka.
“Mimi naona Jerry anisaidie tu.” “Hakika utasema mwenyewe ule mpango wako, wala si wangu. Sema na wewe ukiwa unajisikiliza.” “Ni nini mama?” JJ akamuuliza kwa upendo. “Tulikubaliana..” “Hapana Tuma. Sema vizuri. Usiongeze neno.” “Kwani hatukukubaliana?!” “Hapana. Ila wewe ndio ulitoa wazo. Sasa liseme hapa ili mpaka Hilda akusikie.” “Unanifanya mpaka nishindwe kusema wakati ni jambo la msingi.” “Si ndio useme sasa kama kweli ni la msingi?” Mama J akadakia.
Akacheka na kuanza kufikiria akiangalia chini. Akaanza kwa hofu. “Mimi hapa nilibahatika nyumba ya kupanga kule Kigamboni. Ndio nikasema…” Akawatizama wote wanamuangalia, akaanza kucheka na kufanya waanze kucheka.
“Ona yanavyokuchekesha wewe mwenyewe!” Jerry akafanya wazidi kucheka ila na maswali. “Sema tu mama, usiogope.” JJ akamtia moyo kutaka kumsikia. “Ndio mimi nikatoa ushauri. Kutokana na matatizo yaliyotokea, nikamkosea vile vyakufanya jambo alilokuwa ameshanikataza. Nikasema kuliko kuharakisha kama mwanzo, pengine anidatekwanza.” Bwana walicheka hapo. Walicheka sana.
“Nyie jamani! Mjue ni wazo zuri sana! Ni ili ajue anaoa mke wa namna gani asirudie tena kosa!” Wakazidi kumcheka. “Labda tuanze taratibu. Mmefikia wapi kwenye hilo wazo?” Akauliza mke wa JJ. Tuma akawa hajaelewa mpaka akamtizama na Jerry kutaka amueleweshe lakini akabaki akimtizama na yeye, kisha akarudisha macho kwa mkewe JJ.
“Labda niweke swali langu vizuri. Sasahivi hapa, mmetokea nyumba gani?” Bwana Tuma alicheka. Alicheka mpaka akaondoka hapo akikimbia. Wakapata jibu na kufanya wacheke sana.
“Sasa huko unakokimbilia ni chumbani kwa mama mwenye nyumba.” Jerry akamfanyia kusudi. Akasimama. Akarudi kwa haraka. “Ila ni Jerry. Jerry hafuati ushauriwangu. Ila mjue kabisa, nilirudi na mipango mizuri sana. Nilikuwa nimejipanga. Nikamwambia Jerry kwenye simu, akawa ananiitikia vizuri tu. Eti tunakutana, ndio akanigomea! Ila sio mimi.” Wakazidi kucheka, Jerry akimtizama.
“Mimi naona ombi langu libakie palepale.” “Utaratibu wa mahari?” Hilda akamuuliza JJ akicheka sana. “Kabisa mama. Wote tutaonekana wahuni. Tunakaa na binti ya watu kimyakimya! Hapana Tuma. Wakati nyinyi mnaendelea na huko kudate, sisi tukalipe mahari.” Alicheka Tuma mpaka akaweka mto usoni.
“Waendelee kudate tu, ila wewe unakwenda kulipa mahari?” Kijana wake akauliza kishabiki akicheka na yeye. “Kabisa. Tutakuja tia aibu zaidi. Wazazi watuone sisi wote ni matapeli tu.”
“Halafu kweli nyinyi mnataka kuniponza. Mnataka huyo mama mzazi aje hapa duniani anikute naendesha familia kihasara hivi! Anakuja kukutana na maisha ya ndoa isiyo takatifu! Nitamuangusha sana mama yangu. Ataona sifai kabisa!”
“Nataka siku anakuja hapa duniani, akute tumejipanga kila kitu kipo sawa, tena kwa ufanisi. Anaishi kwenye nyumba yenye ndoa takatifu, na nyinyi mnakwenda kanisani, kwamba mmerudishwa kundini. Wakristo mnao eleweka” Ikamgusa kila mtu hapo jinsi JJ alivyoichukulia kwa uzito. Wote wakajua amefurahia sana huyo mtoto kuitwa jina la mama yao.
“Nitazungumza na mama, kisha nitamwambia mama J, utaratibu mzima.” “Hapo utakuwa umefanya vizuri.” “Nimefurahi!” Tuma akafanya wacheke tena. “Hutaki kudatetena?” “Mimi naona tufanye kama alivyosema Jerry tu. Tuendelee kudate mpaka kifo.” Basi kukawa na kucheka. Tuma waliyekuwa wakimsaka, amerudi na kicheko. Akaleta tumaini jipya kwenye familia yao.
~~~~~~~~~~~
Mke wa JJ huenda na upepo. Alipoona mumewe amefurahia sana mtoto wa Tuma, akabebea bango. Ilimradi tu kumfurahisha mumewe. Jumanne haikuwa mbali, lakini akahangaika mpaka akapata nafasi ya Tuma kuonwa siku ya jumatatu. Akawapigia simu usiku wakiwa wanakaribia kulala.
“Kesho saa nne, anaweza kumuona Tuma. Sio kwa kliniki ya kawaida, ila kwa hivyo vichomi ili tujue ni kupanuka tu kwa tumbo au kama kunatatizo jingine.” “Nakushukuru sana. Nitamwambia Tuma.” “Naweza kumsindikiza kama wewe utakuwa umetingwa.” “Ningependa kuwepo. Nahisi nimeshapitwa sana.” Wakacheka.
“JJ, anaomba picha za kwenye ultrasound.” “Kwani umepata na ultrasound kabisa?” “Lazima Jerry. Hata Jemimi amesema aangaliwe vizuri tujue tatizo ni nini. Kwa hiyo tumezungumza na daktari nikiwa na Jemimi. Wameshauriana. Amesema atamuona na ndipo atafanyiwa ultrasound. Ataisoma kesho hiyohiyo kisha atatupa majibu.” Jerry akafurahi sana.
“Kwamba kesho nitamuona kabisa!” “Sasa usitunyime picha, za mama mkwe.” Jerry alicheka sana. “Nitahakikisha kesho hiyohiyo wote mnapata. Asante sana shemeji yangu kwa kutuhangaikia na nitamshukuru na Jemimi.” Wakataniana kidogo, na kuagana. Akampa taarifa Tuma. Yaani aliweza muona jinsi alivyofurahi. Na huyo Jemimi ikawa ndio daktari wa familia nzima. Kila tatizo la afya, wanaanza naye yeye ndipo wanatafuta daktari.
Jumatatu.
Kesho yake wakawahi muda mzuri tu kwa huyo daktari. Alikuwa na kliniki sehemu ingine, siko anakomuona Tuma kwenye kliniki zake za kawaida. Akamwangalia kwa umakini. Akafanyiwa vipimo vingine na ndipo wakaenda sasa kwenye kliniki ya ultrasound.
~~~~~~~~~~~
Wakiwa wanasubiri simu ya Jerry ikaanza kuita. Akamuona ameshangaa sana, na kupokea. “Kwema?” Ndilo swali alilomsikia akiuliza wakati akisimama na kutoka hapo walipokuwa wamekaa. Akasikiliza kwa muda, akamsikia akijibu, “Sawa. Asante kwa taarifa.” Akarudi kukaa akiwa ametulia sivyo alivyokuwa. Tuma akamuacha. Akabaki akiwaza yake na kupotelea mawazoni.
Akahisi amejishuku, maana akajirudi kwa haraka, lakini tayari yeye akawa amebakia kwenye ile simu. Amepoa. Akaongea hili na lile, Tuma akimsikiliza mpaka walivyoitwa. Haikuchukua muda mrefu tokea wafike hapo na kuingia kwenye vipimo.
Wakamwangalia mtoto mpaka wakachoka. Akaridhika kweli ni wakike. Akataka atolewe picha tatu, na video akawa amechukua. Hapohapo akawarushia hiyo video ndugu zake. JJ na Jeremi. Hapohapo JJ akapiga wakati Tuma akivaa.
Akamuona jinsi alivyobadilika tena, amejawa furaha ya ajabu. Anacheka kweli na kaka yake. Tuma mawazo yamebakia kwenye simu iliyombadili mudi kisha kujirudi. “Atakuwa ni Sandra tu.” Akabakia akiwaza huku akiendelea kuvaa, na Jerry kumsaidia huku anazungumza kwenye simu na JJ kisha Jeremi akajiunga. Vicheko mpaka kwa sauti ya juu kabisa wakimzungumzia huyo mtoto.
~~~~~~~~~~~
Ni nani na nini tena kimebadili mudi ya Jerry na kujirudi kama aliyekumbuka Tuma ndio amerudi tu, hataki kuharibu tena.
Ndoa ya Jerry iliisha kwenye makaratasi, lakini amemuacha Sandra na vijana wake wawili. Hata kama mtoto akinyea mkono, huukati.
Yapi tena yamejiri na je Safari hii Sandra atarudi kwa staili ipi?
Tuma atahimili vishindo?
Inaendelea..
0 Comments:
Post a Comment