Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Love At First Sight - Sehemu ya 89. - Naomi Simulizi

Love At First Sight - Sehemu ya 89.

 Alifika kumchukua mida ya saa moja kamili asubuhi, akamkuta Tuma yupo tayari. Akatoka na kijikapu kidogo. Eti akashuka kabisa kumpokea. “Sio nzito!” “Najua umepika, acha na mimi nisaidie hata kusogeza.” Akampokea na kupanga garini ndipo akaondoa gari. “Ulilala muda wa kutosha kweli? Mbona kama umepika sana?” “Ukiona, utafurahi. Na sio vingi, vitu vyepesi tu. Na wewe ulilala salama?” “Hata sielewi kama nililala au la! Kichwa kina mambo mengi sasahivi.” “Pole.” Akamwangalia akiendelea kuendesha.

Wakatulia tu hapo garini mpaka kazini. Kama kawaida Tuma akaanza usafi, alipopaweka hapo sawa ndipo wakaa kula na kuendelea na siku. 

Saa mbili na nusu mama J akaingia. “Bora umekuja. Mimi nahamia stoo. Ukinitaka, nitakuwa kule.” “Napita tu. Nitarudi saa sita na nusu.” Akamsikia akimuaga mama J na mama J naye akimuaga. “Basi hapo ndani kila kitu kipo sawa, na maandazi yapo. Kula kabla hujaondoka.” Kisha akaondoka. Jerry alikuwa ofisini.

“Ndio jumamosi kuna kuaga busy hivi!” Jerry akatoka kumfuata jikoni. “Sana, na Tuma anapawezea. Asipokuwa huko wale mafundi wote wanahamia huku na kulalamikakwa kila jambo. Lakini akiwa nao kule, panatulia kabisa.”

Historia Ya Mbaki&Tuma

Alishajipanga jinsi ya kumuuliza. “Na anawahi!” Akatupia sifa kiuchochozi ili kumchota Hilda. “Si hilo tu. Sifa zote anazo. Akiwa kule jua hutapoteza pesa, na weekenditaisha kwa utulivu. Ananidhamu ya kazi, si mbishi, anajituma mwenyewe, amejitoa hapa kama kwake! Hataki jambo liharibike hapa. Atafanya juu chini, siku ya kazi ifanyike na iishe kwa utulivu mpaka kwa wale vijana kule. Namtunza Tuma kama mboni ya jicholangu.” Akacheka taratibu kuzidi kumchota. 

“Hana familia?” Akajidai kama hajui. “Anaishi na mdogo wake. Lakini…” Akamuona anacheka kama anayefikiria. “Nini?” “Kuna kijana anaitwa Mbaki. Ni wale vijana walibahatika, nafikiri na akili nzuri anayo, akamaliza tu chuo na kuajiria bodi ya mikopo ya vyuo. Ana cheo kikubwa tu na pesa. Wanasumbuana na Tuma, mimi na Jeremi tunaambia mwisho watakuja kuoana tu.” Akaanza kumvuruga.

“Maana wana historia ya muda mrefu na Tuma! Tokea Tuma anasoma chuo kikuu kile cha Dodoma, mwaka wa kwanza tu akakutana naye huyo Mbaki. kaTuma ni kazuri sana. Ila uwe umetulia na akupe muda wake. Yaani na yeye awe ametulia, ukamwangalia vizuri, utagundua ana uzuri fulani hivi! Halafu kwa haiba yake ni mtulivu sana. Sio muhuni wala hana tamaa. Nafikiri Mbaki alipomgundua kama ni lulu ya kutunza, akambana kuanzia wakati huo. Na kuhakikisha wapo kwenye mahusiano yale ya mpaka kwa wazazi wajulikane kuwa wapo pamoja, ili asije zidiwa mahesabu na wanaume wengine.”

 “Mbaki anaishi Dar, Tuma alikuwa akisoma Dom lakini wenyewe kila weekendwapo pamoja. Kwahiyo Tuma akawa anajulikana mpaka kwa kina Mbaki, hapa Dar. Mbaki ametokea kwenye familia fulani hivi, zile zenye uwezo. Na yeye akafahamika mpaka kwa kina Tuma huko kijijini. Vikawa vimekuwa serious, Tuma akamaliza shule mipango ya harusi ikaanza.”

“Haya, huku na kule Mbaki si akakutana na mapepe Umi! Kama unavyomjua Umi, yeye ilimradi uwe na pesa, hana shida. Na Umi anauzika kwa harakaMuonekano ‘A’.Juu mpaka chini wakati wote anajipangilia na Mungu akampangilia vizuri. Kama unatamaa, na hujatulia, rahisi kumvaa kama hujamjua.”

“Wakafanya siri hapa wakaenda kujificha Zanzibar eti Mbaki anafanya siri Tuma asijue! Wakiwa kulekule, mimi nahisi kuna kilichotokea kati yao, ndio Mbaki akamwambia ukweli kuwa mchumba ni Tuma, na ni mke anayejulikana mpaka kwao. Wanatarajia kufunga ndoa. Nafikiri, lakini sijui kilichotokea huko ila kwa kesi ilivyokuwa ni kama Umi alimpenda sana Mbaki.”

“Haya, Umi akarudi hapa baada ya kudanganya alikuwa msibani, kumbe kaachwana mimba, na Mbaki alishampiga marufuku asimtafute tena. Ikawa shuguli hapa, hapakaliki. Umi mjamzito wa Mbaki, anatapika, Mbaki kamfungia simu. Ikabidi mimi nimtafute sasa Mbaki maana tulikuwa karibu nao sana. Nikamwambia Mbaki amekosa. Lazima nimwambie Tuma, maana Tuma ni kama mdogo wangu. Ungemuonea Mbaki huruma, wakati aliifuata dhambi yeye mwenyewe! Huku hataki kumpoteza Tuma, na huku Umi mjamzito ushahidi anao akiwa na Mbaki huko Zanzibar.”

“Ikawa kesi kubwa sana, ila mwishoe Tuma akavunja uchumba.” “Kwamba huyo Mbaki bado alitaka kumuoa?!” “Haa! Hata leo Tuma akisema ‘ndiyo’, atamkimbiza kanisani haraka sana.”

Anampenda Tuma, na anasema Tuma ndiye mkewe, hakuna mwanamke anayeweza kuwa naye isipokuwa Tuma. Siku Tuma anamrudishia pete ya uchumba, bwana Mbaki alilia! Alilia kama mtoto. Lakini kama umemgundua Tuma, anamsimamo sana. SANA. Akiamua jambo, hayumbi ndio maana yupo hapa kazini na hutamtuma kitu, anajituma yeye mwenyewe ni kwa sababu aliamua kutulia hapa.”

“Akamrudishia pete ya uchumba, alikuwa amempangishia nyumba nzima, akahamiauswahilini. Halafu alimnunulia gari zuri sana. Nzuri mno, ya thamani. Kubwa. Mpyaa. Alichofanya Tuma akaliuza hilo gari pamoja na thamani nyingine za ndani kwake, dhahabu alizokuwa nazo zote aliuza, na nyingine nilinunua hata mimi. Hereni na sheni zake. Pesa zote akaanza ujenzi. Yaani alibadili maisha yake kwa haraka sana.”

“Tuma ambaye ungekutana naye kipindi yupo na Mbaki usingedhani kama anaweza ishi hivi. Eti kula ugali tembele hapa, au kupanda daladala! Usingedhania. Alikuwa Tuma kwelikweli! Lakini alibadilisha maisha yake kwa haraka sana, na sijamsikia akilalamikahata mara moja!”

“Kwa hiyo ndio hivyo. Lakini ndio Mbaki hajaoa mpaka leo, anasema Tuma ndio mke. Na Tuma naye anasema amemalizana naye ila naye hata atongozwe vipi, hakurudi tena kuwa na mahusiano mpaka namuuliza amezira! Maana hapa wanakuja wanaume wa kila namna, na ndipo mwenzie Umi anapotajirikia hapa.”

“Walikuwa wanakujaga mpaka humu ndani kumtongoza, nafikiri aliingiwa na hofu, hajarudia tena kuwa na mahusiano. Ila mama yake Mbaki alipofariki, alikuwa huko. Wakipatwa na msiba, wanamuhesabu Tuma kama familia. Na Mbaki akiumwa, utafikiri hapa ni hospitalini, atataka Tuma ajue na amuuguze. Na asimkose Tuma kwenye simu, hata kama ni usiku ataniamsha. Utafikiri nyumba inawaka moto anavyokuwa akitapatapa.”

Anampenda sana Tuma ila kasoro yake nyingine mbali ya wanawake ni pombe. Anaweza akakupigia usiku mwingi amelewa, anamuulizia Tuma mpaka Jeremi alikuja kuzungumza naye kwa ukali ndio akapunguza. Sasahivi akipiga kwangu, anapiga kwa kisingizio kuwa mgonjwa au kwao kuna matatizo.”

“Na alichokifanya Tuma cha akili, alipohama, hakumwambia anakoishi. Kwa hiyo asipompata kwa simu ndio amekwama. Ila mwenyewe Mbaki anasema watoto wake wanamacho kama ya mama yao, yaani Tuma.  Anayapenda macho ya Tuma, haishiwi kumsifia, zaidi akilewa. Eti anasema ashaona wanae jinsi walivyo wazuri na tabia nzuri kama mama yao. Hawezi changanya mbegu na mwanamke mwingine. Namuuliza sasa kama anampenda Tuma, kwa nini hutulii! Maneno mengii akijidai amebadilika!” Jerry akapoa mpaka moyoni. Akagundua kumbe mahusiano ya Mbaki na Tuma sio yakuvunjika kirahisi! Akapotelea mawazoni.

“Ila Tuma ni binti mzuri sana. SANA. Na kwa kuwa aliishi naye, anajua. Na mwenyewe anasema kabisa. Kuwa hatakaa kuja kupata mwanamke kama Tuma ndio maana haoianamsubiria.” Akazidi kugongelea msumari na kumnyong’onyeza zaidi Jerry.

“Acha niende nikamsaidie Jeremi mpaka saa sita kamili ndio nitoke. Sita na robo au nusu nitakuwa nimesharudi ili na nyinyi mtoke.” “Nashukuru na samahani kwa usumbufu. Tukifanikisha, najua na wewe utafurahi.” “Ila nikuombe kitu shemeji yangu.” “Nini tena?” Hilda akakaa sawa.

~~~~~~~~~~~

“Naomba kwa kipindi hiki, kazi za mikono acha. Kaka yenu analalamika.” “Mbona nilizungumza naye jana!” “Hayakuisha. Usiku kama kwenye saa nne na nusu alimpigia tena simu Jeremi na kuanza upya anasema anashindwa kulala, ameumia sana vile alivyokukuta kule unatokwa jasho unabadili matairi.” “Lakini nilimueleza bro, kama nataka kujifunza!” 

“Na Jeremi akamwambia hivyohivyo, akasema sasahivi tekinologia imekwenda mbele, si sawa wewe peke yako urudi nyuma. Akampa mfano wa kuwasha moto. Akamwambia sasahivi watu wamegundua mpaka majiko yanayowaka moto kwa kubonyeza tu au kuzungusha kitufe, hata kiberiti hakitumiki tena. Sasa eti inakuwa kama mtu anakuwa kwenye ulimwengu huo, lakini yeye peke yake ndio anasugua mawe ili kupata moto.” Jerry alicheka sana.

“Kweli tena! Naomba kwa sasa ambako ana habari zako mbayaacha kwanza. Unamjua kaka yenu. Unaweza kuta tena na leo akaacha shuguli zake zote akaja tena kukuangalia.” “Na yule hashindwi!” “Basi usimfanye akasononeka zaidi. Malizana na Sandra. Akuone umesimama kabisa, ndio uwe huru kufanya utakalo. Lakini sio sasa.”

“Jeremi anasema amemwambia anakumbuka vile mlivyoachwa na wazazi wenu mkihangaika. Anasema yeye amelipa na anaendelea kulipa garama kubwa sana ili nyinyi wawili msirudi kule tena. Anamwambia Jeremi kitendo cha kukuona jana hapa, vile, hawezi kulala kabisa.”

“Sasa akianza hivyo yeye, ujue na mkewe atanitafuta na unamjua mkewe! Sauti ya kubembeleza ila hamalizi.” Jerry akacheka sana. “Tafadhali shemeji yangu. Asije sema tunakutesa.” Hapo ndipo akafunguka. “Kumbe! Basi kama itabeba picha hiyo kweli nitaacha. Nitakuja jifunza pakitulia.”

“Yule mwanasheria mwenyewe ananiambia bro anamuhimiza sana kutaka hili jambo liishe kwa haraka, Sandra asiendelee kunidhalilisha. Sasa mimi namwambia Sandra hanisumbui tena, hataki. Anasema kitendo cha Sandra kunidai chupi mbele za watu na yeye yupo haikinamnyima usingizi!” “Basi na jana amerudia kwa Jeremi. Bwana Sandra amemuumiza kaka yako! Nahisi kuliko hata wewe alivyokuumiza. Mpaka Jeremi anasema ashukuru Sandra alizaa na wewe, lakini angemlipiza kisasi.” 

“Na mimi nilihisi hivyohivyo nikamuwahi bro, na kumkumbusha namwachia Sandra watoto wangu, ndio kidogo akatulia maana alishaanza kukumbushia vitu fulanifulani vya msingi akisema atamkumbusha hakufanya kwa ajili yake ila yangu. Ila usijali. Nitaongeza umakini kwa sababu yeye yupo na uchungu, mimi mwenzie nafurahianaona kama nimetuliwa mzigo.” 

“Bora angekuacha bila matusi. Ile fedheha ndio inauma!” “Hakuna jipya kwa Sandra. Wewe nenda uwahi kazi, nitaenda kumsaidia Tuma.” “Sasa usiende ukapitiliza huko gereji, kaka yenu akaja hapa, akakukuta kama jana. Sitaki kesi.” Jerry akacheka tu, Hilda akaondoka ila akamuacha na mawazo juu ya Tuma, akiona vile ilivyo rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko yeye kupenya katikati ya Tuma na huyo Mbaki.

~~~~~~~~~~~

Hakuwa amepanga, wala kutarajia, katikati ya wakati mgumu, kwenye ndoa iliyovunjika kwa fedheha na kashifa zinazozungumzwa kila kona ya jiji, lakini kwa Tuma akajikuta anajisikia tofauti. Hisia zinampeleka sivyo! Moyo unataka unachojua ngumu kupata. Ikawa kama Tuma ndiye anayemuwezea, lakini tena kumbe Tuma huyohuyo ni majibu ya Mbaki! Moyo ukazidi kunyongonyea.

Si Kila Kukataa Ni Kukosa Huruma

Wahenga husema, ‘Si kila anayekunyima mkono wa msaada ni mwenye moyo mbaya, wengine hubeba mizigo yao kimya kimya, wakijufunza kusimama kabla ya kuinua wengine’. Na wengine husema, ‘si kila ukimya ni uovu’. Ndivyo ilivyo kwa wengine wanaoamua kujitenga na watoto wa nje ya ndoa, baada ya kusameheana na ndoa kupona.

Si wanawake wote ni Raza aliyekusudia kuyavulia maji nguo, na kuamua kwenda kuogelea kwenye kina kirefu

Na si wanawake wote ni Mina, wenye uwezo wa kumuachia mama wa kambomtoto, tena baada ya jaribio la kutaka kumua mtoto huyohuyo

Na pia, si wanaume wote ni Pius, kwamba wakaweza kukomesha mahusiano ya kimapenzi ya wizi, nje ya ndoa, KUISHIA kuwa WAAMINIFU wakabaki kulea mtoto yuleyule mmoja. Wengine katikakati ya msamaha, wapili na wa tatu huzaliwa hukohuko nje ya ndoa

Kwa Andy, kamwe hakurudia kosa. Macho yake hayajawahi kutoka kwa Mina wala Pius kuhakikisha hakuna mwanya wa mkewe kuguswa tena kimapenzi. Aliongeza umakini, tena bila ya kuzembea akiweka mipaka mikali, ya waziwazi.

 ~~~~~~~~~~~

Ayvin bado alikuwa sakafuni, Ayan akaanza na yeye kulia kwa hofu amejificha kwa dada yao, Raza ndio anapiga yowe kwa hofu, Poliny akampigia simu wa kwanza Paul ambaye ni daktari wa familia. “Anko, Ayvin ameanguka vibaya sana kutoka juu mpaka chini. Hajafungua macho wala hatingishiki lakini nimemshika bado anayo mapigo ya moyo. Nimsaidiaje?” Poliny akiwa ametulia kabisa, akamfanya anko wake na yeye atulie na kumuelekeza jinsi ya kumpa huduma ya kwanza huku akimwambia mwenzie. 

“Nisaidie kuita gari ya wagonjwa, iende kwa Pius, haraka. Waambie ni mtoto.” Akamsikia akimwambia mtu mwingine asijue alipo kisha akarudi kuzungumza naye.

“Sasa hivi anaendeleaje?” “Yupo vilevile.” “Lakini umemsaidia oxygen kwenda kwenye ubongo. Taratibu, bila kupaniki, endelea. Wanakuja kumchukua sasahivi, mtanikuta hospitalini.” “Usikate simu anko.” “Siwezi. Nipo na wewe mpaka wafike hapo kumchukua.”

Pius aliingia hapo kama simba. Akambeba mtoto. “Twende Poliny. Na usikate simu ya anko wako. Endelea kufuata maelekezo.” Wakaondoka hapo bila kusubiria gari ya wagonjwa. Kikabaki kilio cha hofu cha Raza.

~~~~~~~~~~~

Msichana wa Mina na yeye bila kupoteza muda akatoka na mtoto nje, akampigia simu Mina akamwambia alichokiona wakati wanafika hapo chini ya ngazi, kuwa Raza alimsukuma mtoto, ameanguka kutoka juu mpaka chini ya ngazi. 

“Poliny anasema anamapigo ya moyo, lakini dada, hata hatikisiki! Amekuja kuchukuliwa, anakimbizwa hospitalini. Sijui ni wapi! Ila Ayan naye analia sana, ameingiwa hofu baada ya kuona mama yake mkubwa alichomfanyia mdogo wake.” “Nitakupigia baadaye.” Akakata simu.

Bila ya kupoteza muda, hapohapo akampigia simu Pius. “Mnaelekea hospitali gani?” “Samahani sana Mina, nili…” “Tafadhali niambie unapompeleka mwanangu.” Hapo Mina akasikika asiyetaka kutolewa kwenye la msingi. Pius akamuelekeza. Bila ya kuongeza, akakwapua pochi yake akatoka hapo saluni na tumbo lake kama akikimbia. Alikuwa akioshwa miguu, baada ya nywele ili akitoka hapo wakutane na Andy kwa chakula cha mchana. Bado Andy alikuwa kazini.

Njiani akampigia simu. “Ayvin anakimbizwa hospitalini na Pius, nimeambiwa na Judy, hali sio nzuri. Naomba muombee, na mimi naingia kwenye maombi.” Akamtajia anapopelekwa na kukata akiendelea kukanyaga mafuta. 

~~~~~~~~~~~

Mina alianza maombi hapo garini kwa sauti akimsihi Mungu asimchukue huyo mtoto. Alikuwa akiomba huku akitubia dhambi zake hata ambazo alishasamehewa! Alikuwa akirudiarudia kwa hofu akimsihi Mungu kwa machozi. 

Alikumbuka jinsi mimba ya Ayvin ilivyotungwa kwa hila! Na vificho alivyokuwa navyo na Pius akiwa mjamzito wa huyo mtoto, na kuzidi kuogopa akijifananisha na mtoto aliyezaliwa na mke wa Uria kwenye bibilia aliyezaa na mfalme Daudi. Hofu ilimjaa Mina, akajua na Mungu naye anamrudi kama alivyomrudi mfalme Daudi kwa kumnyang’anyamtoto aliyepatikana kwa hila mbaya. Akazidi kulia kwa hofu huku akitubia bila ya kutosheka, njia nzima mpaka hospitalini.

~~~~~~~~~~~

Anafika hospitalini mtoto alishapokelewa. Alishakausha machozi garini ila wazi alionekana alikuwa akilia. “Yuko wapi?” “Paul yupo naye ndani na daktari, wanamuwekea oxygen kisha atapelekwa kufanyiwa kipimo cha MRI kujua alipoumia kwa hakika.” “Ameweza kufungua macho?” “Hapana Mina.” Pius akajibu kama alie. Akajitenga pembeni akaanza kuomba tena.

“Ilikuaje Pius!?” Akasikia sauti ya Andy akiuliza kwa kulaumu, lakini hakugeuka akaendelea kuomba. Anazunguka na tumbo lakukaribia kuzaa huku akiomba. “Niliwaacha wanacheza. Wote walikuwa sebuleni. Ndio Raza akanipigia simu akilia, sikuwa nimeelewa ila nilichoweza kuelewa kutoka kwenye kilio chake ni kuwa, Ayvin yupo matatizoni. Ikabidi hapohapo nigeuze, nirudi nyumbani.”

“Nikiwa njiani ndio Paul akanipigia simu na kuniunganisha na simu ya Poliny aliyekuwa amempigia kumuomba amsaidie huduma ya kwanza kwa Ayvin aliyekuwa bado hajapata fahamu. Hapo ndipo niliposikia akimwambia anko wake kuwa aliangukakutoka juu ya ngazi mpaka chini.” Andy akatingisha kichwa akikataa kabisa.

“Aliwezaje kufika juu? Na kwa nini awepo juu bila Judy au mtu wa kumwangalia!?” “Sijui Andy!” Wakaja mzee Ruhinda na mkewe. “Hapana Pius, huyu mtoto bado mdogo sana na niliwauliza wewe na Raza kama mtawaweza! Niliwaambia nyinyi wawili, siku mnapokuja kuchukua hawa watoto, LAZIMA muwe na muda nao, usio na mwingiliano. Ayvin hajaweza kutembea vizuri na anataka kufika kila mahali. Nikawasisitiza tena na tena, kwa kurudia. Isiwahi tokea mnawachukua wakati mna mambo yenu. Iweje mtoto anaanguka peke yake?” “Alikuwa na mama.” Akadakia Poliny kama aliyekuwa akimuokoa baba yake aliyekwisha kukubali lawama zote.

“Sijaelewa! Kwamba alianguka akiwa na Raza!? Aliangukaje?” Hapo Andy hasira zimeshampanda. “Tulikuwa wote sebuleni kama alivyosema dady. Wote walikuwa wanacheza mimi nasoma kitabu, lakini hapohapo walipokuwa wakishindana magari na Polla. Nilimuona dady akitoka kwa kunyata, baada ya muda mama naye akaondoka kwa kunyata akipandisha juu. Ayvin hakuona akawa anaendelea kucheza palepale sebuleni. Nafikiri hapo ndipo tulipojisahau.”

“Kilichofuata nilisikia sauti ya hofu ya juu ya mama. Wote tukakimbilia kujua amepatwa nini na ndipo tukamkuta Ayvin akianguka kutoka juu mpaka chini na mama akiwa pembeni yake.” Andy akakunja uso akiwa hajaelewa kabisa. Maana ni kama kulikuwa na gape, tokea kelele ya Raza, watu kukimbilia tukio na mtoto kuanguka. 

“Raza yuko wapi?” “Analia sana kwa hofu anko. Yupo nyumbani.” “Sasa akiwa analia nyumbani, mtoto yupo hapa, madaktari watamsaidia vipi mtoto?!” Andy akazidi kugomba zaidi kwa mshangao. 

~~~~~~~~~~~

“Tafadhali apigiwe simu Raza aeleze kilichompata mtoto ili asaidiwe.” Hapohapo yeye mwenyewe akatoa simu yake akampigia.

Akapokea na kuanza kujitetea na kuzidi kumtibua Andy. “Tafadhali acha kulia na kujitetea, niambie kilichompata mtoto ili wajue jinsi ya kumsaidia. Na Raza, iwe juu ya mtoto tu, na si kujitetea kwako hata kidogo. Hali ya mtoto ni mbaya, tunataka kujua jinsi alivyoumia ili kusaidia matibabu ya haraka.” Akaweka kwenye spika.

“Amejigonga kwenye chuma ya ngazi, kisha akaanguka mpaka chini.” “Alijigonga sehemu gani ya mwili wake?” “Kichwani.” Raza akajibu akisikika akitetemeka kama yupo kwenye baridi kali, kila mtu aliweza kusikia. Andy akafunga macho kabisa, na kukata simu. 

~~~~~~~~~~~

Hapohapo akaingia ndani. “Paul, huyo mtoto kabla ya kuanguka kutoka juu mpaka chini ya zile ngazi ndefu za kwa Pius, aligonga kichwa.” “Hizo taarifa ni za muhimu sana. Tulitakiwa kujua tokea mwanzo!” Wakaanza kumuangalia kichwa.

Wakasikia daktari akisema, “Hii sio nzuri. Inamaana ame absorbed the whole impact!Angevimba, ingekuwa afadhali.” Ilikuwa sauti ya daktari aliyeanza kukagua kichwa kizima na kukosa uvimbe hata mdogo. “Inaama ameumia mpaka ndani!” “Inabidi afanyiwe MRI kwa haraka ili kama kuna bleeding ya ndani asaidiwe kwa haraka.” Paul akaongeza. “Wapigie simu theater waambie waandae chumba. Baada ya MRI lazima tuanze na upasuaji wa mbavu. Hii ya kushoto imevunjikia kwa ndani, inabana mapafu, inazuia hewa kupita. Sitaki kujae maji au damu.” Alishituka Andy. Pius akasimama kama mshale hapo nje. “Mungu wangu!” Akasikika mama Ruhinda, mikono kichwani. 

“Patel amenihakikishia atakuwa hapa baada ya muda mfupi sana.” Paul akawa akimwambia daktari mwenzie. “Afadhali. Muhakikishie theater imeshaandaliwa kwa ajili yake, aende huko moja kwa moja, nitampelekea mtoto bila ya kuchelewa.” Wakawa wakizungumza huku wakitoka. Mina akageuka aliposikia wanatoka. 

Akawakimbilia mpaka pale kitandani. “Lazima aende sasahivi Mina.” Wakavuta kitanda kabisa kuashiria hamna muda wa kupoteza, Mina akawa anafuta kwa kukimbia pembeni ya mtoto wake mpaka chumba cha MRI, wakaingia akabaki nje, wengine nao ikabidi wafuate. Wakabaki nje, Mina akajitenga tena na kuendelea kuomba akiwa amesimama.

Andy akamsogelea na kumshika mkono. Akageuka. “Njoo.” Ikawa kama anamtuliza, akamkumbatia na tumbo lake, akatulia begani akimpapasa mgongoni taratibu. Kila mtu kimya anawaza lake.

~~~~~~~~~~~

Baada ya muda akatolewa hapo akawa anapelekwa chumba cha upasuaji. Andy akamuachia Mina na kumsogelea Paul kwa haraka. “Vipi kichwa?” “Naomba kwa sasa tuache Andy, ila jua yupo kwenye mikono sahihi. Patel anamsubiria.” “Ni mbaya sana?” Wakamuona anasita. “Paul?” Pius akauliza na yeye kuweka msisitizo.

“Naomba nisizungumze chochote mpaka amalizane na Patel, ndiye atakuja kutuambia kila kitu. Acha nisogee huko japo najua hawataniruhusu kuingia.” Paul akaondoka kama ambaye aliyekuwa akikimbia ndugu zake.

~~~~~~~~~~~

Andy akarudi kwa mkewe. “Njoo ukae hapa.” “Nataka kuomba.” “Njoo uombe hapa na mimi.” Akijua na tumbo hilo, anaweza zalia hapo kabla ya siku. Akamvuta mkono kabisa, akaenda kukaa naye. “Nataka kupiga magoti kabisa.” “Mungu atatusikia tukiomba hata tukiwa tumekaa.” Ikabidi amuegemee begani kwa nyuma, palepale akaanza kuomba tena kimyakimya akijua waromani hao, kuomba nao watamchelewesha. Akainama akiomba peke yake, Andy kimya ametulia akimpa nafasi ya kuomba ila akiridhika amekaa. Pakatulia.

~~~~~~~~~~~

 Mara Paulina akafika hapo kama aliyekuwa akikimbia. Akakuta wote wametulia nje ya chumba cha upasuaji. Akaenda kukaa pembeni ya mama yake. “Vipi mtoto?” “Hali sio nzuri. Tupo tunamuombea.” Mama yake akamjibu kwa sauti ya chini. “Kama kuomba, tuombe kweli. Nasikia Raza amemsukuma vibaya sana huyo mtoto. Kutoka juu mpaka chini.” Wote wakashituka.

“Paulina wewe mtoto!” “Sio kwa kusingizia mama. Dada yao hao watoto ameniambia, tena wala si siri amesema wote wameshuhudia akiwa anamsukuma Ayvin. Tena nasikia mpaka Poliny akamuuliza mama yake, kwa nini amemsukuma mtoto vibaya hivyo! Kama naongopa muulizeni Poliny kama hawajamshuhudia mama yao akimsukuma Ayvin.” Ikabidi wamgeukie Poliny.

“Ilikuaje Poliny!?” Baba yake akamuuliza taratibu. “Sijui dad! Hakika sijui mpaka nachanganyikiwa!” “Wewe sema ukweli. Hamjamuona mama yenu akimsukuma Ayvin, mpaka ukamuuliza?” Shangazi mtu akasisitiza swali na kuongeza. “Mpaka mimi nazungumza na Judy, Ayan alikuwa akilia kwa hofu. Judy anasema analia kwa kile alichomuona Raza akimfanyia mdogo wake. Hivi nimemuomba Devi badala ya kuja hapa moja kwa moja, akawachukue na kuwarudisha Kigamboni. Sasa Poliny huyo hapo ambaye mnamuamini. Aseme ukweli.” Paulina akaweka msisitizo.

~~~~~~~~~~~

Wanasema mchawi mpe mtoto akulelee! Ndicho kilichoendelea kati ya Mina na Raza.

Itakuaje hata na kwa Jerry akiwa na hisia asizoweza zizuia na wala hajazitamka kwa wazi kwa Tuma anayesubiriwa na Mbaki mwenye historia naye yenye mizizi?

Inaendelea….

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment