Jo alipitiwa usingizi kwenye kochi, alfajiri kumeshapambazuka. Amelala hana habari kama yupo siku ya ijumaa na jumamosi alishaalika ndugu wa Dorothy. Wakwe na upande wake huyo dada yake na shemejiye. Akamtia hekaheka dada yake, akatafuta mpishi ila kwa ahadi kuwa ijumaa atatoa idadi kamili ya wageni upande wa kina Dorothy watakao hudhuria hapo.
Mpishi akampiga simu dada yake kuulizia idadi kukamilisha tenda, na yeye akawa mpaka muda huo hajasikia chochote kutoka kwa mdogo wake. Ikawa mpishi anasubiri, dada naye anasubiri. “Basi itakuwa walinogewa jana usiku, Dorothy akaamua kulala hapo.” “Labda! Ila ndio ulalaji gani huo mpaka saa sita mchana!?” Dada mtu akauliza akishangaa.
“Ugwadu wa miaka mingi.” Shemeji mtu akaongeza kishabiki, mkewe akacheka tu maana alimjua. Anatafuta jukwaa ili aje amsimange mdogo wake baadaye. “Maana Jo..” “Umeanza. Mwache.” “Anakaba siku mbili! Anakosa utu sasa, hana kiasi.” “Muone. Ushabiki tu. Na nisikuone ukienda.” “Kama kapatwa jambo je?” “Hayakuhusu. Tulia hapa.” Mumewe anacheka mbavu hana.
~~~~~~~~~~~~~~
Huku kwa Dorothy kuona kimya mpaka mchana wa saa nane, hata ujumbe wa jana usiku haujajibiwa, ikabidi kuwataarifu wazazi. Pam akamsikia akizungumza na mama yake. “Imeahirishwa.” Ila ameishiwa nguvu, hana majibu ya kueleweka. “Bado tunajipanga mama.” Akajibu kinyonge baada ya kumuona amesikiliza.
“Mwambie kesho wanakuja hapa, sio kwa Jo. Nimeambiwa nipumzike, nisitoke. Waambie waje hapa, na waje na njaa.” Angalau akamsaidia mama yake. Akarudisha majibu ila safari hii kwa ujasiri zaidi kuwa hawakutani tena kwa Jo ni hapo alipo Pam alikoambiwa apumzike. “Kwa hiyo tunakutana hapa.” Hapo akaongeza na sauti kabisa. Kidogo akamuona anatabasamu, akajua bibi yake huko amefurahi.
“Bibi yako anauliza aje saa ngapi?” “Mwambie muda anaotaka yeye.” Akarudisha majibu, wakaanza kucheka sasa. “Anasema anakuja kunywa chai hapahapa.” Akarudisha majibu kwa Pam. “Nipe mimi simu nizungumze naye.” Pam akapokea na kuanza kuzungumza na bibi yake akicheka na lugha ikabadilika. Wakaongea hapo kisambaa wakitaniana mpaka wakaagana.
Akamuona mama yake amejiinamia kama anayewaza. “Pole mama yangu.” “Umenitoa aibu! Nashukuru. Maana hata sijui ningewaambia nini! Bora waje hapa. Lakini umezungumza na baba Shema?” “Nitamwambia, halafu na kuwakaribisha kina Kamila kusudi ili aje anisaidie kupika.” Wakaanza kucheka.
“Tapeli wewe!” “Nitafanyaje mama yangu? Akisema yupo busy najua mama Komba atatafuta mtu wakuja kutupikia. Waje hapa wote. Familia yao na kina babu. Tule, tucheke, tumalize siku kwa utulivu.” Kidogo akamtuliza mama yake. Wakaendelea kuteta yao, akamtoa mawazo kwa Jo.
Huku kwa Jo.
Kufika saa kumi jioni alipoona kimya, hata hajamjulia hali, na si kawaida ya Jo kutaka kujua waliamka vipi, dada mtu akapatwa wasiwasi, yeye mwenyewe, kimyakimya bila kumwambia mumewe, akatoka kwenda kwa mdogo wake. Hawa watu wote ni watu wazima. Wanajua kuna madhara ya kuishi peke yako. Unaweza anguka na pressure, mtu asijue, ukafa peke yako. Basi kila nyumba inakuwa na funguo zote za nyumba nyingine.
Akagonga mara kadhaa, kimya. Akafungua na kuingia ndani. Akakuta mezani kumeachwa kama waliofanikiwa kula lakini hata vyombo havikutolewa! Akaenda jikoni, hakuwepo. Wasiwasi ukaanza kumuingia, ndipo akaamua kumfuata chumbani kwake. Akamkuta amelala kwenye kochi.
Akamgusa. “Jo? Joel?” Ndipo akaamka. “Nini bwana unanitia wasiwasi?” “Nimelala muda mbaya.” Akakaa ndipo, akawasha taa. “Usiwashe taa, dada!” “Kwa nini!? Mimi sikuoni.” Ndipo akaona uso ulivyo. Akashituka.
“Kwema?” Akanyamaza. “We Jo?” Kimya. “Ni nini?!” “Sijui dada.” “Kuna nini? Maana umekuwa kimya, yule mpishi anataka kujua idadi ya wakwe.” “Sijui hata kama kuna wakwe tena. Sasahivi ni saa ngapi?” “Inakwenda kumi na nusu jioni.” Ndipo kukurupuka kusaka simu, dada yake amemuacha chumbani akimsindikiza kwa macho.
“Kwani leo ni siku gani?” Akamsikia akiuliza kwa sauti ya kupaniki. “Ijumaa!” “This is bad! This is very bad!” Akamsikia akizidi kupaniki huko sebuleni. Akamfuata. “Unanipandisha pressure bila sababu. Ni nini kinaendelea.” “Sijawahi haribu hivi maishani.” “Kama unatafuta simu yako hii hapa juu ya kochi hili nililokaa.” Akarudi kutoka jikoni na kukwapua simu yake.
“This is bad! This is very very bad!” Dada yake akatulia akimwangalia. Akafungua simu na kukutana na ujumbe wa Dorothy. Akamuona anashika kichwa na kukaa pembeni yake taratibu macho kwenye simu. “Kuna nini?” “Nimeharibu vibaya sana. Na mbaya zaidi nimeharibu kwa Dorothy kiumbe asiye na hatia.” “Umefanya nini tena?” Akabaki anaangalia simu. Dada yake akampokonya simu na kuiweka pembeni.
“Haya, anza kuzungumza.” “Jana alipokuja hapa...” Akamsimulia kuanzia mwanzo mpaka hapo walipokaa. “Sijawahi pata hii hali dada!” “Hukuambiwa wewe na shemeji yako ukae chini, utulie, ukubali ukweli kuwa kuna jambo baya limekutokea, uombolezendipo uendelee na maisha? Hukuambiwa wewe?” Kimya. “Ulikuwa na kazi ya kurukaruka ukafikiri utakwepa ukweli. Huwezi Jo! Betty alikuwa mkeo. Na hakuwa mke tu. Mlikuwa mkifanya naye kila kitu pamoja. Kila siku, kila mahali. Hawezi akafariki,…” “Acha kusema hivyo. Usiseme hivyo dada.” Akaanza tena kulia.
“Unakataa ukweli, unakwepa. Mpaka lini?” Jo akazidi kulia. “Huu ni ukweli ambao hutakwepa Jo, na hata mama yake Betty alikwambia. Maisha unayoishi, hata Betty akirudi leo, utamuumiza sana. Hukuambiwa hivyo wewe?” Akazidi kulia na kuondoka kabisa pale.
Safari hakumfuata, akamuacha huko chumbani kwake akilia, yeye amekaa sebuleni. Alilia Jo, akalia sana dada yake kimya sebuleni.
~~~~~~~~~~~~~~
Mumewe akaanza kumsaka kwa simu. “Uko wapi?” “Ndio nyinyinyi. Mtu akiondoka ndio utafikiri ameondoka na roho yako! Dakika 5 tu nimeondoka hapo utafikiri umepoteza roho!” “Mbona kama nahisi namaliziwa mimi hasira, malaika wa Mungu nisiye na hatia!”Ikabidi mkewe acheke tu. Hamuwezi mumewe kwa maneno.
“Upo wapi Josephine?” “Nitarudi.” “Kutokea wapi? Mbona sauti yako kama yakishari! Kwani leo mimi nimefanya nini?” “Nipo kwa Jo.” “Dakika mbili mbele sijakuoa, nakuja.” “Bora tu uje, hapa si pakuondoka leo.” “Kwema?” “Betty kapata ajali ya gari, kafariki.” Ndio akaelewa.
“Leo hiyo?” “Jana akiwa na Dorothy.” “Sikumwambia mimi atulie amalize msiba wa mkewe, akanibishia? Kila nilivyokuwa nikimwambia afanye therapy kama wanae, yeye akawa mbishi, anaruka huku, anarukia kule. Watoto wake wamepona, yeye ndio taarifa zinamfikia!” “Na bado hataki niseme kama Betty amefariki.” “Basi ndio nije na jamvi kabisa, maana naona hapo tutakuwepo sana.” Mkewe akacheka na kukata. Jo analia ndani kama ndio kweli kapata taarifa. Dada yake yupo sebuleni.
~~~~~~~~~~~~~~
Walikaa hapo sebuleni na mkewe, Jo yupo chumbani mpaka saa mbili usiku. Shemeji yake akamfuata. “Hapa kwako hapaliwi?” Yaani anamuuliza Jo, anayelia. “Maana mimi ndio muda wangu wakula, na wewe upo na mke wangu hapa. Nasubiri umalize kilio, naona hayaishi. Basi tupe chakula tuendelee kuwepo hapa. Maana kila msiba unachakula.” Jo akanyanyuka na kuhamia upande wa maliwatoni, akajifungia chooni, anaendelea kulia.
Shemeji yake akatoka. “Huu msiba hauishi leo, na hapa hamna dalili ya kuliwa.” Mkewe kimya. “Likija swala la Jo, mimi nakuwa sina thamani kabisa! Napuuzwa. Sisikilizwi.” Akazidi kulalamika. “Chakula kinaletwa, acha kulalamika.” “Sasa kwa nini kuniacha nikilalama kule kama mjinga kumbe chakula kinaletwa?” “Nilivyokusikia unaulizia chakula kule, ndio nikakumbuka kuna matumbo yana kengele.” Akacheka akikaa.
“Na muda wangu wa kulala ukifika?” “Unaingia hapo ndani unalala.” Akazidi kucheka. "Mpaka lini?” "Ndio msibani tena, utafanyaje?” “Na Jo kumbe naye mliaji kwelikweli!” “Hapo ukute kamkumbuka na mama yake. Nampa muda mpaka saa nne. Kama hamalizi nampa dawa za usingizi, alale na mimi nikalale. Hivi atanipandisha pressure bure.” “Na kweli.” Wakatulia.
“Sasa wameishiaje na Dorothy?” “Ngoja tuangalie simu yake.” Dada yake kufungua simu, ndipo anakutana na ujumbe wa mwisho wa Dorothy na hajamjibu. “Basi akimaliza msiba wa mkewe, mchumba hana.” Shemeji yake akaongeza baada ya kumaliza kusoma na yeye huo ujumbe.
“Na anavyompenda Dorothy! Hapo atakuwa amemleta humu ndani, ndio hukumuyakuona amepata mwanamke mwenye uwezo wa kuziba pengo la mkeo, ndio kilio hicho. Wala hana jingine.” “Itakuaje?” “Acha nitoke nikazungumze na Dorothy.” “Na mimi nakuja.” “Wapi? Tulia bwana! Akitoka huyo akuone hapa, asijione yupo peke yake.” “Basi mazungumzo huko yawe mafupi, Josephine. Sio kuniweka hapa mpweke.” Akamtizama na kutoka na simu ya mdogo wake. “Usinyanyuke hapo. Nikukute.” “Mmhh!” Hao wawili hufuatana mpaka chooni. Hata watoto wao wanawajua. Baba yao hawezi kuwa mahali bila mama yao. Zikizidi dakika 5, hizo nyingi, ananyanyuka na kuanza kumafuta mkewe popote alipo.
~~~~~~~~~~~~~~
Akaanza kwa kumtumia ujumbe. ‘Mimi Josephine, dada yake Jo. Naomba upokee simu yangu.’ Alishituka Dorothy, mpaka kutetemeka. Alisharudi kwake maana Mill hakuchelewa kurudi kwa mkewe. Yeye akaondoka. Alishakuwa amepanda kitandani. Alipoona tu amesoma, akampigia. Naye akapokea bila ya kuchelewa.
“Shikamoo.” Akamsalimia akaitika. “Pole kwa yaliyotokea jana.” “Hamna shida, dada.” “Shida ipo. Huyu Jo, si kwamba alifiwa na mke tu. Betty alikuwa ni rafiki wanao ongozana kila mahali tokea wapo vijana wadogo. Wakatiana kichwa na ndipo kusomea hayo mambo yao ya udaktari, sisi tukijua hawataweza. Katikati ya shule ngumu ya udaktari eti wakafunga ndoa na kuanza kuzaa, napo tukajua yatawashinda tu.”
“Lakini kuna jinsi wenyewe waliwezana, ilikuwa ngumu kusimulia na inakera kwa wengine wenye ndoa ila sio kama wao.” Dorothy akacheka kidogo. “Sikutanii Dorothy, walikuwa watu fulani hivi, huwezi hata waeleza matatizo yako ya ndoa yako maana ni kama wenzetu wao hawakuwa nayo. Wote walikuwa watu watu…” Akawa anatafuta neno sahihi la kuwaelezea Jo na Betty.
“Niseme kuna jinsi walienda. Na Betty naye alijaliwa moyo wa ajabu sana mpaka uishi naye ndipo utanielewa. Mwema wakupitiliza, halafu akajaliwa huruma sana. Usingemkuta Betty anatatizo na mtu, ndivyo alivyokuwa. Halafu akapewa damu ya kupendwa. Ndio akamfanya Jo kama mkia wake. Anamfuata nyuma kila mahali, na kila sehemu kasoro siku hiyo ya ajali, alipofariki Betty.” Dorothy akendelea kusikiliza kujua sababu ya kuzungumza naye.
“Kosa alilofanya Jo, ni kukataa ukweli na shemeji yake alimuonya kwa kurudia rudia. Atulie chini aomboleze kifo cha mkewe, akawa mbishi. Sisi tukawatafutia familia nzima therapist. Yeye akakataa kwenda, wanae wakahudhuria mpaka wakaweza kuendelea na maisha wakikubali kuwa mama yao hayupo tena hapa duniani, lakini Jo akahama nchi kabisa. Mara yupo huku mara yupo kule.”
“Siku zinaenda akiaminisha watu yupo sawa, lakini shemeji yake alikuwa akisema anatembea na bomu ndani, linaweza kuja kumlipukia pabaya sana. Ndio jana.” Dorothy akawa bado hajaelewa.
“Huyu Jo alishakuwa na wanawake wawili lakini wale nao walikuwa majanga tu. Kuanzia yule mzungu wake aliyekuwa amempata huko alikokuwa amekimbilia mpaka yule mtanzania aliyekuja mpata hapa nchini, hapakuwa na cha maana kilichokuwa kikiendelea. Ila napo ukifikiria sana ni kama na Jo naye alikuwa na matatizo yake, alishindwa kuwafungulia moyo. Akaona kasoro nyingi kwao kuliko uzuri wao.”
“Ila sasa wewe, ndio hakutegemea kama unaweza muingia moyoni bila kujijua.” Dorothy akajikuta anakunja uso. “Yaani wewe ni mshale uliomchoma bila kutarajia. Amekuja kushitukia ushaingia moyoni mwake, na akakupenda sana. Amefanya mambo bila kufikiria, akifuatisha moyo wala si hisia tena. Maana kwa hisia yupo makini sana Jo. Si mjinga na anauwezo wakutawala hisia zake. Wewe amekupenda kupitiliza. Anakuja kugutuka, upo moyoni, umechukua nafasi ya mkewe, ndio kilio.” “Mimi aliniacha mzima!” Dorothy aliongea kwa mshangao.
“Hapa nazungumza nipo nje nyumbani kwake, maana humo ndani kwake hapakaliki, ndio ameanza msiba wa mkewe, tunahisi ni hukumu. Tokea jana amerudi hapa alikuwa akilia. Ujumbe wako ndio ameupata sasahivi ndio anazidi kulia anajua ameshaharibuzaidi. Kwa hiyo nilitaka usijeona kimya ukadhani amekupuuza. Mwenzio yupo msibani.” “Poleni.”
“Anachotaka kutufanyia Jo sasahivi, ni kutuua tu. Sisi wenzie msiba wa Betty tulishamaliza japo hatujamsahau. Sasa yeye anaanza leo! Kweli jamani!” “Poleni dada. Poleni sana.” “Na wewe pole kukutana na hali kama hii. Alitakuwa awe alishamaliza. Maisha yaendelee. Lakini sasahivi inamlazimu kurudi nyuma ili aweze kuendelea. Nina ombi.” Dorothy akatulia.
“Upo Dorothy?” “Nipo, nakusikiliza.” “Naomba mvumilie tu. Mpe muda, naomba akirudi mpokee. Ni janga lililompata, huwezi hata mlaumu. Nakusihi uelewe.” “Nitamuombea. Naamini atakuwa sawa.” Wakatulia kwa muda kama Josephine akijaribu kuelewa jibu la Dorothy, ila akaona awe muungwana.
“Vipi wazazi? Maana nilikuwa nikiwaandalia chakula.” “Naona Pam ameona waje tu hapa, njia nzuri ya kumpa nafasi Jo.” Akaelewa. “Nashukuru kwa kumsitiri. Asante.” “Usiku mwema.” Dorothy akaona aage tu. “Asante na wewe. Lakini nina ombi jingine.”Kimya kwa Dorothy.
“Nilijiandaa kwa ugeni kesho, nimeshamlipa mtu nusu ya pesa. Naomba hiyo pesa isipotee bure, hicho chakula kiletwe hapo kwa Pam. Kwa nilivyosoma ujumbe wako, Pam mwenyewe anahitaji mapumziko, si ndivyo?” “Usihangaike.” “Sifanyi chochote zaidi ya kumpigia simu, nampa idadi ya watu na kumtaka akilete hapo kwako hicho chakula. Itakusaidia kupumzika na binti, yako kuliko kuanza mapishi tena!” Kimya.
“Usikatae tafadhali. Nitajisikia ni kama umenisusia.” Akacheka taratibu. “Samahani. Haikuwa nia yangu, sikutaka kukuingiza garama zaidi.” “Kilishalipiwa. Wala si garama mpya.” “Nakushukuru kwa chakula.” “Kwahiyo idadi itakuwa kiasi gani?” Akafikiria kwa haraka akakisia na kumwambia. “Muda gani unataka kiletwe?” “Na hivi umeshanitia njaa, iwe mapema tu.” Kidogo wakacheka.
“Nitamwambia basi kiwe cha mchana. Mle na mpate cha jioni.” Akatulia. “Nikuulize na wewe?” “Karibu.” “Kwa hali ilivyo sasahivi, ninamsaidiaje Jo?” “Huna chakufanya. Sisi wenyewe tupo tu hapa ndani, tumemuacha alie mpaka aridhike.” “Peke yake!?” Akaingiwa tena na huruma.
“Lasivyo hatakaa akamaliza. Alitakiwa awe amemaliza muda mrefu sana hichi kipengele. Tunamuacha tu. Ila nakaribia kuchoka nampa lisaa mbele, nikimuona hanyamazi nampa madawa mengi ya usingizi. Akilala na mimi ndio nitakwenda kulala. Kesho tena tunaanza upya mpaka amalize.” “Usije muacha peke yake.” Alicheka huyo wifi mtu, akacheka sana.
“Hivi vyakulia jambo haliishi mimi sitaviweza. Nishakuwa mtumzima. Alipofariki Betty wakati ule nilikuwa na nguvu, tungekesha naye bila shida. Sasa yeye karukaruka wee, wenzie tulishamaliza, anachokifanya sasahivi nikutaka kunichosha bila sababu! Hapana. Nitampa madawa ya usingizi mengiii. Akija kuamka na mimi ninakuwa nilishaamka, nimekula, narudi tena kukaa hapa nasubiria. Mpaka safari hii amalize.Lasivyo nitaondoka hapa duniani, nimuache mpweke zaidi. Maana kwa sampuli hii mwanamke gani atamtaka?” Kimya.
“Na Jo, hawezi ishi peke yake. Akikupenda, huwezi mkwepa. Ndio maana unamuona amekuganda kila mahali anakufuata mpaka kazini.” Dorothy akacheka sana. “Sisi tunamjua Jo. Na ana watu wake na ndio maana kwenye familia anaambatana na sisi tu. Amekuwa kama ndio kifungua mimba chetu. Yaani nimeenda kwa mume na Jo mgongoni. Mume wangu ananiita Marekani, nikamwambia siwezi ondoka hapa nchini, nina mtoto.” “Jo?!” Dorothy akauliza akicheka.
“Mwingine nani? Huyohuyo Jo. Ndio nikatangulia lakini yeye ndio akawa wa kwanza kwenye familia nzima, kumvuta nilipo. Hajiwezi. Ndio maana nakwambia, wewe mvumilie tu. Atarudi na hutakuwa na jinsi ya kumkwepa. Utamuhurumia.”
“Nimekupigia ili tu kurahisisha ili asijemaliza kilio akajikuta tena mpweke, umeshachukuliwa na mwingine.” Dorothy alicheka sana. “Na uzee huu!” “Mbona Jo kachanganyikiwa sasa? Kutwa kunisumbua na maswali yasiyoisha juu yako kama yupo kwenye kinyang’ang’anyiro hataki kuporwa! Anakazi ya kunituma kununua vitu vyako, sihemi. Shemeji yake anamuuliza, sasa muoji ni yeye au mimi?” Dorothy hana mbavu.
“Ni hivyo tu. Lakini usiku wa jana alijiandaa sana kukufurahisha, mpaka namuhurumia. Alitaka kukufurahisha kwelikweli! Chakula alichokupikia wewe, kilionjwa na watu zaidi ya watatu kuhakikisha utakifurahia.” “Masikini Jo! Kumbe!” “Sana. Gauni hilo alilotaka uvae usiku wa jana wakati wa chakula alichokupikia, tumezunguka sisi wote watatu tukiwa na shemeji yake, tukawa hoi, kuchoka, kisa tunatafuta nguo za Dorothy!”Alivyoongea vile mpaka akamfanya Dorothy acheke kwa sauti.
“Ni zaidi ya dakika 5, Josephine! Ni nini humalizi bwana!” “Mwingine huyu! Yeye na Jo, wasiponiona au kunisikia hata dakika, ni shida. Kwaheri mwaya Dorothy. Tutakuja kuonana.” “Sasa umwambie sio tena aanze kuolewa kwingine, mimi nishajiandaa.” “Umemsikia shemeji yake Jo?” Dorothy akazidi kucheka kwa aibu.
“Maana wanadamu hawanaga jema bwana! Tushakuwahi. Wewe mvumilie tu. Atamaliza, atakuwa sawa.” “Nashukuru. Na asanteni kuzungumza na mimi.” “Karibu. Kesho chakula kitaletwa mapema tu. Msihangaike.” “Asante.” Ndipo wakaagana lakini akamuacha Dorothy angalau na furaha ila hofu nayo ikatibuka.
~~~~~~~~~~~~~~
“Ndio yatakuwa mahusiano ya namna gani haya jamani!” Akawaza. “Jo anaonekana mkewe amemkaa sana moyoni hana nafasi ya mwingine. Haya yatakuwa ni kama yaleyale! Unakuwa na mwanaume lakini moyo wake unakuwa kwa mwanamke mwingine.” Akaendelea kuwaza akikumbuka aina ya ndoa aliyokuwa nayo kwanza, mwanaume kulala na wanawake wengine tena bila kificho kama aliyekusudia kumuumiza kwa wazi kabisa!
Dorothy akajikuta anavuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha taratibu, tayari njia panda. Anajiuliza kama ni kitu anataka tena au la! Na kwa nini? “Hivi na umri huu kuna ulazima gani tena, kama si kujitafutia tu matatizo yasiyo na sababu!” Vikaanza kukosa ladha.
Penzi La Kweli Katikati Ya Dhoruba.
Mill alirudi nyumbani kama kwenye majira ya saa tatu usiku. “Huyu mbona ameishia kulala hapo?” “Kaja na habari ndefuu!! Kaongea hapo weee, akaona aniwekee movie. Asiache niangalie mwenyewe, akaona aanze kunisimulia movie yenyewe, mpaka nikamwambia sasa nina faida gani ya kuiangalia tena? Akawa ananiambia ananisumulia kwa mara ya mwisho. Lakini akaisimulia movie nzima mpaka akamaliza ndio nikaanza kumsikia anakoroma.” Mill akamwangalia na kuanza kucheka vile alivyokuwa amelala kwenye kochi hapohapo chumbani kwao, mguu mmoja unaning’inia na mkono.
“Yaani hapa nathibitisha tu aliyonisimulia. Lakini movie nzima naijua. Mpaka kinachofuata baada ya hapo nilishaambiwa.” Mill akazidi kucheka akimtizama mwanae. “Hivi siatakuwa anaumia?” “Nimemuita mpaka nimechoka, nikaona nimuache tu lasivyo ingekuwa kuanza kuvutana naye mpaka chumbani kwake, nimuumize mdogo wake. Pole na kazi.” “Asante. Acha nimtoe hapa akalale chumbani kwake. Atakuwa anachoka kwa mpira.” “Bora hivyo kuliko angezaa tu humu ndani. Muone anavyokoroma! Sijui tutamsaidiaje mkewe!” Baba yake alicheka, alicheka sana. Akaanza kazi ya kumuamsha na kumsindikiza mpaka chumbani kwake ndipo akarudi.
~~~~~~~~~~~~~~
Akamuona anakwenda kutoa nguo ili akaoge na anamjua baada ya hapo ni kusafisha kinywa, ndio hakuna kitakachoingia tena mdomoni mpaka kesho yake. “Kuna chakula.” “Nilipita kula sehemu na Jerry. Sikutaka kumuongezea mzigo huyo binti tuliyepewa kwa kutusaidia tu. Mwambie mimi asinihangaikie. Mambo yangu nitayafanya mwenyewe. Na kesho nitamwambia dereva alete chakula changu na Shema. Ukaribisho wao wa nyumba isiwe adhabu. Nataka mama ajitegemee kabisa. Maisha yake hapa, yawe kama kule Kinondoni. Awe huru, asijihisi amehamia hapa kwetu. Hatapafurahia.” Akaingia bafuni kuoga.
Akamuacha Pam na mawazo. “Inamaana mazungumzo yaleyale ya jana usiku akiwa na Jerry, na leo pia yaliendelezwa!” Akaendelea kuwaza, Mill akiwa bafuni.
~~~~~~~~~~~~~~
Baada ya muda akatoka akionekana yupo tayari kulala. “Ulipumzika lakini au ndio alikuja kukuvuruga?” “Nimepumzika. Na wewe kazi ulifanikiwa kuzisogeza?” “Kwa asilimia kubwa. Nikuulize kitu?” “Juu ya nini?” Akajilaza pembeni yake.
“Bado unampango wa kwenda kuishi na mimi nchini Marekani au unahitaji muda wa kufikiria zaidi?” “Mill, nimekosa mpenzi wangu. Na ni tabia tu mbaya ambayo nimekuwa nayo. Najifikiria na kujilaumu kwa kukufanyia ubaya. Najiona sina tofauti na baba yangu, kutumia watu vibaya.”
“Najua nimekuumiza au nimekuwa nikikuumiza. Umekuwa muwazi kwangu, tafadhali naomba nisamehe na nipe nafasi tena.” “Nime..” “Hapana Mill. Ninachoomba ni msamaha wa kurudisha mahusiano yetu. Tuwe kama mwanzo. Nisaidie nisiwe Kisha au Pam wa zamani kwenye maisha yetu. Nikimaanisha ukumbuke na naomba ukisimamiekile kiapo chako cha siku ya jumatatu pale mbele ya watu na yule mchungaji.” Mill akapoa kabisa maana hata juma halikuwa limeisha!
“Uliniapia utanivumilia Mill, na utakuwa na mimi katika shida na raha. Nimekosa. Nimekuvunja moyo. Lakini haimaanishi sikupendi au ‘ndiyo’ zangu zote za nyuma uanze kuzitilia mashaka! Unaniumiza na sijui nifanye nini tena!” “Sio nia yangu.” “Sasa kwa nini hunihesabu kama zamani, unarudia kuniuliza mambo tuliyokwisha kukubaliana?” Mill akatulia hakujibu kwa haraka.
“Najua nimekuumiza mpenzi wangu. Uliniandalia kitu kizuri, lakini nikaharibu. Tafadhali nihurumie Mill, jua nimetambua makosa yangu na nimekusudia kubadilika. Sijui Kisha alipanga nini au alinuia nini kwenye maisha yako, lakini mimi nakusudia kubadilika, nisiendelee kukuumiza. Nitaongeza umakini. Si kwa ajili yako tu, na watoto wetu pia. Umenifungua macho, nimeona naathiri wanangu pia. Tatizo si uwepo wako tu, ila hata jinsi ninavyoishi na wewe. Nabadilika. Nitafanya kwa juhudi zangu zote niwe mke bora kwako ili kusaidia wanangu pia.” “Na kile tulichokosa sisi, mimi na wewe, kuwa ndani ya familia ya baba na mama, tuwape watoto wetu Pam. Hicho natamani.”
“Nakuahidi nitafanya juhudi za makusudi. Leo nimeomba mpaka kwa kupiga magoti hapa kitandani kuwa roho chafu iliyopo ndani kwangu, itoke. Hata kama nina maroho ya kurithi, yanitoke. Nimemsihi sana Mungu anisaidie. Nataka kubadilika Mill. Na nakuahidi utaona mabadiliko.” “Nashukuru. Nakupenda Pam, nakupenda sana.” Bwana Pam akajikuta akilia, asiamini.
“Kwako sina jinsi. Wewe nimekupenda Pam. Naomba usilie. Usije pandisha tena pressure. Ila jua nakupenda. Na kukusikia ukisema hivyo, ujue inanifariji.” “Usinikasirikie Mill. Usinikatie tamaa. Nisaidie niwe mama mzuri. Nikikasirika nitajitahidi kuzungumza na wewe kwa heshima, sio ule ukorofi.” “Hapo nashukuru.” Akawa anamsaidia kumfuta machozi kabisa ili atulie, akiogopa wasije zua balaa jingine tena wakarudishwa hospitalini.
“Kwahiyo umenisamehe kabisa?” “Yameisha Pam wangu. Umri umekwenda. Sitaki kuanza tena kama hivi Jerry. Nimezungumza naye sana leo mpaka anatia huruma. Sitakikuwa hapo tena. Nishapita na Kisha, sitamani kurudi tena.” “Nakuahidi nimekoma.” Mill akacheka na kumbusu.
Penzi La mpatano
“Usinibusu hivyo Mill! Nifanyie kama zamani.” Wakasahu kama yupo bedrest, na kama ‘wanamashariti’. Wakaanza kung’ang’aniana kwa uchu. Walifanya mapenzi ila kwa taratibu na uangalifu. Muda wote waking’ang’aniana midomo kwa kiss la msamaha, kujirudi, nilipitiliza hasira, nimekusamehe, nakupenda na ahadi ya kuanza upya kwa vitendo. Ungejua anamuhitaji huyo mkewe, na hapo amefika. Jinsi alivyomshika. Jinsi alivyofanya naye mapenzi, kwa hakika ungejua hapakuwa na kurudi nyuma kwa huyo Pam, shida ilikuwa ni kutengeneza, waendelee.
“Nakupenda Pam. Nakupenda sana.” Ni neno alilokuwa akilirudia kila akimuachia midomo yake, akimnong’oneza kwa upendo asijue ndiyo dawa mkewe aliihitaji. Ile jeuri ilishabadilika ikawa msalaba kwake mwenyewe. Hakuhitaji tena hukumu ingine ila tu muda ili kuonyesha mabadiliko.
Kila kilichokuwa kikitokea na kuzungumzwa baada ya fungate kuharibika akiwa hospitalini alihisi Mungu alimuweka pale makusudi na kumtuliza ili aendelea kuzungumza naye. Mama yake alizungumza mapito yake na baba yake, lakini napo hapo Pam akachukua kama yake. Jerry na kilio chake kwa Sandra, akabeba yeye. Hapo Pam alishashuka moyoni, alichohitaji ni nafasi tu kutoka kwa Mill, Mungu amjalie uhai, aonyeshe kwa vitendo.
Alishafunguliwa macho na kuona kwanza anajipunja yeye mwenyewe kushikilia ugomvi wa wazazi wake, kubeba hasira ya kutelekezwa wakati Mungu alishamtumia mtu kama Mill! Anashindwa kupokea na kufurahia, bado anahofu na hasira ya mambo ya nyuma. Akakusudia kuachilia chuki zote alizobeba kwa baba ambaye mama yake kwanza hataki hata kumkumbuka wala kurudi kwake.
Akajituma hapo taratibu kumfurahisha huyo Mill japo si kama kawaida yao. Maana wawili hao wakianzaga mapenzi, huwa wanaumbali mwingi wanakwenda. Ila usiku huo wa penzi la kwanza, baada ya kufanikiwa kufunga ndoa, wakawa na kiasi. Alimkumbatia vizuri wakati akifanya naye mapenzi, style ya kawaida kifo cha mende, asije tibua kizazi. Aliendelea kumsugua taratibu huku kissing ikiendelea kwa kina na wakati mwingine akimsisimua zaidi akihamia masikioni.
Pam alikuwa akifurahia vile alivyoshikwa, na vile mwili wa Mill ulikuwa mkubwa! Usizo ameegemezea kwenye magoti zaidi na mkono uliopo chini yake alipokuwa amemkubatia, akaweza kumsikia kifuani kwake vizuri, na mara nyingine alimpapasa matiti, na kuamsha raha vilivyo! Na hivi alishakuwa na hamu ya kushikwa huo mwili, alitamani asimalize kwa haraka lakini yeye mwenyewe, akasalimu amri. Naye Mill hakuharakisha, palepale palipotoa matokeo, akaendelea kupasugua mpaka akamsikia amelainika kabisa amejiachia kitandani ndipo akajua amemaliza.
Akamuacha apate pumzi mara hadhaa akiendelea kumpapasa taratibu amejinyanyua. Alipomuona ametulia, akaanza kumkiss tena, hapo akaanza kujipakulia sasa mpaka na yeye akafanikiwa kwa style hiyohiyo, maana hakutaka kumgeuza geuza. Bedrest sex. Akamaliza na kujitupa pembeni.
~~~~~~~~~~~~~
“Kwa mwendo huu nitapona.” Mill alicheka sana. “Sisi wazazi wa ajabu! Siku ya kwanza tu, tushavunja mashariti!” “Nilikuwa na hamu na wewe Mill! Ungeniacha leo ningezidi kusononeka. Nisamehe sikuwa nikijua kama nakuumiza kwa kiasi hicho! Nilikuwa nikikumalizia wewe hasira bila kosa na nilikuwa sijijui.” “Yameisha. Twende tukaoge nije kukupa habari njema.” Wakenda bafuni angalau hata kushikana ikawa kwa upendo. Hawakufanya mapenzi tena ila angalau kulikuwa na kissing nyingi tu.
~~~~~~~~~~~~~
Penzi La Kweli Huhimili Hata Katikati Ya Changamoto.
Na Mara Nyingi Mapenzi Ya Kweli Yaliyopitishwa Kenywe Moto, Hubaki Kama Dhahabu.
Upi Muendelezo Wa Pam&Mill Kuanzia Hapo? Ndoa Huja Na Baraka Zake. Ipi Habari Njema Anayotaka Kumpa Mkewe?
Jo&Dorothy? Penzi La Utuuzimani kila mmoja anayo past yake. Je, Jo atamaliza msiba wa mkewe na kuweza kuendelea na Dorothy kwa wakati na wote kuweza kuvuka past zao na kujenga CHAO wakiwa na kumbukumbu za nyuma?
Je, Jerry & Sandra Nao?
Yapo Mengi Yanaendelea.
Usikose muendelezo...
0 Comments:
Post a Comment