Akiwa kwenye
usingizi mzito, akasikia mlango unafunguliwa kwa nguvu. “Hata kama ni kunidharau
na kuniona sifai, si kwa kiasi hichi!” Raza akakaa kwa mshituko. “Nilikuomba
msamaha, ndio unanirudishia vitu nilivyokupa! Ulitaka nifanyaje? Kwamba unaona
mimi sifai hata vitu nilivyohangaika kuvisaka kwa pesa nyingi
nikijinyima muda wangu, unaona havina maana!?” Akaendelea kulalamika akigomba.
“Kwa kweli sijui
natakiwa kufanya nini hapa duniani! Naona ni kama nimejishusha vya
kutosha!” Akatoka na kumuacha Raza amekaa kitandani ameshikilia moyo kwa
mshituko.
Ndipo akili
ikamjia. Hasira zile si za zawadi aliyomrudishia. Wazi Pius alitaka mambo
yaishe. Ila hali ya uwanaume, anajirudije wakati alimuacha chumbani kwao akiwa
na hasira za wivu juu ya Chezo! Aseme na mimi nimejifikiria naona wote
tunamakosa! Pius! Akajua malalamishi juu ya kurudishwa kwa zawadi
ndio njia ya kurudi na kumtangazia msamaha, akitaka yaishe.
Hata hivyo alimjua
mumewe si muhuni kabisa. Hajui kulala na wanawake mbali na yeye, ndio maana
Mina alimtisha sana Raza. Aliwezaje!?
Akajua hasira
hizo pia nikuzidiwa tu. Na hivi amerudishiwa nguvu zake, anazo za
masaa 24, akajua hizo hasira wala si nyingine. Amezidiwa, na kuomba moja
kwa moja bado ni kama anajishauri kwa Raza. Hasira juu ya Chezo, ila mke anamtaka.
Na Raza alijulia
kumtuliza mumewe. Kwa swala la kitandani tu, alijaliwa mchezo wa ukweli. Hakuwa
mzembe na si mvivu kitandani. Pius alikuwa akirudiwa nguvu ki ukweli,
alikuwa akiweweseka. Ila ni muda mrefu sana wawili hao kufanya mapenzi ya
mwendo mrefu. Ilikuwa kama Pius akifanikiwa, basi hata dakika 5 hamalizi
anakuwa ameshamaliza na hawezi tena kuendelea. Tena mara nyingine Raza alikuwa
akimchezea tu na kumfikisha bila hata kufanya naye mapenzi.
~~~~~~~~~~~~~~
Akatoka hapo
chumbani na kurudi chumbani kwao. Akamkuta amezima taa kubwa amewasha ya
pembeni ya kitanda kama anayemalizia kusoma kitu. “Nilikuwa nikitumia kinga
muda wote. Na pia nilipima kujihakikishia nipo salama.” Akamwambia akikaa
pembezoni mwa kitanda, Pius akimwangalia.
“Nimekumiss Pius!”
Akajilalamisha kusudi kumuonyesha yeye ndio mwenye shida. “Imekuwa muda
mrefu hujanishika mume wangu.” “Wewe si unanikimbia, mpaka umehama chumba!”
Mtoto wa kike hakuongeza neno, akavua nguo hapohapo akimtizama na kupanda
kitandani. Akaanza kumtoa suruali akimvuta miguu ili alale chale. Naye Pius
akajiachia ili ashugulikiwe.
Ukweli Raza
hakuwa na uhakika ana uwezo wa kiasi gani. Alitaka kumnyonya angalau
kumsaidia alale. Yeye hakuwa hata na hamu! Alikuwa amechoshwa na mengi, ya siku
nzima. Tokea adamke asubuhi, kazini, kurudi hapo na kupika! Ya Polla nayo,
kisha kuja kulia hapo kwa mumewe, maombi aliyokuwa akiomba hajui ni lini
atajibiwa, hata mzuka wa mapenzi hakuwa nao.
Ila
akajifanyisha tu ili kumtuliza. Akaanza kumnyonya akimchezea kengele
zake kwa ustadi wote. Ingekuwa zamani kidogo, kwa hakika angeshahitimisha, Raza
alale, lakini usiku huo hola! Mtoto wa kike akafanya yote mpaka midomo
ikaanza kuuma, kitu kimekakamaa, kipo hewani.
Ndipo akaamua kumkamkalia,
amnyongee nyonga mambo yaishe. Kabla hajajiingizia akiwa amechuchumaia, Pius
akamgeuza na kumuweka chali, akaanza romance.
Alifurahi Raza,
hapakuwa na jinsi. Na Pius naye alikuwa taratibu kama ambaye anataka kumthibitishia
Raza, hajazeeka na ni bora kuliko mwizi wake huko nje. Raza
aliimba nyimbo zote usiku huo. Alimnyonya kwa uchu wote. Ile raha ya
kushikwa na mumewe akimromance bila kinyaa ila shauku, Raza alikuwa
akipiga mabao kulia na kushoto.
Alipomgeuza ili
aingie, Raza akaanza kwa kasi akikatika ili tu amfurahishe. “Nashukuru, ila
naomba taratibu. Nimekumiss Raza, nataka kukufurahia. Hatuna haraka. Au
umechoka?” “Nilitaka ufurahi.” “Basi taratibu. Nataka kukusikia mwilini mwangu,
nikufurahie.” Hakuamini! Hayo yakawa mageni kabisa masikioni mwa Raza mwenye
ndoa naye ya zaidi ya miaka 19 umri wa binti yake.
Akamuweka kifo
cha mende, akapitisha mkono chini yashingo yake kama mto, akaanza kumkiss
taratibu kama kumtuliza kabisa huku mkono mwingine ukimchezea titi. Akamlegeza
kabisa huku akimnyonya ndipo akaingia na kumvuta mkono akipishanisha vidole.
Usiku huo Raza
hakuwa akiamini kama ni Pius aliyemuoa kwa miaka yote hiyo! Bwana
alitulia. Halafu akaongeza ufundi kitandani kama ni kwa msichana
mpya kwake kumbe ni yeye mkewe! Yalikuwa mapenzi ya muda mrefu ila ya hisia nzito
za namna yake.
~~~~~~~~~~~~~~
Ukweli wawili
hao hawakuwa na penzi lile la undani tokea mwanzo. Ilikuwa ni kama Raza
ndiye anayebembelezea mahusiano yao. Pius alikuwa wa kubembelezwa wakati wote.
Lakini mpaka wanalala usiku huo, ni kama kitu kipya kikawa kimejengeka
katikati yao.
Na wakati wote ilikuwa
ni Raza kujituma hapo kitandani akimtumikia Pius ili kumfikisha golini
bila kujijali yeye binafsi. Kisha kujipikilisha na kuhakikisha huyo Pius
asiyejua kukaa na njaa anapata milo yote ya uhakika hata kama msichana wa kazi
yupo, basi lazima chakula cha Pius atakisimamia yeye. Na kumtumikia hapo
ndani kama kijakazi wake wala si kimapenzi.
Ila usiku huo
ikawa kama anayelipa deni kwa mkewe. Pius akamuonyesha kitu cha tofauti
kabisa hapo kitandani, mpaka akashangaa kwa furaha.
Jinsi
alivyomshika na kufanya naye mapenzi, ikawa kwa thamani si kufanya ili
yaishe. Alimtayarisha kwa utulivu akimnyonya sehemu alizokuwa akiamsha hisia
kwa utulivu wala si papara. Walilala kimyakimya lakini ungejua hapo kitandani
wamelala wanandoa na si wapangaji wawili waliokubaliana kanisani au msikitini
au kisheria.
~~~~~~~~~~~~~~
Asubuhi aliamshwa
na mikono ya mumewe akimpapasa sehemu za matakoni alipokuwa amempa mgongo.
Akahisi anaota. Lakini akagundua ule mkono umeshafika mbele. Akijitahidi
kupenya katikati. Usiku uliopita alimfuta mumewe vizuri, yeye akarudi kuoga na
kuvaa gauni jepesi la kulalia bila chupi wala sidiria.
Akapenya mpaka
akafanikiwa kufika kunako. Raza akakumbuka mumewe mpenda cha asubuhi.
Akacheka na kugeuka chali. Midomo ikahamia kwenye matiti huku akimchezea
vizuri. Alimnyonya matiti huku akipekecha kidude mpaka Raza akili
zikajua anataka ampigishe bao.
~~~~~~~~~~~~~~
Yeye hakuwa wa
mapenzi ya asubuhi asubuhi. Mwanzoni kabisa wanaoana, ndio ilikuwa kazi hiyo.
Pius hatoki kitandani mpaka apate cha asubuhi. Basi alishamjulia.
Atamtengea. Zaidi kuinama. Akimbana kwa makusudi na kumkatikia kidogo tu Pius
anamaliza. Ndipo anapotoka kitandani na kuanza siku.
Sasa safari za
kikazi zilipoanza kuwa nyingi. Ndipo Raza akaona akammalize nguvu asije
tafuta wa kuwa akisafiri naye, au wakumwamsha huko anakokuwa nje ya nyumbani,
bila ya kujua Pius hakuwa muhuni, yeye mwenyewe Raza alimlemaza.
Alikuwa akimfanyia mambo ambayo kwake yalikuwa mageni kabisa. Pius mwadilifu,
hakupitia wanawake wengi kabla ya huyo Raza mtaalamu wa kitanda.
Na ambao
alishalala nao, wasomi wenzie huko vyuoni zaidi waliyekutana naye nchini
Uingereza alipokuwa akisoma shahada ya pili. Ndiye msichana angalau ungesema
alikuwa na mahusiano naye ya muda mrefu, na alikuwa mdada wa kizungu, kutokea
nchini Poland. Walikutana wote hapo chuoni kwa shahada ya pili. Basi wakaanza
mapenzi na chuo. Walipomaliza ndio kila mtu akarudi nchini kwao na Raza kumdaka
Pius. Pius akiwa na wazo la kuja kumtafuta msichana wake, maana waliishi vizuri
sana lakini Pius alikataa kuishi Uingereza na yeye hivyohivyo.
Irena na yeye
alisema asingeweza ishi nchini Uingereza, lazima arudi nchini kwao. Wawili hao wakaachana
wakiwa wameachiana kumbukumbu nzito za mapenzi, maana waliishi
vizuri sana.
Irena kama maana
ya jina lake lilivyo, kiini cha amani, alijua kumtuliza kweli Pius kwa muda
wote alipokuwa nchini Uingereza. Waliishi pamoja kwa utulivu wa namna yake,
shida tu walitokea nchi tofauti na wote ilikuwa ni lazima warudi makwao.
Pius asingethubutu
kwenda kuishi nchini Poland eti sababu ya mwanamke akiwa kichwa cha familia,
mzee Ruhinda anamsomesha akitegemea arudi nchini aje ashike majukumu mazito
ambayo yeye mzee alishindwa kufikia ndoto zake. Na Irena naye alipelekwa na
serikali yake hapo nchini kwa masomo maalumu. Alitumwa na serikali yao,
walimtegemea arudi nchini kwao kwa makubaliano ya kulipiwa ada lakini ni lazima
kwenda kutumikia serikali yao baada ya kuhitimu angalau kwa miaka 5 ndipo awe
huru kufanya kazi popote.
Japokuwa wote
walikuwa wakisomea shahada tofauti tofauti, lakini waliongozana kusoma kila
mahali na bado waliweza kuishi nyumba moja yaani apartment moja na kufanya
maisha ya shule kuwa rahisi na matulivu.
Raza anaingia
kwenye maisha ya Pius akakuta tayari Irena ameacha kumbukumbu nzito ya mapenzi
tena mwenye machungu. Kwani Pius alifika nchini akiwa bado hajakata tamaa
akiamini watakuja kurudiana na Irena. Alibaki akitafuta njia ya kuja kuwaweka
yeye Irena pamoja wala hakuwa na mpango na mwanamke yeyoye yule. Alikuwepo nchini
akisubiria hiyo miaka mitano iishe, wajipange upya na Irena huku wakiwasiliana
kwa karibu sana.
Baada ya miaka
miwili tokea watengane nchini Uingereza, Irena alipata mwanaume mwingine
akaolewa kitu kilicho muumiza sana Pius. Akasusa kabisa maswala ya
wanawake. Raza alikuja kukutana na Pius aliyejeruhiwa moyo. Akijilaumu kwa hili
na lile juu ya kutengana kwake na Irena. Mpweke. Hajashika mwanamke zaidi ya
miaka miwili.
Irena alikuwa
mzuri sana wa sura. Macho ya rangi ya kijani fulani hivi, midomo mizuri mwekundu.
Pius akakutana na Raza naye amekamilika, ila sasa ikawa zaidi kitandani.
Pius asiyejua mengi akaonjeshwa penzi la mtoto wa Kitanzania. Akaanza
kutafuta muda hata mchana, anamuita Raza akamtulize.
Aliponogewa
akawa akimkaribisha mpaka kwake. Anahudumiwa usiku, asubuhi anaagwa na penzi.
Akamlemaza Pius akawa anamtaka tu kitandani naye Pius anampa pesa kama mchezo
tu.
Pius ametoka
kwenye familia yenye pesa. Mshahara wake haulizwi na mtu na hapo alikuwa
akifanya kazi na mshara wa juu haswa. Raza alipoona huo mjengo anao jenga,
halafu hatangazi ndoa ila kufaidi tu penzi huku bado na hasira za Irena, akaona
ayafanye marefu yawe mafupi.
Shoga yake
akamsindikiza kwa mganga, akafanya yake. Raza mtoto aliyekuzwa na mama mtanzania,
uswahili, maadili kwa mtoto wa kike ni kwa asilimia 100. Shule imekaa
kichwani! Kuja kupelewa kwa kina Ruhinda, na hivi Pius alikuwa amegoma kuoa.
Raza adabu kama mtoto wa Kinyakyusa, salamu mpaka goti, halafu amesoma!
Anajielewa, mama Ruhinda akampigia kifua kwa kijana wake.
Pius akajiambia
maadamu Irena ameolewa, basi yeyote. Akatangaza ndoa na Raza, moyo
kwa Irena. Kwa hiyo wakaingia kwenye ndoa ambayo Pius ni kama ametimiza wajibu,
akipewa penzi tamu, kisha kutoa pesa. Na Raza naye ameingia mjengoni.
Ndoa ya kikristo, tena katoliki, hamna talaka, Pius wake mpaka kifo! Pesa
anayotaka yeyote anapewa. Akabaki akijituma hapo bila kujali hisia zake binafsi
yeye kama mwanamke.
Akajitoa kafara
kwa malipo ya pesa. Anajituma kuanzia asubuhi mpaka asubuhi siku zikienda bila
kufikiana mioyo yao. Raza ni mwanadamu, upweke ukamzidia. Anayo pesa,
hana mpenzi ila ndoa. Ndipo akaja kujitengenezea kundi lake la kumtoa upweke
baa. Akijikuta nyumbani peke yake, pesa ipo, majukumu ya nyumbani ameweka sawa,
Pius ana yake, basi anaenda kwa mashoga zake kunywa na kula baa, akirudi
nyumbani ni kulala. Akimkuta mume anamuhitaji, anamkatia mauno, wanalala.
Maisha yakasonga.
Wabaa hawamfikii hisia zake yeye kama kwanza mwanadamu, pili mwanamke.
Alipokutana na Chezo, na yeye mkewe kisirani. Akianza kugomba mpaka majirani
watajua kwao kuna jambo. Kuzira tendo la ndoa ndio fimbo yake kwa
mumewe. Akimkera tu, hampi tamu.
Ndipo maisha
yakamkutanisha na Raza mpweke ila pesa anayo, hataki kuhongwa ila mtu wa
kumsikiliza tu. Sasa naye Chezo alijaliwa utulivu, halafu mapenzi ya kitandani
kwake ni sanaa kwelikweli. Akimuanzia Raza kichwani ujue atamnyonya mpaka
kidole gumba! Halafu anaweza msikiliza na kumliwaza! Raza anarudi kwake
mwepesi. Maisha ya wawili hao yakaendelea kama wanandoa, ila hakuna aliyepata
moyo wa mwenzie.
Mpaka hapo
majanga yalipowapata na Mungu kuingilia kati ndio Pius sasa kukumbuka romance
za kizungu na penzi la utulivu. Kwa mara ya kwanza akajisikia kitu cha
tofauti kwa Raza. Ndio aina hiyo ya mapenzi hata yeye akajishangaa.
~~~~~~~~~~~~~~
Alimnyonya ziwa
akimchezea kisimi mpaka Raza akapiga bao. Akiwa anahema na bado mbichi
akamgeuza kumuinamisha akiwa amempandisha tu gauni kwa nyuma. Akamkamata kiuno kwa nguvu mpaka Raza alikuwa
akipata shida kukatika! Bwana Pius alijipakulia mpaka akawa anamuamsha tena Raza.
Taratibu, kwa hisia zote, akafanikiwa kumfikia Raza kwenye G spot ambayo
haikutoa bao, lakini raha aliyokuwa akiipata, ilimuacha si mkavu. Hakwenda muda
mrefu sana, mumewe akamaliza na kujitupa pembeni.
“Haya ndio mambo
nilikuwa nakumiss nayo Raza. Ulinizoesha vibaya! Ukanilemaza na penzi
kabla ya kazi. Hivi nini kilitokea?” Yeye Raza alikuwa akikumbuka vizuri sana.
Huko kunogewa ndiko kulikomtisha Raza na kumfunga ili asije kamatwa na
wanawake wengine huko nje awapo safarini.
Akacheka tu
akiwa anajirudisha kulala akihema baada ya kutingishwa vilivyo. Akamvuta na
kumuweka kifuani akihema. “Pumzika hapa kidogo.” Raza alifurahi huyo, penzi na
kuwekwa kifuani! Akajituliza hapo akawa akimpapasa taratibu wakiwa wanajaribu
kutulia.
Akatupia macho
kwenye saa ya ukutani, akajua akiendelea hapo kupendana, atachelewa majukumu ya
hapo nyumbani. “Si unaingia kuoga kabisa au unataka nikusafishe?” “Natulia
kidogo tu ndio nioge. Asante.” “Basi acha mimi nianze siku.” “Hutaki tuoge
wote!” Kwa sekunde kadhaa, Raza akabaki amepigwa mshangao. Hawajawahi
oga wote hata fungate!
“Nisubiri
tukaoge wote.” “Ningependa Pius, lakini nikiendelea kulala hapa jua Polla
anaweza kwenda shule bila kula, tena akachelewa maana haamki amkiamshwa na
mwingine kama sio mimi. Wewe mwenyewe utaondoka hapa na njaa.” “Ujue
umemuendekeza sana Polla, wewe Raza! Umri huo Poliny alikuwa akimka mwenyewe,
anajiandaa, dereva akija hapa anamkuta tayari.” Raza akawa anacheka akielekea
bafuni. “Nilikwambia watoto hawafanani, Pius.” Akabaki hapo kitandani Raza
anaanza majukumu.
~~~~~~~~~~~~~~
Ikawa kama
amejimwagia tu maji na kutoka kwa haraka, yeye akapitiwa tena na usingizi maana
muda wake wa kuamka ulikuwa bado. Akapata usingizi wa asubuhi hiyo tena kama
dakika 45. Kausingizi kazito baada ya sex murua. Alamu yake ilipomuamsha
ndipo akatoka kitandani.
Yaani yeye anatoka kitandani kuoga, Raza
anashugulika kwenye ajira yake ya kwanza. Kuhakikisha Polla ameamka, amejiandaa,
ameshamaliza kumtayarishia kifungua kinywa chake. Akaanza kula huku mama yake
anahangaika hapo jikoni kumuandalia baba yake kifungua kinywa.
Mwajiriwa huyo
kuja kuangalia muda, ameshachelewa. Hana hata muda wa kula. Akarudi chumbani
akikimbia ili kujiandaa. “Vipi?” “Nakaribia kuchelewa.” “Ushakula sasa?”
“Nikisema nikae tu nile, nitachelewa. Nitakula mchana. Ila chakula chako
kipo mezani. Wahi ule kabla hujatoka.” Hayo anaongea akikimbilia tena bafuni kuoga
ili kutoa harufu ya vyakula.
~~~~~~~~~~~~~~
Kidogo Pius
akaanza kumfikiria mkewe. Huruma ikamuingia. Hangaika yote hiyo
ni kwa ajili ya kumuandalia yeye, hata yeye hajala! Akamaliza kuvaa na kumfuata
bafuni. Akamkuta akijipaka mafuta kwa haraka. Alishatoka kuoga. “Nashukuru kwa
kifungua kinywa.” “Mbona kama umekula mbiombio!” “Bado sijala, ndio nakwenda.
Ila nasema asante kwa kudamka, na kututengenezea chakula mimi na Polla.”
Raza hakutegemea.
Huwa anashukuru
akishakula, kama watu wengine. Ila ya siku hiyo aliifanya maalumu na
kumaanisha. “Nakushukuru kujali Raza. Najua ungeweza kuwa na sababu nzuri tu
yakutofanya yote haya kwa sababu hatuna msichana wa kutusaidia hapa kazi.
Lakini kwa kuwa unanijulia. Unajinyima muda wako nakuhakikisha
nakula kitu kizuri. Nguo zangu hazikosi kupelekwa drycleaner. Nazikuta
zimepangwa vizuri, nikajua ni msichana wa kazi kumbe ni wewe! Asante. Nakushukuru.”
Raza akacheka. “Karibu. Nenda ukale usichelewe.” Pius akatoka. Ila alimgusa
vilivyo mkewe.
"Baada ya
Dhoruba, Mapenzi Yamechomoza Tena"
Kwenye mida ya
saa nne, sekretari akapokea fruit basket. Bwana ilionekana vizuri kila
mtu pale ofisini akataka kujua inapelekwa wapi na imetoka kwa nani! Wakamfuata
mpaka ofisini kwa Raza. Raza alikuwa busy, hata hakutegemea.
“Mumeo katuma
mtu akuletee.” Kwa sekunde kadhaa, Raza alibaki ameduaa, asiamini.
Akavuta ile basket karibu. Akakuta kijikadi cha wazi tu kikining’inia
chenye jina kutoka kwa Pius Ruhinda. Raza alitamani kulia, ila akajikaza. Pius
alimfuta machozi na kumtoa aibu kwa hali ya juu hapo ofisini kwao. Maana
alishasemwa sana na wafanyakazi wenzie kuwa mume amemuacha sababu ya kuzaa
watoto wa kike.
Kabla
hajafungua, akapiga picha na kumtumia na ujumbe. ‘Asante SANA kwa
kunifikiria.’ ‘Punguza njaa. Nikimaliza kikao nakuja tukale. Kinaweza vuta, lakini
unisubirie nitakuja kukuchukua tukale wote.’ ‘Nitakusubiri Pius.’ Hakumjibu. Watu wakaondoka mmoja baada ya mwingine wakamuacha Raza kama
haamini!
Kwa Andy.
Wakati mwingine
neno samahani, ni zaidi ya kulitamka kwa mtu uliyemuumiza sana. Pius
alifikiria jinsi ya kujirudi kwa Andy vizuri na kwa heshima, akaona ajishushe,
amuombe msaada, kusudi tu. Akampigia. “Naomba msaada wako.” Kwa sekunde kadhaa Andy alitulia. Ni Pius. Kifedha amemzidi, na
ameshakuwa mjini kwa muda mrefu anajua watu na njia za kumuharakishia mambo.
“Nimependa jinsi ulivyojenga nyumba
yako. Japokuwa ulikuwa busy au haupo mjini uliweza kutumia watu waliokujengea vizuri
na kwa haraka. Tafadhali naomba niige.” Hapo akampata. “Ooh yeah!
Jamaa alikuwa mwaminifu sana. Nilitumia kampuni yake. Naweza kukurushia namba
yake.” “Na unisaidie kunitambulisha tafadhali. Itanirahisishia kuanzia karibu.”
“Haina shida kabisa. Nitazungumza naye, kisha nitakutumia na namba yake.” Hapo wakaanza kwenda sawa.
“Aisee nitashukuru. Utakuwa
umetusaidia sana.” “Ukisema ‘uta’, unamaanisha na mzee?” “Hapana. Ni nyumba ya
Raza. Nataka kumuunga mkono.” “Mpe hongera sana. Ujenzi siku hizi ni garama
sana. Kujenga ni kujimaliza kabisa.” Akasikika ni
Andy aliyetulia si mwenye uchungu.
“Atasikia. Vipi Ayan na mdogo
wake?” Kitu ambacho hakutarajia akamsikia Andy
akicheka. “Vipi?” “Ayvin! Ayvin mtundu sana. Huwa ananikumbusha Mina wa
kwanza niliyekutana naye. Mchokozi na mtundu wakupitiliza. Si
unajua anatambaa sasahivi!” “Aisee! Tayari!?” Pius
hakuamini, ila Andy akazidi kucheka.
“Sasa Ayan anampenda sana,
ila ni mkimya na anapenda akifanya kitu chake, atulie kabisa, na mawazo apeleke
kwenye anachofanya. Azingatie kabisa. Sasa Ayvin hawezi kaa sehemu moja. Akimuona
kaka yake ametulia anazingatia jambo, anakuwa kama anamnyatia, anamfinya. Sasa
jificha yake eti kaka yake asimuone alivyomfinya ndio utacheka.” Andy mwenyewe akawa anacheka.
“Na akianza kucheka. Hata kama
humuoni, utajikuta huko ulipo unacheka tu. Na hata kama upo kwenye simu,
utajikuta unacheka mpaka uliyenaye kwenye simu anaweza asielewe. Anacheka yake
hiyo, halafu kwa sauti. Atacheka mpaka eti anajilaza chini kabisa. Yaani hata
kama una stress, ukiwa naye yule, zinaisha. Nimemrikodi, kicheko chake
ndio nimefanya ring tone yangu.” “Haiwezekani Andy!”
“Nitakutumia video zake. Huwa
nawachua yeye na Ayan, wakiwa hawajui. Tunaishia kucheka na Mina tukiwa wenyewe
chumbani, tunakuwa kama wajinga vile! Hata nikiwa kazini naangalia, nakucheka
peke yangu. Mtundu sana. Halafu mchekaji. Acha nikutumie.” “Nashukuru
sana.” Kwa hakika Pius hakutegemea.
“Halafu ana akili sana. Amemsoma
mama yake, ameshajua huwa anachanganyikiwa akilia. Basi anatumia kilio chake
kama silaha kwa mama yake. Na nimemwambia Mina. Ayvin anaakili
sana. Ashakusoma. Ashajua udhaifu wako. Akimuona mama yake, hali kabisa.
Chakuwa cha usiku huwa namlisha mimi au dada yao, Mina asiwepo. Na
atakula vizuri tu. Akimuona mama yake, ndio mwisho wa chakula, anataka
nyonyo tu.” Pius akawa akicheka.
“Hii nakutumia sasahivi nikiwa
nawaogesha kwenye sinki, Mina alituchukua. Utacheka sana. Huwa nawajazia povu
kwenye sinki la kuogea bafuni kwetu, nawatupiaga hizo toi humo ni za plastiki,
kama hizo za bata, zinakuwa zikielea, kisha nawaweka wote wawili kabla ya
kulala. Inanirahisishia muda. Sasa muone jinsi alivyojitwisha povu kichwani na
usoni, halafu anavyofanya kusudi kumwaga sakafuni ila eti kwa siri maana
nilishamkataza. Sasa wakati nikimsugua mwenzie, yeye ndio anafanya hivyo na
kuficha toi. Nikimgeukia, ndio kicheko hicho.” Ungejua
Andy amepata faraja.
Alikuwa
akisimulia huku akicheka kwa furaha. “Siku za ijumaa, huwa
nawachelewesha kulala makusudi. Maana anapenda sana michezo. Na nyumba
ikichangamka, hata ufanyaje, hutamuweka kitandani kwake akalala.” “Analala bila
kubebwa?” “Ila kusiwe na shuguli nje. Huwezi mfungia chumbani eti awaache
nyinyi mnafurahia nje! Hapo humlazi. Atataka kutoka tu. Ukitaka alale, aone
nyumba imepoa. Taa zimezimwa. Kumetulia. Hapo ukimuweka kitandani, ukamsomea
kitabu, atalala bila shida.”
“Sasa siku za ijumaa au wakati
mwingine jumamosi, nawafanyia kusudi kuwachelewesha kulala ili tuwe nao muda
mrefu usiku. Wakati mwingine Mina yeye analala, ananiacha nao. Sasa akiwa
amechelewa kulala, ajue asubuhi atachelewa kuamka. Hapo nyumba haikaliki bila
yeye.”
“Mimi na Ayan kila wakati tunaenda
kumchungulia kila wakati, tunataka aamke, aanze fujo zake, pachangamke.
Tunajikuta mimi na Ayan tunapeana zamu ya kwenda chumbani kwake mpaka Mina
anagomba. Maana jumamosi siku ya usafi. Ukimtoa Ayvin kitandani kwake, ujue
atazagaa hapo, anataka michezo hakuna kitakachofanyika.”
“Tukifanikiwa kumuamsha,
Mina amekasirika. Ujue hapo nitafungashiwa, na kutolewa naye hapo ndani,
tunaambiwa tuhamie barazani. Naye hana neno. Akianza kucheka barazani, wenyewe
wanatufuata nje. Wanamtaka.” Pius akawa akicheka.
“Bado anakubali kila mtu?” “Hapana.
Amebadikika sana aisee! Kama hakujui, akikuona, anataka nimshike mimi au mama
yake kama yupo karibu. Basi hapo atajificha begeni mpaka mgeni aondoke. Hataki kushikwa
na mgeni. Sura alizozoea ndio hizohizo. Ila babu yake na bibi yake hawasahau.
Baba huwa anacheka hapa, mpaka anaondoka akicheka. Mama huwa anasema hajawahi
ona mzee Ruhinda akicheka hivyo.”
“Kumbe huwa wanakuja kuwaona?”
“Sana tu. Tena siku hizi baba wala hafikii hotelini. Hapahapa alipo cha uchokozi.
Tena mara nyingine anaweza akaja katikati ya juma, utafikiri ameshastaafu jinsi
anavyokuwa ametulia hapa. Namuuliza, ‘huna
kazi mzee Ruhinda?’ Atacheka tu na kuendelea na wajukuu zake. Yeye zaidi kuliko
mama.” “Mama kazi!” “Anavyosema. Ila anasema akijisikia stress zinamzidia
ndio anakuja. Zaidi weekend. Anaweza akaja ijumaa usiku, anaondoka jumamosi
usiku kuwahi misa na wakati mwingine huwa wanaondoka jumapili jioni, misa
wanafanyia hukuhuku na wajukuu zao.” Akamsikia Pius
akicheka.
“Umeamini sasa?” “Ujue anaakili
zaidi ya umri wake!” Pius akaongeza akicheka. “Nakwambia ni
Mina mtupu. Lakini eti anakataa. Anasema yeye alikuwa mtoto mzuri. Roni ndio
huwa ananisaidia kumkumbusha.” “Na Roni huwa anakuja!?” “Sio sana. Ile kazi
niliyomuachia kule inambana! Ila mama yao alikuwa hapa zaidi ya mwezi.
Mina aliugua sana.” “Nini tena?!” Kidogo Pius
akashituka.
“Ni mjamzito. Alikuwa akitapika,
hakuna kinachokaa tumboni. Sasa mimi mwenyewe kazini, Ayan wakumtuma angalau
maji ya kunywa anakuwa shuleni na Ayvin ni wa kumuangalia masaa yote mpaka
alale. Msichana wa kazi naye anakuwa na mambo yake. Mina alilemewa. Ndio
mama yake akatusaidia.”
“Hongereni sana.” “Asante.”
“Anaendeleaje sasahivi?” “Mzima na ananyonyesha kama kawaida.” “Ananyonyesha
tena!?” “Huna lugha ukamwambia Ayvin akaelewa anapokuwa na mama yake, asinyonye.”
“Si angempa maziwa mengine?” “Yote anakunywa. Na si unamuona mwili huo?”
“Amekuwa kibonge!” “Bibi yake alimwanzishia ugali wa dona. Mama yake
asipokuwepo, anakula kila kitu. Lakini akiwa na mama yake, ni nyonyo tu. Na huna
utakalomwambia Mina kwa wanae. Ana jinsi yake kwa watoto wake, ukimrekebisha
anakosa raha kabisa!”
“Huyo Ayan baba mzima, mpaka leo,
hata akitoka shule. Akiogeshwa, akilishwa, anapewa chupa ya maziwa, Mina anakaa
naye mahali, basi anamuacha anyonye hayo maziwa huku akimnusa mpaka
alale.” “Mpaka leo!?” “Mpaka hivi mchana atakaporudi kutoka shule.” Pius akacheka sana.
“Baba ameniambia nimuache tu. Namuuliza
hawatakuwa wazubavu? Akasema wanaakili sana. Washamsoma mama yao, wamejua hiyo
ndio njia ya kumfanya awe karibu nao.” “Akijifungua sasa?” “Hata sijui
Pius! Namuona habari iliopo akilini mwake ni kulea tu hao watoto, na wala si
ajira ya nje ya hapo. Anawamudu vizuri tu na yeye mwenyewe anaafya nzuri tu.
Hajachoka.”
“Mmeshajua mnatarajia mtoto gani?” Akamsikia akicheka tena. “Amejua jana, naona kama hajafurahia!”
“Dume jingine tena nini?” Andy akacheka sana. “Alikuwa
ameshaandaa jina la mtoto wa kike. Akawa akimshika na kumuita Ayana. Kutwa
anawafundisha wanae kuwa ni Ayana, dada yao. Sasa jana kwenye Ultrasound
tumejua ni wa kiume, aisee amepoa sana. Japo hajasema, ila amebadilika.
Nimeona nimpe muda aingize taarifa kichwani, azipokee ndio nianze kumkumbusha maswala
ya jina la huyu mtoto maana yeye ndio hodari wa kutengeneza majina yao.” “Aisee
hongereni sana. Bora ni mzima.” “Nakutumia
hii nyingine na babu yao. Utamuona mzee Ruhinda anavyocheka.” Akamtumia.
Yaani jinsi
alivyozungumza juu ya Ayvin mpaka Pius akafurahia na kutamani kwenda. “Mnampango
wa kurudi huku Dar?” “Aisee namshukuru Mungu, nimepata nafasi ya juu zaidi huko.
Natakiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao. Mina amefurahi sana.” “Naona sisi
tutakuja week ijayo. Acha niweke mambo ya nyumbani sawa, tutakuja
kuwaaona kwa zile siku mlizonipa.”
“Nyinyi karibuni muda na wakati
wowote ule.” “Una uhakika Andy? Maana ni kweli siku za kazi ni ngumu.” “Nyinyi
karibuni tu.” Hilo alilifurahia sana Pius. “Uwe
unanitumia video zake huyu cha utundu na kaka yake. Ni kweli
zinabadilisha siku.” “Umeonaa! Hiko kicheko kikikukuta katikati ya siku ngumu
ya kazi, unajikuta mambo yanaenda.” Pius akacheka
na kuagana naye.
Kwa Mkewe.
Akatoka kumfuata
mkewe kwa ajili ya chakula cha mchana. Akiwa njiani akapokea simu ya mtu
aliyejitambulisha ametumwa na Ruhinda, ana kampuni ya ujenzi. Akajua ni Andy
tu. Wakazungumza na kujipanga ndipo akawa amefika ofisini kwa mkewe. Akaamua
kwenda kabisa mpaka juu ilipo ofisi ya mkewe.
Kama kawaida
yake akaanza utani kwa sekretari wa ofisi. Pius alikuwa mcheshi na wakati
mwingine ilimlazimu kuanzisha mazungumzo ya kawaida ilimradi tu kufanya
apokelewe bila tension kwenye sehemu anazoingia na wanazo mfahamu yeye
na wadhifa wake.
Vikajaa vicheko
Raza akisikiliza ofisini kwake, kidogo akasikia kama ukimya wakizungumza kwa
kuteta. Akatulia kabla hajanyanyuka kujua kulikoni, isijekuwa ni surprise
akaharibu. “Naomba nimfuate ofisini kwake. Usimuite. Si yupo?” “Yupo.” Pius
akaamua kwenda kusudi tu kuweka furaha kwa mkewe.
Raza alifurahi
kumuona ameingia mpaka ofisini kwake na kusimama mbele ya meza yake! Kama
hakutegemea! “Ungenipigia nikakufuata chini. Usingehangaika kuja mpaka huku juu
tena.” “Umenisubiria vyote hivyo, na bado unifuate!” “Nisingejali. Kwanza
nilikuwa busy na mimi.” Akasimama na kuchukua mkoba wake iliwatoke.
Akamvuta karibu.
Akamshika kiuno, akamdaka midomo. Raza hakuamini maana alidhani ni ya
juu tu ya mdomo maana hapo kulikuwa na watu wengine! Ila akashangaa vinakuwa vya
muda haswa kama aliyekuwa na hamu naye wakati na asubuhi waliyamaliza
kitandani!
Bwana alimnyonya kwa utulivu, ya kizungu
matupu! Raza hakuamini, maana haijawahi tokea. Ikawa kama ndio
wanaanzana! Eti Pius kama anayetongoza tena! Alifurahi Raza, alifurahi
sana. Pius alitoa ujumbe hapo na kwa haraka sana akarudisha heshima
ya mkewe. Alifanya kwa utulivu ndio akamuachia. “Pole na kazi.” Wakamsikia
akimwambia mkewe taratibu wakati akimuachia. “Asante. Na wewe.” Wakawa wanatoka.
~~~~~~~~~~~~~~
Njiani Raza
alikuwa akichekacheka nakushindwa kujizuia mpaka wakafika kwenye mgahawa wa
hadhi ya Pius. “Nimezungumza na contractor ambaye ndiye atakaye malizia
nyumba yako.” Raza akakaa sawa kwa mshituko na kumtizama. Maana walipofika hapo
na muhudumu kuwaletea juisi walizoagiza kwa haraka tu ndipo Pius akampa hizo
taarifa.
“Mambo ya contractor
tena! Itakuwa garama Pius! Mshahara niliotoka kulipwa ni kama wote
nimetumbukiza huko. Ndio maana nilitaka kukutana na Chezo ili…” Bwana Pius
nusura aanguke pressure. “Unasemaje Raza!?” “Unapandisha sauti, kila mtu
ametugeukia sisi. Tulia tuzungumze.” “Wewe unataka kunichanganya bila
sababu. Na nikichanganyikiwa mimi, jua na mimi nitamfuata mbele ya bosi wake.”
“Hiyo sauti bado ni ya juu sana kwa mazungumzo ya amani, yanayo tafuta suluhu.”
“Basi SITAKI
suluhu na yeye. Mwizi mkubwa asiye na nidhamu. Anaye…” “Pius!
Tafadhali tulia na punguza sauti. Niambie kile unachotaka tufanye.”
“Nishakwambia, lakini unaona msaada wangu mimi si kitu ila wake. Unaona
mimi sifai. Yeye ndio anafaa. Unanidharau Raza. Unataka
nifanyaje?!” “Tulia. Na HAPANA Pius! Sikudhara
mpenzi wangu. Ungejua ulivyoweka furaha moyoni mwangu! Sema nafikiria swala la
pesa. Nilitaka kujua kama bado hajawapa mafundi na kufanya manunuzi mengine aache
na anirudishie pesa yangu. Maana yeye ana usafiri wa ofisini kwao na ana
muda. Ananunua na kupeleka kule bila shida. Na sijamtafuta kwa heshima yako.
Nilitaka kuzungumza na wewe kwanza.” “Basi mimi SITAKI.” “Sawa.” Raza akakubali
bila kelele.
“Kama ungekuwa
hujakasirika ningekuuliza juu ya pesa yangu niliyompa. Lakini naona
nikuache kwanza. Maana pesa yangu inaniuma Pius! Ni mshahara wangu karibu wote! Utakuwa kama
unapotea hivihivi!” “Acha upotee. Ndio kujifunza kutokana na makosa.”
“Sawa. Kunywa basi hiyo juisi. Inaonekana nzuri kweli!” Akabadili mazungumzo.
“Nimefurahi
sana.” Akajaribu kumtuliza. “Nini?” “Kuniunga mkono kwenye ujenzi.”
“Nimejivunia sana. Unaakili. Sikutegemea. Hata Andy nimemwambia.” “Andy!?”
“Ndiye aliyenipa huyo contractor. Ndiye aliyemjengea nyumba yake ile ya
Kigamboni.” Raza akashangaa sana.
“Pius wewe
unataka mambo makubwa sana! Picha uliyonayo ya nyumba ninayojenga si hata nusu
ya ile ya Andy.” “Usiwe na wasiwasi. Ndio tutakwenda kuiangalia halafu
atatushauri. Kama walikuwa wakikuibia cement wanajenga kwa mchanga tu, ndio
itabidi uanze upya. Na usiogope garama. Mwenzio nitakuwa natumia hiyo
juhudi yako kuwafundisha binti zangu. Kuwa unaakili ya maendeleo.
Umetumia pesa yako vizuri kufanya kitu kikubwa.”
“Pius! Unavyokuza!
Acha uone nyumba yenyewe kwanza!” “Hakika si jambo dogo. Na tutaijenga iwe
nzuri sana. Wakija kuioa, wajue unaakili sana ya maendeleo. Waige.
Nimefurahi sana. Hongera.” Raza akajisikia vizuri. Akamuona Pius anacheka.
~~~~~~~~~~~~~~
“Nini?”
“Nimemuomba Poliny aje atukalie na Polla, kuanzia leo usiku, ili sisi
tukapumzike sehemu, anasema hataweza. Namuuliza kwa nini! Anasema kwanza
Polla mwenyewe hatakubali kumsikiliza. Akimwambia asome vitabu atakataa
ndipo watakapoanza kugombana, kisha kupigana. Ataanza kulia
anamtaka mama yake, huo usiku utakuwa mrefu, hapata pambazuka. Na itabidi
walinzi wote wahamie kulinda ndani na si nje.” Raza alicheka ila kwa mshangao
asiamini.
“Ulitaka tutoke
kabisa?!” “Tumekuwa na wakati mgumu sana. Najihisi ni kama
tulishapotezana japo tulikuwa tukiishi nyumba moja. Nataka muda na wewe Raza.
Tukumbushane nia ya kuona. Tuanze msingi upya. Unaweza usiwe kama
mwanzo, lakini utakuwa mwanzo wetu mpya na naamini utakuwa mzuri zaidi.”
“Nataka twende
sehemu utakayopumzika tu. Hakuna kupika kwa muda wote huo. Na wewe
unaagiza na kutumikiwa kama sisi unavyotufanyia. Nimemwambia sekretari
wangu anitafutie sehemu watakayokupatia full spa. Wakuminye huo mwili na
kukutoa stress zote. Wakutengeneza mpaka ukirudi hapa, unajisikia una
mwili mpya.” Raza alifurahi, alifurahi sana. Kwa hakika
hakutegemea.
~~~~~~~~~~~~~~
Baada ya miaka
ya majaribu na machozi, hatimaye wajikuta wamesimama tena bega kwa bega, mioyo
yao ikiwa imeunganishwa na nguvu mpya ya upendo wa kweli. Walitambua kwamba
kila maumivu waliyopitia yalikuwa darasa lililowaandaa kwa mwanzo huu mpya —
mwanzo uliojaa matumaini, msamaha, na ahadi ya kushikamana zaidi kuliko hapo AWALI.
Jua
lilipochomoza juu ya maisha yao mapya,
WOTE (Love at
first Sight), walitabasamu, wakijua kuwa safari yao haikuwa ya kumalizika, bali ya KUANZA UPYA kwa
upendo uliopevuka na usiovunjika.
USIKOSE Fungate Ya Pili Na Mwanzo Mpya Wa Raza Na Mumewe.
Mungu ajibuye kwa wakati wake, amemjibu Raza kwa MOTO.
Usipitwe na
yale aliyoandaliwa na mumewe.
0 Comments:
Post a Comment