Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Love At First Sight - Sehemu ya 55. - Naomi Simulizi

Love At First Sight - Sehemu ya 55.

Ikawa kama aliyekuwa ametegesha saa. Saa 7:30 mchana Pam akawa anashushwa kwenye gari anajivuta ndani taratibu na kiatu chake cha juu, taratibuuu mpaka ndani. Fatma akamkimbilia ofisini kwao.

“Nini wewe?!” “Kumbe lile toto kule ofisini kwa bosi, kumbe lako!” Pam akashituka. “Shema amekuja?! Mbona sijui?” “Sio leo na wewe! Ila hapa ashakuja akazunguka na baba yake zaidi ya mara moja!” “Wewe maneno mengi ushamchanganya mwenzio. Anazungumzia picha ofisini kwa Mkuu.” Pam akakunja uso. Hata hakuwa ameona hizo picha! Kwanza aliingia tu mara moja, napo hakuangaza macho.

“Alikuja mwanao hapa, ikawa gumzo! Toto zuri hilo! Sasa kila mtu akawa anasema lazima mama yake atakuwa mweupe sana au mzungu. Maana kafanana na baba yake mpaka kucha ila yeye akicheka anabonyea na ni mweupe pee! Kumbe mwanao! Halafu hata usitukonyeze kama kumbe wewe mzazi mwenzie bosi! Unaniacha nabwatuka tu!” “Akitoka, akakukuta hapo! Utamkorofisha zaidi. Rudi pale mbele Fatma, acha umbea!” “Baadaye tutaongea zaidi shoga.” “Wala hakuna lakuzungumza, wewe kafanye kazi, acha umbea.” Akacheka na kukimbia kurudi mapokezi.

“Huyu nani kamwambia yote haya na kumpa pressure?” “Bwana unatafutwa wewe!” “Na nani?!” Akasimuliwa kila kitu wakinong’ona. Pam akacheka na kutingisha kichwa kwa masikitiko wala asijibu. Akakaa.

“Anakuulizia kila baada ya dakika! Nenda Pam, asije akasema sijakwambia.” “Nitakwenda acha nikuuu..” Akaingia Mill mwenyewe.

~~~~~~~~~~~~~~

Penzi la kweli ni kama jua nyuma ya mawingu. Unaweza kujaribu kuficha, lakini mwanga wake huvuja polepole, hadi uangaza kila kona ya moyo. Macho hujieleza, hata midomo ikinyamaza. Kila tabasamu, kila sauti ya moyo, hufichua siri ambayo roho imebeba kimya kwa muda mrefu. Ni NGUMU kujizuia, maana penzi la kweli haliwezi jificha. Hujidhihirisha katika kila pumzi, kila tazamo, na kila hatua inayokukaribia.

“Kumbe umerudi?” Wakashangaa anauliza kwa kujikomba. Wala si hasira! “Muda si mrefu. Ndio nilitaka nimalizie kukabidhisha hapa, halafu nije ofisini kwako maana niliambiwa ulikuwa ukinitafuta.” “Nilipatwa tu na wasiwasi, niliona hurudi muda wako ule wakawaida. Nikadhania umepatwa na matatizo.” Kina Mbise wakaangaliana na kuinama.

“Nilipitia kula. Na nilimuaga na Mbise.” “Ulienda kula wapi?” Pam akaanza kucheka na kumgeukia vizuri. “Ni nini Mill!?” “Wewe nisaidie tu kunijibu mpaka na lile jibu la swali unalojua linanikera ila sijui jinsi ya kuliuliza au nasita kuliuliza.” Pam akamwangalia na kutingisha kichwa kama anaye msikitikia.

“Pam?” “Unashida wewe!” Akamwambia akimsikitikia. “Kwani mimi nakataa! Wewe nijibu tu roho yangu itulie.” Wote wanawasikiliza ila hawawaangalii. “Pam?” “Nilikutana na Eric siku ya ijumaa. Akaniomba tuzungumze. Nikamwambia nina haraka. Tukapanga tukutane leo. Haya, umeridhika?” “Mimi nilikuwa na wasiwasi na usalama wako tu!” Pam akamtizama kwa kumsuta.

“Kweli tena! Sasa umeniletea na mimi chakula?” “Wewe si huwa unatoka na Brenda kila siku kwenda kula?!” “Pam naye! Jambo haliishi! Mambo ya zamani hayo!” Akamtizama na kunyamaza. Maana walikuwa wakizungumzia mambo yote, hapohapo mbele za watu.

Lakini akawa hajamuelewa. “Brenda habari ya zamani tena!” Akawaza na kuendelea kupanga karatasi alizotoka nazo benki. Akajibaraguza hapo, akaondoka lakini safari hii akionekana ametulia. Pakazuka ukimya hapo, kila mtu heshima ikaongezeka kwa huyo Pam. Kwamba ni zaidi ya Brenda tena! Kila mtu kimya akiwaza lake.

Love At First Sight.

Pam yeye akaendelea na shuguli zake kama kawaida heshima kwa Mbise kama kiongozi wake tu. Ilipofika mida ya saa 9:30 jioni, Mill akarudi na maua kibao, tena fresh, roses nzuri haswa na chokleti. Akaingia nayo hapo ofisini. Pam alishituka, moyo ukafanya paa! Kama kulikoangushwa chuma sakafuni.

Hata giza lina mwisho wake, na moyo uliojeruhiwa hujifunza kupiga tena. Mill alijikaza kiume na kuamua kukusanya vipande vya penzi lililokuwa limesambaratika kwa muda mrefu sana, lakini liligoma kufa katika dhorula kali iliyopitishwa. Kwa nje ilionekana  ni kama makumbi ya nazi tu, maganda yaliyotupwa juani kwa muda mrefu, baada ya nazi kufuliwa na kuishia kukauka kabisa. Lakini Mill alijua nguvu yake. Alijua kwa hakika, yakiokotwa kwa garama yeyote ile, huweza washa moto mkubwa tu.

“Naomba msamaha.” Pam akakunja uso akimtizama kama ambaye hakutegemea kabisa. “Samahani kwa kutokukueleza kilichokuwa kikiendelea kwenye utaratibu mzima nilipokuwa ugaibuni. Samahani kwa kutokukuelewa tulipokuwa mapumzikoni Arusha, ambako ulinieleza tokea Lushoto. Samahani kwa kukukasirikia.” Pam akacheka taratibu na kutingisha kichwa kwa masikitiko.

“Sijamaliza!” “Sasa wewe ulikasirishwa na nini?” “Acha nimalizie. Samahani kwenye swala la kuhama.” Kila mtu alikuwa akisikiliza ila kichwa chini. Kwa asili hiyo ofisi ilikuwa kimya, wageni ni wachache sana.

Samahani kwa swala ya Brenda. Nakuahidi hapa na popote alipo Shema, hutamuona tena.” Wote wakashangaa Pam anainama tu bila ya kusema kitu. “Samahani Pam wangu.” Akarudia ila safari hii kwa KUBEMBELEZA haswa, tena kimapenzi wala si kama bosi. Pam akaondoka kabisa hapo na kuelekea chooni. Mill akaacha hayo maua hapo na chokleti kwenye meza yake, akaondoka kurudi ofisini kwake. Hakika walizua ukimya hapo! Saa 10 kamili isivyo kawaida yao, watu wakaanza kutoka kimyakimya. Pam akabakia wamwisho akijua Mill yupo ofisini.

Penzi Lililogaramiwa.

Kuomba msamaha kwa umpendaye si udhaifu, bali ni USHAHIDI wa UKUBWA wa moyo. Ni kama mvua laini inayotuliza ardhi iliyopasuka. Hubeba matumaini mapya, huponya majeraha ya ndani kabisa. Katika MSAMAHA huwa kuna NAFASI ya kuanza upya, kujenga tena daraja lililovunjika kwa maneno na matendo. Kwenye kuomba msamaha ndipo kwenye kuonyesha kuwa penzi lako lina thamani kuliko makosa yako.

Akajisafi kama aliyejua kinachofuata na kumfuata ofisini kwake. Walibakia wawili tu upande huo wa ofisi. Akagonga taratibu. “Karibu Pam.” Akamkaribisha akijua wazi atakuwa ni yeye tu. Akafungua na ndio kwa mara ya kwanza akaangaza macho na kuona picha za mwanae. Moja kubwa ilikuwa ukuta unaoangalia meza yake. Shema alikuwa amevaa jezi ya mpira. Akapigwa picha akiwa anapiga teke mpira. Aliyempiga aliwahi vizuri, akamtoa huyo mtoto vizuri sana. Ilijaa hapo ukutani karibia urefu wa huyo mtoto mwenyewe. Pam akabaki ameduaa akiangalia.

“Nilikuomba msamaha Pam!” “Mbona hakuna hapa picha yangu hata moja!?” “Nilikuwa sijui chakufanya na wewe Pam! Nilikukuta katikati ya mambo mengi! Hata mpaka sasahivi sijajua nafasi yangu kwako ni ipi! Ila jua Brenda nilimalizana naye rasmi jana, nilipotoka pale kwenu, mliponigomea wewe na mwanao. Kwa hiyo sasahivi ni mimi tu. Na ili usinipatie sababu.” Pam akabaki akimsikiliza na cheko la kike.

“Siku ile uliponipa matokeo yako ya UKWIMWI, nusu nilie. Maana ndio nilikuwa kwa mara ya kwanza, nikiwa nishapima na yeye, nikataka kwenda kulala naye, maana nilizidiwa mpaka mwisho, halafu eti na wewe ukaniwahi unanipa habari zako!” Pam alicheka sana.

“Usicheke Pam! Mimi mpaka nikajiambia nina mkosi! Maana nilishatafuta sehemu. Nikamwandaa mtoto wa watu, kuwa tunakwenda kupumzika, narudi kwenye gari naahirisha! Halafu sina sababu ya kueleweka!” Pam akaanza kuvua chupi mbele yake. Mill akapigwa na butwaa.

Na yeye akafanya kusudi, akawa anavua taratibuu huku akimwangalia. “Uvuaji gani huo wa ndani kwa ndani Pam! Vua nione inapotokea sio uingize mikono ndani ya gauni kama kunikomoa bwana!” Pam alicheka mpaka akaacha. “Acha bwana kucheka Pam! Hali mbaya!” “Nakuonjesha kidogo tu, kukupunguzia. Mengine baadaye.” “Hapahapa?!” “Sasahivi!” Mill hakuamini. “Libarikiwe tumbo lililokubeba.” Pam akaanza kucheka tena.

Mill akasimama kwa haraka. Akafunga mlango kwa haraka na kuvua suruali kama iliyoshika moto. “Naomba usitoe hicho kiatu na hilo gauni! Vimenichanganya, nilikuwa situlii hapa ofisini. Nakutaka hivyohivyo, kasoro tu chupi, toa.” Akamalizia kuitoa akiwa bado na kiatu chake kirefu. Mill akamdaka. Akaanza kumnyonya kwa pupa.

“Taratibu bwana Mill! Utaniangusha!” Alichofanya ni kupiga magoti mbele yake. Akaanza kumpapasa miguu akipandisha mpaka kwenye tako. Mikono ikawa ikitembea mapajani mpaka kwenye ule mguu unaomchanganyaga asijue raha anayoiacha kwa Pam. Aliendelea kufanya hivyo kwa hisia zote huku mdomo ukiendelea kunyonya kwa uchu kama ambaye haamini! Yaani yeye mwenyewe Mill alikuwa akipagawa, huku akiacha raha kwa Pam.

Mwili wa Pam ulikuwa ukiachia hisia hizo! Hakutarajia kama angeshikwa tena na Mill ambaye alishajua amempoteza kwa Brenda. Hakuchukua muda akasalimu amri mdomoni kwa Mill akiwa bado amesimama vilevile mwenzie amepiga magoti mbele yake. Mill akamshikilia vizuri asianguke maana alilegea haswa huku anammalizia kwa kumnyonya kwa nguvu akiwa anajua ndio yupo juu kabisa kileleni. Akafanya hivyo mpaka Pam akamaliza kabisa ndipo akamuachia na kusimama.

Jinsi alivyo na umbile kubwa akamnyanyua kama mwewe anavyochukua kifaranga, akampandisha juu kama aliyempakata akiwa amesimama na kujiingizia akiwa amesimama vilevile, bado Pam anahema baada ya bao la nguvu. Kazi yote alifanya mwenyewe akiwa amembeba Pam juu juu akiingiza na kutoa kwa mzuka wote akiwa ameshikilia matako ya Pam. Hata kwa Pam yalikuwa mageni!

Alifanya hivyo kwa muda Pam akiwa amemkumbatia shingoni akimuachia afanye atakalo, mpaka akamaliza akiwa amembeba vilevele! Alimwaga mpaka sakafuni. Akamuweka Pam kochini, kisha akatoa shati na singlendi.

Akamgeuza. Akawa amepiga magoti kochini na viatu vyake vilevile. Akamnyanyua tena gauni kwa nyuma bila kulivua, akaingia kwa uchu. Bwana Mill alikuwa akiita Pam, kama ungekuwa ukipita nje, ungesikia. Aliita mpaka akapata la pili, kisha akajitupa pembeni, na kumvuta Pam, akampakata akihema.

“Asante Pam wangu. Nashukuru mama. Najua sijakutendea haki, ila nimeshindwa aisee! Mbali na hali mbaya niliyokuwa nayo, leo hivyo ulivyovaa, umenitesa siku nzima!” Pam akacheka taratibu na kuanza kumkiss masikioni na shingoni ndipo akahamia midomoni. Akamnyonya midomo kwa hisia hizo, hata Mill alijua na yeye anamuhitaji. Lakini akamuachia. “Nina hamu na wewe Mill! Nina hamu na wewe sana! Ila Mwanao atarudi akute mlango umefungwa. Acha niwahi nyumbani.”

“Naomba niendeshe! Nina hali mbaya, nimetoa, mpaka miguu haina nguvu.” “Nikuendeshe mpaka wapi?” “Nyumbani kwenu. Labda nikifika nitakuwa nimepata nguvu ya kwenda kwangu.”

Akachukua ileile singlendi yake akamfuta nayo. Kisha akaingia chooni kwa Mill hapo ofisini kwake, akaiosha tena na kurudi kumfuta vizuri mpaka akatakata. “Asante mpenzi wangu! Haya ndio mambo yaliyokuwa yakinifanya nikukumbuke.” Pam akarudi kujisafi, safari ya kwake ikaanza.

~~~~~~~~~~~~~~

Wala hawakufika mbali, alichokifanya Mill ni kulaza kiti chake, Pam akashangaa anapotelea usingizini akamuacha akiendesha. Alilala Mill wala asijue alipo! Pam akaendelea kupambana na foleni akiwa amemuwashia A/C kama apendavyo. Baridi hapo garini kama ndani ya fridge.

Uzuri akawahi kabla ya Shema. “Mill, tumefika. Nenda nyumbani ukapumzike.” Akakaa akiangaza macho kujua walipo. “Tupo Kinondoni.” “Ni sawa nikalala hapa kwako kidogo nipunguze usingizi ndio niende kwangu au nitakuwa nikikuingilia?” “Hata kidogo. Twende.” Akaingia mpaka chumbani kwake.

“Humu kuna joto, toa nguo nitakuwashia feni.” Bila ya kujibu, akatoa nguo zote akabakiwa na boksa tu. “Humu, Shema asiingie hata kwa bahati mbaya.” Pam akaanza kucheka akiokota nguo alizoacha sakafuni. Hapohapo Mill akazima kama mshumaa. Akabadili nguo, nakutoka taratibu asimuamshe.

~~~~~~~~~~~~~~

Akakumbuka hana hata jiko. Anapika nini! Akakumbuka ana gari ya Mill, akatoka nayo. Njiani akampigia Shema kujua alipo. “Sasa ukifika nyumbani uache kelele na kucheza mpira sebuleni. Baba yako amelala ndani.” Akashangaa mtoto amefurahi huyo! “Kama kina baba Pili wanavyolala ndani kwao?” Pam akacheka akimfikiria mwanae.

“Sitachelewa. Kwani njaa inauma sana?” “Macho hayaoni, mama!” “Shema muoga wa njaa wewe!” “Sioni kabisa.” “Haya sichelewi, narudi sasahivi na chakula. Na ili usikae hapo ukifikiria chakula, ukifika tu, kaoge.” Akampa maagizo, mwanae akaelewa.

~~~~~~~~~~~~~~

Akala na mwanae mpaka Shema akaenda kulala, bado Mill ameuchapa usingizi chumbani kwa Pam. Akaoga na kuanza kufikiria kama amuamshe au la! Ila kwa vile alivyokuwa amelala kama mzoga, akaona amuache tu.

Akapanda kitandani na kujilaza pembeni yake. Ndipo akatoka usingizini na kuanza kulalamika. “Joto Pam, mimi siwezi kulala na feni.” “Hapa hamna A/C. Jikaze, utoke hapa ukalale kwako.” Akatulia, akamvuta Pam karibu, akamkumbatia vizuri na kupitiwa na usingizi tena.

Kama baada ya lisaa akamsikia tena. “Nateseka joto, Pam!” “Jikaze, uende ukalale kwako kwenye A/C, Mill. Lasivyo tutakesha hapa ukilalamikia joto.” “Mimi hivi siwezi.” Pam akatulia. “Pam?” “Unataka nifanyaje Mill na ushakuwa usiku? Wewe umelala, umepunguza usingizi, ndio unaanza fujo.” “Kwa nini sasa umehamia huku wakati kule kwangu kuzuri kuna kila kitu?” “Kweli ndio mazungumzo hayo unataka tuyafanye sasahivi!? Nenda kwako Mill, wewe usingizi ushakuisha.” “Bado nina usingizi ila siwezi lala na feni.”

Pam akamgeukia. “Nimekubakishia chakula. Kula uende kwako ukalale, au beba ukale kwako. Mwenzio nina kazi asubuhi.” “Kesho tusiende.” Pam akabaki akimwangalia. “Ndio umenisamehe tu! Hata sijakufaidi, unataka kuniacha katikati! Nihurumie mpenzi wangu. Nipe hata siku mbili tu.” “Haa! Na kazini!?” “Nitamwambia Mbise aendelee. Mbona alikuwa akifanya kabla yako? Hawezi shindwa siku mbili.” Pam akatulia akifikiria.

“Niambie kama kweli wewe mwenyewe huna hamu na mimi.” “Kupita unavyodhania. Lakini sitaki kuharibu kazi, ndio nimeanza tu!” “Ikiharibika namfukuza yeye kazi. Wewe usiwe na wasiwasi. Sawa?” “Ndio tunafanyaje?” “Ungekuwa si mbishi, ungehamia pale kwangu. Mwanao akienda shule sisi tunaendelea na yetu kwa kujinafasi. Lakini hebu niambie huku ulipo! Nyumba yenyewe haina madirisha.” “Acha dharau.”

Mill akajiweka sawa. “Niambie kama kweli umenisamehe kabisa na upo tayari kuanza upya na mimi.” “Kwa aina ile ya uombaji msamaha, dhambi zako ZOTE zimesamehewa.” Mill alicheka sana.

Kwakujidhalilisha vile, mbele ya wafanyakazi wako! Haki umenigusa Mill! Asante. Na yameisha KABISA.” “Basi kama kweli umenisamehe na tunaanza upya, hamia kwangu. Kwa mwanzo sitakulazimisha uhamie ndani kwenye nyumba kubwa ninakoishi. Unaweza anza kuishi kwenye kile kinyumba kidogo.  Ukawa huru na kufanya utakavyo kama hapa tu. Lakini ni bora pale kuliko hapa. Usiku hata ukitaka kujiiba uje kwangu wakati mwanao kalala, pia sawa.” Pam akaanza kucheka akifiria.

“Ila hapa nishalipa kodi ya miezi sita Mill!” “Pesa inatafutwa na kupatikana ila tulicho nacho sisi hebu niambie hata kama unayo pesa, unakipata wapi?” Pam akatulia akiona ni kweli. “Wewe umehangaika huko ukaishia kwa Mgaya. Mimi ndio usiseme. Lakini starehe niliyopata leo pale ofisini, tena kwa muda mfupi tu, ikanifanya nilale usingizi niliopoteza karibia umri wa mwanao huyo! Nimepata penzi langu la halali, lililobarikiwa na wazazi pande zote na ndoa ya kisambaa juu.” Pam akaanza kucheka.

“Tushapoteza muda mwingi sana Pam. Umri umekwenda, tumebakiwa na katoto kamoja hakohako kama dawa! Kubali yaishe na sisi tuanze maisha.” Pam akabaki ametulia. “Hakuna chakufikiria hapa, ila kuchukua hatua tukiamini safari hii tutapatia. Twende ukalale pazuri na mimi nataka nikufaidi kama zamani. Taratibu kwenye baridi nzuri sio hapa nikikutingisha tu, mwanao anakuja. Halafu nitaloa jasho hapa kama mpumbavu!”

 “Sasa hapa napafanyaje?” “Wewe chukua nguo tu. Tena mtakazohitaji kesho na kesho kutwa. Tuondokeni. Nikishakushika hata siku mbili tu, akili itatulia, nitajua chakufanya.” “Kwamba tuondoke usiku huu!?” “Wewe hutaki kulala pazuri?” “Shema!?” “Mwanao atalala kwenye gari na akifika atakwenda kulala moja kwa moja, usiwe na wasiwasi.” Alifurahi Pam, akafurahi sana. Anampata tena Mill!

Akaanza kufungasha vitu muhimu kwake na mwanae, akawa akiweka kwenye gari, Mill akamuamsha mwanae. Akamsaidia mpaka garini.

~~~~~~~~~~~~~~

“Nakuendesha, pumzika kidogo kwenye kiti cha mbele. Na safari hii huna sababu ya kukaa nyuma.” Pam akabaki akiweka vitu vyake bila ya kumjibu. “Hakuna wa kukutoa mbele Pam, wangu. Sasahivi ni mimi na wewe tu. Hakuna cha Brenda hakuna cha Mgaya.” “Wewe unahalalisha uchafu wako, kwa kumleta Mgaya. Mgaya ulimkuta. Brenda ulimtafuta katikati yetu.” “Mimi naona tusirudi nyuma. Tuanzie pale kwenye ule msamaha wa kujidhalilisha. Dhambi zangu zote ZIKASAMEHEWA. Kwanza mimi hata simjui Brenda ni nani!” Akamtizama kwa kumsuta.

“Kaa mbele mpenzi wangu. Hakuna wakuja kukutoa tena.” Hakumjibu. Akazunguka kiti cha mbele, akavuta kiti nyuma, akalala kabisa. Kwanza alikuwa amechoka, halafu huyo Pam na mwanae huwa wanalala mapema. Akaongeza mchezo wa nguvu wa ofisini aliompa Mill, akapitiwa na usingizi hata hawajafika mbali. Mill kimya akiendesha, asiamini kama hatimaye anamuingiza Pam na mwanae angalau ndani ya ua wake japo si kwenye nyumba kubwa aliyojenga kwa mamilioni ya mapesa mengi.

Moyo Uliojeruhiwa Kwa Penzi La Dhuluma

Sonia alijua fika mapenzi yana NGUVU nzuri sana, lakini huwa hayakosi miiba yake. Yanaweza kukujaza mwanga, lakini pia kukuacha umechanganyikiwa gizani na kupotea kabisa. Bado alitaka kujua kwa hakika umbali gani Pius yupo tayari kwenda kwa mkewe?! Asijue, kwa Pius, kile kilichowahi kuhisiwa kama joto zuri katika mguso wa mkewe, kwake, sasa kinamchoma kwa uchungu wa USALITI. Lile penzi limegeuka kuwa hasira tulivu inayoteketeza moyo na hisia za Pius polepole, kila dakika anayopata kumfikiria Raza.

“Pius?” Sonia akamtoa mawazoni. “Cha kwanza Raza si wakumtisha. Hutamuweza kwa maneno ya vitisho. Mimi huwa namjulia.” Akamuhakikishia. “Ninajua unao watu wa Usalama wanaoweza kukusaidia. Naomba wawili watakao ongozana na sisi. Nishamtumia ujumbe wa kukutana. Nataka kumchukua niende naye mpaka kwa mganga wake. Najua huko tutajua mengi na kupata sababu sahihi ya kuwashikilia kisheria. Maana najua kesi ya uchawi ni ngumu bila ushahidi. Sasa wewe usijali. Tutapata ushahidi kutoka kwao hawahawa wawili.”

“Kwamba ni kweli utamshitaki?!” “Kabisa! Siwezi muacha hivihivi. Amenitesa kwa muda mrefu, halafu anataka kumuua mtoto wangu! Mimi sijui kutishia Sonia. Huwa nafanya kweli. Nikimuacha yeye, ni kukubali kifo cha kijana wangu asiye na hatia. Hakika SITAMUACHA.”

“Na Chezo?” “Kwangu Chezo hana hatia. Amemtongaza Raza kama vile anavyotongoza wanawake wengine na kukataliwa, ila Raza yeye alimkubali. Haonekaniki kuwa huwa anambaka Raza. Jumbe zao ni za wapenzi wawili. Si umeona hata jinsi Raza anavyozungumza naye?” Sonia akarudisha macho kwenye karatasi zilizobeba jumbe zao hao wawili.

“Hawa watu wamekubaliana kuwa kwenye mahusiano. Raza ndiye amenikosea. Si Chezo. Chezo ni MALAYA tu ambaye kama si Raza, angekuwa mwanamke mwingine. Na inamaana Raza si mwanamke wa kwanza aliyemtongoza. Wapo waaminifu waliomkataa ila Raza amemkubali. Na kwa mujibu ya mazungumzo yao, inaonyesha ni wapenzi wa muda mrefu tu, na hukutana karibia kila siku. Ni wazinifu wasio na kipimo. Mimi nitashugulika na Raza wala si Chezo.” Sonia akabaki akifikiria.

“Nasikitika kuona mimi ndio nimeshindwa kuweka mazingira mazuri kwa kijana wangu na kumuachia Mina. Mimi ndio nawajibika zaidi. Nimeishi na mbaya wangu na kumuacha akifanya uharibifu vile atakavyo. Sasa basi, kabla sijarudi kwa Mina na mtoto wangu, nilazima niweke mazingira mazuri.”

“Tafadhali wasiliana nao, mjulishe Mina kuwa nitahitaji muda wakutengeneza kwanza kabla sijakwenda muona mtoto.” “Lini?” “Sijui Sonia. Hata mimi mwenyewe sijiamini. Huyu Raza anaonekana amenipandikizia vitu vingi sana kwa muda mrefu. Jinsi ninavyokuwa wakati mwingine najihisi kama sio akili zangu! Nakuwa kama niliyepagawa! Iweje nirudi kwa Mina na mtoto kwa haraka kisha niharibu? Au niseme hata kudhuru kijana wangu mwenyewe?” “Pius umeingiwa woga!”

“Hakika nimeingiwa HOFU baada ya kujua kinachoendelea. Hakika sijiamini mpaka nihakikishe mimi mwenyewe nipo salama. Akili yangu imetulia. Na Raza pamoja na mganga wake wapo sehemu ambayo hawataweza KUMDHURU mtu mwingine tena. Lakini si vinginevyo.”

“Wewe mwenyewe utajuaje kama upo salama?” Sonia akamuuliza. “Hata sijui! Lakini kwa jinsi hivi nilivyo, hakika sijiamini. Najihisi nimejawa madudu, sistahili hata kumshika kijana wangu. Nahisi kama naweza muhamishia madudu niliyowekewa na Raza.”

“Mimi ninajua unachozungumzia. Niliishi na watu walio pitishwa hapo unakopita wewe. Mtu kupandikiziwa mapepo na roho chafu, kwa kiasi chakuweza kukana mtoto na mke aliyekuwa akimpenda SANA. Yaani huyo shemeji mtu aliyefanya yote hayo alidiriki kumgeuza dada yake kichaa kabisa kiasi cha kuwekwa kwenye hospitali ya vichaa, Mirembe.” Pius alishituka sana.

“Kwamba alifanya hivyo kwenye familia ya dada yake?!” “Wa kuzaliwa tumbo moja! Akafanikiwa kusambaratisha familia iliyokuwa imesimama kwelikweli.” Ndipo Sonia akamsimulia kwa kifupi mkasa wa Mama Briana aliyekuwa bosi wake, enzi hizo Sonia ni msichana wa kazi za ndani. Akampa mkasa mdogo wake mama Briana, yaani Leah, aliyempenda shemeji yake mpaka wote akawageuza akili kabisa hawajitambui. Kisa chao kipo kwenye (Simulizi ya More Than Saying- Zaidi Ya Kutamka.)

“Ila Pius, huyu Mungu yupo kwa halisi. Mimi nimemuona akifanya mambo, ukisimuliwa ni kama hivyo wewe! HUAMINI. Anaposikia hakuna jambo gumu linalomshinda! Au unaposikia anazo nguvu. Au Yeye ni muweza. Hakika anao UWEZO wa ajabu mno. Anazo NGUVU. Alifanya JAMBO kwenye ile familia ya Nyange na mkewe, hutaamini.”

“Ninachotaka kukwambia ni kuwa, usiogope. Hakuna gumu ulilofanyiwa wewe, Mungu huyu ninayemjua mimi akashindwa kutenda. Tumalize hili kwanza. Kisha nitakukutanisha nao. Watatembea na wewe, na utawekwa huru.” Pius akavuta pumzi kwa nguvu na kutulia akitafakari.

“Unataka kukutana na Raza wapi ili kuwapanga hao askari kanzu? Maana kweli bila ukiri wao au ushahidi wa kueleweka, ni kweli kesi ya uchawi ni ngumu.” Akamtoa Pius kwenye mawazo. Akafikiria, kisha akaona wakutane kwenye mgahawa wanao uza chakula ili amfanye Raza atulia na kumuweza.

“Swali la mwisho kwako Pius.” Pius akamtizama. “Unauhakika na unachotaka kufanya? Maana ukumbuke Raza ni mama watoto wako na mkeo wa ndoa ya kanisani. Utafanyaje na wanao wakijua umemfunga mama yao? Maana kwangu Mina ni mteja wangu na nimeahidi kusimama naye. Na mimi sijipingi. Kwa hiki nilichokiona hapa, siwezi kukiacha. Naendelea kuanzia hapa. Wewe usaidie au usisaidie, jua Raza nitampata tu, na ushahidi nitatengeneza hata kama itachukua muda mrefu, nitakamilisha tu kesi yake. Sasa je, wewe kweli unataka kuendelea na hili? Maana unaweza jitoa, ukaniacha niendelee.”

Nisipomlinda mimi kijana wangu, nani atamlinda? Mimi nina jukumu kama baba Sonia. Siwezi kumuachia Mina kila kitu. Nataka yeye ahangaike na malezi ya mtoto tu. Mengine mimi ndio nifanye. Kumuacha hivi Raza, kwa kisingizio cha kuwa ni mama watoto wangu, nikuruhusu aangamize wengine. Huwezi jua ukute hata Chezo naye anamfanyia madudu hayahaya! Na huwezi jua, pengine ukimya wa mke wa Chezo kuna alichomfanyia. Haya, akiona mkewe hatulii, unajua ni nini atamfanyia?” “Na kweli!” “Sasa nitaacha watu wa ngapi waangamie?” Kimya Sonia akitafari.

“Haya, kwa tabia hii ambayo nitashindwa kuikomesha, unajua umbali gani atakuja kwenda kwa yeyote atakayesimama kwenye malengo yake? Wazazi wangu? Watoto wangu wenyewe? Wakwe zangu watarajiwa? Wajukuu na vitukuu? Haya, atakuja fundisha nini binti zangu kama si haya ayafanyayo na kufanikiwa? Watoto wangu si watakuja kujua njia za mama yao ndio sahihi WAJIFUNZE kwake! Hakika SIWEZI mruhusu Raza aendelee kuwa hivi. Hata kama watoto wetu watakuja nichukia, ila ni kwa faida yao pia.” Pius akazidi kufikiria na kukumbuka.

“Huyu Raza anapika mpaka kwa wazazi wangu na  kwa dada yangu. Unajuaje kama hayo mavitu anayoweka humo kwenye vyakula vyangu anawawekea ndugu zangu wote ili tu kufikia malengo yake?” “Ngumu kujua!” Sonia akajibu akikumbuka majibizano kati ya Raza na mganga wake akimuuliza kama kweli hakusau kumuwekea mumewe dawa alizompa, kwenye vyakula vyake hata mara moja na kama anauhakika hajatoa ya kwenye mto anao lalia Pius. Sonia akaguna.

 “Siwezi muacha Raza aendelee hivi. Kwanza hata yeye namuogopa kuja kuwa naye karibu tena.” “Basi acha nifanye mawasiliano tutoke. Nitakuwa meza ya pembeni yenu. Na lazima kumrikodi.” Wawili hao wakafanya makubaliano yao. Wakaweka mipango.

~~~~~~~~~~~~~~

Kisha akamtumia ujumbe Raza, sehemu na muda anaotaka wakutane. ‘Nakusisitiza tena Raza, usichelewe.’ Kisha akamgeukia Sonia aliyekuwa na yeye kwenye simu yake kama ambaye anawasiliana na mtu kwa ujumbe, “Acha nitangulie. Mtanikuta.” “Na sisi hatutachelewa.” Yeye Pius akatoka.

~~~~~~~~~~~~~~

Pius Anatafuta Ukweli Kwenye Kivuli Cha Giza Nene.

Je, Ni Heri Kuishi Kwenye Kivuli Kinachotuliza, Asichokonoe yote,
Au Kuamka Na Kujiangalia Bila Kifuniko?

Tuendelee Mbeleni Kuona Atakayokumbana Nayo Pius Anapomchunguza Bata Zaidi.


CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment