Mina akaendelea kula, pakawa pamezuka ukimya. Kila mtu
hajui azungumze nini tena. Wakatulia mpaka Andy alipoingia. Wakamuona Mina
anasimama tena kwenda kumpokea. “Sijaja na chakula hapa ili nisikutese.
Nimekula hukohuko kwa haraka. Hapa nimekuletea icecream tu.” “Hata hivyo nashukuru.” “Vipi mtoto?” “Bado
amelala.” Wakakaa.
“Nimemuacha Ayan, amelala.” “Afadhali.” Akatulia
akimuangalia mkewe. “Kuna nini? Mbona kama kuna kitu unataka kuniambia, unasita?”
“Andy mdadisi!” “Ni nini?” “Nitakwambia baadaye.” Wakaona waage. Kuwapisha.
“Nikuletee nini asubuhi?” “Bado nakula kama mzazi.
Asubuhi uji kabisa. Ila sababu hanyonyi huyu, sijui nitafanyaje!” “Kamua.”
“Hataki chupa kabisa, mama! Ukimpa chupa ni ugomvi, hataki. Nikizidisha
kipimo chake, najitesa tu mwenyewe.” “Ila kesho atarudia hali yake. Usijikaushe.
Nitakuletea uji, na supu.” “Na ili usimsumbue msichana wako, yule dada yake
Ayan anajua kupika vizuri sana. Ni kumuamsha tu.” “Haina shida.” Wakaaga na
kutoka.
Andy&Mina
Wakabakia wao wawili. Akasimama kwenda kumuangalia
mtoto. Mina akamuona amepotelea mawazoni. Akamuacha tu akiendelea kula icecream yake. Mwishoe akarudi kukaa naye. Akamuona amekaa na kujiinamia.
Hakujua azungumze naye nini. Mina akamaliza na kwenda kunawa mikono. Akarudi
kukaa naye.
Akamwangalia wakati akikaa. “Bado unanipenda
Mina au nimeshapoteza umaana kulinganisha na vile Pius anavyo kujali?”
Mina akashituka. “Unawezaje kujifananisha na Pius!? Wewe ni mume
wangu, Andy!” “Sijui Mina! Kila nikipiga mahesabu, nagundua kuna kipindi ni
kama ulibaki kuwa mke wangu lakini yeye ndiye aliyekuwa akikutunza.
Alikuwa na wewe kwa uzima, maradhi na matumizi yako binafsi. Hukuwa na shida
tena na pesa yangu.” Mina akakumbuka.
“Ulianza kuninyanyasia pesa Andy! Na hili
tulishazungumza. Ulianza kunigombesha ukilalamika kuwa sithamini
unachokifanya. Ukaweka kuwa ni kama sina shukurani. Ningefanyaje? Na
nilikueleza vile ilivyokuwa mpaka Pius akaanza kunisaidia. Wakati mwingine
alikuwa anakuja ili awe na Ayan, akitaka na mimi nitoke kidogo. Labda
kutengeneza nywele au kufanya manunuzi ya nyumbani. Najikuta nashindwa
kutoka wakati uhitaji upo!”
“Alipogundua tatizo ni pesa. Kwamba ni mpaka nikusubiri
ukumbuke kutuma pesa ndio akasema sio sawa vile ninavyohangaika na mtoto
na ujenzi wa kule Kigamboni, halafu mimi mwenyewe naishia kuwa kama benki tu au
ATM. Napitisha pesa lakini nakuwa nabakiwa na shida. Ndio akaanza
kunisaidia.”
“Lakini hapo nilikuwa nimeshaacha kukuomba pesa
Andy! Kuna siku ulizungumza na mimi maneno makali, machungu, tena
nilikuwa saluni. Nakumbuka mpaka leo. Niliapa sitakuomba tena
pesa ni bora nibakiwe na shida zangu kuliko uje urudie uniambie
yale maneno.”
“Ulibadilika sana Andy. Sio kama tulivyoanzana
mimi na wewe. Ukawa hunijali tena. Kuna kipindi ukaonyesha kama mimi nakuzuia
kufanya mambo yako ya msingi, au nakuchelewesha. Nikakuacha.”
“Na hapo ndipo Pius alitumia huo mwanya!” “Sitakudanganya Andy, Pius alinijali
sana. Na alinijali mimi na Ayan.” “Ila shida yake ilikuwa ni wewe
Mina. Tafadhali usikatae.” “Mimi sijawahi kubisha Andy. Inawezekana. Lakini kwangu
alikuwa na heshima kabisa. Na wema wake alikuwa akifanya si kwa siri,
hata mbele ya ndugu zenu au wazazi. Hapakuwa na hila au kificho.”
“Na mimi nilikuwa na uhitaji wa msaada
wa yeyote atakayekuwa tayari kunisaidia ili kumaliza shule na Ayan asiathirike.
Ningefanyaje Andy?” “Sio kwamba nakulaumu! Ila nipo kwenye majuto
Mina! Najuta. Ila nilishakwambia sio kwamba nilikusudia kukunyanyasa au
kwamba sikujali! Akili ilikuwa inachoka, wakati mwingine nilikuwa nikisahau
kabisa kukuhamishia pesa.” Mina hakumjibu.
“Mbona umeniangalia tu na kunyamaza?” “Kwa sababu
najua kwa hakika uliacha kunipa kipaumbele Andy! Ukaanza kunipuuza.
Ukweli ulikuwa hunijali Andy. Mapenzi yaliisha kabisa
tukawa tukiishi bora siku zisogee.” “Unawezaje sema hivyo Mina!?
Nilikuwa nikihangaika kwa ajili yetu sisi wote!” “Sijui wewe unajiambiaje,
lakini kipaumbele chako kilikuwa majukumu yako ya kazini
na SI nyumbani. Hilo usikatae Andy, kila mtu alikuona.”
“Ulikuwa hata ukija huku Dar, huna muda na mimi
wala Ayan. Utakuwa kwenye simu zako kuanzia unarudi nyumbani, mpaka
unaondoka. Tena hapo ni muda unaokuwa umeamua kuwepo ndani. Vinginevyo ulikuwa
ukifika utafikiri umekuja sababu ya ile nyumba ya Kigamboni. Utashinda
huko kuanzia asubuhi mpaka usiku, kisha unaaga na kuondoka. Hutataka muda na
mimi kama tulivyoanza mwanzoni mwa ndoa. Na ilikuwa kila kitu lazima nikuombe,
huwezi nifikiria mimi kama Mina.”
“Wakati pesa zote ulikuwa ukishika wewe!” “Za ufundi.
Yaani kila pesa uliyokuwa ukinitumia ilikuwa na maelezo, ningewezaje
kujichukulia tu? Na hili tulishazungumza na kulimaliza, Andy! Kwa
nini unarudisha mambo ya nyuma?” Akatulia.
“Hatuwezi endelea kama kila wakati tunarudia
mambo yaleyale, Andy! Makosa yalishafanyika, kwa nini hatuendelei
mbele?” “Ni kama sijui jinsi ya kuendelea Mina! Acha nikwambie
ukweli kwa vile ninavyojisikia.” Mina akamgeukia vizuri.
“Najihisi nimekuwa kama muingiliaji! Nipo
katikati yenu.” Mina akashangaa sana. “Kabisa Mina. Naona kama umekua karibu
na Pius kuliko hata mimi! Kuna jinsi unazungumza na Pius, sio
kama unavyozungumza na mimi. Ni kama mpo kwenye mahusiano
fulani!” “Andy, umeingiwa tu na wasiwasi ambao unakutesa
bila sababu. Sikatai kwamba Pius ni kama ndiye niliyekuwa naye
karibu kipindi wewe haupo, na tumemlea Ayan pamoja. Katika uzima na
furaha, usiku na mchana, amekuwa na sisi na ndio maana hata Ayan amemzoea
sana Pius. Lakini wewe ni mume wangu Andy?”
“Sasa mbona uliondoka, lakini wakati unarudi umemtafuta
Pius, mimi hujanitafuta?” “Kweli Andy hicho ndicho kinakunyima
raha!?” “Kabisa. Mimi ndio mumeo.” “Kumbuka jinsi nilivyoondoka na hali tuliyoachana
nayo! Kweli leo nikutafute kwa tatizo la mtoto ambaye ulishindwa kumpokea!?”
“Nilihitaji muda Mina!” “Na mimi nililiheshimu hilo. Sasa
ningejuaje kama upo tayari na sisi? Halafu hata Pius mwenyewe
nilimtafuta kuepuka lawama. Niliogopa lisije likatokea la
kutokea, wakafanya makosa huko chumba cha upasuaji, Pius asimuone mtoto
wake akiwa hai.”
“Nilimtafuta kuepusha lawama tu. Lakini sikuwa
hata na lengo la kurudi sasahivi nikitaka wanangu wakue kwa amani
si hii fujo inayoendelea.” “Kwa hiyo bado utaondoka?” “Sijui Andy!
Kule nina maisha ya utulivu na amani sana. Naona watoto wangu
wanakua bila ubaguzi na bila hizi kelele za huku.”
“Na ndoa yetu?” Andy akauliza kinyonge! “Mimi
bado nakupenda Andy. Lakini nina Ayvin, mtoto wa Pius ambaye hamuwezi
zungumza hata neno moja mkaelewana! Tunafanyaje?” “Mtoto si
tatizo. Tatizo ni Pius mwenyewe. Ananifanyia kusudi na ananidharau
vibaya sana.” “Kwa nini unamfuatisha? Achana naye.” Akanyamaza.
Kisha akaongeza. “Mimi bado nakuhitaji Mina. Nakuhitaji
sana. Naweza nisiwe na majibu yote, lakini najua nakupenda na nakuhitaji.
Nataka ndoa yetu isiharibike. Na nakuahidi nitabadilika.”
“Kazi yako umeipa kipaumbele sana, Andy! Hutaki yeyote aingilie
ratiba zako za kazi!” “Nakuhidi kubadilika. Kwanza ni kama nimefika
nilikokuwa nikikuhangaikia.” “Hongera.” “Havina RAHA tena.”
“Kwa nini sasa na wewe juhudi zako zimelipa?”
“Kwa garama ya kukupoteza wewe! Havina maana. Nilitaka nikifika
hapa niwe na mke wangu na watoto. Tunaishi sehemu moja, tunafurahia
maisha. Sio hivi. Pesa yote inakosa maana.” “Ilikuwa ikitutunza mimi na
Ayan.” “Sasa si na Pius naye pia alikuwa akikutunza? Hata nisingekuwa
nikukuwekea pesa benki, usingeona upungufu kwa sababu najua fika Pius alikuwa
akikutunza.” Mina akanyamaza.
“Nakuahidi kubadilika Mina!” “Nashukuru Andy,
lakini ndio tunafanyaje?” “Wewe upo tayari kuanza tena na mimi au
ndio umenikatia tamaa?” “Nakupenda
Andy. Na hili nilishakwambia, mwenzio napenda ndoa yetu isife.” “Basi
tujipange kwa upya. Na nakuhidi safari hii sitabadilika tena.
Niambie unataka kuishi hapa Dar au Dodoma?” “Dodoma nilikufuata wewe Andy,
lakini mimi napenda huku Dar.” “Basi nipe muda nifuatilie ile nafasi ya
kazi ya huku. Nikifanikiwa, narudi tuje tuishi wote.”
“Unamaanisha nini?” “Wewe nenda kakae na watoto
Kigamboni wakati mimi naweka sawa mambo. Nikikamilisha uhamisho, narudi huku.”
“Ukikosa uhamisho?” Akatulia kidogo akifikiria. Kisha akawa kama amepata
jibu la kujikana. “Pengine naweza
nikakosa nafasi ya uongozi kama hii lakini sitakosa kazi. Lengo ni nije
kuwa na wewe. Tusitengane tena.” “Sasa mbona unataka kuniacha tena
huku, wewe urudi Dodoma!?” “Umesema unapenda kuishi huku, Mina! Sitaki
ukaishi sehemu usiyopenda.” “Ila tutakuwa wote, Andy.”
Andy hakuamini.
“Kwamba wewe upo tayari kurudi na mimi, sasahivi,
Dodoma?!” “Kabisa Andy! Ukiridhia, na ukawa tayari kuishi
na sisi WOTE, mimi nitakufuata popote. Wewe ni mume wangu
Andy. Sijasahau jinsi ulivyohangaika ili kunioa. Kwenu
wote walikuwa kinyume na mimi, lakini ulihakikisha tunaoana,
nikiwa mimi si kitu kabisa. Hukujua hata aina ya mtoto nitakaye kuzalia!
Ukanipokea na hali yangu ya chini, na aina ya ustarabu wa kwetu. Ulinipenda
vile nilivyo Andy! Siwezi sahau.” Andy akatulia.
“Tokea mwanzo mimi shida yangu ni wewe Andy. Nakutaka
wewe. Nataka tuwe wote, sio uniache kwenye majumba mazuri, kama huko
Kigamboni, halafu wewe haupo! Hivyo mimi sitaki. Tuwe wote Andy. Popote,
tuwe wote. Naamini yale maisha yetu ya mwanzoni kabisa, tunaweza kuja yaishi
tena. Ulikuwa ukinipenda na kunijali sana Andy.” “Nakuhidi tutarudia.
Na asante.” Akamuona amefikiria, akacheka. Mpaka uso ukabadilika.
“Ni nini?” “Nimefurahi! Nimefurahi sana
kukusikia ukiniambia hivyo. Nilijua nishakupoteza!” “Huwezi Andy. Mwenzio
nakupenda.” Akaongea kwa sauti yake ya upendo. “Daah! Nina hamu na wewe Mina!” “Na mimi Andy.” Akainama kupata kiss.
Mina akachangamkia, mkono kwenye zipu. Akamuona anajisogeza na kujiweka sawa.
Akajua anataka. Na alimjua anavyopenda
jinsi anavyomchezea. Wakati anafungua zipu huku kiss ikiendelea, nesi akaingia kumuongezea mtoto maji.
Wakaachiana kwa haraka. Aliwaona.
“Nikiweka hili, nitafungulia taratibu. Sitawasumbua
ili na nyinyi mpumzike.” “Hamna shida kabisa.” Andy akadakia akijirudisha nyuma.
Mina akasimama akicheka.
Alipomaliza kumuwekea mtoto maji, akambadilisha
kabisa matandiko maana alikuwa na catheter. Akamuweka sawa, na kutoka huku akiwaambia wakiwa na
shida yeyote wamuite. Wakashukuru ndipo akawapisha sasa.
Ndoa Na Iheshimiwe
Na Watu Wote.
Andy akamvuta Mina na kuanza kumkiss tena. “Tufunge mlango vizuri twende hapo bafuni. Na
mimi nina hamu na wewe Andy.” Kwa haraka sana wakahamia chooni. Mina wa
mengi, na wala hakuwa na hamu ya mapenzi! Akili zipo kwa mtoto
mgonjwa, mume anamtaka. Akafika naye bafuni, akamshusha suruali na
kuanza utundu wake mpaka mumewe akalemewa haswa.
“Nisaidie Mina. Nina hali mbaya!” Alichofanya Mina ni kuvua chupi hapo mbele yake,
akamuinamia. Andy akashika kiuno. Alivyokuwa na hamu na huyo mrembo ambaye humchanganya
kila akimshika, hakukawia, akapiga la kwanza. Mina akajua ndio amemaliza, akashangaa anaendelezea palepale mpaka akapata la
pili, ndio akamsikia akihema sasa
kama aliyemaliza. Akamkamulia ndani kama alivyomzoeza, alipomaliza kabisa,
akatoka.
“Na wewe?” “Usijali. Tutapata muda mzuri, ila sio
hapa.” Akachukua kitaulo pale, akamfuta vizuri, na kumpandisha boxer na suruali
akamalizia mwenyewe, akiendelea kumshukuru. “Nenda kapumzike kwenye kochi,
nakuja.” Andy akatoka, Mina akarudi kuoga kabisa ndipo akamfuata.
~~~~~~~~~~~~~~
“Njoo nikukumbatie ujilaze.” Bwana Mina
alifurahi kusikia hivyo, mpaka gafla uso wake ukabadilika kabisa! Andy hakuamini!
Furaha aliyoipata hapo baada ya kumkaribisha mikononi amkumbatie, ni tofauti
kabisa na alivyoambiwa anunuliwe gari! Ndio kama akili ikamrudia Andy na
kumkumbuka kwa wazi kabisa AINA ya mke aliyeoa. Mambo yake madogo
madogo yanayo mfurahisha. Hutampa pesa au gari Mina akafurahia kama kumuweka
mkononi.
HABARI zote siku hiyo, kama za gari analotaka
kupewa na Pius, sijui nyumba nzuri Kigamboni, au kufanikiwa SANA
huko kazini kwa Andy, hakuzifurahia KAMA hapo alipoambiwa na mumewe akumbatiwe, alale. Andy
akacheka nafsini kwake akimfikiria Mina, na akajua fika hapo ndipo Pius alipompata mkewe. Kule kuwepo naye karibu wakati wote.
Akamuona anacheka huku akiharakisha kuweka mambo sawa
hapo. “Unacheka nini sasa?” “Nimefurahi Andy! Nimefurahi sana. Umefanya
mapenzi na mimi, halafu utanikumbatia nilale!” “Sasa mbona hata wewe mwenyewe
hujafanikiwa?” “Ile tu kujua wewe hapo bado unanitaka mimi,
halafu ukafurahia mapenzi na mimi! Mwenzio nimefurahi kuliko hata kufika
kileleni. Halafu unanikumbatia
nilale!” Andy akacheka akimtizama.
“Mwenzio nimefurahi Andy. Niliondoka nikiwa sijui kama
utakuja kunirudia tena nikiwa na Ayvin. Nilikuacha Dodoma kwanza ulikuwa
unashindwa hata kunishika vizuri. Kama unayenikwepa! Nikaondoka nikiwa sijui kama utakuja nihitaji
tena. Nikwambie na sababu ingine iliyonifanya niondoke? Ila ilikuwa siri
yangu, sikutaka kumwambia mtu.” “Uje uniambie ukiwa umetulia hapa. Umekuwa na
siku ndefu. Nataka na wewe upumzike, Mina.” “Asante kujali. Hapa naweka
kila kitu sawa, nikitulia hapo kifuani kwako nitulie habisa.
Nimefurahi mwenzio.” Andy akacheka tena taratibu huku akimfikiria mkewe.
Kumuita amkumbatie tu, ndio na siri zote anatoa! “Mina!” Akaendelea
kumuwaza mkewe.
Kiukweli Andy alimpenda Mina ile ya kupitiliza.
Huna sababu utampa akaridhika kuachana naye. Alimtaka kwa udi na
uvumba. Na kwake alikubali kuwa mjinga
ilimradi tu awe na Mina wake.
Alipomaliza hata kumfunika mwanae ndipo akachukua
mashuka waliyokuwa wameletewa. Kochi hugeuka kuwa kitanda, kwa hiyo Andy
alishajilaza akiwa ameegemea mto. Akamfunika Andy vizuri kuanzia miguuni, ndipo
akajilaza hapo. Mtoto wa kike akajaa kifuani. Andy akamuweka sawa ili kupata
midomo huku amemkumbatia. Zikaanza kissing za
uchu. Mina alijawa furaha kupitiliza.
Kabla hajampoteza maana alishalegea, akamuachia.
“Niambie ile siri.” Mina akacheka. “Husahau!” “Na mimi nataka kujua sababu
ingine iliyokuondoa ili tusirudie kosa. Sitaki tena tutengane.”
“Kama ndio hivyo ujue mwezio siondoki tena.” Andy akacheka akimkumbatia
vizuri.
“Kweli tena Andy! Mwenzio niliondoka nikijua hunitaki
tena. Umeshindwa kuwa na mimi sababu ya Ayvin. Nikaona kabla hujaniacha,
bora niondoke tu. Halafu ikawa fujo. Nikajiambia Andy amenileta kwenye fujo
za kwao, halafu ataniacha, bora mimi niondoke kabla hujanitamkia hunitaki
tena.” “Nilirudi Mina. Ukweli nilikuwa na wakati mgumu, sijui
chakufanya. Ila nilijua kwa hakika siwezi kuishi bila wewe Mina. Nilikufuata
siku inayofuata tu baada ya kuondoka Dodoma. Nilifika pale kwa wazazi
alfajiri…” Akamsimulia kila kitu.
“Kumbe bado unanipenda kwa ukweli Andy, sio
kwamba unataka mashindano!” “Nakupenda Mina.” “Niambie tena Andy.” Akaomba kwa deko lake. “Nakupenda Mina. Nakupenda wewe kama wewe.
Uwe unazaa watoto wa kike au wakiume, nakupenda wewe kama Mina.
Na nitafanya lolote kwa ajili yako.” Akamdaka tena midomo.
Wakajisahau kama wapo hospitalini. Mina anapendwa! Hapo akamchanganya kabisa Mina kusikia hayo. Kwa
maneno hayo tu, akamlevya
zaidi ya romance! Alikuwa
akijizungusha hapo na kutoa milio ya huba mpaka
akamuamsha tena Andy.
Alichofanya ni kutoa tena chupi, akamshusha track nyepesi aliyokuwa amevaa, bado akiwa amekaa hapohapo,
akamkalia. Andy alifurahi akajiweka sawa akimpapasa kwa uchu kama ambaye
haamini kama amemshika tena Mina, huku penzi likiendelea bila kelele wala fujo.
Taratibu kwa hamu zote. Walikumbushana mbali wawili hao, wala
haikuhitaji muda mrefu kukumbushia penzi lao. Mina akajituma hapo akiwa ameichuchumailia, akimzungushia nyonga, mpaka mumewe akafanikiwa tena.
“Nakuwa mbinafsi?” Mina akacheka akiwa anatoka hapo. “Mwenzio
nafurahia Andy, wewe hujui tu!” Akaelekea bafuni. Andy akamfuata.
“Nitajisafisha tu, wewe oga.” “Unauhakika?” “Kabisa. Nataka umalize hapa bafuni
kwa haraka, upumzike. Ukija safari hii sikusumbui tena. Nakuacha ulale
kabisa.” Mina akacheka na kurudi kuoga tena akikumbuka ananyonyesha. Maji
yalikuwa mazuri. Akaoga na kutoka.
Akakuta Andy amesimama kitandani kwa mtoto akimuweka
sawa. “Ayvin ni mzuri sana. Amechukua na sura yako kidogo.” Mina akacheka kwa
furaha. “Asante Andy.” Akajua anashukuru kwa zaidi ya sifa ya uzuri
aliompa huyo mtoto.
Akamwangalia. “Nakupenda Mina. Na nakuahidi tutakuwa
sawa.” “Mimi nakuamini Andy.” “Basi njoo ulale, upumzike ili kesho uamke
na nguvu. Mtoto asikukute mchovu. Na ujue nakushukuru Mina. Nilikuwa nakutamani,
ila sikujua kama ungekuwa tayari na mimi.” Mina akamsogelea akampa kiss ya juu ya mgomo. Andy akajirudisha kochini,
akamlalia. Safari hii yeye ndiye akamfunika mkewe vizuri mpaka miguuni. Sababu
ya uchovu wa mengi, akauchapa
usingizi mzito muda huohuo, hapohapo kifuani kwa mumewe.
~~~~~~~~~~~~~~
Alilala Mina mpaka Pius akaingia hapo alfajiri, hana
habari. Andy alifungua macho wakati kaka yake akiingia. Akawaangalia vile
walivyolala, akapitiliza kitandani kwa mwanae bila salamu ndipo akauliza.
“Ameamka hata mara moja, au ndio na nyinyi mlijisahau?” Andy alisharekebishwa na Mina usiku, moyo shwari. Akili ilikuwa ikifanya kazi vizuri, hana hasira. Hakupaniki.
Akamuelezea kilichokuwa kikiendelea usiku huo kwa upande wa mtoto ndipo Mina
akaamka na kukuta baba mtoto amewasili.
“Nilikuwa nimechoka sana. Asante Andy kuwa hapa
na sisi.” Andy akambusu. “Karibu. Na unaonekana ulikuwa umechoka Mina! Ulilala kama mzoga!” Mina akacheka
akitoka hapo alipokuwa amekumbatiwa. “Sasa dripu hii ya mwisho haina dawa ya
usingizi. Wanataka aamke. Nenda kaoge, akiamka akukute upo tayari kwa
ajili yake.” Andy akamwambia mkewe. Mina akaona wazo si baya. Akaelekea bafuni
naye akamfuata na kuzidi kumuumiza Pius.
Alikaa naye huko bafuni akimsubiria Mina aoge kusudi
tu kumkera Pius na kumfikishia ujumbe kuwa yao yapo SAWA. Pia
kumkumbusha ni mkewe kihalali. “Kwani upo likizo?” Mina akaona aulize
akioga. Maana alikaa hapo kama asiye na ajira. “Hapana.” Mina akatulia
akimfikiria. Akaona aulize tena. “Unatakiwa lini kazini?” “Tokea jana.”
Akamuhurumia. “Pole Andy.” “Usijali. Naamini kila kitu kitakuwa sawa.”
“Naamini hivyo. Na asante kujali.” “Karibu.” Akaoga mpaka akamaliza
akimfikiria mumewe.
“Umefikia wapi hapa Dar?” “Nilikwambia nyumba ya
Kigamboni ilikamilika?” “Ndiyo.” Mina akaitika akijikausha. “Ujue nikikwambia
imekamilika, jua imekamilika kabisa. Ina kila kitu. Lakini nimefikia kwa
wazazi kwa kuwa sikujua utaamua kuwa wapi! Nilitaka mlipo ndipo na
mimi niwepo.” Mina akatulia. Kama kawaida Andy akamsoma na kujua kuna kitu
kinaendelea kichwani kwake.
“Nini?” “Andy!” “Wewe niambie hicho kinacho kukera.”
“Sio kunikera, ila sitaki kukuchanganya.” “Juu ya nini?” “Nimeamua
sitarudi kuishi pale kwa wazazi. Kama kusalimia tu ni sawa, lakini
sitaki kwenda kuishi pale. Sitaki.” “Upo tayari kwenda Dodoma
lini?” “Nakusikiliza wewe.” “Unauhakika?” “Kabisa Andy! Sina sababu ya
kunifanya nisiwe na wewe kama umetupokea.” “Basi acha tusikilize
ushauri wa daktari juu ya mtoto. Kama ni dawa tu, atakwenda kutumia hukohuko
nyumbani.” Mina akaendelea kuvaa, Andy akimwangalia kwa kujiiba, macho kwenye
simu.
~~~~~~~~~~~~~~
Wakiwa huko bafuni wakasikia sauti ya wazazi wao.
Wakajua wameshawasili. Mina akaharakisha, wakatoka. Wakasalimiana. “Kaka
alilala salama?” Mina akauliza. Akaona wanaangaliana. Akapatwa na wasiwasi.
“Vipi?” “Acha nikwambie tu ukweli. Nafikiri anawasiwasi umemuacha. Usiku
tulimkuta akiwa macho, alishituka kutoka usingizini, ikabidi dada yake aamke
akae naye. Lakini dada yake alikuwa amechoka. Ruhinda akakaa naye akimsomea
kitabu mpaka akalala. Asubuhi tumeamka na yeye anasubiria
sebuleni. Ameanza kulia, anakutaka.” Mina akatulia akifikiria.
“Naomba ukifika
nyumbani niwekee kwenye video nizungumze naye kama itasaidia. Atakuwa kweli anaogopa
akifikiri nimemuacha. Na muhakikishie leo tutakuwa naye.” “Kwani hali ya
mtoto inaendeleaje?” “Inavyoonekana muda wowote kuanzia sasa anaweza kuamka.
Wameacha kumuwekea hayo madawa yanayomfanya alale.” Andy akajibu yeye. “Basi
Mina ukae, ule. Maana hujui akimka atakuwa na hali gani.” Akashauri mama
Ruhinda.
“Sawa. Ila mjukuu wako huyo, ugomvi wake ni njaa
tu, naona imeongezeka na hilo la maumivu. Akishiba, hana neno. Atashikwa
na yeyote yule, na kucheka kama anakujua! Dada yao huwa anamwambia ataibwa.” Kidogo wakacheka. “Pole baba kwa kukesha na Ayan.”
“Hamna neno. Wewe umelala?” “Nimelala, Andy anasema kama mzoga!” Akakaa na kuanza kula.
“Asante mama kwa chakula.” “Msichana wako ndiye aliyedamka. Tena yeye mwenyewe bila kuamshwa. Nimeamka ili
kumuamsha, nikakuta yupo jikoni. Na anaonekana ana mkono mwepesi japo ni mdogo. Sasa sijui amepika vizuri au la!”
“Angalia kama utapenda. Lasivyo naweza kukimbilia mahali nikakununulia supu na
mtori.” Andy akatoa wazo. “Anapika vizuri tu. Tatizo lake ni usimpe
maelezo mengi kwa wakati mmoja. Anasahau kabisa. Ni wa kumkumbusha
mara kwa mara. Ila nampenda. Msafi halafu anawapenda kina Ayan.
Hutamsikia akilalamika.” “Anaonekana hata Ayan amemzoea kwa karibu.” Akaendelea
kula.
~~~~~~~~~~~~~~
Pius kimya tu macho kwa mwanae. Mara akaingia Paul.
Kisha Paulina na mumewe. Wakasalimia kama wenye haraka. Walikuwa wakiwahi
kazini. Walipojua habari za mtoto, wakajua watatolewa tu. “Basi tutawaona jioni
nyumbani.” Paulina akawa kama anaaga.
“Kama daktari akituruhusu mapema, na kukawa hakuna
mashariti magumu ya mtoto, Andy amekubali kutuchukua.” “Kwamba mnaenda
Dodoma na mtoto mgonjwa?” “Si ndipo alipo mumewe? Wewe ulitegemea
nini?!” Mama yake akamuuliza Pius kwa kushangaa sana. Andy kimya.
“Huyu mtoto ni mgonjwa mama!?” “Aliyekwambia Dodoma hakuna
madaktari na hospitali ni nani?” Mama yake akamjia juu. “Au wewe umesahau
kama huyu ni mke wa mtu?” “Ila Andy ungetumia utu tu. Huyu mtoto
hata sijakaa naye! Nimeletewa mgonjwa, na wewe anataka kuwachukua
wimawima.” Kila mtu akamtizama Pius.
“Wewe ulitakaje? Hembu niambie ukweli Pius.
Kama Mina angekuwa mkeo, ndio amerudi tu, ungemuacha wewe ukaondoka?”
“Ni swala la kuwa muugwana tu baba! Huyu mtoto hajakutana na mimi.
Ndio tunakutana. Kweli anashindwa kunipa mimi siku chache za
kukaa na mwanangu?” “Na yeye mtoto wake? Au umesahau na
yeye kama anamtoto na hakuwa naye?” Mama yake naye akaongeza swali.
“Wote ni mashahidi juu ya mahusiano yake na
mtoto wake. Hakuwahi kuzuiliwa kuwa na mwanae hata siku moja! Lakini
mbona alimtelekeza hapa mjini, yeye akaendelea na maisha yake kwengine?
Mlimuona hilo lilikuwa likimsumbua hata mara moja?” Andy
alimtizama Pius, ila akazuia maneno.
“Hata ukinitizama vibaya, Andy. Huo ni ukweli.
Na kwani huyo Mina ndio umemuoa leo? Si alikuwepo hapa mjini akihangaika
peke yake, wewe unamaisha yako kama kawaida? Hata weekend kuja kutulia nyumbani na familia yako ilikuwa
kama adhabu! Leo uharaka huo wa kuwachukua eti ili uwe nao, unaupata
wapi kama si roho mbaya tu kumkatili mwanangu?” Mina akaumia
sana. Aliona anamdhalilisha mumewe mbele ya watu!
“Kumbe kweli Pius wewe umekusudia kuharibu kwa
mwenzio!” “Hapana mama! Yeye mwenyewe ndio aliharibu kwake. Mwenyewe kwa
maamuzi yake hakuna aliyemsaidia. Na wala si mbali, si huyuhuyu alimpiga Mina
mpaka akamuharibu jicho kwa hasira za kuona amebeba mtoto wangu?
Leo mapenzi hayo mazito kwa familia ambayo hata haijali yanatoka
wapi kama si nia ya kumgeuza mwanangu akue bila baba kama anavyomfanyia
mtoto wake?” Mina akazidi kuumia. Andy kimya.
“Sikuwaambia huyu Pius ana pepo mchafu amemuingia?”
“Kati yangu mimi na wewe Paulina, mwenye pepo mchafu ni nani kama sio
wewe? Wewe si ndio ulikuwa mstari wa mbele kabisa kuwasaidia kuvunja
ndoa yao? Au umesahau?” “Wote nilishawapa sababu, na nikamueleza na
Andy, akanisamehe. Nilijua Mina alitaka kumtapeli, ndio
nikamuwahi kisheria. Nia ilikuwa kumsaidia Andy kama ndugu yangu
na juhudi alizoweka kwenye kutafuta mali.”
“Unafiki tu na uongo. Huna lolote. Tokea mwanzo
ulitaka kumtoa Mina kwenye familia. Yeyote unayeona ana mkaribisha
karibu Mina kwenye familia, unamuona ana mapepo. Katoe yako kwanza ndipo
uje kuninyooshea kidole mimi.” Mina alishakerwa na Pius, safari
hii hata utetezi wake ukawa bure. Kwa mara ya kwanza akamchukia
kabisa nafsini kwake.
Akamgeukia mumewe. “Kaoge na wewe upumzike Andy.
Ukimkuta kaka yupo macho, niwekee video nizungumze naye. Nitakwambia
kinachoendelea huku. Ila nenda ungalau na wewe ufunge macho kidogo. Mimi
nitakuwa na mama mpaka mwisho. Au mama unaondoka?” “Sina ratiba nyingine
leo, ni wewe tu na wajukuu zangu.” “Asante mama yangu.” Mina
akashukuru akimpuuza kabisa Pius.
“Unauhakika chakula kipo sawa?” “Kipo sawa kabisa.
Nashukuru Andy.” “Basi nitawaona baadaye.” Akainama na kumbusu Mina
mdomoni kwa kugandisha wala si kwa haraka kisha akamuachia.
“Asante Andy.” Akashukuru kwa deko akicheka kidogo, Andy
akaondoka bila yakujibu chochote kwenye matusi ya kaka yake.
~~~~~~~~~~~~~~
Pakazuka ukimya hapo, mwishoe Paulina na mumewe
wakatoka. Maana ilikuwa ni kama waliozubaishwa na maneno ya Pius. “Mama,
acha na mimi nianze siku. Kukiwa na chochote mniambie.” “Wewe kafanye kazi.”
“Na baba, utulize mawazo. Angalau sasahivi kila kitu kinakwenda sawa. Tulia na pressure ishuke.” “Nitakuwa sawa tu. Wewe wahi kazini.”
“Mina, uwe na siku njema.” “Asante.” Akajibu tu kwa
kifupi. Paul naye akatoka. Akawaacha hapo ndani kimya. Mina akaendelea kula
bila yakuongeza neno.
~~~~~~~~~~~~~~
Daktari alifika hapo kwenye majira ya saa nne, akakuta
Ayvin bado amelala. Akamwambia nesi amtoe dripu na Catheter ili wajaribu kumuamsha. Akafanyiwa kila kitu akiwepo
na kusafishwa tena vidonda na kufungwa lakini hakufungua hata macho.
Juhudi za
kumuamsha zikaanza. Daktari akaanza kumsugua miguu lakini haamki. Pius
akaanza kupatwa na wasiwasi. Wakamuamsha tena na tena, haamki. Mina
akaacha kula na kusogea karibu. Daktari akarudia tena na tena akitumia njia
zote, lakini Ayvin hakupepesa hata kope wala kujitingisha. Ile hali
ikazidisha wasiwasi. Wakajikuta wote wamesogelea kabisa kitanda kidogo alicholazwa
wakimchungulia kwa wasiwasi. Wakaendelea kumuamsha tena na tena bila mafanikio.
~~~~~~~~~~~~~~
Ni nini
kitaendelea?
0 Comments:
Post a Comment