majirani wakielekea huko wanakocheza mpira. Ikabidi Pam akimbilie huko kujua kulikoni. Akakuta watu wa hapo kijijini, majirani wanaangalia huo mpira wa Mill, mwanae na watu wengine. Akashangaa kulikoni!
Mama Eric naye
akiwa na wazazi wake nao wakaona wakajionee. Mpira ukaendelea. Ila sasa Mill
yeye timu yake alikuwa na mtoto mdogo tu, jumla wawili. Halafu Shema na watoto
wengine kama umri wake watatu. Basi huo mpira ukachezwa kwa ushabiki mpaka wakawashangaza.
Mwishoe timu ya
Mill ikafungwa. Shema akawa anafurahia sana na wenzie. Dogo
ambaye ni timu ya Mill akaanza kulia. Akawa anamkimbilia mama yake akiwa
analia, Mill akamuwahi. Akaanza kumtuliza watu wakimwangalia. Akampa maneno mazuri
mpaka akatulia, kisha akampa na zawadi ya mpira mmoja akimwambia aendelee
kufanyia mazoezi. Dogo akafurahia na kuondoka kwa furaha. Ndio wakarudi
nyumbani sasa.
Mill Na
Ushindani wa Mpira Huko Lushoto.
“Kwani kulikuwa
na nini?” Pam ikabidi kuuliza. “Shema huyo! Eti tumefika uwanjani, yeye ndio kocha.
Anapanga timu. Akaanza kwa mkwara. Kwamba yeye ndio mpangaji wa timu, hakuna
kuchagua. Nikashangaa mimi napewa yule mtoto, halafu wao wamejipanga
wanne kama vile mlivyowaona! Namuuliza mbona sisi timu yetu ipo vile,
akaniambia mimi na wale wengine pale, eti, mtu mchaguzi huyo si mchezaji.”
Wakaanza kucheka.
“Mbona bado!”
“Ehe!” Pam, mama yake, bibi na babu wanataka kujua zaidi. “Basi, mpira ukaanza.
Bwana yule mwenzangu yeye kumbe uchezaji wake si wamiguu tu,
anasaidiwa na mikono pia.” Walicheka mpaka machozi. “Sasa mkumbuke kocha
wetu, ndio na ni refa hapohapo. Basi mwenzangu akigusa tu ule
mpira, filimbi imepigwa, tunapokonywa mpira, tumecheza faulo.
Wenzetu wanatupiana mpira mpaka golini. Mwenzangu yeye kilio,
amepokonywa mpira, hanisaidii tena kupambana.” Walicheka. Mbavu hawana.
“Na timu pinzani
hawasubiri. Refa akipiga filimbi, tunapewa ule mpira wakati
mwenzangu akimalizia kilio, hajapiga teke hata moja, ananyang’anywa mpira.
Badala tupambane tuuchukue, yeye anazidi kulia. Basi tukaendelea kufungwa,
sisi kazi yetu ni kupokonywa mpira tunafanya faulo kila wakati.”
“Dogo alipoona
si kwamba hatufungi tu ila hata kucheza kwenyewe hatuchezi, kila
saa kipenga, akaenda kuuchukua ule mpira
akakimbilia nao kwao.” Walicheka. Walicheka mpaka machozi. “Sasa mimi nikabaki
nimeduaa! Mwenzangu kaondoka na mpira, analia. Hapo mkumbuke
kocha wetu ndiye mmiliki wa mpira pia. Basi, kocha anataka mpira
wake. Haya, ikabidi kwenda kumtafuta mpaka kwao.”
“Naenda, huku
ile timu pinzani inanifuata nyuma, wanasema tumeshashindwa, sisi hatujui
mpira. Ndio sasa ile kelele, wengine nao wakaanza kutufuata nyuma mpaka
nyumbani kwa yule mchezaji mwenzangu.”
“Nikamkuta amepakatwa
na mama yake, na yeye kapakata mpira wa watu.” Hawana mbavu. “Ikabidi
sasa nijitambulishe. Nikasema, mimi naitwa Mill, mume wake Pam, binti
wa Shelukindo, baba yake Shema, ambaye ndiye Kocha wetu kule mpirani.
Huyo uliyempakata tupo naye timu moja. Tulikuwa tukicheza naye, naona amekimbia
na mpira wa Kocha wetu. Pale nao wakaanza kucheka.”
“Ile timu
pinzani sasa, wakaanza kutusemelezea. Sisi hatujui mpira. Tukifungwa
ndio kulalamika, na dogo ndio kakimbia na mpira. Dogo hataki tena kurudi
uwanjani, anasema wale timu pinzani wazulumishi. Kila saa wanafunga wao
tu, sisi wanatupokonya mpira. Ukaanza ubishani, dogo hataki kutoa mpira
wa Shema. Tukazidi kukusanya watu. Basi watu wote pale wakajua sisi wafungwaji,
hatujui mpira.”
“Ndio ikabidi
nizungumze na mwenzangu, kwamba, twende tukafungwe kiume, mchezo
uishe. Mama yake akatuhurumia, akambemba na kumrudisha
uwanjani na mpira pia kashikilia. Ndio ile mechi pale niliyomsihi
hata afanyaje, ASITHUBUTU KUSHIKA mpira, atumie miguu tu. Ndio kama mlivyotuona
pale. Mwanzo mwisho tulikuwa na kazi ya kukimbia tu, hatujashika
mpira zaidi ya sekune 5.” Walicheka hapo. Walicheka sana.
“Shema!
Kakufanyia kusudi.” “Najua. Maana nilimwambia mimi najua sana
kucheza mpira. Sekondari walikuwa wakinitegemea. Sasa nahisi akanifikiria,
akaona anikomoe, abakie yeye mshindi hapa kijijini, mbabe
awe yeye peke yake. Ndio kunipa yule mtoto!” “Sasa na wewe ulishindwa
vipi kuwafunga?” “Nilijua ningemuharibia siku yake nzima! Kule
nimemuacha anasifika, kama sijui mcheza ligi kuu ya Uingereza!
Nimeona nimuache tu. Acha nioge, nikatembee kidogo na Pam.” Akaenda
kuoga na kuwaacha wakicheka.
Mill Aeleza
Ukweli Kwa Pam.
Walitoka
wakitembea taratibu mpaka sehemu moja ilionekana imebeba uzuri mzuri
sana wa asili. Kulikuwa na maji kweli yanayo tiririka kutoka milimani.
Maji masafi sana. Pakajitengeneza bwawa zuri sana hapo chini ya mlima panapo
tiririka maji, ungetamani kuogolea ila ilikuwa baridi.
“Aisee ni pazuri
sana hapa!” “Basi ndio sehemu za kujificha baada ya kutoroka shule au tulikuwa
tukitumwa kuni, tunakuja huku. Tunaogelea ndio tunakwenda kutafuta kuni, au
kuni kwanza halafu ndio tunakuja kuogelea.” “Wenzio wako wapi?” “Wamesambaa ila
hukuhuku vijijini. Walishaolewa na wana watoto wakubwa tu. Wengine
wakubwa kuliko Shema na wengine ndio hao wanacheza na Shema. Wapo.” Mill
akatulia, Pam naye akampa muda.
Walikuwa wamekaa
juu ya jiwe. “Uliyoyasema siku ile, yalikuwa kweli. Japokuwa ulizungumza
kwa hasira, lakini ilikuwa kweli.” Pam akawa hajaelewa ila akaumia.
“Ulisoma barua niliyokuwa nimekuandikia?” “Nilisoma.” “Nilikuomba msamaha
Mill! Na narudia kukuomba msamaha. Sikufanya vizuri, naomba unisamehe.”
“Nilishasamehe Pam. Hiki ni kitu kingine.” Pam akatulia.
“Juu ya wale
watoto. Ulizungumza jambo nilipokufuata kazini kwako. Kwamba nilikutana na tapeli
mwenzangu, akanibambikizia watoto wa tapeli mwenzetu.
Unakumbuka?” Pam akabaki ameinama. “Sasa yale maneno yakaendelea kunikera.
Na wale watoto walishanilemea Pam. Walikuwa wakorofi na hawanisikilizi
kabisa. Sasa kila nilipokuwa nikimwangalia Shema, jinsi alivyonipokea bila
maswali kwamba niliwatelekeza, halafu wale wakawa na kinyongo cha
kuwatelekeza, mama yao aliponifunga…” Pam akazidi kushangaa.
Ndipo ikabidi
sasa Mill amsimulie kwa undani, mwanzo wake na Kisha, jinsi zile mimba
zilivyotungwa, alipomfunga jela na kumuhamishia Trey nyumbani kwake. Akaishia
kumtoa jela kwa makubaliano ampe hao watoto, halafu mali zote amuachie
Kisha.” “Haiwezekani Mill!”
“Acha mama. Na
Kisha wala hakupinga. Alisema waziwazi mbele yangu na wanasheria wetu
kwamba watoto watakuwa ni wa Trey kwa sababu hawakuwahi kuachana,
hata tulipokuwa naye.” “Mill!” Pam akazidi kushangaa. “Kabisa. Kulalamika
siwezi, maana kweli ile ilikuwa ndoa ya mkataba. Nilimlipa
akanifanikishia kupata uraia. Nilibaki naye kila mmoja akiendelea
na maisha yake, japo nakiri wazi kabisa, kwakweli alikuwa na heshima.”
“Hata siku moja
sijawahi mkuta na huyo Trey. Wala usingemkuta kwenye simu na wanaume,
labda aliyafanya hayo nilipokuwa sipo nyumbani. Ila nilipokuwa
nyumbani, ni ukorofi wake tu, ila sikuwahi hata muhisi
anawanaume.” Pam akaumia sana akijua anamlenga yeye.
“Mimi sio muhumi
Mill! Na wala kwangu pale si dangulo! Tafadhali naomba uniamini!” “Hata nisipokuamini,
au nikaamini, haina maana Pam. Tuyaache hayo. Turudi kwangu na kile
ninachotaka kukuomba.” Pam akatulia.
“Basi, hakuwa na
shida akasema yeye atachukua watoto wao kitu kilichokuwa kikinitia wasiwasi kwa
sababu kisheria wale watoto ni wangu na niliwapigania kwelikweli. Hata yule
mwanasheria alikuwa akisema, wangekuwa watoto wa kawaida, hakika ningewalea.”
“Kweli Mill?” “Kabisa. Uwezo ninao, kungekuwa na shida gani? Ningewalea
ila ningewaambia ukweli, ili kama wangekuwa wanataka kurudi kwa wazazi
wao, kila likizo ningewarudisha. Lakini nilifika mwisho Pam.”
“Bwana watoto walilia
wale! HAWAKUTEGEMEA.” “Kwani
walikuwa hawajui?” “Sikuwaambia kwa sababu wakati naenda nao, sikujua
hatima yetu. Kisha ni mkorofi sana. Hakubali kitu kwa urahisi.
Ila kwa jinsi alivyokubali safari hii, mpaka akanishangaza ndio nikajua ALIJUA.”
“Wale watoto
ilibidi kuwaambia ukweli. Aisee, walilia. Safari hii mpaka wakaomba msamaha, wanataka warudi na mimi kwa
ahadi ya kubadilika. Ila nikaona sitaweza kuwa nao wao,
pamoja na Shema. Kwanza ni waongo sana. Wangeweza nikubalia pale mbele
za watu. Nikapewa tena kisheria, wakaja nigeuka.”
“Nikarudi nao
huku nyumbani, wakarudia tena tabia zao, kama mama yao, wakati wameshaniharibia
mahusiano na Shema, mtoto mzuri asiye na hatia. Halafu damu yangu! Nikajiambia hapana.
Mwanangu hawezi endelea lipa garama ya makosa yangu. Ndio nimewaacha
huko, na mama yao, ila nasikia baba yao amekimbia baada ya kumtapeli mama yao.”
“Tena!? Si walikuwa wapenzi wa muda mrefu?” Pam akashangaa.
“Kwa mujibu wa
Kisha mwenyewe. Kwamba wameuza mali zote, ndio akakimbia. Kwa hakika nawahurumia
wale watoto. Maisha niliyoishi nao, na kinachowakabili mbeleni!
Mungu awasaidie tu. Lakini hayanihusu tena. Nimerudi.
Sasahivi nipo mimi kama unavyoniona, na Shema tu.” Kimya.
“Ndipo linakuja OMBI
langu sasa. Kwa kuwa wewe mwenzangu umepata mtu ambaye unataka
kuendeleza naye maisha, na ninaamini Mungu atawajalia watoto, naomba
mimi ambaye bado, nimchukue Shema.” Alishituka Pam, kama anatolewa roho.
“Nyie Mill!”
“Kwa hiyo wewe unataka Shema Mgini, alelewe na Mgaya wakati mimi mwenyewe nipo?”
“Acha nikwambie ukweli juu ya Mgaya. Ni kweli ananipenda sana. Ila
unaona mpaka sasahivi sijamleta huku au hakuna muendelezo ni kwa
ajili ya huyohuyo Shema. Ni kama hajampokea. Mazungumzo yake ya baadaye
ni mimi na yeye na watoto tutakao zaa, lakini hutamsikia mipango juu
ya Shema.”
“Au hutamsikia
hata mara moja akitoa zawadi kwa Shema hata ukimpa habari zake
njema. Umsifie, pengine amekuwa wakwanza darasani! Au amepewa
zawadi shuleni, au chochote kile kizuri kumuhusu Shema, hutamsikia
akiongeza neno. Hiyo ikanifanya nisite kwake. Na Shema mwenyewe ni kama unavyomuona
au kama umemuangalia vizuri, akili yake imekua ya darasani tu, na kwenye
mpira, lakini kwengine hajiwezi bila mimi.”
“Sasa nikawa
nikiwaza, leo ndio najiingiza kichwakichwa kwa yule mwanaume, itakuaje
kwa Shema! Nikabaki mguu mmoja, ndani mwingine nje. Ukweli kwao wananipenda
sana. Sana. Hata wazazi wake wamenipokea vizuri tu. Yeye hajatoka
kwenye familia kama hivi sisi. Kwao ni ile familia inayoamini ndoa TAKATIFU, ya mke mmoja. Wazazi wake wapo pamoja mpaka
hivi tunavyozungumza, na ni wale wakristo wenye upendo.”
“Kaka zake Mgaya
na dada zake, ni wasomi, nao ni wale wenye ndoa takatifu na ni wakarimu
mno. Lakini hapo tu kwa Shema ndipo nimeshindwana na Mgaya ndio maana
mpaka leo umenikuta sina ndoa bado. Ila nafikiri kama angempokea Shema,
pengine angeshanioa.”
“Kumbe ndio mpo serious
kiasi hicho!” “Ndiyo na hapana. Wala nisikudanganye. Ndiyo, kwamba ananipenda
na anatamani kunioa hata kesho. Ila ni mimi tu.” “Kwa hiyo?!” “Hata
sijui Mill! Na yeye pia nimemwambia hivyohivyo juzi tulipokuwa tukizungumza.
Nafikiri wewe ulipokuja, umemtisha ndio ameongeza pressure ya
kutaka tuoane.” Akawa kama amemaliza.
Mill akamgeukia
vizuri. “Sasa umemjibu nini?” “Hata sijui Mill!” “Hapana Pam. Lazima kujua.
Umebeba hatima yangu na mwanangu. Na wewe ndio tunakuangalia.
Huwezi kubakia njia panda.” “Naomba muda Mill. Tafadhali.”
“Kwamba hujui au!?” “Najua lazima niolewe. Sitaki kubakia hivi
peke yangu. Kilichokuwa kikinifanya nisite ni kumuona Shema kama mtoto wa
kambo nikiwa nimeolewa na Mgaya. Sasa, sasahivi wewe upo, na unampenda
hivi Shema, inanifanya nitulie na kufanya maamuzi nikijifikiria
na mimi pia. Sijui kama unanielewa?”
“Maana mwanzoni
nilikuwa nikimfikiria Shema tu. Ila jinsi ulivyorudi, inanifanya nijifikirie
na mimi pia. Halafu kingine, Mgaya si mtoaji kama hivyo wewe. Si
mtu atakukumbuka kwa chochote na mimi kuomba ni mzito
sana. Lazima nitafute kazi yakueleweka kabla sijafikiria mambo
mengine. Mama na kina bibi wananitegemea. Zaidi mama. Nisipomkumbuka
mimi, basi jua ni mzigo wa wakina bibi ambao wanatunzwa na mjomba au niseme
shangazi, mke wa mjomba.”
“Sijatulia Mill.
Nina mambo mengi naona nahitaji kuyakamilisha kabla sijafikiria
maswala ya ndoa na kabla sijamtoa Shema moja kwa moja. Ila nina wazo.
Kwa jinsi unavyompenda Shema na kumjali, tuanze kumzoeza taratibu
kuja kwako hata kulala. Akiweza…” “Kwamba ndio hawezi kulala bila wewe!”
“Hakika hawezi. Bibi yake anakuwa na hamu naye. Anamwambia walale naye.
Anaweza kukubali kwa lisaa, anamwambia hapati usingizi bila mimi kuwepo
kitandani.”
“Pam! Ujue Shema
ni kijana mkubwa sana!” “Naelewa. Ila mazingira tuliyokuwa nayo ni ya chumba
kimoja, kitanda kimoja. Nimelala naye tokea analetwa hapa duniani mpaka leo. Hajui
maisha mengine bila hivyo.” Mill akakwama.
“Tusikate
tamaa. Taratibu. Unaweza hata mchukua siku za ijumaa akitoka shule, ukamjaribisha
kumwambia akalale kwako. Akiona kuna chumba kinamsubiria, anaweza
akajaribu.” Akatulia.
~~~~~~~~~~~~~~
“Kazi unataka
kutafuta wapi?” “Popote pale. Mwenzio sijasoma Mill. Sina sifa za kuchagua
kazi. Yeyote na popote.” “Mimi nina kliniki yangu ndani ya hospitali ya familia
ile uliyowaona wamekuja siku ya Shema anapewa zawadi. Unawakumbuka?” “Siku ile
nilikuwa na maumivu, niliyemuona pale kwa hakika ni Shema na wewe. Hata
wale wanao siwakumbuki vizuri.”
“Basi
walikuwepo. Ni kliniki yenye mashine ya vipimo mbalimbali. Nimeajiri watu
baadhi. Na wewe unaweza pata nafasi. Nitakulipa vizuri na inakuja na
gari na nyumba.” Pam alicheka sana.
“Yaani mbali ya
mshahara utanipa nyumba na gari!” “Kabisa. Ila si wote nawafanyia hivyo.
Ni wewe nakupa kwa kunizalia Shema. Na usiogope. Gari linakuwa lako
kabisa kama lile la mwanzo. Na nyumba tunaandikishana kabisa. Ni padogo
kama pale tulipokuwa tukiishi pamoja.” “Kwa Mike!?” “Ewaah!” Pam akakunja uso.
“Inamaana
nitakuwa nikiishi nyumba ndogo ndani ya uwa wako?” “Na sitakubughudhi. Unaingia
na kutoka utakavyo. Utakua huru.” Pam akatulia. “Najua umesema umejitengenezea
watu wako, lakini Pam, pale mnapoishi, sipo. Pako duni sana. Najua
ulifanya uwezavyo kukabiliana na maisha, lakini sasahivi nipo. Na
si lazima ukaachana urafiki na kina mama Batuli.” Pam akacheka.
“Ushawajua
majina?” “Nitafanyaje na ndio hao nimeambiwa ni bora, wanaaminika kuliko
mimi! Halafu wananitunzia na mwanangu! Tafadhali fikiria.” “Sina
haja hata yakufikiria Mill. Nilivyo na shida! Hakika nimekubali
na nakushukuru sana. Hata kwa magoti nakushukuru.” “Sasa acha kupiga magoti
bwana!” “Ujue nakushukuru sana. Nilikuwa natamani mabadiliko, lakini hapakuwa
na dalili. Asante sana.” “Karibu.” Wakatulia.
~~~~~~~~~~~~~~
“Ungependa
tukitoka hapa tukatembelee mbuga za wanyama kabla hatujarudi Dar?” Pam
akamwangalia. “Unamaanisha sisi?” “Wewe na Shema.” “Kwani ulitaka tuondoke
wote?” “Si mnahama? Ndio nafikiria kupata muda kabla shule hazijafungua, aanze
kuzoea mazingira.” Pam akatulia.
“Unaonaje?”
“Ningependa Mill! Ningependa sana. Asante. Nashukuru.” “Pam kwa shukurani!”
Akacheka. “Nayajua maisha kwa kuyaishi Mill! Na nimekuwa na Mgaya, nimemuona
jinsi inavyomuwia vigumu kutoa. Si jambo rahisi.” “Kwamba ndio mgumu
hivyo!” “Nahisi nikilema chake. Yaani mnaweza kukutana hata kwa
kinywaji. Mkala tu chips yai, lakini utamuona jinsi anavyohangaika
ikifika kwenye swala la kulipa. Mpaka inabidi kulipia.”
“Haiwezekani Pam!”
“Hakika.
Usifikiri ni bure kuniona nipo naye njia panda! Kwa binadamu kama
binadamu, ni mwanaume mzuri tu. Hana makuu. Si muhuni hata. Pale mtaani
anasifika. Mpole na mnyenyekevu.” “Hilo nimeliona. Japokuwa nilimpandishia
sana, aliweza kutulia mpaka akanishangaza!” “Basi ndivyo alivyo. Lakini!
Mmmmh!” Wakatulia.
~~~~~~~~~~~~~~
“Mill.”
Akamwangalia. “Najua ulinihangaikia nije kuwa na wewe Marekani. Lakini
natamani ungeniambia juu ya maswala ya kuoa.” Mill akavuta pumzi
kwa nguvu na kuzishusha akashindwa cha kujibu. “Ila nashukuru kuja huku.
Mama amefurahi sana, SANA. Alikuwa anasononeka,
anajua nitaishia kama yeye ndio maana nilijiambia lazima niolewe ili tu kumfuta machozi. Asante
kwa kuja huku milimani.” “Nakupenda Pam. Nakupenda sana. Hakuna umbali nitashindwa
kwenda kwa ajili yako.” Pam akainama akifikiria.
Mwishoe
akamuuliza. “Ulitaka tuondoke lini?” “Ukiwa tayari, hata kesho tuondoke. Huku
kuna shida ya mtandao. Mambo yangu ya mtandaoni yanakwama. Ni hilo tu. Ila
nimejichukulia kilikizo ili niwe na nyinyi.” “Basi acha
tujiandae, tuondoke hata kesho mchana.” Wakakaa hapo wakijipanga, mwishoe
wakaondoka kurudi nyumbani.
Hatimaye Mill,
Pam & Shema Mapumzikoni.
Kesho yake
majira ya saa sita, watatu hao wakawa wakiondoka Lushoto ila akawa ni kweli ameosha.
Kila mtu pale kijijini alishajua Pam ni kama mama yake tu. Kuzalishwa na
kuachwa. Wenzie Pam walishakuwa na familia za kueleweka hapo kijijini na
walitulia na waume zao. Kitendo cha Mill kurudi na kujitambulisha ni mumewe
hata kwa majirani! Ikawa amemfuta machozi hata mama Eric.
Hata Mill
aliweza muona jinsi alivyokuwa na furaha hapo ndani ya gari. Alikuwa ametulia
kiti cha mbele, Shema cha nyuma, ila akiangalia nje ya dirisha. Mara kadhaa
aliweza ziona dimpozi zake kama ambaye amekumbuka kitu kikamfurahisha.
Hakuacha kumuonyesha Mill hiki na kile huko barabarani ilimradi tu alijisikia
vizuri.
Njiani
walisimama na kupata mlo mzuri kwenye migahawa ya maana. Ukweli watatu hao walipendeza,
ungependa kuwaangalia. Pam alivaa kila kitu alichokuwa ameletewa na Mill.
Akanukia vizuri kama mtoto wao. Mill alikuwa amejawa na furaha ya
kupitiliza.
Walifika Arusha
ilishakuwa usiku. Mill akalipia vyumba viwili kwenye hoteli nzuri sana ya
kitalii. “Nimechukua vyumba viwili.” “Mimi nalala na mama.” Akawahi Shema kwa
haraka na akili zake za miaka karibu 10, lakini mrefu kuliko huyo mama yake.
Pam akacheka kimyakimya.
“Hapana
Shema. Umeshakuwa mkubwa. Nakuomba jaribu kulala peke yako.” Bwana mtoto
alishangaa huyo, kama baba yake anamuomba roho. “Kwa nini!? Mimi huwa nalala
na mama yangu!” Ikabidi Mill ashike kazi ya kumuelezea, Pam ametulia kimya
akiwasikiliza huku Shema akiuliza maswali ya kushangaa sana wakielekea
huko vyumbani. Mpaka wakala na kumaliza, bado Mill anamuelezea mwanae ila
hawafiki popote. Shema haelewi kabisa. Pam kimya akisikiliza, akijua
lengo la Mill ni kumzoeza ili akihamia kwake aweze kuwa akilala peke yake
asijue anajingine.
Akajieleza mpaka
akaishiwa, ikabidi aombe msaada wa Pam. “Wewe ushamuuliza Dula kama huwa
analala na mama yake?” Akatulia akifikiria mpaka akapata jibu. “Ila Dula yeye
mtoto mbaya, sio kama mimi mama!” Akampa mifano ya rafiki zake wote pale
mtaani tena wadogo kuliko yeye. Ndipo akaanza kutulia.
“Ni kwa sababu
sikuwa na uwezo Shema. Lakini si sawa.” Akapoa. “Jaribu mtoto mzuri.
Tuanze taratibu. Mimi nitakuwa hapo kitanda cha pembeni. Silali mpaka wewe
ulale.” “Na mimi nitakaa hapohapo na mama. Mkilala tu, ndio naondoka.”
Akakubali.
Kila mmoja
akaingia chumbani kwake kuoga na kuvaa nguo za kulalia. Vyumba alivyokuwa
amekodi milango ya ndani inaingiliana. Kwa hiyo huhitaji kutoka nje koridoni
kuingia chumba kingine. Mill alimaliza yeye kuoga akahamia chumbani kwao.
Akajilaza kitanda alichojua atalala Pam.
Shema yeye
alishaoga akabaki kitandani kwake na baba yake kitanda kingine. Pam alioga huko
bafuni na kubadili nguo kabisa akatoka na nguo za kulalia ila za heshima.
Akaanza kubabaika pakukaa. Mill alitulia kimya kama hamuoni huku
akizungumza na Shema, wote wamelala kila mmoja kitandani kwake, akawa
amemuachia Pam nafasi.
Akaanza kukaa
kwenye kochi. Akatulia hapo kwa muda kisha akamuona anahamia kwenye
pembe ya kitanda. Akaanza kumuona anahangaika baridi, akamuhurumia. “Njoo
nikufunike hapa. Nitakukumbatia, hutasikia baridi.” Akacheka kwa wasiwasi kama
amwambie huoni mtoto! “Njoo.” Akajisogeza na kulala kwa mbele.
Mill akamfunika
na kumchungulia kwa mbele. “Naweza kupunguza baridi kama imezidi au niwapigie simu
mapokezi wakuongezee comfoter?” “Naona vyote. Punguza baridi na
naomba comfoter jingine.” Akanyoosha mkono na kuwapigia simu mapokezi
kuomba comfoter mbili, kisha akapunguza baridi kidogo tu.
“Mkijifunika na
mkalala kwenye kiubaridi, ndio mtalala vizuri.” Alishamjua Mill kwa kupenda
baridi kali. Baada ya muda mfupi tu wakaletewa. Moja akamfunika mwanae, jingine
akamfunika Pam. “Huwa mnaangalia movie?” “Kwetu hatuna tv.” Akajibu
Shema. “Lakini kama ni kuangalia movie, mngependa movie gani?” “Ya
kupigana.” Akawahi Shema. Wote wakacheka.
Akatafuta movie,
akaweka. Pam akashangaa na yeye anaingia ndani ya yale macomfoter kitandani
kwake. Akatulia ila rohoni akifurahia. Akamsogelea vizuri kisha
akamkumbatia kwa kumvuta kabisa kwake kama katoto kapaka. Pam akacheka
akijisogeza. Mill akamkumbatia vizuri.
“Unavyojua kukumbatia
Mill! Kama kifaranga cha kuku!” Mill akacheka. “Nilivyokumiss kukuweka
mkononi!” Pam akacheka taratibu na kutulia, movie ikiendelea. Akazipata
sawia pumzi zake. Pam mwenyewe akaanza kulemewa.
Aliujua mchezo
wa Mill. Alijua kuuchezea huo mwili kupita atakavyoeleza Pam mtu akamuelewa.
Mill akawa ametulia tu. Mara wakaanza kusikia Shema anakoroma. “Huyo mpenda movie
za ngumi, ashalala.” “Ndio anakoroma hivyo!” “Hapo bado. Anakoroma
huyo! Sababu ya kuchoka kucheza mpira siku nzima.” “Sasa unalalaje?!” “Inanibidi.
Sina jinsi Mill! Ni mwanangu na sina pakumuhamisha. Hivi leo ndio kwa
mara ya kwanza amelala peke yake, tokea mama alivyoondoka naye akiwa mdogo
sana, tena kwa muda mfupi, maana nilishindwa kulala kabisa alivyoondoka
naye. Hawezi kulala bila mimi. Mpaka nahisi uchovu ndio umemlaza na
kujua nipo hapa.” Wakawa wanamwangalia.
“Ila kama ni
mtoto mzuri, hakika Mungu amenipa. Nakushukuru kwa kunizalia na
kunitunzia. Nitakuenzi daima.” Pam akacheka na kujirudisha pale
alipokuwa amekumbatiwa.
“Nenda na wewe
kapumzike Mill. Umeendesha muda mrefu! Najua umechoka.” “Nigeukie nikuulize kitu.” Akageuka.
Akambusu usoni. Pam akacheka. “Huna hamu na mimi kabisa, Pam? Maana
nimeona nilikushika ukaruka kama nimekuchafua! Ndio umepetwa kinyaa
na mimi kwa kiasi hicho?” “Ni tofauti kabisa na hivyo unavyofikiria.” Mill
akakunja uso kama hajamuelewa.
“Pale nilikuwa
nakimbia kwa sababu ulinishika, ukaamsha hisia zilizokuwa zimekufa
Mill. Halafu tulikuwa nyumbani, kina mama walikuwa nje wanasikia kila kitu.
Nikaogopa nisije nika…” Akakwama. Mill akaanza kucheka kwa furaha.
“Kumbe ndio hujiwezi
hivyo mbele yangu!” “Unanifanyia makusudi Mill wewe! Bila kujali madhara
yake!” Mill alicheka hana mbavu. “Mimi nilikuwa nikiangalia jeraha. Kosa lipo
wapi?” “Huna lolote! Unaangalia jeraha kama ulivyokuwa ukinifanyia zamani,
ukitaka kufanya mambo yako?” “Mambo yetu bwana!” Halafu akawa
kama amekumbuka kitu alichosema.
“Unaposema madhara,
unamaanisha madhara gani?” “Bado nipo kwenye mahusiano na Mgaya! Na wewe
unataka kuanzisha jambo wakati sijafikia muafaka na yeye.” Hapo akapoa
mpaka uso ukabadilika.
“Uliondoka
Mill. Ukaoa na kuanzisha familia huko. Kweli ulitegemea mimi nibakie vilevile?
Mpaka lini?” “Hapana. Upo sahihi. Upo sahihi kabisa.” Akamuachia kabisa,
akimfunika.
“Nisikilize
Mill. Najua kwa hakika Mgaya akinioa itamvuruga Shema, haswa akija
kuelewa maana ya ndoa hapo baadaye, na wewe ukiwepo.” “Unafikiri
sasahivi haelewi?” “Mrefu kwa kimo tu. Ila akili yake huyu ni ya mtoto kabisa.
Ukikaa kuzungumza naye ndio utajua ni mtoto na mawazo yasiyo na hatia.
Mgaya ameshindwa kabisa kumpokea.”
“Unajirudia
Pam. Hayo yote ulishayasema. Na najua wewe unaakili, unajua kitu
chakufanya, ila unaogopa kwa sababu nilishakutenda, na Mgaya ni
kama unauhakika wa kuwepo kwake sio kama mimi. Unashikilia huko, na huku
kwangu unajua kutoka moyoni kuwa nakupenda, ila unaogopa kurudia kosa
japokuwa nimekuahidi haitakaa ikatokea tena.”
“Hujaniambia
hivyo Mill! Na wala sina uhakika ni kwa nini isitokee tena. Wewe ni raia
wa Marekani, Mill! Inamaana upo hapa nchini kama mgeni. Ukiamua kuondoka
tena?” “Kwa sababu IPI initenge na mwanangu au wewe? Nilifanya yote kwa
ajili ya sisi tuwe pamoja. Nimekamilisha kwa makosa, na kulipa garama
kubwa sana kwa ajili yetu. Narudi kwako na wewe unaniadhibu!”
“Sasa nakuadhibu
kwa lipi?!” “Najua, unajua mimi si malaya, Pam. Unajua kabisa sikuwa na
mwanamke tokea wewe zaidi ya Kisha.” “Ningejuaje?” “Nimekwambia! Na najua kwa
vile ulivyo na akili, ulishajua kwa tabia yangu sijafanya uzinzi huko
nje.” “Mimi sijui!”
“Basi jua hivi.
Tokea mimba ya Mia, sijalala na mwanamke kwa hofu ya kumpa mwanamke
mwingine mimba au kusingiziwa jambo kwa vile nilivyokuwa nimefanikiwa
kule Marekani. Niliogopa kuanzisha lolote au hata kuwa karibu na wanawake
sababu ya kuja kusingiziwa jambo, maana wanawake wa kule hawakawii kukusingizia
kuwashika kwa namna wasiyotaka wao, wakakusingizia ukaishia jela. Ndio
nikawa namuachia Kisha awe anadili na wafanyakazi wote, mimi nikajiweka
pembeni.”
“Sasa kwa namna
hiyo unafikiri naishije mimi na sina tatizo lolote kama mwanaume, kama
si na wewe kunitesa kusiko na sababu?” “Mimi sikujua!” “Najua unajua,
ila unaogopa. Na sina jinsi ingine ya kukuaminisha kuwa nipo kwa
ajili yako isipokuwa hivi ninavyokwambia Pam. Sasa ni juu yako. Ila na mimi ujue
sitaendelea hivi daima. Sina sababu yakuendelea kujitesa. Kama unaendelea
na Mgaya, niambie na mimi nijue moja. Nianze kufikiria jinsi ya kutafuta
MKE, maisha yaendelee.”
“Moyoni na
akilini bado nakutambua kama wewe ni mke wangu na ndio maana kila mahali najitambulisha
hivyo.” “Na mimi nakushukuru kwa hilo. Umenirejeshea heshima pale
kijijini.” “Lakini siwezi kuendelea kuwa mume jina, Pam! Siwezi
kuendelea kujitesa bila sababu! Kama umenikataa moja kwa moja, niambie
nijue moja.”
“Naomba muda
Mill!” “Mpaka lini?” “Niweke sawa jambo la Mgaya. Huyu mtu amenitambulisha
mpaka kwao! Ndugu zake wote wananifahamu na wanajua siku moja atanioa.
Siwezi nikahitimisha kiholelaolela au bila kufikiria.” “Sasa wakati ukihitimisha
huko, mimi unanisaidiaje?” “Mill!?” “Kwa hiyo unataka usikie nimefungwa
kwa kubaka ndio uelewe nilizidiwa?” “Hakuna kubaka wala
kulala na mwanamke mwingine.”
“Hunitaki,
wivu wa nini?” “Naomba utulie Mill.” “Kwani hilo ni tatizo. Wewe niambie
natuliaje na hali hii.” Akajitoa kwenye shuka kabisa, mzee amesimama
wima.
Pam akaanza kucheka. “Unanifanyia kusudi
Pam!” “Wewe usipeleke mawazo huko. Tulia tuweke mambo sawa halafu…”
“Ndilo nililokuwa nikilifanya miaka yote. Na ndio maana nikaweza. Sasa,
sasahivi wewe upo, siwezi tena. Labda kwa kipindi hiki uwe unanisaidia.
Halafu hakuna kulala na Mgaya tena.” Pam akakaa.
“Kwamba
unamaanisha tuwe tunafanya mapenzi!?” “Kila ninapojisikia,
unanisaidia.” Pam alicheka mpaka machozi. “Hivi unajua nakujua sana Mill wewe!
Sitakaa nikamaliza kukusaidia. Na naijua dozi yako. Ni
asubuhi, mchana na jioni. Na ndio maana vya asubuhi vilikuwa vikikutana na vya
mchana, kisha usiku. Tunajikuta hatutoki kitandani, ni mapenzi mfululizo.”
“Nitakuwa na kiasi.” Pam akacheka akimtizama.
“Hakika
tena. Nitakuwa na kiasi. Ila na wewe ukitaka nikusaidie
usisite kuniambia. Mimi si mchoyo. Muda na wakati wowote.” Pam alicheka
mpaka machozi tena. “Mill! Kwamba wewe ndio mwema wa kiasi hicho?”
“Kabisa. Haswa kwako.” “Sawa, tutakuona.” Ikawa amehamasika kupata
penzi.
Akaruka
kitandani na kuanza kupata kiss iliyomsisimua sana Pam. Akaanza kulegea.
Ni Mill wake. Mwanaume wake wa kwanza. Alishakuwa na hamu naye tokea anamuona
aliporudi. Ile mikono mwilini mwake, akajiachia kabisa. “Tuhame hapa, Mill. Sio
sawa mbele ya Shema.” Akatoa wazo lakini Mill akaendelea kunyonya shingo
aliyokuwa akiipenda, lakini gafla akagutuka.
Tamu Yageuka
Shubiri.
“Subiri
kwanza Pam. Ulipokuwa ukijamiiana na Mgaya, mlikuwa mkitumia kinga?!”
Pam alishituka, hakuamini. Kicheko chote kikamuisha. “Nina maana
yangu Pam. Sasahivi tuna mtoto. Uzembe wowote ule unaweza muathiri
yeye zaidi. Nayajua madhara ya kufanya ngono bila kinga. Imenigarimu
muda na asilimia 80 ya mali yote niliyotafuta kwa shida sana huko ugaibuni.”
“Kama ningekuwa
nikitumia kinga na Kisha, ningeweza kujua kwa haraka kama wale watoto si
wangu, na pengine hata asingeweza nisingizia. Lakini nilifanya uzembe.
Madhara yake ndio hayo Mungu amenitoa kwa garama kubwa sana.
Lakini nimetoka.”
“Kosa
la maradhi ya kudumu kama UKIMWI, tusipo kuwa waangalifu tutamuacha
Shema yatima. Nataka kujua kama mlikuwa mkitumia kinga? Na mara
ya mwisho kujamiiana ni lini ili hata tukienda kupima, tujiridhishe.”
“Mill!” Pam hakuamini.
“Hakika katika hili sinaga masihara.
Asiee nipo makini mno. Baba yangu alikufa na kisukari. Mungu alimuokoa
na UKIMWI, lakini kwa
kumsikia yeye mwenyewe akisema tena akiwa amelewa, akizungumza na wale vijana
wake kuwa ilikuwa hata alewe vipi, hasahau kinga na hajawahi
muamini mwanamke wa barabarami mpaka akae nao awachunguze ndio alikuwa
akijiachia, tena kwa lengo la kuzaa nao. Ndio mama zetu, na alikuwa akisema
alitakaga watoto wengi. Alikuwa hazai hovyo na kila mwanamke.
Na alisema wazi, katika watoto wake wote, hajawahi zaa na wanawake aliokuwa
akikutana nao ulevini. Kwamba hajawahi bambikiziwa watoto, wote alijua
ni wake bila swali, kwa aina ya wanawake waliokuwa wakirudi na watoto
wake.”
“Kwa hakika kiliniingia
sana hicho kitu. Na kwa kuwa nilitaka kuwa tofauti na yeye tokea zamani, mimi
nikaongeza uwaminifu na kuacha tamaa za hovyo kwa wanawake, na
bado nikaangukia kwenye mitego ya Kisha. Na nimeapa sitarudia hilo kosa.
Ndio maana na wewe na kuuliza. Mara ya mwisho kujamiiana na Mgaya
ilikuwa lini? Je, mlikuwa mkitumia kinga?” “Kwamba huniamini?!” Akauliza
kwa jazba.
“Wewe, nakuamini,
ila Mgaya simuamini hata kidogo kwa sababu simfahamu kwa undani.
Sijui siku alizokuwa akikuhitaji na wewe upo busy na mtoto, haja zake
alikuwa akitimiza wapi! Hilo jibu hata kama unamuamini
vipi, huna uhakika nalo. Ndio maana nakuuliza Pam. Kwa heshima kabisa.
Kama unaona haupo tayari kunijibu, tafadhali nijulishe utakapokuwa
tayari.” Pam hakuamini.
“Japokuwa NAKUHITAJI sana, lakini sitahatarisha maisha yangu ambayo ni hatima ya Shema.” Akakaa
kabisa akimtizama. Kimya. Pam akishindwa kujibu. “Basi, kwa kuwa wewe haupo
tayari na mimi, nakuacha mpaka utakapokuwa tayari, utanijulisha kwa kuyajibu
haya maswali. Vinginevyo sitakubugudhi, tutalea huyu mtoto kwa upendo
wote.” Akaendelea.
“Nafasi ya kazi
na ahadi ya nyumba pamoja na gari vipo palepale. Havitabadilika.
Tutatumia ua mmoja, nyumba yako itakuwa ikijitegemea. Kama utaendelea na
Mgaya, sitakuzuia. Ila kuwa makini, halafu nijulishe siku anakuja kukutembelea,
ili Shema ahamie nyumba kubwa.”
“Mtakapokuwa
tayari kabisa kwa ndoa, nashauri tuzungumze na Shema. Ajifunze kutoka
kwako na mimi nitafanya hivyohivyo. Kitakapofika kipindi naoa, sitafanya
siri. Nitatembea naye kwa hatua, ajue njia sahihi ya kupata mwanamke kihalali.”
Pam hakuwa akiamini. “Kwamba huyu amefikia hatua yakuniambia ataoa mwanamke
mwingine!” Akawaza moyoni akijua anamaanisha kabisa, japo hakuwa
tayari kumjibu.
“Hofu ya Mgaya
kuwa hamtaki Shema, sasahivi ondoa. Sasahivi mimi baba yake,
NIPO. Kama unampenda na kumuamini, usiendelee kuishi hivyo. Halalisheni,
muishi kihalali. Usiku mwema.” Kama utani, Mill akatoka kitandani na kuondoka. Nyege
zote zilikata kwa Pam, akapoa kama amemwagiwa maji, haamini.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Inaendelea…
0 Comments:
Post a Comment