Kama baada ya lisaa na madakika, akamka. Andy
akamuona, akaenda kumfuata pale kitandani akajilaza pembeni yake.
“Unajisikiaje?” “Naona sasa hivi hata ukinipa jembe, naweza kulima.” Wakacheka
kidogo.
“Nataka kukuuliza kitu Mina.” “Nini?” “Hukunijibu juu
ya swala la zile karatasi.” “Kwamba tunaweza kuzichana na kuendelea?”
Mina akauliza. “Ndiyo.” Andy akajibu. “Kivipi Andy wakati ulinirudisha
nyumbani na kumwambia mama na Ron kuwa umeniacha! Sasa tunarudiana
vipi kimya kimya tena!?” Mina akamuuliza akiwa ametulia tu ila kwa mshangao.
“Mwanzoni ulianza ukisema unafanya kwa heshima.
Hata kuwa kwenye mahusiano na mimi ulikwenda ukazungumza na Ron
kwanza ndipo ukaenda kwa mama. Leo unataka iwe kimya kimya!? Au umeshanidharau
kwa kuwa nina mimba, unaona thamani yangu haipo tena?” Mtoto huyo
wa kike mwenye shule robo ya watoto wa Ruhinda akaanza kuwazungusha vichwa
vijana wa Ruhinda.
“Hapana Mina! Sitaruka kitu hata kimoja.
Nilitaka kujua kama umeridhia kuwa na mimi tena. Ndipo nirudi nyumbani.
Sitafanya chochote mpaka niende kwa mama na Ron.” “Hapo sawa. Sasa ukienda
utasema nini?” Andy akatulia. Ghafla thamani ya Mina ikarudi. Mina akawa
wakubembelezwa na kung’ang’aniwa.
“Maana unaweza ukajikuta aidha unaenda kumuombea msamaha
Pius, au kumfunga. Hapo lazima ufikirie.” “Na mimi SIWEZI kwenda kumuombea
msamaha kama hajaniomba mimi msamaha. Hakika lazima aniombe
msamaha.” Andy akajitutumua na yeye.
“Basi itabidi kusubiri mpaka Pius aamue kujirudi,
akuombe msamaha ndipo na wewe ukazungumze na mama pamoja na Ron, ndipo
tufikirie kurudiana.” Mina akamuwekea na yeye ngumu. Andy akapoa. Inamaana hamtaki mpaka arudi
nyumbani kwao.
Pakatulia, na chakula kikaletwa kabisa. Wakala, Mina
akamuona amepoa kama anayefikiria kitu. Na yeye akawa kimya na mwanae,
akimtaka ale vizuri ashibe.
Baada ya kula akampeleka bafuni kuoga. Akamvalisha
nguo za kulalia. Akamlaza kitandani kwake yeye. Pale alipokuwa amelala, na
chupa kubwa ya maziwa, akamfunika. Ayan akamnusa na kumkanyaga
mama yake, mpaka akalala. Mina akamtoa hiyo chupa mdomoni, akamfunika vizuri.
Akabaki amejilaza pembeni ya mtoto wake, wameacha kitanda kingine kisafi kwa
ajili ya Andy.
Andy alipoona mtoto amelala na Mina ametulia, akamuita.
“Mina!” Mina akamwangalia. “Mimi naona sitamsubiria Pius. Nitakwenda
kuzungumza na mama kivyangu.” “Utamwambia nini?” “Sitaongea mambo mengi,
nitamwambia nataka kumrudia mke wangu, basi.” Mina akamwangalia na
kunyamaza.
“Unafikirije?” “Mimi sijui Andy! Wewe fanya kile
unachoona ni sawa.” “Sasa unafikiri mama atanielewa?” “Sijui Andy! Mambo
mengine yatajijibu huko huko. Ila mimi huko kwa
mama, sitarudi leo wala kesho. Mama alinifukuza nikiwa namuhitaji
sana. SIRUDI. Wewe nenda kwa wakati wako.” Mina akajifuta machozi.
Akamuona Andy anatoa simu mfukoni. Akapiga. Ikaita bila kupokelewa. Akafanya
hivyo mara tatu, akaona simu iliyopigwa haijapokelewa. Akamuona amekunja uso.
Kwa Ron!
Baada ya kama nusu saa akamuona anapokea simu. “Mzima Ron?” “Mzima kabisa Kiongozi. Kwema huko kanda
ya kati?” “Kwema. Lakini
nipo mjini. Upo
nyumbani na mama? Nilitaka kuja kuwaona.”
Pakazuka ukimya. “Ron?” “Kuna nini tena? Maana kama ni
Mina, si ulishaachana naye? Au kafanya nini tena?” “Hapana. Ni jambo la
amani?” Pakazuka ukimya mwengine.
“Ron?” “Labda uzungumze na mimi Andy.” “Kwa
nini nisije kuwaona kabisa?” Akauliza
Andy kwa kubembeleza kidogo. “Nisikilize Andy. Kumbuka
mimi ndiye niliyekukaribisha na kukufanya uwe karibu na mama. Ukavunja
mahusiano kwa namna yako. Labda hujaelewa. Na nikukumbushe nilivyokwambia
mwanzoni kabisa. Chochote kitakachotokea kati yako na Mina, nilikwambia
nitakuwa upande wa Mina.” Ron akaendelea.
“Tulikukabidhi Mina akiwa mzima
kabisa. Lakini ulimrudisha Mina aliye mjamzito, tena mgonjwa.
Ukamtelekeza hapa bila hata pesa ya matumizi. Ikawa ni kama msichana uliyemuokota
tu. Uliondoka bila hata kugeuka nyuma, wala kuuliza juu ya mama uliyemrudishia
mtoto mjamzito, kujua anaendeleaje! Ukamuachia fedheha, hata mjukuu
hukumrudisha kusalimia. Hivi
unajua kama Mina alifukuzwa hapa nyumbani?” “Nafahamu Ron, ndio maana nataka
kuja kutengeneza. Najua niliharibu.” Mina akabaki kimya akisikiliza.
“Unakuja kutengeneza wapi Andy? Kwa nani?
Mama aliyekuwa akilia kanisani akimtafuta mtoto wake arudi nyumbani, aliweza kumfukuza
huyo mtoto. Hajazungumza naye kwa kipindi chote hicho cha miezi karibu 7
sasa! Unaweza kufikiria hali ya mama ilivyo?” Andy kimya.
“Haya, Mina ulimuacha kama malaya
tu. Mimi sijui kilichotokea kati yenu. Lakini ulimjua Mina tokea mwanzo.
Ukasema unamchukua hivyo hivyo. Kwa hiyo ulimuoa ukimjua Mina vizuri sana. Uliwezaje
kumuacha anahangaika mjini peke yake wewe unafanya kazi mikoani? Ulishindwa
vipi kuwa na familia yako popote unapokwenda? Ukamuacha Mina anahangaika
peke yake mjini, watu baki ndio wanamtunza! Anakuja kupata mimba, unamuacha
vibaya vile!”
“Halafu kwa jeuri uliyokuwa nayo, ukashindwa
kuzungumzia kabisa swala la mtoto ambaye Mina alikuwa akihangaika naye
zaidi ya miaka mitatu mfululizo, peke yake! Shule na kulea kwa taabu.
Akihangaika kila mahali na mtoto! Ulimrudisha Mina nyumbani na masanduku
tu! Unaposema unakuja kutengeneza, ni kwa nani?” Ron akawa mkali kweli.
“Inawezekana umetuangalia na kutudharau
Andy. Kwa vyovyote ilivyo na ulivyotukuta, tulikuwa na amani SANA.
Ulimkuta Mina ametulia nyumbani, ukamtoa hapa, ukaenda kumchanganya.
Akabaki akihangaika mjini hajulikani kama ana mume au la. Akawa
kama kijakazi wako ukimtuma huku na kule na mtoto mgongoni. Leo
unataka kuanzisha nini tena?” “Mina ni mke wangu na namtaka mke wangu.” Andy na yeye akaongea kwa ukali.
“Wewe si ulimuacha? Sasa mke wako
kivipi!?” “Uliona wapi ndoa ya kanisani inavunjika?” Andy akauliza kwa ukali na kumshangaza hata Ron. “Nilifanya kosa, nilishatubu kwa Mina tokea nipo
Uswiz. Mina akanisamehe na tukakubaliana nikirudi tunaanza upya
nikiwa nimebadilika. Nilipo ndipo na yeye atakapokuwepo. Akaniambia
madhaifu yangu yote. Nikataka hata kuacha mafunzo nirudi nyumbani niwe naye
baada yakugundua ni kwa kiasi gani nimemuumiza mke wangu. Mina mwenyewe alinitia
moyo nibaki tu nimalize, atanisubiri.
Narudi nyumbani namkuta mjamzito. Mimi kama binadamu nilipaniki.
Nikafanya makosa bila kufikiria. Pengine ni sababu ya uchovu!” Andy akaendelea.
“Wewe uliponiona siku namrudisha
Mina nyumbani nilikuwa na furaha?”
Andy akauliza kwa kugomba. “Au ulitaka unione nalia
mbele yako ndio ujue na mimi nimeumizwa? Na mimi nilikuwa kwenye maumivu
Ron! Nikafanya makosa nikiwa kwenye hasira. Siku namuacha Mina pale kwenu,
tayari nilishakuwa na hamu na mke wangu hata kabla sijaondoka
kwenu.” Mina akashangaa sana.
“Hakuna usiku uliopita tokea niachane
na Mina, nikalala kwa furaha nikijua Mina hayupo kwenye maisha yangu! Nampenda
mke wangu. Nakwambia namtaka mke wangu. Sitajali alivyo,
namchukua Mina vile alivyo sasahivi na nitampenda kama mwanzo au zaidi nikiwa
nimejionya kutorudia kosa, na wewe unaniwekea ugumu!
Unataka Mina azae peke yake? Au wewe umesahau kama Mina ni mama wa mtoto
wangu pia? Unataka kuniwekea ugumu ili mwanangu akue bila mama yake? Na juhudi
zote za Mina, shida zote alizopitia Mina nikimuacha nyumbani, mimi
nikihangaika kufika hapa nilipo, iwe bure? Yaani matunda haya aje ale mtu mwingine?” Kimya.
“Wewe vipi Ron?!” Andy akashangaa kwa hasira kama hajakosa! “Sasa nimeshakwambia nataka kuja kumuona mama na wewe.
Niwaombe msamaha na niwatarifu kuwa namrudia mke wangu. Unikaribishe
usinikaribishe NAKUJA.” Andy naye akaweka ubabe.
“Wewe unajua Mina alipo?” Akauliza Ron kwa kutulia. “Ndiyo, najua. Wewe niambie nije saa ngapi.” “Ratiba ya
jumapili kwetu ni ileile. Labda jioni.” “Mimi nakuja sasa hivi. Kesho asubuhi
narudi Dodoma. Jumatatu natakiwa kazini.” “Sasa hivi Andy!?” “Sitakaa muda
mrefu Ron! Mbona kama unaniwekea ugumu wa MAKUSUDI tu? Au unataka nini kitokee!?”
“Daah! Andy ukiamua jambo wewe! Unakuwa mbishi na mgumu
kubadilika!” “Nakuja Ron. Tafadhali niwekee mazingira mazuri.” Andy
akakata simu. Mina mwenyewe akashangaa jinsi Andy alivyo ng’ang’ania.
~~~~~~~~~~~~~~
Ila alishamjua, akimnyima penzi, anakuwa kama mwehu. Atafanya lolote lile atakalomwambia ilimradi tu amuweke
kitandani. Alimnyima mapenzi kabla ya ndoa, Andy akahamisha
milima mpaka akafanikiwa
kumuoa nchini Nairobi. Na usiku huo alimuwekea ngumu kusudi, akapambana
mpaka kurudi kwa wazazi ili kwenda kuomba msamaha.
Taka Cha Uvunguni.
Ilikuwa saa tatu na nusu usiku Andy alipokuwa mlangoni
nyumbani kwa kina Mina. Ron akamfungulia. “Karibu.” “Asante.” Andy akapita na
kumkuta mama Ron amekaa tu hapo sebuleni. Amepoa kuliko kawaida yake. “Shikamoo
mama.” “Marahaba Andy mwanangu. Karibu.” Andy akakaa.
“Majibishano yako na Ron ndio yameniamsha. Kwa sehemu
nimekusikiliza. Zaidi hapa mwisho na kama nimeelewa vizuri, umesema
unajua Mina alipo na unataka kumrudia. Hivyo hivyo alivyo!?” Akauliza
mama Ron kinyonge sana tena kwa mshangao bila kupoteza muda.
“Ndiyo. Hata kisheria nilikuwa sijaachana na
Mina. Yale makaratasi niliyowaonyesha siku ile, yalianza kuwa mzigo siku
ileile nilipomuacha Mina hapa. Nilijuta sana, hata sikuyarudisha
kwa mwanasheria ili iwe talaka halali
japo nilikuwa na hasira na sikujua hata kama tusipoachana tutaendelea vipi
kuanzia pale akiwa na mimba ya mtu mwingine.” “Sasa, sasa hivi ushajua utaishije
naye? Maana ni kweli ni ngumu. Inamaana huyo mtoto atakuwepo kwenye
maisha yenu yote ya ndoa akikukumbusha yeye sio mwanao na
aliingilia katikati.” Akauliza mama Ron kwa upole kama aliyefedheheka.
“Hivi tunavyozungumza naishi na Mina. Kama
miezi miwili iliyopita aliomba nimpelekee mtoto, yeye ndio aishi naye.
Nikakumbuka jinsi Mina alivyohangaika na Ayan. Nikajua sitamtendea haki
nikimuwekea ugumu. Alikuwa akiishi Iringa.” Wote wakashangaa. “Iringa kwa nani?!”
Akauliza Ron.
“Alipanga kajinyumba kadogo tu kenye chumba cha kulala
kimoja. Alikuwa akiishi peke yake. Ndipo nikampelekea Ayan. Niliwaacha kama
majuma mawili au moja na siku. Lakini mama, nilishindwa. Mina
alihangaika na mimi kujenga ile nyumba ya Kigamboni. Yeye ndio kwa
sehemu kubwa alihangaika na ule ujenzi mimi nikiwa nipo safarini kikazi.
Achilia mbali shida alizopata na mtoto wangu wakati mimi sipo! Nilishindwa
kumuacha Mina kwenye kile chumba kimoja na mtoto, wakati nilikuwa nikihangaika
kwa ajili yao wao wawili. Nikawachukua na kurudi nao Dodoma ambako nilinunua
nyumba huko.” Andy akaendelea, wakimsikiliza kwa makini tu.
“Tukaanza maisha kama wazazi tu wa Ayan. Lakini nataka
mke wangu. Naona naweza kuishi na Mina vile alivyo na akawa mke wangu. Nampenda
Mina, namtaka mke wangu. Nimerudi hapa kuomba radhi jinsi
nilivyoondoka vibaya. Naomba mnisamehe. Nilikuwa nimekasirika na
nilifanya vibaya.”
“Juu ya makosa ya nyuma, nishazungumza na Mina
tokea nilipokuwa Uswiz, tukasameheana kama
nilivyokuwa nimezungumza na Ron.” “Nilisikia Andy, mwanangu.” “Basi ni hilo
mama yangu. Nimekosa, naomba unisamehe kama vile ambavyo ungeweza
kumsamehe Ron.” Ron akacheka na kutingisha kichwa.
“Wewe mzee nimekuvulia kofia! King’ang’anizi mpaka ukweni!” Angalau wakacheka. “Naona
unataka kuninyima mke wangu! Siwezi kukubali! Mina anafahamika
mpaka ofisini kama yeye bado ni mke wangu. Nilishindwa kumtoa kabisa.”
Wakatulia kidogo.
“Kwa hiyo, hilo moja, na nishukuru kunisamehe. La pili,
najua mama jinsi ulivyohangaika na Mina. Nilitaka kukutaarifu kuwa nipo
naye. Tunaishi Dodoma. Ni mjamzito wa miezi 7 na siku chache. Anaye daktari
mzuri tu anamfuatilia afya yake. Anaendelea vizuri kabisa, naomba mama usiwe na
wasiwasi.” “Nashukuru Andy mwanangu. Mungu akubariki baba.
Nawaombea kila la kheri.” Andy akapumua kwa nguvu na kucheka.
“Sasa hivi nakwenda kuchana zile karatasi. Naendelea
na mke wangu.” Wakacheka lakini kama wanawaza. “Ron anayo namba yangu mpya.
Najua hampo kwenye mawasiliano na Mina, ila mkiwa na maswali yeyote, muda na
wakati wowote mnipigie. Mama, ukitaka kuzungumza na Ayan,
tafadhali usisite kupiga. Halafu Dodoma si mbali. Kule tunayo nyumba kubwa sio
kama pale tulipokuwa tukiishi mwanzo. Karibuni muda na wakati wowote.
Hata ukitaka nauli, tafadhali usisite. Nijulishe. Mimi na Ron tutafanya
mipango, uje kuona wajukuu.” Mama Ron akafuta machozi. “Asante Andy.
Tunashukuru.” Ikabidi Ron ndio ashukuru kwani mama yake bado alikuwa akilia
akikumbuka jinsi walivyoachana na Mina. Andy akaaga na kuondoka.
Mina & Andy Tena.
Alirudi hotelini akamkuta Mina anakula chakula
walichokuwa wamebakiza. Andy akaingia na cheko. Mina akacheka na kutingisha
kichwa. “Hivi ujue Ron ni kama baba yako mkwe, wewe Andy!” “Hata kama
angekuwa mzee Ruhinda! Ndio atake kuninyima mke!” Mina akamwangalia na
kuendelea kula. “Sasa mbona huniulizi mambo yaliendaje?” Andy akauliza.
“Kwani mimi sikujui wewe, unapotaka kufanya jambo lako? Nilijua
hutarudi hapa mpaka uwaweke sawa.” Andy akacheka sana.
“Ujue sasa hivi wewe ni mke wangu kihalali?”
“Mbona sasa mimi hujaniomba turudiane?” Mina akauliza. “Ngoja kwanza
nikaoge vizuri, niwe msafi ndio nije kuomba msamaha wangu.” Mina akatoa
tabasamu huku akiendelea kula kama aliyeelewa. Hata Mina naye alikuwa na hamu
na Andy. Alijua mchezo wa Andy sio wakitoto. Akajua usiku huo atalala vizuri.
~~~~~~~~~~~~~~
Andy akamsogelea pale baada yakupata tabasamu, akajua amekubaliwa.
“Nilivyo na hamu na hiyo midomo!” Mina akacheka taratibu kama kwa aibu.
Akamsogeza karibu, akasimama naye kwa kumvuta juu. “Pole kwa kukutelekeza
mpaka ukaingia matatizoni. Na samahani kukuacha vibaya. Nisamehe.”
“Yameisha Andy. Mimi mwenyewe nimefurahi tunarudiana. Napenda
ndoa yangu.” Andy akainama kupata busu. Mina akatoa ushirikiano.
Hali ikabadilika, wakachukia kwa Ayan kuwepo hapo.
“Heri tungemchukulia chumba chake huyu! Atanipunja sana usiku wa leo.” Mina
akaanza kucheka taratibu. Andy akamvutia bafuni. Akaanza kumtoa nguo.
“Tukirudi Dodoma tunachoma yale makaratasi moto.”
“Asante Andy.” “Na mimi nakushukuru Mina. Leo umenirudishia heshima
nyumbani.” “Na wewe leo umenirudishia heshima nyumbani.” Wakakumbatiana
na kissing za uchu zikaendelea Andy akiwa na hamu na Mina, ya
karibia mwaka, yaani miezi 11. Ilibidi hapo bafuni pafae tu. Andy
hakuweza kusubiri.
Wakarudi chumbani, wakazima taa kabisa, wakahamia
kwenye kitanda alichokuwa ameachiwa Andy. Mina na tumbo hilo la miezi 7 akatoa ushirikiano wa nguvu. Walifanya
mapenzi kama ndio wapo fungate kasoro kupunjwa uhuru sababu ya mtoto. Lakini
walilala wakiwa wameridhika. Mina akiwa amekumbatiwa. Akashukuru angalau
atarudishiwa pete zake za ndoa, atazunguka na tumbo akiwa ndani
ya ndoa. Na angalau hataendelea kuwa kicheko kwa ndugu.
Mwanzo Wenye
Sura Mpya
Siku inayofuata walirudi Dodoma, Andy akiwa na furaha
yakumpata Mina, japo kilichowapeleka ni kama hakijaweza kuchukua picha
inayo eleweka. Pius hakuomba msamaha, ila Andy akawa ametulia kabisa.
Mina alionyesha kumuheshimu na kumthamini mbele ya familia ya
Ruhinda ambako alikuwa na uhakika kabisa alipoteza heshima kwao. Wawili
hao ungejua ni wazazi wa Ayan, waliingia nyumbani kwao hata Judy akajua lipo badiliko.
~~~~~~~~~~~~~~
Mina akapata muda na Judy. Akamshuhudia yote
yaliyotokea huko na kumshukuru sana Judy. “Wala sio mimi mama Ayan. Ni Mungu
wako huyo. Tena amekujibu kwa haraka sana na amekurejeshea heshima.
Mshukuru Mungu.” “Nilikuwa namshukuru njia nzima. Hakika amenitendea makubwa.
Amenisamehe na kunirudisha kwenye ndoa ambayo wengi walibashiri sitaweza
kuishi na mume! Hakika nashukuru Judy. Nimepata utulivu wa hali ya juu.”
Wakacheka hapo jikoni, Andy akiwa na mwanae sebuleni.
~~~~~~~~~~~~~~
Wakiwa ndio wamerudisha amani na furaha katikati yao, nyumba imetulia, siku ya ijumaa mzee Ruhinda akampigia simu Andy na
kumuomba kwa heshima ya Mina, ampokee tu Pius. “Hata
kama utashindwa kusamehe tokea moyoni, tafadhali fanya hili jambo liishe
Andy. Najua ni ngumu, lakini nimezungumza sana na Pius. Nimeona amefika
kwenye majuto ya kweli. Tafadhali naomba urahisishe haya mambo. Wewe upo
na hiyo dhamana.”
“Mpokee, ili mjue mtafanya nini kuanzia
hapo. Mungu akipenda huyo mtoto atazaliwa. Na Pius anaonekana anataka mahusiano
na huyo mtoto. Lazima wewe uwe katikati yao na uendeshe huo
uhusiano bila kuzembea. Sijui kama umenielewa?” “Nimeelewa baba.” Andy akakubali bila shida. Na hivi ashahakikishiwa
penzi na Mina! Hakuona tatizo tena.
~~~~~~~~~~~~~~
Siku ya jumamosi mchana, Andy alituma dereva akamfuate
kaka yake uwanja wa ndege ili amlete nyumbani. Alifika Pius peke yake,
hakusindikizwa na yeyote. Alikuwa mstaarabu mpaka akamshangaza Mina!
Hakupoteza muda, akaenda moja kwa moja kwenye lililompeleka.
“Naomba unisamehe Andy kwa kulala na mke wako. Nilikosa
na hakuna jinsi ya kujitetea katika hili. Naomba unisamehe.” Andy
akamwangalia. Mina akashangaa kimya. Na yeye akanyamaza. “Unaposema unataka mahusiano
na mtoto, unamaanisha nini? Maana sitaki uje unizunguke tena Pius.” “Sitarudia tena. Naahidi hata kwa Mina.”
Akakiri Pius.
“Sasa nataka ujue kabisa, mimi na Mina tumerudiana.
Mina ni MKE wangu kihalali kabisa. SITAKI uwasiliane na mke wangu
bila mimi kujua. Na uache kumtumia mke wangu pesa. Tabia yako ya
kwenda kumuwekea mke wangu pesa benki, iishe Pius.” “Nataka kumtunza
mtoto wangu! Sitaki mtoto wangu..” “Sasa unamuona mtoto wako hapa?” Andy
akauliza kwa ukali. Mina kimya.
“Usiniudhi zaidi Pius!” “Nisikilize Andy.
Nataka huyo mtoto azaliwe kwenye mazingira mazuri na..” “Wewe unaona
hapa tulipo tupo kwenye mazingira mabaya? Au uliona Ayan alizaliwa
kwenye mazingira mabaya?” “Sitaki sasahivi mumpeleke kwenye kliniki za ajabu ajabu. Maana kliniki aliyokuwa akienda Mina, kule Iringa
ilikuwa nzuri na ni mimi ndiye niliyemtafuta huyo daktari kwa kuwa
niliambiwa ni mzuri. Nataka Mina ahudumiwe na daktari mzuri ili
mtoto wangu awe kwenye mikono mizuri na salama.” “Sasa, sasahivi Mina hayupo
Iringa, yupo Dodoma. Tafuta daktari yeyote unayemtaka hapa, niambie,
nitakuwa nikimpeleka.” “Sawa.” Hapo wakakubaliana.
“Kuna jambo jingine.” Mina na Andy
wakamwangalia. “Japokuwa Mina hakutaka kujua jinsia ya mtoto, lakini
mimi nilizungumza juzi na yule daktari aliyekuwa akimshugulikia Mina kule
Iringa, nikamuulizia jinsia.” Mina akabaki akimtizama. Andy
kimya.
“Nimekuja na jina. Hilo jina ndio nataka tuanze
kumuita huyu mtoto kuanzia sasa hivi ili ajue tunamfahamu na tunamsubiria.”
“Ujue wewe Pius unataka kuniharibia ndoa yangu wewe!” Mina
akashangaa sana. “Hapana Mina. Nia yangu ni nzuri tu.” Pius akajitetea. “Nia yako nzuri ipi? Niambie
jina lenyewe.” “Pius Junior Ruhinda.” “Haya
naomba uondoke Pius.” “Subiri kwanza Mina!” Mina akasimama kama
anayetaka kuondoka.
“Naomba wewe maliza kuomba msamaha, uondoke.
Lasivyo utataka kuniudhi uje urudi tena kuja kuomba msamaha mwingine.”
“Mbona naongea kwa amani tu! Tatizo liko wapi?!” “Cha kwanza, umekwenda
kuangalia jinsia ya mtoto nikiwa nimekwambia wazi sitaki kujua, nataka
kukutana naye siku anazaliwa. Hilo moja, halafu unajua wazi hii ni familia
ya Andy. Unakuja kupenyeza jina lako hapa katikati ya familia ya
mwenzio kama hutaki mimi niondolewe
na huyo mtoto mwenye jina lako ni nini?” Andy kimya.
Pius naye akasimama. “Naomba mnielewe jamani! Huyo
ndio mtoto wangu wa pekee wa KIUME.” “Ujue Pius umechanganyikiwa
wewe!” Mina akamshangaa sana. “Tafadhali Mina. Nataka mtoto wangu akue akijitambua
kama nampenda na ni mtoto wangu MIMI.” “Nani amekwambia upitishie mtoto
wako kwenye hii familia yetu kama sio fujo ni nini? Nenda kazae mtoto
wako na Raza, ndio ukampe hayo majina yako halafu marefu. Ondoka
Pius.” “Raza hana uwezo wa kuzaa tena.” “Ujue Pius umechanganyikiwa wewe,
nenda hapo kwenye hospitali ya vichaa ukapimwe wewe!” Mina alikuwa akimshangaa
sana asielewe.
“Mpaka nahisi nia yako ilikuwa mtoto wa kiume
kwa mke wangu Pius! Uliona Mina amenizalia mimi mtoto wa kiume,
ukaona akuzalie na wewe mtoto, ukiamini atakuwa ni wa kiume
tu.” Andy akaongea kwa kuumia sana. “Jamani mbona hili jina la Pius Junior halina tatizo? Maana kama mnataka afanane na watoto
wenu, kumbukeni wote ni kina Ruhinda.” Hakutaka hata kujibu shutuma,
akaendelea na hoja ya jina kwa mwanae.
“Unaondoka au nimpigie simu mzee Ruhinda nimwambie
hujaja kwa amani unataka kuvuruga ndoa yangu?” “Mimi naondoka Mina. Ila
naomba mnifikirie na mimi.” “Nakuhakikishia Pius, kwa namna yeyote ile
utakayosababisha hapa ndani pakosanike amani sababu ya huyu mtoto ambaye
unataka aanze kuonekana ni tatizo wakati mtoto wangu sio tatizo,
ujue atakuwa huyu mtoto bila kuwa na mahusiano na wewe
kabisa.” Mina akamtisha.
“Basi Mina, nimeomba tu. Naomba na wewe ufikirie.”
Pius alikuwa ameshafika mlangoni. “Huyu mtoto atakuwa kama Ayan, na kama mtoto
wa hii nyumba. Acha kuanza kutuwekea hekaheka zisizo na sababu.” “Basi
kama alivyoniruhusu Andy, nikimpata daktari mzuri wa wakina mama, nitawataarifu
ili uanze kwenda huko. Nitazungumza naye pia anishauri ni wapi utajifungulia.
Sitaki kutokee kosa lolote. Nataka siku hiyo akili na mawazo ya kila
atakayehusika kwenye kujifungua kwako viwe kwako tu na mtoto. Na
mimi nitakuwepo siku hiyo ili kuhakikisha hakuna uzembe. Naamini katika
hilo ni sawa jamani! Mtoto wangu azaliwe na mimi nikiwepo.”
Mina akabaki kama ameduaa kwa muda.
“Njoo kwanza ndani.” Mina akamvuta mkono mpaka ndani.
“Kaa hapa.” Pius akakaa. Mina akachukua simu ya Andy, akampigia simu mzee
Ruhinda. “Ni mimi baba.” Mina akajitambulisha
mara mzee Ruhinda alipopokea na kumuita Andy. “Hujambo
Mina mwanangu?” “Mimi ninashida kubwa sana baba yangu. Hapa nilipo, nahisi kuchanganyikiwa.”
“Nini tena mama?” Mzee Ruhinda akamuuliza kwa upole.
“Pius anataka kunivunjia tena ndoa
yangu, baba.” Mina akaanza kulia. “Tulia kwanza unieleze. Tulia kwanza mama.” “Ulisema anakuja kuomba msamaha, lakini hajaja kuomba
msamaha. Amekuja kuanzisha familia yake ndani ya FAMILIA ya mwenzie.”
“Hapana Mina! Mbona mimi nimeomba tu!” Pius akaongea kwa unyenyekevu.
Akaenda kumpokonya simu Mina. “Baba,
mimi sijafanya fujo. Nimeleta maombi yangu tu!” Pius akajitetea. “Hayo maombi anayoomba baba, ni yakumchanganya tu
Andy. Ananiharibia mahusiano ya huyu mwanangu na Andy. Anataka mtoto
wangu azaliwe aonekane tatizo humu ndani na si baraka.” “Mpe simu Mina.” “Naomba upokee na simu yangu baba.”
Pius akarudisha simu kwa Mina na yeye akampigia simu baba yake. Wakaweka kwenye
conference
call. Andy kimya. Akiwaangalia.
“Naomba utulie tuzungumze mama.” “Siwezi kutulia baba!
Pius ananiharibia kwangu wakati akitoka hapa, anarudi nyumbani kwake,
kwa mke wake na watoto wake!” “Naomba
unisikilize na mimi baba. Mina ana mtoto wangu wa pekee wa kiume.
Nimeomba ajifungulie sehemu nitakayotaka mimi. Hilo hata Andy amekubali.
Nikaomba wampe jina la Pius Junior Ruhinda na siku akijifungua niwepo.” “Sasa hebu fikiria baba,
inakuaje hiyo yakumpa mtoto jina la Pius Junior katikati ya familia ya Andy
kama sio kutaka mtoto wangu aonekane ni tatizo humu ndani na kuchanganya
watoto wa humu ndani?” Mina akamuuliza mzee Ruhinda huku akilia.
“Mbona hilo ni jina tu baba!? Lina shida
gani?” “Lakini wewe ulitoka hapa kwa makubaliano unakwenda kuomba msamaha
Pius! Hujaweka mambo sawa, unaanza kupeleka mahitaji yako! Hivi
unatambua kwamba umekosa na unahitaji kuwapa muda wenzio wajenge imani
tena na wewe?” “Basi baba. Inawezekana nimewahi sana.” “Hata baadaye, huyu mtoto
hataitwa jina lako humu ndani.” Mina akaweka msisitizo.
“Tafadhali fanya lililokupeleka Pius. Sitaki
uharibu huko kwa mwenzio.” Mzee
Ruhinda akamtahadharisha Pius. “Ndilo analolifanya
hapa baba. Hata msahama wenyewe bado kwa Andy hata hajapewa, ameenza
kuleta mahitaji yake! Halafu nilimwambia asizungumze na mimi
mpaka aende akazungumze na mama pamoja na Ron. Lakini anazungumza
na mimi wakati ameniharibia mahusiano yangu na mama yangu, hilo hajali! Naomba umwambie aondoke tu. Tafadhali
baba. Mimi mwenyewe nitazungumza na Andy.” Mina akawa analia.
“Naomba kuzungumza na Andy, Mina. Nikiwa nao
wote hao. Nataka amani.” Mina akamsogelea
Andy huku akifuta machozi. “Baba anataka kuzungumza
na wewe.” Andy akapokea. “Baba!” “Vipi Andy?”
Mzee Ruhinda akauliza kwa kujali. “Sijui baba! Hakika sielewi!”
Andy akajibu kwa kuchoka. “Nataka kwanza amani.”
“Unategemea kutakuwa na amani gani baba, wakati Pius yupo katikati ya ndoa yangu!?”
“Nisikilize Andy. Hiki kitu kimekuja wote hatukukitegemea. Kinashitua
na kuumiza sana. Tafadhali naomba tujipe muda wa jinsi gani ya kukikabili.”
“Pius, naomba waache kwanza. Kwa leo naomba
omba msamaha tu, ondoka. Waache kabisa.” “Sawa baba. Lakini nilishaomba
msamaha.” Pius akajieleza kwa upole. “Andy umesemaje?” Mzee Ruhinda akakuliza. “Nimemsikia baba.” Andy akajibu kwa kuumia pakatulia
kidogo. “Andy?” Baba yake akataka aendelee. “Sijui baba, Pius haonekaniki kama alikosea wala kujutia
alichofanya! Pius ALIKUSUDIA kuzaa na Mina, baba! Sasa hivi ndipo nakumbuka
vile Pius alivyokuwa akitaka mtoto mwingine akisema anauhakika kama Raza
asingekuwa na matatizo, pengine angemzalia mtoto wa kiume. Nahisi
ukaribu wa Pius kwa Mina, aliufanya makusudi ili amzalishe mke
wangu.” Andy akalalamika.
“Pius hajakosea baba! Naumia kuona amemchagua
mke wangu kumzalia mtoto.” “Naomba hayo mengine muachie Mungu, Andy.
Fanya kwa nafasi yako.” “Sawa baba.”
Akakubali Andy akisikika na maumivu bado. “Haya Pius
naomba uondoke bila hata kuongeza neno, au hata kuaga. Nashauri acha kwanza patulie.”
“Sawa.” Pius naye akakubali kuondoka bila kukanusha tena shutuma za
mdogo wake. Ikawa ni kama aliyekubali zile shutuma. “Namaanisha
hiyo ‘sawa’ niisikie ukiwa nje kabisa ya hiyo nyumba.” Bila kuongeza
Pius akatoka kimya kimya. Andy akakata simu. Wakabaki pale ndani wamezubaa.
Mina kwa Andy.
Mina akamshika Andy mkono mpaka chumbani kwao. “Naomba
nisikilize Andy. Naomba usichoke kabla huyu mtoto hajazaliwa.
Najua kitendo ni kibaya. Lakini huyu mtoto hakuchagua azaliwe
hivi Andy! Ni kama vile Ayan hakuchagua azaliwe na mimi pamoja na wewe.
Nakuomba uwe na mimi katika hili.” “Sijui ndio itakuaje Mina!”
“Hata mimi sijui mpenzi wangu. Lakini najua sisi tunapendana. Si ndiyo?”
Mina akamuuliza kwa upendo.
“Au umeshaona hamna jinsi tukaendelea tena?”
“Hapana. Ila naona kama itakuwa na mchanganyiko fulani hivi!” “Labda
kama mimi na wewe hatutakuwa upande mmoja. Nitahakikisha huyu mtoto
anakuwa akijitambua hapa ni kwao na sisi ni wazazi
wake wa kwanza. Sitafanya kitu chochote bila kushauriana na wewe.
Nataka mimi na wewe tusigombane kwa ajili ya huyu mtoto Andy.
Huyu mtoto hana hatia. Tafadhali Andy.” “Sawa. Lakini sitaruhusu
mawasiliano kati yako na Pius au..” Mina akaanza kumtoa suruali, na kumshusha
boxer haraka, akapiga magoti mbele yake na tumbo lake, akaanza utundu. Kichwa
mdomoni, mkono ukimchezea taratibu. Akamsikia akicheka taratibu kwa hisia.
“Sasa nitaongeaje Mina!” “Mimi nakusikiliza. Wewe
endelea kuniambia yote ambayo huyataki na kuyataka. Atayafuata
tu. Nakupenda Andy wangu. Nataka tubakie wote, hili lisitutenganishe
tena.” “Kwa mwendo huu, sidhani!” Mina akacheka na kuendelea kumnyonya
huku akimchua mpaka akalemewa, maneno hayatoki tena. Andy kwa penzi la Mina
huwa hajiwezi. Akachangamkia penzi. Mchana kweupe, Mina akajituma hapo
chumbani mpaka akamuona Andy ametulia. “Kabla yakujifungua si tutakwenda
mapumzikoni?” “Lazima Andy. Fungate ya pili.” “Nahitaji Mina! Bado sitosheki,
naona kama tunabanwa! Muda na mazingira. Lakini tukienda sehemu, tunatulia huko
kwa muda mpaka akili iamini wewe ni wangu na hakuna wakukutoa kwangu.” Mina
akamdaka midomo, kissing zikaendelea.
Pius kwa wazazi.
Pius alimuomba baba yake kwa magoti amsindikize
kwa mama yake Mina. Ikabidi Mzee Ruhinda ndio ampigie simu mama Ron, amuombe
kikao. Mama Ron akiwa anajua ni kuhusu Andy kurudiana na Mina, akakubali
kwa heshima. Akawatayarishia juisi na nyama tu za kukaanga za kuku
ambazo alizikaanga vizuri sana. Ilikuwa ni siku ya jumamosi jioni kama kwenye
saa kumi hivi.
Pius alisindikizwa na wazazi wake wote wawili.
Walimkuta Ron na mama yake wakiwasubiria. “Karibuni kwanza chakula.” “Naomba
nikuombe kitu mama Ron. Tafadhali tusikilize kwanza ndipo utukaribishe
chakula chako.” Mama Ron akacheka. “Mimi naona kama kuna kupigana kwenye hayo mazungumzo, tupigane tukiwa angalau kuna
kitu tumboni, mama Ruhinda.” Akalazimishia wageni wao, wale kwanza. “Hata hivyo
ni chakula tu kidogo. Mjitafune msiondoke bila hata kula.” Wakahamia mezani.
Mina alishapabadilisha kwao. Mama huyo akawa
ameshaingiwa na ustaarabu wa visu na uma. Glasi nzuri alishanunua akiwa
na Mina Ruhinda. Makochi na meza safi yakulia, tena za kioo nzuri ya thamani. Mwanae
alimnunulia kipindi yupo na Andy mwanzoni kabisa. Pesa ya Pius nayo ikaongeza nguvu.
Nyumba hiyo ikawa imesakafiwa vigae safi na madirisha yakawekwa aluminium tupu,
nje akaweka madirisha ya urembo wa vyuma. Safi.
Watoto hao wakashirikiana, wakaweka ukuta,
chini kukajengewa matofali mazuri mpaka getini. Kwa kifupi Mina aliwekeza
kwao. Ndani na nje pakavutia haswa. Ndio maana Mina hakuamini siku anafukuzwa
pale na mama yake. Ni kama alipajenga upya akisaidiwa na Ron, tena
kidogo tu. Ila wazo la nini kifanyike hapo alikuwa ni Mina.
~~~~~~~~~~~~~~
Basi kina Ruhinda wakaandaliwa kwa hadhi yao. Meza
safi mpaka na napkins. Wakala lakini wakawaona sio kama wanavyojitahidi
kuwachangamkia wao! Wakawa wamepoa mno! Hata wao wenyewe wakawa
hawaongeleshani. Ron na mama yake wakaona watulie. Wakajua kuna kubwa
lililowaleta.
Wakamaliza, Ron akasafisha, wakahamia sehemu ya
sebuleni. “Kwema?” Akauliza mama Ron. “Naomba kwa heshima yangu tu, mama Mina,
umpe nafasi Pius, ajieleze.” Akaanza mzee Ruhinda, mama yake kichwa chini.
“Karibu baba.” Mama Ron akamkaribisha kwa moyo mweupe akijua wema na upendo
wa Pius. Alimjali sana Mina hata yeye alikuwa akilijua hilo. Na alishafika
hapo mara kadhaa kuwaleta Mina na mwanae au kuwachukua akiwa na zawadi
tofauti tofauti kwa mama huyo.
Vyakula
mbali mbali au hata matunda. Hakuwahi kufika hapo mikono pitupu. Kwa hiyo walifahamiana kwa karibu tu kama Andy, ila
Pius alikuwa na ucheshi zaidi, Andy mkimya. Walikuwa wakizungumza na
stori hata za kazini kwa mama Ron, huko kwenye shule anakofundisha na kutaniana
kwa hili na lile.
~~~~~~~~~~~~~~
“Siku ile matokeo ya Mina yalipotoka.” “Matokeo yapi
tena!?” Akauliza mama huyo mwalimu. “Yale ya chuo.” Akajibu Pius. “Ooooh! Na
nilisahau kuwashukuru. Najua na wewe ulimsaidia sana kumaliza shule
yake. Na wazazi pia. Nashukuru jamani! Najua bila wote kuingilia kati,
pengine asingemaliza. Asanteni sana.” Akashukuru mama Ron kwa kumaanisha, lakini kimya. Akashangaa mbona hawaitiki,
wanyonge!
“Sasa siku ile nikasema kwa juhudi alizofanya Mina,
tununue champagne. Nikanunua yenye kileo,
tukanywa. Wote tukalewa ndipo nikajisahau nikalala naye.”
Pakazuka ukimya, yule mama akabaki ameduaa nakushindwa hata kupepesa
macho.
“Wewe ndiye uliyempa Mina mimba!?” Akauliza Ron
kwa mshituko mkubwa. “Kabla sijajibu hilo naomba niseme hivi, hata Mina hakujua
kama hilo lilitokea. Alilewa sana. Namaanisha hata hakujua kama tulifanya
mapenzi usiku ule, hakuwa akijua. Yaani swala la kuwa ni mjamzito
alilijua hospitalini alipopelekwa na Paulina. Na hakuwa akijua
hata aliipataje hiyo mimba, mpaka siku chache zilizopita.” Akajieleza
Pius akimtetea Mina, akiwa amejawa na wasiwasi sana mpaka jasho lilikuwa
likimtoka.
“Ila wewe ulijua kama mimba ni yako?” “Nilijua
kwa asilimia 99, kwa kuwa muda mwingi nilikuwa na Mina, Mina hakuwa
na mahusiano yeyote yale ya kimapenzi nje ya ndoa yake. Na miezi
miwili kabla ya kugundulika kuwa ni mjamzito au mwezi mmoja kabla ya tukio,”
“Sema kabla hujambaka.” Akaongea Ron kwa hasira.
“Mina alikuwa kwenye siku zake na aliugua sana na
tumbo, mimi ndiye niliyempelekea dawa za maumivu. Maana alikuwa
akilalamika siku nzima akashindwa hata kutoka hapo nyumbani. Kwa hiyo najua
Mina sio kwamba alishika hiyo mimba kwa umalaya. Ni pombe
ilinizidia. Naomba radhi.” Pius akapiga na magoti.
“Nimetoka nyumbani kwa Andy na Mina, nimeomba msamaha
kwao. Na nyinyi nimekuja kuwaomba msamaha.” Mama Ron akaanza kulia. “Kweli mwenye nacho anaongezewa na asiyenacho
ananyang’anywa kabisa!” Akaongea mama Ron kwa uchungu, akilia. “Yaani katika wanawake woote hawa mjini, ukaamua
kwenda kuniharibia mimi ambaye mali yangu ni hawa watoto
wawili tu, jamani! Kweli Pius?” “Ni pombe mama yangu. Lakini nimemwambia
hata Andy, nitawajibika kwa asilimia 100, na nimeomba kumtunza mwanangu.” “Itasaidia nini kama sio kuongeza tu matatizo!?
Yaani kweli Pius wewe umeenda kupenyeza mtoto wako katikati ya
ndoa ya mwanangu!” Mama
Ron alikuwa akilia sana. Akajifunika kabisa akizidi kulia kama amepewa taarifa
za kifo.
“Natamani ungemchagua mtu
mwingine wakumfanyia ukatili huo lakini sio yule mtoto. Mina ndio anatulia
kwenye maisha, na wewe ndio ukaamua kwenda kumkatili! Nimehangaika
na hawa watoto, imekuwa kama mkosi jamani! Utafikiri mwanangu ndio
ameandikiwa matatizo daima!” Mama
huyo alilalamika huku akilia.
“Nimekosa mama yangu, na sikukusudia kumtesa Mina
milele. Ningeweza kunyamaza kabisa. Lakini sikuwahi hata kumuacha hata dakika
moja. Tokea anaondoka hapa nyumbani, nilimtafuta na kuhakikisha anatibiwa.
Nikamsaidia pesa ya sehemu ya kuishi mpaka nikahakikisha anapata daktari
mzuri hata huko Iringa. Japokuwa sikuwa nimemwambia kama ni mimi, lakini
nilikubali kuwajibika. Nikahakikisha simuachi akihangaika na
mimba peke yake, mpaka akachukuliwa na Andy, bado nilikuwa nikimtunza.” Pius
akajitetea huku amepiga magoti.
“Na nimewaambia nitasaidia kwa kadiri
watakavyoniruhusu.” “Wewe unafikiri hivyo ndio
unasaidia au unaendelea kumtesa Mina? Inamaana wewe na huyo mtoto mtakuwa katikati
ya maisha ya Mina na Andy daima! Huo msaada wako unaosema hapa, niambie utasaidia
vipi katikati ya ndoa yao, kama sio utakuwa mwiba daima!?” Mama Ron akaendelea kuuliza kwa kuumia sana akilia kwa uchungu.
~~~~~~~~~~~~~~
Wanasema
disco imeingia mmasai, ila wasafari hii, ni mmasai wa uchi.
Mina
amerejeshewa ndoa, ila na mtoto wa Pius juu.
Ni hali ya taharuki, hakuna ajuaye chakufanya
kwenye hali hiyo.
Akiwa amejaza WEMA
kwa wote. Ametenda zaidi ya wote na kila mtu anamjua Pius
mtu wa kujali. Sasa je, na huko kwa mama Ron atapokea msamaha, au ndio kutaongezeka kesi kwa shitaka
la kumbaka Mina kama Ron alivyotangulia kusema?
Na je ndoa ya Mina mwenyewe, penzi pekee kati yake na Andy, litatosha
kuponya na kujenga kwa upya ndoa yao, akiwepo huyo mtoto wa Pius katikati yao?
Usikose
kufuatilia sintofahamu hii.
0 Comments:
Post a Comment