![]() |
Kwa Shangazi.
Alikutana na
sifa mbaya za Pam zilizomchanganya Mill. “Umalaya umemponza.”
Akaongeza shangazi mtu. “Wewe ulivyonikimbia hapa na kwenda kulipa
mahari kwao huko Milimalini, akajihakikishia wewe keshakukamata, ubaya
au uzuri kwake wewe si haupo hapa nchini, huko alikohamia chumba akakigeuza
dangulo. Unaambiwa pakawa kama chumba cha kulala wageni sema ni wakiume.”
“Anawaingiza na
kuwatoa atakavyo, mpaka akashika mimba. Anambambikizia nani tumbo
hilo, na mwanaume si mmoja! Walivyoona hivyo akaanza kukimbia mmoja
baada ya mwingine kama laana ya mama yake vile! Nasikia akaachwa anahangaika
peke yake! Kama sijakosea ashazaa wawototo wawili kama si watatu na
mabwana tofautitofauti. Mwili ule anautembeza kila mahali! Hata
kama ni mzuri wa namna gani, wanaume wanachoka!” Mill aliondoka hapo amepandwa
hasira asijue ni nini.
~~~~~~~~~~~~~~~~
“Pam!” Hakuwa akiamini. Akahisi hasira za kumuacha ndizo zimemfanya awe
malaya. Basi akazira kabisa, kana kwamba yeye ametokea nyumba ya watawa
wakati na yeye alikuwa na mwanamke na watoto wawili juu! Akasusa na kuacha
kumtafuta Pam huku roho ikimuuma, halafu wakati mwingine kujipongeza
kumuacha, kwamba amejiepushia.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Wakati upelelezi
ukiendelea watu wakitajana hata kwa kusingiziana ilimradi tu
kuipata hiyo pesa, ila kukwama kwenye ushahidi. Maisha ya Mill na hao watoto wa
kimarekani yakaendelea kwa SHIDA sana. Mali zipo lakini ulezi
mgumu kwelikweli. Watoto wajeuri hawamsikilizi hata kidogo!
Akawatafutia
shule inayoendana na huko kwao Marekani. Angalau akawa anapata muda wa
mambo mengine mbali na wao. Wanatoka asubuhi kwenda shule, wanarudi jioni, kila
mmoja chumbani kwake.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Kuna mambo
alifikiria kufanya hospitalini kwa Komba. Mill ni nesi. Anaakili na ufahamu ya
mahospitali ya huko ulimwengu wa kwanza. Kuna vifaa vya upimaji alitaka
aingize nchini, ikiwepo cha Sonography. Tatizo akawa tayari ni raia wa nchini
Marekani, si Mtanzania tena.
Akazungumza na
Colins. Akamsaidia kumuombea kibali cha kufanya kazi hospitalini kwao. Ndipo
sasa akaingiza vifaa vya kisasa vya hospitali nchini, kupitia Colins na kupewa
sehemu maalumu, akaweka mashine zake hapo hospitalini kwao. Mzee Komba akawa akijisifu
sana kupata kijana mwingine mwenye akili na anayesaidiana na Colins.
Kwamba wana nyanyuana. Wawili hao wakashikana kwelikweli. Undugu ukanoga.
Ukienda kutibiwa
hospitali kuu ya Muhimbili, ukikutana na mzee Komba, ukataka kipimo,
atakuelekeza hospitalini kwa mwanae. Na hapo ndipo utakutana na vifaa
vya kisasa vya Mill. Na kama endapo utafika hospitalini kwa kina Colins,
ukiandikiwa vipimo, basi vingine vitafanyika upande huo wa Mill.
Ukifuata vipimo
tu hapo kwenye upande wa Mill, basi utakutanishwa kwa kuelekezwa upande
wa pili, hapohapo kwa madaktari hospitali anayosimamia Colins. Ikawa neema
kwa wote. Mill anaingiza pesa na Colins hivyohivyo
Damu Nzito
Kuliko Maji.
Siku hiyo Mill
alikuwa ofisini kwa Colins, wakawa wakizungumza. Akawa amekaa mbele ya meza ya
Colins wanaangaliana wakizungumza. Akamuona Colins anacheka. “Nini?” “Ushawahi
sikia duniani wawili wawili?” Colins akamuuliza akicheka, Mill asimuelewe.
“Kuna siku nilikuwa pale mapokezi nikakutana na mtoto. Mkubwa tu. Bwana Mill, unafanana
naye, mpaka nikabaki nimemkodolea
macho!”
“Yaani
nimekuangalia sasahivi hapa ulivyotulia, ndio nimekumbuka. Unaona hayo macho
yako yalivyo? Hivyo ulivyotulia sasahivi.” Colins akaendelea, akicheka. “Yaani
hivyohivyo, halafu si unajua masikio yako madogo fulani hivi, halafu kama
yamejikunja kwa juu? Bwana hivyohivyo!” Moyo wa Mill ukapasuka paa! Kama
kumeangushwa chuma sakafuni. Ila akajikaza.
“Walikuwa wakinitania
masikio yangu wakati nipo shule ya msingi. Mpaka wengine walikuwa wakiniita masikio.”
Colins akacheka sana. “Basi huyo mtoto yupo hivyohiyo, kasoro tu yeye ni mweupeee!
Nikasema kama ungekuwa umekana mimba enzi hizo za ujanani, ungeumbuka.”
“Kwamba ni kijana mkubwa wa kiasi hicho?” “Oooh yeah! Mkubwa kama miaka
12 hivi.” Akapiga mahesabu kwa harakaharaka, akajua hawezi kuwa wake.
Miaka 12 iliyopita hakuwa ameanzana na Pam. Akahema.
“Alikuwa
mgonjwa?” Lakini akajikuta tu anauliza akitaka kujua zaidi. “Kilichonifanya
nimwangalie ni aliyekuja naye, ni kijana tu alikuwa akimwambi mpira usio
na kiasi, utamuua. Sasa na dogo mwenyewe akawa na maumivu akawa
anamwambia aache kumuongelesha. Wakazidi kubishana pale mapokezi
wakisubiria zamu yao ifike, wahudumiwe. Nahisi ameumiza mkono, dogo
akawa analalamika maumivu ndio nikawaambia wamsaidie kwanza akamuone
daktari. Sijawafuatilia tena, nikaondoka zangu. Ila mmefanana aisee! Sana.”
Mill akacheka na kunyamaza.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Kile kitu
kikazidi kumsumbua nafsini mwake, japo kwa umri ashajiridhisha si
wake. Wazo kwamba wao ni wakubwa kimaumbile, lilishaondoka. “Hawezi
kuwa wangu.” Akajifariji. Lakini usiku huo akashindwa hata kulala kila
akiwaza jinsi alivyomuacha Pam! Moyo unapasuka kwa mshituko.
Asubuhi yake
wakati anasaidia wanae waende shule akaanza kuwaangalia kwa makini kama
hata wamerithi chochote kutoka kwake. Hakuna hata ukucha! Wote
wanafanana na mama yao. Akafikiria na kuamua kupuuza.
Zikapita siku
mbili nyingine, lakini hana amani kabisa anamfikiria huyo mtoto tu.
Akaonelea aanze kumtafuta tena Pam. Safari hii akaamua kwenda kazini kwa kaka
yake.
Kwa Eric.
Watoto wake
walipotoka tu, akashika safari mpaka kwenye benki aliyokuwa akifanya kazi kaka
yake Pam. Napo alihama benki muda mrefu zaidi ya miaka 9. Akaulizia alipohamia
ilikuwa benki nyingine ila amepanda cheo. Anafanya makao makuu.
Akaenda, akaomba
kumuona. Baada ya muda mfupi akamuona anatoka kwenye lifti. Hali yake nzuri tu.
Alishituka sana kumuona Mill.
“Umekuja kudai
mahari yako nini?” Kabla hajajibu akaendelea. “Nilijua tu mambo yatakufikia
huko uliko. Lakini sikulaumu. Pam amebadilika sana. Sisi wote
tulijua atatulia na wewe! Lakini wapi! Shangazi aliniambia habari zake, mpaka
nilitokwa na machozi na kumuomba radhi kwa niaba yake na mama.
Anasema kumbe nilipomuacha pale kwa shangazi akaanza umalaya akibadili
wanaume mchana na usiku. Chakusikitisha alikuwa akifanya uchafu
wake mbele ya watoto wa shangazi aisee!”
“Na nasikia
usiku alikuwa akizungumza na wanaume zake, palepale chumbani wengine
hawawezi kulala! Yaani shangazi anasema alivyosikia tu anachumbiwa,
akajua sababu ya kukimbilia kulipiwa mahari huko kwa mama, ni kuficha aibu
ya uchafu wake huku mjini. Anasema alijua tu angeachika. Sasa
ndio yakampata ya kumpata mpaka ukamuacha.” Mill akakunja uso, akawa
hajaelewa.
Eric akaendelea
kwa jazba. “Halafu sasa nasikia hata mimba yenyewe haijulikani baba kwa
sababu alikuwa na wanaume kibao! Wanaume wote walimkimbia baada ya
kushika mimba. Shangazi anasema akamkamata mume wa mtu kutaka kumbambikizia,
nasikia jamaa alikataa kabisa, hataki kusingiziwa mtoto peke yake
wakati walikuwa wengi. Ndio kasusiwa mtoto, analea
mwenyewe.”
“Mbaya zaidi,
nasikia alipoona maisha magumu, ana tumbo lisilo na baba, akaanza uwizi
pale nilipokuwa nimemtafutia kazi kwa Sandra. Sandra akachoka, akamfunga.”
Mill ALISHITUKA sana. “Unamaanisha kumfunga jela!?” “Kumbe! Wewe
unacheza na Sandra? Yule hana mchezo na pesa yake. Na nilimwambia
kabisa Pam. Hajasoma, ila kazi niliyokuwa nimemtafutia ni muujiza ambao
hautakaa ukatokea tena. Awe mwanangalifu, makini na anyenyekee.
Akaanza tamaa mpaka wakamfunga.”
“Sasa eti yupo
jela ndio ananipigia simu nikamsadie! Mke wangu akaniambia hatakaa
akajifunza. Amejiingiza mwenyewe, ajitoe mwenyewe.
Sikumtafuta tena. Ila nilikuja kumtafuta Sandra kumuomba radhi, maana
mimi ndiye niliyemuombea nafasi ya kazi pale. Akasema alilipa pesa yote
aliyokuwa akimuibia, kwa gari alilokuwa nalo Pam.” Mill akasikia kutetemeka
miguu.
“Bwana Pam sijui
aliingiwa na nini aisee! Na nilimsihi sana kabla sijamleta mjini. Babu
akazungumza naye kwa mifano kabisa. Amekuja mjini, ameanza tamaa zisizo
na sababu, ona alipo sasahivi.” “Unajua anako ishi?” Mill akauliza akiwa amevurugikiwa
kabisa.
“Mimi!? Aisee hapana.
Nilienda kunawa mikono mbele ya bibi na babu. Tena mama yake
anayemuendekeza alikuwepo. Nikawaambia nimefanya kwa sehemu yangu, yeye
mwenyewe ameshindwa. Sitaki tena kuja kumuona kwangu wala kumsikia.
Na mke wangu ndio hataki hata kumsikia. Tuna binti waliopevuka,
hataki Pam afike pale aanze kuwachanganya. Wakajifunza njia zake.
Kwa hiyo kama unadai mahari yako, andika maumivu. Wazee ndio
wamezeeka kabisa. Nina uhakika hata pesa ulizotoa walishasahau. Na mimi sin…”
“Eric, sikuja kudai pesa. Uwe na siku njema.” Mill akaondoka.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Alifika kwenye
gari, akashindwa hata kuondoa gari. Akahisi kuna kitu hakijakaa
sawa. Yeye ndio alikuwa mwanamme wa KWANZA kulala na Pam. Akakumbuka damu
alizomwaga siku anamtoa bikra. Maana ni Mill yeye mwenyewe ndiye aliyefua shuka
pale kwenye damu, ndipo akayapeleka yote nyumbani kwa Mike kufuliwa na mashine.
“Hapana. Kwa
swala la umalaya,…” Akataka kumkania lakini akasita. “Pengine
alibadilika nilivyoondoka.” Akili ikamrudisha kwenye shutuma za simu. “Inavyoonekana
hizo simu alizokuwa akizungumza usiku akiwa kwa shangazi yake, ni kabla
sijamchumbia. Pam alikuwa na maringo sana. Hakuwa na mwanamme wakuzungumza naye
usiku isipokuwa mimi! Ni nini kinaendelea?” Akazidi kuwaza bila jibu.
Ila kitendo cha
Sandra kumpokonya gari, kilimuuma sana. “Sio hawa waliniambia Pam ni
mwaminifu sana hawezi iba hata pesa ambayo Sandra mwenyewe hakuwa akijua kama
ipo?” Akajiuliza na kushangazwa sana. Akaamua kumsaka Jerry.
Kwa Jerry.
Simu ikaita,
Jerry akapokea kwa haraka sana. “Kwema kaka?” “Samahani naomba
kukuchukulia muda wako wakati wa kazi. Kuna kitu kinanisumbua kidogo.”
“Bila shaka.” Jerry akajibu.
“Ni kwa nini mlimfunga Pam?” Pakazuka ukimya hapo mpaka akahisi simu imekatika. “Jerry?”
“Kulitokea wizi hapa, ikaonekana yeye ndiye amechukua hiyo pesa.” “Unamaanisha
Pam yuleyule mliyekuwa mkimsifia ni mwaminifu sana, hata Sandra anaamani
pesa yake ikiwa mikononi mwake?!” “Na mimi nilimkumbusha hilo Sandra,
ila akaniambia watu wanabadilika.”
“Kweli Jerry ukakubali afungwe
jela kwa kosa ambalo hamkuthibitisha?” “Yeye Sandra alisema alikuwa na uhakika.
Sasa mimi ningefanyaje!?” “Hata ungeniambia mimi nilipe hilo deni.” Mill akalaumu na kumshangaza sana Jerry na kumpandisha hasira juu.
“Mill! Unazungumza nini kaka!?
Unaongea nini wewe?! Si wewe ulioa kimyakimya, ukaniweka mimi
mbali? Tena mimi niliyekuwa nikikusaidia kipindi kile na Pam? Ukamuacha
yule binti bila huruma na kwenda kuoa huko! Kama vile mimi ni ADUI yako,
ukamkaribisha tu Mike na Kamila kama vile hunijui au nidharau
ukaona mimi sina pesa kama nyinyi!”
“Nakuja kugundua mtandaoni!
Nikamuuliza Mike, Mike akaniambia umeamua iwe siri. Hata Pam hajui
na nisiseme. Ulitaka mimi nifanye nini na wakati kwanza ulishaoa
huko, bila kutaka mimi kujua, ukiniona ni mtu baki tu, sina maana?” Jerry alimbadilikia vibaya sana.
“Kwanza lazima utambue hili, ni WEWE
ndiye uliyemuingiza yule binti matatizoni Mill. Maana hiki kitu kimekuwa
kikiniumiza sana na Mike nilimwambia waziwazi.” Ikawa kama Jerry amefunguliwa funguo.
“Ulimkuta yule binti ametulia
sana hapa kazini. Alikuwa akiheshimiwa na kila mtu. Ukaanza kumfutilia.
Nikakupa madhara yake. Na hata Sandra alikwambia wazi kabisa. Alikuwahi
Lona, huwezi kuendelea na Pam. Ni SHERIA na walisainishana hapa.
Nikakwambia waziwazi, achana na Pam.”
“Ukatuthibitishia unampenda na utamuoa.
Ukaja ukatangaza hapa, ukamtia matatizoni akawa CHUKI na MSALITI
kwenye hii ofisi. Akabakiwa akiwindwa na kila mtu ili kulipizwa
kisasi, halafu wewe ukamtelekeza huku. Halafu usivyo na huruma
hata simu zake ukamfungia, ukaendeleza starehe zako huko
Marekani, mkisaidiana na rafiki yako kipenzi Mike.”
“Sasa kabla hujamlaumu mke wangu
kwa makosa YAKO, jua hivi, ALISHINDWA kumfukuza kazi kwa heshima
yako na Mike, mpaka ulipotokea huo wizi.”
“Pam ambaye isingekuwa WEWE,
hata kungeibiwa mamilioni ya pesa, na kamera zikamuonyesha anachukua,
watu wote wangemtetea. Lakini wewe ulikuja, ukamtia dosari
yule binti, alitolewa hapa na pingu na wote wakimshitaki
kwa polisi waliokuwa wameletwa na Sandra. Wakajitolea hata kutoa ushahidi
mahakamani, ilimradi tu KUMTOA hapa ofisini, wakimuhesabu ni msaliti wanaogopa
asije akaendelea kuwaibia mabwana zao.”
“Nakushauri ushauri wa mwisho,
kabla hujamtafuta aliyemuua Mike, nashauri angalia kwenye kioo, umtafute
aliyeua au kuangamiza maisha ya Pam, binti aliyekuwa AMETULIA na kuendesha
maisha yake hapa mjini bila TAMAA, akiwa anazungukwa na vishawishi.
Ukimpata ndiye yeye umlaumi, akisindikizwa kwenye maangamizi
yake na rafiki yake kipenzi Mike. Lakini sio mimi mliyekuwa mkinitenga
na kuniona sifai hata kuwa karibu na nyinyi kwenye safari zenu za
mapumziko.” Simu ikakatwa.
Mill alibaki
kama amepigwa na shoti ya umeme. Mwili wote umekufa gazi. Nyayo zinatoa jasho
wakati gari ameweka baridi mpaka mwisho.
Kwenye Vita Ya
Tembo….
Siku moja ya alhamis Andy alikuwa amefika hapo
nyumbani kwao kumchukua Ayan. Wakati akiegesha gari, akaona na gari ya Paul
inaingia getini. Akamsubiri. “Vipi?” “Nimeleta dawa za mama.” Paul akajibu. “Na
mimi ameniambia hajisikii vizuri ndio maana nimekuja leo. Vipi na wewe kazi.”
Paul akatulia kidogo kama anayefikiria akamwangalia Andy tena kisha akatulia
kidogo.
“Kwema?” Ikabidi Andy aulize. “Mimi mambo si mabaya.
Nitakwenda India mwezi ujao. Kwa ajili ya mambo ya moyo.” “Mama aliniambia.
Hongera.” “Asante. Lakini Andy, kuna jambo nataka kukwambia.” Andy
akatulia. “Ongeza umakini kaka.”
Andy akatulia.
“Najua upo makini, sana tu. Lakini nashauri, uongeze
umakini. Ni hilo tu.” “Kwa upande gani?” Andy akauliza. “Wewe ni mtu mzima
Andy. Fungua macho, ona. Najua
wazazi wanaogopa kukwambia. Lakini kaka, ongeza umakini.”
Paul akaingia ndani na kumuacha kaka yake hapo nje akitafakari.
~~~~~~~~~~~~~~
Maneno ya Paul mdogo wake yakaanza kumsumbua,
lakini hajui anamaanisha nini! Akafikiri labda ni swala la kumuacha
mtoto kwenye mikono ya watu. Akabaki akitafakari. Hata yeye hakujua kama mambo
ya kazini yangechukua muda mrefu kwa kiasi kile ili kuweza kutulia na
kujua kwa hakika makazi yatakuwa Dodoma au Morogoro au Iringa. Alitamani
kulijua hilo kwa hakika ili atulie na mtoto wake nyumbani, lakini ikawa ni mvurugano.
Anaambiwa azunguke kwenye maofisi yao, afundishe kile alichojifunza yeye
huko Uswiz. Ikawa na yeye hata hajui juma hilo litamkuta mkoa gani!
Hiyo kazi ikawa imeshamgharimu NDOA, sasa MTOTO.
Na yeye mwenyewe akawa wakuhangaika tu! Wakamuahidi akiweka mambo sawa,
ndipo atapewa sasa kitengo maalumu. Lakini ikawa shida. Akiwa Dar, angalau
aliweza kuwa na Ayan. Anampeleka kwao asubuhi na kwenda kumchukua jioni akitoka
kazini.
~~~~~~~~~~~~~~
Miezi minne ikawa imeshapita tokea aachane na
Mina. Mina akawa anakaribia kumaliza mimba ya miezi 5 kwa wakati huo.
Alisharudisha nguvu na afya yake baada ya kuacha kutapika. Angalau akawa
anaweza hata kukaa siku nzima hajatapika. Akawa ameshajua ni vitu gani
vinamfanya atapike. Akawa mtu wakujiwinda kweli ili asitapike.
Mama Ni Mama Tu.
Siku moja Andy akiwa Dodoma akapata ujumbe kutoka kwa
Mina. ‘Sina nia ya kukukera Andy, naulizia hali
ya mwanangu. Na ninajua anakaribia kutimiza miaka minne sasa. Tafadhali Andy,
naomba niruhusu kumuona mwanangu. Hata hiyo siku ya birthday yake tu. Nimletee zawadi, nimsalimie
kidogo, niondoke.’ Andy hakutegemea.
Alikuwa kati kati ya kikao, akabaki ameduwaa. Hakujua hata birthday ya Ayan inakaribia. “Nimekosa ngapi!?” Akajiuliza Andy.
Akaadhimia kutomjibu Mina mpaka awe ameweka mipango
mizuri ya hiyo birthday.
Hapo hapo akatoka na kwenda kumpigia simu mama yake. “Birthday ya Ayan yakutimiza miaka minne ni alhamisi
hii. Naomba tumfanyie sherehe.” Ilikuwa
jumatatu asubuhi. “Mbona babu yake ameshaanza
maandalizi! Amewaambia watu wote. Na keki nimeshaenda kuweka oda.” “Nashukuru
mama.” Andy akajisikia vibaya sana, lakini angalau akashukuru
Mina amemkumbusha, hajaingia aibu.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Mina akaona amesoma ujumbe, lakini hamna majibu.
Akanyamaza. Alisubiri siku nzima ili ajue kama anarudi Dar kumuona mtoto wake
au la. Akasubiri mpaka usiku. Kwenye saa nne hivi, ujumbe kutoka kwa Andy
ukaingia. ‘Itafanyika sherehe yake siku ya jumamosi,
Msasani kwa wazazi. Mida ya jioni. Unaweza kuwepo.’ Mina hakuamini. Akakaa na kuanza kulia.
‘Asante Andy. Ni sawa mimi nikamuona siku ya
alhamisi yenyewe ya birthday yake? Kwa muda mfupi tu. Popote alipo, nitamfuata. Angalau
nimsalimie na nimpe zawadi yake.’ Kimya.
Andy akajua Mina anataka kumuharibia utaratibu. Alhamis hawezi kuwepo
Dar, alitaka kwenda ijumaa, ili akae mpaka jumatatu. Na hakutaka Mina ajue kama
UTABIRI wake umetimia, kuwa hawezi kuja kutulia, kazi
inamlemea.
‘Itatoa utulivu kwenye sherehe ya
Ayan akiwa na familia, Andy. Fikiria kwa sasa, mimi niwe katikati ya ndugu zake
Ayan, sidhani kama ni sawa. Tutaharibu sherehe muhimu ya mtoto. Bora
kuwapa nafasi bila mimi kuwepo kuwakera.’ Hapo Mina alikuwa sahihi hata Andy akaafiki. Lakini atafanyaje na yeye
yupo Dodoma! Andy akabaki akifikiria. Mina akajua ndio amekataa. Akaweka
simu pembeni, akalala na kumuacha kabisa kama kumpa nafasi yakufikiria.
Asubuhi alipoamka, akakuta ujumbe kutoka kwa Andy. ‘Unaweza kufika siku hiyo ya jumamosi asubuhi pale Msasani.
Utamkuta Ayan. Mkapata muda kabla ya sherehe jioni.’ Mina naye akaona ni
sawa. Akajua Andy hataki kabisa afike nyumbani kwake kule kwenye apartment. Lakini akaona ni haki yake. ‘Nitafanya
hivyo. Nashukuru.’ Akarudisha majibu.
~~~~~~~~~~~~~~
Mina
aliondoka Iringa siku ya alhamisi. Akarudi kwenye hoteli ile ile aliyotumia alipofukuzwa
kwao. Kesho yake siku ya ijumaa akaiita siku
ya kujisafi. Alikwenda kuoshwa miguu na kupakwa rangi. Akabandika kucha
nzuri sana, zikamkaa vizuri. Akasukwa vizuri. Hata yeye Mina alijua amependeza.
Aliporudi hotelini ndipo akamtafuta shem Pius.
Mina na Pius tena.
Pius alitoka kazini moja kwa moja kwa Mina, hotelini.
Alifurahi sana kumuona Mina. “Umekonda lakini ukapendeza. Mtoto
anaendeleaje?” “Si nilishakwambia anacheza?” Mina akauliza akicheka.
“Uliniahidi tukionana, akicheza utaniruhusu nimshike.” Mina akacheka sana.
“Sawa. Mbona na mifuko sasa?” Mina akauliza. “Zawadi
zako na mtoto.” “Asante sana P. Mungu akubariki.” Jina la shemeji walishaliua. “Nilikuwa na hamu ya kukuona
Mina!” Mina akacheka kama anayefikiria. “Lakini nikushukuru kwa kutunza ahadi
yako yakunitafuta na kutunza mawasiliano kati yetu.” “Na mimi
nikushukuru kwa ahadi ya kunitunza vizuri. Nashukuru P.
Naishi vizuri, na daktari wa wakina mama uliyenitafutia ni mzuri. Ananisaidia sana mimi na mtoto.
Nakushukuru. Asante.” Pius na Mina wakakaa kitandani wakiongea.
Wawili hao ni kuonana tu, lakini walikuwa wakiwasiliana
sana. Asubuhi, mchana na jioni. Kila siku. Vikajaa vicheko hapo, kama
marafiki wa muda mrefu kukutana. “Umekula?” “Nilikula nikiwa
nimechelewa, bado nimeshiba. Wewe unanjaa?” “Nitakwenda kula nyumbani.” “Sawa.”
Wakaendeleza mazungumzo.
Katikati ya mazungumzo Mina akashituka kidogo. “Nini?”
“Anacheza P!” Mina akamshika mkono na kumvutia tumboni. “Atakuwa mcheza mpira nini! Mbona fujo!” Mina akacheka sana. “Si
nilikwambia, akianza kama unasinzia nilazima uamke!” Pius akaanza
kumpapasa tumbo taratibu na kwa makini. Akambusu tumboni mara kadhaa. Akashangaa
Pius anafurahia sana.
Mina akamuona amepotelea mawazoni akiendelea kumpapasa
taratibu. “Utanifanya nilale bwana P! Acha kunibembeleza.” “Basi nenda
kaoge kabisa, upande kitandani nikubembeleze mpaka ulale.” Mina akacheka.
“Kweli?” “Kweli, nitakusubiri.” Akasimama kwa haraka kuelekea bafuni.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Pius alikuwa akimtunza kwa kumtumia mapesa haswa. Na ni yeye Pius ndiye aliyemuomba waache
kuitana shemeji. Ndoa ilishakufa.
Na talaka alishapewa! Akamwambia wasiitane shemeji. Mahusiano mengi yakawa yakubembelezana
kwenye simu. Mpaka akamvutia Mina na kumbadili hisia kabisa. Kwa kuwasikiliza
kwenye simu, wazi ungejua mambo
yameshabadilika. Zipo hisia
zingine kabisa katikati yao, japo hawakuwa wameambiana kwa simu.
Timing…
Wanasema timing is everything. Ndicho alichokuwa akifanikiwa
nacho Pius. Alijua kusoma majira na nyakati ya kila kitu mpaka kuweza kupata kila
kitu anachokitaka, nakufanikiwa pande zote. Alijua kusoma watu
na mazingira. Andy akiwa amemuacha Mina, tena kikatitili kama
hawara tu, yeye Pius ndio akaingia ndani ya picha.
Akaziba pengo la Andy kwa upande wa matunzo
na kujali kwa kila namna. Kisha akaziba pengo la mama Ron kwa haraka sana, kwa kumjali sana Mina huku akimfariji
na kumtafutia matibabu mazuri.
Kwa hasira, WOTE wakamkosa Mina, wakiwa wamemzira, lakini
Pius aliyebeba siri ya dhambi ndani yake, akajishindia Mina kiulaini na kujihalalishia juu! Talaka kapewa. Mina si mke wa mtu tena, halafu amembebea mtoto
wake! Pius akajihalalishia Mina. Na hivi alishaonja asali, akakusudia kujenga mzinga kwa garama yeyote ile.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Akaoga
harakahara, akatoka na nguo yakulalia. Nzuri tu. Pius akimtizama. Akajua usiku
huo hata akiomba penzi, atapewa
tu.
“Bado hutaki kujua jinsia ya mtoto?”
Pius akauliza taratibu tu. “Naona haina maana. Kwangu mtoto ni mtoto tu. Sina uchaguzi.
Atakayekuja ndio huyo huyo.” “Ngoja mimi nimuulize mwenyewe.” Akaenda pale
aliposimama Mina, akamvutia kitandani. “Si naruhusiwa kuuliza?” Pius akauliza
taratibu. Mina akacheka akitingisha kichwa kukubali akiwa amejilaza hapo
kitandani, amejiegemeza kwenye mto.
Pius akaanza kumpapasa tumboni huku akiongea na huyo
mtoto. Juu ya tumbo, chini. Juu karibu na matiti kabisa, chini kabisa. Mina
ambaye mwili huo haukuwa umeshikwa na mwanaume akiwa na fahamu yake
karibia mwaka, akalegea
kabisa hapo kitandani.
Pius akajua ameridhia. Akaenda kumbusu
midomoni. Akashangaaa Mina anamkumbatia kwa nguvu zote. Pius
akachangamka, kama aliyeokota lulu. Yakaanza mapenzi. Pius alimtoa nguo
zote na kuzitupa mbali kama hazitakiwi tena. Akatoa zake kwa haraka.
Mapenzi yakaendelea hapo Mina akimkumbatia kwa hisia zote.
Pius mwenyewe hakuamini kama Mina na tumbo lile
angempa ya ukweli kiasi kile. Mina alijitoa hapo kitandani akilipa
fadhila. Alijitahidi kumfurahisha Pius, Pius akabaki akilia kama mtoto.
Mina alihakikisha anamfurahisha na kumshukuru kwa maneno mbali na
hivyo vitendo. “Hii ni kwa kunitunza mimi na mtoto.” Akajituma tena na tena,
ndipo sasa Pius akarudisha kumfurahisha. Ilichezwa mechi hapo, kama wanao
gombania kombe la dunia! Kila mtu akatoa ujuzi wake kwa kujinafasi mpaka
wakaridhika. Alirudi kuoga tena, akambembeleza mpaka akalala ndipo akaondoka
akiwa amemuacha amelala.
~~~~~~~~~~~~~~
Jumamosi asubuhi sana, Pius akarudi tena hapo
hotelini. Ikaanza romance ya
nguvu iliyoambatana na mapenzi jingine tena. Wakaendelea hapo, Pius akishindwa
kutosheka mpaka kwenye mida ya saa tatu asubuhi, ndipo Mina akamwambia anataka
alale kidogo kabla ya kuondoka kwenda kumuona mtoto wake.
Akamshukuru, akaondoka akiwa na tumaini na
penzi la kudumu la Mina. Kwani safari
hii alimpa penzi kwa akili yake timamu, na alimuonyesha ni WAKE, hawezi kumnyima.
Pius akafurahia juhudi za kumtunza, zimemlipa. Ataendelea kumfaidi
Mina bila shida wala kipingamizi. Akamuacha amelala akijua watajipanga zaidi
baadaye.
~~~~~~~~~~~~~~
Huwa Mara nyingi, Maisha ya wazazi huendelea baada ya
Talaka, wanabakia watoto kuwa wahanga, wakilipa
gharama ya maamuzi ya wazazi wao.
Huachwa kwenye majumba makubwa na ya kifahari, lakini wakiteseka.
Ndicho kinachompata Ayan. Baba yake anaendelea kukimbizana
na ndoto zake, mama yake anafarijiwa na Pius, yeye
ameachwa akimangamanga kwenye majumba ya watu akiteswa.
Inaendelea….
0 Comments:
Post a Comment