![]() |
“Yaani unataka kunipunja mimi sababu ya maisha
yako ya nyuma!?” “Nakosa ujasiri!” “Hapana Mina. Sio na mimi. Mimi nimechukua
hatua kubwa sana kwako. Nimejifunga kwako, na kila mtu anajua sasa hivi
mimi ni wako. Ndiye niliyetakiwa nifaidi yote kuliko wote. Sasa
tena mimi ndio napunjwa! Utakuwa hunitendei haki!” “Samahani
Andy, basi nitajitahidi.”
“Unajitahidi vipi? Kwani hujisikii hata kunigusa?!”
“Najisikia ila ukumbuke mara ya mwisho hali niliyokuwa nayo Andy. Niliingiwa na
hofu. Kitu kilichokuwa hai, kikafa ndani yangu! Halafu ikabidi kitolewe
na kusafishwa, tena bila ganzi! Iliuma Andy, hakuna jinsi nikakwambia
ukaelewa. Mwili mzima unauma kila nikifikiria hivyo. Natetemeka.”
Hapo Andy akaelewa vizuri.
“Samahani Mina. Hapo nimekuelewa sawasawa. Basi
tuchukue taratibu. Nitakusubiri.” Mina akacheka na kumsogelea. “Wewe ni
mtu mzuri Andy.” Andy akacheka.
“Nikumbatie tena.” “Una uhakika?” Mina akatingisha
kichwa kukubali. Akamkumbatia vizuri. Mina akajipanga hapo kwenye kochi, Andy
alikaribia kuvua suruali. Mina alimpa mabusu yakumchanganya, akabaki
akitetemeka huku amemkumbatia kwa nguvu.
Maana alitulia hapo mwilini kwa Andy akiwa amemlalia.
Andy akaona anajipunja, akamvuta zaidi, akanyoosha mguu mmoja kwenye kochi,
Mina akawa katikati ya miguu, akajilaza kifuani huku akiendelea kunyonywa
midomo yake kwa uchu. Mabusu hayo yakaendelea Mina akijizungusha katikati ya
mapaja yake, akishikwa kwa uchu.
Alijaa kifuani, Andy akabaki aking’ang’ania hajui tena
pakushika. Baada ya muda, Mina akajilaza kifuani na kumkumbatia kwa kupitisha
mikono yote miwili pembeni ya kifua. Wakabaki wakivuta pumzi kwa nguvu.
Baada ya muda akanyanyua uso, akakuta Andy
akimwangalia. “Nakupenda Andy, naomba hilo usilitilie shaka.” “Nimefurahi
kukusikia na wewe ukiniambia Mina. Hukuwahi hata kuropoka!” “Ni hofu tu na
aibu, Andy. Ila nakupenda.” “Basi nimefurahi kusikia hivyo. Inanipa ujasiri
zaidi. Nilikuwa naona ni kama nalazimishia kila kitu!” Mina akacheka na
kujirudisha kifuani. Wakatulia kwa muda.
“Acha nirudi nyumbani. Nisichelewe zaidi.” “Natamani
tubaki wote!” Mina akacheka na kumbusu pale alipokuwa amemuegemea. “Urudi
tena.” “Lini?” “Naomba tufanye jumamosi na jumapili ndio siku zetu
zakuwa pamoja.” Mina akakaa.
“Lakini mimi naabudu kwengine na wewe unakwenda
kanisani na wazazi wako. Itakuaje?” Hilo likawa swali la msingi na gumu. Andy
ni mwaRC damu. Mina hajui kanisa jingine na la msingi la kung’ang’ania kama
alivyomuona mama yake akifanya, kama Lutheran. Inakuaje?
“Cha kwanza nataka ujue wewe kwanza. Katika
kila nilifanyalo nitakutanguliza wewe.” “Jamani Andy!” “Kweli Mina.
Najenga familia yangu na wewe. Lazima nikuangalie wewe. Halafu
juu ya baadaye itakuaje, naomba tulifikirie hilo. Mmoja wetu ni lazima alipe
garama ili tuweze kuwa pamoja.” Mina akainama kama ambaye ashaona historia ya
mama yake inataka kujirudia na kwake.
“Naomba tufikirie kabla hatujaweka au kuona ugumu
wowote. Tumekubaliana kuwa tunapendana, si ndiyo?” “Nakupenda Andy.”
“Basi hilo ndilo la msingi. Mengine naomba tujipe muda wakufikiria.” “Sawa.”
Andy akamrudisha mpaka nyumbani. Akasalimia ndani, ndipo akaondoka.
~~~~~~~~~~~~~~
Maisha ya wapenzi hao yakaanza. Mina akitoka shule,
anakwenda ofisini kwa Andy moja kwa moja. Anamsubiri mpaka akitoka, anamrudisha
nyumbani. Ghafla Tegeta kukawa karibu sana kwa Andy. Andy akawa haonekaniki
tena nyumbani kwao. Si jumamosi, si jumapili. Jumapili ya pili nayo ikaisha.
Ikaja ya tatu pia akatoa udhuru.
Kila mtu nyumbani kwao akajua ni sababu ya kutoelewana
jumapili ya mwisho kuwepo kwao kwa kutoendeleza mahusiano na Lora. Tokea
aondoke hapo siku ile, Andy hakurudi tena. Alikuwa akituma ujumbe kila
siku ya jumapili asubuhi akiwataarifu wazazi wake kuwa siku hiyo hatafika
kanisani na nyumbani. Hivyo tu, basi. Hataonekana kwao wala kusikika
tena mpaka jumapili nyingine tena akitoa udhuru.
Akazoea midomo ya Mina, akawa kama mwenye kiu
naye kila wakati. Mikono yake wakati wote ilitaka kumpapasa. Jumamosi
zikawa ni za Mina kuwekwa mikononi. Hata wakiwa na mipango siku hiyo, basi
itatafutwa sababu ya Mina kuwepo hapo mikoni mwake. Akawa kama ameshachanganywa
na Mina. Akili na mawazo ya Andy yakawa Tegeta kama hayupo hapo na Mina.
Jumamosi asubuhi anaanzia mazoezini, anarudi nyumbani
kuoga. Saa nne asubuhi, anakuwa ameshafika nyumbani kwa kina Mina.
Anatoka naye kwenda sokoni. Wananunua vitu vya nyumbani kwao, na nyumbani kwa
Andy. Wanapeleka vitu kwa kina Mina, kisha wanarudi kwa Andy. Watakaa hapo kwa
Andy wakishikana hapa na pale. Huku wakipika hiki na kile na kufundishana hili
na lile mpaka usiku anamrudisha kwao.
~~~~~~~~~~~~~~
Na ili asimpoteze aje amuoe, Mina alikusudia aendelee hivyohivyo kumuonjesha mpaka
atangaze ndoa,
afunge watu midomo. Alimpenda sana Andy. Alitamani yeye ndio awe mwanaume wa
mwisho kwake kwenye safari ya mapenzi. Lakini alijua fika, akishampa tu penzi, na hivi siku za jumamosi na jumapili
wanakuwa wote, atakosa sababu ya kumuoa. Akakusudia ambane, awe anamuonjesha vya
kupitiliza, lakini asimvulie nguo mpaka
atangaze ndoa yeye mwenyewe. Akisha muweka ndani ndipo ampe yenyewe.
Basi akawa akimfanyia makusudi.
Ulalaji wake hapo wakipeana kiss, ungemuhurumia Andy. Atajilegeza juu ya suruali ya mwenzie, huku
matiti yote yapo kifuani, akimnyonya midomo mpaka masikio huku kucha zikipita
shingoni. Basi Andy anakuwa kama bwege hapo
kwenye kochi, hawezi hata kusogea! Hajui muda. Hajali yeyote ila huyo Mina tu. Atamng’ang’ania
hapo abaki amemlalia mpaka aagwe.
~~~~~~~~~~~~~~
Jumapili, Andy mtoto huyo wa kikatoliki anaishia kanisani alipo Mina. Wakitoka hapo
watakwenda kula kama familia. Mina akila na kisu na uma kama Andy. Vitajaa
vicheko, wanawarudisha Ron na mama nyumbani, au Ron ataondoka na mama yake,
Andy anarudi kwake na Mina amfanyie anayomfanyia mpaka usiku ndipo anamrudisha
kwao.
~~~~~~~~~~~~~~
Mwezi na week vilipoisha, ikabidi mama yake ampigie
simu Andy. “Nipo mama. Nakuwa na Mina.” “Sasa kwa nini
usimkaribishe nyumbani?” Andy
akabaki kimya. “Itakuwa vizuri na sisi tumfahamu.”
Mama Ruhinda akaongeza ushawishi. “Basi
nitazungumza naye tuone.” “Inamaana ndio mmefika mbali hivyo!”
Mama yake akashangaa. “Mama! Asante kwa mualiko,
nitakujulisha kama tutakuja.” Andy akajibu na kuaga.
~~~~~~~~~~~~~~
Siku ya jumamosi akiwa na Mina. Yakaanza mabusu. Safari
hii akaongoza yeye mchezo. Akampapasa kwa kupitiliza kwa makusudi, mpaka
akamuona ametulia kabisa kifuani na yeye amezidiwa. Akamwachia midomo taratibu huku
mikono akiirudisha kiunoni mpaka Mina akaona aibu maana alifika juu haswa. Akajilaza
kifuani akihema. Andy akambusu kichwani mara kadhaa akitulia.
Kisha akamchungulia pale alipokuwa amejilaza kifuani
kwake amemkumbatia. “Naomba nikukaribishe na mimi kanisani kwetu.” Mina alishituka
mpaka akakaa. “Andy!” “Utakuwa na mimi. Na baada ya hapo tutakwenda wote
nyumbani kwa wazazi kwa ajili ya chakula cha mchana.” Mina akakosa raha kabisa
mpaka Andy akamuona. Akajivuta pembeni kabisa.
“Kama haupo tayari ni sawa Mina. Nitasubiri.”
Hilo likamfanya kumuhurumia, akaona ajirudi. “Natakiwa kuvaa aje?” “Kama
kawaida unavyovaa kanisani kwenu. Kuwa kama wewe, usiogope.” Akabaki
akifikiria. Akajua historia ya mama yake inataka kujirudia kwake. Maswala ya dini.
Wakidhani ukristo na uislamu ni tatizo, sasa hivi ni madhehebu ndani
ya ukristo.
~~~~~~~~~~~~~~
Kesho yake asubuhi alikwenda kumchukua Mina nyumbani
kwao. “Umependeza Mina! Sana.” “Mwenzio nimemuamsha mama tokea saa 11 anisaidie
kujiandaa.” Andy akacheka. “Alifanya nini sasa?” “Yeye tokea zamani anajua
kuzichana hizi nywele zetu, tumetoa kutoka upande wa baba. Alikuwa akimchana na
Ron, zinakaa vizuri sana. Sijui anafanyaje, lakini hata zangu anaweza kuzitoa
nimenyooka vizuri zaidi! Sasa leo amenichana na kuzibana hivyo.” “Zimekupendeza
sana. Unaonekana vizuri.” Mina akacheka.
“Umeona na hereni zangu lakini? Na Cheni!” Andy
akacheka. “Umependa?” “Sana. Si umeona jinsi vilivyonipendeza? Nanukia vizuri.
Asante Andy.” “Karibu.” Akataka kuinama na kumpa busu. “Utatoa mafuta ya mdomo
Andy bwana!” “Yaani hayo mafuta ni muhimu kuliko mimi, Mina!? Hujaniona tokea
jana!” “Basi Andy.” Akajinyanyua pale kitini, kabla Andy hajatoa gari pale
nyumbani kwao.
Akaanza kumpa denda. Midomo hiyo ya Mina, huwa hatoshekagi. Kama ambaye hana haraka tena,
Andy akaendelea kufurahia hiyo midomo ndipo akaondoa gari. “Umefurahi sasa?”
“Kiasi.” Mina akacheka. “Tukitoka kwenu nitakukiss mpaka utosheke.” “Siwezi.” Mina akazidi kucheka.
“Leo utatosheka. Nakuja kivingine.” Andy
alicheka. Akashindwa kunyamaza. Kila alipomwangalia Mina alicheka. “Can't wait! Itabidi tuharakishe kuondoka nyumbani.” “Hapo utafanya
nikupe double dose.” Mina akaendelea
kutoa ahadi za kupagawisha, Andy anacheka. Walifika kanisani wakiwa wanacheka
kwa kujibishana maneno.
Andy alienda kumfungulia mlango wakaanza kutembea huku
amemshika mkono kwa kupishanisha vidole vyao, akamvuta mkono mpaka kwapani, kwa
hiyo akawa amemvuta Mina karibu wanatembea taratibu wakisogelea kanisani. Mina
hakuwa akijua ndugu wa Andy kwa kuwaona japo aliona baadhi ya picha nyumbani
kwake, lakini akili zilikuwa zimezama kwa Andy anaongea huku akimwangalia yeye
na mbele ila wakicheka sana.
Mina Na Kina
Ruhinda.
Akaona ameongea kitu cha kuchekesha hacheki!
Akamwangalia usoni. “Andy?” Akaona anaangalia mbele na yeye akaangalia akaona
watu mbele yao wamesimama kama kundi. Akarudi kumuangalia Andy, na yeye
akamwangalia. Akajua ndio ndugu zake. Wakawasogelea.
“Shikamoo baba na mama. Huyu ndiye Mina.” “Deeng’iii!”
Akasikika Paul huku akimtizama Mina kuanzia juu mpaka chini. “Shikamooni.”
Akasalimia Mina akiangalia mmoja hadi mwingine taratibu. Kimya. Akarudi
kumtizama Andy. Akamvuta kidogo kama anayemuita. Andy akainama, akamsogelea
sikioni. “Nilitakiwa kufanya nini?” Akamnong’oneza sikioni huku amemshika sikio
kama wengine wasisikie. Wote wakabaki wakiwatizama wao vile wanavyo
nong’onezana. “Ni sawa.” Andy akamjibu. Mina akajisogeza karibu ya Andy na
kunyamaza.
“Huyo mtoto umemtolea wapi, Andy!?” Akauliza
mama yake kama aliyeshituka kutoka usingizini na kukutana na maajabu.
Andy akabaki kimya akimwangalia mama yake. “Una miaka mingapi wewe mtoto?
Umetimiza hata 18 kweli!?” Akamgeukia Mina. Mina akamwangalia Andy na kurudisha
macho kwa mama Ruhinda. “Ninatimiza miaka 22-week ijayo.” Paul akaanza kucheka,
wote wakamwangalia Andy kwa mshangao.
“Twende kanisani Mina.” Andy akawazunguka huku
amemshika Mina mkono. “Wooo, Wooo!” Paul akaenda kusimama mbele yao. “Mbona
hamna utambulisho Andy!?” Akamsogelea Mina. “Mimi naitwa Paul, mdogo
wake Andy.” Mina akampa mkono. “Nimefurahi kukufahamu Paul. Mimi naitwa Mina.”
Akajitambulisha huku akimwangalia Andy. “Karibu kanisani Mina. Ujisikie upo
kwenye Misa takatifu.”
“Asante.” Andy akaingia kanisani na Mina. Wakakaa upande uleule anaojua familia
nzima wanakaa. Ndugu zake wakaingia na kujipanga pembeni yao, wazazi wao mbele
na wajukuu. Misa ikaendelea, Mina akifuatisha hiki na kile, lakini kimya kimya
mpaka Misa ilipoisha, wakatoka.
~~~~~~~~~~~~~~
“Si tunaongozana nyumbani?” Akauliza baba yake. Andy akabaki kama anayefikiria
bila jibu. Mina yupo pembeni. Wote wanawaangalia. “Sijui baba!” “Mimi
nafikiri mkaribie tu nyumbani kama hamna mipango mingine. Tule chakula pamoja
ndipo tuachane. Msiishie tu hapa kanisani.” Tayari kukawa na kusita
kwa Andy. Akabaki kimya bila yakutoa jibu. Mzee Ruhinda akamgeukia Mina.
“Karibu mama nyumbani.” Akampa mkono. “Asante.” Mina akaitikia na goti. Ndipo
wengine wakampa mkono. Lakini Mina akahisi kama kuna uzito tayari. Kama
kawaida yake akanyamaza ili kuepusha shari.
Mina Nyumbani Kwa Kina Ruhinda.
Alifika hapo kwa kina Ruhinda, ndipo akawaelewa ni kwa
nini wanamshangaa. Jumba lenyewe la huyo mzee Ruhinda, linatangaza
ustaarabu na utajiri. Halafu kila mtu alijua nini chakufanya na wapi pakwenda,
mpaka watoto! Akabaki ametoa macho. “Hatutakaa muda mrefu. Usiogope.”
Andy akamnong’oneza. Wakakaa sebuleni, akaona yupo pale na wanaume tu.
Akaangalia kulia na kushoto, akagundua wanawake wapo
jikoni. “Labda na mimi nikasaidie jikoni.” Akamnong’oneza Andy sikioni. Wakati
tv imewashwa hapo sebuleni. “Sawa. Twende nikupeleke.” Wakanyanyuka.
Walifika jikoni wakakuta ukimya wa namna yake. “Mina
anataka kusaidia chochote.” “Hamna kitu anachoweza kufanya humu ndani.”
Akawahi mama Ruhinda kwa jazba. Andy akacheka na kumshika Mina mkono kama
anayetaka kuondoka naye. “Labda aje anisaidie mimi kuandaa mboga za majani
wakati natayarisha mchuzi.” Akawahi mke wa kaka yao, Raza.
“Paulina atapika hizo mboga.” Akajibu tena mama
Ruhinda. “Kama Paulina anapika mboga, basi yeye aandae hata viungo ili
asijikute amekaa tu.” Akaongeza Raza. “Hivi mmemuona huyo mtoto jamani au ni macho yangu tu!” Akaanza kwa ukali mama
Ruhinda. Wote wakamgeukia.
“Akiungua huku jikoni au akijikata! Hiyo kesi
si itakuwa yangu mimi?” Andy akacheka na kutingisha kichwa. Akainama kwa
kuchoka kabisa.
“Lakini mimi huwa napika kabisa! Naweza kupika kila
kitu. Labda viwe vyakula vya kigeni.” Akaongea Mina kwa upole na unyenyekevu.
“Na nitakuwa mwangalifu, sitajikata.” “Nyumbani kwenu. Lakini sio
hapa kwangu. Hapa wewe ni mgeni, kakae sebuleni. Usubiri
chakula.” Andy akamchukua Mina wake, wakarudi sebuleni kimya. Baba yake naye ni
kama akajionya. Kimya. Mina akajisikia uchungu, akaona aende tu chooni akatulie.
~~~~~~~~~~~~~~
“Vipi lakini kazi?”
Pius akajaribu kubadili hali ya hewa pale akimuuliza Andy. “Nzuri tu.
Tunaendelea.” Jinsi alivyojibu, hapakuwa na jinsi ya kuendeleza mpaka Mina
akarudi na kukaa pembeni ya Andy. Akawasogelea mtoto wa Pius.
“Mina, kuna game za
kwenye tv, unataka tukacheze?” Akauliza mtoto mdogo wa Pius. Mpaka mzee Ruhinda
akacheka. “Mpaka watoto wanamuona ni mtoto
mwenzao!” Akaongeza mama Ruhinda huko jikoni lakini kwa sauti ya juu ili kila
mtu asikie.
“Mimi sijui kucheza hizo game. Labda unifundishe.” Mina akajibu vizuri tu. “Twende. Nirahisi sana.”
Mina akamwangalia Andy. Alipomuona anacheka, akambusu shavuni bila hofu,
palepale mbele ya ndugu zake na baba yake. Akasimama na kuondoka na mtoto wa
Pius.
Kama alivyo Mina, akaanza kucheka kule chumba
cha watoto anakocheza. Wakamsikia akicheka kwa sauti ya furaha kweli! Watoto
wakawa wanacheza naye, Mina akawa ashasahau ya jikoni, anacheka, hana
habari kama yuko ukweni! Kadiri alivyokuwa akicheka, wakamuona na Andy
naye anacheka huku ameinama.
Alicheka vizuri Mina, ungejua hana hila moyoni
mwake. Hata watoto waliokuwa wakisoma na kuchora wakahamia hapo kwenye game alipokuwa akicheza. Wakashindana kuendesha magari
kwenye tv, watoto wanapiga kelele, na Mina naye anacheka kadiri anavyogongesha
gari lake. “Mbona sasa mimi siwezi kama wewe?” Wakamsikia Mina anauliza huku
akicheka. “Utazoea. Inabidi utulize mkono kabisa. Halafu uwe makini bila hofu.”
Yule mtoto akawa anamuelekeza.
Mina alikuwa amekaa chini kabisa na mtoto mdogo wa
Pius mwenye tabia kama mtoto wa kiume mpaka walisema alitakiwa awe wa kiume!
Michezo yake mingi alipenda yakiume. Ndiye akawa sasa mwalimu wa Mina.
Wakacheza hapo watoto wakifurahia. Hawakuwa wadogo. Vibinti vya miaka 10 kwenda
juu.
Huyo mdogo,
Raza alimzaa akiwa amekata tamaa. Ndiye aliyekuwa na miaka 10. Wote
wakajikusanya hapo kwa Mina. Hakuna hata aliyesoma au kufanya jingine ila
kujisogeza hapo kwa Mina wakionekana kumfurahia. Wazazi wao wakahamisha masikio
huko kwenye sebule ndogo ambayo wapo, wakawa wanawasikiliza wao.
Mama Mkwe!
Wakaja kuitwa na Raza kuwa chakula tayari. Mina na
wale watoto wakatoka na kukuta kila mtu mezani. Mina akaenda kukaa pembeni ya
Andy. “Nimeweza mwenzio.” Andy akacheka. “Nimesikia ulivyokuwa ukisababisha
ajali!” Mina akaanza kucheka. “Dereva wewe lazima tuanze mafundisho ya nguvu.”
“Lakini sasa hivi Mina amekuwa mtaalamu, anko! Ameshajua.” Mtoto mdogo wa Pius,
aliyekuwa akimfundisha, akamtetea. “Kwa kuwa na wewe ni mwalimu mzuri ndio
maana nimeelewa haraka.” Akaongea Mina na moyo wake washukurani. Ikawagusa
wengi hapo mezani.
“Asante Mina. Utarudi tena tuje kucheza?” “Tutapanga
na Andy. Halafu atazungumza na mama yako tuone.” “Yess!” Akasikika kufurahia
mtoto wa Pius. “Kwa game huyu!”
Baba yake akaguna.
“Wewe Mina umesema una miaka 22, umesomea mambo ya
nini?” Mama Ruhinda akarusha hilo swali katikati ya hayo mazungumzo. Mina
akatulia kidogo. Akajiweka sawa. “Ndio nasoma mambo ya kompyuta. Kudesign
website, logo na mambo mengine.” “Hongera sana mama.” Akadakia mzee Ruhinda.
“Asante.” “Unasomea wapi?” Akauliza Paulina. “TQ Tech.” Pakazuka ukimya, wakiangaliana
kama wanashangaa.
“Ndio wapi!?”
Akauliza tena Paulina. “Ni chuo kidogo tu, kipo mtaa wa Samora.” Akajibu
Mina taratibu tu bila hata wasiwasi. Andy akamsogezea chakula. Akapakua.
“Subiri kwanza Mina. Unasoma kompyuta kwa level
gani?!” Akauliza mama mtu sasa. Mina akakunja uso akamgeukia Andy. Hakuwa hata
ameelewa. “Anasomea certificate.”
Akajibu Andy. Nakuzua ukimya mkubwa, mpaka Mina akashangaa. “Na mimi nataka
kusomea kompyuta. Nilimwambia dad.” Mtoto mdogo wa Paulina akadakia.
“Kwa nini usomee certificate na sio degree?”
Akauliza tena mama Ruhinda. Mina akamwangalia Andy. “Kwani hilo ni swali gumu
huwezi kujibu mpaka Andy ndio akujibie?” Mama Ruhinda akauliza kwa
ukali.Wengine kimya.
“Nimeanzia hapo, ndipo Ron aliponitafutia. Mwanzoni
nilitaka kusomea sekretari. Ndio..” Wakamsikia Paul anaanza kucheka taratibu.
Mina akamwangalia kama haelewi, kisha akaendelea.
“Lakini kwenye chuo hicho hicho kukawa na mambo ya
kompyuta. Ndio nikamwambia Ron, nataka kusomea kompyuta. Ndio Ron akanilipia.
Nikaanza kusoma kompyuta.” “Hiyo sio kusomea kompyuta. Unajifunza kutengeneza website kitu ambacho yeyote anaweza kufanya.” “Mama please!” Andy akalalamika.
“Nini Andy? Namueleza maana anaonekana hata haelewi ni
nini anataka! Ameanza sekretari, amekuja kwenye kutengeneza website! Huhitaji kwenda shule kujifunza kutengeneza website. Ukiwa na kompyuta tu na Internet hata nyumbani kwako
unajifunza.” “Kumbe!” Akashangaa Mina bila hila.
“Kwanza shule
ya form six ulimaliza wapi?” Akauliza tena mama Ruhinda. “Niliishia kidato cha
nne.” Paul akashindwa kuvumilia, akacheka kwa sauti. Mina akashangaa.
“Bwana jumapili ya leo nzuri sana. Karibu Mina kwenye familia.” “Asante.” Mina
akamshukuru Paul aliyekuwa akicheka kishabiki, lakini alishukuru akiwa
hajaelewa vizuri. Ila hakutaka matatizo kama kawaida yake, akajiambia
atamuuliza Andy baadaye. Lakini Paul
akazidi kucheka na kuzidi kumchanganya Mina.
“Kwani nimekosea!?” Ikabidi Mina aulize sasa
lakini akaonekana ameshaingiwa hofu mpaka uso ulionyesha wasiwasi.
Akamwangalia Andy na wengine. “Mimi napenda nywele za Mina. Ndefuuuu! Halafuu
nyingii. Zipo kama zimejiviringa hivi!” Mtoto wa Paulina ambaye ndio mrembo
zaidi akaongeza. “Mimi nampenda mdomo wake. Yupo mzuri kila kitu.” Mtoto mkubwa
wa Pius, Poliny na yeye akaongeza
akionyesha kumkubali sana Mina.
“Basi vile nilivyokwambia baba unipeleke wakaniwekee braces, mama akakataa ujue ningekuwa na meno yaliyojipanga
vizuri kama hayo ya Mina!” Akalalamika mtoto huyohuyo mkubwa wa kwanza, mrembo wa Paulina. “Mina wewe mzuri sana. Mama
amesema nikinenepa kidogo tu, nisiwe kimbaumbau nitapendeza. Labda nitakuwa
kama wewe.” Na mtoto wa Pius yule mdogo, mwalimu wake wa game, Mina, akaongeza. “Asanteni.” Paul akazidi kucheka
mpaka alikuwa anatokwa machozi.
Mama Ruhinda alikuwa amebaki ametoa macho anamwangalia
Andy, Andy anaendelea kula. “Kwa hiyo Mina wewe uliishia kidato cha nne tu?”
Akauliza tena Paulina. “Ndiyo. Lakini sasa hivi nasoma. Nimeshachukua na fomu
za IFM, Andy alinisindikiza. Nitaanza mwenzi wa 9 chuo kikianza.” Akajibu Mina
taratibu. “Na mimi nataka kusoma IFM, mama, kama Mina.” Mtoto mdogo wa Pius
akamwambia Raza mama yake nakumfanya Paul azidi kucheka.
“Ni mpaka uwe na cheti ndio wanakupokea. Kazana baby.” “Wala sidhani kama wana vigezo vigumu huko IFM.
Mina si huyo ameishia kidato cha nne na yeye anaenda kusoma!” Akaongeza
mama Ruhinda kwa dharau.
Mina akaanza kukosa raha. “Kula Mina.” Andy akaongea
taratibu. “Kula.” Akaongeza Andy kwa kumbembeleza. “Sikutegemea Andy!” Akaanza
tena mama Ruhinda. Andy akaweka kisu na uma chini na kumwangalia mama yake.
“Mimi nashauri tumalize kula, mama.” Akasihi mzee Ruhinda taratibu.
“Kwa hiyo wewe unaona hivyo alivyokwenda kuokota
hicho kitoto, kisicho na mbele wala nyuma ndio
sawa?” Ugomvi akaununua
mzee Ruhinda. Lakini kila mtu alijua hasira itamwishia yeye tu. Na yeye
alifanya makusudi ili kumsitiri Mina pale mezani. Alishamuona amekosa
raha.
“Ndiye tuliyeletewa mama! Mpe nafasi. Leo ndio siku ya
kwanza kumuona. Mpe nafasi.” “Mtoto huyo
anafanya naye nini? Ni project ambayo hatakaa akaimaliza! Amsafishe
mpaka atakate. Haya, amsomeshe yeye na watoto atakao zaa! Atakuja
kujenga kweli!” Mina aliumia sana.
“Kwa nini kwenda kujitwika mizigo mizito
wakati wapo mabinti wazuri ambao hana hata haja yakuwahudumia? Anatafuta
nini!?” Mina akamvuta Andy, Andy akampa sikio. Akaweka mkono, Mina
akamnong’oneza. “Nyumbani kwenu wabaya Andy! Sio
watu wazuri.” Akamwambia Andy masikioni huku akitokwa machozi.
“Samahani Mina.” Andy akanong’ona lakini sio sikioni,
akimtizama usoni na kumfuta machozi. Mina akaweka kila kitu mezani. “Mimi naenda kula kwa mama Ron!” Akaongea Mina
huku akisimama nakufuta machozi.
“Ungekula kwanza Mina. Kaa ule mama.” Akamsihi Mzee
Ruhinda taratibu. “Mimi naenda kwa mama Ron! Mama
Ron ukila hawezi kukwambia maneno mabaya. Hata kama umekosea, mama Ron
anasubiri mpaka ule ndio anakwambia. Nyinyi kwenu ni wabaya.” Akaongea
Mina akilia. Hapo anamjibu mzee Ruhinda.
“Mnadharau watu.” Akaongeza Mina palepale mbele yao. “Kwetu hatudharau mtu yeyote yule. Mama na Ron
walimkaribisha Andy, wakamuonyesha heshima na kumkarimu.”
Mina akaongea kwa upole huku akilia. “Andy hajaniokota,
amenikuta nasoma. Hata kama sio kitu cha maana ninachosomea, ila mama na
Ron wameniambia najitahidi. Na ninapata zote 100! Mimi, mama yangu na
Ron wananitunza vizuri tu. Wala sijawahi kumuomba mtu hela hata
siku moja. Ron na mama ndio wananisomesha, wananinunulia kila kitu, wala
sio Andy. Andy nampenda tu.” Mina akaendelea.
“Hata kama sisi hatufanani na
nyinyi, lakini sisi hatuwaambii watu maneno mabaya! Na kila mtu akija
kwetu tunampokea vile alivyo. Tunamkarimu na kumwambia maneno mazuri na
ya heshima. Muulizeni Andy. Nyinyi ni wabaya,
mnadharau watu. Na Mungu hapendi na amewasikia maneno yenu yote mabaya
mliyosema juu yangu.” Kulikuwa kimya hapo wote ni kama hawakutegemea afanye hivyo.
Kila mtu akimtizama Mina akiongea na kulia tena bila hofu mbele yao.
Andy akasimama na yeye. “Twende Mina.” Andy akamshika
mkono na kumvuta pembeni. “Mimi naenda zangu kwa
mama Ron! Wewe malizia kula na ndugu zako. Usiondoke kwenu,
ila mimi naondoka. Kwenu ni wabaya, Andy. Hawapendi wageni
na wanadharau watu. Ningejua kama hawafanani na wewe, mimi
nisingekuja.” Mina akaendelea kuongea taratibu huku akilia, wote
wakiwasikiliza.
“Twende nikusindikize nyumbani.” “Hapana Andy. Wewe baki tu. Nitachukua usafiri hapo nje.
Nikifika kule karibu na nyumbani, nitamwambia Ron aje anichukue. Wewe malizia
siku yako na ndugu zako. Ila mimi naondoka.” Wakasikia mlango
unafunguliwa, ukafungwa. Kimya.
~~~~~~~~~~~~~~
Kishaumana Ukweni!
Wakiwa bado hawajaweka msingi
wa kueleweka, matofali ya ndugu yameanza
kuyumbisha penzi, hayajengeki!
Love At
first Sight!
Inakuaje hapo?
Inaendelea…
0 Comments:
Post a Comment