Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Love At First Sight. - Naomi Simulizi

Love At First Sight.

SIMULIZI hii imejaa Visa na Mikasa ya Familia, na jamii kwa ujumla. Inagusa jamii kwa maisha ya kila siku. Malezi ya watoto. Vile matarajio MAKUBWA ya wazazi kwa vijana wao Yanampokutana na UHALISIA WA MAISHA. Ukweli juu ya penzi la kweli lisivyoangalia ELIMU, SURA, MAZINGIRA ILA HISIA za NDANI KABISA.
Walio BAHATIKA kupata hizo HISIA kwa mtu, na Kufanikiwa kuwapata hao watu na kuweza kuwa PAMOJA ni wachache, na watasimulia haikuwa rahisi. IPO garama ya kulipa kwa kuwa vikwazo ni vingi. UNAWEZA bahatika MTU, ila uchumi au ELIMU ikapungua. WAZAZI NAO WANAKUJA NA MATARAJIO YAO. JAMII NAYO INAKUWA NA MTIZAMO WAKE.
BADO NYINYI WENYEWE WAWILI KUWEZA KUISHI PAMOJA KAMA BINADAMU na haiba zenu tofauti tofauti MBALI NA HISIA ZA MAPENZI.
Katika SIMULIZI hii utakutana na Andy, kijana aliyetoka kwenye familia ya kisasa, na mazingira ya hali ya juu, anakutana na Mina, aliyelelewa na Single mama, anayepambana na maisha kukuza watoto wake wawili kwa hali ya kawaida sana, na mshahara wa ualimu tu. Kwa haraka sana, Mina haendani kabisa na alikotoka Andy, lakini ndiye Andy amependa akiweka mbali matakwa ya wazazi. Ni nini kitatokea kwa wawili hao na mazingira yapo kinyume nao, historia za nyuma pia zipo mbele yao.
Pia utakutana na Mill kijana aliyechagua kuishi nchini Marekani, akitamani kuoa nyumbani ila kila wakati alijikuta akiangukia kwa wanawake matapeli mpaka kuja kukutana na Pam  aliyebeba VIGEZO vyake vyote. Pam ni mkazi wa nchini Tanzania, Mill yupo nchini Marekani na ndoto kubwa sana za Maisha.
Lakini kwa mara ya kwanza, Mill anakutana na mrembo wa ndoto zake, udhaifu wake wote, tiba ni Pam, mrembo anayegombaniwa na wengi, lakini anahistoria Ngumu, yakusikitisha inayomfanya kuona mwanamme kama shetani. itakuaje?
FUATILIA SIMULIZI HII.

Love At First Sight.

Kwamba unamuona tu, moyo, Roho na nafsi, vinakushuhudia ndiye. Huwezi kula wala kunywa, mawazo yapo kwake tu. unaamini kwenye

Love At First Sight?

KARIBU KUWA NA MIMI KWENYE SIMULIZI HII.

 

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment