![]() |
Kwanza wanao oa wenyewe walikuwa na wadhifa wa juu huko
kazini, pili walikuwa vijana wa mchungaji wa kanisa la watu wenye pesa zao
wanao mpenda na kumuheshimu sana huyo mchungaji. Wakaweka juhudi kumfanikishia
harusi ya vijana wake.
Japokuwa mchungaji alitangaza itakuwa ni harusi isiyozidi
dakika 45, yaani ibada nzima, kuanzia mwanzo maharusi hao wawili Jelini na
Emelda wakiingia, mpaka mwisho wakitoka kama mume na mke, lakini, kanisa
lenyewe lilipambwa kwa unadhifu na garama kubwa sana, utafikiri
ni harusi itakayofungwa kwa juma zima!
Ukumbi wenyewe walikodi kutokana na wageni wao, kwa hiyo
nao ulichukua pesa ya kutosha kwani kulipangiliwa kwa muundo wa harusi mbili.
Jukwaa au sehemu yao wanne hao, ilibeba thamani kubwa sana. Kila mwenye
macho na kujua tukio hilo, walitaka kuhudhuria.
Junior na Ezra walivaa suti nzuri sana, zinazofanana kila
kitu pamoja na pete zao. Emelda na Jelini nao walivaa kila kitu kinachofanana
mpaka pete zao zote. Za uchumba na hizo walizotegemea kuvalishwa siku hiyo pia
zilifanana.
~~~~~~~~~~~~~~~
Mchungaji alishakuwa amesimama mbele na vijana wake,
pamoja na wasimamizi wa kiume pamoja na wakike wanne kila upande wakisubiria
bibi harusi hao waanze kuingia, wakitaka kujua wanaingia kwa staili gani.
Kinanda kilipoanza kupigwa, watu wote wakasimama
wakitaka kushuhudia. Wakaanza kuingia watoto wakike wawili. Wazuri wakuvutia.
Wametengenezwa kwa nadhifu mno. Wote walishika vimto vyeupe, vilivyozungushiwa
na rembo za rangi ya dhahabu iliyozidi kupendezesha hivyo vimto vilivyokuwa na muundo
wa moyo. Vilibeba pete. Waliingia vizuri, kwa ustadi, wakavutia macho.
Kisha wakafuata vijana wawili, wakiume, safi, wakawa
wanavuta kapeti jekundu, kuanzia mlangoni mpaka juu kabisa madhabahuni
alipokuwa amesimama mchungaji. Likatanda na kuenea kwenye hiyo njia katikati ya
viti. Kisha wakaingia watoto wawili, wakike na wa kiume, wakimwaga maua juu ya
hilo kapeti mpaka juu madhabahuni.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Ndipo Mungu anayetengeneza njia pasipo njia. Mungu
anayejibu kwa moto. Yule anayefanya mambo ya ajabu ambayo hakuna
mwanadamu anaweza hata kuyafikiria. Ampaye amtakaye, na hakuna wa
kumuuliza kwa nini! Akamtoa mwanamke aliyekuwa akichekwa na kuzomewa
kijijini, akichechemea kwa maumivu ya kipigo cha kudharaulika,
manyanyaso na mumewe. Mwanamke aliyekuwa akilala topeni. Njaa ni sehemu
ya maisha yake. Hata lugha ya kiswahili hakuwa akiizungumza sawasawa.
Siku hiyo akaingia kwenye majibu ya muujiza
uliokuwa ukiombwa kwa kufungwa na maombi si ya siku moja! Ni tokea vijana hao
wapo shule ya sekondari walikuwa wakimsihi Mungu kwa ajili ya siku hiyo.
Watu wakiwa wanashuhudia maajabu hayo. Pesa iliyomwagwa
kwa ajili ya harusi hiyo, kumbe ni majibu ya maombi yaliyoombwa, na kuishi
maisha ya kujikana kwenye tamaa za ujanani. Siku hiyo Ezra na Junior,
Mungu wao akiwaheshimisha hadharani, basi na mama Emelda naye
akawa mmoja wao. Mungu alimkumbuka mama huyo aliyekuwa akilea hao watoto
kwa kilimo, huku ni mgonjwa.
Mwanae naye akaenda kuweka hazina ya kumdai Mungu
kwenye nyumba ya mchungaji kwa kutumika bila kuchoka wala kiburi.
Baraka alizokuwa amebeba huyo binti hapo, kutoka kwenye kinywa cha
mchungaji na mkewe, ziliwaka usoni mwake kama taji aliyokuwa amevaa, na shela
ya thamani. Nyeupee kama theluji iliyokuwa imetupiwa vimawe vya kung’aa kama
alumasi. Wakati akiingia na mama yake amemshika mkono, ungejua ni Mungu
mwenyewe, wala si kazi ya mwanadamu aliye waheshimisha.
Ungedhania mama Emelda, ni mama wa mjini. Mama mchungaji
alimuosha na yeye akaosheka. Alivaa kwa thamani, akavutia na binti yake
ambaye naye, alijitunza, akikana shida zake na tamaa za mwili za
ujanani mpaka siku hiyo Mungu akimuheshimisha kwa kumpa Junior.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Junior akaanza kusugua mikono kwa shauku kadiri Emelda
alivyokuwa akiwasogelea, mpaka mchungaji na Ezra wakacheka. Alivutia Emelda
kama tausi! Watu walikuwa wakishangaa wasijue aina hiyo ya shela aliitolea wapi
huyo Emelda, msichana wa kazi za ndani, asiye na elimu kubwa kichwani,
aliyekuwa akitumika upande wa watoto muda wote hapo kanisani wala haonani na
washirika wengi useme aliona staili fulani fulani.
Ilikuwa ya kipekee na tofauti sana. Alivuta taratibu
gauni lake lenye mkia mrefu, uliotengenezwa kwa unadhifu wa hali ya juu, akiwa
amefunikwa na shela ambayo nayo ilining’inia mpaka kuanguka nyuma kwa chini
kabisa. Kwa hakika aliwaka.
Mchungaji aliwapokea walipofika pale mbele. Junior naye
akawa pembeni ya baba yake. Mchungaji akauliza, “nani anamtoa binti huyu,
Emelda, kuwa mke wa Junior?” Mama Emelda akajibu, “Ni mimi.” Kukazuka shangwe
hapo. Vigelele. Vijana wakaanza kuimba na kucheza wakati mchungaji akimalizia
maneno yake katikati ya Junior, mama Emelda na Emelda.
Junior akamshika kama alivyokuwa ameshikwa na mama yake,
akasogea na Emelda wake pembeni, Ezra akisaidia kutengeneza shela na mkia wa
gauni. Waliposimama pembeni, Ezra akapanga shela vizuri na hilo gauni.
Junior akamgeukia. “Nina hamu na wewe Emelda!” Akamsikia
akimnong’oneza kwa kulalamika. Zilishapita siku 5, hawajaonana. Akamgeukia akiwa
bado amefunikwa shela. “Na mimi nimekumiss Junior. Leo tutakuwa wote.”
“Nilikuwa nakusubiria kwa hamu!” Emelda akacheka na kuongeza. “Umependeza sana!”
“Nafanya kwa ajili yako mpenzi. Wewe umependeza zaidi.” “Asante. Na asante kwa
kila kitu.” Wakaendelea kuzungumza wawili hao wengine wakishangilia.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Ukasikika tena mlio uleule alioingia nao Emelda. Kanisa
zima wakanyamaza na kugeukia mlangoni kwa haraka wakijua ni Jelini tu. Swali ni
je, kama Emelda amependeza hivyo, huyo Jelini mtoto wa mjini, na anayejipenda
hivyo, je?!
Wakaona watoto wengine wawili tena, wanaingia wakimwaga
maua juu ya hilo kapeti vilevile kama wa mwanzo. Ikawa kama wanaoongezea maua
juu yake. Hawakupunja. Yalimwagwa vizuri na kuenea kwenye hilo kapeti jembamba
lakutoshea watu wawili kupita kwa wakati mmoja. Zito na zuri ambalo haliwezi
kujikunja kwa urahisi.
Ndipo na mama Jema naye, kwa mara ya pili, akapata
heshima ya kumsindikiza mwanae kwenye safari ya ndoa. Jelini hakuwa na tofauti
na Emelda. Kila kitu kilifanana. Kuanzia juu mpaka chini. Kwa hakika na yeye
alipendeza.
Chachu ndogo, huchachua donge zima.
Ikawa mabadiliko ya mtoto mmoja tu ndani ya nyumba hiyo
ya kipagani. Waliokuwa hawamuabudu Mungu wala hawana ugomvi na shetani.
Maisha yao yanakwenda kwa kadiri mama yao anavyoongoza. Jema alipompa
Yesu maisha, haikuwa kazi rahisi. Kukataliwa na kupingwa kwa hali
ya juu. Lakini Jema alikutana na Mungu wa kweli. Alionja uhuru na furaha
ya wokovu wa kweli.
Akasimamia imani kwa shida. Kutoka kwenye familia
iliyokuwa haimjui Mungu wala kuamini kwa mwanamke kuolewa! Yaani kuwa
chini ya mwanamke! Yeye Jema akamlilia Mungu wake nyuma ya pazia. Huku
akisimama na huyo Jelini, tokea anashinda baa. Akimtunza bila kuchoka huku akimuombea,
mpaka hapo mama yake anavuna matunda.
Chachu ndogo ya Jema, ikachachua donge zima kwenye
familia yake. Je, wewe, unaleta mabadiliko gani kwenye familia yako?
~~~~~~~~~~~~~~~
Jelini akawa si majibu tu ya Jema, naye akaingia
kwenye majibu ya Mungu ajibuye kwa moto. Muujiza wa Ezra. Mungu ampaye
amtakaye. Jelini aliyekuwa akibakwa mchana na usiku huku akiteswa na
mwalimu wake. Aliyepita kwingi kwenye mahusiano ya wanaume! Kina Kasa!
Jelini mshinda baa! Mlevi mchana na usiku! Mwenye mtoto tayari!
Eti Mungu huyohuo anayeyajua yote hayo, asimpe Ezra mwanamke bikra, akamkabidhi
Jelini.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Jelini aliyejua anachokitaka tokea zamani, japo jamii
ilijua anaomba au kutamani kisichowezekana, wake wa peke yake!
Nani ajuaye Mungu ana watu wengi? Kwa sababu umezungukwa na
waovu, HAIMAANISHI Mungu hajajisazia
watu waamini kama kina Ezra.
Vijana waliofanikiwa kwenye maisha katika kila eneo. Wakajitunza.
Na kubakiwa na hofu ya Mungu. Mungu hajaishiwa. Bado kina Joshua,
Junior na kina Ezra wapo katika ulimwengu huu huu wa wanaume waliokosa
uaminifu.
Kama Jelini angekata tamaa. Na kusikiliza wengi, pengine
asingeishia na Ezra siku hiyo akiwa anasubiriwa na ndoa yenye msingi imara,
Yesu kristo. Haimaanishi hawatapitia majaribu kama wanandoa wengine! Hapana.
Lakini msingi wao utabaki imara.
Na ili kumpata Ezra, na kile alichokiamini, Jelini
ALIBADILI maisha
yake kabisa. Alirudi kanisani. Akawa kama wao. Kufunga na kuomba, na
kuhakikisha yupo nao kanisani kila inapolazimu. Si kazi rahisi kukana nafsi na
kufuata njia nyembamba inayosonga, njia ya uzima, haswa ukiwa
umeshaishi maisha ya kujirusha kama Jelini. Kutoka kukesha klabu mpaka kukesha
kanisani!
Akikana hisia nzito za penzi la mwanzo kabisa, penzi
la Colins aliyerudi na kumkuta alishatoa ‘ndiyo’ yake kwa Ezra. Yote
hayo alifanya akiwa ameshajua anachohitaji, akapata na watu waliosimama naye
kumkumbusha ni nini bora na nini alitaka, kina Jema, mpaka siku hiyo Mungu
alipo mzawadia na yeye.
~~~~~~~~~~~~~~~
Furaha ilizidi kuongezeka kwa kadiri alipokuwa
akimsogelea Ezra. Kulijaa shangwe na vigelegele, lakini wawili hao walibaki wakiangaliana
wao tu. Alijawa checko ndani ya shela yake ungeweza liona. Macho kwa Ezra.
Akashindwa kuvumilia, akampungia mkono taratibu akitumia
mkono wa kulia ambao hakuwa ameshikwa na mama yake. Ezra naye akajikuta
akimpungia mkono. “Nakupenda Jelini.” Akajikuta akisema. Jelini akazidi kucheka
ila aliweza kumuelewa, alisoma midomo yake. “Na mimi nakupenda Ezra.”
Akarudisha wakiendelea kusogea mpaka walipowafikia pale juu madhabahuni.
~~~~~~~~~~~~~~~
Hapo napo mchungaji akamuuliza mama Jema kama alivyo muuliza
mama Emelda. Alipojibu na Ezra kupokea ule mkono, tayari Junior alishafika hapo
nyuma ya Jelini kumsaidia mkia wa gauni. Kukawekwa mazira ya kuwa na nafasi ya
kutosha hapo katikati. Jelini akiwa ameshikwa na Ezra, Junior akisaidia kubeba
gauni la Jelini asijikwae au kuanguka huku wakisogea mpaka pale alipokuwa
amesimama Emelda.
Wake zao katikati, wao pembeni yao. Akamchungulia
Emelda, na kumfinya kidogo. Uchokozi mpaka kanisani! “Jelini!” Emelda
akamgeukia akicheka. “Tulia bwana!” “Upo serious sana bwana.” Wakaanza
kuongea wakati walishinda wote saluni wakipambwa. Wameachana kwenye limousine
hapo nje ya kanisa. Cheko limemjaa.
“Umemuona Junior lakini?” “Kapendeza sana mpenzi wangu.”
“Kama Ezra.” Jelini akadakia kwa haraka. Wakacheka, Junior na Ezra
wakawachungulia pale katikati. “Tupo kanisani Jelini!” “Ni mkeo huyo ndio
ameanza, sio mimi.” “Jelini!” Akashangaa Emelda, wote wakacheka wakijua ni
Jelini tu asiyeweza kutulia wala kunyamaza.
Watu wakiendelea kushangilia, wanne hao mbele ya
mchungaji walikuwa na yao mpaka aliposikika mchungaji akisema, “Amen, Amen.”
~~~~~~~~~~~~~~~
“Hii ibada ni ya kuwaombea baraka hawa wanne. Kama yupo
mwenye kizuizi, aseme sasa lasivyo asisema daima. Maana atakacho kiunganisha
Mungu hii leo, mwanadamu yeyote, hata hawa wanne wenyewe, asikitenganishe.”
Shangwe na vigelegele wakijua ndio ibada imeshaanza hivyo. Akaomba ukimya wa
dakika tatu, kuwapa nafasi watu wenye kipingamizi.
Kimya mpaka muda ulipoisha. “Kwa ukimya huu, inamaana
nina kibali cha Mungu na serikali kufungisha ndoa hizi.” Vigelegele. Kelele na
shangwe.
Kama waliokuwa wamejipanga, bila kuambiwa. Kila mmoja
akamgeukia mwenza wake na kushikana mikono baada ya mabwana harusi hao kusaidia
maharusi hao kutengeneza shela zao. Wao ndio wakawa waoaji na haohao nao
wakawa wasimamizi wa wake zao.
Watu wakazidi kuvutiwa na jinsi wanavyofanya kwa ustadi.
Mchungaji akashuka kutoka mimbarini na kuwasogelea.
“Ezra!” Wakamsikia mchungaji akimuita Ezra. Akajua ni
nafasi yake. Akashuka kiapo chake mbele ya kanisa, akiwa anamwapia
Jelini. Alitengeneza kiapo kizuri sana. Kwa hakika kilivutia. Watu
walishangilia sana.
“Junior!” Mchungaji akasikika akimuita Junior,
wakashangaa sio Jelini. Junior akaanza kwa kusema, “Emelda!” Akarudia kiapo
kama cha Ezra. Neno kwa neno mpaka wanawake zao wakashangazwa. Kama waliokuwa
wamekiandika pamoja na kukikariri. Watu walishangilia sana. Ndipo akaja
Jelini, kisha Emelda. Wawili hao hawakuwa wamejipanga kwa pamoja.
Kila mmoja alitoa chake. Emelda yeye alisema kwa kifupi
tu. “Nakupenda Junior. Nakupenda kwa moyo wangu wote, mpaka kifo
changu.” Junior akamnyanyua mkono wa kushoto uliokuwa wakulia kwake, na kumbusu
kiganjani akimwangalia, mwenzie akaendelea. “Nakuahidi kusimama na wewe
katika kila hali. Nitakuombea bila kuchoka. Nakuhidi kuwa mwaminifu
kwako kama kwa Mungu wangu. Na Mungu anisaidie.” Watu walishangilia sana
wakati sauti nzuri na tulivu ya Emelda ikimalizia.
Ndipo akamalizia Jelini. Kanisa zima kimya. “Ezra wewe ni
majibu ya maombi yangu ambayo kila mtu aliniambia naomba kitu kisichowezekana.
Umekua mwaminifu kwangu. Unanijali na kunipenda kwa dhati.
Umeyabadili
maisha yangu kwa kusimama na mimi bila kunikatia tamaa, kuhakikisha nakuwa
mwanamke niliyeweza kukaa kanisani na kuweza kumuomba Mungu peke yangu.” “Usilie sasa.” Ezra akasikika akimtuliza kwa upendo.
“Basi hapo ataharibu vipodozi vyote!” Akasikika Junior na
kufanya watu wacheke kidogo. “Mimi sasahivi sijali.” Jelini akajibu na kuendelea akisikika akitokwa na
machozi. “Umenitoa mbali Ezra, tena bila kunichoka wala kunikatia tamaa.
Umenivumilia ukionyesha uthamani wangu hata wakati mwingine kwa wengine
ilipokuwa haileti maana.”
“Nakupenda Jelini.” Ezra akamjibu na kumfuta kabisa machozi.
“Na mimi nakupenda Ezra. Nakupenda sana mpenzi
wangu. Nakuahidi kuwa mke mwema kwako. Nitakuwa mwaminifu kwako. Kamwe sitakusaliti.
Nitakuwa rafiki mzuri zaidi ya Junior!” “Jelini!” Akasikika Junior akihamaki, wote
wakacheka mpaka Jelini mwenyewe.
Kisha akaendelea. “Katika magonjwa, shida, huzuni, jua Jelini
wako atakuwa na wewe. Hata ukifukuzwa kazi, ujue mimi…” Junior akawa wa kwanza
kucheka. “Jelini!” Junior akasikika. Watu wote wakazidi kucheka. “Kweli! Hata
kama Ezra wangu akiishiwa kila kitu, ajue amejiwekea hazina yake kwangu.” Watu
wakazidi kushangilia.
“Nitakutunza Ezra wangu. Nitakupenda. Nitakuheshimu.
Nitasimama na wewe katika kila hali na kila kitu. Nitawaunga mkono wewe na
Junior katika maamuzi yenu, sababu nyinyi wawili ni wa kuaminika.” Watu
wakashangilia sana, mpaka Junior na Ezra wakapiga makofi.
“Watoto wa Emelda na Junior watakuwa wetu pia. Katika
shida na raha, nitaombea ndoa yetu na ya kina Emelda pia, pamoja na watoto wetu
Mungu atakao tujalia, akiwepo na Jeremy, na Mungu anisaidie.” Jelini
akahitimisha watu wakishangilia mpaka kushindwa kukaa. Kulikuwa na miluzi humo
kanisani. Shangwe za aina yake. Mtoa kiapo mwenyewe ni mrembo Jelini! Mungu
ampe nini Ezra! Kichwa kikazidi kuwa kikubwa akimshukuru Mungu wake.
Mwishoe akasikika mchungaji. “Mungu wa mbinguni awaabariki nyinyi na watoto wenu.
Mkono wake usiondoke juu yenu na watoto wenu.” Wanne
hao waliposikia tu hivyo, wote kama walioambizana, wakapiga magoti kwa haraka
mikono juu. Mzee alitamka baraka hapo, wakajua ndio ibada inahitimishwa.
Kimya kikatanda kanisa zima, kila mtu akanyoosha mkono kwa maharusi hao
waliokuwa wote wanne wamepiga magoti.
Mchungaji alitoa baraka utafikiri hatakuja bariki tena!
Aliombea safari yao nzima, ndipo akamaliza na “Ameni”. Watu wote wakaitika. Ndipo maharusi wakasimama.
“Sasa mmekua mke na mume, ruksa.” Wakageukiana na kiss
zikaanza hapo mbele ya watu wakishangilia sana. Ikawa ya stara, watoto
wa mchungaji hawakufanya mengi. Maandalizi yalikuwa nyuma ya pazia.
~~~~~~~~~~~~~~~
Wakati Jelini anatoa viapo siku hiyo, ndio ilikuwa maandalizi
ya kumrudisha Kamila alikolelewa. Kina Komba kujitambulisha huko kwa masista,
na kusema lengo la kutaka kumuoa huyo Kamila. Mzee Komba aliona afanye hivyo
kuliko kuolewa kimyakimya. Kwamba baada ya hapo na taratibu za huko kwa masista
kukamilika ndio vikao vya harusi vianze na Colins naye apate mke.
~~~~~~~~~~~~~~~
“Junior na Ezra, kabla hamjatuacha kwa mwezi mzima naombeni
wimbo mmoja kwa ajili ya kumshukuru Mungu kukamilisha hii safari.”
Akasikika mchungaji na kufanya wanao wajua hao kwa uwimbaji, kushangilia sana.
“Jamani, kuona wamesimama hapa mbele yenu hivi,
hawa wawili na hiki walichokifanya hapa, na hawa wake zao hawa, hakika
haikuwa kazi rahisi hata kidogo. Huu ni ushuhuda naona mama yao ndio
atakuja kushuhudia siku nyingine, maana hawa wawili wanaweza wasieleze ukweli
wote.” Junior na Ezra wakacheka kwa masikitiko.
“Kwani ni uongo? Mtafunga hata tatu kavu. Mnajinyima nao.
Mnamlilia Mungu. Akijibiwa mmoja ujue hayo maombi bado
hayajajibiwa wala hawatafurahia. Unabakia na kazi ya kubembeleza na kuwaambia, tushukuru
kwa kila jambo! Napo wala havisaidii. Unalaumiwa weweee, utafikiri
wewe ni Mungu! Bora mje hapa mnisaidie kumshukuru Mungu wangu. Maana katika hili,
hana deni. Au mnasemaje? Si wake wazuri hawa?” Wakawaachia wake zao watu
wakishangilia haswa.
Junior akashika kipaza sauti na kwenda kukaa kwenye
kinanda. Mchungaji mwenyewe akachukua gitaa la bezi. Ezra akachukua
gitaa la kawaida, kiziwanda wa mchungaji, Noah, kwenye ngoma. Zilikuwa shangwe,
kelele, hawakutegemea.
“Acha tuwafaidi kwa mara ya mwisho kabla kawajaondoka
hapa kanisani. Nishajua nitakuwa na ibada nne, bila wao. Acha watuage.
Na nimewashitukiza makusudi wajue japokuwa wameoa, bado ni watumishi.
Jumapili ya tano kuanzia sasa, watahitajika hapa kanisani na wake zao,
asubuhi na mapema kabla wengine hawajafika hapa.” Akasikika mchungaji na
kufanya watu washangilie zaidi. Tayari wakajua wanne hao wana fungate la
mwezi mzima.
“Wao na wake zao, bila kukosa. Si ndicho wake zao walicho
tuahidi hapa?” “Ndiyoooo!” Wakazidi kushangilia. Jelini na Emelda wakazidi
kucheka.
“Sasa tuone vitendo. Utumishi wa waume zenu, ni wenu.”
Akaongeza mchungaji na kuanza kupiga gitaa watu wakishangilia. Kwa hakika ilipendeza
mno. Junior aliimba vizuri, akisindikizwa na vyombo vya mziki kana kwamba walikuwa
wamejipanga kutoa hiyo sadaka ya sifa kwa Mungu, kumbe walishitukizwa tu, akili
ilishakuwa fungate.
Watu walicheza mpaka kuvua viatu. Ibada ikageuka kuwa ya
sifa, hata wafanyakazi wenzao wengine wasio kwenda kanisani, siku hiyo
walijikuta kanisani wakimsifu Mungu na wao. Ikapendeza sana.
Fungate.
Waliposikia alichokifanya Kumu siku ya kwanza ya ndoa yao,
wakakusudia kuiga. Baada ya watu kula na kunywa ukumbini, wanne hao
wakaagwa rasmi kama mke na mume. Wakakimbilia kwenye limousine, kila
mmoja na wake, kissing za nguvu zisizoisha mpaka wakashushwa majumbani
kwao.
Zikaendelea kissing mara tu walipoingia ndani.
Nyumba yenyewe iliandaliwa vilivyo. Maua yalimwagwa kuanzia mlangoni mpaka
chumbani.
Sasa huku kwa kina Jelini, wao mambo yao yakaendelea. Jelini kashazoea
mchezo na alishakusudia kumfurahisha Ezra vilivyo. Mzoefu. Siku ya mwisho Ezra
alipokwenda nyumbani kwao kutengeneza, waliachana kwenye gari kwa ahadi ya kuweka
kumbukumbu kwenye usiku wao wa kwanza. Na walipokuwa ukumbini Ezra
alimnong’oneza akimdai. Jelini akamjibu yupo tayari kumlipa. Hapo hapakuwa na
maneno, vitendo tu.
Shela ilishatolewa tokea hawajapandisha ngazi. Hapo
Jelini alikuwa na chupi tu na sidiria. Walipofika tu juu, akamshusha suruali
akiwa amesimama katikati ya chumba, kwa mara ya kwanza Ezra akapata midomo
ya mwanamke. Ni vile alijikaza kiume, asitie aibu, lakini Jelini mwenyewe
alijua anampa raha kwa ute uliokuwa akimtoka.
Alimnyonya huku akimchezea kokwa vilivyo. Sasa na yeye
Ezra alikuwa na uchu wa kumtizama Jelini. Yale aliyokuwa akiyaona kwa
nje, basi ayashuhudie kwa macho. Mchungaji alishatoa ruhusa. Jelini alipokuwa
anapumzika mdomo akimchua kwa mikono akiwa amepiga magoti mbele yake,
akamnyanyua na kuanza kiss huku akimmalizia kumvua chupi na sidiria na
kumuweka kitandani.
Akawa akimwangalia
huku akimalizia kujivua nguo kwa haraka maana jamaa alichomolewa tu na kuanza
kunyonywa. Jelini hakujiachia hovyo hapo kitandani, akajipanga vizuri. Biashara
matangazo. Akaupanga mwili wake, kuvutia zaidi. “Jelini wewe ni mzuri!”
Akafurahi huyo Jelini, “Na wewe nimekukubali.” Maana mzee wa haja alikuwa
hewani. Akajirusha kitandani, safari yao ya mapenzi ikaanzia hapo.
~~~~~~~~~~~~~~~
Sasa huku kwa mabikra wawili romance iliendelea
Junior akijua Emelda hajawahi kufanya mapenzi kama yeye tu. Kwa hiyo lazima
amtayarishe. Akafanya utundu wote waliojipanga na Ezra mpaka Emelda, na
kuongezewa kwenye bag party. Akafanikiwa bao la kwanza, kabla hajampa la
pili, Junior mwenyewe akalemewa, ashasubiri tokea anabalehe, na hapo kwa mkewe
napo asubiri! Uzalendo ukamshinda. Akaingia akijua mwenzie yupo tayari.
Anamalizia kupiga bao, Emelda anatokwa damu kama mbuzi
aliyechinjwa. Junior akapaniki. Akambeba mkewe kumkimbiza hospitalini na
kuwapigia simu kina Ezra. Fungate ya nyumbani ikaishia hapo kwa hao wawili.
Jelini na Ezra wao wakaendelea kupeana dozi kama kawaida wakimuuguza Emelda.
Naye Junior kwa hukumu akijilaumu pengine alipiga pupa
mpaka kumuumiza mkewe, akamgeuza mgonjwa wa kulea kitandani. Kila kitu anampelekea
hapohapo, hataki hata atembee asije akajitonesha, damu zikaanza tena. Bafuni,
chooni anambeba. Uzuri Emelda hakuwa na mwili mkubwa kama Jelini, anabebeka
kiurahisi. Emelda deko, pumu imepata mkohozi. Wala hajivungi kudekezwa.
Hapakuwa na kupika. Walikuwa wakiletewa vyakula.
Wakiamka, wanakuta vyakula vimeletwa. Kazi ya mama mchungaji. Kuanzia cha
asubuhi mpaka usiku. Kazi ikabakia kula, starehe, hakuna hata kuosha vyombo.
Baada ya siku tano Emelda alipopona kabisa, ndipo
wakasafiri sasa hao wanne kwenda kuanza fungate rasmi.
Vai&Bale.
Vai na Bale walibarikiwa ndoa nzuri iliyojaa mafanikio
tele ya mali, lakini hapakuwa na mtoto. Walihangaika kupita kiasi kumfanya Vai
kushika mimba lakini haikuwezekana.
Alikuwa akifunga na kuomba bila kuchoka akimsihi Mungu
akumbuke tumbo lake na yeye aje ashike tena mimba. Alitoa sadaka kila
alikoshauriwa, ilimradi tu kugusa moyo wa Mungu bila mafanikio. Hiyo
hali ikaendelea kiasi cha kuanza kupunguza furaha kwenye ndoa yao. Majuto na
kujilaumu kusiko isha. “Pengine Mungu hajanisamehe.” Hilo ndilo
likabakia moyoni kwa Vai.
Wakiwa kwenye hiyo hali, ndipo Bale akakumbushwa moyoni
wazo lake la mwanzoni kabisa, na kujirudi hata kumsaidia Vai mkewe
aliyekuwa amechanganyikiwa na swala la mtoto huku na yeye akimsindikiza kila
mahali bila mafanikio.
“Najua shida ni mtoto. Lakini nataka kujua unataka
kunyonyesha au mtoto?” Vai alikuwa kwenye kilio cha uchungu. “Nataka
mtoto Bale.” Akamdai mumewe kama Raheli kwa Yakobo. {Mwanzo30:1}
“Basi turudie mpango wetu wa mwanzoni. Tunaanza na
mtoto gani?” “Mimi sishiki mimba.” “Zungumza
na mimi, kana kwamba ndio umebahatika kuzungumza na Mungu uso kwa uso. Halafu anakuuliza
jinsia ya mtoto wako wa kwanza, ungemuomba yupi?” “Wakiume
kwanza. Lakini simpangii Mungu.”
Akajibu Vai. “Basi tulia.” Akamtuliza mkewe usiku huo, angalau wakalala.
~~~~~~~~~~~~~~~
Bale akaanza kufanya utafiti kwenye vituo vya watoto
yatima, akaulizia utaratibu wote na kujiridhisha hatamuumiza mkewe, hata
akimwambia kusije tokea kushindikana katikati ya process ya adoption.
Alipojiridhisha kwamba wanaweza pata mtoto kwenye vituo vya watoto yatima,
ndipo akamwambia Vai.
Hakuamini utayari wa Bale. Alikuwa tayari kwa moyo mmoja.
Akampeleka na kuonyeshwa watoto wa pale. Vai akajikuta akipenda kitoto cha
mwaka mmoja cha kiume, ndipo safari yao ya uzazi ikaanzia hapo.
Wakwanza alipokaribia miaka miwili, wakaenda kuchukua
mtoto wa pili. Napo wakapenda wakiume tena. Safari hii Vai akapatwa hamu ya kunyonyesha
kabisa. Wakamchukua kachanga kabisa. Vai akaanza kunyonyesha kama aliyezaa. Wakalea
watoto hao wakiume wawili kwa upendo kana kwamba ni wao wa kuwazaa kabisa. Na
ndugu wa karibu nao waliwapenda hao watoto, na kuacha historia nzuri kwa
walichokifanya.
Nyumba yao ikajawa furaha na fujo zote kama za
familia zenye watoto wadogo. Wakasahau kabisa swala la kuzaa au kutafuta kushika
mimba kwa Vai. Sex nje nje wakati wote wakipata kimwanya. Hakuna uzazi
wa mpango wala kinga, si Vai hashiki mimba! Wakawa wanajiachia.
Akiwa bado ananyonyesha mtoto hajafikisha miezi sita, Vai
akaanza dalili za mimba. Akajua ni homoni tu, zinabadilika sababu ya
kunyonyesha. Akapuuza. Lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, vikazidi. Vai hawezi
kula chochote na ananyonyesha. Hakuna kinapita kooni hata mate yake mwenyewe,
hayaendi.
Akaendelea kupambana na yote. Kazi, watoto wawili,
tena wakiume, huku anakazana kunyonyesha. Siku na hiyo Bale akiwa kazini
akapata simu kutoka kwa msichana wa kazi kuwa, mkewe ameanguka na kuzimia akiwa
anatoka kwenda kazini, mchana. Uzuri Naya alikuwepo tu nyumbani, na ni karibu,
akamuomba akamwangalie.
Naya akampeleka hospitalini kwani alikuwa amekaukiwa
haswa. Baada ya vipimo, akawekewa maji na kupumzishwa Bale naye akawasili.
Kufika na majibu nayo yanatoka, Vai ni mjamzito. “Mwanangu bado mdogo!” Akalalamika Vai akijisau kama alikuwa akitafuta
hiyo mimba kwa muda mrefu wa kuchanganyikiwa. Wakati wa Mungu ukawa si
wakati wake.
~~~~~~~~~~~~~~~
Jelini na Emelda wakaweka na wao uzazi wao wa mpango.
Kuomba Mungu na kushika mimba kwa pamoja na kuzaa kwa pamoja. Kukawa na mapacha
wengine wa nje, kwenye familia hizo, mbali na baba zao.
Wote wakaendelea na ndoa zao, na changamoto za mahusiano
kama wengine.
~~~~~~~~~~~~~~~
MWISHO.
Usipitwe Na
Simulizi Mpya,
Love At
First Sight.
Huko Utajua Kwa Undani
Ø
Kilichompata Mike, Wa Kamila.
Ø
Sababu Ya Wawili Hawa Kushindwa Kupata Mtoto.
Ø
Penzi La Mill Kwa Pam. Mwanzo Wao na jinsi ilivyo rahisi KUBOMOA lakini huchukua muda KUJENGA. Na mengine
mengi ya kuburudisha na kujenga.
§
KARIBU.
0 Comments:
Post a Comment