“Nitakwenda. Si ni kwenu?” “Ndiyo. Na
najua una kazi. Unaweza kuniacha mimi hapa ukanipa majukumu yako nikufanyie
wakati ukienda.” “Daktari mzima unataka kuuza duka la urembo!” “Naona unazidi
kupendeza tu Jelini, inamaana si biashara mbaya!” Jelini akacheka akifikiria.
“Acha niende tu sasahivi kabla ya
jioni watu hawajawa wengi.” Connie alifurahi, na kumshukuru sana Jelini. “Hivi
hapa natangulia kukusubiria nyumbani. Au unataka nikusubiri twende wote
kabisa?” “Hapana. Nitakuja tu, usiwe na wasiwasi. Siwezi danganya.” Connie
akaondoka akiwa na imani.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Akataka kumpigia simu tena Jema,
akasita. Tayari Jema alishapoteza imani kabisa na si Colins tu mwenyewe
aliyekuwa mstari wa mbele kumtetea, ila hata wazazi wake. Baada ya kusikia taarifa ya kuwa anaishi na Love na
anakwenda kazini kama kawaida, maisha yake yanaendelea, alishamtoa kwenye
mahesabu kabisa. Halafu kitendo cha wazazi wake kuja kumtukana mama yake na
Jelini, nyumbani kwao! Bila hatia! Mbele yao tena bila heshima, kilimuuma sana.
Na kwa mama yake moyo
ukasita kabisa. Alishasema ameshachoshwa na mambo ya kina Colins, na
hataki hata kuwasikia tena. Alisema walimdharau vibaya sana na ndio maana
walipata ujasiri wa kwenda kumtusi nyumbani kwake. Na huyo akasita
kumshirikisha. Akaona ampigie tu yeye kwa linalomuhusu. “Nina mgonjwa, naenda kumuona. Nikichelewa naomba unisaidie hapa dukani.
Wasijione wameachwa peke yao.” Mama Jema akaitika kwa haraka bila hata
kufikiria. Jelini akaelewa yupo katikati ya mambo yake, hataki kupoteza muda
kwenye simu. Ila akashukuru Mungu amekubali bila maswali, na anamjua mama yake,
maadamu amekubali, basi atafanya tu.
Akiwa njiani akabaki
akimfikiria wakumtaarifu, akaishia kwa James shemeji yake, rafiki wa kweli wa
Colins. Akamueleza ilivyokuwa. “Nikwambie ukweli
Jelini, mimi nilijua kwa hakika kuna kitu hakipo sawa. Hata iweje, Colins sio
mtu wa kukata mawasiliano gafla! Nijulishe kama kuna kitu kitahitajika
nisaidie.” “Nashukuru shem, lakini eti nilikuwa nikiogopa!” “Wasingekuja wote kutaka msaada wako wakiwa na nia ya
kukuangamiza tena ukiwa uliwaacha kama walivyoomba! Wewe nenda. Baada ya muda
nitakupigia kujua unaendeleaje.” “Hilo litanitoa
hofu. Nashukuru. Ila kwa sasa, usimwambie kwanza Jema. Acha nikajue
kinachoendelea ndipo nitajua chakuwaambia.” “Sawa.” Wakaagana angalau akapata
amani kupata baraka za shem wake.
Alishawauliza hivi, hata hao wazazi
wakija kusema neno, ‘samahani,’ watarudi kuwa na mahusiano ya namna
gani! Akawatoa kabisa kwenye mahesabu, tena wakizungumza kwa kupokezana na mama
yao mbele ya Jelini na James. Jelini alipolikumbuka hilo, akaona amuache
kumuhusisha na mambo ya kina Colins.
Na kwa mama yake moyo ukasita kabisa.
Alishasema ameshachoshwa na mambo ya kina Colins, na hataki hata kuwasikia
tena. Alisema Walimdharau vibaya sana na ndio maana walipata ujasiri wa kwenda
kumtusi nyumbani kwake. Na huyo akasita kumshirikisha. Akaona ampigie tu yeye
kwa linalomuhusu. “Nina mgonjwa, naenda kumuona. Nikichelewa naomba unisaidie hapa
dukani. Wasijione wameachwa peke yao.” Mama Jema akaitika kwa haraka
bila hata kufikiria. Jelini akaelewa yupo katikati ya mambo yake, hataki
kupoteza muda kwenye simu. Ila akashukuru Mungu amekubali bila maswali, na
anamjua mama yake, maadamu amekubali, basi atafanya tu.
Rafiki Wa Kweli.
Ukweli familia ya kina Colins
walishamtia hofu Jelini. Na alijua wazi hawampendi. Akaingiwa hofu
kwenda huko kimya kimya bila mtu kujua alipo, akihofia chochote kinaweza tokea.
Maana hata mama yao alimkaribisha kwake akisema Colins ni mgonjwa.
Na Connie naye alisisitiza alifuatwa pale hata na baba yao sababu ya ugonjwa
wa Colins. Akajua imewalazimu kumfuata lakini si
kutaka kwao.
Akiwa njiani akabaki akimfikiria
wakumtaarifu, akaishia kwa James shemeji yake, rafiki wa kweli wa Colins.
Akamueleza ilivyokuwa. “Nikwambie ukweli Jelini, mimi nilijua kwa hakika kuna kitu
hakipo sawa. Hata iweje, Colins sio mtu wa kukata mawasiliano gafla! Nijulishe
kama kuna kitu kitahitajika nisaidie.” “Nashukuru shem, lakini eti nilikuwa
nikiogopa!” “Wasingekuja wote kutaka msaada wako wakiwa na nia ya kukuangamiza
tena ukiwa uliwaacha kama walivyoomba! Wewe nenda. Baada ya muda nitakupigia
kujua unaendeleaje.” “Hilo litanitoa hofu. Nashukuru. Ila kwa sasa, usimwambie kwanza
Jema. Acha nikajue kinachoendelea ndipo nitajua chakuwaambia.” “Sawa.” Wakaagana
angalau akapata amani kupata baraka za shem wake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi
kila akifikiria anakwenda kukutana na Colins! Akajikuta akitabasamu peke yake
na kulamba midomo. Alishakuwa na hamu na huyo kiumbe, akawa hana jinsi. Lakini
kila moyo ulivyokuwa ukipokea hizo hisia, wasiwasi ukazidi
kumuingia na uhalisia kumsumbua. Akili zikamkumbusha jinsi Colins anavyokuwa
linapofika swala la Love. Yeye husubiri. Na si yeye tu, hata wazazi
wake wanakuwa kama wanachanganyikiwa linapofika swala la Love.
Sasa iweje leo atafutwe yeye! Akahisi
kuna kitu hakijakaa sawa. Wazo likamjia, kumpigia anti wake, mwenye saluni
anakokwenda kutengeneza nywele Love, kujua kinachoendelea. Maana alisha acha
kupokea yanayoendelea juu ya Love, Kemi na Colins. Akayazira, maana yalikuwa
yakimuumiza tu roho.
Ukweli Halisi.
“Niambie anti langu la
ukweli.” Akaanza Jelini. “Nipo kipenzi. Nipe mpya za
mjini.” Jelini akaanza kucheka. “Anti kwa
kupenda mpya!” “Ndio yanayotuweka mjini je!” “Wewe ndio nipe za Love.” Akaanza
kucheka. “Acha nitafute mahali, nikae nikwambie kwa kituo.” “Anti!” “Kumbe!
Wasomi wale wa kingereza, wamegeukana. Bi dada anadai shoga yake wa uzunguni,
kampa mganga wa kienyeji akimwambia nabii sijui mtume au mtumishi, watajuana wenyewe, lakini
analalamika amemlogea mwanaume.
Kawa tahira kabisaa.” Jelini alishituka sana.
“Anti!” “Walahi! Bora
ulijiachia anti langu. Unaambiwa mwanaume amekuwa wakufunga na kamba! Yule mtumishi alijidai alikuwa akimuombea,
kumbe madawa ya kienyeji!” “Kwamba yeye alikuwa hajui?” “Bwana kama
ulikuwepo hapa. Nasra alimuuliza hivyohivyo. Si unamjua Nasra mdomo hauna
kufuli?” “Maana kweli! Kwani uchawi siri?” “Bwana wewe akili yako kama Nasra.
Nasra akamuuliza hivyohivyo. Akamwambia, uganga wa tunguri na wa hawa matapeli
wa siku hizi wa maombi vinafanana ila kama upo makini utajua tu.” “Sasa
akasemaje?” “Anasema eti alikuwa akimchukua kumuombea chumbani.” “Muongo.
Mshenzi mkubwa.” Jelini akawa amekasirika.
“Bwana Nasra akaambadilikia
mpaka ikabidi nimtulize. Nikamwambia atanifukuzia wateja. Maana wakija hapa,
wanaongea yao, sisi kuwasikiliza na kuwapamba si kuwakashifu! Sasa Nasra akawa
anamwambia eti yeye mwanzo alivipenda, mpaka daktari akazidisha dozi,
eti ndio ameanza kukimbia.” “Akasemaje huyo Love?” “Yeye anavyodai yule mzungu
mwenzie, Kemi, ndio amemchezea mchezo. Na amemfungia simu zake, nasikia hampati
tena pamoja na huyo mtumishi wake. Ni kama lishamvujia hivi!” Sasa Nasra akawa
anamwambia eti yeye mwanzo alivipenda, mpaka daktari
akazidisha dozi, eti ndio ameanza kukimbia.” “Akasemaje huyo Love?”
“Yeye anavyodai yule mzungu mwenzie, Kemi, ndio amemchezea mchezo. Na
amemfungia simu zake, nasikia hampati tena pamoja na huyo mtumishi wake.
Ni kama lishamvujia hivi!” Akaendelea
kumsimulia Jelini.
“Sasa tokea
aanze kuusema ubaya wa mwenzie hapa saluni, na yule mwenzie, Kemi, akifika hapa,
mashauzi. Anagawa soda za bure kwa kila mtu. Acha wapenda vya bure wa
hapa wambadilikie! Wanamwambia hakudanganywa na Kemi, aliyataka yeye mwenyewe,
ila vimemdodea, ndio hayataki matokeo.” “Na kweli.” “Basi hajarudi tena
tokea siku hiyo. Nina kazi ya kuwalaumu hawa, wamenipotezea mteja mpya maana
hapa aliletwa na huyohuyo mwenzie Kemi.” Akaendelea kumueleza mengi na kuzidi kumuumiza
sana Jelini.
“Sasa tokea aanze kuusema ubaya wa
mwenzie hapa saluni, na yule mwenzie, Kemi, akifika hapa, mashauzi.
Anagawa soda za bure kwa kila mtu. Acha wapenda vya bure wa hapa wambadilikie!
Wanamwambia hakudanganywa na Kemi, aliyataka yeye mwenyewe, ila vimemdodea,
ndio hayataki matokeo.” “Na kweli.” “Basi hajarudi tena tokea siku hiyo. Nina
kazi ya kuwalaumu hawa, wamenipotezea mteja mpya maana hapa aliletwa na
huyohuyo mwenzie Kemi.” Akaendelea kumueleza mengi na kuzidi kumuumiza sana
Jelini.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Akafika mpaka kwa kina Colins,
akafunguliwa geti kama aliyekuwa akisubiriwa mpaka na mlinzi! Akavuta gari
mpaka ndani, akaegesha na kubaki ndani ya gari akisikiliza kwa undani kujua
kilichokuwa kikiendelea huko Kigamboni.
Connie alipoona hashuki garini,
akamfuata nje. Akamfanyia ishara anyamaze, ila akamkaribisha ndani ya gari.
Connie akapanda. Akamfanyia ishara yupo kwenye simu. Akataka kushuka,
akamkonyeza asikilize. Jelini akaweka kwenye spika. Bado gari lilikuwa linawaka,
wanakula upepo kwa ndani. Jelini waliyemkataa hajasoma, siku hizi mambo yake
safi. Hapo ametulia ndani ya gari hata Connie mwenyewe anayesomea udaktari
haendeshi gari nzuri kama hiyo ya Jelini.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Upo anti langu?” “Nipo nipo. Nimeweka gari pembeni kukusikiliza vizuri. Aliyoyasema Kemi juu ya Love.” Akataka aendelee alipoishia. “Si ndio shoga yake alikuwa akimsema hapa kuwa ni mnyama mbaya kuliko chui! Kwamba Love hakutaka kusema nyumbani kwao kuwa huyo mwanaume wenu alianza kuugua ili aendelee kutumia yeye mshahara wake! Na nasikia shida yake kubwa ni hilo jumba la wazazi wao huko Kigamboni. Hakutaka kusema ugonjwa wa mwenzie ikaonekana wameshindwa kuishi huko, wakatolewa kwenye hilo jumba akarudi kuishi kwao. Kwa hiyo mwanaume alivyokuwa tahira, yeye akalinyamazia, akawa anajishindia tu mihela ya huyo bwana. Maana nasikia yule mwanaume alikuwa akilipwa mihela ya maana tu, kwenye hiyo kampuni ya wazazi wao, na jumba hilo ndio roho yake huyo mwanamke wake.” Akaeleza mengi mno mpaka uchungu. Connie akalia sana, akisikiliza.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Wasomi hao wawili, Kemi na Love
wakageukana vibaya sana, wakianikana kwenye masaluni kama waliokuwa
maadui, kumbe walishirikiana kuhakikisha wanamtoa Jelini kwenye maisha ya
Colins, ili Kemi amlipize kisasi Jelini. Halafu kwa upande wa Love ndio hivyo,
maslahi. Kemi alipomkabidhisha ushindi Love, na kuhakikisha Jelini na yeye
amekosa, akawa amemaliza kazi yake. Akajiweka pembeni na
kumuachia Love uwanja.
Hakutaka tena hata mahusiano na Love.
Love alikuwa njia ya kusadia kulipiza kisasi tu. Lakini hapo
ndipo Jelini akaamini maneno ya Colins, kuwa ni kweli Love hakuwahi kumpenda yeye
kama Colins. Anti yake akawasimulia mengi mpaka akaridhika ameyamaliza, na
kuwaaga.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Nisikilize Connie. Cha muhimu hapa
ni maombi. Najua huwa yanasaidiaga sana. Nimeona kwa Jema. Mimi sijasimama sana
kwenye dini, ndio nimeanza tu. Hata leo nimeomba kabla yakuja hapa. Tumeshajua
kilichompata Colins. Akiombewa kwa ukweli, atafunguliwa tu. Usiogope.” “Ni
hivyo hujamuona. Coly anatisha, Jelini wewe! Ngumu kumtambua. Sasa najiuliza
huyu Love alitaka kumfungia huko mpaka lini?!” “Hayo hayatasaidia. Mwishoe wote
tutajikuta njia panda, kutafuta majibu ambayo hata tukipewa, hayatasaidia.”
Simu ya shemeji yake ikaingia.
“Hata ndani sijaingia shem. Nilikuwa
nipo kwenye gari nikielezwa yaliyompata Colins. Naona ulikuwa sahihi.
Nitakusimulia nikitoka hapa.” “Basi nitakupigia tena baada ya nusu saa ili
nihakikishe upo salama.” “Hapa nipo na Connie, nahisi ni salama. Usiwe na
wasiwasi.” “Hapana Jelini. Nataka kukusikia ukishamuona Colins.” “Sawa.” Wakaagana.
Ndipo wakaingia ndani.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kwa asili nyumbani kwa kina Colins
pametulia. Ila alikuta hali ya simanzi. Wazazi walikuwa sebuleni kama waliokuwa
wakimsubiria. Jelini akawasalimia akikaa. “Karibu.” “Asante. Colins yupo wapi?”
“Amelala.” Jelini akatulia kidogo kama anayefikiria. “Ila hajalala kwa dawa.
Hatachukua muda mrefu kuamka.” Akaongeza mama yake kwa sauti ya kusihi. “Ni
sawa nikiingia kumuona? Maana mimi nina muda mfupi sana, nataka nimuone, nirudi
kwenye majukumu yangu. Nimeacha pale bila uangalizi wa maana.” Kama wambebe
mpaka huko chumbani!
Hatimaye!
Akaongozana na Connie mpaka kwenye
hicho chumba. Jelini alishituka kumuona pale alipolala, mpaka pochi, simu na
funguo za gari vikaanguka na kubaki ameshika mdomo. Alikuwa ni mzee kuliko babu
yake aliyemfuata kwao na. kumuonya amuache. “Hataki
kula! Ndio kinachomfanya achoke zaidi, mama anamuwekea dripu.” Jelini
akamsogelea pale kitandani.
Alikuwa Colins. Akakaa taratibu.
Akamvuta mkono wa kushoto ule uliokuwa upande wake na kuupakata. Kisha Connie
akamuona anaingiza mkono ndani ya shati na kumshika kama vile Colins mwenyewe
anavyojishika. Akautuliza huo mkono hapo juu ya ziwa lake la kushoto, kisha
akampapasa kidogo. Colins akafungua macho.
Akamtizama kwa muda kama anayefikiri
ni ndoto au kweli! Jelini akamuwahi kabla hajafunga macho. “Pole Colins.”
“Jelini!” Akamuita kwa sauti ya chini sana, dhaifu. Ila akamsikia. “Nimekuja
kukuona.” Akamuona machozi yakimtoka. Akamfuta taratibu. “Pole. Unasikia
baridi?” Akakubali. Connie akamsaidia kusogeza shuka. Wakabaki
wakiangaliana.
“Nikupe chakula kidogo ule?” Akabaki
akimtizama. “Ni mimi Jelini. Nataka kukupa chakula. Halafu…” Akainama
kumnong’oneza sikioni akimwambia, “Nitakubembeleza ulale vizuri.” Akakubali.
“Nisaidie hata uji, nimpe.” Connie kama akimbie! Akabaki akimpapasa, akamuona
anafunga macho. “Usilale mpaka ule. Sawa?” Akafungua macho, akamwangalia.
“Jelini!” “Nipo hapa na wewe Colins. Pole.” Akahema kwa nguvu, akamuona
anatulia.
Baada ya muda akarudi na bakuli la
viazi vyakupondwa na nyama ya kusaga. Vimechanganywa. “Kinanukia vizuri!”
Jelini akasifia. “Kaa vizuri nikulishe.” “Acha baba aje amuweke vizuri.” Mzee
akaingia kwa haraka kama ambaye alikuwa mlangoni, akasikia! Jelini akamuona
vile anavyomuweka kwa makini, akamuweka akawa amemuegemeza kwenye mito. Kisha
akawapisha. Akabaki akimwangalia Jelini.
“Ukikazana kula, utapata nguvu. Wewe
fungua tu mdomo, na kutafuna. Nitakuwa nikikuwekea mdomoni.” Akakubali. Akaanza
kumlisha taratibu kama mtoto. Anatafuna taratibu, lakini anameza. Akala mpaka
akakaribia kumaliza, akamuona anajiegemeza kama alale. “Umekula vizuri.
Ukikazana hivi, utapata nguvu kwa haraka. Unataka kunywa maji? Akakataa.
Connie akamsaidia kuondoa vyombo pale
chumbani. Jelini akajivuta juu kabisa ya kitanda. Akaegemea kitanda.
Akamuonyeshea asogee, ambembeleze alale. Akamsaidia kumvuta mpaka mapajani.
Alijilaza vilevile kama alivyokuwa akimlalia zamani. Mpaka Jelini akacheka.
Akaanza kumpapasa taratibu. Akageuka kumtizama. “Jelini!” Akamuita tena
taratibu. “Nipo Colins. Ni mimi.” Akabaki akimwangalia. Akaanza kumchezea
nyusi. Connie kurudi kuwakuta vile, akatoka taratibu.
“Jelini!” Akamuita tena. Akamvuta
mkono wake, akauweka shavuni kwake. Vidole vilikuwa kama njiti! Akamshika
vizuri, akabaki akimpapasa Jelini shavuni. Wakabaki wakiangaliana mpaka
akamuona anaanza kusinzia. Mkono ukaanguka. Akaudaka na kuungalia jinsi ulivyokuwa
na alama na kuzidi kuumia nafsini mwake. Akamuita Connie.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Nisaidie kunipa shuka jingine. Naona
vipele vya baridi vinaongezeka. Na mwili upo kama unajoto!” Wakaingia wazazi
wake kwa haraka kama ambao walikuwa wamesimama hapo mlangoni wakisubiria. “Acha
tumpime homa.” Kweli akakutwa na homa. Haikuwa kali. Lakini baba yake
akamchukua na damu, akaondoka kwenda kuipima. Akabaki amempakata kichwa
akimpapasa akarudi tena kulala maana aliamka wakati baba yake akimtoa damu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
James akapiga simu. “Nipo naye shem. Lakini
anahoma. Ndio ametolewa damu kwa vipimo.” “Aisee mpe sana pole. Nikitoka kazini
nitapitia.” “Nashukuru shem.” Wakaagana.
Huyo Jelini hapo akawa kama amefika.
Wakashangaa haondoki hapo kama alivyosema ameacha dukani hakuna mtu! Muda wote
wala hakumuweka pembeni. Naye Colins akifungua macho anamuangalia kwa muda,
kisha anamuita kama kuhakikisha. “Jelini!” “Nipo Colins. Usiwe na wasiwasi.”
Akawa anamtuliza, kisha anarudi kulala.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Wala haukufika muda wa kutoka kazini,
James naye akawasili hapo. Alifurahi kumuona Colins, ikapita muonekano. “Vipi
wewe?” Akawa akimuuliza huku akicheka kama aliyeokota lulu, haamini! Baba yake
akarudi na dawa. “Itakuwa hayo madonda ndiyo yanampa homa. Ila hana infection yeyote
ile.” Akamuanzishia dawa ya kukausha madonda.
James akamsaidia baba yake jioni hiyo
kumuogesha. Akabadili mashuka, pakawa pasafi hapo kwenye hicho chumba. Wazazi
wa Colins wakashangaa anafanya bila kinyongo, wakikumbuka onyo la kutokuwa karibu
na kijana wao. Akafanya kwa moyo wote kama na yeye aliyekwisha kuwa na hamu
sana na huyo Colins.“Kula ugali urudi mtaani bwana! Acha kula kama JJ.” Angalau
pakawa na utani, ila Colins akawa akimwangalia tu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ikabidi Jelini amuite James sebuleni
wazungumze. Wakatoka Colins akiwa amerudi kulala. Akamsimulia kwa sauti ya
chini kama mtu aliyekuwepo pembeni asisikie. Akamwambia yote
aliyosikia mchana huo, na Connie akiwa naye garini wakisikiliza. Kumbe wazazi
nao walikuwa wakisikiliza kila hayo mazungumzo. Kwa hakika hao wazazi waliumia
sana. Walibaki na majuto yasiyokuwa na maelezo.
“Mimi ninachoona anahitajika maombi
ya kweli. Lakini mimi sijui kuomba.” Jelini akajitoa. “Mimi namjua mtu
anayetembea na hofu ya Mungu. Si mchungaji, lakini yule jamaa anampenda Mungu
wake. Na amefanikiwa mno kwenye kila jambo. Mungu ameweka mkono wake mpaka kwa
mke na watoto wake. Anamjua Mungu na kuishi naye si kwa mazingaombwe kama
hawa watumishi wa siku hizi. Ni kama Baba yake kweli. Ukiwa
naye, utajua yupo Mungu aliye hai.”
“Ni nani shem?” “Bosi wake Jema.
Anaitwa Joshua Kumu. Yupo busy sana. Lakini ni mtu wangu wa
karibu. Mkihitaji mtu wa kuomba kwa ukweli, yeye atakuwa msaada.” Wazazi wake
wakaangaliana.
“Hapa tulipo sasahivi, sidhani kama
tuna msaada mwingine bila Yesu. Maana tumetumia kila dawa tunayojua ingeweza
kumsaidia, lakini ni kama hivyo mnavyomuona.” Akasalimu amri baba Colins. “Na
mama je!?” “Nina majuto James mwanangu, sina jinsi nikaeleza mtu
akanielewa. Sijui nilipatwa na nini! Ninachotaka ni apone tu.” “Basi acha
nimpigie simu. Ila huwa hatoki kabisa, akifika kwake. Ana mapacha umri karibu
na JJ.” “Tafadhali mjaribu. Akishindwa leo, tumuombe wakati atakao weza.”
James akatoa simu. Akampigia. Ikaita
mpaka mwisho haikupokelewa. Hakupiga mara ya pili. Akasema waache, atakuja
kurudisha simu atakapokuwa na nafasi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Baaada ya masaa kama mawili hivi,
tena James alikuwa akikaribia kuondoka, ndipo akamrudishia simu. “Nilikuwa
nikimalizia siku na kina Kumu. Hata sikuwa na simu.” “Usijali kaka.” Akamuelezea
kwa kifupi. “Daah! Hiyo ni ya kushugulikia kwa haraka. Acha nizungumze na Naya,
akitoa baraka zake, nije mara moja niungane na nyinyi kwenye maombi.”
“Nashukuru Kumu. Na samahani kwa usumbufu.” “Bila shaka.” Akaaga.
Wawili hao tokea Bale aweke ombi lakumuoa Vai, na James kuomba muda wa
kufikiria, hawakutafutana tena. Ndio Joshua anamsikia James usiku huo.
Akufaaye Wakati Wa Dhiki,
Ndiye Rafiki Wa Kweli.
Baada ya lisaa, Kumu akawa ameingia
hapo. “Hujambo Jelini?” Jelini akacheka. “Kumbe unanikumbuka!?” “Siwezi
kukusahau. Si ulisema kwenu wewe ndio mtoto mzuri. Mpole kuliko Jema.” “Kabisa.
Mimi ndiye kiziwanda wa mama Jema. Ni mtoto mzuri kuliko Jema.”
James akamtizama na kutingisha kichwa. Wakacheka.
“Nashukuru kwa kuja Kumu.” “Ni vile
sababu ni James. Nisingerudisha simu kwa haraka. Nina watu wangu wachache sana
kwenye maisha yangu, na simu zao huwa hazisubiri, pengine niwe sijaona kwa
wakati. Na wenyewe wananijua mimi na ratiba zangu. Kuna mida nikiona simu zao,
najua si za kurudisha kwa kuchelewa, ni dharula. Na najua pia ni kusudi la
Mungu ili na mimi nishiriki kwenye maombi.” Wakamuona vile alivyo mnyenyekevu.
“Mimi mwenzio sijui kuomba. Ndio Jema
amenifundisha leo. Eti ni kama kuzungumza hivi na wewe?” Wakacheka vile
alivyojiwahi. “Kabisa. Huyu Mungu mwenye enzi yooote, ametupa
bahati ya kutufanya na sisi kuwa Wana. Huhitaji maneno
ya aina fulani kuzungumza naye. Ni kama hivi mimi ninavyozungumza na wewe hapa.
Na uzuri, hana tatizo la kusikia. Maandiko matakatifu
yanasema, sikio lake si zito, hata akashindwa kusikia.”
“Halafu yeye mwenyewe anatuita tusemezane naye. Anataka
mazungumzo na sisi. Kwa hiyo hapa tunachokwenda kumwambia ni kuwa, Colins anaumwa,
tunaomba aingilie kati, amponye afya yake. Maana hata maandiko
matakatifu kutoka kwenye bibilia yanasema, ‘ukiwa huwezi, basi ita wazee wakuwekee
mkono’. Vinginevyo hata yeye mwenyewe angeweza kujiombea akapokea
tu uponyaji.” Akazungumza nao kirahisi sana, wakabaki wakimsikiza.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kumu mwenyewe anajiwakilisha haswa.
Ukimtizama kuanzia juu mpaka chini, na aina ya gari aliyoacha hapo nje, harufu
ya neema aliyoingia nayo hapo ndani. Jinsi alivyosimama kwa ujasiri. Nadhifu
hata mida hiyo. Haonekaniki na shida ya aina yeyote ile. Ukimuona tu, utajua
kuna utoshelevu ndani yake. Hata akizungumza huwezi tilia mashaka anachozungumza.
Anasikika kwa wazi, kirahisi na kifasaha haswa. Mungu anayemzungumzia yeye,
hajamuweka kwenye mafumbo. Alimtambulisha kwao kirahisi mpaka wakajisikia
kufunguliwa wao wenyewe kwanza hata kabla ya Colins.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ndipo wakamuingiza chumbani kwa
Colins. “Msiogope, na msiondoke. Njooni tuombe pamoja.” “Yule mtumishi wa
kwanza alikuwa akitaka kubaki naye peke yake ili amfanyie maombi.” “Bibilia
inasema, ‘wawili au watatu, wakikubaliana lolote chini ya jua, nalo litakua’. Tufunge na
kuharibu roho za uharibifu, tumuite Yesu aliyekuja kutoa uzima tele,
kwenye maisha ya Colins. Tushikane mikono hapa kumzunguka hapo kitandani,
tuombe.” Wakafanya wote kama alivyowashauri.
Nalikuja Ili Wawe Na
Uzima, Kisha Wawe Nao Tele.
{Yohana10:10}
Colins alikuwa amefungwa na nguvu za
giza. Haikuchukua muda mrefu, Kumu akaamuru mapepo yatoke kimyakimya, yamuache
huru, bila kuleta uchonganishi kwenye familia, asijue walishamjua mbaya wao. Na
kweli, akaomba, Colins akafunguliwa. Ukweli Colins alifungua macho akionekana
wazi amefunguliwa. Japo hakuwa na nguvu, lakini alionekana anao ufahamu wake.
“Wewe si kama yule mtumishi mwingine
aliyeniombea. Alinifanya nisiweze kufanya ninachotaka. Halafu nikawa siwezi…”
Ni kama akashindwa jinsi ya kujieleza. “Huyo ndiye Yesu tunayemtumikia. Tokea
anafika hapa duniani, na pia ilitabiriwa hata kabla hajaja hapa dunia kwenye
bibilia Isaya 61:1-4 kisha kuja kusema yeye mwenyewe kwenye Luka 4:18, ‘Roho wa Bwana yu
juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha
huru waliosetwa.’ Hizo ndizo kazi zake Yeye.” Kumu akaendelea akiwa na
furaha kana kwamba yeye ndiye aliyewekwa huru.
“Na anapopita sehemu
utajua tu kama ni Yeye amepita. Maana anaacha hizo sifa. Utasikia uhuru
wa kweli.” Akazungumza na Colins kwa taratibu, wote wakimsikiliza. “Kazana
kula. Umepata nguvu za nafsi na roho, lakini mwili wako unahitaji kupona.
Chakula ni muhimu.” Akawaombea wote mle ndani akitubu kwa niaba
yao, akawabariki na kuwaombea amani.
“Sasa sisi tuna watoto wadogo. Na
mimi nashinda kazini siku nzima. Usiku wakilala hivi, ndio na sisi tunapata
muda wetu. Nikichelewa kutoka hapa, nitamkuta Naya ameshalala. Naomba niwaage.
Wewe James niseme baadaye.” Wakamshukuru, James akamsindikiza akimshukuru
lakini ndio akawa ameongeza deni. Bale anataka kuoa dada yake
kabla hajamaliza shule, na ana baraka za Kumu. Inamaana wakati yeye anasuasua
kutoa jibu, Kumu na Geb wanamsubiria tu, huku wakimfanyia yake
kwa haraka bila kuchelewa hata katika mida isiyo rafiki kama siku hiyo. James
akabaki na deni zaidi.
Kilichokuwa Kikiendelea Kwa
Colins
Baada ya muda James akarudi. “Sasa
mzee?” Akimuuliza Colins kama anayetaka kumuaga. “Ni nini kilitokea James!?
Mbona kumbukumbu zangu hazijakaa sawa!?” Akamuuliza kwa sauti yake ya kudhoofu.
“Ni hivi Colins. Sasahivi umedhoofu sana. Kikubwa na cha msingi, kurudisha
nguvu kama alivyokwambia Kumu. Hicho ndicho kiwe cha kwanza. Cha pili
kinachotaka kufanana na hicho, ni chakula kingi ili upone. Mzee umechoka! Na
una madonda ambayo unahitaji kutulia, kula, kunywa dawa, upone kwa haraka,
urudi mtaani. Kisha ‘mengine’ ndiyo yafuate.”
Colins akavuta pumzi kwa nguvu wakamuona anafunga macho.
“Umeshaoga. Umekula. Umekunywa dawa.
Nashauri ulale.” “Najisikia vizuri. Yaani ndani najiona mwepesi sana. Kuna
uhuru wa ajabu ndani yangu. Sijajisikia hivi mufa mrefu sana. Ilikuwa kama…”
Akatulia akifikiria. “Mtu mwingine anaishi akiutumia mwili wangu kufanya anachotaka
yeye si mimi. Hata nikitaka kukataa, yeye analazimishia na
sina jinsi ya kupinga. Niliteseka, sikuwa na jinsi ya kujisaidia.”
“Aisee pole sana. Mimi nitarudi hapa alfajiri kabla ya kwenda kazini.
Nikishakuosha na kula, ndio nitaenda kazini ili nimpokee mzee.” Wakamuona
anatokwa na machozi.
Wa Rohoni.
“Usiwe na wasiwasi James. Nimeagiza nesi anakuja kesho asubuhi.
Ata..” Jelini akashituka kama kapata habari mbaya. “Kwamba huyo nesi ndio awe anamuogesha Colins!?”
Akauliza kwa kupaniki. “Na kumsafisha madonda.” “Mhhh!” Wakamsikia akiguna.
“Anahitaji muuguzi mbali ya mama yake, zaidi ninapokuwa kazini.” “Kwamba huyu
nesi ni mdada!?” Swali la pili likawafanya watulie, ila kushangazwa wivu kwa
Colins aliyekuwa kama kinyago! Haikuingia akilini. Wakaona haiwezekani.
“Nimempata kwenye moja ya kliniki
zetu. Ni binti mzuri tu, aliyetulia. Na…” “Hapo mzee wangu ndio naona unaelekea
kwenye kuongeza tatizo.” James akamuwahi, mzee asielewe. Jelini akashangaa kwa
sauti kabisa. “Kwamba binti ndio aje hapa, halafu ndio
aanze kumuogesha Colins!?” Akahamaki na kuongeza. “Mimi hivyo
sioni kama ni sawa.” Akaongea bila hata hofu kana kwamba Colins
mumewe.
“Au kwa nini usizungumze na Judy? Ni
mdada mtumzima na anahekima.” Akasaidia mama Colins. “Tena hao kina dada watu
wazima ndio wabaya kabisa. Unakuta wana vijimambo vyao halafu nguvu ya
kumsaidia mtu kama Colins hawana. Unadhani wana msaidia, kumbe
wanakuwa na lao jingine. Halafu huku nyuma wakati nyinyi hampo wanakuwa wana
mnyanyasa kwa siri. Nyinyi mnaendelea na shuguli zenu huko, mnadhani mmemuacha
Colins kwenye mikono salama, kumbe huku yeye anakuwa akimnyanyasa. Hivyo
mimi sitaweza.” Jelini akaongeza akilalamika kabisa, kana kwamba
anahusika kwenye maamuzi. Colins amelala kitandani anamtizama. Wazazi wakakwama. Ila
na mshangao kama waliochanganywa tayari.
“Mimi naenda kumletea Colins maji ya
kunywa.” Akatoka hapo chumbani alipoona wamenyamaza. “Nyinyi hamjamjua Jelini.
Ana wivu na Colins. Hivyo hataki mtu mwingine amguse wala si
sababu nyingine.” James akanong’ona. “Colins mwenyewe alivyochoka hivyo!?”
Akaongea mama yake kwa mshangao akimtizama huyo Colins mwenyewe. “Kama huamini
mama CJ, akirudi hapa mjaribisheni kumwambia mtamleta mwanaume. Muone kama na
huyo hatamletea kipingamizi.” James akaongea akinong’ona pia.
Akarudi na glasi ya maji. “Unatakiwa
kunywa maji, Colins.” Colins akamtizama vile alivyobadilika. “Usikasirike.”
Colins akamwambia kwa upendo. “Watu hawaaminiki. Huwezi kuleta kila mtu karibu
yako.” Akaongea akimtizama Colins lakini kama anayewaambia wote hapo chumbani.
James akamfanyia ishara baba yake Colins. Akajua ndio anamwambia amjaribishe.
“Ni kweli mama. Si kila mtu wa
kumuamini. Basi nafikiri nimletee nesi wa kiume mwenye nguvu ambaye anaweza
kumsaidia vzuri.” “Mmmmh!” Akaguna tena na kubaki akimtafutia na huyo sababu.
Baba CJ akamuwahi. “Huyo nitakayemleta nitahakikisha namuweka sawa kabisa.
Colins anahitaji msaada wa ukweli. Tena mwenye ujuzi wa kiuuguzi.” “Sasa hao
ndio wabaya kabisa baba CJ. Unakuta wewe si ndio unamuamini
hivyo. Anajua umempa sifa zote hivyo! Kwamba wote tunamtegemea yeye hapa kwa
Colins. Mwenzio anaanza kiburi na ujuaji. Yaani anaanza kuishi na Colins vile
anavyotaka yeye, mwishoe anaanza manyanyaso. Wote tunakuwa tunamfuatisha
anachotaka yeye. Mimi hivyo sitaki.” Nusura wacheke. Wakaamini
maneno ya Colins.
“Sasa wewe unashauri vipi.?” Ikabidi
mzee amuulize. “Mimi sijasema siwezi kumlea Colins, mimi
mwenyewe!” Akaongea bila shida, kama asiye na majukumu yeyote yale na hapo ndio
kafika. “Peke yako hutaweza mama! Na kunatakiwa utaalamu kwenye hivyo vidonda.”
“Kwani si mama yake anifundishe, nifanye mimi mwenyewe! Kwanza mimi nilitaka
kuwa nesi. Muulizeni Colins kama nadanganya sasahivi. Ila tu sitaki kwenda
shule.” Connie akashindwa kujizuia akacheka.
“Mimi sidanganyi hata Colins ni
shahidi yangu. Napenda mambo ya unesi. Ukinipa dawa ukaniambia jinsi ya
kuzitumia, mimi sishindwi. Kwanza nitakuwa mtu wa kuaminika kuliko hawa
wasichana wanakuja hapa, wanaanza kumchungulia tu na
kumshikashika bila adabu. Wanakuwa wanamuona kama sijui nini! Hapana.
Hivyo mimi SITAKI.” Hapo Jelini anakatalia wazazi wa Colins, halafu sasa ni
nyumbani kwao, kijana ni wao, ndio ameitwa tu kuona mgonjwa, lakini
anavyokataa, na mabega juu, kwamba yeye hataki, kana kwamba yeye
ndio amewakaribisha kwake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Mimi sijasema siwezi
kumlea Colins.” Akaongeza huku ameshikilia glasi yake yenye maji, na kuangalia
yale maji aliyosema anampa mgonjwa. Analalamika hapo mbele ya kila mtu kama alie
vile, kuona anapokonywa mgonjwa! Hapo hakumbuki lolote isipokuwa Colins.
Si majukumu mazito aliyonayo ya kibiashara, mama
yake ambaye ndiye msimamizi wa hizo biashara na kupanga kila kitu, mtoto wake.
Kikubwa zaidi hata Ezra hakupita akilini mwake. Akili
na mawazo yake vyote vilikuwa hapo kwa muda wote asikumbuke lolote ila Colins
tu. Kila kitu hataki tena.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Basi mama. Mimi
nahisi tufuate ushauri wako. Ukihitaji msaada utatuambia.” Akaongeza mama CJ
kumtuliza. “Mimi msaada ninaotaka ni wa shem tu. Ndiye namuamini na Colins. Na
nyinyi mmeona jinsi alivyomuogesha leo na kumvalisha kwa furaha bila shida.
Watu baki sitaki.” Mabega yakamsaidia kukataa. Akaweka glasi chini,
asimpe mgonjwa. Akaanza kumfunika huyo Colins akiwa hasikii baridi. James
akawatizama akicheka na kutingisha kichwa.
“Sasa huyo ndio
Jelini, halafu sasa ujumlishe na Colins mwenyewe ambaye ubishi ndio
umezaliwa kwake. Halafu ndio uwe nao siku nzima. Ujikute katikati yao! Lazima
kichwa kichemke.” Wakaanza kucheka. “Sisi wote tunawajua hawa wawili. Na huwa wanawezana
wao wawili tu. Huna jinsi ya kubadilisha uamuzi wa hata mmoja wao, isipokuwa
wao wenyewe. Na usiombe uwe katikati ya ugomvi wao. Utakaukwa mdomo. Hawashauriki.
Msimamo mkali. Kila mtu kashika pakali. Basi mimi na Jema ndio tunabaki
kuhangaika.” Mpaka Jelini mwenyewe akacheka.
“Sasa wewe shem
unataka tena vitoto vidogo vianze kujazana humu ndani!?” “Si umepewa mpaka watu
wazima wewe?” Akapandisha mabega kukataa. Wakacheka tena, lakini kwa faraja.
Maana huyo Jelini anayemng’ang’ania huyo Colins, hapo kwenyewe yupo
njema. Jelini ni mzuri bwana! Na anajua kujiwakilisha popote.
“Nyinyi wazazi wangu
tulieni. Huyu Colins atakuwa sawa kabisa. Tupeni mimi na Jelini hata juma mmoja
tu. Tutatathimini hali nzima. Lakini naamini atapata nguvu. Uzuri Colins
mwenyewe si mvivu wa kula. Naamini baada ya muda mfupi sana atakuwa na nguvu
yakuweza kusimama mwenyewe bafuni na kuoga. Tukianza kumletea wauguzi hapa,
tutampa hali ya ugonjwa, hatatoka hapa ndani kwa haraka.” James akaongeza.
“Atakuwa sawa tu. Asubuhi na jioni nitakuwa
nikipita. Na muda na wakati wowote wazazi wangu mtakaponihitaji, mnipigie. Huyu
Jelini ndio tutakuwa tukiwasiliana.” James akaaga na kutoka kwa haraka na yeye
kuwahi mkewe lakini wakiwa wameweka mipango na mikakati endelevu ya faraja kwenye
hiyo familia.
Rudi Kwenye Uhalisia.
Wakamgeukia Jelini.
Baada na yeye kuaga. Ila mama CJ akawa kama amekumbuka kitu baada ya Jelini
kusema atarudi hapo alfajiri na kushinda naye siku nzima. “Sasa na wewe Jelini
kazi?” Ndio akagutuka. Akabaki ameduaa. Anamwambiaje mama Jema aliyekwisha kinahiwa
na hiyo familia? Wamfukuze kwa kijana wao akiwa mzima, leo ageuke kuwa muuguzi
wakati hajiwezi!
“Ulisahau?” “Nilikuwa
wala sikumbuki tena! Hivi leo nimemuachia mama biashara zote!” Akabaki ameduaa ndio kama taarifa
zinamfikia na kumgutusha kumpa uhalisia wa mambo. Zikaanza kupita
taarifa nyingi kwa wakati mmoja. Maisha yamebadilika. Haipo kama
ilivyokuwa tokea aachane na Colins. Mengi yalishaendelea. Wakamuona anaanza
kusaka pochi yake kwa kupaniki. Wakabaki wakimwangalia.
Akaipata na kuifungua
kwa haraka kama anayewahi kitu. Akapora simu yake mwenyewe ndani ya hiyo pochi.
Ndipo akakutana na missed calls zakutosha kutoka kwa Ezra. Kabla
hajatulia simu nyingine ya Ezra ikawa inaingia. “Mungu wangu, Ezra!” Jelini
alishituka kama aliyefumaniwa, mpaka pochi ikamuanguka na vitu vyote vya ndani
kumwagika, na kusambaa. Pale chumbani wote, mpaka Colins kimya wakimuangalia.
Alionekana kupaniki
kwa kuvurugikiwa haswa. Ni kama kwa muda fulani hivi, ulimwengu wote
ulisimama, ilikuwa yeye na Colins tu. Kumbe yupo na Ezra! Aliyempa viapo vyake
na asubuhi hiyo pia akagongelea msumari. Kwa makubaliano mengi ikiwepo
kula chakula cha usiku huo pamoja. Kuonana kabla ya kulala. Kuzungumza
kabla ya usingizi kuwatoa kwenye ulimwengu huu wenye mengi. Akabaki
ameduaa akiitizama simu yake, vitu vilivyokuwepo kwenye pochi vilivyozagaa hapo
na kumzunguka na vyenyewe vikimwangalia kama wenyeji wake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ni Nini Kitaendelea Katikati Ya Wanaume Hao Wawili?
Nani Zaidi?
Je, Ni Nani Atabaki Kwenye Moyo Wa Jelini?
Na Nani Atamfikisha Kanisani Mrembo Huyo?
Inaendelea.
0 Comments:
Post a Comment