COPY & PASTE. NIMEJIFUNZA MENGI KUPITIA HII, NIKAONA NIWAPE NA WASOMAJI WANGU, PENGINE NA NYINYI MTAOKOTA KITU, MJIONGEZE.
Mdau 1: Wanawake zetu kabla hatujawaoa walikuwa wasafi wananukia haswa, baada ya muda wamejiachia mwanamke kwapa kama kichaka cha mende harufu ya jasho sasa mwamba analala tu bila kupewa piriton.
Mdau 2: Hao wake zetu wanatupa msongo wa mawazo sana mke anajua stail za judo zote alafu anataka saa lizima na bado hafiki kilele alafu anasema mimi ndio nina shida wakati niko fiti tu, makasiriko sasa baada ya hapo utafanyiwa visa mpaka ukome
Mdau 3: Kero yangu ni tabia ya mke kuamua kufanya majukumu yangu kila nikitaka kulipa ada ameshalipa, nikileta chakula kashaleta, mbaya zaidi anasema kwa marafiki zake yeye ni super woman ananimudu
Mdau 4: Mke wangu wanashinda kanisani ibada kila siku, kila ninacholeta nyumbani anapeleka kwa mchungaji, tendo la ndoa napewa Akipata kibali rohoni
Mdau 5: Mhhhh kichefuchefu kabisa mke yule sijui nilikuwaje kipofu, ana dharau classic alafu anarudi nyumbani siku akiwahi ni saa tano usiku eti boss alimpa kazi nyingi, mara trip za kazi , tendo napangiwa ratiba mara moja kwa mwezi.
Mdau 6: Hivi huwa hamfundishani kuhusu nguo za ndani?? Mtu anavua nguo pichu imechanika rangi sasa kama kinyonga kapita au maua kitenge, sidiria ameifunga mafundo kwenye kwapa huangalii marambili alafu mtu anasema my husband you have lost attraction with me.. which attraction?
Mdau 7: Nachefukwaaa na damu ya hedhi anairundika mara aweke chini ya kitanda, mara bafuni tena juu ya sinki, anaweza akawa hedhi akaoga next day alafu sasa akiwasha feni hewa inasambaa najihisi niko kiwanda cha matairi.
Mdau 8: Kanirundikia ndugu zake wakubwa kwa wadogo, nyumba kama danguro, wanangu hawafurahii maisha maana hata bajet ya kula vizuri imeisha. Vikao sasa vya kunijadili na kunikebehi, nikimwambia anasema sipendi ndugu zake.
Mdau 9: Mke ni mshirikinaa jamani kila siku mara kaoga chumvi mara majivu mara kafunga mafundo, kashanitishia sana kuninyoosha nikimsaliti, nilichoka siku hiyo alizani nimelala kumbe namuona kakojolea kopo alafu akanywa mkojo wake huku anasemea maneno.
Mdau 10: Haaaaa wangu Ni mtumishi wa Mungu huko anakowahudumia ni malaika number one wa mbinguni lakini ndani ni kapepo mkata raha na amani, kuna saa natamani nikamchambe mbele ya waumini wake, anawapa shuhuda feki za namna ndoa yake ilivyotamu kumbe hamna kitu.
KERO KUTOKA KWA MEN CONFUSED WITH MARRIAGE 11 MPAKA 20
Tunaendelea na kero za wadau wengine 10 ambao ni waume wa ndoa walioamua kutapika kero zao dhidi ya wake zao.
Mdau wa 11: NYWELEEEEEE JAMANI, Waambie wanawake wanatutesa pua zetu na harufu ya nywele, na zilivyo bandia usiombe zilowane na kujikaukia ZINANUKAA alafu mke anataka usiku mkilala akulalie kifuani: ili kuepuka pumu najifanya kifua kinauma nageukia upande mwingine.
Mdau wa 12: Mke wangu nimeamua kumuacha kabisa kila akibeba mimba anatoa , madai anataka amalize kupersue Carrie yake. Anataka awe na PhD na hapo nimemuoa nikaanza kumsomesha certifate, diploma juzi kati kamaliza degree mimba zinatolewa tu , nimekimbia nisije kujirusha ghorofani atakapomaliza elimu na kusema I AM NOT HER TYPE.
Mdau wa 13: Wangu ni mchoyo, mbinafsi sana , ndugu zangu wakija anaficha vyakula na kama ni wa kulala basi kutapikwa maharage dagaa mpaka waondoke, alafu anawaletea watoto chips, matunda atayakata na kuwaita chumbani awalishe. Ndugu zake wakija anawahudumia kama wafalme. Namchukiaaa nimechoka sema sitaki wanangu wakae single parented.
Mdau wa 14: Mke wangu Habebeki jamani, kila nikimfungulia biashara inakufa atakula mpaka mtaji na hatulii dukani kutwa na mashosti kujua kijiwe gani kipya na mziki gani mpya mjini, baada ya hapo ni kelele mpaka nitamfungulia tena na inakufa, Sikujua ndoa ndio hivi Wallah
Mdau 15: Wangu tumefika mwisho kila mtu na chumba chake watoto ndio wanatuweka na hata hivyo naogopa kuwapima DNA maana sioni wakinifanana, mwanamke yule ni Malaya katembea na ndugu na marafiki zangu mwisho nilimkuta na houseboy ndio nikasema basi. Lile kabila nilionywa nikabisha kumbe pepo la ngono ni asili yao.
Mdau 16: Wangu sijui ana shida gani, sina magomvi nae nahudumia vizuri tu lakini AKIANZA KUTUKANA WATOTO NA KUWALAANI ALAFU NI WADOGO TU Na sasa watoto wanamchukia wanasema dady we need another mom. Kwa muelekeo wake nitamuacha asiniharibie watoto kwa kichaa chake kisichojulikana.
Mdau 17: 😂 😂 😂 Kwanza nicheke kama mazuri vile puuuuu... wangu akiamka saa 12asubui mpaka saa 6 usiku ni simu na tamthilia anahamia dstv,Adam, zuKu hahaha daaa wanaume mateso, basi utasikia DADAAAA DADAAAA MPE BABA ABC Sasa dada niliyenae mhhh nakaribia kuanguka nae kabisa maana na yeye ni kama ameona fursa.
Mdau 18: SIJAWAHI KUMSALITI lakini nimechoka na tuhuma zake za kunishuku, kinachonikera zaidi anataka akipiga simu nimpe kila aliyeko karibu yangu aongee nae hadi bosi wangu, nikikataa uwii nitaoga matusi, mara alie, mara anitishie kuachana, Sasa akipiga asikie mwangwi weee kama niko toilet itabidi nitoke nimpe simu aliyekuja toilet ili tu ajue siko na mwanamke, MADAI YAKE AMESOMA MITANDAONI KUWA MUME ANAWEZA KUSALITI MCHANA UKIDHANI YUKO KAZINI jamani sipumui I am fed up.
Mdau 19: MKE MCHAFUUU: Nanunua mashuka ya kutosha lakini kuyabadilisha ni mbinde, bora hata nikiwepo nitamhimiza au nitabadili mwenyewe, nikisafiri nikarudi nakuta shaka zinanata, mito Sasa imejaa michoro ya udenda inanuka, nje Sasa ni mrembo wanja mrefu na lipstick unasema mwanamke si huyu hapa
Mdau 20: SIDHANI KAMA NITAOA WALA KUAMINI MWANAMKE TENA: Nilikuwa na mali nyingi, nilimpa mke kila anachotaka lakini haridhiki, nimeshanusurika kufa na sumu marambili na sikujua kama ni yeye, aliponitumia majambazi wakakamatwa ndio nikamgundua, Nimemuachia kila kitu nimeanza upya lakini bado akanitelekezea watoto na mapaka Sasa anatafuta habari zangu sijui nilimkosea wapi
SEHEMU YA MWISHO
MEN CONFUSED WITH MARRIAGE
Mdau 21: Mke wangu ni mhamasishaji wa malezi ,tena watu wazima wenzake humuita mama maana anaonekana bonge la role model lakini ni FAKE FAKE FAKE, Tuna watoto wanne lakini hakuna wanachojifunza kutoka kwake, madhaifu magomvi kati yetu yote anawashirikisha watoto, Ananiongea vibaya kila sehemu, Tuna mabinti wawili na vijana wa kiume wawili sasa sijui watakuwa waume au wake wa namna gani maana anawafundisha unafiki tu embu badilikeni nyie sijui influencers, counselors mnasaidia watu nje na kuonekana wa maana ndani mko very broken. Mtu unafundisha msamaha lakini wewe husamehi, malezi na haulei ipasavyo SHAMEEEEE.
Mdau 22: Washikaji 😂 sijui nani alimuambia mke wangu kuwa yeye ni mbaya kwa rangi yake , Nimemuoa na chocolate color baada ya muda akaanza kujipaka vipodozi kwanza vinavyonuka humo chumbani mimi nafanya kutoka , baada ya muda anafanana na vigingi vilivyounguzwa, kajichubua For real ananiiritate sana mpaka sina nguvu ya kusimamisha akivua nguo napata hasira sana bora hata gizani.
Mdau 23: Mimi nilikuwa mume na baba bora, nilihudumia familia yangu ipasavyo, Bahati mbaya tukapunguzwa kazi, ikabidi mke wangu aanze kuhudumia maana ana kazi nzuri tu, sasa ananifanyia visirani sana, ananinyima tendo la ndoa, kibaya ananinyima chakula 😭😭😭😭😭 amesahau ghafla hata kazi nilimtafutiaga mimi, anasema mitandaoni mnajifunza kutomuendekeza mwanaume.
Mdau 24: Inauma sana nilinusurika kuua watoto ,nashukuru rafiki yangu alikuja kunikimbiza na kunipeleka kwa counselors, ni baada ya mtoto kuugua akahitaji transplant kupima nikajua sio wangu, nikaenda kuwapima wote Wallah sikuamini watoto watatu wote sio wangu kumbe mwanamke ana bwana ake walikula yamini wazalishane baada ya yeye kukataliwa upande wa yule jamaa, wanawake hii dhambi itawagharimu sana.
Mdau 25: BADO HAMJASEMA, 😆😆😆😆 Mimi nilikuwa nalipa kodi kwa miaka 7 kwa mwezi laki 5 kumbe nyumba ya wife aliijenga kimyakimya, siku niliyogundua uume uliparalize miezi 6 hata ile dinda ya asubui haipo wanawake salute kwenu, kwakweli nimeshindwa kumsamehe nimeshaachana nae yuko analialia tu baby nilitaka nikusuprise, suprise gani ile wadau?
WADAU WENGINE:
👉🏻hapigi mswaki alafu anataka romance
👉🏻Mlevi na hukoroma
👉🏻Mvivu
👉🏻Hanisaidii kufanya hata followup ya watoto kimasomo yupo tu kama boga lililochacha kila kitu nifanye mimi sijui usaidizi wake uko wapi
👉🏻Mbea kusutwa mtaani kutwa
👉🏻Anapenda vigodoro ananitia aibu
👉🏻Mdhulumaji anakopa watu wanafwata vitu ndani nikipita wanasema mume wa tapeli yule
👉🏻Anazurura hiyo kama Kala miguu ya kuku na hana cha maana anafanya
👉🏻Ananiibia pesa kwenye wallet ,suruali
👉🏻Anapenda maisha makuu wakati uwezo wetu hauruhusu
👉🏻Ananivizia nikilala anakagua simu, ananigusisha fingerprint anachokitafuta atakipata siku
👉🏻Hajui kubana bajet ukinunua samaki ni mpaka ziishe ndio atabadili mboga, hajali kabisa maana sio yeye anahudumia.
👉🏻unamnunulia mtoto nguo ya elfu 70 anamvisha nyumbani baada ya siku 2 hana nguo za kutokea hazifai mradi tu awatikise majirani
👉🏻Hana shukrani jamani, hata ummpe nini, na kunifafanisha na wanaume wa majirani na mitandaoni
👉🏻Nilimfuma akisoma content inasema how to kill your husband silently Eee mbona nikakimbia
SIO VIBAYA KUSOMA BILA KUNYOOSHEA MTU KIDOLE, ILA KUJITIZAMA MWENYEWE NA KUKUBALI KUBADILIKA PALE UNAPOONA PAMEKUGUSA, ILI KUPONYA NDOA ZETU. MAANA HIYO NIMETOA MAHALI NA KUIPENDA MAANA IME COVER MAPUNGUFU MENGI SANA. KAMA HUJAGUSWA, BASI SAIDIA NA WENGINE.
NDOA IHESHIMIWE NA WATU WOTE. HII NI MPAKA WANANDOA WENYEWE, TUNAPASWA KUHESHIMU NDOA ZETU.
0 Comments:
Post a Comment