“Ni nini kilitokea, Bale?” “Mama alifariki na kansa ya
mapafu. Ila baba na mdogo wangu, walikuwa na bibi pamoja na mtoto mwingine
alikuwa akilelewa na bibi, walikufa siku moja. Mimi nikiwa nimeshiriki
kuweka mipango ya kuchoma moto mali za baba, nikidhani niliyekuwa nikiweka naye
mipango hiyo tupo pamoja. Kama kumfundisha baba yangu adabu kwa kumkumbusha
alikotoka. Kumbe mwenzangu alikuwa na nia nyingine kabisa. Alikusudia kumtoa
baba yetu hapa duniani, ili yeye ammiliki Naya atakavyo!” Akazidi
kumchanganya Vai, ila akawa mvumilivu kusikiliza.
“Kwa hiyo vijana waliotumwa kuchoma gala ya baba tukidhani
au nikidhani ni utajiri aliopata kutoka kwa huyu mume wa Naya, Joshua, kama
njia ya kumrubuni baba atoe baraka zake amkabidhi Naya kwake kama mke, mpaka
kumuozesha kwake na si Malon mwanaume wa kwanza wa Naya, ambaye ndiye
tuliyekuwa naye kwenye hiyo mipango ya kumuangamiza baba. Mimi nikidhani
hao wachomaji wamepewa maelekezo ya kuchoma tu hilo gala, kumbe walikuwa
na maagizo ya tofauti kutoka kwa Malon.” “Kwa hiyo ukaja kugundua baba yako hakuwa
amehongwa hizo mali ikiwepo hilo gala ili kumuozesha Naya?” “Hapana aisee Vai! Kumbe
mzee alikopa. Na nilibidi kuja kulilipa hilo deni kubwa sana. Na si kwamba
alipewa na Joshua, ila Joshua alimuunganisha kwa mtu mwenye biashara
kama hiyo. Ndio wakawa wakimpa baba mazao, anauza, asilimia fulani ya mauzo,
analipa deni huku akijiendeleza. Niliumia Vai! Sina jinsi nikaeleza mtu
akaelewa. Lakini ikawa ni mjukuu wa majuto. Nimechelewa, nishafanya uharibifu.”
“Nilimpokonya baba tonge mdomoni. Kitu alichokuwa akifunga
na kuomba kwa muda mrefu sana, akimsubiria Mungu kwa unyenyekevu
bila kutaka kuharibu mahusiano yake na Mungu, kama mimi nilivyofanya
mabaya mengi ili kupata pesa kwa haraka mpaka kuuza bangi niliyojua inadhuru
watu, lakini pesa yake ya haraka. Nilikuwa na pesa Vai! Asikwambie mtu. Pesa haswa.
Lakini sikuwa nikilala kwa amani na usingizi mzuri, kama nilivyokuwa
nikilala nyumbani kwa baba yangu nilipokuwa nikipadharau, na kupaona fukara. Ule
usingizi haujawahi kurudi tena Vai. Na nilipata yote niliyokuwa nikihangaikia,
tena kwa haraka sana, ila nikapoteza ndugu, furaha na amani.”
“Kweli nilimpita mbali sana baba kimaendeleo. Yaani hilo
deni alilokuwa akidaiwa, la biashara tuliyoangamiza, nililipa kama mchezo tu,
mpaka wenyewe hawakuamini. Maana baba yangu alitaka kulilipa taratibu kwa
kadiri ya uwezo wake, hakutaka kona kwenye maisha, akaomba wampe muda. Wakakubaliana
hivyo na yeye akawa akiwalipa kutokana na anavyopata pesa.”
“Vai, baba yangu alimpenda Mungu mpaka kero kwa mtu
unayemfahamu kwa undani. Alitulia akimsubiria Mungu kwa kila jambo,
wakati unajua kabisa, angefanya hiki au kile kwa kukata kona fulani fulani, angefanikiwa
kwa haraka na kutoka kwenye shida aliyokuwa nayo. Mimi nilishindwa
aisee. Nilimdharau kupita nitakavyokwambia. Nilimuona mjinga, mzubaifu
hajui mambo halafu hashauriki! Nikaamua kuachana naye. Kuondoka nyumbani
kuhangaika kivyangu, kumbe nikawa napishana na majibu ya Mungu,
utafikiri mimi ndiye niliyekuwa nikiyazuia wakati wote!”
“Yaani mimi natoka tu, ndio
mafanikio ya mali, si vinginevyo. Maana kwetu tulikuwa na kila kitu ila utajiri
ndio ilikuwa hangaika yangu mimi na mama nakupitwa na ile furaha,
amani na utulivu vilivyokuwepo pale nyumbani. Nikakosa wakati mzuri nyumbani,
wakati wote sisi ni vilio tukitaka ziada kwenye maisha. Mungu akiwa ndio
amemjibu, ameunganishwa na watu sahihi kumsaidia kufikia ndoto zake za muda
mrefu. Akiwa ndio amefanikiwa tu na mimi nikaingilia kati, tena
akiwa anahangaika kunitafuta, kunirudisha kwenye familia, ndio
mimi nikarudi kumuangamiza kabisa. Akiwepo huyo mdogo wetu, ambaye ni
kinyume kabisa na mimi pamoja na Naya. Mpole. Mtoto asiye hatia. Nikawaangamiza
kwa ujinga tu. Haraka zikinisaidia.” Bale kwa mara ya kwanza akapata mtu
wa kumsimulia upande wake wa maisha. Ila safari hii akikubali kuwajibika,
majutoni. Si kumtupia lawama zote Malon.
Alikiri kila kitu bila ya kuficha na kumshangaza sana Vai. “Bale!
Sasa Naya naye aliishia wapi?” “Kwanza hivi unavyoniona mimi, ndivyo Naya
alivyo. Tulifanana na mama yetu mpaka ukucha. Huu urefu ni wake mama. Lakini kujibu
swali lako, Joshua alimpenda sana Naya. Japokuwa alirudi akiwa amejeruhiwa
vibaya sana na Malon na hamkumbuki tena Joshua!” Bale akainama na kuanza
kulia.
“Pole sana Bale.” “Aisee hapa
duniani Mungu ana watu wake Vai! Kile kingekuwa kipindi cha Joshua
kumtelekeza au kututelekeza. Lakini yule mwanaume anampenda Mungu aisee. Ndiye mtu
wa pili mbali na baba yangu, nimemuona hapa duniani, mwenye hofu
ya Mungu. Japokuwa alijua kwa hakika tupo yatima. Hakuna anayemuangalia.
Hata mkewe hamkumbuki, Joshua alimchukua Naya, akamtibu na kumuweka
kwake mpaka aliporudi kumkumbuka. Na usifikiri ni siku chache!”
“Aliishi naye, Naya akiwa hakumbuki chochote
mpaka tena huyuhuyu Joshua alipokuja kuniokoa na mimi nikiwa nakaribia kufa. Sina
mtu! Nimeibiwa kila kitu. Huu mguu umeoza! Sina hata mtu wakunipa maji
ya kunywa, achilia mbali chakula! Nalala kwenye maboksi, nasubiria kifo, ndio
Joshua akaja kunitoa pale.” “Pole sana, Bale.” Bale alisimulia akilia kwa uchungu sana.
Akamsimulia Vai mpaka hapo alipo, Vai akabaki akimwangalia na yeye akikumbuka
ubaya waliomfanyia Nanaa wakati wakiishi naye. Akapoa haswa akishindwa
kumuhukumu, maana hawakuwa na tofauti kubwa na Bale.
“Imekua ngumu kurudi kuwa ndugu tena.” Mwanaume akajifuta
machozi na kamasi mbele ya huyo mrembo. Alishindwa kujizuia. “Undugu haufi
ila mahusiano.” Vai akaishia kusema hivyo, na kubaki akifikiria. “Natamani
majuto yasingekuwa mjukuu. Natamani kurudisha siku nyuma, niyaishi yale
maisha ya nyumbani tena. Hatukuwa na vingi, lakini tulikuwa pamoja. Hatukuwahi
kulala njaa. Hatukuwa tukila kama matajiri, lakini Vai, nahisi kile chakula kilikuwa
na mkono wa Mungu aisee! Tangia nimetoka nyumbani, sijawahi kula nikaridhika
kama pale kwa baba, mpaka nikawa nashangaa!”
“Nilikuja kushika pesa kama nilivyotamani. Lakini sikuwahi
kulala usingizi kama wa nyumbani kwetu, sikuwahi kutosheka. Unafikiri
unahamu ya kula hiki, ukila, unashiba, lakini hutosheki! Inakuwa ni kama
unayekimbiza tu upepo! Unalala umechoka, unaamka umechoka. Unaingiza
mamilioni ya pesa, lakini bado unahangaika kutafuta mamilioni ya pesa.”
Akamsimulia maisha aliyoishi akiwa na Malon mpaka kufika hapo, wakiwa wamekaa
hapohapo mezani bila kujali muda.
Ya Upande Wa Vai.
“Daaah! Unahistoria ngumu Bale!” “Husikii kukimbia?” Bale
akamuuliza. “Nitakuwa nikikimbia kivuli changu mwenyewe. Wala hatuna tofauti
sana aisee, mpaka nimeshangaa na kuamini, tabia huvuta watu wa tabia moja!
Unakumbuka nilikwambia Mungu aliwapa wanadamu akili ya kutengeneza viungo
vingine mbadala ya alivyoumba mwenyewe na vingine ameficha wanadamu
ufahamu. Kiasi ya kwamba unapewa na Mungu mara moja tu. Ukiharibu ndio umeharibu.
Unakumbuka?” Vai akauliza.
“Ulinipa wakati mgumu wa kutafakari!” “Uliweza kuelewa?”
“Ndiyo.” Bale akajibu akimtizama. Vai akatulia kwa muda kisha akacheka kwa
hujihurumia. “Yaani hivyo unavyotamani wewe siku zirudi nyuma, upate tena
nafasi na familia, basi mimi nilifika mahali nikiwa naishi na mwanaume,
ambaye nilitamani sana anioe, kumbe alishanigundua hata siku zangu sikuwahi
kupata tokea niwe naye. Na yeye kwao ni mtoto wa kwanza wa kiume na anategemewa
sana. Hawezi kuoa mwanamke ambaye hazai! Aliniacha Bale.” “Pole.”
“Acha aisee! Mtoto wa mwisho kumtoa, yule alikuwa mkubwa
kabisa Bale. Mkubwa wa kucheza kabisa namsikia. Lakini mwanaume
aliyekuwa amenipa ile mimba au mtoto wa mwisho niliyeua, alinidanganya
hajaoa, na angenioa. Akawa akinitunza vizuri na mapenzi yanayofanana
na kweli kabisa. Nikajiachia mpaka kushika mimba. Tukaja kugundua ni ujauzito
wa karibu miezi miwili. Nikamwambia, hakuonekana kushituka. Kumbe ni
baba wa familia yake, mimi nilikuwa mtu tu wa nje, hana mpango wa kumuacha
mkewe, na hana mpango wa mtoto mwingine.” “Sasa mlikuwa mkikutana wapi!?”
“Acha Bale. Kuna watu ni washenzi waliopitiliza
aisee. Na mtu husikia anachotaka kusikia, hata kama anaambiwa au
kuona tofauti. Ndio mimi. Niliona na kusikia kile akili ilitaka kusikia
na kuelewa kwa yule mwanaume, japo haikuwa kweli. Kumbe tulipokuwa tukikutana
wakati wote nikidhani ni kwake kumbe palikuwa kwa rafiki yake! Mimi
naenda pale mpaka nalala siku nzima! Kupika mimi siwezi. Na wakati ule nilikuwa
sitaki kazi yoyote ya mkono. Basi tunatumikiwa hapo, chakula tunakula
nje au kutuma kuletewa hapo ndani, kumbe sio kwake! Sasa alipojua nimeshika
mimba, si akaanza kunidanganya, eti amehamishwa kikazi hapa Dar, ameambiwa
lazima akaripoti Dodoma. Kwa hiyo anakwenda kuandaa mazingira yangu mimi na
mtoto wetu.”
“Kama mjinga vile, nikaamini. Akawa anatuma pesa,
mimi najua yupo Dodoma, kumbe tapeli yule yupo hapahapa mjini. Mawasiliano
yakaanza kupungua. Ukimuuliza anakwambia anakuwa vikaoni. Mchezo huo ukaendelea
huku mimba nayo inazidi kukua mpaka akapotea kabisa. Simpati kwa simu wala
ujumbe. Ndio nikarudi tena pale tulipokuwa tukikutana. Nikamkuta huyo
rafiki yake, ikabidi anieleze ukweli. Na akasema jamaa ana ndoa yake na
familia yakueleweka. Yupo mjini lakini mimi nishakuwa tatizo
ambalo hatakubali liingie kwenye familia yake. Akanimbia ofisi
anazofanyia kazi.”
“Ulikwenda?” “Nilikwenda Bale. Nilitaka tu kujiridhisha.
Nikamkuta ametulia tuli ofisini kwake. Sikutaka kesi nikajua tu nishatapeliwa.
Kwa hasira na haraka nikaenda kununua dawa zakua yule mtoto, nikiamini
mimba itatoka. Acha Bale. Mtoto aliniuma yule! Nusura kufa. Nilioza
mpaka nikawa natoa harufu, maana kuna vipande vyake vilibakia ndani. Vikaoza
mpaka kuharibu kizazi. Mama akanipeleka hospitalini. Ndio kusafishwa.” “Walitoa
kizazi?” “Sijui na wala sitaki kuhakikisha.”
“Ila kama nilivyokwambia, baada ya hilo tukio ndio nilikuja
kuishi na yule kijana. Ikawa tena tofauti. Mwanaume huyu anataka mtoto, mimi sishiki
tena mimba. Na tulikaa naye muda tu. Akanifukuza. Tena alinifukuza vibaya
sana, kwa kunirudisha nyumbani akinionya nisiwahi kuja kurudi tena
kwake, kwa kuwa sina uwezo wa kuja kumzalia watoto. Niliumia Bale! Niliumia
sana nikitamani hiki kingine kama ulichotamani wewe.” “Kwamba kama majuto yasingekuwa
mjukuu?” “Kabisa. Maana nilikaa kama mgonjwa kwa muda mrefu sana. Ila
nikifikiria pia nasema bora hakunioa, maana na yeye aliishia kufungwa jela.”
“Nini tena!?” “Aaah! Walisoma na kaka. Wakawa kundi kubwa la marafiki. Wakageukana
kama tu hivyo stori yako wewe ilivyo. Wakafikia hatua yakutaka kuuana. Ndio mwenye
pesa zake na akili, akawawahi kuwashitaki kisheria. Sijui tena habari
zake.”
“Ila ninachojua, nalipa garama yake Bale. Na huyo ni
mmoja, nikajitia kichwa ngumu. Nikajiingiza kwenye mahusiano na mwanaume
mwingine. Na yeye hakutaka hata twende mbali. Mapema, akaniambia anataka
kuanzisha familia. Tupime, tuanze kuzaa.” “Bila ndoa!?” Bale akashangaa sana.
“Acha Bale. Nimepita kwingi mimi! Kwa hiyo na kwa huyo japokuwa nilikuwa
nikipata siku zangu, na yeye akishuhudia, lakini mimba iligoma kabisa. Akasubiri
mwezi wa kwanza na wapili, akaniaga, wala yeye hakutaka kupotezeana muda
au kuzungushana. Akasitisha mahusiano kwa wazi kabisa.”
“Ikaniingizia hofu kupita kiasi. Nikashindwa kabisa kurudi
kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Nikaona nitulie tu. Kwanza nishafanya mengi,
sina nililobakiza. Nikakaa nikijifikiria. Mimi shule sina, kuzaa sitazaa
tena, halafu sina maisha ya kueleweka! Nikapiga mahesabu. Nikajua kimoja nishaharibu,
sina uwezo wa kubadili. Ila hivyo vingine, naweza nikajikaza nikafanikiwa.
Basi ndio wifi yangu akanikalisha chini na kuniuliza kama nilishawahi kuwa na
ndoto zamani. Nilipomwambia nilitamani kuwa daktari, akaangalia vyeti vyangu,
akazungumza na kaka, wakanirudisha shule. Kwahiyo ndio nimejificha hapo. Shule
iwe mkombozi. Nisikose vyote. Maana najua ndoa na maswala ya watoto imeshindikana.
Ila shule, hiyo nitapambana nayo mpaka kieleweke.”
Bale akabaki kimya akitafakari. “Nimekukumbusha watoto
ulioacha na wewe mtaani nini?” Vai akamchokoza kwa swali kama kumrudisha pale. “Mimi
katika upande huo, sikujaribiwa kwakweli. Nilifanya mabaya mengi, lakini
si wanawake. Na sijui kwa nini, aisee! Ni jambo ambalo halikuwahi
kuwa tatizo kabisa. Ila chuoni nilipata msichana. Tukataka kama kuanza hivi,
nafikiri akagundua mbali na muonekano wangu wa nje, sina kitu. Akaweka
mazingira ya wazi kabisa, kuwa hataki mahusiano ya kimapenzi kati yetu. Na
nafikiri hata yeye alichangia kwa asilimia fulani kutaka maendeleo ya
haraka.” “Kwa nini?”
“Kuna jinsi fulani hivi alinibadilikia, halafu
akaanza kuzungumza kwa mafumbo kwamba maisha ni zaidi ya muonekano. Kwamba watu
wanapenda kukimbilia kwenye ndoa, wakizinguliwa na muonekano wa mwanaume
mwanzoni na kusahau uhalisia. Wakishaingia kwenye ndoa, wakikutana na uhalisia,
wanaanza majuto. Sasa kwa kuwa na mimi nilitoka kwenye mazingira ya
familia kama aliyo zungumzia, nikamuelewa kwa haraka sana. Kukosekana amani
nyumbani kwetu sababu ya mama kulalamikia maendeleo au ufukara,
nikamuelewa kwa urahisi sana yule binti.”
“Japokuwa alikuwa mzuri sana. Mzuri tu, na kwa hakika
alivutiwa kwa haraka sana na mimi mpaka alipokuja kujua ufukara wangu. Nikamuacha
kabisa wala sikutaka tena ukaribu naye, akili nikahamishia kwenye
harakati ya kutafuta pesa, nikitaka nisiwe kama baba yangu. Kumbe bora
vile alivyokuwa baba, kuliko nilivyokuwa mimi. Kufanikiwa bila baraka za Mungu.
Kwa hiyo kujibu swali lako, sijawahi kuwa na mwanamke maishani. Nilijiona ni bora
niwe peke yangu, au niseme niliona matatizo niliyo nayo yanatosha, sikutaka
kukaribisha hata kwa bahati mbaya, fujo za mapenzi.” Wakatulia hapo kila
mmoja akiwaza lake.
Kuja kugutuka tayari nje kuna giza. Vai akasimama. “Nikusaidie
nini kabla sijaondoka?” “Hamna. Acha nikusindikize tu. Ila unakaribishwa siku
nyingine. Ukichoka kelele na chakula cha mtaani. Wewe niulizie nilipo, kama
nina nafasi, nitakupikia uje kula.” “Hiyo ofa sitaifikiria mara mbili. Na wewe
ukipika tu kingi kama hivi, ukajisikia huwezi kula. Wewe niite nije
kukusindikiza.” Bale akacheka sana.
“Mimi nakwambia ukweli.” “Basi acha nikufungashie chakula
kesho.” “Bora nipate sababu yakurudi nikijidai narudisha chombo.” Angalau
wakacheka wakizungumza hiki na kile mpaka Bale akamsindikiza kituoni. Wakafika tena
kituoni, wakakaa wakizungumza nakushindwa kuagana kwa haraka. Daladala zinakuja
na kuondoka, wao wamekaa tu.
Ikawapata hisia ya uhuru kati yao. Hakuna wakujificha kwa
mwenzie. Wote walikosa sana, hakuna wa kumuhukumu mwenzie. Hapakuwa na kujidai
tena kati yao. Wakakaa hapo mpaka wakagutuka kuona kituoni hakuna tena daladala
zinazopita. Wakaanza kucheka ndipo wakaanza sasa kusaka taksii.
“Si kwangu umepaona palivyo patulivu?” Vai akamwangalia
kutaka kujua anataka kuzungumzia nini! “Kipindi hiki cha sikukuu, karibu uje
usomee kwangu na mimi nitakusaidia kusoma. Ukimaliza mtihani wa tarehe 28,
tunapumzika angalau siku hiyo kwa kwenda hata kuangalia movie. Halafu tukitoka
nakusaidia tena kusoma kwa mtihani wa tarehe mbili.” “Kwako!?” Vai akauliza kwa
wasiwasi.
“Ndiyo, kwangu. Unakua na uhakika wa utulivu, na chakula
kizuri. Usiku nakurudisha chuo. Unaonaje?” Vai akatulia kidogo. “Itanisaidia na
mimi Vai. Nakua mpweke, sina mtu wa kuwa naye. Nakua peke yangu!” “Basi
nitakuja, Bale. Na asante kunikaribisha.” “Ulikuwa mwema kwangu wakati nikiwa
mkali kwako. Uliniokota na kunisafisha. Wewe ni rafiki mzuri Vai.” “Nimeshakuwa
rafiki!?” “Kabisa. Au hutaki?” Vai akacheka akijifikiria kisha akajibu. “Ujue
mimi ni rafiki mzuri sana?” Bale hakutegemea, akaanza kucheka.
“Umeona ujisifie mwenyewe?” “Acha nijiuze. Mbele ya kupikiwa
na kusadiwa kusoma!” “Usijiuze sana. Ushanunulika hivyo ulivyo. Kitendo cha
kujua maovu yangu bado ukabaki na kunitizama kama mwanzo, kimenifariji sana
Vai. Nashukuru kunisikiliza. Nilihitaji mtu kama wewe, wakunisikiliza
tu.” “Karibu. Muda na wakati wowote. Hata usiku ukishindwa kulala, wewe piga
simu kwangu. Na nikwambie ukweli Bale, fungua moyo. Naamini utakuwa sawa
tu. Usijikatie tamaa. Na wewe hujaharibikiwa kama mimi. Unanafasi kubwa
sana yakutengeneza na ukawa na maisha mazuri tu ambayo uliyatamani. Kwa kuwa
umegundua kosa na kwa kukusikiliza, nimegundua hutaki kurudia kosa. Utakuwa sawa
kabisa. Usiogope.” “Nashukuru. Na hayo uliyoniambia, usiache kunikumbusha Vai. Huwa
naingiwa hofu, nashindwa hata kula au kulala.” Wakaendelea kuzungumza wakitembe
kutafuta usafiri. Bale akalipia, ndipo Vai akaondoka na kumuacha Bale kwa mara
ya kwanza baada ya muda mrefu wa machungu, na furaha. Angalau ushauri wa Joshua
ukaanza kuleta matunda. Amejitengenezea rafiki wa kwanza.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
‘Nashukuru kwa ushauri na maombi Joshua. Nimefanyia
kazi. Mwanzo si mbaya. Nilifanikiwa hata kwenda gym.’ Hapohapo Joshua akampigia.
“Ulifikaje gym maana gari ilikuwa hapa siku nzima!” “Niliamua
kumuacha Lembo apumzike leo. Nikapanda daladala. Lakini Joshua, nimekua na
wakati mzuri sana leo.” Joshua akacheka. “Afadhali.
Hata kusikika, unasikika lipo tumaini. Ila nina wazo lakutaka uthubutu
wako.” “Nini?” Bale akauliza.
“Haya magari siku hizi tunaendesha na mguu mmoja. Kwa
nini usijiendeshe mwenyewe, Bale?” “Unakumbuka sina mguu wa kulia?” Bale akauliza kwa
masikitiko kidogo. “Lakini unao mzima, wa kushoto. Ni akili
tu. Unaweza kutumia wa kushoto na ukafanikiwa vizuri kama unatumia wa kulia. Umeshaona
jinsi watu wasio na mikono yote miwili na bado wanaweza kumudu mazingira yanayo
washinda hata wenye mikono miwili?” Bale akaanza kuhamasika. “Sitaki kukulazimisha, lakini nafikiri itakurahisishia sana
wewe kwenye mizunguko yako hapo mjini. Usafiri binafsi si jambo baya.” “Sasa
hata nikiweza kuendesha na mguu wa kushoto, napata wapi gari, Joshua?”
“Kuna magari hapa nyumbani hata tukitoka mimi na mke
wangu wote kila mmoja akatumia lake, na bado magari yanabakia. Kweli utakosa
gari hapa! Wewe ukiwa tayari mwambie Lembo tuwasiliane ili nizungumze na Naya,
amkabidhi akuletee gari. Sidhani kama hilo si tatizo.” Bale akapatwa ganzi
akabaki kimya. “Usiwe na haraka. Fikiria.”
“Naomba nianze kutendea kazi kesho. Lakini nianze
nikiwa na Lembo.” “Nitazungumza na mke wangu. Tukiwekana sawa, kesho
nitamwambia aje nalo kabisa. Hapo kwako pako salama. Na mwenye nyuma ana ulinzi
mzuri. Zungumza naye ulaze kwake ndani anapolaza magari yao.” “Nakushukuru sana
Joshua. Asante.” “Karibu na usiku mwema.” Wakaagana, Bale asiamini.
Siku Ya Kufa Nyani, Miti Yote Huteleza.
Jelini akatua Dar
majira ya saa tatu asubuhi, taksii mpaka nyumbani kwa Zenda. Getini
wanamfahamu, toto ya mzee, anapita bila yakusubiri. Jelini akawa amehamasika
kwelikweli. Alifika hapo na pochi tu. Anashida gani anazo nguo kwa Zenda kama
kwake tu.
Kumbe yeye akiwa
anahangaika usafiri ya jinsi ya kufika hapo kwa Zenda asubuhi kumfurahisha, Koku aliamka akataka cha
asubuhi. Zenda yupo usingizini, anasikilizia raha ya kunyonywa. Akadhani ndoto.
Akaendelea kufurahia ndotoni. Lakini kadiri Koku alivyoendelea kumnyonya, Zenda
akahisi fujo isiyo ya kawaida, unyonywaji wa Jelini una utamu wake na
ladha ya tofauti, si hivyo. Akafungua macho na kugundua kweli ananyonywa.
Harufu ya pafyumu ikamuingia kichwani akagundua ni Koku. Akashituka sana na
kuruka pembeni.
“Unafanya nini wewe!?”
“Jana hukuniridhisha vizuri.” Koku akajilalamisha kwa deko lakini akazidi
kumchanganya Zenda. “Unazungumza nini wewe!?” “Unakumbuka jana uliponiomba
tuje wote hapa, ukiomba nikusaidie penzi?” “Haiwezekani!” Mzee akahamaki
kwa mshituko mkubwa. Koku akacheka kumtuliza. “Nimalizie basi na mimi niende.
Nina hamu na wewe Kasa! Jana umenifanyia nusunusu si kawaida yako.
Nisaidie.” “Siwezi Koku. Sasa hivi nipo kwenye mahusiano. Siwezi kumsaliti…”
“Na jana nilivyokusaidia wewe hukuwa kwenye mahusiano, leo mimi nakuomba ndio
unaniletea jeuri! Kwani mimi nimekuomba ndoa?” Koku akamjia juu akimlaumu kuwa
yeye ni mbinafsi. Akiwa anataka yeye, huwa yeye Koku anaahirisha mambo yake na
kumfuata amridhishe. Lakini yeye anamuwekea ngumu!
“Sasa mimi nishafika
hapa, nimekutuliza jana, leo siondoki mpaka unikamilishie.
Usinifanye mimi mtoto mdogo hapa.” Koku akamjia juu. “Ila naomba leo iwe mwisho
Koku. Tafadhali. Nimekusudia kutulia na Jelini tu.” “Unaongea sana Kasa.
Utatumia muda mrefu kuniamsha tena. Acha kufikiria kesho. Kwani jana
ulipanga kuwa na mimi? Lakini mbona uliniomba na nikakubali
kukukamilishia? Saa iweje unalalamikia jambo ulilotaka mwenyewe? Tulia
tufurahie, hii si adhabu.” Basi Koku akaanza kumuamsha mzee.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Huku Jelini akafika.
Jumba la Zenda kubwa kama hekalu. Mbaya kwake Zenda, Koku hakuweka alamu.
Jelini alipofungua mlango mkubwa bila kelele, akajua Zenda ameamka. Akanyata
mpaka sebuleni. Akavua nguo zote akicheka akijua ataweka furaha
asubuhi hiyo kwa mpenzi wake, maana Zenda alikuwa na likizo ambayo anarudi
kazini tarehe 5 mwezi wa kwanza. Ilikuwa Jelini akirudi mjini, wakajifungie
mahali siku tatu ndio Zenda arudishe akili kazini. Na walisubiria hizo siku
tatu kwa hamu sana.
Basi Jelini akiwa
uchi kama alivyoletwa na mama yake hapa duniani, ila ameshikilia matiti, na
tabasamu kubwa usoni, akaendelea kunyata mpaka kwenye korido ya karibu ya
chumbani kwake Zenda. Akasimama maana hapo nje ya chumba palikuwa na sebule ndogo
tu. Pazuri sana kulikosheheni thamani za hali ya juu mno lakini na kabati kubwa
lenye vitabu.
Kabla hajaingia
chumbani Jelini akaanza kusikia sauti za mapenzi. Kwa haraka sana akahisi Zenda
anaangalia movie. Lakini kadiri alivyoendelea kusikiliza akisogelea
kitasa cha mlango kwa kunyata na tabasamu akagundua sio sauti ya kutoka
kwenye tv, ni kama watu waliopo ndani wakifanya yao. Tabasamu ikaanza
kupotea kadiri alivyoendelea kusogea na kusikia sauti ya mdada akilalama
kimahaba. Jelini alishituka, akahisi anaota.
Kwa haraka sana,
akili ikamtuma akimbie hapo kabisa ili wasimuone na yeye asije shuhudia
Zenda akimsaliti. Akataka kuondoka ili baadaye Zenda hata aje amdanganye
hakuwa yeye, lakini miguu ikashindwa kunyanyuka kabisa kama iliyokufa ganzi,
lakini sasa imekakamaa au umegongelewa misumari. Kuondoka anashindwa,
kufungua mlango hawezi anasikia Zenda anavyofurahia mchezo, na
mdada anavyolalama.
Jelini alisimama pale
kama aliyeadhibiwa na kuambiwa, ukisogea tu, nakuchapa, SHUHUDIA. Basi
akasimama pale nje akisikia kila kitu, machozi yakimtoka. Akahangaika
mpaka akafanikiwa kukaa chini kabisa, akakunja miguu na kuinamia magoti
akijaribu kufunga masikio, asisikie. Ikawa tena kama kuna nguvu ya ajabu
imemkamata, anatetemeka na kulia kwa uchungu sana. Jelini alilia kwa kwikwi
huku ameficha uso wake katikati ya mapaja na kuziba masikio.
Zenda anamalizia
kupiga bao na kujitupa pembeni akihema kwa mechi nzito, maana Koku mashine
kubwa haswa. Alijaliwa maeneo mengi tu. Mla chips yai lazima uchemke kwa mrembo
Koku. Sasa Zenda mfanya mazoezi kila siku, chakula bora kila mlo, alishamjulia
zilipendwa wake. Alijua wapi ashike, mchezo upi acheze ili kumuingiza kwenye
ulimwengu wao. Hapo Zenda alikuwa hoi, ametoka kujituma kweli kweli, Jelini akisikilizia fujo zao, amejitupa kitandani
akihema haswa.
Wakiwa wanatulia hapo
kitandani, kila mmoja pumzi zikianza kurudi kuwa za kawaida, wakasikia kama mtu
analia. Wote wawili wakatulia. Wakaangaliana. Kile kilio kikaanza
kusikika sasa bayana, maana si mchezo umeisha! Magoli yashafungwa,
washangiliaji wameondoka na kombe, kiwanja shwari. Sasa, sauti iliyobaki hapo
ni ya shabiki ambaye timu yake imefungwa. Hasibu wake ndio kaondoka
na ushindi. Ile sauti ikasikika mpaka kwenye moyo wa Zenda.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ni nini Kitaendelea?
Nani kawa surprised?
Usikose Muendelezo……..
0 Comments:
Post a Comment