“Mimi ni muwazi na
sitataka unipotezee muda kwa kuninyima raha.” Zenda akawa mkali wala asione
aibu mbele ya mama Jema. “Jinsi unavyomshika na kumfunika Jelini sipendi na SITAKI.
Hata kukuona hapa mara kwa mara sifurahii, naona unazidisha! Sijui kama
unanielewa?” Kimya. “Jelini ni jukumu langu mimi, naomba ibakie hivyo na wewe
uliheshimu hilo, maana nilishakupigia simu kukuulizia juu yake, ukajiweka
pembeni. Ibakie hivyo. Unanielewa Colins?” “Kwa hiyo siruhusiwi kuja kumjulia
hali mtu ambaye anaumwa!? Jelini yupo na maumivu, yaani ulitaka mimi nisijue
maendeleo yake! Siwezi.” Mpaka Jelini akashangaa. Maana alitegemea Colins
angekata tamaa, akaondoka! Lakini bado yumo tu!
“Kwa nini?! Na wewe
kama nani kwake?” “Nafahamiana naye, na nasikia uchungu akiwa kwenye
maumivu.” Mpaka mama Jema akashangaa ila moyo wa Jelini ukashituka na kujawa
furaha ya ajabu. Hakutegemea kumuona Colins bado anapambana kujieleza kwa wazi
vile mbele ya mzee Kasa, wala hakubabaika wala kuondoka kirahisi ila kueleza
hisia zake! Akajawa na furaha japo mwenzie yupo matatizoni.
“Lakini sivyo
ulivyoniambia siku nakupigia simu kukuulizia juu ya Jelini! Unakumbuka?”
“Ndiyo. Lakini..” “Usinipotezee muda wangu. Kuwa na msimamo. Acha kutuyumbisha.
Sitakuruhusu, na sitaki kukuona tena kuja hapa. Haya ondoka.”
Colins akamuangalia Jelini, akakuta akimtizama.
“Na ninakuonya,
usimguse wala kusogelea kitanda chake. Hapo uliposimama, iwe ndio
mwisho. Hatua ingine utakayopiga, iwe ni ya kutoka kwenye hichi chumba.” “Ugua
pole Jelini.” Colins akatoka. Pakazuka ukimya hapo, Zenda akasimama pale
alipokuwa amekaa na kuingia bafuni.
Raha Ya Penzi, Kupendwa.
Jelini akabaki pale
kitandani akitafakari. Baada ya muda Zenda akatoka. Jelini akamuita na kumshika
mkono vizuri. “Usikasirike, utakuwa na siku mbaya leo. Naomba tulia.”
Akamzungumzisha taratibu, kwa upenzo na kumshangaza zaidi mama Jema jinsi
Jelini alivyotulia. “Leo wanakupunguzia dawa kali.” “Nashukuru kuwa na mimi
hapa. Asante. Najua unachoka, hulali vizuri. Naomba nitoke hapa Zenda,
nikajiuguze nyumbani na wewe upate masaa ya kulala na kufanya kazi vizuri.
Tusikwame wote kwenye swala moja la ugonjwa.” “Acha nitazungumza na madaktari
tuone.” Jelini akambusu ule mkono.
“Tutakuwa sawa Zenda.
Usiwe na wasiwasi.” “Una uhakika?” Mama Jema akashangaa hilo swali! “Kwa
asilimia zote. Naomba utulize mawazo hapa nilipo mimi.” Akabaki
akimwangalia, ila akajua anatulia. Mama Jema akatoka kama kuwapa nafasi. Zenda
akashukuru. “Nahisi nimekumisi Jelini. Hatuzungumzi! Hata nikiwa hapa
huniangalii! Nikileta zawadi pia huna habari nazo!” “Mimi nakutaka wewe
Zenda, kuliko chochote kile utakachonipa. Na ndio maana ukiwa hapa mimi
nalala usingizi mzuri nikijua Zenda wangu yupo.” Hayo maneno yakawa faraja kwa
Zenda aliyekwisha tishwa na Colins.
“Nitatoka na tutakuwa
wote. Pole.” “Ukitoka hatutakuwa wote Jelini!” “Kwa muda tu mpaka niwe sawa.
Nahitaji msaada wa mama, wewe ukiwa kazini. Sijui nitakuaje bila hizi dawa na
wakinitoa hii mirija ya haja ndogo. Sijui kama nitakuwa na kizunguzungu au la!
Lazima niwepo na mama kwa muda mpaka niwe sawa. Nikijisikia vizuri tunaendelea
na maisha yetu, kama kawaida. Usiwe na wasiwasi.” Akatulia kama anayefikiria.
“Nenda kazini, na
ukatulize akili. Kila kitu kitakuwa sawa.” “Nataka ubadili namba ya simu ili
Doro asiwe na mawasiliano yako. Anakutafuta sana na jumbe zake kwako ni za
kukushawishi vibaya.” Jelini akashangaa amejuaje! Zenda akajua. “Ninayo
simu yako. Na Gumbo sijui nani, hao wanaume wa huko baa wanakutafuta mchana
mpaka usiku wa manane! Hapana Jelini. Mimi hivyo SITAKI.” “Basi kweli
tubadili namba. Na nini tena?” Akamuona anafikiria na kusita.
“Ni juu ya Colins?”
“Kwani ni nini kinaendelea kati yenu?!” “Wala hapana stori ndefu. Usiwe na
wasiwasi.” “Mimi nina wasiwasi Jelini. Anakuganda kupita kiasi bwana!”
“Colins anaye mchumba wake. Na hata mimi aliniambia kabisa. Wapo serious. Ni
mwaminifu kwake, hawezi kumsaliti.” “Usiseme hivyo Jelini! Hujamuona jinsi
alivyokuwa hapa na wewe.” “Nafikiri Colins ni wale watu, watoto wa mama. Wanahuruma
zile za kupitiliza. Sidhani kama ni nia mbaya.” “Sitaki huruma zake
kwako.” “Ulishamfukuza, sasa unawasiwasi gani?” “Naomba na wewe uwe na msimamo
naye. Tafadhali Jelini. Ajue wewe huna nafasi yake.” “Sitakusaliti
Zenda. Tafadhali naomba uniamini.” “Nitakuona baadaye. Na wakikuruhusu nitakuja
kukuaga.” “Sawa. Ila ujue nimefurahia umeniuguza. Sitasahau Zenda. Asante.”
Zenda akainama na kumbusu mdomoni, juu tu. Akaondoka.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mama yake akarudi.
Wakaanza kucheka taratibu. “Kazi ipo.” “Namuhurumia Zenda wangu. Sitaki
awe na wasiwasi.” “Lazima. Ungemuona huyo Colins!” “Kwani alikuwa akifanyaje!?”
“Mmmh! Tutakuja kukusimulia mimi na Jema. Alikuwa akija hapa asubuhi, mchana na
jioni.” “Colins!?” “Unafikiri kafukuzwa bure? Alijaa hapa na akiingia hapa
utafikiri hakuna mtu mwingine ila wewe tu. Na anavyokugusa!” “Mimi siamini!
Maana yeye alikuwa chaguo langu la kwanza, wala sikudanganyi mama yangu. Colins
nilimpenda kutoka moyoni wala sitaona haya kusema.”
“Nikawa nikimuona au
tu ile kumfikiria, napatwa na hisia za ajabu sana. Nasikia raha ile tu kujua
yupo mtu kama yeye hapa duniani. Nikawa namuwaza mchana na usiku, siwezi kujisaidia.
Nikajisikia kumpenda kupita kiasi na haikuwahi kunitokea kabla! Mpaka nikawa
najishangaa!” “Jelini!” “Wala sitakuficha mama. Na hivi unanihangaikia hapa, bora
tu nikwambie ukweli. Kwa mara ya kwanza, japo nazungukwa na wanaume na
natongozwa na wengi, moyo wangu ukampenda sana Colins. Sasa
nikajidanganya kutokana na kutongozwa kwingi na wanaume, nikisifiwa uzuri wangu
mchana na usiku, nikajua itakuwa hivyohivyo kwa Colins, atavutiwa na mimi.
Lakini ikawa kinyume kabisa! Aliniambia hata nisimsogelee anaye
mchumba wake! Niliumia mama! Niliumia sana.”
Akashangaa na machozi yanamtoka. “Moyo uliniuma
kama niliyekuwa nikikatwa moyoni. Pombe ikanisaidia kuweza kulala. Maana kila
nilipokuwa nikimfikiria yeye yupo hapa duniani, na si wangu, halafu hanitaki!
Nilikuwa nikiumia sana.” “Pole mama yangu.” Jelini akacheka na kufuta
machozi.
“Lakini mama, pia alizidi
sana kunivutia na kuweka shauku mpya ya mimi kupata mtu wangu.
Nikajiambia inamaana unaweza kupata mwanaume mzuri vile. Msomi na mwenye
maendeleo kama Colins, na bado akawa muaminifu! Ikanigusa sana. Mbali na
Jema na yeye akaongezeka kwenye kichwa changu. Kwamba si watu wote ni
malaya.” “Na kweli. Maana si angeendelea tu na wewe huku akiwa na
mwanamke wake?” “Sawasawa. Ila kitendo cha kunikataa mimi sababu ya mahusiano
aliyokwisha kuwa nayo, na mimi najijua si mbaya, kiliniuma sana. Ila
nikajiambia si wanaume wote au watu wote ni malaya na Colins ni kama
Jema.” “Mbona humtaji na James?”
“Mimi nawajua
wanadamu kwa kuishi nao mtaani mama. Wakiwa hawana macho ya watu wanao wafahamu
kwa karibu, ila washikaji tu ambao wapo huru kufanya chochote mbele yao.
Wanafanya mambo ya ajabu, lakini ukiwakuta kwa wenza wao au nafamilia
zao, hutaamini kama ni wale wanaume wanao vuliwa suruali na malaya popote.
James simjui kiundani ila kumsikia tu. Jema nimeishi naye, nimeyaona
matendo yake akiwa hana pesa na anayo. Na Jema ni mzuri mama. Anavutia, mtoto
wa mjini. Kitendo cha kuepuka vishawishi na kujituliza vile, amenigusa
sana. Na namsemea Colins kwa kuwa alikataa hata nisimsogelee japo wenzie walibabaishwa
sana na mimi, mpaka mtoto wa Zenda, lakini Colins alibaki kuwa mwaminifu kwa
mpenzi wake. Aliniumiza sana, lakini pia alinigusa sana.”
“Na kweli Zenda pia alishampigia simu kumuuliza
kama ananifahamu. Akanikana! Sasa iweje aje, ajae hapa amchanganye Zenda
wangu?!” “Mimi sijui kinachoendelea kwenye kichwa chake Colins, lakini mmmh!
Lipo jambo!” Jelini akabaki akifikiria, ila moyoni kufurahia kumuona Colins
kuwa amejali kuugua kwake na amekuwa akienda kumuona. Akafurahia, ila akajionya
kwa haraka, kujiongeza zaidi ya pale juu ya Colins. Asije kuharibu kwa
Zenda.
“Kama kuna watu
wanaweza kuwa waaminifu, na mimi nataka kuwa miongoni wa hao waaminifu mama. Si
kwa ajili ya Zenda tu, hata kwa ajili yangu mimi mwenyewe. Nitakana
nafsi yangu kama Jema na yeye mwenyewe Colins, ili na mimi niongezeke kwa hao
wachache waamini.” “Kweli Jelini!?” “Kabisa mama. Mimi sijawahi kuwa kwenye
mahusiano kama hivi mimi na Zenda. Na kama Colins angenikubali yeye kwanza, kwa
hakika nisingekuwa na Zenda hata iweje. Lakini alinikataa, sasa hivi nipo na
Zenda, nitabaki kwake Zenda. Japokuwa nampenda san.…” Akasita. “Sitamsaliti
Zenda kwa yeyote yule. Mimi nitabaki kuwa mwaminifu tu.” Jelini
akajithibitishia, mama yake akimsikiliza huku akashangazwa naye. Hakuwa akimjua
Jelini kwa namna hiyo. Alishajua ni mtoto aliyeshindikana vibaya sana na
hatengenezeki tena! Akabaki kimya akitafakari.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Jelini akaruhusiwa,
Zenda ndiye alilipia garama zote, mama Jema akashukuru, wakarudishwa nyumbani, Zenda
hana raha. Kila akimkumbuka Colins na aliyokuwa akimfanyia Jelini, huko
nyumbani asipomuona si ndio atahamia! Kuanzia Jelini anaondoka hapo
hospitalini, mzee roho juu, Jelini hana habari. Anafikaje nyumbani kwao na
kuhakikisha hakuna anayemsogelea! Hawezi. Alishindwa hata kumpa simu
yake. Akabaki nayo. Wala Jelini hakumkumbusha simu yake. Akamuacha tu ili
kujaribu kumtuliza.
Alipofika nyumbani
kwao yeye akapitiliza chumbani, kitandani, usingizi. Ilipofika jioni ya saa
kumi na mbili, dereva akaja kuleta simu. “Nimetumwa kumuangalia na kama
mnahitaji kitu chochote.” “Tokea afike hapa, hajatoka kitandani zaidi ya kwenda
chooni. Na naona hapa tupo vizuri, hakuna uhitaji. Tunashukuru.” Mama Jema
akajibu kwa shukurani. Devi akaondoka kurudisha majibu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Jioni yake kina mama
G na Nanaa wakaleta vyakula hapo ilimradi tu kuonekana wapo na hiyo familia.
“Ibakie kazi ya kuuguza tu lakini isiwe tena unafikiria kupika. Mpaka
vitafunywa tumekuletea. Vitakusogeza.” Mama Jema akashukuru sana. “Kwani huna
msichana wa kazi?” Nanaa akamuuliza kwa kujali. “Siwezi. Nilishindwa.
Nilijaribu kuweka mmoja wakati huyu Jelini mdogo, nikashindwa.” Wakaanza
kucheka jinsi alivyojibu.
“Hakika nilishindwa.
Niliona amejaa humu ndani, nina kazi ya kumfundisha tu, halafu haelewi wakati
mimi nina watoto wawili wakufundisha pia. Nikaona kazi moja ambayo ningefanya
mimi mwenyewe kwa dakika 5, inachukua masaa! Unaelekeza. Halafu inakosewa.
Inabidi kurudia! Nikamtoa haraka sana, nikabakia na wanangu. Kuanzia wakati
huo, sijatafuta tena mtu. Labda nje tu. Ila ndani, ni mimi na wanangu tu.
Sitaki kero. Nimebaki kusikiliza visa visivyoisha vya dada yangu na wasichana
wake wa kazi. Kwake kunapita kila kabila na vijambo! Mimi hivyo siwezi.” Kwanza
mama Jema mwenyewe alionekena mtu wa kazi. Mwepesi haswa kwa kumtizama tu
haitaji msaada wa mtu kumpikia chai. Wakaendelea kuzungumza wakicheka, mwishoe
wakaondoka na kumuacha mama Jema na faraja. Ukweli mahusiano hujengwa.
Wakaanzisha kitu kingine kati ya mama G na mama Jema.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Akampigia simu Jema
kumwambia. “Basi nikitoka kazini nakuja na mimi kula.”
“Jema!” “Sasa vyakula vyote hivyo si vitaharibika mama na wewe!” “Wameviweka
vizuri na kupanga kwenye friji. Nenda kapike kwako, mumeo ale.” “Wala usiwe na
wasiwasi. Nitamwambia mkweo usiku tukutane hapohapo kumuona Jelini kumbe nataka
niponee kwako. Wewe tuandalie. Tukija tunakula, anaenda kwenye mambo yake, mimi
narudi kwangu kulala tu. Kesho naenda kazini mwepesi.” Akawa kama
amekumbuka tena kitu kingine.
“Tena
nifungashie na sambusa pamoja na vitumbua vya kunywea chai kazini, sitaki
maandazi.” “Jema wewe mtoto! Na utataka na vya mumeo!” “Mama naye? Sasa unataka
mkwe akanywee chai nini?”
Mama Jema akakata simu, Jema akabaki akicheka.
Mapenzi.
Juma hilo likaanza
kuwa zito kwa Zenda, mikono, akili, macho na moyo vinamtaka Jelini. Jelini hana
habari analala asubuhi mpaka asubuhi. Ukali ukazidi huko kazini, hakuna
kinachoenda sawa. Anagomba kuanzia anaingia mpaka anatoka jioni. Akawa kama
mwehu. Kwenye mazungumzo ya Devi na dereva wake yeye mwenyewe Zenda ndipo Devi
akagundua hiyo hali. “Mimi nahisi ni mwanamke wake. Ananituma kwao kila
wakati!” “Sasa kabla wote hatujakosa kazi, akafunga kampuni, tafadhali nenda
kazungumze na Jelini.
Kabla hawajaenda
mbali kwenye mazungumzo yao, simu ya Zenda ikaingia. “Huyu hapa.” “Aisee pokea
kwa haraka.” Devi akasimama kama anayemuona. Bila ya salamu, akamwambia aende
akashinde hukohuko kwa kina Jelini na awe anamwambia kila anayefika hapo.
Devi akahamia
nyumbani kwa mama Jema asiseme alichotumwa. Sasa mama Jema akawa anashangaa
Devi haondoki! Amekaa tu. Mama Jema akamuhurumia. “Hapa hakuna kazi Devi. Nenda
tu kapumzike.” “Yule mzee atanipiga bastola, aniue.” Mama Jema akawa hajaelewa.
“Nimeambiwa nikae
hapa mpaka mnakwenda kulala.” “Ukifanya nini!?” “Mama yangu acha tu. Hapo kwake
kuna vunjwa vitu vya thamani mchana na usiku. Nikikwambia vitu vya thamani ni
thamani zile za mapesa mengi. Meza za vioo na marembo ya glasi yale mazuri
haswa. Anapasua kwa hasira kwa jambo dogo ambalo hakuwahi kuwa na tatizo nalo
kabla. Kashafukuza wafanyakazi wake wa ndani na wa nje wote. Hakuna sababu.
Nasikia huko kazini hali ni mbaya. Amekua mkali kuliko pilipili, japo mwenyewe
pia ni mkali, lakini nasikia vimezidi. Sasa watu wanahisi ni sababu ya Jelini.”
“Makubwa! Sasa si aje amuone!” Devi akacheka.
“Mama wewe hujaelewa.
Mimi nipo hapa kulinda pia. Mzee wivu. Hataki mtu amsogelee Jelini. Sasa
na hivi hata simu zake hapokei! Akiniuliza namwambia dada Jelini anakuwa
analala tu, ndio akiamka wakati anakula ndio anaweza kupiga simu, anazidi
kuchanganyikiwa.” “Basi kazi ipo!” Jelini akiwa usingizini akasikia hayo
mazungumzo, akaamka na kusikia kila kitu, akatoka chumbani. “Acha niende
nikamtulize mama. Namjua Zenda, atarukwa akili.” “Sasa utafanyaje na wewe
mgonjwa?” “Acha akaniuguze yeye mwenyewe ndio akili yake itamtulia.” “Unarudi?”
“Nitakaa kama siku mbili hivi. Nilale bila wasiwasi wa kupigiwa simu zake na
kuzikosa. Kesho ijumaa. Nilale na jumamosi, jumapili nitarudi.” Jelini
akajikusanya, akatoka na dereva.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Akajiegemeza kwenye
kiti, akalala mpaka nyumbani kwa Zenda. Alimwambia yule dereva asimwambie kama
anakwenda naye. Kwa hiyo alipomuamsha kuwa wamefika, ikabidi atembee mpaka
mlangoni. Akabonyeza kengele. Baada ya muda Zenda akafungua. Hakuamini
alipomuona Jelini. Bila salamu akaanza mabusu. Alimkumbatia nakuzidi kumbusu
hapohapo mlangoni. Devi alipoona hivyo akaenda kuegesha gari, siku ya kazi
akajua ndio imeisha.
Uchu wa Mapenzi.
Jelini alimsikia
jinsi anavyotetemeka huku akiendelea kunyonya midomo yake. Akamuacha tu kisha
akamvutia ndani na kufunga mlango kwa mguu. Akaendelea kwa muda akinyonya
midomo yake, kisha akamkumbatia tu bila hata kuvuka mipaka. Akatulia.
“Nilikumisi Zenda wangu.” Akazidi kumloga. “Unajisikiaje?” “Sio mbaya. Bado
natumia dawa kila baada ya masaa 8 ili nisisikie maumivu sana.” “Pole sana.
Nimefurahi umekuja kuniona. Nilikuwa nahamu na wewe, sikujua chakufanya.
Sikupati kwa simu kwa wakati, wala hakuna zile jumbe zako nzuri zinazo
niliwaza! Nipo mpweke kuliko nitakavyokwambia.” “Ndio maana nimekuja.” Akambusu
tena na tena ila juu ya mdomo.
“Naomba leo tulale
Jelini. Najua itakua ngumu kufanya mapenzi kwa kuwa unaumwa lakini angalau
nikushike tu.” Jelini akaanza kumchangamkia. Akaanza kumchezea mashine yake,
Zenda anagugumia asiamini kuwa hatimaye mikono ya Jelini ndio inamchezea.
Akalainika kama mtoto wa kike. Akamsogeza mpaka kochini, akamtoa suruali laini
aliyokuwa amevaa kushindia hapo ndani. Ndio aina ya nguo zake anazovaa akiwa tu
nyumbani. Akamwinamia na kuanza kunyonya huku akisikia maumivu ya kichwa, kisha
akamkalia. Zenda akamtoa kigauni cha juu na sidiria, akaendeleza kumpapasa matiti
na mwili kwa uchu huku penzi likiendelea. Kisha akamuinamisha kwenye kochi,
ameshikilia tako huku penzi likiendelea mpaka akamaliza. Akarudi kukaa
akamvutia Jelini kifuani, wakaendelea kuhema mpaka wakatulia.
“Asante kunifikiria
Jelini wangu. Nilikuwa na hali mbaya kimawazo! Naona imeshakuwa ngumu kuishi
bila wewe.” “Twende tukaoge, nilale.” Wakaoga bila mambo mengi, Zenda akijua
Jelini si mzima. Ila alifurahi sana kuwa naye usiku huo.
Lakini Motoni, Tui Hufura.
Zenda akamwangalia
akiwa amemlalia kifuani, ametulia Jelini tuli kama tui la nazi. Akambusu na
kumtoa Jelini mawazoni, akamrudisha pale, akacheka taratibu kama kumuonyesha
yupo naye pale. “Najua unajua kama Colins alikuja nyumbani. Lakini nilishindwa
kumuona.” “Acha kunichanganya Jelini! Ulishindwa kumuona!?” “Ni lugha
tu. Lakini nataka kukwambia hatukuonana.” “Najua.” Jelini akatulia.
“Na ilinibidi kumfuata
na kuzungumza naye.” Jelini alishituka mpaka akakaa bila kutarajia na ndipo
akaelewa ni kwa nini Colins hakurudi tena. Tui lishatiwa motoni, mkaa
umechochewa. Kumekuguswa pabaya, sirini. Jelini akasikia kumuhurumia Colins. “Unashituka
nini? Kwamba ulitaka awe anaendelea kukufuatilia?!” “Mimi nahisi umekuza Zenda.
Yule kijana…” “Unasema nini Jelini?!” Akauliza kwa ukali mpaka Jelini akatulia.
“Naomba tulia Zenda. Tulia.” “HAPANA. Sitaki michezo ya kijinga na SITAKI
kuingiliwa.” Akazidi kukaripa.
Jelini hakujibu tena,
akajirudisha kujilaza kwenye mto si kifuani tena. “Kwamba umekasirika mimi
kumfuata Colins!?” Ukweli moyo wa Jelini uliumia sana asijielewe kinachomuuma
ni nini wakati yupo na Zenda wala Colins si mpenzi wake! Lakini akakumbuka ahadi
yake mwenyewe. Kuwa muaminifu. “Nawajibika kwenye furaha ya Zenda.”
Akajionya na kujirudi kwa haraka akizizidi hisia zake.
“Eti Jelini?” “Hapana Zenda. Ila naona macho
yako, yako kwingi na si kwangu na ninacho kwambia.” “Yapo kwako na ndio maana
naona wanaotaka kuniharibia.” “Kwa nini huwaachi tu, sisi tukatulia na yetu?”
“Jelini!” “Mimi natulia na wewe Zenda na ndio maana nipo hapa. Hakuna
mtu atanitoa kwako isipokuwa wewe mwenyewe ukianza kuwa na wanawake nje.
Hapo tu ndio nitashindwa. Maana katika hilo tulikubaliana hapatakuwa na
mjadala.” Jelini akamjibu taratibu akijaribu kumtuliza maana alishajua hasira
zimempanda mpaka mwisho.
“Ndio maana na mimi sitaki mtu atuingilie.”
“Basi ndio maana mwenzio natulia, najiangalia mimi na ahadi zangu kwako
ili nisije kukukosa. Kwa hiyo tafadhali tujiangalie sisi kuliko wengine. Ni
hilo tu Zenda. Sitakusaliti hata iweje. Na ninamaanisha.” Jelini akajirudisha kulala akiwa amempa
mgongo.
“Sitaomba
msamaha kwa kumfuata Colins. Mimi nakupenda na nitakulinda.” “Na ninashukuru
kwa hilo. Nimefurahi kuwa hapa na wewe Zenda.” Akamwambia kwa upole ili
kumtuliza. “Nilikumisi mpenzi wangu.” Jelini akaongeza kwa upendo, ujeuri wote wa
Zenda ukaisha. Akamsikia akimsogelea, kisha akamkumbatia kwa kumuwekea mkono.
Akajivuta juu kabisa kwenye mto akaanza kumbusu masikioni na shingoni mpaka
Jelini akamgeukia.
Wakaendeleza kiss za
haja, akamuona anaingia ndani ya shuka, akaanza kucheka akijua kinachofuata.
Zenda alizama huko akimnyonya vizuri mpaka Jelini akafanikisha bao. Maana mara
ya kwanza ni Zenda ndio aliibuka mshindi. Akamtoa kinguo cha kulalia,
akamnyanyua miguu juu nakuilaza mabegani kwake, akawekwa mtu kati. Akawa
anaangalia vile anavyoingia na kutoka taratibu huku akigugumia yeye mwenyewe
kama anayesikia raha ya ajabu. Amekamata hips za Jelini kwa nguvu zote, kama
asiyeamini usiku huo yupo naye. Naye Jelini alimsindikiza kwa sauti ya huba,
akilalama kwa utamu na kuzidi kumpagawisha Zenda.
Alianza taratibu kwa
hisia zote mikono ikiendelea kubarizi kwenye paja zake, akimbusu mara kadhaa pale
kwenye miguu ilipotulia mabegani kwake huku akiendelea na Jelini akizidi kulalama
kwa raha aliyokuwa akiipata. Si mara zote Jelini alikuwa akipiga bao kwa staili
hiyo, lakini alikuwa akimgusa maeneo yaliyokuwa yakimpa sana raha. Taratibu kwa
utulivu mpaka akamaliza na kujilaza pembeni yake kama mfu. Jelini alimfuta na
kumfunika, hana habari. Usiku ukaisha bila kutajwa tena Colins, na Jelini akajionya
kabisa asipeleke mawazo huko kwa Colins. Akamtizama Zenda vile alivyolala,
akambusu na kumkumbatia vizuri na yeye akapotelea usingizini.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Unaweza kutawala Hisia.
Itaendelea…
Mazito Na Mazuri Yapo Mbeleni. Usipitwe.
0 Comments:
Post a Comment