Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Mapenzi & Pesa! - PART 2 - SEHEMU YA 10. - Naomi Simulizi

Mapenzi & Pesa! - PART 2 - SEHEMU YA 10.

Siku ya harusi Jema alikuwa na furaha kwani James alihakikisha anapata kila kitu anachohitaji, cha ndoto yake. Alivaa gauni la tausi kama kwenye sinema ya ‘Coming to America’ ila lake jeupe pee! Na kuwekwa vitu vinavyong’aa. Wakati anaingia kanisani, ilichukua muda wa kutosha, kuweza kuhakikisha hilo gauni lipo mbele, alipo yeye. Na rangi yake nyeusi, na vile alivyomwembamba, alipendeza sana mpaka akainua kitu ndani ya mdogo wake, Jelini. Kwa mara ya kwanza na yeye akatamani na yeye siku moja aje afike hapo. Kanisani na mwanaume atakayekuwa akimpenda kama vile Jema alivyompenda na kupendwa na James. Cheko la Jema lilijaa ndani ya hiyo shela, mpaka nje! Kwa kumtizama tu ungejua siku hiyo ndato zake zimetimia, na ni siku yake Mungu aliyoifanya kwa ajili yake. Kwa hakika alipendeza sana.

Mama yake ndiye aliyemuingiza kanisani na kutembea naye. Mama wa Kichaga aliyelea mwenyewe kwa kuuza hiki na kile kwa upendo kwa hao binti zake wawili, bila kuchoka au kulalamika akilea kwa kadiri ya uwezo wake, siku hiyo alipendeza, akaingia kanisani ameshika binti yake mkono akimpeleka mbele kanisani kumkabidhisha kwa James. Mama Jema alipendeza sana. Kwa pesa aliyokuwa amehongwa na Kasa, Jelini alimgaramia mama yake akihakikisha siku hiyo anatokea wa tofauti. Alimpeleka saluni nzuri sana, akatengenezwa mpaka Jelini mpenda vizuri akaridhika.

Siku hiyo anatembea kanisani mbele za watu, moyoni akasikia kufutwa machozi. Alipata wakati ambao hakuwahi hata kuufikiria maishani kumbe ni ndoto za mwanae. Akatembea kwenye ndoto za Jema aliyeomba mbele za Mungu akisubiri bila kukata tamaa. Siku hiyo mama Jema akavuna pamoja na mwanae. Ndoto walizoona ngumu kuja kuzipata kwa msichana kama Jema, akampata James aliyeweka heshima na marafiki zake wakamwaga pesa kwenye hiyo harusi, kanisa lenyewe lilipambwa kinadhifu mno. Mama G aliyekuwa hana jukumu ila hiyo harusi, yeye, Nanaa na Grace walihakikisha kunakuwa na kila kitu cha hadhi mno.

Wasomi na wenye nazo walibaki wakimsindikiza kwa macho akitembea taratibu na binti yake aliyekuwa amevaa gauni la kihistoria mpaka mbele kabisa alipokuwa amesimama James na wasimamizi wote. Maua yalishakuwa yamemwagwa. Tena maua mengi na watoto sita waliokuwa wametangulia. Wakiume watatu na wakike watatu. Wakapendeza sanaa. Walipomaliza kumwaga maua, ndipo akaja sasa Jema na mama yake. Mchungaji alipouliza ni nani anayemkabidhisha Jema kwa James, mama huyo kwa ujasiri wote akasema, ‘ni mimi’. Mdogo wake Mode akaanza vigelegele na kuamsha shangwe kwa wengine. Nayo hiyo ikawa shangwe ya kupendeza ya namna yake. Alikuwa akijisikia vizuri sana moyoni. James akampokea kutoka kwa mama yake na kutoa ahadi kuwa atamtunza Jema zaidi ya nafsi yake. Hapo napo kukawa na shangwe ya namna yake.

 Ndipo wakageukia madhabahuni. James alivaa suti nzuri nyeusi iliyokuwa imemkaa vizuri sana. Na vile alivyotengenezwa uso na kichwa, usingechoka kumtizama. James na Jema, walipendeza sana. Wakatoa viapo vyao walivyokuwa wameviandaa. James akamgeukia Jema na kumshika mikono yote, akaanza kuapa kwake, mbele za Mungu na watu. Akayasema yake mazito mpaka Jema akalia watu wakishangilia sana. Mchungaji akamkaribisha Jema. Msimamizi alipotaka kumfuta machozi, James akawahi. “Hii ni kazi yangu.” Vigelegele tena mpaka Jema akaanza kucheka.

“Sasa usitoe vipodozi bwana James!” “Ni katika kutaka kusaidia tu.” Wakaanza kucheka wao wenyewe hapo mbele na kujisahau. “Tunakusubiri wewe Jema.” Ikabidi mchungaji kuwashitua. “Jifunge mwenyewe Jema. Jitie kitanzi mbele za watu, ili usije kuniruka baadaye.” James akamfanya Jema acheke mpaka akainama. Wakarudia kucheka tena ndipo Jema sasa akatoa kiapo chake. “Nakupenda James.” Akamalizia hivyo na kuamsha shangwe nyingine za muda tu. Baada ya kuvalishana pete, na mchungaji kutoa baraka zake, James akambusu Jema kwa kujinafasi. Shangwe na vigelegele.

Baada ya ibada wakaelekea kupiga picha nyingi tu za kutosha. Ndugu wa pande zote, wakaweka kumbukumbu, hapo pakakaa sawa ndipo wakaenda ukumbini. Siku ya send-off Man na Grace hawakwenda na watoto ukumbini. Ni kama walikosa uhuru na shuguli za upande wa wakina Jema. Danny alisubiria mtoto wake amuone, lakini alipomuona Man tu na Grace mpaka mwisho, akakata tamaa. Ila siku hiyo ya harusi akamuona kuanzia kanisani. Akawa na kazi ya kumpiga picha kwa kujiiba na hakutaka amuone. Fili alipendeza sana. Alivaa suti nzuri sana kama Man. Na hivi alifanana na mama yake, ungesema ni mtoto wa Geb. Danny alizidi kuumia asijue chakufanya, akabaki akijiiba tu kumchungulia tu.

Jelini alipofika tu ukumbini, akapata bia za haraka. Akaanza kuchangamka. Akamuona Kasa, akafurahi sana. Akamfuata mbele za watu na kumsalimia kwa furaha akitaka kujua kama alirudi salama na mengine mengi kitu kilichomfurahisha sana Kasa kuongeleshwa vile na Jelini tena mbele ya wenzake. Akawa ametimiza azma yake. Ila wenzie wote waliokuwepo siku ya uchumba nyumbani kwa James wakashangazwa sana. Jelini alimkataa kabisa Kasa, iweje leo amfuate na kumsalimia yeye tu, nakujifanya kama hajamuona kabisa Colins! Maana Jelini alipofika kwa Kasa alimsalimia yeye tu, hata hakumgeukia Colins na wengineo.

Walipojaribu kumchokoza wakimsifia kuwa amependeza sana, akiwa ameshaanza kulewa akawaambia, “Mimi mwenzenu kupendeza ni kawaida yangu. Halafu mimi siwaoni wala kuwasikia. Namuona Kasa tu.” Wakazidi kucheka ila mwishoe wakajua ni akili tu za Jelini. Akaondoka akimwambia Kasa, “Mimi najua sana kucheza. Ukitaka mtu wakucheza naye, niambie mimi.” Hapo akawa amekamilisha furaha ya Kasa. “Jelini na mimi najua kucheza.” “Akuuu! Mimi sitaki kucheza na wewe. Kwanza utaniangusha bure.” Akaondoka.

Kwa hakika alikuwa amependeza sana. Saluni ileile aliyotengenezwa mama yake ndiyo na yeye alitengenezwa vizuri sana maalumu sababu ya hiyo shuguli. Kweli kipindi cha mziki, Kasa akaenda kumchukua akacheza naye vizuri tu. Akamrudisha kukaa, akashukuru. Mara ya pili bia zikiwa zimeshaingia sawasawa kichwani yeye ndio akaenda mezani kwa Kasa kumtaka akacheze naye lakini hakumkuta Kasa. “Sasa atakua ameenda wapi?” Akawauliza wenzie akilalamika bila aibu kama mwenye miahadi na Kasa. “Ila mchumba Colins yupo.” “Akuu! Colins amenipiga marufuku nisimsogelee. Amesema yeye anampenzi wake, hataki nisimsogelee KABISA.” Wakashangaa sana, wote wakamgeukia Colins aliyekuwa na mpenzi wake, na walisikia. Colins akajikausha kabisa. Wakaona wabadilishe mazungumzo. Jelini hata hakuwaangalia.

“Kwa hiyo ndio Kasa amekua mchumba?” “Akuu! Mimi Kasa ni kampani yangu kama Doro. Kasa yeye hana roho mbaya. Roho yake ya shukurani na anautu. Hajui kumuumiza mtu hisia zake.” Akajibu hivyo na kuondoka, Kasa akiwa nyuma yake, wote wakasikia. Kasa alitamani amkimbilie na kumkumbatia kwa shukurani kwani alitimiza zaidi ya alivyotarajia kwa wenzie, ila akajipandisha uanaume. Haiba yake ya kiburi cha pesa ikarudi. Akajidai ni kawaida tu. Akaaa.

Lakini ikawa tofauti kwa Colins akashangaa moyo unaumia kwa maneno ya Jelini. Akajali alichosema. Akajua anamuona hana utu wala shukurani. Na amemuumiza hisia zake. Akanyamaza tu. Watu wakaanza kumtania Kasa sasa, kuwa Jelini anampenda yeye. Akajisikia vizuri. Sherehe zikaendelea kwa kufana haswa, Jelini yeye akaendelea kunywa mpaka akajisahau alipo na yeye ni nani.

Hayawihayawi, Yamekua.

Hatimaye usiku waliotizamia kwa hamu ukafika. Wakafikishwa kwenye hoteli nzuri ambayo wanakamati walimlipia James kwa siku tatu ndipo wasafiri kwenda mapumzikoni kwa majuma mawili huko kwenye visiwa vya Seychelles vilivyopo katikati ya bahari ya Hindi, upande wa Afrika ya Mashariki karibu kabisa na kaskazini mwa Madagascar. James aliichukua hiyo likizo makusudi. Alilundikiza siku zake za likizo kwa muda mrefu makusudi kwa hiyo fungate na baada ya hapo awe na Jema nyumbani kwao, aweke biashara zake vizuri akimtambulisha mkewe ndipo aanze kazi. “Jema amejitunza aisee. Anastahili fungate nzuri.” Akajisemea James moyoni akitaka kuweka historia nzuri kwa mkewe. Alikuwa akifanya kazi na biashara bila kupumzika.

Walipoachwa hotelini, chumbani kwao na masanduku yao ya fungate, msimamizi akiwa ameondoka na ile shela kubwa ila kumuacha Jema na gauni tu. James yeye alimpa msimamizi wake suti kabisa. Hakutaka kusafiri na hiyo suti. Wakajikuta wamebaki wenyewe hapo chumbani.  Jema akaanza kuingiwa na hofu, mpaka akasahau ni nini avae baada ya kutoa gauni na aanzie wapi. James akamuona anavyohangaika. Mwishoe akamuona anaelekea bafuni. Akajifungia. James akasubiri mpaka akachoka, akajua amepaniki hajui aanzie wapi.

Akagonga taratibu, baada ya muda akafungua macho mekundu kama aliyekuwa akilia huko bafuni. Akamvuta karibu mpaka kwenye kochi. Akakaa na kumpakata, akaanza kumkisi taratibu akiwa ametulia tu mpaka akamuhisi hofu inamtoka mwili unaanza kulegea. “Nakupenda Jema wangu. Na leo ni usiku wetu mimi na wewe. Kwa vyovyote itakavyokuwa, ni mimi na wewe mpaka kifo, si ndivyo tulivyoapa mimi na wewe?” Jema akatingisha kichwa kukubali. “Basi tuweke msingi wetu sisi. Unaweza usifanane na wengine, lakini kile tutakachokubaliana, kitakuwa chetu na tutakishikilia. Usiogope kabisa. Ninachotaka ni uwe hapa na mimi, basi. Na usiogope kuwa huru.” Akamuona ameridhika.

Akaanza sasa kumkisi kila mahali, tena kwa kituo. Shule ya mahaba ilishapotea kichwani kwa Jema, akawa hana ajualo tena. James akamchangamkia yeye. Akaanza kumnyonya taratibu akimtoa nguo, Jema akaanza kufurahia mikono ya kiume mwilini mwake. Zipu ya gauni juu ikaanza kufunguliwa huku midomo ikitembea kila mahali zaidi shingoni kulikozidi kumsisimua Jema. Akamtoa mikono akabakiwa na sidiria juu, gauni chini kiunoni amepakatwa akipewa mabusu msisimko.

“Twende tukatoe jasho la siku nzima, kisha turudi tufurahie usiku wetu wa kwanza.” James akaongea akimfungua vishikizo vya sidiria hapo kochini mpaka akamaliza na kuitupa sidiria sakafuni. Kabakiwa na Jema matiti wazi mbele yake. “Waoooh! Una matiti mazuri!” James akasifia kwa hisia, Jema aibu! James akajiegemeza kwa kulaza uso hapo katikati ya hayo matiti na kumkumbatia. “Hii itakuwa starehe yangu.” Jema akacheka taratibu angalau akapata ujasiri kuona James anamsifia, ila bado aibu hajui atamtizamaje.

Hapo akafurahia alipokuwa hamtizami, akabaki anampapasa kichwa pale alipokuwa amejificha kwake. Hajakaa sawa hata dakika kupita akashitukia mikono ya James imepenya ndani ya gauni akimchezea ndani ya chupi taratibu. Mwili mzima ukaanza kumsisimka. Mara ya kwanza kushikwa hivyo! Tena na James! Jema alitamani asimame kwa haraka atoe nguo zote afurahie ile mikono ndani kabisa, ila akatulia. James akahamia kwenye matiti. Midomo kwenye chuchu hizo ngumu ambazo bado hazijapata shoruba ya midomo ya kiume hata mara moja wala hakuna mtoto aliyenyonya na kung’ata akijikunia mapengo! Ziwa zuri, gumu limejaa hapo kifuani! James alikuwa akigugumia raha kwa hisia zote. Na hivi alifundishwa jinsi ya kunyonya mwili mzima wa mwanamke na kina Geb. Akionywa afikapo kifuani asinze kujisahau na kuanza kunyonya kama ndama, basi alicheza na hizo chuchu, mwili mzima ukawa ukimtetemeka Jema.

Akamnyanyua kumtoa gauni la harusi pamoja na chupi. Yeye alikuwa na taulo tu. Jema akawa ameshaloa, hajiwezi tena, kila kitu kigeni kwake, romansi hiyo tu kwake ikawa tosha anataka aingiliwe hapohapo. James akajifanya hajamuelewa ila alishajua amelemewa. Jema mwembamba, anabebeka. Akanyanyuka naye pale mpaka bafuni. Wakakuta upande wa sinki ya kuogea, jakuzi, kumeandaliwa kifungate. James akaona hana muda na Jacuz.

Akaingia naye kwenye shower akiendelea kumnyonya midomo, akamsimamisha na kuendelea kumnyonya kwa uchu huku akimpapasa akiwa uchi. Akamuacha pembeni akachanganya maji kwa kufungulia maji ya bomba aina yote. Baridi na moto mpaka akaridhika joto lake. Akamvutia ndani. Jema akashangaa anamuogesha kwa kumpaka sabuni taratibu, akampaka kila mahali, wakati akijisuuza, na yeye akajilowesha na kumsogelea nyuma yake. Akashitukia mkono wa James mbele ukiosha mbele kuanzia kwenye matiti mpaka chini katikati ya miguu. Akampanua miguu kabisa akaanza kumuosha Jema mwenyewe.

Taratibu bila haraka kama akimchua. Ndani nje mpaka tunduni kwa nje, akishika tumashavu, basi anatusugua taratibu akaanza kumchezea akiwa amesimama nyuma yake. Jema alilegea, akabaki amemlalia mgongo kifuani kwake miguu ikitetemeka haswa. Akamgeuza na kupata midomo, kisha akashuka taratibu mpaka kifuani, hapo akawa mkono kwenye K ya Jema, midomo matitini. Jema alikuwa akilalamika hajiwezi akiwa ameegemea ukuta wa bafu. Akili imepotea, James akainama. Akammalizia kwa kumnyonya. Jema alipiga kelele wakati akipiga bao mpaka akaona aibu wakati akimalizia. Akajifunika uso. Alisahau kabisa mpangilio wa sauti kama alivyofundishwa na Jelini, kwa raha ambayo kwa mara ya kwanza mwanaume anampa, tena James! Anavyompenda! Akimshika tu ni romansi tosha.

James hakutoa mdomo huko, akabaki akimnyonya mpaka alipohakikisha amemaliza kabisa na Jema ametulia. Akasimama na kumkumbatia. “Nimesikia raha ya ajabu! Asante James.” Akaongea kwa deko, James akacheka taratibu akiendelea kumsugua mgongoni. Alipotulia ndio akili ikamrudia asisimame hapo kama sanamu. Shule yote hata na ya mamdogo Mode ikamrudia. Kunyonya na kuchezea kengelea. Kwanza akafurahishwa na jogoo wa mumewe. Ukubwa wa nguvu, wakutoshea. Akakumbuka maneno ya makungwi wake, akacheka moyoni mwake akijipongeza. “Kweli hapa kama ni karata, basi mimi Jema nimelamba dume!” Akajisemea moyoni akimchezea mumewe kwa ustadi kama aliyekubuhu kwenye hiyo shuguli, mpaka James akashangaa.

Akamchanganya James ambaye na yeye hakuwa amewahi kushikwa hivyo na mwanamke. Kwanza mwanamke apate wapi zipu ya James! Maisha yake yote wanawake aliwaona dada, hakuthubutu kuweka mazoea ya kupitiliza na mtoto wa kike. Na akishakuona unajitongozesha tu, anaweka sura ya kazi. Ndio maana mwanzo wao kabisa Geb alicheka sana alipobabaishwa na kumkatalia Jema chakula. Akajua tayari ndege mjanja yupo tunduni.

Jema akawa mjuzi kwa hizo kengele za mumewe, James mwenyewe akaongoza njia kama kondoo machinjioni. Akakisaka kitanda kilipo. Walipofika kitandani, James akakataa kufa kijinga. Akakumbuka kuambiwa aache uvivu mbele ya mtoto wa kike. Usiku huo ni wa historia, yeye mwanaume, ajikaze, asilemewe kijinga. Gafla mchaga akawa mtaalamu wa kateroli. Akamlaza Jema chali, miguu pande, na kuanza kupigisha jogoo wake kwenye K ya Jema. Anamsugua taratibu akitumia kichwa chake mpaka Jema akaloa kabisa, yeye mwenyewe akaanza kutaka tena James amuingizie.

Yale aliyoyakataa kuyasema kwa Jelini akisema hataweza kumwambia James, usiku huo akajikuta akililia James amuingizie. Jema akalalama ndipo James akamsugua kwa nguvu na mashine yake kisha akahamisha ulini aliokuwa ameukakamaza. Juu mpaka chini katikati ya matako. Alipoona amezidiwa, akakamata K yake na kuimumunya kwa nguvu akiikamua kama ng’ombe wa maziwa. Kwa mara ya pili, akapiga bao, mumewe hajapata kitu. Na James alifanya makusudi maana aliambiwa kwa usiku huo kama hatafanikiwa kumfikisha mkewe kwa romansi, basi anaweza asimpe furaha mkewe kwenye siku yake ya kwanza maana aliambiwa ategemee maumivu makali kwa Jema ambaye alikuwa bikra. Kwa hiyo alichomfanyia alipanga kabisa. Akafurahi kuona amefanikiwa.

Jema alikojoa kwa muda wa kutosha na wala mumewe hakumkatisha aliendelea kumnyonya tu mpaka akamaliza. Akajinyoosha hapo kitandani kama ametoka shamba. “Jema wewe ni mzuri mpenzi wangu. Napenda kila kitu chako. Na hata ningepewa nafasi ya kuchagua tena, hakika bado ningekuchagua wewe.” James hakujua thamani ya yale maneno kwa mkewe. Ilimuongezea ujasiri na nguvu hata ya kujiachia hapo kwa mumewe. Ni James jamani. Si kuwa na yeye ni bikra kwa kuchina! James ni mzuri haswa. Si mrefu kama kina Geb na Joshua, lakini hakuna kitu ataweka mwilini akachukiza. Mzuri sana wa sura. Rangi inawaka hata gizani! Amesoma mpaka vyuoni kwenye warembo wa kila namna. Halafu sasa anayo pesa. Si yakubadili mboga! Pesa ya kuweza kuzungumza mbele ya wenye nazo na yeye akasikilizwa. Ajira nzuri, halafu mtoto wa mjini kwamba anazungukwa na warembo wa kila aina, kila siku. Halafu anayo hekima. Kwamba hata akitokea naye katikati ya watu, hana neno akifungua mdomo. Halafu eti leo anamsifia Jema! Furaha iliyokuwa ndani ya moyo wa Jema, hata ungemwambia hakuna tena jehanamu, bado yeye angebaki na Mungu aliyempa James.

“Asante mpenzi wangu. Na mimi nakupenda SANA. Na nilishakwambia hata kanisani. Hata iweje, nitakuchagua tena na tena, mpaka kifo changu.” Mzuka ukampanda James, akaanza kumchezea tena taratibu. Ikawa rahisi sana kwa Jema kuamkwa tamaa. Sasa sijui ni kwa kuwa alimpenda sana James na maneno yake aliyompa muda mfupi uliopita! Kile kitendo chakufikiria anashikwa na James, nakuuona mwili wake, kuliamsha hisia za ajabu ndani yake, nakumtaka tu mumewe. Ila akawa muungwana asizidiwe tena akashindwa kumfurahisha mumewe. Akamsukuma taratibu, James akajua anamtaka alale yeye chali.

Jema alimchezea kuanzia masikio mpaka mashine yenyewe. James akasahau kama yeye mtoto wa kiume. Wanasema hakuna jasiri kwenye penzi. Ndiyo yaliyompata James. Akamwaga kila kitu hadharani akajiachia na kubaki akiweweseka, maana Jema alijua kuchezea mashine yake vilivyo. Kila msitari aliofundishwa na jinsi ya kuuchezea akakutana nao hapo kwa James, akamtenda haki. Na uzuri James alifundishwa na wenzie jinsi ya kusafisha mashine yake ili kutoa harufu mbaya, asije mkera mpenzi wake. Hapo Jema alikuwa akipumbazwa na harufu nzuri sana ya kiume ya Blue lavender. Na alishaanza kuitumia kwa muda wa kutosha tu mpaka ngozi yake ikazoea hiyo harufu ya sabuni ya maji ya kuogea/body wash, lotion yake pamoja na body spray. Jema alibaki amezama huko chini akilevya na hiyo harufu nzuri.

 James akawa anachuliwa juu chini. Akimnyonya kichwa basi ujue mikono ya mkewe ipo chini ikimkanda uume wote, akiuminya taratibu huku akishuka chini na kupanda juu. Alipozamisha kunyonya yote, mikono ikahamia kwenye kengele. Basi Jema akawa ananyonya juu mpaka chini akimbana haswa huku akichezea kengele.

Alipozidiwa karibu akojolee mdomoni kwa mkewe, akamuweka mkewe chali kwa haraka akamnyonya kwa pupa kama kumlinisha tu maana japokuwa alizidiwa lakini akakumbuka mkewe ni bikra akaanza kuingiza kichwa taratibu na kutoa, anamsugua kisimi, Jema analalama, anataka James amalizie. Taratibu mpaka akafanikiwa kuingiza yote. Jema aliruka, raha yote ikaisha, James akamkumbatia akiwa hajatoka.

“Pole. Maumivu makali sana?” Machozi yakaanza kumtoka Jema. “Nitoke kwanza?” James akauliza kwa kubembeleza akisikika kumjali yeye zaidi mpaka Jema akamuhurumia na kukumbuka hajapata kitu tokea waanze. Akakataa kwa kutingisha kichwa, ndipo James akampa kifo cha mende kikamilifu. Akamkumbatia vizuri, akawa mstaarabu akimpelekea mashine kwa upendo akitafuta hizo G spots huko ndani alizoambiwa lazima azipate ili mkewe apate raha, atulie. James kwa hofu akimuhurumia mkewe vile alivyokakamaa akiwa amemkumbatia James kwa nguvu zote akitetemeka, akashindwa kuzipata hizo G spots kwa haraka. Utamu wote umeisha, hofu na maumivu. James akajiambia lazima atulie atafute. Mwanaume akawa kama yeye sasa ndio anayekatika akisaka utamu wa mkewe kwa uume wake huko ndani, mpaka akapata. Akamuona mkewe anaanza kulegea na kulalama kwa huba taratibu. Alifurahi James, nusura achomoe ashangilie kwanza, lakini akaogopa kuipoteza.

Aliendelea kuisugua hiyo G spot taratibu akimnyonya midomo mpaka Jema akatulia kabisa hapo kitandani na kumuacha mumewe aendelee kwa huru si vile alivyokuwa amemkaba kama kumpa roba ya mbao! Japokuwa hakupiga bao, lakini James akafanikiwa. Hatimaye kwa mara ya kwanza maharusi hao, wakatoana bikra. Wakalala wamekumbatiana kwa furaha yote.

Maombi Ni Hazina. Hayaozi.

Wakati wengine wakifurahia harusini, ikawa tofauti kwa Joshua. Moyo wake ukakosa amani kabisa mpaka akashindwa kuvumilia. Akamnong’oneza mkewe kwamba anatoka kidogo, atarudi. Naya alishituka sana furaha yote ikaisha. “Usije ukaniacha Joshua!” “Siwezi.” Akamuona mpaka amebadilika kwa hofu. “Geb yupo hapa usiogope.” Akamnong’oneza. Maana hapo mezani walikuwa wamekaa sita. Man na Grace. Joshua na Naya. Geb na Nanaa. Lakini Naya ikawa ni kama anaachwa Kariakoo, katikati ya watu asiowajua. “Naogopa sana. Usiniache Joshua.” Joshua akafikiria kwa haraka. “Basi twende wote.” Akamshika mkono, akamuaga Geb kuwa watarudi baada ya muda mfupi, akarudi ndani ya gari yake.

“Tunaondoka?” Naya akauliza taratibu mara walipoingia garini. “Tokea asubuhi nimejiwa na Bale mawazoni.” “Bale yule ndugu yangu!?” Naya akauliza kwa hofu. “Ndiyo. Lakini nimejaribu kumpuuza, nimeshindwa. Nikaamua kumpigia simu, simu yake haipo hewani. Nikamtumia ujumbe ili nione kama utafika, lakini kila saa naangalia kama umefika, unaonekana bado. Wasiwasi unanizidia. Nimekwama, sijui chakufanya Naya. Sina amani na shindwa kufikiria kabisa. Nakumbuka vile baba yako alivyokuwa akifunga na kuomba kwa ajili yake na kwenda kumtafuta bila kujua pakumpata. Ila imani tu. Acha nijisalimishe kwa Mungu, na mimi nione jinsi atakavyonisaidia.” “Naogopa Joshua! Akirudi na yule rafiki yake na kutaka kunichukua tena?” “Mungu wetu hatatuacha Naya. Acha nimuombe. Anionyeshe alipo ili nitulie niweze kufikiria. Usiogope kabisa.” Basi Naya akabaki amekaa kiti cha mbele mumewe akahamia kiti cha nyuma, akaanza maombi.

Bwana Joshua anajua kuomba! Aliomba na suti yake ya thamani kubwa sana, iliyokuwa imemkaa vizuri. Dume la nguvu mbele ya macho ya wanadamu. Lakini mbele za Mungu, ukimuona, unaweza ukadhani siye yeye. Aliomba mpaka Naya akapotelea usingizini, Geb akahisi mandhari ya romansi kwa James na mkewe yameibua kiu kwa Joshua na Naya, wameondoka kwenda kukumbushia ndoa yao, kumbe Joshua yupo mbele za Mungu wake. Amemimina moyo wake, hata hajui alipo.

Pombe Sio Chai.

Jumapili baada ya harusi wakati Jema akifurahia ndoa kwenye hoteli nzuri sana jijini, huku mdogo wake, Jelini aliamka asubuhi hajui alipo. Ila amelala sehemu nzuri sana. Kitanda kisafi cha hadhi ya juu mno hajawahi lalia kitanda kama hicho maishani, ila hapajui kabisa. Kila alipojaribu kujinyanyua hapo alishindwa kwani kichwa kilikuwa kizito kwelikweli na hakuwa amejifunika ni kama aliyekuwa ameachwa tu hapo hovyo. Baridi ya upepo uliochujwa, A/C, ilimtesa Jelini mpaka kwenye mifupa.

Akaanza kuangaza macho ndani ya kile chumba, kutaka hata kujua kama ni nyumba ya kulala wageni au nyumbani kwa mtu, lakini kumbukumbu zikagoma kabisaa. Akashindwa hata kujua jinsi alivyofika hapo. Pakawa kimya hakuna hata sauti ya kuku nje. Hofu ya ajabu ikamuingia kila alipofikiria na anavyojisikia. Akili iliishia ukumbini akinywa na kufurahia harusi ya dada yake. Akajua alilewa, akapitiliza. “Watakuwa wamenifanyia mambo mabaya bila mimi kujijua!” Akaanza kulia kwa hofu.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Jelini&Bale wako wapi?

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment