Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Mapenzi & Pesa! - PART 2 - SEHEMU YA 8. - Naomi Simulizi

Mapenzi & Pesa! - PART 2 - SEHEMU YA 8.

Jumamosi ya kikao Cha Mwisho.

Jelini aliamka mida yake ileile ya kizembe akatoka kumfuata mama yake alikuwa tu ndani sebuleni. “Kwa hiyo leo ndio siku unaenda kwa Doro?” Mama yake akamjaribu. “Ila silali. Naenda tu na kurudi. Sitaki aone namziria. Amekua akinisaidia sana.” “Kununua pombe?” Jelini akaanza kucheka. “Doro anapesa isiyo na matumizi. Kwake pazuri, ukilala chumbani kwake pana A/C. Umeme ukikatika, genereta inapokea kazi. Basi unalala usingizi mzitooo..” “Kinachokushinda na wewe kujenga kwako ni nini?” “Umeanza mama, na wewe!” “Kuna leo na kesho Jelini, mwanangu. Wewe una mtoto. Na mwanao anapenda sana shule. Nikifa, utafanyaje naye?” Jelini akaondoka kabisa hapo. Baada ya muda akamsikia akimjibu akiwa chumbani. “Huyo mtoto ni wako. Omba usife, umlee mwenyewe.” Mama Jema akaguna.

Atafutaye Asiyechoka.

Kilikuwa kikao cha mwisho ili ianze kitchen party kisha send off ya Jema ndipo Bigday, harusi. Wakapanga mengi ya mwisho, Jelini akapewa jukumu la kuwahi ukumbini na kuhakikisha kumepambwa vizuri na vyakula vimewasili bila kukosekana hata kimoja kama walivyolipia. Alipopata majukumu yake akamnong’oneza mama yake, kisha mama yake akamuuliza. “Kwa hiyo usiporudi niwe na wasiwasi?” “Nipigie kabisa. Sitachelewa. Na si umeona hata sijanywa hapa! Sikutaka nishindwe kufikiria. Nitarudi.” Akachukua bodaboda na kuondoka kuelekea Kunduchi kwa Doro.

Alifika ni kama alikuta watu wengi hapo bustanini kwa Doro wakinywa, hakutegemea. Akaingia kwa kujificha mpaka ndani sebuleni napo akakuta watu wengine! Doro alipomuona tu ameingia hapo, akamkimbilia. “Mbona watu wengi hivyo!? Mimi nilijua wachache!” “Walevi wote hao wameitana kukesha wakinywa hapa kwangu, wala usihofu.” Jelini akaangaza macho. Akamuona anacheka. “Ni nini?” Doro akauliza. Mara Kasa akasogea. “Yaani wewe ni msafi kila wakati na kila mahali!” Jelini akampokea kwa hizo sifa kitu kilichomfurahisha sana Kasa. Amesifiwa na Jelini! Hakutegemea.

“Na wewe ni msafi Jelini.” “Asante.” Wakacheka Doro akiwatizama. “Sikujua kama unafahamiana na dada Doro!” “Dunia ndogo.” Akajibu Kasa. “Kwa kweli. Ila nimefurahi kukuona tena.” Akaongeza Jelini na kumshangaza zaidi Kasa. “Kweli au unaongea tu? Maana si ulichokisema mara ya mwisho tulipokutana Jelini.” Jelini akakunja uso. Doro akaona awapishe. “Kasa na Jelini, nyinyi karibuni. Mjisikie huru popote. Na msisimame hapo. Jikoni pametulia hakuna mtu.” Jelini akacheka bado na mshangao usoni kwa kile alichokisema Kasa, Doro akaondoka.

“Naomba twende jikoni.” Jelini akaongoza njia Kasa akamfuata nyuma akicheka. “Niliongea jambo baya kwako!?” Jelini akamgeukia na kumuuliza mara walipofika jikoni. “Tena mbele za watu.” Kasa akajibu, akamuona ameshituka na kujifunga mdomo. Kasa akabaki akitingisha kichwa kumuhakikishia alisema huku akimpa tabasamu. “Naogopa hata kujua nilichozungumza. Ni kibaya sana?” “Mimi kiliniumiza Jelini. Hukuwa ukinifahamu ila ukanichagua kati ya kundi zima kunishutumu.” Akafunga macho. “Naomba nisamehe...” Akawa kama anayefikiria jina. “Kasa.” “Yeah, Kasa. Nisamehe kaka yangu. Mwenzio Jema anasema eti mimi mropokaji. Halafu nikishakunywa, nakua naongea sana. Ndio maana nataka kupunguza pombe. Zinanifanya sifikirii vizuri na..” Akasita alichotaka kuzungumza.

Akaona ombe msamaha tu. “Nisamehe Kasa. Sikukusudia kukuumiza. Mwenzio sipendi kumuumiza mtu.” Kasa akafurahi sana, hakutegemea kukutana na Jelini wa namna hii. “Yameisha.” Jelini akawa kama hajaridhika. “Niliongea neno baya sana?” “Yameisha bwana. Kweli yameisha na nimefurahi kukusikia kuwa hukumaanisha.” “Ni vile hujanizoea. Mwenzio naongea sana. Ila nakuahidi kubadilika. Nitakuwa makini na maneno yangu. Na nimefurahi umenisamehe.” Kasa akacheka akimwangalia.

“Umekula au ungependa nikutafutie kitu cha kula? Mimi hapa ni mwenyeji kidogo. Nilikuwa nikilala hapa kwa dada Doro. Kwa hiyo ni mwenyeji.” “Ulikuwa ukilala, Kwa hiyo umeacha?” “Nimeacha kupenda kwa watu.” Wakacheka. “Kwa hiyo umehamisha kijiwe kwengine?” “Kwa mama Jema. Ndio hanichoki.” Kasa akavuta kiti na kukaa. “Wengine wanakuchoka?” Jelini akacheka. “Niambie ungependa kula nini nikutayarishie.” “Mimi nataka nikae na wewe tuzungumze tu, au unataka kwenda kunywa nje na wenzenu?” “Leo narudi kwetu. Sitaki kunywa sana. Kwanza mtu kama wewe unataka kuongea nini na mtu kama mimi!?” Akajishika kabisa kwa kushangaa.

“Wewe ukoje na mimi nikoje?” “Wewe unaonekana unatokea kwenye daraja la juu sana kwenye maisha. Mimi mwenzio hata sijasoma! Washikaji zangu ni walevi wa baa ambao hatufikirii chakuongea. Kinachokujia kichwani ndio hichohicho unakitoa mdomoni.” Jelini aliongea akicheka kama mazuri. Kasa akacheka na yeye. “Mimi na wewe hatuwezi kufanya mazungumzo hata kwa dakika 10. Utachoka bure. Bora niende kwa wale walevi kule nje tunaozungumza lugha moja.” “Unataka kurudi nyumbani saa ngapi?” “Nikipata bia mbili tu, naondoka kabla sijazidisha.” “Unarudije nyumbani?” “Bodaboda, daladala, bajaji, chochote kile sichagui ilimradi tu kufika nyumbani.” “Hutaki nikusogeze?”  Jelini akacheka akifikiria.

“Vipi?” “Mwenzio misaada ya watu naogopa. Watu wanapenda kukupa kitu halafu wanakuja kukudai baadaye.” Kasa akabaki akimwangalia. “Kweli tena. Unakuta unapewa kitu vizuri tu. Unakua na haraka yakupokea, kumbe mwenzio anakuwa na lengo jingine. Sisemi kama ndio tabia yako! Lakini mimi mzito wa kupokea misaada hata kama ni midogo kiasi gani.” “Nakupa lifti sio nakupeleka. Maana na mimi naondoka sio kwamba nalala hapa. Kwa hiyo usihesabu kama ni msaada. Hesabu kuwa gari inaondoka hapa ikiwa na nafasi.” “Sitaki kukusumbua au kukuchelewesha.” “Nilifikiri hutachelewa!” “Stori zinaweza kuzidi, nikabaki kucheka.” “Hudhani kama utapitisha maamuzi ya unywaji kwa usiku wa leo utakapo baki na wenzio wakiendelea kunywa?” Hapo akamfanya afikirie.

“Basi bora hata nile tu niondoke, dada Doro asijisikie vibaya. Anaweza dhani bado nimemchukia kwa maneno mabaya aliyonipa.” “Maneno gani tena!?” “Acha nisiyarudie kwa sababu nilishamwambia nimemsamehe. Ila acha anione hata nimeshika sahani ya chakula, ataridhika.” “Utakwenda kula wapi?” Hilo swali likamfanya Jelini acheke akifikiria. “Nataka kuwepo, ulipo.” Akaongea Kasa akibembeleza kidogo na kumshangaza Jelini. “Kwani wewe hunywi?” “Bia hapana. Ladha yake mdomoni imenishinda kabisa. Ila nakunywa vinywaji vingine.”  Akacheka na kusimama. “Basi acha nikachukue chakula, nakuja kula hapahapa. Maana najua hata waliopo hapo sebuleni hawaendani na wewe. Na sijui kwa nini alikukaribisha katikati ya watu kama sisi!” Akatoka.

Akarudi na chakula mkononi. “Unauhakika hutaki kula kitu chochote?” “Umekuja kwa kuchelewa Jelini. Mimi nilishakula mapema. Huwa ikizidi saa 12 jioni sili tena. Kwa hiyo nilipofika tu nikala.” Jelini akamtizama na kunyamaza. “Mbona sasa sikuoni na bia?” “Kwa kuwa wewe upo. Na nilishakukosea, sitaki kukunyima raha na bia kitu ambacho si rafiki kwako.” Akamuona ana utu. “Lakini nisingejali.” “Haina shida. Bia huwa zipo tu.” Akaendelea kula huku akimtafakari asiamini kama amekaa naye na ametulia si mapepe kama alivyokutana naye mara ya kwanza.

Pakawa na utulivu wa namna yake. Jelini akijiwinda na maneno yake. Akaingia Doro akijihami. “Dada Doro chakula kizuri sana. Ila ni kawaida yako.” Akamgeukia Kasa. “Dada Doro anapika sana. Akikutengenezea nyama ya foili, utakula mpaka basi. Halafu usafi wake ni wa mpaka bafuni! Ndio maana napapenda kwake.” Kasa akamtizama Doro kama kumkumbusha swali lake wakati akimsema Jelini. Kwamba, ‘Je nikikaa na Jelini naye atakusema hivyohivyo kama wewe?’ Akakumbuka na kujibaraguza. “Kawaida tu.” Akajibu Doro akimkwepa Kasa.

“Mimi nikimaliza kula naondoka dada.” “Sasa si tulale tu leo? Gimo kaleta pombe kibao!” “Acha ninywe siku nyingine dada yangu, leo nirudi tu nyumbani.” “Jelini naye!” “Acha dada nikue kidogo. Nimezidisha michezo na nyinyi wenye maisha yenu wakati mimi sina kitu kabisa! Nakimbizana tu na nyinyi! Kweli si sawa. Hata hivyo naona nipunguze pombe, nianze kufikiria.” Doro akacheka. “Wewe nicheke tu.” “Nakuaminia. Nimekuona siku mbili tatu hizi! Si mchezo! Basi nisubiri nikurudishe nyumbani.” “Mimi nitamsogeza.” Hapo Kasa akatoa macho kwenye simu na kumtizama Doro kwa amri. “Bora, ili asiwe peke yake na usiku huu.” Akajirudi Doro kwa haraka. Jelini akawa hajaelewa ila akaona anyamaze.

Doro akataka kutoka. “Dada Doro, naomba nikuage kabisa.” “Huji hata kuwasalimia kina Gimo?” “Acha iwe wakati mwingine. Gimo ataanza kunichokoza ilimradi tu nikae tuanze kelele, wakati mama Jema ananisubiria nyumbani. Tutawasiliana na nashukuru kunikaribisha leo.” “Kwa ugeni gani wa hapa na wewe!?” “Wewe pokea shukurani zangu. Ungeweza kutonialika na nisijue kama umealika watu hapa. Nimefurahi.” Kasa kimya, Doro akacheka. Jelini asijue hiyo yote ni pesa ya Kasa na amefanya kwa ajili yake.

Chai Rangi, Huwezi Tia Tui La Nazi.

Wakaondoka kimya kimya watu hawakuwaona. “Nashukuru kwa ushauri wakutobweteka pale. Na kwa jinsi ninavyojijua mimi, nisingeondoka leo pale.” Jelini akavunja ukimya mara tu Kasa alipotoa gari hapo nyumbani kwa Doro. Kasa akacheka. “Kweli tena. Zile kelele pale zote zinanihusu. Watu wangu sana. Dada Doro ndio kampani yangu. Tukianza kunywa na kucheka, tunajisahau mpaka tunakuja kufukuzwa baa inafungwa.” “Umemzoea sana Doro?” “Sana kuliko hata Jema. Mtu mzuri sana halafu tunaendana sababu ya pombe. Jema dada yangu yule mtakatifu, halafu hawezi kelele. Sasa dada Doro mshikaji wangu. Tukianza kucheka, hatumalizi mpaka wakati mwingine tunajisahau tulichokuwa tukicheka. Ni dada mzuri sana.” Kasa akanyamaza.

Akamuelekeza kwao. “Jumapili huwa unafanya nini?” “Mimi ratiba ya jumatatu na jumapili hazina tofauti na hazijulikani. Napenda sana kulala. Na nikipata kitanda kizuri na upepo uliochujwa kama pale kwa dada Doro, ndio nalala siku nzima.” Kasa akacheka akimtafakari Jelini ila akaona amchukulie taratibu. “Kanisani?” “Mimi na mama yangu ni wakristo jina. Hatuendagi kanisani. Kwa hiyo kama hivi nikimkuta macho, tunaanza stori mpaka tuchoke ndio tunakwenda kulala na bibi pia yupo kwa hiyo stori haziishi. Kingine mama hafanyi kazi siku za jumapili. Basi hapo ndio kuja kuamka ni mchana. Kula, stori, siku imeisha.” “Nikikukaribisha kanisani kwetu utakuja?” Alicheka Jelini. Kisha akacheka sana.

Mpaka Kasa akaanza kucheka. “Sasa unacheka nini?” “Mimi nahisi nikiingia kanisani, malaika wote watatoka wanipishe mimi na Mungu.” Kasa alicheka sana. “Kwa nini?” “Kiumbe cha ajabu ambacho hawajawahi kukiona!” Kasa akatingisha kichwa. “Hapana bwana. Utakuwa sawa.” “Nashukuru, lakini hapana. Kwanza sitaki kwenda kanisani. Sio sehemu hata nawaza kuja kwenda.” Kasa akashangaa sana.

“Ulikosana nini na kanisa?” “Ni sehemu ambayo sina mazoea nayo kabisa. Hata hivyo kesho nataka kuwepo tu nyumbani. Najisikia kutulia nyumbani.” Akajibu hivyo kwa msimamo kama ambaye katika hilo hakaribishi tena nyongeza, kisha akamuona ametulia. Kasa akabaki akimtafakari na kujaribu kufikiria jinsi ya kumchukulia! Akapata wazo jingine akaona amjaribu. “Jioni ungependa nije kukuchukua tukapate ice cream?” Jelini akashangazwa. Akamtizama kabisa. “Unakumbuka nilikwambia nataka kuwepo ulipo?” “Huendani na mimi na wala masikani zangu. Kwa kukuangalia tu, maisha yangu na yako ni tofauti kabisa Kasa. Hutanimudu mimi, bora nikwambie mapema usijipotezee muda.” Jelini aliongea kwa wazi bila hata kumficha. Kasa asiamini anaweza vipi kukataa ukaribisho rahisi vile kutoka kwa mtu kama yeye! Gari yenyewe anayoendesha Kasa ilionekana ipo neema. Kwamba ipo ahadi ya kunufaika kuwa karibu yake. Lakini haikuwa hivyo kwa Jelini! Na hakuzungumza kama mtoto wa kike akitingisha kibiriti!

“Nakua mkweli kwako, Kasa. Mimi najijua.” Akaumia, nakuhisi kukataliwa vibaya. Ni Kasa! Warembo wanammezea mate! “Nikuulize kitu?” “Niulize tu.” Jelini akakubali kwa utulivu tu. “Kwa hivi nilivyo na unavyonifikiria nipo. Kama kweli ningekuwa ni mtu ambaye unataka kuwa naye karibu. Umempenda kabisa. Ungefanyaje?” Hapo Jelini akanyamaza akifikiria. “Eti Jelini? Maana mimi nimekuwa mkweli kwako.” “Hunijui kabisa mimi Kasa. Na ninauhakika kama ungekuwa ukinijua mimi, wala usingenipa hata hii lifti.” “Nimekupa lifti kwa kuwa nakufahamu Jelini. Mwenzio sikuishia tu siku ile nyumbani kwa James. Niliendelea kukufuatilia mpaka nikahakikisha leo nakuona. Nilikuwa pale nikikusubiri wewe.” Jelini akashangaa sana.

“Kasa!” “Nataka kuwa ulipo Jelini. Na sitakuchukulia muda mrefu. Ilimradi tu kesho nikuone.” “Mimi!?” “Wewe Jelini, ndiyo. Naomba nikuone kesho jioni kama kanisani umenikatalia.” Jelini akacheka. “Bora ice cream kuliko kanisani.” “Basi iwe jioni ya saa 11.” Wakakubaliana lakini Jelini akiwa na maswali mengi sana juu ya Kasa. “Naomba nikuombe kitu cha mwisho Jelini?” Jelini akacheka vile anavyobembelezwa. “Nini?” “Namba ya simu.” Akamuona kama anasita. “Unasita nini?” “Usinielewe vibaya Kasa. Nimezungukwa na watu, mimi tabia zao nazijua. Wengi hawaishii vizuri na mimi. Wanatakaga na kadhalika. Halafu ukiwakatalia wanakuwa wakali mpaka kutaka kunidhuru.” “Nakuhakikishia mimi si mtu wa namna  hiyo na sitafanya kitu ambacho hatujakubaliana. Huoni kanisani nilikuomba, ulipokataa si uliona sikukulazimisha?” “Lakini kweli.” “Mimi nataka kampani kama unayompa Doro.” Jelini akashangaa sana.

“Doro ni mpweke. Hana mtu.” “Basi na mimi sina tofauti naye.” “Bwana Kasa unanidanganya! Nilikukuta katikati ya marafiki. Na kwa hali yako lazima una watu wengi.” “Nisingekuwa hapa kama kuna mtu mwingine. Si tutakuwa wote, utaona.” Jelini akatulia, akamuona anamkabidhi simu yake. Naomba jipigie kwa kutumia simu yangu.” Jelini akafanya kama alivyoombwa lakini kwa hakika Kasa alijua amemlazimisha si kitu alichokifanya kwa moyo. “Tayari.” “Nashukuru. Nitakushusha uliponiomba, ila naomba usipande bajaji ili usianguke. Panda taksii ili ufike nyumbani salama, kesho tukutane kwa ice cream.” Jelini akacheka tu na kunyamaza. Akamsogeza mpaka karibu na sehemu aliyojua angepata usafiri. Akamlipa kabisa dereva, ndipo wakaagana.

Akiwa ndani ya taksii akielekea kwao, mahela yakaingia kwenye simu yake. Akashituka sana. Akabaki ametoa macho akiangalia simu. Mwishoe akaamua kumtumia ujumbe. ‘Unanitisha bwana Kasa! Hii pesa ni nyingi sana.’ ‘Usijali. Kawaida tu.’ Akarudisha kwa haraka na ujumbe mwingine ukaingia. ‘Umeshafika nyumbani?’ ‘Bado, lakini nakaribia. Asante kwa pesa.’ Akaona awe muugwana. ‘Karibu. Ukifika nijulishe ili nilale nikijua upo salama.’ Jelini akasikia kujaliwa kwa namna yake. Kutoka kupigwa kibao cha usoni na Colins, kuja kubabaikiwa na Kasa, kidogo ikamrudishia ujasiri. Akacheka nafsi kwake.

Alifika kwake, Kasa amejawa tumaini. Jelini aliyekutana naye siku hiyo akawa tofauti kabisa. Alitaka kumpata na kumlipiza kisasi kwa kumdhalilisha, lakini akajikuta anatizamia kwa hamu kuja kumuona tena, wapate muda naye zaidi. Kadiri alivyokuwa akimuwekea ngumu, ndivyo alivyoamsha hamasa kwa Kasa na kutaka kumfahamu zaidi. Kasa hakuzoea kuhangaishwa. Walio mfahamu kama ni kijana aliyetoka kwenye familia ya aina yake, walikuwa wakiomba hiyo nafasi anayoiringia Jelini. Kwanza kupanda gari ya Kasa yenyewe ilikuwa ni bahari ya mtende. Jelini aliringia! Akaibua kitu cha tofauti kwa Kasa. Akili ikamzunguka na kumfikiria kwa tofauti na alivyomsikia. Msichana wa baa tu! Akabaki akisubiria ujumbe mpaka akahisi amemsahau.

Akiwa anakaribia kupotelea usingizini ujumbe ukaingia. ‘Samahani nilichelewa kukwambia kuwa nilifika salama. Usiku mwema Kasa.’ ‘Na wewe Jelini.’ Jelini akacheka na kutulia. Kasa wa viwango hasa anayethamini shule, akaanza kuingiwa na Jelini moyoni. Aliyekuwa naye usiku huo alikuwa ametulia haswa. Akabaki akimtafakari na kujigeuza kitandani akitamani ingekuwa tofauti. Angalau Jelini atokee daraja hata la chini yake kidogo tu, lakini kumlinganisha Jelini na aliko yeye, ni kama yeye yupo gorofa ya 102, halafu Jelini yupo gorofa ya 12. Mtengano mkubwa sana. Akakwama hapo akitafakari. Aendelee kuweka msisitizo, au kweli aachane naye! Akapotelea usingizini akiwa hajapata jibu.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Kama kawaida yake, ratiba yake si ngumu. Kula kulala. Alishashiba usiku, basi akalala hapo mpaka saa tano asubuhi. Akatoka kumsaka mama yake. Akamkuta akipika na kufua. Bibi alikwenda kwa mama mkubwa kwa siku chache kabla ya shuguli kuanza. Wakabaki wao tu watatu kama kawaida yao. Zikaanza stori. Yeye amekaa tu ila kumchekesha mama yake. Akampigia mtu wa pikipiki waliyezoea kumtuma hapo kwao ili alete mtori na chapati akataka na soda ya mwanae Fanta orange. Mama yake akimwangalia tu. Vikaletwa vingi tu.

“Jema amekupa hela?” “Mimi si mjinga mama. Usianze kunichota.” Akanyanyuka wakicheka. “Naona umejaa!” “Na nguo zako zote za shuguli nakulipia mimi. Na kaka namnunulia mashati ya shuguli zote.” “Sasa Jelini mwanangu kama unayo pesa yote hiyo mama yangu, si uanze kufanya kitu kitakachokusaidia kukuingiza kipato?” “Umeanza mama.” Akaondoka kabisa hapo. “Ila nashukuru kwa msaada wa nguo.” Hakujibu, akajua ameshakasirika. Akamsikia akimuita mtoto wake akale.

Baada ya muda alipomaliza kula na kujitayarisha akaondoka. “Utarudi?” Mama yake akamuuliza wakati akitoka. “Siendi baa.” Akamjibu hivyo. “Sawa mama yangu, nitakuwa nakusubiri.” Akajua mama yake anachomaanisha, haamini kama kweli atarudi, wala hakumjibu, akatoka. Alikuwa amependeza sana, kama kawaida yake hajikosei.

 Kweli akaenda kumnunulia mwanae nguo. Zaidi chupi. Hicho hakuwa akisahau. Jelini alipenda sana chupi. Akamnunulia nyingi kama kawaida yake hanaga kuwaza kesho ila matumizi. Akajinunulia na yeye vitu vyake. Akalipia kwa fundi nguo zake na za mama yake, akarudi nyumbani na kuku mzima wa kuchoma na ndizi. Mama yake akimwangalia tu.

Akaoga tena. Akabadili  nguo, akajitengeneza na kuaga. “Ndio safari ya baa sasa?” Akaanza kucheka. “Mama Jema siku hizi umekua mwingi wa maswali wewe! Utakufa pressure bure! Wewe tulia.” “Kwa hiyo ni baa?” “Siku hizi mambo ya baa napunguza.” “Pombe tena basi?” Akazidi kumdodosa taratibu. “Si pombe ni ya kurithi jamani? Ukoo mzima wanakunywa, kwa nini na mimi nisinywe?” “Wewe unarithi kunywa pombe tu, na mengine?” “Kuzaa pia nimekurithi mama yangu. Wala si kimoja.” Mama yake akaguna kwa masikitiko. “Na wala sitachelewa, usianze lile swali lako la kama narudi.” “Bora.” “Na nitakuletea bia mbili za kulalia. Au unasemaje?” “Na mimi Fanta ingine.” Akaongeza Jeremy, mwanae. “Msijali.” Akatoka.

“Tuone vitu alivyokununulia.” Akaenda kumletea bibi yake na kushanganzwa sana. “Huyu pesa kapata wapi?!” “Mwenzio nimefurahi!” Jeremy akamwambia bibi yake akirudia kuangalia vitu vyake. “Basi hela yote itapata matumizi asifanye cha….”  Akaona anyamaze tu.

Taka Cha Mvunguni.

Kasa alikuwa akimsubiri barabara kuu. Alipomuona tu, akamfungulia akapanda. “Umependeza Jelini!” Akacheka akifunga mkanda. “Asante. Na asante kwa hela.” “Ulishashukuru jana, bwana! Vipi siku yako?” “Nzuri tu. Na wewe kanisani?” Kasa akacheka. “Ibada ilikuwa nzuri tu.” Akatulia asije akazungumza neno baya kwa kuropoka.

Hawakwenda mbali sana, ila sehemu ya hadhi kama kawaida yake Kasa. Wakaagiza ice cream, wakaanza kula taratibu tu, Jelini kimya kama aliyejionywa na kama anayesubiria kitu. Maana alijua kwa upewaji ule wa pesa, kuna kitakachofuata. Na Kasa naye alishamsikia akisema watu wanapenda kumdai kila wakimpa kitu, akaona anyamaze. Wakala ice cream taratibu tu.

“Vipi maandalizi ya send off?” Akavunja ukimya. “Yanakwenda vizuri sana. Jema anauungwaji mkono mkubwa mpaka mama ameshangaa. Hakujua kama ana watu wengi. Tulijua tungefanya kitchen party ndogo, lakini kumbe anamarafiki wengi sana. Kila mtu anatuma mchango. Tuliishiwa vikoi, ikabidi mama aagize tena.” “Hata James amepata uungwaji mkono mkubwa sana. Ukishiriki mambo ya watu, na watu watajituma kwako.”

“Wewe umeoa?” Alishituka sana, hakutegemea hilo swali. Akacheka na kumuonyesha mkono kwamba hauna pete. “Kujibu swali lako, hapana sijaoa.” Jelini akacheka taratibu. Wakatulia. Akaona ni muda wa kuweka ombi lake mapema kutimiza azma yake, kufunga midomo rafiki zake. “Siku ya harusi utakuwa na nani?” “Mama na kina mama mdogo. Dada Doro pia atakuwepo.” Akajibu bila ya kufikiria, na Kasa akajua. “Mbona unacheka?” Jelini akamuuliza. “Nikimaanisha mtu wako.” Jelini akafikiria kidogo na kupata jibu. “Oooh!” Akaanza kucheka kama kawaida yake.

“Unamaanisha mchumba?” Akauliza akicheka hana mbavu. “Au boyfriend.” Akaongeza Kasa kama kupunguza uzito na hilo likamfanya azidi kucheka. “Jelini!” Kasa mwenyewe akajikuta akicheka. “Mwenzio sitaki tena mambo hayo. Unakua unagandwa na mtu! Huna raha wala uhuru na maisha yako, na mimi nataka kuwa huru sio simu zakuanza kuulizwa upo wapi na unafanya nini!” “Hutaki?” “Akuuu! Yaani unajikuta gafla eti mtu mmekutana naye tu, anaanza kutawala ratiba yako yote! Eti uwe wapi na ufanye nini! Hapa hapafai! Pale panakufaa! Sasa unajiuliza huyu mtu vipi! Umekutana naye tu, basi tayari eti anajua nini unataka! Au eti nini unatakiwa kufanya! Halafu anaanza kukukataza bila kujali furaha yako!?”

 “Wewe furaha yako nini?” Ikabidi Kasa aulize akiwa amechoka kabisa. “Kuwa na washikaji baa, kucheka. Kila mtu anahaiba yake. Ukikaa na wengi, unapata mengi. Siku inanoga. Sasa unakua na mtu mmoja, pengine yeye mwenyewe kisirani. Mnajikuta wote mmekwama kwenye hasira zake! Halafu maisha yako yanakuwa hayana raha! Akuu! Mimi hivyo sitaki.” Kasa akacheka taratibu akitafakari alichozungumza.

Mwishoe akasema akiwa mawazoni. “Mimi nafikiri mahusiano ni kuzungumza na makubaliano.” “Huo mwanzo mzuri sana. Ila baada ya hapo, unajikuta ni yeye tu ndio anataka mambo yake yafuatwe. Hakusikilizi tena. Kwa hiyo kwa kifupi mimi sina mchumba wala boyfriend. Na sitaki hiyo adha. Kwa hiyo siku ya harusi nitakuwa na yeyote atakayekuwepo karibu, na anayetaka kufurahia. Sio tena matatizo.” Kama kawaida yake akajibu kirahisi, asitake kuchosha akili zake kuanza kufikiria jinsi ya kujibu akiwa amewaza nini Kasa anamaanisha! Hapana. Alichokisikia ndicho alichokijibu kirahisi tu. Kasa akatulia kabisa akiendelea kukubaliana na utofauti wao kimaisha. Hata moyoni akaona kweli hatamuweza msichana kama Jelini asiye na mipaka! Akaanza kujirudi na kukubaliana naye yeye mwenyewe na hata Doro alipomwambia hatamuweza Jelini.

Wakamaliza, akamuaga. “Narudi nyumbani.” “Leo baa huendi?” “Acha nikwambie ukweli Kasa. Najua Doro ni rafiki yako, ila mimi ni kampani yangu kubwa. Ndio sababu ya kuwa nakuwa baa kwa uhuru nikijua na yeye yupo. Sasa kwa sasa hatupo vizuri sana. Kuna ukweli aliniambia. Sijui kwa nini umeniuma sana nashindwa kurudia tulivyokuwa zamani. Sasa sijui kwa kuwa ni yeye aliyeniambia hivyo au jinsi alivyoniambia kwa kunitusi! Sijui! Ila nahisi ni vile nilivyomtegemea kwangu na kule tulikotoka.” “Mmetoka wapi na Doro?” Kasa akauliza.

“Mbali sana. Kama utakuwa umemfahamu muda mrefu, utajua alikopita. Mimi ni mdogo sana kwake, lakini nilisimama naye kwa karibu sana bila kinyongo wala kulalamika. Sasa kuja kuniambia maneno makali, tena bila kosa! Imenivuruga kidogo hata hamu ya baa imepungua. Nimeona nitulie tu nyumbani kwa muda.” Kasa akatumia akili kumuuliza kijanja kujua sababu. “Mmegombana muda mrefu?” “Wala si kugombana, maana mimi siwezi kutukanana. Alinipigia simu nikiwa nimelala nyumbani kwake, yeye akiwa kazini, ndipo akaanza kuniporomoshea mvua ya matusi. Ila aliomba msamaha akisema alikuwa na siku mbaya kazini. Nimemsamehe, lakini yale maneno yananisumbua kweli! Ila kujibu swali lako, leo baa sitakwenda. Narudi tu nyumbani.” Wakaondoka hapo kurudi garini.

Walipopanda tu garini, Kasa uzalendo ukamshinda tena. Sitaki nataka. Ukweli Jelini anavutia haswa. Anatamanisha kwa namna zote, kasoro tu hizo tabia zake. Na mwenyewe hazifichi na wala haoni tatizo na alivyo. “Unafikiri tutakuja kuonana lini tena?” Jelini akakunja uso akiwa anafikiria huku akijiweka sawa kitini. “Eti Jelini?” “Hata sijui Kasa! Ila siku za harusi zimekaribia, vikao vitakuwa vikifanywa karibu kila siku. Halafu mama anataka Jema arudi nyumbani apumzike siku chache kabla ya harusi. Jema mkali sana kwangu sio kama mama. Hataki niwe natoka hovyo. Kwa hiyo sijui.” “Basi niombe vitu viwili.” Jelini akamwangalia.

“Usikatae kabla ya kufikiria.” Jelini akacheka. “Siku ya harusi uwe kampani yangu, tukae wote. Na jumatano tutoke kwa chakula cha usiku.” Jelini akatulia. Ukweli hakumpenda Kasa kimapenzi hata kidogo. Kuja kuwa naye harusini na haiba yake ya ustaarabu, akaona atamnyima raha hata ya kunywa. Akapoa kabisa, akiwaza jinsi ya kumkatalia.

“Jumatano tunaweza kutoka. Ila harusi si nitakuwa upande wa bibi harusi wewe bwana harusi?” “Hatutapanga viti kwa namna hiyo. Tumekusudia kupanga viti kwenye meza za duara, watu 10.” “Kwa hiyo wewe hutakaa na wenzako?” “Unaweza kukaa na sisi.” Hapo pakawa pagumu zaidi. Jelini anapenda uhuru wake kama ndege. Leo kumuweka katikati ya wastaarabu, wanaohesabu na kufikiria maneno ya kuzungumza, wengine kama Kasa wanaosema bia inayompa yeye kiu eti ina ladha mbaya mdomoni, nikumziba pumzi.

“Mbona unakua mzito hivyo Jelini!?” “Nikwambie ukweli lakini usikasirike?” “Niambie tu.” “Hapana.” Kasa aliumia sana. Pesa yote aliyompa, hadhi yake, leo anamkatalia! Ikamuuma sana mpaka akabadilika. “Labda niulize ni kwa nini?” “Mimi na kina mamdogo tumepanga mipango yetu siku ya harusi. Wale wana fujo kunizidi mimi. Hutaweza kumudu hiyo fujo na kelele zetu. Hutaweza kukaa kwenye meza yetu na mimi najihisi nitajipunja sana kukaa na nyinyi. Hadhi yako ni kubwa sana Kasa. Usiku wote nitakuwa nikijiwinda maneno. Acha siku hiyo nifurahie na ndugu zangu.” Jelini aliyedhani ni malaya kwa kumtizama na chakaramu tu, anamsimamo wake tena mgumu haswa.

“Tafadhali usichukie. Mimi najijua mwenyewe.” “Nimeelewa, na nashukuru kuwa muwazi zaidi. Kwa hiyo unafikiri hata hutanisalimia kabisa?” “Siwezi kutofanya hivyo. Nishakufahamu kwa karibu hivi! Lazima kukutafuta kujua umekaa wapi. Kama utaniruhusu lakini.” Hapo Kasa akaridhika sana. “Si ni sawa? “Kabisa tena ruksa.” Wakacheka, lakini hilo likamfurahisha sana Kasa. Shida yake ni kurudisha heshima mbele ya rafiki zake akionekana mtoto kama Jelini anamfahamu kwa karibu. Ila hata yeye alishamuona si mtu ambaye wanaendana hata kidogo.

Kasa alilelewa kwenye mazingira ya hadhi ya juu sana. Kwenye pesa ile yakutowaza baada ya miaka mitano maisha yatakuaje. Baba yao alikuwa na pesa sana. Alikuwa na vitega uchumi vya uhakika akitumia akili na nguvu kuhakikisha pesa haikauki kwake. Kasa alikuwa akiingiza pesa kutoka kwa baba yake kila mwezi, kubwa kuliko mshahara wake. Yaani kwa kumtizama tu kasa, ungejua ni samaki wa kukaangwa. Amejaa mafuta. Ni mstaarabu wa asili sio wakujifunza ukubwani baada ya kufanikiwa. Alizaliwa ustarabuni. Haitachukua hata dakika moja akimpeleka Jelini katikati ya jamii ya kwao na kuonekana ni wa tofauti. Akamshusha kituoni, akaondoka.

Chachandu Kuwekwa Pilipili.

Hilo juma likawa kimya kati yao, Kasa naye akaona amuache tu maana Jelini hakukosea hata kumtumia ujumbe wa kumjulia hali. Busy na yeye kwa maandalizi ya shuguli ya dada yake. Jioni aliyoingia Jema hapo kwao ikawa furaha, mwali ameingia. Mama zake wote na bibi walikuwepo hapo. Wao wanakunywa na kucheka bila kikomo. “Mimi mwenzenu vyakukesha sitaviweza. Pombe sinywi, halafu tokea alfajiri nilikuwa busy kazini kuweka mambo sawa ili kumsaidia bosi wangu kabla sijaondoka.” Jema akataka kuingia chumbani alipoona shangwe haziishi. “Jema naye! Anajua kukata watu stimu! Sasa kulala sasahivi wewe Jeremy?” Mama yao mdogo ambaye anamfuata mama yao akalalamika. Ila huwa anapata nao sana hao watoto wa dada yake. Mlevi ndio maana na Jelini anampenda. Tofauti yao ni yeye anaijua pesa mpaka shilingi. Ana maduka ya nguo za jumla, Kariakoo na vipodozi duka ameweka Sinza. Amejijenga haswa, kwa hiyo wakati mwingine walikuwa wakitafutana na Jelini kwenda kunywa. Hakubahatika mtoto wala ndoa.

“Kaa basi nikupe ya mjini.” “We Koma wee! Mbona umemkazania mwanangu!? Ulitaka kukesha naye hapa ili umfanyaje?” Mama yake akaingilia. Na Jema alijua atamtetea tu. Wote wakaanza kucheka. “Keshakwambia pombe hanywi, na amechoka. Unataka kesho atokee mbele za watu kama kazee!?” “Nataka kumpa ya mjini na wewe dada!” “Jelini huyo hapo mtaka ya mjini. Mwache Jema.” “Mimi yote nayajua mama yangu. Twende Jema nikakuulize maswali ya msingi.” “Sasa na wewe Jelini usianze.” “Sasa kwa taarifa yako mama, hata yeye atanishukuru huyo Jema. Msianze kunipinga. Hii ndio zawadi yangu kwake.” Jema akacheka na kutaka kujua.

“Ndio twende sasa kabla sijampigia simu mpenzi wangu, maana nikianza kuzungumza naye sikati mpaka nilale.” “Sasa wewe nenda kamuage. Usizungumze sana maana nilikuwa nakusubiri nikufundishe jambo zuri sana. Muage tu wakati mimi namalizia bia yangu kutoa aibu.” Wakaanza kushangilia zaidi mama mdogo alishajua. “Mimi mwenyewe nakuja.” “Sasa utamtia aibu Jema jamani! Mimi namjua dada yangu huyu. Haya kwake mazito.” “Kwani mnaenda wapi?” Akauliza mama yake mkubwa.  

“Kuna shule hiyo, mamdogo aliniita, wakati shoga yake anaolewa. Yule mwali alikuwa dizaini kama hivi za Jema. Akafungiwa ndani siku 20, huyo mama akawa anaenda. Ndio shoga yangu huyu akaniita na mimi niende.” “Kukata mauno?!” Mama yao akashangaa sana.

“Sasa dada wewe acha ubishi. Hapo hata mimi Jelini nampongeza maana nilisahau kabisa. Bwana tulipewa shule ya nguvu!” “Sasa wewe badala umuite huyu kwenye mambo ya maana, unakwenda kumuita kwenye kukata viuno! Mama unamsikia mziwanda wako?” mama Jema akawa amekasirika. “Kila mtu kuna alichoandikiwa dada, bora mkono uende kinywani. Kama yeye kachagua ya kitandani, si bora awe mjuzi kuliko anazunguka kwenye vitanda vya watu akitia aibu!” Mamdogo alishalewa, na walimjua kwa kupenda vitanda vya wanaume. Jelini anacheka mbavu hana.

“Wewe unafikiri duka la Sinza lile nililifungua kwa pesa yangu?” “Waambie mamdogo.” “Haki sidanganyi. Mimi sikutia uvivu. Nilijifunza kwa yule bibi, nikatoka hapo nikamkamata mwenye nazo. Bwana yule mzee alikuwa akitoa hela bila kuombwa!” Wakaanza kucheka. “Haki siongezi. Niliyokuwa nikimfanyia yule baba, akawa kama mjinga! Jamani ipo siri kubwa sana ya kitandani. Mapenzi yapo sikatai. Ni kama chachandu tu, lakini ikiwekwa pilipili, vyaongeza ladha.” “Tena yule bibi alikuwa anasema chakula ni chakula. Lakini kisicho na chumvi na chenye chumvi tofauti.” Wakazidi kushangilia wawili hao wakipokezana maneno. Pombe ishaingia kichwani.

Ila hapo wakamgusa Jema. Akakumbuka James anavyotizamia fungate, halafu hana ajualo! Akajirudi. “Mimi nataka kujifunza, mama!” Jema kasema, wote wakaanza kushangilia pombe ikisaidia kupiga kelele. “Wewe unataka ujifunze mambo ya kitandani kwa malaya hawa! Utamuogopesha James.” “Sasa kwa taarifa yako Jema, ukitaka ndoa inoge, ukifika chumbani kuwa malaya.” Jema alishituka sana. “Haaa! Mamdogo jamani!” “Basi ujue malaya wa mjini watakusaidia. Hakuna ulokole kitandani Jema. Shauri zako, utanikumbuka! Wakimshika mzungu wako yule, wakamuonjesha ya uswazi, huna utakalofanya akarudi. Utanikumbuka, labda asije onjeshwa.” “Basi mamdogo na wewe njoo.” Jema akafanya wazidi kucheka vile alivyoonekana ameingiwa hofu anataka msaada kwa kila mtu. “Hutaki tena kumpigia simu mpenzi akubembeleze ulale?” Jelini akamkejeli akicheka. “Nishaona nitatia aibu. Bora mje mnisaidie kujiandaa.”

Wawili hao wenye vichwa vinavyofanana waliohundhuria unyago wa bibi, wakamfuata Jema nyuma tena kishabiki. “Pumu imepata mkohozi. Na Mode anavyopenda ushangingi huyu!” “Watamtia ujinga hapoo!” Mama Jema akaongeza kwa dada yake wakiendelea kunywa.

Mwali Hafundwi Hadharani.

“Kwanza tupe staili zako ulizojiandaa nazo.” Akaanza Jelini. Hilo swali likawa gumu kwa Jema. “Kwani kunatakiwa ziwe ngapi?” “Wewe tuonyeshe ulizo nazo.” Akaongeza Mode, mama yao mdogo. Jema akaanza kubabaika. “Acha masihara Jema wewe! Kwamba huna moja!? Kwani huwa mnafanyaje?” Wakazidi kumnyima raha. “Mimi na James hatufanyi mapenzi.” Jema akajibu kwa aibu kidogo akionekana mnyonge mbele yao. Bwana walicheka mpaka wakaaa chini.

“Nimeona nije, kabla hamjamtia hofu akaona hataiweza ndoa.” Akaingia mama Jema na bia yake mkononi wao wakiendelea kucheka ila kwa mshangao. “Hivi ujue mama Jema bado ni bikra!” Mpaka mama yake akashangaa. “Sema kweli?!” Mpaka mama yake ikawa ngumu kuamini. “Mama naye!” Jema akajichekesha. “Sasa na huyo James unamtulizaje?” “Jamani si kila mwanaume ni mdhaifu kwenye hilo jambo. James anataka tusubiri mpaka ndoa.” Walishangaa kama wameona chatu hapo chumbani.

“Kama hamnifundishi, ondokeni, mwache kunishangaa.” “Mimi nitakufundisha dada yangu wala usijali.” “Na mimi nitakuandalia begi zuri sana la fungate. Nguo za uchokozi. Chupi za ukweli sio machupi yakizee. Utamkera mumeo.”  Akaongeza Mode. “Wewe una kaumbo kazuri Jema, lazima ujifunze kujiacha wazi mbele ya mumeo uvutie.” “Acha kunidanganya Jelini. Wewe ndio una umbo zuri.” “Mimi najijua mzuri navutia.” “Pumu imepata mkohozi.” “Kweli mama. Kwani uongo mamdogo?” “Aaah sana tu.” Kama kawaida yake kumpa sifa Jelini shoga yake. “Lakini na wewe Jema mzuri. Tena unavutia kwa namna yako dada yangu ndio maana James anakupenda wewe.” Jelini akamtia moyo dada yake mpaka mama yake akafurahi.

“Kila mwanamke ana uzuri wake. Wala usijifiche mbele ya mumeo, maana hutakaa ukawa mimi na wala mimi sitakaa nikawa wewe. Tumia ulivyonavyo vizuri, tena kwa ujasiri. Mimi kibonge, najua jinsi yakuweka mwili wangu mbele ya mwanaume, kwa kunitizama tu, kabla hajanishika, mnara upo hewani. Lakini nikiwa mtupu na hizo nguo za ndani alizokwambia mamdogo Mode.” Jema akawa anaona aibu. Mamkubwa naye akaingia. “Mama ameenda kulala nikasema na mimi nije nipate shule.” “Sasa na wewe usianze maneno mengi ukamfanya Jelini apotee pointi. Alikuwa akizungumza naye vizuri tu hapa. Tafuta mahali, kaa.” Mama Jema akamwambia dada yake.

“Kwa hiyo umesema ujasiri? Maana eti mimi sijioni kama navutia.” Jema akaongea kwa wasiwasi. “Hakuna mwanamke asiyevutia mbele ya mwanaume dada yangu. Toa aibu, jiamini. Mimi kila siku nasema biashara matangazo. Unavyojiuza kwa mwanaume, ndivyo atakavyokuchukulia. Ukijiweka thamani, na yeye atakuthamini.” Wakaanza kumshangilia Jelini, kidogo aibu ikaanza kutoka kwa Jema.

“Tuanze na ukaaji kitandani. Mtoto wa kike hukai kitandani kama shuka au mto.” Walicheka, ila Jelini akawa yupo serious. “Nakaaje sasa?” “Kwanza inategemea unataka kufanya nini hapo kitandani. Kama unataka kuanza romansi. Kwamba umekaa kichokozi ili usimame umtoe nguo au..” “Jelini wewe! Mimi ndio nimvue?!” Chumba kizima walicheka mpaka mama yake. “Msinicheke bwana! Sasa si ataniona mimi nimek…” “Tulikwambia nini wewe?” “Chumbani natakiwa kuwa malaya.” Akajibu Jema mwenyewe na cheko.

“Ushawahi ona malaya chumbani?” Jelini akamuuliza. “Hawana aibu ndio maana wanalala na mabwana zenu wasomi, tena bila hofu. Halafu pesa yote ambayo ilitakiwa ije kwako na watoto, inaishia mtaani. Sasa kwa nini utake mtu akamfanyie mumeo kitu unachoweza kufanya mwenyewe.” “Haya basi nifundisheni.” Ikaanza shule ya kwanza. Yeye Jema aweje kabla ya tendo. Jelini akamfundisha kwa vitendo kabisa. “Na unayaweza!” Mama yake akamwambia. Akacheka na kuendelea.

“Na unapotoka kitandani unamfuata kuanza romansi, sio tena unatembea kama unakwenda migombani kwa bibi na jembe! Taratibu ili akuone vizuri ukiwa na lingerie yako mwilini, zile nguo zako za uchokozi. Na sio ukifika midomoni tena umetulia tu unanyonywa midomo, unakazi ya kuachia mate tu mpaka yadondoke! Hapana. Mdomo msafi, ladha jitafutie mwenyewe hata pipi au spray za mdomo kwa harufu utakayochagua. Zuia mate yasijae mdomoni, hiyo tena kero na kuleta kinyaa. Na wakati wa denda, lainika Jema. Sio umekakamaa kama upo kwenye gwaride bwana!” Jema akaanza kujifikiria alipokuwa akipewa denda alikuwa akifanyaje! Akahisi alikuwa akikakamaa.

“Na mwanamke ni multi tasks. Tuna uwezo wa kufanya mengi kwa wakati mmoja na hatukosei. Ndio uwezo wa kipekee tumepewa sisi wanawake na Mungu. Sasa hiyo zawadi unatumia hata kwenye mapenzi. Unapata denda huku mikono yako ya kike ikibarizi mwilini mwake.” Jema aibu. “Mamdogo simama.” Mode akasimama, Jelini akamwambia Jema aangalie. “Mpaka kushika huko!” Jema akashituka sana. “Hee kumbe! Tena sio ushike kama andazi unataka kutozea kwenye chai! Koni inachezewa kabla ya kulambwa.” Jelini alicheka mpaka akakaa chini. “Ndio je! Wewe Jema vipi bwana! Tena kama amevaa suruali ili kumchanganya unafungua zipu tu, unachomoa mzigo wote mpaka kengele zake halafu unamchezea huku ukila denda, unanyonya mpaka masikio uone kama hajaivua suruali haraka akilia bila msiba!” Wakacheka mbavu hawana.

“Wewe unaenda haraka bwana mamdogo Mode! Huyo hajui hata jinsi ya kushika koni.” Wakacheka na kugonga. “Malaya nyinyi!” Mama Jema akamwambia Jelini na Mode na kuzidi kucheka. “Mpe mpaka shule za kengele za mumewe.” Wakacheka na kugonga. “Zile kengele zina mistari.” “Mnamchanganya bwana! Hamjamaliza koni yenyewe.” Jelini alicheka sana. “Kumbe mamkubwa unataka na wewe!” “Acha nijifunze bwana. Hakuna kufudhu maishani. Kila siku ni kujifunza tu.” Basi hapo Jelini akajiachia akamfundisha romansi tu. Akamuelekeza mengi hatua kwa hatua.

“Ulale mwali, kesho romansi ya kumchanganya kama hutaki mambo mengi kitandani. Umechoka. Unataka kumpa vya chapuchapu, ulale. Sasa unavyoandaa viungo, jinsi ya kukaanga kabla hujatupia mhogo ndani mpaka kuivisha kwa tui. Taratiiibu bila yeye kujua kwa wakati huo wewe hutaki, unahitimisha tu.” Wakacheka wenyewe kama waliokumbuka jambo! “Halafu sasa staili za kutiana. Sio kutwa kitandani mpaka mchakaze godoro!” “Au kuharibu chaga!” Mamdogo akaongeza na kugonga kwa Jelini. “Mwanamke jua kutumia mazingira. Akijileta jikoni, unaye. Bafuni, unampa. Ukimkuta kwenye kochi baada ya taarifa ya habari, unamkojoza taratibu.” “Akiingia ndani kutoka kwenye shuguli zake unampokea zipu ya suruali sio mkoba tu.” Walicheka wawili hao, kama mazuri.

“Mamdogo, akiingia tu?” “Kumbe. Mkono mmoja mkoba, mwingine zipu ya surulia midomo inamnyonya kama pipi tamu. Ukipiga goti mbele ya suruali, ukimaliza hapo, anaacha pesa yote anarudi kwa mkewe mtupuuu.” “Jambazi huyu!” Mama Jema akafanya wacheke. “Na lugha ya kufanya mapenzi, Jema. Nilitaka kusahau.” “Na mihemo na sauti zake. Sio kujikaza  mwenzio anahangaika, umetulia tuli kama unachomwa sindano!” “Au gogo!” “Au kugugumia kama unatolewa mwiba!” Walicheka mpaka basi. “Jemaaa!” Mama yake mkubwa alicheka sana vile alivyomuona Jema ameshangaa. “Hivyo mtaninyima raha. Sitaweza vya milio au kuongea.” “Sasa ukianza lugha za kwenye bibilia kitandani, utamkata stimu mumeo. Ongea jambo mpaka limsisimue.”

“Au unatoa mhemo ukilia kama unakunwa na ukakunika. Sauti nzuri, laini mpaka ajipongeze anafanya jambo zuri. Sio tena kimya kama mpo kwenye kikao cha bunge, unamsikiliza spika!” Wakazidi kucheka. “Kesho tunaendelea Jema dada yangu. Tutakufundisha hema ya romansi. Na ya wakati umemwaga mchele, ukitaka atie mboga. Na wakati akikwea mlima.” “Na akiwa chumvini.” Walicheka hao, kama mazuri, Jema akajifunika uso. “Mnazidisha bwana!” “Haa! Wewe mama hujasikia wale wanawake wananyonywa, wametulia kimya mpaka mwanaume anagairi!” Jelini akauliza bila aibu. “Basi mimi napata stori zao baa kwa wale wanaume malaya. Mamdogo yupo sahihi. Wanasema kuna wanawake wapo kama wanakamuliwa jipu! Onyesha kwamba ni tamu. Tena mwambie tamu, nataka tena. Uone kama hujawa unapiga mabao kulia na kushoto.” “Haaa!” Jema akashangaa kwa mshituko, akakimbilia kitandani na kujifunika na mto. Alifanya wacheke sana. “Ila nimefurahi sana kunifikiria Jelini. Hakika ningetia aibu.” “Karibu, shule nyingine kesho kabla ya kichen party na baada.” Wakatoka kumpisha apumzike.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment