Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Mapenzi & Pesa! - PART 1 - SEHEMU 38 - Naomi Simulizi

Mapenzi & Pesa! - PART 1 - SEHEMU 38


 Wakati anamvuta kwa nguvu Naya akilia, wakashangaa mbele yao gari ya Joshua imewapita kwa kasi na kwenda kugonga gari ya Malon kwa nguvu sana, kisha akarudi nyuma, akakanyaga mafuta na kuivamia tena gari ya Malon ubavuni, akaibamiza mpaka kwenye ukuta wa kina Magesa. Kulitoka milio ya sauti kubwa mpaka wa ndani wa kashituka, na Malon mwenyewe alishituka akabaki amemshika Naya kwa nguvu, Naya akilia.

Joshua akatoka ndani ya gari kwa haraka akamkimbilia Malon kumrushia ngumi. Malon mtoto wa mtaani alishaiona ile ngumi mapema sana, akakwepa. Naye Joshua kama aliyejua angekwepa, akampiga ya kushitukiza kwa haraka za mbavuni mfululizo kisha usoni. Wakazidi kupigana, Naya amesimama pembeni. Geb akatoka, alipomuona Naya, Joshua na Malon, akakimbilia kule walipokuwepo na askari walipoona vile bosi wao anakimbia, mmoja wao akatoka na kumfuata.

Badala Geb agombanishie, akaanza na yeye kuchangia. Malon hakuzidiwa. Akaendelea kupigana nao wote wawili. Mama G, Grace, Nanaa wanatoka, wanakuta hiyo fujo. Naya analia pembeni, wanaume hao watatu wanapigana karibu kutoana roho. Joshua na Geb wakamvamia kwa pamoja ndipo wakaweza kumuangusha chini. Wakaanza kumpiga mateke kwa pamoja mfululizo.

“Geb Magesa!” Sauti ya mama G ikasikika kwa juu na ukali ndipo Geb akawa kama amezinduka. Akasimama. “Unafanya nini!?” Mama G akamuuliza. “Huyu ni Malon, mama. Anatufuata mpaka nyumbani kwangu! Hapana mama. Hiyo ni dharau.” Joshua alikuwa akiendelea kupiga mateke pale chini kama aliyepagawa. “Na wewe Joshua, inatosha. Acha hivyo sasa.” “Nimemkuta anataka kumchukua tena Naya! Huyu ni mshenzi mama. Ameona tumemnyamazia, ndio anaona sisi ni wajinga.” “Inatosha Joshua. Acha hivyo. Mwache huyu askari amfunge pingu apelekwe polisi, vyombo vya sheria viamue. Toka  hapo Joshua kabla hajakuharibia maisha yako, ukafia jela kwa kumuua.” Askari akamuweka pingu na kumnyanyua pale kwa nguvu.

“Unanifunga kwa kosa gani wakati mimi nimesimama hapa kwenye eneo la nje, la uma! Sijaingia kwenye eneo la mtu yeyote yule? Huo si ujinga tu!” Malon akaongea akitema mate yenye damu huku akicheka. Na alikuwa sahihi. Pale ni nje ya uzio, sio ndani ya mpaka wa Geb. Geb akamsogelea na kumpiga ngumi ya tumbo kwa nguvu mpaka akainama. “Geb Magesa!” Mama yake alishituka nusu aruke. “Huyu ni mshenzi mama.” “Sasa nimekwambia acha. Unanisikia Geb?” Geb akanyanyua mikono juu kama aliyesalimu amri kwa mama yake na kurudi nyuma. Nanaa alikuwa ameshangaa, amepigwa na butwaa, mdomo wazi karibu mate kumdondoka. Hakuwahi kumuona Geb akimpiga mtu vile.

Akamsogelea Malon karibu. “Sura yako ikionekana tena kwenye hili eneo ambalo anaishi mama yangu, mke wangu na watoto wangu, nakupiga risasi. Na sikutishi. Usinijaribu.” Akamgeukia yule askari. “Piga simu ofisini kwenu, ita gari ije imchukue huyu jambazi.” Malon akacheka sana akiwadharau. Geb akawa kama amekumbuka kitu. “Hivi ni nani aliyemfungulia mlango Naya na kumruhusu atoke nje bila idhini yangu na mimi niliwaambia Naya asitoke ndani na wala asiruhusiwe kuingia mtu ndani bila kuulizwa?” Geb akauliza na wote wakamgeukia yule mlinzi vizuri.

Joshua akamsogelea Naya karibu. Bado alikuwa akilia kwa hofu. “Naya, niangalie mimi ni Joshua, na upo salama. Hakuna wa kukuchukua tena wala kukuumiza.” Naya alikuwa amepatwa hofu ya ajabu, anatetemeka kama aliyekuwa amewekwa kwenye barafu! “Unakumbuka nilikuahidi nitahakikisha hata wakikusogelea hawatakuchuku tena?” Naya akakubali akilia. “Basi jua upo salama. Naomba utulie na usiogope.” Joshua akamvuta karibu zaidi, akamkumbatia vizuri. Akaendelea kumbembeleza akimsugua taratibu.

“Ni Chalo. Anasema alikuwa akifanya kazi na huyu jamaa zamani, kwenye kampuni hiihii. Akasema wanafahamiana sana na ni mtu wa Mungu sana. Alishajua kama anaye mwanamke wake anaitwa Naya tokea wakifanya naye kazi. Kwa hiyo alipoomba aitiwe mkewe, akisema yeye hataki kuingia ila atoke tu wazungumze hapa nje, ndipo nikamruhusu Chalo akamuite.” Wakamuona Geb anatoa simu. “Nakutaka ufike hapa na walinzi wengine watakaonilindia kwa leo wakati nikitafuta kampuni nyingine ya ulinzi.” Kabla hajajibu, Geb akakata.

“Hatukujua..” “Mnachotakiwa kujua ni maagizo ninayotoa mimi na si vinginevyo. Nenda kaweke silaha chini, subiri gari ije, ili haya unayoeleza hapa, ukaeleze polisi, ndio wao waamue kama sio kushiriki njama ya kumtorosha mke wa mtu.” Hapohapo Geb akatengeneza kesi. “Samahani sana ila..” “Hapo ndio unaharibu kabisa. Wewe ondoka kabisa hapa. Nenda kasubiri pale kibandani. Hicho unachotaka kukifanya nikumpandisha hasira zaidi. Wewe nenda, uje kuzungumza na kiongozi wenu, yeye ndio atazungumza na wewe.” Grace akamkatisha na kumwambia hivyo yule mlinzi. “Nataka kuomba tu msamaha.” “Sasa mimi ndio nakwambia muache sasa hivi, huna utakachozungumza ukatengeneza ila kuharibu zaidi. Kama huamini, basi wewe endelea kutofuata maelekezo yake.” Grace akamtahadharisha. Akaondoka na Malon akiwa amefungwa pingu.

Mama G akamgeukia Joshua. “Samahani sana Joshua. Ni kitendo cha muda mfupi mpaka nahisi ni kama waliokuwa wakimvizia abakie peke yake maana wote tulikuwa nje tukifanya kazi kwenye meza za wageni. Sasa tukamuacha akigawa pipi kwenye hizo meza. Tukasema tumuache kama kumpa nafasi afanye kwa uhuru tena akigawa kwa kuhesabu.” “Nashukuru mama, lakini bado Naya hajafika kwenye uwezo wa kuwa peke yake. Naomba tumpe muda zaidi.” Joshua akawa kama analaumu.

“Maana ningechelewa kidogo tu, angefanikiwa kumuingiza kwenye gari yake na kuondoka naye tena! Bado Naya hana nguvu ya kushindana na mtu. Alikuwa akimvuta kikatili sana huku akilia!” “Samahani baba. Naomba tusamemehe.” “Na mimi nisamehe Joshua kwa kuwa nilikuahidi nitakuwa naye kila mahali. Samahani.” Nanaa naye akaongeza. Joshua alikuwa na hasira. Akatamani aondoke lakini Magesa ndio alikuwa akimtegemea yeye ampigie kinanda ili aimbe.

Bila kuchelewa wakiwa bado kwenye ile taharuki, walifika walinzi wengine wawili na kiongozi wao wakiwa na gari. Wakawapakia wale walinzi wawili pamoja na Malon kuelekea kituo cha polisi. Geb, Joshua na Naya wakafuata na gari ya Geb. Nao wakafika kituoni, wakaandikisha maelezo, wale askari nao pia wakawekwa ndani, Joshua alishaita dereva wake akitaka aletewe gari ingine na gari yake aliyotumia kugonga gari ya Malon ichukuliwe. Mpaka wanarudi nyumbani kwa Geb, hata gari ya Malon haikuwepo nje ya uzio wa kina Magesa, Geb alisema hataki aikute tena pale.

Akaomba chumba ambacho anaweza kumtuliza Naya. Akampa dawa ya maumivu na kubaki naye kitandani, Naya akiwa amemng’ang’ania shati pande za mbavuni, Joshua amejilaza chali ameegemea mto. Alipohisi anaachia mikono, akajua ameshalala. Ndipo akatoka hapo kitandani na kwenda kujisafisha, Geb akampa tisheti yake, akavaa.

Muda wa shuguli ukawa umeshafika. Wakaamua kuanza keki kwanza. Joshua akakaa sehemu maalumu iliyotayarishwa kwa kupiga kinanda ambacho kilikuwa cha Magesa mwenyewe, ila kimetolewa nje kwa ajili ya hiyo shuguli ya siku hiyo akitaka amuimbie dada yake. Tangia aone kinanda nyumbani kwa Joshua na kupenda, basi wazazi wake wakamnunulia na yeye Magesa hicho kinanda na akawa ameshatafutiwa mwalimu wa kuja hapo na kumfundisha kukitumia. Kwa hiyo hata hapo Joshua alikuwa akitumia kinanda chake.

Akaanza kumpigia ili Magesa aanze kuimba. Naya akatoka akimtafuta Joshua. Akamuona. Akawa anajisogeza alipokuwa akipiga kinanda huku akimwangalia yeye tu. Watu wote wakimsindikiza kwa macho, akawapita wote akaenda kukaa chini kabisa majanini pembeni ya kiti alichokuwa amekalia Joshua ambaye na yeye alikuwa akiendelea kupiga bila kuacha huku na yeye akimsindikiza kwa macho mpaka pale alipokaa. Akajiegemeza kwenye kiti alichokalia Joshua na kuinamia magoti yake. Joshua akamchungulia pale alipokaa kama kumwambia anamuona na ni sawa. Akatulia kabisa.

Magesa akaimba vizuri sana, wageni wengine nao wakamsaidia kuimba alipowaruhusu yeye, wakamuimbia Liv ndipo wakaja kumuimbia na yeye Magesa sasa wakiongozwa na Joshua akiwapigia kinanda na kuimba. Aliimba vizuri sana lakini walijua Joshua hayupo sawa. Akaimba mpaka akamaliza ndipo akamgeukia Naya pale chini alipokuwa amekaa ameegemea kitu chake. “Twende.” Akamsaidia kusimama. “Unaenda kazini tena?” Wakamsikia akimuuliza Joshua kwa sauti ya chini lakini iliyoweza kusikika na wasiwasi kidogo kama asiyetaka kuachwa tena. “Hapana. Twende ukapumzike.” Wakatoka hapo kuelekea ndani.

“Bado naogopa Joshua! Ujue kama ungechelewa, angenichukua!” “Unakumbuka tulimuomba Mungu pamoja?” Akakubali kwa kutingisha kichwa. Wakakaa kwenye kochi ndani wakati watu wote wapo nje. “Basi Mungu amekulinda na mimi nitaongeza umakini Naya. Sitakuacha tena sehemu ambayo hakuna uangalizi mzuri. Nitahakikisha wakati wote unakuwa sehemu salama.” Naya akapandisha miguu juu, akaikunja akiwa kama amelala lakini akamlalia tena upande wa kushoto wa ubavuni kwake, akapitisha nikono mbavuni kwake, akajilaza akiwa ameficha uso akiangalia kochi nyumba ya Joshua wala si mbele.

Mama G akawa ni kama aliyekuwa akiwapa muda wakae hapo ndani na watulie, muda mfupi sana akaingia. “Vipi Naya?” Joshua akamchungulia kule alikokuwa amejificha. “Naya?” Mama G akamuita kwa upendo lakini Naya akabaki kimya. “Au amekwisha lala tayari?” Joshua alikuwa akimsikia jinsi vidole vyake vikipita huko mwilini mwake kwa nyuma karibu ya mgongo, akajua hajalala. “Naona ameingiwa tu na hofu na amechoka. Naomba mniruhusu akapumzike.” “Hamtakula!? Naomba msubiri tule pamoja, Joshua mwanangu. Najua tumekuangusha kwa kuwa ulituamini na kama tumeshindwa, lakini utusamehe baba. Usamehe kabisa. Naomba hili la watoto liishe, ndipo muondoke. Itawauma sana watoto kuona mnaondoka hata hawajawalisha keki!” “Basi tutasubiri.” Naya hata hakunyanyua uso kumtizama anayezungumza, akabakia vilevile alivyokuwa amejilaza. Ila wakasubiri mpaka mwisho na Joshua naye akatoa zawadi yake akimuakilisha na mkewe pia, ndipo wakaondoka.

Ndoa Na Iheshimiwe Na Watu Wote.

Wawili hao walirudi nyumbani ikawa tofauti kabisa kwa Naya. Alitaka kuwa na Joshua kila wakati na kila mahali. Akiwa anaoga chumbani kwake kwenye bafu lake lililotengwa na chumba chao kwa kioo maridadi haswa, yaani mpaka mlango ulikuwa wa kioo kizuri chenye urembo mzuri. Yaani ukiwa chumbani unaona mtu aliyepo

maliwatoni na hivyohivyo ukiwa maliwatoni, unaweza kuona mtu aliyepo chumbani. Japo upande wa choo, kuliwekwa faraga. Kulizungushiwa kioo kizito na kikawekwa giza lililovutia hata kuingia humo chooni. Ila mtu wa ndani ya choo anaweza muona  mtu aliyepo hapo maliwatoni ila ukiwa nje huoni ndani.

 Joshua akamuona amemfuata huko juu chumbani na kwenda kukaa nje ya mlango huo wa maliwatoni ila amempa mgongo kama asimuone akiwa mtupu. Akajua na yeye alimaliza kuoga. Akafanya haraka ili asimuweke hapo chini muda mrefu.
 Akajikausha ndipo akatoka akiwa na taulo tu, akaenda kumsaidia kusimama. “Njoo ukae hapa kitandani, unisubiri tulale, usikae hapo chini.” Naya alikuwa amenyongea sana.

Alipokaa tu, Joshua akakaa pembeni yake. “Kuna kitu najua unaweza usikikumbuke Naya. Lakini kuna ahadi nilikupa mpenzi wangu. Tena kabla ya ndoa. Naomba niirudie tena.” Naya akawa ametulia tu amejiinamia. “Unataka kusikia tena au umechoka?” “Naogopa. Naogopa sana. Unajua ungechelewa kidogo tu, angenichua? Tena alinikataza hata kukimbia, alisema ataniumiza vibaya sana. Sasa sijui alimaanisha nini! Ungechelewa je! Naogopa sana Joshua, naona kama sipo salama!” Naya akaongea kwa wasiwasi akisikika anaelewa anachozungumza.

“Nakuelewa. Na usifikiri niliwahi pale kwa bahati tu! Ni Mungu alisaidia Naya. Kama alisaidia leo, naomba amini pamoja na mimi kuwa na siku ingine atasaidia kwa sababu nimemuomba Mungu tena na tena anisaidie kwenye ile ahadi niliyokuwa nimekupa hata kabla ya ndoa yetu.” Naya akamwangalia kama anayetaka kumsikia zaidi. “Unataka kujua?” Akatingisha kichwa kukubali.

“Uliniahidi nini?” Naya akauliza taratibu tu. “Nilikwambia hivi, ‘Nitakulinda, na kukupigania mpaka kifo changu. Wewe ni wangu. Na hutarudi kwa Malon.’ Najua unaweza usikumbuke. Lakini nilikuahidi tukiwa pamoja tena uliniomba wewe mwenyewe kuwa nikuahidi kukung’ang’ania wewe tu.” “Kwa hiyo ulishaniahidi hivyo?!” “Kabisa. Kwa kuwa mbinu zake za kutaka kukumiliki hazijaanza leo. Alikuwa ndio mwanaume wako wa kwanza, mkaachana ndipo tukaanza mahusiano mimi na wewe, kisha akataka kukurudia tena. Lakini Naya, ulikusudia kabisa kuwa na mimi. Na kwa kadiri alivyokuwa akitusumbua kwenye mahusiano yetu, ukahofia ningekuacha. Ndipo ukaomba nikuapie kama sitakuacha. Ndipo nikakupa hicho kiapo. Na ninakusudia kukisimamia daima.”  

“Niambie tena Joshua. Niambie tena, ili hofu ipungue. Naogopa sana. Anaonekana si mtu mzuri. Sitaki anichukue.” “Unaweza kunipa muda mfupi nijipake losheni na kuvaa nguo za kulalia?” “Unataka nikusubirie hapo nje?” “Hapana. Wewe ni mke wangu Naya. Sina chakujificha kwako.” Naya akatulia akiwa ameinama akifikiria. Joshua akambusu shavuni na kusimama.

Akafanya yote hapohapo chumbani Naya akiwa ametulia tu kitandani. “Joshua!” Akamuita tena taratibu. “Niambie.” “Nilipenda tulivyolala wote jana. Nililala vizuri, kwa kwa kuwa ulikuwa ukinibembeleza.” Joshua akacheka. “Wewe ni mtu mzuri Joshua. Unanisubiri mpaka nilale!” “Nakupenda sana Naya. Sana.” “Kama hujachoka, naomba na leo tulale wote. Naogopa!” “Hata usipoogopa, unatakiwa kulala na mimi. Na hapana, sitakuchoka Naya. Nimeomba Mungu anisaidie.” Naya akatulia. Joshua akamuona anaanza kukosa raha, akajua anajaribu kukumbuka.

“Niangalie Naya. Niangalie mimi na uache kukunja uso na kufunga macho kwa nguvu. Utasababisha kichwa kuanza kuuma tena na hutakuwa na jinsi ya kukituliza kwa kuwa si muda wa dawa.” “Sikumbuki Joshua! Kwa nini mimi sikukumbuki?” “Sikuhitaji ukumbuke chochote.” Joshua akaenda kukaa pembani yake. “Tulia kisha niangalie.” Naya akafungua macho. “Unataka tulale hapa ambapo ndio chumbani kwetu au unataka turudi kule?” “Wewe unapenda wapi?” Naya akauliza kwa upole na kuendelea. 

“Mimi nataka kuwa na wewe tu Joshua. Na hata ukitoka, uwe unaniacha hapahapa. Naomba kwa sasa niwe na wewe tu. Najua umezoeana na kina Magesa, lakini mimi siwakumbuki kabisa! Tafadhali usinipeleke na kuniacha huko. Hata kama unahitaji kutoka, naomba nikusubirie hapa.” “Samahani kama nililazimishia uende kwa kina Magesa, mpenzi wangu. Nilifikiri ingekusaidi! Ila sitarudia tena, mpaka wewe mwenyewe utakapokuwa tayari.” “Sio sasa hivi.” “Sawa. Basi nikiwa nakwenda kazini, utakuwa ukibaki hapa. Ukitaka kitu utakuwa ukiniambia mimi mwenyewe.” Hapo akaridhia. 

Kitanda Cha Ndoa Tena.

“Basi naomba turudi kulala wote kwenye kitanda chetu cha ndoa.” Naya akakubali. Wakaweka mambo sawa ndipo wakapanda kitandani. “Utaniahidi tena?” Joshua akacheka. “Naona kumbukumbu zako zipo sawa.” “Nakumbuka mpaka pale tulipokutana tena Joshua. Vile ulivyokuwa ukinibembeleza unisaidie.” “Kumbe unakumbuka!” “Nakumbuka Joshua. Lakini pale nilikuwa kwenye maumivu makali sana, hata kufikiria sikuwa naweza. Ila nakushukuru kunilazimisha.” “Kwa kuwa niliweka ahadi kwako na mbele za Mungu kuwa, nitakulinda, na kukupigania mpaka kifo changu. Katika uzima. Maradhi. Shida na raha. Wewe ni wangu Naya. Na ndipo ninapoomba utulie na uanze kupata amani kuwa, nitafanya kila niwezalo, usirudi kwa Malon. Na Mungu anisaidie.” “Asante Joshua. Sasa hivyo ulivyonishika usiniachie mpaka nilale kabisa.”

“Unajua hivi ndivyo ulivyokuwa ukilala tokea tumeona? Na hapa ndio kitanda na sehemu yetu ya kwanza kuanza mapenzi mimi na wewe.” Naya akajivuta zaidi kana kwamba alikuwa mbali. “Eti Joshua? Mimi nilikuwa mtu mzuri kwako?” Naya akamuuliza. “Na usinidanganye.” “Ulikuwa mzuri sana Naya. Sana. Tulikuwa na wakati mzuri mno. Nakwambia tulikuwa tukifanya mapenzi mimi na wewe hatukinahiwi ila tu kuchoka. Hujawahi kutosheka na mimi Naya. Na hukuwa ukinidanganya. Nikweli ulikuwa ukinifurahia na ukinijali sana. Uliniahidi utabaki kuwa wangu daima.” “Nikikwambia tena itakuwa sawa au kwa kuwa sikumbuki zamani, haitaleta maana?” “Sitachoka kukusikia mpenzi wangu. Na sijali ni wakati gani utakao kuwa ukiniambia.” Joshua akayaongea hayo kwa sauti nzuri, karibu kabisa na uso wa Naya.

“Ila kabla hujaniambia chochote, naomba nirudishe zile pete nilizokuwa nimeweka kidoleni mwako. Unaona hii?” Joshua akamuonyesha mkono wake wa kushoto. Naya akageuka vizuri. “Hii pete yako ni nzuri sana, Joshua! Kama vitu vyako vyote!” Joshua akacheka. “Asante. Lakini hii ni pete yangu ya ndoa, na ni wewe ulinivalisha. Na nilizokuvalisha mimi, mbili. Moja ya uchumba, ingine ya ndoa, zote zipo hapa. Zilibakishwa kwenye gari siku ulipopotea. Itakuwa sawa nikizirudisha kidoleni ndipo uniambie unachotaka kuniambia au unaona haupo tayari?” “Nataka univalishe wewe Joshua. Nitafurahi na mimi kuwa na pete zako kidoleni kwangu.” Joshua akacheka kwa furaha, moyoni akisema, “wewe ni Mungu, na badala yako hakuna mwingine.” Akatoka kitandani kwa haraka kwenda kufuata hizo pete.

Akarudi kitandani, Naya akakaa kabisa akionyesha utayari. Akampa na mkono. Joshua akamvalisha moja baada ya nyingine Naya akimuangalia mpaka akamaliza. Na yeye akajiangalia kidole chake. “Wewe Joshua unapenda vitu vizuri tupu! Hata hizi pete ulizonivalisha ni nzuri sana!” “Na ulizipenda sana. Nitakuja kukuonyesha picha ulizokuwa ukijipiga kila wakati halafu unaniringishia kuwa kidole chako kimependeza kuliko changu.” Naya akacheka sana akijiangalia yeye kisha akavuta mkono wa Joshua, akaangalia tena kama kuhakikisha. “Lakini kweli bwana! Naona sikukosea, zangu zimenipendeza zaidi.” “Sawa Naya.” Kwa mara ingine tena wakarudisha kicheko cha kweli ndani ya hicho chumba. Wakacheka na kurudi kujilaza kama mwanzo ila safari hii Naya akijiangalia mkono wake uliokuwa na hizo pete, akigeuza kila pande. Taa ikiwamulika hapo kitandani.

“Joshua!” Akamuita taratibu. Joshua akaitika kwa busu pembeni ya kichwa sehemu iliyokuwa karibu na uso wake Joshua, wakati Naya macho bado yapo kwenye mkono wake akifurahia bado pete zake kana kwamba ndio anakutana nazo  kwa mara ya kwanza. Naya akamgeukia vizuri, akamwangalia. 

“Nataka mimi nibakie kuwa wako wewe tu, mpaka kifo.” Joshua akambusu mara kadhaa juu ya midomo ambayo ilikuwa karibu sana na uso wake. Alipoona ameridhia, akamnyanyua uso vizuri akaanza kunyonya midomo yake, mikono ikipanda mapajani taratibu.

Akamuona anafurahia akanyanyua mguu mmoja juu yake zaidi. Joshua akapitisha mkono mpaka ndani ya chupi aliyokuwa amevaa, akaweza kumshika makalio yake vilivyo. Naya akaanza kujisogeza zaidi. Mkono wa Joshua ndani ya chupi ya mkewe ukaanza kuzunguka mle ndani mpaka katikati ya matako akitaka kufika mbele, Naya akijitahidi kujinyanyua kama anayetaka aendelee. Akaona ile chupi inamnyima uhuru. Bila kutoa midomo ya Naya kinywani mwake, Joshua aliyekuwa na uchu na mkewe, hakuwa amemsahau, wala hakuhitaji juhudi nyingi zifanyike ili kupandisha hisia za mapenzi kama kwa Naya aliporudi amemsahau, akaanza kuivua ile chupi huku akimminya vizuri, Naya naye akazidi kumng’ang’ania mpaka akamsaidia kutoa chupi yake mwenyewe, pale alipoona Joshua anamchelewesha kwani mikono iliyokuwa ikitembea katikati ya mapaja yake kutokea nyuma mpaka mbele, Naya hakutaka ipotee kwa muda mrefu huko. Akaona amsaidie ili Joshua arudie kufanya alichokuwa akimtendea na kumuamsha hisia zote.

Bila kupoteza muda, Joshua naye akaanza kutoa nguo yake ya juu ya kulalia huku Naya sasa akitembeza kucha na vidole sehemu ya juu iliyokuwa tupu, zaidi kwenye kifua cha Joshua kilichokuwa na nywele, huku akiendelea kumnyonyo na yeye midomo yake kwa uchu. Joshua akashangaa japokuwa Naya alisahau kila kitu, lakini utundu wake wa kucha, na umaridadi wa mikono yake kila anapogusa na kuminya, akichua taratibu, ulibaki vilevile kama zamani. Ikabidi Joshua aharakishe kutoa nguo kwani mkono mmoja wa Naya ulishakuwa ndani ya pensi hiyo laini, yenye lastiki kiunoni, kitambaa cha silki, safi kwa kulalia.

Joshua akaendelea kufurahia kila kunakopitishwa kucha na anaposhika mkewe akimchua taratibu. Mpaka Joshua anamalizia kutoa hiyo pensi, nguo ya chini, Naya alishafika mbali sana. Midomo yake ilikuwa ikitembea mwilini kwa Joshua na kumuacha Joshua hoi.

Alipokuwa akirudisha midomo kifuani, napo alikitendea haki kifua cha mumewe. Alikuwa akipitisha ulimi kwenye kifua cha Joshua na kuvuta kwa midomo zile nywele za kifuani, taratibu na kumsisimua Joshua zaidi. Na anaporudisha midomo hapo kifuani, mikono alibakisha kwenye uume wa mumewe akimchezea kwa utulivu, akimchua mumewe taratibu bila papara. Ikawa sasa yeye ndio anacheza na mwili wa mumewe zaidi bila kuchoka tena bila papara. “Naya hajasahau utundu wake kitandani!”  Joshua akashangazwa mawazoni, akifurahia midomo ya Naya mwilini mwake.

 “Nakupenda Joshua.” Hilo neno lilisikika kwa nguvu na msisimko wa ajabu sana masikioni kwa Joshua. Akapata nguvu kama aliyejiongezea nguvu za kiume. Shauku na tamaa kwa mkewe ikaongezeka. Hamu na mwili wa mkewe ikaongezeka akataka amuingilie tu afurahie joto lake. “Nitakuwa makini, nisikuumize.” Akamwambia akibembeleza akiwa anamgeuza mkewe, akimtoa mwilini mwake, amuone mtupu akiwa amelala chali pale kitandani. Akaanza yeye sasa kunyonya na kugusa huo mwili wa Naya. Yaani kabla hata Joshua hajamuingilia mkewe, Naya alishamaliza safari ya kwanza. Alipomuona ananogewa, anataka kwenda mara ya pili, ndipo Joshua akamkumbatia vizuri. Matiti ya Naya yakaenea kifuani kwa mumewe. Akadaka midomo yake, Joshua kwa mara nyingine tena, usiku huo akafanya mapenzi na mkewe akiwa amemkumbatia kwa furaha zote.

Wawili hao wakaendeleza penzi la haja. Kama alivyosema Joshua, Naya akashindwa kutosheka mpaka yeye mwenyewe akasalimu amri. “Nikumbatie tena, nilale.” Joshua akajua amelemewa. Yeye mwenyewe akamsafisha hapohapo kitandani akiwa anasinzia, aliporidhika msafi, akajirudisha na yeye hapo, akamuweka kifuani, kwa mara nyingine tena, Naya akarudi kulala kifuani kwa mumewe akiwa mtupu kabisa, na Joshua akimpapasa kwa uhuru wote akimshukuru Mungu wake kwa kuuweka na huo usiku wa siku hiyo hapa duniani. Siku hiyo iliharibiwa na kutaka kuisha vibaya, ila wakaimaliza vizuri sana.

Jumapili.

Siku ya jumapili nayo hawakutaka mgeni. Kwanza hata kina Magesa walionelea wawaache kwa vile Naya alivyoondoka kwao akikataa hata kuwatizama ila kujificha ubavuni kwa Joshua wakati wote. Mikono ya Joshua ndiyo iliyomtoa usingizini akimpapasa taratibu. Akafungua macho akiwa mwanzoni amedhani ni ndoto. Akamkuta Joshua akimtizama. “Joshua!” Akaita taratibu. “Umeamka salama?” akatulia kwanza kabla ya kujibu akakaa na kuangaza chumba kizima kisha akajiangalia kwa wasiwasi mpaka akamtia hofu Joshua akiogopa asije dhani amembaka.

Akajikuta yupo uchi. Akavuta shuka taratibu na kujifunika Joshua akimwangalia kwa hofu, hakutaka kuongea chochote ili amsikie yeye kumbukumbu zake zinamwambia nini, na anafikirije juu ya mapenzi waliyofanya usiku uliopita. Kisha akamgeukia baada ya kujivuta mwisho kabisa ya kitanda. Joshua kimya akimsihi Mungu amrehemu Naya asimbadilikie. “Nilifikiri nimeota!” “Juu ya nini?” Akatulia kidogo kama hilo swali limemtia wasiwasi. Akaegemea magoti kama anayejaribu kukumbuka na kupingana na anachokumbuka.

“Naya?” Joshua akamuita taratibu kumtuliza. “Abee.” “Naomba niambie unachofikiria. Na usigope.” “Sijui ni ndoto?” “Juu ya nini?” “Kwamba usiku tulipata wakati mzuri?” akaongea kwa kutojiamini. “Inawezekana ni mawazo tu.” “Ni kweli Naya. Na naomba usijitilie mashaka. Wewe si mjinga hata kidogo ila uliumia sehemu ya kumbukumbu za nyuma. Chochote unachokumbuka usikitilie mashaka. Nishirikishe ukijua mimi ni wewe na nipo pamoja na wewe katika kila hatua. Kwa hiyo usiniogope kabisa. Na ni kweli tulipata wakati mzuri sana. Ulinitoa simanzi yote. Na ukalipa ile ahadi yako uliniahidi siku ile kabla hujapotea.” Akacheka. “Kweli ulinifurahia?” “Sana Naya.” “Mimi mwenyewe nilifurahia sana. Unajua kunishika vizuri na napenda unafanya mapenzi na mimi. Taratibu ukijali mwili wangu bila kutaka kuniumiza. Halafu huna kinyaa!” Joshua akacheka sana.

“Kweli! Mimi umenishangaza Joshua. Hata katikati ya mapenzi bado unatumia midomo yako kunilainisha! Au sio kweli?” “Nimekwambia huna tatizo la kumbukumbu. Ni zile za zamani tu.” “Joshua wewe unanipenda! Japokuwa nilikuwa nikikushangaa lakini vile ilikuwa ikinisisimua sana na kunifanya nitake kuendelea kila wakati.” “Mpaka ukalemewa na kulala kabisaa, ukaniachia kila kitu.” Naya akacheka na kujifunika. “Nilijua ungechoka tu. Nilikosa kiasi. Nilikuwa na hamu na wewe Naya!” “Nimerudi Joshua. Hakikisha hawanichukui tena.” “Nitajitahidi na Mungu nisaidie.” Ikawa ahadi iliyochanganyikana na maombi.

“Asante Joshua. Basi acha mimi nikaoge. Nililala mchafu.” “Nilikusafisha.” Naya akacheka na kujifunika shuka. “Kila mahali?” akauliza akicheka ndani ya shuka. Joshua akajivuta mpaka katikati ya miguu yake ndani ya shuka. Naya akazidi kucheka alipomuona humo ndani. Akaiachanisha miguu yake mpaka amafika juu mapajani. Alipofikisha ulimi, ikabidi Naya ajiegemeze kwenye mto vizuri akiwa amekaa, mkono wa Joshua ukafikia matiti yake. Basi siku hiyo nayo ya jumapili, ikawa ni penzi mfululizo. Naya akimfuata Joshua kila mahali akitaka kuchoka mzinga kama nyuki. Naye Joshua akijua amebakia mwenyewe kwenye maisha ya Naya, hakutaka kufanya kosa, alitumia nafasi yake vizuri akimpumbaza kwa hili na lile ili huko kichwani kwa Naya abakie yeye tu. 

J.3

Kurekebisha makosa. 

Wakiwa ofisini, Nanaa akijaribu kutafuta jinsi ya kujirudi kwa Joshua ili kuwa karibu tena na Naya, maana Joshua aliomba siku ya jumapili wao wasiende nyumbani kwao kwa chakula cha mchana baada ya ibada, ili abakie na Naya aliyeonekana bado yupo kwenye mshituko. Wakajua wanawakwepa tu kwa kosa la kumuacha Naya karibu kuchukuliwa tena na Malon.

Sekretari wa Geb akamwambia anaye mgeni. Alipojua kama ni Bale na akamwambia amefika pale ili kupunguza deni la baba yake, Geb akamwambia sekretari amwambie asubirie chumba cha mkutano. Akamuita Joshua ili awe shahidi wao na yule mwanasheria. Akaamuru Bale apewe anachotaka wakati akisubiria hao watu wawili wafike. Baada ya lisaa watu wote wakawasili. Ndipo  wakajongea chumba cha mkutano.

“Sitaki fujo na mtu, ila kutaka kulipa pesa mnayomdai  marehemu baba yangu.” Akatoa hizo pesa. Kila mtu akashangaa. Bale alikuwa akilipia karibu nusu ya deni la baba yake. Pesa nyingi maana ni deni la kuanzia ujenzi wa gala la kisasa baba yake alijenga kwa hiyo pesa aliyowekeza Geb. Na Garama za barabara ya vitofali iliyowekwa upya kuzunguka nyumba nzima mpaka galani kurahisisha kuingizwa kwa bidhaa. Garama ya kubadili mfumo mzima wa umeme na kuwekwa mzuri kuweza kusambaa kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi na galani. Ndipo deni likaongezwa na mazao sasa aliyokuwa akichukua kwa kina Magesa bila kulipa ila kurudisha hiyo pesa kila akiuza. Japokuwa Naya alipewa na Joshua pesa ya kulipia sehemu ya kiwanja walichonunua kutoka kwa jirani yao, lakini bado deni la ujenzi mzima na mazoa lilikuwa juu. Ndio Bale akafika kulipa nusu! Wakaandikishana mpaka wakamaliza.

“Labda mimi nikuulize Bale, unalipa deni lote hili ili iweje?” Geb akauliza. “Nataka kufanya kile baba yangu alitaka kufanya tokea mwanzo.” Wote wakawa wametulia wakimsikiliza Bale aliyerudi safari hii akimtamka baba yake kwa heshima! “Baba alitaka kiwanja kiwe cha Naya, kitabaki kwa jina la Naya, ila nitamsaidia kukiendeleza kisibakie vile kilivyo. Nataka kulipia chote. Mumpe Naya hati yake kisha tujenge kwetu. Na sisi tuwe na kwetu. Najua mimi na Naya hatutashindwana.” Wote wakamshangaa vile alivyobadilika.

“Ngoja nikuulize Bale. Kwamba sasa hivi upo tayari ujenge pale na bado kiwanja kibakie kuwa cha Naya!?” Joshua akamuuliza. “Kabisa.” Wote wakawa kama hawamuamini. “Acha nikuulize zaidi Bale, japokuwa najua mimi unanichukia sana. Hutaki niwe na dada yako, japo unajua wazi ni mke wangu.” “Mimi sijasema nakuchukia! Ila ukweli mimi na wewe hatuendani, Joshua. Ninachoamini na harakati zangu za maisha, sio kama wewe. Ndio nikaamini mimi nitaendana na Malon.” “Ndio ukaamua kumtoa Naya kwangu, na kwenda kumkabidhisha kwa Malon mpaka akamfanya ndugu yako awe kama mjinga!? Kana kwamba haitoshi bado unamuelekeza Malon aje amchukue tena! Kweli unajenga urafiki na Malon kwa kiasi cha kumdhuru dada yako kwa kiasi hiki, Bale!?” “Subiri kwanza Joshua. Inamaana Malon amerudi tena huku?!” Bale akawa kama haamini.

Wakamsimulia kilichotokea siku ya jumamosi. Wakamuona kama amekasirika. “Hivi nyinyi mnamjua Malon nyinyi? Hakuna jela yakumfunga yule mtu. Nina uhakika leo atarudi tu uraiani. Na mimi sikuwa nikimjua kama vile alivyokuwa akisema Naya, ni mpaka nilipoishi naye. Malon alinidanganya na moja ya sharti la kunitoa jela na kuniweka huru uraiani bila kesi, yani kesi yangu mbaya iliyokuwa ikinikabili aliniahidi itafutwa kabisa, endapo nitamsaidia kumpata Naya. Na mimi nilikuwa na hali mbaya jamani. Nipo rumande kwa zile tuhuma. Sikujua kama nitapata tena msaada maana alinisikilizisha majibu ya kila mmoja wenu wakati akiwaambia mnisaidie kutoka jela. Alichonisikilizisha ukweli kiliniogopesha sana, nikaona sina jinsi isipokuwa kuwa na yeye tu na kumsaidia kile anachokitaka. Naya.” Bale akawasimulia mwanzo akiwa amefungwa mpaka mwisho.

“Siku ile Nanaa aliponiambia juu ya baba kuugua kwa ajili yangu, ilibidi kwenda kusaka ukweli Tunduma, kwa kuwa sivyo Malon alivyokuwa ameniaminisha! Sikuwa nikijua hata kama mlifika kule kunitafuta! Yaani baada ya kutoka Tunduma, na kurudi kwake na kunitisha sana nimrudishie Naya lasivyo atanirudisha tena jela. Mimi nikaondoka kwake nikimwaminisha nakuja huku kumfuata Naya ili nimrudishe tena kwake. Lakini sikuwa hata na mpango wa kumrudisha kwake kwa kuwa kwanza nilishagundua alimtesa sana Naya, na nikachukia kuona ametumia ujinga wangu, kunifitinisha na Naya mtu ambaye sikuwahi kumuumiza kwa kiasi hicho!”

“Lakini niliporudi nilipokuwa nimemuacha Malon na Naya, ili kumchukua Naya nimlete hapa kama wewe Geb ulivyosema kama ni moja la sharti lako kabla yakutoa hati yetu, Malon akaniambia Naya anajifanya vile makusudi ili kunidhulumu. Na mimi kwa kuwa tayari nilishakuwa na uchungu, chuki kwake nikijua ananifanyia makusudi kwa kuwa hanipendi, na mimi ikabidi kupambana naye bila kujua kama kweli Naya hayupo sawa.”

“Nafikiri alimpiga vibaya sana au sijui ni nini kilitokea, ila vipimo vilionyesha amegongwa mpaka ameviba sehemu ya ubongo ndio maana hakumbuki! Kwanza alikuwa amevilia damu mwili mzima kwa kipigo mlichokuwa mkimpa.” Bale akaumia sana. “Mimi sikumpiga sana. Ni siku ile tu nilipokwenda kumchukua. Tena ni makofi tu. Itakuwa ni Malon ndiye aliyekuwa akimpiga sana. Na ndio maana hata safari hii alipotaka nimsaidie kumrudishia Naya, nilimkubalia tu lakini sikuwa na nia ya kumrudisha. Nia ilikuwa ni kumtuliza wakati nakusanya hii pesa na kujipanga kisheria, kabla hajanirudisha tena polisi. Ndio nikaja huku Dar nikimwambia nimekuja kumfuata Naya.” Bale akaendelea kujieleza akisikika yupo tayari kutoa ushirikiano kwa kina Joshua.

“Sasa huwa nikiwa huku, naishi nyumbani kwake Kunduchi. Nilipofika sasa nikiwa nimeshajua amenidanganya kwenye mengi, ikabidi sasa nianze kusaka ukweli. Katika kufanya uchunguzi wangu, nikakuta ameficha chumbani kwake moja ya laptop yake aliyotumia kutengeneza kile alichotaka nikisikie. Ndipo nilipochanganya ukweli wa kule Tunduma na mazungumzo yote aliyowarikodi nyinyi wote mkimjibu akitoa ushauri wa kupatikana kwangu, mpaka majibu ya marehemu baba. Malon amenitenda unyama mpaka kusababisha kifo cha baba yangu!” Bale akaendelea.

Bale Atoa Ukweli.

Wote wakashituka ila wakatulia kumsikiliza wakijua ameanza kujutia. “Kuna kitu nataka kuwaambia, lakini naombeni msinipeleke polisi wala msinirikodi. Ila mjue nitalipiza kisasi kama nilivyomlipisha Mbabe.” Wote wakataka kusikia, wakajiweka sawa. “Nipo kutengeneza nilipoharibu na Malon ndiye aliyeniponza. Kama nilivyowaambia, yeye ndiye aliyenitoa jela, kwa kutumia askari kabisa. Wakanificha mpaka alipofika mwenyewe na kuniaminisha kile alichojua ningeweza kuamini kwa haraka. Ukweli nilijawa sana chuki. Akaniambia lazima kuwakumbusha kule nyumbani zaidi baba na Naya vile yeye alivyomuhimu kwenye familia, kwa kuwarudisha chini kabisa. Na akaniambia kwa vile alivyonitoa jela, malipo ni kumrudishia Naya.” Bale akaendelea.

“Ukweli Malon ni mtoto wa mtaani anayejua afanye nini ili kupata chochote anachokitaka. Tena kwa urahisi mpaka huwa ananishangaza! Kwa mfano maswala yako wewe Joshua na Benadina.” Joshua akashituka sana. “Wewe ulimjuaje Benadina!?” Joshua akauliza. “Mimi nilikuwa najua tu jina lake moja, tena kusikia kutoka kwa Naya alipokuwa akimsimulia baba juu ya historia yako ya maisha zaidi upande wa uwaminifu kwamba huna mambo ya kupenda wanawake ila huyo Benadina tu. Na nilimsikia Naya akimwambia baba kwamba mlipoachana na Benadina, hukutafuta mwingine tena.”

“Sasa wakati nilipokuwa na Malon, mwanzoni tu hata kabla sijaondoka na kwake kwa mara ya kwanza, na yeye alitaka kukufahamu zaidi ili kuweza kukugombanisha na Naya, akuone na wewe ni muhuni tu, amrudie yeye. Sasa aliponihoji juu yako nikamwambi kile nilichosikia kuhusu wewe na Benadina. Akaamini kwa kuwa hukuwa na mwanamke mwingine baada ya Benadina, basi ulimpenda sana, kwa hiyo haitakuwa shida kurudisha majeshi endapo Benadina akirudi pichani. Sasa alipotaka kumfahamu zaidi, sikuwa na taarifa zenu zaidi ila nilijua shule mliyokuwa mkisoma naye. Kwa taarifa hizo tu, Malon akaniambia ameshampata. Sikuamini, nikacheka tu!” Joshua akashangaa sana.

“Ni kweli alimpata, akampa namba zangu za simu na kunitafuta. Ila siku ileile ya kwanza Benadina aliponipigia simu mimi nilimshitukia. Tena ndio siku tulikuwa kwenye mshituko wa baba yako kutekwa nyara huko Tunduma akiwa anaomba na Naya. Alinipigia nikiwa ndio nimerudi Kiluvya kuwa na Naya, pamoja na Zayoni sababu ndio walikuwa kwenye huo mshituko, baba Naya ndio ametoka kutekwa muda mfupi sana. Sikutaka hata kuzungumza naye ila nilimgombesha sana Benadina na kumuonya asijewahi kurudia kunitafuta.” “Ndio maana wewe Malon amekushindwa!” Akawa kama huyo Bale anasadiki mawazoni kwake.

“Na ndio maana hapo alikwama. Lakini ninachotaka kukwambia ni kuwa Malon anauwezo wa kupata chochote anachotaka. Zaidi akiamua. Ila nina uhakika wewe unamtisha sana Malon. Mpaka sasa hakuwa akijua ni jinsi gani atakuweza, kitu kinachompandisha sana hasira na kumfanya mwenye chuki zaidi kwako. Ila turudi kwa kitu nilichotaka kuwaambia juu ya alichonisababisha nifanye huyu Malon.” Bale akaendelea akisikika na mengi, na yeye Joshua akatulia maana majibu ya maswali yake yaliyokuwa yakimuumiza na kumchanganya, yalikuwa yakijibiwa siku hiyo.

  “Malon anajuana sana na walinzi au tuseme anajua tabia nyingi za walinzi kwa kuwa alishakuwa na yeye mlinzi kipindi Naya alipomtoa jela. Akasema tabia za walinzi wengi wanapenda bangi. Ili kuwafanya marafiki basi nikuanza kuwapa bangi. Ndipo tukaanza sasa kuwa karibu na wale walinzi wa pale nyumbani. Wakawa wakipitishiwa bangi kila wakati, bila kulipa. Walipoona ni deni kubwa ndipo sasa tukauliza ratiba za pale nyumbani kujua siku gani kunakuaga na mzigo. Ili sasa kuchoma gala zima.” Joshua akaumia sana.

“Mimi sikujua kama atachoma na baba yangu na Zayoni, pamoja na bibi!” “Hudhani kama ilikuwa bahati mbaya?” Wakamtega kwa swali. “Kwa jinsi ninavyomjua Malon sasa hivi, haikuwa bahati mbaya hata kidogo. Kilichotokea kwa Naya juzi ndio ulikuwa mpango wake tokea zamani, mimi sikuwa nikijua! Kumtoa baba duniani, aliyejua anampenda sana Joshua sio yeye tena, ili Naya abakiwe peke yake, ammiliki yeye bila kipingamizi. Alijua akiondoka baba, yeye atakuwa huru na Naya. Sitashangaa hata nyumbani kwako Joshua, au kwako wewe Magesa, ametumia mbinu ileile kuwa karibu na walinzi wenu ili kumsaidia kujua kinachoendelea majumbani kwenu ili amtoe Naya.” Hapo akawashitua zaidi na kuanza kuamini.

“Kwa kuwa jinsi anavyofanya nao urafiki, hata akikuomba kitu kwanza hutaona kama ni jambo la hatari, na pili huwezi kumkatalia. Ninauhakika na hichi ninachosema maana ndivyo tulivyofanya pale Kiluvya. Sasa kinachoniuma ni kule kuvuka mpaka mpaka kuua watu wa nyumbani kwetu! Hakika atalipa.” Wote wakabaki kimya kwa muda.

“Mimi nashauri uache sheria ichukue mkondo wake.” Mungai, wakili wa Magesa na baba Naya akashauri. “Malon hajasoma shule ya darasani ila amefudhu ya mtaani. Anajua kucheza na askari kupita nitakavyokwambia. Ninapokuhakikishia kuwa leo anarudi mtaani, niamini atarudi mtaani. Na huwa hakubali kushindwa kwenye mambo yake aliyokusudia. Ndio maana amefanikiwa sana kiuchumi kitu kilichonivuta kwake zaidi. Na hatatulia mpaka amrudishe Naya kwenye himaya yake. Na kinachoniuma ni sijui ni nini amemfanya Naya mpaka akawa vile! Mimi aliniambia Naya anajidai tu, ila ni mzima ndio maana na mimi nikiwa kwenye hasira, nikawa mkali kwa Naya kumbe ni kusudi tu ili kuendeleza kumsadia kwenye mipango yake miovu. Alinipandikiza chuki bila sababu mpaka kudhuru watu wa nyumbani kwangu! Sasa mimi mwenyewe nitamuwekea kikomo.” “Nashauri usijiingize kwenye vita na Malon, Bale. Mmebakia nyinyi wawili tu,  acha..” “Hakutakuwa na kutulia kati yenu mpaka Malon adhibitiwe. Si mmesema amekuja mpaka nyumbani kwenu nyinyi kina Magesa?” Kimya.

“Sasa ndio mjue hana mipaka kwa analolitaka. Ana jinsi yake ya  kupata anachokitaka. Na hajui jibu la hapana wala hajui kushindwa na jambo ndio maana anafanikiwa katika mambo yake. Hataacha hata kwa kudhuru watu mpaka apate anachokitaka, Naya.” Hapo akagusa pabaya. Kimya kila mtu akiwaza lake na hofu ikaanza kuwaingia juu ya Malon aliyejithibitisha ni katili wa kupindukia kwa alama alizoacha mwilini kwa Naya mpaka kumfanya tahira na teja. Na asiyekuwa na mipaka. Alishafanikiwa kuingia mpaka kwenye ua ya Joshua kwa kupitia marehemu bibi!

 “Magesa, nitarudi na pesa yako nimalizie deni lako na ndipo niendeleze kwetu.” Bale akasimama. “Naomba msaada wako Bale. Unajua ni aina gani ya madawa waliyokuwa wakimpa Naya? Maana wamegundua ni madawa ya kulevya.” Bale akaumia zaidi. “Ni mshenzi yule. Amekataa kabisa kuniambia. Mimi alinidanganya kama ni dawa tu za usingizi. Ila hakuniambia kama ni dawa za kulevya! Hata nilipomsihi aniambie, akawa mkali. Ndio sasa najua ni kwa nini alikuwa mkali kwangu! Alitumia ukali kama silaha tu ya kuficha ukweli kwa kuwa yeye Malon mwenyewe hatumii madawa ya kulevya, ila bangi tu. Asingethubutu kuniambia eti ampe Naya madawa ya kulevya!”

“Na si hivyo tu Bale. Naya amepoteza kumbukumbu sababu yakuumizwa kichwa. Mimi sijui mlikuwa mkimpigaje mke wangu, lakini mmemumiza kichwa vibaya sana mpaka amekutwa nauvimbe kichwani, kama nilivyokwisha kukwambia! Kwamba amepigwa sana kichwani.” “Itakuwa tu ni Malon. Mimi ndio siku ile nilimpiga, tena makofi tu! Hakika nitamuwekea kikomo.” Bale akajitetea tu hivyo na kutoka. Lakini wakawa wamemaliza upelezi hata wa kesi ya Kiluvya, ila hofu kwa walinzi wa majumbani kwao ikaongezeka.

Chalo Naye Aeleza Ukweli.

Wakatoka hapo kuelekea polisi walikokuwa wameshikiliwa wale walinzi wa Magesa walio mtoa Naya ndani kumpeleka kwa Malon. Na kweli Malon alishakuwa ametoka kwa dhamana. Wakaeleza janja ya Malon kuwahonga bangi. Wale walinzi walipobanwa, Chalo aliyekwishafanya kazi na Malon, na ndiye aliyeenda kumuita Naya ndani, kumbe kweli alipewa hongo ya pesa nyingi na Malon siku ile, akamuomba awe anamfuatilia Naya mpaka atakapoachwa peke yake ndipo amuite. Ila alimuhakikishia ni mkewe. “Anaonekana alimfuatilia tokea mbali, maana ni kama alifika naye pale nyumbani. Akaishia baa ya kule nyuma baada ya kujua alipofikishwa huyo Naya aliyeniambia mimi  nimkewe. Aliponiwekea salio na kuomba niwasiliane naye punde Naya atakapokuwa peke yake ndipo asogee. Nilipomjulisha kuwa ameachwa peke yake pale nje, ndipo akaniambia ili kumuamini yeye, nimwambie tu ni mumewe. Hivyo tu, basi atatoka. Na kweli, nilipomwambia hivyo Naya, akatoka kwa haraka, mimi sikuwa na wasiwasi.” “Naya ameniambia ulipomuita na kumwambia hivyo, kuwa mume wake anamuita, kwa kuwa alikuwa akinisubiria mimi, yeye moja kwa moja akajua ni mimi.” Joshua akaongeza ila kwa wasiwasi akijua kwa namna yeyote ile na walinzi wake wamefikiwa.

~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Wanafanyaje? Endelea kufuatilia.

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment