Walitua jijini Dar siku
ya jumatano mchana. Wote wakarudi nyumbani kwa Nanaa na Geb kwanza. Baada ya
mazungumzo kidogo Grace yeye akaenda nyumbani kwake. Alipewa ujumbe na msichana
wa kazi kuwa watoto wamekwenda shule, jioni watarudishwa. Alipouliza juu ya
Danny na Sara, yule dada akaanza kucheka. Alikuwa mzungumzaji sana kwa Grace.
“Walihama mara baada yakurudi safari. Waligombana hapa nusu wapigane. Mimi
nikachukua watoto, nikaingia nao ndani.” Grace akakaa.
“Wanagombania nini
tena?” Grace akauliza. “Eti Sara kachukua pesa bila kumwambia baba Fili, halafu
anamjibu mbovu. Anasema alienda kubadili matairi ya gari yake.” “Sara ana gari!?”
“Acha dada! Kanunuliwa gari na simu mpya kama hiyo yako mpaka
rangi. Basi fujo! Shopping kila siku. Eti anasema ile gari ina matairi
asiyoyapenda. Ndio kachukua kadi ya baba Fili, akaenda kutoa pesa bila
kumwambia. Bwana nusura wapigane hapa. Baba Fili kakasirika, Sara naye anamjibu
mbovu. Lakini wameondoa vitu vyao vyote. Kaka Jeri alituma watu wakusafisha,
naona kumesafishwa kila mahali. Sasa hivi ni sisi tu dada.” Grace akapiga
magoti akaanza kumshukuru Mungu wake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Walipotulia, mama G
akawaita Geb na Nanaa. Wakakaa. “Mimi nataka kuzungumza na nyinyi.” Mama G
akaanza baada ya kuwalaza watoto kwa usingizi wa chana. “Kwanza niwashukuru kwa
heshima kubwa sana mliyonipa. Nanaa, nakushukuru kwa kurudi na kuamua
kunisamehe ili utuweke pamoja. Naomba uniamini tu, kama isingekuwa wewe
kukubali yaishe, sisi tusingekuwa hapa, tena tukiwa na hii furaha. Asante
mama.” Nanaa akacheka. “Mimi nishakuzoea. Sasa, sasahivi tukigombana,
tunanuniana tu, hakuna kutengana.” Wakacheka.
“Lakini
Nanaa na Geb, kuna kitu amenisimulia James, nimesema niwaambie tu na nyinyi.”
“Juu ya nini?” Geb akauliza. “Kumbe yale yote yaliyokuwa yakiendelea usiku ule
Nanaa alipotoka hospitalini, ulikuwa ni mpango uliokuwa umepangwa kwa muda
mrefu sana. Na Gozi alikuwepo pale, akiwa kama mpeleka habari kwao. Muda wote
alipokuwepo pale alikuwa akituma ujumbe.” Mama G akawasimulia kila kitu. “James
ameumia sana.” “Hata mimi mama. Imeniumiza sana. Hawa watu mimi nimekuwa
nikiwasaidia kupita kiasi. Ni kwa nini wanataka kushindana na mimi!?” “Wivu!”
Nanaa akadakia.
“Sawa sawa Nanaa. Ni
wivu tu. Wanataka kukuangamiza. Na ninaona kwa upande fulani wanafanikiwa.” Geb
na Nanaa wakakunja uso. “Kivipi wakati sisi tunaendelea na maisha yetu?” Geb
akauliza. “Maisha haya ya kubanana hapa!? Si wamefanikiwa kuwatoa pale kwenye
nyumba yenu nzuri ya thamani wakawaleta hapa, kwa kuwajengea hofu! Sasa hivi
mnaishi kama wao.” Geb alijua wazi anachokifanya mama yake. Nanaa akanyamaza
kidogo kama anayejifikiria na mama G akanyamaza makusudi.
Akagundua wote
wanamwangalia yeye. “Ila niseme ukweli mama, sasahivi hofu imeisha. Muulize
Geb. Alinikuta nikiota ndoto mbaya sana za kubakwa. Nilikuwa silali! Usiku
kucha naota napambana. Ilibidi Geb aniombee ili kuweza kutoka hapo.” “Nilifunga
Nanaaa. Kwa siku tatu mfululizo nikimuomba Mungu akutetee.” Mpaka machozi
yalimtoka Nanaa. “Asante Geb. Kweli nilikuwa
nikiteseka. Mpaka nilikuwa nauogopa usiku! Ilikuwa giza likiingia nilikuwa
najiambia ndio mateso yangu yanaanza.” “Usilie
sasa. Utakaribisha tena hofu.” Walikuwa wamekaa kochi moja. Geb akamvuta mkono
na kuubusu. “Huko umeshatoka Nanaa. Hutarudi tena.” “Amina. Na mimi naamini hivyo Geb.” Nanaa
akajifuta machozi.
Mama G akafyonza kwa
hasira kama asiyejua chakufanya. “Lakini ipo siku yao na wao Mungu atawalipa
tu.” Mama G akaongeza kwa hasira. “Wamekuachia kovu baya kumbe ni wivu wao kwa
Geb! Wajinga kabisa.” “Lakini mama angalau sasa hivi sioti tena.
Nimefunguliwa.” “Kwa hiyo tunaweza kurudi pale?” Mama G akauliza. Geb akamwangalia
Nanaa. Nanaa akavuta pumzi. “Tutakuwa wote Nanaa. Huna haja yakuogopa.” Nanaa
alishaanza kusugua mikono. “Niangalie Nanaa. Upo salama. Hakuna mtu atakayeweza
kutuingilia pale tena. Nimebadili mfumo mzima wa ulinzi na wale wote hawawezi
kurudi pale tena.” “Sio pale tu, hawatakaa kurudi kwenye maisha yetu.” Mama G
akaongeza.
“Tukalalie
kitanda kile kile Geb!? Najiona sipo tayari. Nahisi kama sitaweza kulala.” Tayari
machozi yalishajaa machoni. “Hujui
unyama alionitendea Malii, Geb. Naumia sijui jinsi yakufanya. Naogopa kuingia
kwenye kile chumba najiona kama ndio siku ile ananiingiza kwenye kile chumba
nakunifunga mikono yangu.” Geb akajisogeza karibu yake zaidi. “Pole
mpenzi wangu. Pole sana.” Geb alijaribu kumtuliza. “Naomba unisikilize Nanaa.
Naomba utulie kabisa. Kwanza huna haraka yakuhamia pale. Ni mpaka utakapokuwa
tayari. Ila pia nataka ujue kile chumba nilikibadilisha kila kitu. Tena kwa
kuchoma moto vitu VYOTE vilivyokuwepo pale ndani usiku ule Malii alipoingia
ndani ya chumba chetu. Nilitoa kila kitu kikabakia kitupu kabisa ndipo nikaanza
kukifanyia marekebisho. Tokea siku nimekufuata au kukupata pale hospitalini
ukiwa umelazwa Muhimbili, nilimwambia Jeri aanze kusimamia hiyo kazi. Nilikuwa
niko na wewe pale hospitalini, tukahamia kumuuguza wote Magesa, muda wote ule
kulikuwa kuna kazi ikiendelea kwenye kile chumba.” Nanaa akashangaa. Hakuwa
hata akijua.
“Kimebadilika sana.
Twende ukaangalie. Hata rangi ya chumba nilibadilisha. Hakuna kitu hata kimoja
unachokifahamu pale ndani. Kila kitu niliweka kingine. Ukiingia pale hutaweza
kujua kama ni kile chumba chetu.” Kidogo Nanaa akaanza kutulia. “Twende
nikakuonyeshe. Na nilifanya hivyo kwa ajili yetu, zaidi wewe. Ili usipate hizo
kumbukumbu tena.” “Asante Geb. Mimi sikujua!” “Basi ujue kipo na kilikuwa
kikikusubiri wewe muda wote. Twende ukaangalie. Utakipenda zaidi.” Nanaa
akaanza kutabasamu. Akamshika mkono ili kumsaidia kusimama.
“Nakushukuru Geb
mume wangu.” Mama G akaguna. Nanaa akacheka sana. “Sasa
unaguna nini mama?” “Nisikilizeni Geb na Nanaa. Mnaenda kuangalia chumba na
kurudi hapa.” Geb na Nanaa wakazidi kucheka. “Unanisikia Nanaa? Nawasubiria
hapa tuzungumze. Sio muende huko, safari moja ianzishe nyingine.” “Mama!” “Mama
nini? Kwani siwajui nyinyi? Na hivi ni chumba kipya! Ushashikwa mkono hapa na
kuambiwa kimetengenezwa kwa ajili yako! Humtakaa mkarudi hapa.” Nanaa na Geb
wakacheka mpaka wakarudi kukaa.
“Kwanza mimi naona
nimalize mazungumzo yangu kabisa. Hizi habari zakuwasubiria nyinyi hapa, hapana.”
“Kwa nini unakosa imani na sisi, mama G?” Geb aliuliza huku akicheka sana. “Leo
yenyewe mlituchelewesha uwanja wa ndege. Ilibaki kidogo tu tuachwe na ndege.
Watu wote tumekaa pale chini hotelini tunawasubiria nyinyi! Simu hampokei, na
wakati tuliagana vizuri baada ya kifungua kinywa. Mkasema mnaenda chumbani
kwenu mara moja mtarudi baada ya muda mfupi. Hatukuwaona tena.” “Ni Geb huyo!”
Nanaa akajitetea. “Mmmh!” Mama G akaguna. “Kweli mama. Ni Geb. Na nilimwambia
tutakosa ndege, akasema yeye anaenda na muda.” “Lakini kwani nilikosea?
Hatukuachwa na ndege.” Geb na yeye akajitetea.
“Mimi ninachoomba tumalize mazungumzo ndio muende mkaangalie chumba mtakavyo!” Wakazidi kucheka. “Sawa mama. Lakini ujue nimefurahi Geb.Asante kwa kubadilisha kile chumba. Nilikuwa nakiogopa sana. Ndoto zangu zote nilikuwa nikiishia kubakwa pale pale kwenye mazingira ya kile chumba. Kwa hiyo nashukuru sana.” Nanaa akampa na busu la mkono. “Karibu.” Geb akajibu, Nanaa akaendelea.
“Halafu nimefikiria, nimeona tukihamia pale itasaidia pia kwa hiyo siku ya jumamosi. Tutakaribisha wakwe wa Grace kwa uhuru.” Mama G akasimama nakuanza kupiga vigelegele huku akizunguka. “Mama mjanja nyie! Yaani kumbe hiyo ndio ilikuwa shida yako? Turudi kwa ajili ya huo ugeni!” “Kumbe! Lakini pia Nanaa, hapa sio kwako mama. Hapa washakaa watu wengi wa kila namna. Pale ndio kwako. Anza ndoa yako nyumbani kwako na wanao. Jenga familia yako sehemu nzuri ambayo Mungu amewajalia. Majaribu yanatakiwa kukukimbia sio uyakimbie.”“Kweli mama.” “Basi naomba leo tukalale kwetu.” Geb akamalizia kwa haraka. Nanaa akacheka. “Sawa.” Mama G akaanza kushangilia tena.
“Basi nampigia simu Jeri
aje sasa hivi na watu wawili watusaidie kuhama.” Geb akambusu Nanaa mdomoni. “Nakushukuru
sana.” “Kumbe na wewe ndio ilikuwa shida yako Geb! Kwa nini hukuniambia?”
“Nilitaka mapumziko mazuri. Sikutaka uanze kunililia kwenye fungate
nililosubiria miaka yote tokea mtoto.” Nanaa alicheka sana. “Nilikuwa
nikizisubiria hizo siku tatu kwa hamu sana. Kwanza ni vile tu tulikuwa na
watoto na afya yako inasumbua. Nilitaka tupate mapumziko marefu sana.
Tunastahili Nanaa.” “Kweli. Lakini ulisema nikijifungua salama, Jimmy
akichangamka tu, tunamwachia mama, halafu sisi tunarudi tena fungate? Au umebadili
mawazo.” Nanaa aliongea kwa sauti ya chini ili mama G asisikie.
“Siwezi kubadili mawazo.
Ujue mwenzio nimeshaanza kusubiria hilo fungate la pili!” “Kweli Geb?” “Kabisa.
Maana hapo utakuwa sio mjamzito. Ni mimi na wewe tu.” Nanaa akacheka kwa sauti
ya chini. Wakataka kuanza kupeana
mabusu, mama G akawawahi. “Mimi naona umpigie simu kwanza Jeri.” Nanaa akacheka
sana. Geb akasimama na kutoka pale. “Yaani mama nyie!” “Mimi nawafahamu nyinyi.
Hata hapo kwenye hilo kochi pia msingenyanyuka leo. Mwiteni Jeri aje, tuhame,
muendelee na fungate tukiwa kwenye ile nyumba nyingine. Roho yangu ndio
itatulia. Hamtanisikia hata nikiwaita. Na hivi mke wa Jeri anaanza kuja kesho
kunisaidia kazi, sitakubugudhi kwa lolote.” “Haya mama yangu.” “Lakini Nanaa,
umenifurahisha sana mwanangu. Sasa hivi nina amani yakukaribisha wale wamasai.
Angalau wakija kwenye ile nyumba nyingine, heshima itaongezeka.” Mama G na
Nanaa wakaendelea kuongea.
Nanaa, Na Umama
Magesa!
Geb akarudi. “Jeri
atakuja na watu wakutusaidia kuhama. Naomba utulie Nanaa. Mimi na mama
tutatafanya kila kitu. Nimemwambia pia amtume mkewe aje.” “Leo!?” Mama yake akauliza. “Ndiyo leo.” “Mimi
nilizungumza naye aje kesho.” “Mwache aje kuanzia leo. Tutamuhitaji tu.” “Njoo
Geb nikwambie jinsi nilivyofikiria.” Geb akarudi kukaa.
“Mnisahihishe lakini.
Binafsi najisikia kumfanyia kitu kizuri Grace. Amekuwa upande wangu tokea
ananifahamu. Amenipenda kwa upendo ambao sijui nisemeje. Ananifundisha mambo mengi bila kunikatia tamaa na...” “Sasa hapo utapandisha
pressure!” “Bwana mama!” “Kwa nini unalia jambo la kheri?” Nanaa akaanza
kucheka huku anafuta machozi. “Usilie bwana. Haya Endelea. Mimi nataka
kukusikia.” “Haya mama. Nilikuwa nasema hata katika wanawake wote aliokuwa nao
Geb, Grace alisimama na mi.. ” “Nanaaa!” Geb akashituka kidogo. Mama yake
akacheka.
“Nilikuwa na Liz tu!”
Nanaa akazidi kucheka. “Akaja na Frida?” Mama yake akaongeza kama kumkumbusha.
“Mama na wewe! Mambo hayaishi.” “Ndio utulie.” “Kwani nilirudia tena? Mungu
mwenyewe alinichukua akaenda kunifundishia jela!” Nanaa na mama G walizidi
kucheka. “Na ulikomeshwa!” “Si kidogo mama. Baadaye nikamwambia Mungu, hili
somo angenifundisha kwengine mbona ningeelewa tu? Kwani ilikuwa lazima shule
ile nikaisomee jela!?” Nanaa alikuwa akicheka mpaka machozi. “Kichwa chako
kigumu. Akaona akikufundishia kwenye mazingira mazuri wewe, usingeelewa.
Endelea Nanaa.” Nanaa akafuta machozi.
Geb alikuwa akitingisha kichwa.
“Nataka mimi ndio
nishugulikie mambo yote ya Grace kabla
ya harusi yake.” Mama G akapiga vigelegele kwa furaha. “Sijamaliza mama.”
“Niambie mama Magesa. Naona umepokea jina na majukumu!” “Sitaki utani.” Mama G
alizidi kucheka. “Nakusikiliza Nanaa.”
“Kwa sasa, hapa kwenye haya mazungumzo, naomba uniite mama Magesa, Geb.
Sio Nanaa.” Yaani mpaka Geb alicheka. “Sawa mama Magesa. Ehe?” Geb akaongeza
huku akicheka. “Basi. Nataka kwanza nimwandalie shuguli nzuri sana. Siku ya
mahari, sitaki ahangaike kama anavyohangaika kwenye mambo yetu. Mama
umsisitizie atulie na sisi tumfanyie. Nitaomba mnipe namba za simu za mpishi.
Yule mama anayetufanyia mambo ya ‘catering’. Nitampigia simu na kumpa idadi ya watu
tutakao watarajia, na aina gani ya vyakula tutakavyo hitaji.” Mama Magesa
alizidi kufurahia.
“Nitaandaa pale pale nje. Bustanini.
Nitaomba Geb aniletee viti na meza za duara. Nitapamba kama alivyonipambia ile
siku ya kikao chetu cha kwanza cha harusi nikaishia kupata matatizo ya miguu.”
Kidogo wakatulia. Kama waliokumbuka ile siku. “Nitatengeneza vizuri ili
afurahie. Nyinyi mnasemaje?” Nanaa akawatoa kwenye mawazo. Kisha akaendelea
kabla hawajajibu. “Pia baada ya mahari tu, nitamwambia asirudi tena kwake. Waje
wahamie kwetu. Yeye, watoto na msichana wake wa kazi. Atulize mawazo kwenye
harusi tu. Sisi tumsaidie swala la watoto. Asijiguse kwa chochote, ni yeye na Mungu
wake tu.” “Hakika hapa umepata mke!” Mama G alisikika kufurahishwa sana.
Nanaa akaanza kucheka.
“Umepitisha mawazo yangu?” Nanaa alimgeukia mama G. Akionekana kutaka kumsikia
yeye zaidi. “Sio katika hili tu. Nilitaka kukuona kwenye umama, na kuanza
kufanya mambo mengine mengi. Kwa kasi hiyo! Hakika umenifurahisha. Lazima kuwa
na mipango mbali na kujua Geb anakula nini, uwe unasimama na kufanya mambo kama
hivyo. Hakika mtafika mbali sana.
Hongera Geb.” “Mimi mwenyewe siamini!”
Nanaa akampiga ngumi kidogo. “Kweli Nanaa. Nimefurahi kuona kuwa unamipango.
Tena mikubwa na ya kueleweka. Itanisaidia sana, kuliko kuniongezea kazi ya
kuanza kukuvuta katika kila jambo. Hicho ndio kitu nilikuwa natamani. Unaona
jambo, unatafuta nafasi yako katika hilo, unafanya bila hofu wala kusitasita.
Tutajikuta tunafanya mambo mengi kwa wakati mmoja.” Nanaa akajisikia vizuri
sana.
“Hata Grace atafurahi
sana. Asante Nanaa.” “Na mimi nimefurahi kama mnaona nimefanya jambo zuri.
Najifunza. Ukiona kuna kitu nilitakiwa kufanya halafu nikazembea, uwe
unaniambia mama.” “Ukitoa ruhusa ya hivyo, mbona itakuwa aghueni kwangu!
Tutasaidiana mambo mengi. Na hivi Grace anaondoka, pengo halitakuwa kubwa
sana.” Wakaendelea kuzungumza na kuhama.
Mahari ya Grace.
Siku hiyo ya jumamosi ilijaa heka heka ya
namna yake hapo nyumbani kwa kina Magesa.Nanaa na Mama G walikuwa wakihangaika
kuandalia wageni wao. Nanaa ndiye aliyekuwa mstari wa mbele. Akipiga simu huku
na kule akiagiza vitu gani viletwe na kuelekeza meza zipangwe wapi na kufanywe
nini. Asubuhi Geb alikwenda kazini, lakini Jeri alikuwepo hapo na vijana kadhaa
ili kusaidia kazi. Geb alisema Nanaa asinyanyue kitu, aagize tu. Mkewe Jeri
ndiye aliyekuwa na watoto pamoja na msichana wa Grace.
Kwa kuwa zilikuwa familia mbili tu, na kwa kina Magesa walikuwa wachache,
aliongezeka James tu, hawakuweka viti vingi sana na meza pia zilikuwa chache
wakijua watakuwa wachache. “Inatosha Nanaa. Twende tukaoge upumzike.” “Na kweli
naona nimechoka. Nahitaji kunyoosha hii miguu.” Wakarudi ndani kuoga ili
kupumzika, wakisubiria wageni.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Watoto wa Grace
walikuwepo hapo. Kila mtu alikiri wale watoto walibadilika. Walikuwa watulivu
sana. Wakati wote walitaka wawe karibu na mama yao. Grace aliwatoa shule. Kwa
hiyo siku ya alhamisi na ijumaa walikuwepo tu nyumbani na mama yao. Alishinda
nao kitandani siku nzima. Kama kuzungumza na Man kwenye simu, walizungumza
akiwa hapo hapo kitandani nakuendelea kucheza na watoto wake. Grace alijaribu
kuwachangamsha, wakaishia kuangalia tu tv. Walilala hapo hapo kitandani kwa
mama yao kwa siku hizo mbili mpaka jumamosi walipohamia nyumbani kwa kina
Nanaa.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Tofauti
na walivyotarajia, kina Ole walikuwa wamejiandaa kweli kweli. Kwanza walifika
wengi zaidi ya hata walivyofikiria. Japokuwa mama G hakutaka mahari, lakini
Mzee Ole alisisitiza ni lazima kufika kutoa mkono wa shukurani kwa kumlea Grace
na kufahamiana zaidi. Walifika hapo nyumbani mapema tu. Walikuja wengi, Nanaa
akabaki akiangaliana na mama G. “Tutawaweka wapi watu wote hawa!?” Kama Malisa
alijua mawazo yao. Akawasogelea. “Kwanza naomba msishtushwe na wingi wa watu.
Niwatulize kabisa, hawa watu ni wachache sana. Hawa ni ndugu tu. Tena
wakaribu.” Nanaa akaanza kucheka.
“Wote hao!?” Nanaa
akauliza. “Unafikiri nakutania Nanaa? Subiri siku ya harusi utaona. Pili,
hawana shida. Masai huwa hawajui kukaa.” Wakacheka. “Mimi huwa wananijaliaga
kwangu hivyo hivyo. Wala sijigusi. Na nyumbani kwa Mzee Ole ni kama sebuleni
kwao. Kuanzia jumatatu mpaka jumatatu wanapishana hapo nyumbani kwake.
Watasimama hivyo hivyo wala hawatahisi kuwa kuna upungufu. Wanachotaka nikuwepo
tu hapa. Mzee Ole amechinja ng’ombe leo. Nionyesheni sehemu ya kuziweka, watu
walioshugulikia kuzitengeneza wapo njiani wanakuja nazo. Wote hao mnao waona
hapo, wanasubiria hiyo nyama kwa hamu sana. Msiwe na wasiwasi juu ya chakula.”
Kidogo wakatulia maana walishafikiria kitu cha kuwalisha.
Walikuwa wamejaa,
ilibidi magari yao wayaache nje. Ni gari la Mzee Ole tu ndilo lililoingia hapo
na Malisa. Wengine waliacha nje magari yao. Kulisikika vicheko kwa masai hao wa
mjini, na ni kama wengi waliambizana. Ungejua tu ni masai. Kama hawakuvaa hiki,
basi kile chakuwakilisha mila zao. Kulikuwa na wazee baadhi ambao walikuwa
wakionekana ni Masai wa mjini lakini walitupia shuka za kimasai. Hata Mzee Ole
mwenyewe alifunga lubega. Kama alivyosema Malisa, vyakula vilijaa hapo.
Walikula na kusaza. Hata wasiwasi wa kuwa walitoshea vipi hapo haukuwepo. Kila
aliyesogezewa kiti, alisema yupo sawa tu, watasimama. Vilijaa vicheko na
pongezi kwa Man na Grace.
Aliwashukuru kwa zawadi,
zaidi heshima waliyompa. Ndipo mipango ya harusi ikaanza. Mzee Ole
aliwakaribisha tu. Hakuta wafanye chochote zaidi ya wao kutokea siku hiyo ya
jumamosi. “Man anastahili harusi nzuri. Atafunga kanisani. Nimeshazungumza na
mchungaji. Amekubali kufunga hiyo ndoa. Baada ya hapo kaka yake amemuandalia
tafrija. Kina Ole tupo wengi sana. Hapa hatujafika hata robo.” Wakacheka.
“Siku hiyo mtakutana na
Masai wengi sana. Mjiandae.” Wakacheka tena. “Tutakula nyama mpaka mchoke
nyinyi. Kwa hiyo mjiandae kwa hilo pia.” Kila mtu alifurahia. “Malisa, nataka
kumuona Grace kwenye shela refu sana.” Wote
wakacheka. “Usijali dad.” Walikula, watoto wakacheza, na kuagana kwa ahadi ya
kuja kukutana siku ya jumamosi kwenye harusi.
Maandalizi Ya
Harusi Ya Grace.
Hiyo week ilikuwa ni ya
heka heka kwa Grace na mama yake. Walitakiwa kutafuta nguo na vitu vya harusi
ndani ya siku 4. Mama yake alimtaka pia ajitahidi apate siku mbili zakupumzika
ndani bila kutoka wala kufanya kazi yeyote kabla ya siku ya harusi. Malisa naye
aliungana nao kusaidia kupatikana kwa gauni na shela aliyoitaka Mzee Ole. Grace ambaye aliolewa kwenye harusi ya pilau
na soda. Tena sherehe ilikuwa hapo hapo kanisani, leo anaolewa tena kanisani na
shela ndefu, halafu bwana harusi ni Man ambaye anambembeleza kama yai,
hakuna jinsi yakueleza furaha ya Grace. Malisa alihangaika nao, mpaka
wakakamilisha mambo yote kwa haraka, ndipo akatulia nyumbani kwa Geb. Akijindaa
kwa harusi.
Yeye na wanae na
msichana wa kazi walihamia hapo nyumbani kwa Nanaa kwa juma nzima, kama
alivyotaka Nanaa. Yeye Nanaa ndiye aliyesimamia swala la watoto na mambo yote
ya mle ndani, wakati Grace, Malisa na mama G, wakishugulikia swala la harusi na
hata walipomaliza hakutaka Grace ajisumbue na chochote. Alimwambia ajifikirie
yeye tu na aagize chochote atakacho, atafanyiwa.
Grace na
Danny
Ilipofika siku ya
alhamisi akiwa ametulia ndani akisubiria harusi yake, akapokea ujumbe kutoka
kwa Danny. ‘Kesho
saa 12 jioni nitafika kuchukua watoto. Tunasafiri jumamosi asubuhi sana. Naomba
mwambie Tere, watoto wawe tayari kwa wakati.’
Grace akakaa kwa mshituko. Akaamua
kumpigia. “Nisikilize
Danny. Weekend ile wakati Geb anaoa, hukutaka wanangu wahudhurie harusi yake.
Mimi nilichumbiwa siku hiyo, wanangu hawakuwepo. Weekend hii naolewa. Lazima
watoto wangu wahudhurie harusi yangu. Washuhudie na wajifunze kuhalalisha mambo
na wajue mahusiano yote ni lazima yafikishwe mbele za Mungu, ili wasidhani sisi
wote tuna akili zakufanana. Tunaishi tu na watu bila ndoa.”
Kimya.
“Kwa
hiyo, hutaweza kuwapata hawa watoto ijumaa mpaka siku ya jumapili.
Utaletewa pale nyumbani. Kwa sasa hatupo pale. Kwa hiyo usije nyumbani kuwachukua siku ya
ijumaa. Wataletwa pale siku ya jumapili asubuhi ya saa 4. Ukija hutamkuta mtu
hapo.” Kimya. Grace akajua ni jeuri ya Danny,
asijue mshituko uliompata mwenzie.
Akili zilimchukua Danny
mpaka siku alipomuona Man akibusu shingo ya Grace, mbele yao, baada ya
kukamilisha talaka. Kitu kilimtembea Danny kutoka utosini mpaka kwenye unyayo.
Akahisi kuishiwa nguvu. Uzuri alikuwa amekaa kwenye kiti, ofisini kwake.
Akahisi giza machoni lakini akashangaa kuona mikono ya Man, imepita kwenye
kiuno chembamba cha Grace huku amemuegemea begani, akiwa amesimama nyuma ya
Grace, karibu sana, wakati mama G akizungumza naye. Akashangaa kwani siku ile
alikuwa kama hajaona. Lakini leo ile picha ikajirudia sawia. Man alinong’ona
kitu sikioni kwa Grace, kisha akambusu kichwani. Akakumbuka kuona tabasamu
usoni kwa Grace baada ya kunong’onezwa. Hilo likamjia tena Danny.
Grace akaangalia simu
kama imekatwa. Akaona bado. Danny maneno mengi yupo kimya! Grace mwenyewe
hakuamini akaona ni wakati mwafaka wakuendelea kumuweka sawa. “Na ninakuonya Danny, acha kupiga wanangu.
Kama unamahasira yako, jimalizie wewe mwenyewe. Acha kabisa kutesa watoto na
kuwanyima raha. Usifanye wanangu kama watu wazima nakushindwa kucheza! Hapana
Danny. Kama wewe umeshindwa kuona wanangu wakizungumza kwa uhuru, na kucheza,
basi niachie mimi mwenyewe mpaka watakapokuwa watu wazima ndipo uwatafute. Acha
kujifanya kama umechanganyikiwa.” Grace akakata simu.
Danny hakujua ile simu
ilikatwa saa ngapi, ila simu ya Sara ndio iliyomtoa mawazoni. Mambo mengi
yalikuwa yakipita kwenye akili za Danny baada ya kumsikia Grace akimwambia
anaolewa. Alipigwa na butwaa asielewe imekuaje au ni nini kinaendelea kwenye
maisha yake. Kwa dakika kadhaa ni kama maisha yalipoteza dira bila yeye kujua.
Kama ndio anatoka usingizini, akiwa bado haelewi vizuri. Ndio alikuwa ameingia
ofisini asubuhi hiyo ya saa mbili. Alipofika tu ofisini alikusudia kuwa jambo
la kwanza nikumtumia ujumbe Grace juu ya watoto kabla kazi kuchanganya hapo
ofisini, akasahau. Kwani alikuwa akisafiri jumamosi. Kwa hiyo alitaka kuweka
mambo sawa juma hilo ili akirudi kazini asikute viporo vingi, kwa hiyo alikuwa
na kazi nyingi.
Alipoangalia simu wakati
anataka kupokea simu ya Sara, akagundua tayari ni saa tatu na nusu. Inamaana
alibaki ameduaa pale zaidi ya lisaa! Grace alipiga na kutoa taarifa za kuolewa
kwake. Hakujua hata alichoendelea kuzungumza baada ya pale lakini alijua hawezi
kupata watoto siku hiyo ya ijumaa kwa kuwa jumamosi wanatakiwa kuhudhuria
harusi ya mama yao.
“Grace anaolewa!?” Danny akawaza kwa
sauti, asijue ni kwa nini. Lakini hata masikio yake yakasikia. Hakuwa tayari kuzungumza na Sara kwa wakati
ule. Alimuacha amelala. Lakini ni kama
alijua sababu ya kupigiwa simu mida ile. Akajua ndio ametoka usingizini.
Kama alikuwa akimuona pale kitandani alivyokuwa amejifunika kama mgonjwa huku
ameegesha simu yake sikioni. Akaamua asipokee.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Mama G akaingia. “Mbona
umeamka na hasira? Kwema?” Mama yake akakaa. “Si Danny anataka kuniletea ujinga
mimi! Eti anataka watoto kesho. Kwa maana nyingine wanangu wasihudhurie kwenye
harusi yangu, wote tuonekane tunaishi na watu tu bila ndoa! Unafikiri tutakuwa
tunakuza watoto wa namna gani?” “Kwa hiyo mmefikia vipi?” “Nimemwambia aende
akachukue watoto pale siku ya jumapili saa 4 asubuhi.” “Sasa atawarudisha
lini?” Grace akabaki kimya.
“Ukumbuke utakuwa kwenye
fungate.” “Nilizungumza na Man, tufanye fupi ili tuje tuwahi watoto. Tutapata
mapumziko ya siku chache, halafu tunarudi. Na yeye alisema atarudisha watoto
hiyo siku ya ijumaa. Aliwataka kwa siku 7 tu.” “Sasa ijumaa utakuwa umerudi?”
Grace akafikiria kidogo. “Itabidi niwepo mama, ili niwe na wanangu na yeye
asipate sababu.” “Sawa.” Nanaa akaingia.
“Kwema bibi harusi?”
Nanaa akauliza. “Basi mama nipishe hapo mimi ndio nijilaze, wewe kakae pale
kwenye kochi.” “Lakini umenikuta Nanaa.” “Mama naye! Mimi mgongo unaniuma.” “Si
ukalale chumbani kwako?” “Naona uvivu bwana mama. Sogea.” “Nanaa naye!” Grace
akaanza kucheka. “Nataka kulala na Grace.” “Umbea tu! Unataka kujua alikuwa
anagomba nini asubuhi hii.” Nanaa akaanza kucheka. “Muone. Wewe kakae pale
utasimuliwa.” “Sitasikia raha nikiwa mbali na nyinyi. Havitanoga. Wewe nenda
kakae pale kwa kuwa ushasimuliwa, sasa hivi zamu yangu.”
“Nanaa acha umbea wewe
mtoto! Ndoa itakushinda.” “Akuu! Nishamuaga mpenzi wangu vizuri tena kwa kituo.
Usinione hivi. Shule yako na ya Grace
mbona nimeielewa?” “Sasa yuko wapi?” “Atakuja kukuaga sasa hivi, kabla hajaenda
kazini.” Nanaa akajilazimishia hapo kitandani, akamsukuma mama G kidogo mpaka
akapata nafasi hapo kitandani. Akalala pembeni ya Grace. Lakini mama G
hakuondoka. “Nanaa yupo huku?” Wakasikia
sauti ya Geb. “Wewe si ulisema umeaga wewe!” Nanaa akaanza kucheka. “Njoo
mpenzi wangu. Ni mama huyo!” “Nanaa wewe mtoto! Mimi nimefanyaje?” Geb akaingia
mpaka pale. “Umesahau kunywa dawa. Umeziacha pale mezani. Naomba kaa unywe sasa
hivi kabla sijaondoka.” “Mwenzio kaletwa na umbea ndio maana dawa kasahau!”
Nanaa akakaa huku anacheka. “Mama hana dogo!” Nanaa akapokea dawa.
“Vipi G?” “Si Danny
anataka kuniletea ukorofi.” Grace akamsimulia kaka yake kila kitu. “Nataka kuwa
na wanangu Geb. Wanione ninaolewa.” “Hata kama hatakubali hapa hawezi kuingia
kwa kuwa hataruhusiwa. Na siku ya harusi hawatatoka hapa mpaka jioni. Naomba
utulie. Pata muda wakupumzika. Acha kuwaza mawazo unayojua yatakunyima raha.”
Grace akatulia.
“Lakini Grace amezungumza jambo kubwa
sana. Nyinyi mnaweza msione kwenye ulimwengu wa roho. Lakini kuna roho za
kurithi. Lazima kusimama na kumlilia Mungu juu ya hili. Mnaweza msielewe ni kwa
nini nilikuwa mkali sana kwa Grace, kujitunza mpaka ndoa. Nilijua yale
niliyoyafanya mimi na baba yenu. Sikutaka hiyo roho ihamie kwa Grace. Naona
tukajitahidi wee, vikawezekana kwa Danny lakini kwa Man tukarudi kule kule.”
Grace akanyamaza.
“Nanaa na Geb, na nyinyi
watoto wote mmepata nje ya ndoa. Jamani hiyo ni roho! Lazima tuikatae na iishie
kwetu tu. Kwa Grace iwe mwisho. Tumlilie Mungu isiende kwa kizazi cha tatu kina
Fili na Oliva! Lazima kufanya juhudi za makusudi kumlilia Mungu. Kwa kutubu
haswa, ili Mungu aturehemu. Mnaweza msione sasa hivi, lakini inauma sana
ikitokea kwa mtoto uliyemzaa wewe. Ukiwa wewe unafanya hivyo, unajihesabia
haki nakuona ni sawa kwa sababu hii na ile. Sasa subiri aje afanyiwe hivyo
Oliva au aje aishi hivyo Fili. Inauma sana. Tuombeni rehema.” Kulizuka ukimya
wa gafla kila mmoja akiwaza lake.
Geb alibaki amesimama
kama sanamu. Mama G aligusa pabaya. Oliva! Liv wake aishi na mwanaume bila
ndoa! Akahisi ataua mtu. “Ndio tunafanyaje?” Geb akauliza. “Lazima kukiri kuwa
ni kosa. Tutubu kabisa. Ingekuwa tumefikiria hili kabla, Nanaa na wewe,
mngetubu kwa pamoja mbele ya mchungaji kabla hajawafungisha ndoa. Lakini
hamjachelewa. Mpate muda nyinyi wawili, mtubu. Kwa kumaanisha na kumsihi Mungu
arehemu kizazi chenu chote.” Akamgeukia Grace.
“Wewe na Man, mnayo
nafasi. Zungumza na Man, kabla mchungaji hajawafungisha ndoa, mtubu. Mungu
awasamehe kwa kuwa mlitenda dhambi. Nyinyi mnataka ndoa takatifu, basi muingie
mkiwa mmejitakasa.” Grace akavuta pumzi kwa nguvu. “Nitazungumza na Man.” “Sawa
na pia itabidi mkishatulia. Tutafute siku moja ambayo wote tutafunga na kuombea
kizazi chetu. Katika hilo eneo tu.” “Wazo zuri.” Geb akachukua glasi kutoka kwa
Nanaa, na kumbusu mdomoni. “Utanipigia ukifika kazini?” “Nitakupigia.” Geb
akamjibu Nanaa. Akambusu mama yake kichwani pale alipokuwa amekaa. “Uwe na siku
njema. Ulinzi wa Mungu usiondoke kwako. Uzidi kufanikiwa.” “Amina mama.” Geb
akatoka.
“Mimi naomba tuombeni
mama. Wala tusisubiri siku nyingine. Leo leo tutubu. Tutubu kwa niaba ya Geb
& Man. Grace aliniambia maombi ya mama yana nguvu sana. Mimi naombeni
tuombe mama. Tutubu na tuombee watoto wetu. Hiyo roho ikome kabisa.” Wakaanza kutubu. Waliomba hao wanawake
watatu bila kuchoka. Grace na mama yake walipiga magoti, Nanaa alikuwa
amesimama akizunguka hapo chumbani. Walimuita Mungu na kumsihi awasamehe.
Sara kwa
Danny!
Huwezi kukwepa simu ya
Sara, hasa akikusudia kuzungumza na wewe. Labda uzime simu yako. Napo Danny
alijua endapo atazima simu, baada ya muda mfupi atakuwa amefika hapo ofisini
kwake. Aliendelea kupiga kama nyumba inawaka moto na yeye amefungiwa ndani.
Mwishowe Danny akaamua apokee tu japo alijua ni nini anataka. “Ni nini Sara?” “Kwa nini hupokei simu
zangu sasa!?” “Wewe si unajua kama nipo kazini?” “Mimi ni mpenzi wako, natakiwa
unipe kipaumbele. Kama nina tatizo je?” “Unataka nini?” Danny
akaona afupishe maneno. Alikuwa amepoa kama sio yeye Danny.
“Mbona hujaniachia pesa ya matumizi?” “Matumizi gani?” Danny
akauliza. “Uliza
wanaume wenzako wote hapo ofisini kama wanaondoka majumbani kwao bila kuacha
pesa! Wewe vipi Danny?” “Kwa kuwa wake zao wanamatumizi ya hizo pesa. Kama
kununua chakula ili wapike, au sabuni ili wafue nguo na kusafisha. Wewe hayo
huyafanyi. Na kama ni pesa za matumizi yako binafsi nimekupa juzi. Ukasema
umemaliza pesa yote kwenye nywele, kununua nguo za ndani na kubadili kucha.
Nikakuuliza kwa hiyo umekamilisha kila kitu, ukasema ndiyo. Sasa ndio
nakuuliza, unataka pesa ya nini tena?” Danny
alimuuliza taratibu tu.
“Ikitokea dharula?” Sara akauliza
akionyesha kuishiwa nguvu. “Dharula
ipi na wewe ndio unaamka? Hata kitandani bado hujatoka! Gari yako nimejaza
mafuta. Sasa unazungumzia dharula ipi?”
“Huwezi
kujua.” “Basi utakapojua, utanipigia tena simu. Naomba kurudi kazini.” Danny
akakata simu. Baada ya sekunde kadhaa ikaanza kuita. Sara tena.
Danny akapokea. “Mbona unanikatia simu!?” “Nimekuaga Sara.
Labda kama unataka ugomvi tu na mimi?” “Unanidharau Danny. Unaniona mimi sina
maana sababu sijapata kazi.” “Sema huna kazi. Ukisema ‘sijapata’, inamaana
umetafuta halafu umekosa.” Ukaanza ugomvi asubuhi hiyo hapo kwenye
simu. Sara yupo nyumbani kwao, kitandani amelala, anamlalamikia Danny
anamdharau. Danny yupo ofisini, kazi haziendi analumbana na Sara.
Man kwa
Grace.
Moyo wa Grace ulijawa
furaha mara baada ya kuona simu yake ikiita na Man ndio mpigaji. Akapokea kwa
haraka. “Mbona
unasikika kama huna furaha?” Man
akamuuliza Grace asubuhi hiyo alipompigia simu. “Hapana nipo tu sawa. Usiwe na wasiwasi.
Vipi umeamka salama?” “Nimeamka salama. Sema nimechelewa kukupigia simu sababu
kuna mambo nilikuwa nafanya tokea saa 10 asubuhi. Nilitingwa.” “Pole. Nini
tena?” Grace akauliza. “Ni mambo tu ya hapa. Ila
nimesharekebisha.” “Utarudi kulala?” Grace
akauliza akisikika kujali. “Siwezi.
Nataka nikazane kufanya kazi niache mambo sawa. Ili nikija huko akili ziwe
kwako tu sio niwe nawaza na huku.” Ilimgusa sana Grace. “Nina hamu na wewe Grace, mpaka nahisi
kuchanganyikiwa. Nishazoea kuamka pembeni yako.” “Pole. Tumebakisha siku chache
tutakuwa wote. Na mimi nina hamu na wewe Man.” Nanaa
na mama G wakatoka kuwapisha.
“Ila sipendi hivyo unavyosikika. Umekasirika kwa kuwa
nimechelewa kukupigia simu.” “Hata kidogo Man. Najua upo kazini mpenzi.” “Ni
nini sasa?” Man akaendelea kuuliza kwa kubembeleza. “Tutaongea ukija.” “Hapana. Nikija
nakuhitaji wewe Grace. Naomba tumalize matatizo yote kabla ya siku yetu.” Grace
akatulia. “Niambie
tu.” “Labda ukapumzike. Ukiamka ndio tuzungumze.” “Nilikwambia sitarudi kulala
Grace. Na siwezi kutuliza mawazo kama nikijua kuna jambo linakunyima raha.”
“Sio kuninyima raha. Ni jambo la kuzungumza tu. Ila nahisi Danny naye alinikera
asubuhi alivyonipigia.” “Ni nini tena?” “Nafikiri pia nimemchukia tu. Hakuna
baya amefanya. Ila alitaka watoto ijumaa wakati harusi yetu ni jumamosi.
Nimemkatalia.” “Ikawaje?” Man akaendelea kuhoji taratibu.
“Sidhani kama tatizo ni hayo mazungumzo. Ni kile kitendo tu
cha kumfikiria kuwa nitakuwa naye daima na hawa watoto! Hilo linanikera Man,
siwezi kujisaidia. Halafu anapiga sana wanangu, hilo ndilo linaniumiza zaidi.
Watoto wamebadilika. Fili ananiambia huwa anawachapa sana. Najilaumu naona ni
tabia niliyofungia macho tokea kwa Fili, sasa sasahivi ndio mbaya zaidi kwa
kuwa sipo nao kipindi hiki. Nawaza akishawachapa hivyo, ni nani anakuwepo kuwatuliza?
Fili ndio anawabembeleza wadogo zake! Naumia Man. Na makosa yenyewe
wanayochapiwa hawa watoto, ukiwauliza au ukimuuliza dada yao, ni ya kitoto Man.
Kuruka au kucheza! Kweli? Sasa sijui wameingiwa na hofu, unajua hawataki hata
kucheza? Wamekaa tu hapa kama wajinga! Hawa mapacha mpaka wamejifunza kunyonya
vidole. Nahisi ni kama njia yakujiliwaza. Naumia sana Man.”
“Naomba usilie Grace. Umebaki muda mfupi sana tutakuwa nao.
Hesabu siku. Halafu hatujachelewa. Tukiwa nao, tunaweza kuwarudisha wakawa
watoto wa kawaida. Kuwaambia kwa vitendo kuwa ni sawa kucheza, kuzungumza
wanachofikiria na mengineyo. Nakuhakikishia watarudi kwenye hali ya kawaida.
Usihofu mpenzi. Nikifika tu jumamosi nitakuja kuwachukua, nikae nao kidogo,
kabla ya harusi.” “Sidhani kama watakubali Man. Wameingiwa hofu, wapo kama
wanaogopa watu! Wamening’ang’ania hawataki hata niwaache kwa dakika 5! Wananifuata
mpaka chooni!” “Basi baada ya harusi, wakirudishwa tutapata muda nao. Kila kitu
kitakuwa sawa. Umenisikia?” Grace akatulia.
“Sawa.” “Na nini tena?” Man
akaendelea kuuliza. Grace akamueleza kila kitu juu ya yale aliyoambiwa na mama
yake. Man alitulia akisikiliza. Hakuwa hata na wazo. Hakujua kama ni dhambi.
Kwanza si anamuoa? Tatizo liko wapi akila vyake kabla ya ndoa! Akasikiliza
hapo, kimya. “Man!”
“Nipo mama. Nasikiliza.” “Sasa upo tayari kutubu?” Man
akaanza kucheka. “Bwana Man!” “Kwani si nakuoa mwenyewe?
Tatizo liko wapi?” “Kwa hiyo unataka tukija kuzaa watoto wetu, labda tuseme ni
wakike, aje afanye kama sisi? Aanze maisha ya ndoa kabla ya ndoa, ni sawa?”
“Nitamchoma mkuki huyo mwanaume. Na nitahakikisha hatawahi kuja kulala na
mwanamke mwingine tena.” Grace akaanza kucheka. Alicheka sana.
“Acha kutoa mifano hatarishi bwana Grace! Ujue mdomo
unaumba?” Grace alizidi kucheka. Akili ya Man
ilirudi likizo kwa haraka. Gafla maandiko ya bibilia yakaanza kumrudia. “Ujue imeandikwa kwenye
{mithali 18:21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao
waupendao watakula matunda yake}.” Grace alizidi kucheka. “Acha kutamka hivyo kwa binti yangu!”
“Ndio uje tukatubu halafu tuanze kutamka uzima.” Hapo
Man akapoa na kukubali kwa haraka. “Na ukemee kabisa hiyo roho.” Grace
akazidi kucheka. “Umesikia
Grace?” “Uje tukemee wote.” “Wewe anza. Nitakuja kuongeza nguvu.” Grace
alizidi kucheka.
Siku Ya
Harusi Ya Grace & Man
Man alitua jijini siku
ya jumamosi asubuhi tayari kwa harusi.
Grace hakutaka kwenda saluni. Aliletewa watu pale pale nyumbani. Walihamia
nyumba ndogo ya kina Geb ili kuwa huru kutengenezwa. Walikuwa wakisimamiwa
harusi na kaka yake mkubwa Man, na mkewe. Kwa hiyo mke mwenzake Grace na
wasimamizi wa kike walikuwepo hapo kwenye
hiyo nyumba tokea asubuhi wakitengenezwa.
Ni kama walihamisha saluni ya huyo dada kwenye nyumba hiyo.
Alikuwa na wasaidizi
wengi wa kumsaidia mambo ya nywele, kucha na makeup. Alikuwepo hapo na marafiki
zake. Malisa naye alifika mapema kidogo kuhakikisha kila kitu kipo sawa. Hakika
alishugulika mpaka mama G akamshukuru. Alionekana alikuwa na kazi nyingi sana. “Pole
mama. Pole sana.” Malisa akacheka. “Asante. Nimeamka saa 11 asubuhi mama yangu,
na nililala saa 7. Mzee Ole anapenda vitu vizuri sana. Sitaki afike kanisani au
ukumbini aanze kugomba. Maana huwa hanaga aibu yule. Asipopenda kitu, hafichi.”
Wakacheka.
Hakika Grace alipendeza.
Alikuwa kama binti mdogo. Geb aliwanunulia watoto wake suti nzuri sana. Tena
zilifanana na Magesa. Oliva kama kawaida yake alipendeza usingechoka kumtizama.
Alifundishwa kumwaga maua. Nanaa ndiye aliyekuwa mwalimu wake wa kwanza. Alikuwa
akimfundisha kumwaga hayo maua lakini yeye akashindwa kumfundisha Liv. Ilikuwa
ndio kazi yake week nzima hapo nyumbani. Baba yake alinunua mengi. Akawa na
kazi yakufanyia mazoezi. Anatembea hatua mbili anamwaga katikati, kulia na
kushoto. Hapo atacheka mpaka anakaa chini, kuja kuamka hapo, Nanaa ambaye ni
mwalimu anakuwa ameshachoka. Wote wanacheka. Atagaragara kwenye hayo maua na
kuyamwaga yote chini kisha anayalalia. Huku akitaka mama yake amwangalie. Nanaa
alimwambia Geb hadhani kama Liv ataweza. Heri atafutwe mtoto mwingine. Yeye
anafanya mchezo. Geb aliamua kumfundisha yeye mwenyewe. Tena hakuchukua hata
muda mrefu, Liv akaweza. Alikuwa akimwaga huku akicheka lakini sio kukaa chini.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Man alishafika kanisani
mapema, akabaki akimsubiria Grace wapate muda wakutubu mbele ya mchungaji kabla
ya harusi. Ilikuwa wafanye hayo yote siku moja kabla, lakini bado Man alikuwa
na majukumu huko Arusha akashindwa kufika siku ya ijumaa. Malisa alimtuliza na
kumwambia atamfikishia hapo bibi harusi mapema tu tena akiwa amependeza.
Waliingilia mlango wa nyuma ili kufika ofisi ya mchungaji. Man na Grace
wakaeleza kuwa wanahitaji kutubu. Wakapiga magoti, wakaombewa ndipo wakahamia
kanisani kwa ajili ya kufungishwa ndoa.
Hakika watu walijaa hapo
kanisani na kushangaza familia hiyo ya Magesa. Wazee walivaa suti za maana
lakini walitupia mashuka ya kimasai begani. Mzee Ole mtu wa watu, kila mtu
alitaka kuhudhuria. Liv alifanya kama alivyofundishwa na baba yake, Geb alikuwa
akimpiga picha na kumchuku video. “Dad!” Liv alimwita baba yake mara alipomuona.
Nanaa akaanza kucheka. “Basi hapo tena kazi ndio imeisha. Geb asingemsogelea au
asingeingia huku ndani kumpiga picha. Angebaki huko huko nje alipo Grace!
Ataacha kile kikapu pale pale chini ili abebwe.” Mama G akacheka. “Nimemsikia
akizungumza naye asubuhi. Akamwambia baba yake ameelewa. Na hivi hasahau,
subiri tuone.” Wakabaki wakimwangalia. Wasimamizi walishaingia wote.
Ilikuwa zamu ya Grace
kuingia. Liv ndiye aliyekuwa msimamizi wa mwisho kupita hapo akimwaga maua ili
apite bibi harusi na baba yake, ambaye atasimama Geb, badala ya Mzee Magesa,
kumkabidhisha kwa Man. Sasa Geb aliamua kwenda kumpiga picha na kumchukua video
mwanae, wakati akifanya hilo zoezi, ndipo arudi amshike mkono dada yake
amwingine ndani, ibada ianze. Liv alikuwa akimwaga maua kila sehemu ambayo anti
yake anatakiwa kupita. Alimwaga na kumpungia mkono dad wake, Geb naye
anampungia ndipo anamwaga tena. Alifanya hivyo mpaka akafika pale mbele, baba
yake akaondoka.
Kama aliyekumbuka kitu.
Akarudi nyuma kidogo, akaonekana anahesabu hatua mpaka mbele kabisa
madhabahuni, katikati. Akamwaga kulia na kushoto. Akasimama. Hapo baba yake
alishaondoka. Kabla ya ibada kuanza, Malisa na Geb waliingia hapo ndani
kumfanyia mazoezi. Wakajua amekumbuka. Wakampigia makofi. Akacheka. “Sasa pale
ndio mwisho wake mama. Muone.” Liv alimaliza kazi yake kwa wakati ule. Ila
pakusimama ndio ukawa mtihani kwake. Aliangalia upande aliotakiwa kusimama na
wasimamizi wa kike, hakuona sura anayoifahamu hata moja. Wakamwita. Akacheka tu
hata kusogea. Nanaa akajua tarayi.
Bado alikuwa amesimama katikati.
“Usimwangalie mama. Akituona tu, atakuita palepale mbele ukambembe. Inama.”
“Anatafuta sura ya mtu anayemfahamu.” “Nakumpenda yeye. Lasivyo bibi harusi
atamkuta palepale.” Nanaa akamaliza kwa kunong’ona. Man aliyekuwa amesimama
upande wa wanaume akamwita. “Liv!” Akamgeukia na kucheka. “Njoo!” Akamchekea
tena na kumsogelea Man. Fili alikuwa pembeni yake na wadogo zake, wametulia
sana kama sio wale watoto wa Danny. Alipowaona na wale watoto, akafurahia.
Kakaenda kusimama pembeni ya Man na kina Fili. Ni yeye peke yake msimamizi wa
upande wa kike aliyekuwepo upande wa kiume. Matron au msimamizi wa Grace
alikwenda kutaka kumchukua. Akamnong’oneza Liv kitu. Liv akamwangalia Man akiwa
ameshabadilika rangi. “Akimgusa tu, atalia. Na akilia yule, tutabeba mpaka
harusi iishe. Nimfuate?” Nanaa akataka kusimama. “Mwache kwanza.” Wakamuona Man
anamnong’oneza kitu yule shemeji yake ambaye ni msimamizi wa Grace. Wakacheka, na kuondoka pale kurudi alipokuwa amesimama.
Akamuacha Liv, uso umeshakuwa mwekundu. Cheko imeisha.
Watu wakasimama baada yakusikia wimbo ulioashiria
bibi harusi anaingia. Geb akiwa amemshika Grace mkono wakaanza kuingia
taratibu. Hakika walipendeza. Ile shela ndefu aliyoitaka Mzee Ole, alivaa
Grace. Ilikuwa imebebwa na watoto wanne nyuma. Walipofika katikati ya Kanisa,
wakaiachia. Ilisambaa vizuri, Grace akawa anaivuta kwa mwendo wa taratibu.
Ilikuwa ni shangwe ya namna yake. Mzee Ole alisikika akishangilia pia. “Hapo
amependa!” Malisa akanong’ona.
Liv alifurahi sana
kumuona baba yake. Akaweka kikapu cha maua chini. “Dad!” Geb akampungia mkono
kwa chini kidogo. Alicheka kwa sauti kisha akaweka vimikono vyake juu
akishangilia kama amepata mkombozi. “Pale ujue ndio kamaliza mama. Sidhani kama
ataendelea! Hawezi kusimama na wale watu asiowajua ndio maana alikwenda kwa
Man.” “We subiri.” Geb akamfikisha Grace mikononi kwa Man, akarudi alipokuwa
amekaa Nanaa na Mama yake.
“Dady!” Hapo Liv alikuwa
amenyanyua mikono juu, uso mwekundu tayari. “Pale amemaliza yule. Muone upande
aliokaa, na kikapu kaweka chini. Mikono yote juu anakuita. Nenda kamchukue
kabla hajaanza kulia pale mbele.” Nanaa akamnong’oneza Geb. Geb akasimama na
kumfuata pale mbele. Akainama kumnong’oneza kitu. Wakamuona Liv anambusu baba
yake shavuni. Akaokota kikapu na kuhama upande. “Ahaaa!” Nanaa akashangaa sana. “Jamani nyie Liv anakusudi huyu
mtoto!” Mama G alizidi kucheka. Geb
akarudi kukaa.
“Lazima uniambie ulichomwambia Liv akakuelewa
kwa haraka kiasi hicho! Hakika kama mimi ningemfuata pale, tungetumia zaidi ya
nusu saa kuelekezana na pia asingekubali kubaki pale.” Geb akacheka. “Ila
anakusudi Liv nyinyi! Anachagua nani wakumuelewa na nani asimuelewe.” Nanaa
akalalamika kidogo. “Liv hana tatizo la kuelewa hata kidogo.” Geb akaongea kwa
kusifia, Nanaa akabaki bado haamini. Alikuwa ametulia, upande wa wasimamizi wa kike na kikapu cha
maua kashika mkononi. Hakuweka chini tena. Kila wakati alimpungia baba yake mkono
mwanzo wa ibada mpaka mwisho. Wakati wakutoka alimwaga maua baada ya wasimamizi
wote kutoka. Yeye akawa wa mwisho kabla Man na Grace hawajatoka. Akamwaga huku
akimwangalia baba yake aliyekuwa mbele yake akimpiga picha na kumchukua video. Alikuwa akicheka sana huku akimwaga maua na
kumpungia baba yake mkoni. Na vile alivyopendeza, ungependa kumpiga picha. Kila mtu alikuwa akicheka na yeye alikuwa
akicheka zaidi lakini anamwaga maua.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kufika saa kumi jioni,
Grace akawa mke halali wa Man na si Danny tena. Zilichezwa ngoma za kimasai
hapo nje ya Kanisa, kama wapo Masaini. Japo kulikuwa na minong’ono mingi ya
kuwa inawezekanaje Grace kuolewa tena kanisani akiwa alikuwa na ndoa ya kwanza
ya kanisani? Ndoa za wakristo hazivunjiki! Walilalamika. Wengine walisema ni
sababu ya utajiri wa Mzee Ole, amehonga Kanisa. Wengine walisema aliachika
kihalali sababu ya kosa la uzinzi. Wengine walisema Kanisa hilo limefanya
upendeleo kwa Mzee Ole, sababu ya michango yake hapo kanisani, ingekuwa ni mtu
masikini au muumini tu wa kawaida, basi Kanisa lisingekubali kufunga ndoa ya
aina hiyo.
Basi ikawa ulalamishi wa
hapa na pale wa chini chini. Wengine wakijiuliza inawezekanaje kijana kama Man
kwenda kumuoa mama mwenye watoto watatu kama Grace wakati alikuwa na uwezo
wakuoa binti mdogo tena mzuri tu zaidi ya Grace!? Wakuendelea kusengenya
waliendelea, lakini Man alishapata mke. Waliocheza walicheza mpaka jasho
lilikuwa likiwamwagika. Grace ni wa Man! Nyimbo za kimasai ziliimbwa ndipo
wakaelekea kwenda kupiga picha.
Wakiwa kwenye kupiga
picha, Man na Grace walibadilisha nguo wakavaa za kimasai. Hakika walipendeza
na mavazi hayo ya asili. Walipiga picha nyingi sana. Na watoto wa Grace pia
walikuwepo kwenye kuweka kumbukumbu ya siku hiyo. Man alianzisha familia akiwa
amempokea Grace na watoto wake wote. Picha nyingi walipiga wakiwa wamebeba wale
watoto kama ni wa Man na Grace waliozaa pamoja.
Ukumbini!
Walipotoka hapo ndipo
wakaenda ukumbini. Hapo ndipo walikutana na Masai halisi. Wengi walivaa
kimasai. Wazee kwa vijana. Wanawake kwa wanaume. Hapakuwa na wavaa suti wengi.
Wengi walivaa kimasai. Ilikuwa ni hoteli kubwa kama ile anayosimamia Man kule
jijini Arusha. Lakini hiyo alikuwa akisimamia kaka yake.
Kulijazwa nyama kama
alivyosema mzee Ole. Nyama za kila namna zilikuwepo. Vyakula vingine vilikuwa
vichache, lakini nyama ndizo zilijaa. Grace alikuwa akitembezwa na Man hapo
ukumbini kusalimia watu mbali mbali. “Kweli Grace safari hii amebahatika!”
Nanaa alinong’ona. “Na ameingia kwenye ukoo mkubwa! Na wanaonekana wana umoja
sana.” Mama G akaongeza.
Nanaa akaanza kucheka.
“Unacheka nini?” Geb akauliza. “Muone
Magesa. Ameshiba mpaka anasinzia na nyama mkononi. Mtoto kwa kula huyo!” “Sijui
karithi wapi!?” Geb akauliza. “Mimi hata sijui!” Nanaa akajibu huku aking’ata
nyama. Geb na mama G wakacheka. “Utafikiri hujala mwaka!” Mama G akamchokoza
Nanaa. Alikuwa anakula kwa juhudi zote. James alikuwa akimwangalia dada yake na
yeye anacheka. “Mambo kama haya hayatokea kila mara. Acheni mimi nile jamani.
Meza imejaa nyama na wahudumu wanapita kila mara kubadilisha aina ya nyama!
Mungu anipe nini mimi Nanaa!?” “Basi mwangalie mwanao. Kashiba, lakini hataki
kuweka nyama chini.” Nanaa alikuwa akicheka huku wakimwangalia Magesa. Geb akajaribu
kutoa ile nyama mkononi, Magesa akapiga kelele akitaka nyama yake. Wakazidi
kucheka. “Mwacheni mwanangu. Kula baba. Kula ni karama ya Mungu. Hata mbinguni
tutakuta kuna kula.” Nanaa aliongea huku akiendelea kula zile nyama.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mzee Ole alipewa nafasi
ya kuzungumza. Akamshukuru sana Man kwa heshima aliyompa. “Nilikuwa nikiogopa
kufa kabla sijamuona Man akioa. Mama yake alinitia moyo akasema nizidi
kumuombea. Lakini siku zilizidi kwenda bila kuona matunda. Niliposikia yupo
Grace. Nikasema hiyo ndio Grace yangu mimi. Mungu amenirehemu kabla sijafa.
Nikamwambia mama yake, Mungu ametuletea Grace, ndio muujiza wangu. Maana huyu
Man, bwana! Hapakuwahi hata kutokea fununu ya mwanamke!” Watu wakaanza kucheka.
“Kila siku nauliza vipi
huko Arusha, hujapata mtu? Majibu hayaeleweki! Sasa niliposikia tu yupo Grace,
nikasema niletewe haraka sana. Nilipomuona tu, na mama Ole alipokaa na Grace
kwa muda mfupi tu, akasema huyu ndio mke wa Man.” Watu walianza kushangilia.
Vigelegele huku wakicheka.
“Tukakubaliana siku ya
leo. Mvua inyeshe, jua litoke, lazima Grace awe Ole.” Watu wakashangilia sana.
“Sikutaka habari ndefu. Nikaita wanangu. Wakagawana majukumu. Na nyinyi
mliponiambia mpo tayari kuja kuungana na mama yake Man, kumchukua Grace,
nikasema asante Yesu wangu. Nashukuruni sana kwa kuja. Sasa Grace!” Akamgeukia
Grace. “Karibu mama. Karibu kwenye ukoo huu mkubwa sana kama unavyotuona.
Nawaombea maisha marefu na uongozi wa Roho mtakatifu.” “Asante na amina baba.”
Grace aliitika taratibu. Vikainuka tena vigelegele.
“Sasa kwa niaba yangu na
mke wangu, zawadi yetu ni kukuongezea share kwenye ile hoteli.” Vigelegele
vikaongezeka. Wakashangilia sana.
“Katika hoteli hii hapa, kaka yako yeye ni asilimia 70, mimi 30. Sasa na
wewe kwa kuwa unaanza maisha na familia tayari, itakuwa hivyo hivyo na wewe.
Yangu ni 30 tu ili tuendelee kunywa maziwa hapa mjini. Na bado niweze
kumnunulia mama yako magauni.” Man akasimama, akaenda kupiga magoti mbele ya
baba yake. Akamuwekea kichwa pale magotini alipokuwa amekaa kama kushukuru.
Malisa akamsogelea Mzee
Ole akiwa na mumewe. “Na sisi. Kina Ole wadogo.” Malisa akimuonyeshea mumewe.
Watu wakacheka. “Tutagaramia mapumziko yote ya honeymoon.” Vigelegele tena.
Malisa alikuwa msomi sana na kazi yake ilikuwa ikimlipa vizuri. Kwa kumwangalia
tu yeye na mumewe ambaye naye alikuwa na kazi ya maana, ungejua ipo neema.
Ndipo wakaona uwe ni wakati wa zawadi tu. Kwa kuwa hakuna aliyekuwa
amechangishwa, watu walikuja na zawadi nyingi sana. Nyimbo zilipigwa, sherehe
ikakolea.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Daah! Hakika mimi bado
siamini mwenzenu!” “Nini kaka?” Nanaa akauliza. “Namuhurumia sana Danny. Nahisi
nipo ndotoni.” “Wala usimuhurumie. Ni vile ulikuwa hujamsikia alivyokuwa
akimsema vibaya Grace. Hakujua kama Grace atakuja kuolewa kwa haraka hivi.
Alijua vile alivyozaa watoto wa tatu ndio amekwisha. Akawa anajisifia eti yeye
anaoa msichana mdogo. Sasa nasikia ameshaanza kusoma namba za kichina. Sara
anamuendesha kama gari bovu.” Wote wakamgeukia Nanaa.
Akaanza kucheka. “Haya,
wewe umejuaje?” Mama G akamuuliza Nanaa. “Mimi ni rafiki wa Tere.” “Nanaa wewe
mtoto acha umbea wewe!” “Yeye mwenyewe ananipenda mama. Akiniona nimejilaza
sehemu, ananifuata.” Geb alikuwa akimwangalia na kutingisha kichwa. “Haya
kakwambia nini?” “Umeniambia niache umbea mama. Heri tu ninyamaze” “Nanaa
usinitanie!” Nanaa akazidi kucheka. Alimjua mama G. “Mimi mwenyewe nataka
kusimulia.” “Nanaa!” Geb akashangaa. “Kidogo tu mume wangu.” Geb akatingisha kichwa
na kugeukia pembeni.
“Haya anza.” Mama G
akamgeukia vizuri. “Basi nasikia kanunuliwa gari jipyaaa! Tere anasema akataka
na simu kama ile ya Grace mpaka rangi. Danny akamnunulia. Akaiba kadi ya benki
ya Danny akaenda kuchukua pesa kwenye ATM, akaenda kubadilisha matairi.” “Kwenye
hilo gari jipya!?” Mama G akashangaa. “Kumbe! Pesa si ipo bwana? Ana shida
gani?” “Atamfilisi Danny mpaka amchanganye akili. Sara hatosheki na pesa.”
“Subiri sasa mama. Unaambiwa shopping ya nguo na viatu ndio kila siku. Anavaa
nywele za milioni. Kucha ndio za malaki. Na akirudi anazungumza na simu zake
anajingamba hapo mbele ya Tere kuwa amehamia saluni za watu wazima.” “Anafanya
makusudi kwa kuwa anajua Tere anampenda Grace. Kwa hiyo anajua ujumbe utafika
tu.” “Sasa huo ugomvi wao!” Nanaa
akaendelea.
“Unaambiwa mpaka watoto
wa Grace wanakimbia. Tere anasema wakianza kugombana hapo! Huwezi kukaa. Watoto
wanalia wanaenda kujifungia chumbani, wanaogopa.” “Na wamekutana. Danny
anahasira, na Sara hawezi kunyamaza. Ndio maana wale watoto wamekuwa kama
wanahofu! Hawaongei, wakimyaa!” Mara Grace na Man wakaja kwenye meza yao.
Wote wakasimama kasoro
Nanaa. “Niambie bibi harusi wangu.” Grace alimchokoza Nanaa. “Anakazi ya kula
tu hapo. Kama huyo mwanae. Hata kusimama hawezi.” Wakacheka. Man akamnyanyua
Magesa kutoka pale alipokuwa amekaa kwenye kigari chake, anasinzia.“Naona kaka
ananyama mkononi.” “Ukitaka aamke hapo, mpokonye.” Wakacheka huku wakimwangalia Magesa.
Anasinzia na nyama yake mkononi.
“Hongereni sana.” Geb
akatoa mkono. James alibaki akimtizama Grace. Grace akacheka. “Nimefurahi
umekuja James. Inayofuata ni harusi yako.” “Mniombee. Na mimi nimetamani. Ila
sitaki aina ya kina Sara.” Wakacheka. “Nitakutafutia kaka yangu.” “Yamekupata
Nanaa! Amesema tuombe.” “Na kumsaidia mama.” Geb alikuwa akimwangalia. “Si eti Geb?”
Nanaa akauliza kwa mumewe ili kupata utetezi. “Mimi naona tukazane kuomba.”
Wote wakacheka. “Geb naye! Hongereni mwaya. Mmependeza sana. Grace wifi yangu
pongezi.” “Asante. Hapa nina raha zote.” “Mmmh!”
“Sasa mama wewe unaguna nini?” Man akacheka. “Twende zetu mwaya mume wangu.”
Nanaa akafurahi sana. “Graceee! Sema tena umrushe roho mama!” “Mume wangu Man. Kwa raha zote!” “Hata mimi
nakuona.” Mama G akajibu nakurudi kukaa. Kila mtu alikuwa akicheka. Man
alimrudisha Magesa kwenye kiti chake. Akambusu, wakaondoka kuelekea meza
nyingine kusalimia.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Wakati wakufungua mziki,
alikaribishwa Man na mkewe kwanza. Kama kawaida yake Man alitafuta zilipendwa
za enzi hizooo. Wimbo wa mwana dada wa kimarekani, Brandy, ‘Have you ever!’ Kama kawaida yake Man alitaka apewe kipaza
sauti. Malisa akasikika akitangaza. “Huu ni wimbo aliouchagua Man mwenyewe.
Lakini anatuuliza sisi wote hapa. Ni maalumu kwa Grace, tusikilize maneno kwa
makini pengine wengine wetu hapa tutapata majibu ya maswali yetu ya ‘kwa nini Grace na si mwingine!?’. Man alishaniuliza hayo maswali, akiwa
ametulia kabisa. Binafsi niliguswa. Naomba msikilize na nyinyi. Ila kwa kifupi
Man anauliza, ‘Ulishawahi
kumpenda mtu mpaka ukajikuta unalia! Anaendelea kuuliza zaidi, Ulishawahi kumuhitaji mtu maishani mpaka
ukashindwa kulala usiku?’ Karibuni mumsikilize Man mwenyewe.” Malisa
aliongea na yeye kwa hisia sana na kuvutia watu kusikiliza.
Wimbo ukaanza. Kwa
hakika Man alijaliwa sauti. Ungependa Brandy atulie kidogo, Man asikike.
Aliimba mpaka akamtoa machozi Grace. Walicheza blues vizuri sana. Ungependa
kuwaangalia wanandoa hao. Ukumbi mzima ulikuwa kimya, wakiwatizama wao tu na
kumsikiliza Man akiimba kwa hisia mbele ya Grace. Kuna wakati mwingine
alimkumbatia kwa mkono mmoja, kwa kuwa mwingine ulishika kipaza sauti, wakati
mwingine alimwachia na kumzungusha huku akiuliza,
Have
you ever loved somebody so much It makes you cry,
Have
you ever needed something so bad
You
can't sleep at night
Have
you ever tried to find the words
But
they don't come out right
Have
you ever, have you ever
Have
you ever been in love
Been
in love so bad
You'd
do anything to make them understand
Have
you ever had someone steal your heart away
You'd
give anything to make them feel the same
Have
you ever searched for words to get you in their heart
But
you don't know what to say
And
you don't know where to start
Have
you ever loved somebody so much It makes you cry
Have
you ever needed something so bad
You
can't sleep at night
Have
you ever tried to find the words
But
they don't come out right
Have
you ever, have you ever
Have
you ever found the one You've…
Have
you ever found the one
You've
dreamed of all of your life
Just
about anything to look into their eyes
Have
you finally found the one you've given your heart to
Only
to find that one won't give their heart to you
Have
you ever closed your eyes and
Dreamed
that they were there
And
all you can do is wait for the day when they will care
Have
you ever loved somebody so much It makes you cry
Have
you ever needed something so bad
You
can't sleep at night
Have
you ever tried to find the words But they don't come out right
Have
you ever, have you ever
What
do I gotta do to get you in my arms baby
What
do I gotta say to get your heart
To
make you understand how I need you next to me
Gotta
get you in my world
Cause
baby I can't sleep
Have
you ever loved somebody so much
Man alicheza kwa hisia huku akitengeneza
mlio mzuri kwa vidole vyake uliondana na bits za huo mziki. Alicheza Man
akiuliza ulishawahi kupenda na kusubiria kitu uje
kukimiliki? Alicheza mpaka wimbo ulipoisha.
Akaomba kuongea kidogo
wakati akimfuta Grace machozi huku amemkumbatia. “Watu husema, ‘Love comes once in a life time’ Ndicho
kilichonipata kwa Grace. Mungu aliponikutanisha naye kwa mara ya kwanza,
nikavutiwa sana mpaka nikajishitukia. Nikajaribu kujisogeza, lakini kitu cha
kwanza alichoniambia, ‘mimi sio
msichana, ni mama wa watoto watatu’. Wale pale ndio watoto
wenyewe. Wana macho mazuri kama ya mke wangu.” Watu wakapiga vigelegele.
“Lengo la Grace
lakuniambia hivyo ni kunisukumia mbali. But guess what? Nilishindwa hata
kulala. Kwa mara ya kwanza, Man mwenye maneno mengi niliishiwa maneno sahihi
yakujieleza kwa Grace ili anielewe. Nilihangaika kutafuta maneno yakuzungumza
naye bila mafanikio. Lakini kama mnavyomjua mke wangu, ni mkimya sana.
Ukifanikiwa kuwa naye karibu utajua nini naongelea. Upo utulivu ambao sikuwahi
kuupata maishani, mpaka nilipofanikiwa kuwa karibu naye. Hapo nikathibitisha
kuwa ni wangu. Swali ni jinsi gani nitammiliki moja kwa moja ndio ikawa
changamoto. Vikwazo vikawa vigumu. Lakini Mungu akatuvusha. And thanks to my
precious sis, Malisa…” Malisa akasimama. “That’s me people. ‘The precious sis’,
ndio mimi.” Watu walicheka sana. Maana Malisa alisimama kama mshale
nakujitambulisha.
“Yeap, that’s her.” Man
akathibitisha kwa kumnyooshea kidole dada yake. “Yeye ndio aliharakisha mambo.
Kwa mara ya kwanza anamuona Grace, akampenda sana. Akaanza kufanya juhudi za
makusudi awe wangu. Namshukuru Mungu na mama yangu akampenda sana Grace.
Nakumbuka siku Mzee Ole alipotaka kumuona Grace, akataka nimpeleke nyumbani,
moyoni nilikuwa na wasiwasi na mama. Mzee Ole huwa mnamjua jamani. Kila
mwanadamu kwake ni mzuri tu.” Watu wakacheka na kushangilia. Wakaimba wimbo wa “baba, baba, babaaaa…”
“Ila mama mpaka
azungumze, ujue hicho kitu kimemgusa sana. Hana neno na mtu. Kimyaa.” Wakaimba
tena “Mama
mama mamaaa..”
Mpaka Man akaanza kucheka. “Grace alipofika
nyumbani, akapata muda na mama. Sikujua hata walizungumza nini! Mimi nilikuwa
na Mzee Ole tunazungumzia mambo ya biashara. Tulipoondoka, akanipigia simu siku
inayofuata. Akaniambia kama nataka pumziko hapa duniani, basi nihakikishe Grace
anakuwa mke wangu.” Vilisikika vigelegele, watu walishangilia sana.
“Mama yangu ananijua
kuliko nitakavyoeleza hapa. Yale mabaya yote ambayo ninaficha kwa watu, yapo
moyoni mwa mama yangu. Kwa yeye kusema Grace ndiye, nikajua ni jibu langu
kutoka kwa Mungu. Kama kawaida ya Mzee Ole, huwa hajui kusubiri, akasema leo
lazima Grace awe wangu kihalali. Nawashukuruni woote kwa kuacha shuguli zenu
zooote, kuungana na Mzee Ole, kuhakikisha leo tunamfanya kuwa Ole, kama
alivyosema mwenyewe Mzee wa Ukoo.” Watu wakashangilia sana.
“Sasa naomba msituchoke.
Leo ni siku yetu mimi na Grace. Naomba wimbo mwingine wakucheza na mke wangu.
Anaupenda sana huo wimbo. Kuna siku aliniomba niusikilize wote vizuri. Anajua
huwa napenda zilipendwa. Najua leo ukipigwa atakamilisha siku yake vizuri.”
Grace akacheka kama aliyekumbuka.
“Huo kweli ni mzuri Man.
Uwe kwa ajili yako.” Grace aliongea kwa upole. Man akambusu. “Najua hamjamsikia
Grace wangu. Lakini amesema uwe kwa ajili yangu.” Watu wakacheka. “Si ni siku
yetu jamani! Hata tukitaka kucheza nyimbo tatu si ruksa?” “Ruksa kaka.” Malisa
akajibu na vigelegele juu. Watu wakampokea vigelegele. Na yeye alivaa kimasai.
Alipendeza sana Malisa.
“Basi naomba mtuwekee ‘Brown eyes wa Destiny’s Child’. Najua
Malisa alishaziandaa.” “Zipo kaka yangu. Dj fanya vitu vyako, tumsikie na Grace
na yeye anamwambiaje Man!” Wote wakacheka mpaka Grace mwenyewe. Malisa alikuwa
mtundu wa bila kujizuia. Man alikuwa akicheka.
“Thanks Mal.” Man akamshukuru, Malisa akamkonyeza kaka yake. Alikuwa amekaa
meza ya mbele kabisa na mumewe pamoja na wazazi wao.
Remember
the first day when I saw your face
Remember
the first day when you smiled at me
You
stepped to me and then you said to me
I
was the woman you dreamed about
Remember
the first day when you called my house
Remember
the first day when you took me out
We
had butterflies although we tried to hide it
And
we both had a beautiful night
The
way we held each others hand
The
way we talked the way we laughed
It
felt so good to find true love
I
knew right then and there you were the one
I
know that he loves me 'cause he told me so
I
know that he loves me 'cause his feelings show
When
he stares at me you see he cares for me
You
see how he is so deep in love
I
know that he loves me 'cause it's obvious
I
know that he loves me 'cause it's me he trusts
And
he's missing me if he's not kissing me
And
when he looks at me his brown eyes tell his soul
Remember
the first day, the first day we kissed
Remember
the first day we had an argument
We
apologized and then we compromised And we haven't argued since
Remember
the first day we stopped playing games
Remember
the first day you fell in love with me
It
felt so good for you to say those words
'Cause
I felt the same way too
The
way we held each others hand
The
way we talked the way we laughed
It
felt so good to fall in love
And
I knew right then and there you were the one
I
know that he loves me 'cause he told me so
I
know that he loves me 'cause his feelings show
When
he stares at me you see he cares for me
You
see how he is so deep in love
I
know that he loves me 'cause it's obvious
I
know that he loves me 'cause it's me he trusts
And
he's missing me if he's not kissing me
And
when he looks at me his brown eyes tell his soul
I'm
so happy so happy that you're in my life
And
baby now that you're a part of me
You
showed me
Showed
me the true meaning of love
And
I know he loves me
I
know that he loves me 'cause he told me so
I
know that he loves me 'cause his feelings show
When
he stares at me you see he cares for me
You
see how he is so deep in love
I
know that he loves me 'cause it's obvious
I
know that he loves me 'cause it's me he trusts
And
he's missing me if he's not kissing me
And
when he looks at me his brown eyes tell his soul
He
looks at me and his brown eyes tell his soul
Man alikuwa amemkumbatia kwa karibu
sana, wanacheza. Mara kadhaa walimuona Man akimnong’oneza kitu masikioni na
Grace anacheka sana. Jinsi alivyomshika na kumwangalia, ungejua tu Grace yupo
kwenye mikono salama. Alikuwa akicheka wakati wote na Man alionekana kumfurahia
mikononi mwake. Alionyesha ni kama aliokota lulu. Walicheza vizuri sana. Zaidi
ile furaha kwa Grace, ungejua kuwa wawili hao walikusudiwa tu.
Baada ya hapo ikawa Man
na mama yake. Na wenyewe walicheza wimbo wa ‘nani kama mama’. Akaja
Grace na mama yake. Wakacheza huo huo, ulipofika nusu, Nanaa na Geb nao
wakaunga msafara. Man naye akaenda. Mziki ukaendelea. Wakacheza kama
walivyocheza jijini Arusha. Wakimtunza mama G. Wajukuu wote walikuwa wamelala.
Wakacheza tena mpaka mwisho. Wakawa hawajaridhika. Malisa akamuomba DJ arudie,
na yeye akaunga msafara. Wakacheza hapo mpaka mama Ole naye akasimama.
Ukarudiwa tena. Wadogo zake wengine Man wakasimama. Wakacheza mpaka wakaridhika
ndipo wakaruhusiwa wengine kuingia kucheza.
Jumapili, Kwa Danny
Siku ya
jumapili asubuhi ambayo ilikuwa ni safari ya Danny, Sara pamoja na watoto,
ilikuwa ni kama moto unawaka huko kwa Danny na Sara. Danny aliamka akiwa haoni
kadi yake ya benki. Sara anaapa hajachukua. Wapo wanaishi kwenye apartment hiyo
wao wawili tu. Nani kachukua? Ndio swali lililozua ugomvi. Danny hakuwa
amepoteza wallet, na wala hakuwahi kuisahau popote. Inamaana mtu aliyemwibia ni
wakaribu naye sana, ambaye anauwezo wakuichomoa alipovua suruali. Ni nani kama
sio Sara? Sara naye anasema anatafuta sababu yakummalizia tu hasira zake kwa
kuwa amejua Grace ameolewa, anaona wivu.
Angalau hapo Sara
akafanikiwa kubadilisha mazungumzo. Kutoka kwenye kadi ya benki, mpaka kwa
Grace. Ugomvi ukawa ni Danny anamtumia wakati mapenzi yako kwa Grace.
Alimdanganya ili amvue tu nguo. Danny akamuuliza kwa nini atumie uongo kulala
naye wakati ni yeye mwenyewe Sara alijileta kwake!? Hapo napo yakatokea matusi
ya haja. Kila mmoja anampaka matope mwenzie. Sara akamkumbusha matusi yote
aliyomtukana Grace, akimsifia yeye. Mwishoe Danny akajitetea hana hisia zozote
kwa Grace, alishamtaliki hana shida naye, Sara anamwambia ni muongo. Kwa nini
akose raha gafla baada yakujua Grace anaolewa?
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Danny mwenyewe ndiye
aliyerudi nyumbani siku alipozungumza na Grace akiwa kama mgonjwa. Sara
alipomuuliza kulikoni, akajikuta anaropoka, “Grace anaolewa.” Sara akashangaa
sana. “Kwa hiyo ndio unaumia roho!?”
“Kwa nini niumie roho? Ninachomaanisha ni kuwa, Grace anaolewa siku ya
jumamosi, anataka watoto wahudhurie harusi yake. Inamaana ametuvurugia sisi
mipango yetu. Ilitakiwa tuondoke jumamosi, sasa itabidi tusafiri jumapili.”
“Kama sio uongo ni nini!? Kuna ubaya gani wakuondoka jumapili na si jumamosi?
Kwani tulikuwa tunawahi wapi? Usinifanye mimi mjinga Danny!” “Mimi nakwenda na
mipango Sara.” Danny alijitetea.
“Mipango gani ya kipuuzi
hiyo!? Kutumia mahela yote hayo eti kwa ajili ya kwenda Tabora kwa wazazi wa
Zinda ndio mipango ya maana hiyo kama sio upuuzi mtupu!?” “Unanitukana mimi!?”
Danny kahamaki zaidi. Haamini Sara anayemuweka mjini na kumgaramia pesa zote
hizo kama anadiriki kumwita yeye mpuuzi!
“Sijakutukana nakwambia
ukweli. Kwanza wanakutumia tu. Wale sio ndugu zako na wala hawatakaa wawe ndugu
zako. Mtoto wa kiume unajipendekeza kwa mwanaume mwenzio, ili iweje kama sio
upuuzi huo?” “Sara angalia maneno yako wewe?” “Utanifanyaje? Unataka
kunimalizia hasira za kuolewa kwa Grace? Wewe ulifikiria hataolewa? Ukisema cha
nini wenzio wanalia watakipata lini. Hata mimi ukiniacha leo, ujue kesho nipo
kanisani na shela nyeupe!” Danny akaamua atoke pale kwa haraka kabla hajamchapa
makofi. Hiyo siku ikaisha kwa kuwa Danny aliondoka pale
~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Sasa na leo Sara akaona
ni wakati mwafaka wakumgeuzia kibao kumchanganya zaidi ili asikumbuke maswala
ya kadi aliyokuwa ameificha. Alishakusudia amwibie pesa ya maana. “Najua sana
kuwa unanitafutia sababu. Unatafuta kunimalizia mimi mahasira yako kwa kuwa Grace ameolewa na mwanaume mwingine
tena baada ya wewe kumchafua! Umeamka asubuhi hii ukakumbuka mwanaume mwingine
anamfaidi sasa hivi Grace huko hotelini. Ndio unajidai mimi mwizi. Sasa ujue
Grace kaolewa, na hatakaa arudi. Jamaa kaanza jana usiku kula mzigo kihalali.
Pasuka sasa!” Sara akambadilikia kweli kweli.
“Kinachokufanya uhangaike
na maswala yangu mimi na Grace ni nini Sara? Yanakuhusu nini?” “Ahaaa! Unaona
unavyojifunga mwenyewe? Kwa hiyo ulitaka kumrudia? Inamaana mimi nikipoozea kiu
chako, kumbe mawazo yapo kwa Grace?” “Acha kelele Sara. Mambo yangu na Grace
hayakuhusu hata kidogo.” “Maadamu nipo hapa na wewe kama mwanamke wako, basi
jua yananihusu na sitanyamaza. Usinichezee mimi akili.” Sara alikuwa anawaka
kwelikweli.
“Wewe mwenyewe ndio ulimuacha Grace. Sikukushauri wala
kukuingilia. Kwa akili zako mwenyewe ulisema umelogwa, unajitoa kwa kina
Magesa. Ukasema humtaki Grace kwanza hajui mapenzi, maji matupu! Sasa
kinachokutoa povu sasa hivi ni kipi? Mwenzio kaonjeshwa mara moja tu, katangaza
ndoa. Wewe unajidai kununa! Kama mambo huyawezi, ungesema tu. Sio kila mwanaume
kaumbiwa shuguli nzito.” Nusura Danny asimame ampige lakini na hapo akatoka.
Ndipo akaenda sasa
kumpigia simu Tere, kutaka watoto wake haraka sana. Asichelewe. Akamuwashia
moto Tere, ikabidi Tere kuanza kuandaa watoto wa Grace kwa haraka. Mama G
alihakikisha wameshiba. Geb alitoka akacheza nao kidogo mpaka Jeri alipokuja. Hao
watoto hawakuwa wakitaka kuondoka pale. Nyumba zima iliamka kwa kilio chao.
Mama yao hakuwepo hapo. Walitokea ukumbini kwenda kwenye fungate. Man
aliwaambia ijumaa baada ya kuchukua watoto, watakuwepo hapo kwa chakula cha
jioni. Kwa hiyo akabaki Geb, mama G na Nanaa kuwatuliza hao watoto. Geb
alizungumza nao akawaambia baba yao anataka kusafiri nao. Wakirudi, mama yao atawachukua
na kuwaleta tena hapo.
Walikuwa wakilia mpaka
Nanaa naye akaanza kulia. Ilibidi kupandishwa kwenye gari hivyo hivyo ili
wasimchelewe baba yao ambaye alishaanza kumpigia tena simu Tere akiwa anafoka
sana. Kuwa yupo getini nyumbani kwa Grace, mlinzi amemwambia watoto
hawajarudishwa. Hao watoto waliondolewa pale wakiwa wanalia sana. Fili
alimng’ang’ania shati Geb, hakutaka kumuachia. Waliacha ile nyumba imepooza
kila mtu akiwahurumia.
Msiba Mzito.
Ilikuwa yapata saa kumi
jioni wakati James anaingia akionekana amechanganyikiwa. “Kwa nini hampokei
simu jamani!” James aliingia akabaki amesimama mlangoni, bila salamu ila
lawama. Alikuta wamekaa tu hapo sebuleni. “Tumechoka baba. Tumelala siku nzima
sababu ya uchovu wa harusi ya jana. Sijui kata simu yangu yenyewe iko wapi!”
Mama G akakaa. “Pole kaka. Mimi simu yangu nimeacha chumbani, nafikiri imezimwa!”
“Na mimi yangu nilizima na kuiacha makusudi huko chumbani ili nipumzike leo.
Kwema?” Geb akauliza akimtizama. “Sio kwema kabisa.” James akawasogelea mpaka
pale walipokuwepo kwenye makochi, akakaa.
“Mbona unatetemeka kaka? Kuna nini?” James alibadilika rangi akawa mwekundu sana. Hata Nanaa aliyekuwa amelala, akakaa. “James!” Geb akamuita. “Sijui nianzie wapi aisee!? Ndio maana nilitaka Geb aje, asikilize na kujionea mwenyewe. Mungu nipe nguvu.” Geb akasimama. “Ni Grace?” Geb akauliza kwa kwa wasiwasi sana.
~~~~~~~~~~~~~~~~~
Shetani huwa hana usingizi wala
hajawahi kuchukua LIKIZO.
Wakati mapacha hao wameshampamba mama
yao vilivyo mbele ya umati wa watu, Geb kampata Nanaa wake & Grace kaolewa
baada ya talaka ya aibu.
Ni jana yake tu walikuwa ukumbini wote
na wajukuu wote,
wakicheza kwa furaha nakumtukuza
Mungu, leo James
naye anakuja na taarifa za kustua!
Nini kimetokea tena katikati ya Amani hiyo!?
ENDELEA KUFUATILIA.
0 Comments:
Post a Comment