Geb
alimtizama Nanaa mara kadhaa. Bado alionekana mwingi wa mawazo. Ni kama hakujua
wapi alipo na wala hakujali tena aendako. Ni kama alipoteza ladha ya kila kitu.
Kila alipomuuliza swali, alitoa tabasamu ambalo Geb mwenyewe alijua
anadanganywa tu. Ni mke ambaye anatarajia kumuoa masaa machache yajayo kama
anavyohesabu Geb mwenyewe. Wakati wengine wamehamasika, muolewaji mwenyewe ni
kama yupo tu anafanya bora liende. Uso ulishaonyesha kulemewa.
Geb akakumbuka maneno mengine ya
Man. “Unasimama mbele ya mchungaji
anayefungisha ndoa, unahisi ni kama upo mahakamani unahukumiwa kifungo cha
maisha!” Akamtizama tena Nanaa aliyekuwa akisugua tumbo lake taratibu kama
anayembembeleza Jimmy huko tumboni. Tayari walisha wasili kwenye viwanja vya
ndege vya Mwalimu J. Nyerere wakisubiria muda ufike waingie ndani, waanze
safari.
“Vipi?” Geb akamsogelea huku
akichungulia wanae kwenye kile kigari. “Safi tu. Hapa natamani kitanda tu,
nilale kama Magesa.” Akajibu na tabasamu huku na yeye akimwangalia Magesa
aliyekuwa amelala, hana habari na alipo. Nanaa amebadilika gafla. Ni jana yake
tu alikuwa amejawa furaha tele na maneno mengi kwa Man. “Naona kila Jimmy
anavyozidi kukua ndivyo na mimi nalemewa. Usingizi hauishi!” Nanaa akaendelea
kujitetea kwa ukimya ulioanza gafla. Hakika alishindwa kujizuia. Moyoni
alishajiona yeye ni wa pembeni. Kazi yake ni kuzaa tu kwenye hiyo familia.
Wenye pesa zao wapo wao kama wao,
na wana jinsi yao ya kuzungumza. Na yeye alishakumbuka mifano ya siku iliyopita
aliyotoa Man, akimlenga Danny. “Hata
mimi ni wale wale tu. Sina tofauti na Danny. Tuliozaliwa kusiko pesa wala mali.
Tunahadaika na vipesa vichache. Ndio akili za matajiri wanavyotuona! Ndio maana
hata Geb ananipa na kunionyesha kile anachoona ninastahili tu! Hawezi kufunguka
kwangu zaidi.” Nanaa akawaza nakuzidi kujiona hana chakuzungumza katikati
yao. Ndio maana aliondoka kwenda kukaa pembeni na wanae.
Liv naye ni kama alikuwa akimjua
mama yake. Akiomuona ametulia, na yeye anatulia kimya. Alikuwa amekaa pembeni
ya kaka yake kwenye hicho kigari chao. Magesa amelala, yeye akimwangalia mama
yake muda wote. Geb alijaribu kumchekesha Liv, akapata cheko ambalo hata na
hilo Geb alijua anadanganywa tu. Hakumchangamkia sana wala hakutaka ambebe.
Alibaki ametulia kimya kwenye kiti chake macho kwa mama yake. “Naona na yeye
anasinzia.” Nanaa akajaribu kumtetea mwanae.
Geb akajua mambo yameshaharibika.
Hakutaka kuachana na familia yake kwa namna ile. “Naomba tuzungumze kidogo.”
Nanaa akamtizama kama asiyeelewa. “Nanaa?” “Sijaelewa unamaanisha nini!”
“Nataka tukazungumze pembeni kidogo.” Nanaa akamwangalia Liv. “Hatutakwenda
mbali. Atakuwa akikuona tu.” Nanaa akasimama kama anayesumbuliwa, akamfuata.
“Umekumbuka kubeba dawa?” Geb akauliza. “Nimebeba.” “Nakupenda Nanaa.” Nanaa
akatabasamu. “Najua Geb!” “Naomba nivumilie pale ninapopelea. Najifunza
taratibu. Tafadhali nipe muda. Naamini ipo siku tutajikuta tupo ukurasa mmoja
na tutaongea lugha moja. Lakini kwa sasa najisahau. Wakati mwingine najikuta
nafanya mambo nikijifikiria bado nipo kama zamani. Nipo peke yangu.
Najiamulia tu.” “Hamna neno Geb. Mimi naelewa.” Nanaa akajikuta
machozi yapo kidevuni.
“Hapana Nanaa. Sitakiwi kufanya
hivyo. Naomba nisamehe. Nimefanya maamuzi makubwa sana bila kukushirikisha.
Nisamehe. Baada ya harusi yetu, nakuahidi tutapata muda wakuzungumza zaidi.
Utanifahamu kwa undani na tutaanza maisha tukiwa na mipango ya pamoja.
Hatutaishi kama mtu na hawara yake. Nakuahidi mpenzi. Nitabadilika.” Nanaa
akajifuta machozi na kutingisha kichwa akikubali. “Njoo.” Akamvuta karibu.
“Nakupenda sana Nanaa. Nimefurahi tutafunga ndoa. Jamii itakutambua kama wangu
kihalali. Na ndivyo utakavyokuwa.” Nanaa akacheka. Geb akamfuta machozi.
“Sasa usiku itakuaje? Nitakuwa
mpweke!” Nanaa akacheka tena. “Lala ukijua usiku wa jumamosi utakuwa mikononi
mwangu.” Geb alifurahi sana. “Daah! Nimefurahi sana kusikia hivyo. Usisahau
utakuwa usiku wetu wa kwanza baada ya miezi karibia nane sasa ya ukame.” Nanaa
akacheka.
“Nitafanya mapenzi na wewe mpaka
niridhike.” Nanaa alizidi kucheka. “Nitakubusu kila mahali. Nitapata muda na
matiti ambayo Liv alinipokonya kwa muda mrefu sana.” Nanaa alicheka kwa sauti
mpaka watu wakawageukia. Akampiga ngumi Geb. “Unahitaji msaada Geb. Akili gani
hizo!?” Liv alipomuona mama yake anacheka, akamwita. “Mama!” Ikabidi warudi
pale walipokuwa wamewaacha watoto.
“Nampenda mama!” Liv aliongea na
cheko, kidole chake kimoja tayari mdomoni, dimpozi zote zimeingia ndani. Mpaka
Nanaa mwenyewe akashangaa. Liv yule aliyekuwa anasinzia kama mama yake sie huyu
wa sasa. Geb akajua kazi atakuwa nayo. Akamuomba ambebe ili amuage. Liv
akakubali. “Nampenda dad.” “Na mimi nampenda Liv.” Akacheka sana mpaka kina
Grace wakawasogelea. “Liv anapenda kupendwa! Muone anavyoyachekelea hayo mabusu
ya baba yake!” Geb alishamtoa kifuani kwake, akawa anaendelea kubusu kauso
kake.
Kwa Danny na
Sara.
Sara alitoka pale ni
kama amechanganyikiwa. “Afadhali Mungu amejibu maombi yangu. Maana nilikuwa
nina shida sana na usafiri.” Akaendelea. “Halafu unajua nini Danny? Kuna
apartment zipo maeneo ya Ocean Road. Karibu kabisa na bahari, tunaweza kuhamia
hapo kwa muda wakati tunatafuta eneo la kujenga nyumba yetu.” Kimya. Sara
akaona aendelee na mipango. Pesa si ipo! “Halafu kingine, tunaweza kwenda
kwenye ile yard ya pale Msasani, wanakuwa na magari mazuri sana. Hamna haja
yakuagiza magari sijui Japan, sijui wapi! Leo leo naweza kupata gari yangu.”
“Mbona wewe unafikiria tu kutumia sio kujenga!?” Danny akamgeukia.
“Mbona wewe unagari, kwa nini na
mimi nisiwe na gari!?” “Si tutumie hili?” Danny akamuuliza. “Na ukiwa unaenda
kazini? Mimi nitatumia usafiri gani!?” Sara akauliza kwa mshangao. “Kwenda wapi
wakati huna kazi?” “We Danny vipi!? Yaani pesa ndio umeipata leo tu, halafu unaanza
ubahili!? Mimi mpenzi wako, hutaki niwe na usafiri wangu!? Kwa hiyo unataka
hata nikitaka kwenda saluni nikusubiri unipeleke!? Kwa nini!?Mbona Grace
alikuwa na gari yake tena gari ya garama kuliko yako!?” “Usiwahi hata
kujilinganisha na Grace.” Lile neno lilimshangaza sana Sara. Ni Danny huyu huyu
aliyekuwa akimtukana Grace. Iweje leo!
“Wewe ndio wakuniambia leo nisijilinganishe
na Grace!?” Sara akahamaki. “Ulinisifia na kuniambia nipo bora na nimempita
mbali sana Grace kwa mambo ya kitandani na muonekano wangu hata wa …” “Acha
kelele zisizo na maana. Ninachokwambia sasa hivi hapa ni kwamba, katika mambo
ya maendeleo na mipango usijilinganishe na Grace. Grace alikuwa mwajiriwa na
analipwa pesa nyingi sa..” “Kwa hiyo mimi sina mipango? Unaniona mimi mpumbavu
sio kama yeye!? Mbona ulisema..” Wakaendelea kubishana.
Walibishana mpaka walipofika
benki, ili kuweka zile pesa. Sara hataki
Danny aweke pesa yote, Danny anataka pesa yote iwekwe kwanza benki ndipo warudi
nyumbani wafanye mipango wakiwa wametulia. Walibishana mbele ya yule meneja wa
tawi, asijue awasaidie vipi. Mwishowe Danny akamkabidhi yule meneja wa tawi ile
pesa yote huku Sara akiendelea kulalamika kuwa Danny ni mbahili, hamfikirii
yeye. Anamtumia tu, wala hamjali. Kubishana kukazidi mpaka yule meneja wa benki
aliporudi pale ofisini kwake alipokuwa amewaacha wakibishana, akawaambia
amekamilisha kuweka hiyo pesa kwenye akaunti husika. Ambayo ilikuwa ni ya
Danny. Akawakabidhi slip katikati ya malumbano yao, akabaki amesimama kama
anayewaomba watoke ofisini kwake. Walisimama na kutoka bila hata kushukuru.
“Kwanza nataka pesa za shopping
kabla hatujasafiri.” “Wewe si nilikupa pesa juzi tu! Tena ukasema hivyo hivyo
za shopping kabla hatujasafiri! Unanunua nini hicho kisichoisha!? Kwanza ujue
tunakwenda Tabora. Ni kama ukweni. Kwahiyo huhitaji vitu vingi zaidi ya zawadi
zao tu wao. Nilikwambia beba magauni hata matatu tu. Hatutakaa muda mrefu. Siku
mbili tu.” “Hapana Danny. Nimefikiria nimeona siwezi kubadilika kwa sababu yao.
Kama wewe tunayeishi wote umenikubali hivi nilivyo, inabidi na wao wanipokee
vile nilivyo. Kwanza sio wazazi wako, zawadi nyingi za nini!?” Nalo hilo likawa
lakubishania.
Hakuwa kama Grace aliyekuwa
akijaza gari zawadi pindi Danny anapotaka kwenda kwa kina Zinda, huko Tabora.
Aliwaheshimu wazazi wa Zinda kama wakwe. Malumbano yakaendelea. Danny mwenye
hasira na maneno mengi, na Sara asiyekubali kushindwa na mtapanyaji.
Harusi ya Geb & Nanaa.
Ilikuwa siku ya jumamosi majira ya
saa 2:30 asubuhi wakati wapambaji
walipoingia kwenye chumba alichokuwa amelala Nanaa, mama G na watoto.
Alishaoga na kupata kifungua kinywa. Harusi ilikuwa saa tano asubuhi. Alishazungumza
na James, akamwambia yupo njiani anakaribia hapo. Jeri ndiye aliyekwenda
kumpokea Fifi. Kwani yeye Jeri alishatua jijini Arusha siku ya ijumaa na mizigo
akiwa anaendesha gari kubwa maalumu ya watoto hao wa Geb. Fifi alikuwa akifika
na ndege ya saa nne asubuhi. Daktari wa Nanaa na mkewe, walifika hapo ijumaa
usiku. Alihakikisha anampa matibabu mazuri, Nanaa akaamka akiwa ametulia.
Hata hakuamka pale alipokuwa
amekaa. Walimtengeneza vizuri akiwa amekaa tu. Nywele alishasuka, kwa hiyo
walizitengeneza tu vizuri. Man aliwapa mfanyakazi mmoja wa pale hotelini akawa
akisaidiana na mama G, kuwahudumia watoto. Uzuri wa watoto wa Nanaa, ni wamuone
tu mama yao. Wakimuona amekaa sehemu, wao watacheza pembeni bila shida. Mchukua
video na mpiga picha waliingia ndani. Wakaanza kazi yao tokea Nanaa anapambwa
mpaka anamaliza. Grace alikuja kuvalia hapo chumbani kwao. Kwa hiyo aliomba
mama yake na watu wote watoke wawaachwe wao tu.
~~~~~~~~~~~~~~~
Mama G akaondoka na watoto,
kuungana na watu wengine kule upande wa bustanini kunakofungiwa harusi.
Akaangaza macho kwenye ile sehemu, akajua kwa hakika pesa imemtoka mwanae.
Kuanzia mapambo. Vile kulivyotengenezwa kwa umaridadi na kupangwa kwa ustadi! Maua
yaliyojaa pale ya asili. Akajua pesa kubwa imemtoka Geb. Akakumbuka bei ya
gauni na vitu tu vya Nanaa, ilikuwa pesa nyingi. Na vyote Geb aligaramia kwa
haraka akimwambia Grace anunue chochote anachotaka Nanaa. Pete zao za harusi
pia zilikuwa pesa nyingi sana. Gold ile ya garama na zilikuwa nzito. Napo hapo
Geb alitoa pesa ndefu tu.
Akaendelea kuangalia kwa kupafurahia
sana pale mahali. Akamuona Geb na Man upande mwingine. Geb alipowaona
akawasogelea, akataka kumyanyua Liv. “Mwache bwana!” Geb akacheka. “Amependeza
sana, Oliva wa Geb! Natamani hata kupata busu.” Liv akacheka. “Si uiname tu!
Unataka mchafuane sasa hivi, uniharibie picha.” Geb akatingisha kichwa.
“Shuguli yako mwenyewe!” “Kumbe! Wewe unajua uchungu wa kubeba mimba ya mapacha,
tena warefu?” “Hapana mama G.” Geb akajibu. “Basi tulia.” Geb akacheka huku
akimtizama mama yake. Alimjua jinsi anavyopenda kupora shuguli.
Man naye akasogea. “Nashukuru sana Man
mwanangu. Mmeandaa vitu vizuri sana. Wafanyakazi wenu wazuri. Tumetunzwa hapa
kama wagonjwa!” Wote wakacheka. “Nimefurahi kama mmependa. Hata Geb
amefurahia.” “Kabisa.” Geb akajibu. “Halafu mmependeza sana. Na mmeendana!” Man
na Geb wakacheka. “Lakini naomba niwaombe kitu. Na niombe radhi kabisa!” Wote
wakamgeukia Man vizuri ili kumsikiliza.
“Msinikasirikie mkaona
nachanganya mambo.” Wote wakatulia wakimwangalia kwa makini kutaka kuelewa ni
nini anachozungumzia maana mpaka hapo hawajaona kilichochanganywa. “Leo nataka
kumchumbia Grace.” Wote wakabaki wameduaa. “Kabla hamjasema kitu kwenye hilo,
naomba niongezee jingine, ndugu zangu watahudhuria.” Man akaweka uso wa hofu
huku akisugua viganja kwa wasi wasi. “Okay. Kabla hamjakasirika zaidi, labda
nimalize kila kitu ili mjue kila kitu. Hivi tunavyozungumza, Mzee Ole ameshatua
uwanja wa ndege. Nimepigiwa simu, yupo njiani na mama wanakuja. Nikisema
njiani, namaanisha karibu na hapa.” Kimya. “Sasa mnaweza kusema chochote. Ni
hivyo tu. Namchumbia Grace leo, nimekaribisha wageni kwenye harusi yenu bila
kuwataarifu, na Mzee Ole anakuja kukutana na nyinyi kwa mara ya kwanza.” Man
akawa anawaangalia kwa zamu.
“Ila sikuwa nimepanga hayo yote.
Ni Malisa huyo na baba! Mimi niliwaambia kwenye harusi ya Geb, kaka yake Grace
nita propose kwa Grace. Nilikuwa nimepanga kumfanyia tukiwa safarini. Sasa,
sababu tutakuwa na watoto, hakuna tena safari na nikaona siwezi kusubiri.
Nikaona nimuombe tu leo awe mke wangu. Malisa ndio mvurugaji. Akang’ang’ania
kuwa lazima na yeye awepo kwa kuwa Grace ni rafiki yake. Nikamwambia hapana.
Hii harusi sio ya watu wengi. Akasema yeye sio mtu, sasa hivi ni familia
ya kina Magesa.” Mpaka Mama G akacheka.
“Hakika sio mimi mama. Ni Malisa.
Na Malisa huwa hajui jibu la hapana. Hivi anakuja na familia yake na wazazi.
Naomba mnisamehe jamani. Lakini Geb, naweza kufanya hivi, nitengeneze sehemu.
Wapaandae kabisa. Baada ya harusi yako mimi nimwite Grace sehemu watakayokuwepo
familia yangu, ndipo ni propose huko ili tusichanganye mambo.” Geb akacheka
kidogo, maana Man alikuwa na wasiwasi mpaka ukaonyesha usoni. Harusi ya Geb
hakutaka watu wengi. Alitaka watu wachache tena anaowafahamu yeye. Leo Man
ameleta wageni!
“Kwanza nafikiri ni heshima kubwa
sana mtakayokuwa mmempa Grace. Binafsi nimefurahi. Na sidhani kama ni jambo la
busara, Mzee aje mpaka huku asihudhurie harusi yetu! Kwangu naona itakuwa ni
jambo la heshima kubwa sana. Tunahitaji baraka zake.” Man akahema kwa nguvu
kama aliyepata aghueni. Geb akacheka.
“Ndio maana ulikuwa umekosa
raha?” “Wewe hujawahi kumuona Malisa. King’ang’anizi kupita kiasi. Akitaka
jambo lake, anakukaba mpaka useme ndiyo. Hapa nilikuwa nikimuomba
wakifika hapa wasije huku mpaka nizungumze na nyinyi. Imekuwa kosa. Anapiga
bila kupumzika, mwishoe ameniomba namba yako eti ajitambulishe mwenyewe. Ndio
maana imebidi tu nije hapa kabla hajakutafuta yeye. Maana alisema nisipompa
namba yako, anamuomba Grace. Sasa nikaona ni heri nijisalimishe mimi mwenyewe.”
Wakacheka.
“Hamna neno kabisa.” Geb
akasisitiza.“Kwanza tukiwa wengi ndio itanoga.” “Usiseme hivyo mama yangu! Wewe
hujakutana na hiyo familia yangu. Kwanza wakikwambia wanakuja wachache, ujue
hawatapungua 15. Na wanaharaka kuliko nitakavyokwambia. Hawajui neno hapana
wala hawajui kusubiri ndio inakuaje. Yaani wanaweza hata kukuomba
wakulipe mahari leo leo!” “Haiwezekani Man!” “Wewe acha mama. Mimi mwenzenu
nina baba! Kumjua Grace imekuwa nongwa. Silali. Kila siku wanaulizia tarehe ya
harusi. Na baba naye anaongeza hukumu eti nataka mpaka afe ndio nioe.”
Simu ya Man ikaita. Wakati anataka kupokea, muhudumu naye akawa anakuja huku
anakimbia. “Mzee amefika.” Wakamuona Man anavuta pumzi. “Nakuja. Asante.”
Akawageukia Geb na mama yake. “Si naruhusiwa kuwaleta hapa?” Mama G alikuwa
akicheka. “Man mwanangu, naomba uwe huru kabisa. Fanya kile unachoona kitafaa.
Hii shuguli ni ya kwetu wote.” “Nashukuru mama yangu. Ila sitarudia tena.” Man
akaondoka.
Geb na mama yake wakaangaliana.
Wakacheka. “Grace atafurahi sana. Na anavyompenda Man!” Mama yake akaongea kwa
sauti ya chini. “Au wewe unasemaje Geb?” “Mimi nataka awe na furaha mama. G
anastahili mwanaume kama Man. Hana sababu yakutaka kumuoa Grace kama sio
mapenzi ya kweli.” “Nimefurahi safari hii umetoa baraka zako.” Geb akacheka.
“Kweli Geb. Hukufurahia kabisa
Grace kuolewa na Danny.” “Kwa kuwa mimi namfahamu Danny, mama. Nilikuwa najua
hawezi kumfanya Grace akawa na furaha. Lakini nilipoona wewe umemkubali,
nikaona nikuache tu.” Wakawaona Man na familia yake wanakuja upande walipo.
“Naona wameamua kweli!” Mama G akanong’ona. Mzee Ole alikuwa akisukumwa kwenye
wheelchair. Man alifanana sana na Mama yake. Hawakuhitaji hata utambulisho.
Wakawasogelea, nakuanza
kusalimiana. “Dad, huyu ndio Geb kaka yake Grace.” “Acha bwana Malisa! Mimi
ndio natoa utambulisho.” “Naona unachelewa na sisi tumekuja kusherehekea!” “Si
nilikuwa nasubiria mpumzike kidogo?” “Ndio hayo ninayosema. Unatuchelewesha
Man.” Akamgeukia Geb na Mama G. “Mimi naitwa Malisa. Huyu ni mume wangu. Na
yeye anaitwa Ole. Mungu ametujalia watoto wawili ambao leo tumewaacha ili
niweze kusherehekea vizuri.” “Wanae ndio wale vipepeo wawili niliowasimulia
habari zao.” Wakacheka.
Malisa akacheka tena. Kisha
akacheka tena na tena. Ikabidi wote wacheke. “Yaani sijui huko wana hali gani
jamani! Watoto wale! Yaani hapa Man amewataja, ndio sura zao zikanijia.” Malisa
aliongea huku anacheka. “Wangekuwepo hapa, yale mapambo yote pale mbele na
kwenye viti, yangekuwa yamezagaa kila mahali. Hakuna hata jani lingesalia
mezani au kwenye viti.” Malisa akaongeza na kucheka. “Haya. Huyu ni baba yetu
na mama yetu kipenzi. Yeye ni mkimya sana. Watu wakimuona na Ole wangu wanajua
ndio mama yake. Sema tu sura amefanana na mimi.” Wakacheka tena.
“Haya, huyu ni Man. Kaka yangu
mimi. Akitoka yeye ndio mimi. Grace ni rafiki yangu. Nimemaliza, lakini Masai
wengine wanakuja baadaye kidogo.” “Ni wangapi tena!?” Man akauliza kwa
mshangao. “Surprise!” Malisa akajibu. “Surprise wakati ni harusi ya watu!”
“Acha kupaniki Man. Eti Geb wewe unatatizo na wageni?” Malisa akauliza.
“Hapana.” Geb akajibu huku akicheka. “Na mama?”
Malisa akamuuliza na mama G. “Hamna neno kabisa.” “Basi ushapata jibu.
Na Mzee Ole kashazungumza na Yusufu, amemwambia aongeze chakula kwa ajili ya
wageni wetu 25.” “Jamani Malisa na Mzee Ole! Watu 25!?” “25 TU.” Malisa akajibu kwa msisitizo. “Huwezi ukawa unaoa kimya
kimya. Lazima watu wajue.” Mama yake akajibu. “Mama na wewe upo upande wao
hawa! Ujue wameshakuharibu!? Hukuwa hivyo mama yangu.” Mama yake akaanza
kucheka.
“Unisamehe mama Magesa. Mtoto
mwenyewe wakiume ninaye mmoja tu. Nimewaambia ndugu wa karibu wa hapa Arusha,
wakaomba na wao waje washuhudie. Tena hao ni wachache kwa kuwa hatukutaka
kuingilia harusi ya Geb.” “Mama wewe! Mmeleta watu 25! Na nyinyi mpo wanne
hapa. Jumla 29. Bado hamuoni kama mmeingilia harusi ya watu!?” “Hata kidogo.
Marafiki zangu wote imebidi kuwatuliza wasije leo, wasubirie harusi.” Mzee Ole
akaongeza. “Naona umepata majibu yako. Kwa asili sisi ni wastaarabu sana.
Hatupendi kuharibu shuguli za watu na ndio maana hatujavuka 30.” Malisa
akaongeza.
“Lakini naomba muwe huru. Kama kuchanganya
mambo kwenu sio sawa, sisi tutaelewa. Kuna ukumbi mwingine hapa. Naweza
kutafuta watu wakatengeneza kwa haraka. Pakaandaliwa vitu. Baada ya harusi ya
Geb, tukahamia hapo ili tusichanganye mambo.” Mama Ole aliongea kwa upole. “Na
ninaomba msijisikie vibaya. Mimi hapa Arusha ni mwenyeji sana. Haitanichukua
hata masaa mawili kuweka sawa kila kitu. Na nina uhakika tutapata kitu kizuri
tu.” “Hamna haja yakufanya hivyo mama Ole. Hizi zote ni baraka. Hata hivyo sisi
wenyewe tupo wachache sana. Hatujafika hata 20! Hamtaharibu chochote kwa kuwepo
hapa. Binafsi nachukulia ni kama Mungu ametuletea watu wafurahi pamoja na sisi
siku muhimu kama hii. Naomba muwe na a mani
kabisa. Au wewe Geb unafikirije?” “Sioni tatizo lolote. Kama wewe mama
umeridhia, ni sawa.” Hapo mama G akajisikia vizuri.
“Daah! Nashukuruni sana.” Man akasikika
ametulia. “Nawashukuruni sana. Na mtusamehe. Swala la Man kupata mwanamke kwetu
ni muujiza.” “Acha basi mama.” “Kwani uongo? Ni kweli anavyosema mama.
Hakujawahi tokea, mpaka tukakata tamaa.” “Naomba unyamaze Mal.” Malisa akaanza
kucheka. “Basi mimi naomba nikusalimie mama kwa kukukumbatia ndio nitaridhika.
Halafu ndio niende alipo Grace, huko chumbani nikamsaidie yeye na bibi harusi
wetu.” Akamkumbatia Mama G. “Nimefurahi kukufahamu Malisa mwanangu.” “Mimi ndio
zaidi mama. Asili ya kina Ole tunapenda watu. Ukoo ukipanuka hivi, ndio furaha
yetu.” “Kabisa.” Mzee Ole akaongeza.
“Si umemsikia Mzee Ole? Basi ujue
sisi ndio tunafuraha sana. Tunapenda kuongeza watu kwenye maisha. Hapa ingekuwa
sio harusi ya Geb ni siku tu ya kawaida, kungefurika watu. Baba hakutanii.
Imebidi kutuliza watu ili leo wasije. Na sijui habari zimesambaa vipi! Njia
nzima kutoka Uwanja wa ndege mpaka hapa baba alikuwa akijibu shutuma ni kwa
nini hawajaalikwa. Kana kwamba haitoshi wakataka waje sasa hivi hapa ili
wamuone Mzee Ole. Amewakatalia ili harusi yenu Geb iwe na utulivu. Na usione
hapa pako kimya, tulishaomba ulinzi mapema kabla hatujaingia hapo. Polisi kibao
wapo hapo nje, wanazuia watu wasiingie, mpaka baadaye kwenye tafrija, tena
itabidi Ole wangu ndio aende kuwatambua ndio waruhusiwe kuingia ndani. La sivyo
pasingetosha hapa. Na wote hao ni rafiki zetu tuliowafanya kama ndugu. Kwa hiyo
mama, sisi tumefurahi zaidi. Ukimuona mama yetu anaongea hivyo, ujue kafurahi
kutoka moyoni.” Wakacheka kidogo.
“Na kweli huwa hazungumzi mama.
Ni kucheka tu.” Man akaongeza na kumsogelea mama yake akambusu kichwani.
“Asanteni kwa upendo wenu.” Ndilo jibu aliloweza kutoa mama G. Kisha akampa
mkono Geb. “Hongera sana Geb.” “Nashukuru Malisa.” “Basi ngoja mimi niwaache,
nikashuhulikie mambo ya harusi. Nataka niwaletee Grace na Nanaa wakiwa swafii,
macho yawatoke.” “Si niliwaambia juu ya Malisa!? Hapo kashapora na harusi!
Ukoje Mali jamani!?” “Unanichelewesha Man. Grace ameniita muda mrefu sana.
Jamani, baadaye. Tutakuja hapa na biharusi wetu.” Malisa akaondoka. Akaacha
baba yake anacheka. “Daah! Yaani hapo atajaa, kama amealikwa kumbe amejialika.”
“Ndio vizuri amsaidie mwenzie.” Mama G alikuwa akicheka.
Sasa ndipo wakapata wakati
mtulivu wakusalimiana na mzee Ole na mke wake pamoja na mume wa Malisa. “Sasa
mama Magesa, mimi nimekuja nimejiandaa. Nataka tumalizane kabisa leo leo.” “Baba
please! Hata Grace mwenyewe hajakubali! Tusubirini kwanza.” “Acha woga wewe.
Masai wawapi? Nilikwambia mmpange Grace vizuri. Mimi siwezi kuwa nimekuja mpaka
huku halafu uniletee uswahili. Leo namalizana na mama kabisa. Au Mama Magesa
unasemaje?” Mama G akamgeukia Geb. “Nafikiri tusubiri kwanza kusikia kutoka kwa
Grace mwenyewe. Akikubali, basi taratibu nyingine zinaweza tu kuendelea.” “Nipe
mkono.” Mzee Ole akanyosha mkono kwa Geb. “Asante sana.” Geb hakujua aseme
nini. Walicheka tu.
“Mungu anapoamua kubariki, usizubae.
Sasa mama, Mungu wako amekutembelea. Ameamua kukubariki. Hizi zinaitwa ‘Double blessing’. Mapacha wote
wanapata wenza kwa wakati mmoja.” “Basi ndio mjue ni wapi Malisa amerithi. Mzee
Ole aking’ang’ania jambo!” “Huko tumeshamaliza. Wewe panga maneno yakutongoza.
Usiniangushe. Sio tena ung’ate maneno turudi Dar mikono mitupu.” Wafanyakazi
wengi wakaja kumsalimia mzee Ole. Alikuwa mcheshi akitaniana na kila mtu pale.
Wafanyakazi wote walionekana kumpenda.
Baada ya muda Malisa akasikika
kwenye kipaza sauti, akiomba watu watulie kwenye viti vyao ibada inakaribia
kuanza. “Malisa! Malisa! Ameshakuwa MC!?” Man akashangaa sana. Baba yake
akaanza kushangilia. “Lakini anafanya vizuri. Mwache tu aendelee.” Geb alitoa
hiyo ruhusa. Ni kweli Malisa alifanya kazi nzuri sana. Akapanga watu kwenye
viti. Akamfuta Geb na kumnong’oneza. “Una mziki wowote unataka Nanaa aingie
nao?” “Perfect!” Geb akajibu kwa
haraka bila kufikiria mara mbili. Wakamsikia Malisa akicheka.
“Mbaya?” Geb akauliza. “Safi
sana. Yaani umenifurahisha sana Geb. Nimekupenda gafla.” “Naomba uondoke Mali.”
“Vipi lakini? Nafanya vizuri?” Akamuuliza kaka yake. “Sana. Asante. Nimekumbuka
tulisahau swala la MC. Hatukutafuta.” Malisa akamkonyeza kaka yake. Akaondoka.
“Utamzoea tu. Akili zake kama baba yake.” Geb akacheka.
Wimbo wa perfect ulipoanza kusikika kwenye spika ndogo zilizokuwa zimewekwa hapo bustanini, Malisa aliomba watu wote wasimame. “Kasoro dad.” Malisa alisikika kwenye kipaza sauti. Man akatingisha kichwa. “Hapa Mc tumempata!” Alinong’ona, Geb akacheka. Man alishuka kwenda kumpokea Grace. Akaja naye mpaka pale mbele. Malisa alipiga vigelegele huku baba yake akipiga makofi. Mama yake alikuwa akicheka tu. Mara Nanaa aliingia akiwa ameshikwa mkono na James. Hata James alikuwa amependeza sana japo alionekana amekwisha mwili. Alivaa suti nyeusi iliyokuwa imemkaa vizuri. Nanaa alijua amenunua mpya. Ilimkaa vizuri sana. Kama hukuwa ukimfahamu mwili wake, usingetambua kama amepungua. Hata uso wake ulionekana umebadilika. Yale majonzi yaliisha. Fifi alipomuona tu Nanaa, na yeye akaongeza nguvu kwenye vigelegele vya Malisa.
“Nanaa amependeza sana.” Geb
alinong’ona. Kisha akavuta pumzi kwa nguvu huku na tabasamu usoni. Walikuja
taratibu. Alikuwa amevaa viatu vya chini kabisa. Na gauni lililokuwa limechanua
vizuri lakini sio kubwa sana na mkia mrefu kiasi kama ndoto zake. Alitengenezwa
vizuri, Nanaa akapendeza. Geb alishuka pale na kuwasogelea. Mchungaji akauliza.
“Nani anamtoa Nanaa?” James akaitika kuwa ni yeye. Geb akapokea mkono, harusi
ikafungwa ndani ya dakika 15 Nanaa akawa mke wa Geb kihalali. Hakuna jinsi
Nanaa angeweza kueleza furaha yake mtu akaelewa.
“Siamini mama.” Alimwambia Mama
G, aliposogea kuwapongeza. “Hongera Nanaa, mwanangu. Hongera sana.” James naye
akasogea. “Hongereni.” Nanaa alishindwa hata kuongea mbele ya kaka yake.
Akaanza kulia. “Mimi mwenyewe siamini. Nakushukuru sana James. Asante kwa kuja,
asante kwa kunilelea Nanaa. Nakushukuru. Sasa hivi naomba ukalale kabisa. Nanaa
ni mke wangu.” James akacheka. “Sasa hivi nitalala.” Mazungumzo yakaanza na
vicheko vikakolea.
Fifi akasogea pale walipokuwa
wamesimama maharusi hao na ndugu zao. “Mtoto mbaya wewe!?” Nanaa akaanza
kucheka. “Nimefurahi umekuja dada.
Kabla ya lawama nikumbatie basi.” Fifi
akamkumbatia. “Hongera Nanaa mdogo wangu.” “Asante dada yangu. Nashukuru kwa
kuniongoza vyema kipindi kile. Umechangia mimi kusimama hapa leo.” “Wee! Watu
hawaachii neema mdogo wangu. Kwanza dume lenyewe la nguvu. Unataka kwenda
kutuletea mbegu za ajabu ajabu!” Nanaa akaanza kucheka. Alimfahamu Fifi.
“Sasa ubaya wangu uko wapi tena?” “Kumbe unakaka mzungu, halafu hutaki kunitambulisha! Kipi usichoelewa kuwa mimi ni mjane?” Nanaa akamvuta James. “Naomba nikutambulishe kwa dada Fifi. Nilikwambia habari zake kwa kifupi. Ndio huyu.” “Nashukuru sana kwa kuwa na Nanaa, kipindi chote kile. Na asante kwa kuja hapa.” James akampa mkono. Fifi akabaki akicheka tu. Nanaa akamshangaa. “Dada Fifi!” Akamsukuma kidogo. Bado James alikuwa akiwatizama. “Kaka amekushukuru.” “Asante.” Akajibu. “Haya, fahamianeni wakati naenda kwa mume wangu.” Fifi na James wakacheka. Nanaa akawaacha.
~~~~~~~~~~~~~~~
Nanaa alikataa kubadilisha gauni.
Akamwambia Grace hamu bado haijamwisha yakuvaa shela. Wakamkubalia abakie hivyo
hivyo hata wakati wa tafrija. Na uzuri ni kuwa gauni lilikuwa na mkiwa unaoweza
kutoa, wakajua hatasumbuka endapo atatakiwa kusimama na kutembea. Walimrudishia
vipodozi, wakaelekea ukumbini kwa sherehe.
namna vilikuwepo kufurahisha wageni wao waliokuja
kushuhudia Man akichumbia. Na kwa kuwa walipata baraka zote kutoka kwa Geb na
mama yake, Man hakuona shida kualika watu wake wakaribu. Hiyo cocktail yenyewe
iliwatoa macho waalikwa. Vilijaa vicheko hapo nje ya ukumbi wakati wakisubiria
maharusi na ndugu wa karibu wamalize kupiga picha.
Mida ya saa nane mchana, ndipo
sherehe ilianza rasmi hapo ukumbini. Waalikwa wote walitakiwa waingie ndani ya
ukumbi mara baada ya cocktail party iliyofanyika nje ya ukumbi wakati maharusi
wakipata picha za ukumbusho. Hata wao hawakuamini wakati wakiingia ukumbini
hapo. Watu walijaa. Ukumbi pia ilibidi mama Ole atengeneze kwa haraka sehemu
nyingine. Pesa huwa inauwezo wakufanya yale mambo magumu kutokea kwa haraka
sana. Kuanzia muda kina Magesa wamesema ni sawa wao wawepo kwenye harusi yao,
mpaka hapo, yule mama alishafanya kazi kubwa sana.
Waliitwa wale wale wapambaji.
Wafanyakazi wote waliambiwa kazi iliyokuwepo kwa wakati ule ni kuhamisha kila
kitu kwenye ukumbi huo mdogo, kwenda kwenye ukumbi mkubwa. Akaamuru
kisibadilishwe kitu chochote. Mapambo yawe yale yale. Hakika alifanikisha.
Chini ya usimamizi wake huyo mama mkimya, akawatengenezea ukumbi mkubwa na
nadhifu sana. Walishangaa watu waliokuwepo hapo na vile ilivyo ni kama
walipanga mwaka mzima.
Geb alikuwa akicheka kila mtu
alimuona. “Sijawahi kuona Geb anafuraha hivi!” Grace akanong’ona. “Aliniambia
ni kitu kilichokuwa kikimsumbua sana.” Man akajibu. Wakaendelea kuwaangalia
walivyokuwa wanacheza. “Lakini anaonekana anampenda Nanaa! Angalia jinsi
anavyomwangalia.” Man aliongeza. “Sana. Anampenda bila kujisingizia. Hajui
maisha mengine bila yule mtoto. Heri wameona tu, watu watulie.” Man akacheka.
“Kweli Man. Kila mtu alikuwa anasema Nanaa ni wake. Heri sasa hivi heshima
itaongezeka. Wawaache watulie, walee sasa watoto.” Grace akamalizia kwa upole.
Akawa kama anafikiria.
“Maisha ni kitu cha ajabu Man!
Wakati mwingine unaweza kufikiria umemaliza, kufumba na kufumbua, unajikuta
unatakiwa kama sio kuanza, basi hujui tena. Maisha yanaweza kukupotezea
muelekeo.” Grace aliongea kwa upole. Man akambusu. Wakamsikia Malisa
akitangaza. “Wakati mziki wa taratibu ukiendelea, Geb na Nanaa wanaenda
kupumzika. Lakini tutapata wimbo kutoka kwa Manesa Ole. By the way ni kaka
yangu. Anaomba mtu yeyote asisimame kucheza. Nyinyi mburudike tu. Ila anataka
msikilize maneno kwa makini. Karibu Man.” Grace akakunja uso. Man akambusu na
kusimama. Akamgeukia Geb na kunong’ona. “Sijawahi hata kumsikia akiimba
bafuni!” Geb akacheka.
Kwa Wengine
Bahati Huja Mara Mbili.
Man alisogea alipokuwa amesimama dada
yake. Akapokea kipaza sauti. “Najua hii ni harusi ya Geb na Nanaa. Nitaimba,
lakini ni maalumu kwa ajili ya Grace.” Malisa akaanza kupiga makofi. “Malisa atanisaidia kuimba.” “Nilijua
utanisahau!” Wakacheka. “Maalumu kwa
ajili yako Grace. Ni zilipendwa. Enzi hizoo, lakini imebeba maneno ambayo
nataka Grace ayasikie na kuyaelewa.” Grace akaonekana kuingiwa hofu. “Relax G!”
Geb alijaribu kumtuliza. Walikuwa wamekaa meza ya duara.
Take me back in the arms I love, Need me like you
did before
Touch me once again, And remember when
There was no one that you wanted more
Don't go you know you will break my heart
She won't love you like I will, I'm the one who'll
stay
When she walks away, And you know I'll be standing
here still
I'll be waiting for you, Here inside my heart
I'm the one who wants to love you more,You will see I can give you
Everything you need, Let me be the one to love you more
See me as if you never knew, Hold me so you can't
let go
Just believe in me, I will make you see
All the things that your heart needs to know
I'll be waiting for you, Here inside my heart
I'm the one who wants to love you more, You will see I can give you
Everything you need, Let me be the one to love you more
And some way all the love that we had can be saved
Whatever it takes we'll find a way
I'll be waiting for you, Here inside my heart
I'm the one who wants to love you more
Can't you see I can give you, Everything you need
Let me be the one to love you more
~~~~~~~~~~~~~~~
Man aliimba ule wimbo, hakufika
mbali, Grace akainama akilia. Alishajua kinachofuata. Man na Malisa walikuwa
wakiimba vizuri sana. Walipata mlio/instruments wa huo wimbo, lakini maneno
waliimba yeye na Malisa. Ungependa wasimalize. Grace alikuwa ameina akilia.
Wakati wanarudia beti ya mwisho Man akamsogelea Grace akapiga magoti. Grace
alikuwa ameolewa. Lakini Man alimfanyia mambo aliyokuwa akiyaona kwenye tv.
Hakuwahi hata kuwaza kama mtu anaweza kupropose kwa staili ile kama msichana
mdogo, wakati ni mama wa watoto watatu!
Akamvuta mkono. “Mary me Grace.” “Unauhakika
Man!?” Grace akauliza kama asiyesadiki anachotaka Man.
Alikuwa amependeza sana. “Sijawahi kuwa na uhakika wa jambo maishani kama
katika hili. Nakupenda Grace. Wewe sema tu Ndiyo.” Bado Malisa alikuwa
akiimba vizuri sana. Taratibu. Ukumbi mzima macho yalikuwa kwa Man na Grace. “Tafadhali
kubali. Nakuahidi hutajuta. Nitakupenda mpaka kifo chetu Grace.” Bado Man
alikuwa akibembeleza.
“Nakupenda Man.” “Kwa hiyo ndio umekubali?”
Man akauliza. “Ndiyo.” Man akasimama.
“Mzee Ole! Amekubali aisee.” Watu wakaanza kucheka. “Maliza sasa kabla
hajabadili mawazo. Masai wa wapi wewe!?” Kila mtu akaanza kucheka. Man akarudi
kupiga magoti, akavuta mkono wa Grace akamvalisha pete ya uchumba. Akamnyanyua
na kuanza kumbusu.
“Hatimae na mimi naoa jamani!”
Kila mtu alikuwa akicheka. “Sasa maharusi na wasimamizi wenu mnaweza kuja
kucheza pamoja, kabla hatujaleta wazazi.” Malisa alisikika tena. “Ila naomba
turudie wimbo wa Geb. Alitaka apigiwe Nanaa wakati anaingia. Sijui kama
alisikiliza. Naomba Nanaa usikilize tena wakati mkicheza. Nao umebeba maneno
mazuri.” Nanaa akaitikia kwa kichwa huku akitoa tabasamu lililotengeneza
dimpozi nzuri sana mashavuni. Geb alimsaidia kumshikia gauni mpaka sehemu ya
kucheza. Wimbo wa Perfect wa Ed
Sheeran, uliobeba maneno haya, ukaanza taratibu. Geb
akamshikilia Nanaa, Man akamvutia karibu Grace, wakaanza kucheza taratibu.
-
I found a love for me, Darling just dive right in, And follow my lead
Well I found a girl beautiful and sweet, I never knew you were the someone
waiting for me 'Cause we were just kids when we fell in love, Not knowing what
it was
I will not give
you up this time, But darling, just kiss me slow, your heart is all I own, And
in your eyes you're holding mine,
Baby, I'm
dancing in the dark with you between my arms, Barefoot on the grass, listening
to our favorite song, When you said you looked a mess, I whispered underneath
my breath,But you heard it, darling, you look perfect tonight
-
Well I found a woman, stronger than anyone I know,She shares my dreams,
I hope that someday I'll share her home I found a love, to carry more than just
my secrets,To carry love, to carry children of our own We are still kids, but
we're so in love,Fighting against all odds, I know we'll be alright this time, Darling,
just hold my hand Be my girl, I'll be your man,I see my future in your eyes.
Baby, I'm dancing in the dark, with you between my
arms, Barefoot on the grass, listening to our favorite song When I saw you in
that dress, looking so beautiful, I don't deserve this, darling, you look
perfect tonight.
Baby, I'm dancing in the dark, with you between my
arms, Barefoot on the grass, listening to our favorite song I have faith in
what I see, Now I know I have met an angel in person And she looks perfect, I
don't deserve this You look perfect tonight
Wakati wanacheza
huo wimbo, Grace bado hakuwa akiamini. “Man!” Grace akaita taratibu. Man
akaegesha sikio pale begani alipokuwa amelala Grace. “Sikutegemea! Asante.” Man
akambusu. “Nakupenda Grace. Nataka tuishi wote. Naamini tutakuwa na ndoa
nzuri.” “Naamini hivyo Man. Ila ujue nimefurahi sana. Ndio maana mzee
Ole yupo hapa na mama?” Grace akauliza. Man akamvuta mbele kidogo ili amtizame
machoni. “Ndiyo.” Grace akacheka. “Ujue hao waalikwa wengine Malisa aliniambia
wapo hapa kwa ajili ya kuja kumuona Mzee Ole. Hawajamuona muda mrefu. Wamekuja
kumpa pole. Kumbe wapo hapa kwa ajili…” “Yetu sisi.” Man akamalizia. Bado Grace
hakuwa akiamini. “Wote wamekuja kushuhudia nikikuchumbia Grace.”
“Nimefurahi sana. Sikutegemea!
Sikuwa hata nikifikiria kama utakuja kunichumbia! Nilijua hata kama tuta..!”
Grace akasita. Man akambusu tena kwenye kipanda uso huku wakiendelea kucheza. “Utanioa
kanisani?” “Kabisa! Na nitataka uvae shela.” Grace akaanza kucheka. Man
akainama na kuanza kumbusu midomoni.
James Atoa
Siri Aliyogundua.
James hakuwa ameelewa. Akavuta
kiti karibu na mama G, maana walikuwa wamekaa meza moja. “Mama!” Mama G alikuwa kimya anajiangalizia
tu mapacha wake. Akamgeukia James. “Sijaelewa! Mbona Grace anachumbiwa tena!?”
“James mwanangu, jumatano alipewa talaka yake rasmi. Ndoa ilishaisha miezi
karibia nane sasa.” “Mungu wangu Danny!!” James alishituka sana. “Ndio hivyo.
Kwani hukusikia?” “Hivi unavyoniona mama, ndivyo nilivyo na nimemaliza. Rafiki
wamenitenda vibaya mama! Marafiki niliodhani ni ndugu, wamemtendea dada yangu
unyama mbele ya macho yangu! Hakika sina rafiki mama. Najilaumu kila iitwapo
leo. Maana najiona ni kama nilimsababishia dada yangu matatizo. Isingekuwa mimi
kumtambulisha Nanaa kwao, wasingemtendea ule ubaya.”
“Wanatengeneza kundi la kiharamia
chini kwa chini huku wananichekea usoni!? Hapana mama. Nimeogopa sana. Gozi
anacheka na sisi pale kumbe anawasiliana na Malii, kumwambia sasa anaweza
kuingia pale, wageni wote wameondoka!” Mama G akashituka sana.
“Haiwezekani James.” “Niliumia sana
mama. Ikabidi kuanza kufanya uchunguzi wangu. Nilijiuliza Malii alijuaje kama
wageni wote wameondoka, na ule ndio ulikuwa muda wa kuja na watu wake?
Nikamuhisi Gozi. Unakumbuka ni kama Gozi ndiye aliyekuwa akifukuza wenzake
waondoke ili Nanaa apumzike kwa kuwa ametoka hospitalini?” Mama G akaanza
kuvuta kumbukumbu. “Tena tukawa tukicheka. Kumbe alikuwa anatumwa.”
“Ulijuaje!?” Mama G akauliza. “Kumbuka nilisomea mambo ya electronics mama
yangu. Kazi zangu ni za mitandao. Ilibidi kuingia kwenye simu yake bila
kumwambia mtu, tena nikiwa kazini kwangu. Ndipo nikaangalia historia nzima ya
jumbe zilizokuwa zikitembea kati ya Gozi na Malii. Pale Gozi alikuwepo kama
mpeleka habari tu. Alikuwa pale akituchekea kumbe anatuma jumbe kwa Malii
kumwambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwa wakati ule. Nimeumia sana mama.
Sana. Nimeshindwa kuamini wale wote wale, wamewezaje kumtendea Nanaa, mtoto
ambaye nilikuwa nikiwasimulia shida zake!! Wanapanga mbinu ya kumkomoa
Geb, kwa kupitia Nanaa!?” Hilo nalo likazidi kumchanganya mama G.
“Kwani shida ilikuwa ni Geb!?”
Mama G akauliza kwa mshangao. Mazungumzo hayo yalikuwa yakiendelea wakati bado
maharusi na wasimamizi wao wakiendelea kucheza. “Wewe unafikiri ni nini mama!?
Zile zote nisababu tu. Malii ni mpinzani wa Geb tokea zamani. Hakubali apitwe
na Geb. Kwani wewe hulijui hilo!?” “Geb aliniambia kila kitu.” “Basi. Ndio ujue
ni hivyo. Tamaa kwa Nanaa ilimzidi Malii, pale alipoona Geb anamzidi. Wanawake
wote walioonekana wanamtaka Geb, Malii alihakikisha analala nao yeye kwanza
kabla ya Geb. Ni Nanaa peke yake aliyemkataa yeye kwa ajili ya Geb. Lakini
wengine wote walimkubali. Geb alikuwa akijua na kumuachia tu. Na yeye alikuwa
akijua kuwa Geb hawezi kupita alikopita yeye. Kwa hiyo ni kama alikuwa
akimkomoa.”
“Analala nao yeye wa kwanza, ili
Geb asiweze tena. Na alihakikisha wote tunajua kama alilala na hao wanawake
kama kumkera au kumkomoa Geb. Kama aliyekuwa akitaka kuonyesha kuwa anamzidi
Geb kwa mambo fulani fulani. Sasa kwa Nanaa kumkataa, hapo alishindwa
kukubali.” Mama G akazidi kuumia. Kuona alimuadhibu Nanaa bure.
“Nimeumia sana mama. Sana. Naona
mimi ndiye nilimuingiza mdogo wangu kwa watu wabaya.” “Nisikilize James. Mwangalie sasa hivi Nanaa.
Mwangalie pale alipo. Angalia hawa watoto hapa. Yote haya ni kazi yako wewe.
Usingekuwa wewe kumtambulisha Nanaa kwao, na kuweka uthamani wake mbele zao,
wala mimi sasa hivi nisingekuwa na hawa wajukuu hapa. Wala Nanaa asingempata
Geb mwanaume anayempenda.” “Lakini kweli.” “Kabisa. Achana na uongo wa ibilisi.
Nanaa anakupenda. Umehangaika na kujinyima mambo mengi sana ili kumfikisha hapo
alipo. Leo sherehekea. Sherehekea sana tu. Furahia kazi yako. Achana na wale
vijana. Wamejawa wivu tu. Usikubali kubeba mzigo usiokustahili.” James akacheka
kidogo.
“Lakini mama, namuhurumia sana
Danny!” “Hata mimi. Lakini James, wale vijana nimewasamehe, lakini nimeamua
hawatakaa wakawa kwenye maisha yetu tena. Danny na wenzake wote.
Wamebeba uovu mkubwa sana ndani yao. Wanacheka usoni kumbe moyoni wanaumia!
Wamemjaribu Nanaa kwa uchawi, vitisho na ukatili wote ule, lakini James,
alilokusudia Mungu, mwanadamu hawezi kulipinga. Hata mimi siwezi kusimama
kwenye kusudi la Mungu. Nanaa yule pale. Leo amekuwa Nanaa Magesa mbele za
Mungu na macho ya watu. Tuwe tunapenda au hatupendi. Sasa hivi Nanaa siye Nanaa
watu waliyekuwa wakimfikiria. Mungu amemuinua haswa. Geb anasubiri watoke
mapumzikoni akamkabidhi nafasi ya Grace, si kama mfanyakazi kama alivyokuwa
Grace, lakini kama mmiliki mwenzie. Sasa unafikiri ni dogo hilo!?” James
akacheka lakini akiwa ameshangaa sana moyoni, Mmiliki mwenza wa Geb Magesa!
“Acha kucheza na mkono wa Mungu
James! Humbariki amtakaye YEYE. Na wala hakuna wakumuuliza kwa nini.
Alikokuwepo Nanaa, huko Moshi, amefungiwa. Yeye mwenyewe anasema hakuwa hata na
tumaini lakumtoa pale kwenu. Hapakuwa na muujiza au hakuna mtu angejua leo
angeweza kusimama kwenye hoteli kubwa kama hii. Eti Geb amemwaga mamilioni ya
pesa kwa ajili ya siku moja tu, sababu ya Nanaa! Huyo ni Mungu James. Shukuru
Mungu umetumika kwenye kutimiza kusudi lake, na yeye hatakuacha hivyo. Naomba
ujipe amani ya makusudi. Samehe kwa ajili yako, lakini jiweke nao mbali kabisa,
basi.” Mama G na James waliendelea kuongea kwa sauti ya chini.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Wakati wakiendelea kuzungumza,
wakasikia kwenye kipaza sauti MC akitangaza kuwa ni muda wa baba wa bibi
harusi, kucheza na bibi harusi. Grace na Man wakasogea, wakaenda alipokuwa
amekaa Mzee Ole na mkewe. “Hongereni sana.” Mama Ole alitoa mkono. “Asanteni
kwa kuja mama na baba. Nimefurahi sana! Sikutegemea kabisa. Na wala sikujua
kama mlikuja hapa kwa ajili yetu!” Grace alimfanya mzee Ole acheke. “Tuone pete
aliyokuvalisha.” Grace akanyoosha mkono kwa mzee Ole. “Hajanitia aibu.”
Wakacheka. “Sasa mimi nataka nikapumzike. Lakini nilitaka kuwaombea baraka, ni
sawa?” “Nitafurahi baba yangu. Asante.” Grace akamwita Malisa.
Akasogea. “Baba anataka kutuombea
kabla hajakwenda kupumzika.” “Unataka wasubiri mziki wa bibi harusi na baba
yake?” “Tafadhali.” Grace akajibu mkono ule wenye pete ukiwa kwa mama Ole na
yeye akiangalia ile pete. “Very beautiful.” Mama Ole akasifia. “Naona mambo sio
mabaya!” “Usifanye mchezo mama. Namuoa Grace!” Wakacheka. Malisa alikuwa
amekwenda kuzungumza na Geb. Geb akasema ni sawa kabisa. Akatangaza kwamba mzee
Ole anakwenda kupumzika, lakini anaomba muda mfupi sana wakumuombea Grace na
Man.
Malisa alimpa baba yake kipaza
sauti. “Naomba nianze kwa kushukuru kwa heshima mliyotupa. Kina Ole huwa tuna
tatizo moja. Hatujuagi neno ‘hapana’
na ‘haiwezekani’. Na huwa tunajua
vitu vizuri. Tukishatambua hiki ni kizuri, huwa tunatatizo jingine tena,
hatuwezi kusubiri mpaka tukimiliki.” Watu wakacheka kidogo.
“Geb na Nanaa, hongereni sana kwa
hatua kubwa na muhimu mliyochukua kwenye maisha. Mngeweza kuendelea kuishi tu,
lakini mlitaka Mungu aweke mkono wake kwenye ndoa yenu, hakika hatawaacha.
Nawaombea heri na mafanikio.” Akavuta mkono wa Grace kutoka kwa mkewe,
akaushika yeye.
“Sasa Geb, sisi tunaoa kwenu. Na
kama nilivyokwambia, hatutasubiri. Huyu Grace nataka awe wa kwetu kabisa.
Sitaki kuja kuzidiwa mahesabu baadaye.” Watu wakacheka. “Sasa jumamosi ijayo
mama ameniambia mtakuwa mmesharudi nyumbani, na sisi tutakuja kulipa mahari
yetu. Jumamosi inayofuata tena, harusi.” Watu wakashangilia sana wakishangaa.
Grace hakuwa akiamini. Akamgeukia Man. “Man!”
Man akamvuta mkono wa kulia, akaubusu. “Hatuna sababu yakusubiri Grace.
Au unataka muda wakufikiria zaidi?” Man akamuuliza kwa kunong’ona. “Sio mbali
na wewe.” Grace akajibu taratibu wakacheka, Man akambusu shavuni.
“Haya, pigeni magoti niwaombee.”
Grace na Man wakapiga magoti. Mbali na ucheshi ule, yule Mzee alimfahamu Mungu.
Alimshukuru sana Mungu kwa ajili ya Grace. Akawaombea wao wawili. Aliomba
amani, furaha na umoja katikati yao. Akaombea mipango yote ya kukamilisha swala
la harusi iliyopo mbele yao, akawaombea baraka Geb na Nanaa, pamoja na watoto
wao, akamaliza. “Asante baba.” Grace akashukuru na Man anaye akashukuru. Mzee Ole
akacheka. “Nitawaona kesho asubuhi wakati wa kupata kifungua kinywa.” Wakaagana Mzee Ole na Mkewe wakaondoka.
Mziki Bibi Harusi na Baba Yake.
Nanaa akamsogelea kaka yake. “Tunatakiwa
kucheza kaka.” James akacheka. Akasimama na kumshika mkono mpaka sehemu ya kuchezea. Mziki ukaanza. “Asante
kaka.” Nanaa akaanza. “Asante kwa kila kitu. Kunifikisha mpaka
mikononi kwa Geb! Nakushukuru.” Machozi yalishaanza kwa Nanaa. “Karibu. Na usianze
kulia, maana utaondoa urembo wote
machoni!” Wakamuona Nanaa anacheka huku anafuta machozi.
“Umependeza sana. Gauni zuri,
umetengenezwa vizuri. Hongera.” James akamsifia dada yake. Nanaa akacheka.
“Asante. Nimefurahi kweli! Bado siamini kaka. Ujue sasa hivi mimi mwenzio ni
mama Magesa?” James alicheka mpaka akasimama. “Nanaa!” “Oooh! Usinione hivi.
Mimi ni mama Magesa mwenyewe. Mke wa Geb. Sio mchezo!” James alizidi kucheka.
“Ulinifundisha mwenyewe. Ukaniambia akija, nitajua tu moyoni. Geb ni wangu
kaka. Ninafuraha ya kupita kiasi.” “Na mimi nimekuona.” Wakaendelea kidogo,
mziki ukaisha. “Hapa nipo hoi, heri nikakae tu. Siwezi tena.” James
akamwangalia tumbo. “Ila umejitahidi! Hongera.” Geb akaja kumchukua,
akamsindikiza mpaka kwenye kiti. “Nimechoka! Nipo hoi.” “Pole. Ngoja nikacheze
na mama, kisha tukapumzike.” “Sawa.” Nanaa akajibu huku akijiweka sawa.
Mziki Bwana Harusi Na Mama Yake.
Geb alitakiwa acheze na mama
yake. Malisa akatangaza kuwa Geb aliomba wimbo maalumu kwa mama yake. Wakatulia
kusikiliza, ndipo wimbo wa ‘Nani kama
mama’ ukaanza
kusikika. Hakuna aliyewahi kumuona Geb akicheza hivyo!
Alitoka akicheza kutoka alipokuwa amekaa na Nanaa, mpaka alipokuwa amekaa mama
yake. Akaenda kumshika mkono pale alipokuwa amekaa akamnyanyua. Akamvuta kwenda
sehemu ya kuchezea, huku akicheza vizuri sana. Geb alicheza kwa hisia huku
akimzungusha mama yake mara kadhaa. Alimbusu mara kadhaa kwa kuwa ni kweli ule
wimbo ulimgusa Geb aliyelelewa na mama G peke yake.
Alisimama naye katika kila hali.
Ni kweli usiku yule mama hakuwa akilala kama Geb halali, yupo kwenye matatizo.
Geb alilala kitandani kwa mama yake akimuombea na kumtuliza mpaka alipompata
Nanaa. Hata alipokuwa na Liz, bado Geb alilala na mama yake. Alijiona amekua
baada ya kumpata Nanaa. Shule ya pesa nyingi aliyomsomesha akiwa hana kitu.
Aliuza kila kitu kwa sababu yake! Hakuacha kumfundisha Geb hata alipokuwa na
watoto. Garama aliyomlipia huyo mama yake, Geb alijua hatawahi kuja kumlipa
hata siku moja. Alikana nafsi yake ili kuwalea yeye na Grace. Alijua wazi mama
yake aliachwa akiwa msichana mdogo sana.
Mzuri na kuvutia kama Grace.
Angeweza kuolewa na kuanzisha familia nyingine, lakini wakati wote alisema
hakuna mwanaume anayeweza kulea watoto wa Magesa isipokuwa yeye mwenyewe.
Alikusudia kutuliza mawazo kwa hao watoto wa Magesa tu. Grace na Geb.
Akajifunga mkanda. Kwa maombi na kuhangaika mpaka kuwafikisha hapo walipo. Nani
kama mama G?
Geb alimzunguka mama yake kwa
kucheza bila kuchoka. Alicheza Geb na kumfanya mama G, aliyenyimwa machozi,
aanze kulia. Nanaa naye akasimama kwenda kucheza. Grace naye akasogea.
Wakacheza wao watatu wakimzunguka mama G, aliyekuwa akilia. Geb akaenda
kumchukua Oliva na Magesa, akarudi nao kucheza. Wimbo ulipoisha, Malisa akasema
urudiwe. Ndipo Man akasimama kwenda kumpokea Geb mtoto mmoja ambaye ni Magesa.
Walikuwa wakicheka hao watoto kadiri walivyokuwa wakizungushwa mikononi wakati
waliowabeba wakicheza. Walicheza kwa kumpepea mama G, huku wakimzunguka. Hakika
ilipendeza.
Wimbo ulipoisha, Nanaa na Geb
wakapata muda wakutoa shukurani zao. Walishukuru watu wote. Zaidi Man na Grace,
kwa maandalizi mazuri tena kwa muda mfupi. Nanaa alisema amefurahia kila kitu.
Zawadi kutoka kwa familia ya Ole iliwakilishwa na Man. Alisimama akiwa
amemshika mkono Grace. Akasema kwa niaba ya familia ya Ole, wanawapa siku tatu
za bure za mapumziko hapo hotelini. Watalishwa na kunyweshwa bure kwa muda wa
siku hizo tatu. Geb alishukuru na hilo pia. Kwani aliwachukulia wageni wake
wote vyumba hapo.
Fifi alikuwa akalale kwenye
kitanda alichokuwa akilalia Nanaa tokea afike hapo. Kwenye chumba hicho kikubwa
alichokuwepo mama G na wajukuu zake. Daktari na mkewe walikuwa na chumba chao.
James alisema anaondoka usiku ule ule kurudi kwa baba yake Moshi.
Baada ya shukurani wakati watu
wanaburudika tu, Geb na Nanaa wakaomba wao wakapumzike. Ni muda ambao Geb
alikuwa akiusubiria kwa hamu sana. Alikuwa na ukame wa miezi karibia kumaliza
8. Heri Nanaa yeye hakuwa akitamani hata kujigusa huko chini baada yakubakwa.
Lakini sio Geb. Malii aligusa ambako hakuweza kususa. Ni Nanaa wake! Kadiri
alivyokuwa akimuona ndivyo alivyokuwa na hamu naye. Hata wazo la kusema eti
Malii alipita hapo, halikumsumbua tena. Alichokuwa akitamani ni yeye apate
bahati ya kuja kumvua tena nguo Nanaa, amfaidi mpenzi wake. Alipomuona mawazo
ya mapenzi hayapo kabisa kwa Nanaa, ni kama anakwepa. Na kumsikia akimwambia
mama G kuwa anaogopa kujigusa, Geb akaanza juhudi za makusudi kumuandaa
taratibu kumrudisha kwenye mapenzi yao yazamani. Hakuacha kumwambia mambo
atakayomfanyia usiku huo. Alimwambia hiki na kile. Hata wakati wanaagana uwanja
wa ndege, alimwambia anasubiria matiti yake. Hisia za kimapenzi zikaibuka kwa
Nanaa. Na yeye akawa na shauku na usiku huo ambao Geb aliupamba kwa mipango mingi
ya mahaba.
Grace na Man walitoka nao hapo
ukumbini ili kuwafikisha kwenye chumba maalumu walichoandaa kwa ajili ya usiku
huo wa fungate. “Naolewa mwenzio Geb.” Geb akacheka. “Nione pete yako.” Grace
akamuonyesha kaka yake. “Nzuri. Ni Tanzanite nzuri sana. Imekupendeza kidoleni”
Geb akasifia wakati akiiangalia ile pete kidoleni kwa Grace. “Halafu hata sijui
huyu Man aliitengeneza lini!” Man akacheka. “Lakini imekukaa vizuri sana mpenzi
wangu. Hata mimi najua kama nimeweka kitu kizuri kidoleni kwako.” Nanaa na yeye
akaiangalia wakati wapo kwenye lifti kwenda chumbani kwao.
“Halafu mimi naona silver
imekukaa vizuri kuliko Gold!” Nanaa akaongea wakati akiangalia. “Na mimi ndio
nimeona hivyo. Sikuwahi kufikiria kuvaa silver maishani. Lakini hii silver
imebeba hili jiwe vizuri sana.” Grace akaongeza huku na yeye akiangalia kidole
chake asiamini. Waliwafikisha chumbani kwao.
“Nanaa, kila kitu chako kipo
kabatini na nimekupangia nguo zako za ndani na za kulalia kwenye ndoo hizi
hapa. Naomba pata muda wakupumzika. Usifikirie watoto wala Geb atakula nini.
Nimeshaongea na Yusuf, mpishi wa hapa, nimemuelekeza vyakula anavyokulaga Geb.
Jana alipofika hapa, alimpikia. Naona amekula bila shida. Kwa hiyo usiwe na
wasiwasi hata na Geb. Ni siku tatu tu, naomba
ziwe ni zako tu.” “Wanangu Grace?” Nanaa akauliza wakati Man akizungumza
na Geb upande wa sebuleni.
“Mama anawasaidizi kibao. Na mimi
nipo kumsaidia. Ninaweza kuwaleta kesho mkakaa nao kidogo.” “Hapo sawa. Liv
huwa anakosa raha kama asiponiona.” Nanaa aliongea kwa kulalamika kidogo. “Basi
usijali, nitawaleta. Lakini tutakuwa busy nao sana. Man anataka tukazurule nao
kabla hawajarudi Dar. Anataka akamtembeze mama na watoto sehemu mbali mbali
hapa Arusha. Kwa hiyo muda mwingi na sisi hatutakuwepo hapa.” Kidogo Nanaa
akaridhika. “Kama ni hivyo sawa. Nilijua watakuwa tu chumbani.” “Tunamipango
nao hao, watarudi Dar wapo hoi.” Wakacheka nakutoka pale chumbani. “Sisi
tuwaache jamani. Mapumziko mema.” Grace akaaga mara baada yakuwafikia Man na
Geb.
Fungate
Nanaa & Geb.
Nanaa akamgeukia Geb mara mlango ulipofungwa. “Sasa huu ndio ule wakati wakutimiza zile,
ahadi zako Geb.” Geb akaanza kucheka. “Hata hatuogi kwanza Nanaa!?” “Sasa
tunaogaje kabla yakuchafuka Geb! Njoo kwanza. Nikushukuru kwa kutimiza ahadi
yako kwangu.” Nanaa akamvua tu suruali akabaki na koti na shati lake na tai
ikining’inia. Akapiga magoti mbele yake. Akaanza utundu wake. Kisha
akamchungulia usoni. “Asante kwa kunioa baada ya kunizalisha!” Tayari
alishapagawishwa. Alishaanza kupotea pale. Geb hakuwa ameshikwa kimapenzi kwa
muda mrefu sana.
“Acha basi Nanaa. Shukurani za
nini tena? Unanikata!” “Acha haraka Geb! Mimi hapa nakushukuru tu.” “Mwenzio
hali mbaya endelea tu, utanishukuru baadaye.” “Nimekuahidi nitakukata kiu zote.
Yaani baada ya hizo siku tatu, utatoka hapa mwepesiiiii.” “Endelea basi
kunishukuru kwa vitendo. Usiache.” Nanaa akarudi huku akimcheka. Geb akaanza
kugugumia tena.
Uzalendo ulipomshinda,
akamnyanyua Nanaa kutoka pale alipopiga magoti akambeba mpake kitandani na
tumbo lake. Kumtoa nguo aliona anachelewa. Yeye akiwa vile vile nusu uchi
alichomudu kufanya nikumtoa Nanaa chupi. Alimvuta mpaka mwisho kabisa wa
kitanda na yeye akaanza kumchezea ili tu aweze kupenya bila kumuumiza. Alipoona
kelele za Nanaa zinazidi, hakupoteza muda, akasimama kwa haraka, akabeba miguu
ya Nanaa akiwa amejilaza vile vile kitandani na shela yake, yeye amesimama, Geb
akaanza raundi ya kwanza akiwa na hali mbaya sana. Sio kwa kumuhisi tu kuwa
ameingia, Nanaa alimsikia akigugumia zaidi mara baada ya kufanikiwa kupenya.
Alikuwa ameng’ang’ania mapaja ya Nanaa kwa nguvu huku akiingia na kutoka
taratibu na hisia zote. Wote walikuwa na hali mbaya. Kila mmoja alikuwa na hamu
na mwenzie.
Geb alishaamsha hisia zote za
Nanaa, na Nanaa hivyo hivyo. Hakuna aliyekumbuka kuoga. Awamu ya kwanza ilipoisha,
ndipo walipoweza kuvua nguo na kupanda sasa kitandani vizuri. Geb aliyekuwa na
uchu na hayo matiti, alimlaza chali lakini kama ubavu. Wote wakiangalia mbele,
zaidi tumbo la Nanaa. Alifanikiwa kupenya huko nyuma, lakini midomo ilikuwa
kwenye matiti ya Nanaa. Alitumia mchezo mzima wa roundi ya pili hapo kifuani
kwa Nanaa, kama mtoto aliyekuwa na njaa kali. Aliendelea kuyanyonya taratibu
mpaka akafanikisha kwa Nanaa na kwake, ndipo alipoweza kutoa midomo yake kwenye
matiti.
Ilitoka midomo ikahamia mikono
kifunia hapo, akichezea matiti huku akihema pembeni yake. Nanaa alijua huwa
anapenda matiti yake. Hata wakiwa wamekaa chumbani wakiangalia movie, kipindi
ananyonyesha, basi Geb atataka angalau mikono itulie hapo kifuani, aachwe
achezee atakavyo. Kitendo cha kunyonyesha mfululizo na kushindwa kurudishwa
yeye hapo kifuani anyonye sio kushika tu, alikuwa akimlalamikia Nanaa wakati
wote kuwa wanae wanamkatili.
Akanyanyuka na kumbusu Nanaa
katikati ya matiti yake kisha akamtizama usoni kuona hali yake. Nanaa hoi, na
tabasamu usoni. Geb alishamfikisha mara mbili, na mimba ile, hakutaka hata
kuoga, akataka alale tu wakati Geb ndio alikuwa akianza. Akainama na kurudi
kwenye matiti. Nanaa alimjua Geb. Akajua ile purukushani yote pale ndio alikuwa
anapata ‘appetizer’. Alijua kwa
Geb, mchezo wenyewe bado kabisaa.
“Tutaendelea kesho bwana!”
“Huogi?” “Nimechoka Geb.” “Jikaze basi tukaoge wote. Angalau nipate cha mwisho
cha bafuni kabla hujalala. Nihurumie Nanaa. Nimekungoja siku zote hizo tena
hata sijakusumbua mpenzi wangu! Uliniahidi…” “Acha kulalamika Geb jamani! Leo
siku imekuwa ndefu. Tangia saa 12 asubuhi mwenzio nipo macho.” “Basi usijiguse,
wewe niachie nihangaike mwenyewe mpaka niridhike.” “Yaani Geb! Kwa nini
usisubirie kesho?” “Wewe lala tu hivyo hivyo niachie mimi mwenyewe niendelee.”
“Geb!” Geb alisharudi kifuani. Hakujibu
tena.
Alikuwa na utundu wake kwenye
hayo matiti, wakati wote Nanaa alijikuta akisalimu amri Geb awapo kifuani
kwake. Akaendelea kwa muda, akahamia masikioni kidogo na kurudi kifuani kwa
muda kisha akarudi shingoni, akaenda sikioni na kumnong’oneza. “Nakupenda
Nanaa.” Hapo hali ya Nanaa ilishabadilika. “Na mimi nakupenda Geb. Nakupenda
sanaaa.” Geb akarudi midomoni.
Akaanza kunyonya midomo ya Nanaa,
taratibu. Hata yeye hakujua ameingia saa ngapi, ila alianza kusikia migugumo ya
Nanaa wakati akiendelea kunyonya midomo yake. Akiwa amewekeza nguvu nyingi
kwenye mikono yake na miguu yake ili asimlalie Nanaa na tumbo lake,
akajirudisha kwenye matiti, hapo ndipo yeye akapotelea kabisa, mpaka akamaliza
kabla ya Nanaa.
“Sio sawa Geb! Umeniamsha mwenyewe.
Mimi nilikuwa nimeshajiamulia kulala. Huwezi kuniacha hivi. Sitapata usingizi.”
Geb alikuwa akicheka sana. “Na ninajua sana kuwa umefanya kusudi! Sio vizuri.”
“Hapana Nanaa. Mimi naona wazo la kusubiri mpaka kesho ni la busara. Umechoka.”
“Usinitanie Geb. Utanikuta bafuni.” Hilo ndilo lilikuwa lengo la Geb.
Akafurahia sana. Wakahamia bafuni.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Zilikuwa siku tatu nzuri sana. Si
kwa Nanaa na Geb tu, hata mama G alipata
wakati mzuri sana na familia hiyo ya Ole. Mzee Ole, mkewe, Malisa na mumewe,
waliondoka siku ya jumapili jioni.
Lakini walimuonyesha yule mama heshima kubwa sana. Siku ya jumapili ambayo Geb
na Nanaa walipokuwa wamejifungia ndani, wao walipata muda mzuri wa pamoja.
Kuanzia kifungua kinywa mpaka chakula cha mchana, walikula pamoja. Wakiongea na
kucheka. Walipanga mipango ya jumamosi. Wakakubaliana mida ya saa 12 jioni
watafika hapo nyumbani kukamilisha mahari ya Grace. Mama G alikataa kulipwa
mahari. Akawaambia wamekubaliana na Geb kuwa hawatapokea mahari ya Grace. Mama
Ole akamwambia basi iwe ni siku ya kuunganisha undugu. Wafike nyumbani japo
watoe mkono wa shukurani kwa kuwazalia Grace. Hilo mama G akalikubali.
Watu wengi walifika hapo kumsalimia
Mzee Ole, aliyeishi hapo jijini Arusha kwa miaka mingi sana na mkewe huyo.
Waliwapa pongezi juu ya Man huku wakitaka kujua afya yake. Lakini hawakumsikia
yule Mzee akizungumzia ugonjwa wake hata kidogo, zaidi ya kuwatania. Alikuwa
mcheshi kwa kila aliyefika hapo kumuona. Hakukosa utani wakusalimia na
kuwashukuru kwa kufika kumuona.
~~~~~~~~~~~~~~~~
Wakati wanakula
kabla hawajaagana, wakamuona Malisa anacheka. Alicheka mpaka machozi. “Umeanza
Mali.” “Subiri kwanza bwana!” Akacheka tena. Halafu tena na tena. Mpaka wote
wakacheka. Hakuwa na tofauti na Man. “Dad!” Akamuita baba yake. “Unajuaga ule
usemi watu wanasemaga watoto wapo kama malaika?” Mzee Ole naye akaanza kucheka
tena kama aliyeelewa kila kitu. “Hawa huwa wanajuana wao wawili. Hapo baba
ameshamuelewa kila kitu.” Man akaongeza.
“Mimi najua kwa aina ya wale watoto wa Ole, hukusaidiki.” Baba yake
akajibu akimaanisha watoto wake Malisa mwenyewe. “Sawa sawa baba yangu.
Unaakili wewe!” Malisa akamsifia baba yake. Man, Ole mumewe, na mama yao
walikuwa wakiwaangalia tu nakucheka.
“Mtawazoea tu
hawa. Ni wao tu wawili ndio wanazijua akili zao.” Man aliwaambia Grace na mama G. “Nisikilize
Man. Sasa ule usemi wa watoto kama malaika, mimi nikawa naupinga kweli
kama alivyosema dad. Mimi si naishi na wale watoto wa Ole!” Akampiga bega
mumewe. “Hakuna jinsi ukakubali kama wale watoto ni malaika!” Watu wakaanza
kucheka upya mpaka mumewe. “Basi mimi
ule usemi nikawa naupinga tu mpaka jana nilipokutana na hawa watoto wa Geb na
Nanaa. Hapo ndipo nikaamini kweli watoto ni kama malaika.” Wote wakacheka. Liv
na kaka yake walikuwa wametulia kimya pale walipokuwa wamewekwa kwenye kiti.
“Lakini sasa
nikaamua kuwagawa hawa malaika. Si mnajuaga kuna malaika wale wa vita na wale
watoa habari njema?” Kila mtu alianza kucheka upya. “Sasa wale watoto wa Ole
wale wawili, wale ni malaika wa vita. Kazi yao kwenda kuangamiza Sodoma na
Gomora. Maombi yasipojibiwa, basi ujue watatumwa wao kwenda kupigana na mfalme
wa anga mpaka aachie majibu ya maombi ya watakatifu. Yaani wao kazi yao ni vita
tu. Hawana kazi nyingine na Mungu hathubutu kukosea kuwatuma sehemu zenye
amani.” Baba yake na Man walikuwa wakicheka sana. Mama yake, mama G na Grace
wao mpaka machozi yalikuwa yakiwatoka kwa kucheka. Mumewe alikuwa akimtizama
huku akicheka na kutingisha kichwa.
“Sasa ukija kwa watoto wa Geb na
Nanaa, wapo kama malaika Gabriel. Kutoa habari taratibuuuu! Kubariki watu.
Kujibu maombi yale yaliyojaa amani na utulivu.” Malisa alizidi kucheka yeye
mwenyewe. Yaani ukikaa nao hao watatu. Mzee Ole, Man na Malisa, lazima ucheke
tu. Kwanza huwa wanaanza kucheka wao wenyewe. Na watacheka sana. Wakikusimulia
stori yenyewe, watacheka zaidi. Uzungumzaji wao wenyewe, watacheka. Lazima
ucheke tu.
“Naweza kuja nao siku ya mahari,
ukawaona mama Magesa. Ni wale Masai haswa! Yaani wale Masai wakuruka na mshale
juu. Mimi huwa wakiniita shuleni kwao, nawaambia someni jina lao la mwisho.
Wakisoma, nawaambia basi mmepata jibu. Watoto wanadamu ya Kimasai ambayo
haijachanganywa na kabila lolote hapa duniani. Angalau wangekuwa wamechanganya,
ingekuwa nafuu labda ingesaidia kulainisha ile damu ya kimasai. Huna jinsi
yakuwaambia watulie wakaelewa.” Malisa aliendelea kuwachekesha. Mpaka inafika
muda wa kwenda uwanja wa ndege, walishazoeana. Na mama G, akaona kweli mwanae
safari hii anaenda pazuri.
v Mama G amefutwa machozi
vilivyo. Wasomi hao aliosimama nao tokea alipoachwa na Mzee Magesa, baba yao,
akahangaika mchana na usiku mpaka akafanikiwa kuwaketisha na wakuu, leo
anafutwa machozi kwa heshima zote ndani ya hoteli hilo la kitalii. Nani alijua
magoti ya Mama G, akiwa sirini leo yatamuweka mwangani kwa heshima ile!
v Geb ameshaoa,
Grace amechumbiwa kwa aina yake. Mzee Ole anataka amlipie mahari haraka amiliki
kihalali kabla hajazidiwa mahesabu. Amesema hatatulia mpaka Grace awe kwenye
familia yake. Heshima aliyopewa ni kama binti mdogo wakati ni mama wa watoto
watatu!
v Mipango
imepamba moto. Bandika Bandua. Leo Geb kapata mwenza kihalali, baada ya majuma
mawili ni Grace. Watafanikiwa kutulia!?
v James naye
amezua jipya juu ya Gozi na aliyoyafanya siku ya ubakwaji wa Nanaa. Itakuaje?
v Kwa Danny moto umeanza mapemaaa! Ila pesa
amekimbiza benki. Atakuwa salama na Sara mwenye uchu wa vitu?
v Hatima ya
Watoto wanao mlilia mama yao! Man ameliona hilo, ndio wapo kwenye mchakato
wakuwatoa kwa Danny. Hatima yao ni ipi?
Unapofikiri kuna Amani, shetani huwa halali…..
Usikose kufuatilia.
0 Comments:
Post a Comment