“Unamuwaza Danny?” Man
akauliza. Grace akavuta pumzi taratibu. Akatulia kwa muda. “Hata yeye
namfikiria. Nafikiria hatima yetu. Nini chakufanya nikitoka huko mbugani! Wapi
niende! Kwa muda gani! Je nipo tayari kuja kuishi maisha mengine bila wao! Nini
nilikosea kwake? Kama kuna kitu kibaya kilimpata, kwa nini nimemuombea na
akashindwa kubadilika? Kwa nini moyo wangu umekata tamaa mapema? Nilishawahi
kumpenda yeye kama Danny au nilipenda aliyokuwa akinifanyia nikashindwa
kufikiria, kama Geb alivyoniambia?” Grace akafikiria tena.
Akaongeza kwa upole. “Nataka
kujilaumu kama anavyonilaumu Geb, lakini najirudi.” “Geb anakulaumu nini?”
Grace akatulia kidogo. “Mwezi mmoja kabla ya kufunga ndoa na Danny, nilipata
muda wa mazungumzo naye. Nilimwambia vile ninavyomchukia Danny. Na mambo
mengine mengi. Unakumbuka nilikwambia aliondoka pale tulipokuwa tukiishi naye
kabla ya ndoa, baada ya mimi kuleta nyumbani mwanaume mwingine anioe?”
“Nakumbuka.” Man akajibu.
“Sasa hayo yote Geb ananiambia
ni kama Danny alinifunika kitambaa kwa mambo mengi aliyokuwa akinifanyia. Kwa
hiyo alipoondoka niliharakisha kumkimbilia. Nikitaka arudi aendelee kunifanyia
aliyokuwa akinifanyia, nikasahau upande wa mapenzi. Sasa najiuliza, kwani
mapenzi ni nini? Mapenzi si pamoja na mtu kukujali! Kukufanyia mambo mazuri?”
Man akanyamaza.
“Niambie Man. Mtu ukimpenda si
utamfanyia mambo mazuri?” “Umesema sahihi kabisa. Kuwa mapenzi ni pamoja na
kumjali mtu Grace. Yapo mambo mengi yanabeba penzi. Halafu pia kuna watu
wanafanya mambo mengi kwa sababu tofauti tofauti. Ni ngumu kujua kwa nini mtu
anakutendea jambo hili au lile. Ila ninachojua upendo wa kweli huwa umebeba
sifa nyingi, Grace. Mtu unayempenda ni lazima utamsitiri. Huwezi kumuanika nje,
kwa kile ulichokikuta ndani. Tena sirini! Upendo huwa hautafuti mambo yake wenyewe.
Upendo unavumilia. Upendo hauhesabu wingi wa dhambi. Hata kukiwa na sababu.
Watu tunakasirika, lakini huwa kunakujirudi sababu ya ule upendo.” Grace
akafuta machozi.
“Unafikiri na
mimi nimekosa upendo? Nimeshindwa kuvumilia?” Grace akauliza. “Swali
gumu sana hilo, Grace. Ni ngumu kujibu kwa haraka kwa kuwa ni wewe na Danny
peke yenu mmepita mlikopita na mnapita hapo mlipo. Ila sijui inakuaje pale
mwenza wako anapokukataa na kutafuta mwanamke mwingine! Hapo sijui
inatakiwa kufanya nini kwa wewe unayebaki. Ila kama akijirudi, akatubu, hilo
nalo nafafikiri ni swala jingine. Japokuwa bibilia imeruhusu kuachana
kwa kosa la uzinzi, lakini kuna kipengele cha kusamehe saba mara
sabini.” Man alimueleza taratibu.
“Ni ngumu sana.
Ni ngumu mno Man. Kuna matusi ananitukana akiwa na Sara. Sara anakuja kuyarudia
mbele yangu na mbele ya msichana wangu wa kazi. Vile Danny anavyonilinganisha
mimi na yeye, Sara huko kitandani. Ni aibu mno. Naumia nashindwa kata
kumsimulia mama yangu mzazi, kwa aibu. Nabaki nayo nikiumia sana. Nashinda hata
kuwa mama kwenye nyumba niliyojenga mwenyewe, kwa fedheha! Aibu kwa wafanyakazi
wangu ninaowalipa mshahara! Nashindwa hata kuwaongelesha kwa vile ninavyoanikwa
vibaya. Si kijana wa maua, si walinzi getini. Wote wanajua mapungufu yangu ya
ndani kabisa.” Grace akaendelea kulia. Wakajisahau walipo.
“Nyumba ni yangu
mwenyewe, lakini naogopa hata kurudi, Man. Nafikiria narudije tena pale?
Naogopa mpaka nakosa raha! Halafu kwa kawaida mimi nimuoga sana wakuwa peke
yangu. Nafikiria labda nikija kurudi, niende nikaishi na mama. Lakini napo
najihisi aibu zaidi. Jamii itaniona nimeshindwa na mtoto mdogo! Lakini najua
wazi sina nguvu za kupambana, na hata Mungu akinijalia nguvu, sipo tayari
kupambana tena. Nimekinahiwa Man. Sitaki tena. Nafikiria narudije kwa
mwanaume aliyeanika mwili wangu nje kwa kiasi hiki!? Tena kwa kunitukana sana.
Naweza kusamehe hata kabla sijaombwa
msamaha, lakini narudije kumvulia nguo mwanaume kama Danny!?” Grace
alilia kwa uchungu sana. Kila alipopata nafasi, alitoa dukuduku lake.
“Njoo hapa karibu yangu.” Grace
akajisogeza. Akamshika mkono. “Naomba nikuombe kitu. Jaribu kutulia. Unakumbuka
jana uliniambia unahisi umetengeneza rafiki?” Grace akatingisha kichwa
kukubali. “Basi naomba ujue unaye rafiki wa kweli. Katika shida na raha
tutakuwa wote Grace. Muda na wakati wowote utakaonihitaji nitakuwepo na wewe.
Naomba ujue haupo peke yako tena. Tukifika, tutapata muda wakupanga mambo
vizuri. Ili usiishi kwa shida tena.” “Na likizo yangu
ikiisha nikatakiwa kuondoka?” Grace akauliza.
“Nimekwambia nitakuwa na wewe
wakati wote.” “Wewe maisha yako, yako huku Man. Mimi maisha
yangu yako Dar. Huko ndiko naogopa hata kurudi. Sasa tukiachana itakuaje?” “Nimekwambia
tutapata muda wa mazungumzo Grace. Nimepita hapo ulipo. Tena mimi nikiwa sina
mtu wakunishika mkono kama hivi. Au hata mtu wakuzungumza naye, ila kutendwa
mabaya tu. Hatutashindwa kupata njia. Kuwa mvumilivu.” Grace akatulia.
Man akajiegemeza kwenye kiti,
akamsogeza karibu. Grace akarudia kumkumbatia kama jana yake usiku. Sema safari
hii walikuwa kwenye gari akihema karibu sana na shingo yake, kwa kuwa alikuwa
amekaa. Man akaanza kumpapasa taratibu. “Is gonna be okay,
Grace. I promise.” Alimnong’oneza na kumbusu akimwakikishia kila kitu
kitakuwa sawa. Grace akajivuta kwake zaidi. “Asante.” Grace akashukuru.
Ukisema Cha Nini,…
Grace mwanamke anayependa
kupendwa na kubembelezwa tokea mtoto. Mikononi ndio sehemu zake zakujidai. Baba
yake ndiye aliyemwanzishia hilo. Alikuwa mikononi mwa baba yake mpaka kifo chake.
Hajui maisha mengine ila kukumbatiwa na watu wamuonyeshe wanamuhitaji. Danny
amempitisha kwenye wakati mgumu ambao hakuwahi hata kudhania kwa uzuri uliokuwa
ukisifiwa na kila amtizamaye, gafla Danny anatangaza kukinahiwa! Ametoka Dar
akiwa mnyonge, ametua kwenye mikono ya Man! Mwanaume aliyekuwa na yeye
akitafuta penzi! Mungu awape nini?
Man alishachezea nywele za
kizungu kwa muda mrefu. Hakushindwa kumtuliza Grace kifuani na kumpa yakizungu.
Mabusu ya hapa na pale, bila kuvuka mipaka, yaliendelea huku wamekumbatiana,
dereva akiendelea kukanyaga mafuta. Mara kadhaa Grace alinyanyua uso kumtizama
Man wakati wanazungumza. Napo hapo Man akabusu kipanda uso, huku akiweka sawa
nyusi nyingi za Grace na kumtuliza.
Grace alitulia kama kitoto cha
paka, mikononi mwa Man, akiendelea kuchezewa nywele huku akiliwazwa kwa sauti
tulivu bila kelele kama Danny. Wote walishakuwa kwenye ndoa. Wote walisalitiwa.
Ila Man yeye tokea mwanzo aliingia kwenye ndoa aliyotegwa. Tena akiwa mtoto
mdogo. Akafungiwa ndani na huyo mama wa kizungu. Akageuzwa yaya kisha
kuhamishiwa jela alikotendwa unyama. Alitua nchini, hana hamu ya mapenzi.
Akashangaa imekuaje kwa Grace! Tena kwa
haraka vile. Malisa ndiye aliyepeleka mambo kwa haraka. Lakini alikusudia
kumvuta Grace taratibu huku akisubiria kujua hatima yake na Danny, ili na yeye
ajipenyeze kwenye moyo wake. Lakini anajikuta Grace yupo kifuani. Anafurahia
kifua chake kama yeye anavyofurahia kifua chake kulaliwa. Anatamani historia za
kilio cha Grace kiendelee ili apate sababu ya kumuweka kifuani. Mwanamke
mtulivu, asiye na papara hata na maneno yake. Leo Danny anatangaza kukinahiwa!
Mungu amjalie yeye hiyo nafasi. Ndio ombi lililobaki kwa Man.
Mambo Ya Mbugani.
Wallifika
hotelini, dereva akaegesha gari mbele ya hoteli, lakini hakuna aliyetamani
kushuka. Wakabaki wakiangaliana huku
wamekumbatiana. Wote walijua wameshawashiana tamaa njia nzima. Dereva akaamua
ashuke na kuondoka kama kumpa nafasi bosi wake. Man alirudia kumbusu Grace
kwenye kipanda uso mara kadhaa huku akimpapasa. Lakini safari hii aliongeza
nguvu kidogo mpaka Grace akahisi mikono ya kiume ikipita mwilini mwake.
Ni miezi zaidi ya 6 sasa tokea
Grace ashikwe vile na mwanaume kimapenzi. Hata hivyo mbali na Danny hakuwa
akimjua mwanaume mwingine. Mwili mzima ulikuwa ukipiga kelele ukimtaka Man
asaidie kutuliza. Man naye ni miaka mingi. Hakuwa hata akikumbuka ni lini
aliweza kuwa na mwanamke kitandani. Akatoa ujuzi wake wa kiume, akamfurahisha
mwanamke. Hisia alizokuja kuamsha Grace mwilini mwake, zilikuwa zimefukiwa muda
mrefu sana.
“Watakuwa wanakusubiria. Ngoja
na mimi nishuke nikaangalie chumba nitakachokuwa nimetafutiwa na Beka.” Grace
alianza kujitoa taratibu. “Na hapa pia nina chumba kama kile ulichompisha
Malisa na familia yake. Tunaweza kutumia wote.” Grace akacheka kidogo, akainama
kama ambaye hajui aseme nini. “Ukishindwa, mimi nitalala kwenye makochi.
Usiogope.” Man akaongeza kwa upendo huku akimtengeneza nywele zake. “Sawa.”
Grace alikubali kwa sauti ya upole huku akitabasamu. Wakatoka.
Hawakuwa na haja ya kwenda
mapokezi. Man alikwenda kwenye chumba chake moja kwa moja. Kalikuwa kajumba
kadogo kanacho jitegemea. Vinyumba vingine vilionekana vina milango miwili.
Kuashiria wanaweza kukaa wageni wawili, tofauti bila kuingiliana. Ila kutumia
baraza pamoja. Palikuwa pazuri na patulivu. Grace akaanza kujisikia vizuri.
“Mmejitahidi kuwekeza kweli!” Grace akasifia wakati Man anafungua mlango.
Alikuwa amebeba mizigo yote ya Grace. Yeye alisema vitu vyake vyote vipo hapo
kama ilivyo kule. Walipofungua, chumba kilikuwa kisafi sana. Kimetengenezwa na
kuwekwa vitu vizuri.
“Inamaana vyumba vyote vipo
hivi!?” Grace akauliza. “Nimejitahidi kuwa hivyo. Lakini hapa ni zaidi kwa kuwa
ni kama nyumbani kwangu. Sina maisha mengine ila hapa na Arusha. Nikiwa Dar,
nakuwa kwa mama na baba.” “Tena nilitaka kukuuliza wazazi wako wapi.” “Kwa hiyo
umepata jibu. Wote wako wanaishi Dar. Kasoro tu mimi ndio ninaishi huku.”
“Unapapenda?” Grace akauliza. Man akafikiria kidogo.
“Mwanzoni ilikuwa kama
inanilazimu. Sikuwa na namna. Nilipoanza kuzoea, nikaona patanisaidia kufukia
mawazo yangu hapa. Nikajichimbia kwenye kazi tu mpaka imefanyika kwangu. Hata
hivyo sikuwa na sababu yakuchagua niishi wapi hapa Tanzania. Ilikuwa popote.”
Grace akakaa kwenye kochi. “Unataka ukazunguke kidogo sasa hivi, au leo unataka
kutulia tu ndani mpaka kesho?” “Nimependa wazo la pili. Leo nikae tu humu
ndani, nipumzike. Kesho ndio nitoke.” Man akaenda kukaa pembeni yake.
“Basi nitarudi baadaye kidogo.
Ngoja nipite niangalie kama mambo yamekaa sawa. Nitarudi na chakula.” “Sawa.”
Grace akaitikia. “Kuna kitu chochote maalumu unataka kula?” Grace akafikiria
kidogo. “Hapana. Chagua chochote tu.” Akabaki akimwangalia. Grace akashangaa
hasimami tena. Akacheka. “Nimefurahi upo hapa na mimi Grace. Naamini tutakuwa
na wakati mzuri.” “Hata mimi. Nimefurahia mikono yako. Mwenzio napenda
kubembelezwa.” Man akacheka sana.
“Usinicheke bwana!” “Nilikuona tokea siku ya kwanza. Nikajiambia jamaa
atakuwa anafaidi! Umekaa kama mtu wakushika wakati wote. Na unatia raka ukiwa
mikononi. Unautulivu fulani ambao unaambukiza mtu anayekushika.” “Kwa hiyo na
leo usiku utanikumbatia?” Grace akauliza huku amefunika macho akicheka.
Man alizidi kucheka. “Ila
usinifikirie vibaya. Mbali ya Danny, wewe ndio mtu wa pili kumruhusu
anikumbatie na kunishika hivyo. Sio kila mtu nakuwa namruhusu.” Grace
akajitetea.
“Mimi sijui mambo ya nyuma.
Ninachojua, Mungu wangu amenirehemu.” Grace akacheka sana. “Usije ukajuta na
wewe kama Danny.” “Huwa siongozwi na hisia Grace. Ingekuwa hivyo sasa hivi
ningekuwa na msururu wa watoto na wanawake.” “Sasa unaongozwa na nini?” Grace
akauliza. “Nitakuja kukwambia nikirudi.” “Kwa hiyo nisilale nikusubirie uje
unikumbatie huo usiku?” Man akacheka tena. “Kwani natakiwa kusubiri mpaka
usiku?” “Sasa si ndio utakuwa umemaliza kazi zote? Tunakaa kitandani,
tunatulia. Hamna kutoka tena.” Man akacheka.
Akamsogelea. Kwa mara ya kwanza
akambusu mdomoni, lakini kidogo tu. “Nitakuja kukukumbatia.” Grace akacheka
huku ameshika midomo yake kwa vidole. “Asante.” Akashukuru taratibu. Macho ya
Grace yalikuwa ni ngumu kumruhusu mwanaume amwache hivi hivi hasa akiwa
amekukaribisha. Akambusu tena kwa haraka mdomoni. Grace akacheka kwa deko. Man
akaona arudie tena, ila safari hii apunguze haraka. Akambusu midomo ya nje kwa
muda kidogo huku amemshika shingoni. “Asante Man.” Grace akashukuru tena wakati
Man akimwachia.
“Nimepatwa na uzito wa kutoka.
Natamani kubaki hapa na wewe.” “Usiwe na wasiwasi. Mimi nipo hapa nakusubiri.”
Grace aliongea kwa upendo, akibembeleza.
Hata yeye alionekana anahali mbaya. Man akafunga macho nakujiegemeza kwenye
kochi. Grace akajisogeza kifuani. Akamkumbatia tena. Man akavuta pumzi kwa
nguvu akafungua macho. Wakabaki wameangaliana. Kwenda ameshindwa, kuendelea
ameshindwa.
“Hali yangu mbaya Grace.
Sijafanya mapenzi zaidi ya miaka 8. Na sijafanya mapenzi nikaridhika zaidi ya
miaka kumi.” “Pole.” Grace akamuhurumia. “Natamani nibaki na wewe hapa ndani
hata siku tatu tu. Unafikiri tutakuwa tumeharakisha sana, pengine ungehitaji
muda zaidi? Samahani Grace. Najikuta nakuwa muwazi sana kwako mpaka naogopa.”
“Lakini hivyo ndio nafurahi Man. Asante. Ila nashauri ukaweke mambo sawa, ili
tukiamua kujifungia humu ndani isiwe usumbufu tena.” Bado Grace alikuwa
amemkumbatia.
“Naomba basi nikubusu hata kwa
dakika mbili tu ndio nitoke.” Grace akatoa tabasamu la kukubali. “Lakini nataka
nikubusu kwa uhuru wote, Grace.” “Ndio unatakaje?” “Nikuweke kitandani,
nikubusu nikiwa nimetulia na kwenye nafasi.” “Okay.” Grace akajibu kwa upole.
Wakatoka pale kwenye makochi, wakahamia kitandani.
Grace akavuta mto akajilaza.
“Lakini Grace, mimi huwa si busu tu midomo. Napenda kuwa huru.” “Okay.” Grace
aliendelea kukubali taratibu huku akifikiria aina gani ya busu anayotaka
kupewa. Tayari mwili wake ulikuwa ukichemka. Man akaanza utundu wake pale.
Alinyonya midomo ya Grace, akaja shingoni. Masikioni. Akarudi midomoni. Shingoni
kuelekea kifuani ambako alishuka taratibu huku akiminya minya mwili wa Grace
taratibu. Miguno na mihemo ya Grace ikaanza kuchanganya. Aliharibu alipofikisha
midomo yake kwenye sehemu juu ya matiti ya Grace, ambayo yalikuwa bado kwenye
shati, ndani ya sidiria. Grace alianza kuhangaika. Man akajua anataka
amfungue.
Akarudi midomoni nashingoni
wakati akimtoa nguo taratibu. Alirudisha macho kifuani wakati amemalizia
kumfungua sidiria nyuma ya mgongo. “Waw!” Man akapagawa baada ya macho yake
kutua kwenye matiti ya Grace. Ilimchukua zaidi ya dakika mbili kutoka kifuani
kwa Grace. Alihama titi moja hadi jingine. Kulia na kushoto kama mtoto mwenye
njaa kali, mpaka akasahau midomo.
~~~~~~~~~~~~~
Kwa kuwa walishakuwa
wamewashana tamaa tokea njiani, hakuna jinsi angemuacha Grace vile, eti Man
akatoka kwenda kusimamia kazi. Usiku uliopita walijikaza, wakalala wakiwa
wamekumbatiana. Miili imegusana kwa karibu vile! Man alishamtamani huyo Grace
tokea anamwona kwa mara ya kwanza. Alitamani kugusa huo mwili mara nyingi tu.
Grace naye alishamtamani Man. Alishapagawishwa na umbile lake. Ni kama alikuwa
mwanaume wa ndoto zake. Kinachowazuia ni nini!? Grace akasahau kabisa maombi ya
kufunga na kuomba juu ya Danny.
~~~~~~~~~~~~~
Ndani ya muda mfupi sana,
wakawa kama walivyozaliwa pale kitandani. Man akigugumia na yeye. Kila
aliposhika, macho yake yaliitwa na pengine. Man akabaki kama amechanganyikiwa
na Grace pale kitandani. Akaona ili asionekane mjinga, kwa umbile lile
alilofanikiwa kuliona kwa macho, aingie tu ili roho yake itulie. Alikwenda
kumkumbatia Grace kwa mkono mmoja huku akipenya taratibu. Alishamlainisha kwa
mabusu ya kila mahali na unyonywaji ambao Grace hakuwahi kufanyiwa hivyo tokea
anazaliwa. Danny ni mtu wa kinyaa na Grace alikuwa mwanamke wake wa kwanza.
Mtoto aliyelelewa na mapadri, hakuwa na mengi. Sasa huo mwili ukakutana na Man.
Mtoto wa uzunguni! Alinyonya huo mwili kana kwamba anakula ice cream. Grace
mkimya sio huyu kitandani kwa Man. Man aliutenda huo mwili wa Grace, akabaki
akilia nakuomba rehema ya Man.
Kwa mara ya kwanza baada ya
miaka mingi, Man anamwingilia mwanamke. Tena mweusi wa rangi anayoipenda yeye! Alitua
ndani huku roho yake imejawa hamasa. Alijitahidi kutulia huku akisugua meno,
akawa anapanda na kushuka taratibu bila papara. Alikuwa amemkumbatia Grace kwa
mkono mmoja huku akimsugua taratibu. Kilio alichokuwa akikitoa Grace, Man
akajua anachokifanya mwilini mwa mwanadada huyo, kinapokelewa. Mara kadhaa
aliinama kunyonya midomo yake, shingo na masikio huku akifanya naye mapenzi.
Alikuwa akitoka midomoni kwenda shingoni na masikioni huku akiendelea kufanya
naye mapenzi taratibu na kwa hisia zote. Mkono ule mwingine ulikuwa na kazi ya
kutembea mwilini mwa Grace.
Alishika kiuno, huku akimnya
minya hips zake kwa uchu. Grace aliendelea kunung’unika kwa huba pale
kitandani. Man aliongeza nguvu kwa kadiri ya uhitaji wao. Baada ya muda
wakutosha wa mapenzi, Man alipomfikisha Grace kileleni, akaridhika kuwa
ameridhika ndipo na yeye akamkamata kwa nguvu, Grace akahisi ameongeza nguvu si
kawaida maana hata kalio alilokuwa amekamata, alilishikila haswa akiwa juu yake
mpaka akamalizia. Wote wakawa wamekata kiu kwa muda huo. Man akamvutia kifuani,
wakabaki wanahema.
Grace alimbusu mara kadhaa
kifuani akimshukuru. “Asante.” “Karibu. Na mimi nakushukuru Grace. Asante sana.
Naomba usiondoke hapa kifuani, nilale kidogo.” “Okay.” Grace akajivuta karibu
zaidi. Man akambusu midomoni. Hapo hapo akalala. Grace akabaki amelala kifuani
kwake, amejawa na furaha. Akafurahia vile alivyoweza kuenea pale kifuani kwa
Man. Akafurahia ile hali ya utulivu. Aina ya mapenzi aliyofanya naye. Grace
aliyejua aina ya mapenzi ya Danny tu, akaonjeshwa penzi jingine lisilo na
kinyaa. Man hakumpa hata style za ajabu. Moja tu, lakini alimtenda vilivyo.
Hapakuwa na papara wala kinyaa.
Alimtuliza hapo kitandani. Akatembeza midomo kila mahali na kumuacha Grace
hajitambui. Alijawa na furaha. Hakuna jinsi ungemwambia kuondoka kwa Danny si
uamuzi sahihi, akakuelewa. Hata kama ingekuwa malaika ametumwa kumwambia hivyo,
asingesadiki tena
~~~~~~~~~~~~~
Zilipita siku tatu mfululizo,
Man na Grace wakihudumiwa humo ndani bila kutoa hata mguu nje. Kwa muda mrefu
sana tokea aanze hiyo kazi au apokee majukumu kutoka kwa baba yake, Man aliweza
kumwachia kijana mwingine majukumu yote nakutaka aachwe kabisa apumzike.
Familia yake wote walijua yupo na Grace kitu kilichomfurahisha zaidi Grace
kujua amepokelewa vile alivyo na kwamba ni mama, lakini halikuwa tatizo
kwao.
“Sasa kama huyo sio Mungu amejibu maombi yangu ni nini?” Grace
aliwaza asubuhi hiyo akiwa na Man pale chumbani, akimsomea ujumbe kutoka kwa
mama yake. Alituma ujumbe wa kuwatakia mapumziko mema. Hakuna jinsi yakueleza
furaha ya Grace. Ilionekana mpaka usoni. Muda wote alikuwa mikononi kwa Man,
akipapaswa. Mabusu ya hapa na pale ndio yalikuwa hayahesabiki kwani walianza na
kumaliza kila wakati.
Damu
Nzito,..
Ilikuwa siku ya ijumaa, mida ya
saa nane mchana, Grace na Man wakiwa katikati
ya mapenzi, simu ya chumbani kwa Man iliita. Man alikasirika sana. “Ni nani
anapiga na wakati nimeshawaambia labda iwe muhimu sana?” Grace akacheka.
“Pokea. Labda ni muhimu.” Man akanyoosha mkono akapokea. “Kuna nini?” “Ni simu ya Grace. Kuna mtu
amesema ni lazima azungumze naye.” Man
akakunja uso, akamwangalia Grace. “Nini?” Grace akauliza. “Simu yako.” Man
alionekana kuishiwa nguvu kabisa.
Grace akavuta shuka,
akajifunika vizuri, akasogelea simu. Akaivuta karibu. “Halow!” Grace aliitika kwa
upole. “Subiri.”
Muhudumu akamjibu. “Grace!”
Akasikia sauti ya Geb. “Umenishitua
bwana!” Grace akalalamika. “Wewe ndio unanitia wasiwasi G. Kwa nini
unafanya hivyo? Uliniahidi nini?” Geb
alilalamika na yeye. “Samahani.
Nilisahau!” “Wewe sio msahaulifu G. Umepuuza.” Grace
akacheka. “Usicheke bwana!
Mama pia anawasiwasi.” “Msiwe na wasiwasi mimi nipo salama. Kwanza nimepitisha
siku..” Grace akanyamaza. Akakumbuka alitakiwa ampige simu siku ya
jumatano.
“Samahani Geb. Basi kesho nitapiga.” “Upo salama?” Geb
akauliza. “Nipo salama. Vipi
wewe na watoto?” “Tunaendelea vizuri.” Geb akajibu. “Na Nanaa?” Grace akauliza tena. “Namshukuru Mungu hajambo.” Geb
akajibu. “Umeshamuomba
umuoe?” Grace akauliza. “Hata akikubali nitataka muda wa kwenda naye kwenye fungate.
Nani nitamuachia kazi?” “Hapana Geb. Hiyo isiwe sababu. Kwanza tumeweka mfumo
mzuri sana ambao mimi au wewe tunaweza kufuatilia mambo ya kazini tukiwa mbali.
Sio lazima tuwepo hapo.” “Sasa unataka niwepo kwenye fungate huku nafuatilia
mambo ya ofisini? Ungekuwepo hapo sawa. Lakini hata kupiga simu kutujulisha
kuwa upo salama, inakuwa shida!” “Ni mara moja tu Geb na wewe! Na nimekuomba
msamaha kaka yangu. Kwani hujanisamehe?” Kimya.
“Geb jamani! Utaanza kuninyima raha.” “Basi Grace. Usije
ukaanza kulia. Nahisi nimekuwa na hamu na wewe.” Grace akacheka. “Hata mimi nina hamu na wewe.” “Si urudi
sasa?” “Bado nataka muda Geb.” “Mbona unasikika kama huna matatizo?”
Grace alicheka sana. “Hukuondoka
na kicheko hicho Grace! Naona umeshapumzika inatosha. Njoo bwana na mimi nioe.”
Grace na Geb, ni watu waliozoea kuwa karibu wakati wote. Japokuwa
usingewakuta wakiongea sana, lakini kila mmoja alithamini uwepo wa mwenzake.
“Wewe zungumza na Nanaa. Akikubali hata kesho, mimi nitarudi
kwenye harusi yenu na nitachukua vitu vyote vitakavyonisaidia kuendesha mambo
ya ofisini ili wewe utulie huko kwenye fungate. Unajua siwezi kukutupa kipindi
unachonihitaji Geb. Nitakuunga mkono kwa kila hali. Lakini sipo tayari kurudi
kwa sasa. Nimekusudia kuwa mbali na hapo kwa hizo siku 30. Acha nione nini
kitatokea baada ya hapo. Naomba niunge mkono katika hili.” “Sawa.” Geb
akaitikia.
“Sasa utamuomba Nanaa?” Grace akauliza. “Natamani sana kumuoa kabla hajajifungua.”
“Sasa kinachokuzuia ni nini Geb? Unampenda sana huyo mtoto.” Geb
akanyamaza. “Huwezi kuishi
bila Nanaa. Nakujua Geb. Heri umfanye awe mkeo kihalali, mmalize hilo mtulie.”
“Tatizo sio mimi Grace. Ni yeye. Anajihisi kama sio msafi kwa kuwa amebeba
mtoto wa Malii!” Geb akaongea kwa uchungu kidogo.
“Huu ndio wakati wa wewe kumuonyesha kuwa hata aweje, wewe
bado unampenda na kumuhitaji. Hakuna kitu atafurahia kama akiona unamuoa vile
alivyo. Mwambie hujali kama amebeba mtoto wa Malii au vipi. Unamtaka yeye.”
“Nimemwambia G!” “Hapana Geb bwana! Acha ku sound kama umekata tamaa tayari, wakati mimi nakujua wewe ni mtu
ambaye hushindwi na jambo! Acha kukata tamaa na kukubali Nanaa ambaye yupo
katika hali hiyo ndio awe muamuzi wa maisha yenu wote na watoto! You always manage to stay on top
of all games. Inakuaje sasa?”
Geb akanyamaza.
“Unanisikia Geb? Na ukute wakati mwingine anakujaribu kujua
upo tayari kwenda naye umbali gani. Lazima umuonyeshe hata kama maji yana kina
kirefu kiasi gani, upo tayari kuzama naye. Unanisikiliza lakini.” “Nakusikia.
Sasa akikubali, utakuja? Maana sitaki kuwa peke yangu siku hiyo.” “Nakuahidi
nitakuja Geb. Nitaanza kwa kumuomba msamaha hata kwa ujumbe, halafu nisubiri
nione atajibu nini. Akisamehe na kunifungulia mlango, nitakuja hata kusaidia
kumtafutia nguo za harusi. Mkikamilisha jambo lenu, na mimi nitarudi mapumzikoni.”
“Asante G. Basi nitazungumza naye.” “Nakuombea ufanikiwe Geb.” “Asante.”
Wakakata simu.
~~~~~~~~~~~~~
Man alikuwa akimsikiliza jinsi
anavyozungumza na kaka yake. “Mnaonekana mpo karibu sana na Geb!” Grace
akacheka. “Ni pacha mwenzangu. Na ananipenda sana Geb. Hawezi kuniona nalia.
Tokea tupo watoto. Anaweza kufanya chochote kwa ajili yangu. Ni kama baba
kwangu.” Man akacheka. “Kwa nini anakutafuta?” Grace akamsimulia makubaliano
yao ya kumpigia simu mara moja, kila baada ya siku tatu. Man akacheka.
“Hivi anajua kama wewe ni dada
yake?” “Anachukia hiyo kitu! Kwanza hataki hata nimkumbushe hivyo au mama
amkumbushe. Hataki hata kuzungumzia udogo wake kwangu. Anatamani mimi ndio
ningekuwa mdogo.” Wakacheka. “Ni vizuri kupata watu wanao kufuatilia kuliko
ungekuwa peke yako kwenye kipindi hiki kigumu.” “Lakini hata awe karibu yangu
kwa kiasi gani, unajua siwezi kumwambia yeye kila kitu. Na mama ndio kabisa.
Namlaumu kwa kumleta Sara kwenye maisha yetu. Najua na yeye anajutia, lakini
amenitenganisha mimi na wanangu.” Wakaanza kuongea.
Grace alisimulia mambo mengi.
Huku akilia, kulaumu na kusononeka. “Lakini mimi naona unamlaumu mama bure
Grace. Mbona Geb aliyeletewa huyo mwanamke asimchukue, halafu Danny kwa kumuona
tu akamchukua?” Grace akafikiria. “Inamaana kama asingekuwa Sara, basi angekuwa
Jamila au Jane au Yusta! Imekuwa Sara, kwa kuwa alikuwa karibu na yeye
alikuwa kwenye mawindo.” Man akaendelea.
“Unasema mama alimfukuza Sara. Umeshajua ilikuaje Danny yeye akampata huyo
Sara? Inamaana walitafutana. Na Danny akakubali kumpokea yeye.” Man
akasisitiza.
“Usitake kuniambia eti leo
ugomvi wa Malisa na mumewe, halafu mama Ole akaingilia, kumtetea mtoto wake
Malisa, eti wewe leo ukufanye uanze
kutafuta mahusiano mengine mbali na mimi kwa sababu mimi nilijua, halafu
sikuongea kitu! Useme unawaadhibu ndugu zangu kwa kupitia mimi! Kweli Grace?
Wewe inakuingia akilini au alikutafutia tu sababu?” Man ikabidi awe muwazi.
Grace akabaki akifikiria.
“Imekuaje sasa Geb na Nanaa
tena wako pamoja?” Man akahoji na kumtoa Grace kwenye mawazo. “Sijawahi ona Geb
akipenda, kama alivyompenda huyu mtoto.” Man akacheka. “Ukisema mtoto,
unamaanisha nini?” “Nanaa ni mdogo sana kwetu. Halafu kazuri kama katoto. Hata
watoto anaomzalia Geb, utapenda kuwaangalia tu. Wazuri sana.” Man akacheka.
“Ndio maana Geb hawezi kuishi bila yeye?” “Sio hivyo tu. Katika watu
wanaomjulia Geb, ni Nanaa. Anamjulia sana, hata mimi huwa sijui anawezaje.
Yaani kipindi cha miezi mitano waliyokuwa wametengana, Geb akiwa amemkasirikia
Nanaa, Geb alikonda akawa kama babu mzee. Ungemuona, ungesema ana upungufu
wa kinga mwilini. Ni kwa kuwa Nanaa hakuwepo kwenye maisha yake.” Akamsimulia
Man mwanzo mpaka mwisho wa mahusiano ya Geb na Nanaa.
“Hawezi kulala usingizi mzuri,
wa masaa mengi mbali na yule mtoto. Yaani Nanaa akiumwa akalazwa, Geb anahama
nyumbani, anahamia hospitalini. Unaweza kufika asubuhi kumuona mgonjwa,
ukamkuta Nanaa amemkumbatia yeye Geb, kwenye kitanda hapo hospitalini, amelala
utafikiri yeye ndio mgonjwa!” “Haiwezekani Grace! Yaani analala wodini?” “Ili
asikatazwe na mtu, au asiingie aibu, inamlazimu kumpeleka Nanaa hospitali zile
za ghali, tena atake alazwe chumba cha peke yake. Ili na yeye aponee hapo
hapo.” Man alicheka sana. “Haiwezekani Grace!” “Sisi wenyewe tulikuwa
tunashangaa, mpaka tukawazoea.” Walitumia muda mwingi kufahamiana. Man
alimueleza mambo ya kwao na yeye Grace akamueleza kila kitu cha kwao.
Geb na
Nanaa.
Geb akapiga simu kwa Nanaa mara
baada ya kuagana na Grace. “Hivi nilipoondoka nilikwambia nakupenda?” Nanaa
akacheka sana kisha akajibu. “Mimi
hata sikumbuki!” “Basi nakupenda Nanaa.” “Asante Geb.” Kimya. “Kweli Nana?” “Nimesema asante,
hujasikia?” “Hayo ni majibu ya jumla sana bwana.” “Ukija, nitakupa jibu
jingine. Usichelewe kurudi sasa.” “Utanifanya nirudi sasa hivi.”
Nanaa akacheka sana. “Fanya
kazi dad. Eti Liv?” Nanaa akampa simu Liv. “Bye dady!” “Mbona ananiaga kabla ya salamu?” Geb
akauliza Nanaa akacheka.
“Anamfundisha Magesa kupanga blocks. Nimemchoza makusudi kwa
kuwa wamenitenga.” Geb akacheka. “Na asivyopenda kusumbuliwa akiwa na mambo yake huyo!”
“Kamkaba Magesa wangu! Mwanangu hana raha! Kila akiondoka, anamfuata anamwambia
lazima ajifunze. Sasa unamjua Magesa alivyo na mambo mengi. Mambo ya msingi na
yeye, vitu viwili tofauti. Raha yake yeye ashike kila mahali, sio akae chini
afanye jambo moja.” Wakacheka.
“Mnafanyaje sasa?” Geb akauliza. “Tupo tu. Wametoka sasa hivi kusafisha
humu ndani, ikabidi kuwatoa watoto nje. Dada akiwa na pajama zake hivyo hivyo.
Wamecheza hapo kwenye mabembea. Hapa nasubiri amalize shule yake kwa Magesa,
akaoge. Maana kila nikimwambia twende tukaoge, ananiambia ‘subiri kwanza mama!’ zaidi ya dakika 20 sasa. Mwenzie nilishamuogesha tokea
asubuhi, yeye kachelewa kuamka kama kawaida yake. Anataka amueleweshe Magesa,
Magesa anaona anapotezewa muda, basi hawamalizi.” Geb akacheka.
“Nawatamania.” “Lazima. Kwa nyimbo hizi za ABCs zinazoimbwa
kuanzia dada akimka mpaka tukilala! Lazima utamani kuwepo humu ndani.” Geb
akazidi kucheka. “Hapa kichwa
kimejaa nyimbo za akina Diego.” Geb akaongeza. “Mwenzio naimba za Sofia bila kutarajia.
Kila mdomo ukifunguka naimba ‘Sofia the Great!’.” Wakazidi kucheka. Kila
Liv alipokuwa akiamka, alihakikisha kila tv ya humo ndani inawashwa cartoon
zake. Hakuna kinachoendelea ila mambo ya kitoto tu. Wakaendelea kuzungumza huku
wakicheka.
~~~~~~~~~~~~~
Japokuwa hawakurudi kufanya mapenzi,
lakini walilala pamoja. Amani na furaha vilitawala kati yao. Geb akawa mtulivu
sana, hata Nanaa akawa akishangaa jinsi alivyobadilika asijue na yeye
alishaonjeshwa joto ya jiwe akajifunza, hasira hasara. Mungu
alimrudishia utulivu hata na kwa watoto wake pia. Aliweza kurudi kwenye
mazingira aliyokuwa akiyafurahia hakuna sababu asiwe mtulivu. Kama kawaida
yake, Nanaa alikuwa akienda kumpokea kila alipotoka kazini. Kila akishuka
kwenye gari, alikutana na mapokezi ya kufurahisha na kumfanya awe anatamani
kurudi nyumbani kila anapochoka na majukumu ya siku.
Nanaa na
wanae wanakuwa wakimsubiria na akafanya tukio la kumpokea ‘dad’ ni kitu
cha kufurahisha sana mpaka wanae wakawa wakisubiria kwa hamu. Akishafika Geb
basi watamshangilia kwa furaha, watapata mabusu kutoka kwa baba yao. Nanaa atabeba
chochote alichokuja nacho Geb, yeye Geb anabeba watoto.
Anaweza kurudi nao kwenye
mabembea ya hapohapo kwenye apartment wacheze tena kidogo. Au kama hajachelewa
au hajachoka, basi anaweza kuwapeleka sehemu nyingine kama kwenye mgahawa mzuri
wenye sehemu ya kuchezea watoto, wakati Nanaa akila kama kawaida yake haishiwi
na njaa kama mwanae Magesa. Au mara nyingine humpeleka kumfundisha kuendesha
gari uwanjani. Inategemea muda atakaorudi nyumbani na hali yake, au watoto wao.
Upendo wa kweli ulionekana
katikati yao. Ila Nanaa alijua wazi Geb anateseka kuwa mbali na mama yake.
Japokuwa alimchagua yeye, lakini alijua wazi analipa garama ya kuwa mbali na
mama yake. Hakujua wanaonana wakati gani, ila akaacha kuchukua watoto na kwenda
nao kwa bibi yao. Hakuwa akiaga kama anakwenda, ila alijua wanaonana na
kuwasiliana tu.
Ni kweli Nanaa alikuwa
amemkasirikia sana mama G. Lakini ni mtu ambaye walikuwa naye karibu sana. Mama
G alimpenda Nanaa, hakuwahi kumuonyesha ubaya mpaka kwenye tukio la ubakwaji
wake. Tokea anahamia kwao, mpaka anamuita amsaidie maswala ya Liv wakati amezaliwa
na yeye ana mitihani, mama G amekuwa upande wake tu bila unafiki ila
upendo usio na hila. Mpaka Malii alipoingiza roho chafu sana siku ile usiku.
Roho chafu iliyomwingia kila mmoja wao aliyekuwepo pale, nakuwaacha
hawajitambui ila kusambaratika vibaya sana.
~~~~~~~~~~~~~
Bado James hakuwa amemtafuta Nanaa, huo ulikuwa
mwezi wa sita tayari wanatafuta wa saba kitu ambacho si kawaida yao. James
hakuwahi kuacha kumtafuta Nanaa tokea analetwa nyumbani kwao ni kachanga
kabisa.
Haya, alivunja ndoa na mahusiano ambayo
hayakutegemea kuvunjika kamwe. Grace na Danny. Ndoa yao haikuwa ya ajabu sana.
Kulikuwa na mapungufu yao, lakini ni kama kila mmoja wao alishajiamulia ni
mpaka kifo. Hata Grace hakuwa hata na wazo la kumuacha Danny japo alimuona na mapungufu
mengi aliyoyajua yeye. Japokuwa alijua kuna mambo fulani watu hufanya kwenye
mapenzi, Danny hakuta kuyafanya kwa kinyaa akishangaa ni kwa nini watu wawe
wanafanya mambo kama hayo, akiona ni uchafu, Grace ambaye hakuwahi kufanyiwa
hivyo maishani, akakubaliana na mumewe, ndoa ikaendelea bila shida. Mpaka
alipokuja Malii na kumwaga hiyo roho chafu, iliingilia hiyo ndoa yao pia. Ilivunjika
hata usingeweza amini kama ni wale ambao walipenda kukaa pamoja kila wakati.
Hiyo roho chafu ilipenya mpaka
nafsini kwa Danny kiasi cha kumfanya kutilia mashaka kila kitu. Yale mazuri
yote aliyokuwa akijisifia kwa watu juu ya mkewe, ndiyo hayo hayo akayatumia
kumchafua nayo.
Upande wa
kuvunjika urafiki na wema wa Nanaa wote ukaweza kusahaulika kwa usiku mmoja tu ambao
Malii alitoa siri ya kuwa alishamvulia nguo. Ilikuwa ni kama neno la ajabu
sana. Likatiwa nguvu ya ufitini, ubaya
uliopita kiasi, uuwaji ndipo hiyo roho ikamwingia na mama G, na kumtibua nafsi
yake kupita kawaida na kumchukia Nanaa kupita kiasi. Hata akaamua kumtafutia
mwanae, mwanamke mwingine ambaye hata hakumchunguza. Akaamua kumuunganisha na
Geb, aliyezaa na Nanaa ambaye alikuwa akimpenda na kumpongeza kwa kumzalia
wajukuu wawili. Alisahau kabisa maneno yake yeye mwenyewe. Alipomkaripia Geb na
kumwambia mwanae kwa kinywa chake mwenyewe kuwa, hakuna mwanamke mwingine
atakayekuja kuishi naye mle ndani isipokuwa Nanaa. Yote hayo mama G
aliyasahau, akamkimbia Nanaa.
Haikumuacha salama na Nanaa
mwenyewe aliyetendwa ubaya. Baada ya yote hayo, Nanaa akamchukia kabisa mama G. Akasahau yooote
ambayo alishawahi kumtendea. Akabakiwa na kosa la kumnyang’anya watoto na kumtafutia Geb mke. Gafla yeye ndio akawa ameshika
makali. Mama G akaachwa kwenye nyumba peke yake. Bila Geb, wala wajukuu ila lawama pande zote.
Grace akimlaumu kwa
kumtafutia mumewe mke. Danny akimlaumu kwa kupokonya watoto wa
Nanaa. Japokuwa Geb hakumwambia mama yake, ila alijua wazi na yeye anayo
malalamiko yake juu yake. Akajua mpaka muda huo anajua kwamba alificha barua ya
Nanaa. Na japokuwa hakurudia kuzungumzia tena wala kumlaumu tena ila
alishamwambia anajua alikuwa akizuia Nanaa asishike wanae. Geb alizungumzi mara
moja tu, hakurudia tena kulaumu.
Hata watoto hawakuachwa salama.
Mahusiano ya watoto wa Grace na mama yao yalivunjwa kiajabu sana. Urafiki wa
Fili na Liv ulivunjika pia. Hawakuwa wakionana tena. Na hata walipokuwa
wakikutanishwa, Liv anakuwa akimlilia mama yake, hawezi hata kumtizama Fili.
Ikajengeka chuki kwa Liv hakuwa akimtaka tena bibi aliyekuwa akimlea kwa upendo
sana, sababu alimchapa akiwa amechoka na kuwaona wanaishi nao bila mama yao
ambaye wakati wote walipokuwa wakikutanishwa, waliachana na mama yao akiwa analia.
Moja kwa moja Liv akajua wao ndio wanahusika na kumtenganisha na mama yao.
Akawachukia mpaka baba mtu alipomrudisha kwa mama yake, hapo urafiki ukarudi.
Magesa naye ameshaonja mikono ya mama yake, akajua utamu wa mikono ya mama,
gafla akamkataa bibi yake aliyemlea toka anazaliwa. Ikawa mahusiano ambayo
hayakuwahi kufikiriwa kuvunjika, yakavunjwa kwa dhambi moja tu iliyoingia kati
kati yao.
~~~~~~~~~~~~~
Jioni hiyo Geb akarudi,
akamkuta Nanaa amepooza tofauti na utani waliokuwa wakitaniana asubuhi kwenye
simu. Akaanza kuwaza ni nini amekosea tena! Ahadi ya kuja kuambiwa kama
anapendwa tena, mbona imegeuka kuwa huzuni! Geb akaanza kujiwinda kila
anachoongea ili asiharibu zaidi. Alichelewa kidogo kutoka kazini. Akafika
watoto ndio wanaandaliwa kwenda kulala. Akasaidia kwa juhudi zote huku akimsihi
apumzike.
“Leo nimechelewa kidogo, kulikuwa kuna
kitu narekebisha. Nilitaka kusimamia mimi mwenyewe ili nihakikishe wanamaliza.”
“Pole.” Nanaa akajibu kifupi wakiwa wamebaki wao wawili tu hapo chumbani.
“Inabidi uanze kutembelea miradi yote Nanaa. Ili ujue ni nini tunamiliki.
Kwa mfano leo nilikuwa kwenye ile bohari kubwa, nikisimamia ukarabati. Hasa
umeme. Niliona bili imeongezeka. Kumbe ni nyaya tu ndio zimechakaa. Nikaamua
kupaweka nyaya mpya, ili nione kama kutakuwa na mabadiliko yeyote.” Geb
aliendelea kujiongelesha huku amejilaza kwenye mto, Nanaa amejiegemeza kwenye
kitanda akimchezea nywele.
“Sijui
hata kama amesikia nilivyosema miradi yetu! Yaani na yeye nimemuweka.” Geb
akawaza wakati akimwangalia Nanaa, alipokuwa akipitisha kidole kwenye nyusi zake
nyingi huku akifikiria. Alionekana kuna jambo anafikiria.
“Nanaa!” “Pole sana.” “Acha
kunidanganya bwana. Wala ulikuwa hunisikilizi.” Nanaa akaanza kucheka. “Unawaza
nini?” Nanaa akatulia. “Eti mpenzi wangu?” Gafla akamuona machozi yanatoka
akajifuta. “Vipi? Ni nini nimekosea?” “Hivi unajua
karibia watoto wangu wote ni mama yako ndio amenisaidia tokea wanazaliwa?” Geb
akanyamaza asijue anapoelekea. “Nakumbuka alivyonisaidia
kipindi cha Liv. Leo nimekumbuka vile nilivyokuwa nikiogopa na nilikuwa sina msaada,
akaja kunisaidia mpaka nikamaliza mitihani. Unajua alikuwa halali anahangaika
na Liv tu! Mpaka nilikuwa nikimuhurumia. Asubuhi na mapema alikuwa anakuja
kukaa na sisi mpaka usiku.” Nanaa akaendelea kuongea.
“Unakumbuka
uliponifukuza ukanifungia nje? Nilikuwa nimejaa damu. Mama akanisafisha tena
bila kinyaa! Alinilea vizuri sana. Aliishi na mimi kwa upendo sana.” Nanaa
akaendelea. “Unakumbuka kipindi alipozaliwa Magesa vile
alivyokuwa akinipongeza kwa kumzalia Magesa? Akamlea mtoto wangu mimi nikiwa
mgonjwa. Akawa ananiletea wanangu asubuhi na jioni bila kuchoka.” Geb
kimya. Aliogopa hata kupenyeza neno asije kuharibu.
“Sijui alipatwa
na nini!? Akanigeuka kwa kosa lakutomwambia kama eti nilimvulia nguo Malii! Ni
kama mtu aliyekuwa akinitafutia sababu yakunifukuza.” Hapo
Geb akaanza kuona anataka kurudi kwenye mabaya. Akatamani akumbuke kitu kingine
kizuri. “Lakini Geb, kila nikifikiria maisha yangu na
mama. Vile tulivyoishi naye kwa upendo. Ni kama alikuwa zaidi ya rafiki.
Tulikuwa tukicheka kila tukionana. Unakumbuka vile alivyokuwa akihangaika
kuleta vyakula kule hospitalini hata kabla sijajifungua?” Nanaa
akauliza tena.
“Wewe hukumbuki?” Kimya.
“Au ni mimi tu kwa kuwa nimemmiss?” Alivyosikia
tu hivyo akadakia. “Nakumbuka sana. Nakumbuka.” Nanaa akazidi kulia. “Nina hamu naye, japo ameniudhi sana.” Geb akatamani kumwambia
amtafute lakini akaona ni heri anyamaze kwanza. “Na
ninachoogopa ni kumkaribisha sasa hivi tena kwenye maisha yangu. Alinipokonya
wanangu. Asije kurudia tena. Nahisi kwa kuwa aliwalea tokea wanazaliwa ndio
anaona ana amri nao. Hapana. Heri kumuacha tu. Nyinyi endeleeni na maisha yenu,
mimi niendelee na wanangu.” Mpaka hapo ombi la ndoa likawa gumu.
Mwisho haukuwa mzuri hata kidogo.
“Naomba utulie Nanaa. Mimi nipo
hapa na wewe. Na nilikwambia nilishagundua kosa langu. Nikashindwa kusimama
kwenye nafasi yangu kama baba na mume kwako. Siwezi kuruhusu hilo litokee tena.
Kwanza kwa faida ya wanangu. Siwezi kuondoa hiyo furaha ninayoiona kwa sasa
hivi. Sithubutu. Nitakuwa nawakatili mno. Kwa garama yeyote ile, nimejiapia
kuwapa wanangu hiyo furaha. Pili, nimekusudia kusimama na wewe Nanaa. Jua
litoke, mvua inyeshe. Nimekuchagua wewe Nanaa, kwa kuwa nakutaka
wewe. Sina maisha bila wewe.” Nanaa akajisikia vibaya sana. Akaona vile Geb
alivyojitoa kwake.
“Asante Geb. Kweli umeamua kuwa
na mimi. Nimeona mpenzi wangu. Nakushukuru.” Geb akajiweka sawa. “Uliniambia
nikija utaniambia kitu.” Nanaa akacheka na kufuta machozi. “Nilitaka kukwambia
na mimi nakupenda Geb. Na ninakushukuru kuacha kila kitu kuwa na mimi hapa
kwenye kipindi hichi kigumu. Unanifariji. Unaniombea. Na usiku ninapo ogopa au
kuwa na ndoto mbaya, unakuwa na mimi unanisubiri mpaka nilale. Na nimeona hata
ndoto mbaya zimeanza kuisha. Siku hizi naweza kulala mpaka asubuhi na naona
Jimmy alikuelewa. Amebadili muda wa kucheza.” “Anamsikiliza baba yake je! Jimmy
atakuwa mtoto mzuri sana. Msikivu, naona kuliko wote.” Nanaa hakuamini.
“Unamtambua Jimmy kama mtoto
wako!?” “Kama nakutambua wewe kama mke wangu, sasa Jimmy atakuwa nani? Tutamlea
kama Liv na Magesa. Hapatakuwa na tofauti. Au madaraja kwao. Kile Mungu
atakachotujalia, ndicho tutakachompa.” “Nakushukuru Geb. Umenitia shauku ya
kujifungua salama, tuje kulea wote hawa watoto. Lakini…” Nanaa akasita.
“Lakini nini?” Geb akauliza.
“Itakuaje kama nikifa wakati najifungua?”
“Nitafanya kile utakachotaka nifanye na huyo mtoto. Ukinipa nimlee kama
Magesa, ujue nitafanya hivyo. Chochote kile, mimi nitafanya. Lakini
nimezungumza na Mungu wangu, nimemuomba akupe miaka mingi sana. Uje
unizike mimi na si vinginevyo.” Nanaa alilia sana.
“Nakupenda Geb.
Na asante kwa upendo wako.” “Kama kweli unanipenda Nanaa, kwa nini
hutaki tuhalalishe ndoa yetu?” “Sio kwamba sitaki. Kuna
mambo mengi yalikuwa yakinifanya nisite. Kubwa umeshalijibu sasa hivi.” “Juu ya
Jimmy?” “Ndiyo. Unafikiri ningeleaje watoto wa baba
wawili sehemu moja? Kama wewe huna shida ya huyu mtoto kulelewa hapa, angalau
imenipunguzia mzigo.” Geb akambusu.
“Naomba unyamaze kulia, kisha
uniambie kikwazo kingine.” Nanaa akatulia. “Familia yako?” Nanaa
akajibu. “Imefanyaje?” “Bado sitaki kuwa nao karibu.” Geb akanyamaza. “Hilo
ndilo tatizo. Najua unataka ndugu zako, na mimi siwataki.” “Hilo sitaki kuliingilia
Nanaa. Nakuachia wewe. Ila nataka ujue, wakati baba anakufa, aliniomba rasmi
nimtunzie mkewe na Grace. Ni ombi ambalo alinisisitiza sana. Tena akiniambia
nisisahau kama mama ni yatima. Mimi ndio niwe ndugu ambaye awe na
uhakika hatapoteza. Ndio maana nilifurahi sana kuona nyinyi wawili mnaelewana
na mnapendana. Nikajua haitaniwia ngumu kuwa na nyinyi wote. Ndio maana
nilikuomba tokea mwanzoni kama tunaweza kuishi na mama.” Geb akaendelea.
“Lakini Nanaa, mimi ndiye
niliharibu. Namjua mama. Najua udhaifu wake wa kupaniki kipindi cha matatizo.
Nafikiri hata wewe nilikwambia. Sio mtu wakumtegemea kutoa maamuzi yenye hekima
kukiwa kuna tatizo kubwa. Siku ile asubuhi wakati tunaondoka na watoto,
nilikuwa na hasira sana. Sikujua hata kama alikutamkia maneno mabaya. Ni kweli
nilikusudia kuondoka na watoto. Lakini uwe unaletewa jioni na asubuhi. Mbaya
zaidi sikufuatilia utekelezwaji wa hilo, sababu ya kujitupia kazini ili
kujaribu kupunguza hasira. Sikutaka hata kuwa na watoto karibu ili wasinione
vile nilivyokuwa nimekasirika.” Geb akaendelea kwa makini asije kuharibu.
“Nikamuachia mama majukumu yote
ya watoto. Majuzi nilienda kumuuliza mama kwa nini alimpa maagizo Jeri
asikukubalie watoto au hata asiruhusu wewe ushike watoto, akatuambia mimi na
Grace. Tena Grace aliumia sana. Mama akasema alikuwa na nia nzuri. Malii ni Malaya
sana. Halafu ulikuwa ukinyonyesha watoto wote wawili. Akasema aliingiwa na
hofu, pengine ungekuwa amekuambukiza magonjwa ambayo jamii ilikuwa ikisema
Malii anayo, halafu na wewe ukaambukiza watoto. Kwa kuwa ni kweli Malii
alishatembea na mama mmoja ambaye alikuja kufa kwa UKIMWI. Akaona ni heri tuje
kumlaumu yeye lakini aokoe watoto.” Nanaa akalia sana. Geb akamvuta nakumlaza
vizuri, akamkumbatia.
“Naomba tulale Nanaa. Inatosha
kwa leo. Mambo mengine hayana majibu kwa haraka. Naomba tumuachie Mungu” Geb
akaona asiibue mengine. “Tuombe.” Geb akaanza kuomba. Akamuombea Nanaa hekima
na afya nje. Akamuombea utulivu, furaha na usingizi mzuri. Akazungumza kidogo
na Jimmy. Wakalala.
~~~~~~~~~~~~~
Geb aliinua hukumu moyoni kwa
Nanaa. Inamaana mpaka hapo ni yeye tu ndiye amebeba majibu ya mambo mengi sana.
Kujenga familia hiyo ya Magesa. Anajenga na nani na nani anamuacha? Akubali
kuingia kwenye ndoa wakati haelewani na mama G, ambaye ndio kiungo kikubwa sana
cha hiyo familia? Ni kweli alimudhi sana. Kitendo cha kumnyang’anya watoto wake
na kumtafutia Geb mke! Nanaa alishindwa kusamehe. Hata kama alipata sababu
nzuri na ya msingi ya kumnyang’anya watoto na kumkataza asinyonyese wanae,
lakini si kwa matusi makali vile, na si kwa kumtafutia mwanae mke. Nanaa
alizidi kupata sababu yakumchukia yule mama.
Lakini katika muda wote
alioishi na yule mama, alihisi upendo mkubwa sana. Zile kumbukumbu za mambo
yule mama aliyokuwa akimtendea, zikaanza kumrudia. Zilikuwa zikija moja hadi
nyingine huku zikimuonyesha yule mama hakuwa na sababu yakufanya hivyo. Lakini alifanya
hata pale Geb alipomuonyesha yupo kinyume naye, lakini mama yake alisimama
kumtetea yeye, Nanaa. Japokuwa alikuwa akiendelea kujipa sababu ya kumchukia, lakini
wema ukazidi ubaya.
~~~~~~~~~~~~~
Asubuhi siku ya jumamosi ambayo
Geb aliahidi hatakwenda kazini, alikuwepo tu hapo na familia yake. Tokea
asubuhi anazunguka na Nanaa humo ndani. Wameacha gorofa, wanaishi kwenye
apartment ya vyumba viwili tu, na watoto wao. Liv aliamka akitaka kumfundisha
kaka yake kujenga nyumba kwa matofali ya mbao. Mchezo aliokuwa amenunuliwa na
baba yake. Magesa hakuwa na huo muda. Alitaka kuzunguka na kufanya shuguli
nyingi kwa wakati mmoja. Nanaa alimwambia Geb, wanyamaze waone mwisho wake.
Liv alihangaika naye, mpaka
akachoka. Kila alivyojenga kabla yakufika mwisho, Magesa alipiga ngumi
nakucheka sana. Nyumba nzima ilikuwa ikianguka kitu ambacho kilikuwa
kikimsababisha Liv, aanze upya kila mara. Mwishowe akamvuta mpaka kwa mama
yake. “Kaa hapa, usije tena kule.” Geb na Nanaa wakacheka. “Mwanao kafukuzwa.
Nilikwambia Liv hapendi shuguli nyingi. Anataka akianza jambo lake moja,
amalize. Kama Grace.” “Njoo mwaya mwanangu. Magesa wangu yeye anataka kucheza
sio mambo ya msingi.” Magesa akawa anamchekea mama yake huku anamfuata.
“Yuko wapi Fili?” Liv
akamkumbuka rafiki yake kipenzi. “Unamtaka Fili?” “Magesa anaharibu. Namtaka
Fili.” “Basi ngoja nimpigie mama yake Fili tumuombe Fili aje acheze na Liv.
Wakikubali, Dad ataenda kumchukua. Sawa?” “Nampenda mama.” “Hata mimi nampenda
Liv wangu.” Liv akacheka akawa anasubiria mama yake apige simu. Geb akataka
kumkataza, lakini Nanaa alishanyanyua simu na kupiga wakati Liv anachekacheka
mbele ya mama yake, akisubiria. Geb akanyamaza.
Kuliko Ungua Mpini.
“Simu ya Grace imezimwa.” Nanaa
akaongea. “Amekataa?” Liv akauliza kwa masikitiko. “Hapana Liv. Subiri.”
Akampigia simu Danny bila kusema anapiga wapi.
Geb akabaki kimya anawaangalia. “Halow! Ni mimi Nanaa.” “Upo? Habari za
siku?” Danny akauliza. “Nzuri kabisa. Vipi wewe na familia?”
“Mimi maisha yangu na wanangu yanaendelea vizuri. Mungu amenipumzisha na kina
Magesa.” Nanaa akashangaa. “Unamaanisha nini!?” “Kwani hujasikia?” “Juu ya nini?” Nanaa
akahoji. “Unajua yale
mangurue pori?” Nanaa hakuwa ameelewa. “Yanakuwa manene meusi hivi. Basi nimeamua kuachana na ngurue
pori na ukoo wake wote. Wachawi, roho zao mbaya kuliko shetani. Unakumbuka
walichokufanya?” Nanaa alikuwa bado hajaelewa.
“Sasa walipokufukuza wewe tu na kukupokonya watoto, na mimi
nikawageukia. Nilichukia sana walivyokunyanyasa wewe mtoto yatima. Kama
walivyokupokonya watoto wako, na mimi nilihakikisha nimewapokonya watoto.
Sitaki hata Magesa mmoja ashike mtoto wangu.” Danny
aliongea maneno mengi machafu akimtukana Grace.
Nanaa aliona machozi
yanamwagika. “Dude zito kama
gunia! Linakuweka roho juujuu kila wakati lisije likalalwa na wanaume wengine
likakuu kwa magonjwa! Unakazi ya kulilinda tu! Watu wanataka kulivua nguo
kuliangalia kuna nini ndani, kumbe hamna kitu. Bure kabisa. Maji matupu.” “Danny! Danny!” Nanaa alimwita huku akilia. “Nimejitafutia kasichana kazuri. Nalala bila presha.
Unanyanyua popote. Una..” “DANNY!” Nanaa akaita kwa ukali.
“Subiri kwanza. Hapo unamuongelea Grace!?” Nanaa akauliza kwa upole huku akilia
taratibu. “Kumbe nani?
Majitu makatili kuliko shetani. Hapa nimeshatayarisha hati zangu za talaka.
Amekimbia nyumba. Namsaka. Nikimpata tu, nataka aweke saini nioe, mtoto
mchangaa.” Nanaa aliumia sana.
“Kweli Danny? Matatizo yangu na Geb yamekufanya umesahau
alipokutoa Grace wewe? Leo unamtukana hivyo!” “Sasa ngoja nikwambie ukweli wote, Nanaa.
Grace alinifuata yeye mwenyewe kwa kuwa alitumwa na familia yake wanichukue
mimi kuniweka kama kafara yao. Waligundua nyota yangu ipo juu, ndio
maana walitaka kuniweka kwenye maisha yao ili wanitumie kujipatia utajiri. Ndio
maana mara tu baada yakumkubalia Grace
kurudi naye huku Dar kutoka Tabora, mama yake akahakikisha namuoa kwa haraka.” Nanaa
aliendelea kusikiliza.
“Na ukipiga mahesabu, ni baada ya kuniingiza tu kwao. Mimi
kuingia kwenye agano na Grace, ndio pacha wake akaanza kufanikiwa. Kama
ukichunguza vizuri, ni wao tu wawili ndio wanamiliki kampuni ambayo hatetereki
hapa nchini. Hata uchumi uwe mgumu vipi, wao wanafanikiwa tu. Hata umwambie
Grace kuna ofisi itamchukua kwa mshahara watakao mlipa mara mbili wa anaolipwa
na kaka yake, hakubali. Anataka tu kufanya hapo hapo kwenye hiyo kampuni. Geb
anafanikiwa, kwa agano la mimi nililoweka na Grace. Grace na Geb wanashiriki
nyota. Kwa hiyo agano nililoweka mimi ni kama nimeweka na Geb pia. Wote
wananufaika kwa kupitia mimi. Nimeambiwa ndio maana wananiweka karibu. Ndio
maana hawataki kunikorofisha. Unaambiwa nikiondoka kwenye maisha yao hao,
hawana kitu.” Nanaa alikuwa haamini anachoongea Danny.
“Sasa unaambiwa mambo hayo alianza mama yao. Mama yao ni
mshirikina sana. Alitukusanya watoto wengi sana. Tukawa tunakuja hapo kwao. Geb
anajidai sisi ni marafiki zake, kumbe anatafuta janja yakutuweka karibu na mama
yake atusome nyota. Alipoona nyota yangu inafaa kuliko vijana wengine wote,
ndio wakaanza kunilisha mambo ya ajabu. Ndio kisa cha mimi kuwa kama
nimechanganyikiwa kwa Grace. Usifikiri yalikuwa mapenzi yale! Unaambiwa
walinichezea sana. Ndio nikawa kama nimechanganyikiwa. Namtaka Grace tu. Kumbe
ni madawa waliyokuwa wamenilisha
yakunifanya nioe kwao, wachume pesa. Mimi ndio nawaletea utajiri.” Danny
akaendelea.
“Sasa vijana wote wameshawajua tabia zao hao. Wakawa
wanatafuta jinsi yakuniokoa mimi na wewe. Malii alipokuja siku ile alituambia
kwa kiasi. Lakini aliponitoa pale ndani akaenda kunitupa njiani, alinieleza
kila kitu kwa kina. Ndio nikawekwa sawa na wenzangu mtaani. Sasa walipoona mimi
nawakimbia, si ndio wakamtafuta sasa mwanamke mwingine mwenye nyota kali. Mama
yao akamtafutia Geb mwanamke ili amuoe, ili hata mimi nikimuacha Grace, wapate
nyota ya mtu mwingine. Lakini ujue hapo ni baada ya kuhangaika sana na mimi
kutaka kunirudisha kwenye familia yao, nakuona nimewagundua. Nakwambia
niliwaambia machoni hivi. Wakashindwa hata kubisha. Wakabaki kimya kabisa.” Danny
aliendelea kuzungumza kijasiri.
“Mimi ndiye niliyemshitua Sara, mwanamke waliyekuwa
wamemtafutia Geb. Ili wamtoe na yeye tambiko. Hapa ninapokwambia nipo naishi na
Sara. Mapenzi ya ukweli. Nimetulia, sio kama nilivyokuwa na Grace. Yaani
najisikia nipo mimi kama Danny wa miaka iliyopita. Nimepandishwa cheo kazini.
Maisha yangu mimi na Sara yapo raha mstarehe. Ila nimeapa kumsaka Grace mchana
na usiku, kutoa kiapo changu kwenye maisha yake. Nimetangaza kuvunja agano nao.
Huko sirudi tena. Kwa hiyo Nanaa, shukuru Mungu aliyekutoa mapema. Ila ombea
wanao. Nasikia wanatoa watoto wao pia kafara. Jaribu kujiiba hata ukaone wanao.
Vimebaki mifupa mitupu, na wote wapo wanawaangalia bila huruma. Kumbe watoto
wapo kwenye dawa kuwaletea pesa. Nimepiga marufuku wasiwasogelee wanangu
kabisaaa.” Daany akawa ameshika kasi.
“Mimi sijui kilichokupata Danny. Lakini hivi tunavyozungumza
nipo na wanangu hapa. Naishi na watoto wangu na Geb. Na Mungu akipenda
tutafunga ndoa.” “Mungu wangu Nanaa! Hao watu wamekuloga!” Danny
akashituka sana. “Danny! Ni nini
kimekupata wewe!?” Nanaa alikuwa haamini. “Kama unafikiri mimi nimechanganyikiwa, kwa nini hushangai
kuwa kwa nini bado Geb anataka kufunga ndoa na wewe? Geb ni mkororfi sana.
Hawezi kukubali akuoe baada yakubakwa na Malii. Kuna jambo ambalo
ananufaika na wewe. Ukute ni hao watoto aliowatoa kafara pia. Ameona walikuwa
wanakaribia kufa, ndio amekurudisha, umsaidie kuwalea hao watoto ili wazidi
kuwaletea pesa kwenye familia yao” Danny akasisitiza.
“Naomba kuongea neno la mwisho Danny. Maana nimejua hakuna
jinsi nikabadilisha unachoamini sasa. Ila ujue kabisa, Grace alikua mkeo. Na
iwe kwa hila au la, mliingia agano mbele ya Mungu. Wakati wote Mungu anaangalia
agano lake ili alitimize.” “Agano lenyewe…” “Subiri kwanza Danny. Mimi
nimekusikiliza tokea mwanzo mpaka mwisho. Naomba nisikilize na mimi.” “Sawa.” Danny
akakubali.
“Mungu anaangalia agano lake, na hatakubali mtu yeyote yule
asimame kwenye agano aliloahidi ataweka mkono wake. Kuwa sana makini. Ndoa yako
na Grace ni ya kanisani. Mimi nakujua kwa sehemu Danny. Ila nimekujua ukiwa na
hasira, huwa huna uwezo wakufikiri kabisa kaka yangu.” “Unanivunjia heshima
Nanaa.” “Hapana Danny. Naomba unisikilize. Nimekusikiliza muda wote ukitukana
viungo vya kike vya Grace, ukumbuke na mimi ni mwanamke. Natokwa damu na maji kama
Grace. Kuna siku nakuwa na joto na kuna siku nakuwa baridi kama Grace. Uliza
wataalamu wa
afya watakufundisha juu ya joto la mwili
wa mwanamke utaelewa au mzunguko wa mwili wa mwanamke. Nimevumilia kukusikiliza
mpaka ukamaliza. Naomba na mimi nisikilize.” Nanaa
akasisitiza.
“Mbona naishi na Sara hayupo hivyo?” “Unajidanganya Danny.
Unaongelea Sara mtoto wa mjini huyo!? Mtoto ambaye hajui hata kusukuma mtoto
mmoja leba! Mtoto ambae kama amefanikiwa kubeba mtoto akakaa tumboni kwake si
zaidi ya miezi miwili, akamtoa. Unamlinganisha na Grace aliyekuzalia watoto
watatu! Anawanyonyesha mpaka wamefika hapo unaponiambia umewapokonya na
kuzurula nao! Amewafundisha kujisaidia na kukaa! Unamlinganisha na Sara ambaye
anaweka madawa huko kwenye uchi ili kila mwanaume anayelala naye amtoe bikra
iliyokwisha tolewa tokea yupo mtoto!” Nanaa alishachukia.
“Sio Sara.” Danny akapinga. “Humfahamu Sara kama ninavyomfahamu mimi,
Danny. Mimi nilikuwa napewa habari zake na mtu aliyekuwa karibu naye na
aliyekuwa akimuona akinunua hizo dawa za shabuu ili kuziweka huko kwenye
sehemu za kike ili kufunge. Niambie tu ukweli Danny, hukumtoa bikra Sara?” Nanaa
akauliza. “Mbona hata na
Grace nilimtoa?” “Sijui juu ya Grace, ila mimi ninauhakika na bikra uliyotoa ya
Sara.” Nanaa akajisahau hata kama Geb yupo pale. Aliongea kwa
machungu sana.
“Bikra ya Sara sio yenyewe, Danny. Anaziweka kutokana na
anayetaka kumfurahisha. Hata uliyotoa wewe ni yakuweka. Tena nina uhakika
alikuwekea baada ya kufukuzwa kwa kina Magesa. Kwa kuwa aliyokuwa amemuwekea
Geb, alikuwa akilalamika mbele ya huyo mtu kuwa Geb anamchelewesha kumtoa ili
aendelee na maisha yake. Alipoona Geb haitoi, na wanaume zake wanamsumbua,
akaenda kutolewa na mwanaume mwingine, ili aendelee na wanaume zake mtaani. Hapo
kabla hata hajafukuzwa kwa kina Geb au hata hajaja kwenu.”
Nanaa akaongea kwa hasira.
“Huyo anayekuletea habari za Sara, ni muongo.” Danny
akapinga. “Sawa Danny.
Lakini nakwambia kabisa, Sara atakuua kwa magonjwa. Sio muhuni. Huyo msichana
ni Malaya wakutafuta wanaume walale naye.” “Huna utakachoniambia juu ya Sara
nikaamini. Sara amekuwa baraka kwangu. Maisha yangu yamebadilika. Ninapesa.
Tena yakulipwa kwa jasho langu. Na hayo yote hayo nimeyapata baada ya kuachana
tu na Grace.” Nanaa hakuamini.
“Danny wewe! Umepatwa na nini!? Hivi hujui kuwa sasa hivi
wewe na Sara, mnakula matunda ya Grace!? Mnavuna alikopanda Grace! Hakika Mungu
hatawaacha Danny. Ipo laana ya mke. Itakushika tu.” “Kwanza ujue Grace sikumuoa
kwa akili yangu. Kwa hiyo hakuna agano kati yangu na Grace. Pili, wewe ni mtoto
sana kwangu Nanaa. Nayajua maisha kuliko wewe. Namjua Mungu kwa kulelewa
kanisani. Najua mambo ya mjini kuliko wewe kwa kuwa wakati wewe uko migombani
unabadilishwa nguo, wenzio tulikuwa tumeshafika mjini.” “Sawa Danny kaka yangu.
Na samahani pale nilipokuvunjia heshima.” Simu ikakatwa.
~~~~~~~~~~~~~
Nanaa alikuwa kwenye mshituko
akabaki ameduaa. Akagundua Liv alishaondoka pale mbele yake yupo chumbani
anacheza na mdogo wake. Geb ametulia pale pembeni yake kwenye kochi ameinamia
simu yake. Nanaa akamtizama. “Wewe Geb!” Geb akamtizama. “Wewe unajua haya yote?”
“Nafahamu Nanaa. Najua kila neno alilokwambia. Tena kutoka kwa Danny mwenyewe.
Nilimfuata kujaribu kuzungumza naye juu ya familia yake. Hatima yake na Grace.
Tena baada ya Grace kuondoka.” “Subiri kwanza Geb.” Nanaa akawa ameshachanganywa.
Ndipo Geb ikabidi na yeye
amuelezee kila kitu. “Danny amemtukana dada yangu, mbele ya macho yangu! Huo
uchafu anaokwambia juu ya Grace, ameniambia na mimi. Bila hofu, wala aibu, au
huruma. Anamchafua Grace na sisi huko mtaani! Hakuna tulichobakiza Nanaa. Mama
ndio anaitwa mchawi. Na hivi amebaki peke yake, utamuhurumia. Vijana wote
wanamsema vibaya. Wale wote waliokuwa wakija kula na kunywa pale nyumbani,
wanamtishia kumfanyia mambo mabaya. Wanasema kuwa alikuwa akiwaroga walipokuwa
wakija pale ili mimi nifanikiwe. Wanasema mama ameiba nyota zao wote,
amenitengenezea mimi ili nitajirike. Na ndio maana nimefanikiwa kuliko wote.”
Nanaa akaumia sana.
“Kwa hofu ya kuja kumdhuru
mama, kuanzia jumatatu nimeamua kumfungia ndani na kuongeza ulinzi. Kuna
waliokuwa wamemfuata na wake zao na watoto kule kazini kwake, wanaomba
wawafungue watoto wao.” “Kivipi!?” Nanaa akauliza huku akilia kwa
uchungu sana. “Si unajua waliokuwa wameoa, kila walipokuwa wakijifungua mama
alikuwa akiwahudumia wake zao na watoto? Tokea wanazaliwa mpaka sasa. Sasa wake
zao wanakuja kusema sijui mama aliiba vitomvu vya watoto wao.” “Mungu wangu Geb!” Nanaa alizidi kusikitika.
“Kama vile
alivyokuwa akisafisha kitomvu cha Liv wakati mchanga?” Nanaa
akauliza. “Ehee! Sasa wanasema kila vile vitomvu vilipokuwa vikianguka, mama
alikuwa akiviiba, anaficha ili aje afanyie uchawi. Ilikuwa ugomvi mkubwa. Wale
wanawake wanamtukana mama, kama hawamfahamu! Ndio mfanyakazi mmoja wa mama
akanipigia simu. Ikabidi kukimbia kwenda. Kufika nikakuta mama anahali mbaya.
Wamemzunguka. Wanamdai vitomvu vya watoto wao. Na mambo mengi sana. Niliumia
Nanaa! Niliumia sana.” “Pole Geb.” Nanaa alizidi kuumia.
“Sasa
ukafanyaje?”“Sikusema kitu Nanaa. Nilimchukua mama na kumrudisha
nyumbani. Alikuwa kwenye hali mbaya sana. Nikakaa naye mpaka jioni niliporudi
hapa.” “Kwa nini hukuniambia Geb?” “Nikwambie nini Nanaa kwa yote
tuliyokufanyia? Mama anaamini anastahili hayo yote kwa aliyokufanyia.
Unakumbuka ulipowaambia umewaacha juu ya madhabahu ya bwana?” “Ni hasira tu Geb!” “Basi mwenzio anaamini ndivyo Mungu
anavyomlipa kwa mabaya aliyokutendea.” “Hapana Geb. Mimi
niliongea kwa hasira tu.” Nanaa akazidi kuumia.
“Sasa Grace
anasemaje?” Nanaa akazidi kuhoji. “Aliamua kwenda kupumzika.
Alishindwa. Alijitahidi kuvumilia, akiomba na kujaribu kubaki na watoto, lakini
kama ulivyomsikia Danny. Alikuwa akisema Grace anamtaka warudiane kwa ajili ya
kuendelea kumfanyia mambo ya kishirikina. Grace alituambia walikuwa wakifanya
mapenzi na Sara kwa sauti kama kumuumiza.” “Mungu wa
mbinguni Geb! Ni nini kinatokea?” Nanaa hakuamini.
“Sasa mbona
sijampata Grace kwenye simu?” “Alizima simu yake kabisa. Amechoshwa na
picha za Danny na Sara alizokuwa akitumiwa na watu. Wengine walijidai wanakosea
namba. Lakini ilikuwa makusudi tu kumfikishia ujumbe wa matusi yaliyosambaa
mtaani kutoka kwa Danny.” “Pole mpenzi wangu. Poleni
sana.” “Nashukuru Nanaa. Ila najua Mungu ataturehemu tu.
Tulipokosa, atatusamehe. Yataisha siku moja.” Nanaa akabaki amenyamaza kama
aliyepigwa na bumbuazi.
~~~~~~~~~~~~~
Muda wote Geb amekuwa akirudi
nyumbani akionekana ametulia bila kumuonyesha Nanaa kile kinachoendelea.
Alimchukulia kwa upendo, kumbe anakabiliwa na matatizo makubwa sana. Alibaki
Nanaa akiwaza. Akakumbuka usiku uliopita jinsi alivyomwambia Geb juu ya ndugu
zake kuwa hawataki kuwa nao karibu. Akamuhurumia Geb. Katika yote hayo, bado
amemchagua yeye! Anakuja nyumbani kwa wakati. Anajitahidi kuwa naye bila
kulalamika! Amemuonyesha upendo wa ajabu sana. Amempokea yeye na mtoto wake!
Nanaa alizidi kuumia akihukumiwa.
~~~~~~~~~~~~~
“Kwa hiyo mama
yupo peke yake?” Nanaa akauliza kwa uchungu sana. “Awe na nani tena? Grace
aliondoka akiwa anamlaumu kuwa amemtafutia mumewe mke. Mimi nipo hapa na
familia yangu. Sasa unafikiri anabaki na nani? Halafu naogopa Nanaa. Kwa fujo
walizomfanyia kazini kwake, siwezi hata kuruhusu mtu afike pale nyumbani.
Nimeongeza ulinzi. Nimemwambia asitoke pale. Maana wanaweza kuwa wanamuwinda
nje. Nataka asubiri kwanza kwa muda mpaka patulie.” “Kweli Geb unanipenda! Umekubali kuwa hapa na mimi ukamuacha mama yako
peke yake!” Nanaa akazidi kuumia. Geb akanyamaza.
“Mimi nimesamehe Geb.
Nimesamehe kabisa mpenzi wangu. Niambie jinsi yeyote unayotaka nikusaidi katika
hili. Nimechagua kusimama na wewe kama vile wewe ulivyosimama na mimi.”
“Nakushukuru Nanaa. Lakini narudisha ombi langu lile lile. Naomba urudie tena
kujenga nyumba yetu. Sio jengo. Maana hata wewe umekuwa shahidi. Tumeacha
nyumba kubwa ya thamani. Tena iliyonigarimu pesa nyingi sana, tupo hapa
tumejibana kwenye apartment ya vyumba viwili. Inawezekana kabisa na mimi
nilichangia kuharibu nyumba ya kwanza tuliyojenga. Lakini naomba usichoke.
Naomba anza upya. Pata muda fikiria ni jinsi gani yakufanya.” “Wewe unataka
nini?” Nanaa akauliza.
“Ni zamu yako mpenzi wangu.
Naomba ufikirie. Nimeshakwambia nini nataka. Naomba wewe fanya kile ambacho
unajua hakitakufanya ujute baadaye. Panga matofali yako vizuri, ili nyumba
isije kutuangukia tena baadaye.” “Naomba nianze kwa kuwa mkweli. Sina tena kitu
ambacho nimekuficha Geb. Mungu wangu nishahidi. Hata mazungumzo yangu ya mwisho
na Malii, nimekwambia. Sasa kama aliendelea kuwasiliana, sijui. Mimi nili mblock
na nilikwambia nilimkabidhi dada Fifi kila kitu na pia karibu na siku za
kujifungua pia nitamkabidhi simu yangu na nitafungulia mawasiliano ya Malii ili
yamsaidie yeye baadaye.” Nanaa akaona awe muwazi zaidi.
“Nashukuru kwa hilo. Ila
sijisikii vizuri vile ulivyomwamini Fifi kuliko mimi.” “Kwa kuwa hatukuwa wote
Geb!” “Sasa hivi tupo pamoja Nanaa. Na nimekuahidi kusimama na wewe wakati wote
hata atakapozaliwa Jimmy. Au umeshindwa kurudisha Imani yako kwangu kwa mabaya
niliyokuwa nikikutendea, tena kwa kurudia rudia. Huniamini tena na Jimmy?”
“Ninakuamini Geb. Na mimi nimekwambia nimeamua kusimama na wewe.Tumesha sameheana.
Huko tumepita. Nitaenda kuchukua kila kitu nikukabidhi wewe.” “Hapo sawa.” Nanaa
akacheka. “Una wivu Geb wewe!” “Sio wivu Nanaa. Hata Fifi mwenyewe atakuwa
hatuelewi. Tunatuma ujumbe mbaya sana kwenye jamii. Na mimi nafahamika hata na
nisiowajua!” “Basi mpenzi wangu. Hilo tumeshalimaliza.” Wakatulia.
“Unaenda kumuona mama saa ngapi?”
“Leo na kesho nilimwambia siwezi kwenda kwa kuwa nitakuwa na nyinyi. Kwa hiyo
mpaka jumatatu.” Nanaa akamuhurumia. “Ni sawa tukaenda wote?” Geb akamtizama
kama kutaka uhakika. “Kama unaona sio sawa, basi. Ila nashauri uende
ukamwangalie. Usimwache peke yake hasa baada ya hayo matatizo.” “Hapana. Nataka
uwe na uhakika Nanaa. Sitaki ujisikie kama unalazimika.” “Wewe unafikiri
atafurahi kuniona na hii hali niliyonayo?” “Hali gani?” “Mjamzito na mjukuu
ambaye sio wake?” Geb akafikiria kidogo.
“Mimi naona nisubiri mpaka
nitakapojifungua Geb. Tuache tu.” “Hapana. Kama unajisikia kwenda, twende.
Inawezekana huu ndio ukawa wakati wa bwana. Usimzuie Roho wa Mungu kufanya kile
anachotaka kufanya. Kuhusu anajisikiaje juu ya ujauzito wako, naweza nisiwe na
majibu yote. Ila amekuwa akituma salamu kwako na watoto. Amekuwa akisema
nikusalimu. Na Grace ameomba nikusalimu, nikwambie anakupenda na anakuombea Mungu
akurejeshee miaka yote uliyopoteza na wanao.” Nanaa akazidi kuumia na
kuwahurumia.
Ilikuwa ni familia ya watoto
watatu tu. Mama na watoto wake wawili mapacha. Upande wa baba walishawakataa
kuwatambua tokea uhai wa baba yao. Mama yao ni yatima. Kwa hiyo kila mjukuu na
mkwe aliyekuwa akiongezeka kwao, ndio familia pekee waliyoitegemea. Na walikuwa
wakijitoa kwa moyo wote kupenda na kusaidia watu bila ubaguzi.
Ukipanda Mema, Utavuna Kwa Wakati..
Geb arudi kwa mama yake akiwa
na familia yake yote. Hata yeye hakuwa akiamini. Lakini kwa kuwa alikuwa akimuomba sana Mungu, akajua
maombi yake yameanza kujibiwa. Kila wakati Nanaa alikuwa akimtizama, asiamini
ukimya ule ulikuwa umebeba mazito ya kiasi kile. Geb aliegesha gari mbele ya
nyumba. Akafungua watoto wake. “Twende Liv.” Mama yake ilibidi amuite baada
yakumuona amesita baada yakushuka. “Twende mama yangu. Twende ukamsalimie
bibi.” “Hapana mama. Bibi chapa.” Nanaa akasimama na kumwangalia vizuri.
Moyo wa Geb ukapasuka. Akajua
tayari mambo yameharibika tena. Alishakuwa amefika karibu na geti dogo la
kuingilia ndani. Akasimama akiwa amembeba Magesa. “Bibi alikuchapa!?”
Nanaa akauliza kwa mshangao. “Chapa hapa.” Liv akamuonyeshea kwenye matako.
Akamtizama Geb, Geb kimya kama kawaida yake. Akarudisha macho kwa Liv.
~~~~~~~~~~~~~
v Haya tena, wanandoa hawa
wameanzisha penzi jipya. Kila mmoja ni kama amepata mwenza wa ndoto zake. Grace
aliyekuwa akilia, sasa anafutwa machozi kwa herufi kubwa na Man. Danny
anaimba kupata kimwana. Laini, mweupe, rahisi kunyanyua popote, Sara.
Anakula vitu FRESH sio makapi.
LAKINI, ‘Alicho kiunganisha Mungu, Mwanadamu asikitenganishe.’
v
Nanaa ameamua
kurudi kwa mama G. Liv naye anaanzisha jambo jingine.
Nanaa aliwaacha
wahukumu wake madhabahuni mwa Bwana.
-
Je, bado Mungu
anapatiliza mabaya?
-
Bado Mungu analipa
kisasi?
-
Ubaya wao
utawafuata mpaka wapi?
v Mama G amejikuta yupo kifungoni. Imebidi
mwanae Geb kumfungia ili wasimdhuru. Ni kama Nanaa amebeba hatima ya yote.
Amesimama nje ya mlango. Ataingia?
v
Nini kitaendelea
kwa mapacha hawa wa mama G, waliofanikiwa kielimu, kiuchumi lakini kwenye
mahusiano imekuwa shida.
-
Ndoa ya Grace
itaishia wapi?
-
Geb anataka kumuoa
Nanaa katikati ya mvurugiko huo, mwisho ni nini?
Usikose Muendelezo.
0 Comments:
Post a Comment