Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Ni Wangu! - Sehemu ya 52. - Naomi Simulizi

Ni Wangu! - Sehemu ya 52.

Nanaa aliendelea kulia mbele ya Malii, akimsihi amsamehe. Mmoja wa kijana wa Malii akamsogelea kwa hasira kama asiyetaka apoteze muda zaidi, akamnyanyua pale alipokuwa amepiga magoti na kumuweka kwenye kochi kwa nguvu. Malii akavua mpaka chupi, nakubaki kama alivyozaliwa. Jogoo alishakuwa hewani. Kila mtu akainama. Nanaa alikuwa akipiga sana kelele pale alipotaka kufungwa kwenye kochi. “Unajisumbua tu Nanaa. Hakuna wakukusikia wala kukusaidia. Walinzi wa Geb njaa tupu. Nimewapa makopo ya soda, yote yanadawa za usingizi. Sasa hivi wanakoroma tu.” Malii aliongea kibabe na kejeli.

“Hapana. Nguo namvua mwenyewe. Huyu nataka kumvua taratibu. Nifaidi kuanzia macho mpaka mzee akiingia ndani kabisa, nisikilizie raha yake.” Akamkataza huyo kijana wake. Nanaa alilia kama anayechinjwa. Naomba usinifanyie unyama huu mbele za watu, hasa kaka yangu. Tafadhali Malii.” “Nilijua ndipo ulipochagua! Haya ongoza njia mpaka chumbani kwa Mzee G E B.” Malii alidhihaki. Wakamfungua mikono, Nanaa akatoka pale kwenye kochi huku akilia. “Kaka nisaidie. Niokoe kaka yangu.” Nanaa alikuwa akilia huku akimtizama kaka yake. “Hawezi kukusaidia huyo. Hana shida ya wewe kulalwa na wanaume. Haimsumbui hata kidogo. Ndio maana anakuacha hapa bila shida akijua Geb anakulala bila heshima.”Malii akacheka kwa kudhihaki tena.

“Eti gafla James anajidai amesahau kuwa Geb alikuwa akilala na Liz nyumba ambayo na wewe ulikuwepo! Anajidai amesahau kuwa Geb alikuacha nje ya ukumbi siku ya harusi yangu wakati yeye Geb, anapeana mabusu na Liz ndani, na James akiona! Eti leo gafla James anajidai amesahau kabisa, anatoa baraka zake uzalishwe humu ndani ya familia hii wasaliti! Wanafiki wakiongozwa na mama yao anayejidai mcha Mungu. Mtoto wake analala na wanawake ndani ya nyumba hiyo hiyo ambayo na yeye yupo, lakini hana shida! Sidhani kama ataumia nikilala na wewe hapa na yeye akiwepo. Eti mama Lao?” Akamgeukia mama G, akiwa vilevile uchi.

“Utaumia na mimi nikiendelea kwa Nanaa? Maana Geb alitoka kulala na Liz, akaja kulala na Nanaa, na bado mama unatoa baraka zako tu. Naamini hatakuwa na shida hata na wewe ukitoka kulala na Geb, ukaja kulala na mimi pia sasa hivi. Au mama G, unabisha!?” Malii akauliza kwa kejeli akijua wote wamefungwa midomo hawawezi kuongea.

“Si nilikwambia Nanaa? Hamna mwenye shida na sisi tukiendelea. Twende zetu wangu. Tukale vitu vyetu taratibuuuu. Bila jasho. Kipupwe kikitupuliza chumbani kwa Geb.” Wote walifungwa mikono, miguu na midomo. Wakabaki wamekaa wamenyoosha miguu huku wamesimamiwa na risasi. James alikuwa akisikika akilia sana. Aliinama muda wote akilia.

Akamshika Nanaa kwa nguvu, kutoka pale alipokuwa akilia pembeni ya kochi. “Umeona uroho wa pesa unavyo kuponza? Leo unaweza kukosa vyote.” Malii akacheka huku wakipandisha ngazi akimvuta na Nanaa na kijana mmoja wao akiwasindikiza. “Ulikataa kulala na mimi ili Geb asijue akakufukuza kwake. Sasa leo mbele yake, nakutia mpaka nichoke. Si alijidai hataki niwe karibu na wewe nisiwasimamie harusi! Sasa leo nakukula kitandani kwake, huku AC yake inanipuliza. Kwanza hataumia, hakupendi. Heri mimi ninaenda kukulala na ninakupenda.” Alisikika Nanaa akilia tu.

Walifika mpaka mlangoni mwa chumba. “Waungwana eeh! Tusisumbuane. Nataka kula vitu vyangu kwa nafasi. Taratibu mpaka niridhike.” Malii aliongea kwa sauti ili wakina Geb wasikie. Wakaingia chumbani. Malii alimvua Nanaa nguo zote, yule kijana akamfunga pale kitandani. “Naomba usimfunge mdomo. Nataka nimsikie sauti yake wakati nikimfaidi. Ndio itaniongezea molali.” Malii aliongea huku akimtizama Nanaa pale kitandani.

Alimfunga mpaka akamaliza. “Naomba sasa utupishe.” Yule kijana akatoka. Nanaa akazidi kulia. Ilisikika sauti ya Nanaa tu akilia. Baada ya muda, Malii akatoka akiwa vile vile uchi. “Nimeshamaliza raundi ya kwanza. Nataka kinywaji baridiii ili niendelee.” Malii alikuwa akiongea huku anashuka ngazi, akiwa mtupu kabisa kama alivyozaliwa. Akaelekea jikoni na kutoka na jagi la juisi. “Mpaka hii iishe yote, nitakuwa nimekata kiu zote.” Malii aliongea kwa kujigamba huku akipandisha ngazi kurudi chumbani kwa Geb alikokuwa amemuacha Nanaa akilia. Aliendelea kunywa ile juisi bila kutumia glasi. Alikunywa hivyo hivyo kutokea kwenye jagi. Uchi kama alivyozaliwa. Nanaa alisikika akilia kwa uchungu sana. Malii akaingia na kufunga mlango.

“Yaani nikikuona tu mwili wako, akili inavurugika. Hakika Nanaa wewe ni mzuri na mtamu.” Malii aliendelea. “Uwiiiii! Heri mama yangu alinizaa mwanaume jamani! Starehe hii ningepata wapi mimi?” Malii alisikika akishangilia huko chumbani, Nanaa akilia sana. 

Baada ya kama lisaa tena ndipo Malii akatoka. “Jamani nawashukuru kwa ushirikiano wenu.” Malii aliendelea kuzungumza nao huku akivaa. “Nimeoga kabisa. Nahisi nimefutia taulo lako Geb. Taulo kama sufu!” Malii aliendelea kukejeli huku akiendelea kuvaa pale pale mbele yao. “Nimekuwa maskini, lakini sijutii. Kwa niliyoyapata huko juu! Si mchezo. Sasa Geb una baraka zangu zote. Na wewe endelea kuchezea tu. Hata ukimwaga mipesa pale kwa Nanaa, mimi naelewa kabisa kaka.” Akamgeukia James.

“James! Dada yako mtamu! Si mchezo kaka. Kama walikuwa wanakupa vijipesa visivyoeleweka, anza kumchuna kubwa kubwa. Unastahili ndugu yangu. Si kwa utamu ule wa Nanaa! Eeh bwana eeh! Kaka heshima zako. Umekuza, na mimi leo nimefaidi matunda yako. Mtoto mtamu kuanzia machoni mkapa ndani!” Malii akamaliza kuvaa.

“Sasa jamani, kilichotuleta kimekamilika. Tuondokeni, nisizidi kuchelewa. Nanaa nishamfunga huko juu. Mchukueni huyo mke mdogo wa Geb, Danny. Ameolewa na kaka mtu na mdogo wake. Basi jamaa hapa kafika. Na yeye anataka aitwe Danny Magesa. Huyo tutaondoka naye. Mkijitahidi kujifungua na kupiga simu polisi, mjue mmemuua Danny. Danny ndio tiketi yangu yakunitoa hapa salama. Ukiita polisi tu, sisi tunamuua Danny, halafu tunamtupa. Tukijiridhisha kua tupo salama, tutamwachia ili arudi kuwafungua. Sasa uwamuzi ni wako Geb, Grace,

James, Gozi na mamaa ya busara. Mnamtaka Danny au kuingilia penzi langu na Nanaa? Maana kwangu mimi Nanaa ana penzi la kweli, kwenu nyinyi wanawachuna tu. Wachanga wawili wamehamia jijini. Biashara zimewashinda, James kaamua kumtumia mdogo wake ajinufaishe mjini. Sasa Grace kazi kwako wewe uliyezalishwa kama panya. Vidume vitatu bila baba, au yangoswe umuachie ngoswe.” Malii aliongea bila wasiwasi.

“Haya, Danny twende. Aga mkeo kabisa. Maana wewe yatima ndugu yangu. Wanaweza kukutoa kafara. Nawajua hawa watatu. Tena mama yao ndio kiongozi wao. Wabinafsi kweli. Watu wa maana na wathamani ni wao watatu tu. Mama na mapacha wake hao wawili. Hawakawii kukutoa muhanga mtoto yatima. Twende baba.” Danny akanyanyuliwa pale chini. “Ukiwahi kurudi mkuu, wewe ndio utawafungua wote.” Malii akaongeza.

“Ila Nanaa aoge jamani. Geb, usiguse kabla hajaoga. Niushauri tu kaka, na kukujali kwa ule umbali tuliotoka mimi na wewe. Nimemwaga kila kitu humo humo. Na si kwa ukame niliokuwa nao. Kama bahari vile. Utaenda kujionea mwenyewe. Mtoto kawa mwekunduuu kwa shuguli.” Malii akacheka nakuongeza. “Bwana leo ndio ujue pesa si kila kitu na ni kila kitu pia. Leo pesa yako imeshindwa kukulinda wewe na mama yako ambaye ndio Mungu mtu kwako. Ndani ya mjengo wako, nimefanya kila kitu kwa pesa yangu mimi ambayo huwa unaiona chache, huku pesa yako nyingi umeifungia benki. Ningetaka kukuua ningekuua kirahisi tu. Wewe na mama yako mwanadamu pekee unayemthamini hapa duniani.” Malii akacheka tena.

“Halafu naomba niongeze kwenye pesa ni kila kitu. Kwanza nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipotambua juhudi zako Geb. Umenipa kitanda kizuri. Mashuka safi. Hewa nzuri. Nimemlala Nanaa bila kutokwa jasho. Nimeoga maji mazuri. Bafu safi. Taulo lako zuri. Nakushukuru milionea wetu. Pesa yako imenitunzia Nanaa mpaka na mimi nimemfaidi. Nimemfaidi humuhumu kwenye nyumba yako. Iliyozungukwa na walinzi na ukuta mkubwaaa. Eti mwenye kisu kikali ndio mla nyama! Usemi wa kishenzi huo. Tena Zinda anasema ni usemi aliombiwa na mama yako. Akijinadi kuwa wewe ndio mwenye kisu kikali, wengine hatuwezi kumpata huyo Nanaa. Sasa mama, nakutaarifu kabisa. Haikuwa shuguli ndogo. Nimepiga kisawa sawa. Gozi fikisha ujumbe kwa wote. Mwambie Zinda, leo na yeye nimemlia. Geb! Baba, nimekula. Nimekula haswaaa! Haaaa!” Malii alianza kucheka na kushangilia. “Uuuuuu!! Ibarikiwe siku ya leo jamani. Twendeni ndugu zangu. Inatosha.” Wakatoka huku wakimvuta Danny. 

~~~~~~~~~~~~~~

“Huyu Danny ndio kafara yao. Mwekee kabisa risasi ya tumbo. Ukiona chochote usichokielewa, fyatua tu. Hamna hasara yeyote. Kwanza hapo alipo sio binadamu. Anatembea kama mzimu tu. Wamemfanyia uchawi. Ndio maana mnamuona hapo kawa kama fala. Hao wote kina Magesa, wamemuoa huyo. Na yeye wanamlisha kama mtoto wao au kama Nanaa. Basi Geb na dada yake wanavuna mipesa tu kwa zindiko walilomtoa huyu. Unaambiwa walishamzika muda mrefu sana. Ndio maana wanapesa nyingi  yeye yupo kama fala tu. Hajitambui.” Malii akaendelea kumwaga sumu na kuibua kitu cha tofauti kwa Danny.

“Unaambiwa mama yao mchawi kweli kweli. Anakijiduka kidogo tu, lakini weee! Anamijihela hatari. Watu wanajiuliza, kiduka kile na pesa zote hizo, wapi na wapi!? Ipo namna tu. Sasa unaambiwa kila mwezi lazima Geb aende Iringa kwa mganga wao. Huyu Danny ndio chuma ulete wao. Wamemfanya kama jinga! Hajijui tu. Lipo kama toto la kike! ” Walimsikia Malii akiongea huku wakielekea kwenye gari. Baada ya muda wakasikia gari likiondoka.

~~~~~~~~~~~~~~

Vilijaa vilio vya miguno yataratibu na sauti ya uchungu ya Nanaa ilisikika kutoka juu chumbani kwa Geb. Hakuna aliyeweza kumtizama mwenzake. Mlio wakufunguliwa geti kwa nguvu, ulimwamsha mmoja wa mlinzi getini. Akajaribu kuangalia kamera, akaona ni gari aliyoingia nayo Malii. “Kwa nini atoke kwa kasi hivyo!?” Mlinzi akajiuliza. Akaamua kwenda ndani kujua kama ni salama. Asijue alishachelewa. 

Alikuta mlango wazi. Akaingia. Alishituka sana kukuta ile hali. Alipigwa nabutwaa, asijue afanye nini.  “Samahani nililala kidogo.” Akaomba msamaha huku akitetemeka, asijue kama alilala zaidi ya lisaa. Bosi yupo chini sakafuni. Plasta mdomoni, mkononi na miguuni, huku akilia kama mtoto. Alikuta hali iliyomchanganya sana. Kwa kuchanganyikwa akawaacha wa pale chini, akakimbilia chumbani kwa Nanaa. 

Alimkuta na hali mbaya sana. Kwanza mke wa bosi wake, halafu yupo uchi nyang’anyanga pale kitandani. Akamfunika kwanza ndipo akamfungua huku akiendelea kulia. Nanaa hakutoka pale kitandani. Aliendelea kulia kwa uchungu mnooo. Mlinzi akawa ameshajua kilichotokea.

Akarudi tena kuwafungua James, Gozi, Geb, mama G na Grace. Mlinzi mwenyewe akaanza kulia kwa hofu. “Ngoja nipige simu polisi.” “Hapana. Usithubutu. Watamuua mume wangu. Wewe acha kama ilivyo. Mmeshindwa kulinda, acha na wala usimwambie mtu yeyote. Umenisikia?” Grace akauliza kwa hasira huku akilia. “Hata walinzi wenzio usiwaambie. Sisi tupo sawa tu. Wamemchukua mume wangu. Ukisema chochote, watamuua Danny. Ondoka na kaa kimya.” “Sawa mama.” Mlinzi akajibu, nakutoka huku anatetemeka.

Hakuna aliyeweza hata kunyanyuka. Walikaa pale mpaka Danny akarudi huku anakimbia. Grace alisimama na kumkumbatia huku analia. “Hawajakuumiza?” “Hapana. Nani amewafungua?” Danny akauliza huku akitetemeka. “Mlinzi. Lakini tumemwambia asimwambie mtu ili wasikudhuru. Hawajakuumiza?” Grace akarudia tena huku akimwangalia mumewe kila mahali. “Walinifungua na kunishusha katikati ya kwenye mataa ya hapo Buguruni. Nusura kugongwa!” Danny aliongea huku akionekana amepaniki.

          “Naomba tuondoke Grace. Tukachukue watoto tuondoke sasa hivi. Sitaki kuendelea kukaa hapa. Twende.” Grace na Danny wakaenda kuchukua watoto wao, wakaondoka. James akatoka hapo kimya kimya, huku akivuta kamasi. Na Gozi akafuata nyuma. Akabaki Geb na mama yake. Geb na yeye  akatoka. Hakurudi tena, mama yake alikesha akilia.

Asubuhi Ya Baada Ya Balaa.

Nanaa alilia usiku kucha bila kunyamaza wala wakumbembeleza. Ikabidi tu aamke. Ilishakuwa asubuhi, mtoto wake alishaanza kulia. Akajua ni njaa tu. Akakimbilia bafuni kuoga huku akiendelea kulia. Akavaa haraharaka akatoka bila hata kupaka mafuta. Magesa alianza kwa sauti ya chini. Mpaka Nanaa anamaliza kuoga, tayari nyumba  ilijaa kilio chake. Akakimbilia chumbani kwa mama G, alipokuwa analala na watoto wake. Akasita mlangoni. Lakini akajikaza. Akafuta machozi, akaingia kama ananyata.

“Unaenda wapi?” Hilo ndilo lilikuwa swali lililomshangaza Nanaa. “Nakuja kumnyonyesha mtoto wangu.” “Huna aibu wala huruma wewe Nanaa!? Umeyaharibu maisha ya Geb, sasa hivi unataka umuharibu mtoto wake! Unamauchafu ya mwanaume mwingine, unataka umnyonyeshe nayo mtoto! Unataka kumuharibu awe mlemavu na tahira? Umenyimwa aibu wewe mtoto! Nguvu ya kukutoa juu mpaka hapa unatoa awapi?” “Nimeoga mama!” Nanaa alijibu huku machozi yakimtoka. Midomo ilikuwa kitetemeka sana.

“Ila sikushangai. Ndio kawaida yako. Umeshazoea kuwahudumia wanaume kwa siri, halafu unarudi hapa nyumbani unajidai, Mama! Mama! Huku unajichekesha. Mnafiki mkubwa wewe. Unawavulia nguo kina Malii, halafu unarudi kwangu unajidai unajiliza unampenda Geb! Ukatuaminisha kuwa wewe ni binti mzuri. Tukamshawishi Geb kuwa wewe ni mke wakuoa! Mwanangu akazaa na wewe, kumbe wewe ni Malaya, huna shida kuvulia nguo wanaume wengine! Unachotaka ni pesa tu kutoka kwa mwanangu! Umaskini gani huo uliokutoa utu na kututapeli kwa kiasi hicho? Umechanganya kundi zima la marafiki. Unamvulia nguo huyu, unalala na huyu. Jana ulitaka kusababisha kifo cha Geb sababu ya umalaya wako. Nimechanwa mdomo kwa ajili yako!” Nanaa alikuwa haamini.

Geb akarudi. Akaingia na vijana wawili. Nanaa akashangaa wale vijana wanapandisha juu chumbani kwao. Geb akampita Nanaa. “Nimbembe yupi? Liv bado anaonekana amelala.” Geb akamuuliza mama yake bila kumtizama Nanaa. “Mnaenda wapi na wanangu?” Nanaa akauliza. “Tumegundua hila zako. Na hazitafanikiwa Nanaa. Labda usubiri mimi nife, ndio utacheza na wanangu na wajukuu zangu. Twende Geb.” Mama G alionekana ameshajitayarisha.

Shilingi Yatumbukia Chooni.

“Geb please!” Nanaa akapiga magoti, akatambaa mpaka alipo Geb akamshika. “Usiwahi kunishika tena Nanaa. Wewe ni muongo na muuwaji. How could you that!? Eti Nanaa? Umewezaje kunifanyia mimi hivyo? Ni siku ngapi nilikuwa na wewe pale hospitalini? Sikukuomba unieleze ukweli wote juu yako na Malii, ukanidanganya?” “Sikukudanganya Geb. Sikutaka kukuumiza. Tafadhali nielewe.” Nanaa aliendelea kulia.

“Nimekuelewa. Tena nimekuelewa vizuri sana Nanaa. Hutawahi kuja kubadilika. Japokuwa nilikuomba usije kunidanganya. Nikakuomba uwe unaniambi ukweli hata kama unajua utaniumiza. Nilikurudia zaidi ya mara tano. Ndio kitu pekee nilichowahi kukuomba kwa kurudia rudia. Lakini uliamua kunidanganya. Tena umefanya na rafiki yangu! Nimekaa na wewe hospitalini Nanaa. Nikiteseka kwa ajili yako! Muda wote nipo pale. Nalala kwenye kiti! Ili tu kuwa na wewe. Nimeacha shuguli zangu zote ili niwe na wewe, lakini umenilipa ubaya wa ajabu sana. Tena huku ukiniangalia machoni! Unawasiliana na Malii, huku ukilala na mimi! Anakuomba penzi na kuzungumza maswala ya mapenzi, huku unalala na mimi. Umemfanyia yale yale unayonifanyia mimi! Je ni wanaume wangapi unawafanyia kama unavyotufanyia mimi na Malii, tena ukirudi kwangu ukijidai unanipenda?” Geb aliongea kwa uchungu sana.

“Ulitaka nikupe nini ili uridhike Nanaa? Ulitaka nikuoe ili uje umiliki mali zangu halafu ndipo ufungue makucha yako? Kwa kuwa mimi sikutoshi kwa chochote, kwa hiyo upo hapa kwa ajili ya mali yangu tu? Sasa, kwa kuwa kwa bahati mbaya sana, umezaa watoto wa pekee ninaohitaji hapa duniani, sina jinsi ya kukufukuza. Kwa kuwa najua ipo siku Magesa atanilaumu sana, nakuachia hii nyumba. Sio kwamba nakupa. Umeshaichafua vyakutosha. Si mimi, watoto wangu wala mama yangu wanaweza kuishi tena humu. Umeinajisi kwa kiwango kikubwa mpaka Mungu aliponihurumia, ndipo akaja kukuadhibu mbele za watu na kunifungua macho. Ulikuwa ukienda kwa wanaume zako, unaenda kufanya unayoyafanya kisha unarudi hapa. Unadanganya kila mtu!” Geb alikuwa mkali na muongeaji, Nanaa hajawahi kumuona.

“Utaishi hapa, kwa vile unavyotaka wewe. Lakini huruhusiwi kuleta wanaume zako humu ndani. Nenda kaendelee kulala nao huko huko nje. Siku ambayo utaleta mwanaume hapa ndani, ujue ndio mwisho wako wakuishi humu ndani. Usithubutu kunitafuta kwa la kheri wala la shari. Leo ndio mwisho hata wa kuiona sura yako.” “Geb usiniache!” Nanaa akaendelea kulia.

“Watoto watakuwa wanaletwa hapa. Dereva akikukosa, ujue ndio basi. Hawaruhusiwi kulala hapa. Utawaona kwa muda mfupi kisha, watarudishwa kwa mama. Wataletwa kwa muda na wakati mama atakaoona unafaa.” Nanaa hakuwa akiamini.

“Mama!” Geb akamgeukia mama yake aliyekuwa akimnyonyesha Magesa maziwa ya chupa. “Huna sababu yakubeba chochote humu ndani. Tutaanza upya mimi na wewe. Mungu atatusaidia tu.” Geb akambeba mtoto wake wa kike, akatoka. Nanaa alibaki amepiga magoti akilia. Baada ya muda Mama G naye akasimama nakutoka. “Mnafiki mkubwa wewe!” Alimsikia mama G akiongea kwa hasira.

Msiba wa Nanaa.

“Mungu uliyeniumba nisaidie mimi! Mungu wangu nisaidie jamani.” Nanaa alibakishwa pale chini kwenye sakafu ya chumba alichokuwa wakilala wanae na mama G. Aligaragara akilia bila kunyamaza. “Mungu nisaidie! Mungu wangu nisaidie. Mungu njoo nisaidie.” Nanaa aliendelea kulia. “Nimekosa nisaidie. Nimekosa nisamehe Mungu. Na wewe usiniache. Nisaidie Mungu wangu.” Nanaa aliendelea kulia bila kunyamaza.

Hakuwa akijua wameenda wapi na watoto wake. Hakujua ni lini atarudishiwa hao watoto. Mtoto aliyeteseka naye hospitalini karibia kufa, anatenganishwa naye akiwa hata hamfahamu mama yake vizuri. Hakuwahi kumuogesha, wala kumvalisha! Hajawahi kukaa naye hata zaidi ya masaa 5 wakafahamiana na mtoto akajua joto la mama yake! Joto analolifahamu Magesa ni la bibi yake tu. Nanaa aliendelea kulia kila akimkumbuka Magesa mtoto ambaye ni kama amemzalia mama G. Alimtoa pale hospitalini na kummiliki kama wake.

Kila alipomkumbuka Liv mtoto wake, alizidi kuomboleza asiamini kama ndio ametenganishwa na mtoto aliyembeba kwa shida akiwa chuoni. Alibakishwa pale peke yake akilia mchana na usiku.

~~~~~~~~~~~~~

 Baada ya siku tatu, mchana, akasikia simu kutoka getini. Anatakiwa kutoka, anamgeni. Alikuta gari ya Geb nje. Akajua ameletewa watoto. Akakimbia mpaka kwenye gari. Jeri ambaye ni dereva akashuka. “Nimeambiwa nimlete mtoto.” “Magesa yuko wapi?” Nanaa akauliza huku analia. “Nimeambiwa nimlete huyu tu.” Nanaa akapiga magoti nje ya gari akazidi kulia.

Alijua muda mfupi atakao kuwa akiletewa hao watoto, angalau Magesa atamfahamu. Alilia mpaka Liv na yeye ndani ya gari akaanza kulia. Akasimama kwa haraka na kufungua mlango ili amchukue mtoto. Jeri akamuwahi. “Nimeambiwa haruhusiwi kunyonya wala kuingia ndani.” “Sasa hapa nijuani. Nitasimamaje na mtoto hapa!?” Nanaa kauliza. “Nimeambiwa pia asitolewe ndani ya gari.” “Haiwezekani jamani! Huku nikumwadhibu mwanangu. Ona mtoto anavyonililia. Mimi namtoa.” “Hapana dada. Nimekatazwa kabisa.” Jeri akamzuia kabisa. Nanaa alizidi kulia kama amefiwa. Liv analia, mama yake naye analia.

“Naomba umuondoe hapa. Huku nikumtesa mtoto wangu tu. Mwambie Geb, Mungu anamuona. Waache kuwaadhibu wanangu kwa kosa nililolifanya mimi.” “Lakini kuna kitabu hiki. Natakiwa mimi nikifika hapa nikiweke saini, na wewe uweke saini kuwa umeona watoto.” “Sitafanya hivyo.” Nanaa akajibu kwa jeuri huku akilia. “Nimeambiwa ukikataa nikwambie hawa watoto hawatarudi tena.” Nanaa akazidi kulia. Akaweka saini.

“Unarudi tena lini?” “Sijui dada yangu. Ni mpaka nitumwe.” “Naomba wakikutuma tena uniletee watoto, hakikisha unakuja na Magesa.” “Unajua siwezi dada yangu. Nafanya kile ninachotumwa.” Liv alikuwa akilia sana akimtaka mama yake. Mikono yote ilikuwa juu. Analia akiita mama, mpaka akawa mwekundu kabisa.

“Kama hutaniruhusu kumshika mwanangu, naomba mtoe hapa.” Bila kuongeza. Akapanda kwenye gari, akaondoka huku Liv analia sana.

~~~~~~~~~~~~~

Nanaa akarudi ndani huku akilia asiamini ukatili anaoendelea kufanyiwa. “Mungu! Usiruhusu wanangu wapitie nilikopita mimi. Kama unapatiliza dhambi ya mama yangu, natubu. Natubu Mungu wangu msamehe mama yangu, nisamehe mimi na wanangu. Tusamehe baba. Warehemu wanangu kama unavyowarehemu watoto wengine. Hawakuchagua kuzaliwa na mimi! Wewe ndio umewachagulia watokee kwangu. Kama nikuchagua kuzaliwa, basi wangechagua wazazi wanaopendana na wenye ndoa nzuri. Lakini Mungu, usiwahesabie hatia wanangu. Kumbuka rehema Baba yangu. Wakumbuke wanangu.” Nanaa aliomba siku nzima akilia kwa uchungu sana.

Hiyo siku ikapita, na kesho yake pia. Baada ya siku tatu tena, Nanaa akaletewa watoto wote, lakini wakiwa wamelala kabisa. “Kwa nini wananifanyia kusudi jamani? Hawataki niwashike wanangu! Halafu wanawaleta wamelala! Ndio natakiwa kufanya nini?” “Saini hapa.” Jeri alishashuka na kukaa upande aliokuwepo Nanaa ili asije kufungua mlango. “Hakika sita saini. Kawaambie nimekataa. Labda waniruhusu nishike wanangu. Nina saini ujinga tu. Hapana.Yule dereva akarudi ndani ya gari. “Hivi Jeri una watoto wewe!” Nanaa akamuwahi kabla hajaondoa gari. Akauliza huku akilia kwa kwikwi. Jeri akanyamaza. “Nijibu tu.” “Ninao dada.” “Sasa unafikiri hivi wanavyowafanyia watoto wangu ni sawa?” Kimya. “Hata kama mimi ningekuwa mbaya wa namna gani, wangeniadhibu mimi. Lakini sio watoto wangu.” “Lakini nilimwambia bibi kuwa Liv anamtaka mama yake. Akasema..” “Sitaki kujua alichokujibu. Ila hivi sio sawa kabisa.” “Naomba niondoke dada yangu. Wanasubiriwa hawa watoto.” “Naomba nisaidie namba yako ya simu.” Nanaa akamuwahi tena. Jeri akaindika mahali, akamkabidhi Nanaa. Akaondoka.

Nanaa akarudi ndani akilia sana. Alilia Nanaa bila kujua chakufanya. Kwa muonekano wa Magesa, alionekana amelishwa vizuri na ameshiba. Alikuwa akivutia. Wazi alionekana anatunzwa vizuri. “Huyu mtoto hatakaa anijue kama mimi ni mama yake.” Nanaa alizidi kulia. “Liv wangu jamani mimi! Mungu nisaidie.” Nanaa akaendelea kuomboleza.

~~~~~~~~~~~~~

Zilipita siku saba Nanaa akilia bila kuletewa watoto. Akakata tamaa. Akakumbuka hakusaini lile daftari kuwa aliona watoto, na aliambiwa asipoweka saini yake, ajue ndio hatakaa aone watoto wake tena. Akajua ndio basi tena. Kwenye chumba chake na Geb hakuwahi kurudi kulala tena. Aliishia kulala kwenye makochi huku akishindwa kupata usingizi. Kila akifunga macho, alimuona Malii anamfanyia hiki au kile. Akaishia kukesha. Pengine kusinzia kidogo hapo hapo kwenye makochi lakini sio kulala vizuri.

~~~~~~~~~~~~~

Njaa nayo ikaanza kumsumbua. Hakuna wakumpikia. Inabidi ajipikie mwenyewe. Akajua maisha mapya yameanza. Maziwa yalikuwa yamejaa sana. Alishakamua mpaka akajaza kila chombo humo ndani akawa anaweka kwenye friji, hana wakumpa au kuyanywa. Akaamua kutoka kwenda duka la madawa, kuulizia kama kuna dawa yakukausha maziwa. Hakupewa jibu lililomfurahisha sana, kwani walimwambia ayaache tu. Asikamue tena mpaka yakauke yenyewe.

Kwa asili Nanaa alijaliwa maziwa mengi sana. Yalikuwa yamejaa, yanamuuma kama majipu. Ikawa kama bahati tu, akakutana na mwanaume, sio mtumzima sana, alikuwepo hapo pembeni, akadakia kwa kumpa ushauri wa kiasili tu wala si kidaktari. Akamwambia awe anaweka maganda ya kabichi, yabaridi kwenye matiti yake. Akamtupia huo ushauri kuwa ayaweke maganda hayo ya kabichi kwenye friji mpaka yapate baridi ndipo ayaweke kwenye matiti yake yakiwa vile vile ya baridi.  Nanaa akaondoka hapo kwa uchungu sana akiumizwa na wazo kuwa mwanae anapewa maziwa ya kopo wakati yake yapo tu! Aliumia sana.

~~~~~~~~~~~~~

Mwisho wa mwezi ulikuwa umepita kama siku mbili. Geb alikuwa ana mtindo wakumuwekea pesa kwenye akaunti yake. Akaamua kupitia kwenye ATM, akangalie na huko nako kukoje na achukue pesa baadhi. Akakuta hapajawekwa pesa mwezi huo. Akajua safari hiyo Geb amemuamulia kweli kweli. Akapanda daladala yakurudi kwake akiwa na pesa kidogo yakumsaidia matumizi yake endapo atataka kitu.

Akatembea taratibu mpaka getini. Mlinzi akamwambia watoto waliletwa, lakini hawakukaa sana kwa kuwa hakuwepo. Nanaa alianguka chini nakuanza kulia pale mbele ya yule mlinzi. Yule mzee akamuhurumia. Akamshika mkono nakumwingiza ndani huku akilia sana.

Alipotulia akaamua kumpigia simu Jeri, dereva wao. “Nilisharudisha watoto. Hapa nimetumwa maziwa ya mtoto.” Nanaa akazidi kulia. Akajua ni maziwa ya Magesa. Unaweza kuwaleta? Nimerudi.” “Sidhani dada. Baba yao ametupa glasi kwa hasira baada yakumwambia haupo nyumbani. Sidhani kama watarudishwa tena.” “Waambie nilienda duka la madawa tu. Nimerudi.” “Acha nikwambie ukweli dada, hakuna anayekusema vizuri pale. Hasa bibi. Anakulalamikia vibaya sana. Na leo ameapa kumtafutia mwanae mke, aoe, ili alee hao watoto. Wakufute kabisa kwenye maisha yao.” Nanaa alihisi kuchanganyikiwa.

~~~~~~~~~~~~~

Presha nayo haikukawia kutibuka. Nanaa akaanza kujisikia vibaya. Akajua wazi pressure ipo juu. Alihofia kutoka tena pale asije kuwakosa tena wanae pindi watakapoamua kuwarudisha tena. Akavumilia tena siku tatu mbele, akaona kimya lakini hali ikawa inazidi kuwa mbaya. Wakati mwingine hakuwa akiweza hata kutoka pale alipokuwa amelala kwenye kochi.

Akaona kwa ile hali hata akibaki pale akaletewa watoto awapakate, hataweza. Akajiamulia kurudi hospitalini akaonane na yule daktari aliyekuwa akimtibu. Dokta Lyamu. Alimtafuta kwenye simu. Akamwambia kwa wakati ule hana pesa. Wakashauriana wakutane hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako haitamgarimu sana, kama kule alikomuona kwa mara ya pili kwenye hospitali ya kulipia, ambako Geb ndiye aliyekuwa akigarimia matibabu hayo. Akaona wazo zuri.

Alitoka pale akiwa na hali mbaya sana. Akatembea kwa shida mpaka kwenye kituo cha daladala. Akiwa ndani ya daladala yakuelekea muhimbili akaanza kutokwa jasho jingii. Akaomba apishwe kwenye kiti. Akakaa. Daladala iliposimama tu, akashuka na kuchukua taksii. “Naomba nikimbize hospitali ya taifa ya Muhimbili. Najisikia vibaya sana baba yangu.” Yule Mzee, dereva taksii akaondoa gari. Nanaa akajilaza kiti cha nyuma.

Alimfikisha mpaka mbele ya dokta Lyamu huku amemshikilia mkono. “Vipi?” Akauliza mara alipomuona anakuja huku ameshikiliwa. Na yeye alikuwa akitoka. “Najisikia vibaya sana.” Nanaa akajibu huku akitetemeka. Dokta Lyamu akampokea. “Na mimi natoka mara moja, nitarudi baada ya muda mfupi sana. Nesi atakupima vipimo vya awali. Kisha nitakuja kuendelea.” Nanaa akatingisha kichwa kukubali.

Akaingizwa kwenye chumba cha pembeni. Akaanza kufanyiwa vipimo. “Unakaribia kupata stroke, dada. Pressure yako ipo juu sana!” Yule nesi aliongea akionekana ameshapaniki. Hapo hapo akampigia simu dokta Lyamu. Akarudi kwa haraka sana. Nanaa akapewa huduma ya kwanza na kupelekwa wodini. Sababu ya mawazo mengi, walisumbuka sana kushusha pressure yake. Aliishia kuchomwa sindano za usingizi ili kumfanya alale. 

Msiba Na Mwenzie.

Alijikuta mwezi ukiisha akiwa bado hospitalini. Akajua kwa uhakika hatapata tena watoto wake. Kila alipokuwa macho, alikuwa akilia. Si mchana si usiku. Matibabu yaliendelea huku presha nayo ikiendelea kuwa vile vile bila kushuka hapo alipokuwa amelazwa wodini. Sio kwenye chumba cha peke yake kama alivyozoeshwa na Geb kuwekwa chumba cha peke yake, tena kwenye hospitali za garama sana, na za huduma za hali ya juu. Hicho hakikumsumbua hata kidogo. Hakuwa hata na mtu wakumtembelea. Hilo nalo alilitegemea. Alijua kaka yake James atakuwa hana uwezo hata wakumtizama tena machoni. 

Siku zilizidi kwenda akiwa bado hospitalini, ikabidi aanze kujishauri mwenyewe. “Nimerudi sifuri kabisa!” Nanaa akajiwazia. “Lazima niwe imara. Leo wamefanikiwa kunipokonya watoto wangu. Lakini ipo siku wanangu watanitafuta tu. Mungu yupo. Sasa wasije kupatwa na akili, wanataka kumjua mama yao, na mimi nimekufa! Lazima nitoke hapa nilikojificha.” Nanaa akajishauri.

“Uzuri nilisoma. Naweza nikahangaika kupata kazi, lakini nitafanikiwa tu. Mungu wangu upo.” Nanaa akawaza na kujitahidi kutulia. Geb alikuwa akimuwekea pesa yakutosha. Kwa hiyo hata akaunti yake ilisoma vizuri. Akaanza kupiga mahesabu pesa aliyonayo. Akajua anamwanzo mzuri kabisa. Wapi pakuishi. Ndio ukawa mtihani. “Siwezi kuendelea kuishi pale. Nitajitesa tu. Heri nikatafute kwangu.” Nanaa akakusudia. Akaamua akitoka pale, akaanze maisha yake sehemu nyingine. Angalau akaanza kulala vizuri. Na vilio vikakoma. Ikawa inaendelea mikakati tu kichwani mwake. Anawaza hili na kupanga lile, ilimradi maisha yasije simama mara baada yakutoka pale. 

~~~~~~~~~~~~~

Mwanamke wa jirani yake akamuona ameanza hata kuchangamka.  “Habari za asubuhi?” Nanaa akasalimia wakati anaelekea msalani. Yule dada akaitikia. Nanaa akapita. Aliporudi yule dada akamsemesha. “Naona leo umeamka na nguvu!” Nanaa akamwangalia tu, nakunyamaza. “Unajisikiaje?” Akaendelea kumuhoji. Akamfananisha yule dada na mama G. Alimuanza kwa upendo lakini mwishowe akampokonya na watoto. Akapanda kitandani akajilaza bila kujibu.

“Na mimi nilikuwa nikilia hivyo hivyo! Tena mimi nilimkasirikia mpaka Mungu. Basi kufa hufi, unabaki unajitesa tu mwenyewe. Nilikaa kwenye hali hiyo mpaka nikaamua  kujifariji tu. Maana wakunifariji pia sina! Mtu uliyekuwa na mume na watoto, gafla unabaki peke yako! Maisha ni kitu kingine!” Kidogo akaanza kumgusa Nanaa.

“Una watoto wa ngapi?” Nanaa akamuuliza. “Wakike wawili.” Nanaa akanyamaza. “Unataka kuona picha zao?” Akamuuliza tena Nanaa. Akamtizama kwa muda, akamuona analia bila kujibu. Huo ndio ukawa mwanzo wakufahamiana kwa yule dada na Nanaa. Siku nzima Nanaa na yule dada wakawa wakizungumza. Nakufahamiana.

Yule dada akamueleza historia ya pressure aliyonayo. Nanaa akamuhurumia sana. “Pole.” Ndicho kitu pekee alichoweza kusema baada yakumsikiliza kwa muda mrefu nakumuhurumia. “Nitafanya chochote humu duniani kupata hata dakika tano tu nyingine na mume wangu na wanangu. Nakwambia chochote. Niliumwa karibu kufa. Hawa wauguzi wote wameshanizoea hapa. Vikitibuka tu, nakaa nao hapa mpaka wananichoka.” Nanaa aliendelea kumsikiliza.

“Pole sana.” “Ndio maisha mdogo wangu. Wakati mwingine unapata hiki, kile kinaondoka. Tulipokuwa tumefika na mwenzangu, nilikuwa sidhani kama kuna kitu nitataka tena hapa duniani. Siwezi kusema tulianza chini sana, kwa kuwa wote tulitoka kwenye familia zenye aghueni. Lakini mtaji wetu mkubwa ilikuwa penzi. Acha dada yangu. Mimi nilipendwa! Tena penzi la dhati, achana na haya mapenzi ya kwenye tv. Penzi la haja! Lakini Mungu alinipokonya mchana kweupe!” Yule dada aliendelea.

“Ilikuaje? Kwani wewe hukuwepo kwenye hiyo safari?” Nanaa akauliza tena. Maana yule dada alikuwa akisimulia kama Nanaa anafahamu kila kitu ila anarudia tu. “Si ndio nilikwambia tulikubaliana mimi nibaki. Nipokee mzigo, halafu nimfuate baada ya siku mbili. Nikishaweka mambo sawa, basi nimfuate. Sasa kaka yake ndio anasema anahisi alipata hiyo ajali baada ya kumpigia simu na kumwambia mama yao amefariki huko hospitalini. Kwa hiyo asiende moja kwa moja hospitalini kama alivyokuwa amesema, aende tu nyumbani. Sasa mume wangu alikuwa kipenzi cha mama yake. Nahisi ndio kuchanganyikiwa na kupata ajali.” Yule dada aliongeza.

“Yaani Dada! Pale pale, wote wanne na mtoto wa shangazi yake tuliyekuwa tukiishi naye. Alikuwa kijana ambaye tunashirikiana naye sana kwenye biashara zetu. Yaani tulishibana na yule kijana kama yeye ndio alikuwa mdogo wangu mimi. Mungu aliwachukua siku moja! Kufunga na kufungua nikajikuta sina mume wala watoto. Kijana ambaye labda ungesema angebakishwa tusaidiane, na yeye hapo hapo akafariki. Tulizika watu watano kwa siku moja. Mama mkwe ambaye ndio alikuwa mgonjwa, wakawa ndio wanakwenda kumwangalia, mume wangu, binti zangu hao wawili na huyo kijana!” “Pole sana.” Nanaa aliishia kusema hivyo tu.

“Tena nilizaa watoto wanaakili dada! Asikwambie mtu. Namba moja tokea wanaanza shule mpaka kifo. Mmoja alikuwa ndio amemaliza la saba, mwingine ndio alikuwa la tano. Nazunguka na picha za hao watoto kama mwehu! Utafikiri wapo nyumbani wananisubiri.” “Pole sana.” Nanaa akaongeza. 

“Nimeachiwa mali na nyumba. Lakini asikwambie mtu, nyumba ni watu. Na watu mnaopendana. Hata ukiwa na gorofa 3, na kila kitu ndani halafu uliowapenda hawapo, havina ladha.” Nanaa akajihisi anamsema yeye.  “Lakini ndio maisha bwana! Nimekuwa kama mwehu. Wakati mwingine hata mimi nahisi nimechanganyikiwa. Nikaacha kila kitu, nipo hapa kama unavyoniona. Vikitibuka nakuja kukaa nao hapa. Wakitaka kuniruhusu wakati mwingine nakataa. Naona heri nikae hapa kidogo. Haya, ukikaa hapa, ukisikia matatizo ya wengine, wakikupa na vijidawa vya usingizi, unajsikia vizuri. Unaona matatizo yako sio makubwa kama wengine. Basi siku zinasogea. Au unasemaje?” Nanaa akacheka nafsi mwake.

 Mabadiliko Yalazima.

“Huko nikujidanganya.” “Heri kujidanganya kuliko ukweli wa dunia.” Nanaa aliropoka tu. Hakumaanisha. “Sasa utajificha hapa mpaka lini? Ni heri ukakae hata kwenu.” “Kwenu, huna pesa!? Hujakutana na ndugu zangu wewe. Walinipa pesa ya mtaji nianze biashara. Halafu nikajidai naomboleza nikapoteza mali zote. Hakuna anayetaka kuniona tena. Wakiniona tu wanajua nataka kuwakopa.” Nanaa akashangaa.

“Kwani imekuaje kwenye hizo biashara zako?” “Ipi!? Biashara gani!? Nani afanye? Kwa kichwa kipi kwa mfano hapa? Nakwambia kuna wakati hata moja jumlisha na moja sina jibu! Nilipoteza kila kitu. Nimebakiwa na nyumba tu. Ndipo hapo ninapoishi kama sipo hapa.” Nanaa akamtizama.

“Unanishangaa?” Akamuuliza Nanaa. “Na huyu mwanaume anayekuja kukuangalia wakati mwingine?” “Ndugu wa mume wangu. Tena undugu wa mbalii. Ndiye nimebakiwa naye. Tena ukimuona kaja hapa, ujue mkewe hafahamu.” “Kwa nini!?” Nanaa akauliza tena.

“Wivu tena! Anahisi kama nitamuibia mumewe. Eti  kwa kuwa mimi sina mume.” “Kwani mume wako amefariki lini?” Ikabidi Nanaa kuuliza maana huyo dada ni mzungumzaji haswa ikabidi amkatize kwa swali. “Juzi ya juzi tu! Kama miaka miwili iliyopita.” Nanaa akakaa vizuri kwa mashangao “Miaka miwili!?” “Acha tu mdogo wangu!” Nanaa akabaki akimtizama. Gafla akaona matatizo yake sio kama ya huyo dada. Yaani yule dada anahitaji msaada wa haraka sana kutoka hapo kuliko yeye. Gafla akaona amsaidie.

 Akamuhurumia na kuamua kumpa historia yake. Akamsimulia historia nzima ya maisha yake mpaka kufikia hapo alipo. “Kilichonisaidia pekee mpaka unaniona hapa wodini na wewe, nikusimama na kuchukua hatua.” “Pole sana. Kumbe na wewe yamekukuta!” “Hakuna na wala hakuna atakayekuhurumia kama hutasimama wewe mwenyewe. Leo napata pole yako, kwakuwa nilitoka pale kwenye kochi nikaja hapa nikiwa nakaribia kupata stroke. Sijui kama unanielewa?” Nanaa alishabadilika.

“Umeniona hapa nalia, ukashangaa. Nilikuwa nalia kuanzia siku nabakwa mpaka natoka pale getini. Tena kwa sauti ya juu. Nilipohisi nitakufa, ndio nikajiona vile nilivyomjinga. Nitakufa niwaache wanangu. Ndugu zao wanapesa sana. Watawapa kila kitu. Watawapeleka wanangu kokote. Baba yao ataoa mwanamke yeyote yule. Hata kama huyo mwanamke atakuwa anawaka kama nyota, lakini na pesa zao zote, hawawezi kuwapa wanangu mama mzazi. Ipo siku watanitafuta tu. Sikutaka waje waonyeshwe kaburi. Nilitaka waje kukutana na mimi mwenyewe. Ndio maana nipo hapa.” Nanaa aliongea kwa ujasiri kama sio yeye.

“Leo nimeamka tofauti kwa kuwa nimeamua kuacha kujiliza na kujionea huruma. Itakula kwangu mazima! Nina mpango wakutoka hapa na kutafuta pakuishi nikaanze maisha. Nimekataa kuwatesa wanangu. Au mwanangu mkubwa. Akiniona analia sana. Anataka nimshike, na mimi siruhusiwi.” “Lakini ni washenzi sana hao watu!” Yule dada akapandwa na hasira.

“Hapana dada yangu. Acha wakasirike tu. Wana haki. Lakini najua hawajui kama wanawaadhibu watoto. Wale watu walijitoa sana kwangu. Yule mwanaume alikuwa akilala na mimi hospitalini. Kuanzia siku naingia mpaka natoka hospitalini. Haniachi. Alinipa mapenzi ya kweli. Mimi mwenyewe nimeharibu. Nimesikia wanamtafutia mwanamke aoe. Naumia sana. Lakini lazima nifanye kitu dada yangu. Kama nilivyokwambia historia yangu, sina mama mimi, wala baba. Na ninajua kaka hataki tena kuniona. Kwanza nimemwaibisha mnoo. Hakutegemea. Tokea ametoka pale, hajarudi tena wala hajanitafuta tena. Na yeye alishaniulizia kuhusu huyo mwanaume aliyenibaka, ambaye alikuwa rafiki yake kama nilivyokwambia, lakini sikumwambia ukweli au niseme nilinyamaza. Sasa hebu niambie, nikijilaza hapa nakulia, mwisho wake nini?” Yule dada akabaki kimya.

“Angalau wewe una hata shemeji wakuja kukutizama. Mimi nikikaa hapa, ndio kila kitu kimelala. Nataka dokta akipita, nimwambie aniandikie dawa, niondoke.” “Basi naona na mimi niondoke tu.” “Kumbe! Tena angalau wewe unahata pakuweka kichwa.” “Sina hata shilingi!” Yule dada akalalamika. Nanaa akajua ndio maana watu wanamkimbia kwa kuomba pesa.

“Wewe si una nyumba? Anza kuipangisha. Pangisha vyumba baadhi, bakisha hata kimoja upate pesa.” “Yaani nikaishi na watu!? Sijawahi mwenzio.” “Kwa hiyo ni heri hivyo unavyotangatanga ukiomba? Jiwekee muda wakujiweka sawa. Kubali kuishi na watu, ili upate pesa Ukianza biashara, ikichanganya, unawatoa wapangaji wako, unaendelea kuishi peke yako.” Kama mwanga ukamulika kichwa chake.

“Umenifungua dada yangu. Maana ndugu zangu waliniambia niuze.” “Hapo ndipo utakapochemka mara 100. Nyumba ni kitu ambacho hakishuki thamani. Usiuze. Pangisha. Na mimi nitakuwa mteja wako wa kwanza.” Wote wakacheka. “Sikutanii. Si nimekwambia natafuta pakuishi? Ndio niwekee chumba.” “Tena umenipa wazo zuri hivyo! Wewe nakupa chumba chenye bafu na choo chake kabisa. Cha nje, ujitegemee.” “Hayo ndio maneno.” Nanaa akachangamka, tumaini jipya likachipua.

Yule dada naye akamshukuru Nanaa, wakabadilishana namba za simu na kupeana sasa majina. Akamwambia anaitwa Fridah, lakini watu wamezoea kumuita Fifi. Wakakubaliana kuishi pamoja, wakitoka pale. Waliruhusiwa siku moja. Nanaa akamwambia atahamia kwake siku inayofuata.  

Kuliko Ungua Mpini.

Zilishapita siku zaidi ya 35 tokea Nanaa atoke hapo nyumbani. Alirudi akiwa na nguvu sio kama alivyoondoka. Akapita ndani pale getini kusalimia walinzi. “Sisi tulijua umeondoka dada.” Nanaa akacheka kinyonge. “Nilikuwa hospitalini. Mna ujumbe wowote wa kwangu?” “Walileta watoto mara mbili, naona baada ya kukukosa. Wameacha.” “Haya. Asanteni.” Nanaa akataka kupita. “Kulifungwa. Tukaambiwa tukae na fungua kama utakuja kurudi. Ziko hapa.” Nanaa akarudi kuzichukua akaelekea ndani.

Akaingia stoo. Akatoa vitu vyake vyote na kuviweka sebuleni. Akaanza kufungasha taratibu. Madaftari kuanzia yupo chuo mwaka wa kwanza, yalikuwepo hapo. Akacheka. “Kweli shule ndio utakuwa mkombozi wangu. Sasa hivi ni muda wa kuingia kazini.” Aliviambia vyeti vyake. Akakusanya kila kitu chake. Hakuacha hata kimoja.

Vyote alivyokuwa amenunuliwa na Geb, akabeba. Akachukua na mabegi ya Geb aliyokuwa akisafiria. Akapanga vitu vyake humo. Akaingia chumba alichokuwa akilala mama G na wanae. Akachukua nguo moja moja za watoto wake. Nazo akabeba. Usiku kucha alikuwa na kazi yakupanga, kusafisha na kuchoma moto vitu ambavyo hakuvihitaji tena.

Wakati panapambazuka, akawa amemaliza. Kila kitu chake kikawa kipo mlangoni. Akaingia kuoga, akatoka akawa amekaa anawaza. Akaamua kumuandikia ujumbe Geb.

Barua Kwa Geb.

“Geb mpenzi wangu, nimekukosea sana. Najua hakuna jinsi unaweza hata kunisikiliza tena, lakini naamini ipo siku Mungu atakupa rehema yakunisamehe. Nashukuru kwa kuniruhusu kuendelea kuishi hapa, lakini Geb, kumbuka hii nyumba tulihamia mimi na wewe. Wote wawili ndio ilikuwa mara yetu ya kwanza kuhamia hapa. Nakumbuka usiku wetu wa kwanza chumbani kwetu, ulinisistiza na kuniomba nikutengenezee ‘home’. Ukasema hili jengo halina maana kama sisi wote hatutakuwepo humu ndani na kama hakutakuwa na amani. Nakiri kuivunja hii nyumba kwa mikono yangu mimi mwenyewe. Sina chakujitetea. Nakutetea hata mbele za Mungu, ulifanya kwa nafasi yako. Tena kiuaminifu sana. Sijawahi pata mapenzi kama uliyonipa Geb. Nakiri, na ninakutetea mbele za Mungu, hata mbele za watoto wetu hapo baadaye. Hakika huna hatia Geb. Upo sahihi kuniacha. 

Nimeshindwa kutimiza jambo kubwa nililokuwa nimekuahidi Geb, lakini nakuahidi kukuombea. Nimetubu. Na nitaendelea kutubu kwa kutokukwambia ukweli wote na kuishia kukuumiza mpenzi wangu. Najua Mungu atanisamehe na kunisikiliza. Nimeambiwa unatafutiwa mke ili uoe. Nakuahidi kukuombea mpenzi. 

Nitakuombea bila kuchoka ili Mungu akupe mwanamke atakayekupa yale yote niliyoshindwa mimi kukupa. Na asikuumize kama nilivyokuumiza mimi. Nakuombea faraja na amani ile ipitayo fahamu zote, ikufunike Geb. Najua unaweza ukaona haitawezekana kwa yale niliyokusababishia. Lakini Geb, Mungu yupo. Jipe muda tu, ipo siku Mungu atarejesha furaha yako kwa upya.

Hili jengo na vitu vyote vilivyomo humu ndani ni vya thamani sana. Lakini haviwezi kukamilika kama wewe na watoto hampo humu ndani. Sitaweza kuishi humu ndani peke yangu. Hata hivyo naona itakuwa mateso makali zaidi kwa Liv. Analia sana akiniona. Anataka nimshike, wakati umeweka masharti magumu sana kati yangu na wanangu, Geb. 

Ni heri niondoke wazoee kuwa hawana mama, kuliko hivyo wanavyolia nakushindwa kuwabembeleza wanangu. Inaniuma kuliko nitakavyokueleza. Unajua jinsi nilivyokuwa nikiwazaa kwa shida. Ilikuwa kufa na kupona ili wao wazaliwe. Sikubahatika kuwa na mama. Ningependa wanangu wanione. Lakini sio kwa mateso kwa kiasi hicho Geb. Sitaki wanangu walipe garama ya kosa langu. Ni heri niondoke tu. Naamini Mungu atawasaidia kwa namna nyingine. 

Sitarudi tena hapa. Kuwa huru kuuza tu. Najua hutaweza kuja kuishi tena humu kwa yale yaliyotokea humu ndani. Hata mimi sijaweza kupata usingizi tangu usiku ule. Imekuwa mateso matupu. Kwa hiyo kuwa huru kufanya chochote na hii nyumba yako. Mimi nakwenda kuanza upya, sehemu nyingine. Hakika nakushukuru Geb. Asante kwa mapenzi ya kweli uliyonipa. Nakuombea kila la kheri. Mungu akujalie hekima ya kuwalea watoto wetu vizuri. Mungu azidi kukufanikisha katika kila eneo la maisha yako.

Nanaa.

~~~~~~~~~~~~~

Machozi yalikuwa yakimtoka Nanaa. Simu ya Fifi ndio iliyomtoa kwenye majonzi wakati anarudia kusoma barua yake. “Unalia tena? Mbona ni kama tuliwekeana mikakati yakutokulia tena!?” Nanaa akacheka kidogo. “Shikamoo dada Fifi.” “Marahaba mdogo wangu. Sasa ndio kumekucha. Inakuaje?” “Nishamaliza kuweka kila kitu. Hapa nataka nikaite taksii ije inichukue mimi na mizigo yangu. Inilete kwako. Ushanitayarishia chumba?” Nanaa akamuuliza. “Ndio ilikuwa kazi ya usiku kucha. Ujue ni chumba alichokuwa akiishi yule kijana! Sijawahi kukifungua tokea tuwazike. Mama yake alikuja akachukua vitu vyake, nikakifunga.” Nanaa akatulia asijue asema pole au afadhali.

“Wewe Nanaa?” “Nipo nakusikiliza dada yangu.” “Sasa usafiri utapata wapi? Maana mwenzio tokea mume wangu apate ajali, sijarudi kuendesha. Nina gari liko hapa. Nina kazi ya kulipasha moto tu lisiharibike. Kuna kijana anakuja kulichukua, analiendesha kidogo, na kulirudisha.” “Bwana njoo unichukue dada Fifi, acha mambo yako!” “Nimeingiwa hofu mwenzio. Sitaki kuendesha.” “Tulizungumza nini na wewe unafanya nini sasa?” “Hatua ndogo ndogo kama za mtoto mchanga, Nanaa mdogo wangu! Ni jana tu umenitoa kule hospitalini. Leo unataka kuniingiza barabarani!” “Acha kujilalamisha dada Fifi bwana! Njoo unichukue. Nitakulipa. Badala nimlipe dereva taksii si heri nikulipe wewe usie na pesa.” Akamsikia anacheka. 

“Unakuja?” “Nanaa akianza jambo! Basi nakuja. Lakini ujue mwendo wangu utakuwa kama kinyonga!” “Wewe hata ukifika usiku wa kesho. Wewe njoo tu.” “Haya ndio mambo. Basi nisubiri.” Wakaagana.

~~~~~~~~~~~~~

Akaendelea kuweka kila kitu kwa usafi ili asipaache pachafu. Alishafua mashuka ya kitandani kwao. Akaacha chumba kisafi lakini hakina nguo zake wala za Geb. Geb alishahamisha vitu vyake siku ile ile alipokuja kuchukua watoto wake. 

Baada ya kama lisaa, Fifi akampigia simu amuelekeze nyumba ilipo. Alikuwa karibu tu. akamuelekeza mpaka akafika pale. Alimkuta Nanaa getini akimsubiria. Akaomba afunguliwe Geti. Fifi alitoa macho baada yakufika pale. 

“Acha utundu dada Fifi!” “Kumbe ulikuwa unaishi ikulu!?” Nanaa akacheka. “Twende ukanisaidie kutoa mizigo. Halafu unagari nzuri hivi! Lazima kulifanyia kazi.” “Yaani tumelinunua mwaka ule ule aliokufa mume wangu! Lilikuwa bado jipyaa! Utaona ndani.” “Basi huyo mumeo huko atakuwa anasikitika sana!” “Usiseme hivyo Nanaa! Kwanza kwa nini?” “Si umemvunja moyo! Yaani amekuacha pazuri, ukajigeuza omba omba! Aibu zako dada Fifi.” “Kufiwa kubaya Nanaa wewe.” “Pole dada yangu. Mimi nakuchangamsha tu.” Wakasaidiana kupakia mizigo ya Nanaa ndani ya gari mpaka wakamaliza.

“Nisubiria hapo nje getini. Nataka kuzungumza na hao walinzi kabla sijaondoka.” Nanaa aliongea huku akifunga milango. “Lakini nataka uhakika Nanaa. Kweli unatoka kwenye nyumba kama hii unahamia kwenye chumba kimoja! Kweli!” “Hapa si kwangu dada. Na mimi nilipakuta, na kupashangaa hivyo kama unavyoshangaa wewe. Halafu sijaweza kulala humu ndani tokea nifanyiwe ule unyama. Silali dada. Nakesha nikizunguka humo ndani kwa hofu. Sitapaweza. Uzuri huo ni wa macho tu. Nikiendelea kulala hapo, nitakufa siku si zangu. Acha nikaanze upya dada. Ipo siku na mimi nitakuwa na kwangu. Hata hivyo nimechelewa tu. Nilitakiwa niwe nimeshafika mbali.” “Bado mdogo sana Nanaa. Utafanikiwa tu.” “Amina dada.” Fifi akatoka.

Nanaa akarudi getini. Akawakabidhi funguo. “Naomba niwashukuru kwa heshima mliyonionyesha tokea nahamia hapa mpaka leo. Naona sina kitu chakufanya hapa. Nimeamua kuondoka.” “Unaacha jumba lote hili dada!” Nanaa akacheka. “Tumeambiwa tukulinde.” “Sina chathamani chakulindwa baba yangu. Nimepoteza kila kitu. Acha nikaanze upya.” “Nakuombea heri mama. Mungu awe nawe.” “Amina baba yangu.” Wakazungumza kidogo tena. Nanaa akaacha funguo na barua akatoka, akijua wote wanajua yaliyompata. Maana mmoja wao ndio alikuja kumfungua siku aliyobakwa. Akajua japokuwa wanabadilishana, lakini lazima habari zimeenea. Akaondoka.  

~~~~~~~~~~~~~

Haikuwa nyumba kama ya Geb, lakini si pabaya hata kidogo. Walijenga nyumba yao mitaa ya Kawe, njia ya kwenda Mbezi. Ilionekana bado ni nyumba mpya tu. Lakini hapakuwa hata na ua moja wala ukoka hapo nje. Nyumbani kwa Geb palikuwa kijani haswaa. “Heee! Mbona pakame hivi kama jangwani? Huna maji?” “Tulichimba kisima. Nina maji mpaka yanatoka kwenye shawa. Utaoga mpaka uchoke.” Nanaa akacheka.

          Wakaingia ndani kwenye geti. Nyumba ilizungushiwa uzio mzuri tu, lakini mfupi. Uliweza kuona kila kinachoendelea ndani. Nanaa akapelekwa mpaka kwenye hicho kinyumba cha nyuma ya hiyo nyumba kubwa. “Na huo upande mwingine nani anaishi?” “Nakwambia hamna mtu.” “Na pako kama hapa?” Nanaa akaendelea hukoji baada ya kuonyeshwa sehemu yake. “Kama unavyopaona hapa, ndivyo huko navyo kulivyo.” Nanaa akaweka mizigo yake yote ndani.

“Njoo kwanza dada yangu.” Fifi akasogea. “Japokuwa sijajua utanidai kiasi gani, lakini naomba nikushukuru. Asante. Naona mwanzo wangu si mbaya.” Wakacheka. “Au utanipokonya kitanda?” Nanaa akauliza. “Nipeleke wapi mdogo wangu? Hapa nataka kukwambia uchambue kile kitakacho kufaa, usivyotaka tutoe nje.” “Mbona nakushukuru. Basi naomba tumshukuru Mungu kwa mwanzo wetu mzuri.” Fifi akabaki amekodoa macho.

“Wewe unamwamini Mungu!?” “Nisingefika hapa bila Mungu. Alikonitoa huyu Mungu! Huwezi amini.” “Umenisimulia. Sasa lakini alikuwa wapi wakati unabakwa?” Fifi akauliza. “Pale pale alipokuwepo wakati namdanganya Geb. Alikuwa pale pale wakati akinisisitiza nimwambie Geb ukweli wote nikashindwa. Alikuwa pale pale alipo wakati napanda gari na kwenda kwa Malii. Nikamvulia nguo huku nikijua wazi nazini. Hajawahi kuhama. Mungu wangu yupo pale pale dada yangu. Yote niliyoyapata, yananistahili kabisa. Sina hata wakumlaumu dada Fifi. Hakika sina. Hujui ni kwa kiasi gani nilisukumwa kumwambia Geb ukweli wote, lakini nikapinga. Nimetubu. Naamini nitasamehewa tu.” Fifi alilia.

“Ninaadhibu watoto wangu kwa kushindwa kumtii Mungu. Dada Fifi, mimi namjua Mungu kwa kumuona akinitendea mambo ya ajabu. Namfahamu Mungu si kwa kumsoma tu. Amejidhihirisha kwangu mara kadhaa. Ameniokoa mara kadhaa kwenye shimo la mauti. Leo nipo hapa kwako, si kwa bahati mbaya, ni kwakuwa nimekaidi, dada. Wanangu wanalia kwa sababu mimi nilikaidi. Nimemuumiza mwanaume mwenye mapenzi ya kweli, kwa kuwa mimi nilikaidi dada. Kwa hiyo, usiwe na wasiwasi juu ya uwepo wa Mungu wangu. Yupo.” Nanaa aliongea taratibu lakini kwa uchungu sana.

“Hata kukutana na wewe, si kwa bahati mbaya dada. Najua alikuandaa makusudi kwa ajili yangu. Unaweza usielewe, lakini nina uhakika nipo sehemu sahihi. Acha nimshukuru kwa kuwa najua hajaniacha.” Nanaa akafuta machozi.

Ilikuwa bado ni asubuhi tu, wakati wanashikana mikono na kuomba pamoja. Fifi alimsikia Nanaa akiomba sala fupi tu. Lakini alishukuru kwa machozi, huku akiombea watoto wake na Geb. “Warehemu watoto wangu ewe Mungu wangu. Nawaombea faraja, wao na baba yao. Sijui utafanyaje, lakini ile faraja inayopita fahamu zetu, ndio ikawe juu yao. Watunze, mfariji Geb wangu. Mpe hata yale ambayo hajui kama anayahitaji.” Nanaa akaendelea kidogo. Akamuombea na Fifi, wakamaliza.  

 “Mmmh! Mpaka umenisisimua!” Nanaa akacheka. “Sasa mwenzio nataka kuandika.” “Unaandika nini tena?” Fifi akauliza na kujirusha kitandani. Palikuwa hata hapajatandikwa. “Naanza kuandika barua za kuomba kazi. Lakini dada, nina wazo.” “Lete mawazo yako. Nimeshaanza kukuogopa Nanaa.” “Acha hizo bwana!” Wakataniana kidogo, Nanaa akaendelea.

“Mwenzio ni mjuzi sana wakupika.” “Unataka tufungue hoteli?” Fifi akamdaka. Nanaa akacheka sana. “Kwanza nimefurahi ulivyojiweka na wewe. Naona akili imetoka likizo.” “Nilijichetua tu, mdogo wangu. Lakini mimi muhangaikaji sana Nanaa. Usinione hivi.” “Basi kama ndio hivyo mbona tushafanikiwa? Tutafute mahali tufungue sehemu yetu. Jumatatu mpaka ijumaa. Siku za jumamosi na jumapili, tuwe tunatafuta tenda, tunafanya catering.” Fifi akakaa.

“Wewe mtoto kabila gani?” “Bwana dada Fifi acha utani! Nataka kutengeneza pesa ili niweze kulipa kodi. Sitaki niwe nakukimbia.” Wakacheka. “Wazo zuri sana. Lakini shida ipo kwenye mambo mawili. Mimi si mpishi mzuri. Zaidi yakusonga ugali na kupika wali, hamna ninalojua.” Nanaa akacheka.

“Sikutanii Nanaa! Mume wangu alikuwa anapika vizuri kunishinda mimi. Mwenzio nilitoka kwenye familia yakusoma tu. Kazi za ndani tulikuwa hatufanyi.” “Wewe usiwe na wasi wasi utajifunza tu. Ni rahisi sana. Haya nipe tatizo jingine.” “Pesa. Mwenzio si nimekwambia sina hela?” Fifi akajitetea.

“Kwanza nakulipa kodi yako ya miezi 6. Hata leo ukitaka twende kwenye ATM, au nakurushia. Halafu kabla hatujaweka vikwazo vingiii, tutafute eneo. Tujue garama zote. Au tunaweza kuanza kwa kufanya catering. Tukaanza kupika humu humu ndani, tunapeleka kwenye shuguli za watu. Hasa kitchen paty ndio wengi wanapenda vitafunwa. Tuandike.” Nanaa akavuta karatasi.

“Sambusa, vitumbua, chapati, bajia, kalumati, kachori na maandazi.” “Vyote hivyo unaweza kuvipika!?” “Ndiyo. Na wewe nitakufundisha. Halafu wateja wetu wa kwanza ni wale wale wateja wako uliokuwa ukiwasambazia vifaranga wewe na mumeo. Leo utawapigia simu wote, utawaambia umebadili biashara. Sasa hivi unafanya Catering. Usisahau hao ndugu zako wasomi.” “Sasa wakisema wanataka tuwapelekee sample?” “Mbona unakuwa na vipingamizi vingi hivyo?” “Nauliza         tu mdogo wangu! Tusije tukatangaza, halafu tukaishia kuonekana wote machizi.” “Basi anza kutuma ujumbe sasa hivi tukusanye oda. Halafu tupike, waambie kesho tutawapelekea maofisini wakaonje.” Fifi akabaki amemtolea macho Nanaa.

“Mbona unaniogopesha Nanaa wewe! Umechangamka!” Nanaa akacheka. “Sasa ujumbe usemeje?” Nanaa akavuta karatasi, akaandika. ‘Tunatoa huduma ya kusambaza bites. {Sambusa, bajia, maandazi, chapati, kachori, kalumati na egg chop}. Kwa ajili ya sherehe kubwa na ndogo. Tutatoa chai na kahawa pia. Tunaweza kukuletea ofisini, kwa mlo wa kila siku au hata kwenye vikao na majumbani. Tutakuletea popote ulipo kwa oda kuanzia elfu 50 na kuendelea.”

          Akamsogezea ile karatasi Fifi. Hebu soma. Halafu uongeze na wewe. Fifi akasoma nakumtizama Nanaa. “Una friji?” Nanaa akamuuliza. “Ndiyo. Lakini chafu.” Fifi akajibu. “Haya twende tukaioshe, wakati unapigia watu simu na kusambaza ujumbe. Ukimaliza, tunaenda kununua vitu.” Fifi na Nanaa, wakachangamka kweli kweli. Matumaini yakawajia. Mpaka inafika jioni, walikuwa na tenda zakupeleka kesho yake maofisini.

“Nanaa wewe!” “Lazima kuchangamka dada. Mimi nimeona jinsi watu wazima wanavyomuheshimu yule baba watoto wangu. Kijana mdogo lakini akiongea watu wanamsikiliza. Akikaa mahali, utajua pesa ipo. Kwa kuwaza tu. Akanifundisha kuchukua hatua pia. Anasema yeye kila wazo analifanyia kazi. Sikudanganyi dada Fifi, yule kaka anapesa. Kuna mahali nilienda naye, wafanyakazi wa benki, wanao zijua akaunti zake, walisimama wanaume wale wakawa kama wajinga mbele yake. Na usifikiri anafanya mambo ya ajabu! Ni kuwa makini tu. Sasa tuanze kazi dada yangu. Heshima haiombwi mjini.”  Wakacheka. “Mbona nakushukuru mdogo wangu! Mwenzio watu walikuwa wananikimbia.” Usiku huo huo wakaanza kazi wakiwa wameshanunua kila kitu, mpaka lunch boxes zakufungia vitafunio hiyo kesho yake.

Huku Nyuma Nyumbani Kwa Geb.

Jeri alipita tena kuleta watoto. Lakini mlinzi akamwambia akiwa pale pale getini. Kuwa Nanaa ameondoka rasmi. Na ameacha barua. Akakabidhiwa hiyo barua aliyokuwa amemwandikia Geb, na kugeuza baada ya kuzungumza kidogo, wakiteta. Wala Geb hakuhamia mbali. Walirudi kuishi pale walipokuwa wakiishi zamani na mama yake.

Muda huo huo wakamuona anarudisha tena watoto. Bibi yao akatoka. “Hajarudi tu!?” Akauliza baada yakuwafikia kwenye gari. “Wamesema ameondoka moja kwa moja. Amewaaga kuwa hatakaa arudi tena pale. Kumbe ule mwezi aliopotea pale, hakuwa kwa wanaume bibi. Alikuwa hospitalini amelazwa.” Mama G akatulia kidogo kama anayefikiria. “Ameacha na barua hii hapa, amesema apewe baba yao hawa.” “Nipe mimi hiyo barua. Halafu niachie mimi nitazungumza kila kitu na baba yao. Wewe usimwambie chochote. Nimemtafutia mwanangu binti mzuri. Ametulia na atamfaa tu. Mwache aende zake, kwanza Geb hamtaki tena.” “Sawa.” Jeri akamkabidhi hiyo barua, akasaidia kushusha watoto, akaondoka zake.

Geb alirudi kutoka kazini. Akamkuta Liv amekaa kwenye kochi ametulia kama anaangalia tv. Akamgeukia baba yake, akarudisha macho kwenye tv. Wala hakuchangamka. “Walipelekwa kwa mama yao?” “Na leo pia hawakumkuta.” Mama G akajibu kwa ufupi tu akificha ukweli wote. Geb akanyamaza. Akaenda kukaa pembeni ya Liv. Akaendelea kuangalia cartoon na mtoto wake.

~~~~~~~~~~~~~

Mrembo aliyekuwa ameletwa hapo na mama G, kama msaidizi wa watoto, Sara, akatoka na glasi ya juisi. “Pole na kazi.” Akatoa salamu kwa Geb. “Asante.” Geb akajibu huku macho yako kwenye luninga. Akavuta stuli, na kumwekea ile juisi. “Karibu.” “Huyu anakula nini? Mbona kama amekaa tu hapa?” Geba akauliza akimaanisha  Liv. “Anavyoringa huyo mwanao! Haambiliki. Anataka tufanye vile anavyotaka yeye.” Moyo ulimpasuka Geb, akamtizama Sara. Ni Liv wake!

Mama G aliposikia lile jibu, akatoka kwa haraka kule jikoni. “Ameshakunywa maziwa, natengeneza chakula chao cha usiku.” Akamuwahi Geb kabla yule msichana hajaendelea. “Wala hakuyanywa! Karudisha chupa jikoni.” Sara akamalizia nakurudi jikoni. “Atakula chakula cha usiku. Atakuwa sawa tu.” Mama G akajaribu kupoozesha.

“Liv!” Geb akamuita. “Unataka kula nini?” Akamwangalia baba yake, nakurudisha macho kwenye luninga. “Unataka nikupakate?” Geb akaendelea kumuuliza taratibu. Liv akasimama, nakwenda kumkalia baba yake. Akalala muda ule ule akiwa ameshikilia mtandio aliozoea kujifunika ili anyonye kwa mama yake. 

Geb akamwangalia. Akamuweka sawa, akavuta rimoti akabadili channel ya tv. Kutoka pale walipokuwa wamemuwekea Liv, akahamisha kwenye mpira. Wakabaki kimya pale kwenye kochi. Mama yake akatoka. “Kunywa hiyo juisi.” “Huyu amelala. Alikula kweli mchana?” Geb akauliza. “Amekula vizuri tu.” Sara naye akatoka jikoni, akajibu yeye.

“Naomba nikamlaze chumbani.” “Mwache kidogo.” Geb akajibu huku akimwangalia mtoto wake kama anayetaka muda naye zaidi. “Ameking’ang’ania hicho kimtandio, kama nini sijui! Kila anapokwenda anacho. Na ukitaka alie, mpokonye.” Sara akaongea kama utani huku akikaa kochi la pembeni. “Angalia nisije nikaunguza.” Mama G alimkatisha nakumtaka arudi jikoni. Alishaona anakoelekea ni kumtibua Geb “Na unavyopika vyakula vingi, kama hotelini!” Sara akasimama kurudi jikoni. Hakuna aliyejibu. 

~~~~~~~~~~~~~

Kalikuwa kabinti kazuri sana kwa muonekano. Ndio alikuwa amemaliza chuo kikuu cha Mzumbe, mjini Morogoro. Aliitwa Sara. Mzuri. Msafi wa mwili wake. Alikuwa mdogo kidogo kwa Nanaa. Bado alionekana ni binti mchanga. Mwili haujapitishwa kwenye uzazi wala majukumu mazito. Mama G alifahamiana na shangazi yake. Alipomweleza balaa la Nanaa, ndipo shangazi mtu akamuelekeza kwa huyo mtoto wa kaka yake.

Akamwambia ni binti aliyetulia na yupo tu nyumbani anasubiri matokeo yake. Anaishi na wazazi wanaoeleweka na wana uwezo mzuri tu. Kwa hiyo huo ndio muda wa kuwaunganisha vijana wao. Aende pale kama kuwalea watoto, huku wakisomana tabia na Geb. Ndipo mama G akamtuma aletwe.

Ilishapita week moja tokea aletwe hapo wakati Nanaa amepotea, hajulikani alipo. Kumbe yupo hospitalini. Geb alimkuta humo ndani, hakuuliza. Mama G akamtambulisha kwa Geb nakumwambia yupo pale kumsaidia swala la watoto. Naye Sara akasema anapenda sana watoto. Huwa ni kitu anafanya kwa furaha zote. Geb akasikiliza, nakunyamaza tu. Sara alianza kwa mbwembwe zote, lakini akakutana na Liv. Kichwa kama ya baba yake! Hapo ndipo Sara alipoanza kuchoka.

~~~~~~~~~~~~~

Mama G akamfuata jikoni. Akamsaidia kutayarisha vyakula, akavitoa pale. Wakati anatoka na vyakula, Geb naye akawa anasimama na mtoto wake. “Mbona unaondoka na chakula tayari?” Sara akamuuliza Geb. “Au utarudi? Maana kishaiva.” Kimya. “Ungekula kwanza ndio ukalale. Usilale bila kula.” Geb akamtizama bila yakumjibu kitu, akapitiliza chumbani kwa mama yake. Alimbadilisha nguo mtoto wake, akamlaza kitandani. Mama yake akamfuata. “Naona huyu hataamka tena mpaka kesho.” Geb akaongea huku akimfunika vizuri binti yake. “Chakula kipo tayari.” Mama yake akaongeza.

“Nilikuwa na kikao na mtu sehemu wanayouza chakula. Nikala. Kwa hiyo nipo sawa tu.” Geb akajibu na kuuliza. “Magesa ataamka tena?” “Amekula ndio akalala. Hapo tena mpaka usiku, ndio ataamka tena, anywe maziwa, arudi kulala mpaka asubuhi.” Mama G akajibu. “Vipi maziwa hayo uliyombadilishia? Anayapenda?” Geb akauliza. “Sana tu. Yaani huyo mdogo anakula bila shida. Akianza kuvuta chupa yake, kama mchwa! Lakini si huyo dada mtu. Anafanya anachotaka yeye, na anakula akitaka. Kama leo nzima alikuwa kisirani! Bibi yake akasema labda apelekwe kwa mama yake. Ndio kumkosa mama yao, akarudi nakujiweka kwenye kochi mpaka kapitiwa na usingizi. Lakini watoto wanabadilika. Nikumpa tu muda. Bado mdogo huyo. Atasahau tu mateso ya mama yake.” Sara aliingia na kujiweka kitandani kwa mama G huku akiongea. Wote wakanyamaza.

“Sasa mimi naenda kula chakula changu chumbani. Kuna tamthilia yangu huwa naifuatilia. Ndio mida yake hii. Nitakula huko huko na kulala. Nitaosha vyombo kesho. Leo siwezi tena. Kwanza nimechoka.” Sara akasimama nakutoka pale chumbani. “Atakuwa kweli amechoka. Anajituma kweli!” Mama G aliongea, akionekana hata hoja yake haina nguvu. Geb hakujibu kitu.

Maisha Ya Nanaa.

Biashara ikamchanganyia Nanaa. Akawa busy, hana hata muda wakupumzika. Akimaliza kupika usiku na kutayarisha vitu vya kumalizia kupika asubuhi yake, anakuwa amechoka sana. Hoi kitandani tayari kwa asubuhi kumalizia kupika ili wakasambaze maofisini kabla muda wa kunywa chai kupita. Pesa ndogo zikawa haziwapigi tena chenga, yeye na Fifi kitu kilichomuongezea morali Fifi, kwani alifanikiwa kuacha kukopa hovyo hovyo. Hakuna aliyekuwa akimsikia kwa shida ila kuwauzia vitafunwa.

Urafiki kati yake na Nanaa ukanoga. Hakuacha kuomba na Nanaa. Mwezi wa pili akiwa anaishi na Nanaa, akaamua kuhama nyumba kama alivyoshauriwa na Nanaa. Akaikodisha nyumba kubwa, akahamia nyumba ya uwani pembeni ya Nanaa. Huko ndiko walipokuwa wakikesha kwa kufunga sambusa na kuongea.

Hakuna Msiba Usiokuwa Na Mwenzie.

“Nikwambie kitu d ada Fifi?” “Niambie tu.” “Lakini usianze kushituka kama kawaida yako.” Fifi akacheka. “Sema bwana. Tumepata dili nyingine nini? Maana mtoto wewe kwa pesa!” Nanaa akacheka kinyonge. “Unajua huu ni mwezi wa tatu tokea nikwambie nimebakwa?” Fifi akatoa macho. “Usiniambie una mimba!!” “Acha tu dada yangu. Sijui nitafanyaje. Nilijihisi tokea mwezi wa pili. Lakini nikajipa muda. Unakumbuka leo wakati tunatoka posta kupeleka mzigo?” “Pale uliponiambia tusimame duka la madawa ndio ulikuwa unanunua kipimo!?” Nanaa akacheka.

“Dada Fifi unaakili ya haraka yakufikiria! Mpaka unaniogopesha.” “Mtoto mbaya wewe! Sasa ulikuwa ukinificha nini? Ndio maana nimekuona tokea asubuhi huna raha!” “Naogopa dada.” “Wala usiogope mdogo wangu. Atakua tu.” “Hilo sina wasiwasi nalo. Ila sikutaka mtoto wakubakwa dada. Au niseme sikutaka kuzaa na yule mwanaume. Halafu mimba yangu ya mwisho ilikuja na presha mbaya sana. Ilinibidi kulazwa mpaka nilipojifungua. Sasa nafikiria, sijui itakuaje?” “Hapo nakuelewa. Lakini Nanaa, huko usiwaze. Wewe si unamwamini Mungu? Basi amini na hilo liko ndani ya mapenzi yake. Atakupigania tu.”

“Angalau umenituliza. Lakini nimekuwa nikisita kweli kwenda kuangalia afya yangu. Malii alikuwa mchafu sana. Hakuna mwanamke anampita.” “Wewe usijipe presha buree. Ukaanza kuugua. Tulia. Ukianza kliniki, utajua yote.Watakupima kila kitu. Hatua moja umeshaifanya. Ushajua mtoto yupo. Yaliyobaki mwachie Mungu.” Nanaa akanyamaza. “Tena unaweza kuta huyo mtoto ndio akawa faraja yako.” “Mmmh dada!” “Kweli tena. Si unasema umepokonywa watoto wewe? Basi huyo atakufaa.” Nanaa akaamua anyamaze.

~~~~~~~~~~~~~

Hakuna siku iliyopita asiache kuwakumbuka wanae na kuwaombea. Tayari hofu ya kuzaa na Malii ikawa imemkamata kupita kiasi. Hakuwa akiweza kulala vizuri. Lakini hakutaka kumuonyesha Fifi. Ila alimuona wazi amebadilika. Muda mwingi alimkuta akifikiria. Vicheko vilipungua kabisa kati yao. Nanaa akawa mtulivu wakupita kawaida yake. Akili ilikuwa imemvurugika asijue tena chakufanya. Mipango yote aliyokuwa amejiwekea, akaanza kuona hamna tena tumaini. Anazaa na Malii! Hicho ndicho kilikuwa kikimuumiza. Heri angekuwa amebeba mtoto wa Geb. Hakukumbuka hata kuomba kazi kwenye ofisi yeyote ile. Akabaki akipika vitafunywa. Nakusambaza maofisini huku akiwa hajui hatima yake.

~~~~~~~~~~~~~

Mambo yanazidi kumuharibikia Nanaa. Mama G amembadilikia kabisa na ameshamtafutia mwanae binti mchangaa! Alishajisifia wanae hufanya kile anachotaka yeye.

Sasa Je, Safari hii ndoa kwa Geb itafanikiwa baada ya kushindwa kwa Nanaa.

Nanaa yu mjamzito tena. Mori wote wa maendeleo umemuisha.

Nini kitaendelea?

 

 


CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment