Geb akaingia kwa tahadhari kama
asimuamshe. Nanaa akamwangalia. “Umeambiwa ulale Nanaa. Hata dawa hazifanyi
kazi!” Nanaa akacheka kidogo. “Labda ukilala pembeni yangu halafu
ukanikumbatia, ndipo nitalala.” “Wewe unataka nifukuzwe hapa.” “Hawawezi bwana.
Shida yao wanataka nilale. Ukinishika shika, ndio nitalala vizuri. Nina hamu na
wewe Geb. Hatujalala wote muda mrefu!” “Hata mimi. Basi ngoja nikawaweke sawa
hao manesi. Nakuja.” Geb akatoka. Akazungumza na manesi. Kwa kuwa kilikuwa
chumba chake tu, wakamruhusu.
“Wamesema
hamna shida.” Geb akarudisha jibu. “Muone alivyofurahi!” “Hata mimi nataka
kukushika. Unafikiri nilikuwa sina hamu na wewe?” Nanaa akacheka. “Ila ujue
ndio nimejifungua leo.” “Nakumbuka Nanaa! Siwezi kuvuka mipaka bwana. Nashika
tu.” Nanaa akacheka sana. Geb akapanda kitandani upande usiokuwa na dripu,
mabusu yakaanza. Baada ya muda, wakaona walale tu, hali ilishakuwa mbaya.
~~~~~~~~~~~~~
Baada
ya muda mlango ukafunguliwa. Mama G alikuwa amerudi na Grace wakiwa na vyakula.
“Sasa hapo si alitakiwa kulala mtoto!?” Nanaa akaanza kucheka. “Mwache mama.
Amechoka.” “Basi kazi unayo. Liv naye akija anataka alale hapohapo! Baba yake
naye alale hapohapo! Magesa naye alale…” Mama G kama akakumbuka kitu. “Kwanza
mtoto mwenyewe yuko wapi?” “Wamemchukua. Maziwa hayatoki mama. Alikuwa
ananyonya, lakini hashibi. Ndio daktari amesema aanzishiwe ya kopo. Halafu
wamesema atakuwa analala huko huko. Watakuwa wakimleta kidogo tu. Presha bado
ipo juu. Wanataka nilale.” “Pole Nanaa. Ni kweli utahitaji kula vizuri na
kulala.” Wakakaa.
“Lazima
ule sana. Utakuwa ukikamua kama kwa Liv. Halafu nitakuwa nikiwapelekea hao
manesi, wawe wanampa ya kwako wala si ya kopo. Najua hupendi.” “Ndio maana
nakupenda mama yangu.” “Ndio ukazane kula sasa.” “Kwani hilo unawasiwasi nalo
mama yangu?” Mpaka Grace akacheka. “Nanaa!” Grace akatingisha kichwa. “Hapa
tuzungumze, huku nakula.” Nanaa akatoa wazo. Mama G akacheka.
“Hapana
Nanaa. Unatakiwa kula na kurudi kulala. Sio uzungumze.” Geb aliongeza akiwa
amelala pale pale kitandani kama mgonjwa. “Kumbe upo macho! Haya aamka na wewe
ule.” Geb akakaa. “Nitaomba msaada kwa mtoto mama. Uwe unakwenda kumwangalia.”
“Wala usijali. Mbona hapa nishaweka mipango yote. Liv anahamia kwa Grace kwa
muda. Nikitoka tu hapa naenda kumwangalia walipomuweka mume wangu.” Mama G
akacheka kidogo. “Alivyofurahia!” Grace akamtizama mama yake.
“Kumbe!
Mtoto yupo kama Magesa, mme wangu! Kasoro rangi tu.” “Naomba kusikia hiyo
mipango mpaka mwisho mama.” Geb alimkatiza. “Haya baba. Mwenzio ninafuraha ya
ajabu. Kwanza sikutegemea. Nilivyo..” “Mama wewe! Si umeambiwa useme mipango
kwanza? Acha kuzungumzia furaha zako kwanza, bwana. Mweleze Geb hiyo mipango.”
Grace alimkatiza. Nanaa akawa anacheka tu.
“Haya.
Nitaenda kuchukua ratiba nzima ya huyo mtoto. Nijue saa ngapi anaogeshwa. Muda
gani anakula na muda gani anatakiwa aje huku. Hata kama ni asubuhi, nitakuwa
nakuja kumuogesha mwenyewe na kumpa maziwa. Nikiona yupo sawa, ndio namuacha
mpaka jioni. Lakini hapo nitahakikisha namuacha na maziwa yakutosha. Kwanza
natamani kama wanipe niende naye kabisa.” “Mama!” Nanaa akashangaa. “Ndio
vizuri nilee mwenyewe. Kwanza ndio nitakuwa na amani na usafi wake, maziwa
anayopewa, na nitaweza kuwa na wote wawili pamoja na dada yake. Naweza
kukuletea asubuhi na jioni.” Wazo likasikika zuri.
Geb
na Nanaa wakaanza kushawishika. “Kwanza huwezi jua. Wanaweza kuanza kuchanganya
vitu vyake na watoto wengine waliozaliwa na magonjwa hatarishi. Halafu
akaambukiz..” “Bwana mama acha kutuogopesha.” Geb alimkatisha. “Sasa ulifikiri
wanahuyo mtoto mmoja tu huko kwenye wodi za watoto!? Siku hizi hakuna
kunyanyapaa. Watoto wote wanachanganywa pamoja.” “Mama wewe? Hapa ni
hospitalini wapo makini bwana. Acha kuwatia hofu Geb na Nanaa.” “Na manesi
wenyewe wanakuwa wanachoka. Swala la kupitiwa ni ubinadamu kabisa. Huwezi
kuwalaumu chochote kikitokea.” Mama G akasisitiza.
“Kwa
hiyo umesema unaweza kukaa naye nyumbani?” Geb akauliza. Mama G akafurahia
moyoni. Akajua mtego wake umenasa. Aliwaogopesha kwa makusudi. “Mkitaka
wenyewe. Sitaki kuingilia.” Akajibu mama G, kiuungwana. “Eti Nanaa?” Geb
akamgeukia Nanaa. “Kwanza hapa nishaanza kuwaza kama bado yupo salama! Unaweza
kuta watoto wako wengi, akalia mwanangu wakampuuza. Naomba ukazungumze na
daktari wamruhusu tu aondoke na mama. Si wamempima wanasema ni mzima kabisa?”
“Ndivyo walivyoniambia.” Geb akajibu. “Basi naona aende tu na mama.” Bila
kuongeza, Geb akasimama na kutoka nje.
Wakamuona
Nanaa analia. “Umeona umemuogopesha Nanaa? Bwana usilie Nanaa wifi yangu.
Mwanao atakuwa mzima.” “Nalia kwa furaha
mwenzio. Ujue mimi nilipozaliwa tu, mama akafariki. Hakuna aliyetaka kunichukua.
Sasa kuona hivi mnawapokea wanangu, nimefurahi sana. Asante mama. Kumbe hata
ningekufa wanangu wangelelewa vizuri tu!”
“Kwanza wala usilie. Kufa haufi. Maneno yote yale yalinitoka ili kumuogopesha
Geb, chaubishi. Nilijua bila kumtia hofu ya maradhi kwa mwanae, wala
asingekubali niondoke na huyo mtoto wakati mimi namtaka sana huyo mtoto.” Wote
wakacheka.
“Hivi
mama wewe ukoje? Kwa nini kutumia lugha ngumu hivyo? Si ungesema tu kama
unataka kuondoka na mtoto kuliko kutia watu hofu?” Grace alilalamika. “Kwani
wewe humjui Geb? Hapa nilikuwa nimepanga kumtia hofu zaidi mpaka akubali. Ni
hivyo tu kakubali haraka. Nilimwandalia maneno ya hofu zaidi ya haya.” Nanaa
alizidi kucheka. “Mbishi sana Geb, kama baba yake! Akiamua jambo ndio basi. Habadiliki
kirahisi. Sasa mimi huwa namjua pakumpatia.” Mama G akawa amefurahia kweli kuwa
mtego wake umenasa.
“Sasa
utawaweza wote wawili!?” “Wala usitie hofu. Ninavyomtaka huyo Magesa. Acha
nikahangaike nao tu. Asubuhi na
jioni utakuwa na wanao hapa. Mchana nakuacha upumzike.” “Nakushukuru mama
yangu. Nahisi hata presha itashuka.” Wakaanza stori. Mama G akiwa amechangamka
kweli. Furaha ilionyesha usoni. Kila mtu akajua.
Geb
akarudi. Mama yake akanyamaza. “Unacheka kwa sauti sana mama jamani! Nanaa
anatakiwa kupumzika.” “Heee! Hata kucheka haturuhusiwi?” “Si ndio maana
ameachwa hapa? Nanaa akiendelea hivyo tutachelewa kutoka hapa. Na mimi nataka
arudi nyumbani kwa watoto.” “Kwani wamenikubalia kuondoka na Magesa?” Mama G
akahoji. “Wamesema daktari wa watoto ametoka kumuona sasa hivi. Anaonekana kila
kitu kipo sawa. Hata wao wameona ni wazo zuri kama kuna mtu wa kumwangalia kwa
karibu, achukuliwe tu.” Mama G akajisahau tena, akaanza kushangilia.
“Punguza
sauti mama bwana!” Geb akalalamika. “Halafu uwe unamleta kama ulivyosema. Usije
ukajisahau naye.” Geb alimtahadharisha. “Sasa maziwa nitapataje na wewe!? Mbona
kama hufikirii.” Mama yake akambadilikia. “Hapa nitaletwa na mawili. Kuleta
chakula kwa mama yake, na kuchukua maziwa. Nyinyi nikamulieni hayo maziwa.
Myahifadhi vizuri, nikiwa nakuja, nakuja kuyafuata.” “Mama alivyofurahi!
Mipango mingiii. Kazi tena basi?” Grace akauliza. “Nimepata kijana mwaminifu
sana. Atanishikia kwa muda. Acha nimlee mume wangu.” “Na kwa Liv ulisema hivyo
hivyo.” “Sasa yule si ndio mwenyewe? Alelewe na nani kama sio mimi?” Geb
akabaki akimwangalia na kutingisha kichwa.
Mama
G alijawa mipango mingiii, wote wakabaki wakimsikiliza. Aliacha vyakula hapo
hospitalini. Cha Nanaa, Geb na wauguzi wote waliomsaidia Nanaa kujifungua.
Akapewa mtoto, wakaondoka na kumuacha Nanaa na Geb. Wakala, na kurudi kulala.
~~~~~~~~~~~~~
Maisha
yakaanza. Watoto wanaletwa asubuhi na jioni. Nanaa akawa akiwanyonyesha wote
wawili huku akiwa na uhakika wa maziwa mengine ya Magesa kwenye chupa. Mida
ambayo anajua Nanaa analala mchana muda mrefu, Geb alitoka kwenda kazini.
Wakati mwingine mpaka jioni. Anarudi hospitalini kulala na Nanaa, akiwa
ameshapitia nyumbani. Anaoga na kubadili nguo. Wakati mwingine alichukua
nyumbani nguo za kesho yake kazini.
Magesa
na Liv walikuwa wakiletwa hospitalini wakiwa wasafi na wanavutia. Ungependa
kuwaangalia. Mama G alishika usukani wa hao watoto, hata Nanaa hakuwa na
wasiwasi. Kwanza aliona wanalelewa vizuri na mtu mwenye uzoefu zaidi yake. Na
ni bibi yao. Aliyekuwa akiwapenda sana.
Baada
ya siku tatu tu, Geb akamwamisha Jeri, dereva wake wa kazini wa muda mrefu
sana, nyumbani. Jeri alikuwa mwaminifu na aliheshimiana na Geb. Yeye ndiye
aliyemuona anafaa kumuweka kuwa dereva wa watoto wake tu. Alimwambia kila siku
asubuhi awe anaripoti nyumbani, kwa mama G. Atamwambia kitu gani chakufanya
siku nzima. Kama ni kumtuma mahali au kazi za pale pale ndani. Basi afanye kwa
wakati huo yeye na Nanaa wakiwa hospitalini. Akakabidhiwa ile gari ya Geb ya
kifahari, yenye viti 8, waliyosafiri nayo kwenda Marangu kwenye harusi ya
Malii. Kwa hiyo Jeri ndio akawa dereva wa nyumbani. Mama G akawa akikaa nyuma
na watoto, Jeri anawapeleka atakapo na hao watoto.
~~~~~~~~~~~~~
Nanaa
akawa anapata muda mwingi wamapumziko. Hakuwa na majukumu mengi isipokuwa yeye
na akiletewa watoto kwa muda mfupi. Kilichomshangaza na kumchanganya Nanaa
zaidi ni pale Geb aliponyamazia na kutozungumzia kabisa juu ya yale aliyoongea
Manka, mke wa Malii. Hakujua kinachoendelea kichwani kwa Geb. Hiyo ilizidi
kumsumbua Nanaa na kumuongezea wasiwasi kila akikumbuka mkasa wake na Malii.
Kila wakati maneno ya mkewe Malii yalikuwa yakijirudia na kujisikia hofu.
Matibabu
yakaendelea. Baada ya siku chache, presha ikaanza kushuka. Alikaa hospitalini
siku 11. Ndipo daktari akawaruhusu warudi nyumbani. Nanaa na Geb walifurahia
sana. “Lakini bado unahitaji mapumziko Nanaa. Sijajua ni nini kinachofanya
presha yako isirudi kuwa yakawaida kabisa. Vipimo vyote vinaonyesha huna tatizo
lakukufanya usipone kabisa. Kwanza wewe bado mdogo. Hutakiwi kuwa na maradhi ya
pressure.” Daktari huyo wa mambo ya moyo alikuwa akizungumza na Nanaa alipokuwa
akipita kumwangalia.
“Labda
kwa kuwa nipo mbali na wanangu.” Nanaa akaongeza huku akificha ukweli wa kile
kinachoendelea moyoni mwake. Hakuna aliyejua hofu iliyomjaa Nanaa. Malii aliapa
ni lazima atampata. Hilo hakulisikia kwa mkewe Malii tu, hata Malii
mwenyewe alishamwapia. Na wala hazikuwa siku nyingi. Lakini pia hakumwambia
Geb. Kitendo cha kumsikia mkewe akirudia mbele za watu, akajua Malii hatanii. “Asije kuja kumwambia Geb ukweli wote!”
Hiyo ndio iliyokuwa hofu iliyokuwa ikimuweka macho Nanaa.
“Tuombe
Mungu hiyo ndio iwe sababu. Sio vizuri kuanza kusumbuliwa na pressure kwa umri
wako. Hata hivyo kesho nitakuruhusu, pengine itasaidia. Lakini nilazima
upunguze mawazo na ukapumzike huko nyumbani.” “Nitafanya hivyo.” Nanaa akajibu.
Nanaa Atolewa Hospitalini.
Nanaa aliamka akiwa na nguvu na amechangamka kweli kweli kwa furaha yakurudi nyumbani kwa watoto wake. Oliva na Magesa. Tena Magesa aliyekuwa amebebewa utabiri. Nanaa hajawahi pata shida ya kushika mimba. Anazaa kutokana na anavyotaka Geb! Alitaka wa kike, Nanaa akamtolea binti wa nguvu. Haya Mzee Magesa alitabiri juu ya Magesa, bila ya kuhangaika, Nanaa akatoa Magesa wa nguvu! Mungu ampe nini Nanaa? Nani mwanamke kama Nanaa? Nanaa anaheshimika kwenye ukoo huo. Nanaa muendelezo ukoo! Umesikia sifa za Nanaa hata kutoka kwa mke wa Malii, Manka. Unaambiwa, ‘Nanaa maji marefu’. Marafiki walioliana amini, leo wanashikana mashati kwa ajili ya Nanaa yule aliyekuwa akivaa jalalani! Mungu amempandisha juu, na amemjaza dhahabu! Gari ya kifahari inamngojea hapo nje ya majengo hayo ya hospitalini, dereva ni Geb, ili amrudishe kwenye jumba la thamani! Utamwambia nini Nanaa?
Akaingia
bafuni kuoga. “Mbona sikuoni kama unavaa kitu zaidi ya chupi tu?” Geb alimfuata
bafuni. “Nilishamaliza mwenzio. Hapa nipo safi.” Nanaa akajibu huku akitaka
kuvaa. “Mbona sasa hukuniambia!?” “Wewe Geb! Tupo hospitalini.” “Nimebanwa
Nanaa. Nisaidie mpenzi wangu. Kidogo tu.” “Hapa hapa kwenye bafu la
hospitalini!” “Kidogo tu, tutamalizia nyumbani.” Geb akaendelea kubembeleza.
Nanaa akacheka.
Geb akajua ndio amekubaliwa. Akaanza kumfaidi Nanaa hapo hapo bafuni. Hata Nanaa alikuwa na hamu na Geb. Alikuwa mtundu na mtulivu sana kwenye mapenzi. Popote na wakati wowote alipomshika Nanaa, alifurahia penzi lake. Mpaka akakamilisha raundi ya kwanza, ndipo akamwachia. “Daah! Asante Nanaa wangu. Hali ilikuwa mbaya!” “Hata mimi nilikuwa na hamu na wewe. Asante kunivumilia Geb. Tokea wakati ule wameniweka bed rest mpaka leo! Unastahili pongezi. Tukifika tu nyumbani, tupandishe juu. Kama lisaa tu, ukate kiu yote ndio tukakae na watoto.” “Lisaa tu!? Nitamwambia mama tunahitaji muda Nanaa. Ni siku nyingi sijalala na wewe mpenzi wangu. Bado mwenzio nakuhitaji. Akili yangu haijatulia.” “Basi nitaenda kukutuliza. Usijali.” Geb akamkumbatia na kumbusu kwa muda nakumuachia.
“Nakupenda
Nanaa. Nakuthamini kuliko nafsi yangu. Sijawahi kupenda hivi. Amini nakupenda.
Wewe ni wangu. Si kile kitanda wala nyumba inayoweza kukalika kwa furaha, kama
wewe haupo. Nikilala pembeni yako ndio naweza kulala vizuri.” Nanaa akacheka.
“Asante.” Nanaa akashukuru kwa upole huku akimfikiria Geb. Alitamani kumwambia
kila kitu asimfiche chochote kile. Lakini akaogopa. “Anaweza kubadilika. Ukweli unauma! Heri nijiachie tu.” Nanaa
akawaza.
~~~~~~~~~~~~~
Akaruhusiwa,
Geb akaenda kulipia, akarudi chumbani kumchukua Nanaa. Walitoka pale chumbani
wakimshukuru Mungu wao. Hawakuacha kuwashukuru wauguzi wote, tena kwa kuwashika
mikono. Ndipo wakatoka hapo. Wakati wapo kwenye gari Geb akaanza. “Naomba
nikuombe kitu Nanaa.” “Nini?” “Tuingie mahali kidogo tupumzike hata masaa manne
tu.” “Geb! Na watoto?” “Mama alishachukua maziwa yakutosha asubuhi. Tukifika
nyumbani watakuganda. Heka heka zakulea zitaanza. Mimi tena itabidi nisubiri. Naomba
twende kwa muda huo mfupi tu. Angalau na mimi unipe hayo masaa machache.
Nipumzike tena kifuani kwako. Nilale hata masaa mawili bila kelele. Nikiamka
ndio twende.” Nanaa akamuhurumia.
Alijua
tabia ya Geb yakutafutia usingizi mwilini mwake. Hasa kifuani. Akishalala ndipo
alipokuwa akitoka kifuani kwake, nakulala kwenye mto. Tena baada ya Nanaa
kumchezea nywele na masikio. Alikuwa akilala usingizi mzito. “Au umechoka?”
“Hapana Geb. Hata mimi nitafurahia wakati mtulivu na wewe. Twende tu.” Geb
akatoa gari hapo kwenye viwanja vya hospitalini mpaka kwenye hoteli aliyojua
italeta utulivu. Palikuwa kimya, na ipo maeneo mbali na barabara kubwa.
Akalipia, wakapata chumba, akarudi kwenye gari. Akamchukua Nanaa na kuelekea
kwenye hicho chumba.
Geb & Nanaa
Hapa
ndipo Nanaa alipojua kama Geb alikuwa na hamu naye. Alihangaika na mwili wake
bila papara, akiwa anafurahia kila kitu. Walifanya mapenzi kwa muda mrefu.
Nanaa akafananisha na uchu aliokuwa nao mara ya kwanza mjini Morogoro, wakiwa
ndio wamepata fursa kwa mara ya kwanza kufanya mapenzi. Alifanya mapenzi na
Nanaa kwa taratibu na tahadhari, mpaka aliporidhika. Ndipo akajilaza hapo
kitandani, nakupitiwa na usingizi mzito huku amemshikilia Nanaa.
Alipoona
amepotelea usingizini, akajivuta pembeni na kuchukua simu ya Geb, akamtumia
ujumbe mama G. ‘Ni mimi Nanaa. Bado unamaziwa
yakutosha?’ Baada ya kama dakika 13
akajibiwa. ‘Kwani mnakuja saa ngapi? Mwanao
anakazi ya kula tu. Hana kingine anachokifanya hapa.’ ‘Geb ndio amelala. Sijui
ataamka saa ngapi!’ ‘Sasa wewe muendekeze huyo, ulezi utakushinda.’ ‘Amechoka
sana.’ ‘Sawa.’ Nanaa akacheka baada yakusoma ile ‘sawa’ ya mama G.
‘Akiamka tu,
tunakuja bwana mama. Wewe mpunguzie kula.’ ‘Mtoto unahatari mbaya wewe! Yote
hayo ili baba yake asisumbuliwe?’ ‘Kumbe? Walitukuta hao!’ Nanaa akajibu. ‘Basi umama
umeshakushinda.’ ‘Hamna bwana. Nakuja mama yangu.’ ‘Tena uje kweli. Ikifika saa
12 jioni hajaamka, lazima umwamshe huyo. Uje nyumbani. Acha kumfuatiliza Geb.
Anapenda kupendwa kama huyu mwanae hapa anayenirembulia macho. Njoo Oli wangu.’ Nanaa akacheka huku akimsikiliza akimwita mjukuu
wake. ‘Bye. Nitakuona baadaye.’ Nanaa akaaga. ‘Na uwahi Nanaa. Usinitanie.’ ‘Nakuja mama. Usiwe na wasiwasi.’ Alipotuma huo ujumbe wa mwisho, Nanaa akazima simu
kabisa. Akajilaza pembeni ya Geb. Mpaka saa 12 jioni ndipo wakaamka.
Nyumbani.
Walirudi
nyumbani wote wakiwa wametulia na mawazo yapo kwa watoto wao tayari kwa ulezi.
Walikuta marafiki na familia zao wakiwasubiria. Geb akamwangalia mama yake
nakutingisha kichwa. “Nichakula cha usiku tu baba. Nilitaka watu waje,
tumshukuru Mungu pamoja. Basi.” Mama G akajitetea kwa Geb. “Kwani huwa huwezi
kusubiri mama jamani? Yaani ndio Nanaa amerudi tu. Hata hajapumzika, ushaita
watu!” “Si mmetoka kupumzika nyinyi!?” Geb akajua hawezi kushindana na mama
yake. Akanyamaza.
Walikuwepo
hapo marafiki wa Geb, wakike na wakiume. Waliosoma pamoja na baadhi wa ofisini
kwake. Mama G alitaka walete na watoto wao. Kwa ajili ya kusherehekea birthday
ya Liv na huyo Magesa ambaye alishaanza kuchangamka. Sababu ya kucheza sana na
Fili, Oliva alishaanza kutembea bila hata ya kuanguka. Wengi walisema aliwahi
kutembea. Mama G alimuomba mama mmoja ambaye ni rafiki yake anayefanya mambo ya
catering. Akamletea chakula kizuri sana hapo nyumbani.
Walimwimbia
Oliva, akakata keki kwa mikono yake bila kisu. Akaanza kumlisha kila mtu
aliyeambiwa na anti yake. Grace ndio alikuwa akimwambia amlishe nani na baada
ya yupi. Basi Oliva alifanya huku akicheka. Walimchukua video nyingi tu huku
akipigwa picha. Vilijaa vicheko. James naye alikuwepo.
Nanaa
alirudi kukaa kwenye kochi na watoto wake. Liv akimchezea nywele huku
akimwangalia Magesa. Hakuna furaha ungemwambia Nanaa ipo ya zaidi ya vile
anavyojisikia wakati ule. Alizungukwa na watoto hao wawili, ambao kila mtu
alikuwa akimsifia na kumpongeza. Mara nyingi watu walimuomba kumshika Magesa,
nakumrudishia. Mwishowe bibi yake akataka akalazwe. “Hata hamu haijaniisha mama
jamani!” “Kelele sana hapa, ndio maana anashituka shituka. Kesho siku nzima
nitakuachia.” Nanaa akacheka na kumkabidhi.
Wakabaki
wakiangaliana na Oliva. Akamuona Liv ameshuka kutoka kwenye kochi, anakwenda
kuchukua kitambaa kama mtandio aliozoea kumpa mama yake ajifunike ili anyonye.
Akarudi nao. Akasimama mbele ya Nanaa huku akicheka. “Liv wewe! Huoni aibu
mbele za watu? Bwana umeshiba. Nimemuona dad akikulisha. Nenda kacheze na
Fili.” Liv akabaki amesimama mbele ya mama yake. “Nenda kacheze kidogo Liv.
Huna njaa bwana! Haya nenda mama yangu. Nenda eeh!” Nanaa akabembeleza lakini
Liv akamgomea. Japo alikuwa katikati ya wenzake. Wakicheka na kelele nyingi, lakini
macho yake wakati wote yalikuwa kwa Nanaa, mpenzi wake. Geb akawaona.
Akawasogelea.
“Eti Liv anataka nyonyo jamani wakati ameshiba!” “Huyo sio kwamba anataka
nyonyo sababu ya njaa. Liv anahamu na wewe. Akiwa na hamu na wewe, ziwa pekee
ndilo linamfariji huyo mwanao, kama hujamjua. Ameona wamemchukua mtoto, ndio
akaona na yeye amepata nafasi.” Geb akamjulisha Nanaa. “Kumbe!” “Wewe huoni leo
hataki kucheza na yeyote. Hata Fili amemkatalia kucheza. Anataka awe hapo
karibu na wewe tu.” “Jamani Liv wangu! Hata mimi nina hamu na wewe mama yangu.
Sasa kwa kuwa wewe ni mtoto mzuri, twende chumbani ukanyonye vizuri, halafu
unipe habari za hapa.” Liv akacheka.
Geb
akataka kumnyanyua, akakataa. “Mama hawezi kukubeba Liv. Mimi nataka kukubeba
tu ili nikupeleke huko chumbani. Namsaidia mama.” Nanaa alikuwa amesimama. Liv
akajificha kwenye gauni alilokuwa amevaa mama yake. Alilivuta upande,
akajifunika usoni. “Huna utakalomwambia huyo akakubali. Akishaamua kitu huyo,
kaamua.” Mama G akatoka akamkuta Geb anaongeleshana na mwanae. “Njoo mtoto
mzuri.” Geb alimjaribisha tena. Akamchungulia kutoka kule alikokuwa amejificha
uso, akamcheka baba yake akarudi pale pale. Mpaka Nanaa akacheka.
“Na
tabia yake ndio hiyo hiyo. Unaweza dhani cheka yake ndio anakukubalia! Kumbe
wala. Anakuchekea huku anakukatalia. Wewe mshike mkono mpande naye hizo ngazi.
Wala usimbembe.” Bibi yake akatoa wazo.
Nanaa akainama. “Eti Liv?” Bado alikuwa akicheka. “Muone vidimpozi vyake! Haya
twende.” Wakaanza kuondoka. Wakamuona Geb anawafuata nyuma. “We Geb! Hebu rudi
hapa. Wote wapo hapa kwa ajili yenu. Sasa sio muende mkajifungie huko!” Geb
akacheka. “Narudi mama. Nawasindikiza tu.” “Mmmh!” Mama G akaguna. Mpaka Grace
naye akacheka.
Geb
alirudi kwa rafiki zake, akamuacha Nanaa anamnyonyesha Liv huku wakizungumza.
“Nilikuwa na hamu na wewe Liv!” Liv akamwangalia huku ziwa la mama yake lipo
mdomoni. Akaendelea kunyonya. “Unampenda Magesa?” Nanaa akamuuliza. Liv
akatingisha kichwa kukubali. “Wewe ni dada mzuri Liv! Lazima umpende sana mdogo
wako. Umesikia Liv? Akilia tu, unambembeleza nakumpa chupa yake yamaziwa.”
Nanaa akaendelea kuzungumza naye taratibu huku wamejilaza kitandani. Liv
ananyonya huku akimsikiliza mama yake. Nanaa alikuwa akimchezea nywele taratibu
huku akimshikashika kwa upendo mpaka wote wakalala.
~~~~~~~~~~~~~
Geb
alikuja kumuamsha ili anywe dawa. “Kaka hajaamka?” Nanaa akauliza huku
akimsogeza Liv. “Alivyojikunja hapa, kama kitoto cha paka!” “Huyo mtoto
anakupenda sana Nanaa. Ukikosekana hata siku mbili tu, anabadilika. Kila mtu
anajua.” “Jamani Liv wangu! Sijui ni vile nilivyokuwa nikizungumza naye sana
wakati yupo tumboni?” “Ni Mungu tu amekupa mtoto anayekupenda.” “Namuombea na
mdogo wake awe hivyo hivyo. Lakini sijisikii vizuri hivyo anavyokuwa anapewa
maziwa ya chupa. Hana connection na mimi! Hatakuwa na hisia kwangu. Kuanzia
kesho namwachisha kabisa maziwa ya kopo. Namrudisha kifuani.” “Utachoka Nanaa.
Magesa ni mlaji. Wewe muulize mama. Anakula kama mchwa.” Nanaa akacheka.
“Kwa
kuwa umerudi mwenyewe, jiongezee muda naye. Mnyonyeshe, lakini pia usimwachishe
na chupa. Utachoka kuamka usiku kila mara.” “Nitaangalia. Sina kazi nyingine
kwa sasa isipokuwa hawa watoto Geb. Nachoshwa na nini?” Geb akafurahia kuona
akili ya Nanaa imetulia na anafikiria tu watoto au mambo ya pale nyumbani. “Mbona
pako kimya?” “Ujue sasa hivi inakaribia saa 4 usiku? Watu wameondoka kasoro
Danny nafamilia yake, James na Gozi ndio wapo bado wanazungumza. Naona Gozi
alikuwa na haraka, lakini gafla yeye ndio amegeuka mwendesha kikao. Maneno
hayamwishi. Ila nimemsikia Grace anataka waondoke.”
“Tumelala
sana na Liv.” “Kwani hotelini hukulala?” “Sio sana. Nahisi nimekuja kumaliza
uchovu wote hapa. Sasa hivi najisikia vizuri.” “Afadhali. Sasa itabidi huyo
atoke hapo. Arudi kitandani kwake, mimi nichukue nafasi yangu.” Nanaa akacheka.
“Ngoja nikamshukuru Grace kwa kumsaidia mama na kazi ya hawa watoto. Twende.”
Geb akambeba mtoto. Wakatoka.
~~~~~~~~~~~~~
“Sasa
huyo amebakisha maziwa ya mdogo wake kweli?” Grace akauliza, Nanaa akacheka. “Nilishakamua
wakati nilipokuja tu. Nimempa mama tayari.” Nanaa akakaa. “Naomba nikushukuru
Grace wifi yangu. Asante kwa kumsaidia mama na shuguli za hawa watoto.
Nashukuru pia kwa kuja kuniona hospitalini.” “Karibu Nanaa. Nakuombea upone na
Mungu akupe hekima uwe mama mzuri kwa wanao. Umejaliwa watoto wazuri sana. Kazi
ni kulea tu.” “Asante kama unaniombea, maana ni kweli nahitaji maombi.” Nanaa
akajibu.
“James
anazidi kuzeeka!” Danny akatania. “Si mchezo! Wajukuu au maanko wawili! Mzee
umekua dingi.” Gozi akaongeza wote wakazidi kucheka. Geb akarudi kukaa pembeni
ya Nanaa baada yakumlaza mtoto. Mama G akamletea mtori. Bila kujivunga akaanza
kula kwa juhudi zote. “Asante mama yangu. Mbona sasa Geb wangu hali?” “Nilikuwa
na njaa kama sijala mwaka. Nimekula wakati mmelala na Liv.” Nanaa akamwangalia
na kucheka. Akakumbuka shuguli waliyokuwa nayo hotelini.
Wakati Kunapoonekana Kuna Amani,
Ndipo Na Uharibufu hunyemelea.
Wakati
stori zikiendelea kupamba moto, mida ya saa nne na nusu hivi, hata Danny na
Grace walishasahau kama walishaaga, mlinzi akapiga simu. “Vipi?” Geb akapokea. “Malii yupo
hapa getini na vijana wanne. Anasema ni marafiki zake.” Geb akanyamaza
kidogo na kuangalia saa ya ukutani. Ukweli muda ulishakwenda. Wageni karibia
wote walishaondoka. “Kuna nini?” Mama yake akamuuliza. “Malii yupo getini.” Geb
akajibu. “Kwani ulizuia Malii asiruhusiwe kuingia humu?” “Hapana. Ila mlinzi
anasema ana vijana wanne ambao Malii amewatambulisha kama rafiki zake.
Amewaangalia kwenye orodha ya watu, hawapo kwenye system ndio maana anauliza.”
“Labda ameona alete watu baki mje kuzungumza. Hamkuachana vizuri pale
hospitalini wakati mmekuwa pamoja kwa muda mrefu sana. Ni bora kumsikiliza.
Pengine anataka myamalize” Geb akasita kidogo.
“Wewe
msikilize tu. Usiache kumsikiliza. Halafu maamuzi ndio fanya kwa wakati wako.
Lakini si sawa kumzuia kuingia getini.” Mama G akasisitiza. Akiwa anasita sana
rohoni Geb akaona asimkaidi mama yake pale mbele za watu wote. “Waruhusu waingie.” Geb akamjibu
mlinzi, akakata simu na kurudi kukaa.
Moyo
wa Nanaa ulipasuka kama kulikoangushwa chuma sakafuni. Tayari akakosa raha.
Alitamani amwambie Geb asimruhusu, lakini hakujua atasema ni kwa nini.
Akakumbuka ndoto mbaya aliyoota wakati yupo hospitalini, alipoota akiwa na
Malii. Akahisi si kwema. “Naomba nikamalizie chakula changu chumbani.”
Akamnong’oneza Geb. “Nisubiri twende wote.” Geb akamjibu taratibu. Nanaa hakuwa
na ujanja. Ila kubaki.
Wakasikia
kengele mlangoni. Geb akasimama kwenda kufungua. Wote walikuwa kimya kabisa.
Wametulia wakimsubiria Malii na hao rafiki zake. Aliingia na vijana wakubwa na
wageni kabisa kwao. Hawakuonekana na sura za kirafiki hata mmoja wao. Malii
alipita kukaa, lakini wale vijana wakasimama.
“Kwema?”
Akaanza mama G. “Tutajua yote baada ya kukamilisha kilichonileta.” Malii
akajibu. Lakini si kama walivyomzoea. Alikuwa na sura ya tofauti waliyomzoea
kumuona nayo. Mara nyingi mida ya jioni huwa anakuwa alishaingiza mwilini bia
za Safari kadhaa. Lakini muonekano wa leo haukuwa wa
‘Safari’. Ni zaidi yake.
“Funga
mlango na kushusha mapazia.” Malii akatoa amri kwa mmoja wa kijana aliyekuja
naye na kuogopesha wenyeji. “Hee! Kwani vipi Malii mwanangu?” Mmoja wa wale
vijana akamsogelea mama G nakumpiga ngumi ya nguvu kwenye shavu. Mama G akatema
damu nyingi, kuashiria kupasuka kwa ndani. Hapo ndipo Geb akataka kusimama ili
kumtetea mama yake, na yeye akapigwa teke la nguvu la tumbo, lililomtupa
sakafuni. Hapo ndipo wakajua hali si shwari.
“Naombeni muwafunge wote na muwasogeze wote pale pembeni. Sitaki kuingiliwa”
Malii akaamuru. Walitoa tape. Gundi kali ya plastiki nyeusi. Kubwa na pana. Wakawabandika mdomoni ili wasiongee au wasisikike hata kama wakitaka kupiga kelele. Waliwafunga wote mikono yao kwa nyuma. Ndipo wakawafunga tena kila mmoja, miguu yote miwili kwa pamoja, kwa kutumia gundi hiyo hiyo, kasoro Nanaa. Malii alimvuta kutoka pale alipokuwa amekaa kwenye kochi, akabaki amemshikilia huku wamesimama.
“Ukitulia,
sitakuumiza.” Malii alizungumza naye akiwa amemkumbatia kiunoni. Akambusu, Nanaa
akamkwepa. “Leo ndio unanikana mbele za watu!?” Malii akauliza nakushangaza
kila mtu. “Mimi sio kama Zinda.” Malii akaanza. “Mimi ni mtu wa action. Vitendo
tu. Sasa nimekuja kuchukua kilicho changu.” Malii akaendelea. “Nyinyi wote
hamjui kilichokuwa kikiendelea kati yangu na Nanaa, baada ya Geb kutamka wazi
wazi kuwa hamtaki Nanaa. Wewe James, ukiwa rafiki wa karibu. Mtu wa nyumbani.
Umezuzuliwa na vijisenti vya Geb, ukaamua kumpa dada yako ili upate pakuvunia
pesa, ukasahau kuwa Geb alimkana Nanaa.” Malii akatulia.
“Labda
niwaeleze kwa kifupi. Mimi nilijua wazi hisia za Geb kwa Nanaa. Kwa kuwa mimi
nilikuwa karibu sana na Geb kuliko nyinyi wote. Tuseme alikuwa akizungumza na
mimi kuliko nyinyi wote. Nilijua alikuwa akimfuatilia Nanaa. Miaka yote
tulikuwa tukisikia habari za Nanaa, lakini James alikuwa akimficha huyu dada
yake mpaka siku ile ya birthday ya Fili ndio kila mtu akamuona Nanaa, nakusahau
kama Geb alikuwa akimfutilia Nanaa. Lakini sio mimi. Mimi sikupagawa. Nikasema
nifuate utaratibu. Kwa kuwa Geb ni mtu wangu, tumetoka mbali. Na wote tulijua
kama Geb alikuwa akimfuatilia Nanaa.” Malii akaendelea.
“Usiku uleule. Sikutaka hata kupoe. Wakati watu wanaondoka. Mimi nikamwita Geb pembeni. Nikamuuliza, itakuaje juu ya Nanaa na wakati ule yupo kwenye mahusiano na Liz? Haya ndio yalikuwa majibu yake.” Malii akatoa simu aliyokuwa amemrikodi Geb akijibu juu ya Nanaa, na Liz. “Hamna kitu bwana. Mimi nilikuwa nikimuulizia tu.” Geb alisikika akijibu.
“Kiuungwana
tu. Ili nisikanyage waya za umeme nikiwa nimeloa. Nikasubiri kuona
kitakachoendelea. Nikasikia watu wakisema. Tena sio watu, ni huyo Gozi.
Akaniambia Geb kavuta kifaa ndani. Yaani Nanaa. Nikashituka sana. Nikaamua
kumtafuta tena Geb. Nikamuuliza, ‘Nasikia umemuhamishia Nanaa nyumbani kwako.
Ndio umeamua kuchukua hatua?’ Haya ndio yakawa majibu ya Geb. “Acheni uzushi jamani. Nanaa yupo kwangu kwa kuwa James aliwaomba Grace
na Danny waishi nae kwa muda. Sihusiki na Nanaa kuwepo nyumbani kwangu. Anasaidiwa
tu na kina Grace. Yeye na kaka yake James wakiweka sawa mambo yao, ataondoka.” Geb akasikika akitoa jibu.
“Binafsi
nikajua hilo jibu ni la jumla sana. Nikaamua kuwa muwazi kwa Geb. Nikamuuliza.
Hakuna hisia zozote za kimapenzi? Kama mnavyomfahamu Geb, jeuri imemjaa.
Akanyamaza. Nikaweka msisitizo. Nikauliza tena kutaka uhakika ili kusije kuwa
na lawama baadaye. Nikauliza, ‘Unauhakika hakuna
hisia za kimapenzi kwa Nanaa?’ Geb
akanihakikishia kuwa yeye alikuwa akimfutilia Nanaa kama mdogo wa James tu, na
si vinginevyo.” Malii akaendelea.
Nanaa
alikuwa akilia sana. “Naomba niache
Malii. Usiniguse.” Malii akacheka. “Nimekuhakikishia
ukitulia, sitakuumiza Nanaa. Usifanye fujo. Hakika nitakuumiza.” Nanaa
akaendelea kulia. “Tokea juzi najifunza kuvuta bangi kwa ajili yako.
Usinikorofishe, nakuahidi sitakuumiza. Tulia.” Akaendelea.
“Basi.
Kwa kuwa milionea Geb akawa amekiri hana shida wala hisia zozote kwa Nanaa,
kama na nyinyi mlivyomsikia kwenye rikodi yake ya mwisho, mimi nikaanza kutupa
ndoano kwa Nanaa. Tukaanza akiwa hanifahamu. Lakini jumbe na simu za hapa na
pale kati yangu mimi na Nanaa zikaendelea. Kila siku nilikuwa nikipata nguvu
yakuendelea na maisha baada ya kuwa kwenye ukurasa mmoja na Nanaa. Akasisitiza
tufahamiane kwa kuonana. Nikaweka mipango. Tukaonana.” Malii akaendelea.
“Tulipokutana,
nikajitambulisha bila kumficha. Nilimwambia kuwa nilimfahamu tokea tupo
sekondari kwa kupitia kaka yake. Nikamueleza kila kitu. Nikamwambia hata siku
ile ya birthday ya Fili na mimi nilikuwepo na nilimuona. Sema watu tulikuwa
wengi pengine hakuniona vizuri. Nanaa akasita kabisa. Siku ya kwanza tukaachana
akiwa anaonekana wazi anataka kukatisha yale mahusiano. Mimi niliendelea na
jumbe zangu za kuomba radhi kwa kutojitambulisha vizuri tokea mwanzo huku
nikimfariji kwa jumbe, mpaka Nanaa akasamehe. Mawasiliano yakarudi. Ninazo
jumbe kibao zangu na Nanaa. Sitawaonyesha kwa heshima ya Nanaa.” Malii
akaendelea.
“Nilimwambia
ninaye mwanamke nataka kumuoa. Ila akinikubali, sitamuoa huyo mwanamke. Hapo
napo Nanaa akasita lakini hakukataa moja kwa moja kwa umbali tuliokuwa tumefika
mimi na yeye Nanaa. Ilikuwa ni week ya birthday yangu. Nikamwambia Nanaa.
Akaniuliza ninataka zawadi gani, nikamwambia namuhitaji yeye. Tukazungumza sana
na nikambembeleza. Nanaa akanikubalia tukutane, tukafanye mapenzi.” Kila mtu
akamgeuka Nanaa, akainama huku akilia.
“Akaletwa
na taksii mpaka nyumbani kwa Gozi. Nilimuomba aniachie funguo kipindi kile
anakwenda Japan kwenye mambo yake ya kikazi. Basi, tukapata muda mzuri sana na
Nanaa. Vilijaa vicheko, habari za hapa na pale. Nikajua Nanaa amenikubali kwa
hakika.” Malii akaendelea.
“Kumbuka
ombi langu la mwisho lilikuwa ni akubali nimuoe. Kuwepo pale kukamilisha
mapenzi na mimi, nikajua nimepata mke. Sikutaka kupoteza muda zaidi, nikamvutia
chumbani. Romance ikaendelea tukiwa kwenye ukurasa mmoja. Nikiwa nishamvua nguo
zote, yupo kitandani, akiniona hali yangu mbaya kabisa, nilazima nilale naye,
eti akanibadilikia! Akakaa na kujifunika. Hakika alinikatili vibaya sana Nanaa.
Nililia kama mtoto nikimsihi angalau anisaidie tu. Ameshanionyesha mwili wake,
amenibadili hali yangu, sijiwezi tena, anisaidie. Nanaa akakataa kata kata bila
hata huruma hakuwa nayo.” Malii akaendelea.
“Hakuna
mwanaume ambaye atafanikiwa kuona mwili wa Nanaa akabaki alivyo. Nanaa anavutia
ndani bwana!” Nanaa akampiga kibao cha mdomo kwa haraka. “Kaka
yangu yupo hapa. Mshenzi wewe!”
Nanaa akaongea kwa hasira. Malii alimrudishia kofi la nguvu, likamsindikiza
Nanaa sakafuni. “Wewe ndio mshenzi Nanaa.” Malii akamjibu kwa hasira akiwa
ameshakasirika zaidi usoni.
“Unajua
madhara uliyonisababishia lakini? Kila mwanamke ninaye lala naye, nakuona wewe.
Umeharibu ndoa yangu. Kila nikimshika mke wangu, au niseme aliyekuwa mke wangu.
Maana nishampa talaka yake. Tena ni kwa sababu yako Nanaa. Nimeshindwa hata
kufanya naye mapenzi kwa kuwa hafanani na wewe. Silali mchana wala usiku bila
kukuona ukiwa umelala uchi kitandani. Unaniumiza kupita unavyofikiria.
Nilikwambia siku ile tulipokutana mimi, wewe, Geb na Manka. Walipotoka
nikakuomba. Nikakwambia nisaidie basi hata mara moja tu ili niweze kuendelea na
maisha yangu kwa kuwa uliniacha pabaya. Unakumbuka uliondoka na kuniacha kama
mbwa?” Malii akamuuliza Nanaa aliyekuwa akilia pale chini.
“Nilikwambia
wazi Geb hakupendi. Anachokupendea labda ni hiyo rangi na kiuno tu. Geb
anapenda wanawake smart kama Liz. Ukanijibu kwa jeuri hata wewe ni smart. Kama
wewe ni smart na kama kweli Geb anakupenda na kukuzalisha watoto wawili,
ameshakuoa? Unaweza kusema hapana sababu ya hili au lile. Basi ni jibu hata
kama anakushirikisha katika mali zake. Hata unajua anakiasi gani benki!? Unajua
anamiliki biashara ngapi? Unajua anatengeneza kiasi gani kwa mwezi? Unajua
anapokwenda kila siku asubuhi anapokuaga kuwa anakwenda kazini? Wewe unajua
huwa anakwenda kwenye biashara ipi? Mtoto wa kichaga unayeijua pesa, unakubali
kugeuzwa Fala! Anakufanya kama mbwa tu, hana hisia zozote zakimapenzi na wewe.
Anachotaka ni hichi. Mashine ya kumfyatulia watoto, basi. Huna thamani yeyote
kwake. Mimi ndio nilikupenda kwa dhati.”
Nanaa aliendelea kulia.
“Sasa
sitaki tupotezeane muda. Nimefuata haki yangu, ili maisha yangu yaendelee na
wewe nikuache hapa hapa ili uendelee kula na kulala bure. Maana ndio shida
aliyojua Geb unayo wewe na kaka yako. Huna pakuishi, wala kaka yako hana uwezo
wa kukulisha tena. Mchaga huyu wa kiume, amefilisika na amechoka kupambana hapa
mjini ili aweze kukutunza wewe dada yake ndio maana amekusukumia hapa kwenye
pesa ili ule na kulala bure. Huku akikubali uzalishwe bila ndoa wakati yeye
mwenyewe James, hathubutu kuvulia nguo mwanamke yeyote yule. Anamsubiria
mkewe.” Malii akacheka.
“Hakika
James wewe ni mshenzi sana. Unatudhalilisha wachaga, James. Sisi ni
wahangaikaji bwana! Huwezi kushindwa kuyamudu maisha kwa kiasi chakuuza dada
yako! Yaani umeshindwa kumtunza dada yako mwenyewe, umeamua aje alalwe hapa ili
ale na kula bure!? Kweli wewe kiboko!
Sasa kwa kifupi, nimeamua kuanza maisha mapyaaa. Nikatulie mahali kimyaaa.
Lakini siwezi kuanza nikiwa na Nanaa kichwani mwangu. Nimekuja tumalize
tulichoanza, ili..” “Haiwezekani Malii!
Huwezi kunifanyia hivyo.” Nanaa alizidi
kulia.
“Labda
hujanielewa Nanaa. Unanigarimu maisha yangu, kupita utakavyodhani. Hapa nilipo
sina kitu wala mtu kwa sababu yako. Nimeuza kila kitu ikiwemo nyumba ya kaka
yangu niliyokuwa nikiishi na Manka, ili niweze kuwalipa hao vijana, waje
wanisaidie kukamilisha ndoto zangu. Natembea kama mjinga humo mabarabarani
sababu yako! Nimezidisha pombe kwa ajili yako! Napenda ngono, lakini nayo
siifaidi sababu yako! Kwa kifupi nimekuja kujikomboa na maisha yangu.
Nimetangaza kufa leo, au kupona. Ilimradi unitimizie ulichokuwa umekianza
mwilini mwangu. Sijaja kuomba. Ni heri nitoke maiti hapa, kuliko mzima ambaye
hujanikamilisha. Wewe ndio unahatima yangu. Kufa au kuondoka hapa nikiwa tayari
kuanza maisha yangu mapya nikiwa nimetulia akili.” Malii aliendelea.
“Hao
vijana wanne, nimewalipa pesa za kifo chao. Niliwatahadharisha kuwa ni kazi ya
kifo. Pesa waliyonitajia, huwezi amini. Lakini nimekubali kuuza kila kitu.
Mpaka gari yangu, ili niwalipe kabisa. Waache urithi kwa ndugu zao kabla
hatujaja hapa. Hawana chakupoteza tena. Lililotuleta hapa ni mimi kufanya
mapenzi na wewe Nanaa. Basi. Na ninakuhakikishia, leo nitalala na wewe mpaka nitosheke
ndipo nitakapoondoka hapa. Kwa hiyo naombeni mtulie.” Malii akawageukia
wengine.
“Kilichotuleta
hapa ni Nanaa tu. Na Geb.” Akamsogelea karibu Geb. “Usithubutu kufanya
chochote, hakika nitakumaliza. Unajua nina hasira na wewe. Umenidhalilisha
vyakutosha. Umemchukua Nanaa kutoka kwangu ukiwa huna mapenzi ya dhati kwake
ila tu kututhibitishia wewe unayo pesa. Hakika tulia. Lasivyo utawaacha watoto
wako wakiwa bado wadogo sana. Ninachuki na wewe, kukuua haitanisumbua.”
Akampiga teke la nguvu kwenye miguu, kisha akamtemea mate. “Mshezi mkubwa wewe
Geb. Leo nakuonyesha pesa sio kila kitu.”
Akawageukia
wengine. “Sasa nisikilizeni, hao vijana nitakao waacha hapa, wapo kikazi.
Hamuwajui, hawawajui. Washachukua pesa zangu zote. Wameapa kunisaidia
kukamilisha lengo langu. Hawatasita kuwadhuru kwa namna yeyote ile. Tulieni
kimya ili mimi na Nanaa tukamalizane. Nitamwacha hapa hapa na yeye Geb aendelee
kujifidia misaada yake.” Akamvuta Nanaa.
“Naomba niache Malii.” Nanaa alizidi kulia.
“Unakumbuka ulivyonianza kwa mbwembe mpaka ukaniamsha na ukaniacha nakulilia?
Sasa leo unaenda kumaliza ulichokianza mwilini mwangu. Ila nakupa uhuru wa
kuchagua. Hapa kwenye kochi mbele ya kaka yako na Geb, au chumbani kwa Geb.
Maana hapa sio kwako hata iweje. Geb anathamini mali zake kuliko mtu wala kitu
chochote hapa duniani. Hutakaa ukamiliki chochote kwa Geb. Labda hao watoto
aliokuzalisha. Mimi namfahamu Geb.” Nanaa akashika kochi kwa nguvu.
“Ooh!
Kumbe unataka hapa hapa kwenye kochi? Basi mmfungeni hapo hapo kwenye kochi
mimi niendelee kukata kiu.” Vijana wawili wakamsogelea. “Hapana
Malii. Naomba nisamehe tafadhali. Nisamehe kwa ukatili niliokufanyia na
nisamehe kwa kila kitu. Lakini usinibake tafadhali Malii.” Nanaa
aliendelea kuomboleza wakati Malii akivua nguo pale pale mbele za watu. “Hakuna
kitu cha ajabu utanipa tofauti na unachompa Geb.” Nanaa akampigia magoti. Malii
akabakiwa na nguo ya ndani tu. Alishavua mpaka soksi.
~~~~~~~~~~~~~
Malii amekuja kudai na yeye haki yake kwa Nanaa.
Tena ndani ya jumba hilo lililojazwa mali za thamani na ulinzi wa nguvu
wa masaa 24. Thamani ya pekee hapo ni Nanaa peke yake. Ameuza kila kitu ili tu
kukamilisha alichokianzisha Nanaa sirini. Yupo na wanaume wa nguvu
wanne, waliokubali kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kutimiza azma yake.
Nanaa hana mtetezi. Aliokuwa nao wote wamefungwa, hawawezi kujitetea hata wao wenyewe. Geb
alishapigwa teke, mama G anavuja damu za mdomo.
Upo wapi ulinzi wa Geb?
Unaweza kufikiria hali ya Geb moyoni mwake kwa wakati huo pale sakafuni
akiugulia maumivu ya teke, mama yake amepigwa, anavuja damu, hawezi kumtetea, na kudhalilishwa mbele ya watu?
Sababu ni Nanaa aliyemficha ukweli tena akiwa amembembeleza kwa kurudia
rudia awe anamwambia ukweli wote hata kama anajua utamuumiza sana.
Sasa kuja kujua ukweli wote kutoka kwa Malii, akiwa ameyatoa maisha
yake
kwa kiasi hicho kwa Nanaa. Walikuwa wote hospitalini
muda wote huo, na bado Nanaa alimficha ukweli!!
Usikose kujua yatakayojiri. Nani
wa Nani?
Endelea kusoma…
0 Comments:
Post a Comment