Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Ni Wangu! – Sehemu Ya 44. - Naomi Simulizi

Ni Wangu! – Sehemu Ya 44.

 Ujauzito Wa Olivia

Nanaa na Geb wakaendelea kula wakiwa hapo hapo kwenye makochi. “Umependa huo ugali?” Nanaa akamuuliza. “Nimependa. Naona kweli wameupika sasa hivi. Bado laini.” Geb akaendelea kula, huku Nanaa akiendelea na yeye kula kwa mara ya pili. “Nimefurahi unakula tena.” “Nahisi nilikuwa nimekasirika tu. Sasa hivi naona hali imerudi ileile! Na mpaka nijifungue, nahisi nitanenepa mpaka nitapasuka.” Geb akacheka. “Kwani kwenye mimba ya
Liv hukuwa ukila? Nilikuona ulikuwa umekonda sana.” “Kipindi cha ujauzito wa Liv kilikuwa kigumu sana kwangu Geb. Nilijitahidi kupambana kwa kadiri ya uwezo wangu. Kipindi kile mambo mengi yalikuwa yakiendelea kwenye maisha yangu. Sikuwa nimetulia, ingekuwa ngumu kunenepa.” Nanaa akatulia kidogo.

“Kwanza sikuwa na pesa ya kutosha. Au niseme nilikuwa nikibania pesa ili Liv akizaliwa asipate shida. Halafu nilikuwa nikijitahidi kula vyakula vya kunijenga afya yangu zaidi. Kwa hofu nisijekuwa dhaifu nikashindwa kujifungua. Nikaishia kufa mimi au mtoto. Kwa hiyo sikuwa na uhuru wa kujichagulia. Nilikuwa napika vitu ninavyojua mwili unahitaji huku nikinywa dawa za virutubisho kwangu na kwa mtoto. Nyingine nilikuwa nikinunua gali! Ni hizi za GNL za kina mama wajawazito. Lakini nilifanya makusudi ya kuingia garama ili nisipatwe maradhi.” Nanaa akatulia kidogo, kisha akaendelea.

“Halafu ukumbuke nilikuwa nimebeba mimba ya Liv nikiwa najua nimefanya kosa kama alilofanya mama yangu. Kuzaa bila makubaliano. Kwa hiyo nilikuwa najilaumu huku nikijua umerudiana na Liz. Sikujua kama utakuja kumkubali Liv. Kwa hiyo nilijawa wivu na majuto ya kupita kiasi. Nilikuwa silali vizuri. Wakati mwingine nilikuwa nakuota labda unanibusu shingoni nikiwa nimelala. Kama hivi nilivyozoea nikilala ubavu ubavu huwa unanibusu huku shingoni au vile unavyokuwa ukinichora mgongoni taratibu. Basi nilikuwa nikiota unanifanyia hivyo, nashituka kutoka usingizini, nashindwa hata kulala tena. Kwa hiyo sikupata wakati mtulivu wakujifikiria sana. Nilikuwa nakula chakula kama dawa kwa ajili ya mtoto.” Nanaa akaendelea.

“Na ukumbuke ndio nilikuwa mwaka wa mwisho. Napambana angalau nimrudishie kaka cheti kizuri ili asione juhudi zake zilikuwa bure. Niliogopa nisije kurudi na mtoto tu, tena asiye na maelezo yakutosha, badala ya kumpelekea cheti kizuri. Kwa hiyo nilikuwa nikipambana kufa na kupona na masomo huku nikijitahidi kumfariji Liv huko tumboni asihisi hayupo sehemu sahihi. Wakati wote nilikuwa nikizungumza naye na kumwambia namsubiria kwa hamu. Wakati hata sikuwa nikijua kama ni wakike au wakiume! Jina sikuwa nalo! Wala sikuwa nikijua pa kumuweka baada ya kuzaliwa. Nilijiambia kila kitu nitakitatua kila kinapojitokeza. Sikutaka kuanza kujipanikisha nikashindwa kufanya mambo yanayonikabili kwa wakati ule. Kwa hiyo kwa kujibu swali lako, sijui hata mimba ya kwanza ilikuwaje. Sikuruhusu sijui vile viugonjwa vya mimba vijitokeze au sijui nataka kula sijui nini! Sijui nina hamu ya nini! Hapana. Kile nilichojua kitamfaa mwanangu, kililazimishwa kupita mdomoni na kukaa tumboni bila kutapika.” “Pole. Lakini nashukuru Mungu umenizalia binti mzuri sana. Oliva ni mtoto wa ajabu sana. Huwa natamani muda wa kumuweka kifuani kwangu ufike. Halafu ajifiche kwenye shingo yangu huku amenikumbatia na vimikono vyake!” Nanaa akacheka.

“Yaani Nanaa, sijawahi kupata hiyo furaha moyoni. Mtoto mtamu bwana! Asikwambie mtu.” “Tena umelea mwenyewe!” Nanaa akaongeza. “Bwana mtoto huyu akaniita na kunitafuta baba yake mapemaaa. Yaani alipozaliwa tu, akaona amtafute baba yake. Nikamfuata mpaka Mlimani kule! Hakuna jinsi nikamweleza mtu furaha Mungu aliyonipa, akaelewa. Ni zaidi ya utajiri au ni zaidi ya chochote Mungu alichowahi kunibariki nacho. Mbali na wewe lakini.” “Nilikuwa nakusikiliza tu.” Wote wakacheka. 

“Lakini Nanaa. Kesho lazima turudi nyumbani. Nina mambo muhimu sana yakufanya ofisini.” Kimya. “Si tunarudi wote?” Geb akauliza. Nanaa akabaki kimya kama anawaza kitu. “Naomba turudi nyumbani Nanaa. Tafadhali sana. Twende tukapambane tukiwa pamoja.” “Tutarudi wote Geb. Kwanza wewe mwenyewe umeshuhudia kuwa siwezi kuishi tena bila wewe. Mtu anagonga mlango tu, nakupigia wewe simu!” Geb akacheka. “Kweli tena. Najiona sitayaweza tena maisha bila wewe Geb. Ila nafikiria mahusiano yetu pale nyumbani. Naona yamevurugwa! Zamani ilikuwa inatia raha kusikia unarudi nyumbani. Lakini sasa hivi! Sijui itakuaje? Moyo unakuwa mzito kweli.” “Wewe ndio kiungo muhimu sana pale nyumbani. Ukiamua wewe, utaweza kuwaunganisha tena wote. Au unaweza kuwavuta tena pamoja. Sasa hivi wote wanaishi katika hukumu. Wanajua wamekusaliti. Au wamesababisha kutofanikiwa kwa harusi yetu. Inawauma sana.” Nanaa akavuta pumzi kwa nguvu akifikiria.

“Naomba simu nimpigie mama. Naona nianzie hapo kwanza. Au unafikiri atakuwa amelala, ni usumbufu?” “Najua atafurahi sana kukusikia. Ni wazo zuri sana. Na ninakushukuru Nanaa.” Nanaa akacheka kidogo. “Kweli. Unafikiri wewe ukinuniana na mama G, mimi nitakuwa kwenye nafasi gani?” “Yameisha Geb. Na nimekuelewa. Hata hivyo namuhitaji sana mama. Ona hapa nilipo. Najua ningekuwa nimezungumza na mama wakati ule aliponipigia Mira, sasa hivi tusingekuwa hapa. Najua angenishauri vinginevyo. Nimekimbia nyumba kwa hofu tu. Mama ni mshauri wangu mzuri sana. Namuhitaji. ” Geb akampa simu yake.

Ukipenda  Boga, Penda Na Ua Lake.

Nanaa akampigia mama G. “Pole mama. Nimekuamsha?” “Hapa natamani kuruka ruka. Sikutegemea kukusikia.” Nanaa akacheka. “Nilikununia hivyo ujue!” “Mbona hilo nalijua.  Sasa hasira zimeisha?” Nanaa akacheka. “Nina hamu na wewe ndio maana.” Mama G akaanza kucheka. “Kwanza asante kwa blangeti na mtori. Liv alikuwa anatetemeka kwa baridi mpaka nikaogopa!” “Pole mwanangu. Naomba nisamehe.” “Yameisha mama yangu. Hapa nilipo nina mambo kibao ya kukwambia. Naona hiyo kesho mbali.” “Kwani mnarudi kesho!?” Mama G akauliza kwa mshangao. Alijua labda Geb angekaa hapo kidogo na familia yake ili kumtuliza Nanaa.

“Geb ana kitu cha muhimu kesho ofisini. Anataka kesho asubuhi tuwe tumeshafika Dar.” “Basi nitakuja kuwapokea.” “Asante mama. Tutaongea zaidi tukionana.” “Haya mwananngu Nanaa. Mungu azidi kuwatunza na kuwabariki.” “Amina mama yangu. Nikupe Geb?” Nanaa akauliza. “Nipe tu.” Nanaa akamkabidhi simu Geb. “Pole na safari.” “Asante. Mambo yote yakienda sawa, tutakuwepo hapo uwanja wa ndege  wa Dar, saa tatu na nusu asubuhi.” “Sasa na huyo mpenda usingizi!?” Mama G akauliza akimaanisha mjukuu wake. “Itabidi kumuamsha tu. Atalala tukifika nyumbani. Kuna mtu nakutana naye saa sita mchana. Lazima niwahi.” “Basi mtakuta nikiwasubiri hapo uwanjani.” “Asante mama.” Geb akashukuru. “Karibu. Wewe na familia yako muwe na usiku mwema.” “Na wewe pia mama.” Wakakata simu.

Hakuna Deni.

 “Kitu cha mwisho na chamsingi kabla hatujaenda kulala.” Nanaa akamgeukia Geb kwa utulivu na umakini. “Naomba ujue sasa hivi hauishi na mimi kwa kuwa nilimlipa mama mkubwa ile pesa.” Nanaa akainama. “Ninapokuangalia wewe Nanaa, siioni ile pesa. Sifanyi mapenzi na wewe kwa kuwa najifidia ile pesa. Hata kidogo.” Nanaa alipooza, akashindwa hata kuongeza neno. “Sikudai na wala sitakuja kukudai wewe wala mtu yeyote yule. Naomba tusije wahi kuizungumzua tena hiyo pesa. Maishani mwetu kote. Naomba isitajwe tena. Ninapokutaka kimapenzi naomba uwe huru, kubali au kataa. Usifanye mapenzi na mimi ukijidhania wewe ni mtumwa wangu. Sinunui penzi kwako Nanaa. Nakupenda. Nataka uwe wangu wa milele. Si kwa pesa ila upendo wa dhati. Sijui kama umenielewa?” “Nimeelewa na samahani.” “Basi. Ni hilo tu.” Geb akasimama. Nanaa alimjua huwa hawezi kuweka kitu moyoni. Huongea. Akabaki ameinama pale kwenye kochi.

~~~~~~~~~~~~~~~~

           “Sasa leo itabidi kulala na Olivia. Hatujabeba kitanda chake. Tukimuacha pale kitandani peke yake, tutamkuta chini ya uvungu.” Nanaa akamgeukia mwanae aliyekuwa amelala ndani ya blangeti lililokuwa likimpa joto. “Nikuulize kitu Geb?” Geb akageuka. “Uliza tu.” Nanaa na yeye akasogea pale alipokuwa Geb, karibu na kitanda alicholala Liv. “Ulimwambia kaka?” “Ilibidi Nanaa. Nilijua umekimbilia kwake.” Nanaa akanyamaza kwa muda.

“Hata Grace na Danny wanajua. Nilikuwa nimechanganyikiwa. Ilibidi na wenyewe kuwapigia simu. Nilijua ndio umenitoroka moja kwa moja. Hata hivyo sikutegemea kama ungenipigia.” Nanaa akamtizama kwa mshangao. “Ni kweli Nanaa. Sikujua ni nini  alichokuwa amekwambia Mira! Sikujua umeamini kwa kiasi gani! Nilijua utakuwa umenikasirikia kwa kukuficha. Nikajiambia na hivi unayo pesa ya kutosha, itachukua muda mrefu sana kunitafuta. Hakika sikutegemea kukusiki kwa mapema hivi. Eti unanifikiria mimi niliyekukosea! Eti kunitoa tena wasiwasi! Sikutegemea. Nilishakuwa nimekata tamaa.” “Nakupenda Geb.” Nanaa akaongea kwa upendo.

           “Hilo nimelithibisha Nanaa. Na ndilo nililokuwa nikilitafuta maishani mwangu kote kabla yako. Wengi wananipenda kwa sababu moja au nyingine. Nafikiri nilikwambia. Kama sio pesa zangu, basi watataka kuzaa na mimi ili wapate watoto kama mimi. Hakuna anayeweza kunifikiria mimi kama wewe. Hata niwe nimekukosea vipi, wakati wote inapokuja swala langu, unaweka hasira pembeni kwanza. Unahakikisha nipo sawa, ndipo unaendelea. Nakushukuru kwa kunijali. Asante.” Nanaa akajisikia vizuri. Akatoa tabasamu la mwito wa mapenzi.

Geb hakumchelewesha. Hapo hapo wakahamia kitanda cha pembeni. Baada ya kufanya mapenzi ya nguvu, Nanaa akalala hapo hapo kitandani. Usingizi mzito wa mimba, ukamchukua. Hata hivyo alikuwa na siku ndefu iliyojaa hofu na vitisho. Mapenzi aliyofanya na Geb mara alipofika na wakati huo, yalimtosha kulala usingizi mzito. Geb akambusu mara kadhaa, kisha akamfunika vizuri.  Yeye akahamia kitandani kwa mtoto wao ili asianguke. Alibaki akimtizama Liv vile alivyolala vizuri. Akajikuta akicheka. Hakusahau, akashuka kitandani, akapiga magoti na kuanza kumshukuru Mungu wake. Akaomba kwa muda ndipo akarudi kulala.

~~~~~~~~~~~~~~~~

Olivia alifungua macho, akamkuta baba yake akimwangalia. Akaanza kucheka. “Hata mimi nilikuwa na hamu na wewe Liv.” Geb akambusu akiwa amelala pale pale kitandani. “Pole nimekuamsha mama yangu. Lakini lazima tuondoke. Utalala vizuri nyumbani. Sawa eeh?” Liv alicheka tena akiwa anaonyesha wazi bado ana usingizi. Ilibidi baba yake amwamshe ili waondoke. Nanaa alikuwa akipata kifungua kinywa kwa haraka. Alimka asubuhi na kuanza kulalamika njaa. Geb akamuagizia kifungua kinywa wakati anakusanya vitu. Oliva ndio alikuwa wamwisho.

Waliondoka jijini Arusha, kurudi jijini Dar. Geb akiwa amejawa shukurani kwa Mungu wake kuwa amemrudishia familia yake. Hata hilo jaribu la shetani alilokusudia kumuangamiza nalo, wamevuka. Mungu amewashindia. Tena wanarudi nyumbani wakiwa wamejawa furaha na amani.

Kulikoungua Mpini, Kukabaki Shoka.

Walitua jijini, Mama G akiwa anawasubiria. Walipotoka tu, akamkimbilia Oliva. Alimchukua kutoka mikononi kwa baba yake, akamkumbatia kwa muda mrefu, wakamuona machozi yanamtoka. “Asante kwa kurudi Nanaa. Mungu wangu akubariki mwanangu. Nahisi ningekufa siku si nyingi kwa upweke.” Mama G aliongea huku akifuta machozi. Nanaa akajisikia kuhukumiwa zaidi. Liv alikuwa akimchekea bibi yake. “Samahani mama. Haitatokea tena. Sasa hivi ukiniudhi nitakuwa nakununia huku tunaongea.” Wakacheka na kuelekea kwenye gari. 

Geb alifika tu nyumbani, akala na kutoka kwa haraka. Alimuaga Nanaa na kumwambia hatakawia kurudi nyumbani. Baada ya kutoka tu, Nanaa akamgeukia mama G. “Sasa nafanyaje na Danny? Naona amekosa kweli raha!” Mama G akaguna. “Tuongee wakati namlisha huyu dada. Tumbo naona limeingia ndani!” “Utamlisha nini sasa?” Nanaa akauliza. “Nilisha mpikia ndizi, nikatupia hapo mboga kibao na samaki.” “Asante mama.” Nanaa akashukuru, wakaelekea jikoni. 

Mahusiano Hujengwa.

Baada ya kumuwekea Oliva chakula chake na kuanza kumlisha, mama G akaanza. “Kwanza ujue Danny yupo kwenye machungu mengi. Anajiona amempoteza Zinda. Mtu aliyemchukulia kama kaka yake wa damu. Hakutegemea kama Zinda anaweza kwenda umbali aliofika kwa ajili ya kitu ambacho anajua fika, Geb alikuwa akikupenda wewe tokea wapo sekondari. Na wote walikuwa wakijua. Lile kundi lao lote la vijana, walikuwa wakijua juu ya hisia za Geb juu yako. Sasa Danny yupo kwenye mshituko. Hakutegemea kama Zinda anaweza kutenda ukatili wote huo. Alijua angekasirika, lakini sio kwa kiwango hicho. Imekuwa ni kama mtu aliyekuwa amebeba mambo mengi moyoni. Akionyesha kuna amani, kumbe yeye ana lake moyoni.” Mama G akaendelea.

“Kingine anajilaumu na kuona aibu. Aibu kama vile ulivyosema. Yalikuwa mambo ya ndani sana, ya kwetu tu. Aliwezaje kuyatoa nje!?” “Najuta mama! Ningejua nisingesema vile. Wala sikuwa na wazo kama ni yeye ndio alikuwa akimwambia Zinda. Nimejisikia vibaya!” “Wala sio kosa lako Nanaa. Ni kweli Danny amekosea. Hakutakiwa kuongea vile. Wakati wote mimi huwa nawaambia wanangu, kuna mambo ya familia yale mazito. Hayo hayatolewi nje hata iweje. Halafu kuna mambo ya kawaida ambayo unajua hata yakizungumzwa hayataleta madhara yeyote. Hivyo hivyo kwenye ndoa. Japokuwa Grace anazungumza na mimi sana juu yake na Danny, najua kuna mambo mengine hawezi kuniambia. Ni yake na Danny tu. Na siwezi kuvuka mpaka, kumdodosa kutaka kuyajua zaidi. Kwa kuwa mimi ndiye nimemfundisha.” Nanaa akabaki akiwaza.

“Nitafanyaje mama? Sitaki hili nalo litutenganishe.” “Na hilo ndilo la msingi Nanaa mwanangu. Kosa limeshatokea. Lakini kutengana ndio litakuwa anguko kubwa sana. Alimwambia Grace ni lazima warudi kwao. Hawezi hata kumtizama tena Geb. Anasema kama isingekuwa yeye, mwezi huu mngefunga ndoa yenu. Lakini yeye ndio anakwamisha. Hataki tena kuwa karibu na watu. Grace anasema hata kuzungumza hawazungumzi. Anamuhofia anaweza kuugua kwa mawazo.” “Itabidi mimi na Geb tuzungumze naye. Sitaki tuje kutengana sababu ya chuki za nje.” “Labda hivyo itasaidia.” Waliendelea kuongea wawili hao. Wakasahau hata kama kulikuwa na tatizo kati yao. Geb aliporudi jioni, akakuta vimejaa vicheko na kutaniana. Moyoni akapumua.

Zinda Na Chuki Yake.

Katika kuhangaika kumuangamiza Geb na Nanaa, Zinda alipata wazo la kwenda kwa mama yake mkubwa Nanaa. Akiwa anaifahamu hiyo familia ndani na nje, hakupata shida ya kuwaweka mama yake James na wanae hao wawili upande wake. Pesa tu ndio ilifanya kazi. Zinda alichukua mkopo wa pesa maalumu kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kunyang’anywa Nanaa. Alikusudia kumtesa zaidi Geb aliyekuwa akimuona hakustahili utajiri wote aliokuwa ameupata kwa haraka zaidi yao.

Geb alifika nchini kutokea masomoni nchini India, wengi wa marafiki zake walishakuwa wameanza kazi. Akiwepo Zinda. Wakati Geb anahangaika mtaani akitafuta kazi na hana pesa ya kutosha, tayari kina Zinda walishakuwa na viwanja. Tena kama Zinda alishakuwa amemaliza msingi. Alishakuwa anamiliki gari kabla hata ya Geb na Danny.

Enzi Geb anahangaika na kutafuta pesa, ndio zilikuwa enzi za Zinda kula starehe bar na wanawake anaowataka. Kwa asili Zinda alizipenda pombe. Yeye ndio alikuwa akiongoza kwenye kundi lao kwa mshahara unao eleweka. Wakati huo Danny bado yupo chuo akisoma shahada yake ya pili. Na ndio wakati huo hata familia ya mama G ndio walikuwa wakiishi kwa maombi ya kufunga na kuomba ya huyo mama, huku wakiishi wote kwenye kajumba kadogo. 

Haikuwa kufumba na kufumbua kama wao walivyodhani, kwa Geb kumiliki thamani nyingi. Ilimgarimu haswa, na pia ni kweli mkono wa Mungu ulijionyesha dhahiri juu yake. Kijana huyo alijaliwa akili ya kufikiria kwa haraka. Na kwa kuwa aliachiwa ramani na baba yake juu ya maisha, Geb ambaye alijaliwa kutosahau mambo, akaanza kupambana jijini.

Mshahara wake wa kwanza alioupata kutoka hapo BOT, alihakikisha wanahama pale walipokuwa wakiishi. Mama yake alimng’ang’ania kumpa asilimia kumi ya huo mshahara wa kwanza. Kila Geb alipoingia na kutoka, mama G alidai hiyo asilimia 10. “Nimeweka agano na Mungu wangu Geb. Nataka hiyo asilimia 10 nikatoe sadaka kanisani. Lazima nitoe hiyo nadhiri.” Geb alimpa mama yake hiyo pesa. Mama G akaenda kuitoa sadaka kama alivyokuwa amemuahidi Mungu wake wakati akimuombea mwanae.

Wazo la gari halikumjia kwa kwanza. Akaamua kuwekeza kwa haraka. Kwa hiyo alianza kazi na biashara ni kama kwa wakati mmoja. Alipoanza kupata faida, ndipo akamnunulia mama yake gari. Wakati mwingine alikuwa akipelekwa kazini na mama yake, na wakati mwingine alipanda daladala. Mida ya jioni kutoka kazini, hapo ndipo alipotafuta marafiki walio karibu yake kumsogeza pengine karibu na kwao au alipanda tena daladala. Wengi walikuwa wakimshangaa. Hasa marafiki zake. Walikuwa wakimwambia huo ndio wakati wa kustarehe. Lakini haikuwa hivyo kwa Geb. Ule ndio ulikuwa wakati wa kuwekeza. Alikuwa akiweka mipango bila kuchoka. Asilimia kubwa ya mshahara wake iliingizwa kwenye biashara.

Kipindi cha mwanzoni hakupata faida. Wakati mwingine malori aliyokuwa akikodi kwenda kuchukua mazao, yaliharibika njiani na kuharibu kila kitu. Na kuishia kupata hasara kwa asilimia yote. Mshahara unapotea, na biashara inakuwa imekufa. Mzigo wa kwanza ulikuwa wa matunda. Aliyatoa Lushoto kwa nia ya kuyafikisha jijini Dar. Tena akiwa amepata soko tayari kutoka kwenye kampuni yakutengenezea juisi hapo hapo jijini. Kabla hata lori hilo halijatoka Lushoto, kukiwa na mvua kali. Likakwama mlimani. Mpaka kukauka kwa barabara na kuweza kutoa lori hilo barabarani, matunda yote yalikuwa yameoza. Geb akaingia hasara. Lakini hakukata tamaa.

Akakusanya tena pesa, akaamua kuagiza vitunguu kutokea mkoani Singida. Lori hilo ambalo alilikodi, dereva wake hakuwa amelifunika vizuri. Mvua ikanyesha tena na kuozesha vitunguu karibia vyote. Ni vichache sana alivyoweza kuuza kwenye masoko. Tena kwa wauzaji wadogo wadogo. Hakurudisha hata nusu ya pesa aliyowekeza. Mama yake alimshauri kuachana na hiyo biashara na kufikiria nyingine, lakini Geb hakukata tamaa.

Akahamisha akili kwenye tikiti maji. Safari hii alihakikisha anatuma lori huko Bagamoyo na yeye mwenyewe akaenda kusaidia upakiwaji. Alirudi nao mpaka alipohakikisha yanashushwa salama kwenye kiwanda kilichokuwa kikinunua matikiti hayo. Na baadhi kwa wateja, wauzaji wa matunda wenye masoko madogo madogo. Hapo ndipo alipoanza kuingiza pesa.

~~~~~Lockheg martl~~~~~~~~~~~

Ilikuwa mida ya jioni wakati alipompigia mama yake James simu na kutaka kuzungumza naye. Akiwa ana milioni 30 ya kwanza aliyokuwa amelipwa na Geb, mama huyo mchaga alishakuwa amerudi Dar na harakati za kuwekeza pesa hiyo ulishaanza. Hakutaka kubadilisha maisha yake na wanae kwa haraka. Akachukua chumba. Akawa anaishi hapo yeye na watoto wake wakike wawili na mjukuu. Aliondoka nyumbani akiwa amegombana kabisa na baba James. Alimlaumu kuendelea kuzunguka na mabinti hao bila kuwaongoza kwenye kujitegemea.

Bado binti hao wakubwa walikuwa wakitegemea kupewa kila kitu mpaka sabuni zao za kuogea. Angalau Viola alikuwa akipokea pesa kiasi kwa ajili ya mtoto wake kutoka kwa mzazi mwenzake, Alex. Lakini Vai yeye alitaka kupewa mpaka pesa ya wanja na lipstik. Aliamka muda anaotaka na alilala usiku mwingi sababu ya kuangalia tv. Walipotoka nyumbani kwa James wakiwa wamekimbia mahari ya Nanaa na kurudi nyumbani kwao mjini Moshi, baba yao aliumia sana alipouliza kama waliweza hata kusoma kozi fupi tu za kuongeza elimu na kupata jibu la hapana. Si Viola wala mdogo wake hata walioongeza ujuzi wowote. Walirudi warembo na kiswahili cha jijini tu.

~~~~~~~~~~~~~~~

Alipoelekezwa wanapoishi hapo jijini, Zinda hakutaka kuchezea bahati. Alinunua kuku wawili wa kuchoma, ndizi na chips. Soda kreti zima akabeba na chupa za bia kwa kuwa alijua mama yake James ni mnywaji. Alipokelewa kwa heshima sana. Wakaanza kula na kunywa. Alipoeleza tu shida yake, hapo ndipo alipojua atafanikiwa. Akaanza kupewa mawazo ya nini cha kufanya kuhakikisha anamuangaiza kabisa Nanaa. Yeye akiwa na nia ya kumkomoa tu Geb, akakutana na mahasimu wa Nanaa.

Zinda alipewa njia nyingi sana. Akapewa madhaifu mengi sana ya Nanaa. Huku akimwagiwa yeye sifa kuwa ni mwanaume mzuri. Akaambiwa Nanaa hajatulia au hawezi kutulia na mwanaume mmoja ndio maana ameshindwa kukubali kujifunga kwake tu. Akaambiwa huwa anakimbilia wanaume wenye pesa, ndio maana huwa haoni wanaume wazuri kama yeye Zinda. Akapewa faraja ambayo hakutarajia. Mvua za sifa zikamlowesha Zinda. Alisifiwa kwa kupokezana. Kuanzia uzuri wake wa nje mpaka roho yake. Bia zilizokuwa zimeshaingia ndani yake kabla hajafika hapo, zilimsaidia kufurahia sifa hizo. Matumaini ya kufanikisha lengo lake la kumkomoa Geb na Nanaa, iliongezwa mara dufu. Alitoka hapo ndani, Zinda akiwa na tumaini jipya. Aliagwa kama mfalme na shukurani kede kede kutoka kwa mama James na wanae.

Ugomvi ukaanza mara tu baada ya kurudi ndani baada ya kumsindikiza na kugundua Zinda ana usafiri. Aliacha gari nje. Tena sio gari mbaya. Ni gari ya kawaida tu, yakueleweka. Na alishasema anamalizia kujenga nyumba nzuri sana na yakifahari ambayo hiyo ndio alitaka ahamie na Nanaa. Viola na Vai wakaanza kutukanana mwishowe ngumi zikaanza. Kila mmoja wao akawa anamtaka Zinda. Wakajaza watu kwa kupigana mpaka kuvuana nguo hapo chumbani kwao. Huku mama yao akishindwa kuingilia kabisa.

Vichaa, Wamepewa Rungu.

Mashindano yakaanza. Zinda akaanza kuthaminiwa kama mfamle. Akifika hapo, walishindana kumtayarishia na kumuhudumia kwa maneno mazuri. Kila mmoja alijitahidi kwa nafasi yake. Zinda akiwa amefika hapo kuzungumza na mama yao na kuhakikisha wapo ukurasa mmoja, lakini akajikuta hali ya uanaume aliyoona Nanaa ameipuuza, warembo hao wawili wameitambua. Hakuna jinsi ungemwambia Zinda asirudi kwenye hiyo nyumba akakubali. Aliagwa huku akibembelezwa arudi tena kesho yake. “Kwanza unaishi peke yako. Sitaki ulale njaa bwana. Ukitoka kazini njoo ule ndipo ukalale.” Hayo ni maneno ya Vai asiyejua hata kupika uji, akiwa amesimama dirishani mwa gari la Zinda akiwa anamuaga. Viola alipitwa. Alimpeleka mtoto wake chooni.

Safari za hapo zikaanza kuwa nyingi. Kila akitoka kazini, basi alipita nyumbani kwa mama James na binti zake. Wakati mwingine hakuwa akimkuta mama yao sababu ya kuhangaika kutafuta jinsi ya kuwekeza mjini. Mama huyo muhangaikaji aliyetoka kwake na kumuacha mumewe kwa kishindo huku akimtambia atamsikia kwenye vyombo vya habari tu, akiwa amefanikiwa sana. Na kweli hakutaka mchezo. Alihangaika kwa kadiri ya uwezo wake kuwekeza pesa aliyolipwa na Geb.

Zinda naye akalipa tena mahari ya Nanaa kwa pesa tu. Maana mama huyo alimwambia akitaka amsaidie, alipe na yeye hiyo mahari. Bila kipingamizi, huku ikifahamika wazi kuwa mahari za Kichaga huwa hazimalizwi, lakini mama James alitaka alipwe pesa yote, na Zinda naye akamlipa pesa yote. Na Zinda ndiye aliyempa wazo mama James la kumdai  tena Geb pesa. Alimwakikishia kuwa Geb anapesa sana. Kwa kulipwa tu milioni 30 ni kama kujidhalilisha. Zinda alimsifia yule mama kwa malezi ya Nanaa huku akimuonyesha kumuhurumia kwa kazi ngumu. Akamtia moyo, wakakubaliana kwenda kusimamisha hiyo harusi ya Geb na Nanaa. Ndipo usemi wa ‘umoja ni nguvu’, ulipotimia siku ile kanisani. Wakafanikisha nia zao. Mama James akapata pesa, Zinda yeye akafurahia kusimamishwa kwa harusi.

~~~~~~~~~~~~~~~

Akiwa na pesa yakueleweka, Mama huyo wa kichaga anayeifahamu pesa na akili ya kuzalisha, akaanza kusugua kichwa. Nyumbani akawa hapatikani sana. Binti hao wawili waliozoea kuhudumiwa na hawawezi kazi, hawakutaka kuhangaika na mama yao. Wao walikuwa wakibaki tu nyumbani. Kwa hiyo mara nyingi Zinda akajikuta anabaki nao hapo nyumbani.

Viola mwenye mtoto au jukumu la mtoto, mara nyingi mtoto alimfanya akose nafasi ya kumganda Zinda ipasavyo. Hapo ndipo Viola alipomjutia yule mtoto. Chuki kwa mwanae pia ikaanza. Aliona anamzuia kwenye mambo yake. Alianza kumpiga bila kosa. Hakuruhusiwa kumwita mama yake pale Zinda anapoingia mle ndani ili na yeye apate muda na Zinda.

Mama James alipata eneo ambalo kwa akili yake ya haraka akajua akipakarabati hapo, anaweza kufungua baa. Ilikuwa ni nyumba ya mzee ambaye alifariki akaachia watoto wake waliokuwa wakipigania hiyo nyuma. Alipokuja mama James akitaka kupakarabati na kupakodisha, wakamkubalia. Mama James mchapa kazi. Anaamka asubuhi kuelekea huko Msimbazi Centre kwenye ujenzi wa baa yake, kurudi usiku sana amechoka. Hajui linaloendelea kwa mjukuu wake wala bintize.

Siku hiyo Zinda akiwa ndio ameingia tu pale, ndio Viola naye alikuwa ametoka kumchapa sana mtoto wake, alikuwa akilia. Vai akamdaka Zinda na kumuomba watoke pale kwa sababu ya kelele. Zinda hakukataa. Akaona ni kweli Viola anahitaji muda wa kumtuliza mwanae. Walipoingia tu kwenye gari, Vai hakuchelewa. Akamshauri warudi nyumbani kwake, apike yeye, wale. Zinda hakubisha. Hata yeye aliona ndio utakuwa mwanya wa kumpata Vai kimapenzi, kitu alichokuwa akikitamani tokea Vai alipokuwa akijitongozesha.  

Vai Nyumbani Kwa Zinda.

Alipoingia tu ndani, uvuaji wa viatu wa Vai ulimfanya Zinda aliyekuwa nyuma yake ashindwe hata kusogea. Hali yake ikaharibika kabisa. Vai alikuwa amevaa sketi ya kuchanua fupi. Ndani alikuwa na chupi yenye mikanda kila mahali. Alipoinama vile, mabaja yote yalikuwa wazi mbele ya macho ya Zinda. Aliendelea kuvua viatu hivyo kichokozi mpaka akahakikisha Zinda anaona kila kitu.

Akiwa amejawa uchu, Zinda hakupoteza muda. Badala ya kumuonyesha jikoni kama Vai alivyokuwa akisisitiza njiani akiwa amekaa pembeni yake na nusu ya mapaja yake nje akijaribu kuyafunika ili kuhakikisha Zinda anayaona, Zinda alimwingiza chumbani. Vai mtoto wa mahaba. Aliyejua wanaume tokea utoto, hakufanya mchezo mdogo. Alihakikisha anampagawisha Zinda kiasi cha kumuacha hajielewi.

Akajituma vilivyo bila kuchoka huku akimgeuza kulia na kushoto bila kujali hisia zake mwenyewe, ila Zinda. Nyumba hiyo ndogo yakupanga ambayo haikuwa na kiyoyonzi, au AC siku hiyo Zinda alitamani ingekuwa tofauti. Vai alimtoa jasho kwa purukushani hapo kitandani, akaishia kuhema na hushukuru kama mpumbavu. Vai alimuamulia siku hiyo ili kumdhibiti asimfikie tena Nanaa wala Viola.

          Zinda alipoona mchezo umekolea, akamtumia ujumbe kijana wake aliyozoea kumtuma hapo mtaani, alete chips kuku na bia. Vai hakuwa mnywaji hata kidogo. Akaletewa soda. Wakala. Zinda akaona usiku umeingia akaamua kumrudisha Vai nyumbani kwao. Vai akiwa amekusudia kulala, hakubisha. Akaingia kuoga, akatoka akiwa anajikausha. Mtoto wa kike kama alivyozaliwa. Akaanza fujo pale chumbani. Zinda akiwa ameshalewa, akajiambia amfurahie binti huyo tena kidogo, kisha atamrudisha baada ya hapo. 

Alikuja kuamshwa na alam ya kumtaka ajiandae kwenda kazini. Kwa purukushani nyingi za usiku uliopita, Zinda aliamka kichwa kizito, mbio bafuni kuwahi kibaruani. Alimuaga Vai akimuahidi kuwasiliana baadaye. Na akamwambia akiwa tayari kuondoka kurudi kwao, amtaarifu ili amuelekeze wapi pakuacha funguo za nyumba yake.

Mpaka anatoka jioni, hakuwa amepata simu yeyote ile kutoka kwa Vai na wala Vai hakuwa akipatikanika. Akaamua kuanzia nyumbani kwake. Akamkuta Vai ametulia tuli kochini. “Mbona sikupati kwa simu!” Zinda akahoji akiwa haelewi kinachoendelea. “Simu iliishiwa chaji tokea jana. Nimeshindwa kuondoka kwa kuwa sijui jinsi ya kufunga mlango.” Vai alijibu na kusimama. Binti huyu aliyefahamika hana nidhamu, kumbe alijua kujituma.

          Akasimama kumpokea Zinda. Alimpa busu la kutulia, lakini mkono ulishakuwa umefika kwenye zipu ya suruali. Tayari akili za Zinda zikaanza kuvurugika. Akaona achangamkie kwa haraka kabla hajamrudisha kwao. Mabusu yale yakawapeleka kitandani, Zinda akihema hovyo anadai angalau roundi moja ndipo waondoke. Walipotua tu kitandani akiwa amepagawa, Vai akasimama. “Naona unirudishe tu nyumbani. Tusije chelewa kama jana.” Aliongea kwa heshima zote huku akijiweka sawa na kuashiria utayari wa kuondoka. “Naomba usiniache hivi Vai! Tafadhali sana.” “Unaonekana wewe mwenyewe hufurahii kulala na mimi Zinda.” Vai akajilalamisha.

“Hapana Vai! Mbona mimi nafurahia sana tu. Ila.” “Ila sifanani na Nanaa?” Vai akamkatisha maneno. “No no noooo. Namaanisha ila sikutaka kukutia matatizoni kwa mama. Nimefurahia sana kuwa na wewe Vai. Sijawahi kupata usiku mtulivu kama wa jana. Nimelala kama mtoto mchanga!” Vai akacheka kwa huba. “Hata mimi sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume kama wewe Zinda. Ujue jana umeniliza wewe!” Sifa zikaanza. “Sijawahi kulala na mwanaume mwenye maumbile kama yako Zinda. Yaani ukinishika nasikia kama kuchanganyikiwa. Ukiingia humo ndani, ndio kabisa, sijiwezi. Lakini naogopa kunogewa halafu ukakumbuka penzi lako kwa Nanaa. Ukaniacha nateseka.” Vai aliendelea kumtesa Zinda aliyekuwa yupo juu zaidi ya mlima Kilimanjaro.

Hapo Vai anaongea huku titi moja lipo nje. Tena titi ambalo halijawahi kunyonyesha mtoto hata mmoja. Weupe wa Vai kama wa kaka yake James, wamechukua kwa mama yao. Macho ya Zinda yalikuwa yakiangalia chuchu iliyokuwa ikikaribia rangi ya pinki kama ya mtoto wa kizungu. Mungu ampe nini tena? Aliyokuwa akiyaona kwenye tv, leo yapo ndani ya chumba chake cha kulala! Zinda akabaki akiangalia lile titi.

“Mimi naona niondoke tu Zinda.” Kosa akarudisha lile titi ndani ya shati lililokuwa na vifungo mbele. “Tafadhali Vai. Naomba usinitese. Nanaa hayupo hapa. Kwanza nataka nini kwa Nanaa ambacho wewe utaninyima! Eti Vai? Au kuna unachotaka kuninyima?” “Hapana Zinda. Ila sitaki ujute.” Zinda akasimama kwa haraka akaenda kumshika mikono yote miwili. “Nakutaka wewe Vai.” “Sasa nikirudi hapo kitandani halafu ukanichanganya? Wewe mwenyewe unajijua jinsi ulivyomtamu Zinda. Ukianza huwa sitaki kumaliza. Nataka tuendelee tu. Na wewe unaonekana ni kama hupo huru na mimi.” “Mimi nipo huru. Nilikuwa namuhofia mama tu. Lakini kama unasema mama hana neno, basi naomba tubaki wote. Tafadhali Vai.” Vai akajifanya anafikiria kidogo.

          Akajua juhudi zake za jana zimezaa matunda. Akamsogelea karibu kabisa na sauti akaishusha. “Unauhakika?” Akamuuliza na kupiga magoti mbele yake. Akamalizia kumtoa ile suruali na kuanza kumchezea akiwa amepiga magoti vile vile. Alipoona Zinda analalamika zaidi, akasimama. “Nimekuuliza kama una uhakika Zinda. Sio tena unatoka hapa unaniacha nateseka mwenzio.” Zinda alitamani kulia. Alikuwa anakaribia kupata goli la ushindi palepale alipokuwa amesimama.

Hapakuwa na kiapo alitakiwa atoe wakati ule akashindwa. Hakuna neno alilotaka kulisikia Vai kwa muda ule asilitamke. Ilimradi tu Vai amnusuru. Vai alimuachia akaenda kujirusha kitandani. Mapaja yote yalikuwa nje. Zinda aliendelea kuteseka pale alipokuwa amesimama. Macho mapajani, hana nguo. “Naweza kukupa muda wa kufikiria. Mimi nitakuwepo tu nyumbani Zinda. Utanifuata wakati wowote utakapokuwa tayari.” “Mimi nipo tayari. Nakutaka wewe Vai. Sidhani kama kuna mwanamke yeyote hapa duniani anaweza kunipa unayonipa. Nakufurahia sana. Natamani usiondoke hapa.” Zinda akajitia kitanzi yeye mwenyewe huku akimfuata kitandani akiwa amevaa shati tu.

“Kweli Zinda?” “Nakuapia Vai. Natamani usiondoke. Nataka leo tupate usiku kama wa jana.” “Hata mimi Zinda. Napenda hivyo unavyonikamata kwa nguvu wakati tunafanya mapenzi. Naridhika. Natamani uwe wangu wa milele.” Tayari mkono wa Zinda ukatua mapajani. “Hivi kinachotuzuia ni nini Vai? Eti mpenzi?” “Kweli upo tayari kuwa na mimi?” Vai akaanza tena utundu wake. Alihakikisha anawasha taa, nakumvamia Zinda pale kitandani. Alimlaza chali. Akamkalia juu. Macho ya Zinda yalikuwa yakitazama mwili uliokuwa ukiwaka kama alumasi. Vai alijinyanyua juu na chini. Kata dakika tano hazikupita, Zinda akakata kiu yake. Vai hakufanya haraka kujitoa pale kwa Zinda. Akabaki amemwinamia huku akimbusu midomo, shingoni na masikioni.

“Kweli Zinda wewe mwanaume. Sijapata ona. Duuuh! Yaani bila kuhangaika umenifikisha na mimi! Nakushukuru sana. Asante mpenzi. Nakushukuru sana.” Vai hakuwa hata amesikia chochote kile wakati anafanya mapenzi. Lakini alimuongopea tu ili kumfurahisha. “Daah! Nahisi Mungu amenifuta machozi. Sikutegemea kupata mwanamke kumzidi Nanaa. Hakika umeniweza Vai.” Zinda alishanogewa vyakupitiliza. “Tafadhali lala na mimi leo. Tumjulishe tu mama kuwa uko kwangu.” “Sawa.” Vai akakubali kwa haraka sana.

~~~~~~~~~~~~~~~

Hapo walishakuwa wamesimamisha ndoa ya Geb na Nanaa. Kazi ya Zinda ikabaki kujipongeza tu. Mungu amemfuta machozi. Akaletewa kimwana kama Nanaa, ndani ya nyumba. Kwa rangi watoto wa mama James na Nanaa hawakutofautiana kabisa. Wote walichukua weupe wa bibi yao. Hata mama mkubwa alikuwa mweupe sana. Maumbile tu ndio walipishana na Nanaa. Lakini hata wao walikuwa na maumbile mazuri ya kike, yakumvutia mwanaume yeyote yule. Viola na Vai hawakuwa na vitu vilivyozidi sana mwilini mwao kama Nanaa, lakini wachaga hawa, walikuwa wa namna yao. Usingechoka kuangalia. Kama ulifika nchini ukaambiwa wachaga wana sura au umbile baya, basi ukikutana na ndugu hao, utajua umedanganywa tu. Binti hao wote waliokuwa wamelelewa nyumba moja, walijuana madhaifu yao na uzuri wao. Kwa hiyo haikusumbua kuangamizana.

Vai alitumia kipindi hicho vizuri sana kumliwaza Zinda aliyekuwa akilalamika kusalitiwa na rafikize. Vai akageuka kuwa BFF wa Zinda. Akatulizwa kimya nyumbani kwake. Kazini, nyumbani kwa Vai. Wakati wote alipewa penzi la nguvu. Alikuta nyumba safi. Nguo zimefuliwa na chakula kipo mezani, Vai kochini akimsubiria. Na salamu ya Vai ilimfanya Zinda kuwahi kurudi nyumbani. Alihakikisha anarudi nyumbani peke yake bila rafiki. Na akiingia tu anafunga mlango kwa nyuma tena kwa haraka, kwani Vai alikuwa akimvulia suruali mlangoni. Mpaka Zinda anaenda kukaa kwenye kochi, na kuulizwa habari za kazini, basi ameshajishindia bao moja la bila kutoa jasho.

           Vai alikuwa akimwambia hiyo ndio ilikuwa pole yake ya shuguli za siku nzima. Alimtaka asimame tu. Yeye anampa pole ya kazi bila kujigusa. Basi hapo ndipo Vai alipomliza mtoto huyo wa kiume, nakujikuta hajiwezi mbele ya Vai. Ni muda aliokuwa akiutamani ufike, arudi nyumbani apate ukaribisho huo ambao Vai aliutendea haki.

Zinda alijitenga na kila mtu ambaye alijua angemtaka siku za weekend wakutane au amjibu jumbe yeyote. Kwenye makundi ya whatsapp akawa hasikiki tena. Bia anazikuta kwenye friji yake nyumbani. Hapakuwa na sababu yakumtoa Zinda nyumbani kwake tena. Huwezi kumkuta Zinda na simu akiwa na Vai. Vai alijua kumtawala na kuziteka fikra zake ipasavyo. Wanawake aliokuwa akiwalipa baa ili afanye nao mapenzi, hakuwalinganisha na Vai. Vai yupo nyumbani. Anamlilia mapenzi! Anapewa penzi muda na wakati wowote ule. Hata wakati mwingine anaamshwa na mabusu mwilini. Vai anakuwa yupo tayari akimlilia kuwa ameshindwa kulala, mpaka amtulize. Utamwambia nini Zinda?

Kwa Kina Nanaa.

            Huku kwa Nanaa na Geb, walishakubali kushindwa. Wakaendelea kuishi bila ndoa. Nanaa na Geb wakajitahidi kurudisha amani kati yao. Walimtafuta Danny yeye peke yake wakapata muda wa mazungumzo naye. Walijaribu kumfariji na kumuhakikishia yeye sio sababu ya yote. Adui yao ni shetani. Geb akamwambia Danny, wakikubali kutengana hapo ndipo kutakuwa kushindwa kwao. Walimpa maneno mengii ya kumfariji Danny mpaka akaanza kurudisha ujasiri.

Furaha ikaanza kurejea kati yao. Lakini Grace na familia yake hawakurudi tena kuishi pale. Ikawa kazi ya Nanaa na Liv kwenda nyumbani kwa Grace. Geb na mama G wanapokuwa wakiaga kwenda kazini, Nanaa na yeye anajifungasha na mwanae, nakuhamia kulala kwenye makochi ya nyumbani kwa Grace. Kuanzia asubuhi anapofika hapo mpaka jioni. Mama G hakuwa akikaa kazini siku nzima. Kwa hiyo alifanya kazi nusu siku. Tena inapolazimu na kumfuata Nanaa nyumbani kwa Grace.

Grace alishapata mfanyakazi aliyekuwa akimsaidia swala la watoto. Jeri, dereva wa muda mrefu sana wa Geb, ndiye aliyekuwa dereva wa Nanaa na Liv, na ndiye aliyemtafutia Grace msichana wa kazi. Alikuwa binti mzuri, mwaminifu na mchapa kazi kama Jeri. Aliwapenda hao watoto na kuwahudumia bila kuchoka. Kwa hiyo muda mwingi Grace alijikuta wakipata muda na Nanaa. Grace akimsaidia kumlea Liv. Kwani Nanaa alikuwa akilala kupita kiasi. Wakajua mimba ya Nanaa imempenda Grace.

Akiamka tu asubuhi, anambeba mwanae hivyo hivyo na nguo zake za kulalia, anahamia kwenye kochi nyumbani kwa Grace au kwenye chumba alichopewa hapo nyumbani  Grace. Atalala hapo siku nzima, huku Grace akifanya kazi zake hapo pembeni yake, hapo hapo nyumbani. Ni kama Grace alihamisha ofisi yake nyumbani. Basi Nanaa atalala hapo mpaka muda anaojua Geb anakaribia kurudi nyumbani. Wakati mwingine alipika chakula cha nyumbani kwake hapo hapo kwa Grace na kukibeba, au alimtaka Geb apitie hapo nyumbani kwa Grace ale ndipo warudi kwao. Ukimtaka Nanaa, muulize Grace.

“Huyu atakuwa na mimba ya mtoto wa kike. Naona umenipokonya mapenzi yangu.” Grace akamcheka mama yake. “Mimi naona anataka kuiona tu hii sura. Unafikiri hata akifika hapa ananiongelesha sana? Hata Danny amchokoze vipi, atacheka kidogo tu, baada ya muda mtamsikia anakoroma hapo hapo pembeni ya Danny.” Wakacheka. “Nasikia sana mnavyonisema!” Nanaa alitoka usingizini akasikia Grace na mama yake wakimsengenya jikoni. 

“Turudi nyumbani Nanaa! Ni nini unapendea hapa?” “Wewe mwenyewe hutabiriki bwana mama. Mara uniambie unaenda kazini mara moja unarudi, halafu sikuoni tena sijui mpaka masaa mangapi! Na mimi sitaki kukaa pale peke yangu. Liv anataka tucheze wakati mimi nina usingizi. Naona heri aje hapa achangamshwe na kina Fellius, wakati mimi nalala. Grace akila ugali, amlishe wakati mimi nalala.” Nanaa akakaa. “Tumbo hilo limeshaanza kuwa kubwa zaidi yako. Si ukubali tukaangalie jinsia ya mtoto?” “Bwana mama! Acha kuwa kama Geb. Mbona hamna subira? Eti Grace?” “Mimi ndio huwa siwezi kusubiri kabisaa. Naanza kuulizia jinsia pale tu nikijijua ni mjamzito.” “We Grace!” “Ili nijue nilichobeba na kujiandaa.” Grace aliongeza. “Bwana mimi sitaki. Nyinyi subirini mtoto mwingine anakuja.” “Mmmh! Kazi ipo.” Mama G akaongeza huku akimtolea matango aliyokuwa amemtayarishia. Nanaa akakaa.

“Mmempikia Geb wangu?” Nanaa akauliza huku akitafuna tango. “Ujue umenyimwa aibu Nanaa wewe?” Mama G akamfanya Nanaa acheke. “Pika mwenyewe.” “Mimi na wewe mama yangu? Najua utakuwa umenisitiri tu. Geb hawezi kutoka kazini asikute chakula.” Nanaa akaongea huku anacheka. “Sasa leo atakula wali na mchuzi wa nyama.” “Hapo ndipo kuachika. Haya naomba mnipishe hapo nianze kuchangamka. Akija hapa akute chakula.” “Si ukapikie kwako Nanaa? Ni nini kung’ang’ania kwenye majumba ya watu!” “Mama naye kunifukuzia mgeni! Wewe mwache.” Grace akalalamika. “Wala sio mgeni. Na kesho tena nitarudi mwaya Grace. Haya twende mama kabla sijalala tena.” Wakacheka na kutoka.

 ~~~~~~~~~~~~~~~

Ilishakuwa miezi minne imepita tokea Zinda asimamishe harusi ya Geb na Nanaa. Maisha kwa kila mmoja yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Hakuna aliyezungumzia swala la harusi kati ya Geb na Nanaa. Nanaa ndio hakuwa tena na habari. Kazi yake kulala  na kula kuhu analea mimba. Oliva alishaanza kushika mahali na kutembea.

Mama yake James baa yake ikaanza kuchanganya kwa pesa alizokuwa amelipwa na Geb. Alifungua baa ambayo iliuzwa vinywaji vya kila namna, pamoja na chakula. Mama huyo alikuwa na shuguli kuliko maelezo. Alidamkia baani kwake kuhakikisha kunakuwa na kifungua kinywa kizuri wateja wasimkimbie. Na kwa kuwa alikuwa mzungumzaji, na bei yake haikuwa juu, alikuwa na wateja wengi. Baa yake ilikuwa ikijaa kuanzia asubuhi mpaka usiku. Utani na sifa kibao kwa wateja wake. Wote walimtaka wamkute pale baani. 

Aliifanya hiyo kazi kwa bidii zote kumuhakikishia mumewe na James, kuwa hata yeye anayaweza maisha. Na Nanaa mbaye ndio mkosi wake, ameshamkata kwenye ukoo wake ndio maana anafanikiwa. Ukweli kwa muda mfupi sana mama James alikuwa na pesa.

 ~~~~~~~~~~~~~~~

Vai nae ni kama alihama kabisa nyumbani kwao wakajua anaishi kwa Zinda. Kilichokuwa kikimshangaza Viola na mama yake, ni wanaishije au Vai anafanyaje. Kwa kuwa Zinda alikuwa akimsifia swala la usafi na chakula kizuri. Vai anafahamika kuwa hajui kupika wala hawezi kujituma kufanya chochote.

Maisha yakaendelea. Vai na Zinda. Furaha na mapenzi mazito huku Vai akiomba Mungu afanye muujiza, ashike mimba amzalie mtoto Zinda ili amuombe wafunge ndoa awe wake kihalali ili asije kurudi tena kuishi na mama yake, Viola na mwanae. Wivu ulikuwa ukimsumbua sana Viola. Kwanza aliona Vai ni kama amemuibia mwanaume wake kwani yeye ndio alimuwahi Zinda tokea siku ya kwanza wakipigana. Alimwambia mama yake na Vai kuwa atahakikisha Zinda anamuoa yeye. Lakini Vai akamwambia na yeye ameshamuwahi Zinda kuwa atakuwa wake. Ngumi zikapigwa, na ndipo Vai akamuharibia kwa Zinda kwa kumwambia tayari Viola anamtoto, na alizaa na mwanaume wa wizi. Akajitahidi kumchafua kwa kadiri ya uwezo wake mpaka akamzidi mahesabu dada yake, yeye akaibuka mshindi.

Kila alipokuwa akienda kutembelea nyumbani kwao, Vai alifika akiwa nadhifu. Tena alikwenda na Zinda wakiwa wanaendesha gari ya Zinda. Vai alijitahidi kila akienda hapo nyumbani ana nguo mpya na pochi. Maringo kwa dada yake yakaongezeka. Na alihakikisha Viola hapati hata dakika moja peke yake na Zinda. Alimfahamu dada yake. Kila Viola alipotaka akaribishwe nyumbani kwa Zinda na wao wakawatembelee, Vai alidakia kwa haraka, kuwa atatafuta siku na kuja kuwachukua. Wawe wavumilivu.  Hayo yalikuwa majibu yake akiwepo Zinda. Lakini alipokuwa akimtanguliza Zinda kwenye gari, yeye akibaki nyuma, alihakikisha anampiga mkwara dada yake kuwa hamtaki nyumbani kwa Zinda. Nia yake ilikuwa ni mpaka ashike yeye mimba ndipo amkaribishe Viola aliyekuwa akitumia kubeba mimba kama silaha ya kumpata mwanaume yeyote anayemtaka yeye. Hata kama ni shemeji yake. Vai alishamshuhudia akitoa mimba nyingi tu alizokuwa akiwabebea makusudi wanaume ili wasimkimbie. Alipokuwa akiachwa na mimba zake, alizitoa. Ni mtoto wa Alex tu ndiye aliyemtunza kwa kuwa Alex alikuwa akituma pesa na alimuahidi angemuoa.

Ukweli maisha ya Zinda yalibadilika. Alikuwa kwenye mahusiano mazuri na matulivu. Vai alituliza mawazo, mambo ya kitoto akaweka pembeni. Akakusudia kushika mimba atulie na Zinda aliyekuwa na muelekeo. Zinda alikuwa akimalizia nyumba yake ili ahamie. Vai alishakusudia yeye ndio atakuwa mama mwenye hiyo nyuma. Mvua inyeshe, jua litoke, yeye ndiye ataishi hapo na Zinda.  

Historia Ya Vai.

Miezi minne ilishapita tokea Vai aanze kuishi na Zinda. Mapenzi ya mchana na usiku lakini hakuwahi kushika mimba hata mara moja. Wasiwasi ukamwingia Vai. Akakumbuka mimba alizokuwa na yeye akitoa tokea yupo shuleni sekondari. Nyingine hata mama yake hakuwa akijua. Alipokuwa kidato cha pili, alitoa mimba mbili. Akiwa anaishi hapo hapo nyumbani, na mama yake hakujua. Mimba ya mwisho ndio alikaribia kufa. Kwani alimtoa mtoto ambaye tayari alishakuwa ameanza kucheza. Ilikuwa mimba kubwa kabisa.

Vai aliugua na kulazwa kwa muda mrefu. Wakiwa wamehamia hapo jijini, Vai alipata mme wa mtu. Kwa kuwa alikuwa na gari na alikuwa akimpa pesa, akaamua kufanya kama dada yake. Akambebea mimba ili amuweke awe hata nyumba ndogo ili kuendeleza starehe na mgao wa pesa uongezeke. Alikuwa akimpeleka kwenye mahoteli ya garama na kumnunulia vitu vya garama.

Lakini ikawa kinyume kabisa na matarajio yake. Alipomwambia ni mjamzito, yule baba hakuonyesha kushituka. Akaendelea kukutana naye kwa siri, lakini haikuwa kama zamani. Mimba ilipofikisha miezi mitano kwenda 6, kukiwa kumeshaanza ugumu wa mawasiliano kati yao, yule baba akamwambia Vai ameamua kusitisha mahusiano. Na amemwambia mkewe, mkewe amemsamehe. Ameamua kutulia kwenye ndoa yake. Akampiga marufuku asimtafute tena, iwe mwisho.

Vai hakupoteza muda, akaenda kutoa mtoto mkubwa kabisa. Alirudi nyumbani kimya kimya bila kumwambia mtu yeyote kile alichokifanya. Siku zilidi kwenda, huku akiteseka kwa maumivu makali ya tumbo. Harufu ya kama kitu kilichooza ilipoanza kusumbua kwenye chumba hicho walichokuwa wakilala na mama yao, ndipo ikajulikana alitoa mimba. Vai alikuwa na homa kali sana. Mama yake alimkimbiza hospitalini.

Vai alimweleza daktari waliyemkuta kuwa alikuwa mjamzito, lakini mimba ilitoka. Mama yake na Viola walijua ni uongo. Ni kwamba alimtoa mtoto. Tena vichochoroni ambako hakupewa huduma ya kueleweka. Ilibidi kusafishwa kizazi na kutibiwa kwa majuma kadhaa akiwa alishapoteza damu nyingi na infection ya kizazi.

Alipotoka hapo, Vai alitulia kabisa mpaka alipokuja tena Zinda, akaamua kutulia na Zinda. Alishaonjeshwa kifo. Alishatapeliwa na wanaume, basi akakusudia kuwa Zinda ndio atakuwa wakuzikana. Alikuwa akimtetemekea huku akijipongeza kwa kufutwa machozi. Akajiapia kutulia kabisaaa.

Kwanza anatafuta nini? Hajasoma na hana kazi. Lakini Zinda anamtunza vilivyo. Ahadi zote kwa Nanaa, Zinda akazitimiza kwa Vai. Mungu ampe nini tena? Hata ungekuwa na nini, kama ungekutana na Vai wa safari hii, hata ungemtongoza asingekubali. Katulizwa na Zinda. Anapewa kila atakacho kwa kadiri ya uwezo wa Zinda. Na Zinda hakuwa akimgasi kwa shule wala kazi. Hakumtaka arudi shuleni wala atafute kazi. Alishamwambia mshahara wake utawatosha. Basi, maisha yakaendelea.

Zinda.

Zinda mtoto wa kiume mkubwa kwenye familia yao. Ndiye anayetegemewa kwao kwa mambo mengi sana japo bado baba yake anajishugulisha kwa biashara ndogo ndogo. Danny aliongezeka kwenye familia hiyo. Akawa msaada mkubwa sana. Alikuwa akituma pesa bila kumtaarifu hata Zinda mwenyewe. Wadogo zake Zinda au wazazi wa Zinda walipokuwa na shida, hawakusita kumpigia simu Danny na kumuomba msaada. Lakini baada ya kujihesabu amesalitiwa na Danny kwa kumuunga mkono Geb kumchukua Nanaa, aliwapiga marufuku ndugu zake wote wasiwahi kuwasiliana tena na Danny.

Hata wazazi wake aliwaambia mabaya mengi sana yaliyowaumiza juu ya Danny. Alihakikisha amejenga uadui kati yao. Wazazi wa Zinda hawakumtaka tena Danny. Si kwamba Danny mtoto yatima alipoteza tu kaka ambaye ni Zinda, alipoteza na wazazi wa pekee aliojichagulia ukubwani. Aliwapenda wazazi hao kama wake. Akisikia hata mmoja wao ni mgonjwa, basi Danny atawasha gari na kukimbilia Tabora kuwaona.

Maombi ya mama yake Zinda ni aoe na apate watoto wa kurithi. Mke wa Zinda alisubiriwa kwa hamu sana na familia nzima. Mama yake alishampa majina ya wasichana wengi tu wa pale pale kijijini kwao, lakini Zinda aliwakataa. Akampa baraka zote, alete atakayempenda yeye, ilimradi aoe.

Swala la kwamba kama Vai ataweza kuishi na ndugu zake likaanza kuwa mtihani. Nia ya Zinda ni kuhamishia baadhi ya ndugu zake pale jijini ili kuwasaidia. Wanaoweza kwenda shule waende na wanaoweza kufanya biashara wafanye. Lakini wasihangaike mahali pakuishi. Yeye ndio awasaidie malazi. Na ndio maana alijenga nyumba kubwa iliyokuwa ikimtoa mate Vai, japo haikuwa ya kisasa sana, ila Zinda alijua itamtoshea yeye na nduguze.

Hamu ya mtoto ilikuwa ikimsumbua Zinda. Kelele za kulinganishwa na rafiki zake hasa Danny ambaye tayari ana watoto watatu, zilizidi kumtesa Zinda. Kila mara mama yake alimtolea mfano kwa mwenzie Danny. Akamwambia anachelewa kuanzisha familia. Na ni kweli umri ulikuwa ukikimbia. Zinda alijiona mtu mzima. Habari ya kuambiwa na Vai kuwa ameshika mimba, aliisubiria kwa hamu sana bila mafanikio. Walikuwa wakikaribia kumaliza mwezi wa tano tokea Vai aanze kuishi nae hapo.

~~~~~~~~~~~~~~~

Alijitahidi asionyeshe huo wasiwasi, lakini uzalendo ukamshinda. “Hivi unatumia njia yeyote ya uzazi wa mpango?” Zinda alirusha swali siku hiyo ya jumamosi walipokuwa wakipata kifungua kinywa asubuhi. Hakuwa ameenda kazini. Waliamka kama mida ya saa nne hivi baada ya kuchelewa sana kulala usiku uliopita. Alitoka kazini akamkuta Vai amejitengeneza akimsubiria watoke. Zinda akiwa amechoka, akaona itakuwa ni kumkatili tu Vai. Alishajitengeneza vizuri. Aliingia bafuni kuoga, akatoka kwa haraka akiwa ameshavaa na yeye. Alimwambia anahamu ya kwenda kula samaki choma. Zinda akaendesha gari mpaka mtaa wa Kawe, ambako alijua atapata samaki wazuri wakuchoma. Madhari waliyokutana nayo huko, iliwatuliza na kuwafanya wakae hapo kwa muda mrefu. Zinda akinywa pombe zake, Vai akinywa soda na chakula.

~~~~~~~~~~~~~~~

Vai alishituka sana. Hakujua swali hilo linamakusudi gani. Kwamba hataki mtoto, kwa hiyo anamkumbushia kutumia kinga. Au anataka mtoto lakini anamshangaa hashiki mimba kwa muda wote! Kichwa kikamzunguka. Akakumbuka ni kweli hakuwa anatumia kinga yeyote ile. Sasa kwa nini hajashika mimba muda wote huo!? Mawazo yakamrudisha siku ile alipokuwa chumba cha upasuaji akisafishwa. Akakumbuka mazungumzo ya daktari aliyekuwa akimuhudumia akiongea na wasaidizi wake huku yeye amelala kwenye meza hiyo. Daktari alikuwa akisisitza kuwa amekuta uozo mkubwa humo ndani. Anajitahidi kusafisha kwa makini kwa kadiri ya uwezo wake ili kumsaidia apone na asipoteze kizazi. Maumivu makali aliyokuwa nayo wakati wakimsafisha, Vai hakujua hatima ya kizazi chake. Alikuwa akilia kama anayechinjwa.

Alishamuomba mara kadhaa huyo daktari mchome sindano ya kupunguza maumivu, lakini hakukumbuka hata kama alichomwa au la. Waliishia kumuhoji maswali ya jinsia ya mtoto aliyekuwepo humo na umri wake kabla hajatolewa. Kwa kuwa alikuwa na maumivu makali, hakuwa akijibu bali aliendelea kulia.

~~~~~~~~~~~~~~~

 “Vai!?” Zinda akamtoa kwenye mawazo. “Kwa nini unaniuliza hivyo?” Vai akauliza na yeye huku akinyanyua kikombe chake cha chai na tabasamu kumuashiria yupo sawa. Lakini hofu ilishamwingia. “Nataka tu kujua.” Zinda akaongeza. “Unajua Viola alifanya kosa maishani, sitaki na mimi kurudia kosa.” Vai akajitetea.

 “Kosa gani?” Zinda akauliza. “Nilikwambia kuwa alimpokonya mwanamme wa mtu akazaa naye akijua ataolewa. Yule kaka akamzalisha Viola, akaishia kuoa mwanamke mwingine. Viola amebaki anahangaika na mtoto. Anamtumia pesa za matumizi za mwanae tu. Lakini bado mzigo ni wake yeye. Mtoto akiumwa anahangaika yeye peke yake. Mwanaume anafurahia na mwanamke mwingine. Nimejiapia mimi kuzaa ni mpaka ndoa. Mwanaume anayekupenda kwa dhati, hakuchezei tu. Anakuoa ndio mnazungumzia swala la watoto. Mambo ya watoto kwanza, binafsi naona ni kwa wale wanaume wabinafsi.” Hapo Vai akamfunga mdomo Zinda. 

Walishaishi pale kwa muda wote huo, bila kumtamkia ndoa. Akajua hapo anaambiwa yeye. Kwa ukweli hakuwa ameona mapungufu yeyote ya ajabu sana kwa Vai. Kwa nini asimfanye mke? Akamkumbuka Nanaa. Nanaa alishakuwa na sifa zote za kuwa mkewe. Alimuona jinsi alivyomudu kuishi na familia ya Geb pale kwake bila shida yeyote wakati Liz alikuwa akilalamika akitaka waishi peke yao, wengine waondoke au Geb awatafutie mahali pakuishi. Danny alishamwambia sifa za Nanaa. Jinsi anavyopika vitafunio vizuri na vile anavyomjali Geb na kila mtu pale ndani. Heshima na upendo kwao. Danny alishamwaga sifa nyingi tu kwa Zinda. Kwa hiyo Zinda alikuwa akimtongoza Nanaa aliyekuwa akijua atamfaa yeye na familia yake. Ndio maana tokea mwanzo kabisa, hakusita kumwambia Nanaa, atahamisha ndugu zake mjini. “Nanaa ndio angekuwa mke mzuri kwangu.” Zinda akawaza. 

“Lakini hawana tofauti sana. Hata Vai anafaa tu. Lakini atawaweza ndugu zangu kweli wakati dada mmoja tu aliye naye amemshindwa! Kila akiongelea juu ya dada yake, anakuwa akimuongelea vibaya! Sipendi jinsi anavyomjibu mama yake. Atamuweza kweli mama yangu yule muongea kilugha wakati wote? Lakini kwangu ni mwema sana. Vai anaweza kunifaa. Japo hatamfikia Nanaa. Nanaa..” Zinda aliendelea kuwaza. “Au wewe bado unahisia za mapenzi kwa Nanaa?” Vai akarusha swali la haraka lililomfanya Zinda akaribie kupaliwa. Ni kweli alikuwa akimuwaza Nanaa. Akakumbuka kiuno cha Nanaa alichokuwa akikitamani hata kujitambia mbele ya kina Geb, Danny na James. Akiapa siku akimkamata Nanaa kitandani, hatatoka. Alishasema atalipia mpaka sauti ya Nanaa! “Yule mshenzi ndio anafaidi sasa hivi! Mpaka mtoto amempa!” Zinda alizidi kuchukia moyoni.

“Eti Zinda? Maana tunaishi wote hapa. Sikusikii hata ukizungumzia hatima yetu. Ndio nauliza bado upo na hisia za kimapenzi kwa Nanaa?” Vai alisisitiza swali lake.  “Kwa nini ufikirie hivyo Vai? Huo ni ukurasa ambao nishafunga. Sina mpango naye hata kidogo. Hata akirudi leo kwa magoti, simtaki. Wanini tena? Kwanza ni kama umenikumbusha wewe sasa hivi kwa kumtaja jina lake. Sijawahi hata kumfkiria mjinga yule. Nilishamfuta kwenye kumbukumbu zangu.” Zinda aliongea huku amekunja uso.

“Sasa ili asikukere zaidi, mpe talaka yake muachane moja kwa moja?” Hapo hapo Vai akamuwahi. Zinda akashangaa. “Kama kweli umemfuta mawazoni basi muache kihalali.” Huo ulikuwa mtihani kwa Zinda. Ndio adhabu aliyokuwa ameishikilia kwa Geb na familia yake na akaapa kuwaumiza ipasavyo. Aliweka uthibiti wa cheti cha ndoa ambacho alikitafuta kwa shida sana, akadanganya mpaka akapata hicho cheti cha ndoa yake na Nanaa. Akakiweka hadharani ili hata ikitokea Geb anataka kufunga ndoa hata serikalini sio kanisani tena, ashindwe. 

“Mimi sioni sababu ya talaka. Kwanza ndoa yenyewe ya magumashi. Waache walipe kwa ubaya walionitendea.” Zinda akazungusha. Vai akambadilikia. “Kwa hiyo bado unaumwa na penzi la Nanaa!? Mimi nipo na wewe hapa. Nakupa penzi langu. Leo unanitamkia Nanaa ni bora kuliko mimi!?” “Sijasema hivyo Vai!” “Unamaanisha nini? Kama kweli huna hisia naye tena, kwa nini kutaka kuendelea kulipiza kisasi kwa mtu asiyekuhusu? Inamaana bado unampenda Nanaa!” “Hata kidogo. Sina mpango na yule Malaya.” Zinda aliongeza msisitizo.

“Kinacho kushinda kumpa talaka sasa ni nini?” Vai alishakuwa mwekundu. Mtoto huyo wa kichaga hakutaka ujinga. “Ndoa yenyewe ni ya uongo Vai. Kwa nini tunagombana kwa ajili ya hilo? Kwanza ni wewe mwenyewe ndio ulinipa hilo wazo mkisaidiana na Viola! Kwa nini sasa unataka kunigeuka?” “Sasa kama mimi ndio nilikupa hilo wazo, ukakubali, ndio nakupa tena wazo jingine. Kampe talaka, sisi tuendelee na maisha yetu. Maana sasa hivi yeye anashindwa kuolewa kisheria kwa kuwa inajulikana ana ndoa na wewe kihalali,  na wewe hutaweza kuoa kwa kuwa kisheria unajulikana una ndoa naye halali. Labla uniambie unasikia wivu kuona Nanaa anaolewa.” “Wivu wa nini sasa?” Zinda akaona amebanwa.

“Kama kweli huna mpango naye na huna wivu, mwandikie talaka. Muachane kihalali ili maisha mengine yaendelee.” Zinda akasimama bila kujibu. Akakusanya vyombo pale mezani akaingia jikoni. Vai akamfuata.

“Kweli nimeamini ulikuwa ukinichezea. Sasa hapo ndio ningeshika mimba! Si ungeniacha na mtoto wangu ukarudi kwa Nanaa?” “Naomba punguza sauti na hasira Vai!” “Kwa nini?” Vai akauliza huku ameshika kiuno. “Mwenzio maisha yake yanaendelea kama kawaida! Anaishi na mpenzi wake. Amezaa naye mpaka mtoto. Eti wewe umebaki hapa unamsubiria! Kama sio ujinga huo ni nini?” “Mimi simsubirii Nanaa. Kwanza wewe mwenyewe uliniambia Nanaa hajui kupenda.

Anamwibia tu huyo Geb. Sasa kwa nini leo unamtamka kama mpenzi wake?” Vai alitamani kupasuka kwa hasira.

“Hivi unawazimu wewe Zinda? Yaani katika mazungumzo yote hayo umesikia neno ‘mpenzi wake’ tu? Mambo yote hujasikia!? Sasa umeshanithibitishia unamtaka Nanaa kuliko chochote hapa duniani. Yaani upo radhi ukose kuanzisha familia yako. Ya mke na watoto, ilimradi uhakikishe Nanaa haolewi! Kwa hiyo unabaki vile vile kama ulivyoapa mwanzoni kama wewe hutampata Nanaa, basi hakuna atakayempata?” “Sio kweli Vai.” Zinda alijitetea kwa shida sana. Vai alimkaba vilivyo.

“Unajua mimi ndio kaka nategemewa nyumbani kwetu. Natakiwa kuoa na kuwa na watoto. Siwezi kumuacha Nanaa akaharibu ndoto zangu na familia yangu.” “Basi kama huna taarifa, ujue Nanaa amekukwamisha. Huwezi kupenda wala kuwa na familia kwa ajili yake. Husogei wala hutasogea hapo.” “Sio kweli Vai. Yote niliyofanya ni wewe ulinishauri! Sasa kwa nini kunigeuka?” “Usinifanye mimi mtoto mdogo Zinda. Unarudia mambo tuliyokwisha ongea. Nimekwambia kama ulinisikiliza mwanzoni, basi nisikilize na sasa hivi. Kinachokushinda kufuata ushauri wangu tena sasa hivi ni nini, kama sio kuwa unaona nakushauri kuwa mbali na Nanaa?” Vai alikuwa amemtolea macho akimuuliza maswali ya kweli. Watoto wa mama James huwawezi kwa kuongea. Wakikuamulia, huweki neno kama mama yao. Vai alimkaba Zinda, akabaki akirudia hoja.

“Sasa nisikilize Zinda. Endelea na maisha yako. Tafuta mwanamke mwingine utakayeendelea kumchezea na kumtumia humu ndani kama mimi. Umlale usiku kucha na asubuhi kabla ya kwenda kazini. Akufulie nguo zako na kukupikia. Mwanamke atakayekuwa anakufikiria wewe wakati wote, wakati wewe unamfikiria Nanaa. Kwa heri.” Vai akatoka pale jikoni kuelekea chumbani kufungasha.

~~~~~~~~~~~~~~~

Kwa Zinda kumewaka. Vita ya Wenyewe Kwa Wenyewe.

Wakati Nanaa na Geb wametulia. Maisha yanaendelea, Geb amesema wamuachie Mungu na Nanaa ameridhia. Amani na umoja vimerejea kati yao. Hakuna hata anayekumbushia ubaya wa watu walio watenda. Lakini kwa Zinda mambo yanatibuka. Zinda achague leo. Kusuka au kunyoa. Vai ambaye hana uhakika kama anazaa lakini yupo hapo kwake akimridhisha vilivyo. Penzi zito, ametulia ndani, au Nanaa ambaye anazidi kumzalia Geb watoto?

Nani wa nani?

Usikose muendelezo kujua kitakacho jiri.

Safari hii Mungu Anatoa Muujiza Upi?

Wakati Mwingine Mungu Hutumia Hata Adui zako Kukufanikisha. Anaweza kutumia hata jiwe, kujipatia utukufu!

Je, Ndilo atakalofanya kwenye hili pia?

Endelea kufuatili

 

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment