Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Ni Wangu! - Sehemu Ya 37. - Naomi Simulizi

Ni Wangu! - Sehemu Ya 37.

Fillius & Fillan

Siku Grace anajifungua ilikuwa siku ambayo wote walikuwepo nyumbani. Waliamka  akiwa amelala na maumivu makali ya kiuno. Asubuhi wakati tu anatoka kitandani, chupa ikapasuka. Danny alitaka kumgusa, akakataa. “Kaniitie mama.” Bila ubishi Danny akatoka. Akamkuta mama G anamsafisha Oliva. “Kumekucha!” Danny akanong’ona. “Nini?” Mama G akauliza. “Chupa imevunjika sasa hivi, nimetaka kumsaidia, amekataa hataki nimguse. Anakutaka wewe.” “Kamsaidie kubadilisha nguo Danny. Mimi nina kazi na huyu mtoto hapa.” “Mama! Ujue mwenzio kasimama anakusubiria!” “Haiwezekani Danny!” Mama G akabaki ameduaa.

Mama!” Grace aliita akisikika anaanza kulia. “Nakuja mama. Nilikuwa namuogosha mtoto.” Wakamsikia analia. “Sasa wewe kamgongee kaka yake na Nanaa. Kumeshakucha hapa. Na kazi ndio imeanza. Mwambie Nanaa afanye haraka aje hapa.” Danny akatoka, akaona aanzie chumbani kwa mkewe kwanza amtulize ndipo apandishe juu kwa kina Geb. Alimkuta amesimama vile vile kama alivyomuacha wala hajajigusa, analia. “Pole Grace.” “Mama mbona haji jamani? Sijui nifanyeje?” “Labda nikusaidie kuoga halafu…” “Namtaka mama, Danny. Nimekutuma ukamwite mama halafu unanipuuza! Hujali ninachokwambia! Unafikiri hapa najisikia raha? Sijui kama naumwa njaa au usingizi! Usiku kucha wakati wewe unakoroma mwenzio nilikuwa nateseka peke yangu. Sasa hivi nakutuma jambo dogo tu una…” Danny akatoka kwa haraka na kurudi kwa mama yake.

“Naomba nipe mimi huyo mtoto mama. Grace atajifungua amesimama. Amelowa machozi na maji. Na bado amesimama vilevile, palepale. Naomba msindikize akaoge twende hospitalini. Unajua kuanzia sasa hivi hana atakayemsikiliza ila wewe. Nenda mama yangu.” Mama G akatingisha kichwa. Alishamvalisha Liv, akamuweka kitandani. “Wewe muache hapa hapa mpaka mama yake aje, nenda kawagongee.” Grace alikuwa akilia kwa sauti ya maumivu.

Geb alishituka sana Danny alipogonga. “Kwema!?” “Grace chupa imevunjika.” Geb akacheka. “Naona Mzee umeshapaniki.” “Ameshaanza kulia. Hataki hata nimguse!” Geb akacheka tena. “Mama si yupo naye lakini?” “Ndio ameenda sasa hivi.” “Ngoja na mimi nivae, nakuja sasa hivi.” “Mwambie Nanaa mtoto alishaamka.” Danny akaondoka. 

Nanaa aliamini maneno ya mama G. Grace hakuwa hata akitaka mtu mwingine amguse au kumuongelesha zaidi ya mama yake tu. Mpaka inafika jioni Grace anajifungua, mama G hakuwa akiweza hata kuongea kwa kuchoka. Geb na Danny walikuwepo hospitalini, Nanaa alibaki nyumbani na watoto huku akiwasiliana na Geb kujua kinachoendelea. Mara zote alipotaka kuzungumza na mama G, Geb alimwambia haitawezekana mpaka Grace ajifungue. Hata wao hawawezi kuzungumza na mama yao kwa vile Grace alivyomtawala. Hata alipopitiwa na usingizi hapo hospitalini, alitaka mama yake aendelee kumsugua kiunoni yeye apumzike wakati uchungu umetulia.

Mama G na Geb walirudi usiku wote midomo ikiwa imewakauka. “Pole mama.” “Hata maji kunywa ilikuwa kazi. Hivi alininyweshwa Geb.” “Kwa nini sasa!?” Nanaa akauliza. “Mikono yote ilikuwa na kazi yakumsugua mzazi. Ikitoka hapo kiunoni au tumboni, na yeye anaamka nakuanza kulia. Kuja kumnyamazisha tena, ni nusu saa.” Nanaa akaanza kucheka. “Pole mama yangu. Lakini nimezungumza naye muda si mrefu, anasikika anafuraha.” “Ndivyo alivyo. Shida ni pale akiwa anataka kujifungua.” “Na lazima asubuhi mama awepo pale. Azungumze na manesi na kushika wale watoto wake mpaka aruhusiwe.”  Geb akaongeza. “Na nisichelewe kwenda huko hospitalini. Lasivyo nitakuta analia kama mgonjwa vile.” Mama G akaongeza, wakacheka. “Pole mama. Kaa hapohapo nikuletee chakula.”

Mahari Ya Nanaa Yawa Ya Misuko Suko.

Baada ya kama miezi 3 ya hekaheka ya ulezi wa watoto hao wanne ndani ya nyumba moja, Oliva akiwa anakaribia miezi 6, na watoto hao wawili wa Grace ambao walikuwa wanakaribia miezi 3, ndipo  James alipiga simu akimtaka Geb na Danny wakutane nae mahali ili wazungumzie swala la mahari ya Nanaa. Geb alitoka kazini kwa haraka, akiwa amejawa furaha. Akamkuta Danny na yeye ndio anaegesha gari yake. Wakasalimiana, wakaingia ndani wakijua James alitangulia maana gari yake waliiona imeegesha hapo nje.

Wakamkuta amekaa kwenye meza peke yake, lakini hana furaha. Wakajua ni kazi nyingi tu za siku hiyo, maana ndio juma lilikuwa lipo ukingoni. “Kwema kaka?” Danny akasalimia. “Kwema.” James akajibu huku akimvutia Danny kiti. Wakakaa.

 “Samahani kukuchelewesha kwenye swala la mahari Geb. Sio kwamba nilisahau, ila mambo yamekuwa magumu mno. Lakini naomba usimwambie Nanaa. Hii kitu imezua ugomvi kupita kiasi.” “Ni nini tena!?” Geb akauliza.

“Daaah! Sijui niwaambie nini! Lakini gafla sasa hivi kila mtu anamtambua Nanaa, na kila mtu anataka kupokea yeye hiyo mahari ya Nanaa.” “Kwa nini sasa tusiwape wote?” Geb akauliza. “Subiri kwanza Geb. Unamaana ulipe mahari ya Nanaa zaidi ya mara moja!? Kwa nini wasipokee kwa pamoja wakagawana!?” Danny akauliza. “Hawataki.” James akajibu.

“Mimi nitawalipa kila mtu. Nataka haya mambo yaishe jamani.” “Basi naona akili ya Geb ikawa kama yangu. Nikawaambia kila mmoja wao. Yaani bibi na mama. Wanipe tarehe zao wanazotaka tuwapelekee hiyo mahari. Kila mmoja aandike anachotaka atalipwa kwa wakati wake. Hapo napo kukazuka maneno. Mama anasema bibi alimkana mama yake Nanaa na alikataa hata kumwangalia Nanaa mwenyewe. Akamuachia mzigo wote. Iweje leo atake kulipwa! Nikajaribu kumwambia yeye asihangaike na atakacholipwa bibi, aniambie anachotaka yeye. Pia akakataa. Akasema kama bibi atalipwa mahari ya Nanaa, yeye hataki. Ni kama akazira.” “Kwa nini hukuzungumza na Mzee?” Danny akauliza.

“Hapo napo pakazua ugomvi wa aina yake. Mama anasema baba naye alimkana Nanaa tokea mwanzo. Hataki hata kumsikia anamtaja Nanaa. Nimehangaika wee, ndio nikamwambia basi yeye anipe mahari anayotaka kulipwa. Akasema nimuahidi kuwa bibi hatawahi kupokea hata shilingi ya Nanaa. Nikamwambia huko siwezi kuingilia. Akazira karibia siku 20. Nikimsalimia haitikii. Haya, week mbili zilizopita akanipa orodha ya vitu anavyotaka apelekewe na pesa anazotaka kulipwa kwa ajili ya kumlea Nanaa. Akanitajia hiyo pesa, nikamkatalia kabisa. Nikamwambia hawezi kumuuza Nanaa kama ng’ombe! Akasema yeye alikesha akimlea Nanaa, lazima alipwe. Nikakataa. Akazira tena.” “Anataka kiasi gani?” Geb akauliza akitaka kufupisha mambo.

James akabaki anatingisha kichwa huku akisikitika. “Ni kiasi gani?” Geb akauliza tena. “Nashindwa hata kukutajia Geb. Lakini ujue muda wote huo nimekuwa nikihangaika kumbembeleza apunguze.” “Umefikia wapi?” Geb aliendelea kuhoji. “Daaah! Yaani mpaka najisikia aibu kutaja.” “Sema tu James.” Danny akasisitiza. 

“Yaani amepigia hesabu mpaka maziwa aliyokuwa akimnyonyesha Nanaa, kifuani kwake! Garama za miaka yote aliyokuwepo Nanaa pale nyumbani. Chakula, malazi na mavazi. Muda uliomgarimu kutofanya kazi na kukaa nyumbani kumlea Nanaa. Akataka…” “James! Nataka kujua anataka kiasi gani, basi.” Geb alimkatisha. “Daah!” Bado James alisita kutaja. Waliuona ule ugumu mpaka kwenye macho ya James.

“Naombeni mnisikilize jamani. Nilazima nitamuoa Nanaa. Kwa garama yeyote ile, nitamuoa Nanaa, kwa kuwa ndiye mke wangu. Hakuna jinsi nyingine. Kama kazi yote ninayofanya, kuanzia asubuhi mpaka usiku, haitaweza kulipa hiyo garama ya Nanaa, basi nitakopa hiyo pesa. Ninachotaka kujua tu, ni kiasi gani?” Geb akasisitiza. “Nitakusaidia Geb.” James akaongeza. “Unisaidie kumuoa Nanaa!?” Geb akamuuliza James kwa kumshangaa sana.

“Sitaki ufikirie ni kama nimekula njama na mama yangu ili kupata pesa kutoka kwako! Na sitaki uone ni kama unamnunua Nanaa. Ndio maana nataka wewe umlipe nusu, nusu nitampa mimi na nyingine kama atadai. Kwa sababu hata hicho kiasi, nimemtajia jana kwa kumsisitiza kuwa ndiyo atakayo lipwa. Si zaidi ya hapo.” “Akakubali?” Danny akauliza. “Atakubali tu.” “James? Mbona unashindwa kuzungumza? Mama amekubali hicho kiasi au la?” “Amekubali.” James alijibu akionyesha hana uhakika.

“Amekubali kwa kiasi gani?” Geb akauliza tena. “Milioni...” James alitaja kwa upole sana. “Duuuuh!” Danny alishituka sana. “Lini yupo tayari nilete hiyo pesa?” Geb akauliza bila wasiwasi. “Utalipa pesa yote hiyo!?” Danny akauliza kwa mshangao. “Ninamuoa Nanaa. Naomba uniambie ni lini natakiwa kuja kulipa hiyo pesa, nimalizane nao yaishe.” “Mimi nitakusaidia Geb.” Danny akajitolea. “Asante Danny. Lakini mimi ndiye ninaye muoa Nanaa. Acha nitalipa mwenyewe tu.” “Lakini kuna orodha ya vitu vingine vinatakiwa Geb, acha tukusaidie.” “Hapana. Baba yangu angekuwa hai, hilo ndilo lingekuwa jukumu lake. Lakini hayupo. Na mimi ndiye Magesa mwenyewe. Nikishindwa kumuoa Nanaa sababu ya pesa, nahisi sistahili kuwa mtoto wa yule Mzee. Ninachotaka msaada kutoka kwenu ni kunisindikiza tu. Lakini garama zote ni juu yangu. Nitamuoa Nanaa, mimi mwenyewe kwa jasho langu.” Danny na James wakanyamaza.

“Kama hamna kitu cha ziada, naomba mimi niwahi nyumbani. Najua sasa hivi Liv na Nanaa watakuwa wakinisubiria. Siku hizi Liv akiniona tu ananyanyua mikono yote juu huku ananichekea akitaka nimbembe. Kwa hiyo naomba niwahi.” Danny na James wakacheka kidogo. “Basi nitamkabidhi Danny kesho. Nilishindwa kuja na hiyo orodha kwa kuwa sikujua kama utakubali kulipa hiyo pesa yote.” “Hakuna shida. Hata hivyo nashukuru sana James. Uwe na usiku mwema. Danny, tutakutana nyumbani.” Geb akanyanyuka na kuondoka. Alimuacha Danny na James wakifikiria. Jinsi pesa ilivyo ngumu kwa wakati huo, halafu mtu adai mamilioni yote hayo ya pesa! Hakika haikuwa ndogo hata kwa tajiri. Waliamini kuwa Geb amekusudia kuoa kweli kweli.

~~~~~~~~~~~~~~

Na kweli Geb alipoingia tu nyumbani Liv akaanza kucheka. Moyo wa Geb ulijawa na furaha ya namna yake. “Njoo mama yangu mzazi. Njoo.” Ile furaha iliyojaa moyoni, kumuona Liv na mama yake pale nje barazani, wakimsubiria yeye! Tayari akaona yale mamilioni ya pesa ni kiasi kidogo sana kulinganisha na anachojisikia kwa wakati ule. “Muone anavyocheka.” Nanaa akamkabidhi kwa baba yake. Geb akambusu mara kadhaa, akamkumbatia kwa kumuweka kifuani kwake. “Mmmmh!” Geb alisikika akisikilizia ile raha rohoni mwake. Oliva alizidi kucheka.

“Dimpozi kama za mama yako!” Geb akambusu tena mashavuni. “Ananirembulia tokea saa moja. Ikabidi kumtoa hapa barazani kucheza naye ili asilale bila kukuona.” “Poleni. Nimechelewa. Nilikuwa nakutana na James.” “Kwema?” Nanaa akauliza. “Kwema. Ni mambo ya mahari.” Nanaa akatulia kidogo. “Usiwe na wasiwasi. Tutafanikiwa tu.” “Sidhani Geb. Nahisi kuna kitu kinaendelea tu, lakini kaka hataki kuniambia. Unajua ni zaidi ya miezi mitatu sasa tokea tumuombe afuatilie mambo ya mahari? Nilimpigia simu majuzi, akababaika kweli, akashindwa kunipa jibu la moja kwa moja! Nikahisi kuna kitu ananificha.” “Lakini naona amefikia pazuri. Kesho amesema atamkabidhi Danny orodha ya hiyo mahari.” Nanaa akanyamaza.

“Tutafanikisha Nanaa. Usiwe na wasiwasi.” “Natamani iwe hivyo Geb. Na mimi natamani kuvaa shela! Nisimame na wewe kanisani.” “Shauku yako itatimia hivi karibuni. Tuendelee kuomba.” Geb akamvuta karibu kwa mkono wake wa kushoto, akawakumbatia wote wawili. Nanaa na Oliva. Alimbusu Nanaa kichwani. Wakasimama pale kwa muda wakicheka na mtoto wao, kisha wakaingia ndani.

~~~~~~~~~~~~~~

 “Ungechelewa kidogo tu, huyo angelala leo bila kukuona.” Mama yake alimuwahi wakati wanaingia. “Nimechelewa kidogo leo. Nilikuwa na Danny na James. Hivi nimemuacha Danny huko huko.” “Kwema?” Grace akamuuliza. Geb akambusu mwanae. “Kwema. Ni mambo ya mahari.” Alijibu huku akimwangalia mwanae. Kwa ujibuji ule, Grace na mama yake wakajua hataki maswali zaidi. Wakaamua wanyamaze.

“Umeshindaje na watoto?” Geb akamuuliza dada yake. “Wanakazi ya kunyonya tu. Basi hapa hamna kingine ninachofanya zaidi ya kunyonyesha! Mpaka mgongo unauma!” “Nimekuletea kitu chakufunga kiunoni. Kusupport mgongo wakati unanyonyesha.” “Afadhali. Asante.” “Nimeacha kwenye gari. Nitafuata. Ngoja niongee na Oliva kidogo. Eti mama?” Geb akambusu na kupandisha naye juu chumbani kwake. Nanaa akafuata nyuma.

~~~~~~~~~~~~~~

Kesho yake Danny akarudi nyumbani na orodha ya vitu vya mahari anayotakiwa Geb kulipa. Akataka kumkabidhi  Geb lakini mtoto wake akamuwahi. Aliwakuta nje, Geb na Fili wakicheza. Fili akamkimbilia baba yake. “Nimemfunga anko.” Akajisifia kwa baba yake. “Hongera mwanangu. Uendelee kumfunga hivyo hivyo.” Geb akacheka akitingisha kichwa. “Wewe Fili! Nani kamfunga mwenzake hapa?” “Wewe 3, mimi mbili.” Fili alijibu kwa kujiamini. “Sasa mimi si ndio mshindi?” “Lakini na mimi pia nimekufunga anko.” Danny na Geb wakacheka. “Kichwa hicho, hukiwezi kwa hoja.” Danny alimsifia mwanae. “Kweli simuwezi!” Wakacheka.

“Vipi huko ndani? Maana nilipigiwa simu nusu saa iliyopita, nikasikia kumechangamka kweli! Kama wodi ya watoto!” Geb akacheka. “Naona kumetulia.” Geb akajibu. “Afadhali. Maana nimeambiwa nirudi haraka nije kuchukua wanangu wote.” Geb alizidi kucheka. “Ndio maana nimemtoa huyu nje. Naona wanamchangamsha kweli Grace!” Danny akacheka. “Ngoja niwahi ndani kabla ya yeye mwenyewe hajaanza kulia. Maana hakawii Grace!” Danny akaingia ndani.

Baada ya muda Geb naye akaingia. “Usingerudi kwanza Geb! Mwanao akikuona, hatakula tena.” Mama yake alimuwahi. Oliva alivyomuona tu baba yake akanyanyua mikono yote juu huku anacheka. Chakula chote alichokuwa ameweka mama yake mdomoni kwake, kikaanza kutoka. “Liv jamani! Cheka gani hiyo mpaka unatema chakula bwana!?” Nanaa akalalamika. Walikuwa wamemkalisha kwenye kiti chake, wanamlisha.

“Mbona mwanangu anaonekana hafurahii hicho chakula? Mnamlisha nini?” Geb aliuliza huku akimsogelea. “Ndio namkazania. Leo siku ya pili tumemuanzishia uji.” “Basi naona hataki.” “Usiseme hivyo bwana Geb! Huyu mtoto lazima aanze kula.” “Sasa kama hataki!?” Geb akauliza huku anamchekea mwanae. Tayari Liv alishaanza kufunga vidole vyake na kuvifungua kama anayemwita baba yake. Geb akamsogelea na kumbusu.

          “Eti Liv mama?” Mtoto akaanza kujinyanyua pale kwenye kiti ili baba yake ambebe. “Mwache bwana Geb!” Nanaa akalalamika. “Sasa kama hataki kula hicho chakula chenu?” “Basi huyo atatonya tu mpaka anaanza shule!” Mama yao aliingilia. “Atakuja kula bwana mama.” “Lini wakati unamtoa hapo? Mwache mama yake amlishe kidogo.” “Sasa ananitaka je!” “Haya!” Mama G akaamua anyamaze. “Njoo mama. Njoo eeh!” Nanaa alibaki akimwangalia Geb na mwanae. “Muone naye anavyocheka! Basi kazi yake ni hiyo tu. Kucheka. Ukimpa kitu chochote ale, yeye anakuchekea huku anatema.” Geb akacheka. “Eti Liv. Hutaki kula?” Geb akambusu.  

Mahari ya Nanaa, Mzigo mzito.

“Hii karatasi ya nini?” Grace aliokota karatasi aliyokuwa ameangusha mumewe. “Ni ya Geb hiyo. Amenipa James nimkabithi. Ina orodha ya mahari ya Nanaa. Nilitaka kumkabidhi mwenyewe pale nje, Fili akaniwahi na maneno mengi, nikasahau.” “Afadhali!” Grace akafungua huku akionyesha kufurahia. Wote waliisubiria kwa muda mrefu sana. “Haleluyaaaa!!” Mama G akaanza kupiga vigelegele vya shangwe. Akasimama huku anapiga vigelegele. 

“Mama! Utafikiri yeye ndio anaolewa!” Grace alikuwa akimwangalia mama yake asimuelewe. Nanaa akacheka akasogea. “Hatimaye. Maana nilishaanza kuingiwa na hofu!” Nanaa alifurahia sana. “Hebu isome. Kesho nataka mkaanze kununua hivyo vitu, tukalipie. Mchakato wa harusi uanze.” Mama G, akaongeza. “Tulia basi mama!” Grace alimtaka mama yake akae. Akakaa, Grace akaanza kusoma huku Danny amebeba watoto wake wote wawili, ametulia kama Geb aliyekuwa amebeba na yeye mwanae. Kimya, akijua ule mzigo unaomkabili Geb. 

Grace akaendelea kusoma ile orodha. Mwanzoni ilikuwa vitu vya kawaida sana. Alipofika karibu ya mwisho akatoa macho na kubaki ameduaa. “Nini!? Hebu maliza kusoma bwana, usinitie presha.” Mama yake akamsisitiza. Grace akasita lakini akaona asionyeshe wasiwasi mbele ya Nanaa. Akasoma. “Na fidia ya kumlea Nanaa tokea anazaliwa mpaka anatoka nyumbani kwa mwanangu James!” Kisha akatulia kidogo.

“Iliandikwa  Milioni 100. Naona ikafutwa kwa kukatwa mstari hii tarakimu nzima. Kisha mbele yake imeandikwa hapa milioni 80. Nayo pia nimeona imekatwa tena. Ikaandikwa tena Milioni 50. Ikafutwa tena kwa kukatwa mstari. Naona imeandikwa tena Milioni 30 kwa kalamu nyingine, tena sio ile ile ya bluu. Hii milioni 30 imeandikwa kwa kalamu nyeusi.” Grace alitambua muandiko wa pili ulikuwa wa James. “Tena ni mwandiko wa James huu!” Ukimywa mkubwa ukatanda. Nanaa akachukua ile karatasi akaanza kuisoma upya.

Mama G ndipo akaelewa kwa nini jana yake Geb hakutaka kuongelea swala la mahari. Walimuona Nanaa anafuta machozi wakati akisoma. Geb akamsogelea. “Njoo.” Geb alimuita lakini Nanaa akashindwa hata kusogea. Aliendelea kulia huku akisoma. “Daah! Hii pesa wanayotaka ni ndefu sana jamani! Kwa nini wanafanya hivyo!?” Grace alilalamika. Danny kwa mara ya kwanza akanyamaza. “Usilie Nanaa. Njoo.” Nanaa akakataa kwa kutingisha kichwa huku akilia sana.

“Nanaa!” “Hapana Geb. Hii imezidi jamani. Mimi naona sitaweza tena. Ni heri tuache haya mambo. Heri ukaoe mtu mwingine. Wanakuwa wananiuza kama ng’ombe jamani! Hii sio haki kwangu. Tena watu wenyewe hata hawanithamini! Majina yao yenyewe walikataa nisitumie. Sio la baba yake James tu, hata bibi alikataa nisitumie jina la ukoo wao. Nikaishia kuitwa jina la mama yangu ndio kama jina la ukoo au la baba yangu! Yaani maisha yangu yote nimeishia kuitwa Nanaa Wini. Nimekaa kwao nikiwatumikia tokea mtoto huku wakiniambia nalipia chakula ninachokula na malazi. Kweli mpaka leo hiyo garama yangu sijamaliza kulipa tu!? Hapana Geb. Inatosha.” “Kwa hiyo unaniacha?” Geb akamuuliza, Nanaa akazidi kulia.

“Nanaa?” “Sijui Geb. Lakini hapana. Na usidhani hapo kwa kaka kuandika hiyo milioni 30 kwa mwandiko wake ni bure. Ujue wameshindwa kufikia muafaka. Mwandiko huu ni wa  mama mkubwa. Na Grace hujasoma karatasi ya chini. Ameandika fidia anazotaka alipwe mpaka maziwa niliyomnyonya kwenye matiti yake! Wakati na mimi alishanilipisha hizi fidia zote, jamani! Alisema haajiri mfanyakazi mwingine pale ndani sababu mimi natakiwa kulipa fadhila ya hivi vitu vyote alivyoandika hapa. Alinitajia kila kimoja wapo hapa, Geb. Yaani hii orodha hapa kwangu mimi sio ngeni. Nimekuwa nikitajiwa mchana na usiku. Kama ilivyo hivi hivi. Tokea nakua mpaka ananifukuza pale kwa kaka. Naweza kuwatajia hivi vitu vyote hapa bila hata kusoma, vile vilivyokaa kichwani kwa kuvisikia mara kwa mara. Tena nikiambiwa nilazima nilipie. Na nilikuwa nalipia kimoja baada ya kingine. Hivi hivi kama ilivyoandikwa hapa. Hapana. Inatosha Geb. Hivi vitu nilishalipia kwa mateso mengi sana. Nitadaiwa mpaka lini?” Nanaa aliendelea kulia. 

“Njoo Nanaa mwanangu.” Mama G na yeye akamwita. “Hapana Mama. Hapana. Kuzaliwa kwangu na kukua kwangu kumekuwa ni shida tupu mama yangu. Hujui mateso niliyopitia kulipia hii orodha nzima. Nimelipa kwa machungu makubwa sana. Mama mkubwa hanidai. Nishalipia mimi mwenyewe mama. Hakika nimemlipa. Heri nisiolewe kuliko kumlipa tena. Nilikuwa wakati mwingine nafungiwa nje. Usiku. Baridi kali. Nafua nguo za watoto wake, mpaka vidole vinakuwa vinakufa ganzi kwa baridi. Hapo sina sweta, sijala wala kupumzika tokea asubuhi. Anasema natakiwa kulipia hiki au kile. Hapana mama yangu. Kama ni hiyo ndoa basi.” Nanaa akaendelea kulia kwa uchungu sana.

Kipenda Roho.

Geb akamkabidhi Liv kwa mama yake, akaenda kumchukua Nanaa. Akamshika mkono, wakaelekea juu chumbani kwao. Kila mtu alikuwa kimya. “Hapana Geb!” Nanaa aliendelea kulia. Geb akamkumbatia. Nanaa alilia, huku Geb akimsugua mgongoni. Wakahamia kitandani. “Nakupenda Nanaa.” “Utapata tu mwanamke mwingine Geb. Mimi hapana.” “Niangalie.” Nanaa alifanya kosa la kumwangalia. Geb akambusu. Akarudia tena na tena huku amelala naye pale kitandani akimpapasa taratibu. Aliendelea kunyonya midomo yake mpaka akahakikisha akili ya Nanaa imerudi pale kitandani.

“Nakupenda wewe Nanaa.” “Na mimi nakupenda Geb, lakini…” Geb akamuwahi kwa busu kabla hajamalizia kisha akaongea yeye. “Unajua kitu ninachotamani kila siku asubuhi ninapoamka?” Nanaa akatingisha kichwa kukataa. “Kila nikiamka, najua nilazima niende kazini. Lakini kuanzia muda naondoka hapa nyumbani nakua natamani jioni ifike, nirudi nyumbani, nikukute wewe na Liv, mkinisubiria mimi pale nje. Zile dimpozi za yule mtoto anavyozitoa kwangu. Akicheka na kukunjua vile vimikono vyake akinitaka mimi! Halafu kakitulia hapa kifuani kwangu! Oooh my! Kwangu ni kitu cha thamani ambacho hakuna kiasi cha pesa kinaweza kununua hiyo furaha ninayosikia moyoni. Hakuna Nanaa. Nakuahikishia mpenzi wangu, siku utakayokataa nisikuoe sababu ya pesa, ujue umenimaliza kabisaa.”

“Uwezo mkubwa nilio nao wa kutengeneza pesa sasa hivi, ni kwa ajili yako mpenzi wangu. Nimetulia. Akili inafanya kazi vizuri, sababu ya maisha uliyonipa. Sina jinsi nyingine ya kukwambia ukanielewa. Acha tulipe hiyo pesa, uwe wangu.  Hata kama watataka milioni 100, nitawalipa tu. Waache wakuuze. Uzuri mimi ndio nakununua. Huna chakupoteza. Huingii aibu. Hiyo pesa itarudi tu. Mungu yupo na sisi.” Nanaa hakuamini.

Aliinama akaanza kulia tena. “Huwezi kujua kwa nini Mungu ameruhusu hayo yote yakupate. Lakini maadamu tupo wote, na uwezo upo, mimi nitalipia.” “Labda na mimi nitafute kazi ili nikusaidie kulipa.” Geb akacheka. “Na kaka yako James alitaka kunichangia nusu ya hiyo pesa, nimekataa. Mimi nitalipa Nanaa. Kama nina uwezo wakununua magari ya mamilioni ya pesa, sitashindwa kununua uhuru wako. Tuwalipe tu ili uwe huru. Tena utakuwa wangu kihalali. Wote tutakuwa tukiitwa Magesa. Wewe, Oliva na mimi. Wote tutakuwa Magesa.” Nanaa akacheka.

~~~~~~~~~~~~

“Asante Geb.” “Kavu kavu tu!?” Nanaa akampiga ngumi kidogo. “Yaani kazi yote niliyofanya ya kukubembeleza naishia kupewa asante tu!? Nipoze kidogo basi.” Nanaa alicheka mpaka akageuka upande mwingine. “Geb!” “Kweli tena.” “Mtoto hajala bwana. Baadaye.” “Wewe usijiguse hata kidogo. Na sikuvui nguo zote. Niruhusu chini tu.” Geb alishapiga magoti na kumfunua kigauni alichokuwa amevaa. 

Akaanza kubusu mapaja yake huku mikono ikiwa na kazi ya kumtenganisha na nguo ya ndani nyembamba aliyokuwa amevaa. “My My Myyyy! Uuuuu!” Geb alikuwa akiongea huku akimtizama Nanaa kwa uchu. Wazi alionekana anafurahia anachokiona. “Hii chupi ya wapi tena?” “Nilienda leo madukani na mama.” Nanaa aliongea kwa sauti ya chini iliyojaa kujivunia na kufurahia sifa anazopewa. “Imekupendeza!” “Asante. Nilijua utaipenda tu.” Geb akabusu juu ya ile chupi. Akapitisha kidole chake kwenye lastiki ya kiyo chupi kuzunguka kiuno. Mwili mzima wa Nanaa ukasisimka. Akabaki akisugua mapaja na tabasamu usoni huku akinyonya lips zake.

Midomo ya Geb ikatua kwenye kitovu chake, akambusu na kuweka kidole chake pale. “Nakupenda Nanaa.” “Na mimi nakupenda Geb.” Geb alimgeuza kwa haraka. Akamuweka style ya kupiga magoti akiwa ameinama. “Mmmh! Mh! Mh!” Geb alimpapasa juu ya kiuno huku akimbusu kila eneo juu ya kino chake. “Hakuna pesa inayoweza kununua hii.” Tarati Geb alishaingia. Nanaa alimsikia akisugua meno. Akajua anapata starehe aliyokuwa akitarajia. Akafurahia. Mikono yake ilikuwa imeshika hips za Nanaa kwa nguvu. Baada ya muda mfupi sana Geb akamaliza.

           “Daa! Leo mbona umezidi kuwa wa moto kuliko siku nyingine?” “Umefurahia?” “Sana. Ukatikaji huo nilishakwambia unanifanya nashindwa kujizuia.” “Nilitaka umalize haraka, nikamlishe mtoto.” Geb akacheka. “Mawazo yako kwa Liv, mwili kwa baba yake!” Nanaa akacheka. “Ndio ujue wote tunakuhitaji. Twende tukamalizie siku, uje unipe mwili na akili zako. Navitaka vyote viwe hapa. Na hivi kesho nitachelewa kwenda kazini! Basi acha nilifaidi hilo joto leo.” “Halafu nimepitisha siku zangu Geb.” “Waache waje hao watoto. Hata kama ni mapacha, tutalea tu.” Nanaa akacheka. Akanyanyuka pale kitandani, akakimbilia bafuni. Geb akamfuata.

Kule kumkuta Nanaa yupo uchi huko bafuni akitaka kuoga mara moja ndipo ashuke akamlishe mtoto, ikawa kosa. Hapo Nanaa akasahau hata mtoto. Walizungushana huko bafuni, wakajikuta wamerudi tena kitandani huku wameng’ang’aniana. Mapenzi ya haja yakaendelea pale kitandani. Mpaka waliporidhika ndipo wakatoka hapo chumbani.

~~~~~~~~~~~~

Walikuta watoto wote walishaenda kulala kasoro Fili alikuwa anacheza game kwenye simu ya mama yake huku Grace amempakata na kumbusu kila mara. Alishaogeshwa na kuvaa nguo za kulalia tayari. “Liv yuko wapi?” “Alishakula, akaoga, nimemlaza muda tu.” Mama G, akajibu kama anawasuta. Nanaa akainama huku akicheka. “Lakini kesho nitaenda naye kazini. Nikamfundishe biashara.” Geb akamvuta mkono Nanaa akamkumbatia. “Ni lini James amesema tukalipe hiyo mahari?” Geb akamuuliza Danny. “Jumamosi ijayo ndio mama yake amesema atakuwa na nafasi.” “Basi naomba tujiandae. Jumamosi ijayo tutalipa hiyo mahari.” Geb aliongea akisikika kujiamini.

“Nimeamua kukusaidia Geb. Nusu ya hiyo pesa, mimi nitalipa kwa niaba yangu na baba yako.” Geb akacheka. “Nakushukuru sana mama yangu. Hata James na Nanaa walitaka kunisaidia, lakini nimekataa. Mimi ndio nitalipia mahari ya Nanaa. Nitakachoomba ni muwe tu na mimi. Basi.” Mama G akaanza kupiga tena vigelegele. 

“Basi watoto wote wataamka! Mwenyewe nataka muda na mwanangu Fili tu. Nina hamu naye kweli! Lakini kwa shamra shamra hizi! Wale watoto wawili wa Danny, sijui kama watalala!” Grace alitaka mama yake anyamaze. “Liv akiamka ndio nitafurahi.” Geb akajibu huku akicheka vile mama yake anavyocheza. “Mimi sitaki lile jeshi la Danny liamke bwana! Mgongo wote unauma kwa kubeba!” “Unakumbuka kuvaa ile belti niliyokuletea lakini?” “Wewe si umewaona wakianza kulia wanavyokuwa? Huwezi kukumbuka hata kuvaa nguo!” Geb na Nanaa wakacheka. Danny akatingisha kichwa.

“Muulize mama na Nanaa. Hawa watoto leo asubuhi mpaka waliniliza mimi! Wanalia kama kengele! Nilikuwa naoga, nimetoka bafuni nakimbia. Nimeshinda na taulo siku nzima mpaka walipolala.” Geb alizidi kucheka huku akimwangalia dada yake. “Watakuwa tu. Utapumzika.” “Mmmh! Sioni dalili. Na hivi walivyofanana na Danny hao, nahisi hizo kelele ni za milele.” “Nakwambia lawama zote ni zangu.” “Kumbe unafikiri wamerithi kwa nani? Watoto wawili utafikiri jeshi la Iraq! Mpaka nimekonda wakati nakula kama mchwa! Hongereni mwaya.” Grace alimgeukia Nanaa na Geb.

“Nanaa! Ndoa ni nzuri mdogo wangu. Usikubali watu wakakukosesha baraka za ndoa. Kuna vitu vingine kwenye maisha, vinapaswa kulipiwa garama. Wewe ni wa thamani sana. Ndio maana kila shetani akikuangalia, anashindwa kukuthaminisha. Anaishia kuongeza bei tu.” Mama G akapiga tena vigelegele. “Ongea mwanangu Grace. Umeshindwa shetani!” Mama G akaendelea kupiga vigelegele. “Basi leo hatutalala!” Grace alifanya wote wacheke.

“Asanteni jamani. Na samahanini. Ni kweli najisikia vibaya. Ni hivyo sina jinsi yakufanya.” Nanaa aliongea kinyonge. “Hivi unakumbuka habari ya Yusufu? Yule wa kwenye bibilia? Unakumbuka aliuzwa na ndugu zake?” Nanaa akatingisha kichwa kukubali na kuongeza. “Nakumbuka mama.”“Mwisho wake unaukumbuka? Mbali na mateso mengi aliyopitia, kumbe vyote vile Mungu aliviruhusu ili ajifunze na akomae hata kiroho chake, ili anapomfikisha sehemu ya juu aweze kuishi na ile baraka. Ipo sehemu ya juu sana Mungu amekuandalia Nanaa. Na hakuna anayeweza kukaa hapo isipokuwa ni wewe tu. Kwa kuwa umepitishwa shule kama yako na ukafaulu. Usipokata tamaa na kuishia njiani kama wengine, ukavumilia mapito yako mpaka mwisho, hakika utakuja kumshukuru Mungu. Unakwenda kuinuliwa mpaka ushangae. Utabarikiwa mpaka moyo wako ufurahie na watu wakuite heri.” “Amina mama. Asante. Nashukuru kwa kuwa na mimi mpaka sasa. Hujanichoka.” Nanaa alianza kulia tena.

“Nikuchoke tena!? Wala. Tena hata kidogo. Wala usilie. Ukiona mama G amekukatia tamaa, ujue hata mbingu zimekukataa. Wewe tulia. Furahia. Jiandae kwa moyo mweupe, ukijua utaolewa tu mwanangu. Ngoja tukalipe hiyo mahari tuanze mikakati ya harusi. Nitakununulia gauni hilo, ukiingia pale kanisani watu wataulizana.” “Mama G kwa kupenda shuguli!” Grace alikuwa akimwangalia mama yake, hammalizi. “Watoto wenyewe nilipewa wawili tu. Wakati unaolewa wewe, sikuwa na uwezo. Haya, akishaoa Geb, ndio basi tena mpaka Fili. Sasa ni leo hiyo? Heri nichangamke sasa hivi nikiwa na nguvu.” “Basi mama wakati wewe unashangilia, sisi tule.” “Kesho asubuhi, Danny na Geb mnaenda kununua vitu vyote kwenye hiyo orodha. Na msiniletee vitu vya ajabu.” Mama G aliendelea kusherehekea usiku ule bila kuchoka.

Jumamosi.

Waliamka siku ya jumamosi. Geb akaenda chumbani kwa mama yake moja kwa moja kumfuata mwanae. Oliva alikuwa kwenye kitanda chake wakati baba yake anaingia. Akaanza kucheka huku amenyanyua mikono yake juu. Akifunga na kufungua viganja vyake. “Njoo mama yangu. Leo tunaenda wote kazini.” “Sasa vitu vya mahari mtaenda kununua saa ngapi Geb bwana!? Mbona unataka kuniharibia mambo!” “Sikiliza mama G. Mimi na Oliva tunakimbia kazini mara moja tu. Kuna mzigo unaingia asubuhi hii.  Baada ya muda mfupi tu, narudi. Eti Liv? Utamsindikiza dad?” “Ana kazi ya kucheka tu huyo mwanao. Ukimuogesha, anacheka. Ukimlisha ndio kabisaa. Atacheka mpaka chakula kinatoka mdomoni.” Geb akambusu. Liv akacheka tena.

“Eti mama? Wewe unacheka tu. Huna tatizo na mtu?” Geb akambusu tena. “Naona unazidi tu kupendeza. Umemwambia bibi asante? Haya, twende tukampe bibi busu la asante.” Akaenda kumbusu mama yake kichwani mara mbili. “Hili la Liv, na hili langu.” “Nataka kutoka kwa Oliva mwenyewe.” Geb akamuinamisha mwanae shavuni kwa bibi yake. Olivia akamlamba. Wote wakacheka. “Shavu zima limejaa mate!” “Hapo ndio nimefurahi. Mwache anipake mate atakavyo.” Mama G akajibu akisikika kufurahia busu la Oliva. Geb akambusu tena Liv, kisha akatoka naye nje.

“Twende kwa mama. Akupe nyonyo, halafu tukatafute pesa.” Mama G aliwasikia wakiongea. “Kanywa uji huyo!” Mama G akajibu yeye akiwa bado chumbani. “Mimi ratiba zenu zinanichanganya. Kwa hiyo mwanangu nyonyo ndio basi?” “Sasa mama yake mwenyewe haonekaniki, nitafanyaje? Nikampa uji.” Geb akacheka bila kujibu. Tokea walipoamka walikuwa na Nanaa chumbani. Hakuna aliyemkumbuka mtoto. Hata usiku walimuacha akalala chumbani kwa bibi yake.

Geb akatoka chumbani akiwa yeye, Nanaa na mtoto wao. “Basi hivyo, hamtakaa mkarudi leo. Sasa hapo Nanaa wewe anaenda wapi?” “Kwenda kunyonyesha, mama.” Geb akajibu kwa haraka. “Mmmh!” Akaguna. “Tunarudi mama, usiwe na wasiwasi.” “Naomba uwahi Geb. Tafadhali sana. Nina week moja tu ya maandalizi ya hiyo mahari. Sitaki unitie aibu. Nataka upate muda wakutosha kwenda madukani utafute vitu vya maana. Kama unaona hutaweza mimi nitaenda mwenyewe.” “Mama! Nimekwambia sitachelewa kurudi. Usiwe na wasiwasi. Nitaenda kununua vitu vyote. Na ninakuahidi nitakuletea vitu vizuri kabla usiku hujaingia.” Mama yake akanyamaza. “Sasa mbona huniitikii?” Geb akamuuliza huku akicheka. “Nitakuona kama utawahi!” “Sikudanganyi bwana mama. Acha wasiwasi. Nanaa twende.” Wakatoka.

~~~~~~~~~~~~

Na kweli kabla ya saa nane mchana, Geb akarudisha familia yake nyumbani. “Mimi nipo tayari Danny. Naomba unisindikize.” Danny akasimama. “Mbona hamli?” “Acha tu twende. Tutakula tukirudi. Usiwe na wasiwasi. Ngoja tuwahi wakati hao jamaa wamelala. Nitafanya haraka kurudi ili wakiamka wanikute.” Danny alijibu akimaanisha wanae. Fillius na Fillan. “Sitaki mniletee vitu vya ajabu.” Mama G akasisitiza. “Mbona unarudia rudia mama? Tushaelewa!” Geb alimjibu mama yake wakati anatoka. “Sitaki unitie aibu.” “Sawa Mama G.” Geb alijibu huku akifunga mlango. Wakatoka kwenda madukani. 

Vitenge na mablangeti alisema atanunua Mama G mwenyewe. Akawatuma kwenda kuleta vitu vingine vyote vilivyobaki kwenye hiyo orodha ya mahari ya Nanaa. Walimkusanyia vitu vyote vya hiyo mahari, wakamletea pale nyumbani. Mama G alianza kupitia ile orodha. Aliweka alama ya tiki kwa kila kimoja wapo. Akakuta vyote vipo. Akaanza kuangalia ubora wake, pia akaona wameleta vitu vizuri. Akaridhika. “Sasa hapa naenda kununua mimi mwenyewe vitenge vya maana na mablangeti. Tena mablangeti ya nguvu.” Mama G aliongea wakati anaweka vitu vizuri. Angalau Nanaa akafarijika zaidi kuona mama mkwe wake pia hamuoni mzigo. Yupo bega kwa bega kuhakikisha mafanikio bora.

Siku Ya Kulipa Mahari Ya Nanaa.

Ilikuwa siku ya jumamosi ambayo mama yake James alisema angekuwepo hapo nyumbani kwa James kupokea mahari ya Nanaa. James alipotaka baba yake na bibi wahusishwe, angalau hata kuhudhuria kushuhudia upokelewaji huo wa mahari, mama yake alikataa tena akiwa mkali akisema alimlea Nanaa yeye mwenyewe bila msaada wa mtu, kwa hiyo atapokea hiyo mahari yeye mwenyewe. James hakutaka ugomvi. Akaona akubali, yaishe. 

Alitoka asubuhi akiwa anaelekea kazini kama kawaida siku ya jumamosi kufanya kazi nusu siku, kisha alipanga kupitia kwenye biashara zake, akiwa amekubaliana na Grace aandae watu wakupika, catering, ili hiyo jioni walete chakula hapo nyumbani kwa James ili wanapomaliza shuguli za mahari, basi waliohudhuria wapate chakula cha pamoja, kwa kuwa alimjua mama yake hawezi kuwapikia wageni wa Nanaa.

~~~~~~~~~~~~

Danny alishatuma kwenye group lao la marafiki kuwa jumamosi hiyo watakwenda kulipia mahari ya Nanaa. Chakushangaza wakaona watu wengi wanatoa mwitikio. Wengi walikubali kuhudhuria na kuwapongeza Nanaa na Geb huku wakiendelea kuuliza ni nini cha kusaidia ili kufanikisha shuguli hiyo nzima ya mahari, lakini Danny aliomba uwepo wao tu, nakuwashukuru.

~~~~~~~~~~~~

Ilipofika saa 11:45 jioni, James akarudi nyumbani kujiandaa na mapokezi ya wageni. Walikuwa wamekubaliana wafike hapo saa 12:30 jioni hiyo. Alikuta nyumba chafu kama kawaida, akasafisha haraka haraka. Mpaka anamaliza kuosha vyombo walivyokuwa wametumia usiku uliopita na kusafisha nyumba, tayari wageni walikuwa wamefika. Marafiki wote na wake/waume zao walikuwepo pale. Wafanyabiashara wenzake wa karibu na Geb, Mama G, Grace, Danny, na marafiki, wafanyakazi wenzake Danny na James, wote walifika kwa wakati. Nanaa alibaki kwenye gari na Oliva. Mama G aliwaambia wasubiri mpaka wakimaliza kulipa mahari ndipo wataenda kumchukua kwenye gari na kwenda kumtambulisha Liv ramsi kwa mama yake James.

“Ngoja nimuite mama, maana na mimi ndio nimeingia hapa muda sio mrefu.” James aliaga wageni akiwa vilevile mchafu na akionekana alikuwa na shuguli nyingi hapo ndani. Kwanza shati lake lenyewe lilikuwa limelowa. Aliingi kwenye chumba walichokuwa wakilala mama yake, dada zake hao wawili na mtoto wake Viola, lakini hakuwakuta. Alikuta tv ndio iliyokuwa ikiongea muda wote aliodhani wapo chumbani wamejilaza huku wakiangalia tv kama kawaida yao. Kumbe waliacha tv ikiendelea bila wao.

James akaizima, na kuamua kumpigia simu mama yake. “Wageni wameshafika, mama. Uko wapi tena!?” “Nyumbani kwangu.” James akatulia kidogo, akitamani asiwe amesikia alichosikia. “Unamaanisha Moshi!?” “Kumbe nina nyumba ngapi? Isingekuwa kumlea Nanaa labda sasa hivi ningekuwa na nyumba hata tatu!” “Si ulisema leo ndio waje kutoa mahari ya Nanaa, kwa nini unafanya hivyo mama jamani!?” “Kumbe sikuwa nimekwambia? Niliamua leo kuja kumuona baba yako. Hatujaonana muda mrefu, nina hamu naye.” “Yaani hamu hiyo ya baba inatokea siku ya kupokea mahari ya Nanaa!?” James akauliza.

“Hamu ni hisia. Umenisikia James? Huwezi kunipangia lini niwe na hamu na baba yako na lini nisiwe na hamu naye. Unataka nijenge kwa watu wakati kwangu kunabomoka? Shika adabu yako. Nikikwambia Nanaa amekuloga, huamini. Ona..” James akakata simu, na kubaki amesimama ndani ya kile chumba, asijue kuwa wageni wote walikuwa wakisikiliza. 

Watu wachakula walishakuja,  walikuwa wakisaidiana na Grace kupanga vyakula mle ndani. Grace aliposikia yale mazungumzo, akabaki ameduwaa. Akamwangalia Danny aliyekuwa amekaa na Fili huku akisukuma mapacha wao kwenye kigari chao. Wakajikuta wanaangaliana. Wote wakamgeukia mama yao. James akatoka hajui awaambie nini wenyeji wake, lakini Mama G akamuwahi. “Jiandae, kesho asubuhi tunakuja kukuchukua, tunaenda kumfuata mama yako huko Moshi. Unanisikia James?” “Ndiyo mama.” “Saa kumi na nusu asubuhi, tunaanza safari. Tunakwenda Moshi.” Mama G akasimama.

“Samahanini sana jamani.” James alikuwa ameishiwa nguvu kabisa. “Watakao weza kula mle, Grace utatuletea chakula nyumbani. Twende tukajiandae na safari ya kesho, Geb.” Mama G alikuwa amekasirika sana, akataka kutoka, lakini Malii akamuwahi. “Mama! Mimi na mke wangu tutawasindikiza. Tutakuja kumpitia James hapa nyumbani kwake asubuhi sana kama ulivyosema. Halafu tukutane Kibaha.” Kidogo mama G, akatulia.

“Asante Malii mwanangu. Nakushukuru.” “Na sisi tutawasindikiza. Tutageuza kesho kutwa jumatatu.” Wengi wao wakaonyesha utayari wa kuungana nao. Wakakubaliana kama kawaida yao, wakutane Kibaha ndipo waongozane mpaka Moshi. Mama G akatoka. Geb akafuata nyuma bila yakuweka neno hata moja.

Alipofungua mlango wa gari tu, Nanaa akamuwahi. “Tayari mama?” Nanaa akauliza na tabasamu usoni, mara akashangaa Geb anaingia kwenye gari akiwa amekasirika. Nanaa alianza kuhisi mambo hayakwenda sawa. James naye akatoka, Nanaa akashuka kwenye gari. “Kuna nini tena, kaka!?” “Mama ameondoka.” Nanaa akatulia kidogo. “Sijaelewa. Ameondoka kivipi?” “Yaani hayupo hapa. Waliondoka tokea asubuhi kurudi Moshi. Asubuhi nimeagana nao vizuri, na kuwakumbusha leo ndio siku ya kulipiwa wewe mahari. Tena nikawasisitiza angalau wanisaidie usafi. Lakini nimerudi kutoka kazini, sijamkuta mtu hata mmoja na nyumba chafu kuliko utakavyodhania.” Nanaa aliumia sana. 

Akaanza kulia na kushindwa kujizuia. Akazunguka nyuma ya gari akiendelea kulia. Alilia mpaka Geb akashuka kwenye gari. Mama G akamfuta na Grace naye akatoka, akasikia kilio cha Nanaa kule nyuma ya gari, akamfuata. James naye akamfuata. Wakajikuta wote wamesimama nyuma ya gari hiyo na Nanaa akiendelea kulia kwa uchungu sana. “Ngoja nikwambie Nanaa, kesho asubuhi tunakwenda Moshi kuwafuata. Na kesho tutalipa hiyo mahari yote waliyotaka. Wawepo, wasiwepo, tutaiacha hiyo mahari nyumbani kwao. Na James, waambie wazazi wako, Nanaa ataolewa tu. Wawepo, wasiwepo, harusi itafungwa. Waache kutuchezea akili. Twende Nanaa ukajiandae na safari, kesho saa 10:30 alfajiri, tupo barabarani.” Mama G akaongeza.

 “Pole sana Nanaa. Usilie. Sisi tupo na wewe, naamini kila kitu kitaenda sawa. Acha kulia kabisa. Tulia. Turudini nyumbani. Tule, tupumzike mapema kwa ajili ya safari kesho. Mungu yupo upande wetu. Hakika tutafanikiwa tu. Usilie.” Grace naye akamtuliza.

Safari ya Moshi tena.

Safari hii ni Nanaa&Geb.

Kama alivyosema Mama G, ilipotimia saa 12 asubuhi, tayari walikuwa wameshaliacha jiji la Dar, wakielekea Moshi nyumbani kwao kina James. Yalikuwa magari 13 ya ndugu, jamaa na marafiki walioungana na Geb kwenda Moshi kulipa mahari. Geb aliendesha gari lake kubwa, lililoweza kubeba familia nzima. Alikuwepo Geb mwenyewe, Mama yao, Danny, Fili, Grace, Nanaa, Liv, Fillius na Fillan. 

Safari ilikuwa nzuri na wakafika Moshi mapema tu. James aliwasaidia kupata hoteli nzuri, walitua mizigo yao hapo hotelini, ndipo wakaelekea tena nyumbani kwa kina James. James akiongoza msafara mpaka nyumbani kwao. Ilikuwa ni saa 6 mchana wakati wakiegesha magari nyumbani kwa kina James. Kama ilivyokuwa Dar, Mama G alimwambia Nanaa na mtoto wasubiri kwenye gari. James akawakaribisha ndani, wakawakuta wote wamekaa sebuleni wanaangalia tv.

          “Kwa nini umeleta watu huku nyumbani bila taarifa!?” Mama yake akashituka sana. Hakuna kati yao aliyetegemea huo ugeni. James aliamua asiwataarifu  tena kuhofia kutorokwa. “Naomba utulie mama, tumalize hili swala. Hawa watu wote wamekuja hapa wakitaka kulipa mahari ya Nanaa tu. Naomba tuwakaribishe.” “Unanivunjia heshima. Unaleta wageni nyumbani kwangu bila taarifa!? Halafu unaniingilia ratiba zangu. Sasa hivi nataka kuanza kupika.” “Tutasubiri.” Akadakia Mama G. 

“Hakuna mwenye haraka hapa. Kilichotuleta ni ile heshima tuliyonayo kwa Nanaa na kwenu, basi. Kwa hiyo sisi tutasubiri mpaka umalize shuguli zako zote, tukulipe hiyo mahari.” Mama G akaongeza. “Ni vile hamjamjua huyo Nanaa.” Mama yake James akaanza. Kwa kuwa walikuwa wengi, na wenyeji hawakuwapisha viti, wengi walibaki wamesimama wakisikiliza. James alionekana kuumia mpaka uso wake ulionyesha.

“Mimi namjua Nanaa ndio maana nimesita kupokea mahari yake. Nanaa ni kama mtoto niliyemzaa mimi mwenyewe. Amenyonya haya maziwa, tokea anazaliwa mpaka leo. Namfahamu vizuri sana. Sitaki kuja kudaiwa baadaye mkimrudisha. Nanaa ni mchoyo sana. Ana roho mbaya hawezi kuishi na watu. Mvivu, hatumiki. Kiburi kimemjaa mpaka kwenye kope! Ana kasoro kubwa sana ambayo hakuna mwanaume aliyekwisha lala naye akarudia. Kwanza hazai. Alikaa na mwanaume, akamuacha sababu ya kutoshika mimba. Huyo mwanaume akalala na Viola mara moja tu, mwenzake amezaa. Nanaa..” “Samahani Mama James.” Mama G akamkatisha.

“Mimi ni mama yake Grace na Geb ambaye ndiye mwenzie Nanaa. Wananiita Mama G. Mama G anatabia yakutopenda kuzungushw...” “Kwani....” Mama James alitaka kumkata. “Nimekuomba samahani ili unisikilize. Tafadhali nyamaza. Hawa vijana wote unao waona hapa wengi ni wanangu wakuwalea tokea kina Grace wapo watoto. Tunaheshimiana sana. Na hawa vijana ni watu na majukumu yao ya msingi sana. Nisingeruhusu wamsindikize mwenzao Geb kuja kulipa mahari ya  Nanaa, kama simfahamu vizuri Nanaa.” Mama G akaendelea.

“Kama hufahamu, nimeanza kumuombea mke wa Geb, tokea Geb anazaliwa. Nimekuwa nikimsihi Mungu kwa kufunga na kuomba kwa ajili ya mke wa Geb, tokea sijakutana na Nanaa. Nataka ufahamu kuwa, ninaishi na Nanaa nyumba moja. Namfahamu vizuri sana Nanaa. Na mimi kama mama yake Geb ninakwambia wazi, ni Nanaa peke yake ndiye mwanamke ninayemuona anamfaa Geb, mwanangu. Kasoro za Nanaa zote unazozifahamu ujue ni kosa langu mimi. Kwamba sikumuombea vizuri. Inawezekana kuna mahali nilikosea kuomba. Kwa kuwa sio jana au juzi nilipoanza kumuombea mke wa Geb. Kama nilivyokwambia ni miaka na miaka nilikuwa nikimuombea huyo Nanaa. Naomba nikuhakikishie kabisa, usiwe na wasiwasi juu ya mapungufu ya Nanaa. Niachie mimi kwa asilimia zote.” Mama G alikuwa akiongea kwa kujiamini. Watu wote walikuwa kimya.

    Kisha akaendelea. “Unaona hao vijana wote hao waliosimama hapo mbele yenu? Nimekuza wote hao. Wengine walikuwa yatima, na wengine wazazi wao walikuwa wapo mikoani kama James. Wananiita mama si kwa heshima tu. Ni kwa kuwa nimewalea kama wanangu. Kwa miaka zaidi ya 6 waliyokuwa shule ya sekondari mpaka wanamaliza chuo kikuu, nilisimama nao mimi kama mama. Waliokuwa wakilazwa hospitalini nilikuwa nikiwahudumia mimi mwenyewe mpaka wanapona. Waliishi kwangu kama vile huyu Geb alivyokuwa akiishi kwangu mpaka wanamaliza chuo, tena wakiwa vijana. Lakini nilihakikisha wote wanamaliza chuo, na wanakazi bila hata kuwafahamu wazazi wao." Mama G akaendelea.

“Wote hao wamesimama hapo, kama wanangu wakuwazaa. Mmoja wao akipatwa na tatizo hapo, ni langu. Kabla hawajapigia simu wazazi wao mkoani, wananipigia mimi simu kwanza. Akiwepo mwanao James. Aibu ya mmoja wao hao wote ni aibu yangu mimi. Wala siwezi hata kutangaza ubaya wa mmoja wao hao, kwa mwenzake. Nabeba huo ubaya mimi mwenyewe nikimsihi Mungu aingilie kati na kuhangaika nao hao mpaka tatizo linaisha. Kuna waliooa na wana watoto. Ndoa zao zikiwa na matatizo, nahakikisha zinarudi kuwa na amani, mimi kama mama yao bila hata kuwasiliana na wazazi wao. Nahangaika nao mchana na usiku hao vijana wote na watoto wao wananijua mimi kama bibi yao. Vitoto vyao vimezaliwa mikononi mwangu na kulea mpaka vinakatika vitomvu, mimi nalea.” Mama G akaendelea.

“Na hao unao waona hapo ni wachache. Wapo wengi tu na wengine hawapo hapo wapo safarini kikazi. Ni kina baba, na wanawake na nyazifa walizozipata chini ya uangalizi wangu. Hapa ninachojaribu kukwambia ni kuwa, HAWEZI kunishinda huyo Nanaa, mtoto wa juzi tu! Sasa nataka utujibu swali moja tu ili tusizidi kukupotezea muda. Unapokea mahari ya Nanaa, au hupokei, tuondoke? Na ujue kabisa, Nanaa ataolewa na Geb. Mpende, msipende, Nanaa ataolewa na Geb. Pesa yote mliyotudai ya kumlea Nanaa humu ndani, tumekuja nayo. Mpaka malipo uliyotaka tukulipe kwa Nanaa kunyonya ziwa lako pia tumekuletea. Kwa hiyo naomba utuambie tunatakiwa kufanya nini ili tusizidi kuwapotezea muda wenu, muendelee kuangalia tv.” Kulizuka ukimywa mkubwa hapo kama hapakuwa na mtu. 

~~~~~~~~~~~~

Baba yake James alimwangalia mkewe. Wazi alionyesha kushangazwa na alichokisema mama G, mwishoni. Yule mama alijua wazi mumewe anamwangalia, lakini akakwepesha macho. James pia alikuwa amesimama. Hakupata sehemu ya kukaa. Nyumba ilikuwa chafu, kama hapakuwa na mtu aliyekuwa akiishi humo ndani. Wakati wanawake watatu wapo hapo wamekaa mbele ya luninga, wametulia kana kwamba hawaoni nzi waliokuwa wakizunguka mle ndani. Nzi walikuwa wamejaa. Na wenyeji walionekana hawana neno nao kabisa. Harufu ya kinyesi cha ng’ombe iliyokuwepo hapo ndani, utafikiri wapo kwenye banda la ng’ombe au ng’ombe wanaishi humo ndani.

~~~~~~~~~~~~

Mama G alipoona wapo kimya, akaamua aendelee. “Haya, Gozibeth  na Danny, kaleteni vitu vyote tulivyoleta vya mahari.” Gozi na Danny wakatoka na vijana wengine wawili. Wakaanza kuingiza vitu mle ndani. Baada ya muda mfupi sebule ikawa imejaa vitu vizuri na vya thamani. Vyote mama G alifanya kwa ajili ya Nanaa. “Asanteni sana.” Mama G akawashukuru wale vijana waliokuwa wakiingiza mizigo ndani. Akamgeukia Geb. “Haya Geb! Toa hiyo hundi ya pesa yote waliyodai uwalipe kwa kumlea Nanaa humu ndani na hundi ya pili ya kumalizia mahari ya Nanaa. Ng’ombe mtanunua wenyewe. Weka hapo kwenye meza.” Geb akatoa bahasha, akaweka mezani. 

“Sasa hiyo yote ndio mahari na malipo yakumlea Nanaa, kama mama James ulivyomtuma James. Mkiamua kuitunza sawa, mkiamua kutupa pia ni sawa tu. Ila nawahakikishia hakuna atakayekuja kuwadai hata kitu kimoja wapo hapo au hata shilingi. Fanyeni kile mtakachotaka kwenye hiyo mahari na hayo malipo ya Nanaa. James atawapa tarehe ya harusi ya Nanaa na Geb.” Mama G alikuwa akiendesha mambo yeye mwenyewe. 

“Gozi, nenda kaniitie Nanaa na Oliva.” Gozi akatoka kwa haraka, baada ya muda akarudi na Nanaa na Oliva. Mama G akamgeukia Nanaa, “Nanaa, unawatambua hawa?” “Ndiyo. Shikamoo mama mkubwa na baba mkubwa.” Nanaa alijibu na kusalimia, akiwa bado amesimama huku amembeba mtoto wake. Gozi alipotaka kumbeba Liv, akakataa. Akazidi kumng’ang’ania mama yake huku akijificha. Akamuona bibi yake akaanza kucheka akiwa amebebwa na mama yake. Akanyoosha kimkono chake akitaka bibi yake ambembe yeye. Mama G akasogea akambeba na kumbusu.Liv akacheka.

  ~~~~~~~~~~~~

Alijazwa dhahabu huyo mtoto! Masikioni, mkononi, shingoni na kacheni kadogo alivalishwa cha mguuni. Kazi hiyo ya bibi yake. Nanaa naye alikuwa amependeza sana. Aliachia nywele alizokuwa amesukwa, akafanana na Liv kiasi, hasa rangi. Nywele za Olivia walizichana tu. Zilikuwa zimejaa na kujifinyanga kama mtoto wa kiarabu. Bibi yake aliweka ua pembeni ya kichwa chake. Hakuwahi kumkata nywele tokea anazaliwa zaidi ya vincha vya juu tu. Na vile alivyokuwa akicheka, alipendeza sana. Nanaa alivaa gauni zuri sana. Refu mpaka chini. Hakika alipendeza. Usingeweza kujua kama ni Nanaa yule aliyekuwa akiishi hapo ndani kama mfanyakazi wao. Akiwatumikia mchana na usiku.

~~~~~~~~~~~~

Hakuna aliyeitikia salamu ya Nanaa. Ukimya mwingine ukazuka. “Kuna chochote tumesahau?” Mama G alivunja ukimywa kwa kumuuliza swali James. “Sidhani mama. Nashukuru sana kwa kuja na kwa heshima mliyoweka kwa Nanaa. Mungu awabariki.” James alimsogelea Geb akampa mkono. “Geb! Nakushukuru sana.” “Asante James. Nashukuru kwa kila kitu. Na samahani kwa usumbufu.”  “Hata kidogo. Hujui ni kiasi gani nimefurahi. Nawashukuru sana.” Akamsogelea mama G. “Asante sana mama yangu, kwa kumpokea Nanaa. Na samahani kwa usumbufu wote uliojitokeza. Mungu azidi kukubariki.” “Amina James mwanangu. Na mimi nakushukuru kwa kusimama na sisi kuhakikisha tunampata Nanaa. Asante kwa kutuamini naye.” Wakapeana mikono. Wazazi wake hawakusema lolote. 

“Haya wanangu, twendeni.” Walio pata nafasi yakukaa wakasimama wote kwa pamoja. “Na huyu hapa kwa Kiitaliano anaitwa Olivia, Kiswahili Oliva, nyumbani anaitwa Liv. Ni mtoto wa Nanaa na Geb. Kwa hiyo jamani, mgumba amezaaa!” Mama G akaongeza tena huku akimbusu Oliva aliyekuwa akicheka. Alipomuona tu baba yake, akataka ambembe yeye. Geb akamsogelea mwanae. Akambusu akiwa bado amebebwa na mama yake. Olivia akanyoosha mikono kama anamwita baba yake. Geb akampokea. “Twende Nanaa.” Nanaa alitoka huku akilia. “Wala usilie mwanangu. Mungu yupo na wewe, utafanikiwa tu.” Mama G alisikika akimliwaza. Grace hakuwa ameongea neno hata moja tangia aingie humo ndani. Alikuwa kimya kabisa akiangalia na kusikiliza kama wengine.

Baada Ya Mahari.

Hakuna jinsi ungeeleza furaha ya Nanaa na Geb mara baada ya mahari. Waliporudi tu hotelini, Geb na Nanaa wakakimbilia chumbani kwao bila kuaga mtu, tena kama walijiiba. Geb alimshika tu mkono, Nanaa akaelewa. Wakaondoka kimya kimya mpaka chumbani. Wakajitupia kitandani wakiwa na furaha zote. “Asante Geb. Nashukuru kwa kunilipia garama yote hiyo. Najua sistahili. Asante.” “Nani anastahili sasa?” Geb akamvuta karibu. “Kwanza kuanzia leo, wewe ni Nanaa Wini Magesa. Na baada ya harusi tu, tunaenda mahakamani kubadilisha rasmi jina lako. Na wewe utatambulika rasmi kama Magesa, kama vile mimi na Liv.” Nanaa akacheka.

“Nimefurahi tumekamilisha. Na ninamshukuru Mungu kukupa uwezo Geb. Kama isingekuwa hivyo, sijui ingekuwaje?” Nanaa aliwaza kidogo. “Acha kufikiria mawazo ya ingekuwaje. Hili limekamilika. Tufikirie lijalo.” Wakati wanaanza kupeana mabusu wakasikia mlango unagongwa. Geb akakunja uso, akasimama kwenda kufungua.

“Nataka tumshukuru Mungu pamoja. Tusijisahau jamani! Huyu ni Yesu ndio amefanya.” Alikuwa mama G na Liv. Geb akampokea mtoto wake. “Ni kweli mama.” Wakatoka mpaka sehemu ya mapokezi. Wakawakuta watu wote wamekusanyika pale. Ndipo akaona huo ndio wakati muafaka kuwashukuru wenzie. Aliwashukuru kwa kujitoa kwao bila kuchoka. Kuacha shuguli zao zote na kumsindikiza mpaka hapo Moshi. “Nawashukuru sana.” Geb akamaliza. 

Wakashikana mikono, mama G, akamshukuru Mungu. Hakuacha kumkumbuka Zinda. Alimuombea amani na faraja huku akitubu kwa Mungu kwa chochote alichomkosea. Wakamaliza. Danny naye akashukuru na kuongeza. “Jumamosi ijayo tunaanza kikao cha kwanza cha harusi. Nitatuma kwenye kundi. Naombeni wote mkaribie nyumbani kwetu. Muda nitawajulisha.” “Wapi? Kwako Danny au kwa Geb?” Gozi akauliza. “Kokote alipokuwepo mama G, hapo ndipo nyumbani kwetu wote sisi. Kwa hiyo ni Tabata Barakuda, hapo ndipo tutakutana.” Si mama G tu aliyefurahia lile jibu, hata mkewe alionyesha usoni. Grace akamwangalia mumewe, akanong’ona. “Asante.” Danny akacheka. Akapa busu la mdomoni.

Ilipofika kama mida ya saa moja kasoro usiku wakiwa wanaongea na kucheka, James aliwafuata pale hotelini. “Jamani, nimeshindwa kuvumilia. Naomba tutoke wote tukasherehekee kulipiwa mahari kwa dada yangu. Twendeni sehemu tukale na kunywa. Nimepaandaa kwa haraka haraka, hapatafanana na hadhi yenu. Lakini sitaki mtoke hapa kwetu bila kula. Hii siku niliisubiria kwa hamu sana.” Mama G akaanza kupiga vigelegele.

“Mama wewe! Unasumbua wageni wengine! Ona watu wote wamekugeukia wewe!” Mama G hakuacha. Watu wote walikuwa wakicheka. Wakamalizia vinywaji walivyokuwa wakinywa pale pale hotelini sehemu ya nje, wakamfuata James nyuma. Alifika hapo hotelini na taksii, lakini akaondoka na gari la Malii. Walikuwa wamemuacha James nyumbani kwao tokea mchana walipoenda kulipa mahari.

James alitafuta mgahawa mzuri tu. Akawaomba wapike chakula kidogo na kizuri kwaajili ya wageni wake. Alitoa oda ya nyama choma. Alinunua mbuzi mzima kwa ajili ya shuguli hiyo. Akawaambia wamtengeneze kwa haraka, pamoja na  ndizi za kuchoma na kukaanga. Akataka waongeze na kuku na mishikaki kidogo ya nyama ya ng’ombe. Wakaingia humo ndani, wakaanza kusherehekea. Hakuna ambaye hakuwa na furaha siku hiyo. Walicheza kila mziki uliokuwa ukiwekwa ndani ya huo mgahawa aliowaandalia James. Utani ukaendelea, vigelegele vya mama G, havikukoma. Basi ikawa ni shangwe na kumshukuru Mungu.

~~~~~~~~~~~~

Walirudi Dar, salama.  Walipoingia tu ndani, Geb akaomba ushauri. “Nimefikiria, naona nimtafute Zinda na Liz nizungumze nao. Zinda tumetoka naye mbali sana. Nisingependa akose kitu muhimu kama hiki. Na yupo sahihi, alikuwa kwenye maisha ya Danny wakati mimi nilipokuwa nchini India. Sitaki wakosane sasa hivi kwa ajili ya mapenzi yangu kwa Nanaa.” “Utamwambia nini Zinda!?” Grace akamuuliza.

“Sijui G. Labda nitaanza kwa kumuomba msamaha, na kujibu chochote atakachotaka kujua. Lakini naona maisha yetu hayapo sawa bila Zinda. Najihisi tumepoteza ndugu wa damu.” “Lakini ujiandae Geb. Zinda anahasira sana na wewe.” Danny alimtahadharisha. “Mimi naungana mkono na Geb. Amtumie ujumbe kabla ya jumamosi, amuombe wakutane. Ikitokea anakubali wakutane, basi ujue atakusikiliza. Asipotokea, ujue bado ana hasira. Muache kwanza.” “Sawa mama.” Wakaagana baada ya kuomba kwa pamoja, kila mtu akaelekea chumbani kwake.

Geb alimuona Nanaa amenyamaza. Akaongeza ubusy usio wa kawaida. Aliondoka pale chumbani akaenda chumbani kwa mama G akaanza shuguli kwa mwanae ambazo alikuwa akifanya mama G wakati wote! Aliingia hapo chumbani na kutoka. Akifanya hili na lile bila kumaliza. Mama G alibaki akimtizama. Akajua tu lipo jambo. Geb akashuka kumfuata.

“Leo Liv analala chumbani kwake kule juu?” Geb akauliza. “Sijui mama.” Akajibu kinyonge, akatoka. Oliva alishakuwa tayari kwenye kitanda chake. Alivalishwa nguo zake za kulalia akawa anazunguka tu hapo kitandani kwake chumbani kwa bibi yake. Aliposikia tu sauti ya baba yake, akasimama. “Ana usingizi huyo. Ungechelewa kuingia tu hapa, angelala. Naombeni mumuage, mtoke humu ndani kwangu. Naona shuguli haziishi na mimi nimechoka.” Mama G akajinyoosha kitandani kwake. “Na huyo Oliva analala hapo hapo. Haendi kokote kule.” Mama G akaongeza. Kimya.

Nanaa akahamia kwenye kazi nyingine. Akaanza kukunja nguo za mwanae kabatini bila kujibu kitu wala kumwangalia mtu. “Basi leo hatutalala!” Mama G akamrushia hilo neno. “Namalizia tu mama.” “Sasa kwa nini utoe nguo zilizokwisha pangwa huko kabatini sasa hivi wote tumechoka, halafu uanze kuzipanga upya? Si utoke tu ukazungumze na huyo Geb yaishe?” Nanaa akaendelea kupanga zile nguo bila kujibu, Geb akabaki akimwangalia. Na kweli nguo zote zilikuwa zimepangwa vizuri tu, wala hazikuhitaji kuguswa.

“Wewe Nanaa?” “Namalizia tu mama.” “Huna unachofanya hapo. Mimi nakujua bwana. Wewe nenda kazungumze na mwenzio, mtuache mimi na wajina wangu tulale. Maana naona mnakaribia kumtoa humu ndani. Haya Geb, naomba niwekee mtoto hapo kitandani. Ongoza njia, Nanaa atafuata.” Geb akambusu mwanae mara kadhaa akamuweka kitandani akiwa ameshalevya na usingizi vyakutosha.

“Twende Nanaa.” “Bwana eeh! Nimekwambia utangulie, atakufuata. Mbona hivyo!?” Geb akamwangalia Nanaa, akamuona amejificha nyuma ya mlango wa kabatini kama aliyetingwa na shuguli nyingi huko ndani kabatini. “Nenda wee!”  Mama yake akamfukuza Geb. “Sawa mama, usiku mwema.” Geb akatoka. “Haya na wewe njoo hapa.” Nanaa akatoka pale kabatini akaenda kukaa kitandani kwa mama G. “Sitaki Geb aonane na Liz.” Nanaa akaanza kuongea tu mara baada ya kukaa. “Mpaka lini?” Mama G akamuuliza taratibu. “Sijui mama. Lakini mimi simtaki kwenye maisha ya Geb.” Mama G akatulia kidogo.

“Anamtaka mpenzi wangu mpaka leo! Wakikutana wawili tu halafu akamfanyia vituko? Mimi simwamini akiwa naye peke yao. Hata kama asipomsamehe Geb, basi. Lakini mimi simtaki na sitaki Geb awe karibu naye tena.” “Nitamwambia Grace yeye ndio amtafute azungumze naye kwanza. Kama ataelekea, ndipo Geb naye aungane nao. Nafikiri wazo lako sio baya. Awepo Grace kwenye mazungumzo yao ili kuwekana sawa.” Nanaa akacheka.

“Una wivu wewe!” “Wewe umemsikia Danny anavyosema shetani ni kama simba angurumae. Akimrarua Geb wangu?” Mama G akacheka sana. “Kazi ipo.” “Wala si ndogo. Hivi unajua na jina nishabadilishwa? Nasubiri baada ya harusi tu, nikaape mahakamani.” Nanaa alianza kujisifia. “Ndio utakuwa ukiitwa nani tena mwenzangu?” Mama G akauliza huku akicheka. “Nanaa Wini Magesa!” “Mwenyewe huyoo!” “Kwa raha zangu!” Nanaa akaendelea kujisifu. “Halafu wanipokonye tonge mdomoni? Akuu! Waniache mie Nanaa mtoto wa Wini!” Mama G aliendelea kucheka. 

“Hakuna baya ningefanya Nanaa! Kwanza ningehakikisha nakutana naye sehemu ya wazi.” Geb aliingia wote wakashangaa. Kumbe alikuwa nje ya mlango akiwasikiliza. “Kwanza wewe unaongeaje mambo yako na watu wengine kabla hujazungumza na mwenzio!?” Mama G akamjia juu Geb. Akamgeuka hapo hapo na kicheko kikamwisha usoni. “Nilijua ni wazo zuri.” Geb alijitetea kwa mama yake.

“Yaani wazo zuri la kwenda kumtafuta mpenzi wako wa zamani. Aliyekuwa hanipendi na ananidharau mbele za watu. Unaenda kumbembeleza akubali wewe unioe mimi!” Kimya. Lile swali likaingia kwa Geb na mama yake. Wakabaki wakitafakari. “Kwanza unaenda kumbelezaje!?” “Sio kumbembeleza Nanaa!” “Mimi naona nibakie mimi mwenyewe tu. Wewe nibembeleze mimi tu basi.” Mama G akaanza kucheka.

“Usicheke mama bwana! Sasa yeye anataka kumfurahisha Liz wa nini, kwa mfano?” “Sio kumfurahisha Nanaa! Nikutafuta kuwa na amani.” Nanaa akanyamaza. “Mimi naona tuanze kutafuta amani ya humu ndani kwanza.” Mama G akaongeza. “Sio kwanza mama. Tutafute amani ya humu ndani tu.” Mama G akacheka tena. “Na amani ya nje?” Nanaa akapandisha mabega kukataa. Mama G akazidi kucheka. “Hakuna kutafuta amani na Liz. Mwache kabisa.” “Sawa Nanaa.” Nanaa akaanza kucheka. “Umefurahi sasa?” Mama G akamuuliza. “Mimi nataka kubakia peke yangu kwa Geb, mama.” “Upo peke yako na utabakia peke yako daima, Nanaa.” “Hapo nimefurahi. Sasa hivi twende.” Mama G alicheka mpaka machozi. “Kazi ipo!” “Hamna bwana mama!” “Naombeni muondoke mniache nilale.” Geb na Nanaa wakatoka huku wakicheka.

Bado Kulia Wivu.

Walipoingia tu chumbani, Geb akamtumia ujumbe Zinda kumuomba wakutane kesho yake. ‘Kama ni pesa yako nitakuwekea benki. Acha kunisumbua.’ Hayo ndiyo majibu ya Zinda. ‘Sio maswala ya pesa Zinda! Nilitaka tuzungumze.’ Geb akajibu. ‘Unisimulie vile unavyomfaidi mwanamke wangu? Na Mungu anawaona. Atawalipisha siku si nyingi. Adhabu yenu inawajia.’ Geb akaona asiendele. Amwache. Zinda akatuma ujumbe mwingine. ‘Wewe si umeamua pesa yako ndio iongee hapa mjini? Na huyo Nanaa si anataka wanaume wenye pesa tu? Basi tutawaona mtakapofikia.’ Geb hakutaka kujibu tena. Akam block Zinda kila mahali. Akahakikisha anafungia mawasiliano yote ya Zinda yasiingie kwenye simu yake tena. Kisha akazima simu yake kabisa, wakalala. 

~~~~~~~~~~~~

Asubuhi kabla Geb hajatoka kwenda kazini, akamueleza mama yake majibu ya Zinda. “Basi mwache kabisa. Usimtafute tena.” “Nimemblock kila mahali. Nimeona anazidi kutuma jumbe za matusi na vitisho.” “Umefanya vizuri. Mpe muda. Labda atakuja kutulia tu.” Geb akatoka. Danny na Grace walisikia kila kitu. “Yaani Zinda ameamua kukataa ukweli kabisa jamani!?” Grace akalalamika. “Na sijui kwa nini anafanya hivyo, wakati anajua ukweli wote! Lakini kama alivyosema mama, tumuache tu.” Danny naye akaongeza na kutoka akielekea kazini.

~~~~~~~~~~~~

Juma hilo zima ilikuwa ni maandalizi ya kikao cha kwanza cha harusi ya Nanaa na Geb. Walihakikisha wanaalika watu wote wakaribu kwa kuwapigia simu. Wakapata idadi ya watakao hudhuria. Ndipo wakatafuta mtu wa kuwapikia chakula. Catering. Danny na Malii wakabakiwa na jukumu la vinywaji. Mama G naye alishamtafutia Nanaa nguo ya kuvaa usiku huo. Akabadilisha mtindo wa nywele. Akawa amependeza yupo tayari kwa siku hiyo maalumu waliyokuwa wakiisubiria kwa hamu kubwa. 

Siku Ya Kikao Cha Kwanza Ya Harusi Ya Geb & Nanaa.

Siku hiyo ilifika, kila mtu alikuwa na majukumu yake ya kukamilisha kuhakikisha kikao kinapoanza, mambo yanakwenda sawa. Wageni wao wakae sehemu nzuri, wale na kunywa kwa kusaza. Hata Geb hakwenda kazini siku hiyo. Alikuwa nyumbani siku nzima akiandaa sehemu ya kukutania watu. Walikodi viti na meza. Mpaka inafika saa kumi jioni, kila kitu kikawa kimekamilika.

Kwa mara ya kwanza mama G alimbana mjukuu wake nywele mafungu matatu. Oliva akawa amependeza sana. Kama kawaida yake, akamjaza dhahabu kila mahali. Ungependa kumwangalia. Alihakikisha hata Nanaa anapendeza. Muda wote wa hekaheka za maandalizi, alimwambia Nanaa apumzike ndani. Asifanye chochote. Kwa hiyo ilifika jioni Nanaa akiwa na uso uliotulia, kwa kulala siku nzima.

James alikuwa wa kwanza kufika. Nanaa akafurahi. “Nimefurahi umekuja kaka.” “Siwezi kukosa hata kidogo.” Waliendelea kutaniana Danny na James huku Geb akiwa anacheza na mtoto wake. “Anazidi kuwa mkubwa! Namuomba nimshike.” “Ana maringo huyo mtoto wa Geb! Sijui kama atakubali.” Grace akadakia. “Akimuona baba yake na bibi yake, hata kwa mbali vipi, mikono yote juu na kuanza kucheka. Lakini akija mgeni hapa, ananyamaza kimya. Ukimwita, ananyamaza kama sio yeye. Tena hata hakuangalii.” Wakacheka. 

“Mjaribishe kaka.” James akasimama. Ile kumsogelea tu, akajificha kwenye shingo ya baba yake, akanyamaza kimya. “Si nilikwambia? Tena anaweza kulala hapo hapo kwenye shingo ya baba yake.” Wakacheka. “Na hapo kwenye shingo ya baba yake hatoki mpaka bibi yake amtoe hapo.” Grace aliongeza. “Liv! Liv!” Geb akamwita, akamchungulia. “Nenda kwa anko.” Geb akawa kama anamvutia kwa James, akamuona ametengeneza kimdomo chake kama anataka kulia. “Basi mama. Basi.” Liv akarudi shingoni kwa baba yake. Geb akaanza kumpiga piga mgongoni. 

“Daah! Watoto hawakawii jamani! Ukiambiwa na yeye ameshakuwa mkubwa kiasi cha kukataa watu!” “Na sisi anatushangaza huyu mtoto! Naona akili yake ndio imekomaa mapema. Ameanza kujua watu mapema sana. Watu wote wa humu ndani anawafahamu. Utamuacha hapo kitandani na Fili, utamsikia akicheka kwa sauti tu. Lakini akiingia mtu asiyemfahamu, anabadilika kama sio yeye!” Mama G akaongeza. “Tena atakuchekea kama bibi yake au baba yake hawapo karibu na macho yake. Wakitokea tu, undugu wake na wewe ujue umeisha.” Waliendelea kuongea mpaka wageni walipoanza kuwa wengi ndipo wakatoka nje.

~~~~~~~~~~~~

Kikao kikaanza, Geb akiwa amekaa na Nanaa na mtoto wao. Fili akaja kumkalia Nanaa. Nanaa alimuweka vizuri, kikao kikaendelea. Danny ndiye aliyekuwa akiongoza kikao. Wakagawana majukumu. Wakaainisha kamati zote. Kama kawaida yao, kwa muda mfupi sana wakawa wamemaliza kikao kirefu. Walishajuana nani awepo wapi na atafanya nini, tena bila kusukumana. Kila kiongozi wa kamati akatoa makadirio ya pesa ya kamati yake. Danny akawa akiandika. Alichoona Geb hatapenda kama ukumbi na aina ya vyakula, alirekebisha na kushauriana na wenzake. Mwishowe wakapata makadirio ya juu. Likabakia swala la pesa.

Kama ilivyo kawaida ya kuulizwa bwana harusi kiasi alichojiandaa nacho cha kuoa. Akiwa anamjua vizuri Geb, Danny akamtaka Geb azungumze chochote juu ya hiyo bajeti. “Naombeni niwashukuru sana kwa utayari wa kujitolea. Kikubwa mimi na Nanaa tunachohitaji ni uwepo wenu tu. Najua mnamajukumu mengi na hali ya pesa imekuwa ngumu sana. Lakini mimi, Nanaa, Danny, Grace na Mama, tulishajiandaa. Tulikusanya pesa yakutosha tu anayo Danny. Tunaomba tugaramie kila kitu. Viongozi wa hizo kamati watakuwa wakiwasiliana na Danny. Danny ndio atakuwa na pesa yote. Atasaidiana na viongozi wa kamati zote ili kukamilisha hilo.” Geb akamaliza, lakini pakazuka ukimya mkubwa sana.

Danny akaona aongeze. “Labda kama hamjamuelewa Geb, ni hivi, majukumu yetu yamerahisishwa jamani. Sasa hivi tunaingia kazini tu, ili ndani ya mwezi mmoja tukamilishe maandalizi, hawa watu waoane. Kesho ndio tangazo la kwanza la ndoa yao. Kwa hiyo, hakuna kuchangishana.” “Hapo ndipo lilipo tatizo Danny. Na sisi tunawasaidia vipi kwenye matatizo yenu? Ni kama mnatufungia milango ili tukiwa na shida tushindwe kuwafuata! Hebu mtuambie tu,  kwa hiki mnachofanya nyinyi leo, inamaana kesho Gozi akitaka kuoa mnamwambia akusanye pesa kwa ndugu zake ndipo atuite?” Malii aliona aongee.

“Huo haujawahi, wala haujawa utaratibu wetu. Mnataka kuingiza utaratibu mpya na mgumu sana. Nyinyi mlikaa wanne tu mkachangishana, inamaana mnatuambia mmetutenga sisi? Wakati wote Danny umehubiri tena kwa kurudia rudia kuwa sisi ni ndugu. Mbona kama mnatutenga sasa!? Ni kama mnaanzisha matabaka. Au ni kwamba mnatuona hatuna uwezo?” Gozi naye akalalamika ila yeye akaiweka vibaya zaidi.

“Naombeni tusiende mbali. Nia ilikuwa nzuri tu. Kama tumekosea, basi tusameheane. Naomba tuanze upya. Au unasemaje Geb?” Danny aliingilia. “Kabisa.” Geb akajibu kwa ufupi tu, akawa amemaliza kama kawaida yake. Lakini wenzake walishamzoea hakuna aliyetegemea jibu la tofauti. Ndipo wakaanza kufunguka. “Naombeni na mimi niongee. Sisi tunaomba tuchangie kidogo tulicho nacho, kisha na nyinyi muongeze. Lakini itakuwa dharau kuacha pesa yetu.” Kila mmoja akaongea lake. Mwishowe Danny akachukua kalamu na karatasi akamkabidhi Malii. “Basi anza kuandika pledges au ahadi ya kila mmoja wetu.” Watu wote wakatoa ahadi zao. Vicheko vikaanza na kutaniana.

Wakati Inaonekana ipo Amani&Utulivu, Ndipo Na Muovu Naye Anapopanga Uharibifu.

Geb akamuona Nanaa anajishika miguuni mara kwa mara. “Vipi?” “Nahisi miguu inakufa ganzi, halafu kama inatoa jasho.” “Mshushe Fili. Inawezekana amekulemea.” “Mmmh! Fili mbona nampakata kila siku? Sidhani.” Geb akamwangalia. “Kweli Geb.” “Kwa nini usimshushe tu?” Walikuwa wakinong’ona. Alipomuona Nanaa anasita, akampeleka Oliva kwa mama yake, akarudi kumchukua Fili. Geb ndio akampakata. Nanaa akacheka. “Wala hamna tofauti!” Geb akamtizama, akaendelea kusikiliza maongezi.

Muda wa kwenda kula ukafika. “Twende ukachukue chakula. Au nikuletee?” Geb alimgeukia Nanaa akamuona amebadilika usoni. “Nanaa?” “Miguu imekufa ganzi kabisa Geb! Siisikii. Hata nikiifinya, sisikii kitu!” Geb akakunja uso kama haamini. Akampapasa. “Mbona ina maji!? Fili alikukojolea?” Geb akaanza kumpapasa Fili. “Hapana. Yenyewe ndio nahisi inatoa maji! Gauni lipo kavu kabisa. Kama Fili angekuwa amekojoa, ningeloa kuanzia hapa juu kwenye gauni!”

“Hebu simama.” “Siwezi, Geb.” Geb akamtizama kama haelewi. Akamuweka Fili chini, akasimama mbele ya Nanaa. “Nipe mikono yako.” Nanaa akanyoosha mikono yote miwili, Geb akamvuta kumnyanyua. Akafanikiwa kusimama. Alipomuachia tu, Nanaa akaanguka chini kama gunia. Na kwa kuwa alianguka kwa nguvu, kiti kilisogea, akajikuta yupo aridhini, juu ya ukoka. Geb akashituka sana. Kila mtu akawageukia wao. “Pole. Umeumia?” “Nimeangukia matako.” Nanaa akajibu huku akijaribu kusimama akashindwa.

James akasogea kwa haraka. “Kuna nini?” “Sijui kaka! Lakini miguu imekufa ganzi kabisa na inatoa maji!” James akainama kuangalia. “Halafu inajaa!” James akashangaa, watu wote wakamzunguka Nanaa pale chini. Geb akamnyanyua na kumuweka kwenye kiti. “Inauma?” Geb akauliza. “Nakwambia siisikii kabisa Geb. Naogopa!” “Usiogope. Twende ndani ukapumzike kwanza.” Geb akambeba. Wakati wanatoka pale, wakakutana na mama G na yeye anatoka ndani kumbadilisha diaper Oliva. 

“Kuna nini? Mbona mmebebana na Nanaa analia?” Mama G akauliza. “Sijui mama.” Geb alijibu huku amembeba Nanaa, anamwingiza ndani. Tayari hali ya pale ikawa imebadilika. Wasiwasi ukawa umetanda. James alikuwa nyuma yao, akawafuata mpaka chumbani kwa mama G, ndio chumba kilichokuwa karibu. Akamuweka kitandani.

“Naogopa kaka.” Nanaa aliendelea kulia. “Tulia Nanaa. Labda pumzika kwa kuinyoosha.” James akajibu, Mama G akaingia. “Ni nini!?” Akauliza. “Sijui mama. Miguu inatoa maji, halafu imekufa ganzi kabisa. Hata nikiifinya siisikii.” Mama G akasogea karibu. “Geb! Nitolee taulo kubwa na safi hapo kwenye kabati langu la kushoto.” Mama G akabonyeza mguu mmoja wa Nanaa. Akashangaa ametengeneza shimo pale alipoweka kidole. “Mmmh!” Akaguna. “Naogopa mama!” Mama G akabaki kimya akiangalia ile miguu. Tayari muonekano wa kuvimba ukawa bayana.

“Umekula kitu chochote cha tofauti?” “Hapana mama! Nimekula ugali niliopika mimi mwenyewe mchana. Ndio na nyinyi wote mmekula huo huo.” Mama G akabaki akiangalia ile miguu ya Nanaa. “Ni nini mama?” Geb akauliza kana kwamba mama yake anajibu. “Mama?” “Na mimi sijui!” “Sasa unakosaje kujua mama jamani!?” Geb alishaonekena kupaniki. Alianza kulaumu. “Naomba utulie Geb.” “Naogopa mama.” “Nafahamu. Lakini naomba utulie kabisa. Lasivyo utamuogopesha na Nanaa mwenyewe.” “Naogopa sana mama. Nitafanyaje? Unafiri nitakufa kabla sijaolewa? Au unafikiri nitakuwa kiwete? Watanikata miguu yangu? Eti mama!” “Hapana Nanaa mwanangu.” Mama G naye ni kama akawa amepigwa na kibumbuwazi. Akawa amekamatwa na hofu.

Grace akaingia akamwangalia mama yake, akamuona ameduaa. Akajua ameshaingiwa hofu. “Watoto wote nimemuachia Danny huko chumbani. Naomba James ukawatulize wageni wote. Waambie Nanaa atakuwa sawa, ila sasa hivi anahitaji kupumzika. Wakimaliza kula, ukamwite Danny chumbani amalizie kikao, wafunge tu na awaruhusu waondoke. Awaambie tutawajulisha kinachoendelea ila maandalizi yaendelee kama kawaida tu.” James akatoka bila kujibu.

“Kwenye hali kama hizi, mama huwa unaomba. Kwa nini na wewe unaingiwa hofu kama Geb na Nanaa? Naombeni mtulie tuombe.” Mara Fili akaingia. “Siwezi kupakua chakula mama. Nataka sambusa tu. Naomba twende ukanipakulie.” “Nisubiri kwanz...” Kabla hajamaliza, Danny akatoka chumbani kwao na watoto wote amewashika wanalia. Geb akampokea Liv, Grace akamchukua Fillan, Danny akabakiwa na Fillius. Liv akanyamaza baada ya kubebwa na baba yake. Lakini sio mapacha wa Grace. Waliendelea kulia kama kengele.

“Njaa hiyo!” Mama G akakaa pembeni ya Nanaa. “Narudi sasa hivi. Ngoja nikawanyonyeshe kwanza. Danny kapashe maziwa moto. Fillius atanyonya ya chupa. Lasivyo hapatakalika hapa.” Danny akatoka na Fillius, pacha mkubwa, ndiye aliyekuwa akilia sana. Wakaelekea jikoni kufuata maziwa. Grace alikuwa akikamua na kuweka maziwa yake kwenye friji kama Nanaa tu. Ikitokea wote wanaanza kulia kwa pamoja, basi mmoja atakunywa kwa chupa na mwingine kunyonya. Grace na yeye akaelekea chumbani kwao kunyonyesha mtoto mwingine. Fili akabaki amesimama. Wazazi wote wamemuacha pale.

Geb akamkabidhi Liv kwa bibi yake, akamshika mkono Fili na kutoka naye nje. Akaenda kumtafutia chakula. Kukawa na pilika pilika hizi na zile, hakuna aliyeweza kuomba tena. Geb akarudi na chakula. Nanaa akala, akampandisha chumbani kwenda kulala.

Shetani Hana Usingizi.

Asubuhi ya siku inayofuata, jumapili, ndio siku waliyokuwa wakiisubiria kwa hamu kwenda kanisani kwa ajili ya tangazo la kwanza la harusi ya Geb & Nanaa, waliamshwa na mayowe ya Nanaa. Alikuwa akilia sana. “Mama nisaidie jamani! Mama yangu nisaidie mimi!” Geb aliruka kitandani akabaki anatetemeka. Miguu ya Nanaa ilijaa. Ilivimba kupita kiasi. Iliumuka na kutengeneza malengelenge yaliyojaa maji kama usaha! Kuanzia magotini mpaka chini kasoro kwenye nyayo tu. Huwezi kujua ni kama aliungua au ni ngozi ya kenge imefunikwa juu ya miguu yake, lakini ikaongezeka majipu ya usaha. Nanaa alikuwa akilia hawezi kujiangalia tena. Macho amefunika na kiganja cha mkono wa kulia, mkono wa kushoto aliutumia kupiga kitanda mfululizo.

          “Mama yangu mimi! Jamani nisaidieni!” Ndio sautu ya Nanaa iliyokuwa ikisikika kwenye jumba hilo.

~~~~~~~~~~~~

-       Nini kimempata tena Nanaa?

-       Vipingamizi kila mahali!  Ndio wametoka kuvuka changamoto iliyorushwa kwao ya kulipa mahari. Pesa haikuwa tatizo. Hilo Geb alilikabili bila shida.

-       Marafiki nao wamerusha changamoto zao. Lawama, matusi kuitwa wasaliti na mengine mengi. Hilo nalo halikushinda HEKIMA za mama G. Akawatuliza wote ili tu, kufikia siku waliyokuwa wakiitamani kwa hamu. Kumsimamisha Nanaa kanisani na shela ndefu.

Mama G ajipatie mkwe aliyekuwa akimuomba na kujigamba ndiye mwanamke anayemfaa mwanae. Kwa Geb, ajipatie mwanamke pekee aliyeona atamfaa kumzalia watoto. Kuendeleza ukoo wa Magesa. Tena akiwa ameanza vizuri sana. Kumzalia Oliva. Mtoto wa kike aliyekuwa akimsubiria tokea kijana mdogo.

Wakati wote alikuwa akiwaambia rafiki zake, mtoto wake wa kwanza lazima awe wa kike. Sasa Nanaa ameshusha toto la kike. Binti Magesa. Oliva! Jina la mama G! Nani kama Nanaa! Katika wooote, amekusudia kuwa na Nanaa. Amefunga macho na masikio. Ni Nanaa.

Grace na Danny ndio wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanakamilisha hilo.

Leo Nanaa ameamka na miguu ya ajabu. Geb mwenyewe amemkimbia kitandani.

Nini kitaendelea? Safari hii ni Nani atakayesimama na Nanaa katika hili nalo? Ataweza kusimama mpaka mwisho? Na nani? Kufunga na kufungua historia imembadilikia.

Huwezi kuita ni ulemavu hata kidogo. Ni gonjwa lisiloweza kutamkika wala hakuna mtu angetamani kuwa naye karibu, kwa kutisha.

Ni rahisi sana kuambiana mnapendana kukiwa shwari. Je mambo yanapokwenda MRAMA?

Usikose kufuatilia ili kujua kitakacho Endelea.…

 

 

 

 

 

 

 

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment