Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Ni Wangu! - Sehemu Ya 35. - Naomi Simulizi

Ni Wangu! - Sehemu Ya 35.

Mama G akaamua kumuamsha mjukuu wake, nakuanza kumuhudumia wakati Nanaa naye akijiandaa kivyake. Alimsikia akipiga kelele zakushangilia kila wakati. Mama G akawa akicheka. “Hatutakunywa maji leo!” Akamsikia mama G akiongea chumbani alipokuwepo akimuhudumia mjukuu wake, Liv. Nanaa akacheka. “Wenye wivu lazima watajinyonga mwaka huu!” Nanaa akapita na kwenda kukaa sebuleni.  Mama G akatoka na mtoto msafi na nguo nzuri sana. Akabaki akimwangalia Nanaa pale kwenye kochi. 

“Kama wewe ni mwendaji, twende. Naona macho hayatoki kidoleni!” Mama G alimtoa mawazoni. Alikuwa amekaa kwenye kochi akiangalia kidole chake. “Siamini! Geb ameniokoa mama! Tena nikikwambia ameniokoa, uelewe ameniokoa haswa. Ujue anamfahamu Zac?” “Zac yupi tena!?” “Yule wa juzi?” “Yule mpenzi wako?” Mama G akamuuliza kwa kumchokoza tu. “Wewe mama wewe! Usinivunjie ndoa bwana! Mimi simjui huyo Zac.” Mama G, akaanza kucheka.     

“Gafla!?” Mama G akamuuliza kwa kuhamaki huku akicheka. “Akuu! Mimi simjui bwana!” “Zile sifa zote za juzi zimeisha!?” “Bwana mama! Mimi naona unachanganya stori. Na kama unanisingizia, sikusimulii!” “Basi Nanaa mwanangu. Kafanyaje?” “Basi nikikusimulia stori yangu na wewe utanimalizia ya kwako.” “Ipi tena!?”

“Yako na Magesa.” “Haaaa! Wewe mtoto!!” Nanaa akajifunika uso. “Hukunimalizia bwana!” “Nanaa acha umbea wewe mtoto! Ujue sisi ni wakwe zako?” “Bwana nisimulie tu.” “Yatakushinda Nanaa!” “Simwambii Geb. Wewe nisumulie mimi.” “Anza kuyasema ya Zac kwanza.” Nanaa akacheka.

“Basi tuongee wakati tupo kwenye gari, ili usinicheleweshe kurudi. Leo Geb amesema atawahi kurudi.” Mama G akacheka. “Nataka Geb anikute nimeshaoga, nimetulia kwenye kochi namsubiri mpenzi wangu. Niwe kama wewe vile ulivyonisimulia.” “Kama utaiga, nitakusimulia. Na nina kuhakikishia utafanikiwa Nanaa. Na hutakaa ukaibiwa. Yule mwanamke nilimuweza na kumshinda sababu ya kumpa mumewe kitu alichoshindwa yeye. Magesa hakuwa muhuni hata. Lakini nilimnasa kwa rahisi sana, akawa kama amechanganyikiwa. Alikuwa radhi kuacha kila kitu, anipate mimi. Iga mwanangu.” “Nitafanya hivyo mama. Na wewe usiniache. Ukiona nazembea tu, unishitue.” “Usiwe na wasiwasi. Na hivi una roho ya kufundishika. Tutakuwa wote, wala usijali.” Nanaa akafurahi sana.

~~~~~~~~~~~~~~

“Acha nimpigie simu kwanza mpenzi wangu, nimshukuru. Ujue jana alirudi na zawadi za Liv, nikamuuliza mbona mimi hajaniletea zawadi, akasema yeye ndio zawadi yangu!” Mama G akacheka. “Usicheke mama! Nikifikiria yale maneno na hii pete kidoleni, ni ujumbe mzito sana kwangu. Huyu mtu ananipenda mama. Ndio amenitangazia kuwa yeye ni wangu. Amejitoa kwangu. Sijui Mungu anibariki vipi tena! Lakini hakika amenitendea makubwa mno. Halafu japokuwa mimi sijui vito vya thamani, lakini inaonekana hii pete imemgarimu sana.” “Kabisa. Asingeweza kuweka hapo kidoleni kitu dhaifu. Na anavyopenda ukuu yule! Lazima aweke kitu cha thamani ili kila atakayekuona ajue imewekwa na Geb Magesa.” Wakacheka huku Nanaa akijaribu kuitizama vizuri.

“Kwanza hata Grace angemsema kama angeweka kitu kidhaifu! Kwa hiyo ujue mwenzio ndio kafunga watu wote mdomo! Haswa mimi mjua na mpenda vito vya thamani.” “Kwa hiyo mama hii ni ya thamani sana eeh?” “Sana. Angalia hilo jiwe lenyewe. Hiyo ni alumasi yenyewe. Angalia jinsi ilivyokatwa kwa ustadi! Yaani huo ukatwaji wake tu wenyewe ni pesa. Hiyo dhahabu iliyoshikilia hilo jiwe pia ni ile dhahabu nzuri. Halafu ona ilivyoshikilia hiyo alumasi kwa ustadi!” Mama G alikuwa akizungumza huku akiingalia ile pete kwa makini akitathimini pesa iliyomwagwa na mwanae.

Hapo ndipo Nanaa alipojua amevalishwa kitu cha thamani. Hakuwa hata akielewa kabla ya maelezo ya mama mkwe wake. “Acha nimpigie simu nimshukuru mama.” “Utafanya vizuri.” “Ila naenda chumbani.” “Huo ndio mwanzo wakuchelewa Nanaa, bwana!” Nanaa akacheka.

“Mimi nakujua wewe. Utaenda kuanza kulia badala yakusema tu ‘asante’.” Nanaa alishaanza kulia. “Muone! Ukoje wewe?” Nanaa akajifuta machozi nakuingia chumbani.

Akampigia simu Geb. “Nanaa!” Geb akapokea ilipoita mara moja tu kama aliyekuwa akiisubiria. “Jana uliniambia wewe ndio zawadi yangu.” Nanaa alianza huku akilia. Geb akacheka. “Nakupenda Geb.” Nanaa akaendelea. “Asante sana kwa kujitoa kwangu. Asante kwa hii pete. Nakuahidi hutajuta.” “Asante Nanaa.” “Natamani ungeona jinsi ilivyonipendeza! Na imenienea vizuri kama uliyenipima!” Geb akacheka. “Nilikuona baada ya kukuvalisha na nilikupiga picha nyingi tu.” Nanaa akacheka.

“Ungeniamsha nisherehekee. Lakini ningemuamsha mtoto kwa kelele!” Geb akacheka. “Nimefurahi kama umeipenda.” “Ulijuaje saizi ya kidole changu lakini!?”

Nanaa akauliza. “Nanaa! Nafahamu mpaka saizi ya kiuno chako.” Nanaa akacheka sana. “Geb wewe!” “Ndio ujue nakufahamu vizuri sana.” “Asante Geb. Ninafuraha ambayo sijui kama nitaweza kula leo.” Geb alikuwa akicheka. “Ukija ndio nitakuonyesha furaha yangu.” “Usinifanye niache kazi nije Nanaa!” Nanaa akacheka sana.

“Nipo na mama, na tunatoka. Tulia kazini Geb! Nimekwambia ukirudi. Kwanza naenda kununua chupi mpya ya kuivua usiku.” “Unanitesa Nanaa.” “Na sidiria yake.”  Nanaa akaongeza kwa sauti ya kumvutia. “Iwe na lesi kote ili nione chuchu kabla sijavua.” Nanaa akazidi kucheka. “Basi rangi sitakwambia.” “Ilimradi ionyeshe tu chuchu.” Geb akasisitiza. “Usijali. Wewe kazana kula ushibe.” “Sawa mama Oliva.” Nanaa akafurahi sana. “Kwa heri, mama ananisubiri. Ila ujue nakupenda.” “Asante.” Wakaagana, Nanaa akatoka kwa furaha. 

~~~~~~~~~~~~~~

Alimkuta mama G ametulia hapo sebuleni kimya amempakata mjukuu wake. Akaingiwa na aibu kidogo. “Mimi najua hujasikia mazungumzo yangu na Geb!” Mama G akaangua kicheko. “Twende Nanaa.” “Bwana mama!” “Sasa mimi nimefanyaje!?” “Hata kama umesikia usiniambie kitu.” “Mbona unawasiwasi? Mimi sijasema kitu chochote! Wewe ndio unajishuku.” Nanaa akajificha uso kwa aibu huku akicheka. Wakatoka.akaingia kwenye gari kuelekea kwenye chumba hicho cha Nanaa, alichokimiliki kwa masaa kadhaa. Njiani alimueleza Mama G kila kitu juu ya Zac.

Akamuhurumia sana. “Lakini mama, namshukuru Mungu ameninusuru. Isingekuwa Geb kuja pale mapokezi, inamaana asingemuona Zac. Ningeondoka kwa Geb, nikakubaliana naye. Ningeishia kuolewa na tapeli! Kwa kweli namshukuru sana Mungu. Ameninusuru.” “Niliwaombea sana usiku ule. Nilimlilia sana Mungu juu yako. Nilimwambia Mungu akukumbuke. Upumzike.” Nanaa alilia sana. “Asante mama. Asante kwa kunipenda.” “Unamoyo mzuri sana Nanaa. Nilimkumbusha Mungu kuwa yeye aliahidi ni baba wa yatima. Nikamwambia akukumbuke. Niliomba maombi niliyomuomba Mungu wakati Magesa alipokuwa mgonjwa. Nashukuru amejibu.” “Amenijibu mama. Mungu wako amejibu kwa moto. Kanitoa kwenye mikono mibaya, akanituliza kwenye mikono ya Geb, mwanaume aliyetulia. Ameniambia ananipenda SANA.” Mama G akacheka.

“Ujue nilidhani hanipendi tena?” “Ni hasira tu. Geb ni mkali kama baba yake na hiyo tabia yakutokusahau ndio inamtesa sana. Kuwa makini na kila neno unaloongea kwake. Zaidi jizuie mdomo wako unapokuwa umekasirika. Ni heri unyamaze kabisa. Hata wao wawili niliwafundisha hivyo. Ndio maana unawaona wakati mwingine wanakuwa kama wajinga hata pale wanapokasirishwa na kutakiwa kujibu lakini wananyamaza. Niliwafundisha tokea wako wadogo. Kwa kuwa kwanza nilijua kiwango chao cha uelewa ni kikubwa sana. Hawaendani na watoto wengi wa umri wao na mimi sikuwa na uwezo mkubwa, nikawalea mtaani tu. Sasa nikajua wakiweza kufungua kinywa na kuongea yaliyopo ndani mwao, kwanza watateseka wao wenyewe, pili watashindwa kuwa na marafiki watajikuta wapo wenyewe.” Mama G akaendelea.

“Haswa Geb! Ndio maana unamuona hata akiwa katikati ya wenzake anakuwa kimya kabisa. Najua wakati mwingine inamuwia ngumu kua nao kwa sababu ya aina ya mazungumzo wanayozungumza na kiwango chao cha uelewa. Lakini nilimfundisha kunyamaza na kujitahidi kuwa katikati yao, kama rafiki. Grace hivyo hivyo. Huwezi humsikia akiongea sana akikasirika. Kwa kuwa yeye mwenyewe yale maneno atakayoongea akiwa kwenye hasira, hawezi kusahau. Yatamuumiza daima. Kwa hiyo na wewe kuwa makini sana na maneno yako utakayozungumza akikukasirisha. Geb huwa hasahau. Hata akikusamehe, ujue hilo neno bado lipo kwenye kile kichwa chake.” “Nimeelewa mama. Hata yeye nimemuahidi kubadilika. Nilimtukana sana nilipomfumania na Liz. Nikam..” Nanaa akanyamaza, mama G akamuona machozi yanamtoka.

“Nisikilize Nanaa. Hayo yameshatokea. Kitendo cha kukuvalisha pete, inamaana amesamehe na kukupokea vile ulivyo. Geb hana sababu ya kukuoa wewe kama sio mapenzi ya kweli. Anamsururu wa wanawake kibao. Liz anamtaka mpaka kesho. Jiamini tu, ujue amekupenda hivyo ulivyo.” “Hilo ndilo limenifurahisha zaidi mama. Nimefurahi kuona amenijua na bado amenichagua mimi! Nimefurahi sana mama yangu.” Nanaa aliongea huku akifuta machozi.

“Hata mimi nimefurahi umekuwa mtii na umesamehe. Ungeweza kutokutaka kumsikiliza tena Geb, mkashindwa kufika hapa mlipo. Na wewe nakupongeza.” “Asante mama.” Wakatulia kidogo. “Nimalizie stori yako mama. Maana Geb ni kama aliniambia wakati anakuwa, baba yake alikuwa akija kuwachukua na kuwapeleka kwenye biashara zake. Nikashangaa kidogo. Maana tuliishia pale uliposema mlikuwa mkiishi wote baada ya kufukuzwa kwake, na mkaanza maisha yenu mpaka ukajifungua.” Mama G, akatulia kidogo. Nanaa akaona amepooza.

Mama G & Mzee Magesa.

          “Mambo yalikuja kubadilika Nanaa. Watoto walipofikisha mika 5, mkewe akaanza kuugua. Alipata kansa ya ziwa. Wanae wakamtafuta baba yao, mpaka wakampata. Wakamuomba msamaha na kumlilia sana kutaka arudi nyumbani. Kumbe kwa muda wote ule yule mama hakuwa akiendesha zile biashara kama mwenyewe Magesa. Akaharibu karibia kila kitu. Wale watoto na mama yao waliweka ‘restrain order’ kwa baba yao. Kuwa haruhusiwi kabisa kusogea kwenye hizo mali. Kwa hiyo Magesa aliondoka wala hakutazama nyuma. Ila kumbe alikuwa akijua kila kitu kinachoendelea huko kwa mkewe na watoto. Akatokea Mgoa mmoja hivi, mtu mwenye asili ya Asia, akaanzisha kitu kama kile kile cha Magesa, maeneo ya Kibaha. Akachukua wateja wote wa Magesa. Yule mama akafunga biashara karibia zote.” Mama G akaendelea.

“Basi, ikabidi sasa Magesa arudi kumuuguza mkewe. Mambo hayakuwahi kurudi kuwa kama zamani Nanaa. Magesa akawa busy na mgonjwa huku akipambana na biashara.” “Si angeendelea na biashara za huku kwenu?” Nanaa akauliza. “Hakukubali. Alisema huo ndio urithi wa Grace na Geb. Sasa ukumbuke hapo nina watoto wawili wadogo na biashara. Na Grace alikuwa mlizi sana. Usimuone vile.” Nanaa akacheka.

“Hajui maisha bila mama yake. Tokea mdogo, inabidi kumfikiria yeye tu. Hakuwa akitaka mtu mwingine aishi naye ila mimi. Ukitafuta msichana wa kazi ili akae nao wewe uwe kwenye biashara, ujue haitasaidia. Ujue pale ulipomuacha wakati unaenda kazini, ndio utamkuta hapo hapo. Atalia kuanzia asubuhi mpaka jioni unarudi. Ukirudi tena hapo, ni mgonjwa. Homa. Nianze kuhangaika na watoto, na biashara. Mambo yakawa magumu. Pakumuweka Grace sina! Nipo naye kila mahali kama pochi!” “Kwani baba yao hakuwa akirudi?” Mama G, akaguna.

“Alikuwa akija kutuona! Lakini labda mara moja kwa week. Na akija anafikia kitandani kwa kuwa anakuwa amechoka. Usiku kucha yupo na mgonjwa. Akipata nafasi ni kwenye biashara zake. Kuhangaika kutafuta pesa zakujikimu yeye na mkewe. Haya, akipata mwanya, au akizidiwa huko, kwangu ndio ilikuwa sehemu yakuja kupumzika. Utamuona ameingia, yupo hoi! Grace naye alikuwa akimuona baba yake, utafikiri ameona alumasi. Atamganda. Hataki kushuka mikononi kwake. Hapo na mimi nakuwa nimechoka! Hakuna tena mapenzi. Tukaendela na hayo maisha mpaka yule mama akakatwa ziwa. Akachomwa mionzi, tukajua amepona. Hapo ilikuwa zaidi ya miaka miwili ndio pakatulia swala la ugonjwa.” Mama G akacheka.

“Haya, cha ulizi wangu, Grace akaanza shule yeye na kaka yake.” “Hivi Grace anadeka eeh?” “Sana. Muone vile katulia.” “Basi ukimuona mwenyewe ni kama hana habari na wewe.” “Basi ndio tatizo lake hilo. Yeye anachotaka umtetemekee. Sasa nimuache tu bila kujali! Atalia mpaka aumwe. Kutwa anataka umtafute, umjulie hali. Akiumwa, basi wewe ujue kama anaumwa na asiwe amekwambia. Na ufanye apone.” Nanaa akacheka.

“Alinitia hekaheka kipindi anajifungua Fili, muulize Danny na Geb. Nusura nichanganyikiwe! Anaumwa uchungu, lakini anamtaka mama yake ndio awepo hapo. Alikuwa akilia hataki hata nisogee hatua moja na alipo. Hataki mtu mwingine yeyote amguse, hata nesi ila mimi tu. Alipata uchungu wa masaa marefu, nilikoma Nanaa. Hata chooni hataki niende. Nikiondoka tu, kilio. Anamtaka mama yake. Hivi juzi Danny ndio alikuwa akinikumbusha. Tulicheka kwenye simu na Danny, mpaka machozi. Ananiambia nijiandae. Maana safari hii wanakuja mapacha. Na yeye kutwa anamwambia Danny, akianza tu uchungu, akaitiwe mama yake.” Nanaa akacheka sana.

“Wewe utamuona. Muoga hata wakuumwa kichwa. Akiumwa hata ukucha, basi watu wote mtajua. Na lazima muonyeshe kujali. Lasivyo ugonjwa unazidi.” “Jamani Grace!” “Hivi hapo alikuwa anataka nikaishi naye, lakini namzungusha sababu ya Geb. Nikimuacha Geb, atakufa kwa njaa.” Nanaa akacheka. 

“Sasa ikawaje mama?” “Basi, watoto wakaanza shule. Yule mama akapata nafuu. Ndio tukaanza kuonana tena na Magesa. Lakini haikuwa kama zamani. Akija, anataka kupumzika. Anasema kwangu ndio anapata utulivu. Akiamka hapo, anarudi tena huko Picha ya ndege kwa mkewe na watoto. Biashara zikazidi kuwa ngumu. Upinzani ukawa mkubwa, na yeye umri ukawa umeenda. Akawa anahofia sasa wanae Geb na Grace. Akawa anahangaika mchana na usiku kutafuta kuacha kitu cha kutusaidia mimi na watoto. Akatujengea nyumba nzuri sana. Ilikuwa na eneo kubwa. Akatununulia shamba lilikuwa la ekari karibia 20. Akaandika jina langu, akanihamishia hapo kwenye hiyo nyumba.” Mama G akatulia kidogo.

“Hatukukaa sana, yule mama kansa ikarudi tena. Lakini safari hii kansa ilikuja kugundulika ikiwa imeshasambaa mpaka kwenye mapafu. Jamani mama aliumwa yule, ungemuhurumia. Hapo muuguzi ni Magesa.” “Si alikuwa na wanae wa kike?” “Bwana sijui wale watoto waliwaleaje! Mimi sijui! Hawakuwa wakimjali yule mama hata. Nikaja kusikia walipoona hali ya mama yao mbaya, ni wakuogesha na kusafisha kinyesi, walikimbia hapa nchini. Tena wote wawili. Wakaenda kuanza maisha huko Uingereza.” “Mama!” Nanaa akashangaa sana.

“Kweli tena. Lakini Magesa aliishia kujilaumu yeye. Akasema yeye ndiye aliyewasababishia hayo. Kwa upande mwingine niliona mimi ndiye nilimsababisha Magesa kuvunja familia. Basi. Akamuuguza yule mama, huku anafilisika. Akaishiwa kabisa. Mimi ndiye nikawa nikimtunza yeye na mkewe. Lakini kipindi hicho akiwa na mkewe, ndio kipindi alichokuwa wakati mwingine anakuja kuchukua wanae, anaenda nao huko kwa mkewe. Sababu ya Grace kulia wakiachana, wakati mwingine ili kumrahisishia, akawa anawachukua siku ya ijumaa wakitoka shule. Anaenda kukaa nao hata mpaka jumamosi au jumapili, anawarudisha. Angalau alikuwa anapata muda na Grace huku akimuuguza mkewe wakiwa sehemu moja. Alishindwa tena kujigawa.” Nanaa akamuhurumia.

“Sasa na wewe?” “Ilibidi kuhamisha mawazo kwenye mapenzi, na kuanza kuangalia maisha ya wanangu Nanaa. Niliwazaa nikiwa mdogo, tena na mtumzima sana. Nalingana na mtoto wa mwisho wa Magesa! Yaani mtoto mkubwa wa Magesa, kwangu ni mkubwa. Ikabidi kuchangamka. Nikajua hata nifanye nini, Magesa hawezi kuja kunisaidia tena. Lazima nipambane mwenyewe. Kwa sababu ya matatizo, Magesa naye akawa anazeeka kwa haraka. Ugonjwa wa presha haukukawia. Magesa aliyezoea kushika mapesa, akawa hana kitu, na nguvu yakutafuta tena pesa hana.” “Kwa nini usingemsaidia?” “Nisingeweza kumtoa kwa mkewe Nanaa. Tena ni mke wa ndoa! Nisingeweza. Nilichokuwa nikijitahidi nikumtumia pesa na vyakula.” Mama G, akatulia.

“Pole mama.” “Ndio hivyo Nanaa. Mwishowe akaanza kufa yule mama. Baada ya mazishi, nikakaa siku chache tu, nikasikia Magesa ni mgonjwa sana, na ndugu za mkewe hawamjali. Wanamlaumu kuwa amesababisha kifo cha ndugu yao. Niliondoka kwangu muda uleule nilipopata habari, ilikuwa usiku nikaenda mpaka nyumbani kwake.” “Hukuogopa Mama!?” Nanaa akauliza kwa mshangao.

“Mimi nina roho ngumu sana Nanaa! Mungu hakuniwekea hofu hata kidogo labda nione wanangu wanaumwa au Magesa ndio unaweza kuniona nimeingiwa na hofu. Lakini si vinginevyo.” Nanaa akacheka. “Basi, nikaenda mpaka dukani kwa Chalii, Kibaha. Nikamkuta na mkewe.” “Chalii si yule uliyemkataa?” Nanaa akauliza tena. “Kumbe. Sikiliza sasa. Nilifika tu pale, nikamwita atoke nje ya duka lake. Ile ametoka tu, nikamdaka. Nilimkunja shati, nikamwambia nilazima tuongozane mpaka nyumbani kwa Magesa, akanisaidie kumtoa Magesa pale kwake. Kwa kuwa Chalii alishanifahamu, akaniambia wala nisitumie nguvu kumtoa Magesa. Hakuna anayemtaka pale. Akaniambia niende tu nyumbani kwake, niingie, nizungumze naye Magesa, nimchukue. Hakuna atakayenizuia kwani hata wao wanataka Magesa aondoke.” “Mama!” “Acha Nanaa? Basi. Nikamshukuru Mungu, nikawasha gari mpaka nyumbani kwa Magesa.” Mama G alitulia kidogo.

“Nilifanya kituko cha mwaka.” “Ulifanyaje tena?” “Niliingia bila hodi wala salamu kwa nilio wakuta. Nikazunguka chumba kwa chumba mpaka nikamkuta Magesa amelala. Nikamuamsha. Nikamwambia twende. Akaniambia, ‘Nimeshakwisha Oli. Mimi ni mfu.’ Nikamtoa pale kitandani kwa nguvu, tukaingia kwenye gari mpaka kwangu. Kazi ya kuanza kumlisha ikaanza. Alipata na yeye kansa ya kibofu. Tukaanza matibabu. Upasuaji mdogo mdogo wa hapa na pale kujaribu kutoa vinyama vilivyokuwa vikiota huko kwenye kibofu.”

“Akaanza kushindwa kuzuia mikojo. Magesa akawa mtu wa kujikojolea. Daktari mmoja akatusaidia kumfunga catheter. Lakini ile hali ilikuwa ikimfedhehesha sana Magesa. Mtu aliyekuwa amejaa majivuno, leo anatokwa mkojo bila kujua! Ilimsumbua sana. Lakini nilihangaika naye bila kukata tamaa. Mwanzoni alikuwa mtu ambaye aliweza kutoka na kufanya shuguli zake, lakini ikafikia hatua akawa dhaifu kweli. Anateseka mpaka unamuhurumia. Akikojoa ni usaha mtupu. Maumivu yakawa makali. Mwili mzima ukawa unamuuma. Kumbe kansa ilishaenea mpaka kwenye figo. Figo zikaacha kufanya kazi. Akaanza kujaa tumbo.” “Pole mama.” Nanaa akazidi kumuhurumia.

“Jamani Magesa aliumwa! Alikuwa akilia kama mtoto mdogo kwa maumivu. Alikuwa anaishi kwa madawa ya maumivu tu. Tena makali. Alikuwa akiniomba nimuombee kifo tu. Mpaka akaja kufa.” “Pole mama.” “Lakini namshukuru Mungu, kabla ya kuzidiwa, tulirudi kanisani. Tukatubu na kufungishwa ndoa. Kwa hiyo alikufa akiwa mume wangu halali. Hakuamini vile nilivyokuwa nimefurahia. Nilimwambia nimefurahi na mimi nimekuwa mkewe kihalali. Akawa anaumia kuona hajiwezi tena. Nikawa namtuliza nakumwambia namfahamu nguvu yake akiwa mzima na sasa. Nilichokuwa nikikifurahia ni ile hali ya uhuru wakuwa naye mimi peke yangu bila kumshiriki na mtu. Magesa hakuwa akinielewa.” “Ulimpenda eeh!?” Nanaa akauliza na yeye akishangaa.

“Nakwambia nilimpenda Magesa mpaka siku anakufa. Nilimpenda yule mwanaume karibu yakuchanganyikiwa. Sijaona mpaka leo.” Nanaa akacheka sana. “Lakini nikafurahia sana na mimi niliolewa. Tena na Magesa! Huna utakachoniambia nikaelewa. Hata kama hapakuwa na kufanya tena mapenzi, lakini Magesa alinifikisha kanisani. Nikawa mkewe halali. Basi. Akafa Magesa wangu akiwa ameniachia watoto wazuri. Wakike na wakiume.” “Hongera.” “Naipokea bila shida. Usifikiri naitwa mama Magesa kwa heshima, niliingizwa kanisani na Magesa mwenyewe.” Nanaa akazidi kucheka.

“Lakini alipokufa tu Magesa, ndugu zake na wa mkewe wakataka kunipokonya mali. Tena nilizokuwa nimezihangaikia mwenyewe. Lakini kumbe Magesa aliacha wosia kanisani. Akasema mtu yeyote yule. Hata wanae. Wasichukue kitu chochote kutoka kwangu. Hata kama aliacha shati lake kwangu, ni mali yangu mimi na wanangu. Na vitu vyote alivyoviacha kule kwa marehemu mkewe, ni vya mabinti zake tu. Basi, ndio watu wakatulia.”

“Na vitu vyote alivyoacha Magesa. Yaani nguo na viatu vyake, Geb amevitunza. Amevifungia, anasema anakuja kuonyesha wanae.” “Mama! Miaka yote hiyo!?” Nanaa akashangaa. “Nakwambia mpaka leo vipo. Atakuja kukuonyesha siku moja. Mpaka viatu na kandambili alizokuwa akivaa wakati mgonjwa, ametunza. Anavyo.” Nanaa akashangaa sana.

“Sasa hapo nikawa nimeshakuwa mtu mzima. Najua mimi ndio baba na ndio mama, nikupambana tu. Nikaanza kusomesha wanangu. Bahati nzuri watoto wenyewe wakawa wakifaulu tu. Mpaka alipofeli chuo Geb, ndio nikaamua kuuza kila kitu ili asome. Kumbuka hapo sina ndugu sina wakumkopa pesa. Nikajiambia nitajua mbele ya safari. Nikapata mteja, nikauza kila kitu. Pesa karibia yote nikamkabidhi Geb. Nyingine ndio nikapangishia chumba, na kubakisha ya matumizi yakutusaidia na Grace. Nikajiambia lazima kumtunza vizuri Grace, kwa kuwa alikuwa na uzuri wa kuvutia wanaume, nikajiambia nikilegeza kamba tu, watamzalisha mapema sana. Ndio nikawa najitahidi naye. Angalau kumpa kila anachokitaka. Alivyokomaa kidogo tu, nikagundua sio mtoto mwenye tamaa, na ananisikiliza. Ndio nikahamisha mawazo kwa Geb.” “Uniombee na mimi Oliva awe mtulivu kama shangazi yake. Maana kwa kaumbo kale! Naona atamtoa jasho baba yake.” Wakacheka. “Mungu atakusaidia Nanaa. Tutamkuza vizuri. Atakuwa binti mzuri tu.” “Amina mama yangu.” Nanaa akashukuru.

~~~~~~~~~~~~~~

Wakafika kwenye chumba cha Nanaa, wakachukua kila kitu, Nanaa akarudisha funguo kwa mwenye nyumba. Wakaondoka kwenda madukani kisha wakarudi kwenye apartment. Walimkuta Geb akiwasubiri. Akawatania kidogo. Na kuwaomba wamsubirie sebuleni wazungumze. Yeye akaingia ndani, akamsafisha Oliva vizuri, akambadilisha nguo. “Labda nimnyonyeshe tena kabla hajalala.” Nanaa aliwafuata chumbani akatoa wazo. “Hapo utafanya vizuri.” Mama G akaafiki. “Fanya haraka basi ukatoe jasho uje umnyonyeshe.” Nanaa akakimbilia kuoga.

Alioga harakaharaka kutoa jasho la siku nzima. Akabadili nguo iliyokuwa rahisi kunyonyesha. Akatoka. Alimkuta Geb anacheza na mtoto ili asilale. “Ananirembulia tu hapa.” “Na Liv kwa kupenda kulala jamani! Usingizi haushi! Eti Liv?” Nanaa akamnyanyua. “Lakini muda wote wewe unapandisha mizigo kwenye gari, alikuwa macho, hajalala. Leo amejitahidi.” Mama G akamtetea.

“Basi ngoja nikamnyonyeshe nitarudi. Haya sema bye bye kwa bibi na dady.” Nanaa alinyanyua kimkono cha Liv akawa anapunga mkono. Geb akasimama akambusu, Nanaa akaondoka.  

Wosia wa Mama G, kwa Nanaa na Geb.

Baada ya muda Nanaa akarudi akaenda kukaa pembeni ya Geb. “Nina mambo nataka kuwaambia. Mimi ni mama yenu. Nimeshaishi maisha na ninayajua maisha. Nilipitishwa kwenye magumu mengi sana, lakini namshukuru Mungu kwa kuwa najua ni kwa sababu yenu. Ili msipite nilikopita mimi. Nanaa alipoondoka bila maelewano mazuri kwa sababu ya makosa yangu mimi, niliumia sana. Kwa kuwa siku Grace alipomleta nyumbani, Roho wa Mungu ni kama aliniambia, aliniletea mtoto mwingine kwenye maisha yangu kama alivyoniletea Danny. Kama vile ambavyo ninamuhesabu Danny kama Geb, ndivyo sasa hivi ninavyo muhesabu Nanaa, kama Grace.” “Asante mama.” Nanaa akashukuru.

“Nilikaa na Grace na Danny nikazungumza nao, ndivyo hivyo hivyo ninataka kuzungumza na nyinyi wawili. Mahusiano hasa yakifikia kama yenu, sio kitu shetani anafurahia hata kidogo. Anatuma mitego mingi sana. Tena inayofanana na kweli kabisaa, ili tu kuwavuruga. Nyinyi ni mashahidi. Nanaa uliwakuta Geb na Liz, wote wapo uchi kabisa, ukajua walitoka kwenye mapenzi. Uliamini kabisa, sababu tayari ulishaaminishwa na shetani kuwa lipo jambo la siri, ambalo unafichwa tu na Geb. Hata alipokwambia anakupenda, bado akili yako iliona na kuamini kile ulichokuwa ukikiamini tokea ndani. Na usifikiri huo ndio mwisho! Bado mtajaribiwa sana tu.” Mama G alikuwa akiwaangalia kila mmoja kujua kama wanamsikiliza.

“Kila hatua mtakayofikia ya mafanikio makubwa ya maisha, shetani atatuma jaribu kubwa zaidi. Kila hatua mtakayosogea, na yeye atasogea na nyinyi. Hasinzii wala hata wahi kulala mpaka siku ya hukumu yake. Mungu atakapomuweka kifungoni. Mahusiano yeyote yale si marahisi hata kidogo. Iwe urafiki tu, au mapenzi. Hata mahusiano yangu na yako Nanaa, yalijaribiwa. Tena isivyo ya kawaida. Tukiwa tumetoka kuongea na kucheka, nikakuacha nje ya ukumbi! Mpaka leo najiuliza ni nini kilitokea siku ile, mimi sijui! Kwa nini usiumwe wakati mwingine, uje uumwe siku mimi niliyofanya uzembe!? Tena mimi mama yake Geb! Ni kama nilikuwa nikiadhibiwa! Najua watu wote walinikasirikia. Kwa kuwa mimi nilikuwa chanzo cha wewe kuondoka kwenye maisha yetu.” Mama G akaendelea.

“Lakini Nanaa, nilikosa. Nilimlilia Mungu nikamwambia sikuwa na nia mbaya na wewe. Na sikukusudia kutenda ubaya. Nilitubu sana mbele za Mungu na wanangu. Kitendo cha wewe kuwa na shida na kunitafuta mimi, kwangu nilihesabu ni neema ambayo hakika sikustahili. Mungu angeweza kukuinulia mtu yeyote akakusaidia. Lakini kwa nini mimi!? Zaidi akaniletea na mjukuu uliyenikabidhi ukiwa na imani kubwa na mimi. Mpaka jina ukata ni mpe lolote nitakalo! Niliona uthamani mkubwa ulio uweka kwangu. Japo nilikosea, lakini najua tulishaweka msingi wa maelewano kati yangu na wewe, najua ulijua kabisa mimi ni mtu mwema kwako.” Nanaa akacheka.

“Najua sana kama unanipenda mama.” Wote wakacheka. “Sasa ndio inavyotakiwa ifikie kwako na kwa Geb. Sijui kama mnanielewa? Lazima ifikie mahali, hata ikitokea jambo gani kati yenu. Ujue hili ni kosa tu. Nanaa amekosa kama mwanadamu. Au Geb hakukusudia. Amenikosea kama binadamu. Lazima ifike hapo, mjuane tabia na mfahamiane. Hakuna ubishi au maswali yakuuliza juu yakupendana kwenu. Mimi kama mama yake Geb, najua Nanaa unampenda sana Geb. Nimeishi na wewe nimekuona Nanaa. Na nimeshakuwa karibu na wasichana waliokwisha kuwa na mahusiano na Geb, nakiri hakuna ambaye angemfaa Geb ila wewe Nanaa.” Nanaa alijisikia vizuri sana moyoni.

“Unamjali na kumpenda Geb, bila unafiki. Nimeona hata wakati mwingine mnakuwa hampo kwenye maelewano mazuri, lakini bado unamuhudumia. Kitendo cha kujua Geb amelala na mwanamke mwingine chumba kinachofuata. Tena humo humo ndani ya hiyo nyumba. Kama wapenzi. Na bado unaamka asubuhi unawaandalia kifungua kinywa! Wanatoka wakiwa wao wawili, wanakuacha! Unabaki kupika tena chakula ili akirudi ale! Haya, unatoka, ukimuacha amelala na mwanamke. Unarudi unamkuta hana raha. Anatokwa jasho. Unamfuta na mtandio wako msafi! Unamsafisha vidonda! Tena unajua jioni anarudi kwa mwanamke wake! Kwa kweli binafsi ilinigusa sana Nanaa. Na ndio maana shetani anahangaika sana na nyinyi ili kuvunja hayo mahusiano. Sio wakawaida. Inamaana nyinyi watu wawili mkifanikiwa kuwa pamoja, hakuna jambo lolote linaweza kuwashinda.” Nanaa alibaki ameinama.

“Geb, fungua bibilia yako kwenye kitabu cha {1 koritho 13:4-8}.” Mama G alimtaka Geb ndio asome. Geb akavuta simu yake akafungua ilipokuwa bibilia yake kwenye hiyo App, akaanza kusoma.  4 Upendo huvumilia, pendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno. 5 Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hautafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. 6 Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. 7 Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote. 8 Upendo hauna mwisho. Mama G akamwambia Geb aishie hapo. Akataka na Nanaa naye asome hapo hapo. Nanaa akasoma taratibu huku wakimsikiliza.

“Naomba kila muwezapo, mrudie kusoma mkiwa pamoja. Rudieni tu bila kuchoka mpaka kifo chenu. Mtapona. Kila neno hapo ni lenu wote. Mmepitishwa kwenye magumu, mmetoka. Rudini kwenye ‘upendo hauweki orodha’. Msishinde jaribu mkaanza maisha mapya huku mkikumbushana yaliyopita. Mtachoshana haraka sana. Ukishajua udhaifu wa mwenzio. Samehe tena na tena. Usichoke. Kwa kuwa ‘upendo hustahimili, hauhesabu mabaya.’ Na ukishajijua unaudhaifu unao mkera mwenzio, jaribu kubadilika. Usiseme mimi ndivyo nilivyo. Utanizoea tu. Hapana. Huo sio upendo. ‘Upendo hautafuti kujipendeza nafsi.’ Tafuta kumpendeza na mwenzio. Badilika. Sijui kama mnanielewa?”  Wote waliitika na kusema wameelewa.

“Lakini si rahisi kama mlivyo itika. Wote mnajua historia yangu mimi na Magesa. Japo Geb hufahamu kwa undani kama Nanaa.” Geb akashangaa sana. Wakacheka. “Yule baba na mkewe walikuwa watu wa kanisani. Magesa alikuwa Mzee wa kanisa. Lakini hicho hakimuogopeshi shetani hata kidogo. Ninauhakika Magesa na mke wake wangekuwa watu wanaotembea pamoja katika ulimwengu wa  roho na kawaida, yule mama angejua hatari inayomkabili mumewe akaweza kumlinda. Sijui kama mnanielewa?” Mama G akatulia kidogo kama kuwapa nafasi yakufikiria.

“Wanandoa wenye mahusiano ya kiroho ya pamoja, hao ndio shetani anao waogopa. Na kamwe huwa haruhusu hicho kitu kitokee. Ndio maana utakuta wanandoa au couples, wana muda mwingi wakufanya kila kitu pamoja lakini si kuomba Mungu pamoja au kusoma neno la Mungu na kujifunza mambo ya kiroho pamoja. Watahangaika kukuza kila kitu kwa juhudi zote. Iwe uchumi wa familia. Watoto. Chochote kile watafanya pamoja. Tena watahangaika mpaka utapatikana muda, lakini si kukua kiroho pamoja. Likifika katika hilo eneo, hakuna muda. Hata wafanye nini, hautapatikana muda. Na ndio maana mahusiano mengi yanajaribiwa sana, na huharibika. Kwa kuwa hakuna msingi imara unaowashikilia.” Mamaa G akaendelea.

“Ikitokea leo Geb   unamuombea Nanaa.Nikimaanisha, unakwenda umbali wakupiga goti chini na kumwita Mungu kwa ajili ya Nanaa tu, hakika hutamwangalia Nanaa kwa jicho unalomtazama akikosea. Chuki yako kwa kile alichokutendea, utashangaa itakavyojawa na upendo na rehema juu yake. Kama kweli mtataka mahusiano yenu yadumu, basi nilazima mbadilishe maisha yenu. Lazima mtenge muda wa pamoja na Mungu. Lazima kuweka juhudi za makusudi kuombeana na kumjua Mungu kwa pamoja. Ni lazima, Geb na Nanaa. Msipofanya hivyo, anguko lenu lipo na hakika litawajia. Kama sio karibuni, basi mjue ipo siku. Na mtakuwa mmechelewa.” Mama G aliwahakikishia.

“Geb umekuwa ukiniona nikiomba. Sio kwa kuwa mimi ni mjinga! Ni kwa kuwa nimeishi haya maisha. Nikagundua, sina kimbilio ila Mungu tu. Siendi kanisani kwa sababu mimi ni mkristo. Nakwenda kuungana na wenzangu kuutafuta uso wa Mungu. Siombi pale mambo yanaponiwia magumu tu! Nina mahusiano binafsi na Mungu. Namfahamu Mungu wangu. Naijua sauti yake, mimi mwenyewe. Sihitaji unabii kukamilisha Imani yangu. Nasoma bibilia, naomba, najua Mungu yupo na ananipenda. Ananiwazia mema, kwangu na kwa uzao wangu.”

“Mkinyanyuana mbele za Mungu, mtakuwa na muunganiko wa ajabu sana. Wa  kimwili na kiroho. Nanaa utamuona Geb kwenye ulimwengu wa roho. Utajua kila mtego na hila ya shetani juu ya mwenzio. Hata kama hutajua kwa hakika, lakini kuomba kwa Roho inapaswa. Yeye Roho wa Mungu atapigana badala yako. Ni wewe kuruhusu tu atumie mwili wako.”

“Kadhalika na Geb hivyo hivyo. Huna sababu sasahivi inatakayokuzuia kuishi maisha matakatifu mwanangu. Lazima kubadilika  na kumpa Mungu muda wako. Mruhusu akutumie wewe na mke wako na watoto. Ibada ndani yenu isikome. Lazima kuwepo na ibada ya kweli ndani yenu ili kumruhusu Mungu aendelee kutenda ndani yenu. Hapo mtakuwa salama.” “Mimi sijuagi hata kusali.” Nanaa aliongeza na kufanya wacheke.

“Kweli mama. Itabidi kunifundisha. Wala sijui kusoma bibilia. Kwanza sijawahi. Nikienda kanisani, Padri akisoma na kuongea pale mbele, ndio inatosha. Mpaka tena jumapili kama nitakwenda.” Geb alikuwa akimwangalia Nanaa huku akicheka. “Usinicheke bwana! Ujue ndio maana nilikuwa nashindwa kukulinda kama nilivyokuwa nakuahidi?” “Kwa nguvu zako huwezi kumlinda mwanadamu Nanaa.” “Mbona sasa hivi nimekuelewa! Hata Grace alinihusia. Lakini wakati ule nika… Labda ndio maana tuka..” Nanaa akanyamaza nakukumbuka kila anguko alilopita na Geb. Wakiachana huku wanapendana.

“Hamjachelewa. Huu ndio wakati wa Mungu kwenu na watoto wenu. Tutaomba pamoja. Wote tutaomba toba kwenye maisha yetu. Mungu atutakase. Kisha tutamkaribisha kwenye maisha yenu. Lazima kuanza upya na Mungu. Geb ukipata taratibu za mahari, ulipe. Kisha mrudi kanisani mbariki ndoa. Lakini Oliva lazima akabarikiwe.” “Ndio kama kubatizwa?” Nanaa akauliza.  “Sisi hatubatizi watoto wadogo. Tunawabariki mpaka aje kuwa mkubwa na kujua maana ya anachotaka kufanya. Anafundishwa mpaka anaelewa ndipo anabatizwa.” Geb akamjibu. 

“Hapo nimeelewa. Asante mama. Naona ni wazo zuri. Liv anatakiwa kubarikiwa. Au unasemaje Geb?” “Ni sawa. Ningependa mwanangu abarikiwe. Tumkabidhi mikononi mwa Mungu.” Geb akajibu. “Mama wewe si ndio utamsimamia?” Mama G akacheka. “Kaeni na Geb mkubaliane kwanza.” “Mimi sina neno mama. Wewe fanya vile unavyotaka.” Mama G akafurahi zaidi. “Basi mkitulia, tutaweka mipango ya Oliva kufanyiwa ibada. Na tutafanya kisherehe kidogo. Nataka kuweka kumbukumbu ili akue akijua yeye ni mtoto wa Mungu. Atulie mikononi kwa Mungu.”  Nanaa akafurahia hilo. “Nakushukuru mama yangu.

Asante.” “Karibu. Basi tuombeni.” Mama G aliwaongoza sala ya toba, wakatubu. Nanaa na Geb wakampokea Yesu siku ile wakiwa kwenye magoti.

Mama yao aliwaombea wote kwa kuwashika mikono yao kwa pamoja. Aliwaombea kwa kutubu na machozi. Kisha akawabariki wao wawili na Oliva na watoto wao watakao kuja. Akawaombea ulinzi juu yao. Ndipo akaondoka na kuwaacha. Wakiwa wamejaa furaha. 

~~~~~~~~~~~~

Nanaa alikuwa na furaha ambayo ilionekanika usoni. Kila wakati macho yalikuwa kidoleni. “Umeipenda?” Geb alimchokoza wakati wameachwa pale sebuleni peke yao. “Yaani sio hii pete tu, na ile hali nzima na mimi kuona nimethaminiwa kwa kiasi hiki! Angalia aina yenyewe ya pete!” Nanaa akaenda kupiga magoti pale mbele alipokuwa amekaa Geb. 

“Hebu itazame jinsi ilivyonikaa kidoleni!” Akanyoosha mkono mbele ya macho ya Geb. Geb akapokea ule mkono, akatuliza macho kwenye ile pete kidoleni! “Yaani kidole chenyewe kinajua kimethamaniwa. Mkono mzima unawaka kwa pete! Halafu zaidi moyoni. Ile hali ya moyo wangu kujua kuwa kuna mtu ananihitaji, na anataka kuwa na mimi! Hujui jinsi ulivyonituliza Geb. Moyo na akili zangu vyote vimetulia, kama vilivyopata pumziko.”  Nanaa aliongea kwa hisia zote.

“Nimehangaika sana Geb. Nimehangaika kuliko nitakavyokwambia ukaelewa. Tokea mtoto, hiki ndicho nilichokuwa nikihangaikia. Nilikubali kujidhalilisha kwa hao wanaume, ili tu kufika hapa uliponifikisha wewe. Mpaka juzi nilikuwa pia nipo tayari kumsamehe Zac kwa uongo wowote atakaonidanganya, ili tu anifikishe hapa! Nijisikie hichi ninachojisikia sasa hivi. Siogopi tena kama utanifukuza.” Geb akaanza kucheka.

“Kweli sikuogopi tena. Na wala sina wasiwasi kama utanifukuza. Kwanza hata ukinifukuza nimeamua sitaondoka.” “Kweli Nanaa!?” “Sasa niende wapi?” “Safi sana.” Geb akasifia. “Siwezi kuzima moto aliowasha Mungu wangu au kuzuia baraka alizoanza kunifungulia Mungu wangu. Sithubutu kwa kukimbia. Yaani kwa gafla ni kama mambo yote yananijia pamoja. Nimeanza maisha mapya ndani ya Yesu. Hapo nimejisikia faraja. Nimempata mama. Sio mama tu. Mama G ananipenda kwa ukweli. Sina haja ya kujificha kwake kama mama mkwe wangu. Amenipokea kama nilivyo. Kisha ananiombea bila kuchoka. Haya, nimepata mtoto ambaye sikuwahi kufikiria kama mimi Nanaa, naweza kutoa kitu cha maana kama Oliva.” Geb alicheka sana.

“Kweli Geb. Huwa namwangalia huyo mtoto, siamini kama ni wangu. Mtoto mzuri hivi! Kweli? Yaani mimi Nanaa mtu aliyekuwa akidharauliwa kwa kiasi kile, kumbe kuna mambo makubwa na mazuri ndani yangu! Nikimwangalia Mungu na jinsi alivyonizawadia Liv, hakika ujasiri unajengeka. Nafurahia na ninajivunia umama.” “Hongera.” Geb alikuwa akimtizama pale alipokuwa amepiga magoti mbele yake huku akimsikiliza kwa makini tu.

“Asante. Lakini bado sijamaliza kukwambia baraka zangu, furaha yangu na pale Mungu aliponifikisha.” “Nakusikiliza Nanaa.” Nanaa akacheka kidogo huku akiingalia pete yake. “Haya, Mungu amenipa wewe.” Nanaa akamwangalia. “Asante kwa kunichagua na kunivumilia Geb. Nakushukuru sana.” “Mimi mwenyewe nimefurahi umekubali tuishi wote. Huna makuu Nanaa, unaweza kuishi na kila mtu, na ndio maana nafikiri mama anakupenda.” “Nimehangaika Geb wewe! Huwezi elewa. Nimeumizwa mwili wangu, nafsi na hisia zangu bila kulalamika, ili tu kupata hiki unachonipa wewe. Naomba usinichoke kwa kurudia. Ila ujue nimeshukuru sana kwa hili. Tena unanipa kwa heshima zote! Kwangu sio kitu kidogo Geb. Naomba isitokee tunaachana. Niahidi utaniombea na kunibeba kwenye magoti kama mama alivyotufundisha. Na mimi nitajifunza kukuombea.”

“Nitafanya hivyo Nanaa. Na Mungu atatusaidia. Mimi mwenyewe nimekuwa nikibebwa na maombi ya mama tu. Nataka na mimi nisimame kwenye nafasi yangu kama mume wako na baba wa Liv.” Nanaa akafurahi sana. Wakatulia kidogo kama kila mtu akiitazama ile pete.  “Jumamosi asubuhi tunarudi nyumbani. Na safari hii tunarudi kama kwetu wote.” Nanaa akacheka. “Natamani uone moyo wangu, Geb.” Geb akacheka. “Lakini naomba tukitulia nimwalike kaka James aje amuone mtoto. Hakuwa hata akifahamu kama ni mjamzito! Niliogopa kumwambia.” “Yaani wewe kuwa huru kufanya kile unachotaka. Ni nyumbani kwetu wote.” “Basi kama ndio hivyo, jumapili nitamwambia mama tuandae chakula cha jioni kwa ajili ya kaka James na familia ya Grace.” “Huoni mambo yanavyokwenda vizuri? Nilijua ukiamua kutulia utanitengenezea nyumba nzuri.” Nanaa akacheka.

~~~~~~~~~~~

Nanaa akasimama nakuanza kutoa nguo. “Nilinunua ile chupi. Unataka kuona?” “Sijaoga Nanaa.” “Mimi nimekukaribisha kuona tu Geb! Acha kufika mbali.” Geb akacheka sana. “Nikusaidie kuvua?” “Hapana. Wewe kaa hapo hapo uone. Ukianza kushika tu, utaharibu.” Geb alikuwa akichezesha mguu huku amekodoa macho. “Uwe unageuka sasa! Maonyesho gani hayo ya upande mmoja tu, Nanaa?” Nanaa akacheka.

Alikuwa akivua taratibu huku aking’ata midomo yake. “Tatizo unaharaka Geb. Kuwa mvumilivu.” Nanaa akaendelea kutoa. Mpaka akabakiza sidiria na chupi tu, akabaki amemsimamia Geb pale mbele yake. “Uwiii! Unaniumiza Nanaa!” “Usiamke sasa.” “Kweli Nanaa?” “Sijamaliza maonyesho.” “Au tufanye maonyesho mwishoni?” Nanaa alicheka mpaka akakaa. “Ni nini Geb jamani!? Acha nimalize.” “Njoo unikalie. Hata kidogo tu ndio nitaweza kuendelea na hayo maonyesho.” “Bado hata sijageuka! Subiri kwanza.” “Nanaa naye?” Geb akalalamika. 

         “Kwanza umesema hujaoga!” “Siwezi   tena. Unajua kabisa hiyo rangi jinsi inavyonitesa ikiwa mwilini mwako. Inaamsha kila kitu.” “Umeona jinsi nilivyoweka na kidole changu hapa juu ya paja? Si inawaka?” “Sioni vizuri labda unisogelee hapa karibu.” Nanaa alikuwa anacheka mpaka machozi. “Njoo nikupakate Nanaa wangu.” Nanaa akaenda, akamkalia. “Umependeza sana.” “Asante.” Nanaa alijibu kwa sauti iliyotulia huku akimruhusu Geb ashike na kubusu kila anachotaka hapo mwilini mwake.

Mambo hayakuishia hapo. Pete hiyo ya uchumba ikaenda kusherehekewa na kitandani. Walizungushana hapo kitandani wakicheka na kuzungushana bila kuridhika. Ahadi nyingi ziliwekwa. Ikiwepo ya kifo pekee ndicho kiwatenganishe. Napo pia agano hilo likasindikizwa na penzi la haja wakiitana majina yao masikioni kuhakikisha akili zao na nafsi zinaelewa wapo pamoja.

Jumamosi.

Siku ya jumamosi asubuhi Nanaa alimka, Mama G akaja. Kama kawaida yake ya kumshugulikia mjukuu wake kwanza. Akaingia kwenye chumba kilichokuwa na vitu vya Oliva akamchukua mjukuu wake, wakamsikia akiongea naye. Wakajua atamuogesha yeye mwenyewe. Hakuwa akitaka kuingiliwa na mtu, anapokuwa na mjukuu wake. Nanaa na Geb walikuwa chumbani kwao wakifungasha tayari kwa kuondoka. Geb alimwambia usiku huo lazima wakalale nyumbani kwao. 

“Sisi tupo tayari mama.” Nanaa alimfuata Mama G chumba alichokuwa na Liv. “Huyo Liv anavyovalishwa nguo mpya kila siku! Nyingine atakuwa, na asizivae hata mara moja!” “Hizo zimetoka kwa Grace. Anasema kuna rafiki yake anamuuzia nguo, akaziona hizo za kike, akazipenda.” “Nitamshukuru jumapili akija.” “Wewe mpige picha mwanao sasa hivi, mtumie na ujumbe wa shukurani.” Nanaa akacheka. “Haya mama yangu. Asante kwa hilo.” Pale pale Nanaa akafanya kama alivyoelekezwa na Mama G akamtumia Grace, na Grace hapo hapo akapiga. 

“Mwanao mzuri kweli, utafikiri toto la kuchorwa!” Nanaa akacheka. “Asante.” “Namtuma Danny sasa hivi akai print hii picha na kuniwekea kwenye

fremu ili nije kuitundika hapa nyumbani kwetu.” “Asante sana. Lakini pia ujue mwenzio nimevalishwa pete ya uchumba na Geb.” Kila mtu alianza kucheka. Mpaka Geb aliyekuwa chumba kingine alisikika akicheka. “Nanaa! Mimi sijakupatia mwenzio!” “Sasa sina mwingine wakumringishia mama!” “Kwa hiyo unamringishia Grace?” “Nataka ajue pia ni pete ya thamani. Asije kufikiria ni pete zile zakawaida.” Mpaka Grace alikuwa akicheka. “Hongera sana Nanaa.” “Basi nakupigia picha sasa hivi, nikutumie ili na wewe uone.” Nanaa akaongeza nakufanya wazidi kucheka. 

“Sasa si watakuja kesho wataiona!?” Mama G akamuuliza huku akicheka nakumtizama Nanaa. “Sitalala vizuri mama. Acha tu nimtumie picha aone.” Geb akatoka na kusogea pale kuiona sura ya Nanaa. “Sasa unanicheka nini na wewe Geb? Wewe ushawahi kumuona mtu amevaa pete kama hii?” “Sijawahi ona Nanaa. Wewe ndio wa kwanza. Nilitengeneza huo muundo maalumu kwa ajili yako.” Geb akajibu. “Umeona sasa! Mwambie basi na Grace. Hajasikia.” Mama G alikaa chini kwa kucheka. Grace naye alikuwa anacheka sana upande wa pili. 

“Nimesikia Nanaa.” Grace akaongeza. “Umesikia kwamba hii ni pete ya kipekee iliyotengenezwa maalumu na ‘Geb Magesa’ kwa ajili yangu, mimi Nanaa?” Grace alikuwa akicheka na yeye mpaka machozi. Nanaa alikuwa akiongea taratibu bila haraka. “Ndiyo Nanaa. Nimesikia vizuri sana maelezo ya Geb Magesa.” Grace akajibu akiwa bado anacheka.

“Nisaidie basi kunipiga picha tumtumie Grace ili na yeye aone na kuelewa tunachozungumzia. Asije dhani ni ile miundo ya kawaida aliyozoea kuiona huko mtaani. Kumbe ni muundo uliotoka kwenye kichwa cha Geb mwenyewe.” Geb alikuwa akicheka sana. Akachukua simu ya Nanaa, alikuwa ameshanyosha mkono tayari, akapigwa picha kama tatu. Aligeuza huo mkono ili Geb apate picha pande zote. Hapo hapo akamtumia Grace. Geb akatoka huku akicheka.  

“Basi tutaonana hiyo siku ya jumapili, kesho.” Nanaa akaaga. “Umeridhika sasa?” Mama G akamuuliza. “Sana mama. Leo nahisi nitalala.” Nanaa akajibu. “Kweli ni nzuri.” Grace aliongea akisika akiangalia hizo picha. “Umeona eeh?” Nanaa akauliza. “Nimeona Nanaa. Hongera sana. Pete nzuri na ya thamani kubwa. Hii kweli inaonyesha umevalishwa na Geb Magesa.” Nanaa akafurahi sana. “Asante Grace. Nitakuonyesha vizuri ukija hiyo kesho.” Wakacheka tena.

          “Lakini mwaliko wenyewe naona upo mbali. Yaani kuja jioni!” Grace akalalamika. “Wewe njoo muda wowote unaotaka.” “Afadhali. Nitakuja asubuhi na nguo za kubadilisha za Fili. Mumuogeshe kabisa wakati mimi nalala hapo hapo kwenu. Kwa hiyo basi mtuweke kwenye mlo wa siku nzima.” Nanaa akacheka. “Kuna watu wamenyimwa aibu!” Mama G alidakia na Grace akamsikia. “Yaani mama naye? Nyinyi mkitaka kumkaribisha mtu, mkaribisheni mtu ajisikie vizuri.” “Acha uvivu wewe. Tulia kwako, pikia familia yako, jioni ndio uje.” “Mbona Nanaa mwenyewe amesema hana neno, mama jamani!? Kwa nini kutuingilia?” “Atajuta kukufahamu huyo Nanaa!” “Mwache tu waje mama. Ndio vizuri tuwe wengi.” Nanaa akajibu.

“Basi huyo utamchoka, wewe muendekeze tu. Haambiwi hivyo huyo! Hapo alipo hajigusi kwa lolote. Anataka afanyiwe kila kitu. Na usifikiri akikwambia atakuja asubuhi, anakutania? Atakuja kweli. Hapa nilikuwa namzuia kuja tokea umerudi na Oliva. Nikawa namzungusha, sasa umemwambia akaribie, ujue hatakaa aondoke.” Mama G aliendelea kumtahadharisha Nanaa.“Hamna shida. Mwache aje tumsaidie Fili.” “Afadhali mwaya Nanaa. Basi nitakuja na nguo za kubadili kabisa kwa ajili ya kwenda kazini jumatatu.” “Si nilikwambia wewe Nanaa? Ona sasa!” Mama G akadakia, Nanaa akazidi kucheka. 

“Usisahau basi na za Fili za kubadili.” Nanaa akaongeza. “Nitakuletea sanduku lake la nguo kabisa na begi lake la shule. Geb atakuwa akifanya naye homework, maana Danny anakuwa mkali kweli kwa mwanangu. Sina raha!” “Mmmhhh!” Mama G akaguna. “Sasa mama unaguna nini? Mbona kama hufurahii ujio wangu?” “Mimi naguna na yangu.” Mama yake akamjibu. “Asante mwaya Nanaa, maana bado nina shida na wasichana wa kazi. Kila wakija wakijua nakaribia kujifungua mapacha, wanakimbia.” “Wewe njoo tuishi wote kama zamani. Mimi na mama tutakusaidia.” “Wewe Nanaa! Jisemee nafsi yako. Mimi tayari nina Oliva.” Nanaa alizidi kucheka. “Mama naye kwa ubaguzi! Si wote watoto?” “Sitaki kuingiliwa na mipango yangu. Wewe tafuta msichana wa kazi tulia kwako.” “Mwaya Nanaa tutazungumza vizuri.” “Sawa. Usiwe na wasiwasi, naamini kila kitu kitaenda sawa.” Nanaa akaongeza wakaagana na kukata simu.

~~~~~~~~~~~

“Ujue huyo mwenzio hakutanii? Hana msichana wa kazi, ujauzito una miezi 8, ana mtoto mdogo, hajiwezi kwa lolote.” Mama G alijaribu kumtahadharisha Nanaa. “Tumekubaliana na Geb nibaki nyumbani, nisitafute kwanza kazi ili kumlea Liv, hata wewe utakaporudi kazini, pia nitakuwepo tu nyumbani. Sitakuwa na kazi nyingi zakufanya. Sitashindwa kumsaidia. Usiwe na wasiwasi mama.”

“Unauhakika Nanaa? Maana alikuwa akiomba tangia mimba ina miezi 6 aje tuishi naye, lakini ndio na wewe ukaja na mtoto nikamwambia kwa wakati ule nisingeweza kuna kitu kinanishikilia. Sikutaka aje pale wakati wewe mwenyewe hujatulia. Halafu nikaona tutakulemea.” “Sasa hivi nimetulia mama. Akili na mawazo yangu yote yapo kwa Geb.” Mama G akaanza kucheka.

“Simaanishi hivyo bwana mama! Acha kunicheka.” “Umesema mwenyewe.” “Namanisha hivi, shida yangu nilikuwa natafuta kutulia mama yangu. Sijawahi kuwa na kitu changu au watu wanaonizunguka na kunithamini hivi. Sasa hebu niambie mama, sasa hivi nataka nini nisiyetulia na Geb wangu, na mtoto?” “Kuna vishawishi Nanaa. Na wewe ulivyo mzuri hivyo!” “Ndio maana namtaka Grace aje. Kuna kitu alinifundisha. Lakini alinifundisha kwa kifupi sana. Aliniambia wewe ndio ulimfundisha. Anakitumia hicho kitu na kinamsaidia sana kwenye maisha yake. Hasa mahusiano yake na Danny. Sasa kama na uzuri ule alio nao Grace, ameweza kutulia kwenye mahusiano yake vile, sembuse mimi Nanaa! Waache tu waje tuishi nao mama. Ujue mimi ndio nawahitaji nyinyi kuliko utakavyo dhani.” Nanaa alianza kutokwa na machozi.

“Sijawahi kuwa na watu kama nyinyi mama yangu. Yaani hivi mkitaka tuishi wote mimi ndio nafurahi zaidi. Nimezoea kuona watu wakinikimbia, sio kunikimbilia. Muache tu aje. Hata kama atataka aishi hapo hapo na wanae wote hata akisha jifungua, wewe mwache tu.” Mama G akacheka. “Kweli mama. Kwanza nyumba yenyewe kubwa ile, huwezi hata kusema tutabanana. Halafu kumbuka mimi nilishaishi na Grace na familia yake. Hana muda na mtu mwingine zaidi ya Danny na mwanae. Grace mkimya sana. Ongea yenyewe ni shida. Usiwe na wasiwasi kabisa.”

“Nashukuru Nanaa. Na ni afadhali kama wewe mwenyewe umeridhia. Najua Geb hana shida kama wewe hutakuwa na shida.” “Ulishazungumza naye?” Nanaa akauliza. “Wewe ndio ukazungumze naye, mumeo. Siwezi kuanza kuzungumza na Geb kabla yako Nanaa. Mambo yamebadilika. Sasa hivi mpo wawili sio kama zamani. Lazima niheshimu hilo.” Ilimgusa sana Nanaa, akaona ile heshima anayopewa, akajisikia vizuri.  

“Nashukuru mama yangu.” “Zungumza naye. Mwambie shida ya Grace. Tukifanikiwa kupata msichana haraka, wataondoka.” “Wala usiwe na wasiwasi kabisa mama!” “Nashukuru kunituliza. Namuhurumia kweli! Tumbo kubwa kama amebeba tembo! Hawezi kufanya chochote.” Nanaa akacheka. “Unafikiri nakutania? Utamuona. Akisimama, utaona tumbo na tako tu. Ananikumbusha enzi za ujauzito wao. Sasa heri mwenzangu yeye mrefu kidogo. Sasa mimi nilikuwa sio mrefu vile. Na watoto wawili tumboni, tena warefu! Nilikuwa nachoka kama mkimbia riadha! Kweli anahitaji msaada. Nashukuru kumkubalia.” “Usijali mama yangu.” Waliendelea kuongea mpaka Geb alipoingia na kuwaambia amemaliza kuingiza mizigo yao kwenye gari na ameshalipia, yupo tayari, kuondoka.

~~~~~~~~~~~

“Njoo tuzungumze kwanza huku chumbani wakati mama anatangulia kwenye gari na Liv.” Geb akamfuata nyuma Nanaa. “Vipi?” Geb akamuuliza. “Sijui nimekosea?” “Nini?” “Nimemkaribisha Grace na familia yake tuje tuishi nao tena pale kwa muda kwa kipindi hichi anatafuta msichana wa kazi.” “Nimesikia mazungumzo yote.” Nanaa akapooza. “Nimekosea? Samahani nimemkubalia bila kuwasiliana na wewe kwanza. Mwenzio ninafuraha nashindwa kujizuia.” Geb akacheka, akamvuta karibu Nanaa. Akamkumbatia na kumbusu kichwani.

          “Hapana hujakosea. Wewe unajua historia yetu. Grace nimekuja naye hapa duniani. Tukiwa tunaishi naye kwenye tumbo la mama pamoja. Haya, tumekuwa naye.  Tukasoma naye, na mpaka sasa tunafanya naye kazi. Ofisi moja, kasoro tu vyumba ndio tofauti. Ndiye msaidizi wangu pale kazini au kwenye biashara zangu. Ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu. Lakini wewe kwanza. Nimekuomba ujenge nyumba yetu. Mimi na wewe. Naomba uwe makini, usiingize mambo mengi ambayo utajilazimisha na kukosa amani. Huna kimbilio, na mimi sina kimbilio, isipokuwa kwenye hiyo nyumba utakayoijenga wewe. Ukisharuhusu mianya mingi ili kufurahisha watu, ujue kwa haraka sana itaanza kutulowesha sisi wenyewe. Na mimi na wewe ndio tutakuwa waathirika wa kwanza. Kwa hiyo, narudia tena, nakuomba ujenge nyumba yetu. Mimi na wewe.” Nanaa akavuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha taratibu.

“Kwa hiyo naomba uwe muwazi. Una uhakika kama kweli upo tayari kuishi nao tena? Kama huna uhakika, mimi naweza kuzungumza nao vizuri, ili wasikuelewe wewe vibaya.” “Nina uhakika Geb. Niliishi na Grace wakati ule nikimuhesabu kama bosi wangu. Alikubali kunihifadhi kwako, huku akiniheshimu. Sioni kama kutakuwa na shida yeyote wakija kuishi pale tena. Halafu namuhitaji Grace. Nataka kujifunza kwake mambo mengi.” Geb akacheka. 

“Kweli tena. Kipindi kile cha misukosuko ya  mpaka ukafungwa jela, alinifundisha kitu kizuri sana mpaka nikajirudi kwako.” “Nilishangaa siku ile! Maana tokea unaamka ulikuwa umenikasirikia unanifukuza kwa maneno makali. Nikashangaa jioni yake umeniomba na msamaha.” Nanaa aliona aibu akacheka. “Basi ilikuwa kazi ya Grace ile. Alizungumza na mimi vizuri sana. Sema nafikiri maneno yake niliyafanyia kazi nusunusu. Ninauhakika ningefanyia kazi ushauri wake wote, hakika ningekusikiliza siku nilipowakuta na Liz. Nataka niwe karibu na Grace. Nijifunze kwake. Niulize maswali yote. Labda na mimi nitakuwa mke mwema kama yeye.” Geb alifurahi sana.

“Sawa kama ndio hivyo.” Nanaa akambusu Geb. “Una roho nzuri wewe!” “Nyinyi ndio mmenifundisha Geb. Bado najifunza. Sijawahi ona upendo kama mlionionyesha nyinyi na mama yenu. Sasa hivi najihisi kama Mama G ni mama yangu mimi sio wewe.” “Basi nakuachia moja kwa moja.” Nanaa akacheka sana. “Twende, tusimuweke sana na mtoto.” Wakatoka huku wamekumbatiana wakitembea.

“Nanaa!” Geb akamuita wakati wakiendea gari yao. “Abee!” Nanaa akanyanyua kichwa kumuangalia mpenzi wake. “Kuanzia leo, lazima tuanze kuomba pamoja. Tuhakikishe hatukosi kwenda kanisani kila siku ya Jumapili. Kwa kuwa jumapili hii tayari imeshaingiliana na mipango mingine, basi kuanzia jumapili ijayo tuanze kwenda kanisani. Mama alikuwa akinisisitizia sana maisha matakatifu. Lakini akili ilikuwa haijatulia.” “Sasa hivi imetulia?” Nanaa akauliza na tabasamu. “Ukiwa pembeni yangu hivi, nakujua upo hata nikitoka kazini utakuwepo nyumbani unanisubiri. Si akili tu inayotulia, hata moyo wangu umejawa faraja ya ajabu, Nanaa. Nakupenda kuliko nitakavyokwambia.” “Na mimi nakupenda Geb. Nakuahidi utanikuta nyumbani kila siku, labda itokee dharula au nife. Lakini nitahakikisha unanikuta nyumbani nikikusubiria wewe.” Geb aliinama akamnyanyua kidevu chake. Akambusu.

“Asante mpenzi wangu. Na kingine, unakumbuka ile huduma ya Antii?” “Mambo yalishakuwa mengi, nikasahau mwenzio.” Geb akacheka. “Nafikiri tumshirikishe mama. Tufanye sisi kama familia. Tunaweza kufanya hata mara moja kwa mwezi.” Geb alitoa wazo. “Ni kweli. Kwa kuanzia sio mbaya.” Wakawa wamefika kwenye gari.  

Kwenye Umoja Na Amani, Mungu Huamuru Baraka.

Nanaa, Geb na Liv walikuwa kwenye gari ya Geb, wakati Mama G akiendesha gari yake kurudi nyumbani. Nanaa alishangaa wanapita. “Huyu Liv anasinzia. Ungetushusha sisi kwanza nyumbani, nikamlaze halafu ndio uendelee na shuguli zako.” “Ndio tunakwenda nyumbani kwetu.” Nanaa akakunja uso akamwangalia Geb, akanyamaza. Alishangaa Geb anapiga honi kwenye nyumba yake mpya, geti ikafunguliwa wakaingia. “Kwani hapa si ulisema bado hujamaliza?” “Hivi unajua ni mwaka sasa tokea niseme hivyo?” Nanaa akacheka. “Kwa hiyo ndio tunahamia hapa?” Nanaa akauliza huku akishangaa. “Hapa ndipo nataka ujenge nyumba yetu. Mimi, wewe na watoto wetu.” Nanaa alimwangalia Geb akateremka kwenye gari. Alibaki ametoa macho akizunguka. Geb akashuka na Liv. 

“Juu ni kwetu. Mimi wewe na watoto wetu. Chini ni kwa mama na wageni wetu.” “Pakubwa! Hongera Geb.” Nanaa aliendelea kushangaa. Japokuwa alikuwa akiishi nyuma ya ukuta huo, lakini hakuwahi kufika hapo ndani. “Asante. Lakini hili litabakia ni jengo tu mpaka utakapoijenga ikawa nyumba. Naomba thamani yake iwe ni amani na upendo na si vinginevyo.” “Mungu atatusaidia Geb. Usiwe na wasiwasi.”  Mama G naye akaingia.

Aliegesha gari yake akateremka. “Hongereni.” Mama G akawasogelea, Nanaa akamgeukia Geb. “Hongera hiyo inakuhusu na wewe Nanaa. Hatukuwa hata na mpango wa kuhamia hapa mpaka ulipokubali kuishi na sisi. Muulize mama.”  “Wala si utani. Mimi nilishajiridhikia pale pale tulipokuwa tukiishi. Na hivi magoti yenyewe yananisumbua, sikutaka nyumba za ngazi.” Nanaa alianza kulia. Geb akamkumbatia wakati amembeba Oliva. “Naona mtaniangushia mjukuu. Namuombeni nikamlaze, nyinyi endeleeni kubembelezana.” Nanaa akacheka. “Mama jamani!” “Sasa je! Badala ufurahi, unalia wakati Liv wangu anasinzia!” “Sikutegemea mwenzio! Halafu hata Geb hakuwa ameniambia. Ndio tunaingia hapa na kukutana na hii nyumba! Sikutegemea hata!” “Najua Nanaa mwanangu. Nilitaka tu ucheke. Lakini nakuelewa kabisa. Mungu amekupumzisha. Nawaombea heri, mzidi kufanikiwa.” “Amina mama yangu.” Mama G, akamchukua mtoto wakaingia ndani. 

“Sasa huko ndani atamlaza wapi? Wakati vitu bado vipo kwenye gari, mpaka kitanda chake bado kipo kwenye gari!” Nanaa alinong’ona wakati Mama G akiondoka. “Amenunua kitanda kingine cha Liv akakiweka chumbani kwake ili mchana akiwepo mwenyewe nyumbani awe analala chumbani kwake, hataki kupandisha ngazi.” “Anavyompenda huyo Liv!”  Nanaa akanong’ona. “Sana. Wewe nenda chumbani kwa mama utaona. Mimi mwenyewe nilikuwa namuuliza sasa hicho ni chumba cha Liv au chake!? Kimejaa vitu vya Liv vitupu. Sijui kama atarudi kazini hivi karibuni.” Nanaa akacheka.  “Anambadilisha cheni za dhahabu kila siku!” “Jana yenyewe nimemsikia akiongea na sonara wake, akimsisitiza amalizie bangili za Liv haraka. Kafurahi sana kumpata Oliva.” Geb naye akanong’ona

“Ila amepungua sana. Mpaka nimeshindwa kumuuliza.” “Ungemsifia tu.” “Kweli!?” Nanaa akauliza kwa mshangao. “Kafanya kazi kubwa sana kufika hapo. Ilinibidi kuajiri mtu maalumu wakumfanyia mazoezi. Alikuwa anakuja nyumbani kila siku usiku anafanya naye mazoezi. Mpaka akafikia hapo alipo. Hivi amejiunga kwenye gym yake huyo jamaa. Anakwenda mara 3, kwa week. Tena huyo jamaa alinitafuta juzi kuniulizia mama, maana hajamuuona muda wote uliporudi na Oliva. Ndio nikamwambia asiwe na wasiwasi, ataendelea tu. Daktari alimwambia lazima apungue ndio atapata nafuu ya magoti.” “Na ni kweli sijamsikia akilalamika magoti tena!” “Basi ilikuwa kazi ya mazoezi kupunguza huo mwili.” “Basi nitamsifia. Maana naona hata kula yake ya makini sana.” “Sana. Amebadilika ulaji wake. Sio kama zamani.” Wakaingia ndani.

{Ni kweli hakuna mwanadamu anayeweza kutoa kumshinda Mungu.} Akiwa tayari kupokea familia nzima ya Grace kwenye nyumba ndogo waliyokuwa wakiishi zamani. Kwa ukarimu tu, akimuhurumia Grace na kukumbuka ukarimu aliomtendea zamani akiwa hana pakuishi akiwa amefukuzwa na mama yake mkubwa, Grace akampokea na kumuonyesha upendo wote, wala Nanaa hakuwa akijua kama atakabidhiwa nyumba kubwa vile kwa heshima zote. Tena akitambuliwa kama mke wa Geb, nakupewa heshima zote. {Ni kweli wema hauozi! Ipo siku wema wako utakufuta tu!} Ameshuhudia Grace na Nanaa pia. {Tenda wema, nenda zako. Usingoje shukurani kutoka kwa mwanadamu. Mpe Mungu nafasi ya kukushukuru.}

~~~~~~~~~~~

Na kweli asubuhi ya saa tatu, ya siku ya jumapili Grace na familia yake wakaingia humo ndani. “Mtoto amekuwa mwepesi kama karatasi! Mnampa chakula huyu kweli?” Mama G akaanza kulalamika baada ya kumnyanyua Fili. “Hataki kula, mama. Na mimi nakuwa nimechoka sina muda wakukimbizana naye.” “Na wewe Danny?”  Mama G akamgeukia Danny, mkwewe. “Naomba huyo umuache mama. Anamchapa mwanangu!” Grace akaingilia. “Si umesikia mama yangu? Mtoto huyo hagombeshwi wala haguswi. Grace akikupa chakula umlishe huyo Fili, kwanza anataka ale mahali alipojilaza yeye, na awe amempakata huyo baba mtu mzima! Ukimkaripia tu labda atafune au akae vizuri, basi mama yake pressure inapanda! Kwa hiyo kwa kifupi huyo mtoto hali. Michezo imemzidi na mama yake anamfuatisha kile anachotaka huyo Fili. Anaweza kukuamsha usiku umpashie maziwa moto, wakati amekataa kula yeye mwenyewe. Ukimwambia Grace hiyo ni tabia mbaya, tusimzoeshe hivyo. Anakwambia atakuwa amerithi kwa Geb, na ndio maana eti wewe mama unampikia Geb uji mpaka leo na hulalamiki kwa nini mimi nalalamika! Namwambi angeniacha mimi nimchape huyo mtoto siku tatu tu, angekula. Basi tena hapo mama mtu ndio pressure juu.” Geb alicheka na kutingisha kichwa.

“Anko ndio amemuharibu mtoto!” Grace akaongeza. “Huyo mtoto sio mvivu wakula hata kidogo. Ni shuguli tu ndio zimemzidi. Akichwapwa mara zake mbili au tatu tu, atabadilika.” Danny akaongeza kwa msisitizo, Mama G alikuwa amenyamaza huku amempakata mjukuu wake akimchezea nywele. “Si mmemuona bibi yake alivyo nyamaza? Anajua ni kweli.” Grace akamtetea. “Nyinyi wote hamna muda na huyo mtoto. Mnamuonea bure Fili mjukuu wangu. Niachieni mimi huyo mtoto muone. Ndani ya mwezi mmoja atakuwa amebadilika. Mtoto amebaki mifupa mitupu! Atabadilika tu.” “Mmemsikia mama? Ana uzoefu na watoto wasiopenda kula.” Geb alibaki akicheka.

Kweli Grace alikuwa amechoka. Alipitiwa na usingizi pale pale kwenye kochi akiwa amekaa, mumewe akaomba asiamshwe. Aachwe alale kidogo. “Hajalala usiku kucha. Mbavu zinamuuma. Naombeni tu kitu nimfunike hapo hapo.” “Amekula sasa?” Mama yake akauliza. “Wala usipate shida kwenye swala la kula. Anakula kama mchwa. Ataamka mwenyewe akisikia njaa.” Mama yake aliingia ndani akaenda kumletea shuka na kumfunika vile vile alivyokuwa amekaa. Akabaki akimwangalia. “Unahakikisha kuwa anakunywa maji ya kutosha? Midomo imemkauka, halafu nahisi anakonda! Uzito wake ukoje?” Mama G, akaendelea kumuhoji Danny.

 “Mara ya mwisho nilivyompeleka kliniki walisema kila kitu kipo sawa, lakini akazane kunywa maji.” “Nimeona midomo mikavu!” “Anasema maji hayana ladha.” “Sasa hapo ndipo pakukazana Danny. Sio lazima anywe mengi kwa wakati mmoja. Anywe kidogo kidogo lakini hakikisha anakuwa na chupa ya maji wakati wote. Lazima anywe maji.” “Nitafanya hivyo mama.” “Na vyakula sio unasema anakula kama mchwa, kumbe ni chips mayai. Anatakiwa..” Mama G akanyamaza. “Lakini kwa kuwa yupo hapa, nitahakikisha mwenyewe anakula vizuri.” Akarudi jikoni alipokuwa Nanaa. Nanaa alikuwa akiwasikiliza. Alimuonea wivu Grace. Mama yake bado alionyesha kumjali. Akajiambia ndio faida zakuwa na mama maishani.

Wakasaidiana na Mama G kupika karibia siku nzima. Walikula kuanzia kifungua kinywa pamoja na chakula cha mchana huku wakicheka. Danny hakuishiwa maneno. Kila kitu mle ndani kilikuwa chakuvutia. Nanaa alifurahia ile nyumba, asiamini kama ndio kwake. Ilipofika jioni, akasaidiana tena na Mama G kuandaa meza, akaoga na kuungana na wengine pale sebuleni wakimsubiria James afike ili wale chakula cha usiku pamoja. 

~~~~~~~~~~~

Nanaa alionekana na wasiwasi sana. “Vipi?” Geb akamuuliza. “Namuhofia kaka!” Mara akasikia mlio wa gari nje, akajua ni kaka yake. Nanaa akasimama. “Naomba unipe muda naye hapo nje. Nataka kuzungumza naye kwanza kabla hajaingia humu ndani.” Kabla Geb hajajibu, Nanaa akatoka kwa haraka, akakimbilia nje. “Mbona mwenzio anakimbia?” Mama G akauliza. “Anataka kuzungumza na James kwanza kabla hajaingia ndani. Hajui kama Nanaa ana mtoto na wakati alikuwa akiendelea kuwasiliana wakati wote hata alipokuwa chuoni. Hakumwambia hata kama ana ujauzito. Aliniambia alikuwa akimkwepa sana. Hata alipokuwa akitaka waonane, Nanaa alimtafutia sababu. Hapo walipo hawajaonana zaidi ya miezi 6. Alipogundua tu ni mjamzito, akaanza kumkwepa. Walikuwa wakiwasiliana kwa simu tu.” Kila mtu akanyamaza wakakumbuka ukali wa James kwa dada yake.

Kila Mwenye Dada Hakosi Shemeji.

James alishuka kwenye gari, Nanaa akamsogelea. “Shikamoo kaka.” “Marahaba. Naona unazidi kupendeza tu! Au ndio furaha yakumaliza chuo?” Nanaa akatoa kicheko cha hofu. “Kabla hujaingia ndani, naomba tuzungumze kwanza.” James akatulia kidogo baada ya kuona wasiwasi usoni kwa Nanaa. “Kwema!?” James akauliza huku akiegemea gari lake. “Unakumbuka kipindi kile nipo chuoni ulikuwa ukitaka tuonane lakini nilikuwa nakupa sababu?” “Nilijua ulikuwa ukinikwepa.” “Ni kweli nilikuwa nakukwepa.” “Kwa nini!?” Nanaa akameza mate na kujiweka sawa. 

Akamuona kaka yake amekunja uso kama haelewi. “Nanaa!?” “Kwa sababu nilikuwa mjamzito.” James alitulia kidogo akabaki amkimtizama. “Mimi mwenyewe sikutegemea kaka. Nilikuwa kama nimechanganyikiwa, ndio maana sikutaka kumwambia mtu mpaka nimalize mitihani.” “Mtoto yuko wapi?” James akauliza. “Ninaye.” Nanaa akajibu huku akimwangalia James. “Samahani sana kaka yangu.” “Umejifungua lini?” “Nilipokuwa kwenye mitihani. Kwa hiyo alishatimiza miezi miwili sasa.” James akanyamaza.

“Anaitwa Oliva.” Nanaa akaendelea. “Nilipanga kukwambia nikishapata sehemu ya kuishi.” “Umeshapata sasa?” “Ndiyo.” Nanaa akajibu kwa kifupi na kubaki wakiangaliana na kaka yake kama anayesubiri Nanaa aendelee. “Nimepata sehemu ya kuishi, ni hapa.” James akakunja uso kama anayevurugwa zaidi. “Ni mtoto wa Geb!” Ulipita ukimya wa sekunde kadhaa, James akiwa amepigwa na butwaa. “Amenivalisha na pete, hii hapa.” Nanaa alimuonyesha kaka yake huku mkono mzima ukitetemeka. James alimpita dada yake kwa hasira, na kuelekea ndani bila ya kujibu kitu.

~~~~~~~~~~~

Kumekucha…

 Geb huyu aliyezaa na Nanaa, ndiye aliyekuwa amepigwa marufu hatakumsogelea Nanaa. Leo amemzalisha na kukaa kimya. Anambeba James kwa mbeleko gani? Penzi limenoga kwa Nanaa & Geb. Kazi ya Nanaa ni kujenga nyumba mpya ndani ya huo mjengo wa thamani. Mipango na mikakati ya maisha imeanza.

Je watafanikiwa? Endelea kuwa nao.

 

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment