Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Ni Wangu! - Sehemu Ya 34 - Naomi Simulizi

Ni Wangu! - Sehemu Ya 34

 Geb akaendelea. “Sikujua kama Zac huyu, ndiye Zac uliyekuwa ukimzungumzia wewe. Mpaka hivi leo nilipowakuta mmekumbatiana hapa. Ndio nikajua Zac huyu unayemwita wewe mpenzi wako, ndiye Zac huyu huyu mume wa Ndina.” Nanaa akashituka sana na kuumia. “Kumbe ulikuja kumuoa Ndina!?” Akamuuliza Zac kwa mshangao mkubwa huku machozi yakisindikiza swali lake lililojaa uchungu. Geb alibaki kimya na yeye akimtizama Zac.

“Ndio katika mambo niliyotaka tuzungumze jana, lakini uliondoka.” Nanaa akahisi kizunguzungu. “Nilimuoa ndoa ya mahakamani ili ili, na nihii…” Akamgeukia Geb, aliyenyanyua kikombe chake cha uji kwa mkono wa kushoto akanywa, huku amembeba mwanae kwa mkono wa kulia, kisha akabaki akimtizama na yeye Zac. Akacheka. Geb alikuwa akimtizama Zac kwa dharau. “Hivi unajua jana uliniliza wewe? Nikajua nimepata mpinzani wangu! Kumbe ni wewe tapeli wa mapenzi tu!” “Mimi sio tapeli wa mapenzi Geb. Nilimuoa Ndina, baada ya Nanaa kuniacha, na sasa narudi kwa Nanaa, baada ya kuachana na Ndina.” “Umeruka kipengele kimoja Zac. Ulikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya siri na Ndina, wakati ulipokuwa na Nanaa.” Geb akaongeza na kuzidi kumshangaza Nanaa na kumuumiza.

“Kumbe mlikuwa wapenzi!?” Nanaa akauliza akionyesha kuchanganywa zaidi. “Wakati ule tulipokuwa na wewe, hatukuwa wapenzi, ila tulishakuwa na mahusiano naye tulipokuwa mwaka wa kwanza, tukaachana kabisa. Na yeye akapata mchumba wake, na mimi ndio nikakupata wewe.” Zac akajitetea, asijue kuwa ndio anaharibu zaidi. Nanaa aliinama huku amefunika uso wake akilia.

“Niliwezaje kuwa mjinga kiasi kile nikashindwa kuwagundua!?” “Kwa kuwa sikuwa na mahusiano naye tena! Nilikuwa na wewe tu Nanaa. Nakupenda wewe. Nipe nafasi unisikilize. Twende mahali tukazungumze.” “Hutaondoka na Nanaa hapa, mpaka umwambie ukweli wote, Zac. Na ninakuonya, usimdanganye. Kwa kuwa sitakuruhusu uendelee kumdanganya. Madhara yakukiuka huu ushauri wangu, utayapata  wewe na Ndina mzazi mwenzako. Sikutanii.” Geb alisisitiza. Asijue anazidi kumchanganya Nanaa zaidi. “Umezaa na Ndina!?” Nanaa akauliza akionyesha kuzidi kuchanganyikiwa zaidi ya mwanzo. “Wewe Geb umemfahamuje Ndina?” Geb akamgeukia Nanaa. “Naomba usikie kutoka kwa Zac mwenyewe, ila ujue hivi tunavyozungumza, Ndina ni mfanyakazi wangu.” Geb akajibu na kunyanyua tena kikombe cha uji. Alikuwa amekaa wakati Nanaa na Zac wakiwa wamesimama.

“Nakupenda Nanaa.” Zac akaongeza. “Hayo ndiyo maneno unayojua Nanaa anapenda kuyasikia. Kwa hiyo unayatumia kwa wingi ili kupumbaza akili zake, ashindwe kufikiria. Naomba acha kumdanganya Nanaa, mwambie ukweli.” Geb aliendelea kusisitiza. “Kama unaona haupo tayari kuzungumza na Nanaa, uniambie, nimtume dereva amlete Ndina sasa hivi. Ili yeye ndio ampe ukweli wote Nanaa. Ujinga na umalaya uliokuwa ukiufanya huko nchini Malaysia. Vile ulivyomtelekeza yeye na mtoto baada ya kufika huko. Yote hayo nitataka Nanaa ayafahamu, ili akujue vile ulivyo Zac. Na ajue kwenye hiyo mikono inayomkumbatia sasa hivi, ina uzoefu wa kuliwaza wanawake kama yeye, na hiyo midomo inayombusu sasa hivi, ajue ina uzoefu wa kudanganya na imepita kwa wanawake wengi tu, na wala yeye hatakuwa wa mwisho, kwa kuwa ndivyo ulivyo. Hawakuiti player kwa makosa. Ni kwa kuwa una uzoefu wa wanawake. Unajua kucheza na akili zao na fikra.” Geb akaendelea, akisikika ameanza kukasirika. Nanaa akajua.

“Kwa masaa ambayo hata hayajatimia 24, tokea ukutane na Nanaa, umefanikiwa kuingia kwenye akili zake, yupo tayari kuniacha mimi na mtoto anayempenda kuliko nafsi yake, ili awe na wewe! Umempa njia rahisi sana yakumuwezesha kuwa mbali na sisi, ili tu uwe naye kwa muda. Nanaa amepata familia ya watu wanaompenda, Zac. Hakuna hata mmoja kati yetu asiyetambua thamani ya Nanaa. Ndio maana leo hii siku ya kazi, mimi, Geb, ninayemuweka mjini mkeo na mtoto wako, nipo hapa sasa hivi na Nanaa. Unajua ni pesa kiasi gani napoteza kila saa ninayokaa hapa?” Geb akagomba.

“Tena nikiwa na wewe unayeniharibia siku yangu ninayolipia garama kubwa sana! Siku ya leo ilikuwa yangu, Nanaa na Liv. Nimekubali mambo yote yasimame kwa ajili ya hawa watu wawili, lakini umevuruga. Mama yangu amepika vyakula vyote vile sio kwa kuwa hana mambo mengine yakufanya, au Nanaa hawezi, nikutaka Nanaa atulie, apate muda wakufikiria mtoto na mimi tu, lakini wewe mvurugaji umeingia. Umeacha kidonda kikubwa sana moyoni kwa Nanaa. Kimeharibu moyo wa Nanaa, haamini tena kama anaweza kupendwa kwa dhati.” Geb akaendelea.

“Haamini wanaume wote. Haamini kama wapo wanaume tunaweza tukawa na hamu yakufanya mapenzi, lakini tukamudu kutawala hisia zetu. Haamini, kwa ajili yako.” Geb akaendelea kuharibu zaidi. “Nanaa anajua kama yupo mwanamke wakiarabu unayeishi naye sasa hivi, tena ndiye anayekuweka hapa mjini? Umemwambia kama hizo zawadi unazotaka kumpa sasa hivi, zinatoka kwenye pesa anayotolea jasho mwanamke mwenzie?” “Nitamuacha kama Nanaa akinikubali.” Zac alijibu bila wasiwasi na kumshangaza Nanaa.

“Naomba uondoke Zac. Tafadhali sana, naomba ondoka.” Geb alishamaliza uji wake kwenye kile kikombe kidogo, akabaki akiwatizama. “Ondoka na zawadi zako.”  Nanaa akasisitiza. “Nashauri uweke nguvu kwa mtoto wako, kama umeshindwana na Ndina. Yupo katika wakati mgumu sana. Mtoto wako mgonjwa, na Ndina anasema hutaki kuzungumza naye. Ni wakati ambao mtoto wako anakuhitaji sana, kwani ugonjwa alionao, unahitaji uangalizi wakaribu wa mama yake, na yeye anashindwa kuwa naye wakati wote, kwa kuwa anahitajika awepo kazini, atengeneze pesa. Mtafute Ndina, ujue habari za mtoto wenu. Haya, naomba uondoke kama alivyokuomba Nanaa.” Geb akasisitiza.

Kisha akamgeukia Nanaa. “Kama huyu ndiye Zac uliyekuwa ukinisimulia, hastahili hata tone la chozi lako. Nakuhakikishia Nanaa. Zac unayemfikiria na kumzungumzia wewe, siye huyu hata kidogo. Hastahili umlilie. Na ninakushauri usipokee vitu vyake. Ana mtoto mgonjwa, ambaye hataki kumuhudumia, anazunguka na wanawake tu mjini. Mwanae anahitaji msaada  wa Zac, kuliko hivyo anavyopoteza pesa kukununulia wewe zawadi huko Kariakoo, halafu anakudanganya amenunua nje ya nchi. Amerudi nchini muda mrefu sana. Hawezi kuwa alikununulia zawadi muda wote huo, akazitunza wakati yeye mwenyewe anatunzwa na mwanamke.” Bila kuongeza neno, Zac akatoka akiwa na mfuko wake mkononi, akamuacha Nanaa amesimama anakausha machozi huku ameinama. Aibu! Mbio za sakafuni zikaishia ukingoni.

~~~~~~~~~~~~~~~

Geb akasimama, akaenda kuchukua mizigo yote pale mapokezi, akarudi kwa Nanaa, twende ukale. Wakaanza kuongozana kurudi kwao, Geb akiwa amembeba Liv na vyakula, huku Nanaa akifuata nyuma taratibu. Hakujua aseme nini kwa Geb. Samahani halikuwa neno sahihi. Kwani hakuona kosa kuwa na Zac. Labda Asante, kwa kumfungua macho au kumuokoa kutoka kwenye hatari yakutapeliwa tena. Aibu ilimuingia, akaanza kujichukia. “Nina tatizo gani mimi? Kwa nini nakuwa mjinga wa kupitiliza? Naona swala la mwanaume limeshindikana, heri nitengeneze kwangu.” Nanaa akaendelea kuwaza wakati wanaingia ndani.

“Naona anasinzia huyu. Naomba nisubiri kwanza nibadili hizi nguo, na nioge kabisa kutoa mkosi wa Zac, kabla mwanangu hajanigusa.” Nanaa aliongea mara tu walipoingia ndani, akapitiliza bafuni. Geb alitamani kucheka alipokuwa akimsikia akioga kweli. Akabaki akicheza na mwanae kwa kumrusha rusha ili asilale. “Nanaa fanya haraka. Liv amelemewa.” Nanaa alitoka kwa haraka akiwa na khanga tu. “Nimeona mpaka nivae, nitamchelewa zaidi. Na akilala sasa hivi huyo, hataamka mpaka jioni. Na hata nikimuamsha hapo katikati, hatanyonya vizuri.” Geb akamwangalia. Mwili wa Nanaa ulikuwa mtupuuu. Umefunikwa na khanga tu. Geb akavuta pumzi kwa nguvu kama kujiweka sawa. “Muone anavyorembua!a Anaonekana atalala sasa hivi.” Akamchukua nakuingia naye chumbani. “Nyonya kidogo kabla hujalala Liv mwanangu. Usingizi gani huo hauishi mama! Eti?” Alimsikia Nanaa akizungumza na mwanae huko chumbani. 

Akambadilisha diaper na nguo nyepesi ya kulalia, akamuweka kwenye ziwa. Akavuta maziwa kidogo tu akaanza kulala. Nanaa alibaki akimkuna miguu ili aamke anyonye. Alifanya hivyo kwa muda. Liv anaamka, anavuta maziwa kidogo, anarudi kulala. Hivyo hivyo mpaka alipopotelea usingizini kabisa. Nanaa akacheka. “Yaani Liv wewe! Sijui umekuaje? Wala hatuzungumzi tena kama zamani! Muone. Umelala kama umetoka kulima shamba!” Akamuweka kitandani kwake. 

Alipohakikisha amemfunika mwanae vizuri, ndipo akaanza kujipaka tena mafuta mwilini mwake. Akavaa kigauni kilichochanua chini, lakini kifupi kiliishia juu kidogo ya magoti. Akachana tena nywele zake, akatoka.

~~~~~~~~~~~~~~~

Alimkuta Geb amekaa sebuleni ametulia. “Geb!” Geb akamgeukia. “Kama hutatoka, naomba nitoke kidogo, nikakamilishe mambo yangu ya chumba. Nitajitahidi kuwahi kurudi.” “Nilifikiri ulimaliza jana!” Geb akashangaa kidogo. “Hatua ya kwanza nimefanikiwa, namshukuru Mungu.” “Kwani kuna hatua ngapi?” Nanaa alifikiria kidogo, akamsogelea. “Sina kitu chochote pale kwangu. Nimeweka maboksi ya vitabu, na vitu vyangu vyote chini sakafuni. Na sakafu yenyewe sio nzuri, nahofia maboksi yanaweza kupata unyevu, nikaharibu kila kitu. Mapazia yenyewe niliyoning’iniza ni yale yale niliyokuwa nikitumia chuoni. Madogo sana, ni kama yapo nusu dirisha. Nilifikiria kununua kwanza kabati la vitabu, lakini naona nirudi kwenye wazo la kununua kwanza kitanda, ili ikitokea..” Nanaa akanyamaza akaenda kukaa kwenye kochi la pembeni ya Geb.

Ile gauni ilifika katikati ya mapaja, ikaacha mapaja yake nje. Akaanza kuhangaika kuvuta chini kana kwamba hakuwa akijua kama alivaa nguo fupi. Asijue ndio anavuta macho ya Geb zaidi kumtizama. “Nitajitahidi nisichelewe. Nataka nitoke mara moja nikanunue kapeti hata ya plastiki tu, ya kutandika sakafuni, na kitanda. Sitakawia. Nimeona vinauzwa palepale, karibu na kwenye chumba changu.” “Sitawahi kuja kuthubutu kukufukuza tena Nanaa. Najua huniamini tena, lakini haitakaa ikatokea nakufukuza. Hata iweje.” Nanaa alibaki kimya huku ameinama. Tayari machozi yalishakuwa kama mvua. 

Akaanza kujifuta. “Naomba nipe nafasi nikuhakikishie nimebadilika. Hata yale masharti niliyoweka nimetoa. Upo huru kufanya lolote, kwa huyo mtoto na pale nyumbani. Ila naomba tu tuwe tunawasiliana.” Nanaa akanyamaza huku akifuta machozi. 

Penzi Halitaki Kiburi.

K

imya cha muda mrefu kikatanda, Nanaa akiwa ameinama. Alipoona halii tena, Geb akaendelea. “Eti Nanaa?” “Nashukuru.” “Nanaa! Acha kunipa jibu la jumla la kunitoa njiani.” “Nimekushukuru kwa kuniamini tena. Kunipa     uhuru na mtoto.” “Mbona kama unanikwepa Nanaa?” “Sikukwepi!” “Mazungumzo yote yanayotuhusu mimi na wewe, unayakwepa!” Nanaa akanyamaza. “Umeniambia umenisamehe, lakini mbona hivyo!? Kila nikikuuliza hali yako wewe, unaniambia mambo ya mtoto! Jana nilikwambia nimeacha kwenda kazini, nataka kubaki na wewe na Liv, umeamka asubuhi unajiandaa kuniacha hapa na Liv ili uende kwa Zac! Sasa hivi nakuomba nafasi nyingine, tuwe kama zamani, unaniambia unashukuru! Ni kwamba umeamua kuninyima mimi nafasi ya pili ambayo ulikuwa tayari kwenda kumpa Zac, mwanaume aliyekuwa amekusaliti?” Geb aliongea kwa kulalamika.

“Hapana Geb! Hata jana nilikwambia nakwenda kumsikiliza kwanza ndipo nitaamua. Zac alinionyesha kunihitaji, lakini wewe ulinionyesha kwa maneno na vitendo hunihitaji, Geb. Leo tumekaa hapa kwa sababu ya Liv tu. Kama Liv angekukubalia maziwa ya kopo na kutonihitaji mimi, nina uhakika, usingenitafuta tena, Geb. Nilikuomba msamaha zaidi ya mara tatu, lakini ulishindwa kunisamehe. Hata uliponiruhusu niishi pale kwako, bado ulinionyesha wazi hunihitaji.” “Sio kweli Nanaa.” “Kweli Geb. Unafikiri ni kwa nini nilikuwa tayari kurudi kwa Zac, kama si kunitamkia hunihitaji?” Nanaa alihisi Geb hajui au hakumbuki mambo aliyomfanyia.

“Nanaa, nilikupenda na kuamua kukufanya uwe wangu kabla ya Oliva. Oliva ndio njia yangu pekee ya kukumiliki. Sema nimekwenda umbali ambao hata mimi sikutegemea, nikakuumiza zaidi. Lakini mapenzi niliyokwambia siku ile tukiwa Morogoro, hayajabadilika Nanaa. Bado nakupenda  kuliko nafsi yangu.” Nanaa akamwangalia kama haamini.

“Hivi unajua nimekuwa na Liz kwa muda mrefu sana kuliko wewe?” Nanaa akanyamaza. “Unafikiri kwa nini wewe tumekuwa kwenye mahusiano ya muda mfupi sana, lakini ukawa umeshika mimba yangu?” Nanaa akashindwa kujibu. “Kwa kuwa mimi ndio nilitaka unizalie watoto Nanaa. Haikuwa mimba ya bahati mbaya kama ulivyosema, kuwa mama yako alifanya kosa, na wewe ulifanya kosa kushika mimba bila makubaliano au ndoa. Sio na mimi labda mwanaume mwingine. Mimi huwa sikosei, Nanaa. Silali na msichana bila kondom. Lasivyo sasa hivi ungekuta Liz ana watoto wangu  kwa kuwa alitamani sana tuzae naye mtoto wa kiume na wakike, lakini niliamua Liz hatakuwepo kwenye maisha yangu kwa muda mrefu. Ndio maana ulipokuja tu, nikakusoma haraka, niliporidhika na wewe, ikabidi kutafuta vitu vitakavyokuweka kwenye maisha yangu mpaka kifo. Kwanza nilijua huwa huna tabia ya kuwa na mahusiano ya muda mrefu, ni mwepesi kujitoa kwenye mahusiano, kwa sababu zozote zile, na huwa hurudii matapishi. Mwanaume akikuumiza huwa humrudii hata iweje. Yaani kama hichi unachonifanyia mimi sasa hivi.” “Sio kweli Geb. Ni kwa kuwa sikubahatika tu kupata mwanaume wa kuwa na mimi muda mrefu.” Nanaa akajitetea huku akifuta machozi. 

“Inawezekana ni kweli umebadilika Nanaa. Nimeona ulitaka kuvunja rekodi kwa Zac.” Nanaa akainama kwa aibu. “Hivi unakumbuka uliniacha bila kutaka kunisikiliza? Hata nilipokubembeleza ubaki nijieleze, hukutaka, ukanitukana na kuondoka! Ulibadili namba ya simu ishara ya kuthibitisha kile ulichonitamkia, hutaki nikutafute tena. Hukutaka kurudi tena kwangu, ukakubali kubaki na ujauzito wangu ukaamua kumlea mtoto wangu kwa garama yeyote ile bila mimi! Tena ukijua nakupenda Nanaa. Nikiwa nimekutamkia nilikuwa na wewe usiku kuchwa wakati mgonjwa. Nilikuwa najiiba kuja kulala na wewe usiku ili kukuuguza. Si hospitalini si nyumbani kwa Antii, nilikuwa na wewe. Sikupitisha hata siku moja, nilikuwa na wewe usiku kwa kuwa mchana James alikuwepo na alitupiga marufuku tusikusogelee tena. Kwa kosa la kukusahau nje ya ukumbi. Kama ningekuwa na mapenzi na Liz, au tupo kwenye mahusiano na Liz, si huo ndio ungekuwa wakati wa mimi kuwa na Liz?” 

“Wala sikuwa najua Geb. Nilikuona mara moja tu. Na wala sikujua kama ilikuwa ndoto au la! Kwa kuwa nilipokuwa nikiamka sikuwa nakukuta! Sikufahamu kama ulikuwa na mimi wakati mgonjwa Geb. Nilijua ulinisusa.” “Lakini nilikwambia Nanaa. Nilikupigia simu nikiwa safari. Nikakuomba rudi nyumbani. Angalau nikuone. Ukalalamika sikupendi. Nikajaribu kukuelezea ukweli. Ukaja kunikuta na Liz, ukasahau kabisa nilichokwambia. Kwa haraka sana bila kufikiria ukanitukana na kunitoroka kama ulivyofanya Marangu. Nilijua Liz angekuwepo Marangu. Unafikiri ni kwa nini nilitaka na wewe uwepo? Au hata kwenye harusi. Kama nilitaka mapenzi ya wizi, kwa nini basi nikubembeleze uje kwenye harusi ambayo najua nitasimamia na Liz, tena kwa style yakushikana mikono?”  Hapo ndipo akili ya Nanaa ikaanza kufikiria vizuri sasa.

“Eti Nanaa? Kama kweli mimi ni mwizi wa kiasi hicho kwako, kwa nini nitake na wewe uwepo kushuhudia wizi wangu?” “Mimi sijui Geb? Sielewi!” “Kwa nini huniulizi?” Kimya. “Hivi unakumbuka tulipokuwa Morogoro uliniambia ni kwa mara ya kwanza unajisikia kupenda. Ulikuwa ni ukweli au ni katika kunifurahisha tu?” “Sijawahi kukudanganya Geb.” “Sasa mbona huishi kile unachokisema Nanaa? Kwa nini unanikatia tamaa mapema hivyo? Nilikubembeleza twende wote Marangu. Liz akakutingisha kidogo tu, ukaniacha Marangu. Unanikuta uchi nimetoka kuoga na Liz yupo kitandani, unanitukana na kuniacha bila kunipa nafasi ya kunisikiliza. Unajua kwa nini jana nililia?” Nanaa kimya. 

“Niliona unampa nafasi Zac, ambayo na mimi nilikuomba Nanaa. Ulikuwa tayari kuniacha mimi na Liv, uende ukamsikilize Zac. Kwa haraka na yeye alikuwa na kosa kama langu tu. Lakini mwenzangu ulikuwa tayari kwenda kumsikiliza, mimi ukanipuuza.” “Lakini Geb, nilikupa nafasi hiyo zaidi ya mara 3. Tena mimi ndiye nilikuwa nikikuomba msamaha. Nikitaka yaishe. Ukanikatalia. Zac alirudi, akiniomba msamaha na kunitaka tena. Sasa ningefanyaje tena kama sio kumpa yeye nafasi?” Nanaa akajitetea.  

“Si nilikuomba msamaha siku niliyokufuata na Oliva kule hotelini? Nikarudia tena na tena. Ukaniahidi umenisamehe. Leo unanipa mpango wa kuniacha mimi na Oliva, uje uwe nasi kama mfanyakazi wangu halafu jioni unarudi kwa Zac! Kweli Nanaa?” “Sikujua kama unanihitaji tena, Geb. Uliniambia nipo huru kwenda kwa mabwana zangu. Ila nirudi kunyonyesha mtoto. Ni kweli uliomba msamaha. Lakini nilijua ni msamaha wa kunifukuza siku ile kama ‘paka mwizi’. Sio vinginevyo.” “Kama kweli wewe ulikuwa na mapenzi ya dhati kwangu, kwa nini hukutaka kuhangaikia hiyo ‘vinginevyo’? Kwa nini ulikubali kwenda kuanzisha mahusiano au kufufua hivyo ‘vinginevyo’ kwa Zac, ukaniacha mimi unayekiri unanipenda? Au ni mimi tu ndio nawajibika na ‘vinginevyo’? Ikitokea mimi naacha, ndio inakuwa basi?” Hapo Nanaa akaishiwa jibu.

“Sasa kwa kuwa mimi nina mapenzi ya dhati na wewe Nanaa. Na nilitaka uwe kwenye maisha yangu mpaka kifo, ikabidi kukusoma zaidi ili nijue ni kitu gani kinaweza kukufunga kwangu usinikimbie hata iweje? Ndipo nikagundua siri ambayo nimeitumia, japo nakiri nimefika mbali.” “Siri gani?” Nanaa akauliza kwa upole. “Nilijua kwa makuzi uliyokuwa wewe, kwa namna yeyote ile hata iweje, ukija kupata mtoto, utataka kumtunza huyo mtoto kwa garama yeyote ile. Kwa hiyo nikajifunza mzunguko wako wa hedhi kwa haraka sana, ili kabla hujanitoroka uwe unamtoto wangu.” Nanaa akashangaa sana.

“Geb wewe!” “Ningefanyaje Nanaa na mimi nakupenda? Na ndio maana nilimchukua Liv tokea upo chuoni, nikijua utamfuata tu. Ulipotaka kutoroka naye, nilijua ukifanikiwa kutoka pale, sitakuona tena maishani. Ndio maana nilikuwekea masharti magumu nikimuweka Liv kama chambo yangu nikijua alipo Liv, ndipo utakapo kuwepo daima. Nakiri nilifika mbali kwa hasira kama unavyonifahamu, lakini naomba uniamini Nanaa, ni kwa kuwa nakupenda na ninakutaka uishi na mimi. Ni mpango niliopanga kabla ya Liv hajaja duniani. Nilikuchagua wewe uje kuwa mke wangu.” Zilikuwa ni habari ambazo Nanaa angetamani angeambiwa mapema sana. 

 “Sikuwa na haraka ya mtoto hata kidogo. Kama wewe ungekuwa ni mwanamke mvumilivu, unatulia kwenye mahusiano, ningekuoa baada ya kumaliza tu chuo, halafu baada ya kama miaka miwili ndipo tungefikiria swala la mtoto. Lakini niliamua kulipa garama ya kuzaa kipindi hiki kigumu, ambacho nilishakipigia mahesabu nikajua ni kipindi ambacho kitakuwa kina mambo mengi sana yatakayonifanya nisilale, wala kutoweza kulea, lakini nilikubali yote hayo ili tu wewe uwepo kwenye maisha yangu.” Geb akaendelea.

“Huu sio wakati ambao ningetaka hekaheka za watoto, Nanaa. Mimi huwa napanga mambo yangu kwa makini. Yale ambayo yapo ndani ya uwezo wangu, huwa napanga ni nini kitatokea kwa kipindi gani. Kwa hiyo kama sijaenda kinyume na mipango ya Mungu, huwa najua lini nitafanya nini. Nakuwa pia nimeshapigia mahesabu matokeo ya hicho nitakachofanya, garama ya kulipa, na huwa najiandaa kabisa. Nilikuchagua wewe tokea zamani.” Nanaa hakujua aongeze nini katika hilo.

“Ni nini kinakufanya usilale?” Nanaa akauliza kwa upole. “Mwaka huo uliopita au kipindi hichi cha sasa hivi, nilikipanga kwa muda mrefu kuwa ni kipindi cha mabadiliko ya maisha yangu. Nilipanga kuacha kazi ambayo ilikuwa ikiniingizia pesa bila kuwaza itakuwaje, na kujiajiri mwenyewe kama baba yangu. Nilipenda vile baba yangu alivyokuwa akifanya kazi kwa bidii na nikaona amefanikiwa sana. Aliniambia juhudi huwa haimtupi mtu. Kwa hiyo tokea nakuwa, baba alikuwa akija kunichukua na kunipeleka kwenye miradi yake, nilikuwa nikimwangalia vile anavyofanya kazi kwa bidii tena bila kuchoka wala kulalamika. Nikawa namtamania mafanikio yake. Alikuwa akinifundisha kwa maneno na vitendo” Kidogo Nanaa akakumbuka stori ya Mama G. Historia yake na Magesa. Aliishia wakina Geb wakati wanazaliwa, walikuwa wakiishi na baba yao. “Inawezekana alirudi kwa mkewe!” Nanaa akawaza. “Lazima nitengeneze mazingira ya mama kunimalizia ile stori. Inaonekana ina mwisho mgumu.  Nanaa akaendelea kuwaza.

Akakumbuka anazungumza na Geb. Akamwangalia ili kuendelea kujua kinachomsibu. Geb akaendelea.“Sasa nilipanga kuanzia mwaka jana na miaka miwili mbeleni, yaani miaka 3, iwe ni miaka ya mabadiliko ya maisha yangu. Nijikite kwenye biashara tu. Nilijiwekea ni muda ambao tutafanya kazi mchana na usiku bila kupumzika na pengine bila kupata faida kubwa au kutokupata faida kabisa mpaka nifanikiwe na biashara ikue, kisha ifike kipindi ambacho nitatafuta mtu mwaminifu nitakayemwamini na kunisaidia, halafu pengine wakati huo biashara itakuwa imekomaa, na kuanza kujiendesha yenyewe bila uangalizi wetu mkubwa, ndipo sasa tuanze kufikiria swala la watoto.” “Unamaanisha na mimi!?” Nanaa akauliza kwa upole huku akimtizama Geb, na kumuomba Mungu aseme ndiyo. Geb akacheka tu bila kutoa jibu. 

“Sasa, sasahivi unaendeleaje na mipango yako?”“Mbona unabadilisha mazungumzo yetu Nanaa? Bado unanikwepa.” “Sikukwepi Geb?” “Sasa kwa nini unataka tuzungumzie mambo ambayo sio ya msingi kwetu?” “Ni msingi Geb. Kutokulala kwako wewe, kunaniathiri na mimi.” “Kivipi wakati hunitaki mimi wala vitu vyangu?” Nanaa akanyamaza. “Unanikataa mbele ya watu Nanaa!” “Hapana Geb.” “Ni kweli. Ulikubali kumsamehe Zac uondoke uniache mimi na mtoto, ili uwe na yeye!” Nanaa akajisikia hukumu moyoni akaegemea magoti, nakuanza kulia tena.

“Mama amekuomba uweke vile vitu nyumbani, lakini umemkatalia kwa sababu zile zile ulizonipa mimi nilipokuomba usikodishe chumba, uvilete vitu nyumbani.” “Ulinionyesha hunihitaji tena Geb. Ulinifukuza kwako, ningefanyaje? Sitaki kuhangaika maisha yangu yote Geb. Wewe unajua ninavyoogopa kuwa peke yangu maishani. Ndio maana nilikuwa nipo radhi kumsamehe Zac, ili nisiwe peke yangu!” “Nilikosa Nanaa, na nikakuomba msamaha. Umenipa jibu la jumla kuwa umesamehe huku ukinionyesha wazi hupo radhi kunirudia kama mpenzi. Hapo ulipo unatengeneza sehemu ya kukimbilia siku nitakapo kukosea tena, au niseme umenithibitishia wazi kuwa muda na wakati wowote utatuacha mimi na mtoto wangu. Si ndio hivyo Nanaa?” Nanaa alibaki kimya akilia. 

 “Eti Nanaa? Hivi umeshajiuliza ni lini na wewe utakuwa na kwako, au mtu wako ambaye utamlinda na kumpigania hata iweje?” Kimya. “Uwe na nyumba utakayoilipia garama kama hivyo ulivyohangaika kukutana na dalali. Dalali akakupeleka mpaka kwenye hicho chumba, ukakuta kicho chumba kina watu wengine wawili ambao nao wanakitaka. Ukahangaika kumtafuta mwenye nyumba. Ukahangaika kumfuata nyumbani kwake ili tu kuzungumza naye na kumshawishi akupe wewe hicho chumba. Ukahangaika mpaka ukachelewa kurudi nyumbani kuhakikisha unakipata hicho chumba na kukimiliki.” Nanaa akaendelea kulia bila kujibu.

“Au kwa utayari uliokuwa nao wa kutuacha sisi ili ukaishi na Zac, mwanaume aliyekusaliti! Ukawa tayari kwenda kuanza upya. Kujenga ambako uliamini tu, si kwa kuwa ulikuwa na uhakika na Zac ila Imani tu. Sasa umeshafikiria kujenga nyumba yako? Namaanisha sio jengo, namaanisha nyumba utakayoijenga wewe, yenye mume na watoto. Utakayoilipia garama kama hiyo kuhakikisha una nyumba, yaani watu. Kwa kuwa nyumba sio majengo Nanaa. Kama ingekuwa hivyo mimi nisingehangaika na wewe. Sasa hivi ninayo majengo zaidi ya matatu, tena majengo mazuri na ya gharama. Lakini yote hayakaliki bila wewe na Liv. Zaidi wewe Nanaa.” Nanaa akazidi kulia.

“Muda huu, ningekuwa kwenye moja ya jengo langu linalosifika pale Ubungo. Kila mtu anamtafuta mmiliki wake, amuone. Lakini nipo hapa na wewe, Nanaa. Na ni juzi tu usiku nimeshindwa kulala kwenye jengo jingine kule Tabata. Lenye kitanda kizuri na mashuka ya thamani kuliko haya ninayolalia hapa sasa hivi, ili tu niwe na wewe hapa! Kwa kukubaliana na mimi katika hilo, kuwa nyumba sio jengo. Ndio nakuuliza Nanaa, ni lini na wewe utahangaikia kujenga nyumba yako, na kuacha kukimbia hovyo kwa kila sababu? Yaani ukawa mwanamke wakutegemewa. Mtu anajua hata iweje, ‘Nanaa ni kimbilio langu. Nanaa atakuwepo kunisitiri. Hata kama nimekosa, nakimbilia nyumbani kwa Nanaa, atakuwepo kunisitiri, kuniliwaza na kunisaidia.’ Eti Nanaa?” Ulikuwa ni ukweli uliokuwa ukimuumiza sana Nanaa. Akabaki akilia bila kujibu.

Ukimya wa muda ukapita, Geb akajirudisha kwenye kochi akajiegemeza vizuri, akabaki akiangalia dari. “Geb!” Nanaa alihama kochi, akaenda kukaa pembeni ya Geb. “Nitabadilika.” Geb alibaki akimwangalia. “Kweli nitabadilika.” Nanaa akarudia huku akifuta machozi. “Nakusikiliza.” “Tokea uliponiambia habari za Zac, nikakusudia kutoka moyoni kubadilika. Nitaacha kukimbia, na kwa kuwa nimejua naweza kuwepo kwenye maisha yako, basi  nitahakikisha katika kila mpango ninaouweka na wewe upo.” “Safi sana. Sasa naomba tuanzie kwenye chumba ulichochukua.” Nanaa akaishiwa nguvu. “Kwa nini nisikitunze tu? Kitakuwa kama stoo.” “Nilifikiri umesema katika kila mpango na mimi nitakuwepo!” “Ndiyo, upo.” “Mbona sasa kauli zako za ‘nita’ haziishi?” Nanaa akatulia kidogo akajiweka sawa kama anayefikiria chakuzungumza.

Mwishowe akaamua kuzungumza, maana Geb alibaki akimtizama. “Basi naomba kile chumba nilichokodi, tukitunze kiwe kama stoo.” “HAPANA.” Geb alijibu kwa haraka na kumfanya Nanaa ashangae. “Huwezi kushika huku na kule Nanaa. Unakuwa ni kama mtu usiyejua nini unataka! Au huna uhakika na unachokitaka. Kama umeamua kuwa na mimi, basi ujue kuna garama ya kulipa, ambayo nikuambatana na mimi katika kila hali. Mvua inyeshe, jua litoke tutakuwa pamoja” Nanaa alitamani kuchanganyikiwa. 

“Geb please! Ni chumba tu!” “Hapana Nanaa. Sio chumba tu. Kile chumba ndio level ya commitment yako kwangu. Ni kipimo cha utayari wako kwangu.” Nanaa aliendelea kulia. “Pale tunapoishi tu, kuna vyumba ambavyo hata havitumiki. Nyuma ya ukuta wa ile nyumba, kuna nyumba nyingine kubwa zaidi ya ile tunayoishi na unajua kuwa ni yangu. Kama kweli umeamua kuwa na mimi, na kujenga nyumba yetu, anza kwa kuweka Imani kwangu. Ukishindwa hapo tu, ujue haupo tayari na sitakulazimisha Nanaa. Amua vile unavyotaka. Ila ujue nakupenda, na ninakuhitaji wewe kama Nanaa wala si kama mama yake Oliva.” Nanaa aliinama na kuanza kulia tena. 

Kwa mara ya kwanza maishani ndio amefikia ndoto zake. Kitu alichokuwa akikitamani sana tokea zamani. Awe na kwake kunakojulikana ni nyumbani kwake. Uchungu ulimuingia kila alipofikiria kupaachia sababu ya Geb ambaye amemkuta na kila kitu chake! Anaanzia wapi kujiona ni mmiliki mwenzake? Alitamani awe na kwake. “Geb! Naomba nikibakishe tu kile chumba. Tafadhali Geb.” Nanaa aliongea kwa uchungu huku akitamani Geb amuhurumie akubaliane naye katika hilo.

“Inamaana hilo ndilo jibu lako kwangu kuwa hunitaki tena?” Nanaa akazidi kulia kwa muda, ikasikika sauti yake tu akilia. “Eti Nanaa? Huu ndio mwisho wetu?” Geb akauliza. “Basi nitaenda kuvitoa hivyo vitu.” Nanaa akajibu huku akiendelea kulia kama aliyelazimishwa kujibu. “Unauhakika?” “Lakini ujue nafanya nikiwa nimejawa hofu, Geb. Naogopa sana.” “Na mimi najua Nanaa. Na ninakuahidi hutajuta.” “Kweli?” Nanaa akauliza akionyesha wasiwasi. Geb akamsogelea akumbusu huku akimpapasa. Hakutaka kwenda mbali sana lakini alihakikisha anaamsha hisia zote kwa Nanaa, kisha akamuachia akiwa ametulia kabisa. 

“Kwa hiyo umeamua kujenga nyumba yetu?” Geb akauliza huku akimtizama kwa karibu. “Si na wewe utanisaidia?” “Kabisa.” Nanaa akavuta pumzi kwa nguvu na kutoa tabasamu. “Sitakimbia tena. Nitakung’ang’ania hata iweje, na mimi nitakulinda.” Geb akacheka. “Hapo umekamilisha furaha yangu.” “Na mimi nimefurahi kujua unanihitaji, Geb. Nilijua hunitaki tena, unamtaka mtoto wako tu.” “Liv ndio chambo yangu. Nakupenda Nanaa, na ninajua wewe ndio utaweza kuishi na mimi, na mimi nikayafurahia maisha. Ila lazima tujiwekee utaratibu wa kuzungumza. Hata iweje, tafadhali hakikisha unanisikiliza.” “Nitafanya hivyo Geb. Asante na samahani katika swala la Zac.” Geb akambusu midomo yake. Aliinyonya kwa taratibu. Kwa kiu aliyokuwa nayo Nanaa, alitamani amvue nguo, lakini akamuachia.

“Sasa turudi kwenye lile swali lako.” “Lipi!?” “Uliniuliza biashara inaendeleaje.” Nanaa akacheka. “Kweli una akili ya kutokusahau!” “Kwa kuwa mwenzio nakuweka kwenye mipango yangu yote, tena tokea zamani. Na ndio maana nilikuwa nikisafiri na wewe na kukueleza kila kitu. Jinsi ninavyofanya biashara zangu, hasara ninazoingia na faida ninazoingiza. Nilikuwa nikikushirikisha kwa wazi nikitaka uelewe. Kwa hiyo kwa kujibu swali lako, biashara zinaendelea vizuri, ila bado nipo kwenye hatua ambayo ninahitajika sana. Kuwa karibu ili kuhakikisha baada ya muda mfupi zinakuwa na uwezo wakujiendesha zenyewe, au hata nikimuachia mtu, najua nini chakutegemea.” Geb akaendelea.

“Nipo kwenye kuweka mfumo ambao utanisaidia kuendesha hiyo biashara bila kutumia jasho jingi kama sasa.” “Ungependa nikusaidie nini?” “Swali zuri sana. Cha kwanza, naomba amani kati yetu. Kukiwa na utulivu nyumbani, itanisaidia kutulia na akili zangu zitaweza kufanya kazi vizuri. Najua naweza nikawa na majukumu mengi sana huko kazini, ukajikuta muda mwingi upo nyumbani peke yako, naomba univumilie. Naamini ni kwa muda mfupi tu. Nikiweka mambo sawa, hata ulezi wa watoto nitakusaidia.” “Mtoto mwenyewe mmoja tu, na nipo na mama, sitashindwa.” “Sasa hivi mtoto ni mmoja, watakuja wenzake karibuni tu, halafu mama anakazi zake. Ni vile anakupenda tu ndio maana ameacha majukumu yake, na kuamua kuwa na wewe. Lakini mama anabiashara zake kubwa tu, zinazomtegemea. Najua hivi karibuni ataanza kwenda kazini, utajikuta upo peke yako na mtoto.” “Usijali Geb. Mimi nitakuwa sawa tu. Labda kama kuna kitu kingine unachotaka nifanye, ila kama ni hayo tu, nitajitahidi.” Nanaa alijibu akiwa ameonekana akili yake imerudi likizo. Inafanya kazi kama mama ambaye yupo tayari kwa majukumu.

“Kingine ambacho kilimshinda Liz, naona labda nijaribishe na kwako, sijui kama utakubali.” “Nini?” “Swala la mama.” Nanaa hakuwa ameelewa. “Mama amefanyaje?” Akamuona Geb anasita kidogo. “Ni nini?” Nanaa akauliza kwa upendo. “Nataka kuishi na mama.” “Unamaanisha huyu mama yangu mimi, Mama G au mama gani!?” Geb akacheka sana. “Basi Nanaa. Ombi langu najua limepita.” “Mbona huyo hata akikataa kuishi na sisi tutamfuata huko anakokwenda! Kimbilio langu yule.” “Asante Nanaa. Unajua aliuza mali zake zote kwa ajili yangu?” “Uliniambia. Lakini hata kama angekuwa hajauza, mimi mwenyewe namuhitaji sana Mama G. Ndio mwalimu wangu kwenye kila kitu. Kuanzia mtoto mpaka kwako. Simuachi popote. Kwa hiyo wewe lete hitaji lako jingine.” Geb akacheka. 

“Ni hilo tu. Na kesho anapokuja kukuletea chakula, mwambie akusindikize ukachukue mizigo yako kule ulikoiacha, arudi nayo nyumbani, wewe akuache hapa.” Nanaa akacheka. “Ulivyokazania! Husahau?” “Nahesabu ni kushindwa kwa hali ya juu. Yaani hangaika yote hii, halafu nishindwe kukupatia sehemu ya kuishi! Naona nahangaika bure! Hata Grace na mama wananisema sana. Mama jana amekuacha wewe hapa nyumbani, akanipigia simu na kuanza kunisema sana. Mama anakupenda Nanaa! Amenigeuka mimi, amekufanya wewe kama kiziwanda wake! Umechukua nafasi yangu Nanaa.” Nanaa akacheka sana. 

“Unaona wivu?” “Sijazoea. Alinizoesha kunisifia kwa kila jambo. Mimi nilikuwa malaika kwake. Lakini sasa hivi amenibadilikia, kama hanijui! Mama anakutetea sana. Huna kosa kwake.” “Kweli mimi ni mtu mzuri sana. Sina hatia.” Geb akacheka. “Sawa Nanaa. Lakini kufunga kile chumba, na kuonyesha kuwa umerudi nyumbani moja kwa moja, itakuwa nafuu kwangu. Ujue hata Grace alininunia?” “Grace!?” “Ndiyo Grace, dada yangu.” “Kwa nini tena? Mbona mimi sijaonana naye karibia mwaka!” “Mama alinisemelea kwake. Sijawahi kumuona Grace akiwa mkorofi vile. Lakini amechukia sana kitendo nilichokufanyia, kukufungia nje.” “Jamani mimi napendwa!” Nanaa alimfanya Geb acheke sana.

“Kumbe sina hata haja yakujigombania! Ninao watetezi wangu tayari.” Nanaa alimfanya Geb azidi kucheka. “Hapa tunapozungumza, mama yupo anafanya kazi zangu, ofisini kwangu sio kwake, ili niwe na wewe hapa.” Ilimgusa sana Nanaa. “Ni kweli nimepata familia inayonipenda, Geb. Nashukuru.” Hapo mikono ya Geb ilikuwa juu ya mapaja ya Nanaa. “Nakushukuru kuniokoa kwenye mikono ya Zac. Ningekimbilia kwenye mikono ya hatari ile, nikaacha nyuma upendo mkubwa hivi! Asante Geb.” “Nisingekubali kushindwa Nanaa. Niliamua kubaki leo ili tuzungumze mpaka tukubaliane. Najua unanipenda.”

“Kumbe unajua kama nakupenda?” “Nafahamu. Uliniambia kuwa kwa mara ya kwanza maishani, umejisikia kupenda. Umesahau?” “Nakumbuka Geb, nilijua umesahau!” “Hata kidogo. Siwezi kusahau kitu kama hicho. Iliniongezea upendo na uhakika wa kutaka uwe mke wangu. Kumbuka mwenzio nilianza kukupigia mahesabu hata kabla sijakuona. Na nikaachana na Liz kwa Imani ya wewe kuja kunikubali niwe mpenzi wako. Ulipomkataa Zinda kwa sababu zinazoeleweka, nikaingiwa hofu kuwa unaweza usinikubali. Sasa kuja kuona nakubaliwa busu, halafu ukaniambia umeanza kunipenda, nikaja kukubaliwa sex! Ndio kabisaa.” Nanaa akacheka na kujificha uso.

“Geb, naomba nikuulize. Lakini naomba usinielewe vibaya. Nataka kujua tu ukweli.” “Juu ya Zac?” Nanaa akainama. “Hamna shida na wala sio vibaya. Hata mimi ningetaka kujua ukweli.” Kidogo Nanaa akatulia akitaka kujua Geb asiyekwenda kumbi za starehe wala asiyeweza kujichanganya, amemfahamu vipi mtu kama Zac kwa undani hivyo!

Historia Ya Zac.

          “Kipindi kile nafanya kazi BOT, nilikuwa karibu na kaka yake Ndina. Nilimwajiri. Ni mfanyakazi wangu mpaka sasa. Anaitwa Jeri. Alinifuata akaniambia anaomba nimsaidie kutafuta bank statement yenye pesa nyingi ili ampe mdogo wake, aondoke hapa nchini kwa haraka, yeye na mwanaume wake, kama kuficha aibu. Yaani hiyo bank statement iwe na uwezo wa kuonyesha inaweza kutunza watu wawili huko ugenini.” Nanaa akaanza kuumia.

“Ndipo nikamwambia kama anazungumzia bank statement yangu, nilazima anipe maelezo zaidi, juu ya hao watakao kwenda kuitumia. Ndipo akanipa kisa cha Ndina na Zac. Kuwa Ndina alikuwa na mahusiano ya siri na Zac huku akiwa na mchumba wake. Baada yakumaliza chuo pia waliendelea mpaka mchumba wa Ndina alipogundua. Alipombana Ndina, akakiri na kusema tayari yupo mjamzito.” “Sasa huyo mchumba au Ndina mwenyewe alijuaje kama mimba ni ya Zac?” “Swali zuri sana, maana hata mimi niliuliza.” Geb akajiweka sawa.

Kisha akaendelea kusimulia. “Ndina ametokea kwenye familia ya wacha Mungu. Nikikwambia wacha Mungu, ni wale watu ambao ukiwaangalia kwa macho unajua ni watu wanao mpenda Mungu. Ndivyo alivyo huyo kaka yake, Jeri. Nimfanyakazi wangu wa muda mrefu tu, kwa hiyo namfahamu vizuri sana. Ni wale watu ambao hata ukimzidishia shilingi moja, akaja kujua akiwa kwake, atatumia elfu moja, kukupigia simu ili kukujulisha na kesho yake atairudisha. Kwa hiyo hata huyo mchumba aliyekuwa amemchumbia Ndina, alikuwa mlokole yule wa kweli na ni rafiki wa Jeri. Kwa kifupi, hakuwahi kumgusa Ndina kimapenzi.” “Oooh!” Nanaa akacheka na kuinama.

“Sasa baada ya Ndina kuona ameingia aibu, hawezi kuwaambia wazazi na kanisani kwao atatengwa au atajulikana kama alikuwa mzinifu, akaamua aondoke nchini na Zac aliyekuwa amepanga kuendelea kusoma. Kwa kuwa naheshimiana sana na Jeri, na ninamuamini, nikakusudia kumsaidia. Lakini nilitaka kukutana na hao wapenzi wawili kwanza. Nikamwambia Jeri awalete pale ofisini kwangu. Kule ulikokuwa na wewe ukifanya kazi.” Nanaa akakumbuka zilipokuwepo ofisi zake za zamani maeneo ya Fire, na mama G alishamwambia kuwa walihama pale amenunua jengo maeneo ya Ubungo.  “Hongera Geb. Mama aliniambia umenunua jengo maeneo ya Ubungo.” Geb akacheka kidogo. “Asante.” Akajibu na kufikiria kidogo kisha akaendelea.

“Basi, wakafika kuniona. Alikuwa Zac, Ndina na Jeri. Nikazungumza nao, wakaniambia ilibidi kufunga ndoa ya harakaharaka mahakamani ili kutuliza wazazi baada ya kugundulika hayo mahusiano yao. Na Zac akasema nilazima waondoke pamoja kwa kuwa Ndina ni mjamzito. Kwa hiyo wakaniambia nikiwapa hiyo bank statement yenye hicho kiasi cha pesa, hawawezi kukosa Visa. Basi, kwa kuwa naheshimiana sana na kaka yake Ndina, nikawapa ile bank statement, wakaondoka, wala sikuwafuatilia tena.” Nanaa alizidi kuumia. Alimuacha Zac amepiga magoti nje ya daladala akimsihi arudi wazungumze, lakini kumbe alirudi kuendeleza mahusiano na Ndina! Maigizo gani haya jamani! Hata Nanaa alijiuliza.

“Sasa miezi mitano iliyopita kaka yake Ndina akarudi tena kwangu na stori nyingine kuwa anaomba nimpe kazi dada yake, Ndina. Kwanza nilisita kwa kuwa huwa sipendi kuajiri ndugu wawili, na yeye anajua. Akanihakikishia hapatatokea tatizo. Nikamuuliza shule iliisha? Akasema hapana. Akasema walipofika huko, Ndina akazaa mtoto mwenye matatizo, mlemavu. Akawa anahangaika na mtoto peke yake, Zac anafanya umalaya tu. Mambo yalipomzidia, ndipo ikabidi amtafute tena kaka yake, kaka yake akamtumia nauli akarudi nchini. Lakini mtoto akawa anahitajika matibabu na matunzo. Ndina akawa hana kazi na hana msaada wowote kutoka kwa Zac. Akawa yupo tu nyumbani anategemea wazazi yeye na mtoto wake.” Nanaa alimsikitikia sana Ndina. Alimfahamu kama binti mtulivu, kumbe alikuwa na mambo ya chini chini yaliyokuja kumuweka mwangani!

 “Sasa kaka yake ndio akaniambia wamehangaika sana kutafuta kazi bila mafanikio. Akaniambia nikimwajiri Ndina ni kama nitakuwa nimemsaidia  huyo mtoto mlemavu pia. Basi, nikamwajiri na Ndina. Akaanza kazi hapo kwenye kampuni yangu. Tena anajitahidi sana kazini. Lakini Zac alikuja kukata mawasiliano na Ndina kabisa. Siku tatu zilizopita niliwakuta Ndina na kaka yake wakizungumza, Ndina alikuwa akilia sana. Sikutaka kuuliza kulikoni kwa kuwa kwanza ulikuwa muda wa kazi, na wao wapo wanaongea mambo ambayo nilijua ni ya kifamilia, kitu nilichokuwa nikikikwepa tokea mwanzoni na yeye kaka mtu anajua. Nikaingia ofisini kwangu na kuendelea na kazi, ndipo kaka yake akanifuata kuniomba msamaha na kunieleza kuwa anafikiria kumshitaki Zac, kwa kumtelekeza mkewe na mtoto. Kwani alimaliza shule yake, amerudi nchini na Ndina ameambiwa anaishi na mwanamke wa kiarabu. Ndina alimfuata na kumwambia hali ya mtoto wao sio nzuri, lakini Zac akamfukuza kwa ahadi ya kuja kumtafuta baadaye.” Geb aliguna huku anatingisha kichwa.

“Mama alinipigia simu akiwa amekasirika kweli kweli. Ananitukana kama hanijui! Huku ananiambia yupo mwanaume anaitwa Zac, anampenda Nanaa na kumuonyesha mapenzi kuliko mimi! Mama akaniwakia kuwa yupo tayari kumuoza mwanae Nanaa kwa Zac, kama naendelea kuleta mchezo. Sasa leo kuja kumuona huyo Zac mwenyewe, ndio nikamkumbuka kabisa. Si unajua mimi sisahau? Nikakumbuka mpaka alivyokuwa amevaa siku alipoletwa ofisini kwangu  na Jeri, yeye na Ndina.” Nanaa alishakuwa ameinama.

Akafikiri kwa muda, “Nisamehe Geb. Nilikuwa kwenye hali ya kutangatanga.” “Lakini sasa hivi si nimebaki mimi peke yangu?” Nanaa akacheka nakujifunika uso kwa aibu. “Eti Nanaa? Ahadi ya kunipigania si bado ipo?” “Na kukung’angania pia.” Geb akacheka. “Yameisha bwana.” “Kweli yameisha au utakuja kunikumbushia tena baadaye? Maana wewe husahau Geb.” “Nitajitahidi, nisikukumbushie tena kama kukuumiza. Nakuhakikishia yameisha.” Nanaa akatulia kidogo.

“Najifunza Geb. Naomba nivumilie. Mambo mengine najifunza ‘in a hard way’. Mengine ndio hivyo. Sikuwahi kupata mtu wakunikalisha chini na kunifundisha hivi kama mama yako. Sijapata uongozi mzuri. Nilishazoea kukosolewa katika kila jambo. Hata yale niliyoyaona ni mazuri, bado nilikosolewa. Nahisi ndipo nilipojenga tabia mbaya ya kujihami. Najikuta nakimbia kimbia kila wakati. Sijui kujitetea. Hata kama najua ni haki yangu, nakimbia na kuachia watu wengine wachukue kile ninachojua nastahili. Nitaanza kujifunza kukusikiliza kama ninavyomsikiliza mama, ili unisaidie. Usichoke na ninaomba unisaidie kuto kunikumbushia udhaifu wangu mara kwa mara. Itanisaidia kunijengea roho ya kukuamini kama vile kwa kaka James. Najua huwa namkosea, sana tu. Lakini nafikiri huwa ananivumilia na kunipa nafasi tena na tena. Ndio maana amebakia yeye kuwa kimbilio langu wakati wote. Naamini nitabadilika Geb.” “Nitakuwa na wewe Nanaa. Usiogope.” Nanaa akaridhika na kutulia kidogo. Geb akabaki akimtizama kwa uchu. Ule mkono pale juu ya yale mapaja akaanza kutembea taratibu. 

Kabla hajaharibu mazungumzo, Nanaa akamuwahi. “Nina wazo Geb. Sijui kama utakubali?” “Wazo gani?” “Ili kuleta amani tufanye hivi. Nirudishe ile mizigo nyumbani, halafu nimpikie chakula kizuri Grace na familia yake, tuwakaribishe nyumbani.” “Hapo utakuwa umeniokoa.” “Lini sasa tunarudi nyumbani kwetu?” Nanaa akauliza akijijumuisha na yeye. Geb alifurahi sana. “Kweli umeamua.” “Sitaki mchezo. Nipo kwenye ujenzi mwenzio!” Geb akacheka kwa sauti. “Nakuona Nanaa.” “Kwa hiyo usinicheleweshe.” Geb akazidi kucheka huku akimtizama Nanaa aliyevaa sura ya kazi. “Sitakuchelewesha. Ila naomba unipe siku kama mbili au tatu  nyingine mbele.” “Kwani kuna nini huko nyumbani, mbona hutaki hata nirudi kuchukua vitu?” “Kuna kitu kizuri nakutengenezea. Kikikamilika hicho ndio nitakurudisha.” “Unanitengenezea mimi!?” Nanaa aliuliza na tabasamu usoni. “Sina mwingine Nanaa, ni wewe.” Nanaa alifurahi sana, akaanza kumbusu na yeye Geb. 

Alifanya kama vile Geb anavyomfanyia kumnyonya midomo yake, lakini yeye alivuka mipaka. “Tokea jana sijala zaidi ya kile kikombe cha uji nilichokunywa pale mgahawani. Chakula kilikuwa hakipiti kwa hofu.” “Pole mpenzi wangu. Basi wewe tulia nikushukuru. Kazi yote nitafanya mimi mwenyewe, wewe furahia tu.” Geb akacheka. Nanaa alikuwa mtundu kuliko alivyodhani Geb. Na kweli, alicheza na mwili wa Geb akiwa amemvua nguo zake zote palepale kwenye kochi. Alimchezea mpaka Geb alipofanikiwa kupata goli la shukurani. 

“Daah! Hii ya aina yake.” Geb akasifia. “Umefurahia?” “Sana.” “Basi tukae, tule, ukishiba, unilipe.” Geb akacheka. “Mimi nilifikiri unanishukuru, kumbe utakuja kunidai?” “Si ndio na wewe unatakiwa kunishukuru, kwa kukushukuru!” Geb akacheka sana. “Sawa mama. Nitakushukuru, kwa kunishukuru. Nilikuwa na hamu na wewe Nanaa! Acha nile haraka nishibe, halafu nifanye mapenzi na wewe. Tangia siku ya kwanza unaondoka nyumbani nilikuwa nikikuwaza, huku nikihofia unaweza kutimiza yale maneno yako ya kutafuta mwanaume mwingine. Halafu nikawa sina uhakika kama ulishika mimba au la. Nikajiambia hata kama ilishika, itakuwa ilitoka. Nilijikatisha tamaa. Nikajiambia kwa upasuliwaji ule, na madawa uliyokuwa ukitumia, Liv asingeweza kuishi.” “King’ang’anizi huyo! Ndio maana niliamua kumkatisha jina nimwite tu Liv. Amestahimili mengi kweli.”  Nanaa aliongeza.

“Ndio maana nitamuenzi sana huyu mtoto. Amenisaidia kujipatia mke.” Nanaa akacheka sana. “Ujue Geb unatakiwa uniombe radhi wewe?” Geb akacheka. “Kweli tena. Yaani unapanga mipango yote hiyo halafu mwenzio hunishirikishi!” “Nilijua nikikwambia swala la mtoto, wakati ule ungekataa. Maana uliniambia hutaki kitu chochote kiingilie shule yako.” “Wala hujakosea. Nisingekubali. Tena ningeanza kukukwepa.” “Usingeweza Nanaa.” Nanaa akacheka kwa aibu. “Unatabia mbaya Geb wewe! Ulikuwa unanichanganya kwenye mapenzi makusudi ili niwe nakufuata nyuma kama mjinga!” “Lakini si umeona nilivyokuwa nafanikiwa? Ulikuwa unaning’angania kweli kitandani.” Nanaa akacheka akajificha uso na mto wa makochi.

 “Hata mimi naridhika sana kufanya mapenzi na wewe, Nanaa. Nakufurahia kwa kila namna. Zaidi mwangani nikiwa nakuona mwili wako.” Geb alishaanza kumvua nguo Nanaa. “Napenda kubusu midomo yako. Napenda kufanya mapenzi na wewe huku nikikutazama sura yako. Napenda mlio unaotoa kila unapokuwa mikononi mwangu nikifanya mapenzi na wewe. Nakupenda Nanaa.” Geb alimuweka Nanaa kwenye kochi na kusahau swala la chakula. 

“Ule kwanza Geb.” Nanaa aliongea taratibu akiwa uchi kabisa pale kwenye kochi huku Geb akimbusu mwili wake. “Siwezi kusubiri tena.” Nana akatabasamu akiashiria kumruhusu kufanya anachokitaka mwilini mwake. Hata yeye alikuwa na kiu kali ambayo ni Geb pekee alijua ndiye mwanaume anayeweza kukata kiu ile vizuri. Yalikuwa mapenzi mazuri, yaliyojaa uchu, msamaha na furaha. Nanaa alimng’ang’ania Geb pale kwenye kochi, wakajikuta wamehamia chini kwenye kapeti, nakujisahau kabisa. Waligeuzana huku midomo yao ikigoma kuachiana. Yalikuwa mabusu ya kung’ang’aniana. Ilishapita miezi 8 bila wawili hao hata kugusana kitu ambacho wote kilikuwa kikiwatesa sana.

“Liv amenikatili bwana!” Geb akalalamika. “Kwa nini tena?” “Anamiliki starehe yangu ya kufungia magoli. Ona! Nashindwa kunyonya.” Nanaa akacheka sana huku akijiziba matiti yake. “Geb wewe! Chakula cha mtoto hiki!” “Namsamehe tu kwa kuwa amekuwa mvumilivu. Hata sasa hivi ametulia kimya, baba yake nakula raha. Watoto wengine sasa hivi wangeshaharibu kwa kujiliza!” Nanaa akazidi kucheka.

~~~~~~~~~~~~~~~

Mabusu mengine ya haja yakaanza. Nanaa hakupoteza muda, akachangamkia penzi, akafikishwa alikotaka, na Geb naye akafanikiwa. “Daah! Nahisi ndio maana nilikuwa kama mwehu! Ulishanizoesha vibaya Nanaa.” Geb alishamaliza raundi kama mbili za harakaharaka, na yeye akajilaza pembeni ya Nanaa, alimvuta mpaka kifuani kwake, akabaki akimwangalia. “Umeniumiza sana Geb!” Nanaa akaanza kulia. “Najua, Nanaa. Najua sasa hivi itakuwa ngumu kuja kuniamini tena. Eti Nanaa?” Nanaa akanyamaza, akageukia pembeni na kuendelea kulia.

“Ulinisukuma kikatili sana, na kunifungia nje.” Geb aliumia na kujutia sana.  “Naona hata shida kusema samahani Nanaa. Naona haitasaidia. Ndio maana umenirudishia na pesa zote.” “Sijawahi kutamani mali maishani Geb. Najua hata mimi nikihangaika naweza kuwa nazo. Unakumbuka nilikwambia shauku na kiu yangu, iliyokuwa ikinipelekea kutafuta wanaume?” “Nakumbuka Nanaa. ‘Sense of belonging and Security’.” “Ambavyo umenihakikishia huwezi kunipa Geb. Unanipa kitu kirahisi sana, ambacho hata mama yako anaweza kunipa, pesa. Lakini umenipokonya tumaini kubwa sana ambalo ni wewe peke yako ulifanikiwa kunipa.”

“Umenirudisha kwenye hofu kitu ambacho ulishakitoa zamani! Najiuliza hivi kweli nikikukosea tena, utakuja kunisamehe kweli? Mapenzi haya yatadumu kwa muda gani? Nakuwa naogopa!” “Nisamehe Nanaa. Nakiri nilikosea sana. Naomba nisamehe. Kwanza mimi mwenyewe niliteseka. Wala usifikiri ilinipa furaha. Na bado inanitesa mpaka leo.” Nanaa akanyamaza.

“Naomba safari hii nisitoe tena ahadi, ila niombe kitu.” “Nini?” Nanaa akamgeukia. “Tujenge kisiwa chetu pamoja ambacho hakuna mmoja wetu ataweza kumfukuza mwenzake. Kisiwa hicho itakuwa ni mimi na wewe tu, wengine wataongezeka. Kiwe ni kisiwa ambacho hakitawahi kuvunjika kwa namna yeyote ile, ila kifo. Isiwe ni kazi ya mikono ya mwanadamu, ili isiharibike kwa rahisi. Tafadhali Nanaa.” Nanaa alianza kumbusu tena. Kisha akamwangalia vizuri.

“Kwa hiyo niwe na uhakika kuwa haitakaa ikatokea tena maishani unanifukuza?” “Hata iweje, sitathubutu kukufukuza popote.” “Kwa hiyo niwe na uhakika nimepata mtu wangu wa kudumu?” “Mpaka kifo, ni mimi na wewe tu.” Walirudi kitandani baada ya kuoga, na kutumia muda mrefu huko bafuni, wakishikana na kufanya mapenzi. Ni kama Mungu alituma malaika wa kumlea Oliva siku hiyo. Walijisahau hata kama wanamtoto! Nanaa hakumuamsha ili anyonye, akaachwa alale na njaa yake mpaka usiku.

“Narudi chumbani kwetu na Liv.” “Haitakaa nikalala mbali na wewe tena Nanaa. Nikisafiri tunasafiri wote na mtoto. Usinipokonye tonge mdomoni bwana! Acha nikufurahie.” Nanaa alifurahia, akarudia kumbusu. “Itakuaje sasa?” “Twende tumuamshe mtoto, anyonye, akilala tunamuweka kitandani kwake, sisi tunaendelea.” “Sijamuogesha leo.” “Muachie hiyo kazi bibi yake, atakuja kesho.” “Nashukuru kwa kubaki na sisi leo. Nilikuwa na hamu na wewe Geb!”  “Hata mimi Nanaa. Nimefurahia wazo lakubaki.” Nanaa alikuwa ameshatoka ndani ya shuka, akijitayarisha kutoka hapo chumbani, akajikuta anarudi mwilini mwa Geb, alimpokea wakaanza tena. 

Milio ya huba ndio aliyokuwa akitoa Nanaa na kuamsha hisia za Geb zaidi. Kwa kuwa alishindwa kunyonya matiti yake. Ile style ya kumpakata akifanya naye mapenzi, akaibadilisha. Badala ya kunyonya matiti, chakula cha Liv, akabaki amemkumbatia Nanaa, aliyekuwa akitoa sauti tamu nakumfanya Geb azidi kupagawa, mpaka alipofanikiwa tena. “Daah! Utaniua Nanaa. Mwenzio sitosheki!” Nanaa akacheka. “Hata mimi nafurahia sana. Unanifanya siumii. Japokuwa tunafanya kwa muda mrefu, lakini sichubuki! Napenda jinsi unavyonilainisha ukinihisi nipo mkavu.” “Vipi?” Nanaa akaruka pale kitandani. “Hamna tena Geb. Twende tukamlishe kwanza mtoto.” Geb akacheka akanyanyuka.

Walitoka hapo kwa pamoja, wakarudi bafuni. Safari hii walioga kweli na kutoka. Geb alikwenda kutafuta chakula alichokileta mama yake tokea asubuhi. Nanaa akaingia kunyonyesha. Wakati ananyonyesha, Geb akaingia na chakula alichokuwa amepasha moto. Akawa anakula, huku anamlisha Nanaa aliyekuwa ananyonyesha. “Mimi sijashiba Geb.” Geb akacheka. “Hivi unajua asilimia kubwa ya hiki chakula umemaliza wewe Nanaa!?” “Basi ulipakua kidogo. Safari hii nenda kaweke kingi.” Geb alinyanyuka huku akitingisha kichwa. “Nanyonyesha bwana.” “Mmmh! Acha kumsingizia mwanangu. Tokea nakufahamu, ulaji wako ni huo huo.” Nanaa akacheka. 

Geb akarudi na chakula kingine akamlisha Nanaa mpaka akamaliza. “Angalau sasa hivi.” “Nanaa wewe! Angalau au umeshiba?” “Angalau.” “Basi naenda kukuletea kingine.” “Hapana bwana. Nitaamka usiku nile tena.” “Na wewe hushindwi!” Nanaa akacheka. Kwa uchovu wa mapenzi ya siku nzima na vilio vya hapa na pale, walijikuta wanalala kwenye chumba hicho chenye kitanda kidogo. Oliva alilala ukutani, Nanaa katikati, Geb mgongoni kwa Nanaa kama kawaida yake.

~~~~~~~~~~~~~~~

Waliamka asubuhi wote wakabaki wanacheza na mtoto kitandani. “Huendi kazini?” Nanaa akauliza. Maana Geb alionekana hana haraka. “Baadaye nitatoka kidogo, kisha nitarudi. Bado najiona kama nakuhitaji!” Nanaa akacheka. “Ila nimemwambia mama alete chakula nakuendelea na shuguli zake. Baadaye nitakwenda mwenyewe ofisini kwangu.” “Mtoto hajaoga Geb! Ungemuacha mama aje amuogeshe.” Geb akamnyanyua Liv. “Eti Liv? Unataka kuoga? Kwanza mtoto mwenyewe bado ananukia kabisa huyu. Kesho bibi yake anakuja.” “Jana ulisema hivyo hivyo!” “Acha bwana nipumzike Nanaa. Nahangaika sana mwenzio. Acha na leo nijipe likizo tulivu bila kuingiliwa. Najua mama akija hapa utakuwa busy na mama, mimi nitaachwa. Nataka muda na wewe. Au umeshanichoka?” “Hapana Geb mpenzi wangu. Nakuhitaji mnoo. Nitamfuta tu Liv, atakuwa sawa.” Geb akambusu na yeye Nanaa, kisha akaendelea kucheza na mtoto wake.

Ilipofika mchana wakati Nanaa amepitiwa na usingizi kitandani kwa Geb, Geb aliamka baada ya usingizi mfupi walioamua kulala baada ya kupata kifungua kinywa na penzi la haja. Akatoka. Nanaa alilala karibia siku nzima. Alikuja kuamshwa na Geb mida ya saa 12 jioni akiwa amembeba Liv. “Mungu wangu Geb! Amelia sana?” Nanaa akashituka na kukaa. “Nilipitiwa na usingizi.” Akajaribu kujitetea.  “Acha kupaniki! Nahisi mimi ndio nimemuamsha wakati namuwekea zawadi zake kitandani.” Nanaa akatulia. Kisha akagutuka kama aliyekumbuka kitu.

“Sasa mbona mimi sina zawadi!?” Geb akacheka tu. “Acha upendeleo Geb! Na mimi nataka zawadi.” “Mimi ndio zawadi yako!” “Mmmh! Zawadi hiyo ukiwa umesimama na nguo zako hivyo, mimi wala sitaki.” Geb alicheka mpaka akakaa. “Nanaa wewe ni mtundu wakupitiliza.” “Njoo mwaya Liv. Pole mama. Nilipitiwa usingizi.” Nanaa akampokea mtoto wake na kuanza kumbusu huku akimuongelesha. “Nyonya kwanza halafu ukanionyeshe zawadi alizokuletea dad.” Nanaa akaanza kunyonyesha huku wakizungumza na Geb na kucheka.

Liv alipolala, wakabaki wao wawili hapo kitandani wakizungumza na kufanya mapenzi. Geb alikuwa amemletea Ice cream. Wakawa wakila hapo kitandani. Mara ampake Geb kifuani nakuila kwa kulamba kifua cha Geb. Kule kupiga kelele kwa baridi ya ile ice cream aliyoimwaga Nanaa, ilifuata na kukumbatiwa na kupewa joto na Nanaa. Na hivi walilala mchana, ikawa fujo tupu hapo kitandani. Huyu anyonye hiki ashike hapa, afanye vile, ilimradi kusherehekea kupatana. Wakalala hoi. Kwa mapenzi ya siku mbili mfululizo.

Chanda Chema,…!

S

iku ya tatu Geb alimka na nguvu mpya. Akili iliyotulia hata usoni alionyesha yake yanamuendea sawa. Alitoka kitandani akamuacha Nanaa bado amelala. Alimbusu mara kadhaa, akamfunika vizuri, akaondoka. Hodi ya Mama G ndio iliyomtoa kitandani. Nanaa alikurupuka na kwenda kufungua mlango. Akampokea Mama G vyakula, ndipo wote wakagundua kidoleni kwa Nanaa kuna pete nzuri sana ya uchumba. Nanaa akabaki ametoa macho. “Wala sikujua kama amenivalisha hii pete! Itakuwa amenivalisha usiku tulipokuwa tumelala!” Bado Nanaa alikuwa kwenye mshangao. “Nzuri kweli kweli! Ndio anakuoa?” Mama G akauliza huku akicheka. “Sijui mama!” “Kwani hajakwambia?” “Kanivalisha nikiwa nimelala! Yaani sasa hivi na mimi ndio naiona. Ila nimejawa furaha ya ajabu mama yangu.” “Nakuona, hata usoni umebadilika!” Acha Nanaa aanze kuruka ruka. Alicheza kama mwehu huku Mama G anacheka.

Kidogo kama akakumbuka kitu, akatulia. “Sijui ndio atanioa!?” Nanaa akauliza huku akitaka kujua kama na Mama G atampokea. “Hana mwingine atakayeweza kuishi naye yule. Namjua Geb. Wewe ndio mwanamke utakayemfaa.” “Yeeeeyyyy! Mke wa Geb mieee!” Nanaa aliendelea kuruka ruka. Mama G alikuwa akimtizama huku anacheka. “Hongera mwanangu Nanaa. Naona umepata mume.” “Mume haswaa. Si mchezo! Kama karata, nimelamba DUME.” Mama G akaanguka kicheko.

“Chizi wewe!” “Acha mchezo mama. Na mimi nitaitwa Magesa! Siamini mama yangu.” “Nakuona mama Magesa. Hongera.” “Asante mama yangu. Nimefurahi sana umenipokea mimi kama mke wa Geb. Nimefurahi mnoo.” Nanaa alikuwa akihema kwa kucheza.

 “Sasa sijui nimuulize kama atanioa au nisubiri tu nimuone?” Nanaa aliuliza huku akiangalia kidole chake. Mama G alikuwa akimwangalia huku anacheka. “Eti mama?” “Wewe akipiga simu, mshukuru kwanza kwa hiyo pete. Halafu muache.” “Basi nampigia.” “Huwezi kusubiri!?” “Siwezi mama. Acha tu nimpigie. Nilivyokuwa ninahamu ya kuwa na mtu wangu hapa duniani! Mwanaume anayenipenda na kunithamini kama Geb!” “Mmmh! Naona umemsamehe kabisaa.” “Mama naye kwa kuweka visasi! Mambo gani hayaishi!?” Mama G alicheka sana. 

“Gafla mimi ndio wakuweka visasi, Nanaa mwanangu? Sio wewe uliyejidai unataka uanze maisha yako!” “Mama na wewe! Mambo ya zamani hivyo!” “Si ni juzi tu!?” “Bwana mimi sikumbuki! Kwanza twende tukachukue mizigo yangu, urudi nayo nyumbani.” “Pale kwenye ile nyumba yakupanga, wote tutaonekana machizi. Si uviache hata mwezi uishe?” “Wee! Unataka kunicheleweshea ndoa! Acha tu huyo Geb anione nimekusudia kutulia hapo kwake, anitangazie ndoa.” Mama G alicheka sana.

“Naona umepania?” “Sio kidogo.” Nanaa alijibu kwa kujiamini. “Ujue nakushukuru sana mama yangu! Asante sana kwa kunifundisha kutulia na kuwa mvumilivu. Naanza kuona matunda yake.” “Karibu mwanangu. Mungu awasaidieni nyumba yenye amani na utulivu. Mpate watoto kadiri mtakavyo.” “Si na wewe utakuwepo?” “Ukinihitaji nitakuwepo.” “Nakuhitaji sana mama yangu. Tena sana. Ujue najifunza sana kutoka kwako? Wewe ni mfano wa malezi ambayo sikuwahi kuwa nayo kabla. Najifunza kweli. Nataka tuishi wote ili niendelee kujifunza.” Mama G alifurahia sana kusikia hata Nanaa anamuhitaji. 

Japokuwa alikuwa na uwezo wa kuwa na nyumbani kwake, lakini ameishi na Geb maisha yao yote. Ni mtoto ambaye hakuwa tayari kumuachia kirahisi. Sasa kuona Nanaa amemkubalia kuendelea kuwepo kwenye maisha ya mwanae, ilimgusa zaidi na kuongeza upendo kwa Nanaa.

~~~~~~~~~~~~~~~

Nanaa Amechumbiwa Na Geb. Je Ndio Ndoa? Usikose Kujua Yatakayojiri Huku Wamekusudia Kuzika Ya Zamani. Yapi Yanazikika, Yepi Yatawafuata?

 Usikose Kuwa Nao Kwenye Penzi Zito La Geb & Nanaa.

 

 

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment