Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Ni Wangu! - Sehemu Ya 27. - Naomi Simulizi

Ni Wangu! - Sehemu Ya 27.

Safarini!

Safari ya kuelekea mji kasoro bahari ikaanza kila mmoja wao akitizamia wakati mzuri huko. Ilikuwa mida ya saa kumi jioni wakati wanaziacha kelele za jiji la Dar. Geb alijawa furaha na tumaini jipya. Sio kwamba Nanaa alikuwa na uzuri wa ajabu sana tofauti na wanawake wote aliokuwa nao Geb au wanao endelea kumtongoza Geb, lakini Nanaa aligusa eneo nyeti sana kwenye maisha yake. Aliweza kumfikia Geb kibinafsi. Alimjali Geb kama Geb. Wawe wamegombana, iwe mbele ya watu, kuwe kumetulia au la! Aliweza kumtazama Geb kama Geb na kuweza kujua kama yupo salama au la. Nini anataka! Amekula! Aliweza kuweka chuki pembeni kwanza ili kumuuliza hali yake na kujaribu kumliwaza. Hakukimbilia kuzitapanya pesa za Geb zilizokuwa zikionekana ni nyingi na hazina matumizi makubwa.

Aliweza kumtenga Geb na mali zake, akaweza kuwa na Geb tu. Mengine kwake alijihesabia anaweza kuyamudu, endapo Mungu akimjalia uzima na afya njema. Hakusumbuka na pesa zake. Hakupagawa. Hakupigia mahesabu na kujiwekea mipango kwenye pesa za Geb. Kingine alichokimudu ni mahusiano na mama yake. Aliweza kumuingia mama G, mpaka wakawa marafiki. Geb ni mtu wa familia. Nanaa aliweza kuwa kati kati yao na kuonyesha kuwapenda na kuwajali wote.

~~~~~~~~~~~~~~~

Nanaa akampigia simu mama G kumuaga na kumtaarifu kuwa ndio wanaanza safari. Wakataniana kidogo, Nanaa akakata simu. “Ujue Nanaa wewe ni mtundu sana?” “Mama G, ndio mtundu. Yeye ndio ananifundisha.” Wakacheka. “Naona mmetokea kuelewana sana na mama.” “Ujue nimegundua mama yako hana neno na mtu. Mpole.” Geb akacheka akajua Nanaa hajaujua upande mwingine wa mama yao. “Unacheka nini sasa?” “Usimuone vile mama. Ni mkorofi huyo! Usimuone akikuchekea au akinyamaza. Atakuja kukusimulia habari zake. Mkorofi yule asiyeogopa kitu wala mtu.” Nanaa hakuamini. “Haiwezekani Geb! Alivyo mkimya vile!” “Kwa sababu hujamuona akikorofishwa. Au ukimuona ametulia hivyo, ujue mambo yake yanaenda kama anavyotaka yeye. Mkali sana kwangu na Grace. Hatakagi ujinga.” Nanaa akacheka kama hasadiki huku akimfikiria mama G, shoga yake.

“Ila nakiri amejawa upendo.” “Sana. Na kujali. Huwa namfananisha na Grace. Lile kundi lote la marafiki zangu wanampenda. Wote waliokuwa wakitokea mikoani, walimfanya mama kama mama yao. Na yeye alikuwa akiwajali sana. Wote wale, hawahitaji kukaribishwa na mtu sehemu alipo mama. Wakipata wachumba, lazima waje kuwatambulisha kwa mama. Wakipata matatizo ya ndoa, lazima waje kwa mama. Au mama aende kwao. Wakipata watoto, basi ujue mama G, kapata mjukuu. Vile vitoto vyote ulivyoviona kwenye birthday ya Junior, vinamjua bibi Fili kama bibi yao.” “Niliwasikia siku ile.” “Basi ndio hivyo. Na mama nao anawapenda sana.” Nanaa akafikiria kidogo.

“Ila nikwambie ukweli Geb, nampenda sana mama yako. Anazungumza na mimi kwa ukweli na uwazi. Ukimsikia anavyonishauri na kunitia moyo, utahisi upendo wa dhati wa mama kwa mwanae. Kwa mara ya kwanza maishani, nimeweza kuhisi upendo wa mama upoje. Nikiendelea kuwa naye yule, najihisi nitakuja kuwa mama mzuri sana kwa wanangu.”  Geb akacheka. 

“Unataka kuja kuwa na watoto?” Geb akauliza. “Napenda familia Geb. Lakini sio sasa hivi. Mpaka shule yangu iishe, nijue maisha yangu yanamuelekeo gani.” Geb akamwangalia kidogo. “Mungu akinijalia nikiwa na watoto, nitawapa kile ambacho mimi nimekikosa maishani. Nitawapenda na kuwalinda kwa kadiri ya uwezo wangu. Mungu anisaidie tu nije kuwa na ndoa nzuri.” Nanaa aliinamisha kichwa kama anayefikiria, Geb akamtizama akarudisha macho barabarani, safari ya Morogoro ikaendelea.

~~~~~~~~~~~~~~~

Walifika Morogoro, moja kwa moja wakaelekea Nashera hotel. Wakafika mapokezi. Geb akachukua chumba, safari ya chumbani kwao ikaanza. “Ni pazuri!” Nanaa akasifia huku akiangaza macho. “Ujue sijawahi kufika Morogoro?” “Sikujua.” “Ndio mara yangu ya kwanza.” “Umeona nje? Kuna sehemu ya kuogelea. Utataka kuogelea?” Nanaa akacheka sana. “Sasa unacheka nini?” Geb akauliza. “Mwenzio sijui hata wanaogeleaje.” “Kweli!?” “Hivi mbona unasahau historia yangu ya maisha wewe Geb? Dar kwenyewe nimekuja sababu ya kusoma hapo chuo kikuu. Sehemu niliyokuwa nikisafiri, tena kwa kuhesabu ni kwenda kijijini kwa kina bibi. Tena kama msichana wa kazi haendi. Ili mimi nikafanye kazi. Labda na shuleni Ashira. Safari za Marangu nikienda shuleni. Basi.” “Basi tutakuwa tunasafiri mara kwa mara ili utembee kidogo. Sehemu za mbali hatutaendesha. Ili ukifika usiwe umechoka. Tuzurule uwe unaona na sehemu nyingine.” “Nitafurahi.” Wakaendelea kutembea kuelekea kwenye chumba chao.

 Wakafungua mlango wa chumbani kwao, wakaingia. Geb alizunguka kidogo kama anayekagua. “Naona pasafi.” Alirudi na kusifia. “Tutaenda kuwaona hao wakulima saa ngapi?” Nanaa akauliza wakati anaweka mizigo yake vizuri. “Kesho. Leo nataka tupumzike tu.” Nanaa akacheka kidogo. “Basi ngoja nikaoge. Leo nimekuwa na shuguli nyingi ofisini! Nahisi nanuka jasho.” “Mbona kauli za umoja tu? Na mimi!?” Nanaa akaanza kubabaika. “Sikujua kama na wewe unataka kuoga sasa hivi!” Geb akamsogelea, akamvuta karibu akaanza kumbusu. 

Penzi Jipya Na Tamu Kwa Nanaa.

Baada ya muda mfupi sana Nanaa akajikuta hana nguo hata moja. Geb alikuwa akizivua moja baada ya nyingine wakati akiendelea kumbusu, kisha akamuweka kitandani. “Labda nikaoge kwanza Geb.” Nanaa akinong’ona akiwa kitandani akimwangalia Geb anavyotoa nguo zake. Akaficha matiti yake kwa viganja vyake kwa kuwa macho ya Geb yalitua hapo. Geb akatabasamu na kuinama pale alipokuwa amelala Nanaa. Akamnyanyua taratibu huku akimbusu mpaka bafuni. Yalikuwa mambo mapya na mageni kwa Nanaa. Hakuwahi kuona mapenzi ya namna ile. Geb alionekana ametulia na kila kitu alikifanya kwa utaratibu.

Huko bafuni walichukua zaidi ya nusu saa wakioga, na kupeana mabusu yasiyoisha. Geb hakuacha kumkumbatia na kumpapasa. Wakati wote alikuwa kwenye mikono ya Geb. Geb alikuwa na staili nyingi sana za kufanya mapenzi hapo bafuni, kitu kilichomtoa ushamba Nanaa ambaye alidhania ni mjuzi wa mapenzi. Geb alijua kumridhisha hapo hapo bafuni, Nanaa hakujua kama unaweza kufanya mapenzi bafuni na kuridhika. Alibaki akijiuliza itakuwaje watakapofika kitandani! Alifurahia kushikwa na kufanya mapenzi na Geb. 

Nanaa alitaka kutoa ujuzi wake wote ili kumfurahisha Geb kama alivyokuwa akifanya kwa wanaume zake wengine, lakini akagundua haitakuwa hivyo kwa Geb. Alimuonyesha anataka siku hiyo amfurahishe yeye zaidi. Hakuwa na papara kwenye mapenzi hata kidogo. Alikuwa mtulivu na kila kitu alifanya kwa hisia zote na alionyesha kumfurahia vile alivyo. Kama ni kumbusu, basi alinyonya midomo yake kwa utulivu na kwa hisia kubwa kana kwamba ni kitu anachokihitaji na kukithamini. 

Hakutaka Nanaa atumie nguvu nyingi. Kila alipomuona anahangaika sana, alimvuta na kuanza kumbusu kwa utulivu kama kumtuliza na kuanza kufanya naye yeye mapenzi kwa namna yake, kitu kilichomfanya Nanaa kwa mara ya kwanza kufurahia mapenzi, sio kuona anawajibika kumfurahisha mtu ili apendwe. Kila alipofika kifuani kwa Nanaa, alionyesha alikusudia kufika hapo na ni kitu alichokuwa akikitamani. Alitua kifuani kwa Nanaa, akabusu katikati ya matiti yake. “Waw!” Geb alitazama matiti ya Nanaa, na kuyagusa taratibu. Hapakuwa na jinsi ukamwambia Nanaa, eti Mungu hakuumba kifua chake vizuri. 

Kwa mtazamo ule wa Geb  kwenye kifua chake, wazi alionekana kuthamini kile anachokiona na kukishika. Alipoinama na kuanza kubusu chuchu zake, tayari pumzi za Nanaa zilikuwa za tofauti. Alipoanza kunyonya, ndipo Nanaa alipoanza kunung’unika. Sio kwa unyonyaji ule wa matiti! Alimuhamisha Nanaa katika ulimwengu huu, nakutamani siku zigande. Wabakie kwenye ulimwengu wao wa mapenzi tu. Alifurahia vile Geb alivyoweza kunyonywa matiti yake huku akifanya naye mapenzi.  

Baada ya kushuka, na kutulia. Akakumbuka Geb alishamfikisha kileleni mara mbili tayari wakiwa pale pale kitandani na yeye hajapata kitu tokea magoli mawili aliyofunga akiwa bafuni. Taratibu akafungua macho yake, akaona Geb anamtizama huku mkono mmoja wa Geb ukiendelea kumpapasa kifuani. “Unamatiti mazuri sana Nanaa.” Geb akasifia huku akitoa macho yake usoni kwa Nanaa na kurudisha kifuani. Nanaa akamuona vile anavyoyaangalia kwa uchu kana kwamba hayapo mbele yake. Akakumbuka raha aliyotoka kuipata mara baara ya Geb kuyachezea matiti hayo. Akacheka kidogo na kuuma midomo yake kimahaba. “Asante.” Nanaa akashukuru huku akifikiria kitu cha kufanya ili amridhishe na yeye pale kitandani. Alishachanganyikiwa, akajiona hajui kitu mbele ya Geb.

“Umechoka?” Geb akamuuliza taratibu huku akijaribu kufikia midomo yake. Nanaa akatingisha kichwa. “Naomba tuendelee kidogo. Bado ninahamu na wewe Nanaa!” Ilikuwa kama anaamsha hisia mpya zilizokuwa zimefichwa ndani yake. “Unanifurahia?” Akauliza akionyesha wasiwasi kidogo. “Sana. Ndio maana sitosheki.” Nanaa akafurahi sana kusikia hivyo. Maneno hayo Geb aliyamalizia masikioni kwa Nanaa, akambusu sikio lake. Tayari alishamchanganya Nanaa. 

Midomo yake ikahamia shingoni kwake. Taratibu akinyonya na kubusu shingo yake. Alipoona hali ya Nanaa inazidi kubadilika, akamtoa pale kitandani. Alikaa akiwa ameegemea ukutani, akampakata. Akiwa anamsaidia kumnyanyua juu na chini taratibu huku Nanaa analalamika, midomo yake ikarudi kifuani kwa Nanaa, nakuanza kuyanyonya yale matiti taratibu huku Nanaa akiongeza juhudi ya kuongeza mwendo, kwani alihisi akili ya Geb imeanza kupotea pale. Nguvu ikaongezeka. Alipokuwa amemshikilia kwenye kiuno chake, alizidi kukaza huku akiyanyonya matiti yake kama mtoto mwenye njaa. Nanaa akajua na yeye yupo juu na yupo karibu na golini. Aliendelea kupanda juu huku akishuka kwa staili ya kuzungusha kiuno kidogo ili kuongeza msuguano, hapo ndipo alipomuona Geb akifunga goli jingine kwa hisia zote huku midomo yake ikiwa kwenye matiti.

Alisikia akitamka jina lake taratibu huku akipunguza kukandamiza kiuno chake. “Na n aaa!” Aliitamka kwa utulivu na hisia zote mpaka Nanaa akafurahia. Akajua wazi amemaliza. Akataka kushuka kama kumpa nafasi yakupumzika, lakini akashangaa Geb anamshika kwa nguvu. “Please!” Akamsihi. Nanaa hakuamini. Alifurahi kuona vile Geb anavyo muhitaji. Akajirudisha vizuri pale, akamkumbatia. Mikono ya Geb ikaanza kutembea tena. Nanaa hakuamini. Alijua atataka kumpumzika tena kidogo lakini alionekana bado ananguvu. 

Alibaki amemkumbatia pale pale alipokuwa amepakatwa huku Geb akiendelea kupapasa mgongo wake. Juu ya kiuno, chini kidogo. Juu, chini. Vidole vikaanza kutembea katikati ya uti wa mgongo wa Nanaa, hisia zikaanza kuamka kwao wote wawili. Nanaa akakumbuka anatakiwa kujisafisha kwanza kabla hawajaendelea. “Nikajisafishe kwanza.” Nanaa akanongona. Akajibiwa na busu katikati ya matiti yake. Akagundua mikono ya Geb imetulia chini kabisa ya kiuno. Alipojitingisha kidogo, kumsikilizia Geb mwenyewe, akagundua mtoto wa kiume yupo kamili kama ndio hajafunga bao hata moja.

Nanaa akacheka nafsini mwake. Akaanza kuhisi ananyanyuliwa tena juu, na kushushwa taratibu, akajua Geb alifurahia ile staili ya kumpakata. Akaanza kusadia huku akinyonga nyonga, kiuno kuongeza msuguano. Bado hakuwa amejisafisha. Kadiri mabusu yalivyokuwa yakiendelea na kupapaswa, ndivyo Nanaa alivyoongeza spidi. Midomo ya Geb iliyokuwa akihamia titi moja hadi jingine ilizidi kumchanganya Nanaa kila alipokuwa akijaribu kufikiria raha ile inatokea kwenye matiti zaidi au mikono iliyokuwa ikipapasa mgongo au ni ule msuguano anaoupata kati yake na Geb.

Alipoona Nanaa anazidi kulalamika, akamuinamisha. Nanaa akashukuru, angalau apunguze zile kelele pale mbele ya uso wa Geb. Geb alipiga magoti nyuma yake. Akashikilia vizuri kiuno cha Nanaa, na kupenya taratibu huku akitoka kama amegairi. Alizidi kumchanganya Nanaa. “Usiniache Geb!” Nanaa alianza kulalamika akidhani mchezo umeisha. Hakujua ni wapi aligusa huko ndani na kusababisha kushindwa hata kukumbuka kuzungusha kiuno. Akabaki kama mjinga akiomba rehema za Geb. Ni kama aliyekuwa alishazisomea ‘G’ sports zote za Nanaa. Alihakikisha ile aliyoigundua baada ya kumwinamisha, inatoa matokeo aliyokusudia. Aliisugua mara kadhaa, yeye mwenyewe akiwa amemshikilia Nanaa kwa nguvu sana huku akiendelea. Nanaa alinung’unika huku Geb akiendelea kuongeza mwendo. Baada ya muda Nanaa akafika kwenye ‘point of no return’. Akasalimu amri. Akabaki akilalama bila kuweza kutoa msaada wowote ila kufurahia tu. Baada ya sekunde chache akasikia na jina lake linatajwa kama mwanzo. Akajua na Geb naye amefankiwa. 

~~~~~~~~~~~~~~~

Alishafanya mapenzi mara kadhaa, lakini hakuwahi kufika kileleni mara nyingi vile, zaidi ya mwenzie! Zac alishawahi kumfikisha mara moja, lakini akiwa ameshachubuka sana. Kwa hiyo ilikuwa ni furaha iliyojaa na maumivu. Akashindwa hata aeleze ni nini. Zac siku hiyo alitumia muda mwingi sana kwenye mapenzi akitaka kumridhisha na yeye Nanaa. Akahangaika muda mrefu bila mafanikio mpaka Nanaa akahisi akili yake Zac haikuwa pale. Baada ya muda mrefu wa maumivu kuendelea, Zac aking’ang’ana kutaka siku hiyo kumridhisha na yeye pale kitandani na kushindwa, akaamua kumalizia kwa kumnyonya tu Nanaa, ndipo Nanaa akafika kileleni. Lakini alikuwa hoi, na Zac siku hiyo hakupata kitu. Na ndio ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kuteseka alipokuwa ikifika zamu yake. Wakati mwingine alikuwa akimdanganya Zac kama amemfikisha ili kumridhisha tu na wamalize mchezo apumzike.

~~~~~~~~~~~~~~~

Sasa leo Geb ndio ameweka historia kwa mara ya kwanza kwenye maisha ya mapenzi kwa dada huyo. Yeye ndiye alikuwa mwanaume wake wa kwanza kushuhudia tukio hilo. Walifika kileleni kwa pamoja. Alipata mabao mengi yakueleweka na bado hakuwa amechubuliwa. Geb alipomaliza. Akambusu kiunoni ndipo akaanza kutoka taratibu. 

“Asante Nanaa. Hujui ni kiasi gani umeniridhisha. Nilitamani huu wakati kwa muda mrefu sana. Asante.” Nanaa akashangaa. Ni siku chache tu alikuwa na mpenzi wake huko Marangu. Sasa alimtamanije yeye? Akawaza wakati akijiweka sawa. “Na mimi nimefurahia Geb. Asante.”  Nanaa naye akaona awe muungwana. Atoe shukurani. “Unataka twende tukale?” Nanaa akatingisha kichwa kukataa. “Huna njaa!?” Geb alishamjua Nanaa mpenda kula. Akamuona machozi yanamtoka. “Chakula huwa nakila wakati wote Geb. Na ninajua nitakuwa nacho tu. Lakini sijawahi kuwa na wakati kama huu maishani. Naomba nikuombe kitu.” Nanaa akajifuta machozi. “Unataka nini?” “Nilale kifuani kwako. Unikumbatie japo kidogo tu.” “Okay.” Geb aliitikia kwa upole. Akamsogeza karibu yake. Akamlaza kifuani kwake, akamkumbatia. Nanaa akatulia pale kifuani, asiamini.

Ulikuwa ni wakati wa thamani sana kwa Nanaa. Alihisi kitu cha tofauti kwa Geb, tofauti na wanaume wote aliokwisha fanya nao mapenzi. Geb alimuonyesha anampenda na kumuhitaji yeye kama Nanaa. Aliendelea kumkumbatia wakiwa wametulia kabisa pale kitandani. Mwishoe akahisi amelala. “Nanaa!” Geb akamuita taratibu, lakini hakuitika. Geb akacheka kidogo. “Mpenda kula huyu, amekataa kula! Maajabu!” Geb aliwaza wakati akijaribu kuvuta shuka na mguu ili amfunike, bila kumuamsha. Akamfunika vizuri, akajikuta na yeye anapitiwa na usingizi.

~~~~~~~~~~~~~~~

Akiwa usingizini, akahisi Nanaa ametoka kifuani na kujilaza pembeni yake. Akajigeuza kumpa mgongo. Geb akamvuta tena karibu yake, akamfunika na kumkumbatia Nanaa akiwa bado amempa mgongo. Wakarudi tena kulala. Walikuja kushituka saa 4 usiku. Nanaa akanyanyuka kwenda sehemu ilipo bafu na choo. Alioga kama kutoa uchafu wa hekaheka za masaa machache yaliyopita. Wakati anarudi chumbani kwa kunyata, Geb akamwambia awashe taa. “Samahani nimekuamsha!”. 

Akatoa nguo kwenye begi lake akaanza kuvaa.  “Naomba usivae. Nataka kukuona hivyo ulivyo.” Nanaa akajisikia aibu. “Nasikia baridi, Geb!” “Njoo hapa kitandani, nitakukumbatia. Lakini usivae nguo tafadhali.” Akarudisha ile nguo taratibu. Akarudi pale kitandani, akamruka tena Geb, nakujirudisha pale alipokuwa amelala, akageukia ukutani.

          Walijilaza Geb akiwa nyuma ya mgongo wake. Akaamza kumpapasa taratibu kwa kidole chake, kama anayechora kitu mgongoni kwa Nanaa, kuanzia shingoni mpaka kiunoni, taratibu. “Geb!” Nanaa akaita kwa upole. “Mmmh!” Geb akaitika. “Itakuaje?” Akauliza, lakini Geb akatulia akabaki akimpapasa taratibu, mwishowe akamgeuza Nanaa. “Niambie unataka iweje?” Nanaa akaanza kubabaika. “Sielewi! Naogopa nahisi narudia kosa.” “Siwezi kuruhusu ukarudia kosa Nanaa. Labda usiwe na mimi. Sijalala na wewe hapa kwa bahati mbaya. Huwa sikurupuki kwenye swala la mahusiano. Hata mimi sitaki kuumia. Usiogope. Tutakuwa sawa tu.” “Wangapi?” Nanaa akarusha tena swali jingine.

“Ni mimi na wewe tu.” Geb akajibu. “Na Liz?” Nanaa akauliza tena. Geb akamwangalia kisha akambusu. “Kuanzia sasa hivi, ni mimi na wewe, tu. Basi.” Nanaa akaanza kulia kama haamini kwani Geb hakutoa maelezo yeyote juu ya mahusiano aliyokuwa nayo na Liz. Aliishia kumbusu na kufanya naye mapenzi. Na yeye kwa kuwa alishamtamani Geb, alishindwa hata kujizuia. Akajikuta amerudia yale yale aliyoyafanya kwa Jamal.

“Niangalie Nanaa.” Nanaa akabaki ameficha uso wake kwenye mto akilia. “Najiona mjinga sana. Narudia mambo yale yale naishia kuumia. Na kinachoniogopesha zaidi, nahisi safari hii ni tofauti, Geb.” “Tofauti yake ni nini?” “Unakumbuka nilikwambia nakupenda? Wewe sio wa kwanza kukwambia hivyo. Nilishawaambia wengi ili wawe na mimi tu, bila kujua kumbe kuna zaidi.” “Zaidi!?” Geb akauliza kwa mshangao kidogo.

“Hisia ninazopata unaponishika wewe ni tofauti kabisa. Sijawahi kujisikia hivi maishani Geb. Hakuna mwanaume aliyewahi kugusa upande huu mwingine wa maisha yangu ila wewe tu. Sitaki tuendelee sana, halafu ukaja kuniacha. Nitateseka mno.”  Geb akambusu tena mdomoni kwa muda kisha akamuweka kwenye mto, karibu yake sana akabaki akimwangalia huku akimchezea sehemu za masikio na pembeni ya nywele.

 “Unakumbuka siku tulipokuwa tumesimama pale Mlimani City? Unakumbuka nilikuomba ubaki nyumbani kwangu kwa kuwa nakuhitaji kwenye maisha yangu? Nilikuwa namaanisha Nanaa. Na wewe kukubali kubaki pale nyumbani kwangu, kwangu kuna maana kubwa sana. Na ndio maana nilihakikisha Liz harudi tena kitandani kwangu. Kuna kitu nilikipoteza zamani sana, wewe ndio umenirudishia, na ndio maana nilikuomba ubaki kwenye maisha yangu.” Geb akaendelea taratibu huku akimtizama Nanaa kwa upendo.

“Usifikiri sikutambua ladha ya chakula ulichokuwa ukipika. Mara ya kwanza tu nilipoweka chakula chako mdomoni, nilijua mpishi hakuwa ni mama wala Grace. Moja kwa moja nilijua wewe ndio utakuwa umepika. Najua ladha ya chakula cha mama na Grace. Hata nikikikuta chakula mezani, wao hawapo, nikiweka mdomoni tu, najua ni nani amepika.” Nanaa aliendelea kumsikiliza kwa makini huku akimtizama mara moja moja.

“Nakufuatilia tokea tupo tunasoma na James, ndio maana sijasahau historia yako na ninafahamu kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yako, na ndio maana nilikuomba yale unayomwambia James, unishirikishe na mimi. Usifikiri huwa namwambia hivyo kila mtu, Nanaa. Sizunguki kwenye maofisi ya watu na ‘Vanilla Ice cream’ mkononi! Eti niache kazi zangu, na kwenda kununua Ice cream mchana, jua linawaka, tena ni siku ya kazi!” Nanaa akacheka kidogo.

“Sikudanganyi Nanaa. Huwa sifanyi hivyo. Mimi ni mvivu wa kula kama unavyonijua. Kwa hiyo sehemu zinazouzwa vyakula sio sehemu ningependa kwenda kutembelea na huwa sifanyi hivyo ni mpaka inilazimu. Labda nimemzungusha mama mjini kwa muda mrefu, ndio inabidi kumpeleka sehemu ale, au akiwa na hamu ya chakula fulani kinachouzwa sehemu, ndio nampeleka kwenye hiyo migahawa akale. Hivyo hivyo na kwa Grace. Haijawahi kutokea eti naacha kazi zangu, nakwenda kutafuta chakula kwenye migahawa ili nimpelekee yeye! Hata mara moja. Kwanza nakuwa sina hata wazo la chakula. Najua nahitaji chakula, pale mama anaponikumbusha kula, basi. Nakufuata kazini kukupeleka kula, kwa kuwa nakufikiria Nanaa.” Nanaa alizidi kujisikia vizuri.

“Nakufikiria sana kuliko unavyodhani. Na ndio maana niliumia sana ulipoona nilikupuuza siku uliponiacha ofisini ukasema hujisikii vizuri. Nafikiri nilikuwa kama nimeshituka au sijui nilipatwa na hali gani! Kwanza ilikuwa ni kama nimebahatika kwa mara ya kwanza kukaa karibu na wewe.” Nanaa alicheka kwa kujidharau. “Uliona ni bahati!?” “Kwangu ilikuwa bahati Nanaa. James anakupenda na kukuheshimu sana. Jinsi anavyokusimulia kwetu, yaani kuwa karibu na wewe lazima uone ni bahati. Ameweka thamani kubwa sana kwenye maisha yako. Na kingine kilichonipa kigugumizi nisijue ni Mungu amenipendelea au la, ni pale mama aliponiambia utakuwa ukiishi pale na sisi. Nilihisi kama sikusikia vizuri au Mungu amenibariki zaidi ya ninavyostahili.” Nanaa hakuwa akiamini. 

“Mwenzio nilijua ulikasirika. Kwa kuwa ulinyamaza kwa muda! Niliogopa nikaanza kufikiria pakwenda.” Geb akacheka. “Pale mwenzio nilikuwa ni kama naunganisha matukio. Nilikuwa najiambia ndio Mungu ameniletea mke kabisa ndani ya nyumba yangu, ili nisihangaike. Ndio maana Liz alipotaka nikufukuze..” “Kumbe Liz alitaka unifukuze?” Nanaa hakuwa akilijua hilo. Kidogo ikamsumbua, Geb akamuona amekosa raha.

“Liz hawezi maisha ya watu wengi. Na sio wewe tu aliyetaka uondoke pale. Alitaka niwafukuze watu wote pale, niwatafutie nyumba nyingine, ili tuishi mimi na yeye tu. Na masharti mengine ambayo nitakuja kukwambia wakati mwingine. Nilikubali yeye aondoke, nikiwa sijui hata kama utanikubali. Nakuhitaji Nanaa, kuliko ambavyo nitakueleza.” Geb alifikiria kidogo.

“Nilikusimulia siku niliyokuwa polisi. Nikweli nilikuwa nikikuwaza wewe tu. Nilibambikiziwa kosa la mauaji Nanaa. Nilijua kama sitanyongwa, basi hukumu yangu itakuwa kifungo cha maisha. Nilikuwa nakutaja usiku kucha. Huku nikifikiria jinsi mwanaume mwingine atakavyonipokonya penzi langu.” Nanaa hakuwa akiamini kama yale maneno anaambiwa yeye. Tena kutoka kwa Geb!

“Nakupenda sana, Nanaa. Zaidi nimefurahia kufanya mapenzi na wewe. Kwangu ni bahati. Silali na kila mwanamke mimi. Siku ile ya jumapili, sababu kubwa ya kuishia jela, nikukataa kufanya mapenzi na Rita. Alikuwa akining’ang’ania nilale naye, lakini mimi sipo hivyo Nanaa. Sivui nguo hovyo mbele ya wanawake. Najiheshimu sana. Kwa umri huu nilionao, uwezo Mungu alionijalia, na majaribu yanayonizunguka kama sio kujiheshimu ungekuta nina historia ya wanawake kibao kwenye maisha yangu. Najua nina uwezo wakulala na mwanamke yeyote yule ninayetaka. Lakini wewe ni msichana wangu wa nne, na ninaomba Mungu uwe wa mwisho. Kwangu bado naona ni idadi kubwa sana. Kwanza ningebahatika tokea zamani kupata mwanamke mtulivu, nahisi nisingehangaika na wanawake wengine.”

“Kwa hiyo sasa hivi nitakuwa ni mimi peke yangu tu? Hutamvulia mwingine tena nguo?” “Nakuahidi Nanaa. Natafuta nini tena?Unanitosheleza sana. Kuna jinsi unavyokuwa mikononi mwangu, sichoki kufanya mapenzi na wewe na unanifanya nijisikie vizuri sana. Umekuwa faraja ya kutosha kwenye maisha yangu. Najua unaona kuna watu wengi wamenizunguka, lakini nakuhitaji wewe.” Nanaa hakuwa akiamini. Alivuta mto nakujifunika usoni, akaanza kulia tena.

~~~~~~~~~~~~~~~

Alikumbuka shida alizokuwa akipata. Kuhangaika kuvutia wanaume wampende. Juhudi alizokuwa akifanya kitandani, tena kwa watu ambao hata hawakumthamini! Madonda waliyokuwa wakimsababishia wanapokuwa wakifanya naye mapenzi! Vile ambavyo hawakuwa wakijali kuridhika kwake! Waliutumia huo mwili uliokuwa ukisifiwa mpaka na wanawake wenzake, bila shukurani, na kumuacha kama takataka tu. Leo anampata mwanaume kama Geb anamwambia anamuhitaji! Wamefanya mapenzi zaidi ya masaa mawili! Geb anahakikisha hachubuki! Kila wakati anaamsha hisia, na kurudisha mawazo ya Nanaa pale kitandani. Kila anapokuwa akimalizia, alitaja jina lake yeye Nanaa. Kwake kilikuwa ni kiashiria kizuri sana. Alimkumbatia na kumbusu kama kitu cha thamani sana. Alihisi ni ndoto, akaogopa kuamka. 

~~~~~~~~~~~~~~~

Geb akaingia na yeye chini ya ule mto akatafuta midomo yake mpaka akaipata, akaanza kuinyonya taratibu. Nanaa alizidi kuogopa kufungua macho. “Mungu wangu, kama huu ni usingizi, naomba nisiamke milele.” Nanaa akawaza, huku akihisi mikono ya Geb ikifanya juhudi ya kumtenganisha na shuka alilokuwa amemfunika yeye mwenyewe.

Nanaa alizungukwa na hisia za namna yake zilizomfanya aendelee kujisogeza karibu zaidi huku akitoa mihemo ya raha. Baada ya sekunde chache, walijikuta wote wapo juu ya ule mto, wala shuka halipo tena karibu yao. Geb alishamlaza sawia  juu ya mwili wake huku akiendelea kumbusu nakumpapasa kuanzia juu mpaka chini. Alishangaa kugundua Geb yupo tayari kwa raundi nyingine! Akajua atapenya haraka sana, lakini haikuwa hivyo. Bado Geb hakuwa ameridhika na utayari wa Nanaa. Alishajua ni mlio gani anaofikia Nanaa, ndio aingie. Akamuweka pembeni nakuanza kumchezea zaidi.

Kadiri Geb alivyokuwa akibusu na kunyonya viungo vya Nanaa, ndivyo alivyomsikia akinung’unika. Alihisi Geb anamchelewesha. Akamvuta na kulazimishia kuingiliwa kwa nguvu, akamuona anatapatapa kama aliyekuwa majini. Miguu haitulii. Akamuweka chali, akampandia huku amekutanisha viganja vyao. Alipohakikisha midomo yake imenyonya midomo ya Nanaa, ndipo alipoanza kupanda na kushuka taratibu. Nanaa alikuwa akilalamika sana kama anayeonewa. Kadiri muda ulivyozidi kwenda, ndivyo Nanaa alivyoendelea kulalamika. Alitoa milio ya kufurahia kile anachofanyiwa. Zaidi ule muunganiko wa miili yao na mikono ambayo bado Geb aligoma kuachia. 

Mwana kaka huyo alitawala mchezo mzima, Nanaa akabaki akifurahia tu. Aliendelea kushikilia mikono yake huku akimnyonya midomo yake, na kufanya naye mapenzi. Alipoona Nanaa analemewa, alimkumbatia kwa mkono mmoja, huku akiwa bado juu ya mwili wake. Uzito wake wa mwili aliuweka kwenye magoti yaliyotua kitandani, pembeni ya mapaja ya Nanaa. Ndipo midomo yake ikatua kifuani kwa Nanaa. Kabla hajaamia titi la pili, tayari Nanaa alikuwa amemaliza anaita Geb kama anayetaka amsaidie, anazama. Wakati anamalizia, bila kupoteza muda wala kutaka apumzike, Geb alimnyanyua miguu yote miwili akabaki ameikumbatia, akaweza kupenya kwa urahisi. 

Nanaa alijiambia hiyo ni zamu ya Geb. Akajiambia atajitahidi kumridhisha ili na yeye apate goli moja kabla ya chakula. Lakini Geb aliharibu pale alipogusa G spot nyingine. Alijitahidi kujikaza hata kusogeza kiuno ili Geb asiendelee kugusa lile eneo litakalomfanya apoteze ufahamu, na kushindwa kujielewa akabaki kizembe, lakini akashindwa. Geb alikuwa amekumbatia mapaja yake vizuri. Na yeye akiingia na kutoka bila papara. Alihakikisha Nanaa hasogezi sehemu aliyokuwa akilenga bila kukosea. Nanaa alijitahidi lakini si kwa G spot ile. Labda angegusa nyingine, angejikaza na asiwe mbinafsi. Hapakuwa na kuzungusha nyonga, akabaki akilalama pale kama aliyekuwa na ukame wa mwaka mzima. 

Kama kawaida yake hakuonyesha haraka. Aliendelea kuvuta hisia akiwa ameshikilia mapaja ya mwanadada huyo huku akiyapapasa. Nanaa alijichukia pale alipokuwa amefika kwa mara nyingine tena kwenye ‘point of no return’, akamuhurumia Geb. Kwa mara ya pili katika mchezo huo tena anakosa bao! Akasikia jina lake likitanjwa taratibu. Nanaa akajua tayari. Akafurahi sana, akajua na yeye yupo njiani. Spidi ikaongezeka, akaona anazidi kukamatwa kwa nguvu. Safari hiyo jina halikutajwa mara moja. Lilitajwa mara kadhaa huku akiongeza kasi na kumng’ang’ania zaidi. Asijue ndivyo anavyozidi kumkoleza na kumsogeza Nanaa karibu zaidi ya golini. Wakati Nanaa anafika tu, ndipo na Geb naye anamalizia. Alisogea tena mara tatu, Geb akamaliza. “Daah! Samahani. Nimeshindwa kukusubiria. Nililemewa.” Nanaa akacheka. “Usinicheke bwana! Unanifanya nashindwa kujizuia!”  “Lakini hata mimi nimefanikiwa.” “Kweli?” “Kweli. Asante sana.” Geb akatabasamu na kujitupa pembeni yake. Akafunga macho. 

~~~~~~~~~~~~~~~

Nanaa alijua kwa mchezo ule, ataishiwa nguvu. Akamtolea maji, na juisi aliyokuwa amemfungashia. Ilikuwa ndani ya chupa ya kutopooza. Bado ilikuwa baridi. Akampa. “Kaa unywe juisi na maji.” “Asante. Naona nianze maji. Nahisi nimekaukiwa.” “Pole.” Geb akanywa yale maji bila hata kupumzika, kisha akavuta ile chupa ya juisi. Ilikuwa ni chupa maalumu kama thermos, lakini hiyo ilikuwa maalumu kwa juisi. Ndipo alipomuona mama yake akimuwekea huko juisi. Na yeye akaanza kuweka kwenye chupa hiyohiyo. Alikunywa juisi yote. Akavuta pumzi kwa nguvu akazishusha akarudi kujilaza. 

Kama baada ya dakika tano akaamka. “Twende tukaoge, halafu tukatafute chakula.” “Ni saa 6:45 usiku Geb. Inakwenda saa 7. Sidhani kama tutapata chakula mahali.” Geb akakaa kwa haraka. “Haiwezekani. Utakula nini sasa?” Nanaa akacheka. “Yapo matunda mengi tu. Nitakula. Nitakuwa sawa.” “Daah! Samahani. Nilipitiwa.” “Mwenzio nimefurahia sana, kuliko hata ungenipa chakula.” “Kweli? Au unataka nisijisikie tu vibaya?” “Kweli Geb. Kumbuka mimi ndiye niliyekuomba tubaki wote hapa kitandani. Nilihitaji ku..” Nanaa akanyamaza na kuinama.

“Namimi nilihitaji kupata muda na wewe Nanaa.” “Asante.” Nanaa akashukuru kwa sauti ya chini, akasimama nakuvuta taulo akataka kujifunga. “Usijifunge bwana!” “Si umesema tunaenda kuoga?” Nanaa akauliza kwa aibu huku akijificha kidogo. “Ndiyo, tunaenda kuoga. Lakini naomba usijifunge taulo. Napenda kuangalia mwili wako. Una umbile zuri sana Nanaa.” Nanaa akacheka kwa aibu na kujifunika lile taulo usoni. Alishitukia Geb na yeye amesimama, akamkumbatia.

“Uliniogopesha uliposema ulimwambia Zinda, hutaki mahusiano ya kimapenzi mpaka shule iishe!” “Wewe ndio unanifanya niwe nasema ndiyo wakati nakusudia kusema hapana!” Geb akacheka sana. “Kweli Geb! Wewe ndio unanichanganya na kunifanya nishindwe kujielewa! Na ninajua sana, kuwa unajua.” “Sijui bwana!” “Unajua sana Geb. Wewe huwezi kuwa unasikia mwenzio amekataliwa jambo hilohilo, eti na wewe unaomba jambo hilohilo, tena siku hiyohiyo! Ndio nini sasa?” Geb alizidi kucheka.

“Mimi nilikuwa na mpango na wewe kwa muda mrefu. Zinda yeye alikutamani tu. Kila alipokuwa akikuona, anakumezea mate. Kuna siku mpaka James alimpiga ngumi. Akamwambia aache kukuelezea mbele yake.” “Uwiii! Alikuwa akinielezeaje?” “Maumbile yako.” “Geb wewe!? Kwamba yamefanyaje!?” “Siwezi kukwambia Nanaa. Ila ujue yeye alikutamani, mimi nilikupenda hata kabla sijajua kuwa una kiuno chembamba, matiti mazuri hivi! Dimpozi,..” “Bwana acha kusema hivyo Geb! Nitavaa nguo sasa hivi.” “Hutaki tena kuoga?” Nanaa akacheka, akakimbilia bafuni.

Jumamosi.

Kitu cha kwanza Nanaa alichohakikisha asubuhi mara baada ya kuamka ni kwenda mgahawani na kupata kifungua kinywa cha nguvu. Alimbembeleza Geb mpaka akakubali kula mtori na chapati. Alilalamikia hiki na kile, lakini Nanaa alihakikisha anakula ndipo wakatoka na kuanza kazi. Walizunguka sehemu chache tu, Geb akiangalia ukusanywaji na upakiwaji wa huo mchele. Nanaa alishangaa vile alivyoweza kukusanya mchele kwa bei ya chini. Akauliza bei anayokwenda kuuza jijini, akashangaa. Ndipo akaamini kweli Geb anayo pesa. 

“Sasa huo wote unawateja wa bei hiyo?” “Kasoro mteja mmoja tu. Yeye huwa hanunui. Anachukuaga buree, akijisikia ndio anakulipa.” Nanaa akashangaa. “Ni nani huyo?” “Mama G.” Nanaa alicheka mpaka machozi. “Yaani mama! Kumbe na yeye ni mteja wako!” “Tena anataka yeye ndio awe wa kwanza kushushiwa. Akiwa wa mwisho halipi, anasema wamemchagulia magunia madogo. Au anasema atanilipa mimi. Sasa Grace akawa anamwambia anamuharibia mahesabu. Akawa anamwambia anidai mimi.” Nanaa akawa anazidi kucheka. 

“Sasa wakawa wanakudai?” “Watanidaije, wakati mimi najua magunia yamepakiwa labda 100, yanauzwa kwa bei fulani. Nataka nione vitabu vimeandikwa hivyo na pesa ipo benki. Wananidai, kwani mimi ndio nimechukua?” Nanaa alizidi kucheka nakuuliza. “Sasa Grace akawa anafanyaje?” “Akawa anamlipia. Nilipojua, ndio ikabidi kila nikinunua ya kwangu 100, nahakikisha ya kwake 5 au 10 yapo pembeni. Inategemea ana nafasi ya kiasi gani huko kwenye stoo yake. Tena yeye anatengeneza faida kubwa kuliko mimi. Kwa kuwa yeye akiyapokea, ana kijana wake anamfungia kwa kilo 10 na mifuko mingine ya kilo 5 mpaka kilo 20. Anauza. Kwa hiyo anapata faida zaidi. Usimuone vile. Anapesa kweli mama. Na anaijua biashara kweli.” Nanaa akacheka. 

“Yaani mama! Kwa muonekano anaonekana ametulia! Yupo kimyaa kama haongei sana. Lakini akianza, utacheka mpaka mbavu zikuume. Tena ngoja nimpigie simu.” “Wakati unazungumza naye, ngoja na mimi nimalizane na huyu dereva. Awahi kuondoka. Sipendi safari za usiku.” “Sawa.” Geb akamwendea dereva, Nanaa akaanza kuongea na Mama G. 

Dereva alirudi Dar na mzigo, Geb na Nanaa wakarudi hotelini. Ilikuwa hoteli nzuri, imetulia. Walilala usiku huo wa kuamkia siku ya jumapili.  Waliitumia siku hiyo hapo chumbani wakiagiza vyakula na kufanya mapenzi, kulala kidogo, kula, mapenzi ya utulivu,  mpaka kesho yake tena siku ya jumatatu, asubuhi sana, ndipo waliporudi jijini.

Baada Ya Safari Ya Moro.

Jumatatu.

Geb alimshusha Nanaa ofisini kwake, na yeye akawahi kazini kwake. Siku hiyo pakawa kimya. Alimtumia ujumbe mfupi tu muda wa mchana, akamwambia bado anampenda, ila ametingwa sana. Asiondoke na Grace, amsubirie yeye pale ofisini atakwenda kumchukua. Nanaa akabaki pale ofisini akifanya kazi za ofisi na kumalizia ripoti yake kwa utulivu. Ilipotimu saa mbili usiku ndipo Geb alipoingia. “Pole. Nimekuweka sana?” “Ndiyo. Lakini nimepata muda wa kumalizia kazi zangu zote. Unataka kuzipitia?” “Leo nimechoka. Nataka kurudi nyumbani nipumzike. Tutazipitia kesho.” Wakatoka.

Kulikuwa na foleni sana. Mpaka wanafika Tabata wakakuta Mama G, alishakwenda kulala. Nanaa akataka kumuasha. Geb akamzuia. “Kwa nini!?” Nanaa akanong’ona wakiwa nje ya mlango wa Mama G. “Nimechoka. Nataka tukalale.” “Wewe Geb! Tulikubaliana nini?” “Ni leo tu bwana!” “Hapana Geb. Nenda kalale chumbani kwako, na mimi nikalale kwangu.” “Usinifanyie hivyo Nanaa! Kumbuka hata asubuhi ulisema tuwahi kazini?” “Punguza sauti. Watatusikia.” Danny akakohoa. Wote wakabaki wametoa macho. “Mungu wangu!” Nanaa akanong’ona kwa sauti ya chini zaidi. “Watakuwa wametusikia?” Nanaa akauliza. “Sidhani.” Geb akajibu, wakaondoka kwa kunyata pale mlangoni kwa Mama G. 

~~~~~~~~~~~~~~~

Vyumba vyote vilikuwa vipo sehemu moja. Ukifungua mlango wa chumba kimoja, mtu mwingine anaweza akasikia. Chumba cha Geb kilikuwa mwishoni kabisa. Cha mama G na kina Grace viliangaliana, japo vilipishana kidogo tu. Ndipo chumba alichokuwa akilala Nanaa na kingine ambacho hakikuwa kikitumika, viliangaliana. Na ndivyo vilikuwa karibu na jikoni na sebule.

~~~~~~~~~~~~~~~

Geb akaingia chumbani kwake, Nanaa naye kwake. Kwa kuwa alikuwa amechoka, alipojitupa tu kitandani, akapitiwa na usingizi. Nanaa akalala bila habari na kinachoendelea ulimwenguni. Kwa mbali sana akahisi mtu akimpapasa matiti. Akahisi ni ndoto, sababu ya siku zilizopita zilizokuwa zimebeba mahaba ya namna yake. Akatabasamu moyoni, akajigeuza vizuri. Kumbe ndio alikuwa akimgeukia Geb. Akapata busu, hapohapo Geb akahamia kifuani. Nanaa akafurahi sana. “Geb!” Akaita kwa upendo huku akitoka usingizini. “Usingizi umegoma kuja.” Geb alijibu akiwa kwenye matiti ya Nanaa. “Nilishakumiss mwenzio!” Nanaa akaongea kwa sauti ya kulalamika. 

Hawakupoteza muda. Ndani ya nusu saa, kila mmoja alikuwa akihema vyake pembeni ya mwenzie. “Asante. Nimefurahi umekuja.” Geb akambusu. Nanaa akataka kuamka ili akajisafishe, lakini Geb akamvuta kwa nguvu, akamkumbatia na kupotelea usingizini. Akajua alikuwa amechoka. Akajiweka sawa, na yeye akalala vilevile.

~~~~~~~~~~~~~~~

Huo ndio ukawa mchezo wao. Wanaagana na kila mtu kuwa wanaenda kulala. Kila mtu kitandani kwake, lakini usiku Geb ananyata na kuhamia kitandani kwa Nanaa. Akipata bao moja, analala mpaka asubuhi. Nanaa huamka kabla yake kwenda kupika uji na kutengeneza kitafunwa. Geb akipapasa kitandani akigundua ameachwa peke yake, anafungua macho, anaangalia saa, ananyata tena kurudi chumbani kwake kama mtoto mdogo.

Za Mwizi Arobaini.

Ikawa hivyo mpaka siku ya ijumaa kuamkia jumamosi ya siku ya harusi ya Malii, wote walipopitiwa na usingizi. Wakaamka ilishakuwa saa tatu na robo asubuhi, kila mtu ameamka. Mama G, yupo jikoni ndiye anayeandaa kifungua kinywa. Nanaa akakumbuka usiku uliopita Geb alimpeleka ukumbi wa sinema huko Mlimani City. Walipotoka wakati wanakula, Geb alimwambia gauni alilovaa imemkaa vizuri sana haswa kifuani. Imemtamanisha. Kwa hiyo wasiende popote, warudi nyumbani haraka sana. Nanaa alicheka sana.

“Kweli tena Nanaa. Mwenzio hali mbaya!” “Twende kwenye gari nikahakikishe. Kama unanidanganya je!” Walikuwa wameegesha gari mwisho kabisa. Geb akapanda kiti cha dereva, Nanaa akamfuata na kumfungua zipu ya suruali. Baada ya utundu wa muda mrefu, Geb alimwambia yeye hawezi kuridhika mpaka aingie kabisa. “Geb jamani! Na Ice cream yangu? Sijala week nzima hii!” “Kesho tutaenda kununua. Tena wewe mwenyewe umemchokoza huyu jamaa. Hawezi kushuka hivi hivi.” “Sasa tukiwakuta watu pale sebuleni?” “Tutaingilia jikoni. Kwanza mama tulishamuaga tukamwambia na leo tutachelewa kurudi. Hatuwezi kumkuta anatusubiria.” Nanaa akapanda kwenye gari wakarudi nyumbani.

Furaha ya Nanaa iliongezeka walipofika nyumbani wakakuta watu wote wapo vyumbani kwao. Wakanyata tena kama watoto wadogo, wakaingia chumbani kwa Nanaa. Kwa kuwa kesho yake hawakuwa wakienda kazini, Geb alipigisha round kadhaa ndipo wakalala. 

~~~~~~~~~~~~~~~

Nanaa akamfinya Geb, akashituka. “Leo tumebambwa!” Geb akafikiria. Akaangalia saa, ilishakuwa saa tatu na dakika 17 asubuhi. Mwanga wa nje upo mpaka kitandani. Watu wote wapo sebuleni na jikoni. Akavuta pumzi kwa nguvu. Akacheka baada ya kumuona Nanaa amepooza. “Acha uoga wewe!” Akamlaghai Nanaa pale, akajikuta amebahatika kupata cha asubuhi. “Daah! Weekend yangu imeanza vizuri!” Geb akajisifia wakati anatoka kitandani kwa Nanaa. “Naomba punguza sauti Geb! Na utoke kwa tahadhari.” Geb alitoka huku anacheka.

Nanaa akakimbilia bafuni, akaoga, kisha akavaa kwa haraka nakutoka. “Shikamoo mama.” Alisalimia kwa aibu. “Hivi hapa nilikuwa nakusubiria uamke, tutoke.” “Tunaenda wapi?” “Leo harusi ya Malii. Umesahau?” “Nimekumbuka.” “Unayo nguo?” “Mimi sidhani kama nitakwenda mama. Kwanza nikwambie tu ukweli mama yangu. Mwanao mimi, mshamba. Sijawahi hudhuria harusi hata moja, na wala sijui natakiwa kuvaa nini kwenye harusi ya maana kama hiyo! Nitakutia aibu bure huko. Bora nijibakie tu.” Grace akaingia. 

“Usiogope. Tutakuwa wote. Danny atakuwa na Fili siku nzima. Anampeleka kwa kinyozi muda si mrefu. Mimi nitakuwa huru. Tutakusindikiza madukani ukatafute gauni. Tutakusaidia ushauri. Halafu ndio twende saluni.” Nanaa akamwangalia Mama G. “Sasa unaniangalia nini wakati anayekuongelesha ni Grace?” Nanaa akaanza kucheka. “Heri tu umkubalie huyo Grace, maana hapa hutabaki. Lazima twende wote kwenye harusi. Tena leo nitakaa kiti cha nyuma, nione unavyogonganisha magari.” Nanaa akafunga mdomo.

“Mama wewe! Usiseme hivyo!” “Nakuandaa tu. Maana Zinda atakuwepo huko. Na Zinda mwanangu pombe ndio furaha yake. Sijui utamwambia nini, akakuelewa akiwa ashalewa!” Nanaa akacheka akakimbilia chumbani kwake. “Muite na mwenzio mje mpate kifungua kinywa.” “Geb yupo chumbani kwake.” Nanaa akajibu kwa haraka akiwa chumbani kwake kama anayejitetea kitu. “Ooooh!” Mama G akaitikia kwa kejeli, kila mtu akacheka mpaka Danny. 

“Mimi huku sitoki tena.”  Nanaa aliongea akiwa kule kule chumbani kwake. “Basi mimi na Grace tutakuacha.” “Msiniache bwana mama!” “Ndio utoke sasa.” Mlango ukafungulia, Geb akaingia huku akicheka. “Sasa unacheka nini na wewe Geb?” “Hela ya shopping hii hapa. Ununue gauni zuri na viatu vya maana upendeze.” “Asante. Lakini ninazo hela Geb. Nililipwa mshahara. Unakumbuka?” “Nipeni mimi hizo hela.” Wakamsikia Mama G, anaongea akiwa jikoni. “Yaani mama!” “Ndiyo. Nipeni mimi. Maana naona mwenzangu huna shida ya pesa! Wewe unapewa pesa ya kununulia nguo, unakataa! Mtoto wewe wa wapi?” Nanaa akacheka. “Umemsikia mama? Lakini usikatae pesa yangu tu. Wengine mwiko.” Danny akakohoa. 

“Kwani Danny, kikohozi hicho kimeanza lini?” Geb akatoka chumbani kwa Nanaa huku akimuuliza shemeji yake. Kila mtu alikuwa akicheka. “Hiki cha msimu ndugu yangu. Kinakuja na kuondoka.” “Unatumia dawa lakini?” “Nashangaa kinaponaga chenyewe tu!” Geb akacheka akaelekea jikoni alipokuwa mama yake. “Mwanangu cheko limekujaa wakati wote!” Akamchokoza Geb. “Mimi huwa nacheka wakati wote. Shikamoo mama.” “Marahaba.” “Sasa unacheka nini?” Geb akamuuliza mama yake. “Mimi nachekeshwa na yangu. Kwani kucheka dhambi?” Geb akatingisha kichwa kama anayemsikitikia mama yake.

“Nanaa! Njoo unywe chai.” Geb akamwita, akatoka chumbani kwake huku ananyata. Akasogea pale jikoni. Akamkuta mama G, na Geb wamekaa pale pale jikoni. “Nilikuwa namwambia Nanaa, harusi ya leo nakaa nyuma kabisa.” “Nilikusikia mama.” Geb akamuwahi kama asiyetaka aanzishe yale mazungumzo tena. “Ulinisikia kila kitu?” “Ndiyo mama.” “Kwamba Zinda naye atakuwepo?” Kila mtu akaanza kucheka, Nanaa alitamani kutoka, Geb alicheka na kutingisha kichwa.

“Mama mchokozi wewe!” Geb akaongeza. “Mie tena? Naongea tu.” “Mbona hata Danny atakuwepo?” Geb akauliza. “Tena watakuwepo wengi tu. Sio Zinda peke yake.” Geb akaongeza. “Haswaa! Najua. Tena najua sana. Na nina uhakika wale wote waliokuwepo Marangu, wakasikiliza majibu yako juu ya Nanaa baada ya kumvalisha sweta, najua watakuwepo wote. Ila mimi hapa namzungumzia Zinda mwanangu. Aliyeambiwa shule kwanza. Mambo hayachanganywi!” Watu wote walikuwa wanacheka.

“Mama jamani!” Nanaa alilalamika kwa aibu. “Kwani mimi nimekosea wapi?” “Mbona mimi nilishamalizana na Zinda?” “Najua. Na watu wote walimuona alivyopooza baada ya kumalizana naye. Lakini mimi hapa nazungumzia zile sababu zakukataliwa mwanangu Zinda, ndio zinautata. Mtoto ukakataa nyumba na gari!” “Viatu na gauni pia Nanaa alimkatalia best yangu.” Danny akaongeza. “Hivi kulikuwa na bangili vile eeh!?”  Mama G akamuuliza Danny kwa uchokozi tu. “Hapana mama. Bangili na mkufu wa DHAHABU.” Danny na Mama G, wakaendelea kupokezana. Kila mtu alikuwa akicheka, mpaka Grace.

“Mwacheni Nanaa jamani!” “Kwani sisi tunasemaje Grace? Tunachozungumzia hapa ni zile sababu za kukataliwa kwa Zinda. Hizo ndizo zitatoa jasho watu leo ukumbini pale. Labda watu waendelee kuficha.” “Naona havifichiki tena mama.” Danny akadakia. Nanaa na Geb walizidi kucheka huku Nanaa amejifunika uso na sahani na yeye akicheka.

Penzi Likiwepo Mahali, Halitetewi.

 “Lakini mimi nilishajua havifichiki tena tokea Marangu. Ngoja na mimi niseme. Ujue mama, Geb alikuwa amekataziwa kumpa Nanaa lile sweta. Tena alikatazwa kwa maneno mengi makali. Sasa mimi nimekaa na Danny, nashangaa Geb kanyanyuka, kaenda kufuata sweta, akaenda kumvalisha Nanaa mbele ya Liz. Nikamwambia Danny, hapa tayari shilingi imemgeukia Liz, yeye hajui tu. Na usifikiri huyo Nanaa alivalishwa kwa muda mfupi?” “Eeh?” Mama G, akaitika kishabiki bado akiwa jikoni Grace sehemu ya kulia chakula nje ya jikoni. “Muda mrefu haswa, akawa anavalishwa. Tena huku akiongeleshwa taratibu. Si unamjua Geb?” Geb alikuwa akicheka tu huku anatingisha kichwa.

“Mimi nilijua muda tu.” Danny akadakia. “Sema nilikuwa sijui hizi karata Geb atazichangaje! Nilikuwa kimyaa namsubiria nione.” Danny akaendelea na kusogea pale jikoni. “Huyu mtoto, Geb alianza kumfuatilia muda mrefu sana, tokea tupo sekondari. Yaani sasa hivi ndio nakumbuka. Yaani kila James alivyokuwa akizungumzia habari za Nanaa, Geb alikuwa anauliza maswali mengi kweli! Sasa siku hiyo yeye yupo India chuoni, akampigia simu James. Maalumu anamuulizia Nanaa. Tena siku hiyo nilikuwa mimi na James tu. Hakuuliza chochote kwa James ila Nanaa tu. Tena hatukuwa tumewasiliana naye muda mrefu kweli. Sasa alipopiga James akashangaa kweli.” Danny akaendelea.

“Sasa simu ilipoita, James akaniambia ‘namba hii ya India. Geb katukumbuka.’ Na mimi nikajiweka sawa. Nikajua baada ya kuzungumza na James, na mimi nitapata fulsa yakusalimia. Sasa tukashangaa Geb akamuulizia Nanaa tu! Hakutaka stori ndefu. Akakata simu. Tukaangaliana mimi na James, tukanyamaza. Baadaye James akanifuata tena akaniuliza, ‘Hivi Geb alipiga kwa ajili ya Nanaa tu au mimi sikuwa nimeelewa?’ Nikamwambia wewe ndio ulizungumza naye. Basi James akanyamaza, akaondoka.” Danny akaendelea.

“Sasa niliposikia Liz anamwambia Geb anataka amtoe hapa Nanaa, nikajua ndio mwisho wa Liz. Hata Grace nikamwambia wakati tupo Marangu kuwa Liz anafanya kosa ambalo Geb hawezi kuvumilia tena. Grace akaniambia eti Geb ni mvumilivu sana. Hawawezi kuachana na Liz. Nikamwambia kwa sababu nyingine, labda. Lakini sio Nanaa. Grace hakuamini. Nilipomuona Geb hazungumzi lolote tokea Liz anaanza kumnyanyasa Nanaa, nikajua mwisho ndio umefika. Halafu unakumbuka Geb ulimchukulia Liz na yeye sweta, akamfunika na kumkumbatia hivi?” Geb hakumjibu Danny, akabaki anacheka.

“Eti Grace akaniambia nilikosea. Mbona Geb amemletea na Liz sweta na kumkumbatia? Akasisitiza kuwa Geb hawezi kumuacha Liz. Nikamwambia Geb alishamuacha Liz kwa muda mrefu sana tokea Nanaa anahamia kwenye hii nyumba. Nikamkumbusha vile Liz alivyokuwa akimlalamikia Grace mwenyewe kuwa Geb ameacha kumgusa kwa muda mrefu sana. Hata alipokuwa akija kulala hapa ndani, Geb alikuwa hataki kumgusa, anampa sababu zisizoisha. Mara amwambie amechoka, mara tumbo linamuuma. Ilimradi papambazuke, Liz aondoke” Danny akashituka kidogo akakumbuka anaongea mbele ya mkwewe, mama G. “Samahani mama.” “Mimi wala sijasikia.” Mama G, akajidai hajaelewa.

“Basi ndio Grace akakumbuka. Nikamwambia Geb anashindwa kulala na Liz sabab.. Daah! Samahani mama.” Danny akajisahau tena. “Bwana weee, hebu malizia.” “Yaani mama shabiki wewe!” Geb hakuwa akiamini. “Acha nisikie mimi. Endelea Danny.” “Sasa si unajua Liz na yeye ana akili? Unakumbuka siku ya birthday ya Fili, tulikuwa tumekaa, Nanaa anacheza na Fili. Geb alipotea kabisa pale kimawazo. Akabaki akimwangalia Nanaa. Mimi niliona tokea mwanzo. Nikajua tayari. Liz akamshitua. Maana wewe Grace ulitaka akachukue keki. Basi kila ukimstua Geb, jamaa kapotelea kwa Nanaa. Ndio Liz akampiga kidogo begani, tena akamwambia Grace anakuongelesha. Ukachukue keki ndani. Ndio Geb akasimama akaondoka.” Danny alikuwa akikumbuka kimoja baada ya kingine.

“Tena hata Zinda anajua sana kama Geb alikuwa anamfuatilia Nanaa tokea zamani. Kwani tulishamsema Geb. Tukiwa mimi, Malii na Zinda. Tukawa tunakumbushana tokea tupo sekondari vile Geb alivyokuwa anataka kujua habari za Nanaa kila wakati. Zinda akanikumbusha jinsi Geb alivyokuwa makini na hataki mtu amuingilie James akiwa anazungumzia habari za Nanaa. Zinda anajua sana. Sema sasa alipokuja kutokea Nanaa mwenyewe, Zinda akajifanya amesahau, akajidai amechananyikiwa. Lakini huyu mtoto, Geb alianza kumfuatilia tokea hajamuona. Ehe!” Danny akakumbuka kitu kingine. 

“Tena kuna siku mimi na James tuliangaliana kama kukumbushana kitu. Tulikuwa mimi, Malii, Geb, James, Gozi na Zinda. Zinda akawa anamsifia sana Nanaa. Tena kiundani kabisa. Geb alibadilika, mpaka kila mtu alijua. Ndio James akampiga ngumi Zinda akamuonya asimsifie kwa undani vile au kumtamani dada yake mbele yake. Nakumbuka Geb aliondoka kabisa pale. Tena Zinda alitaka amkope Geb pesa, na Geb alijua. Maana alituambia makusudi anampigia simu Geb aje pale tulipokuwepo ili amwazime pesa mpaka mwisho wa mwezi. Hapo alikuwa ameshatuomba sisi wote pale tulimkatalia. Tulimpa majibu yanayofanana. Tukamwambia siku zile mbaya, kila mtu anasubiria mwisho wa mwezi.”

“Ndio akasema ngoja nimpigie Milionea wetu. Yeye hana tarehe mbaya. Siku zote kwake za neema. Ndio akampigia simu Geb. Akampa maneno mengii wee, mpaka Geb akakubali kutufuata pale tulipokuwa. Nakumbuka Geb alipofika tu, Gozi akaanza kutania kuwa wito ule alioitiwa na Zinda sio wa kirafiki, jamaa anataka kumkopa pesa. Zinda akakasirika kuwa anamuharibia. Anataka amwonyeshe kwa Geb kuwa yeye mahusiano yake kwake ni kumchuna tu wakati wao ni marafiki tokea muda mrefu. Wakabishana sana pale mpaka ukataka utokee ugomvi maana Zinda naye akawa anataja matukio aliyoyapata Gozi na kwenda kuomba msaada kwa Geb, tena akawa anamsema Gozi kuwa yeye huwa anajiliza shida kama mtoto wa kike kwa Geb, ili apewe pesa ya bure wakati yeye Zinda huwa anakopa nakurudisha. Ndio Geb akawa kama anawatuliza akasema kabisa hamna shida.” Kila mtu alikuwa akisikiliza.

“Sasa stori zikaendelea pale watu wakawa kama wamesahau ule ugomvi. Si ndio Zinda akaanza sasa mambo ya Nanaa na kumtibua Geb! Geb aliondoka bila kumpatia Zinda ile pesa. Baadaye Zinda akaja kugutuka akasema Geb amesahau, ameondoka bila kumpa pesa. Mimi nilijua kabisa aliamua kumnyima Zinda, sababu alimtamka Nanaa, tena kimapenzi. Geb huwa hasahau.” Geb aliendelea kunywa uji wake. Huku Nanaa akisikiliza kwa makini na sahani yake usoni akichungulia kila anayeongea.

“Unamkumbuka yule ndugu yake wa kiume Malii? Nanaa unamkumbuka?”  Grace akauliza. “Yule alikuja kuomba kazi?” Nanaa akauliza kwa aibu kidogo. “Ewaa! Sasa yule ilikuwa apewe kazi na Geb. Yaani alishaahidiwa kazi na mshahara mzuri tu. Tena Geb alitaka awe msaidizi wangu. Zile kazi ambazo siwezi kufanya, nimtume yeye. Sasa akaharibu pale alipokwenda kwa Geb kusaini makaratasi ya mkataba wa kazi.” “Alifanyaje na yeye?” Mama G akamuuliza Grace.

“Si akaanza kumsifia Nanaa kwa Geb! Eti akamwambia Geb, amekutana na msichana pale anaitwa Nanaa. Amemchanganya kabisa. Akamuuliza Geb kama Nanaa umeolewa au kama unamchumba. Hivi unajua mama, Geb alimnyima kazi kabisa. Akamwambia akiweka sawa mambo, atampigia. Alimnyima kazi hivi hivi, wakati alishaahidi kumuajiri. Sasa mimi nikashangaa, maana nilimsikia akimwambia hata Malii kuwa angempa ndugu yake kazi. Halafu nikashangaa hata Malii mwenyewe hakulalamika! Mimi nikamuuliza Malii mbona mdogo wake hajarudi tena? Malii akaniambia kuwa Geb alimwambia kwa kifupi tu, eti ameziba hilo pengo, haitaji mfanyakazi kwa wakati ule.”

“Nikamuelezea Danny kisa kizima. Maana hatukuwa tumeajiri mtu, lakini Geb anasema tulishaziba pengo! Ndio Danny akaniambia sababu ni Nanaa. Lakini mimi nilikuwa siamini!” Mama G alikuwa akisikiliza kwa makini. “Halafu watu wananisema mimi ndio nina wivu! Geb ndio anaongoza.” Danny akaendelea.

“Siku ile alipomkatalia Liz asiingie chumbani kwake, unajua alimwambia Liz kwa wazi kabisa kuwa hawezi kumfukuza Nanaa. Tena Liz akamuuliza, ‘kwa hiyo unamchagua Nanaa, sio mimi?’ Nikajiweka sawa kusikia jibu. Unajua bila kung’ata maneno Geb alisimama akamwambia Liz, ‘Ndiyo. Nimemchagua Nanaa. Naomba ufunge mlango wakati unaondoka.’ Geb aliingia ndani. Akanipita hapo sebuleni, akaenda chumbani kwa Nanaa. Liz aliondoka hapa analia.” Nanaa akajifunika ile sahani uso mzima. Alifurahi sana, akabaki akicheka tu nyuma ya ile sahani.

“Sasa leo Zinda atakuwepo. Wewe furahia tu hapo.” Mama G akamgeukia Nanaa. “Acha kumuogopesha Nanaa, bwana mama!” Geb akaingilia. “Sababu zake mwenyewe leo ndizo zitamtoa jasho, wala si mimi. Maana watu watashangaa shule haijaisha, yeye yupo kwapani kwa Geb! Bwana leo mimi kiti cha nyuma kabisa.” “Tutakaa wote mama.” Nanaa alifanya wote wacheke. “Akuu! Sitaki fujo mimi. Wewe nenda huko huko. Aliyekwambia usiseme ukweli nani?” “Mimi sipendi mwanaume anayekunywa pombe.”  Nanaa aliongea kwa upole nakufanya wote waanze kucheka upyaa.

“Hayo ndio unayasema leo? Kwa nini hukumwambia mwenyewe?” “Niliona kama nitamuumiza!” “Kwa hiyo angekuwa hanywi pombe ungemkubali?” Danny akamrushia swali la haraka haraka, Nanaa akapandisha mabega kukataa huku amerudisha ile sahani usoni, ameficha uso. Wote wakacheka. “Sasa leo ndio leo. Utayasema yote.” “Sasa mimi sijawahi hata kumpenda jamani!” Walizidi kucheka. “Kwa hiyo umempenda Geb?” Danny akauliza tena. “Mwacheni bwana Nanaa. Njoo ule ukanunue nguo.” Akamsogelea Geb.

“Kwa hiyo umesema hata Geb humpendi?” Danny akazidi kumchokoza. “Mimi sijasema hivyo. Geb ni watofauti.” Nanaa alijibu na kufanya wote wacheke kwa sauti mpaka Nanaa akatoka pale jikoni. “Mimi sili tena bwana.” “Nanaa! Njoo mwanangu.” Mama G akamuita huku akicheka. “Wewe unanichokoza bwana!” Nanaa akajibu akiwa nje ya pale jikoni. “Njoo mwanangu. Siongei tena mpaka umalize kula.” Nanaa akafungua mlango huku amejifunika uso na ile ile sahani. “Njoo mwanangu. Ule, halafu njiani unipe habari za Morogoro.” “Unaona sasa? Mimi siji.” “Njoo bwana!” “Mama wewe mchokozi bwana!” “Basi nanyamaza. Nataka ule kabla yakuondoka. Haya Danny chukua mkeo muondoke. Nataka Nanaa ale.” Wakatoka huku wanacheka.

Maandalizi Ya Harusi Ya Malii.

Walimzungusha Nanaa madukani. Wakahakikisha anapata nguo na viatu vizuri ndipo wakaelekea saluni. Wakiwa wapo saluni Geb akampigia. “Uko wapi? Mbona nimeona Grace amerudi wewe haupo?” “Nipo na mama saluni. Grace aliomba atengenezwe haraka ili awahi ukumbini kuangalia ukumbi ulivyo na kusimamia mambo yote kabla sherehe haijaanza.” “Unakaribia kumaliza? Maana na mimi natakiwa kuwahi kanisani na kina Malii. Lazima wote tusimame pale mbele.” “Unamaanisha kama wasimamizi!?” “Ndiyo.” Geb akajibu, Nanaa akanyamaza. 

“Nanaa!” “Mimi nilijua tutakuwa wote, Geb! Maana nimesikia mama akiongea na Grace kuwa Malii ameomba mama akae mbele kwenye meza ya wazazi. Sasa mimi nitafanyaje?” Nanaa akaongea kwa kulalamika. “Najua tumewekewa viti mbele karibu na maharusi, lakini nitakuwa nakuja tunakaa wote kidogo.” “Au mimi nisije tu.” “Nanaa Please.” “Sasa hata nikija mimi nitakaa na nani Geb? Grace atakuwa na kundi la marafiki zake, wako kwenye kamati kuu yamaandalizi! Watakuwa wanasimamia vitu pale kwenye sherehe. Mimi naomba kubaki Geb. Hata hivyo nimeanza kujisikia vibaya.” “Unajisikiaje?” “Nasikia baridi halafu napata vichomi.” “Nitakuwa na koti la suti. Nitakufunika. Usiwe na wasiwasi.” “Kwa nini nisibaki tu?” “Hapana Nanaa. Nakuhitaji. Naomba usiache kuja.” Nanaa akanyamaza. 

“Basi nitawaambia sitasimamia tena. Nitakuwepo hapa nyumbani nakusubiria twende wote harusini.” “Usifanye hivyo.” “Ni heri nisisimamie niwe na wewe, kuliko nisimamie, halafu najua upo nyumbani peke yako!” Geb akaongea kwa kujali. Ikamgusa Nanaa. “Basi nitakuja. Ila ujue tutachelewa. Kuna foleni kubwa.” “Naomba niahidi utakuja hata kwa kuchelewa tu.” “Nitakuja na mama. Halafu nitatafuta mahali nitakaa. Harusi ikiisha si tutarudi wote nyumbani?” “Nitakuona ukumbini. Umesikia? Usiwe na wasiwasi.” “Haya.” “Mbona sasa hauna raha?” “Nilijua tutakuwa wote wakati wote Geb.” “Nitakuwepo. Nitajitahidi usiwe mpweke. Sawa?” “Sawa.” Wakaagana.

~~~~~~~~~~~~~~~

Walichukua muda mrefu sana saluni. Mama G akajua kabisa hawataweza kuwahi kanisani. Wakaamua kurudi nyumbani wajiandae ndipo waelekee ukumbini na si kanisani tena. Safari ya kurudi tena Tabata ikaanza. Kulikuwa na foleni kubwa sana. Akampigia mwanae Grace kumuuliza. Akamwambia walishatoka kanisani. Maharusi na wasimamizi wao walikwenda kupiga picha, yeye amerudi tena ukumbini kusimamia vyakula na vinywaji. Wakazungumza kidogo wakaagana. 

Waliwahi kujiandaa, hawakuchukua muda mrefu wakatoka tena nyumbani kurudi Mlimani City kwenye sherehe. “Umependeza Nanaa mwanangu.” “Asante mama. Na wewe pia umependeza.” “Mbona sasa huna raha?” “Sikujua kama Geb atasimamia harusi mama! Ujue sijamuona tokea asubuhi!” Mama G, akaanza kucheka mpaka akapaliwa na mate. “Kwa hiyo hapo unahamu naye?” “Usicheke bwana mama. Halafu sijui hata anasimamia na mwanamke gani!” Mama G, alizidi kucheka. 

“Kwa hiyo hapo unalia wivu?” “Wala sio wivu. Lakini nawaza tu.” “Basi na macho yale, huyo mwanamke atakayebahatika kusimama naye sidhani kama atamwachia Geb, leo. Hivi ushamuona akivaaga suti?” Nanaa akapandisha mabega kukataa. “Weee! Basi mate lazima yakutoke. Dume la nguvu.” “Mwaya mama naye! Saa nyingine unakuwa rafiki yangu, saa ingine huwi!” “Sasa hapo mimi nimefanyaje?” “Unanirusha roho!” Mama G, alizidi kucheka. 

Kila akimwangalia Nanaa, alizidi kucheka. Huku akiendesha gari wakielekea ukumbini. “Kumbe na wewe ndio wale wanawake wa hivyo?” “Wakoje?” “Kama wewe hivyo.” “Bwana mama! Tukifika tu nisindikize chooni.” “Mwenzio magoti yananiuma! Kusimama foleni huko kwenye vyoo vya watu wengi sitaweza. Ndio maana nilimaliza haja zangu zote nyumbani.” “Kuanzia jumatatu tunaanza mazoezi.” “Na nani?” Mama G, aliuliza kwa kejeli. “Si na mimi!” “Mmmmh! Na huyo Geb?” Nanaa akaanza kucheka. “Unanidanganya tu mimi. Nitatembea na Fili, mjukuu wangu.” “Na mimi pia mama.” “Kwani jumatatu ni mbali basi. Kesho kutwa tu. Nitakuona.” Wakaendelea kuendesha huku wakizungumza mpaka walipofika Mlimani City sehemu ya kuegesha magari. Mama G akasogeza gari yake karibu kabisa na sehemu ya kuingilia. 

“Mama!” Nanaa akamuita mara walipotulia. “Vipi?” “Sijisikii vizuri mwenzio. Nasikia baridi mpaka ndani ya mifupa. Halafu kama nina vichomi vikali.” “Pole. Lakini hiyo nguo nayo aliyokuchagulia Grace ipo wazi sana! Nilimwambia akasema ndio mitindo yenu ya sasa hivi na ndio umbile lako litaonekana vizuri.” “Sasa cha moto nakipata.” Wakacheka. “Nimebanwa haja ndogo,  mama. Siwezi kuvumilia zaidi” “Basi nenda chooni. Utanikuta hapahapa.” Nanaa akashuka haraka kuwahi maliwatoni. 

Kisicho Riziki, Hakiliki

Wakati Nanaa ameondoka tu, gari la wazazi wa bwana harusi likaingia. Wakaegesha pembeni ya gari ya Mama G. Akawaona wazazi wa Malii. Kwa kuwa walikuwa wakifahamiana, akashuka kwenda kuwasalimia na kuwapongeza. Vikajaa vicheko. Mama Malii na sauti yake yenye lafudhi ya kichaga, utani ukakolea akiwa na mama yake Malii wa mjini. Yaani mama G. Wakataniana, mwishowe wakashikana mikono mpaka ukumbini. Hawajakaa sawa, maharusi nao wakaingia. Kelele, Dj akaongeza mziki waingie kwa kucheza.

Wakati Nanaa anatoka chooni, ndio anaona maharusi wakiingia ukumbini wakiwa na wasimamizi wao. Kina Danny walipendeza sana. Waliingia kwa mtindo wa wasimamizi wa kiume kubeba mkono wa msimamizi mwenzie wa kike kama maharusi. Wasimamizi waliingia mwanzoni ili kwenda mbele kabisa kujipanga na kuwapisha maharusi waingie wao wawili tu, zipatikane picha nzuri. Hajasogea karibu akamuona Zinda ameshika mkono wa dada mwingine na wao wakaingia ukumbini. Baada ya Zinda akamuona kaka yake James ameshika mkono wa mdada mwingine. Akacheka. “Amependeza kaka yangu!” Nanaa alijiambia. Wakapita marafiki wengine, mara Geb na Liz nao wakaingia kwa pamoja. Geb akiwa ameshikilia mkono wa Liz. Nanaa akabaki ametoa macho. Wasimamizi wote wakaingia, wakabaki Malii na mkewe huyo mpya.

Nanaa akasikia Dj akitangaza watu wote sasa wasimame kuwapokea bwana na bibi harusi. Nanaa akamkimbilia Malii na mkewe ili kuwapongeza. Malii naye akashindwa kujizuia, akaona atoe sifa anazostahili Nanaa. “Umependeza sana Nanaa.” “Asante. Hongereni sana. Hata wewe na mkeo mmependeza.” “Asante.” Akatoka mtu kuwaambia sasa waingie. Nanaa akawapisha, wakaingia huku wakicheza. 

~~~~~~~~~~~~~~~

Nanaa akacheka na kutamani kama ingekuwa ni yeye. “Na nani sasa?” Akajiuliza baada ya kukumbuka sura ya Geb na Liz walivyokuwa wameingia kwa kushikana mikono pale ukumbini. Hakika walipendeza na kuvutia. Wivu ukamshika kidogo. Baada ya maharusi kuingia, akaamua kurudi kwenye gari kumuita Mama G, na kumwambia huo ndio wakati muafaka wa kuingia kwa kuwa kila mtu ameshaingia, hakuna fujo.

Alipofika kwenye gari hakumkuta Mama G, na gari ikawa imefungwa. Akakumbuka simu na pochi yake aliviacha huko kwenye gari. Moja kwa moja akajua yule mama alishaingia ukumbini. Akarudi ukumbini kwa haraka ili kuungana nao. Alipofika mlangoni akakutana na walinzi, tena wenye sare. Wakataka kadi ya mwaliko ili aingie. Nanaa hakuwa na kadi. Wakamkatalia kuingia. “Mimi ni kama ndugu.” Nanaa akajitetea. “Dada, naomba utupishe. Ndugu wa maharusi walishaingia hapa wa kwanza!” “Tena wote walikuwa na kadi zao.” Mwezie yule mlinzi akaongeza kwa kumshushua Nanaa. Nanaa akaishiwa nguvu. Hakuwa na kadi wala hakujua kama kuna mambo ya kadi.

Nanaa akasogezwa pembeni. Hakutaka kukaa mbali sana ya mlango akisubiri pengine ataona mtu anayemfahamu amwingize ndani. Masaa mawili yakapita, huku akisikia mziki ndani ukitumbuiza na msema chochote akichekesha watu. Ilipofika saa nne usiku, mbavu zilizidi kumbana. Vichomi navyo vikawa bayana kwenye mbavu. Alikuwa akitetemeka kwa baridi. Alishasimama pale zaidi ya masaa matatu bila msaada. Akaanza kusikia anakosa pumzi. Akatoka pale mlangoni akasogea pembeni kutafuta sehemu ya kukaa. 

Akakaa hapo kama nusu saa, hali yake ikawa sio nzuri. Hakuwahi kuumwa pumu hata mara moja! Lakini akaanza kusikia dalili kama za pumu. Anabanwa, hawezi kupumua vizuri. Akaona ni heri aombe simu ampigie Geb. Akasogea mpaka Bank ya CRDB akakutana na askari anayelinda hapo. Akamuomba simu. Bila shida na vile alivyopendeza akampa simu. “Usitume ujumbe. Piga kabisa. Pesa ipo nyingi tu humo, haina matumizi.” Mlinzi akajitutumua mbele ya mrembo Nanaa. Nanaa akatoa tabasamu kwa shida akijua ni hongo tu hiyo hamna kingine. Akampigia Geb. Simu ikaita mara mbili haikupokelewa. Akaanza kuhisi anabanwa zaidi, mpaka yule mlinzi akasikia jinsi anavyohema vibaya. “Unahitaji msaada wa daktari wa haraka. Hiyo ni pumu. Wenzio wanakufa. Usipuuze.” “Sijawahi kuumwa pumu hata mara moja.” “Basi kivazi hicho!” Yule askari alikejeli. Nanaa akaomba tena simu. Akampa. 

Kwa kuwa alijua Antii yupo maeneo ya karibu, akaona amtafute yeye, amuombe aende akamchukue. Akampigia. “Mbona una hema hivyo?” “Sijui Antii. Nimeanzwa gafla. Najisikia vibaya.” “Uko wapi?” Ndipo ilipomlazimu Nanaa kumuelezea yanayomsibu na kwa nini yupo pale. “Nisaidie Antii. Sijisikii vizuri.” “Hata mimi nakusikia hivyo. Sasa, sasa hivi upo maeneo gani?” “Hapa benki ya CRDB.” Nanaa akajibu kwa shida. “Basi nakuja sasa hivi. Sitakawia.” Akakata simu akamrudishia yule askari. Naye yule askari aliposikia maelezo ya Nanaa, akataka kumsaidia. “Twende nikazungumze na hao walinzi wa hapo harusini, wakusaidie.” Nanaa akaonelea sio wazo baya, japo anajisikia vibaya, lakini aaingie tu aombe msaada kwa Grace au Geb.

Wakaongozana mpaka pale mlangoni. Askari wa benki akajaribu kumuombea Nanaa bila mafanikio huku Nanaa akiendelea kuhema hovyo. Mara Zinda akatoka. “Zinda! Zinda! Naomba msaada?” Zinda akiwa amelewa, akamsogelea Nanaa. “Mbona upo hapa?” “Nimezuiliwa kuingia ndani, mpaka niwe na kadi. Na mimi sina kadi.” “Inamaana upo hapa muda wote!? Halafu mbona unahema hivyo?” “Nina vichomi vikali sana.” Zinda akavua koti lake, akamfunika.  “Ngoja nikajisaidie mara moja. Nakuja tuingie wote.” Nanaa akashukuru, akajiweka pembeni.

Mara akaanza kubanwa zaidi. Hali ya kichefuchefu ikamlemea. Akaona atoke nje kabisa ili apate hewa safi. Alitoka pale akiwa amewaachia maagizo wale walinda mlango wa harusi kuwa Zinda akirudi, wamwambie amsubirie, hatakawia kurudi. Akatoka kwa haraka akiwahi nje, maana alihisi atatapika. 

Raha Yageuka Karaha.

Walipofika tu mlango wa kutokea nje ya mall ya Mlimani City, akakutana na Antii. Hapo hapo akaanza kutapika mbele ya Antii. Kutapika kule na kuhema vibaya, kukamugopesha Antii. Akaomba msaada, Nanaa akaingizwa kwenye gari ya Antii, akaondoa gari kwa haraka ili kumuwahisha hospitali ya taifa ya Muhimbili. Alipofika maeneo ya Morocco, hali ya Nanaa ikazidi kuwa mbaya. Antii akaonelea ampeleke tu TMJ hospital ambapo ni karibu na pale walipokuwa wakati ule badala ya hospitali ya taifa Muhimbili ambako bado kulikuwa na mwendo mrefu kidogo.

Alifikishwa hospitalini hawezi kuhema kabisa. Ikabidi kuwekewa mashine za kusaidia kupumua kwa haraka. Alilalamikia mbavu kumuuma, huku akilia. Antii alijaribu kumtuliza, akapewa huduma ya kwanza kwa haraka, akapewa kitanda hapohapo matibabu yakaendelea.

~~~~~~~~~~~~~~~

Huku nyuma Zinda naye akarudi kutoka chooni, akapitiliza ndani moja kwa moja akiwa hana hata wazo la Nanaa. Watu wakala na kunywa. Wakacheza. Ilikuwa harusi iliyojazwa pombe za kila aina. Watu walikunywa mpaka wakabaki wakiangalia pombe. Kwa kuwa Zinda alikuwa amelewa sana, kila mziki unaopigwa, alisimama kucheza. Iwe ni wakukaribishwa mama au baba wa maharusi, yeye Zinda alitoka kwenye meza yao iliyokuwa mbele kabisa, pembeni ya meza kuu ya maharusi, aliyokuwa amekaa yeye kama msimamizi pamoja na wasimamizi wengine. Basi alikuwa akicheza mpaka mziki uzimwe, ndipo anarudi kukaa.

Kila mtu alikuwa akicheka. Baadaye Danny akamwita pale maharusi walipoambiwa waanze kufungua mziki rasimi. Zinda akasimama yeye wa kwanza. “Hebu njoo Zinda. Acha ujinga. Kwani wewe ndio Malii?” “Acha nifurahie kaka. Maisha yenyewe yako wapi?” Kila mtu pale meza kuu akacheka. Malii akashuka na mkewe, Zinda akaenda kuweka sawa shela ya mke wa Malii. “Asante sana Zinda.” Malii akashukuru wakati akimshika mkewe mkono ili ashuke, wakacheze. “Pamoja kaka.” Zinda akajibu kilevi huku akitaka kuunga tela na yeye akacheze nao. “Njoo Zinda!” Danny akamuwahi. “Si muda wa mziki huu?” Zinda akahoji. “Hapana Zinda. Maharusi kwanza. Njoo ukae.” Zinda akarudi.

Danny akagundua alitoka kwenda msalani akiwa amekamilika. Yaani suti kamili. Lakini akagundua amerudi bila koti! Akajua pombe zilimzidia. Alipofika chooni akavua koti, akaacha huko huko. “We Zinda!” Danny akamwita. “Koti la suti umeacha wapi?” “Nimempa Nanaa. Nahisi amebanwa mbavu. Alikuwa kazuiliwa mlangoni. Mrembo hana kadi, nguo yenyewe kavaa ipo wazi! Upepo unampiga tokea hata maharusi hawajaingia! Yeye yupo mlangoni, masela wamemfanyia ngumu.”  Zinda alijibu kilevi. Lakini wote waliokuwa wamekaa pale mbele walisikia kwani mziki mtulivu waliokuwa wakicheza mahurusi ndio uliokuwa ukisikika tu.

James akaruka kama swala na kuondoka pale mbele. Geb wakaangaliana na Danny, wakajikuta wote wamesimama kwa pamoja, wanakimbilia nje ya ukumbi kama James. Wakaacha waalikwa wengine wakiwashangaa. Kwa kuwa ulikuwa wimbo mtulivu, na ni maharusi tu ndio walikuwa wakicheza, kila mtu alimuona Geb, James na Danny wanakimbilia nje. Grace naye akatoka kujua kulikoni. Akakuta Geb, James na Danny wanawahoji wale walinda mlango. “Si dada hivi, kiuno chembamba?” Askari akauliza. Danny akamtizama Geb. “Yuko wapi?” “Alikuwa hapa tokea watu wanaingia. Lakini sisi tukamkatalia kuingia. Hakuwa na kadi!” “Mmemuona ameelekea wapi?” Geb akauliza. Mara Mama G, naye akatoka. 

“Alikaa sana hapa. Naona ana pumu, sijui! Akaanza kuhema vibaya. Kuna mwenzenu mmoja alitoka, wakazungumza naye. Akamuomba amwingize. Lakini naona Jamaa mwenyewe alikuwa amelewa sana. Akamuacha hapa baada ya kumpa koti. Alikuwa analalamikia vichomi.” “Mungu wangu!” Geb akatoa simu yake. Akakuta missed call kadhaa, akaanza kuzipiga kwani simu ya Nanaa ilikuwa ikiita tu.

Mara akapokea mlinzi wa benki. Baada ya kuulizana kwa muda kila mmoja akisema hamfahamu mwenzake, ndipo wazo likamjia Geb labda Nanaa alimuomba simu. “Kuna mtu yeyote aliyekuomba kutumia simu yako mida hii ya usiku?” Geb akauliza. “Kuna mrembo mmoja hivi. Kiuno chembamba, aliomba kupiga. Alisema amekuja kwenye harusi hapa, lakini nafikiri jamaa aliyekuja naye amemtosa.” James akapokonya simu. “Yuko wapi?” Kaka mtu akauliza. “Alianza kuumwa. Nahisi ni pumu. Alikuwa akihema hovyo kweli! Sijui alipo.” James akawageukia Danny, Grace, Geb na Mama G.

Akacheka kwa uchungu. “Haiwezekani kama mlimleta Nanaa hapa, kisha mkamtelekeza kama mlivyofanya Marangu!” “Subiri kwanza James. Kabla hujakasirika, naomba tukamwangalie nje.” Danny akamuwahi. James akawa wakwanza kutoka. “Kwani mama ilikuaje!?” Grace alimuhoji mama yake kwa sauti yake ya ukimya, lakini yakulalamika. “Mungu wangu!” Ndilo neno aliloweza kusema Mama G. Wakakimbilia nje, lakini hawakumuona. Aliitwa Nanaa kila mahali mpaka vyooni, lakini hakuwepo. Simu yake ilikuwa ikiita tu.

“Naomba mimi nikamwangalie nyumbani.” Mama G, akatoka. Kufika kwenye gari akakuta pochi na simu ya Nanaa. Akarudi kuwaambia wasihangaike kupiga, kwani simu alifungia kwenye gari yake. “Kwani ilikuwaje mama? Si ulikuwa naye?” Grace alihoji tena. Geb na James wakamsogelea mama G, ndipo ikabidi awasimulie, James akiwa ameshabadilika rangi kabisa. Macho yameshakuwa mekundu kama nyanya kwa hasira na hofu. Akang’ata meno ili asiseme tena kitu, akaondoka huku ameweka mikono kichwani. Akaingia kwenye gari yake. Danny akamkimbilia. “Unaenda wapi sasa James? Tulia.” “Naenda kumwangalia kama amerudi nyumbani.” James alijibu na kuwasha gari kuelekea Tabata. Mama G, naye akaondoka. Geb naye akafuata nyuma. Walifika nyumbani, wakakuta mlinzi ndio anamjibu James aliyekwisha kufika pale, kuwa hawajamuona Nanaa. James akapanda kwenye gari kurudi kumtafuta tena palepale Mlimani City.

James, Geb na Danny walizunguka kwenye mahospitali na zahanati za jirani ya pale Mlimani City bila mafanikio. Wakaenda mpaka Mwenge na Sinza wakiuliza kama kuna mtu mwenye jina la Nanaa, aliyefika pale mgonjwa akilalamika vichomi. Lakini hospitali zote na zahanati hawakuwa wamemuona Nanaa.  Nanaa alitafutwa usiku huo bila mafanikio. Mama G na Grace walibaki nyumbani ili kuwepo mtu kama atarudi ajulishe wanao mtafuta. 

~~~~~~~~~~~~~~~

Kutoka kuelezwa upendo mkubwa uliokuwa ukimsubiri wa Geb, mpaka kusahauliwa nje zaidi ya masaa matatu! Ni kweli kunapenzi au ni maneno ya shangamsha genge? Alimuona akiingia na Liz wakiwa wameshikana mkono. Unafikiri Nanaa hatafikiri hiyo ndio sababu yakusahauliwa? Geb ambaye anasifa ya kutosahau, imekuaje amemsahau Nanaa kwa masaa yote hayo tena Nanaa akiwa amemwambia wazi atakwenda hapo kwa ajili yake wala si harusi ya Malii aliyeonyesha tokea mwanzo hataki kuhudhuria harusi hiyo.

Nini kitaendelea? Usikose  muendelezo

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment