Grace kwa
Nana.
Baada
ya muda kidogo akarudi tena. “Umesahau nini?” Nanaa akamuuliza. Akaingia
ofisini hapo, akafunga mlango kwa nyuma. “Nataka kukwambia kitu.” Nanaa
akajiweka sawa. Grace hakuwa muongeaji. Kwa hiyo akitaka kukusemesha kitu,
nilazima utataka kumsikiliza tu. “Mimi ninavyojua. Naweza nikawa sipo sahihi.
Lakini hata mama alinifundisha hivyo. Kuwa ili mahusiano yeyote yafanikiwe,
yanahitaji juhudi za makusudi, za pande zote. Mama aliniambia kuna wakati
inabidi kukana hisia za wakati huo ili kuwepo kwenye mahusiano ya aina yeyote yale.
Hisia zina mtindo wa kudanganya Nanaa. Kuna wakati unaamka upo na furaha sana.
Wakati mwingine hutaki hata mtu akuongeleshe. Na sio kwa kuwa unaumwa au mtu
amekukosea, ni basi tu, hisia zinakuwa hivyo. Zina mtindo wa kubadilika
badilika.” “Sasa unafanyaje?” Nanaa akauliza.
“Hakikisha unajua nini unataka. Nakuanza
kukitendea kazi bila kufuatisha hisia. Ukisoma kwenye bibilia. Kitabu cha {waebrania12:2}, neno linaonyesha vile Yesu
alivyostahimili mateso ya msalaba na aibu, lakini ni kwa sababu tu alijua mwisho,
tokea mwanzo. Au niseme alijua mwisho wa shida yote hiyo ni nini
atapata. Alijua lazima atembee kwenye mapito fulani ili kufikia heshima
aliyonayo sasa na milele. Kama asingevumilia yote yale, inamaana leo asingepata
heshima yote aliyo nayo. Asingewekwa kwenye mkono wa kuume wa Mungu baba. Amepingwa
na anaendelea kupingwa mpaka leo, lakini hajawahi kuchuja. Unafikiri kwa nini?”
Nanaa akatulia.
“Alijua ni nini anataka. Akajua faida zake, ndipo
akakubali kulipa garama. Akatembea kwenye hatua zote alizopitia mpaka kushinda.
Haikuwa rahisi hata kidogo. Unakumbuka kabla ya mateso alilia pale bustanini
akitaka Mungu amsaidie? Aliingiwa na hofu Nanaa. Sio rahisi kama watu
wanavyodhania. Hakuna kitu kizuri ambacho ni rahisi kupata. Zipo garama za
kulipa. Unamuona Yesu jinsi alivyokubali kutembea kwenye hatua za mateso? Mimi
na wewe tungeweza kufikiri kuwa kipindi kile cha mateso makali ndipo kipindi
ambacho Mungu angetakiwa kutembea naye. Au hata kutuma faraja. Lakini Yesu
aliteseka yeye peke yake. Mpaka msalabani. Mbaya zaidi alijua yupo peke yake.
Akamuhoji hata Mungu akiwa msalabani. Akilia ‘Mungu wangu Mungu wangu, mbona
umeniacha!?’ Aliumia. Alisikia
hali ya upweke. Lakini alihakikisha anamaliza.” Nanaa akaanza kutokwa na
machozi.
“Kuna mapito mengine ni yako peke yako Nanaa. Hakuna
mtu wala kiumbe mwingine anaweza kukuelewa unakopitia. Unaweza kuja kujikuta
wakati mwingine upo peke yako maishani. Ukiwa umezungukwa na watu ambao
ungedhani wanatakiwa kukusaidia, lakini wasikusaidie. Lakini utakata tamaa na kutupa
kila kitu chini? Hapana Nanaa! Lazima kuendelea.” Grace akaendelea.
“Pambana bila kuchoka kuhakikisha unapata kile
unachotaka na kujua ni chako. Usikimbie. Na wala usidhani yupo mtu atakusaidia!
Wewe ndio unawajibika kwa Nanaa. Wewe ndio utampa Nanaa kile anachotaka. Na si
vinginevyo. Usikubali kushindwa. Usikubali hisia zikakukosesha vitu vizuri.
Usikubali hisia zikakurudisha au kukushikilia kwa muda mrefu. Umeelewa Nanaa
mdogo wangu?” Nanaa akafuta machozi.
“Nimeelewa, lakini Geb ameniumiza Grace!
Hajanithamini. Amenipuuza mbele ya Rita.” “Mimi
sitaki kujua alichofanya Geb. Nataka kujua ulichofanya wewe. Wewe ulifanya nini
Nanaa?” “Ningefanyaje Grace?” “Kweli Nanaa!? Yaani unatoka na mtu
wako. Anakutana na msichana mwingine, wewe umesimama tu! Haya, mnaondoka pale,
njia nzima upo naye, kimya!? Asubuhi yake ulinitafuta mimi na mama, kwa nini
hukumtafuta Geb kujua kilichoendelea? Mama aliniambia hakuna atakayeweza
kumlinda Danny, ila mimi mwenyewe. Ni kweli Nanaa. Kama kweli unampenda Geb, na
unataka awe wako, ujue unalazimika kumlinda mwenzio. Hakuna atakayekulindia
Geb, ila wewe mwenyewe.” Vikaanza kumuingia Nanaa. Akakumbuka stori
aliyosimuliwa na mama G, kuhusu Danny na Viola. Alijua lakini akamuacha Grace
ashugulike na ndoa yake.
“Mtu anaweza asikwambie hili. Ila mimi nipo kwenye
mahusiano ya ndoa, nakwambia ukweli Nanaa, kwa upande wako ulikosea mdogo
wangu. Mimi sitazungumzia upande wa Geb, kwa kuwa Mungu ameshazungumza naye. Na
amejifunza kivyake. Lakini na wewe Nanaa, umekosea. Na umeshindwa kulinda
kilicho chako. Tokea mwanzo kabisa, umeruhusu hisia za wivu kukufunika mawazo
yako na kushindwa kufikiria kwa haraka. Mimi si muongeaji kama unavyonijua.
Lakini Danny hatoki kitandani kwangu bila kumshika mikono na kumuombea. Tena
namuombea kwa sauti ili ajue kilio changu kwa Mungu. Ndio maana unamuona Danny
yuko vile kama mwehu kwangu.” Nanaa akacheka huku ameinama nakufuta machozi.
“Mama alinifundisha kumlinda mume wangu. Tena
alinikatalia kabisa eti kuja kuanza kuniambia habari za Danny za mtaani.
Akaniambia nikizubaa, wengine watamchukua. Usifikiri hapati vishawishi! Yeye ni
binadamu kama binadamu wengine tu, tena sasa hivi anapesa sana. Wanawake wengi
wazuri na wadogo kuliko mimi wanamtongoza kweli, Danny wangu. Lakini namuombea
Mungu amsaidie avishinde vishawishi na mimi nikijitahidi kwa upande wangu, kwa
kila namna ili tu kumfanya asiingie vishawishini. Umenielewa?” “Nimeelewa
Grace. Asante sana. Nakushukuru. Nilihitaji kusikia hivyo. Asante.” Nanaa
akaona upande mwingine wa Grace. Grace akaondoka.
Kusamehe Ni
Rahisi Kuliko Hasira.
Alimuacha Nanaa akiwaza na kujutia. Akabaki akiendelea
kuweka mambo ya pale ofisini sawa. Alikuwa akifanya kazi, lakini akiendelea
kukusanya taarifa ambazo alijua zingemsaidia kwenye kuandika ripoti yake ya
chuo. Kwa hiyo alifanya vitu viwili kwa wakati mmoja. Akiwa amezama kwenye
kazi, mlango ukafunguliwa. Alikuwa Geb. Nanaa akajiweka sawa. “Pole na kazi.”
“Asante, na wewe.” “Asante.” Geb akavuta kiti akakaa.
“Vipi?” Geb akamuuliza. “Namsubiria dereva. Alikuwa
Kariakoo, amesema kama baada ya nusu saa atakuwa amefika. Anapesa baadhi,
nataka nizipokee kwanza ndipo nifunge mahesabu ya leo.” “Itamsaidia kumtoa
kwenye vishawishi.” Geb akaongeza. “Vipi na wewe? Ulirudi kazini?” Nanaa
akauliza nakumfanya Geb azidi kutulia maana ni kama amebadilika tofauti na
walivyoachana mara ya mwisho alipokuwepo hapo.
“Yeah! Kuna mambo nilitaka kuyaweka sawa. Hii week
sijafanya kazi vizuri. Nimekuwa nusu nusu.” “Pole.” “Asante. Na kesho nataka
kusafiri.” “Unakwenda wapi?” Nanaa akauliza tena. “Morogoro. Kuna kazi ya
kukamilisha siku ya jumamosi.” “Oooh! Ungekuwa unaondoka jioni,
ningekusindikiza.” Geb akatabasamu kama haamini.
“Kweli ningekusindikiza ili usiwe peke yako njiani.”
“Hata hivyo nitaondoka jioni sana, baada ya kutoka kazini.” Nanaa akanyamaza
kwa muda kama anayefikiria. Geb akamsogelea, akamvuta mkono. “Samahani Nanaa.
Naomba usinichukie.” Nanaa akakumbuka maneno ya Grace, akajishusha. “Na mimi
naomba unisamehe Geb. Najua kuna nilipozembea mpaka ukaingia matatizoni.” Geb
hakuamini.
“Asante Nanaa. Nakushukuru sana. Najua ni ngumu
kusahau, lakini nakuhakikishia nimejifunza sana tu. Niamini haitakaa ikatokea
tena.” “Na mimi nakuahidi tena nitakulinda Geb. Nitakuwa mlinzi wako.” Geb
alihisi yupo ndotoni. Hakuamini. “Asante Nanaa. Asante sana.” Maagano hayo
yakasindikizwa na mabusu.
Alivuta kiti chake karibu na Nanaa, akaanza kumbusu.
Akaona yupo mbali zaidi, akamtoa pale kwenye kile kiti, akampakata kwenye kiti
chake. Akamkumbatia huku akinyonya midomo ya Nanaa bila kupumzika. Alimpapasa
kwa kadiri ya uwezo wake huku akinyonya midomo yake kwa nguvu zote. Alimpapasa
kama kutoa hofu ya kuachwa ndani yake mwenyewe Geb. Hakuwa akiamini kama
amepata hiyo nafasi tena. Alifukuzwa masaa machache sana hapo hapo ofisini.
Safari hii anapewa ahadi ya kulindwa! Hakuna jinsi Geb angeachia mwili huo kwa
haraka na nafsi ikaridhika.
Akaendelea kumpapasa kwa nguvu huku akimvutia mwilini
kwake. Tayari hali ya Nanaa ilishabadilika. Alikuwa akitoa mihemo ya huba huku
mikono yote ipo nyuma ya kichwa cha Geb aliyekuwa amempakata. Waliendelea
kupeana mabusu ya haja, bila kuchoka. Mabusu hayo yalisindikizwa na msamaha,
majuto na ahadi ya penzi la kweli kati yao.
Dereva aliingia akakuta wapo katikati ya ile hali. Geb
amempakata Nanaa, huku mikono yake imemshikilia kwa nguvu akinyonya midomo
yake. Nanaa alishituka, akataka kusimama, lakini Geb akamng’ang’ania kama
kumvuta asiondoke. Akambusu kama sekunde 30 mbele ndipo akamuachia huku
akihema. Nanaa akasimama, Geb naye akasimama kwa haraka. Akamvutia tena karibu
yake zaidi, akamkumbatia kwa kupitisha mikono yake yote miwili mwilini kwa
Nanaa. Dereva alishatoka.
Akarudia kumnyonya tena midomo yake huku akimpapasa
kwa uchu. Nanaa alishapotelea hapo mikononi, hajiwezi. Akahamia shingoni kitu
kilichomchanganya zaidi Nanaa na kutamani amalize kila kitu hata kwa chuma mboga ya haraharaka tu. Lakini Geb si wa papara. Jinsi
alivyokuwa akinyonya hiyo shingo yake, kana kwamba anao muda wote ulimwenguni,
asijue ndio anamaliza nguvu zote za Nanaa.
Geb aliendelea tena na tena, akarudi midomoni. Akapata
ulimi kwa muda, kisha akambusu nje ya midomo yake kama mara tatu ndipo akamuachia.
Akabaki amemkumbatia huku anahema mpaka alipotulia na kurudia hali yake. Maana
hata Nanaa alimuona alishakuwa juu sana. Alijaribu kutulia huku amemkumbatia
Nanaa na amefunga macho. Alimsikia akivuta pumzi mara kadhaa na kuzishusha
taratibu. Kisha akamuachia. Geb akatoka, dereva akaingia.
~~~~~~~~~~~
Yule dereva aliweka pesa juu ya meza, akaondoka bila
kusema chochote. Hakuwa amewafumania. Aliwakuta! Na ni kama Geb alitaka
aelewe hivyo, na ni kama alimfikishia ujumbe. Hakuwa akiiba. Nanaa ni wake.
Nanaa hakutegemea. Alijua labda Geb angemuachia kwa haraka sana baada ya yule
dereva kuingia, lakini alionyesha wazi yeye ndio anatakiwa apishe. Kwani
ameingilia. Akajisikia vizuri, akabaki akicheka moyoni kuona Geb anamtangaza ni
wake.
~~~~~~~~~~~
Muda mfupi tu baada ya dereva kutoka, Geb akarudi pale
ofisini. “Twende tukajiandae na safari ya kesho. Nitakuleta kazini kama
kawaida, lakini mizigo yako utaacha kwenye gari. Nikitoka kazini nitakufuata
ndipo tutaelekea Morogoro.” “Sawa. Nisubiri basi nimalizie hapa.” Nanaa
akahesabu zile pesa mbele ya Geb. Akamtajia kiasi alichokuta, kwa kuwa dereva
aliziweka tu akatoka. Kisha akaandika kila kitu, nakufunga mahesabu ya siku
ile. Wakatoka.
~~~~~~~~~~~
Walipopanda tu kwenye gari Nanaa akaita. “Geb!” Geb
akamgeukia. “Kuna kitu nataka kukwambia.” Geb akaogopa kidogo. “Nini tena!?”
“Mwenzio nakupenda.” Nanaa aliongea kwa upole huku midomo ikimcheza kama
anayeongea kwa hofu. “Nakupenda.” Akarudia tena. “Asante Nanaa. Tutapata muda
mzuri sana tukiwa Morogoro.” Hilo ndilo aliloweza kujibu Geb. Aliogopa kuongeza
chochote kwani ahadi zote alizoahidi siku chache zilizopita aliharibu kama
Nanaa alivyomshutumu. Akaamua safari hii iwe ni vitendo tu.
Nanaa akabaki akifikiria. “Vipi? Umebadili mawazo ya
kwenda na mimi?” “Hapana. Nafikiria sehemu ya kubebea vitu vyangu vya
kusafiria. Unakumbuka kile kibegi nilisafiri nacho kwenda Marangu?”
“Nakumbuka.” “Alinipa kaka. Lilichanika na kuharibika zipu. Sina sehemu ya
kuhifadhia vitu vyangu kama tukisafiri kesho.” “Tupite madukani tukaangalie.”
“Lakini naomba tusiende kwenye yale maduka yako Geb. Sina pesa nyingi.” Geb
akacheka.
“Kwanza vuta huo mfuko hapo kwenye kiti cha nyuma. Ni
wako huo.” Nanaa akageuka. Akakuta mfuko mkubwa nyuma ya kiti cha dereva.
Akajaribu kunyanyua. Ulikuwa mzito kidogo. Akaongeza nguvu, akavuta akaupakata
na kuanza kufungua kuangalia ndani. Kwanza akakutana na boksi la simu. Mikono
ikaanza kutetemeka na kutoa jasho. Geb akamuona anatoa mikono ndani ya ule
mfuko akajifuta jasho kwenye gauni lake, kisha akarudisha ndani akanyanyua kile
kiboksi cha simu. Akafungua huku akitetemeka. Akakuta ni simu iPhone iliyokuwa imeingia wakati huo. Mpyaa! Akameza
mate.
Akamwangalia Geb. “Umeipenda?” Akamuuliza. Nanaa
akatingisha kichwa kukubali kwa kuwa maneno yaligoma kutoka. Akabaki na
kigugumizi. Mwishowe akajifunika uso wake kwa viganja viwili. “Angalia
na boksi la chini.” Nanaa hakufungua. Akabaki amejifunika analia kwa furaha.
Geb akaondoka gari.
Baada ya kutulia. Akajifuta machozi, akatoa ile simu.
Akaweka mapajani. Akafungua tena lile boksi. Alijua kwa hakika ni laptop.
Akafungua huku akivuta kamasi. Alijifuta mara kadhaa machozi kwa kutumia mikono
yake, ndipo akaweza kufungua lile boksi ambalo tayari taa za barabarani
zilishamuonyesha picha ya laptop ya Apple MacBook Air nayo ndio ilikuwa toleo jipya la Apple. Nanaa
hakuamini. Akafungua ndani huku machozi yakiendelea kumtoka. Akakutana na
laptop yenyewe ikiwa na accessories zote. Akafunika kila kitu. Akarudisha
kwenye ule mfuko, akageukia dirishani akaendelea kulia taratibu. Alishindwa
hata kusema asante. Alijua wazi hastaili vitu vyote vile vya thamani. Kwanza
hakuwahi kulipiwa garama kubwa ya kiasi kile. Aliyemuona akihangaika naye ni
James. Tena na yeye alifanya pale alipoweza. Kwa kiwango cha chini sana kwa
majukumu yaliyokuwa yakimkabili. Alijua wazi Geb ametumia milioni ya pesa kwa
kumnunulia vile vitu viwili tu.
Alilia Nanaa, wala asijue wapi wanaenda na wapo wapi
kwa wakati huo. Akahisi wamesimama. “Twende tukaangalie kama tutapata mabegi
mazuri yakusafiria.” Geb akavunja ukimya mara baada ya kuegesha gari yake.
“Usilie bwana Nanaa. Mimi nataka kukuona umefurahi.” Nanaa akainama akajifuta
machozi. Akaweka vile vitu pembeni, akashuka. Geb akamfuata ule upande
aliokuwepo. Akampa busu moja tu la mdomoni.
Akampangusa machozi. “Twende tuingie hapo ndani.
Tunaweza kupata mabegi mazuri.” Nanaa akatingisha kichwa kukubali. Akarudia
kumfuta tena machozi vizuri, akamshika mkono. Wakaingia ndani. Hakuwa ameegesha
gari yake mbali na hapo dukani.
~~~~~~~~~~~
Lilikuwa duka la pochi na mabegi mazuri na yakaonyesha
ni ya thamani kubwa. Nanaa akajua na hapo tena pesa nyingi itamtoka tena Geb.
Akaanza kusoma bei. “Nanaa! Naomba angalia aina ya mabegi unayopenda. Acha
kuangalia bei.” Geb akamsogelea baada ya kuona anahangaika kusoma bei zake.
“Naona hapa ni garama zaidi, Geb. Twende kwengine.” Akamnong’oneza. “Nanaa!”
“Kweli tena.” “Inamaana hakuna set yeyote
uliyopenda hapa? Achilia mbali garama.” Yale mabegi yalikuwa yakiuzwa kwa sets
3 mpaka mengine seti 5. Yaliwekwa kwa pamoja, kuanzia kubwa kabisa, mpaka
kibegi kidogo kabisa chakubebea vitu vidogo vidogo kama vipodozi.
“Niambie ni ipi angalau umependa.” Nanaa akasita.
“Nanaa?” “Sijui!” “Najua unajua lakini unahofia bei. Hivi vitu ni kweli ni vya
garama. Lakini vinadumu muda mrefu. Ukinunua mabegi kama hayo, utakaa nayo kwa
muda mrefu sana bila uhitaji wa mabegi tena. Kuliko kununua kila mwaka mabegi
ya bei ya chini. Sijui umenielewa?” “Nimeelewa.” “Basi muonyeshe huyo kijana,
ni lipi umependa, utanikuta pale mbele.” Nanaa akaanza kuzunguka tena mle
ndani.
Akaona ni heri achukue set ya masanduku. Akapata seti
ya masanduku 5 yenye ukubwa mbali mbali akapenda. Kabla hajachukua akamuita
Geb. “Najua unataka kunisaidia kununua. Lakini naomba nilipie haya hapa,
niliyoyapenda. Ninazo pesa. Halafu kumbuka ulishaninunulia vitu vingi. Ni kama
ulinunua mahitaji yangu yote ya....” Geb akambusu juu ya mdomo mara moja tu, kama
kumtuliza. Nanaa akacheka.
“Naomba kanisubiri hapo nje.” Akatoka huku akicheka.
Geb akamuomba yule kijana amtolee yale masanduku. Akaingia stoo, akatoka na
aina kama ile ya yale masanduku aliyoyapenda Nanaa. Yalikuwa na muundo kama ya
plastiki iliyopakwa rangi ya dhahabu, nzuri sana. Kona zake zilikuwa za chuma.
Ni kweli pesa ilimtoka Geb. Akalipia na kutoka na yale masanduku. Akamkuta
Nanaa ameinama nje ya gari yake.
Akayaingiza nyuma ya gari, akamfungulia mlango. “Sijui
niseme nini Geb!” Nanaa akaanza kulia tena mara walipoingia tu ndani ya gari. “Asante.” “Naomba usifikirie kama unanifilisi au
ndio unaniingiza garama kubwa sana. Naomba huko usifike tafadhali. Wewe furahia
umepata vitu ulivyokuwa ukivihitaji. Ni vyako wala havihusiani na mahusiano
yetu. Hesabu ni kama Mungu amekupa mahitaji yako. Katika ile orodha yako, ni
kama tumemaliza kila kitu. Si ndiyo hivyo?” “Tumenunua kila kitu sasa hivi.
Nakushukuru sana.” “Sasa nashauri usisubiri ikafikia orodha kubwa hivyo. Ukiwa
na shida na kitu chochote kile, tafadhali niambie. Na wala usifikirie mara
mbili. Sawa?” “Nakushukuru Geb.” “Najua.
Lakini umesikia nilichokwambia?” “Ndiyo.”
Nanaa akaitikia na kujifuta tena machozi.
“Lakini naomba unisubiri. Kuna kitu nataka nimnunulie
mama.” “Nanaa!” “Sio pesa nyingi. Nimeona pochi pale ndani. Inamfanania mama
kweli! Itatoshea bibilia yake wakati anaenda kanisani. Nisubiri nakuja sasa
hivi.” Geb akacheka. Nanaa akashuka. Baada ya muda mfupi akarudi na mfuko.
“Twende.” Geb akaondoa gari.
~~~~~~~~~~~
Walipofika nyumbani, Geb akateremka. “Nimekwama Geb.
Nisaidie ili nishuke.” Geb akakimbilia upande aliokuwepo Nanaa. Akafungua
mlango wake. Akainama ili kuangalia mkanda wa gari aliokuwa amejifunga.
Akafungua, Nanaa akamvuta kwa nguvu na kuanza kumbusu yeye huku akimpapasa
nyuma ya shingo yake. Yeye alikuwa amekaa ndani ya gari, Geb amesimama nje.
Akaendelea kunyonya midomo yake kama alivyokuwa akimfanyia Geb bila papara.
Hakuchukua
muda mrefu sana midomoni kwa Geb, akamuachia. “Asante Geb.” Akamshukuru.
“Nakushukuru kwa kila kitu.” Akarudia tena kwa sauti tulivu huku bado amemshikilia.
“Daah! Huu usiku utakuwa mrefu sana kwangu Nanaa.” Nanaa akacheka akiwa
amemuelewa. “Natamani kesho tuwahi kuondoka mapema kidogo. Unafikiri ni sawa?”
“Nitamwambia nini Grace? Nani atapokea pesa?” “Nitamuomba yeye abaki. Danny
ataenda kumfuata mtoto. Nakuhitaji Nanaa. Nataka tukapate muda wa kutosha.
Yaani huwezi amini Nanaa. Muda wote nilipokuwa rumande, nilikuwa nikikuwaza
wewe tu.” Nanaa akamkumbatia.
“Hakika nakupenda Nanaa. Lakini ipo siku utaamini.
Najua sasa hivi ni mapema kuniamini na yale yaliyot..” Nanaa akamuwahi kwa
busu. “Yamepita Geb. Mimi nimejifunza, na wewe umejifunza. Naomba yaishe.” Geb
akarudisha mabusu. Walikaa hapo kwenye gari wakishikana na kunyonyana midomo.
Alipenda vile mikono ya Geb ilivyokuwa ikimkamata kwa nguvu. Hamu ya kuwepo
Morogoro kwa haraka ikamjia. “Nakutamania.” Geb alimsikia Nanaa akiongea
taratibu. “Mwenzio hali mbaya! Hata sijui naingiaje ndani.” “Basi tutoke
tutembee kidogo.” Nanaa akatoa wazo. “Lakini baada ya hii mara ya mwisho.” Geb
akamvuta tena na kuendelea kumpapasa kwa uchu huku akimnyonya bila kuchoka.
Mwishoe wakaachiana. Wakatulia ndipo wakaingia ndani.
~~~~~~~~~~~
Walishakuwa wamekaa hapo nje zaidi ya nusu saa. Na
watu wa ndani walishajua walirudi. Kwani walisikia mlio wa gari ya Geb.
Wakaingia wakiwa wanacheka na wote walionekana wamejawa furaha. Wakamkuta mama
G, Grace na Danny hapo sebuleni. Mama G akaguna. “Sasa mama unaguna nini?”
“Aaah! Nasafisha koo Nanaa, mwanangu. Kwani mimi nimesemaje?” Nanaa akacheka
akainama. “Mbona mmechelewa kurudi? Kwema?” Nanaa akamwangalia Geb kama
anayetaka azungumze yeye.
Geb akaelewa. “Kesho nina safari ya Morogoro. Nitawahi
kutoka kazini. Nilitaka kumwambia Grace kuwa nataka Nanaa anisindikize. Kazi
zake tutamalizia tukirudi jumatatu.” Watu wote wakawageukia. “Upo likizo!?”
Mama yake akauliza. “Tutaondoka Morogoro alfajiri sana. Kwa hiyo nitawahi
kazini.” Safari za Morogoro huwa Geb anafanya kwa siku moja. Anakwenda asubuhi
na kurudi jioni. Tena wakati mwingine hata chakula cha mchana anakuwa anakula
nyumbani. Nanaa akabaki ameinama.
“Hivi ulisema safari hii ni ya wapi tena? Morogoro au
Iringa?” “Ni Morogoro, mama! Naona safari hii nitakuwa na kazi kubwa
itakayonifanya nikae kidogo.” Geb alijibu huku akijua kabisa mama yake
anachokoza tu. “Oooh!” Mama G akaitika kwa
kuwakejeli. Wote wakacheka. “Sasa mama hiyo ‘Oooh’ ya nini hapo?” “Si nimeelewa
kuwa safari hii una kazi itakayokufanya ukae zaidi huko Morogoro. Unaondoka na
Nanaa kuanzia ijumaa mchana mpaka jumatatu asubuhi. Au sijaelewa vizuri?”
Danny, Grace na Nanaa walikuwa wakicheka. Geb alibaki akimtizama mama yake huku
akicheka na kutingisha kichwa.
“Au mama ulitaka nibaki nikusaidie kitu?” Nanaa
akauliza na tabasamu usoni. “Miye huyu!?” “Ndiyo mama. Wewe. Unataka nibaki
nikusaidie kitu?” “Akuuu! Swali hilo ulipaswa uniulize kabla hujamkubalia Geb.
Tuna mipango mingi sana mimi na wewe weekend hii.
Tena mwenyewe ukajidai kuniambia, ‘basi
usiwe na wasiwasi mama, kati ya jumamosi au jumapili tutakamilisha’. Leo
naona mwenzangu umetoka shopping ya safari ya Morogoro! Bwana huyo kakusimamia
pembeni, ndio unajidai kama umenisahau vile. Eti, ‘au mama unataka nibaki nikusaidie kitu?’ Yaani kama vile kujidai
umesahau au hujui! Ili nikukumbushe. Ubaki hapa, nilaumiwe mimi. Akuuu! Wewe
endelea na mipango yenu.” Nanaa alikumbuka akaanza kucheka.
“Basi jumamosi ile ya mwisho wa mwezi mama yangu. Maana
hizi zinazokuja zinamipango na Geb tayari. Ile ya mwisho wa mwezi mpaka
tukamilishe.” “Ile jumamosi ya mwisho wa mwezi ni harusi ya Malii, Nanaa. Na
umenikubalia tunaenda wote.” Danny akaanza kukohoa. “Masikini mwanangu Zinda!”
Watu wote walizidi kucheka. “Mama jamani! Usiseme hivyo!” “Aaah! Namuhurumia tu
Zinda.” “Basi mimi siendi.” “Mama!?” Geb akashituka. “Atakwenda tu. Kwa lazima,
utakwenda. Ushamkubalia Geb huko, ndio leo ujidai kunidanganya eti unamuhurumia
Zinda, huendi na Geb!? Wakati unamkubalia Geb kwenda naye kwenye harusi,
ulisahau ulimkatalia Zinda kwenda naye kwenye sendoff?” Kila mtu alikuwa akicheka.
“Nilisahau mama jamani!” “Kama ulivyosahau miahadi
yetu?” Mama G, akauliza kwa kejeli. “Mwache Nanaa, mama. Atakuwa kasahau.” Geb
akajaribu kutetea. “Na anasahau kweli! Tena anasahau kwa haraka sana. Naona
mimi na mwenzangu Zinda tuandike maumivu.” “Usiwe na wasiwasi mama yangu.
Nikirudi tutakamilisha mipango yetu. Tena mimi naona wala tusisubiri siku za
jumamosi. Hata ijumaa tunaweza kukamilisha tu. Ijumaa ijayo nawahi kutoka,
nakufuata kabisa kazini.” “Unakumbuka ijumaa tulipanga tutoke Nanaa.” Geb
akamnong’oneza, wakasikia.
“Basi
jumapili hii. Wala tusingoje mama yangu. Tutakamilisha usiwe na wasiwasi.”
Nanaa aliongeza kama kumfariji. “Usisahau jumapili hii ndio tunakwenda kule
kwenye mradi wa Antii kutembelea wagonjwa mahospitalini.” Geb akaongeza. “Haya
naomba muondoke. Sitaki kuendelea kudanganywa hapa!” Nanaa akazidi kucheka.
“Tutapanga mambo yetu tukiwa tumetulia. Mimi na wewe
mama yangu!” “Sitaki. Unanidanganya.” “Mimi na wewe mama?” “Mmmh!” “Twende
ndani nikakuonyeshe zawadi niliyokununulia. Nililipwa mshahara na bosi wangu
Grace. Twende.” “Ndio umeninunulia zawadi ya kunipoza?” “Mimi na wewe
hatukosanagi mama yangu. Haya ni mapenzi tu kwako.” Nanaa aliongea huku
anapitiliza chumbani kwa Mama G. “Njoo basi.” “Nakuja. Wewe si unajua nyanyuka
yenyewe mpaka niagane na nyonga?” Walimsikia Nanaa akicheka huko koridoni.
Maandalizi Ya Safari Ya Jiji Kasoro Bahari.
Aliamka asubuhi akaandaa kila kitu. Geb akatoka
chumbani akiwa amechangamka, kila mtu alijua anafuraha. Akala, wakati Nanaa
anajiandaa. Alijaza vitu vipya vitupu ndani ya sanduku hilo jipya na la
thamani. Nanaa huyu sio Nanaa wa siku chache zilizopita. Kila kitu chake
kilinukia pesa. Yeye mwenyewe alikuwa anasikia raha kupanga vitu vyake humo
ndani ya hilo sanduku. Kuanzia nguo za ndani mpaka za usiku za kulalia zilikuwa
mpya na za thamani. Bado alikuwa amevaa mkufu wake wa dhahabu aliokuwa amepewa
na mama G.
Wakaondoka kuelekea kazini siku hiyo ya ijumaa. Lakini
walishaweka mizigo yao kabisa kwenye gari. Kwa makubaliano wapite moja kwa
moja, wasirudi tena nyumbani mpaka jumatatu jioni wakitoka kazini. Hilo Nanaa
akaliafiki bila shida. Hata yeye alitaka muda wa faragha na Geb. Mwanaume
aliyemsubiri kwa hamu, na kwa muda mrefu tu huku akimuwazia Liz alivyokuwa
akimfaidi chumba kinachofuata.
Ilipofika saa tisa mchana, akamsikia Geb ofisini kwa
Grace akisalimia. Wakaongea kidogo na dada yake ndipo akaingia ofisini kwake.
Akarudishia mlango akamsogelea pale kwenye kiti na kuanza kumbusu huku
amemuinamia. Nanaa alinyanyua mkono wake wa kulia mpaka sikioni kwa Geb. Mabusu
yakaendelea huku akichezea sikio la Geb.
Grace akaingia, akakuta bado wanakiss. Nanaa
alitegemea kuona Geb anakurupuka kumuachia. Lakini wapi. Yeye alishashusha
mkono kwa haraka sana, lakini Geb aliendelea kidogo. Akabusu tena mara kadhaa
nje ya mdomo ndipo akamgeukia dada yake aliyekuwa anataka kutoka. “Naomba saini
yako ya pili kabla hujaondoka.” “Ni pesa ya nini?” Geb akauliza kana kwamba
hakuwa amefumaniwa pale. Akapokea ile hundi, akaanza kuisoma.
“Dereva wa lori la Lushoto, ameomba afanye matengenezo
madogo, kabla ya kuondoka kesho kutwa. Anasema itamuhakikishia kurudi kwa
haraka bila kuharibikiwa njiani.” Grace akajibu. Nanaa alikuwa ameinamia
kompyuta yake, akiona aibu kwa Grace.
Geb akasaini na kumrudishia Grace, kisha akamgeukia
Nanaa, “Upo tayari twende?” Nanaa akatingisha kichwa kukubali. Grace akasoma
ile hundi akatoka. “Usingenibusu hapa.” “Kwa nini!?” Geb akauliza. “Hili ni
eneo la kazi Geb. Hawa ni wafanyakazi wako. Nimekuta ukiwa na sifa nzuri sana
hapa. Wanakuheshimu. Sasa huku kutufumania kila mara!” “Hatujawahi kufumaniwa
Nanaa. Wananikuta nakubusu wewe. Hawajawahi kunikuta nikimbusu mwanamke
mwingine yeyote hapa kazini, wewe ndio wa kwanza. Wewe sio mke wa mtu, ni
wangu. Ndio vizuri wajue na wakuheshimu.” “Geb!?” Nanaa akamshangaa lakini kafurahia
moyoni. Akaanza kujifikiria vile watu wengine pale watakavyokuwa wakimchukulia
yeye kama mpenzi wa mmiliki wa kampuni! Akacheka moyoni.
“Kwanza
Grace amekatisha. Nilikuwa nasikia raha ya kukunwa sikio.” Nanaa akacheka na
kujificha uso. “Usiseme hivyo bwana! Ujue mwenzio Grace naheshimiana naye sana?
Sasa aje akute naleta mapenzi kazini!” “Twende bwana. Mwenzio nimefanya kazi
zangu kwa haraka ili nikuwahi wewe, tukapate muda wakutosha Morogoro.” Nanaa
akacheka kwa aibu kidogo, akasimama.
Geb akamshika mkono mpaka ofisini kwa Grace. “Bosi,
naomba nimchukue Nanaa, tuwahi safari.” “Nyinyi nendeni tu. Muwe na safari
njema na Mungu awajalie wakati mtulivu.” Nanaa hakuamini. “Asante Grace.”
Alijikuta akiropoka shukurani yake. Wakatoka. “Si nilikwambia usimuogope
Grace?” “Nimefurahi mwenzio. Nilikuwa naogopa.” Grace aliwasikia wakiongea
wakati wanatoka nje. Akacheka moyoni. “Nanaa
bado mdogo!” Akajisemea mwenyewe wakati akiendelea na kazi.
~~~~~~~~~~~
Usipitwe Na Makubwa Ya Mji Kasoro Bahari.
0 Comments:
Post a Comment