Kisha akajikaza, akarudi pale sebuleni na kuuliza. “Maana
yake nini?” Liz akauliza tena. “Hamna maana nyingine isipokuwa hiyo
tu. Sidhani kama huko ni sehemu salama kwako na vitu vyako vya thamani.
Vinaweza kupotea wakati wowote ule. Hii nyumba haiishi wageni, na Fili naye
ndio naona anazidi utundu. Anaingia kila chumba siku hizi. Sitaki uingie huko,
upoteze vitu vyako, uanzishe kelele nyingine zitakazo haribu amani ya humu
ndani.” Kila mtu alimshangaa Geb, aliyezoeleka kuwa ni mkimya na mvumilivu
lakini siku hiyo anaongea!
Liz akabaki amesimama. “Karibu hapa kwenye
makochi.” Geb akaendelea kwa sauti iliyotulia tu kana kwamba hamna baya
linaloendelea. Kumbe anatoa maamuzi mazito ambayo hata mama yake alitamani
kumuona akiyafanya kwa muda mrefu sana. Liz akamwangalia mmoja baada ya
mwingine, akajiweka sawa. “Naomba twende chumbani tukazungumze.” Liz
akarudia. “Sio chumbani kwangu. Kama unataka kuzungumza na mimi karibu
ukae hapa kwenye makochi, tuongee.” “Ni mazungumzo yanayotuhusu mimi na wewe,
sitaki watu wengine wasikie!” Liz akaongeza. “Basi tutoke
nje.” Geb akasimama.
“Kwa nini tusizungumzie chumbani?” Msichana
huyo aliyezoea kuzungumza kama kwa amri, na watu kutekeleza tena kwa
haraka, akaendelea kusisitiza. “Liz! Najua you are very smart.
Huhitaji mimi nirudie jambo mara mbili. Kama kweli unataka kuzungumza na mimi,
tutoke nje. Lakini si vinginevyo.” “Kwa maana nyingine ni kwamba hutaki kuniona
tena chumbani kwako?” Geb akabaki akimwangalia. “Geb?” Liz akamuita
akitaka ajibu swali lake. “Tunaweza kuzungumza hapo nje?” Geb
akamuomba kiustaarabu. “Kuna mbu.” “Nyumba yangu haina mbu. Na imetoka kufanyiwa
famigation/kupulizwa dawa kuzunguka nyumba nzima hata siku tano hazijaisha!
Hata hivyo, hatutatoka nje kabisa. Tunakaa hapo barazani kulipozungushiwa vioo
na wavu. Hamna mbu. Ukiona kuna mbu, tutahamia kwenye gari.” “Yote hayo ni
kunifukuza chumbani kwako tu?” Geb hakujibu tena, akatoka nje, Liz
akamfuata.
~~~~~~~~~~~~~
“Mbona sikuelewi wewe Geb!?” Walimsikia Liz
akiuliza kwa ukali. “Uliza jambo lolote nitakusaidia
kukuelewesha.” Geb akasikika akiwa ametulia. “Kwa nini hutaki niingie
chumbani kwako?” “Nimekupa sababu, Liz. Kama hujaridhika nayo, basi hiyo ni
kitu kingine. Lakini nilisha kujibu.” “Unamaanisha nini?” “Hata hilo swali pia
nilishakujibu.” “Naulizia juu ya mahusiano yetu ndio yanakuwaje?”
“Unakumbuka masharti uliyokuwa umenipa mara ya mwisho tulipokuwa wote
Marangu? Na ukasema bila hivyo, wewe huwezi kuendelea na mimi.
Unakumbuka?” Liz akanyamaza.
Nanaa akanyanyuka kimya kimya akaenda chumbani
kwake. “Jamani usiku mwema. Na mimi naenda kupumzika.” Mama G, naye
akaaga. Akasimama. “Usiku mwema mama.” “Na wewe Danny mwanangu.” “Nakuja
chumbani kwako mama. Ngoja nikamlaze mtoto kwanza.” Grace naye
akasimama. “Ukitoka chumbani kwa mama, uniambie basi nije
tulale.” Danny akamuwahi mkewe. “Sawa.” Grace akaingia chumbani
kwake, wakamuacha pale Danny peke yake akiwasikiliza Geb na Liz wakiongea hapo
nje.
Penzi Kama Lipo, Lipo Tu!
Nanaa
alipanda kitandani, akashangaa kitu kimemshika kooni. Machozi yakaanza kumtoka.
Aliendelea kulia taratibu huku ameficha uso kwenye mto, wala asijue ni nini
kinachomliza. Baada ya muda mfupi tu akasikia mlango unafunguliwa bila hodi.
Geb akaenda kukaa kitandani kwake. “Hivi yameshapita masaa mangapi tokea
uniahidi utakuwa mlinzi wangu, tena!?” Akamgeuza vizuri. Akaweka kichwa
cha Nanaa kwenye mapaja yake. “Eti Nanaa?” Nanaa akajifunika uso na
kuendelea kulia huku amemlalia Geb. “Sasa kama mlinzi wangu unakimbia,
nani ananilinda tena?” Geb akauliza kwa utulivu, huku akimtoa mikono usoni
na kumpangusa machozi.
“Eti Nanaa? Yaani mlinzi unakimbia! Unafungua
mlango, unaacha mali yako nje, wewe unakuja kujificha ndani!” Akaendelea
kumpangusa machozi. “Itabidi mlinzi wangu nimpeleke chuoni kwanza.
Ukafundishwe ujasiri, kujiamini, na upandiwe roho ya umiliki. Lasivyo
nimeshaona sipo salama kabisa.” “Sijui mipaka
yangu Geb.” Nanaa akajibu kwa upole huku akilia.
“Unapolinda mali yako, kunakuwa na mipaka
kweli?” Geb akainama na kumbusu midomo yake. Mwili mzima wa Nanaa ulipatwa
na msisimko. Geb alikuwa akifikisha ujumbe au jibu ambalo Nanaa
alilisubiri kwa muda mrefu sana. Kwa upande wa wivu:- kila anapomuona
Liz anaingia pale ndani na kulala na Geb usiku kucha au labda mchana tu. Au
anapoweza kumtawala Geb. Au Geb anapomuweka yeye Liz mbele, na yeye kumlazimu
kusubiri. Kwa upande wa uvumilivu :- bila kujali hisia zake.
Akimuhudumia Geb bila kuchoka, hata kama Liz yupo amelala kitandani kwa Geb.
Bado Nanaa aliweza kuvumilia maumivu, akamuhudumia Geb. Akitaka asirudi
kulala bila kula kwenye kitanda anachojua yupo Liz kwa wakati huo, anamsubiria
Geb. Bado Nanaa alivumilia huku akiumizwa na wivu.
Akamtoa pale kwenye mapaja yake, akamkumbati
vizuri kiwili wili chake, akamnyanyua juu kidogo, na kundelea kumbusu taratibu.
Nanaa alikunja miguu vizuri, kama kujiweka sawa asiharibu au kukatisha lile
busu. Alinyonya midomo ya Nanaa taratibu bila haraka, huku amemkumbatia.
Machozi ya furaha yalikuwa yakimtoka Nanaa, akatamani Geb asimuachie. Zilikuwa
hisia za namna yake. Furaha aliyokuwa akijisikia, hakuna jinsi angeeleza mtu
akamuelewa. Geb alimrudisha mapajani kwake, akabaki akimwangalia kwa macho yake
mazuri na matulivu. Nanaa akabaki aking’ata midomo yake huku akijaribu
kukwepesha macho.
Geb akamfuta machozi tena. “Niliogopa, Geb!” “Hutakiwi
kuogopa. Jipe muda, kila kitu kitakuwa sawa.” “Unafikiri
hivyo?” Nanaa akauliza kwa upole huku akikubali kuyaangalia macho ya Geb
yaliyoweza kuyeyusha chochote kinachomkera rohoni, nakumfanya
aseme ‘ndiyo’ hata sehemu alikusudia na kupanga kusema ‘hapana’.
“Nina uhakika.” Geb akajibu, akainama na kuendelea kumbusu.
Alimbusu kwa muda mrefu sana bila kuchoka.
Alinyonya midomo yake ya nje kwa zamu na
taratibu, huku akitaka Nanaa amwachie anyonye na ulimi. Mwanzoni Nanaa hakuwa
ameelewa. Geb aliendelea kutafuta huo ulimi mpaka akaupata. Alitoa pumzi ya
kufurahia na kuupokea. Akaanza kunyonya ulimi wa Nanaa taratibu huku
amemkumbatia. Alifanya utundu usioendana na muonekano wake wa nje hata kidogo.
Nanaa hakuwahi kupata mabusu ya namna ile. Geb hakuonyesha haraka kwa kile
anachokifanya. Alionekana ametulia na akifurahia anachokifanya. Mara kadhaa
alimuachia na kumtizama kidogo, kisha akarudia kumbusu. Kama asiyeamini kama
amemshika yeye Nanaa.
Baada ya muda akamrudisha kwenye
mto. “Asante.” Nanaa akashukuru huku amejawa tabasamu la aibu na
furaha machoni, akitamani aendelee. Alishalitamani hilo busu mpaka akalikatia
tamaa. Akajua hatawahi kulipata kamwe maishani. Aandike maumivu tu. Geb akabaki
akimwangalia kwa utulivu. Kama aliyeamkwa na hamu mpya. Akainama tena pale
kwenye mto, akabusu midomo yake mara kadhaa. Kisha akamuachia.
“Naenda kumuangalia mama, halafu nakuja
kukuchukua tukale. Usilale bila kula.” “Bado nimeshiba.” “Basi nitakuletea kitu
kidogo ule, wakati mimi namalizia uji wangu.” “Na mimi nitamalizia kukutoa
mwiba.” Geb akatabasamu, akainama na kumpa busu moja la mdomoni,
akanyanyuka nakutoka.
~~~~~~~~~~~~~
Baada ya muda, akarudi tena. Walikaa kitandani
kwa Nanaa, wakiwa wamekumbatiana na kuendelea kupeana mabusu bila kuridhika.
Walimaliza na kuanza upya. Kila alipomuachia Nanaa, alihisi kama bado kidogo,
au kuna kitu amesahau, alimsogeza na kuanza tena kumbusu. Alirudia tena na
tena, bila kuchoka kama mtu aliyekuwa na kiu naye, kitu kilichomshangaza Nanaa.
Aliona vile ilivyokuwa ngumu kwake kumuachia. Naye Nanaa akatulia kabisa.
Hakuruhusu hata akili zake zimuwaze Liz. Akajiambia atajua baada ya hapo. “Acha
nifurahie kidogo. Sina chakupoteza kwa mwanaume ninayempenda. Sasa hivi ni zamu
yangu. Mengine yatajijibu baadaye.” Nanaa akazidi kupotelea mikononi
mwa Geb huku akitoa mihemo laini yakumuashiria Geb kufurahia.
Mwishoe Nanaa akakumbuka anatakiwa kazini kesho
yake siku ya jumamosi. Alipoweka tu kituo na kutoka midomoni mwake na
kumwangalia. Akarusha swali kwa haraka kabla hawajaendelea. “Kesho tunaenda
kazini saa ngapi?” Nanaa akauliza. Geb akafikiria kidogo. Akaangalia saa
yake ya mkononi. “Nitategesha alarm yakuniamsha saa tatu na nusu
asubuhi.” Geb akajibu na kuendelea. “Naomba kesho na wewe ulale.
Tutakuwa na siku ndefu sana. Usihangaike kuamka asubuhi kwa ajili ya
kupika.” Nanaa akatabasamu. “Huwa usingizi unaniishia mapema. Lakini
kama nitachoka katikati ya siku, nikirudi nyumbani kutoka kazini basi nitakuja
kulala. Kama leo. Nimeweza kulala mchana.” “Kesho usiku nataka
tutoke.” Nanaa akatoa macho akahisi hajaelewa au hajasikia vizuri.
“Unamaanisha tutoke mimi na wewe au na watu
wote?” Nanaa akauliza na wasiwasi usoni. “Kuna mahali nataka nikutoe
usiku. Ni hoteli nzuri. Na wanakuwa na vyakula vizuri sana. Nataka uvae
upendeze.” Nanaa akainama na kujifunika macho asiamini. Geb alijua analia
kwa furaha. Akamkumbatia. “Naamini tutakuwa na wakati mzuri.” “Asante sana
Geb. Nakushukuru.” “Hata mimi nakushukuru Nanaa. Najua umenivumilia sana.
Asante kwa kuendelea kunisubiria.” Wakatulia kwa muda kila mmoja akiwaza
lake. Nanaa mikononi mwa Geb akichezea mkono wake taratibu. Aliupapasa huku
akiwaza. Mara kadhaa Geb aliinama na kumbusu huku akimpapasa bila kuvuka
mipaka, nakurudi kufikiria na yeye.
“Ngoja nikuache upumzike.” Geb
akamuaga. “Usiku mwema.” Nanaa akajibu kwa sauti ya chini iliyotulia
na tabasamu huku akimwangalia Geb. Geb akamgeuza vizuri. Akaweka mto sawa na
kumrudisha kwenye ule mto. Kama aliyetamani kumuachia lakini bado kuna kitu
akahisi hajamaliza sawa sawa. Geb akainama tena. Akamtengeneza vizuri nywele
zake huku akimtizama kwa uchu. Akainama na kuanza kumbusu tena. Safari hii
hakuchukua muda mrefu. Kama aliyejionya kuwa na kiasi. Akajizuia asifike
asikoweza kurudi kwani Nanaa alishatoa mihemo iliyoamsha hisia zote za mapenzi.
Geb akamuachia na kumbusu mara kadhaa juu ya midomo yake, kisha akaondoka huku
na yeye akiwa na hali mbaya zaidi.
~~~~~~~~~~~~~
Nanaa alibaki pale kitandani asiamini kama
amepata mabusu mazito vile. Akabaki akijishika midomo yake huku akicheka. “Oooh
Myyyy!” Nanaa alichekelea. “Geb Magesa amenibusu Nanaa mimi!” Nanaa
alibaki akichekelea pale kitandani asiamini. “Anajua kubusu, si mchezo!
Hii mpya na ngeni.” Nanaa akaendelea kufurahia. Kila akikumbuka
ametoka kukumbatiwa na kupata mabusu mazito vile, alicheka na kutamani Geb
arudi tena, waanze. Akachukia kutengana na Geb kwa usiku ule.
~~~~~~~~~~~~~
Geb kasimama
kiume. Nanaa ameanza kufutwa machozi kwa staili yake. Haamini kama amepata busu
kutoka kwa Geb. Liz alitoa masharti gani? Atakubali Nanaa kumpokonya penzi?
Endelea
kufuatilia.
0 Comments:
Post a Comment