“Iwe mwisho kurudi
kwa huyu mganga, na mganga mwingine yeyote yule kwa ajili ya Jackson Msindai.
Chochote kitakachompata Jackson, sitakusamehe. Unanitangazia vita kwa muda
mrefu sana, lakini nilinyamaza kwa heshima ya binti yenu. Lakini unavuka
mipaka. Nahofia dawa unazomfanyia Jackson, siku moja zinaweza kumpata.” “Wala
hazitampata baba. Hata ahangaike mpaka achoke, hakuna silaha itakayonyanyuka
kinyume yangu, mume wangu na watoto wangu, itafanikiwa mama. Nilimtuma baba
kwako, kuwa, unapigana vita mbaya sana, na wala hushindani na mimi ila Mungu
aliye hai.” Jackson akawa haelewi mkewe ameyajuaje hayo.
“Uhai wangu, watoto wangu
na mume wangu umefichwa ndani ya Kristo Yesu. Si mimi ninayeishi, bali Kristo
ndani yangu. Ndio maana muda wote unahangaika kutuloga mimi na Jack, hufanikiwi
mama. Acha, kwakuwa yupo Simba wa kabila la Yuda, ambaye halali akihakisha
ananiombea kwa Mungu bila kuchoka. Lipo jeshi la malaika hapa kwangu,
wanazunguka mchana na usiku wakifanya makao. Hakuna uchawi utafanikiwa hapa
kwetu. Nakuhakikishia mama, hutakaa ukafanikiwa. Wewe endelea kuhangaika tu,
ila ujue unamaliziwa pesa yako.” “Hana nafasi nyingine ya kujaribu. Huko
alipotolewa jioni hii kwa huyu mganga akiloga, namuonya hapa mbele yako
Sabrina, ili usije kunichukia baadaye binti yangu, isiwahi kurudiwa
tena.” Hapo Mzee Msindai akaweka msisitizo.
“Linapofika swala la
kulinda kina Msindai, huwa sizembei na Tino nimemwambia. Asichanganywe na rangi
ya hawa watoto wawili. Hawa ni wakina Msindai. Hakuna, narudia tena, HAKUNA,
atakayenipokonya. Mlijaribu kwa uchochezi, mlishindwa. Mkaja kisheria, pia mmeshindwa.
Mmehamia kwenye uchawi ndio leo naweka kikomo. Huna nafasi ingine
ya kukosea kwa kina Msindai, mama Sabina. Umezimaliza zote. Kama umeshindwa
kuona hii ndoa ikiendelea, kaa mbali mama. Hii ndoa imeunganishwa na Mungu, kwa
nini mnacheza na mipango ya Mungu!?” Kimya.
“Baba Sabina, kwa muda
wako, mkumbushe mkeo, nimeshaandikisha shitaka kituo cha polisi. Ninao ukiri wa
huyu jamaa. Kupokea pesa kutoka kwa mama Sabina, akitaka kumuangamiza Jackson.
Mengine sitasema. Lakini nataka ujue huku kurudi kwake mkeo hii leo kwa huyu
mganga, ni mtego nilimuwekea ili niweze kumpa nafasi ya mwisho ya kujitoa mwenyewe.
Niliwaambia wamuache, akishindwa kujitoa yeye mwenyewe ndipo nimkamate kama
hivi. Nikawaambia wamwambie huyu jamaa, amtajie mahitaji magumu, na pesa nyingi
akimtaka ayalete ndipo amfanyie uchawi wake. Kwa asilimia nyingi sana,
nilijifariji pengine ataamua kuachana na ubaya wake, atahesabu garama ya kuangamiza
ni kubwa kuliko kuacha mtoto wangu, lakini bado mama Sabina umeng’ang’ania tu!
Umesaka kila kitu kwa garama kubwa sana ili kumpatia mganga amuangamize kijana wangu!
Hiyo ni dhuluma ambayo SIKUBALI.” Sabrina akaumia sana.
“Kuna swali lolote kabla
sijaondoka, ili baadaye kusijekuwa na kutoelewana zadi?” “Mimi nimeelewa mzee
Msindai, na naomba nikuombe radhi kwa yote. Kuanzia kwa Sabina mpaka mama yake.
Kuna ambayo yalikuwa yakiendelea, hata mimi sikuwa nikiyajua, nimekuja
kuyasikia kutoka kwa Tino alipokuwa akizungumza na mimi pamoja na mama Sabina
hapa.” “Hata hayo mazungumzo yenu ninayo.” Baba Sabina akashituka sana kama
wengine wote pale ndani. Sabrina ndio alitamani aridhi ifunguke hapohapo mbele
ya huyo mzee, apotee na hao wazazi wake.
“Kwamba huamini?” Mzee
Msindai akauliza, wakabaki kama mabubu. “Si Tino amewakataa nyinyi na kusema
hataki hawa wajukuu zangu waje kwenu ni bora wakabi kwangu mimi ninayewapigania
kwa upendo lakini si kutaka kujinufaisha nao?” Wakazidi kuogopa. “Hakuna sehemu
ndani ya hii nchi jina la Msindai likatajwa kwa hila, nisisikie. Nina
masikio kila mahali. Kwa hiyo nakuonya mama Sabina. TULIA. Turudishe
mahusiano yale ya kwanza kabisa. Ila hiki unachofanya, ni hatari mno, kwa kuwa
hutataka kuwa vitani na mimi. Ni mbaya mno, kwa kuwa huwa mimi sijui
kushindwa.” Kimya.
“Nimemaliza. Sasa usafiri
wa kuwarudisha Chalinze na Bagamoyo kwa huyu mganga upo. Kwa kuwa mimi ndio
nimewaleta hapa, nyinyi wawili lazima tuondoke wote kasoro baba Sabina
niliyemkuta hapa. Mtakuja kupanga safari ya kurudi hapa kwa wakati wenu,
vinginevyo Sabrina aseme tofauti.” “Mimi nataka kurudishwa kwangu.” Akajibu
mama Sabrina na kumuumiza sana Sabrina. “Basi, maadamu kuna usafiri wa bure,
acha na mimi niende mama. Nyinyi mpumzike.” Akaaga baba Sabina. Sabrina akabaki
ameinama. Baba yake akarudi chumbani, akachukua vitu vyake na kutoka. Mzee
Msindai akabaki wa mwisho kuhakikisha wote wametoka hapo ndani, ndipo na yeye
akaaga na kutoka. Wakabaki Sabrina na mumewe, kimya wote wamepigwa na butwaa.
~~~~~~~~~~~~~~
“Aibu gani hii jamani! Kushikwa
uchawi na baba mkwe!” Mwishoe Sabrina akajikuta akiongea mawazo yake kwa sauti
huku akisimama. Jack naye akasimama kama mshale. “Wewe Sabrina vipi bwana!
Mbona hupati picha kubwa!? Mama yako anataka kuniua!” Sabrina akamwangalia na
kuondoka, akamfuata nyuma. “Sabrina, au wewe hujaelewa vizuri?” “Acha woga
bwana!” “Naachaje kuogopa? Au anataka nife urudi kwa Tino?” “Labda.” Sabrina
akajibu akiendelea kutembea, Jack akamvuta kwa nguvu. Akageuka. “Utaniangusha
bwana Jack!” “Mbona huna wasiwasi na kufa kwangu au unaona bora nife tu!?”
“Hufi bwana Jack acha kupaniki.”
“Kweli Sabrina wewe
hunipendi! Umesikia natafutwa kuuwawa halafu wewe...” “Tulia kwanza bwana Jack,
halafu nifikirie mimi na aibu niliyoingia.” “Sabrina! Kweli unazungumzia aibu
na sio kifo changu!” “Sasa wewe umekufa hapo ulipo?” “Nitakufa.” “Hufi bwana
acha kupaniki. Hakuna uchawi utakuuwa wewe Jack. Tulia.” Sabrina akaingia chumbani,
Jack akamkimbilia.
“Sabrina!” “Jackson
Msindai, nakuhakikishia hakuna uchawi utakuua, tulia bwana. Mbona imani yako
ipo hivyo? Fikiria langu. Baba mkwe amethibitisha aliyokuwa akiyasema mama
Msindai wakati wote.” Jack akafikiria kidogo, akasimama. “Kaa bwana.” “Tuanze
kwanza langu Sabrina, ndio tuje matatizo yako. Wewe ulijua kama mama yako
ananiloga?” “Nimejua jioni hii. Ndicho baba alichokuja kuniambia.” Jack
akashituka sana.
“Sasa mbona wewe huna
wasiwasi!?” “Kwa sababu najua kwa hakika kama lilivyo jina langu kuwa hakuna
silaha itakayoinuka juu yangu mimi, wewe na watoto wetu, ikafanikiwa Jack.
Nina uhakika kwa asilimia zote wala si 100. Tunalindwa sisi kuliko ulinzi
wowote ule unaoujua hapa duniani. Na hata baba nimemwambia asiogope.”
“Unauhakika gani?” “Kwa kuwa kama ulimsikiliza baba kwa kutulia, mama hajaanza
kukuloga leo alipotolewa kwa huyo mganga wake. Na baba amesema ameanza muda tu
tokea Sabina akamatwe. Baba amesema ameuza mali zao nyingi tu akitaka
afanikishe uchawi wake bila mafanikio. Sasa unafikiri ni nani ametulinda mpaka
sasa kama sio ulinzi wa ki Mungu juu yetu?” Jack akatulia.
“Na ndio maana wewe
ulipotoka tu na kuhamia huko kwenye kambi ya shetani, amekuadhibu vibaya sana.”
Jack akamwangalia mkewe. “Kwani wanaume wangapi wanafanya kama wewe na
hawayapati kama yako? Ona ulivyozua balaa kwa ndugu zako na familia nzima? Upo
mtandaoni mpaka leo kwa starehe uliyokubali kupokea kutoka kwa shetani. Alikuwa
akikutafuta bila mafanikio, kwa kuwa ulikuwa ndani ya ulinzi wa ki Mungu. Ulipotoka
tu, akakuonyesha zawadi, na wewe ukapokea kwa haraka sana. Ona anavyokuadhibu
wewe na familia nzima ya Msindai! Phina mwenyewe yupo matatizoni sababu yako.
Shetani hana zawadi ya bure, Jackson. Na alikuwa akikusaka, mpaka wewe mwenyewe
ulipoenda kujisalimisha kwake, akakupokea kwa mikono yote miwili. Ndio maafa
hayo.” Jack akapoa kabisa.
“Turudi kwangu.” “Sasa
wewe unashida gani, kwani wewe ndio umeshikwa na uchawi bwana!? Baba sio
mkurupukaji. Anafanya mambo yake kwa uchunguzi. Anakujua wewe ni nani. Na kwa
taarifa yako tu, kama hujajua, mzee Msindai anakupenda na kukuheshimu sana Sabrina.
Amekubali kunipa nafasi nyingine ya kunitafutia video ya Uswiz, kwa ajili yako.
Kwa hiyo usiwe na wasiwasi. Baba anakujua. Ila ongeza umakini kwenye maamuzi
yako. Kama hujaelewa, umeshakosa mara mbili na amekwambia kupitia mazungumzo
yake na mama yako. Ulipojifungua Brayan uliondoka na watoto bila kuaga wakati
yeye alikuwa akija kukuona kila siku
pale kwa Pendo.” “Na mimi nilielewa pale. Nitakuja kumuomba msamaha.”
“Hilo ni moja na
kubadilisha wajukuu zake majina bila idhini hata yangu!” “Nilishamuomba msamaha
na wewe Jack, mbona kama unataka kuanzisha jambo jingine?” “Ni hilohilo tu. Ulifanya
maamuzi yako bila hata kumshirikisha hata yeye ambaye alionekana yupo upande
wako tokea mwanzo!” “Nilishakupa sababu.” “Ya kuwasogeza watoto kwa Tino, sawa.
Ila mpaka kubadili majina, Brina!” “Sasa wangesafiri vipi au wangetengenezewa
vipi hat…” Akasita. Akafikiria na kuona anyamaze tu ni kama anaharibu zaidi. Akabadilisha
alichotaka kusema.
“Kwako nilishakwambia sababu
Jack. Ulizini, ukaficha mpaka siri yako ilivyojulikana. Ukapotea, nakuja
kukutana na wewe siku mama yako anatangaza kupokea mtoto wa Phina na si wangu
ambao…” “Mimi najua unajua kama ulikosa Sabrina. Hata ukijitetea, unajua ukweli
kutoka ndani ya moyo wako, unaujua ukweli wa mambo ila ukatenda ulichokitenda.
Basi.” Jack akasimama nakutoka.
Sabrina akakaa hapo
akifikiria akajitetea kwa hili na lile mwishoe akaona amfuate tu. Akamkuta
amekaa sebuleni, amejiinamia kama kawaida yake akikasirika au jambo likiwa
halijamuendea sawa huko kichwani mwake. “Sasa umekasirika nini Jack?” “Wewe
hunipendi kama ninavyokupenda mimi Sabrina. Kuna mambo unanifanyia, mimi siwezi
kukufanyia.” “Jackson Msinda! Kweli wewe unaongea hivyo au ni kwa kuwa sasahivi
umevurugwa na taarifa nyingi?” “Mimi nakupenda Brina. Lakini wewe una…” “Kabla
hujaendelea sana, naomba tulia na ufikirie kila neno linalotoka kinywani mwako
Jack. Inawezekana nilipitiliza kwenye kuwatafutia watoto msaada, lakini hata
kama ungekuwa wewe usingefanya tofauti. Mimi nimekataa kufa kijinga, kuacha
watoto wakiteseka wakati wanaweza kupata msaada hata kama sisi hatupo.
Unakumbuka habari za Hezekia yule aliyeandikwa kwenye kitabu cha Isaya mlango
wa 38?” Jack akanyamaza.
“Yule aliyekuwa mfamle wa
Yuda, Jack?” Jack akakunja uso kuashiria bado hajakumbuka vizuri. “Yeye alikuwa
mfamle mzuri sio muovu kama wafamle wengine waliopita kuongoza Yuda. Ninachotaka
kukwambia ni katika swala lake yeye alipougua na kukaribia kufa. Nabii Isaya
alitumwa kwake na Mungu. Unakumbuka ujumbe aliokuwa ametumwa?” Kimya. “Sio atubu.
Mungu hakumtuma Nabii Isaya akamwambie tubu kwa kuwa utakufa,
aliambiwa Bwana anasema hivi, ‘Tengeneza mambo ya
nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona’. Hakupewa ujumbe mwingine
wowote ila huo tu. Ila unakumbuka ndio baadaye akamuomba Mungu kwa uchungu
akimkumbusha mema aliyotenda hapa duniani, ndipo Mungu akamwambia atamuongezea
miaka mingine 15 na kumuokoa kutoka kwa mfamle wa Ashuru, na ahadi ya kuulinda
mji. Ila ninachotaka kusema, kutengeneza mambo ya nyumbani kwetu kabla hatujafa
ni mpango wa Mungu, Jack. Sio kitu kibaya.” Jack akapoa na kurudi kuinama.
“Naomba twende tukalale
Jack.” “Mimi nimekasirika.” “Sasa umekasirika nini!? Nafikiri mimi ndio
natakiwa kukasirika Jackson. Na ukumbuke kesho una kikao kinachosubiriwa majibu
na mzee Msindai. Naomba twende ukalale, uamke mwenye akili safi.” “Unanichanganya
Brina. Tulianza vizuri. Mimi na wewe tu, lakini naona sasahivi tupo wengi
kwenye hii ndoa. Mara Tino awepo, mara umtoe. Sijui baada ya miezi 6 aliyokupa
baba, mtaamua nini! Kama watoto ni wangu au..” “Si umeshasikia watoto ni wa
Msindai!” “Kwa hiyo?” Jack akaendelea kuuliza.
“Kama mimi na wewe
hatupo, basi ni wa Jacinta. Na Junior ameambiwa na wao ni warithi wa mali za
Msindai. Sasa wewe wasiwasi wako ni wa nini? Maana mimi mwenzio sina tena
wasiwasi. Nishajua hata nisipokuwepo, wanangu watakufa matajiri. Mali yote hiyo
ya Msindai!” “Acha kucheka bwana Brina!” “Wewe unataka kujiudhi bure Jack, mume
wangu.” “Ukiniita hivyo ndio inakuwa afadhali.” “Muone!” “Basi twende tukalale
wote, Brina!” “Tangulia. Acha mimi nikanyonyeshe raundi ya mwisho ndio nije
kulala.” “Acha nikusubirie, labda usiku wa leo unaweza kunihurumia, angalau nikalala
na mke wangu, kesho nikaamka akili imetulia kabisa.” Sabrina akamwangalia na
kuondoka. Jack akamfuata mbio.
“Sasa tutakaa hivihivi
mpaka lini, Brina wangu! Hasira haziishi tu ukanitamani mumeo?” “Acha kelele
Jack!” “Sawa, kwani wewe huna hamu na mimi? Mwenzio nakutamani. Nikimuona vile
Brandon anavyokunyonya nakuwa…” “Naomba kanisubirie chumbani Jack!” Jack
akaanza kucheka. “Au tuanzie chumbani ndio ukanyonyeshe wakati mimi nalala kwa
ajili ya kikao kesho?” “Hapana Jack. Mimi mwenzio akili zitakua hazijatulia.”
“Yessss!” Jack akashangilia mpaka akaruka kwa Sabrina kukubali penzi. “Unapiga
kelele Jack! Unataka mpaka watoto wote waamke tuanze tena kazi ya kubembeleza!”
“Hakika watasubiri. Bora hawana njaa, wala hawaumwi, watanisubiri kwa kweli. Na
mimi nakuhitaji! Haaa! Wanakuganda wakati wote mpaka mimi nasahauliwa!” “Haya
naomba nenda basi chumbani.” Jack akaenda chumbani kwa furaha zote.
Alichokiunganisha
Mungu.
H |
ata Sabrina alikuwa na hamu na mumewe. Tokea siku
wanaagana asubuhi ya Sabrina kwenda kufanyiwa upasuaji wa huyo Brandon, hakuwa
amefanya mapenzi na mumewe tena. Akanyonyesha harakaharaka hata kabla mwanae
hajatoa nyonyo mdomoni kuashiria ameshiba, akamrudisha kitandani na kutoka hapo
kwa haraka asije mkuta Jack amelala. Akamkuta anachagua nguo zakuvaa kesho yake
akamdaka. “Acha nioge kwanza. Wewe chagua tai na mengineyo nakuja sasahivi.”
“Nikuulize Brina?” Sabrina akamwangalia wakati akivua nguo. “Nini?” “Kwani na
wewe ulikuwa na hamu na mimi?” “Sana Jack! Kwa nini?” “Mbona sasa siku ile
tulivyotoka kwenye harusi palikuwa na mazingira yote yakufanya mapenzi lakini
ukataka tulale tu? Mimi nikajua hunitaki tena!” “Mambo mengi yalikuwa yakiendelea,
Jack. Akili ilikuwa haijatulia. Lakini bado nakupenda Jack wangu.” “Eti
nimefurahi kusikia hivyo!” Sabrina akacheka na kuingia bafuni.
Ulikuwa usiku wa kukata
na shoka kwa Jack hata Sabrina mwenyewe. Kila mmoja alisikika kutoridhika na
mwenzie kwa haraka kitu kilichowatuliza wote. Kwa Sabrina akafurahi kuona bado
mumewe anamfurahia japo alipita mrembo Phina hapo katikati yao. Na kwa Jack
akafurahia kuona wala Sabrina hamuonei kinyaa kwamba anaona uchafu kwa kuwa
alilala na mwanamke mwingine. Aliyokuwa akimfanyia kabla, hata usiku huo alimfanyia
tena kwa kina na furaha zote. Jinsi alivyombana kwa mdomo, Jack alikaribia kumalizia
mdomoni ila Sabrina akamuwahi na kumkalia kwa haraka akiwa Jack amelala chali
mpaka hiyo safari wakaimaliza.
Na Japokuwa hakuweza
kunyonya matiti ya mkewe na Sabrina kupata starehe ya ulimi wa mumewe kwenye
chuchu zake, lakini aliipata midomo ya mumewe sawia na kufika kileleni akiwa
anasikilizia midomo ya mumewe inavyomnyonya kwa uchu wote kana kwamba anavuta
kitu kitamu. Jack alipita taratibu na kwa haraka akimchezea kwa ulimi huku
ndevu zikiamsha kamasa vilivyo, mpaka alipotulia akiwa anamnyonya vizuri huku
akikipekecha mdomoni mwake kwa ulimi mpaka Sabrina akamalizia safari yake ya
mwisho kwa furaha zote. Walilala kama waliotoka shamba kwa kuchoka kwa penzi la
kukata kiu.
Mbele Ya Kaisari.
A |
subuhi hiyo Jack akaamka jasiri kama simba. Na
hivi mkewe amemsamehe! Huna kosa utakalomkumbusha Jackson ukamuumiza. Alitoka
hapo mapema sana akiwa amependeza vilivyo. Hakuwa amevaa tu koti la suti. Lakini
shati jeupe safi na alifunga tai yake. Tena lilikuwa miongoni mwa mashati
ambayo Sabrina aliyatoa dry cliner. Safi. Linawaka na kung’aa kwa weupe.
Koti alilining’iniza nyuma ya gari akitaka kulivaa wakati akiingia ofisini kwa
bosi wake, kaka yake akiwepo. Njia nzima alikuwa akipiga miluzi.
Saa nne kasoro 10 akapata
simu kutoka kwa sekretari wake kuwa anaitwa ofisini kwa Waziri wa Fedha.
Akatoka akiangalia saa maana alifikiri ingekuwa saa nne kamili. Tokea yupo nje,
akamsikia kaka yake akicheka na Waziri wa Fedha ndani. Sekretari wa Waziri akamwambia
aingie. Ile hali aliyoikuta mle ndani, ikabidi tu atulie na hofu imuishe.
Hakutaka kujikaribisha wala kuingilia, akabaki amesimama. “Naona mzee hataki mchezo!
Ametuma video mapema kweli, nimekutana nayo mlangoni!” Akaongea bosi wake
akimgeuzia kompyuta na yeye aone. Jack akajisogeza karibu. “Naona ni sauti tu
ndio hamna. Lakini kwa sura anaonekana vizuri kabisa. Unaweza kurudisha kuanzia
mwanzo.” Jack hakuwa akiamini jinsi baba yake alivyofanya mambo kwa haraka. Wamezungumza
jana yake tu, asubuhi hiyo video imeshaingia nchini! Akamsogezea laptop yake,
yeye akarudi kuzungumza na Junior wakicheka. Jack akajivutia laptop karibu.
Ya Nchini
Uswiz.
J |
ack akarudisha hiyo video kuanzia mwanzo.
Akaonekana Phina anatoka chumbani kwake. Akaelekea kwenye lift huku
akijitengeneza vizuri. Lift ikamchukua mpaka gorofa aliyokuwepo Jackson Msindai.
Kweli akaonekana amegonga kwa muda. Kisha akaonekana anazungumza akiwa bado
amesimama nje ya mlango uliokuwa bado umefungwa, akasubirishwa kidogo.
Akaonekana anasubiria nje ya mlango huku akitengeneza matiti yake kuyafanya yaonekane
vizuri kwa nje, na kuweka nywele vizuri wakati akisubiria. Bada ya muda Jack
akamfungulia akionekana anachungulia sio kutoka kabisa. Wakazungumza kidogo.
Japokuwa maneno hayakusikika, lakini akaonekana Jack kurudi tena ndani. Hapo
kukawa na kusubiria tena. Phina akaonekana nje ya mlango kuendelea kujiweka
sawa. Akarekebisha matiti yake tena na tena akiyanyanyua juu zaidi. Akayachungulia
mara ya kwanza, akaonekana kutoridhika. Akasogea pembeni ya mlango. Akayapanga tena
mpaka akaridhika ndipo akarudi tena mbele ya mlango. Akaweka sawa nywele zake, akasubiria
tena, ndipo mlango ukafunguliwa. Safari hii Jackson hakuonekana hata
kuchungulia ila Phina akaingia ndani. Mapigo ya moyo ya Jack yakaanza kwenda
kasi. Akatazama muda tokea Phina alipoingia. Akaandika kwenye kikaratasi.
Akabaki pale akisubiria kuona muda aliotoka Phina, kana kwamba hakuwepo huko
nchini Uswiz siku hiyo na sio yeye aliyemfungulia mlango.
~~~~~~~~~~~~~~
0 Comments:
Post a Comment