Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com MAKOSA! – SEHEMU YA 31. - Naomi Simulizi

MAKOSA! – SEHEMU YA 31.

Akamuona anatuma jumbe kadhaa. Akatulia. “Willy?” Akamuita taratibu. “Hivi uliniambia utakwenda kwenye Pikiniki?” “Sina uhakika kwenda huko kisiwani Pendo. Sioni kama kutakuwa salama sana huko mbali na nchi kavu, halafu vijana wote walevi na wavuta bangi watakuwepo huko! Nahisi itakuwa fujo tupu.” “Nilisikia waziri wa starehe wa pale chuoni akisema kutakuwa na ulinzi mkali, na akaonya hata wanaopanga kwenda kulipizana kisasi huko haitakuwa sehemu yake. Wamesema wamelipia ulinzi mzuri. Nahisi kutakuwa salama.” Pendo akaweka ushawishi. “Lakini nivizuri kusikiliza nafsi yako kile inachokwambia. Kweli itakuwa mbali na nchi kavu, hutaki kwenda halafu ukajuta.” Pendo akarudisha macho kwenye simu. Akamuona anaandika tena.

“Ulisema utakuwa na kina Eva?” “Ndio nilikuwa na chat naye hapa. Mpenzi wake ameshanunua tiketi zetu na za marafiki zake pia. Wanafahamiana vizuri na yule waziri wa starehe wa pale chuoni kwetu. Eva alikuwa akiniambia tutakuwa wengi, nisiogope. Maana na mimi niliogopa kwenda huko Mbudya. Niliona ni mbali, halafu wanakwenda wengi mpaka wanafunzi wa Mlimani! Lakini ndio Eva ananiambia hapa wamehakikisha itakuwa salama. Twende, tutakuwa wote Willy na mimi nitakununulia tiketi.” Pendo akaongea kwa kubembeleza. Willy akacheka. “Au kina Kyande hawatakuwepo?” “Naona Kyande ndio alikuwa wakwanza kununua tiketi! Anaimba hiyo safari mpaka kero!” Wakacheka. “Nitaangalia.” Akajibu Willy. Pendo akaelewa anamipango yake mingine. Na yeye akawa mstaarabu tu. “Sawa.” Akaitika na kurudisha mawazo kwenye simu yake.

Pakatulia kwa muda, kila mmoja akifanya lake. Lakini akili na mawazo ya Willy bado yalikuwa kwa Chris na huyo Pendo. “Kesho ulitaka tuondoke hapa saa ngapi?” Pendo akaweka simu chini, akafikiria kidogo. “Nafikiria mimi niwahi kidogo ili nipate muda wakujitayarisha. Nakutana na Chris kwa chakula cha mchana, na nywele zimeloa! Hazifai.” Willy akabaki akimtizama, Pendo akifikiria. “Nafikiri niondoke kama kwenye saa tatu asubuhi. Nipitie saluni kwanza ndipo niende chuo. Au itakuwa mapema sana nitakuamsha?” “Haina shida. Huo sio muda mbaya hata kwangu. Naweza kusogea chuo nikawepo pale nikisubiria mtihani wangu wa mwisho.” “Lakini mimi sitaelekea chuo kwanza Willy! Nitakwenda saluni kwanza, ndipo niende chuo.” Willy akabaki kama hajui tena chakufanya na huyo mrembo.

“Hayo yote ni maandalizi ya kukutana na Chris tu?” Pendo akababaika kidogo. “Huwa Chris anapenda kwenda kula sehemu za hadhi ya juu, Willy. Sitaki nitokee kama ambaye sijitambui.” Willy akanyamaza. “Nafanya kwa ajili yangu pia. Mvua imeharibu nywele zangu, halafu usiku tutatoka wasichana wote wa darasani kwetu. Tuliamua kwenda kupongezana kwa kumaliza mwaka pamoja. Hatujui nani atarudi nani ataendelea. Tumeona tukafunge mwaka wa kwanza pamoja.” “Kwa maana nyingine unayotaka kuniambia kesho ukiamka hapa hutahitaji usafiri wangu?” “Nashukuru, lakini nitatumia daladala au hata taksii mpaka Kinondoni. Kuna dada huwa anatutengeneza nywele vizuri.” “Sawa.” Willy akajibu, Pendo akafikiria kidogo na kuendelea kuandika huku akiperuzi simu yake, Willy akimtizama tu.

                 Baada ya muda, akamuita tena. “Willy, nataka kulala.” “Umeshachoka?” Pendo akacheka taratibu. “Nimezunguka sana leo, karibu jua na joto lote leo limeniishia mwilini.” Pendo akasimama. “Nikupe taulo dogo? Naona nywele bado zinatoa maji. Umelowa.” “Nitashukuru. Nahisi nitalala na taulo kichwani.” “Njoo huku chumbani.” Chumba kilikuwa na kitanda kikubwa tu, kimetandikwa vizuri. Pasafi, pakawaida. Akamtolea taulo. “Geuka.” Pendo hakujua anataka afanye nini, akageuka. Akashangaa anamfuta mgongoni na kwenye nywele. Pendo akacheka. “Una upendo Willy! Asante.” Willy akacheka. “Kweli. Unakumbuka siku ile nilipoangushwa na Wema?” Willy akabaki akimsikiliza. “Ulinifuata chumbani na kuniuliza ninaendeleaje! Unakumbuka?” “Nakumbuka hata hukunikaribisha ndani!” Pendo akashituka sana na kugeuka.

                 “Nilikuwa nimetoka kuoga Willy!” “Na ulikuwa na haraka yakujiandaa ili kumuwahi Chris.” Pendo akabaki ameduaa. “Uliniambia hutanikaribisha ndani kwa kuwa unajiandaa, Chris anakuja kukuchukua.” “Ukisema hivyo inasikika vibaya bwana!” Akalalamika Pendo, Willy akacheka taratibu. “Lakini ndivyo ulivyoniambia.” “Si ulinielewa?” Pendo akauliza kwa upendo. “Si ndio maana niliondoka kwa haraka!” Pendo akafikiria, akashindwa azungumze nini tena juu ya hilo. Akataka kukaa. “Bado una maji. Njoo kwanza.” “Mwenzio nimejisikia vibaya!” “Kwa nini tena?” Willy akauliza huku akicheka. “Naona mimi nilikufukuza kwangu, ona jinsi wewe ulivyonikarimu nyumbani kwako!” Willy akacheka sana.

“Acha kufananisha kihivyo!” “Kweli Willy! Naomba nisamehe bwana. Nilikuwa tayari na miahadi na Chris, na jambo jingine Chris hapendi kuchelewa. Akija, anataka akikupigia kuwa amefika, na wewe utoke. Sikutaka tufike sehemu tuliyokuwa tunakwenda tukiwa tumenuniana.” “Mimi naelewa Pendo. Wala usiwe na wasiwasi. Geuka.” Pendo akageuka, Willy akaendelea kumkausha kichwa. “Hivyo unavyonifanya, nitalala nikiwa nimesimama.” Willy akacheka. “Acha nikutolee nguo nyingine yakubadili.” Akamtolea tisheti nyingine ndogo, akavaa palepale Willy aligeuka pembeni tu. “Nimemaliza. Asante.” “Basi nipe hiyo mbichi.” Akamuongezea blangeti jingine na taulo jingine Willy akatoka.

Baada ya muda akasikia mlango unagongwa. “Karibu Willy.” Akawa amejifunga taulo kichwani. “Unapendeza na kuvutia na kila kitu Pendo!” Pendo akacheka sana. “Kwa hiyo hili taulo kichwani limenipendeza?” “Sana tu! Unautulivu na sura nzuri sana. Kila kitu chako ni kizuri.” Pendo akacheka na kufikiria kidogo kisha akamwimbia, “Asante Willy. Hata wewe ni mzuri.” Willy alicheka mpaka akainama. “Acha utundu Pendo!” “Kwani hujui! Mpaka wanaume wenzio wanakusifia!” “Haiwezekani!” Willy akazidi kucheka. Pendo akapanda kitandani. Radi ikapiga na kufuatiwa na ngurumo. Pendo akakaa kwa haraka. “Usiniambie huwa unaogopa radi?” Pendo akaanza kucheka. “Muulize Eva. Zikianza usiku, asubuhi anaamka nipo kitandani kwake.” Wakacheka.

“Sipendi radi, eti naona zitaingia ndani na kunipasua nikiwa peke yangu hapo kitandani.” “Mkiwa wawili?” “Sina shida. Tena nyumbani ndio wanajua. Siku za mvua nilazima nitalala na Nancy kama yupo nyumbani. Akiwa hayupo, nahamia chumbani kwa msichana wa kazi.” “Haiwezekani Pendo!” “Hali ni mbaya. Mimi naomba tu uje usomee hapa ndio nitalala. Lasivyo nakuja kulala pale kwenye kochi.” Willy akazidi kucheka. “Tulale wote kwenye kochi?” “Kabisa Willy. Katika hilo wala sitafikiria mara mbili. Lasivyo wote tutakesha hapa.” “Basi ngoja nikachukue vitabu vyangu. Sasa utalala kweli na mwanga wa taa?” “Heri mwanga wa taa kuliko radi.” Willy akacheka na kutoka akiwa na furaha vilivyo. Analazimishiwa kulala kitanda kimoja na Pendo! Mungu ampe nini!

Wakati anakusanya vitu vyake ili arudi chumbani alipokuwa amemuacha, akashitukia Pendo ametoka kwa haraka. “Pendo!” “Naona hauji na radi zinaendelea!” Willy akazidi kucheka. “Ndio hali mbaya hivyo!?” “Hapa nitakufuata mpaka chooni. Wewe niambie nikusaidie nini, twende wote ndani.” Willy akaendelea kucheka huku akikusanya vitu vyake. “Nataka kuzima taa.” “Wewe zima tu, mimi nakusubiria hapahapa.” “Gizani!” “Giza ni bora kuliko hizo radi huko chumbani. Wewe twende tu.” Willy akajua hali ni mbaya. Akawasha simu yake, akazima taa zote wakaongozana chumbani huku wakicheka.

“Sasa utanionea huruma hii hali inikute nipo kwa Chris au tupo safarini!” “Kwa nini?” Willy akauliza taratibu. “Sijui nikwambia  nini juu ya Chris! Sijui ni mtu wa namna gani yule kiumbe! Anabadilika badilika kama kinyonga! Ni ngumu kumtabiri. Halafu kama hivi ulivyonifunika hapa vizuri, Chris huwa hawezi. Hawezi mambo ya kushikana shikana. Anasema yeye hakulelewa kimayai, sijui mwenyewe anajielezea vipi! Lakini unaweza kukuta mpo naye, mvua inanyesha na kuna radi. Anajua wazi mwenzie naogopa, kama amekasirika, anaweza asikujali kabisa. Tena kama mpo hotelini, anaweza hata kukuta anatoka. Anakwambia anafuata kitu upande wa baa. Sasa nikiwaga nyumbani kwake, ninakuwa na kazi yakumfuata kila mahali, mpaka najikuta naamka kwenye kochi, kumbe yeye aliniacha hapo kwenye kochi nilipomfuata, akarudi kitandani.” “Kwa nini hakuamshi sasa ili mrudi naye kitandani!?” Willy akashangaa sana. Pendo akafikiria.

“Aaah! Sijui bwana. Sijui yukoje Chris! Lakini akiwa mwema, utafurahia.” Willy akapanda kitandani na yeye. “Kama leo amekuwa mwema mpaka kesho umekubali kutoka naye?” Willy akauliza kwa wivu kidogo, Pendo naye akacheka kidogo na kunyamaza. Pakatulia. Akamsikia Willy anaanza kuperuzi vitabu vyake, akajisogeza karibu naye, akalala.

Ijumaa.

P

endo aliamka akamkuta Willy akijisomea. “Ulilala vizuri?” Pendo akacheka na kumgeukia. “Sana. Hata sijaota!” Wakacheka. Pendo akaangalia vitabu vya Willy akakaa. “Nataka nioge, nitoke Willy.” “Bila kula!?” “Sitakula kwa kuwa najua nitakula mlo mkubwa mchana. Mwenzio naogopa sana unene. Sili mara kwa mara. Nina asili ya unene kweli! Nikijisahau tu, nakuwa kibonge. Na huwa sichelewi kunenepa.” Willy akatabasamu tu akimtizama huyo Pendo anayeogopa unene. “Huyu hata akiwa mnene au mwembamba atabaki akivutia hivihivi.” Akawaza Willy. Pendo akatoka kitandani kuelekea bafuni. Akajisafi na kuvaa hukohuko nguo ambazo alinunua bila kufua. Akatoka.

“Mbona umetoka tofauti!” “Nanukia mitumba tu hapa. Hili gauni nililinunua jana.” “Umependeza. Lakini naomba nikupeleke huko saluni.” Pendo akashangaa kidogo. “Usijali Willy! Wewe endelea na kujitayarisha na mitihani!” “Nitaendelea kujisomea hata kwenye gari wakati nakusubiria saluni ili turudi wote chuo.” Pendo akakaa. “Willy!” “Sitaki kukuacha barabarani wakati nilikuahidi nitakufikisha chuoni. Usijali. Nisubiri nijitayarishe, tutoke wote.” Ikamgusa sana Pendo. Akamsubiria.

Kweli alimfikisha mpaka saluni. Kulikuwa na baa pembeni. Akamwambia atamsubiria hapo akiwa anapata kifungua kinywa na kujisomea. Hapakuwa na watu wengi na bado ilikuwa mapema tu. Pendo akashukuru na kuingia saluni. Alikausha tu nywele zake alizokuwa ameshonea wiving ya rangi nyeusi tupu. Akamwambia aipige pasi tu, inyooke. Akafanyiwa hivyo. Na rangi yake nyeupe, Pendo akapendeza sana. Akatoka kumfuata Willy baa. Willy akatabasamu alipomuona. “Natamani hiyo bahati ya uwezo wa kukupeleka sehemu yenye hadhi kwa chakula cha mchana ingekuwa yangu!” Pendo akajisikia vibaya. “Lakini tupo wote na wewe hapa, na tumelala wote.” “Hatujalala wote, ila tumelala pamoja.” Pendo akacheka na kuinama.

“Na hapa hatupo kwa chakula, umenifuata tuondoke.” Pendo akafikiria kidogo. “Nikwambie kitu Willy?” “Nakusikiliza.” “Nimekuwa na wakati mzuri sana pale kwako. Wakati wakujaliwa kuliko ninavyokuwa na Chris kwenye mahoteli mazuri na ya gharama. Kwa vyovyote vile, umenipa usiku mzuri. Nimefurahi.” Willy akaridhika. “Kwa hiyo amani na furaha haipatikaniki kwenye vitu vya hadhi ila kwa mtu mwenyewe. Umenijali vizuri. Umelala na mimi, upo hapa ukinisubiria, huo ni upendo wa ajabu sana, sijapata kwa muda mrefu. Asante.” Ikamgusa Willy. “Karibu.” Wakaangaliana na kucheka.

 Wakati wapo njiani kuelekea chuo, Willy akavunja ukimya. “Kwa hiyo leo na kesho utakuwa busy sana?” Pendo akacheka. “Naamini hivyo. Eva ameniambia nijiandae haswa. Tutakula bata kwa mrija.” Willy akacheka. “Unampenda sana Eva, eeh?” “Sana. Mbali na ule ukorofi wake, ni mtu mzuri sana. Kwanza akiamua kukupenda, anakupenda haswa na ujue atasimama na wewe katika kila hali. Nafikiri ndio maana mpenzi wake anampenda Eva.” Willy akacheka na kumfikiria Eva. “Nimemuomba Kaka K aje anichukulie mizigo kesho asubuhi. Ameniambia ataniambia muda atakao kuja. Kwa hiyo itabidi niwepo chuo nikimsubiria.” “K ni nani?” “Kaka yetu mkubwa, anaitwa Kenton, halafu Nancy ndio wakatikati kisha mimi mziwanda wao.” “Ndio maana unadeka Pendo!” Pendo akacheka sana. “Wao ndio wananidekeza lakini mimi sinaga hata mpango!” Willy akacheka sana. “Wewe hudeki?” “Sina mpango kabisa, lakini wao ndio wanataka nideke.” Wakazidi kucheka.

Walipofika karibu na chuo, Willy akamgeukia. “Sasa mimi nitakushusha getini, halafu nakwenda kuegesha gari kwengine.” “Kwa nini huegeshi chuo wakati kunanafasi!?” Pendo akashangaa kidogo. “Sipendi tu. Lakini wewe nitakusogeza mpaka getini, usijali.” Pendo akajua ndio maana hakuwahi kumuona na usafiri. Hakutaka watu wajue kama anausafiri. Hawakuwa mbali na hapo getini wakawa wameshafika. “Nakushukuru kwa kila kitu Willy. Naamini hatutapotezana tena.” “Naamini hivyo.” Wakacheka kidogo. “Mtihani mwema wa mwisho. Mungu akusaidie ufaulu sanaaa.” “Kwa hizo baraka! Lazima nitafaulu tu.” Pendo akacheka na kushuka. Alipoondoka mbele ya macho yake, ndipo Willy akakumbuka hakuomba namba ya simu. Akajilaumu sana. Lakini akajiambia akitoka kwenye mtihani, Pendo atakuwa amerudi chuoni, atamfuata tena chumbani kwake amuombe.

~~~~~~~~~~~~~~~~~

Willy alibaki akisubiria mtihani mawazo kwa Pendo. Akakumbuka hiki na kile, akabaki amekodolea macho anachotakiwa kusoma kabla ya mtihani. “Sasa hivi atakuwa ameshafika kwa Chris wakipanga mipango ya safari.” Willy akawaza na kuumia moyoni. Akabaki ametulia mpaka muda wa mtihani kukaribia, wenzake wakaanza kuingia. “Kumbe umeshafika kaka!” Kyande akamsogelea. “Nipo hapa tokea saa saba mchana. Vipi mtihani wa mwisho?” “Huu lazima nitengeneze msonge mwingine, kaka. Nimekesha nao.” Wakazungumza kidogo akili za Willy zikarudi hapo, wakapitia mawili matatu pamoja. Mtihani ukaanza. Willy akawa wa kwanza kumaliza. Hakuna aliyeshangaa. Akatoka.

Moja kwa moja chumbani kwa kina Pendo. Alimkuta msichana mwingine, akamwambia tokea Pendo atoke, hajarudi. Akatamani kuuliza zaidi, lakini akashindwa. Moyo ukamuuma. Akaangalia saa, ilikuwa saa 12 kasoro. “Chakula cha mchana gani hicho! Itakuwa ameunganisha na kitu kingine.” Willy akazidi kujiumiza. Akarudi kwenye gari yake. Akakaa mpaka kwenye saa moja usiku, akarudi tena. Safari hii hata aliyemkuta mwanzo pale chumbani, hakumkuta. Aligonga na kugonga, kimya zaidi akaona wasichana wanapita na vitaulo wakienda kuoga. Akaamua kuondoka tu. “Pengine sasa hivi amelala kwa Chris! Mimi nahangaika tu.” Willy akawaza na kuamua kurudi kwake. Akakumbuka mazungumzo kati ya Pendo na Chris, akajua Chris amefanikiwa kumshinda.

Usiku huo ukawa mgumu sana kwa Willy. Akatamani kurudi kwa Pendo kesho yake asubuhi, lakini akakumbuka kaka yake atakwenda hapo chuoni kuchukua mizigo yake. “Labda ndio ili awe huru kusafiri na Chris.” Willy akakumbuka habari za safari zao, akakumbuka kuambiwa wanafikia kwenye mahoteli makubwa. Akaona ni heri tu amuache aende. Hatamuweza Pendo.

Jumamosi ya Pikiniki.

W

illy aliamka asubuhi hiyo akiwa mnyonge. Lakini akakataa siku yake kuisha hivyo. Akakimbilia kwenye mazoezi. Akafanya hili na lile lakini moyo ukakataa. Mawazo kwa Pendo. Mwishoe ikabidi ampigie simu Kyande kumtaarifu na yeye atakuwepo huko kwenye Pikiniki. Alijua ndio njia pekee yakumuona Pendo. Akajiandaa na yeye vizuri ili kuvutia zaidi. Akajua mida ya saa kumi wanachuo watakuwa wengi wakitaka kuvuka kwenda huko kisiwani Mbudya. Akaona asubiri kwanza. Ilipofika mida ya saa 12 jioni na yeye akawa amefika hapo wakakutana na kina Kyande kama walivyopanga. Wakakuta kuna boti ambayo unaweza kukodi kwa bei ya juu zaidi, na mnakwenda wachache sio wengi. Wakaona wakodi boti yao. Wakachangishana watu wa darasani kwao waliokuwa karibu, wakaondoka kuelekea kisiwani. Mawazo ya Willy yakiwa kwa Pendo.

Walikuta kumejaa na mziki ukisikika kwa sauti, kila mtu na mtu wake. Wengine walishalewa. Lakini kweli kulikuwa na ulinzi mkali sana mpaka mbwa wa FFU walikuwepo hapo. Hilo likampa tumaini Willy. Sasa wapi pakumpata Pendo! Hiyo ndio ikabakia agenda. Kyande na wanzake wakakimbilia upande wa vinywaji, baa. Willy akawaambia watawasiliana, yeye anazungukia kisiwa. Alizunguka Willy karibia nusu saa ndipo akamuona Eva amekaa katikati ya watu, akajua na Pendo atakuwepo hapo. Akasogelea lile kundi, na kweli akamuona Pendo amekaa katikati yao lakini ametulia sana.

          Akamsogelea na kumgusa. Pendo akageuka. “Willy!” Akasimama kwa haraka. Willy akashangaa amemkumbatia. Akacheka na yeye akamkumbatia vizuri. Wote wakawageukia. “Ndio mmekuja au mlikuwa hapa muda mrefu?” “Hatujafika muda mrefu. Nimewaacha kina Kyande upande ule wa baa. Nimekuja kukusalimia.” Pendo akacheka kinyonge. Willy akamwangalia akajua kuna jambo halipo sawa. “Unataka tutembee kidogo?” Willy akauliza kwa upendo, Pendo akakubali. Akamsogelea Eva na kumuaga. Wakaondoka.

 

Willy & Pendo Kisiwani.

“Umependeza sana Pendo. Lakini huonekani na furaha! Kuna nini?” “Nipo sawa Willy. Na wewe umependeza. Na nimefurahi umekuja.” Willy akatafuta sehemu pembeni ya fujo. “Itakuwa sawa kwako tukikaa  hapa chini?” “Hujaja na mtu wako?” “Unamaanisha msichana?” Pendo akacheka. “Willy!” “Ndivyo ulivyomaanisha. Si ndivyo?” “Ndiyo.” Pendo akakubali kwa aibu na cheko. “Hapana. Kwani nilikwambia nipo kwenye mahusiano!?” Willy akauliza kama anayejaribu kuvuta kumbukumbu. “Hapana.” “Oooh! Nilifikiri nimeanza kuongopa!” Willy akavua koti lake, akakaa chini akatandika koti pembeni yake ili Pendo akae. Akakaa huku mguu mmoja amekunja goti. “Kaa hapa ili usichafue nguo yako.” “Asante.” Pendo akavuta koti, akaliweka vizuri na kukaa. Willy akamuona anapenyeza miguu yake yote miwili chini ya ule mguu wake aliokuwa amekunja goti, kisha kichwa akakiegemeza kwenye goti la Willy. Hilo lilimfurahisha sana Willy. Akashangilia moyoni. “Mungu anipe nini mimi!” Akawaza Willy na kuweka mkono mgongoni kwake Pendo. Akatulia hapo kama kitoto cha paka. Watu wengine walikuwa wamekaa mbele na pembeni yao makundi makundi hakuna mwenye habari na mtu.

“Za tokea jana tulipoachana?” Willy akauliza kwa kujali huku akimwangalia Pendo aliyekuwa ametulia gotini kwake. “Nzuri. Vipi mtihani?” “Sio mbaya. Nilirudi kukutizama chumbani kwenu, nikaambiwa bado hujarudi.” Pendo akamgeukia vizuri akiwa kama na mshangao kidogo. “Nilisahau kukuomba namba ya simu, Pendo. Nilikuja kuomba namba. Nikarudi mara mbili hukuwa umerudi, nikajua bado upo kwenye lunch.” Pendo akatulia kidogo kama anayefikiria. “Safari lini?” Willy akaendelea kudodosa kutaka kujua kama bado Chris yupo kwenye picha. “Na nani!?” Pendo akauliza. “Si safari yako na Chris!” “Nilifuata ushauri wako, nikaona sio sawa kuendelea kumdanganya wakati ananiumiza. Nikamwambia ukweli, japo amekiri hakukusudia kuniumiza. Akaahidi kujirekebisha.” Willy akaanza kukosa raha.

“Kwa hiyo mmetengeneza?” “Hapana Willy! Nimemwambia hakuwa akikosea kwa bahati mbaya. Ndivyo alivyo, na hivyo alivyo, sina furaha yakuwa naye. Alikasirika kidogo, lakini nashukuru alikubali kunipa vitu vyangu.” “Oooh, ndio maana ulichelewa kuridi, kumbe ilibidi kurudi nyumbani kwake ili uchukue vitu vyako!” “Hapana Willy! Vitu anavyoninunulia Chris, huwa anasema ni vya palepale nyumbani kwake na kwa ajili yake. Nitumie pale kwake na niwe naacha ili nisiwe na kwenda na vitu vyangu.” “Sijaelewa Pendo!” “Ni ngumu kumuelewa Chris, ndio maana niliona nisipoteze muda. Nimuache tu. Lakini kuna kijibegi nilikiachaga kwake ndicho kilikuwa na vitu vyangu, nilimuomba aniletee jana, nikijua sitarudi tena kwake.” Hapo Willy akafurahi.

Lakini akaingiwa tena na wasiwasi wa wivu, ikabidi aulize. “Na vitu vyako vingine, kwa hiyo itabidi kufuata wakati mwingine tena?” “Hakuna kitu kingine nimeacha kwa Chris, Willy. Nilikwambia Chris ni mtu wa hadhi. Ni wa hadhi kweli kweli. Huwezi kuingiza hovyo hovyo tu vitu vyako nyumbani kwa Chris.  Hata mswaki tu! Huwezi kupeleka hii miswaki ya kawaida nyumbani kwake ukakaa kwenye sinki lake. Hatumii tu kila mswaki. Anatumia miswaki ambayo mwenyewe anasema inafaa kwa meno na imepitia uchunguzi wa madaktari wa meno. Huo ni mfano tu. Kwa hiyo huwezi kubeba takataka yako ukaingiza kwenye nyumba ya Chris. Ananunua chochote unachotaka, vinakuwa vyakutumia nyumbani kwake siku ukienda kwake. Kwa maana nyingine hata magauni aliyokuwa akininunulia, alikuwa akiyapeleka dry cleaner yeye mwenyewe. Yakisafishwa, anarudisha nyumbani kwake. Ninayatumia kwa shuguli zake yeye, na kurudisha kwake. Si yangu.” Willy akashangaa sana.

“Hiyo sijawahi kuona!” Pendo akacheka kinyonge. “Ndio maana umekosa raha? Usijali tutanua mengine.” Pendo akacheka na kumpiga kidogo. “Hapana bwana! Mimi najua kuridhika na vyangu. Hata hivyo tokea mwanzoni nilijua si vyangu. Yeye mwenyewe alikuwa akiniambia kila akininunulia kitu au akinipa pesa nikanunue kwa ajili ya shuguli zake. Alihakikisha naelewa ni cha pale kwake.” “Haiwezekani Pendo!” Pendo akacheka. “Wewe hujawahi kukutana na kiumbe kama Chris. Na ndio maana nilimtuma tu vitu vyangu. Kwanza nilijua angetupa kwa haraka sana baada ya kuachana naye na kuvikuta kwenye stoo yake. Angeona ni uchafu.” “Sasa unajisikiaje?” “Mbali yakumisi safari za hapa na pale na kulala kwenye 5 stars hotel, nina amani na furaha yakutokuwa karibu na yule mwanadamu. Anachosha! Hujui ni wakati gani au kitu gani kitamfurahisha au kumuudhi! Hicho kipengele nishamaliza. Sirudi huko tena.” Willy akafurahia, akacheka taratibu.

“Sasa kwa nini huna raha? Nimekukuta katikati ya kundi la watu wanaocheka na stori nyingi lakini wewe umenyongea!” Pendo akanyamaza. “Pendo?” “Jana tulirudishiwa baadhi ya mitihani yetu Willy.” Hapo hapo Willy akaelewa. “Imekuaje?” “Nimeshikwa hesabu. Sikufanya vizuri mtihani wa mwisho na hata wastani pia haukuwa mzuri tokea mwanzo tunaanza chuo.” Akaanza kulia. “Nikiwa nawenzangu tu, nafeli! Sasa sasahivi nipo peke yangu ndio nitaweza kweli! Eva hajakamatwa somo hata moja, Willy! Nitafanyaje?” Pendo akalalamika akilia. Mwishoe akainamia kwenye goti la Willy tena na kuendelea kulia. Willy akamsogeza nywele pembeni, mpaka akaacha uwazi kwenye shingo, akainama hapo nakumbusu shingoni kama mara tatu huku akimpapasa.

“Niangalie mimi Pendo.” Pendo akalia tena kidogo, akamgeuzia uso uliojaa machozi akiwa bado amemuegemea gotini. Willy akamfuta. “Nitahakikisha unarudia huo mtihani, na unapita. Na hutakaa ukakamatwa tena somo jingine. Sawa?” “Kweli Willy?” “Mimi ndio nakuahidi. Tutasoma wote. Utajiandaa vizuri. Ukitulia na kujiamini, utarudia na utafanya vizuri kabisa. Wala usikose raha kwa ajili ya hiyo.” “Kwahiyo, hiyo ni ahadi?” “Na ninakusudia kuisimamia, endapo utasimama na mimi.” Pendo akaona hilo sharti lakusimama na Willy ni zuri sana. Alishampenda Willy. Kuwa naye na kufaulu shule, ni bahati ambayo alijiambia haitakaa ikatokea tena. Akamuona ameridhika akajifuta machozi mwenyewe.

“Nilishaogopa Willy! Nashukuru. Eva ameshaondoa mizigo yake yote chuoni na leo harudi tena pale anaondoka na mpenzi wake!” “Nikikuomba turudi kwangu utakubali?” Pendo akamwangalia na kucheka, akageuka pembeni kama anayefikiria. “Sio lazima. Ni ombi tu. Ila namba ya simu naomba sasa hivi. Sitaki kurudia kosa.” Pendo akacheka wakati Willy anatoa simu mfukoni kwa mkono mmoja mwingine ukiendelea kupita mgongoni kwake Pendo, taratibu. Akamkabidhi Pendo simu. “Nikuwekee jina gani? Nisije nikaweka Pendo, kumbe kuna kina Pendo wengine humu ndani.” “Niwekee namba, jina nitakuja kuweka mwenyewe.” Pendo akacheka na kuandika namba yake hapo. Akajipigia. “Tayari nimekuwekea namba yangu bila jina na mimi nimechukua namba yako.” Akamrudishia. “Nashukuru.” Pendo akafikiria akawa kama amegutuka.

“Mbona huweki jina langu sasa hivi? Unataka ukaweke jina baya nini?” Willy akacheka sana. “Unafikiria tanaka kuweka jina gani?” Willy akauliza huku akiendelea kucheka. “Pendo mbaya asiyenikaribisha kwake, ila mimi namkaribisha kwangu bila kinyongo.” Willy akacheka sana. “Hilo ni jina tu?” “Mimi nakuhisi hivyo bwana! Sasa kwa nini hutaki kuweka jina mbele yangu?” “Kwa nini usifikirie nakutafutia jina zuri.” Pendo akacheka huku akifikiria. Akamwangalia. Bado Willy alikuwa akimbembeleza kwa kumpapasa upande wa mgongoni, akiwa amemuinamia kwenye goti la ule mguu aliokuwa ameunyanyua.

“Kama jina gani sasa?” Pendo akauliza. “Soulmate.” Pendo akashituka akabaki akimwangalia. “Baya?” Willy akamuuliza. “Maana yake ndiyo nzito, Willy!” “Ndivyo ninavyojisikia.” Pendo akamwangalia kama ambaye hajamuelewa. “Sijakurupuka Pendo. Ndivyo ninavyojisikia kwako tokea tunaanza chuo.” Pendo akakunja uso akimshangaa. “Sikudanganyi. Nakumbuka kila siku tulizokuwa tukikutana hata kama hukuwa ukiniona au kunisalimia. Nakumbuka kuanzia nguo ulizokuwa ukivaa mpaka aina ya nywele.” “Willy!” Pendo akashangaa taratibu. “Ni kwa vile nilivyokuwa nikijisikia kwako Pendo. Na unajua ni kwa nini nilihama pale hosteli za chuo?” Pendo akabaki kimya. “Kwa jili yako ili kukuthibitishia kwa vitendo kuwa sipo na Wema. Niliona vile ulivyoamini na jinsi watu walivyoubebea bango ule ukweli ambao sio kweli kati yangu na Wema. Nikajua neno ‘sio kweli’ pekee, lisingekutosha kuniamini.” Pendo akabaki hajui aseme nini.

“Halafu nikaona na vile Chris amejaa kwenye picha, hata siwezi kukaribishwa maji!” Pendo akacheka sana. “Unanifanya nizidi kujisikia vibaya bwana Willy! Ulikuja muda mbaya.” “Kweli ulikuwa mbaya.” Pendo akazidi kucheka. “Nikikuomba msamaha itasaidia?” “Sijui! Jaribu.” Pendo akacheka. “Pole na samahani Willy.” “Ukiwa hivyo natamani kukubusu tu.” Pendo akacheka taratibu akainama. “Jana nilishindwa kuomba kwa kuwa bado Chris alikuwa kwenye picha. Lakini leo si ruksa?” Pendo akatulia. “Sitakuchezea wala kukuumiza Pendo. Nakupenda na sijaanza leo. Mimi ni mwaminifu wala hutahitaji kuwinda simu yangu. Nakuhakikishia utakuwa peke yako kwangu.” “Kweli Willy?” “Nipe nafasi uone. Huna hata haraka ya kunikubali, nitasubiri.” “Mimi nataka kuwa peke yangu.” Pendo akaongea kwa deko akimpapasa Willy vinyweleo vya mkono. Willy akacheka taratibu. “Na ndivyo itakavyokuwa. Nakuahidi Pendo. Na sitakubadilikia.” “Na mimi huwa sio muhuni Willy.” Willy akacheka tena. “Basi tutakuwa sisi wawili tu.” Pendo akaonyesha kurudhika akiendelea kumpapasa Willy vinyweleo vya mkono. Pendo akakumbuka ahadi hizo walizopeana siku hiyo kisiwani. Akatulia akimfikiria Willy. Miaka yote hiyo hakuwahi kumbadilikia hata mara moja! Alimdekeza wakati wote, imekua kama kufumba na kufumbua, sasa hivi wanazungumzia talaka! Roho ikazidi kumuuma Pendo.

Mawazo yakamrudisha tena siku ile walipokuwa kisiwani. Akakumbuka jinsi Kyande alivyokuja na kelele na kuingilia ule wakati mtulivu waliokuwa nao baada ya kupeana ahadi. “Unakosa starehe kaka!” Akapiga kelele akiwasogelea. Alipowakuta wamekaa vile, akapoa. “Huyu ni Pendo! Au macho ya kilevi tayari?” Pendo akasimama, na Willy akasimama. “Samahani kuwaingilia. Sikujua kama umeshinda bingo, kaka.” Pendo akacheka na kujirudisha nyuma ya Willy. “Nilijua unapitwa, lakini hapo kaka! Acha mimi niombe msamaha wakuingilia. Naondoka kabisa, narudi kwenye mashindano ya kunywa.” Willy na Pendo wakacheka, Kyande akaondoka akishangilia kilevi. Willy akamgeukia Pendo akamvuta karibu na kumkumbatia. Akamnyanyua kichwa vizuri kwa mkono mmoja shingoni akaanza kunyonya midomo ya Pendo. Kwa mara ya kwanza kwa mwaka mzima wanaanza chuo mpaka wamemaliza mwaka ndio siku hiyo ndio anafanikiwa hata kumshika.

Willy akamvutia vizuri mwilini mwake, akamsikia nayeye Pendo akimkumbatia vizuri, Willy akajua amefurahia. Hakuna kilichoendelea jioni hiyo hapo ufukweni ila hayo mabusu. Wakarudi kukaa, wakakumbatiana tena na kuendelea kuzungumza kidogo na mabusu mengi. “Nilikukaribisha nyumbani.” Pendo akacheka taratibu. “Asante.” “Hiyo inamaana leo usiku tutakuwa wote?” “Bado nina vitu vyangu chuo. Nimebakiza..” “Unataka twende tukavifuate kabla hatujaenda kwangu?” “Au nikafungashe kila kitu ndipo nije kesho?” Willy akambusu tena na tena, akimpapasa kwa heshima bila kufika mbali. “Nitakusubiri wakati ukifungasha. Twende.” “Sasa hivi!?” Pendo akauliza kwa mshangao huku akicheka kidogo. “Kama unapenda kuendelea kubaki hapa, sawa. Nitakusubiri.” “Hata tukitaka kuondoka, tunaondokaje?” “Tutakodi boti iturudishe nchi kavu.” “Basi nisindikize nikamuage Eva.” Hapo napo yakaendelea mabusu ya muda tu Willy akinogewa na midomo ya Pendo, ndipo wakasimama.

Hata Eva akamshangaa Pendo aliyerudi. “Unakwenda wapi wewe?” “Nitakwambia kesho. Ila naondoka na Willy.” “Moja kwa moja!?” “Ndiyo. Naondoka na Willy, nilishakwambia ananivutia. Na ametoka kunikisss.” Wakacheka sana. Willy yupo pembeni. “Pendo!” “Nahisi nampenda. Anajali huyo! Ananipapasa kila wakati! Haachi kunishika.” Eva akacheka kishabiki. “Ujue yule rafiki yake Chale, alikuwa anakusubiria?” “Akuu! Simtaki, mimi naondoka na Willy.” Eva akacheka. Wakaagana. Wakati Pendo anaondoka, rafiki wa mpenzi wake Eva, akamuita.

Pendo akasimama. “Nimesikia Eva akisema unaondoka!” “Ndiyo.” “Daah! Nilijua tutakuwa wote usiku wa leo.” “Yule pale ni mpenzi wangu, ndio amekuja kunichukua.” Wote wakamgeukia Willy, wakakuta na Willy akiwatizama. “Oooh! Sikujua kama una mtu!” Pendo akacheka kiuungwana na kuaga. “Twende.” Akamshika Willy, wakaondoka. Wakakuta kuna baadhi ya watu nao wanaondoka. Wakapanda na kulipia, wakaondoka kurudi nchi kavu. Walikuta gari ya Willy sehemu yakuegesha magari, wakapanda na kuelekea chuo. “Nimefurahi umekubali kuwa na mimi.” Pendo akacheka bila kujibu.

Alichofanya Pendo mara walipofika chuoni ni kukusanya vitu vyake vyote na kuweka kwenye gari ya Willy. “Naomba usiogope ukadhani nahamia kwako moja kwa moja. Vyote hivi vilitakiwa kurudi nyumbani ila nimepishana na kaka K, alipokuja kuvichuk...” “Pendo!” Willy akamuita taratibu. “Sitaki uingiwe hofu.” “Hata ukihamia kwangu moja kwa moja, sitajali. Ndio itakuwa furaha yangu. Unakumbuka nilikuomba orodha ya vitu ambavyo ungehitaji pale kwangu?” Pendo akacheka. “Nilijua unatania Willy!” “Hapana. Nakuhitaji Pendo. Nakupenda wewe. Sijawahi kukaribisha mtu hata mmoja pale kwangu. Hakuna anayepafahamu pale ila wewe tu. Hata Kyande hajui ninapoishi. Na nilikusudia hivyo ili tuwe na sehemu yetu sisi tu wawili.” “Kweli Willy?” “Mimi nilikuwa nikikuwazia kwa muda mrefu sana. Naweza nisiwe na uwezo wa kukupeleka kwenye mahoteli ya hadhi ya juu au nyumba ya thamani kama Chris, lakini nakuhakikishia kukupenda na kukuthamini.” Ikamgusa sana Pendo. Akamsogelea pale alipokuwa amesimama nyuma ya gari akipanga mizigo yake, akambusu.

Walikuwa wamesimama ndani ya geti la chuo, Pendo hakujali. Akamsogelea vizuri na kuendelea kumbusu taratibu bila hata haraka wakati wanachuo wengine wakipita na kuwaangalia. “Asante Willy.” “Asante na wewe.” Willy akashukuru kwa heshima ya kumbusu mbele ya watu bila kificho. Wakamalizia kupakia vitu, nakuondoka hapo chuoni mpaka nyumbani kwa Willy. “Naomba tusishushe vitu ili tena kesho tusihangaike kupandisha.” “Unataka kuondoka kesho!?” “Ndiyo Willy. Kwani ulitaka nikae mpaka lini?” “Isiwe kesho. Usiku mmoja tu! Nahisi mimi unanipunja Pendo.” “Hapana Willy. Nyumbani wanajua nimeshamaliza mitihani!” “Ungefanyaje kama ingekuwa unasafiri na Chris?” Pendo akapoa, akajua amekamatwa.

“Huwa nilikuwa nikisafiri na Chris, inakuwa msimu wa chuo, Willy. Na safari hii nilipanga kutosafiri naye tena au nilishaamua kutokuwa naye tena. Naweza kukwambia nina muda mrefu hata kwake nimekuwa nikimkatalia kwenda. Nilishaona haina hata maana ya kupata naye muda wa faragha! Kwanza alishanikera, hata sikumbuki mara ya mwisho kumbusu Chris! Ni mnyanyasaji kuliko nitakavyokwambia. Hisia zilishakufa kwake. Kama usingeniokoa kwa kuniambia nimwambie ukweli, nahisi mpaka sasa hivi tungekuwa tukisumbuana naye tu.” Willy akabaki ametulia kama aliyeelewa lakini bado anahisi kupunjwa.

Pendo akapiga magoti kwenye kiti na kumbusu mara mbili tu. “Naomba tusifikirie kuondoka kwangu wakati hata sijafika ndani.” “Nahisi ninahamu na wewe zaidi ya haya masaa machache unayotaka kuyatumia kwangu.” Pendo akambusu tena bila kumuachia, Willy akamshika vizuri akiwa amepiga magoti vile vile. “Naona kweli twende tukatumie siku ya leo kwanza.” Willy akaongea sikioni, Pendo akacheka taratibu na kumbusu tena. Akachukua kibegi kidogo ambacho alishakitenga tokea chuo, chenye vitu alivyojua atatumia kwa Willy, akashuka. Willy akampokea na kutangulia. Akafungua mlango, akampisha Pendo aingie. “Karibu.” “Asante.” Pendo akapita.

Akamuona Willy anapitiliza chumbani, na yeye akamfuata. “Naomba nioge kwanza Willy. Ndio nitajisikia vizuri.” “Sawa.” “Kwani tutatoka tena?” “Hapana. Ulitaka tutoke?” “Hapana. Niliuliza ili nijue nivae nini.” “Hatutatoka. Kama utakuwa na njaa, kipo chakula na matunda.” “Sawa.” Pendo akaelekea bafuni na nguo za kulalia, akaoga nakutoka akiwa amevaa nguo zake za kulalia, zikitamanisha haswa. Akacheka wakati Willy akimtizama. Akang’ata mdomo wake wa chini kitu kilichokuwa kikimchanganya sana Willy akifanya hivyo.

“Unavutia hata kwenye nguo za kulalia Pendo!” “Asante.” Pendo mwenyewe alijijua ni mzuri. Na vile Willy anavyomchukulia, ikamuongeza ujasiri sio kama Chris aliyekuwa akimfanya ajisikie mnyonge mbele yake. Akamvutia karibu yake. “Nikwambie ukweli?” “Mmmh!” “Nilishakupigia mahesabu humu ndani, nikaishia kukuweka kitandani, taa ikikumulika.” Pendo alicheka mpaka akajifunika uso. “Willy wewe!” “Hakika. Nilisema labda kwenye kochi. Nikajiambia kwenye kochi sitafaidi kukuona vizuri mwili wako wakati nikikubusu kila mahali. Sehemu pekee niliyoona nitatuliza nafsi yangu ni kitandani, tena ukiwa kama ulivyozaliwa, na taa zote zikitumulika pale kitandani. Nitizame mapaja yako niliyoyaona siku Wema aliposababisha uanguke!”

“We Willy jamani!” “Yaani vile ulivyoanguka siku ile, nguo ikafunuka, ile picha ya mapaja yako ipo akilini kama fomula za mahesabu. Ndio maana nilikimbia kukuinua ili wengine wasije kuyaona. Nikajiambia siku ukija hapa kwangu, jinsi ya kuyaona vizuri, niyashike na kuweka mdomo wangu hapo kwa uhuru, ni kitandani tu. Tena na taa ikimulika. Nishakupigia mahesabu humu ndani, hakuna tutakapokaa usiku huu kama sio pale kitandani, nikaridhika. Na ninataka nikushike kila mahali. Midomo yangu ikiridhika kupita kote nilipokuwa nikipatamani huko mwilini mwako, ndipo akili yangu itatulia.” “Mimi sijui nifanye nini sasa?” “Sitaki ufanye chochote. Niruhusu nifanye kila kitu mwilini mwako. Hatua kwa hatua kama nilivyopanga. Na nguo nikutoe mimi mwenyewe.” Pendo akafurahia sana.

“Nakuahidi usiku wa leo utafurahia Pendo.” “Nimeshaanza kufurahia. Napenda unavyonishika Willy. Nasikia raha!” “Basi niachie usiku wa leo nifanye kile nilichokuwa nikitamani. Kuanzia kukuvua nguo zote mimi mwenyewe.” “Ila sasa nilipooga sijavaa chupi tena!” “Nikikuomba uvae ili mimi mwenyewe ndio nikuvue itakuwa nakusumbua?” Pendo hakutegemea. “Willy!” “Hakika Pendo. Naomba ukavae hapo chumbani wakati nakusubiri hapa, halafu ukimaliza ndipo uniite.” Pendo akaenda chumbani akicheka kama asiyeamini. “Halafu huyu Willy hata hakubadilika! Wakati wote alipenda yeye ndio awe ananivua nguo na penzi iwe mwangani!” Pendo akakumbuka hilo akiwa hapo chumbani kwao akimkumbuka mumewe. “Jamani maisha yananipokonya Willy wangu! Hakuna mwanaume atakayeniwezea kama Willy mimi!” Pendo akakumbuka penzi la Willy na kulia kwa uchungu sana akiwa peke yake hapo chumbani usiku huo akiwa ameachwa na Willy.

Akakumbuka mambo mazuri yaliyomfurahisha usiku huo ambayo hata Chris mwenyewe hakuwahi kumfanyia kwa undani huo. Willy alionekana kufurahia kila anapopanyonya, tena kwa muda mrefu kwa hisia bila papara wala kinyaa. Alifanya kama yeye ndiye anayefaidi zaidi kumbe Pendo ndiye aliyekuwa akifikishwa kila mara wakati Willy hajapata bao hata moja ila kuhangaika mwilini kwa Pendo. Usiku huo kwa mara ya kwanza Willy akabahatika kumshika Pendo aliyekuwa akimtizama akiwa na nguo. Sasa hivi yupo mikononi mwake, mtupu na ametulia kitandani kwake akitoa milio iliyozidi kumfanya Willy apagawe na kila wakati alipokuwa akifika kileleni alimuita Willy jina lake kitu kilichomfurahisha sana Willy na kuona kumbe Pendo yupo pale wala hamfikirii mtu mwingine ila yeye!

Alipoamua kuingia yeye sasa, kwa kuwa alishakuwa juu sana kwa kumpapasa Pendo kwa muda mrefu, haikuchukua muda mrefu akapiga bao. Akajua Pendo atamdharau atamuona hajui mchezo wa muda mrefu ndio maana alikazana na romance, akarudia raundi ya pili iliyomtoa jasho Pendo. Alimgeuza kulia na kushoto safari hii akifaidi Willy peke yake bila kupumzika na Pendo akiwa mwepesi hapo kitandani akimpa ushirikiano kwa kila staili anayotaka kumfanyia, mpaka Willy akatosheka.

Wakati anapumzika hiyo roundi ya pili, Pendo akaweka mkono chini ya kitovu chake na kuanza kumchezea nywele za hapo taratibu na kumuamsha tena Willy. Willy akamgeukia. “Nakufurahia Pendo!” “Na mimi pia.” “Basi naomba tuendelee tena.” Pendo akacheka akijaribu kumfikia midomoni. “Una mwili mzuri Willy! Nasikia raha ukinilalia.” Willy akacheka sana. “Mimi nilijua nakuumiza, lakini nikashangaa mwenzangu ndio umepiga bao kwa haraka!” “Nasikia raha hicho kifua chako kinavyonilalia, halafu huo mkono wako unavyokamata upande mmoja chini ya hips kwa nguvu halafu ukiingia na kutoka, hapo nakuwa sijiwezi tena.” Willy akawa ameshajua staili yake moja inayomfikisha kwa haraka, wakaanza tena penzi. Pendo  akakumbuka furaha aliyokuwa nayo usiku ule, akimfaidi Willy akitamani asimalize anayomfanyia hapo kitandani. Willy naye hakufanya mchezo ulio wakitoto kwani hakujua mwenzie aliyeachwa alikuwa akifika wapi, kwa hiyo yeye akaongeza umakini akihakikisha hafupishi safari na hakuna anakobakisha hapo mwilini kwa Pendo. Akamgeuza kulia na kushoto, ilimradi wote wafurahi.

Asubuhi ya siku inayofuata waliamka wakabaki kitandani. “Naomba na leo tubaki wote Pendo. Umenionjesha tu.” “Hata mimi nataka tubaki wote Willy. Nimefurahia. Nimeamini kweli unanithamini.” Pendo akaongea taratibu pembeni ya Willy. Willy akaanza tena kumbusu. Kama apendavyo Willy akaanza kumtoa nguo Pendo. Walikuwa wamelala hapohapo kitandani, midomo yake ikiendelea kumnyonya midomo yake huku mikono ikimpandisha nguo ya kulalia. Kwani usiku baada ya purukushani zote Pendo alirudi bafuni kuoga. Wakati Willy naye akioga, huku chumbani Pendo akakumbuka zoezi la kuvuliwa nguo huku akipapaswa na kunyonywa mwili wake vilivyo. Akavaa kwa haraka kabla Willy hajarudi hapo chumbani. Basi asubuhi hiyo nayo zoezi la burudani la kuvuliwa nguo likaanza. Kwa hakika Pendo alimfurahia Willy, akajiambia hataondoka hapo, liwalo na liwe huko nyumbani kwao. Atajua chakudanganya baada ya kuridhishwa asubuhi hiyo. Mchezo ukazidi kunoga, akaona uzito kuondoka hata kesho yake.

Akaona atengeneza mazingira ya kukaa hapo zaidi. Akampigia simu baba yake ambaye humsikiliza na kumkubalia kila jambo kwa haraka. Akajiliza kuwa amekamatwa somo moja, tena hesabu. Anatafuta msaada hapo chuoni, na wote waliokamatwa wamebakia chuo kwa muda wakijipanga. Walimjua ni muoga wa hesabu na huwa zinamsumbua. Baba yake akampa pole na kumuhurumia sana. Pendo akajiliza kuwa amewamiss sana. Akaahidi jumamosi jioni lazima arudi nyumbani japo awaone tu ndipo arudi kwa wenzake kujisomea. Hilo likapita bila shida tena kwa upendo na akatumiwa pesa. Willy alitoka kwenda kwenye kupokea mzigo wa mashuka na kuuza. Alipomuacha hapo nyumbani, ndipo akapata nafasi ya kuwapanga wazazi.

Wakakubaliana hiyo week ni ya kupumzika tu mpaka week ijayo ndipo watasoma. Alichofanya Willy baada yakurudi na kuambiwa wazazi wameamini, na atakuwepo hapo week hiyo, akashusha mizigo yote ya Pendo, wakaanza kupanga humo ndani, ikachukua picha ya wao wawili. Pendo akajaa yeye na vitu vyake humo ndani ya nyumba ya Willy. Wakabadilisha na kupaita kwao. Pendo alijawa furaha, na umbali aliofika Willy kwenye mwili wake, hakuna kitu ungemwambia Pendo akaelewa zaidi na anachoambiwa na Willy.

Siku zikawa zikikimbi, jumamosi aliyoahidi wazazi angerudi kuwaona ikafika, ikabidi kurudi nyumbani, lakini akawaendea na ratiba nzima ya jinsi ya kujisomea na wenzake, kumbe ni Willy tu. Akadanganya nyumbani kuwa wenzake wamechukua chumba Kijitonyama, wamefanya kempu hapo wanajisomea, wakijiandaa kwa kurudia mitihani. Akaongea mengi ya uongo mpaka wazazi wakaamini na kutoa baraka zao. Pendo akaahidi kuwa akiwa anarudi nyumbani siku za jumamosi jioni, analala hapo kwao lakini jumatatu atakuwa akirudi kwenye kempu kujisomea na wenzake. Hilo likapita kwa baraka zote. Lakini dada yake Nancy yeye akamwambia ukweli kuwa amepata mwanaume anayempenda karibu kuchanganyikiwa, na kweli atamsaidia sana hesabu. Sifa za Willy zikamvutia na Nancy, akaahidi kumfichia siri.

Maisha kati ya Willy na Pendo yakaanzia hapo. Wawili hao wakaanza kuishi pamoja kuanzia hapo. Willy akawa msaada mkubwa sana kimasomo kwa Pendo, wawili hao wakawa wapenzi wa kutojificha. Likizo nzima Willy alikuwa na Pendo, chuo kilipofungua Pendo hakuchukua chumba chuoni, maisha yakaendelea Kijitonyama kwa Willy. Wanakwenda chuoni asubuhi, usiku wanarudi kwao. Wazazi wakitaka kwenda kumtembelea hosteli, basi kitanda cha Eva ndicho kikawa kikionyeshwa ni cha Pendo. Wazazi watakaribishwa chumbani kwa Eva, watazungumza kidogo. Wakiondoka, na yeye anaondoka na Willy kurudi kwao.

Mwaka huo wa pili katikati ikabidi Pendo amtambulishe rasmi Willy nyumbani kama ndiye mume wala si mchumba. Akaweka msisitizo ndiye atakayemuoa lazima wampokee na waonyeshe kumpenda. Mtoto huyo wa mama akaweka msisitizo, Willy akapokelewa kama Kenton hapo nyumbani kwao. Pendo akiwepo nyumbani, basi ujue na Willy atakuwepo hapo siku nzima wakifuatana kila mahali. Haikuwa tofauti na chuoni. Kutengana muda wa vipindi tu. Lakini kama nikujisomea, utamkuta Pendo kwapani kwa Willy. Hata kama mwenzake yupo kwenye kundi na wenzake wa uhasibu wakijisoma, basi ujue Pendo atakuwa katikati ya hilo kundi la watu wa uhasibu, anajisomea kivyake, wakati Willy anasoma na wenzake. Wakimaliza hata kama ni usiku, wanarudi nyumbani kwao. Hakuna aliyejua wanapoishi, ila wao tu.

Hata ungekuwa na mamilioni ya pesa, ukamtongoza Pendo, asingekubali kwa umbali aliofika Willy kwenye maisha yake. Akilini na mwilini mwake alijaa Willy tu. Uzuri wake na vile alivyo, alitongozwa kila kukicha, lakini akatulia kabisa kwa Willy. Na Willy hivyo hivyo. Ukiwakuta chuoni wakitembea au kukaa, basi wameshikana. Mabusu mbele ya watu kikawa kitu cha kawaida na watu wakawazoea. Pendo akawa hajui tena maisha mengine bila Willy mpaka wanamalizia mwaka wa tatu, Pendo hakushikwa tena somo hata moja na wakafaulu vizuri tu.

Kwa kuwa biashara za Willy zilikuwa zikiendelea vizuri, hawakutaka kukimbilia ajira japo Willy alipata makampuni mengi yakimtaka aanze kazi, lakini Pendo akamwambia lazima wasome wote shahada ya uongozi pamoja. Hapo hata wazazi walishajua wanaishi pamoja. Wakachumbiana na wazazi wakajua wakimaliza hiyo shahada ya pili, walishanunua kiwanja, ndiyo hiyo nyumba aliyopo Pendo au aliyochukua Pendo wakati wakuachana. Walianza kujenga wakiwa chuoni.

Usiku huo Willy amemuacha Pendo hapo kitandani, Pendo akabaki akikumbuka hayo maisha yake na Willy! Akakumbuka mapenzi yao, utulivu waliokuwa nao tokea wakiishi pamoja wakiwa chuoni mpaka wakaja kufunga ndoa, miezi michache sana kabla ya kifo cha mama yake ndio kidogo Pendo akaanza kukumbuka kumuona Willy kubadilika, lakini alimtetea nafsini mwake akijua ni sababu ya kumuuguza mama yake na Willy alipatana sana na mama yake, kumbe aliongezeka na Zelda! Pendo akalia usiku huo akimkumbuka Willy wake huku akimuonea wivu Zelda, akijua anafaidi maujuzi ya Willy. Akalia kwa uchungu mpaka akapitiwa na usingizi.

Talaka ya Pendo na Willy.

K

wa kuwa walikubaliana kila kitu bila shida, Willy na Pendo waligawana mali zao kimya kimya bila ugomvi. Kaka yake akaandaa talaka kwa haraka sana mpaka akamshangaza Willy. Ila akajua ni kwa kuwa amekasirika. Alimjua Kenton jinsi anavyopenda dada zake, zaidi Pendo. Tokea wapo wanasoma chuo, Kenton alimfanya Pendo kama mtoto mdogo. Akajua uharaka ule ni hasira ya kutaka kumtoa kwenye maisha ya mdogo wake asiendelee kumuumiza. Baada ya siku 5 tu tokea atoke nyumbani kwake, Willy na Pendo wakakutana tena kwa mwanasheria kuweka saini zao kwenye hiyo talaka. Pendo alitokea nyumbani kwenda kwenye hizo ofisi za huyo mwanasheria ambaye ni rafiki wa Kenton. Aliwahi kidogo, akafika na kukaa. Akiwa amejiinamia Willy akaingia. Moyo wa Pendo ukaanza kwenda mbio, asijue ni furaha au nini! Alishammiss Willy kupita kiasi.

“Vipi?” Akamsalimia na kuvuta kiti pembeni yake. “Safi. Pole na majukumu.” Pendo akaongea kwa sauti ya chini na ya upendo kama kawaida yake. Willy akatabasamu kidogo na kujibu huku akimwangalia. “Asante na wewe.” “Asante.” Wakamgeukia mwanasheria wao aliyekuwa amekaa mbele yao. “Habari yako Willy?” “Nzuri na samahani kuchelewa.” “Hamna shida, familia haijambo?” Willy akanyamaza kidogo, Pendo akainama. “Haijambo tunamshukuru Mungu.” “Sawa sawa. Sasa kwa kuwa naona mmeamua kumaliza mambo yenu kiuungwana, hatutachukua muda mrefu. Kama utataka muda wakupitia makubaliano yenu tuliyoweka kwa maandishi, pitia tu. Pendo alishapitia wakati akikusubiri. Hakuna haraka.” Willy akapokea zile karatasi. Akasoma taratibu tu moja baada ya nyingine.

Kumbukumbu za Pendo zikamrudisha siku waliposaini kwenye cheti cha ndoa. Harusi kubwa yakifahari. Kulijawa shangwe kubwa, wapenzi hao siku wanakula kiapo kuwa mpaka kifo ndio kitawatenganisha. Pendo akakumbuka ile hali ya furaha aliyokuwa nayo siku ile kuolewa na mwanaume kama Willy. Akavuta pumzi kwa nguvu na kuinama. Akachukia kutoshika mimba mapema. Akajichukia kusababisha kuvunjika kwa ndoa ambayo wengi waliitamani! Akatamani kama ingekuwa vinginevyo! Lakini akajiambia maji yameshamwagika. Willy si wake peke yake tena kama alivyomuahidi miaka hiyo hata kabla ya ndoa, wakiwa wanachuo, kisiwani Mbudya. Yupo Zelda na ujauzito unao msubiria Willy. Pendo akabaki ameinama.

~~~~~~~~~~~~~~~~~

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment