T |
unda akajiweka sawa. Net akajua
anataka kuongea jambo. “Tokea siku ile nitolewe au niseme nifukuzwe kwa bibi yangu
nikiwa darasa la pili, sikuwahi kupata utulivu wa akili. Nakumbuka kwa mara ya
kwanza siku ile jioni nikisikia ndugu zake mama wakitaka nitolewe pale kwa mtu
niliyedhani ndiye mama yangu au nikidhani nyumbani kwetu, na ndio nikajua
mwanamke aliyekuwa akinichukia sana hata alipokuwa akija pale kijijini mara
zote hakutaka nimwangalie, ndiye alikuwa mama yangu wa kunizaa.” Tunda akaanza
taratibu.
“Nilimsikia
jinsi anavyobisha kunichukua akitaka niendelee kuishi pale pale kwa bibi na
babu, yaani kwa wazazi wake. Walipomlazimisha sana, wakitaka lazima niondoke
pale ili kupunguza matumizi ya pale kwa bibi, pale nilipodhani ni nyumbani
kwetu, na mimi ni mdogo wao wa mwisho, ndipo nilipoona jinsi mwanadamu
anavyoweza kubadilika na kuwa mnyama mkali kuliko hata simba.”
“Alinichukua
kwa hasira sana kwa kuwa walimlazimisha lazima anitoe pale. Njia nzima yule
mwanamke ambaye nilisikia wakisema ni mama yangu, alikuwa akinifinya na
kunipiga sana. Kama sio makonzi ya kichwani, basi ngumi nzito sana kwa
kutofanya alichoniagiza kwa mtoto wake. Ni kweli sikuwa nikimuelewa. Kwanza
alinitajia majina ya vitu ambavyo sikuwahi kusikia mimi mtoto mdogo,
niliyekuzwa kijijini, tena wakati huo hata Kiswahili chenyewe sikuwa nikielewa
sawa sawa. Wakati wote tulikuwa tukizungumza kilugha pale kijijini. Pili,
nilikuwa kwenye mshtuko wa kutolewa kwa kufukuzwa kwenye nyumba niliyokulia,
kwa watu niliojua ni wazazi wangu.” Tunda akaendelea taratibu.
“Nakumbuka
ile hali ya kuchanganyikiwa, hofu na wasiwasi nisijue huyo mwanamke anayenichukia
waziwazi, alikuwa akinipeleka wapi! Yeye ndiye alikuwa dereva, nilikaa kiti cha
nyuma na mtoto wake. Mbali na usafiri wa vibasi vya pale kijijini kututoa
kijiji kimoja kwenda kijiji kingine, sikuwahi kupanda gari aina yeyote ile.
Sikujua jinsi ya kushusha kioo cha gari au kupandisha. Na wala sikuwa nikijua
wanafunga na kufungua vipi mlango wa gari! Hilo ni kosa pia lililonifanya
nipigwe njia nzima. Kila aliporudisha mkono wake nyuma tukiwa njiani ilikuwa ni
kunifinya sana au kunipiga kofi.” Net alikuwa akisikiliza kwa makini huku
akishangaa.
“Alijawa
na hasira juu yangu, hata uso wake alionyesha. Nilishindwa kujua ni kwanini,
lakini matusi aliyokuwa akinitukana ndiyo yalinifanya baadaye nihisi labda baba
yangu alimtendea kitu kibaya sana ndio maana alinichukia kwa kiasi kile.”
“Tokea
siku ile, ndipo maisha yangu yalipobadilika kabisa, Net. Na ndio ukawa mwisho
wa kila kitu ambacho wanadamu wengine walibahatika kuwa navyo hapa duniani,
wakichezea na kudharau. Mimi ndio ukawa mwisho wangu.”
“Jina la
Tunda liliisha kabisa. Kila aliyeniona
aliniita vile anavyotaka yeye. Mama yangu mzazi aliniita majina mengi lakini
ambalo lilibaki masikioni mwangu ni ‘Paka’.
Alichukia rangi yangu, macho yangu na sauti yangu ndio ilikuwa kero kabisa,
kwani ilikuwa ikinichukua muda mrefu kidogo kutengeneza sentensi moja ya
Kiswahili, mtu akanielewa. Aliishia kuniwasha vibao vya usoni kila wakati na
kunigeuza bubu.”
“Mambo
hayakuwahi kugeuka tena, mpaka sasa wewe ndiye mtu wakwanza kupongeza kazi
ninayofanya na kunipokea jinsi nilivyo ukijua jinsi nilivyooza, lakini bado
unaniheshimu Net. Ndio maana kila ninapokuwa na wewe, najikuta sina hofu Net.
Sina sababu ya kujificha, au kujibaraguza au hata kubadili jina langu. Napata
amani ya ajabu, najua nipo na mtu anayeweza kunitazama kama binadamu mbali na
maovu yangu yote.” Machozi yakaanza kumtoka Tunda.
“Huu usingizi ninaopata nikiwa na wewe sio ninaopata nikiwa peke
yangu. Tena afadhali sasa hivi naweza kulala hata masaa machache nikijua kesho
nitaenda kazini, kitu ambacho sikuwahi kufikiria kama naweza kufanya maishani.
Wanadamu nilioishi nao wote, walihakikisha wananikandamiza na kunihubiria jinsi
nilivyo kiumbe dhaifu na siwezi kufanya chochote hapa duniani, mpaka kweli na
mimi nikaamini hivyo.” Net alikuwa akimsikiliza kwa kumuhurumia.
Akajifuta machozi.
“Ushawahi
kukaa kwenye jua kali sana mpaka ukachoka, halafu gafla ukahamishwa kwenye
kivuli tena chenye upepo mzuri? Kitu cha
kwanza utakachotamani ni maji ya kunywa ya baridi. Sio kwamba hata ukipewa soda
hutakunywa, utakunywa tu. Lakini kitakachoburudisha moyo wako ni maji pekee.
Ndivyo ilivyo kwangu. Utulivu wa akili ninaopata ukiwepo hapa na mimi,
unanifanya nilale. Ndio maana sitaki hata uniguse wakati ukiondoka, ili angalau
pakuche nikiwa katika ile hali ya utulivu akilini mwangu.” Net alianza kuelewa.
“Mama
alikupeleka wapi siku hiyo alipokutoa kwa bibi na babu kijijini?” Net akauliza
taratibu. “Ilikuwa siku ya maajabu sana kwangu siku hiyo. Alinipeleka kwa baba
yangu. Tena hata sikutambulishwa. Baada ya kushindwa kufungua mlango
aliponiambia tumefika, ilimbidi ashuke aje kunifungulia yeye. Lilikuwa nikosa
ambalo alishindwa kunisamehe. Alifungua mlango kwa hasira. Akanipiga sana,
kisha akanitupia nje ya gari huku akinifinya mdomo nisilie hata kidogo.
Alinivuta mpaka ndani ya hiyo nyumba ambayo alipofunguliwa mlango tuliingia
huku ananivuta kama mwizi, na kuniacha hapo kati kati ya sebule nikiwa
nimesimama na wenyeji wakiangalia tv. Sikuambiwa
kuwa yule ndiye baba yangu ila nilimsikia akimwambia baba, ‘nimekuletea jaluo mwenzako, sijui kabila
gani! Mtajijua wenyewe’. Kisha akaondoka na kuniacha pale.” Tunda
akajifuta machozi.
“Pale pale pakaibuka tena ugomvi kuwa sitakiwi na pale tena.
Baba alikuwa na yeye ameoa, mkewe alianzisha zogo jingine pale pale akitaka
niondolewe usiku uleule, lakini nikafanikiwa kuishi pale kwa muda wa miaka
miwili iliyokuwa migumu na iliyosaidia kuharibu akili yangu kabisa, mpaka
nilipotolewa pale nusu mfu na jirani kama nilivyotolewa nusu mfu nyumbani kwa
mpenzi wako.” Net akakunja uso.
“Mpenzi
wangu mimi?!” “Ndiyo.” “Nani mpenzi wangu!?” “Si Sera? Au mliachana?” “Sera
hakuwahi kuwa mpenzi wangu bwana.” Tunda akakunja uso kidogo. “Sisemi Samatha
yule mdogo, nasemea Sera yule mkubwa.” “Namfahamu Sera na Samatha vizuri sana.”
“Sasa mbona unakataa kama sio mpenzi wako wakati ulikuwa ukija kumuona pale
hata mara mbili kwa siku?” “Nani alikwambia nilikuwa nikimfuata Sera?” Tunda akawa
kama ameshachanganywa kidogo.
“Net
jamani!? Au umesahau?” “Nakumbuka kila kitu. Lakini sikuwa nikimfuata Sera.”
Tunda akatulia kidogo kama anayefikiria. “Kwanza wewe umejuaje kama nilikuwa
nikifika pale? Maana kila nilipokuwa nikija sikuwa nikikuona?” Net akauliza.
“Mle ndani ya ile nyumba, ulikuwa kama lulu! Zilikuwa zikianza kutajwa sifa
zako, hamtahema. Mimi mwenyewe nilikufahamu hata kabla sijakuona.” Tunda
akacheka kidogo.
“Siku ya
kwanza unakumbuka nani alikufungulia mlango?” Net akatabasamu kama anayefikiria
kidogo. “Siwezi kusahau.” “Basi ulipoingia tu na Joe, nilipokuona tu nikajua
ndio Net aliyekuwa akisifiwa mle ndani.” Net akacheka.
“Sera
alikupenda sana. Mliishia wapi?” “Kwani tulianzia wapi?” “Net!?” “Nini?” “Safari
zote zile ulizokuwa ukija pale, ukamfanya Sera achanganyikiwe! Mpaka wazazi
wake walijua mtaoana!” “Walijichanganya wenyewe tu.” “Mmmh! Siamini kama
hapakuwa na mwendelezo wa yale mahusiano. Uliwaalika mpaka nyumbani kwenu?”
“Tunda! Hebu achana na hayo. Naona wote hamkuwa mmeelewa. Kwanza nijibu kwa
nini ulikuwa unanikimbia?” “Weee! Nilipigwa marufuku mwenzio, tena kwa
kumwagiwa ndoo ya maji nikiwa nimelala.” Net akashangaa.
“Kwa
nini!?” “Wewe unacheza na wale watoto nini? Halafu walivyo washenzi, eti siku
inayofuata wewe ulinikuta naingiza godoro ndani baada ya kutoka kuanika baada
ya wao kunimwangia maji wakati nimelala, tena nakumbuka ukauliza, ‘vipi mbona kama kuna wanao hama?’. Eti
wakakwambia huwa nakojoa kitandani. Hivi uliamini?” “Mimi sio mjinga Tunda.
Nilishawasoma watu wote pale ndani, kwa muda mfupi niliwafahamu kwa asilimia
kubwa sana. Kila nilichokuwa nikiambiwa nilikuwa nikijua ni kweli ama sivyo.”
Tunda akatulia kama anayefikiria.
“Unajua
siku uliyoondoka, nilikuja pale kutaka kuongea na wewe?” Tunda alishtuka
kidogo. Akageuka nyuma na pembeni kisha akajishika kifuani. “Mimi?” “Ndiyo.”
“Unamaanisha mimi Tunda?” “Acha utundu Tunda, tupo wawili tu hapa ndani. Kwani
hawakukwambia kama nilimuomba shangazi yako kuja kesho yake, usiku ili kuzungumza
na wewe?” Tunda afikiria harakaharaka.
“Basi
wewe ndiye uliyenisababishia matatizo Net!” “Nilifanya nini?” “Kama uliwaambia
wale, ujue wewe ndio sababu kubwa yakutoka pale nusu mfu.” “Nusu mfu tena?
Wakati mimi nilipofika siku hiyo kuja kuzungumza na wewe kama nilivyowaomba,
waliniambia ulitoroka tena baada ya kuiba!” Tunda akaumia sana, Net akamuona
anaguna.
“Kwani
ilikuwaje?” “Aiii! Haina hata haja yakusimulia, haisaidii chochote.” “Mimi
nataka kujua.” “Tuache tu.” “Kwa hiyo unataka mimi nibaki na sifa yako ya
wizi?” “Nina madhambi mengi sana unayoyajua Net. Kutokuwa mwizi pekee,
hakutasafisha uozo wangu. Tuache tu.” “Siwezi kuacha kama mimi ndiye
niliyekusababishia matatizo Tunda. Nieleze kilichotokea.” Tunda akatulia
kidogo, usoni alibadilika kabisa.
“Tunda?”
Net akaita akitaka Tunda amueleze tu. Tunda akaona amuelezee tu. “Tuliamka siku
ile, shangazi akilalamika amepoteza mkufu wake wa dhahabu. Yeye na watoto wake
wote walisema mara ya mwisho waliona huo mkufu usiku uliopita wakati wanakuja
kwenu. Kwa hiyo tukabaki wezi ni mimi na Nyangeta. Haa!” Tunda akashtuka.
“Nini?” “Jamani Nyange! Hivi bado yupo?” “Sijui. Mimi mwenyewe sikurudi tena
pale.” “Kwa nini!?” Tunda akauliza kwa mshangao.
“Aaah!”
Net alitaka asitoe sababu ya msingi iliyomfanya asirudi tena nyumbani kwa kina
Sera. “Lakini hata hivyo muda wangu wa kurudi chuo ulikuwa umeshafika.
Niliondoka nchini.” “Shule iliisha sasa?” “Nashukuru Mungu iliisha. Niambie
nini kilitokea.” “Kuhusu nini tena?” “Sababu ya kukutoa pale nusu mfu.”
“Husahau!?” “Hilo ndilo tatizo langu Tunda. Sisahu na nikikusudia kufanya jambo
fulani, ni lazima nifanikishe. Hata kama lina gharama kubwa kiasi gani, lazima
nilitimize. Mpaka bibi yangu huwa ananihurumia.” “Lakini ndio maana umefanikiwa
Net” “Nimefanikiwa kwenye nini?” “Ona bishara ulizo nazo.” Net akatabasamu.
“Chakwanza nataka uelewe zile ni biashara za mama
yangu. Mimi ni mwajiriwa kama wewe tu. Nampa tu mawazo kama hivi unavyonishauri
mimi, na yeye anachagua kipi chakutendea kazi, basi.” “Lakini kwa hapo ulipo Net,
ni kama huna kitu unataka maishani.” Net akatabasamu akabaki akifikiria kidogo.
“Nikikwambia pesa hainunui kila kitu hapa duniani,
huwezi kuniamini.” “Mimi tena? Naamini sana tu Net. Nimezihangaikia hizo pesa
jamani! Sitakaa nikasahau maishani. Nilidhani nikiwa na maisha fulani ndio
itanisaidia kurudisha ile hali ya kabla sijatolewa kwa bibi yangu kwa mara ya
kwanza, lakini wapi Net! Nimetafuta kurudisha ile hali kwa mateso sana, lakini
sijafanikiwa. Nimeishia kudhalilika tu.” Tunda aliongea kinyonge.
“Sijui nilipatwa na nini!? Nilikuwa kama mbwa, tena
mbwa wa uswahilini. Mchafu kuliko, sijui nini!” Tunda akatulia kidogo. Net naye
kimya. Hapo hakuongeza.
“Turudi kwenye swali lako Net.” “Ehe!” Tunda akajifuta machozi. “Kweli wewe
king’ang’anizi.” “Sitaondoka leo mpaka nijue.” “Haya bwana. Basi yule Mzee
akaanza kutukaba mimi na Nyange, tutoe huo mkufu wa mkewe.” Tunda akatulia
kidogo.
“Sikukuzwa au kulelewa kwenye mazingira ya
kusikilizwa Net, kwa hiyo sijui kabisa kujitetea. Vile mtu anavyosema juu
yangu, huwa mara nyingi inabaki vile vile. Kwa kuwa siwezi kukanusha, hasa pale
ninaposhutumiwa moja kwa moja. Nakuwa kama ninapatwa na ganzi mwili mzima.
Mwenzangu Nyangeta alijitetea haraka haraka akapona. Mimi nikabaki kama bubu.
Basi pale mimi ndio nikaonekana mwizi moja kwa moja.”
“Yule Mzee akaamuru iletwe mifuko yangu ya nguo.
Maana nilikuwa na mifuko miwili ya plastiki, ndio nilikuwa nikiwekea vitu
vyangu vyote. Hatukuruhusiwa kutumia makabati ya mle ndani chumbani.” “Kwa
nini!?” Tunda akacheka kidogo. “Mimi waliniambia wanaogopa naweza kusababisha
wadudu kwenye hayo makabati ya ukutani. Yalikuwa yamejengewa kwenye ukuta.
Mazuri kweli. Lakini yalikuwa yakifungwa kabisa na funguo ambazo alikuwa
akitunza shangazi. Kwa hiyo tukawa tunaweka vitu vyetu kwenye mifuko tu ya
plastiki.” Net alibaki na mshangao.
“Basi mifuko yangu ikaletwa. Walipomwaga chini vitu
vyangu ili kukagua, ule mkufu wa shangazi si ukaanguka kutoka kwenye huo mfuko
wangu! Tena mfuko wa kwanza tu, hata hawakwenda wa pili. Net! Nilipigwa mimi.
Nafikiri Mungu alinihurumia. Maana alinipiga sehemu iliyonisaidia kupoteza
fahamu, sikujua kinachoendelea mpaka nilipopata fahamu nikiwa hospitalini.”
“Nilijua nilipigwa sana kutokana na maumivu
niliyokuwa nayo, na jinsi nilivyokuwa nimepasuka. Nilipasuka hapa juu ya macho,
midomo, mbavu zilivunjika. Mkono huu ulivunjika, mpaka mifupa ilikuwa
ikionekana kwa nje kuwa imetengana. Bega lilitenguka.”
“Nilikaa hospitalini
zaidi ya mwezi sababu ya kuvuja damu kwenye mbavu, na kutobolewa kuwekwa vyuma,
kama mshikaki. Halafu sikuwa na pakwenda. Kila mahali nimefukuzwa. Ikabidi
kuomba kuendelea kukaa pale pale hospitalini mpaka nipone. Mtu aliyekuwepo hapo kuniuguza ni baba, naye alifungwa
nikiwa bado hospitalini.” Tunda alinyamaza na kufuta machozi.
“Na yeye ni mtu mwingine aliyenikubali vile
nilivyo. Mpaka nilikuwa namshangaa. Alikuwa akipewa habari zangu mbaya tupu,
lakini wakati wote alinithamini. Nililia sana baada ya kumkuta tena kwa mara ya
pili pembeni ya kitanda changu hospitalini.” “Mara ya pili?” Net akauliza.
“Mara ya kwanza ni pale mama aliponiacha
hospitalini baada ya kunitoa mimba. Nilikuwa peke yangu na barua aliyokuwa
ameniachia niisome mara baada ya kuzinduka usingizini, akinitaarifu yeye na
ndugu zake wote hawataki kuniona tena, kwa kosa la kuwa na mahusiano na mumewe.
Lakini hata baba alipoambiwa hilo kosa langu, alikuja kuniuguza mpaka
nikatoka.” Tunda alitulia akainama kwa
muda.
Kisha akaendelea. “Na mara ya pili nilizinduka hospitalini
nikamkuta baba tu, tena hata hapo nikiwa ninatuhumiwa za wizi wa huo mkufu wa
shangazi. Lakini mara zote hizo baba amekuwa akinihudumia bila shida. Siku
aliyokuwa ananiaga kuwa anaweza asirudi tena, aliniambia nisiwahi kufikiri kama mimi ni mtoto wa bahati mbaya. Alinieleza
kuanzia mwanzo wa kuzaliwa kwangu mpaka nilipoishia kijijini.”
“Ilikuwaje?” Tunda alimsimulia Net kila kitu juu ya
baba yake na mama yake, mpaka alipoenda kutelekezwa kijijini. “Daah!
Unahistoria ngumu Tunda!” “Lakini wewe pia ulichangia Net!” Net akaanza
kucheka. “Jamani mimi nilifanyaje?” “Nikifikiria juu ya kile kisa cha mkufu wa
shangazi, sasa hivi ndio naelewa kuwa ni mpango shangazi alifanya na wanae.
Walimtumia yule baba kuniadhibu bila yule baba mwenyewe kujua kinachoendelea.”
Net hakuwa ameelewa vizuri.
“Ukweli kile kitendo cha kuwa na mahusiano na mume
wa mama yangu kilinipotezea uaminifu kwa watu wengi sana. Hakuna aliyeniamini
na mumewe au hata marafiki zao wa kiume. Shangazi mwenyewe alinipiga marufuku
hata kupita pale sebuleni mumewe akiwepo. Sasa na wewe walijua kabisa ungemuoa
Sera, kwa hiyo hawakutaka mimi niwe hata nakuona. Waliniambia kila unapokuja
niwe natoka nje kabisa, nisirudi mpaka wewe utakapokuwa umeondoka.” Hapo Net
akawa ameelewa.
“Samahani sana Tunda. Sikukusudia kukusababishia
matatizo.” “Wala usijisikie vibaya Net. Nilikuwa navuna nilichopanda. Nilikuwa
nalipa uovu wangu.” “Sio kwa njia hiyo Tunda.” Tunda akacheka tena taratibu,
huku akifikiria.
Akawa kama amekumbuka. “Ulitaka kuniambia nini Net?”
Tunda alinyanyua uso, nakumuuliza. “Tuache tu. Sasa hivi haina maana tena.”
“Kwa nini unasema hivyo!?” “Tunda wa wakati ule niliyetaka kuzungumza naye sio
Tunda huyu wa sasa. Umebadilika sana Tunda. Hata nikikwambia sasa hivi,
haitaleta maana tena.” Tunda aliumia sana moyoni.
“Naelewa Net. Naelewa kabisa, wala sikatai. Mimi
mwenyewe wakati mwingine sijitambui kabisa. Nahisi ni kama mtu ninayeangalia
watu wengi tofauti tofauti ndani ya mwili mmoja wakiishi kwa kupeana zamu. Mimi
mwenyewe sijitambui. Nimepotea kabisa. Hata sasa hivi hapa sijui anayeishi kwa
kutumia huu mwili wangu ni nani! Kuna umbali mkubwa sana kati yangu mimi
binafsi na watu wote unaowafahamu kupitia huu mwili wangu. Kuna mambo nilikuwa
nikifanya mpaka mimi mwenyewe nilikuwa naogopa Net! Nilikuwa nikirudi nyumbani
kwangu nashindwa hata kulala kwa mshtuko.” Tunda akaendelea kuongea huku
akivuta kumbukumbu taratibu.
“Ni kweli mwanadamu ana uwezo mkubwa sana. Siku
chache zilizopita kama mtu angeniambia wale kina Anna, Judy, Irini, sijui Pamela,
Nancy, Mwajuma, Latifa, Fina, Lina
wanaweza kuja kuwa mimi nikakaa ofisini nikafanya kitu kinachoweza kuonekana,
nisingekubali. Nilishapotea kabisa katika ulimwengu mingi tofauti, tofauti.”
Tunda aliongea taratibu huku ameinama akichezea vidole vyake.
“Sikuwahi kujua kama kuna siku naweza kula chakula
kwa pesa ninayoweza kutengeneza kupitia kuajiriwa kihalali na si kwa kutumia
kulala na watu, tena wengine walevi, wavuta bangi, wengine wachafu huwezi hata
kuvumilia harufu zao, nisingeamini. Nashindwa kujielewa kama huyu tena sasa
hivi kwenye huu mwili wangu kama ni mtu mwingine kati ya wale watu wengi ambao
wanaishi kwenye huu mwili wangu au la!”
“Nikiwa peke yangu naogopa nasema itakuwaje wale
watu wengine kina Nancy wakaamua kurudi tena, wakaishi? Nina hofu ya kurudia
yale maisha Net. Pesa mnayonilipa wewe na mama yako kwa kuwafanyia kazi mwezi
mzima, nilikuwa na uwezo wakuitengeneza hata ndani ya siku mbili, au moja.
Inategemea na mtu niliye naye. Lakini siyo maisha ninayotamani kuja kurudia
Net. Yanatisha.” “Unao uwezo wakutorudia tena Tunda.” “Sidhani kama ni uamuzi
wangu Net. Sijui.” “Kwa nini unasema hivyo?” Tunda alifikiria kidogo kisha
akacheka na kuguna.
“Unajua watu wote wananilaumu kwa nini nililala na
mume wa mama yangu. Najua hata wewe utakuwa huelewi. Lakini hakuna mtu hata
mmoja aliyewahi kuniuliza ilikuwaje! Hata baba mwenyewe hakuniuliza. Kila mtu
ananilaumu na kunishangaa.” “Ilikuwaje Tunda?” “Kwa
nini unaniuliza leo Net, wakati ulinifahamu muda mrefu tu?” Tunda
akauliza kwa upole huku akijifuta machozi.
“Kumbuka hatufahamiani Tunda. Nimekufahamu kwa
kutambulishwa na watu. Na kote nimekuwa nikitambulishwa majina tofauti tofauti,
nimeamua kubaki na la Tunda, kwa kuwa ndilo nililotambulishwa na ndugu zako. Na
kila nilipokutana na wewe nilikuta upo kwenye matatizo makubwa sana, au tuseme
mazingira ambayo hayakuniruhusu hata kukusalimia kwa kukushika mkono. Nina
habari zako nyingi na nasikitika zote ni mbaya na ni za kuogopesha.” Net
akaendelea.
“Sijui
nauliza nini naacha nini? Nashindwa naanzia salamu kwa kukushika mkono kwanza
ndipo nikuulize jina lako, au nijipe muda labda ipo siku nitajua wewe ni nani!
Nina hofu sijui mwisho wa yote hayo naishia kumfahamu Tunda, au Judy! Yeyote
yule sasa hivi aliyepo ndani yako sikuwa na ujasiri wa kukimbilia
kukuuliza ilikuwaje ukawa na mahusiano
na baba yako wa kambo, wakati nina maswali makubwa sana na ya msingi nilitaka
kujibiwa kabla ya swali kama hili ambalo nilijua nikipata majibu ya maswali ya
msingi, mengine yangejijibu yenyewe.” Net akaendelea.
“Huwa sipendi na ninahofia sana kufikia mwisho wa
maamuzi ya jambo lolote lile maishani mwangu, kwa kuwa ninatatizo la kutosahau
na huwa ni mgumu sana kurudi nyuma. Siwezi na sijawahi. Nikifika mwisho wa
jambo, nikakubali kuwa hapo ni mwisho ujue hakuna mwanadamu mwingine anayeweza
isipokuwa Mungu ameingilia kati. Kwa kuwa huwa natumia kila kitu Mungu
alichonipa katika kukabiliana na mambo yangu, na huwa ni mvumilivu sana.”
“Mpaka mimi nikikwambia nimefika mwisho, ujue
hakuna mwanadamu angeweza kuvumilia. Ndio maana naogopa sana kufika kwenye
kumuhukumu mtu. Kama ni mwanadamu, nataka kumjua si kwa maneno yake tu bali
nataka nimfahamu vile alivyo kwa kuishi naye. Nione na kujua jinsi alipopita
mpaka akafika hapo, na kujaribu kuangalia anatumia vipi nafasi ya pili ambayo
Mungu amempa? Hapo ndipo nachora mstari, si vinginevyo.” Tunda alikuwa ametulia
akimsikiliza Net.
“Leo nimepata ujasiri wa kukuliza kwa kuwa kwanza
nimeona umekuwa tayari wewe mwenyewe kuongea. Nimehisi umeniamini, kitu
kilichonifurahisha. Sikutaka mimi nigeuke kuwa hakimu wako, kukuhoji. Nilijua
ipo siku kama utataka, basi utazungumza na mimi. Lakini sikutaka mimi ndio niwe
naanza kukukera na maswali, nilijua utakosa raha. Ndio maana nilikuwa nikinyamaza
kabisa.” “Asante Net. Asante sana.” Tunda akajifuta
machozi, nakujiona mdogo zaidi. Aliona vile Net alivyokuwa akimfikiria bila
majibu. Akatamani kujua mawazo yake juu yake, lakini Net alionekana ni mtu
makini sana. Hakuwa mropokaji hata kidogo na alikuwa makini sana kwa kila
anachoongea.
“Tunda!” “Abee!” “Nakusikiliza.” Ilikuwa ni mtu wa
kwanza maishani mwake kutaka kumsikiliza Tunda, bila hukumu. Tena mtu wa maana,
msomi, pesa ipo na tena mwenye heshima kwenye jamii! Japokuwa alijua uozo wake
tena kwa kushuhudia, lakini bado alimuonyesha kutaka kumsikiliza. Tunda
aliinama kwa muda akaficha uso wake nakuanza kulia kwa uchungu sana.
Alilia sana hapo mbele ya Net nakushindwa
kujisaidia. Kimya kimya ila kwa kwikwi. Aliruhusu maumivu yote aliyokuwa
ameyaficha moyoni mwake akivumilia akijua kesho itakuwa nafuu, aliyatoa siku
hiyo. Alilia bila kunyamaza. Picha ya mapito yake yote tokea utoto mpaka
siku Net anamtoa kwenye mvua na radi
ilimjia, na kuendelea kulia. Alipoona anashindwa kunyamaza akaamua kuingia
bafuni kuoga.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alitoka
akiwa amevaa nguo zake za kulalia nzuri na huku amejifunika shuka. “Nasikia
baridi sana. Naomba nilale tutaongea wakati mwingine.” Tunda akapanda kitandani
na kujifunika blangeti. Ulikuwa msimu wa baridi kali sana jijini Arusha.
“Naweza kukusubiri mpaka utakapo lala.” Net akasogea pale kitandani akakaa
pembeni yake. Akabaki akimwangalia Tunda kwa utulivu na macho yake yaliyokuwa
yakimpeleka kasi Sera, binamu wa Tunda. Tunda alikuwa ndani ya mablangeti
akitetemeka baridi.
Net akavuta
blangeti vizuri na kumfunika zaidi. Tunda aliendelea kujikunja ndani ya lile
blangeti huku akificha kila kiongo chake ndani, akabakiza uso tu. “Asante.” Net
alitoa tabasamu. “Ninayo machine ndogo ya joto, {Space Heater} pale nyumbani,
kesho nitakuletea.” “Na wewe utatumia nini?” “Mimi sio muoga wa baridi kama
wewe. Jione unavyo tetemeka.” Tunda akatabasamu.
“Unawasiliana
na mama?” Net akauliza. “Nilikwambia jinsi alivyoniambia Net. Mama alisema
nisikanyage tena nyumbani kwake. Hata hivyo hatukuwahi kuwa na mahusiano yeyote
na mama hata tulivyokuwa tukiishi pamoja. Nilimsaidia sana kumlelea yule mtoto
wake wa pili, kwa hiyo hapo ilimbidi awe akizungumza na mimi, kunipa maelekezo
ya mtoto wake na si vinginevyo. Na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyonifanya niwe
karibu na mumewe.” Tunda akatulia kidogo.
“Yeye
alikuwa akifanya nini?” “Ni nesi. Nilimuacha akifanya kazi katika hospitali ya
Muhimbili lakini pia alikuwa na miradi iliyokuwa ikimfanya hatulii nyumbani.
Alikuwa akiingia kazini mida tofauti tofauti. Na kama hatakuwepo kazini, basi
yupo kwenye biashara au miradi yake. Halafu walikuwa pia na msichana wa kazi
naye alikuwa akiishi humo humo ndani. Ila alikuwa muhuni sana. Hatulii
ndani. Mama alipokuwa akiondoka na yeye
alikuwa akiondoka, anaaga labda anaenda kusuka au dukani. Na akitoka hapo
kurudi ni majaliwa.”
“Sasa
huyo baba hakuwa akimuuliza?” Net akaendelea kudodosa japo alishaambiwa
wataendelea wakati mwingine. Ila alikusudia kujibiwa usiku huo. Akaendeleza
taratibu. “Hapana. Ndio muda na yeye alikuwa akiusubiri kwa hamu sana. Kwani
ndio tulikuwa tukibaki naye. Mimi na yeye tu.” Tunda akatulia kidogo.
“Hatukuanzia
kwenye kufanya mapenzi moja kwa moja! Alihakikisha anajenga mazoea ambayo
hakuna mtu alimtilia mashaka. Alimuonyesha mama kuwa ananipenda kama mtoto
wake. Kutoka katika mateso makali ya mama wa kambo, nikaangukia kwenye mikono
ya baba wa kambo aliyekuwa akinipakata na kunitekenya wakati wote.”
“Nilikwambia
nilitolewa kwa baba nikiwa nusu mfu kwa kupigwa. Baba alikuwa na mtoto mwingine
aliyekuwa akiitwa Chale. Yule mtoto alikuwa mwizi Net, hawezi kujisaidia.
Alikuwa akiiba kila pesa anayoona mbele yake. Sasa mara ya mwisho aliiba pesa
kwenye pochi ya mama yake, akanisingizia mimi. Na yule mama alikuwa akijua
kupiga, na ana mkono mwepesi sana. Basi. Alinipiga siku hiyo zaidi ya siku
zote, wakaenda kunitupa nje, majirani wakanipeleka hospitalini. Bibi akaja
kunichukua, nakunirudisha kijijini.” Tunda akatulia kidogo.
“Kosa
alilolifanya bibi, akiwa na nia nzuri, akampigia simu huyo mume wa mama ambaye
hata hakuwa akijua kama mama ana mtoto mwingine.” “Kwani hamkuwahi kuonana?”
Net akauliza.
“Alishawahi
kufika kijijini wakati anamlipia mahari mama, akanitambulisha kama mimi ni
mdogo wake.” Net akashangaa sana. “Basi. Bibi akanitambulisha kwa yule baba
mbele ya mama, akitaka wawe wanatuma pesa za matumizi angalau kila mwezi. Chakushangaza kila mtu mpaka mama, yule baba akanipokea
kwa upendo. Akataka nirudi nao mjini ili wanisomeshe.” Tunda akajifuta
machozi.
“Huwezi
amini hayo mapokezi yake! Alikuwa akinipenda sana. Akiona mama ananigombesha,
basi yeye ananibembeleza na kunitetea hata kwa mama, akimuelewesha kuwa mimi
bado ni mdogo. Natakiwa nifundishwe. Yale mateso ya kwa mama wa kambo, huku
ikawa faraja ya baba wa kambo. Nilikuwa nikivalishwa vizuri. Vyakula vya kila
namna ananinunulia. Akiona kama kuna chakula ambacho yeye hajakipenda mle
ndani, basi alikuwa akitutoa na Tom, mtoto wao mkubwa, kwenda kula nje. Chips
yai na kuku.”
“Wakati
mwingine alikuwa akitupeleka sehemu tofauti tofauti zakucheza. Mara nyingi mida
ya jioni alikuwa akitupeleka kwenye sehemu zinazo uzwa Icecream. Hata kama ni
siku za shule. Anatoka kutuchukua shuleni, anatupitishia mahali kula au kupata
icecream. Na ilikuwa hivi, kama dereva hakuwa akitufuata kuturudisha nyumbani,
basi ni yeye mwenyewe anatufuata. Tulikuwa tukisoma shule yakulipia, kwa hiyo
kama mzazi alitaka watoto wakae zaidi, unaongeza pesa, mnakaa mpaka saa 12
jioni. Hapo mtasaidiwa kusoma na kunakuwa na michezo tofauti tofauti.” Tunda
akaendelea.
“Sasa
kwa kuwa Tom yeye alikuwa mtundu sana, na alikuwa akicheza mpira wakati mwingi,
basi kila alipokuwa akiingia kwenye gari, alikuwa akiishia kulala njia nzima
wakati tunarudishwa nyumbani. Na hapo yule baba ndipo alipokuwa akipata nafasi
nyingine nzuri ya kunichezea ipasavyo. Kumbuka nilikuwa darasa la nne, sio
mkubwa sana, lakini nilikuwa nikielewa kiasi. Mwanzoni nilikuwa nikifikiri ni
mchezo aliokuwa akicheza akitutekenya mimi na Tom hata mbele ya mama, lakini
niliona mimi inaanza kuwa tofauti.”
“Akijua
jioni hiyo mama haingii kazini, atalala nyumbani, basi lazima atakuja kutufuata
yeye shuleni. Akijiridhisha Tom amelala kabisa kwenye gari, alikuwa
akisimamisha gari pembeni ya barabara na kuniambia nifungue mkanda niruke kiti cha
mbele, kisha anaanza kunichezea. Alianza kwa kunisifia nimeanza kuwa mkubwa
nimuonyeshe matiti yangu huku akinitekenya na kujifanya anashika juu ya gauni
na kucheka cheka.”
“Siku
ambazo tupo nyumbani mama hayupo, akawa anataka niwe nakwenda kuangalia tv
chumbani kwake. Na kwa kuwa nilikuwa nikifeli sana shuleni, basi alitaka niwe
nafanya kazi za shule pembeni yake. Kumbuka nilitoka kijijini sijui kuzungumza
hata Kiswahili. Nikapelekwa kwa baba, nikaishi huko miaka miwili ya mateso.
Darasani wanafundisha Kiswahili kitupu na kingereza. Nimetolewa hapo darasa la
nne, sijajifunza chochote kwa hiyo miaka miwili. Nikahamishiwa kwa mama,
nikapelekwa shule ya kingereza kitupu. Hakuna hata wakumuomba maji ya kunywa
kwa kilugha au kiswahili. Nikajua kuongea kingereza kwa mawasiliano tu, lakini
hakuna ninachoeleweka darasani. Kumbuka hapo nipo darasa la 4 ambalo ilibidi
nirudie, sababu kwanza sikufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nne kuingia la tano kule kwa baba. Mkewe alinipiga
na kunivunja mkono huu wa kulia.” “Tunda!” Net akazidi kushangaa.
“Kweli
Net. Mama Chale au mke wa baba, alikuwa mama wa nyumbani, halafu baba yeye
anakwenda kazini asubuhi mpaka usiku, hapo bado safari za kikazi za baba. Kwa
hiyo nikaishia kulelewa na mama wa kambo, huyo mama Chale. Alikuwa akinitesa
yule mama, siwezi kusoma wala kufikiria. Kwenda shule ni siku ambazo anaamua
yeye. Mateso, akili ikawa haitulii kabisa. Nilikuwa kama mwehu kwa hofu.
Akinikuta nimekaa sehemu, kosa. Atanipiga wee na kunipa kazi. Nikifanya
asivyopenda yeye, pia kosa. Atanipiga tena. Wenzangu walifanya mitihani ya
darasa la nne, mimi mkono umefugwa POP kwa kipigo.” “Pole sana Tunda.”
“Asante.
Haya, sasa huku kwa mama nako sina nilichokuwa nikielewa. Nafeli kwenye hiyo
shule ya kingereza kitupu. Ndio yule baba naona akapata mwanya huo. Akamwambia
mama yeye atakuwa akinisimamia masomo. Yaani ni kama alikuwa akijitengenezea
njia yakutoshtukiwa. Basi ikawa inajulikana kwamba kila nikitoka shule, lazima
baba anisimamie kufanya homework zangu.”
“Hapo
sasa ikawa inategemea na ratiba ya mama au alipo yule msichana wa kazi. Inaweza
kuwa sebuleni kama tupo mimi na yeye tu au chumbani kwake. Kama nilivyokwambia.
Tom alipenda sana mpira. Kila alipokuwa akitoka shule, alikuwa akiingia mtaani
kucheza. Yeye hakuhimizwa kufanya homework. Alikuwa anataka awe anatoka hapo
ili atupishe. Na yule msichana ni kama nilivyokwambia kuwepo kwake nyumbani ni
mpaka ajue mama yupo au anakaribia kurudi nyumbani.”
“Na ikitokea msichana wa kazi
yupo hapo nyumbani, basi hiyo homework tunaenda kufanya chumbani kwao. Eti
nikiwa na elimu ya darasa la pili ya kijijini, unipe homework niliyofundishwa
kwa lugha ya kingereza darasani! Mimi niliyekuwa nikizungumza kipogolo tu! Hata
Kiswahili sikuwa naongea vizuri. Kwanza niseme sikuwa nikikijua. Nilikwenda
kukijua kule nilipopelekwa kwa baba. Nilijifunza Kiswahili kwa kupigwa.
Alidhani ni kiburi, kumbe sikuwa na muelewa. Ndio msichana wa kazi akamwambia
simuelewi. Ndio kipigo kikageuka kuwa mimi ni mjinga, mzito kuelewa.” “Jamani!”
Net akashangaa.
“Sasa
eti kwa hali hiyo nikaanza hiyo shule ya kingereza, bila msaada wa mtu. Mama ni
mkali, baba anamalengo yake. Usifikiri hata hiyo homework basi alikuwa anania
nifanye?” “Hakuwa akikusaidia?” “Hata kidogo Net. Ukitukuta chumbani, ujue
mikono yake kama haipo kwenye maziwa yangu, basi ataniambia nilale kama
naandika. Yaani nilale kifudifudi. Niweke daftari mbele. Yeye atakaa huko nyuma
yangu. Atanifunua gauni mpaka kiunoni, ataanza kunichezea. Anakwambia
usihangaike tulia tu. Atakuchezea hapo, wakati mwingine anaweza akanitoa hata
chupi kabisa ananichezea tu.”
“Mwanzoni
hakuwa akiniingilia. Ananichezea tu. Ila alikuwa anapenda sana sauti yangu na
nimwangalie. Kwa hiyo alipokuwa akifika juu sana, ananiambia nimwite dad, dad,
mpaka amalize. Hapo sasa anakuwa amenitoa kitandani, amenipakata. Mikono kwenye
sehemu za chupi nyuma. Ananiminya minya.” Tunda aliogopa kusema makalio. Lakini
Net akaelewa.
“Halafu
huku ananinyonya tumaziwa twangu. Basi hapo utamwita dad taratibu huku
anakuchezea mpaka anamaliza. Na usifikiri anamaliza ndio inakuwa basi. Anaweza
kwenda kuoga. Anakwambia endelea na kazi za shule wakati akioga. Niambie Net,
hapo utasoma tena?” “Huwezi. Pole Tunda.” “Nilikuwa nashindwa. Hasira. Na akitoka kuoga anapumzika kidogo, na mikono
yake anapopumzika inakuwa mwilini mwako. Akikuvua nguo ya ndani, ujue hutaivaa
tena mpaka akuruhusu utoke hapo chumbani kwake. Na ujue hapo sio kitu cha muda
mfupi. Ni mpaka aridhike kweli kweli.” Tunda akajifuta machozi.
“Akaanza
kuzoea ile tabia. Baadaye akaanza kuniita usiku chumbani kwake wakati watu wote
wamelala, mama yupo kazini, kisha anavua nguo na kunifundisha vitu vya
kumfanyia. Nilipomwambia naogopa, aliniambia vile mama yangu asivyonipenda,
hataki niwepo pale, yeye ndiye aliyenitoa kijijini na anauwezo wakunirudisha
kwa baba yangu kama sitamfurahisha.”
“Akawa
ananiambi kukaa kwangu pale, kunategemea na kumfurahisha kwangu. Mama alikuwa
akijua kunitukana Net! Bila aibu wala huruma, hata mbele za watu alikuwa
akinitukana. Ndio ikawa silaha ya yule baba Tom. Akawa ananikumbusha vile
ambavyo mama yangu hanipendi. Na vile nilivyoteswa kule kwa baba yangu. Akawa
ananiambia yeye ananipenda. Hata hayo macho mama anayoyaita ni ya paka na
kuyachukia pamoja na weusi wangu, yeye anavipenda ndio maana anapenda
nimwangalie na nimwite dad.”
“Aliniahidi
kunipa vitu vingi, kama nikimfanyia kile anachotaka na kweli alikuwa
akininunulia vitu. Basi. Nikaanza kujifunza jinsi ya kumfanyia anachotaka. Sina
mtu wa kuniuliza hata ninaendeleaje! Hakuna anayenitizama usoni kama nina
furaha au la. Maisha yangu yakawa ni huyo baba tu. Ndiye anayejua kula yangu,
soma, na vaa. Furaha yangu ikawa inategemeana na kumridhisha. Na kweli, akilala
ukiwa umemridhisha, utafurahia jinsi anavyokuwa mstaarabu.”
“Kazi
yangu ikawa ni yeye tu. Nimejawa hofu na wasiwasi wakati wote. Alianza
kunizoeza kumzoea kumtizama akiwa uchi. Akanifundisha mwili wake na viungo
vyake ili kuweza kuvichezea, na kumfurahisha. Na mbaya zaidi hakuwa akitosheka.
Ukidhani umemaliza, anakwambia unamwamsha zaidi. Labda macho au sauti yangu
ndivyo vinamsababisha asitosheke. Hapo inabidi kuanza upya.”
“Maisha
yangu kielimu yakawekwa pembeni kabisa. Nikageuka faraja yake. Nikiingia
chumbani kufanya homework, anafunga mlango, ananitoa nguo, na yeye anatoa nguo,
tv inawashwa kwa sauti ya juu, kazi inaanza mpaka dada aje agonge kuwa chakula
kipo tayari. Hapo ndio anatumwa kwenda kumfuata Tom huko anakocheza mtaani, ili
aje aoge, ale, alale.”
“Na
usifikiri atakuacha usiku ulale kama mama hayupo?” “Anataka mlale naye!?” Net
akauliza kwa mshangao. “Alikuwa anaanza hivi. Nakwenda kulala kama kawaida.
Tulikuwa tunatumia chumba kimoja na Tom. Tom akisha lala, anakuja kuniamsha.
Tena wakati mwingine ananibeba nikiwa nimelala. Akishanifikisha kitandani
kwake, naweza kushtuka kiwa ananivua nguo au anakunyonya sehemu ambayo lazima
uamke tu.”
“Ukishaamka
tu, anataka uanze kumchezea yeye mpaka aridhike. Na usifikiri ni mchezo wa
masaa mawili au ataridhika kwa safari moja! Hapana. Kwa hiyo alikuwa akinimbia
niendelee mpaka nikimuona amelala, nimsafishe, ndipo na mimi nirudi chumbani
kwangu. Haya, akiwa amekwenda muda mfupi usiku, ujue lazima asubuhi atakuja
kuniamsha tena, nimfanyie kabla hajakwenda kazini na mimi hajanipeleka shule.”
“Ikawa
ndio mtindo huo. Mama akiwepo nyumbani week mbili tatu mfululizo, alikuwa
akitutoa mimi na Tom kwenda kutembea na njiani nilimfanyia hivyo. Au siku za
jumamosi ambazo mama yupo nyumbani, alianzisha tuition ambayo hata sikuwa
nikienda. Alimwambia mama amenianzishia ili niwe nafundishwa inisaidie kuelewa
zaidi. Basi, jumamosi yeye hakuwa akienda kazini. Alikuwa ananichukua, kama
hatutaenda ofisini kwake, anaweza hata kunitafutia nyumba za kulala wageni
niende nikamchezee huko mpaka jioni, ndio ananirudisha nyumbani.” Tunda akaanza
kulia.
“Nilikuwa nachoka
Net, sina jinsi nikakwambia ukaelewa.” “Pole Tunda.” “Unachoka mwili mzima. Hulali vizuri. Sehemu pekee
yakupumzika ni shuleni. Na ukifika hapo darasani kwa kuwa sielewi hata
wanachozungumza, basi nikulala tu. Ukumbuke hapo labda niliamshwa kwenye
alfajiri sana ili kumchezea kabla hatujatoka nyumbani. Haya, unaingia darasani
umechoka, na hapo unajua jioni akija kukuchukua kazi inaanza upya. Kwa hiyo
darasani ikawa ndio kama kitanda. Sikuwa nikielewa chochote kwa usingizi na
hofu.” Tunda alitulia kidogo.
“Nilipofika
darasa la saba wakati mama amejifungua, alikwenda kwa bibi kama likizo ya
uzazi. Mbaya zaidi kwangu, alikwenda na yule msichana wa kazi. Kwa hiyo
tukabakia mimi, Tom, yeye na kijana wa kazi ambaye alikuwa akilala kwenye vyumba
vya nje. Hapo ndipo niligeuka kuwa mke wa yule baba kihalali. Kila Tom
alipopitiwa na usingizi, alikuja kunitoa chumbani na kunihamishia chumbani
kwake, na ndipo kipindi hicho alipofanya majaribio ya kuniingilia mpaka
alipofanikiwa.”
“Haikuwa kazi ya siku moja Net. Ilinichukua miezi kuja kuweza,
na kumudu bila maumivu. Kwa kuwa alikuwa baba mkubwa kimaumbile, usitake kujua
maumivu yake.” “Mama yako hakuwahi hata kuhisi!?” Net aliuliza akiwa
anamaumivu, mpaka uso ulikuwa mwekundu.
“Nilikwambia
mama yangu hakuwa na muda na mimi, Net. Hata hivyo alikuwa busy sana na kazi na
biashara zake nyingine. Na yule mzee alikuwa akiniuguza kwa makini sana. Yeye
ndiye alikuwa akitupeleka shule kwa hiyo kabla hajanishusha alihakikisha
ananipa dawa kali sana zakuzuia maumivu. Kwa hiyo sikuwa nikiishi kwa maumivu,
ni pale tu wakati ananifanyia, na labda nikiwa najisaidia. Napo mwanzoni
alikuwa akinipaka mafuta. Na akawa ananiambia kila nikioga, nikakikishe napaka
mafuta huko chini ili pasikauke, au nisiumie wakati najisaidia. Basi. Mchezo
huo ukaendelea.”
“Nilipozoea
na yeye akanogewa, akazua ugonjwa ambao ukawa unajulikana pale shuleni. Basi
anaweza kuja hata katikati ya muda wa shule, ananiombea ruhusa kuwa ananipeleka
kwa daktari wangu. Na ndio akaeleza huo ugonjwa ndio unaosababisha niwe nalala
sana darasani na kuwa nikifeli vile. Basi walimu wote wakanichukulia kama nina
matatizo.” “Haiwezekani Tunda!” Net akashangaa sana.
“Kweli
Net. Basi, akawa anakuja kunichukua. Nakwenda naye alipopaandaa yeye.
Atanitumia mpaka achoke au muda wa kwenda kumchukua na Tom. Ndio tunamchukua
Tom, na kurudi nyumbani. Alinifundisha kumfanyia hapo hapo kwenye gari. Kwa
hiyo anaweza kuja mida ya mchana. Wakati wa chakula. Anakuita nje, unaenda
kumfanyia kwenye gari. Alikuwa na gari kubwa. Vioo vya nyuma alivifanya vikawa
kama silver kwa nje. Inawakaa. Huwezi kuona ndani. Basi. Mnahamia kiti cha
nyuma. Unamuhudumia, akiridhika, narudi darasani na yeye anarudi zake kazini
mpaka tena jioni. Hayo yakawa maisha yangu. Sasa hebu fikiria utoke kufanya
uchafu kama huo, unarudi darasani, hapo utaelewa nini?” “Huwezi. Pole sana
Tunda.”
“Mchezo
wake ukaendelea hivyohivyo mpaka nikaja kuvunja ungo. Na yule baba alikuwa
hawezi kusubiri Net. Hajui siku za hatari zakushika mimba au siku salama. Yeye
anataka kila wakati na ndipo nikapata na hiyo mimba. Kila nilipokuwa
nikimwambia naogopa, au nikimsihi tuache huo mchezo tutakuja kukamatwa, alikuwa
akiniambia hataweza kuacha tena, na nisiwe na wasiwasi hata mama akitukamata,
atanitafutia pakuishi nitakuwa na maisha mazuri.”
“Siku za
jumamosi ndio tution ikawa kisingizio chakututoa pale nyumbani, tunahamia
nyumba za kulala wageni. Ujue hiyo siku nzima ni kufanya naye mapenzi tu.
Atakuchezea siku nzima mpaka aridhike, ndio anakwambia rudi nyumbani. Ananipa
pesa, nachukua taksii. Ukifika nyumbani kama baada ya masaa mawili au matatu,
na yeye ndipo anaingia. Na akiingia hapo anakuwa mkali kweli kweli. Ataniita
mbele ya mama kuniuliza habari za tuition siku hiyo. Kama nimeelewa au nahitaji
msaada zaidi. Yaani yeye ndio akawa wakunifuatilia zaidi. Na alikuwa mkorofi
kweli. Mama mwenyewe alikuwa akimuogopa. Akianza kufoka hapo, nyumba nzima
inatetemeka.”
Tunda
akatoka ndani ya blangeti akakaa. Akavua ile nguo nzito ya juu ya kulalia huku
amempa mgongo Net. Net akashtuka sana. “Ona huko mgongoni.” Tunda alikuwa na alama
nyingi sana mgongoni mwake. “Hata yeye alikuwa akinipiga sana. Siku zile
nilizokuwa nikimwambia nimechoka sitaweza kutoka kwenda kufanya naye mapenzi,
hapo nilikuwa nikivizia mama yupo. Basi alikuwa akitafuta sababu yeyote ile
ilimradi anichape sana, tena mbele ya mama huku akitutishia mimi na mama
atanifukuza mle ndani. Mama naye alikuwa akiniongezea kwa kosa hilo atakalokuwa
amechagua baba Tom siku hiyo.”
“Kama ni
kuvunja kioo cha dirisha au glasi, basi ilimradi tu. Lakini sikuwa na jinsi
Net. Kunakipindi mwili ulikuwa ukichoka. Nilikuwa mtoto na yeye alitaka niwe
nikimuhudumia kila siku. Kumbuka mimi sikuwa nikipata ladha yeyote, kwa hiyo
nilikuwa siishiwi vidonda. Kwa kuwa nilijua hatanifukuza, nilikuwa nikiwageuzia
mgongo wanipige mpaka wachoke ilimradi angalau nijiuguze, vile vidonda vipone,
ili tukianza tena nisiwe naumia.”
“Na
nilipovunja ungo kila nilipokuwa nikijaribu kumdanganya nipo kwenye siku zangu
haamini mpaka ahakikishe. Kwa hiyo pia nikawa najikata hata kidole napaka
kwenye pedi kumdanganya nipo kwenye siku zangu, ilimradi nipumzike kuingiliwa.
Labda nimchezee tu aridhike au aniache kabisa.”
“Nilipofika
kidato cha kwanza nikaamua kuachana na huo mchezo na nimwambie mama, nilikosea
sana nilipomwambia nia yangu. Akaniwahi kunisemea kwa mama kuwa usiku uliopita
wakati mama yupo kazini, nilitoraka nyumbani sikurudi mpaka asubuhi hiyo.”
“Jamani
sitakaa nikasahu kipigo alichonipa yule mwanamke nakunifungasha mpaka kwa
shangazi yake. Sio bibi. Shangazi yake ambaye hata sikuwa namfahamu. Kijijini
huko, hamna hata umeme. Nilikaa huko karibia mwezi. Hamna chakula, hali mbaya
hata maji ni shida. Nikajua mama alinipeleka kule makusudi. Halafu huyo
shangazi yake mwenyewe alikuwa mzee, hajiwezi. Lakini ikabidi kukaa
hivyohivyo.”
“Nikaishia kuja kuchukuliwa tena na yule yule baba na hapo ndipo
hapo aliponihakikishia sina haki juu ya huu mwili wangu, isipokuwa yeye. Net!
Yule baba alinifanya vile atakavyo. Yeye alipanga ni muda gani na wakati gani
atumie huu mwili wangu. Huku akinihakikishia kuwa yeye ndio aliyebaki kuwa
mkombozi wangu. Na ndipo nikashika na hiyo mimba.” Net
alivuta pumzi kwa nguvu na kufikicha macho yake. Alinyoosha mkono na kushika
yale makovu ya majeraha ya Tunda mgongoni kwake, taratibu sana kama anayefikiria
kitu. Tunda alisikia faraja ya ajabu. Machozi yalikuwa yakimtoka kama mvua.
Japokuwa
kulikuwa na baridi sana, lakini alitamani Net asitoe mkono wake mgongoni mwake.
Net aliendelea kupitisha vidole vyake taratibu mgongoni kwa Tunda, akishika kila
kovu taratibu. “Pole sana Tunda.” Alijibiwa maswali yaliyokuwa yakimsumbua kwa
asilimia 90. Alimrudishia lile shati
bila Tunda kugeuka, kisha Tunda akavaa vizuri ndipo alipogeuka na
kujilaza tena. Net akamfunika tena kila mahali, kisha akajinyoosha pembeni yake
akalala pembeni yake, huku akimwangalia.
“Tunda!”
Akamwita taratibu. Tunda akanyanyua uso
kidogo kutoka kwenye blangeti na kumtizama Net, kwa macho yake
yaliyokuwa yakimchanganya sana Net tokea siku ya kwanza alipomuona. “Ulishaenda
kumuona baba gerezani?” “Sijamuona tena tokea siku
ya mwisho aliponiacha pale hospitalini. Hata sijui yupo gereza gani!” “Kwa
nini hukutafuta kujua?” “Wazo lilinijia Net. Nilitamani sana kumtafuta, japo
kumwambia nilitoka hospitalini, na kumuonyesha ninaendelea vizuri. Lakini
niliogopa.”
“Kwa
nini uliogopa tena?” Net hakuwa anaelewa.
“Kwa kuwa aliniachia pesa ndogo sana Net. Nilijua angeniona tu na hali
ile angekuwa na maswali mengi ambayo nisingekuwa tayari kuyajibu. Mojawapo
najua angetaka kujua nafanya kazi gani, na mimi sikutaka kumdanganya mwanadamu
mmoja tu aliyenipokea maishani mwake vile nilivyo. Tena wakati wote
tumekutanishwa kwenye mazingira ambayo yote nimekamatwa na uhalifu, na pia
sikutaka kumwambia ukweli wa maisha machafu niliyokuwa nikiishi kuhofia
kumuongezea machungu akiwa gerezani. Niliona ni heri niache tu.” Net akatulia
kidogo kama aliyeridhika na ile sababu.
Kisha
akauliza tena. “Ulikwenda wapi baada ya kutoka hospitalini?” “Naomba
nisikwambie Net. Tafadhali.” “Kwa nini?” “Inatosha.” Net akabaki akimwangalia
Tunda, Tunda akajifunika vizuri na kuficha uso wake, akabakiza sehemu ndogo
sana ya macho ambayo hakutaka kumtizama tena Net, akaangalia chini.
“Nikwambie
siri yangu?” Tunda alishtuka sana. “Uniambie mimi siri yako?!” “Ndiyo wewe
Tunda.” Tunda akiwa na wasiwasi asijue ajibu nini, akaamua anyamaze.
“Ushajiuliza ni kwa nini tunapokuwa ofisini mara kwa mara napenda usiwe unanipa
ujumbe kwa simu, bali uje ofisini kwangu wakati kuna simu ya mezani unaweza
kunipigia tu tukaongea?” Swali lilikuwa gumu sana kwa Tunda ambaye hakuwahi
kufanya kazi kwenye ofisi yeyote. Yeye mwenyewe Net ndiye aliyemfundisha kazi
kwa mara ya kwanza.
“Sijui
Net! Mimi nilijua ndivyo inavyokuwa. Sijawahi kufanya kazi ofisini.” “Basi huwa
wanatumia simu kuwasiliana watu wakiwa ofisini, labda iwe kuna kukabidhiana
kitu ndipo watu hutembeleana kwenye maofisi yao.” Tunda akajivuta kidogo nje ya
blangeti kwa mshangao.
“Wewe unafikiri kama bosi ni
mmoja na anawatu kumi au ishirini chini yake, halafu wote wakitaka kuuliza
swali, au kumpa taarifa wanamwendea ofisini kwake, si hiyo ofisi ya bosi
ingekuwa imejaa watu kila wakati na angeshindwa kufanya kazi? Ndio maana pia
kuna email,{barua pepe}. Kwa hiyo kila mwenye swali lisilo na haraka au ripoti
zote hutumwa huko ili bosi ajibu anapopata nafasi.” Tunda akatabasamu kama
aliyepata wazo.
“Basi na
sisi tuanze hivyo!” Net akacheka. “Mimi sikukufundisha hivyo Tunda. Nilikwambia
kila ukiwa na swali uwe unanifuata ofisini kwangu.” “Kwa nini sasa!?” “Ndio
swali na mimi nimekuuliza muda mfupi uliopita. Kwa nini unafikiri ninataka uwe
unakuja ofisini kwangu na sio kunipigia simu au kuniandikia ujumbe?” Tunda
akafikiria kidogo huku akitabasamu kama anayetaka kucheka. Net aliweza kuona
meno yake mazuri, yaliyokuwa yanang’arishwa zaidi na rangi yake nyeusi.
Akamgeukia
Net. “Sijui.” “Unataka kujua?” Tunda akatingisha kichwa kukubali huku akicheka.
Tunda alikuwa na uzuri wa aina yake, hasa anapotulia, akiwa na furaha
hakuchosha kumtizama.
“Kwa
kuwa huwa napenda nikiongea na wewe uwe unanitizama, Tunda. Napenda
kukuangalia.” Tunda alishtuka sana, akajificha tena uso kwa mikono yake
nakuanza kurudi ndani ya blangeti. Katika watu ambao hakuwafikiria hata
kuwatega ni Net. Alimuogopa sana tokea mwanzo kitu kilichomshangaza hata asijue
ni kwa nini amuogope Net, wakati hakuwa akimfahamu hata kidogo.
“Napenda
sana macho yako Tunda. Napenda kukuona mara kwa mara, lakini usifiche macho
yako. Napenda kuona macho yako yakinitizama mimi. Sipendi ninapozungumza na
wewe uangalie pembeni. Nataka unitizame mimi. Kwa hiyo nimekupa siri. Ukitaka
kuniadhibu ufanye kama hivyo ulivyofanya sasa. Nataka uwe ukinitizama kila
tunapoongea ndio nafurahia maongezi yetu.” Tunda aliogopa sana. Hakujua baada
ya kutoka pale alipojificha, atamtizamaje tena Net. Wakatulia kidogo.
Net
akaendelea. “Nimekuuliza swali Tunda. Ulipotoka hospitalini ulikwenda wapi?”
“Net jamani!? Bado tu unataka kujua? Nilimekuomba nisikwambie. Naomba
nisizungumzie hilo. Tafadhali.” Tunda alikuwa ameinama. “Kwa nini?” Tunda
alibaki kimya. “Tunda!?” “Abee.” Tunda akamtizama.
“Ujue
unaongea na mimi, sio mtu mwingine? Huna cha kuficha kwangu.” “Itasaidia nini,
Net?” Tunda akauliza kwa upole huku akimtizama. “Bila ya kuniambia, siwezi
kujua jinsi yakusaidia. Nataka kufahamu kila kitu. Tafadhali usinifiche au
usibakize kitu. Nataka kusikia kutoka kwako wewe mwenyewe.” Tunda alivuta pumzi
huku akionekana kujishauri. Mwishowe akaamua kumaliza tu, kwani ni kama
alishaongea kila kitu. Na kweli hakuwa na chakuficha kwa Net, aliyefanikiwa
kumfahamu kwa majina yote, wakati wengine walimfahau kwa jina moja moja tena ya
uongo. Hata hivyo Net ndio ameshika mpini wa maisha yake kwa wakati huo. Aliona
amalize tu, aone mwisho wake.
“Sikujua pakwenda Net. Baba aliniachia pesa chache
sana. Ilinitosha nauli na kula siku chache. Nilipotoka pale hospitalini
nilikwenda kula kwenye kibanda kimoja cha chips pale pale kituo cha Mwenge,
ndipo nilipokutana na mmiliki wa pale au mkewe ndiye aliyekuwa mmiliki.
Nilipojua anapesa na anasehemu nyingi za biashara, nikajua atanifaa.” Tunda akanyamaza.
“Nakusikiliza Tunda.” “Nimemaliza.” “Sijaelewa
chochote. Nimeishia upo kwenye kibanda cha chips.” “Kumbuka historia yangu Net.
Maisha yangu yote sikuwa na elimu bali ujuzi niliokuwa nimepata kutoka kwa baba
Tom. Mapenzi. Ndipo nikaamua kutumia huo uzoefu wangu kuishi mjini.” Tunda
akaanza kulia.
“Nilikuwa silali Net. Kazi yangu
ilikuwa kutongoza wanaume mchana na usiku! Nilikuwa nikilala na wanume hata
watatu kwa siku, na wengine ilikuwa sio lazima kufanya nao mapenzi, nilikuwa
nikitumia utundu wangu tu kuwaridhisha ilimradi kupata pesa ambazo sijui hata
zilikuwa zikiishia wapi! Nilikuwa nikinunua mavazi ya gharama ili kupata wateja
wa maana.”
“Nilitaka kulipa machungu kwa kuishi
nyumba nzuri na kununua vitu vya kisasa ili kulipiza kisasi kwa manyanyaso yote
niliyopitia, lakini haikusaidia hata kidogo. Ukweli nilikuwa nikipata pesa
ndiyo, lakini nilikuwa nikiteseka sana. SANA.”
Tunda akatulia kidogo. Akafuta machozi.
“Nimefanya mambo ya ajabu hapa duniani! Wakati
mwingine silali kwa hofu na ndoto mbaya. Huyo mwanaume wa kwanza niliyemtongoza
baada ya kutoka hospitalini, nikakwambia nimfanyabiashara mkubwa lakini Net,
kuna maajabu huku duniani, hujawahi ona. Watu wanahangaika kupata pesa, mpaka
unaweza usiamini.” “Vipi?” Net akauliza.
“Yule baba alinitoa pale akanipa maisha. Lakini
nililipia Net. Na sijui nilikuaje. Ni kama akili yangu ilibadilika! Nakwambia
sasa hivi silali sababu ya hofu, utafikiri siye mimi nilifanya.” “Ulifanya
nini?” “Ushirikina.” “Ushirikina!?” Hilo mzungu Net akawa hajalielewa
“Uchawi ule wa hali ya juu! Usiku badala yakulala,
tulikuwa tunakwenda makaburini kufanya ibada za kichawi.” Mpaka mwili wa Net
ukasisimka. “Na usifikiri mnaenda tu? Hapana.
Mnafanya mambo ya ajabu Net. Mnaita majini mpaka majoka yanatokea. Mnafanya
hiyo ibada mpaka yaondoke. Haya, wakati mwingine mnakwenda kwa huyo mganga
mwenyewe. Usiku Net. Giza. Mtakaa huko mpaka pakaribie kupambazuka. Tena mpo
ndani ya mto huko, chini ya miamba. Giza, mnafanya ushirikina. Mpaka
alipokufa.” “Kufa tena!?” Net akashtuka. Tunda akamuelezea mkasa mzima
wa Sadiki na kumuacha Net hoi.
“Ilikuwa ni shida Net! Nimeishi kwa
kuhangaika sana, mpaka wewe uliponitoa mvuani nikijificha kwa hofu ya radi.” “Daah! Pole sana Tunda.” Net alitulia kama
anawaza.
Akamfuta machozi. Akamgeukia vizuri. “Hivi Tunda,
unajua unaweza kubadilisha hayo maisha ukaamua kuishi wewe kama wewe na ukaweza
kuwa mtawala mzuri wa maisha yako?” “Sidhani Net.
Mimi mwenyewe sijijui mimi ni nani!” “Ukitaka kujitambua unaweza Tunda.
Na ukawa kiongozi mzuri sana wa maisha yako. Unaweza ukajiamuru kuwa na maisha
mazuri na matulivu. Najua au tuseme nimeelewa mazingira uliyopitia tokea unazaliwa,
yamekupelekea kuishi maisha uliyoishi. Lakini Mungu amekupa nafasi ya pili.
Nafasi ambayo hukustahili, lakini Mungu amekupa. Kubali kubadilika ili uitumie
vizuri.”
“Mbona nimeshaanza kubadilika?” “Kweli Tunda?”
“Sijalala na mwanaume tokea…” Tunda akafikiria. “Hujalala na mwanaume kwa kuwa
yeye alikukataa Tunda, sio wewe ndiye uliyekataa. Hebu fikiria kama siku ile
Gabriel angekukubali akakupokea, sasa hivi ungekuwa wapi?” Tunda akajifunika na
kuanza kulia.
“Usinifikirie vibaya wala sina nia ya kukuumiza ila
nataka kukuelimisha kwa kukufungua macho. Upo hapa ulipo kwa kuwa mimi
nilikutoa pale. Je, kama na mimi ningetaka kulala na wewe sio kukusaidia, au
tuseme kama ningekutoa pale nikakuweka hapa hotelini nikaanza kukutumia kama
wanaume wengine, ungekataa?” Ulikuwa ukweli mtupu ambao Tunda aliogopa hata
kumtizama Net.
“Inamaana mpaka sasa, ningekuwa na wewe nikiutumia
mwili wako kwa furaha zangu, na wewe ukiteseka moyoni na mwilini, ilimradi tu
utengeneze pesa! Kwa hali niliyokukuta nayo siku ile, maisha hayakukupa uhuru
wa kuchagua kitu gani ufanye ni wewe kupokea kitakacho kujia. Au niambie ukweli
Tunda, ikitokea nakufukuza kazi sasa hivi, utaenda wapi? Huna cheti hata cha
kidato cha nne. Unafikiri akitokea mtu kama Gabriel akakupokea tena mtaani
baada ya mimi kukufukuza kazi hapa, je utamkataa?” Tunda hakujibu, akaendelea
kulia.
Kila Mtu Anastahili Nafasi ya Pili.
Net
akaendelea. “Ndio maana nakuambia hii ni nafasi ya pili Mungu amekupa Tunda,
anataka uanze upya. Usikubali kuiachia.” “Mungu
mwenyewe hata simjui, Net!” “Ukikubali, mimi nitakufundisha. Lakini
lazima ukubali wewe mwenyewe kwanza. Na usikubali kwa kuwa mimi ndiye
ninayekwambia, hapana. Pata muda wakufikiria kwanza. Na hata ukisema hapana,
siwezi kukuchukia na sitaacha kukuombea. Lakini nakuhakikishia ni maamuzi
ambayo hutakaa ujute.” Kidogo akamchanganya. “Ulikuwa
ukiniombea Net?” Tunda akauliza kwa upole sana huku akimtizama Net na
uso uliojaa machozi, nakumfanya atabasamu.
“Wewe ni mzuri sana Tunda, hutakiwi kuchezewa na
watu. Thamani yako haipo kwenye nyumba unayoishi au kiasi cha pesa unachomiliki
au elimu uliyonayo. Usikubali mtu akakwambia vinginevyo.” Tunda hakuwa
akiamini. “Hata wakikutupa jangwani bila kitu chochote, thamani yako inabaki
palepale.” “Unaongea na mimi, Net! Au umesahau?”
“Nimekwambia huwa sisahau kitu. Na hilo ndilo tatizo langu.”
“Sasa hiyo thamani naitoa wapi? Sina
thamani yeyote ile Net. Sipo huru kwenda popote tena. Sina mtu anayeweza
kunisaidia hivi au hata kunisikiliza zaidi yako. Tena hata wewe sikuelewi, Net!
Jinsi ninavyo kudhalilisha, aibu ninayokutia! Kweli sikuelewi! Mimi mwenyewe
nimechoka, nimeamua kujifungia humu ndani. Maana kila ninapoenda naishia
kudhalilika tu. Kama sitakutana na watu niliokwisha lala nao, basi
nilishawahudumia kimapenzi kwa namna moja au nyingine.”
“Kwa kuwa najua kuwa, kila mtu ananafasi ya pili,
hapa duniani. Unayo nafasi ya kuanza upya Tunda. Upya kabisa wewe mwenyewe.
Haijalishi nini umefanya kwenye maisha yako, unaweza kuanza upya na Mungu
asikumbuke kabisa ulichofanya. Hata kama wanadamu tutakumbuka, lakini si kwa
Mungu ambaye ndiye wa muhimu sana. Atakusamehe, atakutakasa, atakupa furaha ya
ajabu moyoni kwako. Atafanya upya nafsi yako na roho yako pia.” “Kwani na mimi
nina nafsi kweli!?” Net akacheka.
“Sitanii. Nahisi hivyo vyote vitakuwa vilishakufa
au mwenye navyo, huyo Mungu alishavichukua.” “Unanafasi ya pili Tunda.
Yakupatanishwa na Mungu. Fanya maamuzi sahihi. Atakurejeshea vyote ambavyo
shetani alivichukua.” “Umesema utanisaidia?” “Kwa asilimia mia moja. Sitakuacha
hata kwa hatua moja.” Tunda alifurahi sana.
“Asante sana Net. Sasa ndio natakiwa nifanyaje?”
“Swali zuri sana. Kwanza nataka kujua kama upo tayari.” “Umeniambia nijaribu.
Nataka nijaribu na mimi nione.” “Najua sasa hivi umechoka. Naomba nikuache
upate muda wa kupumzika, kisha kesho nikupeleke kwa mtu atakayekuambia nini
chakufanya.” “Kesho huendi nyumbani?” “Tutaenda wote Dar, na huko ndiko
nitakupeleka kwa mtu atakayekwambia chakufanya.” “Net!” Net alikuwa akivaa
viatu ili atoke. Tunda akakaa.
“Asante kwa kila kitu. Asante sana.” Net
akatabasamu. “Asante kushukuru, na mimi asante kwa kuniamini na kuniambia kila
kitu tena kwa uwazi.” Tunda akafikiria kidogo. “Nikuulize kitu Net?” “Uliza
tu.” “Baada ya kujua uchafu wangu wote niliofanya, unanifikiriaje?”
“Ninafikiria hiki unachotaka kufanya sasa hivi Tunda, sio maisha uliyoishi
zamani. Wewe hukupata nafasi ya kulelewa kama wengi wetu. Hukubahatika. Ila
sasa hivi umekubali kupokea nafasi mpya kwenye maisha yako, tena ukiwa na mimi
niliyekuahidi kuwa na wewe katika kila hatua ya maisha yako, hilo tu ndilo
linanipa nafasi ya kuweza kuongea kitu juu ya maisha yako, si vinginevyo.”
Tunda hakuamini, akabaki ametulia tu akimwangalia kama asiyemsadiki.
“Nina kusifu Tunda. Ikifika kesho kama sasa hivi,
utakuwa kiumbe kipya kabisa. Pata muda wakupumzika kesho tutaongea vizuri
tukiwa njiani.” Net akaondoka akamwacha Tunda akiwa amelala, kwani alikumbuka
Tunda alivyomwambia kuwa, huwa anapata usingizi pale anapokuwa naye. Alirudi
kukaa pembeni yake, akawasha tv akiwa bado amevaa viatu. Tunda alibaki
akishangazwa na Net alijua. “Pumzika, ulale. Nataka nikuache ukiwa umelala.”
Tunda alitoa tabasamu zuri, lililofanya azidi kuvutia. “Asante Net.”
Alijirudisha ndani ya yale mablangeti na
shuka, huku Net akimsaidia kumfunika vizuri. “Usiku mwema.” “Na wewe Net.”
Tunda akalala na ndipo Net naye alipoondoka.
Tunda akiwa safarini kuanza maisha mapya.
W |
akiwa kwenye ndege kuelekea Dar,
Net alimueleza Tunda umuhimu wakuanza upya na faida nyingi atakazopata katika
hayo maisha aliyoyachagua. “Naona kama ndege inachelewa, natamani kufika haraka!”
Net akacheka. “Lakini kwanza tunapitia nyumbani.” “Kwa mama yako!?” “Tena
atakuwa akitusubiri uwanja wa ndege. Amefurahi uamuzi uliofikia, akaomba tupate
muda wa pamoja mfahamiane kwanza kabla ya kwenda kwa Mchungaji. Ni sawa?”
“Hamna shida, ndio vizuri na mimi nimfahamu bosi wangu. Tumekuwa tukizungumza
kwenye simu tu. Na mimi nitafurahi kumuona. Yeye ni mzungu?” Swali la Tunda
lilimfanya Net acheke sana.
“Nini
sasa?” “Hapana bwana. Mama yangu ni Mtanzania. Baba ndiye alikuwa mtu wakutokea
Canada.” “Sera alikuwa akiringa kuwa anaolewa na Mzungu.” “Mzungu gani?” “Si
wewe?” Net akazidi kucheka. Alikuwa kijana mstaarabu sana na muungwana.
Alijaliwa utulivu ambao mtu yeyote angetamani kuzungumza naye.
“Hakuwa
amenielewa vizuri. Nilijitahidi sana kuwa muwazi kwake na sikuwahi kumuonyesha
hisia zozote za kimapenzi. Sijui kwa nini alifikiria ndoa!” “Atakuwa alikupenda
sana.” Net akamtizama Tunda. “Nini sasa? Kweli! Sera alikupenda.” Net akatabasamu
kisha akapotelea mawazoni.
“Net!
Nikuulize swali?” “Mmh!” “Kwani unamchumba?” “Sijui!” Tunda alikunja uso, kama
ambaye hakuwa amemuelewa Net. “Vipi? Umenipatia mchumba nini?” “Hapana, lakini
nashangaa kwa nini hukumpenda Sera wakati naona alikuwa msichana ambaye mlikuwa
mkiendana sana!” “Unamaanisha nini?” “Wote mmelelewa kwenye mazingira mazuri,
mmesoma, wazazi wenu wanauwezo mzuri, yaani mnapesa. Ni msichana mzuri, na yeye
ni mweupe, halafu Sera hakuwa muhuni kabisa. Hakuwa na mambo ya wanaume.
Alijiheshimu sana.” “Daah! Kama ungekuwa mshauri wangu wa ndoa, ningekufukuza
kazi sasa hivi.” “Kwa nini tena!?” Tunda akaanza kucheka.
“Vigezo
vyako viko dhaifu sana, havimsaidiii mtu kupata mke hata kidogo!” “Jamani Net!”
Tunda akazidi kucheka. “Hebu niambie, weupe, usomi, pesa na nini tena?” Net
akauliza huku Tunda akicheka. “Kulelewa na wazazi wenye uwezo, yaani wote
mmetoka kwenye malezi yanayoeleweka.” “Ehe! Sasa hivyo ndio vinasaidia kuwa na
mke bora?” “Ndiyo. Na mwanamke aliyetulia. Sasa ukioa mwanamke ambaye hajatulia
ndio inakuaje sasa?” Net alicheka kwa kuguna kisha akageuka pembeni. Tunda naye
akaanza kuwaza maisha yake mapya aliyoamua kuanza.
Kwa Mara ya Kwanza Tunda na Mama Cote.
Ndege ilitua viwanja vya ndege
vya Mwalimu Nyerere, Dar. Kweli walimkuta Mama yake Net na msichana mwengine
aliyeonekana mzungu kwa asilimia kubwa sana kuliko hata Net. Alikuwa mzuri sana
na nywele za rangi ya thahabu, tofauti na Net,
zilianguka mpaka chini ya mabega. Macho ya rangi ya blue kama Net. Tunda
alimsalimia mama yake Net baada ya Net kumsalimia mama yake kwa kumkumbatia na
kumbusu.
“Kuna nini tena?” Net akauliza baada yakumuona yule
dada hajawasalimia. “Am leaving with you.” Alijibu yule dada kwa lugha ya
kingereza huku akionyesha uso wakutaka kulia. “I just got here, Maya! What’s
going on?” Net akamuuliza kwa upendo huku akimwangalia mama yake. “Siwezi tena Net. I got enough of her. I want to go.”
Yule dada aliendelea kumlalamikia Net, huku machozi yakimtoka. “Can at list
have a hug first?” Net akamuuliza kwa upendo kama kumbembeleza.
Yule dada akamsogelea Net na kumkumbatia kisha
akaanza kulia. “She doesn’t take me out of her
sight! She took everything away from me.
She is ruining my life, Net.” Aliendelea kumlalamikia Net. “Can
we talk about it later?” Yule dada akanyamaza kwa muda.
“Mwambie anirudishie funguo zangu za gari kwanza.
She listen to you Net. Tell her, NOW.” “You know we have to talk first, Maya.
Naomba utulie kwanza kisha tutaongea tukifika nyumbani.” “I don’t want to talk,
I want my life back.” “I understand, but let’s go back home first.” Walikuwa
wamewapa mgongo Tunda na yule mama, wakati wao wawili wakizungumza.
“Naomba umsalimie Tunda.” “Tunda? Is that a name or
fruit!?” Yule dada akauliza kama kwa kejeli akitaka kujua kama Tunda kweli
linaweza kuwa ni jina la mtu! “I know you are upset Maya, but can you try to be
nice?” Net akamwambia anaelewa kuwa
amekasirika, ila ajaribu kuwa mwema kwa mgeni. “Am sorry.” Maya akaomba msamaha
na kumgeukia Tunda.
“Hey! Am Maya.” “Kiswahili Maya!” Mama yake Net
akaingilia akitaka azungumze kiswahili na Tunda si lugha ya kingereza. “See! Everything am doing to her it’s a problem.”
“She speaks Swahili, Maya. Just use Swahili, please.” Net aliweka msisitizo
akiungana na mama yake kuwa Maya atumie kiswahili. “Fine!”
Akakubali Maya nakufuta machozi.
“Habari yako. Naitwa Maya Cote.” Tunda akajua
lazima ni mdogo wake Net kwani ndiyo jina alilokuwa akitumia hata Net,
Nethaniel Cote. Tunda akanyosha mkono. “Naitwa Tunda, kama vile fruit.” Maya
akacheka kwa aibu kidogo. “Samahani. Mama ananiudhi sana.” “Usijali. Hata shule
walikuwa wakinitania hivyo hivyo.” Tunda alijibu huku akitabasamu, wakacheka.
“You have a pretty face. I love your sleeping eyes.
The way you talk and smil..” “Swahili, Maya.” Mama yake alimkata Maya akitaka
azungumze kiswahili. “See Net! I told you she…” “Maya!” Net akamwita kama
kuweka msisitizo. “Fine!” Maya akamjibu kaka yake. “Wewe ni mzuri sana. Napenda
macho yako na, anyways everything. You pretty.” Tunda akacheka akiona aibu.
“Asante Maya.” Akamgeukia kaka yake na kumwambia, “I like her.” Akisema
amempenda Tunda. Wote wakacheka.
“Ukiondoka unichukue na mimi, sitaki kubaki hapa na
Mama Cote.” Alimnong’oneza Tunda masikioni, lakini kwa sauti iliyoweza kusikika
na kila mtu pale. Tunda akacheka. “Mama akiruhusu, tutaenda wote.” Tunda akajibu
huku akicheka. “Trust me, she wont. Labda Net ndio amwambie. Anafanya chochote
anachoambiwa na Net, lakini siyo mimi.” “That’s enough Maya.” Mama yake akamkatisha.
“See! That’s why I want to go away.” Maya akalalamika na kurudi nyuma akiwa
amenuna. Walionekana wawili hao hawapatani.
“Karibu sana Tunda. Samahani umetukuta katika
wakati mbaya, lakini nimefurahi kukufahamu. Mimi ndiye Mama Cote. Mama yake
Maya.” Maya akamwangalia na kujisogeza kwa kaka yake. Alikuwa mama wakawaida
tu. Hakuwa mweupe wala mweusi. Mswahili kabisa mwenye rangi ya kawaida. Maji ya
kunde. Lakini alizaa watoto wote weupe sana, yaani wazungu. Maya alikuwa ndio
anamwili wa kizungu, nimpaka aongee hicho Kiswahili chake na akuonyeshe mama
yake ndipo utajua amechanganya. Wote walikuwa na nywele nyeusi lakini Maya
alizibadili rangi nywele zake.
“Net aliniambia mnataka kwenda kumuona Mchungaji.”
“Ndiyo.” “Umefanya vizuri. Lakini twende kwanza nyumbani mkale ndio twendeni
kwa Mchungaji.” Walikwenda mpaka nyumbani kwa huyo mama. Alijenga sio mbali
sana na alipokuwa amejenga Net. Maeneo hayo hayo lakini lazima utumie usafiri
kufika kutoka kwa Net kwenda kwa mama yake. Palikuwa na umbali kidogo.
Tunda akabaki ametoa macho. Lilikuwa ni jumba la
kisasa. Kumbwa picha za familia zilijaza hiyo nyumba kwa wingi. Kuanzia
unaingia mlangoni mpaka sebuleni. Kubwa na nzuri. Na hapo ndipo alipoiona picha
ya baba yake Net. Kweli alikuwa mzungu kabisa. Na alifanana sana na Net. Tunda
alipita akiangalia.
Heshima ikaongezeka kwa hiyo familia. Kwa vile
alivyoona pale, na biashara huyo mama anafanya, Tunda akakubali kuwa huyo mama
kichwa yake inafanya kazi. Alimshukuru Tunda kwa kazi nzuri aliyokuwa akifanya
kwenye ofisi yao huko Arusha. Akamsifia kuwa anampunguzia majukumu makubwa yeye
na Net kwa utendaji wake mzuri.
“Net anakusifia sana. Hata wateja wetu wanakusifia.
Asante sana na ninakuomba uvumilie tu, baada ya muda nitaongeza mtu mwingine
wakukusaidia.” “Hamna shida mama. Kwa sasa naona nimeweza kumudu kazi zote,
hata hivyo Net ananisaidia sana.” “Utalemewa pindi Net atakaposafiri.” Tunda
alishtuka sana akamgeukia Net.
“Sisafiri sasa hivi Tunda. Acha kuogopa.” Tunda
akacheka taratibu lakini wazi alionekana ameingiwa hofu. Walikaa pale
wakizungumza mambo mbali mbali. Zaidi Net na mama yake ndio waliokuwa wakiongea
zaidi. Walikuwa wakizungumzia mambo yao ya biashara. Tenda alizoshinda huyo mama.
Tunda alibaki kusikiliza huyo mama, nakumtamania. Alionekana ni mama
aliyefanikiwa sana.
Walikaa hapo mpaka mida ya jioni ndipo walipoamua
kwenda kanisani. Tunda alikuwa amepewa chumba pale pale, akaacha baadhi ya vitu
vyake kwenye hicho chumba, kwani Net alimwambia wangelala hapo siku hiyo mpaka
kesho yake.
Tunda na Mkasa wa Kanisani.
Walipofika
kanisani wakakuta ndio wanamalizia kikao cha wazee wakanisa, ofisini kwa
Mchungaji. Ilibidi wasubiri kwenye viti vya nje. Alikuwa Tunda, Net na Mama
Cote. Waliendelea kuongea mambo mawili matatu wakiwa pale nje, mpaka walipoona
wazee wengine wakitoka kwenye ofisi ya Mchungaji. Mama Cote akasimama
akatangulia humo ndani, baada ya muda, Tunda na Net walianza kusikia vicheko
mle ndani ofisini wakahisi wamesha sahauliwa. “Ngoja nikawashtue.” Net
akasimama na kuingia ndani.
“Shikamooni.”
Tunda akamsikia Net akisalimia huko ndani. Mchungaji akaongea na Net maneno
mawili matatu huku akimtania na kumuuliza habari za Arusha kisha Net akaamua
amkumbushe baada ya kukuta bado kuna wazee wengine watatu mle ndani. “Bado
utakuwa na nafasi yakuongea na Tunda?” Net akauliza. “Kabisa. Umekuja naye?”
“Yupo hapo nje.” “Mkaribishe awasalimie na hawa wazee wa kanisa.” Mchungaji
akajibu. “Ni kweli. Yaani Tunda ni binti mzuri sana.” Mama Cote naye akaanza
kumwaga sifa za Tunda, akimsifia utendaji kazi wake. Net akatoka kwenda kumwita
Tunda.
Net
alimtanguliza Tunda aingie kwanza, yeye akafuata nyuma. Tunda aliingia na
kusalimia “Shikamooni.” Huku akinyoosha mkono akitaka kuwapa mkono wale wazee
na wachungaji kwa heshima zaidi. Wakati anasogea mbele kidogo ili aanze
kuwashika mikono huku akiwaangalia vizuri, Net akamuona Tunda ameshtuka sana,
akainama na kurudi nyuma huku akishusha mkono wake. Mama yake na Mchungaji
hawakuelewa, lakini Net alishaelewa kwani alishakaa na Tunda kwa muda mfupi
lakini alishamuelewa vizuri sana. Net alikasirika sana.
Wakiwa
wengine hawajaelewa kilichompata Tunda, akamgeukia Net na kumsogelea kwa
karibu. “Naomba kuondoka Net.” Tunda akataka ampishe sehemu ya mlangoni. “Vipi
tena!?” Mchungaji akauliza kwa mshangao, huku akisimama. “Eti Tunda?” Tunda
alishaanza kulia. “Naomba niondoke tu.”
Hakuna aliyeelewa, Net aliwageukia wale wazee, akashangaa kuona wawili
wameinama. “No way!” Net alisikika akilalamika huku ameshika kichwa.
“Seriously!?” Net akawauliza kwa mshangao huku akiwatizama wale wazee wawili.
Tunda akamsogeza kidogo Net kwa mkono wake, akatoka nje.
“Tunda!
Tunda! Naomba nisubiri.” “Umenidanganya Net.
Umeniambia nakuja kuanza upya, halafu unakuja kunikutanisha na waliokuwa wateja
wangu, tena mbele ya mama yako! Nilikuamini Net, umenigeuka!” Tunda
alikuwa akilia. “Tunda please. Naomba usiondoke.” Tunda alikuwa ameshatoka nje
ya geti la kanisa, alikuwa akitembea kwa mwendo wa kasi, Net akimkimbilia kwa
nyuma.
“Naomba
usimame Tunda, Please.” Tunda akasimama huku akilia. “Naomba unisikilize.
Unafikiri mimi ningejuaje kama wale walikuwa wateja wako? Sikuwa nafahamu hilo!
Wale wazee wanaheshimika sana hapa kanisani, sikuwahi hata kuwaza kama wanaweza
ku..” Net akasita. “Sasa unataka nifanye nini na
wale watu tena? Ni maisha gani mapya unataka nianze na watu kama wale? Si
yatakuwa ni yale yale tu?” Tunda alikuwa akiongea ukweli kabisa. Net akapooza,
alishindwa chakujitetea kabisa.
Mahali
ambapo alimwahidi Tunda angepata msaada na kubadili maisha yake, anakutana na
wazee aliokuwa akiwaamini sana na wao walikuwa wakiishi yale maisha machafu.
Alibadilika sura akawa mwekundu, nakushindwa kushusha mikono yake. Alibaki
ameweka mikono kichwani akizunguka zunguka pale mbele ya Tunda.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mambo yanazidi kuchanganya....
0 Comments:
Post a Comment