Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! – Sehemu ya 16. - Naomi Simulizi

Nilipotea! – Sehemu ya 16.


A

kiwa hata hajui anaanzia  wapi kumsaka huyo Gabriel. Lakini  akili yake, hisia zake zilimwambia  lazima ampate tu, ikawa kama yeye ndio amebeba mjibu yake yote. Tunda anamtaka kwa hali na mali. Akiwa  njiani kurudi Dar, akaanza kumsaka kwenye mitandao ya kijamii ili kupata  habari zake kamili. Kumfahamu kwa  undani zaidi. Angalau kujua chanzo  cha pesa yake. Akaperuzi jina lake  mpaka kwenye magazeti. Kila mahali  aliandika jina lake kamili. Kwa kuwa  alikuwa na pesa, habari zikawa  zinamfikia Tunda kwenye kiganja cha  mkono wake na kuzisoma kwa makini  sana bila kupuuza chochote. 

Mpaka anatua uwanja wa ndege wa jijini Dar, akawa ameshamfahamu Gabriel  kwa asilimia kubwa tu. Kuwa ni mtu  ambaye yupo busy sana kwa kuwa  anamiliki biashara mpya na ngeni ya  chakula kimoja kikubwa nchini, burger ya aina hiyo aliyoanzisha yeye.  Alisambaza migahawa yake nchini  kwa aina hiyo moja ya chakula.  Burger G ndio jina la hiko chakula kilichoonekana kupata walaji wengi sana. Kuanzia ladha na ufungwaji wake kama hutaila hiyo burger pamoja na chips zilizokuwa zikikatwa kwa muundo wa kipekee, kwenye moja ya hiyo migahawa yake.

Wengine walipenda na aina hiyo mpya ya chakula  cha onion rings pamoja na aina za wings yaani vipapatio vya kuku vilivyokuwa vikitengenezwa kwa ladha tofautitofauti. Hayo yote Tunda akayapata kwa kina na kushangazwa sana. “Alijificha wapi huyu kiumbe hadimu!?” Akajiuliza Tunda wakati akiendelea  kumsoma.  Akagundua pia huwa haendi bar wala  kumbi za starehe. Mtu aliyeshika dini  sana. Na habari iliyopamba vichwa  vya habari vingi ni ile tabia ya siku za  jumapili  migahawa yake yote kufungwa na wafanyakazi wake wote wanatakiwa kupumzika  siku  nzima,  kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Na yeye mwenyewe Gabriel siku  zote za jumapili lazima awepo kanisani  na familia yake. “Ndio maana!”  Tunda akacheka.

Tunda hakuwahi  kuingia kanisani hata mara moja.  Aliweza kuingia kila mahali, lakini sio  kanisani labda kipindi ni mtoto, akiwa  anaishi na mama yake mzazi. Baba Tom alikuwa akilazimisha, lakini  alipomzoea, aliweza  kumkatalia  kwenda nao kanisani. Akawa anabaki  tu nyumbani siku za jumapili wakati  familia ya mama yake wakienda  kanisani. Hakuja kurudi tena huko  kanisani. “Nampataje huyu kiumbe hadimu  hapa mjini?” Swali lililomsumbua Tunda  ambaye muda haukuwa upande wake. 

Mteja wake wa Arusha alikuwa  akimsubiria arudi jijini Arusha baada  ya siku tatu. Na alijiambia hawezi  kurudi bila kumnasa Gabriel ambaye wengi walimtabiria huko kwenye  mitandao ya kijamii kuwa hatafika  mbali, atafilisika tu kwa tabia yake hiyo ya kufunga biashara zake  siku hizo ambazo wafanyabiashara  wengi hutegemea kuingiza pesa yeye alifunga sababu ya kumuabudu Mungu! Chakushangaza wengine walitoa tathimini ambayo Tunda hakujua kama ni ya kweli au uongo,  ilielezwa yeye ndio mfanyabiasha  wakwanza wa migahawa anayeingiza  pesa nyingi zaidi tena akiwa ametoa  hiyo siku moja ya jumapili, kwa juma. “Sasa kabla  hajafilisika, na mimi ninufaike.” Tunda akajisemea.   

Atafutaye Hachoki.

Tunda aliamka siku inayofuata  akaenda kubadilisha aina ya  nywele kichwani mwake, na  kuweka nywele ambayo alijua  wanaume wengi huvutiwa nayo.  Ilikuwa wiving ndefu ya mawimbi.  Alipendeza na hiyo nywele na alikuwa  ameinunua kwa pesa nyingi haswa. Akiiweka  kichwani, utafikiri ni yake. Na  alimpata dada aliyejulia kichwa chake,  hakuwa akibadilisha mtu wakumtengeneza ila yeye tu. Aliporidhika kuwa amependeza, ndipo  akaweka mkakati wakumsaka huyo  Gabriel.  Aliamua kwenda ofisini kwake akiwa  ameshamjua kwa asilimia kubwa. 

Bado biashara kubwa aliyokuwa akijua  Tunda anafanya huyo Gabriel ni hiyo  ya chakula aina hiyo ya burger. Akajua watu husifia chips, onion rings na wings walizokuwa  wakiuza kwenye migahawa yake. Na  wengine walisifia aina za juisi na  icecream za kwenye hiyo migahawa  yake pia. Walisema ilikuwa tofauti kabisa  na sehemu nyingine. Basi Tunda  akaona anazo habari zakumtosha  kuanzia kumtega huyo mfanyabishara  mcha Mungu, Gabriel.

Alifika ofisini kwa Gabriel,  lakini sekretari wake alimkatalia  katakata kuonana naye akamwambia  nilazima awe na miahadi naye.  “Unaweza kuja juma lijalo siku ya  jumatano, saa nane mchana, atakuwa na nafasi na mimi nakuweka wewe wa  kwanza.” Yule sekretari aliongeza  huku akiangalia ratiba ya bosi wake. “Naomba ukamwambie  Nancy anashida yakumuona, tafadhali. Akikataa nitaondoka bila kukusumbua.” Yule  sekretari  akakubali kwa shingo upande huku  akihofia isije kuwa mtu muhimu sana  kwa bosi wake, akaja kujua baadaye  kama amemkatalia hata kufikisha ujumbe, akaingia matatizoni. Akaamua  kwenda kumwambia kama Tunda  alivyomtuma. 

Akiwa hajaelewa bado huyo Nancy ni nani, akaonelea kutaka kwenda kumuona ilipengine sura imkumbushe. Gabriel kijana huyo  mwenye majukumu mazito, alitoka  ofisini. Akakutana na huyo Nancy. Macho yakagongana na Tunda. Akatulia kidogo Gabriel, mwishoe akaamua kuuliza.  “Sijui tumeshaonana kabla?” Gabriel  aliuliza akiwa na uso wenye maswali  kidogo. Huwa unaongea na watu unaowafahamu tu?” Tunda akauliza  na uso wa tabasamu, uliojaa kujiamini.  Hapana, samahani. Nipo kwenye kitu  cha msingi sana.” “Sitachukua muda  wako leo, naomba uniambie ni siku  gani tunaweza kuonana, tukaongea  vizuri.” Gabriel alifikiria kidogo kisha akaonelea kuuliza tu.

Ni juu ya mambo ya  kazi au?”“Naomba nijibu hilo siku  tutakayokutana.Akiwa na mshangao  mbele ya sekretari wake na binti huyo  mrembo wa kuvutia, aliyemsimamia  mbele yake ilibidi Gabriel au Gab  kama wengi wa marafiki wakaribu  walivyozoea kumwita,  akubali  kuonana naye siku inayofuata jioni.  “Sijui saa kumi na mbili jioni itakuwa  sawa kwako? Maana naona nitakuwa  busy sana. Nikifikiria ni muda gani  nikupenyeze kwenye ratiba yangu, ni  huo muda baada ya kazi.” Gabriel akamalizia huku akimtizama kwa  makini.

“Wapi?” Hapa hapa ofisini.” “Sawa.Tunda alihakikisha anaondoka Gabriel akiwa anamtizama.  Alibaki amemkodolea macho Tunda  mpaka alipotoka kabisa nje ya mlango. “Samahani. Sijalipata vizuri jina  lako.” Gabriel alimkimbilia Tunda mara alipotoka nje. Tunda akatabasamu  na kumgeukia vizuri. Gafla kasahau jina! Tunda akawaza. Naitwa Nancy. Akajitambulisha na kumpa mkono.  Gabriel akaupokea mkono laini wa  Tunda. “Nafurahi kukufahamu Nancy,  naitwa Gabriel lakini marafiki zangu  wengi wananiita Gab. Hapa ndipo  ilipo ofisi yangu kubwa, nyingine  zipo..” Gabriel akaendelea kujieleza kama aliyechanganyikiwa huku Tunda  akimwangalia kwa macho yake matulivu. Kulikuwa na kitu cha tofauti  sana kwa Tunda, alikuwa kama na  sumaku kwa wanaume. Alijua wazi  mwanaume akishakubali kumsikiliza  tu, hataweza kuchomoa, hasa akiamua  yeye.

Mwishowe Gabriel akaamua  kunyamaza. Akamuachia mkono,  akawa kama amejishtukia.  “Nimefurahi  kukufahamu  Gab.” Asante sana kwa kuja kuniona. Kwa  hiyo umesema leo saa kumi na mbili  ndio utakuja?Gab akajichanganya.  Nilifikiri ulisema kesho!Tunda  aliongea kwa upole na tabasamu.  “Nina mambo fulani ninafanya sasa hivi, lakini huwa sekretari wangu  anatoka saa kumi na nusu jioni, na  hapo ndio naacha kupokea simu  kabisa. Unaweza kurudi jioni?” Gab  akauliza kwa kubabaika sana. Tunda akamzuga kwa kufikiria kidogo  huku akiangalia kalenda ya simu yake  na kumjibu. “Naweza kutengeneza  muda kwa ajili yako Gab.” Gabriel  alianza kuchekacheka.

Samahani  sana kwa usumbufu, najua hii nenda rudi, sio kitu kizuri. Lakini naamini  jioni tutapata muda mzuri.” Hamna  shida.” “Nikuitie taksii.” “Hapana  Gab. Nipo na usafiri wangu. Asante tutaonana jioni.Tunda akaondoka,  asiamini kilichomtokea. Alitegemea ugumu mkubwa sana kwa  Gabriel. Alishajaribisha kuzungumza  na huyo Gabriel mbele ya kioo cha  chumbani kwake. Akaona amekosea.  Akajaribisha kioo cha bafuni kwake.  Akajaribisha tena jinsi ya kuzungumza  naye kabla hajatoka nyumbani kwake  akiwa sebuleni. Akajaribu tena na tena mpaka akaridhika, ndipo akaita Uber.  Kuja kukutana na Gabriel mwenyewe ndiye anayemuomba msamaha kwa  usumbufu!  Akapunguza  mukari  kabisa.

“Naweza kula toto ya kanisani, mchana kweupee.” Tunda  akajisemea na kucheka akiwa kwenye  taksii iliyokuwa ikimrudisha Mlimani  city.  Ile taksii hakutaka imfikishe kwake,  kwa kuwa aliichukua palepale nje ya  ofisi ya Gabriel. Hakutaka kufanya  kosa. Kama kawaida, akashushwa na  hiyo taksii hapo, akazunguka kidogo  pale Mlimani city, akatoka kabisa pale  kwenda kutafuta usafiri mwingine nje kabisa ya viwanja vya Mlimani City, wakumrudisha nyumbani kwake.   

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Ilipofika jioni ya saa 12 Tunda alirudi  ofisini kwa Gabriel, na kumkuta  Gabriel peke yake pale ofisini.  “Mbona upo peke yako?” Tunda  akauliza wakati anaingia kwenye ofisi  ya Gabriel. Mfanyakazi wa mwisho  huwa anatoka saa kumi na moja  kamili.  Huwa  napenda  kubaki  peke yangu ili kumalizia kazi zangu  bila usumbufu. Na ndio muda wangu  wakufikiria na kujipangia ratiba ya  kesho.  Karibu.” Akamkaribisha  Tunda.  Asante.” “Utapenda kunywa nini? “Red wine.” “Oooh! Hapa kwangu  siweki pombe kabisa.” “Kwa nini? “Sipendi pombe.” “Basi naomba fanta orange.Tunda alivaa gauni lililomfika magotini na lilikuwa na  rangi angavu kidogo.

Kwa hiyo kukaa  kwake kwenye kochi kulisababisha lile  gauni liwe kwenye mapaja na zile  rangi zilivutia kuangalia juu ya mwili  ule Mungu aliouweka rangi nzuri  nyeusi halafu Tunda akaifanya ile  rangi kuwa ya kipekee. Hayo mapaja  yalikuwa  yakifanyiwa  Waxing.  Usingekuta kipele wala kinyweleo.  Safi wakati wote kama mtoto  mchanga. Na ili kuhakikisha Gabriel  anaona alichomkusudia, hakuacha  kulivuta chini hilo gauni huku akihangaika pale kwenye kochi. Gabriel alijitahidi macho yake  yasishuke chini ya uso wa Tunda  aliyejitambulisha kwa jina la Nancy. 

Alimsogezea  soda  akammiminia  kwenye glasi na kumkabidhi Tunda.  Wakati Tunda anaipokea aliipindua ile glasi kwa kusudi, soda yote  ilimmwagikia kuanzia juu mpaka chini  kwenye lile gauni zuri alilokuwa  amevaa.  “Ooh  my  goodness!  Nitafanyaje? Nitatokaje hapa? Ona  nilivyoloa mwili mzima!” Tunda  aliongea kwa sauti ya kulalamika na  imejaa deko, tena kwa lugha ya  kingereza kizuri sana. “Samahani sana  Nancy, sijui nimeshikaje hii glasi! Labda uingie hapo chooni kwangu  ujaribu kujisafisha.” Tunda aliingia hapo chooni ndani ya  hiyo hiyo ofisi na kuvua lile gauni  kabisa. Mbali na chupi hakuwa  amevaa kitu kingine ndani.

“Sijui hata  kama litafaa jamani!” Gabriel  alimsikia Tunda akilalamika huko  chooni. Samahani sana.” “Hivi una  taulo? Nataka nijisafishe kidogo, mwili mzima unanata kwa sukari ya soda!” Vipo vitaulo vidogo vya kukaushia mikono.  Sijui vitafaa?” “Itabidi tu. Viko wapi?” “Huwa wanavipanga hapo kwenye kabati la juu.Tunda  alifungua kabati na kukuta vitu vingine  humo ndani, akijua kabisa silo kabati  aliloelekezwa aliangusha zile chupa  mle ndani  makusudi tu.  Akajilalamisha kama aliyejiumiza tena. “Aiii!”

Gab akakimbilia huko ndani alipokuwa Tunda, akamkuta amevaa chupi tu, akilalamika maumivu yakujigonga huku akijaribu kuokota vitu alivyodondosha sakafuni.  Gab alipigwa na butwaa, akabaki amekodoa macho. “Mbona hunisaidii  jamani!?” Tunda akajilalamisha.  Samahani sana.Gab aliinama na  kuanza kuokota vile vitu  alivyoangusha Tunda chini huku Tunda ameshikilia kipanda uso chake. 

“Vipi, umeumia?” Hiyo chupa imenigonga hapa.” “Tuone.Gabriel  akasogea, huku akitetemeka. Tunda  alikuwa  uchi,  matiti  yake  ameyashikilia kwa mkono mmoja, kitu  alichotamani kama angeachia tu ili  afaidi kote.  Pole sana. Kuna uvimbe kidogo.  Twende ukalale pale kwenye kochi  nikuwekee barafu hapo kichwani.” Tunda alicheka moyoni alijua Gabriel  ameshanasa, kwani hakuwa  wala amejigonga na kitu chochote. Alidanganya tu.

Gauni lenyewe wala halijatakata! “Usijali, nitakusaidia kulisuuza.  Tangulia ukapumzike pale kwenye  kochi, mimi nikusafishie.” Tunda alienda akajilaza kwenye kochi akiwa na chupi tu, tena chupi yenyewe ilificha mbele na nyuma tu. Pembeni  vimikanda vyembamba. Hiyo hips  hapo pembeni na ulaini wa muonekano  wa hilo paja. Usingeacha kutizama.  Rangi moja mwili mzima. Ofisini ni  maeneo  yake  yakujidai  pia. Alishatumiwa huko na baba Tom,  kuanzia mtoto mpaka utuuzima. Hana  asichojua kufanya endapo akitakiwa kutumika hata  hapo ofisini. Iwe mezani, kwenye kiti  cha ofisi au hata kwenye makochi  hayo. Alilala hapo akimfikiria Gabriel aliyekuwa akimfulia hilo gauni huko  bafuni. “Nimuweke wapi huyu kiumbe?”Akajiuliza Tunda akiwa  amejilaza na chupi tu pale kwenye  kochi.

Baada ya muda Gabriel alitoka na  kitaulo kidogo na barafu kwenye  kikombe. Akamkuta vile vile Tunda  amejilaza. Akaenda kupiga magoti  pembeni yake na kuanza kumkanda  Tunda usoni. “Aaauu!” Tunda akajilalamisha maumivu. Pooo.Gab alisafisha  koo baada ya kupaliwa na mate. “Pole  sana.” Tunda alimuona jinsi hali yake  ilivyokuwa mbaya, lakini alimuacha  mpaka yeye mwenyewe aanzishe.  Akaendelea kumkanda hapo kwenye  kipanda uso huku anazidi kutafuta jinsi  ya kuweka mkono mwingine maana  alianza kutumia mkono mmoja  wakulia tu. Wakushoto ukawa  unahangaika. Mara juu kichwani, mara  pembeni ya kochi. Tunda alikuwa pale  kwenye kochi akili zimezama kwenye  maumivu yake.

Mlio wa taratibu akitetemeka ule ubaridi wa barafu  uliendelea taratibu. “Aaaa, baridi!” Pole. Akajidai  anamsugua  mabegani kupunguza baribi. Asante. Tunda akashukuru taratibu. Macho  yakagongana. Gab akazubaa hapo kidogo. Karibu.Akajibu kwa sauti  yakulemewa na mrembo huyo.  Alishagonga hayo matiti mara kadhaa  wakati akimkanda hapo kwenye  kipanda uso. Alishaona hicho kiuno  chenye  cheni,  chembamba  kilichoshikiwa na hayo mapaja.  Taratibu kule kumsugua mabegani na  mkononi kumpa joto, kukaongezeka. 

Alipoona ameanza kumpapasa, Tunda  alijua tayari. Ilikuwa ni mwiko kwake  kulala na mwanaume bila kondomu.  Alikaa taratibu na kumsogelea pale  alipokuwa amepiga na  magoti  kumuashiria yeye ndio alale. Bila kujielewa, Gabriel alipanda yeye  kwenye kochi, Tunda alitumia utundu  wote kumridhisha bila kufanya naye  tendo  la  ndoa.  Alikusudia  kumchelewesha kumfikisha, makusudi  tu ili kuendelea kumchezea kwa muda  kidogo.

Kwanza Gabriel mwenyewe alikuwa akivutia.  Tunda alishavutiwa naye.  Gabriel alikuwa ni miongoni mwa  vijana wachache Tunda aliovutiwa na maumbile yao. Kuanzia nje mpaka  ndani. Kwanza alikuwa akinukia  vizuri, mwili mzuri wa kiume, msafi  mpaka ndani. Halafu pesa huwa  inamtindo wakuongeza ladha yake  kwa mtu. Tunda mwenyewe aliyekuwa  akimchezea, akajikuta akinogewa yeye  mwenyewe,  mpaka  akatamani  kulegeza masharti, lakini akakaza  roho. Muonekano wake pale kwenye   kochi, Tunda alimfurahia.

Gabriel  alikuwa akionekana kufurahia sana  alichokuwa akifanyiwa na Tunda.  Miguno ya kulalama ilipozidi kama  anayeomba rehema za Tunda, ndipo  Tunda alipomuhurumia, akamfikisha.  Alipomaliza kabisa, ndipo Tunda  akamwachia na kukaa pembeni.  Na ndipo akili yake Gabriel  ilipomrudia na kuanza kubabaika pale  kwenye kochi. “Sijui imetokea nini!  Lakini mimi ni mtu ninayejiheshimu  sana, Nancy. Usifikiri ni mtu  ninayelala hovyo na kila mwanamke.  Nampenda sana mke wangu. Nina..” Gabriel alianza kujitetea na kuongea  mfululizo huku Tunda akimtizama  kwa utulivu bila kuongeza neno.  Mwishoe Tunda akasimama. Akaenda kuvaa  nguo yake ikiwa vile vile mbichi,  nakutoka ofisini kwake.   

“Mbona unaondoka sasa?” Gabriel alisimama na kumkimbilia. Ulitaka  nifanyaje sasa? Naona unaongea  habari za mkeo tu, na kulalamika kwa  kitendo ulichofanya wewe mwenyewe! Ulitaka kuniingilia lakini nikakataa,  nimekusaidia, naona unanitupia mimi  lawama! Hujajua nini kimenileta hapa, na wala hatujazungumza!” Tunda akamgeuzia   yeye kibao na kumuongezea hukumu.  Samahani Nancy. Nahisi nimepaniki.  Unajua tokea nimeoa, sijawahi kulala na mwanamke mwingine isipokuwa  mke wangu tu. Nahisi ni hukumu tu ndiyo inanisumbua. Kuona nimeweza  kukuvulia nguo, tena wewe mwanamke  mgeni kabisa! Naomba usinielewe  vibaya kabisa. Hii siyo tabia yangu, nimeruhusu tamaa ini..”Usijali  Gabriel. Mimi ni mtu mzima, naelewa.  Tutaonana wakati mwingine.

Mazungumzo yetu?Gabriel akauliza  na wasiwasi usoni. Naomba utulie  kwanza. Naona bado upo kwenye  mshtuko. Nakuachia namba yangu ya  simu, utanipigia utakapoona upo  tayari kwa mazungumzo.” Tunda  aliandika namba yake kwenye kikaratasi  alichokuwa amekiona pale kwenye meza ya mapokezi, akaondoka  asiamini wepesi aliokutana nao kwa  Gabriel. Hakutegemea kumvua nguo  kwa haraka kwa kiasi kile! “Daaah!  Nimejikubali.” Tunda alijipongeza na  kucheka akiwa anarudi nyumbani  kwake na gauni hilo bichi. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Kesho yake asubuhi, Tunda akapanda  ndege kurudi jijini Arusha kumalizana  na mteja wake. Hakutaka kuwa  muongo kwa mteja yeyote yule.  Alikuwa mwaminifu wa muda na  maneno  yake pia.  Na  hilo  nalo  walimpendea.  Mteja wa safari hii alikuwa ni  mtumzima kidogo, mwenye asili ya  kiasia, anahusika na mambo ya madini.  Alipotua tu uwanja wa ndege  akampigia simu kuwa anaelekea hotelini.  Akamwambia atamkuta akimsubiria.  Alipofika tu, Tunda akamtuliza kwa  mchezo wa raundi kama mbili,  akatulia na kusamehe kumuacha kwa  siku hizo. Wakaendelea kuwepo naye  hapo hotelini huku akisubiria simu  kutoka kwa Gabriel.

Alipoona kimya, akaanza kujilaumu  akihisi hakutumia ujuzi wake ipasavyo  kwa Gabriel. Alirudi Arusha na yule  mteja  wake  akawa  amemaliza  kilichompeleka hapo, siku ya tatu yake wakarudi Dar. Ilikuwa jioni. Alimlipa  pesa nzuri sana. Tunda mwenyewe  akashangaa. Hakutegemea, tena ni  mteja aliyemdharau tu. Alimtongoza  akiwa hayupo hata mawindoni.  Alikuwa anakula tu mgahawani, na  yeye akaenda kukaa pembeni yake.  Tunda akamtizama na kumpuuza.  Kwanza hakuwa na asili ya  Kitanzania. Tunda hakuwahi kufikiri  kuja kulala na watu nje ya watanzania.  Akajiongelesha kwa muda huku Tunda  akila.  Alipomaliza,  muhudumu  alipomletea bili, akaomba alipie yeye.  Tunda akacheka. Akamwambia yeye ni mgeni hapo Dar, anatafuta  mwenyeji. Aliongea kingereza chenye  lafudhi ya kiasia. Tunda akacheka na  kumwambia kwa kuwa amekuwa  mwema kwake, yeye atamzungusha  mjini kidogo. 

Na kweli, walitoka na Tunda,  wakaanza kutembea. Akamsindikiza  sehemu mbili tatu, kisha akamuomba  warudi naye kwenye hoteli aliyofikia.  Tunda hakujua hata kama anayo pesa.  Bado hakuwa amemwambia ni nini  anafanya pale nchini na kama kawaida  ya  Tunda,  hakutaka  kujua  yasiyomuhusu, akaona amzungushe tu.  Akimdharau wala hakumpa umaana anaostahili. Kwanza alikuwa mkubwa  kwa umri na kwa kuwa hakuwa  amevaa chochote cha thamani, Tunda  akaona aende naye tu, akaonje yakigeni huku akijua anampeleka  sehemu ya hovyo.  Alishangaa hoteli aliyofikia. Ilikuwa  nzuri na ya pesa nyingi. Kidogo Tunda  akaanza kumtizama kwa jicho la pili.  Kuja sasa kuingia humo ndani ya  hicho chumba alichokodi, Tunda  akamshangaa na kucheka. Hakuamini  kama anaendana na yale mazingira mle  ndani.

Akamwambia huwa anafanya  vile ili kuwa huru kuzunguka ugenini  na kuweza kuzungumza na yeyote bila  kuvutia wezi. Alimwambia wakati  mwingine, ‘tajiri hana tofauti na mtumwa’.  Kwa hiyo akamwambia wakati  mwingine huwa anajishusha ili kuweza  kuwa huru na kupokelewa na yeyote  kirahisi.

Walikaa humo ndani wakizungumza  machache na Tunda, mwishoe  akamuomba penzi kiustarabu. Tunda  akampa mchezo aliovutiwa nao na  kumuomba wasafiri siku inayofuata.  Walilala usiku huo, kesho yake Tunda  akarudi nyumbani kwake kuchukua  nguo za kuvaa huko Arusha na baadhi  ya vitu. Ndipo jioni yake wakasafiri  pamoja kwenda jijini Arusha na  kumuona Gabriel. Waliachana na  Tunda palepale uwanja wa ndege wa  Dar siku hiyo waliporudi, akimwambia  kesho yake anarudi nchini kwake.    

Gabriel!

 Tunda akarudi kwake akiwa  amefurahia pesa aliyoingiza,  lakini ukimya wa Gabriel  ukaanza kumchanganya. Akiwa ndio  amepanda tu kitandani siku hiyo hiyo  ametokea Arusha, amejilaza kitandani  kwake, usiku. Akaona ujumbe  unaingia kwenye simu yake. ‘Nimepata safari ya gafla nipo Mwanza. Nikirudi  nitakutafuta.’ Tunda akajua ni Gabriel.  Alifurahi mpaka akakaa.  Akafikiria kwa haraka akaamua  kumjibu. ‘Hata mimi nipo Mwanza.  Ukipata nafasi naweza kukufuata ulipo.’ Baada ya muda simu ya Tunda ilianza  kuita.  Tunda alicheka kisha akapokea. “Kama  sasa hivi nipo tu hapa hotelini. Nimerudi  kama lisaa limoja lililopita. Na sina mpango  wa kutoka tena. Unaweza kuja tukaongea?”  

“Kuna mtu naonana naye usiku huu, Gab. Sijui tutachukua muda gani. Na ndiye  aliyenifanya nije huku Mwanza. Nikimkosa  leo sitampata tena. Yuko busy sana. Tunaweza  kuonana kesho au kesho kutwa kama utakuwa una nafasi bado. Mimi nitakuwepo huku  Mwanza kwa kama juma moja hivi.” Tunda  akadanganya.

 Basi naomba tuonane kesho, Nancy. Sipendi  kuingilia mipango yako. Tunda akacheka  kidogo. Mzima lakini? Mbona unasikika  kinyonge hivyo?” Aaah! Dunia hii,  inamambo kweli! Wewe acha tu.” “Nina kama dakika ishirini ndipo nionane na  mwenyeji wangu, tunaweza kuongea tu. Tunda aliongeza kwa sauti ya  kumuhurumia.  Kwa sauti tulivu ya Tunda, Gabriel  akajikuta akieleza mambo mengi  mwishowe akaishia kueleza mikwaruzano aliyonayo kwenye ndoa yake na jinsi  alivyomvumilia mkewe.

“Kwa nini  usitafute msaada wa wazee?” Siwezi hata  kumwambia mtu. Sisi ni viongozi pale  kanisani. Ndoa yetu ndio mfano wakuigwa  mbele ya watu. Yaani tunatolewa mifano kata  kwenye mahubiri. Leo tunawaambia vipi watu  tuna matatizo? Si tutawavunja moyo washirika  wengine?” Pole sana Gab!Tunda  alimliwaza Gabriel mpaka akatulia.  Waliagana Gabriel akiwa anacheka. Kwa mara ya kwanza, Tunda akajikuta  amevunja sharti lake yeye mwenyewe. Kupokea simu ya mteja na kusikiliza  matatizo yake kwa muda mrefu na  kumliwaza. Lakini alishavutiwa naye. 

Mwanzo wa Mengi, Jijini Mwanza.

Tunda&Gab.

S

iku inayofuata asubuhi na mapema,  Tunda alipanda ndege kueleka jiji  Mwanza kumfuata Gabriel. Alipotua tu  uwanja wa ndege wa jijini Mwanza,  akampigia simu.“Vipi Gab, unaendeleaje?” Kwanza nataka kukushukuru  Nancy, umekuwa msaada wangu mkubwa.  Umenifanya nilale vizuri sana jana usiku. Tunda akacheka kwa pozi. Afadhali  kama uliweza kulala. Wakati wowote ukiwa  na shida unaweza kunipigia. Umekula sasa?” Kuna kitu namalizia hapa, halafu kuna watu  watakuja tufanye kikao kifupi, wakitoka tu nitakutafuta ili twende tukale. Tunda  alitamani kuruka kwa furaha.

Akatafuta mgahawa akakaa hapo akisubiria simu ya Gabriel. Ilipofika saa  9 mchana, Gabriel akampigia nakumwambia yeye anafahamika sana. Hawezi  kuonekana hadharani na mwanamke  mwingine mbali na mkewe, akaomba  amfuate hotelini kwake, ili wale  chakula chumbani kwake. Lilikuwa ni  kosa kubwa sana. “Una uhakika Gab? Kama itakuletea  matatizo, sio lazima tukaonana. Tunaweza  kuongea kwa simu tu.” Tunda akamringia  kidogo. Hapana. Hamna shida kabisa.  Nitafurahi kukuona Nancy. Tafadhali usiache  kuja.” Basi kwa kuwa wewe unafahamika.  Na wameshakuona upo hapo hotelini peke  yako, sidhani kama ni sawa wakiona na mimi  naingia chumbani kwako. Kwa nini usinifuate mimi hapa hotelini kwangu? Nafikiri itakuwa  salama.” Wazo likawa zuri sana.  Akamkubalia kwa haraka sana.

Tunda alimwambia wakutane baada ya  dakika 45 ,  angempigia  simu  atakapofika hapo hotelini kwa kuwa  alikuwa mbali kidogo na kwenye hiyo  hoteli  aliyokuwa  amefikia.  Akamdanganya alikuwa ametoka  kikazi hapo hotelini tokea asubuhi.  Gabriel akakubali. Kwa kuwa Mwanza  ni kama uwanja wa nyumbani tu kwa Tunda, hakupata shida kupata hoteli.  Alishafikishwa huko na wanaume  mbali mbali. Alijua hoteli ipi unaweza  kujificha na mtu wa mtu, na  usikamatwe. 

Kwa haraka bila kupoteza muda,  Tunda akachukua taksii mpaka  kwenye moja ya hoteli aliyojua  akienda huko hatakamatwa. Nia ilikuwa na kumlinda  Gabriel mwenyewe pia. Alishamjua  Gabriel ni kuku mgeni. Sio mwizi.  Akaona wakikamatwa kabla ya  hajamuweka sawa,  anaweza kumkosa moja  kwa moja.  Akataka akamkoloze kwanza, akimuachia awe anajua njia yakurudia.

Alifika kwenye hoteli hiyo tulivu,  pembezoni kabisa ya ziwa. Mandhari  na umbali uliopo, lazima uwe na  shuguli maalumu kukupeleka huko  kama sio siku ya weekend wengi wanapoenda kuogelea. Uzuri ilikuwa ni siku katikati ya juma. Nani wa kuwafuata huko! Bei yakulipia tu usiku mmoja  hapo, alijua watu wa hali ya chini  hawafiki huko vyumbani. Akajua hata  kama watafika, ni weekend tena  sehemu ya kuogelea tu. Sio huko  vyumbani. Akajiambia akimfungia  huko Gabriel siku mbili tu, na  kumuachia, yeye mwenyewe ataanza  kumtafuta kama mwehu.  Alichagua chumba kinachoangalia  ziwa. Kizuri. Ndipo akampigia tena  Gab, kumwelekeza upande uliopo hiyo  gorofa alipokokodi hicho chumba na  sehemu zilizopo ngazi za kuelekea  huko juu gorofani kwenye chumba  moja kwa moja. Akamuelekeza na  upande chumba chenyewe kilipo pindi  atakapofika kwenye hiyo gorofa.  Alimwambia anampunguzia kupita  mapokezi au kuuliza kwa yeyote.

Alitaka apite moja kwa moja,  asishangae shangae hapo mpaka watu  wakamuona na kumtambua kama ni  yeye yuko pale. Gabriel akaelewa na kufurahia vile anavyolindwa na Tunda.  Hapo hapo Tunda akaanza kupanga  vitu vyake kwenye meza na droo za  hapo chumbani, ili kumuonyesha  Gabriel alikuwepo hapo tokea zamani  huku akimpigia mahesabu jinsi ya  kumbana mpaka usiku ule alale naye  pale, asiondoke. Swala lakumchomoa  pesa akajiambia litasubiri. Akajiambia  ni kama anawekeza kwanza kwake  mpaka atakapomkoleza amchomoe  pesa atakavyo. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Baada ya muda Gabriel aliingia pale,  akakuta Tunda ameshanunua vyakula.  “Sijui  nimekosea  kukuchagulia  chakula cha kula?” Tunda akauliza na tabasamu zuri, huku akimrembulia.  “Hamna shida kabisa. Hivyo ndio  nimefurahi. Nachukia swali la  ‘ungepeda kula nini! Huwa nalikwepa  sana.” Tunda akacheka. Akaingia  bafuni, akaosha mikono akarudi kukaa  kwenye meza. Gabriel alianza kwa  maombi, kitu kilichomfanya Tunda  acheke moyoni. Aliombea chakula na  mazungumzo yake na Tunda. Tunda  naye alifunga macho akimtafakari  Gab. Alipomaliza kuomba wakaanza  kula taratibu wakiongea hili na  kucheka lile pale sehemu ya mezani.

Taratibu Geb alianza kumlalamikia  tena mkewe. Walihamia kwenye kochi  baada ya kumaliza kula. Tunda  akaanza  kumfariji  tena  huku  akimtizama kwa macho yake matulivu,  akimuhurumia. Kama kawaida yake,  muda wote huo anakuwa mtulivu sana.   

Msikilizaji mkubwa asiyeingilia. Na  usipokuwa makini, unaweza kuongea  mpaka ya ndani sana. Yeye kimya  akikusikiliza kwa utulivu.  Alipoona hamalizi habari zake na  mkewe, akaona afupishe mambo.  “Hebu jinyooshe kwanza hapa kwenye  kochi. Vua viatu, unaweza kubaki na  soksi tu.” Gabriel akavua bila swali au  kubisha.

Tunda alinyanyua miguu yake  nakuanza kuichua taratibu huku Geb  akiendelea kuongea kama yupo kwa  mshauri wa ndoa.  Kwa utulivu ule wa Tunda, Geb  alijikuta akiongea mengi tena ya ndani  akiwa amejinyosha kwenye kochi na  miguu yake ipo mapajani kwa Tunda akionyesha uso wa kumuhurumia huku  moyoni akitamani amalize lakini Gab  aliendelea  kulalamika. 

“Tuliza mawazo Gab, naamini kila kitu  kitakuwa sawa. Jaribu kutumia njia  nyingine kwa mkeo.” Kama nini  Nancy?  Nimejaribu..” Tunda  aliendelea kucheza na miguu ya  Gabriel mpaka alipomuona maneno  yanapungua, safari za chooni haziishi.  Mara ya mwisho alirudi amevua soksi. Akajirudisha kwenye kochi na miguu  akaipandisha tena mapajani kwa  Tunda. “Nashukuru naona masaji  unayonifanyia, inanisaidia kutulia.” Unataka ya mwili mzima?Gab  akasita kidogo.

Usiwe na wasiwasi,  nia yangu nataka utulie. Siwezi  kukuruhusu ufanye kitu kibaya.  Unakumbuka pale ofisini ulipotaka  tu..” “Usinikumbushe ule ujinga  Nancy. Najutia  sana” Tunda  alimsogeza miguu yake taratibu kutoka  mapajani kwake. “Nini tena?” “Sipendi kukusababishia majuto Gab. Naomba uondoke.” Hapana Nancy,  usinielewe vibaya.” Tunda  akanyanyuka kabisa akaenda bafuni  kuoga. 

Alitoka na nguo nyepesi sana zakulalia  ambazo zilionyesha mwili wake wote  kwa kuwa hakuwa amevaa kitu  chochote ndani. Na ile nguo ilikuwa  kama chandarua chepesi. Akajidai  kushtuka Kumbe bado upo! Nilijua  umeshaondoka. Naomba uondoke  nataka kulala Gab.” Tunda alijiweka  kitandani taratibu tena baada ya  kufanya mizunguko kadhaa kama anayeweka kitanda sawa kabla hajapanda. Alijua wazi anamtesa  kwani alikuwa akimsindikiza kila anakopita. Mara kuchomoa shuka  huku, kupanga mito hivi. Kupunguza baadhi ya mito hiyo iliyokuwa imepangwa vizuri kitandani hapo na  kuiweka  kwenye  kochi. 

Aliporidhika na maonyesho yake ndipo Tunda akapanda kitandani. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Gabriel kijana wa kanisani, mtegoni. Anatoka vipi kwa Tunda aliyeshindwa kujitoa wakiwa ofisini? Cha nini kwa mke wa Gab, nakipataje kwa Tunda...

Usipitwe na muendelezo huu wa kusisimua.

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment