T |
![]() |
“Labda niulize ni sababu gani inayokupelekea
kushindwa kusubiri kwa masaa machache
ili turudi wote?” Kimya. “Au ni kwa kuwa
nimekwambia wewe sio Doris na kutaka kujua ukweli zaidi?” Tunda akamwangalia kidogo, maana
alikuwa ameinama kama anayefikiria. “Mimi ni waziri, tena wa mambo ya nje. Nakuja huku kuzungumzia mambo mazito sana. Kweli ulitegemea nisafiri tu na mtu nisiyemfahamu, tena baada ya kukataa mimi nisikate tiketi!?” Tunda
akashtuka sana. Hakujua vile
alivyomkatalia yeye kukata tiketi
kungeibua maswali kwake kwa haraka
kwa kiasi kile. Kwanza hakujua hata
kama kwake inamaana. Tunda
alimkatalia kijanja, akimzuga kwa
penzi zito, asijue mwenzie hakuwa
waziri kwa awamu ya uongozi makini
kama huo na kushika nyadhifa kubwa
kwenye awamu za maraisi wengine
kwa bahati mbaya.
Mbawala alishakuwa balozi
akiwakilisha Tanzania kwenye nchi
za ulaya kwa muda mrefu sana, tena bila
kuvuruga. Inamaana akili ipo. Na yupo
makini. Huwezi kumdanganya kitoto. “Nina maadui, ndani na nje ya nchi. Kuna watu wanatuma wasichana wengi tu kuniwinda kwa mapenzi ili kunitega. Lazima kujua nipo na nani na
kuwa makini na
kila ninachokifanya.”Alizidi
kumtisha Tunda.
“Baada ya kukataa tiketi
ya bure kutoka kwangu, tena kwa
safari niliyoomba mimi, ikabidi
kujiuliza na kukufanyia utafiti. Nisingeweza kuwa hapa
na wewe, bila
hata kukuchunguza!?” Mwili mzima
wa Tunda ulikuwa ukitetemeka,
asijue ajibu nini.
“Lilitafutwa
hilo jina la Doris bila kuleta majibu
yanayoeleweka. Wasiwasi ukazidi
kuniingia kwa kuwa tulishakuwa wote kwenye gari pale Mlimani city lakini
ilikuwa gizani kisha ukapotea tu pale
Mlimani city. Hata mlinzi wangu
alipojaribu kukufuatilia, ukawa kama
umempotea. Yeye akasema jinsi ulivyompotea, ni
kama mtaalamu. Yeye akakuchukulia
kama mpelelezi. Akasema msichana
wa kawaida asingeweza kumpotea
vile.” Tunda akashtuka zaidi.
“Ndio huyo mlinzi wangu
ikabidi kutoa wazo la kupata picha
yako mwangani ili kukuchunguza
zaidi. Sikujua kama umetumwa na nani,
kwa sababu hata namba ya simu uliyoitumia kunipata mimi, ni ya siri. Siwapi watu hovyo. Anayo raisi wetu, watoto wangu, mke wangu na watu wasiozidi hata 7 mbali na hao niliokutajia. Tena nao ni viongozi wa juu sana kwenye nchi zao. Ambao simu zao huwa hazisubiri. Popote pale nikiona mtu anapiga kwa namba hiyo, lazima
nipokee. Hata wewe
nilikwambia.” Tunda alishtuka sana. Akatamani hata kupotea pale. Lakini
na yeye akafikiria kwa haraka.
Kitu kikamshtua na kumuumiza. Akaona aulize. “Subiri
kwanza Mbawala. Usiniambie kuwepo kwako
pale uwanja wa ndege siku ile ilikuwa
njia yakunipata ili watu wako wanipige picha ili unichunguze zaidi!?” Tunda akauliza huku midomo ikimtetemeka. “Ningefanya nini wakati
uli....” “Don’t.” Machozi yakaanza kumtoka Tunda. Akamnyamazisha kwa haraka, na kumwacha waziri haelewi. “Tafadhali acha tu.” Tunda akaendelea kumsihi huku akilia.
“Nilifurahi sana kukuta ukinisubiria pale, Mbawala! Ulinyanyua kitu ndani yangu ambacho sikuwahi kukipata kwa yoyote yule ila kwako wewe pekee. Nilikuja
huku kwa furaha, nikashindwa hata kutoka
nje, nikikutaka tu wewe. Ndio maana
nilikuwa sichoki kila unaponigusa au
ninapokutizama kwa kile nilichofikiri
ni uthamani uliouweka kwangu. Kumbe ulikuwa umenifuata uwanja wa ndege kama muwindaji ili walinzi wako wanipige picha, na sio upendo!” Tunda alisikika akiwa ameumia sana. “Doris!” “Tafadhali usiongee
chochote Mbawala. Please.” Tunda akatoka
pale chumbani.
Tunda alitoka nje kabisa ya lile jengo akaanza kulia kwa uchungu sana hata asijue ni kwa nini. Mbawala alimpokonya
tumaini kubwa alilolijenga ndani ya siku chache sana tokea
wakutane. Alilia sana. Gafla akakumbuka analo tatizo kubwa zaidi ya kuumizwa
hizo hisia zake. Hofu ikamwingia asijue
yule baba amejua nini juu yake. Mambo
mengi yalipita kwa wakati mmoja kichwani
kwake, yakavuruga tumbo lake zaidi.
Akaanza kutapika tena. Safari hii
yalikuwa mate tu yanayotoka. Mwishoe akatafuta
sehemu akakaa. Nje tu. Tena akakaa
chini kabisa kwenye kijiukuta kidogo
kilichojengewa kama urembo
membeni ya maua.
“Nini amegundua juu yangu? Amejua
kama mimi nafahamiana na mwanae?”Akajiuliza kwa hofu. “Au amejua kama niliiba namba yake ya simu kwenye simu ya mtoto wake?” Tunda akajiuliza huku
akitetemeka na machozi yakimtoka huko
ugenini. “Lakini kama tena angekuwa amekumbana na kitu asichopenda, asingenifuata huku na kukaa naye siku zote hizi. Na asingeniuliza ni nani ninayemuhofia kuonekana naye. Angemtaja tu.” Kidogo hilo likamtuliza.
Akakumbuka alivyokuwa akimfurahia kitandani.
“Wote wananifurahia
kwenye mapenzi, halafu wanakuja
kunigeuka. Niache kujidanganya.” Akakanusha ile furaha aliyomuona nayo Mbawala wakiwa naye. Akakataa kujiweka kwamba yeye ndio sababu. “Anajua kama mimi ni Tunda? Amenichunguza wapi? Walifanikiwa baadaye kuja
kufika kwangu ili kunichunguza zaidi?
Nini wamejua juu yangu!? Wanaweza kuwa
wametumia simu yangu mimi
mwenyewe kufika kwangu. Labda kwa
kufuata gps!”
Tunda akazidi kuingiwa hofu na kushindwa
hata kutembea. Alikaa pale bila kujua
muda unazidi kwenda.
Akatamani abadilishe yale maisha. “Naanzia wapi tena?”
Akajiuliza huku akihesabu garama za maisha zinazomkabili. “Halafu nije kuishi kama Tunda tena!?” Hapo machozi yakaanza kumtoka tena kwa upya. Tunda ni mtu wa mwisho kabisa hata yeye hakutaka kumuona. Akaanza kukumbuka maisha aliyoishi zamani kama Tunda. Kuanzia mtoto mpaka mkubwa. Alivyosalitiwa na kufukuzwa kwenye majumba ya watu. Chuki ikajaa. Maana
alikumbuka tukio moja hadi jingine
nakuzidi kumchukia Tunda. Hakutamani
Tunda aje aishi tena duniani. “Tunda ni
jeusi, baya jitu la kutumiwa mwili wake
bila huruma wala heshima.
Linatukanwa na kufanywa vile mtu
anachopenda. Halijasoma. Namchukia
Tunda. Kwanza sitaweza hata kulala
nikiwa Tunda.” Tunda akazidi kulia
peke yake. Akiwaza hili na
kujiogopesha kwa lile. Mpaka akatulia
mwenyewe.
Hapakuwa na jinsi. Hawezi kutoroka kwenda popote. Yupo ugenini na vitu vyake vipo hotelini. “Heri nirudi tu. Yule baba analindwa. Ukute hata hapa walinzi wake wananiona.” Alipoangalia saa yake,
akashtuka sana. Ilishakuwa ni saa nane
na nusu usiku. Akasimama kwa haraka,
akaamua kurudi hotelini. Hakuwa amefika
mbali.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alimkuta Mbawala amelala. Hakuwasha taa. Aliingia kuoga, akaamua kulala sehemu ya makochi. Akajilaza taratibu kama asiyetaka kumsumbua Mbawala. “Njoo ulale kitandani.” Akasikia sauti
ya Mbawala. Akabaki kimya. Akamuona amesimama anamfuata. Akawasha taa. “Twende ukalale kitandani.” Akasisitiza huku
akimshika mkono. Wakarudi kitandani.
Mbawala akamfunika vizuri, akalala nyuma yake,
alikuwa amempa mgongo. Wakatulia
kwa muda.
“Ndege yako
inaondoka saa ngapi?” Waziri
Mbawala akamuuliza taratibu. “Saa nne na nusu.”“Utafikaje uwanja wa
ndege?” “Nitatumia shuttle ya hoteli. Wamesema watanipeleka.”
Tunda akajibu taratibu. “Nina kikao saa tatu asubuhi, najua nitakuacha ukiwa umelala. Kwa kuwa nitaondoka mapema kidogo
ili nikaweke mambo sawa. Mimi ndio
mzungumzaji kesho. Inabidi kuwahi kuwapelekea vitu ambavyo nitahitaji wavionyeshe
kwenye projector. Kwa hiyo nitaondoka kama kwenye saa moja na nusu.” Tunda akatulia akiwa anamsikiliza,
hakujibu kitu.
Wakatulia tena kidogo. “Nimekuwa na wakati mzuri. Asante.”
Waziri aliongea taratibu. Tunda akavuta pumzi na kutulia tu asimuelewe anataka kumfikishia ujumbe gani. Kuwa ameridhika na uchunguzi walioufanya juu yake au! “Unafikiri nitakuja
kukuona tena?” Tunda akatingisha kichwa
kukataa. Mbawala akambusu shingoni.
“Naomba ukibadili mawazo unitafute tena.” Tunda
akajikuta anaanza kutokwa na machozi. “Nilijua ulikuja uwanja wa
ndege kuniaga Mbawala. Sio kuniweka
mwangani kwa walinzi wako!
Nimeumia sana. Umenipokonya kitu
kikubwa sana. Hata
natamani usingeniambia.
Ukaendelea kunidanganya kwa muda.” Tunda akalalamika kwa
kuumia sana.
“Naomba unielewe.” “Hilo ndilo tatizo linaloniumiza Mbawala.
Nimeelewa. Natamani ingekuwa vinginevyo.”
Tunda akaendelea kulia taratibu. “Naomba niangalie.
Tafadhali.” Tunda akamgeuka taratibu. Akawasha taa ya pembeni ya kitanda. “Naomba unielewe mama. Sijui nani nimwamini. Nazungukwa na watu wabaya watupu. Nawindwa
kuliko nitakavyokwambia. Watu wanawinda
roho yangu kwa kila namna sababu ya
majukumu yangu. Wanatumia mpaka watu
wakaribu yangu kuniangamiza.
Inanilazimu kuwa makini sana.” Tunda
alimsikia akiongea kwa kukubembeleza
kama anayejutia. Kidogo ikampa
moyo.
“Uliniogopesha kidogo
uliponitumia ujumbe kwenye simu yenye ile namba. Ndio maana nikakupigia kwa haraka. Sauti yako
ikanivutia, nikataka kukuona. Kumbuka
wewe ndiye uliyependekeza mpaka eneo la kukutania. Nikaingiwa kidogo hofu. Lakini ukawa tena kama unanilinda nisionekane na watu. Ikawa nafuu tena.
Nikakukubalia. Kuja kukuona upo mtulivu
tu, na mapenzi yale, nikafurahia. Lakini
ulipokataa tiketi, nikajua moja kwa moja unakitu unaficha. Ni nini! Ndio nikajua hutaki nijue jina lako kamili. Nikaingiwa tena na hofu. Nikakumbuka mara kadhaa pale tulipokuwa kwenye gari, ulikuwa ukiingia
kwenye pochi yako tena katikati ya mapenzi.” “Nilikuwa nikibadili kondom, Mbawala.” Hapo Tunda
akajitetea.
“Hata hilo wazo halikunijia.
Maana unayo jinsi yako, ni ngumu kuelewa
unapokuwa unabadili. Ni hapa hotelini
ndipo nilielewa kuwa huwa unabadili
kondom hata katikati ya mapenzi,
nikiwa hata sijafika. Ikaniongezea
ujasiri wakujua kuwa nipo salama pia.
Lakini wakati ule hata sikufikiria.
Nafikiri ni sababu
ya hofu. Nikajiambia labda unarikodi au sijui. Lakini
ukumbuke ulianza kwa kuniita waziri Mbawala. Nikakwambia tukiwa wote usiniite
waziri. Unakumbuka?” Tunda akakumbuka. “Lakini
mimi sikujua kama ni kwa kujihami, Mbawala! Nazidi kuumia kuona nilikuelewa vibaya na kujiwekea tumaini
ambalo hata halikuwepo.”
“Tafadhali usiumie, ila
nielewe tafadhali. Nimesalitiwa
sana. Nimeumizwa, ndio maana
umekutana na Mbawala huyu aliyekuumiza
na wewe. Ila sikukusudia kukuumiza kwa
namna hii.” Akambusu mara kadhaa juu ya kipanda uso na kumfuta machozi.
Tunda alimuwekea hukumu moyoni.
Alilia kwa kumaanisha kutoka moyoni.
“Unajua baada ya kukubali kuja huku,
na walipokuchunguza na kukosa
sababu. Wakaniambia sio mtu
hatarishi, basi nikajiambia labda umefurahia tu kampani yangu. Unataka kunitumia kama wengine. Nikajiambia
basi na mimi nifurahie huu muda. Ndio nikakufuata hapa. Kwa muda wote tumekuwa hapa, nimekufurahia
sana. Nikazidi kukusoma nakukuamini sio mtu hatarishi kwangu. Umetulia. Huna papara.
Unanifurahia kila ukiniona. Ila
nimegundua kuna mambo au jambo
unanificha, ndio maana nilikwambia
ili kama utaniamini, basi ufunguke ili
kuendelea kufahamiana zaidi.
Natamani hapa isiwe mwisho.” Tunda
akavuta pumzi kwa nguvu. Hakujua
anatakiwa aombe msamaha au aseme
nini! Kuomba msamaha, inamaana
aeleze ukweli wake wote. Amwambie
amelala na mtoto wake! Hatataka hata
kuja kumuona tena.
“Kwanza atanishangaa nimewezaje kulala nao wote
wawili! Ataniona ni mchafu wa
kupindukia.”
Tunda akapinga hilo wazo. Je, ajibu hata
hilo la wapi amepata hiyo namba yake
ya simu! Amwambie aliiba namba yake ya simu kwa mwanae! “Sithubutu. Atahisi na yeye nimemwibia mambo yake kwenye laptop yake au simu yake. Na hivi alisema anamajukumu mazito, ndio mwanzo wakuishia jela wanifunge.” Tunda akaona bora nusu shari.
“Unataka uwahi kulala ili
kesho usiamke na uchovu?”
“Sio kikao
cha muda mrefu. Kama hapatakuwa na kingine kitakachojitokeza huko kwa wenyeji wetu, kikao kikiisha naweza kurudi kupumzika mpaka jioni nitakapokuwa nikiondoka.” Wakatulia kidogo. Mbawala akiwa amepata jibu lake.
Hataki kuwa muwazi kwake. Tunda akitamani kama ingekuwa tofauti. Alivutiwa sana na waziri Mbawala.
“Naomba uniage.” Tunda akaongea
taratibu na kwa upendo. Mbawala
akachangamkia penzi. Safari hii ikawa tofauti. Wawili hawa wanaagana kutokuonana
tena wakiwa walisharidhishana sana haswa
kitabia. Tunda alishamwambia
hatamtafuta tena. Kila mmoja alijawa
nguvu na huzuni ya kuagana ila wasijue
kile kinachoendelea kichwani kwa
mwenzie.
Kwa Tunda huzuni ya kumpoteza aliyejua ni Sadiki mwingine. Tena bora zaidi. Kwa Waziri Mbawala alipata dogo dogo wa kumtuliza na kumliwaza popote tena kwa wepesi, alijua atajaza pengo kubwa la mapenzi alilonalo nyuma ya pazia,
mbele ya umati akijulikana anayo ndoa
swafi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alamu ya simu ilikuja kumuamsha saa mbili kasoro. Alipoangalia pale chumbani, hakumkuta Mbawala. Akajua alishaondoka. Akaingia kuoga alipotoka akiwa anavaa na kujitengeneza mbele ya meza ndogo aliyokuwa
ameweka vipodozi vyake, akaona bahasha.
Akajua ni pesa tu kutoka kwa Mbawala.
Kwa haraka akaifungua. Alikuta dola
nyingi, mpaka akakaa. “Huyu
Mzee amenifikiriaje kutokana
na alichokigundua kwangu!? Pesa
yote hii!” Mpaka mikono ikaanza
kutoa jasho. Akaiweka chini ile
bahasha akabaki akiitazama.
Tunda akatamani ingekuwa tofauti pengine angemtafuta tena. Lakini moyo wake ulishageuka hapo, akashidwa
chakufanya. “Siwezi
kuja kumtafuta tena. Ananichunguza!
Nitaharibu kila kitu. Atakuja kufufua
mengi mabaya yanayoweza kuja
kuniingiza matatizoni. Mwishoe aje
amfufue na Tunda
ambaye nilishamzika muda mrefu sana. Hapana.” Tunda akawaza akiumia, akijua wazi
inampasa kurudi nchini na kuendeleza biashara ya ngono kwa asiowajua ili aweze
kuishi mjini.
Akavuta Note pad na kalamu vilivyokuwa
hapo pembeni, vimewekwa na hotel, akaamua kumuandikia. ‘Mbawala, asante kwa wakati
mzuri sana na waheshima ulionipa. Asante kwa pesa. Nakushukuru sana. ASANTE.
Nakutakia kila la kheri.’
Hivyo tu, akakiacha hicho kikaratasi
kwenye kona ya kioo. Kwamba lazima angerudi, angeikuta. Bado aliacha
vitu vyake vya thamani humo ndani.
Tunda alichukua vitu vyake tu, na kuondoka pale hotelini. Usafiri wa hotelini ndio alioutumia kumfikisha uwanja wa ndege.
Kama kawaida yake, aliwahi kabla
hata ya muda wa abiria wa kimataifa
wanavyohitajika kufika uwanja wa
ndege. Aliondoka nchini Afrika ya
kusini akiwa ameumia tofauti na
alivyofika hapo. Anamuacha Waziri
Mbawala ambaye alishaanza kuvutiwa
naye! Akajisikia ni kama amempoteza
kwa kifo kama alivyompoteza Sadiki
kwa gafla akiwa
ameshaanza kunufaika. Waziri
Mbawala peke yake, kwa hongo ya kwanza
tu, alionyesha anao uwezo wa kumuweka
jijini bila kuhangaika na wengine.
Akiwa kwenye ndege akaendelea kujifikiria. Hasira kwa ndugu zake zikamjia. Akachukia kila mtu. “Wote ni wasaliti. Wangenitunza hata kimasikini tu kama vile zamani kwa bibi, nisingefika kote huku.” Tunda akazidi kuumia na hasira kupanda. “Nitaanza na Mihayo. Nikimpata yeye, nitalipa kisasi kwa watu wanne kwa mpigo.” Jazba ikazidi kumpanda.
Kisasi.
A |
lipotua
tu uwanja wa ndege wa Mwalimu
Nyerere,Dar akampigia simu Tewele. “Nilikuwa nakuwaza sasa hivi! Ila ikabidi niwe mstaarabu kwa kuwa uliniambia utanitafuta.” “Vipi,kwema?” Tunda akauliza huku akicheka taratibu. “Kwema. Nina safari
ila sio ile niliyokwambia. Ile Mihayo ameninyima bwana. Nasikia anakwenda mwenyewe. Ila kuna kikao cha siku mbili tu Bagamoyo, na mimi nimo kwenye orodha ya watu wachache
aliochagua yeye tuhudhurue. Na yeye atakuwepo. Ameita viongozi wote wa bandari. Ngazi za juu tu.
Tanga, Zanziber na hapa. Sio siku nyingi,
lakini naona zitatufaa. Na hivyo ulivyo
mtulivu, nikakufikiria wewe wakuzitumia hizo siku chache pamoja kwa
utulivu.” Tunda akacheka kidogo.
“Sasa si utakuwa kwenye mkutano?” Tunda akamuuliza kama hataki wakati alitamani kuruka kwa furaha yakwenda kukutanishwa na Mihayo. “Hujaelewa mama. Tuna siku mbili ambazo ni zetu peke yetu. Usiku kucha tupo wawili tu. Hakuna haraka yakuwahi nyumbani. Mimi na wewe. Nakupa ruhusa unipagawishe utakavyo!” Tunda akacheka sana. “Lakini usiku mmoja lazima uutumie na Mihayo, au atakuwa na mwanamke wake?” Tunda aliuliza makusudi ili kujipanga. “Sidhani. Si unakumbuka nilikwambia aliacha kazi? Hawezi kuja kujitokeza mbele ya wafanyakazi, tena ngazi ya juu wa bandari!” “Basi ndio kujipanga vizuri. Tukiwa huko tutazungumza zaidi.” Wakazungumza zaidi na kukubaliana hiyo alhamisi juma lijalo atampitia Mlimani City, waelekee Bagamoyo pamoja.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tunda
akajiambia anazo siku zakupumzika mpaka hiyo alhamisi. Ilikuwa ijumaa aliporudi
nchini. Lakini alikuwa amechoka
na kusafiri. Akamtumia ujumbe
Mbawala Junior, mtoto wa waziri. ‘Kesho yako ikoje? Naweza kuwa na nafasi.’ Hapo
hapo akampigia. “Nakuja
mama. Jumamosi yote na jumapili nakupa wewe.” Tunda akacheka.
“Ukifika hotelini utanijulisha basi,
ili nikufuate.” “Ngoja niangalie tiketi ya kesho asubuhi. Si ni sawa?” “Sawa. Lakini
asubuhi ya saa nne siku ya jumapili, itabidi niondoke, nina miahadi ya saa 6 mchana.” Tunda akadanganya. Asingethubutu kumpa siku mbili. Aliijua
shuguli yake. “Hiyo siku ya jumamosi tuliyoipata,
tutaitumia ipasavyo.”
Tunda alicheka kumridhisha, lakini
alijua hatanii. “Hayupo hata nusu ya baba yake. Yupo rafu!” Akajisemea moyoni. Lakini kwa kuwa alijua kutoa pesa nzuri kama baba yake, hakutaka kumpoteza na yeye kwa kumsubirisha muda mrefu, mpaka akakata tamaa na kumfungia mlango. “Asije tafuta msichana mwingine bure. Acha nimuweke karibu hivyo hivyo.”
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alifika kwake na kujitupa kwa uchovu na mawazo. Alimpoteza Waziri kitu kilichobaki kikimuuma. Alilala siku nzima kwa ushovu wa safari lakini zaidi penzi la Waziri. Alipoamka usiku alikula na kurudi kulala. Asubuhi kabla hajakwenda kwa Mbawala mtoto, akaenda kwenye masaji kufanya mwili wake utulie. Akatengeneza na kucha. Nywele zilikuwa kwenye muonekano mzuri, akaona aziache, lasivyo angemchelewa Mbawala ambaye alimtegemea kufika hapo wakati wowote.
Kwa Mbawala Junior.
I |
liposika
saa tano na robo, Mbawala akapiga simu kumtaarifu kuwa ameshatua jijini na yupo
hotelini anamsubiria. Akamtajia namba ya chumba na kumwelekeza alipo. “Nitakuwa hapo baada
ya dakika 40 kuanzia sasa.” “Nakusubiri
kwa hamu.”
Tunda alijua
kazi imeshaanza. Alishajiambia mapumziko
ni mpaka kesho yake watakapo achana. Mpaka akamuhisi anatumia dawa kumuongezea
nguvu! Lakini alilala usiku kucha na
mchana alipofika kutoka Sauzi. “Nipo
tayari kumkabili.” Akajipa moyo
huku akikumbuka ule muda wa
kupumzika katikati ya mapenzi.
Akapumua kidogo. “Hapo naweza
kupumzika hata kulala na mimi kidogo.”
Lakini akakumbuka Mbawala nayeye huwa analala tena
kwa kukoroma sana. Akachoka gafla kabla
hata hajaanza kazi yenyewe. Lakini akajiambia ni kwa siku moja tu, atakwenda kupumzika nyumbani kwake.
Alifika hotelini mpaka kwenye chumba alichomuelekeza. Akagonga. Mbawala alifungua mlango akiwa anaongea na simu. Akamuonyeshea ishara aingie tu. Tunda akaingia. Akapomkea
na busu. Kama kawaida alikwepesha mdomo, akamkumbatia, akampa la sikio. Mbawala akacheka. Mtu wa kwenye simu bado alikuwa akiongea. “Kwa nini
usimuache tu, baba?” Tunda akachutuka baada ya kusikia hivyo. Akajua anazungumza na baba yake. “Uwamuzi ni wako baba. Wewe amua vile
unavyotaka. Lakini kuwa makini kwa wadhifa wako na hayo mambo
yakienea, yanaweza kukuharibia mipango
yako yote. Hutaki kujitia doa sasa hivi.”Akamsikia baba yake akijibu. “Hapana dad. Huo ni ushauri wangu tu. Unaweza kuuchukua au kuuacha. Ila ninachotaka kukwambia ni kuwa, nakuunga mkono kwa kile utakachoamua.”Akatulia kidogo kama anayesikiliza.
“Dad!?” Akamsikia akiuliza kwa mshangao mpaka usoni. “She is my mom!
Ulitegemea nisimjulie hali!” Akasikia baba yake
akiongea kwa sauti ya ukali. “Dad Please!” Mbawala Junior
akasikika akimsihi baba yake. Mzee
akaendelea kuongea kwa jazba. Bado
Tunda alikuwa hajaelewa
kinachoendelea juu ya huyo mke wa
waziri na familia yake. Akaona atulie
asikilize. “Naomba nikupigie kesho dad. Tafadhali. Am in the middle of something.” Baada
ya muda wakusikiliza, akamsikia
Junior akimuomba baba yake akate
simu.Kimya. “Dad?” Akamuona anaangalia simu yake.
“Amenikatia simu!” Akaweka simu pembeni
akilalamika kidogo. “Kwema?” Tunda akauliza taratibu.
“Daah!
Wazee hawa wanatuchanganya kweli!
Hatujui hata jinsi ya kuwasaidia.” “Nini tena?” Mbawala akasita. “Daah! Ndoa zina mambo yake Fina! Naomba tuyaache tu,
tuendelee na yetu.” Akajibu, na
kuanza kumchangamkia. Tunda akajua hataki kuzungumzia hilo.
Akakubali kutumika tu.
Wakiwa katikati ya mchezo huo aliokuwa akiuendesha Junior kwa uchu wote, simu yake ikaanza kuita mfululizo. Kila alipojaribu kupuuza, ikaendelea kuita tena na tena. Alitoka pale
kitandani kwa hasira. “Ni nini jamani!?” Akapokea huku akilalamika.
Sauti ya kike ikasikika upande wa pili. “Come on!”
Junior akasikika akishangaa kwa sauti. “Sijamkatia simu,
yeye ndiye amenikatia simu! Ila nimemwambia siwezi kuacha kumpigia simu mama, labda ndio maana amekasirika.” Mbawala akasikiliza. “No way T! This is my mom we
are talking about here!” Akabisha na kuendelea kusikiliza. Tunda akajua anazungumza na dada yake Taffy. Akamuona ni kama aliyekubali yaishe. Mwishowe
akajibu, “Fine.” Mbawala akajibu na kusikiliza tena kidogo. “Si nimesema sawa! Ama!?”
Akajibu kwa hasira kidogo.
Nakuendelea kusikiliza zaidi. “Nitakuja kesho
mchana. Sio leo. Leo nina kitu cha
muhimu nafanya na siwezi kuahirisha kwa matatizo
ambayo sina uwezo wa kuyatatua. Mama ameamua
kuendelea na maisha yake, kwa nini na
wewe usimshauri dad aendelee na maisha
yake amwache tu, watu tupumzike! Kwa vikao hivi vya kila siku unafikiri
itasaidia nini?” Hapo Tunda akaelewa kwa
kiasi. Akamuona Junior anasikiliza
tena kidogo. “Nimesema
nitakuja kesho, na wewe zungumza na dad.
Tafadhali Taffy. Huu ni usumbufu, na ni
kama adhabu ambayo hatustahili. Dad is
smart than this. Na wote tunamjua mama
anamsimamo wake. Akisema hapana ni hapana.
Hawezi kurudi, na siwezi kuacha
kuwasiliana naye kwa wao kushindwa
kuelewana!”
Akatulia
kama anayesikiliza. “Basi kama ni
hivyo, atakuwa amenichagua mimi
wakunimalizia hasira zake.” Akamsikia akijibu. “Naomba nikuage, nitawaona
kesho tafadhali. Nakata simu. Sasa sio
na wewe uje kusema nimekukatia.
Nimekuaga.”
Hapo hapo akakata na kuzima simu yake.
Akuitupa kwenye kochi kwa hasira.
Akaelekea chooni.
Ndio Tunda akaelewa sasa. “Labda ndio maana baba yake alisema hamna shida akionekana na mimi hadharani na hana haraka yakurudi nyumbani!” Tunda akawaza. “Nashuguli yote ile,
inawezekana alikuwa na ukame wa miaka!” Akaendelea kuwaza.
Akamuhurumia jinsi alivyomuacha na kumwambia hatamtafuta tena huku waziri
akimwambia anatamani kuja kumuona tena! “Atajiona ana mkosi baba wa watu. Kila mwanamke anamkataa.” Tunda akawaza akiwa peke yake pale chumbani, bado Mbawala alikuwa amejifungia chooni. Hakutaka hata kumfuata. Akaona ajipumzishe. Walishazungushana hapo kwa muda
mrefu bila kupumzika. Mbawala Junior akiendeleza rafu zake.
“Alikuwa Afrika ya kusini, kidogo tukapumua. Akatulia kwa siku mbili tatu wala hakutafuta mtu. Amerudi na kelele. Na T naye anamsikiliza kwa kila jambo! Mimi ndio nakuwa mbaya badala ya mkewe!” Akatoka Mbawala akiwa
amekasirika akiongea. “Umekula?”
Tunda
akamuuliza kwa upole tu. “Naona tuagize chakula tule. Washanichanganya na kunikata stimu yote!” Akajitupa pale kitandani,
Tunda akapiga simu kuagiza chakula. “Hayanihusu tena? Hata nikijua, siwezi kusaidia. Huyu baba anaonekana anatafuta mwanamke wa kudumu.
Nikimtafuta tu, na hivi alishaanza
kunichunguza, atakuja kufufua hata
ambayo hayatamkiki. Atanidharau na
kunihukumu kwa atakayoyasikia.” Tunda akawaza na
kuamua kukaa nao mbali.
Waziri
alikuwa mtu mzuri,
alimfurahia. Lakini katika maongezi na
mtoto wake huyo, alihisi ni kama
anazo mbio za kuja kugombea uraisi. “Na hivi hana shida
yakuonekana na mimi hadharani, watu
wataanza kunichimbua. Watakuja
kuanika uozo wangu wote! Hapana.
Sipo tayari kuja kuzungumzia
hadharani maisha yangu ya nyuma.”Tunda aliendelea kuwaza alipokuwa na Mbawala Junior hapo hotelini mpaka kesho yake muda wote
wanaachana, Mbawala akimwambia anakwenda
nyumbani kwao kwenda kusikiliza matatizo ambayo hayajaisha na wanayazungumzia
zaidi ya miaka miwili.
Tunda
alichukua pesa zake,
akajiondokea hapo hotelini akiwa na
usingizi. Hakika Mbawala huyu
alikuwa mkoromaji sio kama baba
yake aliyekuwa analala
amemkumbatia. Tunda alikesha hapo. Na asubuhi hiyo pia, alimuaga
kama ndio wanakutana wakati
wametoka kulala kitanda kimoja!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tokea anatoka kwa Mbawala pale hotelini alianza kupanga mipango ya jinsi ya kumkabili mjomba wake, Mihayo huko Bagamoyo. Nini afanye? Ajifiche na kumfanyia ujanja au ajitambulishe ili amkumbuke Tunda aliyemtesa ndiye huyu wa sasa! Lakini hakutaka Tewele hata ahisi kuwa wanafahamiana. Atafanyaje? Ndicho kilichokuwa kikimuumiza kichwa Tunda. Juu ya
mapenzi kwa Tewele, hilo hakulitilia
shaka hata kidogo. Tewele mchokaji. Mara moja au mbili kama akijitahidi sana. Tena hana purukushani nyingi. Alimuona mwili wake unamlemea. Hilo alilifurahia sana Tunda
na kujiona anakula pesa kwa urahisi.
Tewele akamuona Tunda kinara, sababu
hakuwa akiweza shuguli nyingi. Sehemu
kubwa, Tunda alifanya kazi yote yeye
akiwa ametulia akifurahia tu.
Tunda
alipiza kisasi chake kwa Ulaini, Mambo
yote yanajipanga huko Bagamoyo
T |
ewele
alimpitia hapo Mlimani city ikiwa mapema
tu hiyo siku ya alhamisi kama
walivyokubaliana. “Ulivyopendeza!” Tewele akamsifia wakati anaingia garini. “Yote hii kwa ajili yako.” “Nakushukuru Irene. Najua
tutapata wakati mzuri. Na hivi
tutalipwa, naamini pesa ya safari hii
haitakuwa ndogo.” Hilo likamfurahisha
Tunda. Walipofika Bagamoyo kwenye
hoteli wanayofanyia huo mkutano na
kulala, ilibidi Tewele ashuke akachukue chumba chake kama mfanyakazi wa Bandari, ndipo ampigie simu Tunda amfuate. Sio kuongoza.
Kama kawaida ya Tunda, akawa ametulia kimya
pale ndani ya gari. Akiwa amekaa, akashangaa kumuona Mihayo
anatoka ndani ya ile hoteli akiwa kwenye
simu. Ikasogea gari aina ya RAV 4 mpyaa, ikasimama karibu kabisa na Mihayo. Ilikuwa gari nzuri sana ya rangi ya damu ya mzee inayowaka vizuri. Tunda akaendelea kuangalia. Akamuona Mihayo, mjomba wake akienda moja kwa moja mlango wa nyuma.
Akapunga mkono huku akicheka. Kwa haraka
sana Tunda akatoa simu yake nakuanza
kuchukua video. Akamuona mjomba
wake anafungua mlango na kuinama
kwa muda. Hakuwa akisikia chochote sababu gari aliyokuwepo ilikuwa imefungwa vioo mpaka juu, gari bado imewashwa.
Mziki ukiendelea kutumbuiza taratibu. Tewele aliacha miziki
yake ambayo kwanza hata Tunda hakuwa
akisikiliza.
Akashuka dereva kwenye ile gari ya aina ya RAV 4,
alikuwa mdada. Alionekana sio mtu mzima,
lakini anamwili mkubwa. Sio kama shangazi yake aliyekuwa mwembamba. Ila
yeye mrembo na ana rangi nyeupe. Akamuona mjomba wake anamtoa mtoto kwenye gari. “Haaaa!” Tunda akahamaki nakuendelea kuchukua video. Akazima redio na kushusha kioo ili angalau aweze kupata maneno. Alikuwa mtoto wa kiume. Mzuri sana. Umri kama
miaka miwili hivi. Nywele zilikatwa
vizuri, na alikuwa nadhifu sana. Mihayo alipomnyanyua
juu huku akimbusu, yeye akiwa amempa
Tunda mgongo lakini mtoto ni kama wanatizamana na Tunda. “Haaaa!” Tunda
akahamaki tena. Walifanana sana na mjomba wake, kama mapacha, kasoro rangi yule mtoto alikuwa mweupe.
Tunda akaanza kupiga picha huku akiwachukua video wote watatu. Hakuwa mbali sana, lakini Mihayo na yule
dada, walionekana kujali mambo yao tu.
Hawakuangalia kulia wala kushoto ila
wao. Akamuona mjomba wake anambusu
midomoni yule dada, tena kwa hatua wala
si haraka. Akiwa amembeba mtoto, dada
amesimama pembeni yao akipokea
busu. Simu ya Tewele ikaingia.
Akachukia Tunda, lakini ikabidi apokee
kwa kuwa ilijaa kwenye kioo chote cha
simu, hakuona tena kinachoendelea
kwa familia hiyo
aliyokuwa akiichukua video.
“Nimekutumia ujumbe wa chumba
nilichopo. Umepata?” “Nakuja
sasa hivi.” Tunda akajibu kwa kifupi
tu, na kukata simu. Akarudisha akili na macho
kwa mjomba wake na nyumba ndogo yake.
Akamuona akiwa amebeba mtoto na badhi ya
mizigo yao, wanazunguka nyuma ya ile hoteli kama wasiotaka kupitia mbele njia ya kawaida, yule dada akifuata nyuma na baadhi ya
mizigo. Akachukia kuwachelewa kidogo akiwa anazungumza na Tewele. Lakini akawachukua tena video huku akiwapiga picha wakati wanapotelea vyumbani.
Wazo likamjia kwa haraka. Akashuka ndani ya lile
gari akawakimbilia kujua wameelekea chumba gani. “Nikikamwatwa
hapa!”
Tunda
akacheka. Alipokata tu kona ili kujua walipo, hakuwaona tena. “Aaaahhaaa!” Akasikitika na kurudi garini
kuchukua vitu vyake asiamini macho yake.
Akajikuta akicheka peke yake. “Looooh!” Akaanza kuangalia
picha alizopata na ile video. “Sasa
hapa ni kuwinda mpaka nipate picha
zao kwa karibu. Wote watatu.
Washenzi wakubwa hawa.” Tunda
akaondoka na kuelekea chumbani kwa
Tewele.
Akamkuta akimsubiria kwa hamu lakini hakumwambia
aliyokutana nayo. “Ngoja nikukaribishe
Bagamoyo.” Tunda akamwambia mara alipoingia. Tewele
akacheka cheka akionyesha wasiwasi usoni. Tunda akamshtukia. “Vipi, mama alikuaga nini?” Tunda akamuuliza. Alimjua ufanyaji wake mapenzi. “Kidogo tu. Lakini si unajua tena?” “Basi usiku zamu yangu.” “Hata sasa hivi tunaweza
kujaribu. Lakini nilitaka kukwambia ukiona
jamaa anagoma, ujue sababu hiyo.
Alinibana, nikashindwa kumkwepa.” “Wala usijali. Tunazo siku
mbili, zetu peke yetu.” Tunda akamtuliza. Kidogo akatoa ile soni.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kesho
yake wakati wamekwenda kwenye mkutano,
Tunda alimka na kuamua kutoka akatembee nje. Ilikuwa hoteli nzuri sana.Wao
walikuwa wakila ukumbini. Akamwambia
Tunda yeye anaweza kula popote. Na kwa
kuwa kilikuwa kikao cha siku mbili,
alimuonyesha ratiba, walionekana kubanwa huko mkutanoni. Iliwalazimu
kuwepo huko kuanzia asubuhi mpaka saa 10 jioni.
Tunda akajiambia ni wakati wakutalii.
Hakuwa amepata hata kifungua
kinywa. Akatoka taratibu mpaka
sehemu ya kulia chakula.
Akaagiza
juisi ya chungwa, mayai mawili na sausage.Wakati anasuburi,
akamuona yule dada na yule mtoto
wanakuja pale. Akasikia akimwita kwa jina la Junior. Ukweli alikuwa mtoto mzuri. Afya nzuri, nguo safi
halafu nzuri. Wazi alionyesha ni mtoto
mwenye matunzo mazuri. Walikuja
wakitembea taratibu, akiwa amemshika
mtoto wake mkono, akimuongelesha kitoto
na kucheka. Rangi ya yule dada ilikuwa
kali. Na ndiyo mtoto wake alirithi. Ila
sura, ni kweli alifanana na mjomba
wake.
Tunda akajidai anatuma ujumbe huku simu imesimama
mbele yake kama ameificha mtu wa nyuma
asione, ikaiiegesha juu ya meza. Akaendelea
kuwachukua video huku akiwapiga na picha. Ile wamemsogelea tu, Mihayo akawa anaingia hapo kwa haraka. “Vipi, mmepata?” Akamsikia mjomba wake akiuliza kwa
kujali. Tunda akavuta nywele mbele kama
kujiziba. “Ndio tunafika. Si unajua tembea yenyewe? Kila anachokutana nacho njiani anataka aokote, ashike. Akiangalie ndio safari
iendelee.” Akajibu mama mtoto. Mihayo
akacheka. Akaina na kumnyanyua.
Mihayo mwenyewe alikuwa msafi kama kawaida yake. Suti kali iliyomkaa sawia mwilini. Tunda hakupoteza muda. Akapata picha za haraka haraka. Za wote watatu, Mihayo na mtoto wake. “Basi mimi narudi kwenye kikao. Baadaye. Naamini utapata tu. Zungumza nao. Hata kwa pesa wewe nunua.” Mjomba wake akamwambia yule mama mtoto na busu kubwa ambalo Tunda
hakulikosa kwa video na picha. “Asante.” Mama mtoto akashukuru. “Acha niwahi. Tupo katikati ya
kikao. Nitawaona baadaye kidogo.
Nitumie ujumbe ukikwama kwa
chochote, nitatoka kwa haraka.” “Usiwe na wasiwasi. Sisi tutakuwa sawa tu. Si ndiyo Junior?” Dada akamgeukia mtoto
wake, akamchukua baada ya kumpa busu
huyo mwanae akiwa mikononi mwa baba
yake. Mtoto akacheka wakati anakwenda
kwa mama yake. Mjomba naye akambusu akiwa mikononi kwa mama yake. “Love youuuu!” Mihayo
akamwambia mtoto huku akimbusu tena kama kumuaga. Mtoto akacheka na kujibu, “Lovu dady.”
“Haaaa!”
Tunda akashangaa kwa wazi. Akajifunga mdomo kwa haraka. Uzuri hakusikika. Mihayo akaondoka kwa haraka.
Furaha aliyokuwa nayo Tunda, hakuna jinsi angeeleza mtu akamuelewa. Hata Tewele asingemlipa, angeondoka hapo ameridhika kabisa. Mambo yalijipanga vizuri. Akapata yote tena kirahisi sana.
Alifika hapo Bagamoyo akiwa bado
hajui kitu chakufanya
pindi atakapomkuta mjomba wake
huko. Lakini akawa kama aliyeagiza
chakula, akaletewa kikiwa kimepikwa
vizuri sana, tena kikapambwa kwa
unadhifu, kisha akasogezewa mpaka mikononi mwake. Alijawa furaha isiyoweza kutamkika.
Akabaki sasa akiwatizama mama na mtoto. Wakasogea mpaka kwa muhudumu, akaomba chupa ya maji ya moto. “Itakuwa kwa ajili ya mtoto wao.” Akajisemea Tunda
huku akiwatizama. Hakuacha kuwapiga picha. Ukweli yule dada alikuwa mnene. Alivaa nguo ya kuachia tu. Gauni jeupe
tu kata mikono. Mwili ukaonekana mkubwa na akaonekana ameridhika. Wakapewa walichoomba, wakaondoka bila hata kumgeukia Tunda.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tewele alimshusha Tunda Mlimani City, akiwa
ameshamlipa pesa nzuri tu. Akashindwa
kurudi nyumbani kwake. “Mpaka kieleweke leo.” Akajisemea Tunda wakati anafuata taksii yakumpeleka
sehemu ya kusafishia picha iliyopo vichochoroni sio mwangani kama hapo Mlimani city. Akamueleza
dereva aina ya sehemu anayotaka kwenda
kusafisha hizo picha, dereva akamuelewa.
Na kweli akamfikisha sehemu
aliyoridhika. Kilikuwa kiji studio
kidogo tu. Akashuka Tunda baada ya kumlipa, akaingia ndani.
Alimkuta mtu
mmoja tu, ambaye alijitambulisha
kuwa ndio anafanya kazi hapo.
Akamuonyesha zile picha kwenye
simu yake, na kumuomba amtolee
nakala tatu tatu kila picha. Yule kijana
akafanya kwa haraka tu. Kwani mteja
alikuwa Tunda peke
yake. Akahakikisha amezifuta
kwenye kompyuta yake. Akanunua
bahasha kubwa tatu. Ndipo akarudi
nyumbani kwake sasa. Alikuwa anacheka
mfululizo kila akizitizama zile picha.
Akazigawa kwa mafungu matatu. Shangazi yake, Sera mtoto mkubwa wa mjomba wake na Samatha
kipenzi cha baba yao.
Akazipanga zile picha vizuri kuanzia vile yule mjomba wake anawapokea mpaka pale sehemu ya kulia chakula. Akaanza
kufikiria jinsi ya kutuma zile video.
Hakuwa na namba zao za simu. Akawaza
Tunda. “Hataa!
Picha huwa wanakanusha. Wanasema
wamebambikiziwa vichwa. Video hawezi kupinga.” Akashindwa hata kukaa
hapo. Akaita Uber ili imchukue kumrudisha
tena kwa yuleyule
kijana aliyemsafishia zile picha.
Alipapenda pale, hapakuwa na watu wengi.
Akajua atakuwa salama. “Umerudi tena dada?” Yule kijana alimuwahi alipomuona anafungua mlango. “Ndiyo. Ila safari hii
ninashida ya tofauti.” Akaanza Tunda.
“Nina video ndefu tu.
Nataka kumtumia mtu, lakini sio kwa simu. Nitamfikishiaje?” “Ushaiweka pamoja na
umeridhika kuituma?” Tunda akafikiria.
Akakumbuka aliichukua kwa vipande. “Naweza kuiweka yote kwenye ile
kompyuta ya mwisho kabisa. Nikakuonyesha
jinsi unavyoweza kuiweka pamoja,
kisha tukawatumia kwa email.” “Hapana. Nataka kuwafikishia
mkononi.” Tunda
akamsahihisha. “Basi tutaweka kwenye flash drive.”
Akamuonyesha
aina ya hiyo flash drive maana alikuwa nazo akiziuza hapohapo, Tunda akaridhika.
“Hapo
sawa.” Tunda akakaa kwenye kompyuta na kuanza kuandaa ile video huku akicheka.
‘Mahaba ya
Bagamoyo.’ Yakawa meneno ya ufunguzi
wa hiyo video. “Mihayo na familia yake ya pili.” Akaweka na
tarehe. “Hapa
akiwa anapokea familia yake iliyompa
mtoto wa kiume wa pekee. Junior Mihayo.” Akaweka tena hayo maneno
chini ya ile video. “Akimkaribisha mkewe kwa busu zito
lililodumu kwa sekunde kadhaa, kama
mnavyoona hapo, na mtoto wake Junior.” Ikaendelea kuonekana
Mihayo akimbusu yule dada na
Junior wakiwa tu ndio wamefika pale hotelini sehemu ya kuegeshea magari. “Huyu
ndiye Junior. Aliyejaliwa rangi ya mama,
sura ya dad.” Akaweka na hayo
maneno. “Huyu ndiye mwanamke aliyeweza kuleta mrithi wa Mihayo hapa duniani.”
Akaendelea kuongeza yale maneno
yakukera. “Mihayo Junior na mama yake.”
Na hayo maneno pia akayaweka kwenye hiyo hiyo video akionekana yule mtoto na
mama yake tu.
“Mihayo akiwa na familia yake. Yeye, mkewe na mtoto wao.” Akaweka
hayo maneno kwenye video aliyokuwa amewachukua kwa karibu wakiwa kule Bagamoyo sehemu ya mgahawani. Akaongeza na baadhi ya picha zao
wote watatu. Nyingine akiwa Junior na
baba yake, nyingine Junior peke yake ilimaradi tu kuwakera zaidi maana ni kweli Junior alifanana na baba
yake. Huwezi kukana.
Akaziweka picha nyingi za yule mtoto
akiwa amemvuta karibu na kuonekana
sawia, kisha mtoto na mjomba wake
kwa pamoja. Tunda akacheka sana. “Duuuuh!” Akajikuta akihamaki kila
akiangalia zile picha alizoziongeza
kwenye ile video.
Akaona aongeze tena picha za wote watatu ili
kuwakera zaidi. “Kweli
watoto wanaunganisha sura za wazazi wao.” Akaongeza hayo maneno chini ya zile picha alizokuwa ameongeza kwenye hiyo video za wote watatu. Basi zile picha akazipunguza mwendo wakupita kwenye ile video. Zikawa zinapita taratibuu. Ni kweli wawili hao walifananishwa na huyo mtoto. Akacheka sana
na kujisikia ameridhika moyoni.
Ilishakuwa usiku wa saa mbili wakati
Tunda amehitimisha kazi yake akiwa
ameridhika nayo. Ni kweli alitumia muda mrefu sana pale kwenye ile studio, na yule kijana akimsaidia.
“Sasa wakati Mzee anafaidi na familia ndogo
Bagamoyo, acha familia ya huku ya
wajuaji, nao wafaidi pia. Wajue kinachoendelea
kwa dad mtukufu.” Tunda akajisemea na kufyoza.
Akatengenezewa na kuhifadhiwa hizo video kwenye flash tatu. Akatumbukiza kwenye zile bahasha tatu. Kisha akamtuma yule yule kijana akamtafutie usafiri. Alirudi na kumwambia amepata taksii, Tunda akamlipa vizuri tu na pesa ya shukurani.
Akatoka.
Akapanda tena taksii mpaka nyumbani shangazi wake,
alipokuwa akiishi kwa mateso akinyanyaswa vibaya sana. Akajua kwa muda huo wote watakuwepo kama bado wanaishi nyumbani kwao. Akamwambia dereva, akamkabidhi mlinzi, na amsisitizie amkabidhi
kila muhusika bila
kuchanganya. Na ahakikishe anawakabidhi mkononi mwao. Kama sio wote, basi mmoja wao awe amepokea. Akamwambia na asubirie jibu kama wamepokea. Dereva akashuka
na kufanya kama
alivyoambiwa. Baada ya muda
akarudi yule dereva ndani ya ile taksii
aliyokuwa amemuacha Tunda. “Mlinzi
anasema amemkabidhi mama.” Tunda
akafurahi sana. “Tuondoke.” Tunda akamuamuru yule dereva kwa furaha zote. Akajua ujumbe umefika kwa muhusika mkuu.
Alimrudisha
Tunda Mlimani City. Hakutaka
dereva yuleyule aliyeletewa na kijana wa pale studio, ndio amfikishe
nyumbani kwake. “Kuna mambo mengi siku hizi. Wanaweza kufuatilia wakajua ni wapi nimetolea
ile video. Wakambana yule kijana, kijana akamtafuta mwenye taksii, wakaletwa kwangu. Sitaki watu nyumbani kwangu.” Akajiambia Tunda wakati
anashuka hapo. Mpaka hapo bado
hakuna aliyejua ni wapi anaishi
Tunda. Hakuwahi hata kuropoka kwa
yeyote, hata usingizini. Hilo
alilikusudia kuwa lake. Baada ya purukushani nyingi za maisha, alijiambia angalau apate pakujificha. Kuficha huzuni zake, kupumzisha mwili na mawazo yake bila mwingiliano wowote hata salamu ya majirani. Alirudi kwake, akalala kama mtoto mchanga kwa furaha zote na kusahau
mkasa uliomuhuzunisha wa waziri kwa
muda.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Hiyo week hakutoka ndani kabisa. Alikusudia kupumzisha huo mwili baada yakutumiwa mfululizo, kwanza ni kama aliingiza
kipato kikubwa sana. Akaona aupongeze mwili wake kwa kuupa mapumziko mazuri.
Mwili huo ulistahili mapumziko. Kwani
alianza nao waziri Mbawala. Alimtumia
sana kwenye gari, wakaja kumalizia Sauzi.
Lakini yeye hakumlalamikia sana
sababu ya ustaarabu wake, japo
ilikuwa mfululizo, tena kwa juhudi
zote. Haya, akaja kwa mwanae waziri,
ambaye huyo ndio shuguli haswa. “Junior!” Tunda akamuwaza.
Masaa machache na huyo kijana, lakini
Tunda alihesabu ni kama kuwapa
wanaume watatu kutumia mwili wake
mfululizo.
Ni kweli alimtumia kwa pupa. “Huyu ni wakumtoa kwenye orodha kwa haraka sana, pindi nitakapompata
anayenihonga vizuri.” Tunda akafyoza kabisa kwa hasira. Haya, akapumzika ndipo akaenda kwa Tewele, Bagamoyo. Tewele haikuwa shuguli nzito. Ni kama alipumzika kidogo.“Ni Kweli nastahili mapumziko.”Akajiambia Tunda.
Kupambana
Kuishi Mjini.
Swali la wapi anampata muhongaji mzuri likaanza
kuwa ndilo linalozunguka kichwani. Ni kweli namba za simu za watu wa maana alikuwa nazo.
Lakini akahofia kuwatafuta, historia
ya waziri Mbawala isije kujirudia. “Watataka kuanza kuchimbua mambo mengii.” Akajiambia Tunda. “Wasomi hao na pesa zao. Nyadhifa wanazoshika ni za juu, wanakuwa wanamaadui wengi.” Akaendelea kufikiria
Tunda. Ikabidi kubadili utaratibu.
Akaamua kuanza kwa upya jinsi
anavyosaka wateja wake. Huku bado akiwa
na yale majina, lakini akaona awatafute
kwa njia nyingine itakayowafanya hata
wao waelewe ni biashara tu, sio
kufuatana nyuma kumtaka kumjua zaidi
na kuanza kusikiliza matatizo ya wake zao
au familia zao. Ndio anafanyaje!?
Akazidi kuwaza Tunda. Akaanza kutembelea hoteli na baa kubwa kubwa tu ambazo alijua atakutana na watu wa maana wenye pesa isiyo na matumizi mengi. Basi, ataingia hapo kwa heshima sio kama changu. Kama msomi, dada mwenye mipango na kujielewa. Hakuwahi kujikosea hata mara moja. Unadhifu wake vilevile na aliendana na siku. Akienda ufukweni, utampenda jinsi atakavyovaa na rangi yake ya pekee aliyojaliwa na umbile lake, huwezi kuacha kumtizama. Na ukitupia jicho kwenye huo mwili wake, hapo ndipo utakutana na mengi, tena mazuri kwenye huo mwili wake.
Akihisi hajafanya vizuri anapokuwa anaingia na kuvuta macho ya wengi, basi atatulia kwenye meza na kuanza kusoma mazingira hapo. Akishakuchagua anaanza kukupigia mahesabu. Hata kama mpo wawili.
Tabia yake yakusoma muonekano wa mtu
ulikuwa pale pale. “Kama anaweka saa ya ya
bei ya chini kwenye mwili wake, hawezi kuhonga
pesa ya kuelewe kwa mwingine.” Alishajiambia Tunda. Aliyejithamini ndiye aliyemfuata. Na alijua ukifanikiwa kukuvuta kwenye mwili wake. Ukamtazama tu, alijua ni lazima atakuchomoa tu. Hata kama upo hapo na
mwanamke mwingine. Atakuchomoa katikati
ya kundi na kwenda kukuhudumia hata
kwenye gari au chooni. Hapo
anakuonjesha. Lazima utakuja kumtafuta tu siku
nyingine tena sio nyingi.
Akiona hujamuona na yeye anakutaka, akiona unanyanyuka kwenda chooni, na yeye anaweza kutoka mezani kwake akijidai anakwenda kuzungumza na simu mbali na pale. Lugha yake na sauti yake, atakavyoanza kuondoka pale akizungumza na ile simu, lazima wa pembeni au aliowaacha nyuma, mtamsindikiza kwa macho. Na hapo ndipo wengine watashikwa na tamaa baada yakumtizama sasa vizuri. Hana kelele, taratibu lakini lazima uvutiwe
kumtizama. Sasa yule aliyesimama na kumfuata, lazima atasababisha ajali
hukohuko kama sio nje ya choo cha kiume,
basi alikoelekea.
Na wakati wote kila anapofika popote, ataagiza red wine. Basi watagongana kwa nguvu, na atahakikisha ile wine inaishia kwa yule mwanaume. Hapo atashtuka mpaka utamuhurumia yeye. Atamuaga
mtu aliyekuwa akijifanya anazungumza
naye kwenye simu. Ataomba msamaha wa
kukubembeleza huku akifuta hiyo wine
mwilini akigusa sehemu utakazopenda
asiache. Ukimwangalia tu, kosa. Kama
sio mwanaume imara, lazima macho yatakuvuta. Anaweza hata kuomba shati lililoingia hiyo wine akafue chooni. Hapo ujue basi tena. Ameshakunasa.
Wale aliowaacha nyuma na wengine
watamuwinda na yeye.
Hapo atakuchangamkia kwa
mahesabu. Sio papara. Kama asiyetaka,
lakini atahakikisha anakuweka kwenye angaza zake, chini yake.
Kama
akishahudumia hapo hapo hotelini na hakupata aliyemwambia anachukua chumba labda wamekuja na wanawake zao, basi atakwambia uje umtafute
wakati mwingine. Tena kwa ujumbe sio
kupiga simu hovyo ukamsumbua akiwa na wateja
wengine. Akaondoa utaratibu wa
kupigiana simu kwa wateja zake wote.
Hakutaka kuzungumza na mtu kwenye simu.
Na alishawafikisha Mbawala Junior na
Tewele sehemu ambayo wanahitaji huduma
yake kwa hali na mali. Akajua
hawawezi kupotea hata
akiwabadilishia utaratibu. Kwa hiyo
akaweka utaratibu huo mpya kwa
wateja zake wa zamani na hao wapya.
Marufuku kumpigia simu na ukianza jumbe
za mapenzi, anakukata mapemaa.
Sijui jumbe za uliamka salama. Unaendeleaje? Uko wapi? Hapana. Hakutaka mahusiano nje ya kile mnachokifanya kwa wakati aliokubali yeye. Alishajiambia wote mnaiba, hakuna
kudanganyana. Na wanaume hao aliokuwa
akiwahudumia, aliwadharau sana. Hata
waliotaka kuonyesha mahusiano au kujidai
wanataka kumuoa ilikuwa kama kumchefua. “Ili uniweke ndani ukaibe nje kama hivi?” Hilo ni swali alilokuwa
akiwauliza bila hata kukwepesha macho. “Wewe furahia hapa, rudi
kwa mkeo au mwanamke wako. Tuachane
kwa amani. Usinidanganye. Mimi sio
mtoto mdogo.” Hapo Tunda ataongea
kwa ukali, bila kificho. Tena unaweza
ukamkera zaidi akakuacha kabisa. Chuki
yake kwa wanaume ikaendelea.
Ilianzishwa na baba Tom, wengine wote aliona ni wale wale. Aliwatumia kama chombo cha kujinufaisha nao. Alimuona vile baba Tom akiiba. Sadiki. Akaja
kukumbuka mjomba wake jinsi anavyojidai
kuwa mtu mwadilifu nyumbani kwa
shangazi yake. Sheria kali kwa watoto
zake na mkewe. Makini kila
anapokuwepo nyumbani na kujiwekea
mikakati mikubwa kama mtu mwadilifu!
Kumbe mwizi ambaye amehamia hukohuko!
Ameanzisha familia ya pili ndani ya
familia inayoonekana bora sana!
Akazidi kuchukia wanaume. Na
akikukamata, anaweza kukuchomoa
pesa yote ukarudi kwa mkeo huna hata
shilingi. Alikuwa akichukua pesa yao
bila huruma.
“Wanaume si wameubwa mateso?
Basi akahangaike kutafuta
nyingine.”
Hapo atawaza kimoyomoyo huku akiingia
kwenye wallet yake. Na macho yake hayo
na sauti, utatoa tu zote. Kama unataka huduma yake unatuma ujumbe tu. Tena mapema. Sio umshtukize. Umueleze muda utakao mtaka awepo hapo, siku na mahali, basi. Kama anakufuata mkoani, basi ugaramie nauli yake. Tena kwa ndege. Anakufuata, anakupa huduma ambayo anajua, ukiwa na pesa inayoendana na garama yake, lazima utamtafuta yeye, au hata
utakopa tu, kumfanya akurudie. Hakuna
aliyeonja penzi la Tunda akatosheka.
Wazee hao wasomi wa mjini na
wafanyabiashara wakubwa nchini, walikuwa
kama watoto mbele ya Tunda.
Wengine
waliokuwa wakisafiri mikoani
kikazi, walimtaka ende nao, au hata
palepale mjini wengine walidanganya kwa
wake zao wanasafiri kikazi kumbe
wapo wamejifungia na Tunda kwenye nyumba za wageni. Alikuwa yupo busy sana, kuanzia jumatatu mpaka jumatatu. Wale wenye wake
wanaojua kubana, walimtumia Tunda
kipindi cha muda wa mapumziko wa chakula
cha mchana wakiwa maofisi. Kwa ujuzi wa
Tunda, hakuhitaji muda
mrefu sana kumridhisha mteja wake mwenye muda mfupi. Alijitahidi kwenda na muda, kitu kilichowavutia wateja wake wengi. Muda wa mchana, katikati ya siku, jua likiwa linawaka nje, basi ndani ya gari yako au kwenye nyumba za kulala wageni. Hata kama una dakika 20 tu,
Tunda alijua kuzitumia vizuri.
Basi wateja wake hao wa muda mfupi, hawakuisha. Wakati mwingine endapo mmoja akichukua chumba labda kwenye hoteli nzuri. Akiondoka kuwahi kazini au nyumbani ili asikamatwe na mkewe, hapo anaweza kuingiza hata wanaume wengine wawili au watatu wa haraka haraka kwenye hicho hicho chumba. Na sheria ni ukifika hapo hotelini, usipite mapokezi. Moja kwa moja kuelekea
kwenye chumba atakachokuelekeza yupo
yeye akikusubiri. Hilo wakapenda wengi
wenye wake wa kali na wasiokuwa na muda
mrefu wa uwizi. Hatakutafuta baadae kwamba ufumaniwe na jumbe za mapenzi. Hataki kujua majina yako, kwamba mtafutane nje ya kile kinachowakutanisha pale na wala hutajua jina lake la ukweli.
Basi ikawa
rahisi kwa wengi. Unapewa huduma
yako. Kama hukufumaniwa wakati wa tukio, basi ujue hutakamatwa kwa
sababu ya Tunda. Kwanza yeye mwenyewe
alikuwa makini. Hakutaka kugonganisha wateja wake. Na wala usingekuta simu ya
Tunda ina kelele hata mara moja. Akiwa
na wewe, ujue ni wewe tu. Simu yake
ipo kwenye pochi. Na haina sauti. Kama mteja akimtafuta, ni kwa ujumbe tu. Kwa hiyo kama siku hiyo na muda huo unaomuhitaji hatakuwa na mteja mwingine, atajibu kwa kifupi tu “OK”. Basi hapo utahitajika kutafuta mahali.
Kwa wale wenye nyadhifa za juu, aliwaelewa. Yeye ndiye aliyekuwa akitafuta sehemu ambazo alijua hata wahudumu hawatamuona. Atakwenda kuchukua chumba
huo muda uliomwambia unayo nafasi, kisha anakutumia ujumbe ni wapi umfuate. Na hataki umcheleweshe. Umuweke hapo masaa, uje umwambie kulikuwa na foleni ndio maana umechelewa! Au sijui mtoto wako anaumwa ukapitia duka la madawa na habari ndefu za kifamilia, hazimuhusu. Na kama hana nafasi atakupa yeye siku na muda atakaokuwa tayari.
Lakini kabla hamjakutana lazima umrushie pesa yake nusu na baada ya kukuhudumia, ndipo unamalizana naye. Hakuwa akipokea pesa taslimu, kwa kuhofia kuporwa. Wateja wake wote walimrushia kwa simu. Na wakati wote hakukosa wateja sababu ya ubunifu wake wa kuwanasa na kitandani.
Na endapo yeye ndiye anayetafuta sehemu ya kukutania, pia pesa unamtumia kabla. Ili kama utachelewa zaidi ya muda mliopanga, akiondoka iwe juu yako. Na pesa ya usafiri wake kumfikisha hapo pia unatuma kabla ya kukutana. Na jinsi anavyoomba kwa upole na unyenyekevu, usingejua kama ni moja ya taratibu za muhimu sana alizojiwekea. Kuwa lazima hayo malipo uyatangulize. Atakuomba kwa upendo na kukubembeleza. Na hata atakapoondoka
endapo umechelewa hapo hoteli wala
hatagomba. Atakutumia ujumbe wa
kukuomba msamaha kuwa kwa kuwa
umechelewa, inabidi aondoke, anayo
miahadi mingine ya muhimu sana,
hawezi kuendelea kusubiri.
Basi
atakusihi wakati mwingine utakapopata
nafasi, umtafute. Huwezi kumchukia. Hapo
ujue amekwenda kwa mteja mwingine.
Ataondoka kwako akiwa hajaingia hasara.
Garama za
chumba na usafiri wakumfikisha hapo ni
mteja amegaramia mwenyewe. Na ukijibu kuonyesha
ni makosa yako mtapanga wakati mwingine,
basi anakuhakikishia hapo ameondoka, lakini
si kweli kwamba ataachia kile chumba mteja alichogharamia, atakachofanya ni kutafuta
mteja wake mwingine. Watatumia chumba
hichohicho, lakini mteja huyu wa pili,
atakilipia tena kana kwamba
hakijalipiwa. Hapo Tunda anakuwa
ameingiza pesa zaidi. Inaweza kufanya
hivyo kwa mteja wa pili na watatu pia.
Inategemea na aina ya mteja. Wale ambao
hawana shida kulala nje na makwao, basi
ndio ujue mtalala naye hapo hapo kwenye chumba
hicho kilicholipiwa na mteja wa kwanza,
na hataingiza mteja mwingine.
Ila ukilala naye usiku kucha, ujue pesa atakayokuchomoa hapo, ni zaidi. Akiona huo mwezi upo kimya. Hajafikisha pesa aliyojipangia. Labda anapata wateja wachache wa pesa ndogo, anarudi kwenye orodha ya majina ya watu aliyoiba kwa Mbawala Junior au Tewele. Ataipitia majina yote. Yule
aliyetaka kumtumia kama ni waziri au mtu mwenye nyadhifa ya juu nchini au pesa nyingi kama mfanyabiashara ambae
hasubirii mshahara, basi
alihakikisha anajua ratiba ya huyo mtu
hata kwa kukufuatilia kwenye vyombo
vya habari. Kisha anachunguza sehemu zake anazopenda kwenda kwa starehe au mapumziko.
Hata kwa
kuingia kwenye istagram zao na wake zao wale wanaopenda kutangaza matukio ya
familia zao, twitter au facebook.
Alifungua huko akaunti sio kwa ajili
yake. Kwaajili yakufuatilia watu. Ajue huyo
anayemuinda alipo. Hata kama upo na
familia yako. Ilimradi ajue kwa wakati
huo uko wapi. Akishajua huyo mtu
anayemuwinda yupo sehemu fulani,
atakwenda akiwa amependeza sana
na amevaa kiheshima tu. Atapita mbele yake, lakini atahakikisha anajua kama amepita. Hata kwa kudondosha simu itakayomfanya
ahamaki kwa kulalamika kwa sauti yake yakuvutia. Akishamaliza kuiokota na pengine kama huyo mtu ni muungwana, atampa pole, pengine na kusaidia hata kumuokotea. Basi, atakushukuru huku
akikutizama na macho yake ya mtego.
Kisha atakwenda kukaa sehemu anayojua utamuona hata kwa mgongo tu.
Na kwa kuwa alikuwa na umbile ambalo alijua akisimama lazima mwanaume yeyote mwenye uchu atamsindikiza japo kwa macho tu, basi akishakaa na kuagiza kinywaji chake kile kile red wine. Mtindo wake uleule,
hataacha kwenda msalani au kujidai
anatoka nje kuongea na simu.
Asipofanikiwa kuona muhudumu
anamfuata kumwambia ametumwa
kutoka meza fulani kumuuliza anataka
nini, basi ujue huyo waziri au mtu,
atamwagiwa wine tu. Hawezi kuepuka
kuloweshwa na kinywaji hicho kama
usipomfuata mapema kwa hiari yake.
Au kama amekwenda kuwinda club,
basi atamkanyaga huyo mtu kwa nguvu mpaka aumie na yeye ndio atampa pole na kubembeleza. Na hapo ujue
hataishia kukubembeleza huo mguu tu.
Na kama anayemtaka akijua ni baba wa familia. Unapenda familia yake. Zaidi watoto ndio wamejaa kwenye akaunti zako za Facebook na Instagram, basi
ataanza kufuatilia sehemu unazopenda
kwenda na hiyo familia yako. Akijua
labda umepeleka familia yako sehemu
fulani, basi atakufuata hukohuko. Hata kama ni kuogelea. Na yeye atavaa nguo za heshima tu za kuogelea.
Lakini kwa jinsi
alivyojaliwa, hawezi kuwepo kwenye
vazi la ufukweni, ukaacha kutizama
hizo sehemu zilizoachwa wazi. Hata
kama mke mtu ndio yupo ndani ya maji na hao watoto, basi atakuwa
mwema kwa mwanamke na wale watoto. Atatengeneza
vimichezo ndani ya yale maji akiogelea
na hao watoto, mpaka watoto
wampende. Wakishaanza tu anti, anti
ndani ya yale maji, basi ujue na baba
mtu atavutiwa.
Hapo ndipo atakufuatilia. Mke na watoto ndani ya maji, yeye anaweza hata kumfuata baba mtu hata chooni akiona
ananyanyuka. Anatoka ndani ya hayo maji
taratibu na kuacha familia yake ndani ya
maji, anamfuata baba mtu sasa. Huko
ndipo atahamisha mitego kwa huyo baba.
Na kwa kuwa ulishavutiwa naye tokea
mwanzo, na nguvu ya ushawishi aliyokuwa nayo, kama hatakuhudumia hapohapo, basi lazima mtawekeana miahadi ya baadaye tu.
Na akishafanikiwa kulala na mkuu
mmoja, labla ni waziri au mbunge, au
tajiri mkubwa mwenye
pesa yakueleweka, basi anakuwa na uhakika wakupata anayefuata mwenye pesa kama huyo.
“Paka anatembea au kuzungukwa na paka wa aina yake.” Alikuwa akijiambia
Tunda. Kwa hiyo meza aliyokaa mwenye pesa mmoja
aliyekuwa akimfuatilia, alijua wenzake
pia watakuwa hivyo hivyo.
Akimpata mmoja wao, ujue atapata na
wengine tu. Kama hakufanikiwa kwa
kujipitisha wakamtongoza, basi ile tabia ya kuiba namba za simu kwa mteja aliyempata, aliitumia kama akiona sio hatari ataiba tu. Iwe wakati huyo mteja akiwa bafuni akioga baada ya shuguli nzito za Tunda hapo kitandani, kabla Tunda mwenyewe hajaingia kuoga naye, ndipo ataiba hizo namba za simu za aliokuona nao na anayemtaka yeye au kama ni mteja wa usiku
kucha, atahakikisha yeye halali mpaka
amepitia simu ya huyu mteja aliyelala
naye hapo ili kupata namba za marafiki
zake.
Utaratibu
wake ukawa ni uleule.
Akishazipata hizo namba kwa
kuzihamishia kwenye simu yake ambayo kwanza ilikuwa inajizima kila baada ya sekunde 10 kama hajaishika, na ilifunguka kwa kuingalia. Yaani macho yake yeye Tunda ndiyo yalifungua simu hiyo ya pesa nyingi sana. Kwanza ukumbuke hakuwa akiitoa hovyo. Ilikuwa ikikaa kwenye pochi yake wakati wote. Kwa kuwa hakutaka muingiliano anapokuwa kwenye kazi moja, mteja wake amuone yupo busy na simu. Labda muwe sehemu ya hadharani yupo na wale wateja wasiogopa kuiba naye. Wakiwa wapo nje, hadharani, labda huyo mteja
anakunywa, basi hapo ndipo utamkuta
ameinamia simu yake anacheza games zake
kwenye simu yake, akiendelea kunywa maji
yake taratibu lakini kama yupo chumbani
na mteja, usingemkuta akichezea simu
au kushika simu yake hovyo akisoma jumbe za wateja wengine.
Labda
kipindi hicho cha kuiba namba. Na
akishamaliza kujihamishia hizo namba
za simu, anairudisha simu yake
kwenye pochi yake, basi. Hutaikuta
simu yake imezagaa hovyo au hata
mezani. Kipindi cha bunge, ndio
kilikuwa kipindi cha neema kwake.
Alikiita kipindi cha mavuno. Alikuwa
na viongozi wake ambao ni wateja
wake wa mara kwa mara. Kwa hiyo
kipindi hicho cha Bunge, anatafuta
kwenda na mmoja wao huko Dodoma, na kuwabadilisha
huko atakavyo.
Yeye ndiye aliyewapanga kwa muda wake, lakini usiku aliishia kulala na aliyemwita au aliyempeleka pale jijini Dodoma. Wakati
mwingine aliweza kuwatongoza wakiwa wamekaa meza moja wakila na kunywa. Ikitokea mteja mmoja amemwita kwenye baa, wakaja rafiki zake kula na kunywa nao.
Akishagundua udhaifu kwenye
maongezi na akajua ni mtoaji,
alihakikisha akiwa anaondoka na
aliyekuja naye, pia ataondoka na
namba ya simu ya atakayemchagua, au
atamuachia yeye namba akiwa na
uhakika wa kutafutwa siku inayofuata,
kwani alikuwa na uwezo wa
kumchomoa anayemtaka palepale mezani, wakatoka kwenda naye chooni au kwenye gari.
Na dakika tano kwa Tunda
zilikuwa nyingi sana,
kuwachanganya kwa ufupi, na lazima
watadai huduma ndefu siku nyingine.
Tunda hakujali ulipo, au hakuangalia
sura, au umbile wala umri wa
mwanaume anayetaka pesa yake. Kila
mazingira alipo alijua jinsi ya
kuyasoma na jinsi yakuyatumia vizuri
kutengeneza pesa. Kwake yeye
kwenye baa au kwenye mahoteli ni
sehemu ya kazi sio starehe. Kwa
hiyo kila alipokuwepo kwenye maeneo hayo
akili yake ilikuwa ikifanya kazi kwa
makini sana. Akiangalia wateja wapya,
jinsi ya kumtoa kwenye meza yako hata
kama upo na mkeo au mwanamke
mwingine, na eneo gani atakalokuonjesha
kwa muda mfupi ili kesho umtafute.
Hakutaka kuwa rafiki na pombe kabisa, ili asije kulala na mwanaume yeyote bila akili yake kujua anachofanya. Japokuwa hakuwa akinywa pombe kabisa, lakini
hakuacha kuagiza red wine kila sehemu
aliyokwenda hasa akiwa anakwenda kuwinda, basi
atakuwa na maji pembeni ambayo
hayo aliyanywa. Tunda alikuwa
mnywaji mzuri wa maji.
Tabia yake ile yakutokulala na mwanaume yeyote bila
kondum, hiyo hakuwahi kubadilika hata
kusahau. Hata uweje au unampa kiasi gani
cha pesa au mtakuwa naye kwa muda gani,
hatasahau kondom. Madhara aliyoyapata
kutoka kwa baba wa kambo, kumpa mimba na
kutolewa kikatili, kuvuja damu kwa wingi na maumivu makali aliyoyapitia baada yakutolewa
ile mimba! Bado aliyakumbuka kana kwamba
yametokea siku iliyopita. Aliapa
kutothubutu kuingiza mtoto wa mtu
yeyote tumboni mwake kama bado
anao huo uwezo, maana kipindi
anaishi kwa shangazi yake, aliwasikia
shangazi yake na watoto wake,
wakimwambia mama yake alimtoa
kizazi kabisa. Hakuwa ameelewa
kwani bado alikuwa akiendelea kupata
siku zake kama kawaida. Alinyamaza,
asijue ni jinsi gani mama yake au hao wataalamu walikitoa hicho kizazi chake.
Lakini pia, hakutaka
kukaribisha mtoto tumboni mwake
wala hakutaka gonjwa lolote mwilini
mwake.
“Malaya hawa, wala situmii nguvu
nyingi kuwatongoza! Wamejawa
tamaa! Wanalala na wangapi? Watakuja kuniua bure.” Tunda akaendelea
kuzingatia huo mkakati. Kuna
kipindi Mbawala Junior
aliponogewa akamuomba waache
kutumia Kondom, Tunda alimkatalia,
na kuanza kumkwepa
kwa kumpunguzia muda wakukutana. Alijua atakuwa amechoshwa na kondom, maana hata katikati ya tendo, Tunda
alipokuwa akimuona anakwenda mwendo mkali na mrefu, alikuwa akimbadilisha kondom, na yeye kujipaka jeli ndipo wanaendelea. Akajua ameanza kuchoshwa na huo utaratibu na kuanza kumzoea. Akaanza kumpunguzia kukutana na muda. Wakati mwingine alimwambia yupo Dodoma anaweza kikazi,
basi kumuona hata kwa lisaa. Basi
hapo
walitumia
hilo lisaa, kisha Tunda anaendelea na
wengine. Akaacha kumpa masaa yakutumia mwili wake.
Hakuwa na rafiki wa kike hata mmoja, hata hivyo hakuwa na muda na marafiki. Muda ambao hakuwa na wateja aliutumia yeye mwenyewe. Kufanya manunuzi ya vitu vya kumpendezesha, au kwenda saluni kutengenezwa
kucha na nywele au alitumia muda huo
kupumzika kwa kulala kabisa tayari kwa
kazi nyingine. Na hakutaka mahusiano hata na watu wanao muhudumia huko masaluni. Akifika anakuwa kimya. Ukijitahidi ni kutoa tabasamu. Hata umuulize jina lake, atatoa tu tabasamu, kimya. Atahudumiwa, na kulipa. Atashukuru kwa heshima zote, na kutoa tip kitu
walichopenda wanaomuhudumia na kuondoka. Na
Hatachangia wala kuzungumza na
simu pale saluni. Hakutaka kuacha stori
zake pale saluni kama alivyokuwa
akisikia za wengine. Mwishoe
wakamzoea! Hapana. Hayo ndiyo yakawa maisha ya Tunda kwa ufupi na urefu.
Mwanzo wa Gabriel.
Tunda
akiwa amepumzika kwenye hoteli moja mjini Arusha wakati mteja wake amemuaga anakwenda kuonana na mtu mahali, aliamua kufungua tv. Alikutana na
taarifa ya habari ambayo ilionyesha
kijana mmoja huko jijini Dar, akitoa
misaada kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mtangazaji alisema kiasi cha pesa
kijana huyo aliyejulikana kwa jina ya Gabriel, alichotoa, ili kuwawezesha walemavu hao kuwa na kitengo chao maalumu. Zilikuwa pesa nyingi sana zilizomtoa mate Tunda. “Huyu ndio mteja ninayemtaka mimi. Akihonga mara moja, hamtafutani tena mpaka baada ya miezi. Na wewe unapumzika kabisa.” Tunda aliwaza.
Aliendelea kusikiliza habari za Gabriel, akajua
ofisi zake zilipo. “Najipa
mapumziko ili kumsaka huyu kaka mpaka
nimpate.”
Tunda alijisemea. Aliporudi mteja wake, alimwambia amepata dharula Dar, lazima aondoke na ndege ya kesho yake. “Mbona hatujamalizana mimi na wewe?” “Nitarudi baada ya siku
tatu.” Tunda akamtuliza
kwa maneno mazuri mpaka akaridhika na
kumruhusu lakini akamuomba aondoke na
ndege ya jioni ili siku hiyo inayofuata
wawe wote hapo hotelini. Tunda akaona ni
haki. Akakubali.
Aliondoka jijini Arusha siku inayofuata akirudi jijini Dar, kumsaka Gabriel, kijana
milionea, aliyemuona luningani.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Usikose mazito na ya kusisimua katika harakati za Tunda, na huyo milionea Gabriel anayemsaka na yeye anayo yake. Usipitwe na kukosa muendelezo. Tunda atapitishwa kwenye mengi mno japo anazo taratibu zake makini alizojiwekea mwenyewe. Ndege mjanja...
0 Comments:
Post a Comment