Naomi Simulizi |+1 205 767 8163 |naomisimulizi@gmail.com Nilipotea! – Sehemu ya 14. - Naomi Simulizi

Nilipotea! – Sehemu ya 14.

 

T

unda akiwa amejilaza pale kitandani, akakiangalia kile chumba kuanzia juu mpaka chini sakafuni, akapadharau. Hapawezi hata kufanana na nusu ya  chumba changu! Akajiambia Tunda na kuamua kuondoka pale hotelini kurudi nyumbani kwake kwenda kupumzika baada ya  kazi iliyomuingizia kipato cha juma hilo mbali na hundi aliyopewa na Kinny.

Aliamka siku inayofuata akakuta  ujumbe kutoka kwa Mbawala. Akimuomba wakutane na anaweza  kumfuata hapo Dar hata kwa usiku  mmoja tu. ‘Hata kama upo busy, basi usiku  mmoja tu, ilimradi tuwe wote, Fina. Sitakung’ang’ania zaidi ya huo usiku.” Tunda hakutaka  maneno mengi akarudisha ujumbe mfupi tu.  “Iwe ijumaa usiku. Na naomba iwe hapahapa Dar. Ijumaa mchana na jumamosi asubuhi nitakuwa na kazi nyingi.” Akakusudia kumnyima muda, akikumbuka shuguli ya  Mbawala. “Huyu shuguli yake nzito, simpi mwili wangu kwa muda mrefu.  Asilete utani.” Tunda akawaza akiwa  hapo amejilaza kitandani kwake.  Dad. Akamkumbuka baba yake. Moyo  ukampasuka. Akacheka.

  Kwa Waziri Mbawala.

Kidogo  akaingiwa  hofu. “Waziri!” Akawaza Tunda. Lakini  sina  kitu  chakupoteza.Akaangalia muda,  ilikuwa saa nne asubuhi. Akajiambia  ni muda wa kazi. Akaamua kumpigia simu akiwa palepale kitandani ndio  ametoka usingizini. Ikapokelewa mara  baada ya kuita tu. Akajikaza. “Na mimi  ninahamu na wewe Mbawala. Sema  nimekuwa busy sana kazini, ndio maana  nimeshindwa kurudi baby. Nisamehe. Ila  nimechukua likizo. Sasa hivi nipo. Nipe kama  siku moja yakupumzika au hata mbili.  Nakuahidi  kulipia  upweke  wote  niliokusababishia. Sawa?” Akaongea kwa  sauti ya kujilalamisha, deko na  usingizi.  Akajua anamsikiliza. Haloo!Akasikia  akiita upande wa pili.

Mbawala!? Tunda akaita kama kwa mshtuko  kidogo. “Ndiyo. Mimi ni waziri Mbawala.” Oooh my Goood! Tunda akalalamika  kwa sauti ya chini kama aliyeshituka sana, akakata.  Baada ya dakika kama tano, akaona  anampigia. Tunda akacheka sana.  Hakupokea ila akamtumia ujumbe. ‘Samahani nilikosea namba. Akasubiria. Majibu yakarudi.  ‘Nipigie.’ ‘Naona aibu mwenzio.’ Tunda  akarudisha hayo majibu. Akaona  anapiga. Akapokea baada ya kuita mara kadhaa.

“Kabla hujaongea chochote, naomba  unisamehe.” Akamsikia anacheka.  Usicheke bwana. Tunda akaongea kwa  deko. Mbawala huyu anayebahatika kulipwa  upweke ni yupi huyo?“Sitaki.” Tunda  akajibu kwa deko huku na yeye akicheka.  Wakacheka wee.  Lakini hebu niambie ukweli. Ni waziri  Mbawala mwenyewe? Au nimejichanganya tena?” Last time I checked, bado mimi ni  waziri wa mambo ya nje.” Oooh my! Mbona unashtuka.” “Hapa nipo kitandani  nimelala, hata mswaki sijapiga! Nikasema  nimpigie simu Mbawala, alinitumia ujumbe  jana usiku. Kwa mawenge ya usingizi,  nimekupigia wewe wakati nilipanga kufuta namba yako! Kuna mtu alinipa namba yako,  akasema nikikutana na waziri mwenyewe,  atanisaidia. Akakusifia wewe ni mtu mzuri sana.” Sasa kwa nini hukunipigia. Tunda  akacheka. 

Nikwambie ukweli?” “Nakusikiliza. “Niliogopa. Nikamwambia huyo aliyenipa  namba kuwa, kwanza huwezi ukapokea simu ya mtu kama mimi na ukakubali  kunisikiliza.” Kwa nini na wewe unanini? Waziri akauliza. Unajua tena, watu kama  sisi hatuna majina wala hatujulikani. Nikajua  utaangalia namba yangu wala hutapokea. Kwanza ujue ni wachache sana wana hii  namba yangu ya simu. Ni watu wafamilia na marafiki wa karibu sana ndio wana hii  namba yangu ya simu.” Tunda akaingiwa  na hofu kidogo. Akajua atakamatwa.

Kwa hiyo hii simu ikiita, hata kama niko  kwenye kikao, lazima nitoke.” Basi na yeye aliniambia hivyohivyo ndio maana nikaogopa.  Nikamwambia  unaweza  kuchukia.” “Hapana. Hamna shida. Ulikuwa  na shida gani?” “Ni muda kidogo. Wizara  yenu ilitangaza nafasi za kazi. Ndio nikataka  kuomba. Lakini nikaja kupata kazi sehemu  nyingine. Hivi hapa nipo likizo ya siku  chache.” Tunda akajikaza na kuendeleza  ule uongo wake. Oooh! Ungenitafuta tu  tukajua jinsi yakukusaidia. Ila kama  umefanikiwa ni vizuri. Tunda akajua  atakata. Akaona amuwahi. 

“Nikuulize swali lisilo msingi sana au upo busy?” Karibu. Yule waziri akajibu. Hivi kama hivyo  ulivyo mtu mkubwa sana hapa nchini, si unakuwa na majukumu mengi sana? Mnapata  muda hata wakupumzika kweli?”Akamsikia  anacheka. Hapo hapo wakaanza  mazungumzo. Tunda sauti yake vilevile ya deko na mahaba. Pole za hapa  na pale hazikuisha. Maswali laini akiwa kwenye tahadhari asivuke mipaka  hayakuisha. Basi muheshimiwa na yeye cheko la hapa na pale likawa jingi. Mpaka mwisho wakajikuta  kama wamezoeana. 

“Nisikupotezee mwaya muda. Nikuache ufanye  kazi. Ujenge taifa.” Wakacheka. Nimepata  muda wa kuzungumza kidogo, nime refresh  akili. Wakacheka. Basi siku nyingine  ukichoka akili, unipigie.” “Mbona mimi sipati  ahadi kama za yule Mbawala mwingine?” Tunda akacheka sana. Tena na tena  akacheka. Wewe nakuogopa bwana!  Huwezi kukubali watu kama sisi.” “Itabidi  nikuone ili nielewe huo usemi wa ‘watu kama Sisi’ ndio mkoje!” Tunda akacheka tena. “Itanibidi tu. Kwanza hata hujanipa jina lako.” Naitwa Doris. Ila kwa watu wangu wa karibu, wananiita Dori.”“Na mimi si nimeshakuwa wa karibu? Eti Dori?” “Eeee. Kajidogosha  kwa kisauti cha kitoto.  Umesema upo likizo?” Siku chache tu. Akajibu Tunda. Ungependa tukutane? Akamuuliza Tunda. Akacheka kidogo kama anayesita. 

“Eti?” Mheshimiwa akauliza kwa kubembeleza. Ndiyo. Kama wewe ukiona sawa. Unaweza kusafiri? Tunda akashtuka  mpaka akakaa. Ndiyo.Akajibu kwa  sauti ya chini huku anacheka. “Nina  safari fupi ya hapahapa Africa. Kuna kikao  Afrika ya kusini. Nitaondoka kesho kutwa.  Unaweza ukatangulia, au ukanifuata. Ni  kutokana na wewe tu.” Moyo wa Tunda  ukapasuka. Sura ya Waziri ikamjia  karibu. Akatulia kidogo.

“Dori?”Nilikwambia nipo likizo. Tunda  akajibu taratibu. Basi panga kuondoka kesho. Nitakuelekeza hoteli ilipo. Halafu mimi  nitakufuata kesho kutwa.” “Ila mimi muoga  mwenzio. Usije kuniacha huko peke yangu.  Nasikia wanachoma wageni weusi, moto.” Akamsikia anacheka. Nakupeleka kwenye maeneo ya watu wanaojielewa Dori. Usiwe na  wasiwasi. Hii simu si inapokea pesa?” “Ndiyo.  Lakini naomba nikuombe kitu. Tuonane leo.  Angalau unifahamu kwa sura kwanza.” “Hilo wazo  zuri sana. Nilitaka iwe hivyo lakini..” Akasita. 

Usijali. Inaweza tu ikawa mchana. Sehemu  ya wazi. Kama Mlimani city. Ukajifanya upo  kwenye moja ya duka hapo, na mimi nikaja.  Na kama ungekuwa huna dereva, ningeweza kukufuata kwenye gari.“Usiwe na wasiwasi  na dereva. Anaweza kushuka kwenye gari kutupa nafasi.” Basi naomba nikuone leo. Sawa. Kwa sauti hiyo ya Tunda, lazima ukubali tu. Wakapanga muda.  Wakaagana. Tunda akaanza kuruka  ruka hapo chumbani akishangilia kama  mtoto wa ndama aliyetoka kuzaliwa. 

 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

 Akaamua kumtoa mate huyo waziri.  Akaamua kujitengeneza kama kawaida  yake, lakini amfanyie kama mwanae.  Amwachie mapaja wazi. “Mwanae!” Akashtuka alipokumbuka miahadi aliyopanga na mwanae. Akakumbuka week hiyo atakuwa na  baba yake Afrika ya kusini.  “Namuweka wapi huyu mtoto wake niliyemkubalia tukutane ijumaa usiku?” Tunda akawa ameshagonganisha  magari. Hapa lazima kuua ndege  wawili kwa jiwe moja. Nijilalamishe  kwa baba yake kuwa naogopa kuwa  peke yangu huko kwa wa Sauzi,  atangulie. Huku nyuma nimpe usiku  mmoja mtoto wake, ndio nimfuate.” Hilo akalikubali.

“Na Mihayo, nitapambana  naye  wakati  nikirudi.” Akajiambia wakati akiendelea kujitayarisha. Alipokaribia Mlimani City akampigia  simu Mbawala waziri. “Umeshafika?” Tunda akauliza. Huwa nina tabia ya  kuwahi dakika  10  kabla ya miahadi.  Kwa hiyo nipo hapa. Tunda akacheka.  Na mimi nipo hapahapa. Unaweza kumruhusu sasa dereva wako atoke.”Hilo  nilishalifanya. Ametoka, nimemwambia  nitampigia baadaye nikiwa tayari.” “Mbona  sasa unajiongelea mwenyewe? Na mimi? Tunda akajilalamisha, akacheka. Basi tukiwa tayari.” “Hapo sawa. Upo upande gani?” “Kama ulivyonielekeza.” Tunda  akacheka.

Akamwambia dereva wa Uber amshushe walipoingia tu getini.  Akaanza kutembea kufuata gari la waziri Mbawala. Akaweza kulitambua kwa urahisi tu.  Akasogea mpaka mlango wa nyuma.  Mbele hakuona mtu. Akagonga kioo  cha dirisha la mlango. Akaona kioo kinashuka macho yakagongana na Waziri. Akamuona  ameshtuka kidogo. “Wewe ndio Doris!?” Tunda akacheka taratibu. Mimi  ndiye.Akabaki amekodoa macho akimtizama kwa makini. Nakaribishwa ndani?” Ikabidi Tunda  aulize huku akicheka. Maana bado  alikuwa amesimama nje ya gari,  mheshimiwa ndani akimshangaa. Giza lilishaanza kuingia.

 “Nimepigwa na butwaa nikasahu kukukaribisha ndani.Tunda akacheka na kuzunguka upande wa  pili. Karibu.” Akafungua mlango na kupanda  garini.  “Gari yako safi!” Akasifia lakini  waziri alionekana bado yupo na  mshangao. Asante. Lakini Dori wewe ni mrembo na upo nadhifu. Akacheka.  Asante.  Nimefurahi  kupata hii nafasi kukaa hivi na wewe! Kwanza bado siamini.” Kwa nini? Akauliza huku anacheka. Mimi kukaa  na Waziri!Mbawala akacheka tena.  Utazoea.” “Kweli!?Akacheka tena. Niambie Dori.” “Mimi ndio  nikusikilize wewe muheshimiwa.” Tukiwa wote mimi sio muheshimi. Ni nani?Tunda akamuuliza huku  anamrembulia. Nakupa wewe nafasi  uchague.Tunda akajidai anafikiria.   

Akamuona anacheka. Umepata jibu?” Waziri  akamuuliza.  Akatingisha kichwa kukubali na  tabasamu  kubwa  usoni.  “Nikunong’oneze?” Tunda  akamuuliza  huku  akicheka. Mmmhh!Akakubali. Unatatizo la miguu?” “Hapana.” “Magoti? Tunda akauliza tena. Hapana Dori.  Mimi mkimbiaji.” “Kumbe ipo  nguvu?” Wakacheka.  Sijui. Nakupa nafasi ya kulitafutia  jibu lake.” “Unauhakika!?Tunda  akauliza kutaka uhakika kama  anaruhusiwa kuvuka mipaka huku  akicheka na wasiwasi kidogo. Ruksa.Akamrhusu akiwa ametulia kabisa.

Okay. Uwe  makini  sasa.  Nitakunong’oneza jina lako nililokupa.  Hilo ni langu tu. Mimi na wewe.  Sawa?”Akacheka huku akionyesha kufurahia. “Sawa.” Akakubali huku  akimwangalia kwa utulivu, na shauku  yakutaka kujua hilo jina.  Tunda akajiweka sawa kwenye kile kiti, akamkalia kwa kupitisha miguu  yake pembeni na pembeni, akaikunja.  Yeye akamuweka katikati. Akamvuta  mikono yake na kuipitisha nyuma yake  taratibu. Aliiweka kwa chini kama  amkumbatie kiuno lakini chini kidogo  karibu  na  makalio.  “Mmmh!” Akamsikia akivuta pumzi baada ya  kumshika. Tunda akacheka na kujivuta  mpaka kifuani, akajilaza masikioni. Akambusu.  Akasikia akitetemeka kidogo kama  aliyesisimkwa.  Akapitisha ulimi hapo sikioni huku  mkono mmoja unamchezea sikio  jingine. Juu ya sikio, chini, nyuma  mpaka kwenye nywele, chini mpaka  shingoni akitumia na kucha pia.

Akaanza kumsikia jinsi anavyohema  na akaanza kumkandamiza kule  alikomshikisha, kwenye makalio.  Akapandisha gauni mpaka juu kiunoni  kisha akaliachia. Na yeye akapitisha  ile mikono ndani kabisa. Akaanza  kumpapasa Tunda kwa nafasi.  Alipofika kiunoni akashika ile cheni,  akaizungusha mara kadhaa, Tunda  akamtolea milio yakumfanya yeye  apagawe zaidi.  Ilikuwa ni milio aliyojifunza tu Tunda.  Na akianza kujiliza hapo, utatamani  utoe nguo. Midomo ilikuwa shingoni.  Hakuwa akijisahau hata kidogo, na  wakati wote alijikumbusha yupo  kazini, kinga ni bora kuliko kifo.  Alijinyanyua, bila kujijua akawa  amevalishwa kinga, kondomu.

Hakuendana na  umri wake hata kidogo. Tunda akashangaa anapewa za kiutu uzima, kama  aliyekuwa amejiandaa. “Kweli embe halianguki mbali na mti wake.” Akajisemea Tunda wakati mzee  ameshika kasi. Na alijua kumshikilia  Tunda asichoke au kuumia, mpaka  Tunda akashangaa. Alikwenda muda  mrefu, lakini Tunda hakutokwa jasho.  Alimaliza, wote wakawa wanahema  pembeni.  Tunda akamgeukia akiwa amejilaza  kichwa pembeni yake.

“Umefurahia?” Akamuuliza kwa kujali. Sana.  Asante.Akamshukuru Tunda kwa  heshima tu. Na wewe?Akamuuliza  kuonyesha kumjali. Nimefika mara  mbili! Kweli unayo nguvu. Utafikiri  ndio unatimiza miaka 21!”Akacheka  sana. Kwa hiyo naamini safari ipo. Kwa mwendo huo, ipo. Nimependa unavyonijali nisiumie.Akacheka na kumbusu kichwani. “Karibu. Naamini  tutapata wakati mzuri huko.” Tunda  akamvuta  mkono, akaukumbatia.  Wakatulia kwa muda wote wakijaribu  kupata pumzi. 

Umeamua nini sasa? Nitangulie au unatangulia kesho?Tunda akafikiria.  Kwa shuguli ya waziri, akaona heri  ajipumzishe mpaka amalizane naye  huko South Africa. “Sitawamudu wote yeye na mwanae kama nitawapanga karibukaribu. Wapo kama chui  aliyeona nyama!”Akawaza Tunda. Lakini nimempenda baba mtu.  Anaonekana anajali. Mstaarabu. Akasikia busu jingine. Au  umegairi?” “Hapana. Nafikiria? “Nini tena? Au una mtu unayemuhofia?” Hapana. Wewe je? Akacheka. Hata mimi nipo huru. Tunda akamtizama machoni, hakuwa ameelewa. Aliona picha zake na  mkewe. 

“Sasa unafikiria nini? Kama ni nauli  usiwe na wasiwasi, hata pesa ya  matumizi ipo. Ningependa utangulie ili nikifika uwe umeshapumzika, unanipokea mimi.” Tunda akacheka na kukubali.  “Sawa. Nitatangulia basi.” “Kama  upo tayari nikate tiketi kabisa. “Nitakata tu tiketi mimi mwenyewe. Usijali. Nilikwambia nipo mapumzikoni kwa hiyo sipo na shughuli nyingi. “Basi afadhali hayo mapumziko  tuyafaidi wote.” Tunda akacheka.  Lakini ningependa mimi ndio nikukatie  hiyo tiketi.” “Ninaye mtu wangu huwa ananisaidia kupata tiketi kwa urahisi  na mimi namlipa kidogo.Waziri  akatulia kidogo kama anayefikiria. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Tunda hakutaka kabisa kukatiwa tiketi.  Kwa jina gani!? Wakimkatia tiketi  inamaana inabidi atoe jina linaloendana na hati yake yakusafiria. Na yeye ameshadanganya anaitwa  Doris. Hati yake ina jina la Ani kama alivyomwambia marehemu Sadiki aliyemtengenezea hiyo hati na kuitumia sana kwenye safiri akiwa na huyo marehemu Sadiki.  Atakamatwa  uongo.  Akagoma  kukatiwa tiketi. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

“Wewe usiwe na wasiwasi, utanikuta  nikikusubiri Sauzi.” Tunda akasisitiza,  huku  akicheka na kumpapasa taratibu.  Akamuona  anachomoa  bahasha  kwenye moja ya mkoba wake kiti cha  mbele. Basi pokea hii bahasha. Ni  yako nilikuandalia. Kesho nitakutumia  jina la hoteli utakayofikia.” Asante. Tunda  akashukuru  taratibu  na  kumbusu pegani. Akajivuta mpaka  kifuani kama kitoto kilichokosa  mapenzi, Mbawala akamkumbatia kwa  mikono yote miwili. “Asante.” Akashukuru taratibu. Wakatulia kwa  muda. Kila mtu akiwaza lake.

Mwishowe Tunda akajitoa mikononi  kwake. “Nikuage ili uwahi nyumbani. Mama  Mbawala asije kuanza kukutafuta.” Usiwe na wasiwasi.” Kwa  hiyo naruhusiwa kukuaga?Mbawala akacheka. Ningefurahi kuagwa. Na  usisahau jina langu.” “Nilikutajia.  Hukusikia?” “Hata kidogo. Ukishika  huko masikioni akili huwa haifanyi  kazi.Tunda akacheka sana. Akajua  sehemu ya kumkunia. Alichofanya  palepale ni kutoa nguo yote, Mbawala  akimtizama. Giza lilishakuwa kubwa  nje, ila mwanga wa taa za nje ndio  zilisaidia kuonana japo si kwa wazi, ila  aliweza kuona kwa kiasi fulani.  Akanyoosha  mkono  mpaka kiunoni kwa Tunda, akampapasa taratibu kiononi. Kisha akamvutia  kumpandisha mapajani kwake. Tunda akatoa ushirikiano, akamkalia tena kama mwanzoni.  Akaanza kumbusu shingoni akahisi anamtoa sidiria. Huku akimpitisha  kidole kwenye uti wa mgongo.  “Mmmh! Huyu Mzee wamo huyu!” Tunda  akashangaa. Mambo anayajua kuliko  hata mwanae!” Akajisemea  mwenyewe wakati Mbawala akitoa ile  sidiria mkononi. Tunda akacheka.  Akabaki mtupu mbele yake, mapajani. 

Akamsogeza kiwiliwili kwenye kiti  cha mbele. Tunda akawa ameegemea  kiti cha mbele huku amemkalia.  “Uliniambia unaniaga.” Tunda  akacheka taratibu na kutingisha  kichwa kukubali. Basi taratibu. Nipe uhuru.Tunda akakubali taratibu.  Akafurahia kupewa huo uhuru.  Alichezea huo mwili wa Tunda na  kumzungusha hapo kwenye gari,  Tunda akabaki  mwenyewe  anamshangaa. Taratibu bila pupa wala  papara. “Huyu Mzee Muhuni huyu!” Tunda akajisemea.

Kuja kumaliza na  kuangalia saa, ni saa tano usiku wakati  Tunda alifika hapo saa moja na nusu. Umeridhika?” Akamuuliza Tunda. “Sana. Nimefurahia jinsi  unavyonishika.Akacheka. Sikutaka  ujiumize.” “Nashukuru kwa kujali. Akajirudisha  mbele  akamlalia  shingoni, kama katoto. Akamuona  anambembeleza mgongoni mpaka  Tunda akapotelea hapo kifuani. Baada ya muda Tunda akashtuka.  “Mpaka nimesinzia!” Nilihisi jinsi  ulivyokuwa ukihema.Wakacheka. Tunda akashuka pale mapajani.  Akaanza kuvaa.

Nimepata wakati  mzuri Mbawala! Nashukuru kwa  kujali. Sikutegemea.  Hakumtumia mwili wake kikatili.  “Karibu. Ipo siku nitakubembeleza ulale vizuri.” Tunda akacheka.  Akambusu  shavuni.  Akavaa  nakujiweka sawa. Acha nikajiandae  na safari.” “Sawa. Nitakupigia kabla  hujaondoka  asubuhi. Tunda  akambusu tena shavuni, akashuka kwenye gari. Yalikuwa yamebaki  magari machache sana hapo uwanjani  na yote yalikuwa mbele sio kule  nyuma walipokuwepo wao.

Alifika nyumbani kwake akatoa ile bahasha aliyopewa na Waziri. Akabaki  ametoa macho. “Anautani na mimi  huyu! Dola!!” Tunda akashtuka sana.  Akaanza kuhesabu huku akicheka.  Akazirusha zote juu huku anarukaruka  kwa furaha. Tunda nimeshika dola! Hakuamini. Akamkumbuka mwanae  aliyemuahidi usiku wa ijumaa,  akaenda kuchanganywa na dad yake, akajikuta anampa yeye siku za  mwanae. “Baba yake anastahili.  Kwanza ananijali sio kama mwanae  huwa hata haulizi kama nimefurahi  au la. Ilimradi yeye aridhike basi.  Hana maana.” Tunda akawaza huku  akivuta simu yake.

 Akamtumia ujumbe palepale.  ‘Samahani Mbawala. Nimepata safari ya  dharula, nasafiri kikazi kesho asubuhi sana. Kurudi inategemea na mambo  yatakavyokwenda huko. Lakini naahidi  kukutafuta nikirudi. Na nitalipiza.’ Akatuma huo ujumbe. ‘Ningejua basi  ningekuja hata usiku wa leo nikuage.’ Tunda  akacheka, na kukumbuka agana yake  na baba yake. Akavuta pumzi kwa  nguvu. Akacheka. “Huyu asingeweza  kuniaga hata nusu ya baba yake.  Aache kunitania.” Tunda akajisemea,  akaamua kujibu. Sikujua wala kupanga hii kusafiri. Ningefahamu mapema, ningetafuta jinsi ya kuonana. Nisamehe.’ ‘Usijali. Naelewa Fina. Tafadhali ukirudi  niwe wa kwanza.’ ‘Promise.’ Tunda akaweka ahadi. ‘Thanks.’ Mbawala Junior akarudisha huo  ujumbe. Akajua amehuzunika, lakini  akajimbia atasubiri kwanza. 

Akaona awe muungwana. Akamtumia  ujumbe baba mtu sasa. ‘Mbawala,  nakushukuru kwa wakati mzuri na waheshima ulionipa leo. Asante kwa pesa pia.’ ‘Karibu.  Na mimi nimefurahia wakati mzuri  tuliokuwa nao. Pumzika. Kesho tutaongea  zaidi.’ ‘Usiku mwema.’ ‘Na wewe Dori.’ Akajibu baba mtu. Sasa ili asije  kujichanganya,  akabadili  majina  kwenye simu ili asije kujichanganya. Tewele{Irene}, Mbawala dad{Dori}, Mbawala  Dodoma{Fina},  Kinny{Fina}.  Akajiridhisha. Akafunga simu na kuanza kujiandaa na safari sasa. 

Tunda alilala kwa furaha kama katoto  kachanga. Kwanza akajisifia mwili  wake kushikwa na waziri. Tena sio  waziri tu. Waziri wa mambo ya nje,  mwenye uwelewa, msomi, mzuri hata kwenye mapenzi, aliyemuheshimu na kumpa penzi zuri. Akacheka tena kisha mawazo yakamrudisha alivyokuwa naye garini!  Jinsi alivyokuwa amemkumbatia  pale garini.  “Naamini tutakuwa na wakati mzuri  huko.” Akakumbuka maneno ya  waziri. Kwa ufanyaji ule wa mapenzi,  kuwekwa mikononi vile, lazima  wakati mzuri utakuwepo.” Tunda  alijilaza pale kitandani akicheka  taratibu huku chumba chake  kimezagaa dola. Mungu ampe nini  Tunda! Na kesho yake anakwenda Afrika ya Kusini!

“Tunda ambaye hata  sijasoma, leo nashika dola, na kukaa  na wakuu wa nchi sehemu moja! Tena naheshimika na wasomi! Kinny  na shule yake alishindwa kumuingia  Mbawala! Mimi nikaweza kumpatia  ile tenda, tena ya mamilioni!” Ujasiri na uthamani ukazidi kuongezeka  kwa Tunda. Furaha pekee ndiyo  iliyomfanya akalala.

  Safari ya kusini mwa Afrika.

N

dege ilikuwa ikiondoka saa nne asubuhi. Akatoka kwake masaa mawili kabla. Kwa kuwa hakuwa akijua anarudi lini, basi akajiandaa vilivyo. Na shauku ikaongezeka zaidi kwa heshima waziri aliyomuonyesha usiku uliopita. Akamtumia  ujumbe kumwambia ameanza safari na  alipata ndege. Akampa na muda  watakaokuwa  wakiondoka  hapa  nchini. Akamtumia huo ujumbe.  ‘Naruhusiwa kupiga?’ ‘Nitafurahi kukusikia.’ Tunda akarudisha majibu.  Simu ikapigwa. “Kuniona je?” Tunda  akacheka. Najua sasa hivi upo kazini.  Huwezi kuniona.” “Utanikuta uwanja wa  ndege nakusubiri nikuage.” “Haiwezekani! Tunda  akajikuta  anashangilia kwa sauti,  Mbawala akaanza kucheka.

“Siamini!” Ukifika  tu,  nipigie  nikuelekeze nitakapokuwepo. Naweza kufika hapo kabla  yako. Sipo mbali na uwanjani.” Tunda  akajikuta anafuraha ya ajabu moyoni.  Akatamani amwambie dereva  aongeze mwendo. Lakini akakumbuka  ajali ya gari aliyoipata na kusababisha  kifo cha Sadiki. Akaona atulie,  amwache aendeshe vile vile kwa  makini. Na kweli alikuwa makini.  Aliendesha mpaka uwanja wa ndege. 

Alipoingiza tu gari pale uwanjani, Tunda akampigia simu. “Nimeshafika.  Nipo..” Akapokea na kumwelekeza sehemu atakayokuwepo. Tunda akafurahi sana.  Akamwelekeza dereva taksii wapi  apite. Wakati taksii iliyombeba inapita  alipomwambia  yupo,  akamuona  amesimama nje ya gari. Moyo wa Tunda ukazidi kujawa furaha alipomuona, asijielewe. Dereva alikuwa  amepita pale alipokuwa amesimama  waziri, kidogo tu. Yeye hakuwa  amemuona waziri. Waziri alikuwa  amesimama kwa nyuma kidogo,  pembeni ya gari yake. Sio kwa uwazi  sana. “Simama haraka.” Tunda  alishuka pale kwenye taksii kama  mshale na kurudi nyuma pale  alipomuona  waziri  amesimama. 

Alikuwa akimkimbilia kwa furaha zote  kama mtu ambaye walipotezana kwa  miaka. Akajikuta anamrukia na  kumkumbatia.  Mbawala  alikuwa  anacheka sana. Tunda alimkumbatia  kwa nguvu akiwa amejilaza shingoni  na Mbawala amemnyanyua huku  amemkumbatia.  Akajishangaa machozi yanamtoka. Usilie sasa.“Sikutegemea! Nimefurahi sana.” Akaanza kumfuta machozi. Asante.

Hata yeye hakujua kule machozi yalipotokea!  Pengine safari ya Sauzi au kujaliwa na  waziri. Lakini Tunda hakuwa mliaji hata! Akajicheka. “Mizigo iko wapi  sasa?” Nimeacha kwenye taksii kwa kupaniki nilipokuona kweli unanisubiria. Sikuamini ulivyoniambia nitakukuta hapa. Mbawala akacheka huku  akimrudisha nywele nyuma na  kumfuta machozi. “Umeshalipia?” Bado. Ngoja nikachukue mizigo  yangu halafu nije. Tunda akarudi  kwenye taksii kwa furaha yote akijifuta machozi ya furaha na kujaribu kutulia.

Akamlipa dereva, akachukua mizigo yake akarudi  kwenye gari la waziri akamkuata bado amesimama nje akimsubiria.  Kumbe kwenye mwanga ndio unavutia hivyo!” Tunda akacheka na  kuinama huku akijifuta machozi vizuri.  Umependeza sana.” “Asante. Ila ujue nimefurahi sana kukukuta hapa.  Sikutegemea.” “Sasa mbona umewahi hivyo!?” Kwa kuwa natumia taksii,  huwa sijui aina ya uendeshaji wa mtu.  Kwa hiyo huwa najipa muda mrefu ili  nisichelewe.” Hapo  sawa. Akamwangalia na kucheka. Nini  sasa?Tunda akauliza kwa aibu  kidogo. Una macho mazuri sana  Dori.  Halafu  unavutia.  Laini, halafu mtaratibu!” Tunda akacheka na  kumshika mkono.

Unakuja lini sasa?” “Kesho nitakuwa huko. Chakula cha mchana tutakula wote. Nitafurahi. Unaondoka sasa hivi? Unataka niondoke?” “Nataka tubaki  wote mpaka niondoke. Twende ndani  ukanikumbatie.” Mbawala akacheka.  Wakaingiza mizigo ndani ya gari,  wakaingia ndani ya gari, wakakaa kiti  cha nyuma.

Tunda akapitisha mikono chini ya  mikono  yake  yote  miwili  akamkumbatia kwa nguvu na kujilaza  kifuani. Mbawala akambusu kichwani  mara kadhaa, wakabaki kimya Tunda  amejilaza,  Mbawala  anamchezea  mgongoni. “Tunarudi lini?” Tunda  akauliza taratibu. Ni mkutano wa siku  tatu tu. Ya nne tunarudi. Nitakuwa  nimekuweka sana?Tunda akatingisha  kichwa kukataa. “Ni sawa.” Akajibu  taratibu. Wakatulia.  Hutaki tuagane leo?Waziri  akauliza. Tunda akamwangalia. Na  mwanga huu!?” “Hapa nyuma hakuna  atakayetuona akiwa nje. Hivi vioo  vimetengenezwa maalumu. Mtu yeyote  akiwa nje, hata kama ni mchana,  huwezi kuona ndani. Ni kwa ajili ya  usalama  wangu.”

“Labda kama umechoka.” Hata kidogo. Nimependa vile ulivyonishika jana. Sikuchoka hata  kidogo. Hapo  hapo  Tunda  akachangamkia penzi. Mzee huyo hakuwa na  papara, alivuta muda akimzungusha  Tunda kwa hili na lile, mpaka  wakaridhika.  Tunda  akambusu  tena shavuni kama anayemshukuru.  “Nitakuona kesho. Asante kwa kuwa  na mimi hapa na kukaa na mimi  mpaka muda wangu umefika.” Mbawala akatoa tabasamu na kumjibu, “Angalau  nimeanza siku vizuri.” Tunda akaanza  kuvaa nguo zake, huku akimsaidia  kumuweka sawa. Aliporidhika na muonekano wake, ndipo akashuka  garini. Akachukua mizigo yake  akaondoka kwenda kupanda ndege. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Akiwa kwenye ndege, Tunda akaanza  kuwaza. “Au Mungu ndio ameniletea Sadiki mwingine?” Tunda akafikiria. Lakini hapana. Mbawala sio Sadiki. Huyu baba anaheshima, halafu amenipokea akifaidika na penzi tu. Kumbukumbu zikamrudisha kwenye  maisha aliyoishi na Sadiki. Mpaka  yeye mwenyewe akasisimkwa mwili kwa hofu. “Nilipatwa na nini!?”Akajishangaa kwa mambo aliyokuwa akifanya na Sadiki!  Jinsi alivyokuwa amekubali kutumiwa  bila mpangilio. Mara amwambie usiku  huo lazima wafanye mapenzi, ndio  usiku wa kheri. Mara wawe wao  wawili tu, usiku sana makaburini  wakifanya  ibada  za  ajabu.  Akakumbuka siku moja kutokewa na  joka katikati ya ibada hiyo hapo  makaburini. Akataka kukimbia, lakini Sadiki  akamshika,  akamwambia  asiogope.

Haya, kila wakitoka  makaburini amwambie ndio wafanye  mapenzi vile vile hata kabla ya kuoga!  Ilikuwa fujo, vurugu mchanganyiko  ambao hata Tunda hakujua alimudu vipi ule ujinga.  Akavuta pumzi kwa nguvu, akili  ikamrudisha kwa waziri Mbawala.  Hapo hapo akasahau mambo yote ya  Sadiki, akacheka akiwa bado yupo  kwenye ndege. Kumbuka ya pesa  alizompa ikamrudia. “Akiendelea hivi,  mmoja tu atanitosha.” Tunda akaendelea kuwaza. Akili ikamrudisha  kwa mtoto wake. Hamfikii baba yake  hata kidogo. Na ndiye atakuwa wa  kwanza kumtoa kwenye orodha  yangu. Yupo rafu sana, japo anatoa  pesa nzuri. Baba yake mstaarabu  sana. Anatumia mwili wangu vizuri.”  

Akakumbuka mapenzi waliyofanya  kwenye gari kabla ya kuondoka. Vile  alivyomkuta akimsubiria pale sehemu  ya kuegeshea magari, pembeni ya gari  yake. Ilimgusa sana Tunda. Akacheka  na kugeukia dirishani.    

Tunda & Waziri Mbawala Sauzi.

A

litua uwanja wa ndege wa kimataifa wa OR Tambo,  uliopo  Johannesburg hapo Afrika ya kusini. Akachukua taksii akawapa ile address kama alivyoelekezwa na Mbawala.  Dereva akaelewa kwa haraka kwa kuwa ilikuwa  hoteli kubwa sana ya kimataifa hapo mjini. Tunda mwenyewe akashangazwa na hiyo hoteli. “Kama Dubai!” Akajiambia  Tunda mtoto wa matawi. Alishafika  Dubai  akiwa  na  Sadiki.  Ila  hakutegemea kukuta nchi ya Afrika  ipo nzuri vile.  Aliingia hapo hotelini, akaonyesha  simu yake pale mapokezi. Ujumbe  aliokuwa ametumiwa na Mbawala wa  booking ya chumba. Akapewa kadi ya  kufungulia mlango. Muhudumu akaja  kumsaidia kubeba mizigo, wakaelekea gorofa ya 8 ndipo kilipokuwa hicho  chumba chao. 

Macho yalimtoka zaidi. “Suite!” Akajisemea huku akitoa macho wakati  anazunguka  hicho  chumba.  Muhudumu akaweka vitu vyake,  akamuuliza kama nahitaji chochote,  Tunda akampa tip kama kumshukuru.  Akaondoka.  Akafurahia ule utulivu pale.  Alipozunguka kote na kujiridhisha na  hicho chumba, akampigia simu waziri  Mbawala kumjulisha kuwa amefika  salama, na yupo hapo chumbani.  “Natamani kama ungekuwepo hapa na  mimi!” Tunda akajilalamisha. Kesho  kama sasa hivi, tutakuwa wote. Kuna kitu cha  muhimu sana lazima nikifanye leo ndipo niweze kuwepo huko kwa hicho kikao. Wakazungumza kidogo, wakaagana. Aliagiza chakula hapohapo  chumbani. Ilipofika usiku, akaoga na  kulala moja kwa moja. Hakutaka hata  kutoka hapo chumbani. 

Kesho yake Mbawala alifika hapo  hotelini mida ya saa sita mchana,  akamkuta  amejilaza.  “Wenzako wanatumia safari kama hizi kuzunguka madukani, wewe  unajifungia ndani tu!” Tunda  akacheka. Pole na safari.” “Ilikuwa  fupi. Nilichukua ndege ya moja kwa  moja, express. Nilikuwa na kikao  asubuhi, nimetokea ofisini.” Kwa  hiyo hujachoka?Tunda alimuuliza  huku akimsogelea. Hata kidogo.  Wewe njaa haiumi?” “Njaa yangu ni  wewe. Njoo kwanza hapa kitandani,  unishike shike ndio tule.Tunda  akamvutia kitandani. Siku hiyo waliitumia hapo chumbani mpaka kesho yake waziri ndio alikuwa anaanza mkutano wake. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Waziri Mbawala alikuwa akitoka  asubuhi kwa masaa kadhaa. Alikuwa  akimuaga  anakwenda  kwenye  mkutano, kisha anarudi na kumkuata Tunda akimsubiria hapo chumbani. “Si utoke  akazunguke kidogo? Au umeshawahi  kufika huku?” Hapana. Ni mara  yangu ya kwanza. Ila napenda huu utulivu humu ndani. Najisikia vizuri. Mbawala akacheka.  Siku ya tatu hakutoka, akamwambia  kikao kimeahirishwa, mpaka saa 10   jioni. Kwa hiyo siku hiyo asubuhi hiyo mpaka mchana akawepo tu hapo  chumbani na Tunda. Kesho yake  jioni ndio walikuwa wakirudi  nchini  Tanzania baada ya kikao chao cha asubuhi kuisha. Kwa hiyo wakawa  wapo tu hapo chumbani.

Walishapata  kifungua kinywa. Penzi la nguvu la  muda mrefu tu likaendelea mpaka  wakatosheka.  Mbawala akakaa upande wa living  room, kwenye makochi kupiga simu  zake nchini akiwasiliana na huyu na  yule huku akiwa anatumia laptop yake kwa  muda tu. Akifanya hili na lile, Tunda akiwa kitandani ametulia kimya kama  hayupo pale.  Akamuona Mbawala anamwangalia.  Macho yakagongana, Tunda akacheka  kicheko chake cha taratibu. “Wewe ni  mtulivu sana! Upo hapo kama haupo!  Umetulia sana! Unawaza nini?” Tunda akacheka tena taratibu bila  kujibu. “Ujue mimi nilijua umelala!” Tunda akatingisha kichwa kukataa.  Mbawala akazima kila kitu, akaamua kurudi na yeye pale kitandani.

Tunda  akajivuta na kujisogeza mpaka chini ya  kwapa lake. Akajikunja na kulala  ndani ya blangeti nzuri ya kisasa.Baridi ya Ac  ilikuwa ikipuliza.  Mbawala akamkumbatia. “Nikuulize  swali Dori?” Tunda akanyanyua  kichwa na kumtizama. Akamlaza nyusi  taratibu  huku  akimwangalia.  Nimegundua unakwepa mabusu ya  mdomoni. Ni kwa nini?” Tunda  akafikiria kidogo. Akatoa tabasamu la  upole. Sitaki kuja kuangukia kumpenda mtu  asiye sahihi.Akamjibu hivyo  taratibu. Mbawala akambusu kichwani.  Yaani mpaka sasa hivi hujapata  mtu!?Akauliza kwa mshangao kidogo. Tunda akatingisha kichwa  kukataa. “Lakini bado unaonekana  mdogo sana Dori. Sidhani hata kama umefikisha miaka 25.” Tunda  akacheka na kuinamisha macho yake chini.

Nimepatia?Tunda akacheka tu akiwa ametulia vilevile. Mbawala  akamnyanyua uso. “Jina lako pia sio Dori.” Tunda akashtuka sana. Lakini ikabidi akubali.  “Hapana.Tunda akajibu kinyonge na  aibu kubwa usoni. Akambusu kichwani. Tunda akageuka upande wa  pili na kunyamaza kabisa. Akamvuta  kiunoni na kumsogeza karibu yake.  Akambusu shingoni. Tunda akavuta  pumzi kwa nguvu na kuzishusha  taratibu. Kimya.  “Nataka  kukufahamu  zaidi.” Akamsikia  akimnongoneza  sikioni.  Tunda akanyamaza akitetemeka mwili  mzima kwa hofu.

Nikwambie kitu?Tunda akatingisha kichwa kukubali. “Nigeukie sasa.”   Akageuka.  Nimepata muda mzuri sana na wewe.  Umetulia. Nimepata utulivu wa aina  yake. Lakini nataka kukufahamu kwa  ukweli.” Tunda alishindwa azungumze  nini akabaki ametulia. Hofu ilishamuingia, akaamua kutoka pale  kitandani kuelekea bafuni bila ya kujibu  kitu.

 ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Alikamatwa vibaya sana. Kulikuwa na  nguvu ya namna yake anapoyavaa yale  majina tofauti tofauti. Kila jina  alilolivaa alilipa tabia zilizoficha  ukweli wa Tunda asilia. Tunda  mwenyewe alibeba historia ambayo hakutaka kumkumbuka hata kidogo.  Yale majina aliyokuwa akijipa,  alikuwa ni kama anapewa utu mpya  nakufanya  anayoyafanya  kwa  kujiamini. Akijiita Fina, basi huyo Fina atampa uwezo wa kuwa mfanyabiashara mzuri sana na atampa  mamlaka yakuweza kuzungumza na wasomi, na  kumfanya afikiri kisomi na kuweza  kutoa ushauri mkubwa uliompa Kinny dili ya pesa nyingi.

Akiwa Irene, anakuwa msichana  anayejielewa. Mwenye mipango na  mikakati ya maisha. Nguvu ya elimu  ipo na uelewa mkubwa wa maisha.  Jinsi alivyojibeba kwa Tewele,  muonekano  wake,  usingedhani  vinginevyo. Akampa ushauri wa  kisomi jinsi ya kumkabili bosi wake.  Akajisikia yupo sehemu sahihi.  Akiwa Doris au Dori, ni msomi  aliyekuwa akitafuta kazi kwa waziri Mbawala. Amefanikiwa. Anachohitaji ni wakati mzuri tu.

Ndio  maana yupo huru kufanya naye mapenzi popote bila shida wala kulia  shida. Kwa kuwa yupo likizo ya  kikazi. Tena kazi nzuri tu. Kuwatoa  Fina, Irene, na Doris kwake, ni  kumuanika Tunda ambaye hakuwa tayari kumuishi hata kidogo. Tunda  alibeba machungu ambayo hakutaka  kumfikiria wala hakuwa tayari  kumuishi. Kina Fina walimsaidia  kuishi maisha nadhifu na ya kitajiri.  Waziri Mbawala anataka kumtoa  Doris! Ili awe nani? Tunda!  Alimnyima raha Tunda, asijue.  Alimtoa kabisa kule mafichoni na  kumkumbusha yale maisha sio yake. Bila ya kujijua, waziri akajikuta anamrudisha Tunda kule alipotakiwa awepo. 

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

     Alikaa huko zaidi ya lisaa. Ikabidi  Mbawala amfuate. Alimkuta amejilaza  kwenye sink, amefunga macho. Tunda  alifungua  macho,  akamwangalia  macho yakagongana. Aliingia hapo  ndani akiwa ameshavaa kabisa, suti  yake na akawa amefunga na tai, kama  anayetaka kutoka. “Kuna movie theater hapa chini ya hii hoteli. Ni  sawa nikienda kuangalia wakati wewe unakwenda kwenye kikao?” Bila  shaka.Ni saa ngapi?” “Nitapiga simu  mapokezi  kuuliza.” Sawa. Akamkubalia.  Mbawala  akabaki  amesimama  akimtizama pale ndani ya maji akajua  kuna kitu kikubwa anaficha. Mwishoe  Tunda alipoona kuna ukimya kama  Mbawala anayemsubiria azungumze  kitu, akaamua atoke ndani ya yale maji  arudi chumbani. Mbawala akajua anamkwepa.

Na yeye akamfuata  nyuma. “Nakaribia kuondoka Dori.” Na mimi nitatoka muda mfupi sana kuanzia sasa. Wameniambia movie  mpya itaanza baada ya dakika 20  kuanzia sasa.Tunda akajibu vile  akijua wazi ni kama anapewa nafasi ya kujieleza ukweli. Lakini akaikwepa na  kuanza kujiandaa.  Akamuona bado Mbawala ametulia  akimtizama.  “Naomba  nikitoka  kwenye movie, nizunguke kidogo  kuangalia mazingira kabla hatujarudi  nyumbani.” Wazo zuri. Ningekuwa  sina  kikao  cha  jioni,  ningekusindikiza.” Tunda akatoa tu  tabasamu na kugeukia pembeni, waziri  akamuona. 

Nini?  Au  hutaki  kuongozana na mimi?” “Siku hizi kila  mtu paparazi. Ukitokea tu sehemu ukiwa na mimi, kesho ujue utajikuta  kwenye vyombo vyote vya habari.” Hilo likampunguzia waziri wasiwasi,  nakuongeza swali jingine kichwani.  Ubaya upo wapi?Tunda akakunja uso kama asiyemuelewa waziri huyu, tena mume wa mtu! Lakini akaona  anyamaze. “Eti Dori? Ni nani unayemuhofia  asikuone na mimi? Au Mbawala yule  uliyekuwa ukiwasiliana naye siku ile ukaishia kwangu ni mtu wa karibu yangu sana?” Tunda alishtuka, akakaribia kuanguka. Mwili mzima  alihisi umepigwa na shoti ya umeme.  Akaamua kugeuka kwa haraka ili  asimuone ile hali ya mshtuko aliyojua  wazi inaonekana mpaka usoni.

“Eti?” Akauliza. Lakini  Tunda alishindwa hata kugeuka, waziri  akamfuata kule alipogeukia. Akamtizama  usoni.  “Ooooh!” Akasikika kama aliyepata jibu lake.  Kisha akaondoka. Mbawala alitoka hapo, akamuacha  Tunda akikaribia kuchanganyikiwa.  Mambo mengi yalipita kichwani kwa  haraka, akasikia tumbo limevuruga,  akakimbilia chooni. Tunda alitapika  mpaka yakabaki mate tu tumboni.  Akaoga na kuamua kutoka pale.  Alihisi bado vile vitu vya Mbawala  pale chumbani ni kama Mbawala  mwenyewe akimtizama. Tunda amekamatwa  vibaya sana. Hakujua atafanyaje. 

Alikuja kurudi saa nne na nusu  usiku. Akamkuta Mbawala akimsubiri  kitandani. Bado usoni alikuwa  amejawa hofu. Ujasiri ulimwisha kabisa. Kwa vile alivyokuwa waziri Mbawala, akajua fika, anamsubiria yeye. akataka kupitiliza bafuni, lakini akamuwahi. “Njoo.”

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Njia ya muongo imekuwa fupi kwa Tunda. Atatoka vipi? Amegundulika vipi, na kwa ukubwa upi? Endelea kufuatilia.

CONVERSATION

0 Comments:

Post a Comment