A |
![]() |
Alijulikana kama Tewele. Tunda akatumia akili ya haraka. “Samahani kipenzi.
Nipo katikati ya jambo. Naweza kukupigia baadaye kidogo, Tere?” Tunda
alipokea akionyesha na haraka kwa Tere,
na sauti nzuri sana. “Nafikiri umekosea namba. Mimi ni Mr. Tewele sio Tere.” “Oooh Nooo. Samahani kaka yangu. Samahani sana. Nahisi kwa kuwa majina yenu
yanafuatana kwenye orodha yangu ya simu,
nimeandika ujumbe nikiwa na haraka huku
nikijilaumu kwa kutomtafuta Tere wakati
anashida na mimi. Naomba nisamehe kaka
yangu. Samahani sana kwa usumbufu.” Tunda alijilalamisha kwa sauti ya deko huku akimwita kaka, wakati ni baba mtu mzima tu tena mkubwa hata kwa umbile.
Akamsikia akicheka taratibu. “Usijali. Hamna
usumbufu wowote ule. Nilitaka
kuhakikisha napata ujumbe wangu sio wa
mwingine ndio maana nikapiga kuhakikisha.” “Samahani sana kaka yangu. Nafuta kabisa namba yako. Sijui nan..”Akajidai
amesita. “Haitatokea
tena.” “Kabla hujafuta namba yangu, na kunitupilia mbali mapema, inabidi uniambie wewe ni nani na imekuaje wewe una namba
yangu, wakati mimi sina namba yako.” Na yeye aliongea kwa sauti iliyotulia na kama
Tunda.
“Ni kwambie ukweli? Ila sitakutajia
aliyenipa namba yako.” “Mbona masharti tena?” “Unataka
kuambiwa ukweli au kudanganywa?” “Ukweli mzuri,
japo wakati mwingine unauma.” Tunda akacheka. “Basi kwa kuwa
nipo kwenye kitu cha muhimu, naomba
nikupigie baadaye tafadhali.” “Nasubiri.” Tunda akacheka kidogo. “Mida gani
mizuri?” Tunda akauliza taratibu. “Kwanza nitajie jina lako, ili
nitunze namba yako kabisa. Nikiona
sipati hiyo sauti nzuri mpaka kesho, nipige mwenyewe.” Tunda akacheka sana. “Nitapiga. Hata
kama haitakuwa leo, lakini nitapiga. Na
nilikuwa na shida na wewe ndio maana
nikapewa hiyo namba, nikaambiwa wewe,
Tewele, ndio jibu la mambo yote.
Nikikupata wewe, shida yangu imeisha.” Tewele akacheka sana.
“Kweli
tena.” Tunda akamuhakikishia. “Sasa mbona hujanitafuta, au nimeshapata msaidizi?” “Mmmh! Kwa kiasi kikubwa ni kama
nimepata ufumbuzi. Nitakueleza zaidi
baadaye. Naomba nikuage kwa sasa, na
samahani sana.” “Hamna shida. Nani tena?”
Tewele akitaka kumfahamu jina. “Irene.” “Asante Irene. Nimefurahi kukufahamu. Naamini tutawasiliana.” “Asante.” Tunda akashukuru na
kukata simu. “Yesss!”Akaruka pale
kitandani akishangilia kwa ushindi.
Mbawala!
I |
likuwa
siku ya jumatano Tunda akakumbuka ahadi yake kwa Mbawala. Akaamua kumtumia ujumbe. “Huyu naye asitake kunizoea. Siku mbili
kwani mimi mkewe!” Akajiambia Tunda
huku akimwandikia huo ujumbe Mbawala. ‘Samahani. Naona ijumaa imeshindikana. Nitakuona jumamosi.’ Hapo hapo Mbawala akapiga. “Mpaka
moyo umepasuka!” Tunda akaanza
kucheka. “Pole.” “Mbona napata siku moja tu?” “Lakini hutakaa ukaijutia. Nimeshindwa kubadilisha ile miahadi
niliyokwambia. Na nimuhimu sana. Ila
nitahakikisha inafidia na hiyo ijumaa.” Tunda akaongea kwa kujiamini. “Yesss!”
Mbawala
akasikika akishangilia. Tunda akacheka. “Ninavyokusubiri
kwa hamu, utafikiri nini sijui!” Tunda akacheka taratibu. “Naamini tutapata
wakati mzuri.” “Asante Fina.” Mbawala akashukuru
kwa heshima zote, utafikiri amepewa alumasi, kumbe ni kutembelewa na Tunda!
“Tena mambo yenu naona
kabla hata ya ijumaa yatakuwa safi.
Mwenzangu ameafikiana kwa haraka sababu
ya bei. Ukija jumamosi, utakuta
nimekuandalia kila kitu. Nitakukabidhi
ukija.” Hilo akalifurahia zaidi Tunda. “Heshima itaongezeka kwa mjinga yule.” Akimaanisha Kinny
ambaye alishamchukia. Inamaana yeye
ndio atamkabidhi Kinny! Na inamaana atalipwa pesa yake bila shida! “Naua ndege wawili kwa jiwe moja!”Akajiambia Tunda.
“Umeongeza umuhimu wa hiyo safari.” “Mbona unanivunja nguvu tena?”
Mbawala akalalamika. “Kwa nini tena?” Tunda akauliza huku akicheka.
“Naona kama umenitoa uthamani.” “Hata
kidogo. Tuombeane uzima, labda shukurani
zangu utazielewa kwa vitendo.” “Ninavyozisubiria kwa hamu!”
Tunda
akacheka. “Naomba
nikuage Mbawala. Tutawasiliana.” “Naruhusiwa kupiga wakati mwingine?”
Hilo ndilo alilojiambia hatakaa akafanya, kuanza tabia
ya kupokea simu au kutumiana jumbe za
mapenzi na yeyote yule. “Naomba
usijisikie vibaya. Nakuwa busy sana. Wakati mwingine mpaka simu naona kero. Naomba uniamini kuwa nitakuja siku ya jumamosi.
Upo kwenye ratiba yangu. Na huwa
sio mbambaishaji.” “Nimekuelewa Fina. Basi niruhusu nikate mimi tiketi na nitume pesa
ya taksii itakayokupeleka uwanja wa
ndege. Ila huku ujue mimi nitakuwa
nikikusubiri uwanja wa ndege.” “Nakushukuru Mbawala. Asante
sana.” Tunda akashukuru na kukata simu bila yakuongea maneno mengi.
Ukimsikia
akizungumza kwenye simu, unaweza
kumdhania ni msomi wa hali ya juu na yupo
na majukumu mazito na muhimu. Kumbe
kama hapo alipokuwa akizungumza na Mbawala na Tewele yupo kitandani kwake ametulia wala hana pakwenda au chakufanya.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mpaka hapo akajiambia anao watu watatu tayari wakumwingizia pesa kwa wakati
huo. Mambo safi. Akacheka. Akiwa kwenye
ile hali ya furaha akaona simu yake imeingia ujumbe kuwa pesa imeingia.
Akatazama ile pesa akajipongeza. Mbawala
ndiye aliyemtumia ile pesa. Hajakaa sawa akiwa anafurahia pesa, ujumbe mwingine
ukaingia. Safari hii ulikuwa ukitoka kwa Kinny. Tunda akafikiria. Hakutaka hata kuusoma. Akaamua kutoka
hapo kitandani na kuelekea maliwatoni, kuoga, ili sasa atoke hapo ndani
akatengenezwe tena huo mwili alioamua kuufanyia biashara.
Mwili wa Tunda ulikuwa ukifanyiwa waxing mara kwa
mara. Usingekuta vinyweleo popote, au
kipele hata kimoja. Laini na nyororo
wakati wote. Akakusudia siku hiyo ya
jumatano mpaka alhamisi iwe ni mwili
wake tu. Utengenezwe. Waxing, sauna,
masaji na kubadili nywele na kucha. Alitoka bafuni akakuta Kinny amepiga simu na kutuma tena ujumbe. Baada ya muda akaona anapiga tena simu. Akajifikiria.
Apokee!? “Huyu mbambaishaji tu. Sina mpango naye kwa sasa mpaka nikitoka Dodoma na kazi yake. Anipe pesa yangu, niachane
naye kwa amani.” Akakusudia kumpuuza. Akaweka
simu pembeni, na kuendelea
kujitengeneza. Akamkumbuka Tewele, akaona amuweke kidogo. Amsubirishe, asije
kumuona anajirahisisha.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Wakati anakaribia kutoka nyumbani kwake ujumbe mwingine ukaingia kwenye simu yake. Akautizama akidhani ni Kinny, akakuta ni Tewele. ‘Natoka kwa ajili ya
chakula cha mchana. Kama ungependa
kuungana nami karibu.’ Akamwandikia jina la sehemu atakayo kwenda kula. Tunda akasoma nakubaki akifikiri chakujibu. ‘Naweza kukupigia sasa
hivi?’ Tewele akatuma ujumbe mwingine. Tunda akampigia yeye. “Umenisahau Irene!” Tunda akacheka. “Lakini
ningekupigia.” “Unanafasi sasa hivi?” “Kwa muda mfupi. Lakini sehemu
uliyonitajia ni wazi sana na wewe mtu
mkubwa sana. Sitaki kuwa magazetini
kesho.” Tewele
akacheka sana huku akifurahia na yeye hilo wazo la kutoonekana naye
hadharani. Hata kwake itakuwa salama
japo alilisahau hilo kwa uchu.
“Basi
chagua ni wapi ungependa tukale. Ili
tufahamiane zaidi. Hiyo sauti imegoma kutoka kichwani kwangu. Nataka
niiweke kwenye sura sahihi.” Tunda akacheka kidogo. “Labda uchukue
chakula, halafu twende tukale sehemu.
Mimi na wewe tu sio hata na dereva wako.” Hilo nalo Tewele
akalikubali bila shida. “Unataka kula nini?” “Mimi sio
mchaguzi Tewele. Utakachokula ndio na mimi nitakula hichohicho. Ni surprise.” Tewele akafurahia na hilo. “Sasa nitakukuta
wapi nikishakuwa na hicho chakula?” “Unafikiri itakuchukua muda gani kuwa na hicho chakula na kufika
Mlimani city?” “Nipe kama dakika 30 hivi. Nimtume
dereva akalete chakula chetu, halafu nikufuate hapo Mlimani city.” “Sawa, lakini naomba usiniweke tafadhali. Ufike baada ya dakika 30 kweli.” Tunda akasisitiza
kama asiyetaka kupotezewa muda. Akamtia hofu Tewele, yakuonekana hovyo kwa mara ya kwanza.
“Basi
sababu ya foleni ambazo hazitabiriki hapa mjini, tufanye baada ya lisaa.” “Sawa.” Tunda akakata simu. Akacheka na kurudi kukaa akisubiria muda. Akaangalia saa yake, akajua ni saa ngapi atoke hapo. Akakaa kwenye kochi akisubiria muda. Ni kweli Tunda hakuwa akipenda kelele. Hata
luninga aliwasha kwa sauti ya chini tu.
Akakaa pale akiangalia luninga huku akimfikiria Tewele. Nini amfanyie ili kumpagawisha
kiasi chakuingia kwenye orodha ya
watakao muweka mjini! Alikaa pale mpaka
muda wake aliokusudia kutoka ulipofika.
Akaita taksii.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Mmmh!” “Mbona unaguna tena?” Tunda akamuuliza wakati anafunga mkanda. “Heri nilivyokuomba tuonane. Ningepitwa.” Tunda akacheka. “Pole na kazi.” Akaanza Tunda taratibu
na tabasamu usoni. “Asante. Na wewe pole
na majukumu.” “Asante.” Tewele akabaki amekodoa macho. Tunda akacheka.
Alikuwa amevaa kigauni tena. Chenye
mikono mifupi tu, mpaka kwenye
viwiko, ila safari hii kifupi zaidi.
Kimechanua kidogo. Rangi moja tu,
rangi ya bahari. Akavaa na kiatu cha
juu cha wazi. Rangi ya kama kile
kigauni. Yaani vilifanana. Cheni
yake vile vile mguuni. Ila alikuwa na
pochi nyeusi iliyoendana na mkanda
mwembamba mweusi kiunoni. Hereni
fupi na cheni yakawaida isiyo na kidani.
“Kina nani hao wanaopata bahati ya miahadi na
wewe mchana?” Tunda akacheka kidogo. “Kuna mtu nilikuwa nakutana naye. Ni mambo ya kikazi, nashukuru Mungu mambo yameenda salama.
Njaa inauma Tewele.
Sijanywa chai, nimekuwa busy tokea
asubuhi!” “Nina chakula hapo
nyuma.” “Naipata hiyo harufu nzuri.” Tunda akasifia huku
akigeuka nyuma. “Chagua sehemu unayotaka
twende tukale, na mimi nishibishe
macho yangu. Umependeza, huchoshi kuangalia!” Tunda akacheka. “Asante Tewele. Hata wewe upo vizuri. Ila naomba nilegeze hiyo tai bwana. Utafikiri upo na raisi!” “Wewe ndio umenifanya
nitoke hivi.” “Mimi
tena!?” Tunda akauliza huku akicheka.
“Ndiyo!
Hukutaka nichelewe. Koti lenyewe
nimevulia kwenye gari kwa haraka. Hilo
hapo nyuma.” “Basi acha mimi nikutoe tai.”
Mbawala
akacheka. “Sawa.” Akakubali. Tunda alimsogelea mpaka karibu sana. “Una macho mazuri Irene!”
“Macho tu?” Tunda akauliza huku
akiisogelea ile tai. “Sauti nilishasifia.
Au umesahau?” Tunda akacheka bila kujibu akiwa amemsogelea akijaribu kulegeza tai. Akamfungua kifungo cha kwanza kilichokuwa kimeshikilia hiyo tai.
Akamtizama machoni, yakagongana. Akacheka na kulamba midomo yake. “Na cha pili?” Tunda akamuuliza taratibu tu. “Hamna shida.” Tewele akakubali
kwa haraka.
Tunda
akakifungua, akaachanisha hilo shati kidogo tu, kwa kupitisha kidole
kimoja ndani kama anayemtengeneza, kumbe nia ni ilikuwa
kumsisimua tu. Akaona amevuta pumzi
kwa nguvu. Akajua amemgusa sawa.
Kisha akamkabidhi tai yake. “Mmmmh!”Akavuta
pumzi kwa nguvu. “Au niitundike tai
hapo nyuma?”
Tunda
akauliza taratibu. “Hujaniambia wapi
ungependa twende tukale.” “Nisawa tukaenda
kuegesha mitaa ya Osterbay kule
baharini? Hakuna watu wengi, hasa mida hii na
siku kama ya leo ya kazi. Tutakula kwa
utulivu na wewe utakuwa salama bila
kashfa.” Hilo akaliafiki na kutoa gari hapo akiwa ametulia. Tunda naye akatulia akiwa amekaa kiti cha pembeni, kigauni nusu mapaja, amekunja nne.
Akamuona Tewele anatupia macho mara kwa mara. Tunda akacheka. “Huwa unaweza kuendesha na mkono mmoja?” Tunda alishamuona anahali mbaya. Hakutaka ajali nyingine. “Kabisa. Kwa nini?” “Nakuruhusu unishike ili utulize akili barabarani.” Tewele akababaika sana. “Hapana. Nimetulia. Ila
nilitaka kuhakikisha umefunga mkanda
vizuri.” Tunda akamtizama kwa kumsuta, akacheka. “Samahani bwana.
Naona nimevutiwa. Sikutegemea
kukutana na..” Tunda akachukua mkono
wake mmoja taratibu, akauweka juu ya
paja lake. Hata hivyo suruali ilishakuwa
imetuna tokea wanatoka Mlimani City.
Akaanza kumpapasa taratibu. “Irene wewe ni mzuri.
Laini!” Akasifia huku akimshika na
kumminya minya. Tunda akacheka na kunyamaza. “Ni hivyo upo na haraka.
Tungeenda kupumzika sehemu.” “Leo ni siku ya kazi Tewele. Tusichanganye mambo.” “Ni kweli.”
Akajirudi
kwa haraka. “Kwani weekend hii utakuwa na majukumu yanayokufunga?” Akamuuliza. “Nitakuwa safarini kikazi. Nitarudi jumapili usiku. Ulitaka nini?” “Tupane nafasi.”
“Basi nitafute week ijayo tupange vizuri. Week hii ipo na mambo mengi kidogo. Hata hivyo leo ni kwakuwa nakuheshimu sana na nilikukosea asubuhi. Nikalazimishia tuonane, ili usije kuniona mimi muhuni tu. Lakini nisingeweza kukuona week hii.” “Hata hivyo nimefurahi kukosea kwako.” Wakacheka. Mkono pajani
anashindwa hata kusogeza.
Tunda akahisi anatetemeka. Akaona amtoe hofu arudi kwenye maswala ya kawaida. Kila swali alilomuuliza, alichukua muda kujibu kama anayesikilizia raha na hataki kusumbuliwa. Tunda akaona
amuache andelee kufaidi hayo mapaja. Wakafika baharini akaegesha mbali kabisa. Wakajikuta wao peke yao. “Tuhamie kiti cha nyuma ili tule kwa uhuru.” Tewele akakubali kwa haraka. Wakashuka
na kuhamia kiti cha nyuma. “Huko ulipokaa mbali
Irene.” “Nilifikiri unataka kula kwanza?” Naweza kula kwa mkono
mmoja pia.” Tunda akacheka.
Alimuona hata ongea yake imebadilika
yupo kama mjinga. Akamsogelea, akamfungua tu mkanda wa suruali. Tewele akaanza kuhangaika pale kitini.
“Naomba utulie Tewele.” “Nakusaidia
Irene.” “Hapana. Tulia tu ufurahie msamaha wa
usumbufu niliokusababishia asubuhi.”
“Sawa mama.” Tewele akaweka
mikono pembeni kumpisha. Kwa kuwa alikuwa
tayari, Tunda hakumchelewesha. Hata dakika tano hazikuisha, Tewele alishamaliza kila kitu. Tunda akajivuta pembeni. Akachukua chakula kwenye lunch boksi moja, akaanza kula wakati Tewele akijaribu kutulia pembeni.
“Wewe ni mtaalamu Irene. Umewezaje ku..” “Kula chakula, uwahi
kazini.” “Nitakuona wapi tena?” “Nimekupa ruhusa
yakunitafuta week ijayo. Umesahau?” “Umenichanganya mpaka
nimesahau!” Tunda akacheka
taratibu huku akila. Walikula hapo
kwenye gari mpaka wakamaliza. “Kwa kuwa unaelekea posta,
naomba lifti mpaka karibu na ubalozi wa
Ufaransa. Nakwenda Saluni.” “Nitakusogeza na kulipia hizo garama za
saluni.” Tunda
akacheka na kushukuru.
Mpaka anaachana na Tewele, akawa ametengeneza
pesa kwa penzi la harakaharaka tena
garini tu. Na ahadi yakutafutwa juma
lijalo juu. Tunda akawa anacheka yeye
mwenyewe akiwa anatembea taratibu kuvuka
barabara kuelekea sehemu ya Sauna na
masaji. Ilikuwa kesho yake ni kutengeneza
nywele na kucha. Anapumzika tayari kwa
safari ya jumamosi, kwa Mbawala. Bila kutegemea, Tewele naye akawa ameingia
kwenye hilo juma pia, ambapo alipanga awe naye juma lijalo. Akaongeza kipato
cha juma hilo na uhakika wa kutengeneza zaidi juma lijalo watakapoonana tena. Akacheka na kufurahia nafsini mwake.
Aliposhushwa tu, akangia sahemu ambayo wanamfanyia masaji na kuna sauna. Kinny akampigia tena. Kisha akatuma
ujumbe. ‘Huna haja
yakuzungumza chochote Fina. Nisikilize tu, tafadhli.’ Tunda
akasoma ule ujumbe. Akaamua kujibu. ‘Nitakurafuta jumatatu inayokuja.’ Akamjibu tu hivyo. ‘Nashukuru Fina.
Nasubiria simu yako kwa hamu hiyo
jumatatu.’ Kinny akarudisha huo
ujumbe, lakini Tunda hakumjibu tena.
Angalau kukawa kimya. Akaendelea
na maandalizi ya
Dodoma. Kutengeneza mwili. Na muonekano wake.
Ijumaa asubuhi Mbawala akatuma tena pesa bila ujumbe wala kupiga simu. Tunda akajiuliza ndio anamkumbushia au!? “Mbona alishatuma pesa, au kachanganyikiwa?” Tunda akajiuliza ila akafurahia kile alichofanya, kutopiga au kutuma ujumbe. “Huyu anaakili na muelewa. Akiambiwa jambo anashika.” Hilo likamfurahisha Tunda. “Nitatuma jumbe za mapenzi kwa wangapi! Au nitapokea simu za wangapi! Ndio mwanzo wakufungulia mlango matatizo ya ndoa za watu kama kwa baba Tom. Sifanyi mchezo wa kitoto tena.” Tunda akajisemea akiwa anaangalia pesa alizotumiwa na Mbawala. Hapo alishakata tiketi ya ndege iliyokuwa ikiondoka kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere siku ya jumamosi, asubuhi.
Tunda & Mbawala Jr.
Jumamosi ikafika Tunda akiwa amejitayarisha
vilivyo, ili kwenda kukutana na Mbawala
na kutumia hiyo siku ya jumamosi mpaka jumapili
pamoja. Aliondoka jijini Dar akiwa
amewahi tu uwanja wa ndege. Alikaa
kama lisaa ndipo ndege ilipoondoka.
Majira ya saa sita na nusu mchana,
Tunda alikuwa akitoka nje ya uwanja wa
ndege wa Dodoma akiwa na pochi
kubwa kidogo mkono wakulia na
ndogo mkono wa kushoto. Alikuwa
amevaa pensi ya kijani, imefika katikati
ya mapaja. Kiblauzi kilichombana juu kikawa kama amekichomekea mbele. Kilikuwa na maua machache yanayofanana na ile pensi. Kilikuwa
kata mikono. Yaani hakina mikono kabisa. Ila kimezunguka
maziwa tu. Rangi yake ya mwili nyeusi ya
mgongoni, laini na yakuwaka, ilikuwa
mpaka miguuni. Akavaa na sendozi ndefu,
akaweka ile ile cheni yake nzito mguuni.
Huo mguu mpaka mapajani, kulikuwa
kunawaka, kwa kuangalia ni kama mtoto
mchanga. Kucha ndefu, zilizotengenezwa
kwa ustadi, zilikuwa na tips
nyeupe.
Mbawala naye akabaki ameduwaa. Tunda akatabasamu
wakati akimsogelea. “Fina!” “Habari Mbawala!” Tunda akasalimia
akiwa anaweka miwani yake ya jua
kichwani, kwenye nywele ndefu
alizokuwa ameshonea, za mawimbi madogo madogo yakaanguka mpaka katikati ya mgongo, ikafunika kidogo mabega kwa pembeni. Akazirudisha zile nywele zote nyuma na ile miwani
aliyoweka kichwani. Hereni kubwa za muundo wa alumasi, zikaonekana masikioni na kuzidi kuvutia.
“Oooh My!” Mbawala akajikuta anaongea peke yake. “Fina!”
Akarudia tena. “Acha
utundu bwana Mbawala.” “Nilitaka tukapitie sehemu tule
kwanza, halafu..” Tunda akacheka. “Twende.” “Sidhani kama nitaweza
kuendesha.” Tunda akacheka sana. “Twende mimi nikuendeshe.
Halafu tuchukue chakula, tukalie
unapotaka wewe.” “Chumbani
kwangu. Hapana, namaanisha
nyumbani kwangu.” Tunda akacheka
na kutingisha kichwa. “Acha
kuchanganyikiwa bwana! Twende.” Tunda akatangulia, Mbawala akamkimbilia na kumpokea mikoba yote. “Unabeba mpaka pochi! Ni nini lakini Mbawala!” “Acha nibebe mama. Angalau na mimi niguse chochote
chako. Maana siku ile ulinipa busu la shavu, nikashindwa hata kuosha uso.” Tunda alicheka mpaka Akasimama.
“Unavyoonekana na haya
maneno, haviendani hata kidogo!”
“Hali
yangu mbaya, kuliko haya maneno. Ni
hivyo mimi mtoto wa kiume. Nimefundishwa
kujikaza.” “Na mama yako?” “Baba huyo!” Tunda akazidi kucheka
huku anatingisha kichwa. Tunda ndiye aliyekuwa anaendesha. Mbawala anamwangalia. Mapajani na usoni. “Daah!” “Ni nini?”
“Hata nikisema
hutanielewa mama. Acha tu niumie ndani
kwa ndani.” “Toa hayo macho huko ulipoyaweka, angalia barabarani
ili tuweze kuzungumza.” “Unafikiri sijajaribu!?”
Tunda
akazidi kucheka. “Kila nikipeleka
macho mbele, shingo inavutwa. Niangalie
hali yangu.”
“Sasa mimi nina wazo.
Ili usiende kutia aibu huko mbele za watu,
tuanzie kwako. Si ndiko ulikosema tunakwenda?” “Nakushukuru mama yangu, kunizaa mtoto wa kiume mimi!”
Mbawala
akaweka mikono kichwani. Tunda alicheka
mpaka akaweka gari pembeni. “Naomba twende Fina. Hali mbaya. Naweza nikajiabisha hapa.” “Ni nini sasa?” “Nakwambia huwezi kunielewa. Basi niruhusu hata kushika tu. Ndio naona nitatulia mpaka nyumbani. Sifiki mbali. Naweka tu mkono hapo kwenye paja wakati unaendesha.” “Usinogewe tu.” “Najua utanielewa mama.”
“Hapana Mbawala.
Mimi sipakumbuki nyumbani kwako. Lazima uniongoze njia.” “Basi nitaweka nidhamu.
Acha tu mkono utulie hapo kwenye paja, roho itulie.” Tunda akatingisha kichwa, akawasha gari.
“Sasa si niweke?”Akauliza tena Mbawala. Tunda akamwangalia na kurudisha macho barabarani, akatingisha kichwa
kama anayemsikitikia. Akaanza
kukohoa kama amepaliwa huku akikodolea
macho hayo mapaja. “Mapaja yenyewe yanatia mpaka hofu kushika! Unaangalia mikono nakujiuliza kama
ni misafi au la!” “Acha fujo Mbawala.” “Sikutanii Fina. Masafiii,
kwa macho tu yanaonekana laini, halafu! Daah! Acha tu nijikaze nishike.”Akajifuta mara kadhaa kwenye shati lake, kisha akaweka
mkono kwenye paja la Tunda taratibu na
kwa tahadhari kubwa. “Ooooh!” Tunda akamsikia akigugumia. Akageuka kumwangalia, akamuona
amefunga macho, mkono pajani.
Taratibu akaanza kuminya kwa tahadhari kama
anayeogopa. Akaingia mpaka ndani ya geti
la Mbawala. Mlinzi akafungua baada yakuona gari ya mwenye nyumba. Tunda akapitisha gari mpaka pembeni kabisa ya hiyo nyumba. Ukifikiri Dodoma ni pakame, hutaamini ukifika hapo kwa Mbawala. Kijani tupu. Na nyumba yake ilikuwa na miti mifupi mifupi iliyokatwa vizuri. Tunda akasogeza gari mpaka kwenye kona ya hiyo nyumba. Akamfanyia kama alivyomfanyia Kinny. Palepale ndani ya gari. Akalaza kiti chake baada ya kujifungua yeye mkanda na kumfungua na yeye, akaanza utundu wake hapo hapo kwenye gari mpaka akafanikiwa.
Tunda akajua amemaliza, ndio atatulia lakini
wapi. “Naomba tuingie ndani Fina.
Siwezi kutulia mpaka ni, ni..” Tunda akacheka. “Nahisi ni ile tamaa ya
tokea siku ya kwanza nimekuona.
Hebu niangalie. Bado kabisa.
Nisaidie mama, ndio tukale.”
“Twende.” Wakashuka kwa haraka
Tunda akiwa ameacha vitu vyake vyote
ndani ya gari. Ile Mbawala amefungua mlango na Tunda ameingia tu ndani, akamdaka. Hapo hapo sebuleni wala hakufika chumbani au kumvua nguo ya juu, akamng’ang’ania kwa muda, kisha akajitupa kwenye kochi. “Umeridhika sasa?” Tunda akamuuliza taratibu. “Naona tu aibu. Lakini
bado. Ningepata..” Tunda akashangaa nguvu
yakiume aliyonayo Mbawala! Maana mchezo
waliotoka kumaliza hapo haukua mdogo. Na bado alionekana kana kwamba ndio
anaanza!
Alijua angechoka, lakini akamtoa hapo na kumvutia chumbani. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Tunda kukutana na mwanaume mwenye stamina kwa kiasi hicho. Ni kama alikuwa amepagawa. Alivyomshika na jinsi alivyokuwa akifanya mitindo yake tu, Tunda alihisi ameshikwa na mwanaume kweli kweli. Wakati wanahamia
chumbani, alikuwa ameshapata mabao mawili, lakini alikuwa kama anaanza. Walishindwa kutoka siku hiyo. Mpaka anamwachia,
Tunda mwenyewe alikuwa hoi, akaishia kulala, hata hamu ya chakula alikuwa hana. Akajiambia amekutana na kiboko yake. Alilala zaidi ya masaa manne bila hata kujua alipo.
Akahisi mtu
anambusu kwenye kitomvu taratibu huku anachezea ile cheni yake
kiunoni kwa chini. Akafungua macho
taratibu na tabasamu. “Fina wewe ni
mzuri sana. Unavutia hata hapo
kitandani!” Tunda akatoa kicheko cha usingizi.
“Umenifurahisha,
mwepesi!” “Na wewe upo na stamina. Unanguvu!”
Mbawala
akacheka. “Nilikuwa na hali mbaya. Ila sasa
hivi angalau umenituliza akili. Nimeweza hata
kutoka na kwenda kununua chakula!” Tunda akacheka huku
akikaa. “Njaa imenikamata kweli!” “Twende tukale.” Wakatoka hapo kitandani. Baada
ya chakula, Mbawala ambaye hakuwa amepumzika kabisa, akataka waanze tena. Tunda aliyekuwa angalau amechukua mapumziko ya masaa machache, akaendeleza kwa bidii zote kutumika. Kuja kufika saa tano usiku, ndio Mbawala akawa amefika mwisho. Hoi.
Baada ya muda mfupi tu, akaanza kukoroma. Tunda akacheka. Akavuta
simu yake. Akakuta imewekwa password ya finger print. Akamtizama vile alivyolala kama mfu, akamtingisha
kuhakikisha kweli amelala kabisa. Akajiridhisha kuwa amelala kabisa. Akaanza kujaribu kidole kimoja hadi kidole gumba cha mkono wa kulia
ndicho kikaweza kufungu hiyo simu. Tunda alitamani kushangilia kwa sauti. Ni Mbawala! Mtoto wa waziri wa mambo ya nje. Na mfanyakazi wa ofisi za Bunge, Dodoma. Tena yupo ngazi ya juu! Mungu ampe nini Tunda! Alichofanya, ni kucopy na kupaste conctact list yoote ya Mbawala.
“Hawezi akawa na mawasiliano ya watu wajinga
wajinga.”
Tunda akawaza huku akiendelea kuiba
namba za simu. “Kwanza alivyo jeuri na dharau huyu, lazima kila mtu hapa, ananufaika naye.”
Tunda
akaendelea kuwaza huku akihamisha zile
namba huku akiomba Mungu, Mbawala
asije kuamka kabla hajamaliza. Alikutana na majina ya mawaziri humo, wabunge, manaibu
wao. Akawa anacheka tu kama aliyekabidhiwa ulimwengu mzima. “Dad!” Tunda
akatulia alipofika hapo kwenye hiyo
namba ya simu. Akabaki ameduaa.
Akacheka baada ya wazo kupita na kulikubali. “Oooh
my Tunda! Nakula dad na mwana!”
Akacheka huku akimtizama Mbawala mdogo
jinsi alivyolala pale. “Lazima nile pesa ya Mbawala mwenyewe pia. Wasiniletee mchezo. Pesa yao haina kazi hawa.”
Tunda
akacheka peke yake. “Ngoja na yeye nikamuonje kama ana nguvu kama za mwanae au uzee tayari!”Akaanza kumfikiria baba yake Mbawala. Akavuta taswira yake akaanza kumfikiria. “Nampataje?” Ndio likawa swali kwa
Tunda. Akaona aendelee kuiba zile namba
zote za simu mpaka amalize, mengine atakwenda kufikiria akiwa nyumbani kwake.
Mbawala alikuja kuamka asubuhi. Tunda
alikuwa amejilaza akimwangalia. Akacheka. “Nakoroma nini?”Akamuuliza Tunda. “Kidogo tu.” Tunda akajibu huku akicheka. Mbawala na yeye akacheka. “Daah! Samahani. Nilicheza kwa puma jana, nikalala hoi! Nisamehe kama
nimekulaza macho.” “Wala usijali. Nipo tu sawa.”
“Acha basi kuniangalia
hivyo Fina, unanifanya nizidi kuona
aibu.” Tunda akacheka sana.
“Lakini kukoroma ni kitu cha
kawaida sana.”
Tunda
akamfariji, lakini ni kweli hakulala.
Tunda hakuwa akipenda kabisa mtu anayekoroma. Kwanza hakuwa akiweza hata kupata usingizi. Akajifariji
atalala akifika nyumbani kwake. Akabaki
pale akimtizama jinsi anavyokoroma huku
akihesabu dakika, muda wake uuishe
aondoke. Walitumia hiyo siku hapo
ndani, mpaka mchana alipokuwa anarudi
Dar.
“Naomba urudi Fina.” Tunda akacheka. “Naomba isiwe juma hili linaloanza au lijalo. Nipo na mambo mengi
sana. Ila kuanzia ile nyingine, naweza
hata kupata kijinafasi.” “Mimi naweza kuja Dar. Tukapata hata siku moja kama hii. Au hata usiku mmoja tu. Lakini
usiniweke nikisubiri kwa majuma matatu! Huko mbali Fina, mama.” Tunda alijua ameshakolea. Akamuweka mteja wa kwanza kwenye orodha ya watakao muweka mjini. Alishamkabidhi bahasha yake ya pesa na yenye nyaraka za Kinny, akarudi jijini
akiwa amefunga juma vizuri na kipato cha
kueleweka.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Juma likaanza likiwa na ahadi ya kuingiziwa pesa
na Kinny kwa kumfanikishia tenda na
Tewele aliyechanganywa na penzi la garini. Tewele na yeye alitaka
kumuweka karibu kama Mbawala. Ila Kinny hakutaka
muendelezo naye kabisa. Alipanga amalizane naye kwa kumpa ile bahasha aliyopewa na Mbawala, waachane baada ya kumlipa pesa yake, iwe basi. Kwa uchovu wa kutolala usiku wa jumamosi kuamkia jumapili huku Mbawala akiwa anampa mchezo wa nguvu, Tunda alikuwa hoi. Palipambazuka, akakaanga mayai mawili na glasi ya maziwa. Akala kisha akarudi kulala. Alilala mpaka saa kumi jioni.
Ujumbe kutoka kwa Kinny ukamtoa usingizini. Akachukia
kutozima simu. Akasoma. ‘Leo jumatatu Fina. Nakukumbushia tu.’ Akaka na
kuangalia muda. Akajibu. ‘Nitakupigia baada ya kama dakika 20 hivi kuanzia sasa. Nina
majibu ya kazi yako.’ Akajibu
hivyo na kwenda kuoga. Akatoka akiwa
amechangamka. Akakuta Kinny amerudisha
ujumbe. Alijua siku moja aliyokuwa naye
pale hotelini, amechanganyikiwa,
anataka tena. Lakini alishamkera
Tunda. Akaamua kumpigia. “Ulisoma ujumbe wangu
wa mwisho?” Tunda akaanza kwa
hilo swali. “Fina! Tafadhali nielewe. Nia yakukutafuta muda wote sio kazi. Ni kuwekana sawa mimi na wewe. Natafuta
amani.” “Amani mbona ipo! Usiwe na wasiwasi. Mimi sina mambo ya ajabu. Namsoma
mtu na kumuelewa kwa haraka sana. Kuanzia hapa
tutaendelea vizuri tu. Hapatakuwa na migongano tena.” Tunda akazidi kumuumiza. “Daah! Nahisi
mimi utakuwa umenisoma vibaya. Mimi sio
mnyanyasaji.” Tunda akanyamaza.
“Fina?”“Hamna shida
Kinny. Nimekamilisha kazi yako. Naomba
tukutane, nikukabidhi.” “Unamaanisha ile kazi ya Dodoma!?” “Ndiyo.”
Kinny akawa
kama hajaelewa. Alitegemea kutafutwa
yeye binafsi na Mbawala. “Unamaanisha ile tenda ya
bunge!?” “Labda tukionana, utaelewa zaidi. Nina
nafasi jioni hii. Kati ya saa 11:30 mpaka 6:30.
Tunaweza kukutana pale pale Mlimani City. Nitakuwa nikikusubiria ndani kwenye mgahawa wa..” Tunda akamuelekeza, wakaagana kuwa wakutane saa 6 kamili jioni hiyo. Kinny alijua Tunda
ameshamtoa umaana. Hapakuwa na kicheko
tena wala kukutana usiku au kwenye
gari yake. Mazungumzo ni nje hadharani. Hakuna faragha tena.
I |
lipokaribia
muda wa kukutana, Tunda akaita Uber, mtu
akaja Ikumchukua na
kumpeleka mapaka Mlimani City. Alikusudia kumuumiza Kinny. Alitaka
humuonyesha hata kama alimuona akiwa
uchi, akapata penzi, bado uthamani upo
na atakosa mengi. Safari hii alivaa
gauni refu mpaka chini. Lilikuwa kama la
mpira tu. Lilimshika kila mahali. Kola
yake ilikuwa imemwagika ikatengeneza
duara kwa nyuma na cheni ikapita kutoka
bega moja kwenda jingine kushikilia ile pindo
ya kola. Ilikuwa ya rangi ya kijani
kibichi ikachanganywa na pink. Alivaa
hereni bila cheni. Kiatu cha juu cha
pink kama moja ya duara lililopo
pembeni ya hips moja. Ile nywele ya
mawimbi, akaibana pembeni na kuacha
chache zimeanguka kwenye kipanda uso.
Ni kweli
Tunda alipendeza. Ungeweza sema ni mwana
mitindo wa Holywood. Kwa kuwa alikuwa na
vidole virefu, alipanga pete mbili mbili
kwenye vidole viwili vya kila mkono. Na kucha alizokuwa nazo, ungependa. Alishika pochi nzuri inayoendana na kiatu chake, akashika na file lililokuwa na nyaraka za Kinny. Ungesema msemaji wa ofisi ya raisi. Alitembea taratibu bila haraka mpaka kwenye ule mgahawa. Akamkuta Kinny akimsubiria nje. Akabaki ameduaa. “Habari yako Kinny?” Tunda akaanza
kwa sauti tulivu. Lakini yakikazi. “Umependeza sana Tunda.” “Asante. Tunaweza
kuingia ndani? Nataka kuagiza chakula.
Njaa inauma.” Bila kusubiria
jibu, akatangulia ndani, Kinny akabaki
amekodolea mgongo. Kiuno, sehemu
ya juu ilipoachwa wazi na nywele
kuwekwa pembeni kama aliyekusudia
kuonyesha ule mgongo, chini ya hicho
kiuno jinsi kulivyobanwa vizuri na
umbile la chini lilivyopendeza kwenye
hilo gauni, Kinny akabaki ameduaa
pale mlangoni.
Baada yakukaa,
Kinny naye akamfuata. Muhudumu akaja, Tunda akaagiza juisi ya embe na chakula. Kinny akaomba na yeye juisi ya embe tu. “Hili faili ni lako Kinny. Kila kitu kimekamilika. Na zipo namba za simu za msaidizi wa Mbawala. Amesema kama utakuwa na swali lolote, umpigie yeye huyo msaidizi wake ili kuwekana sawa. Ila kila kitu kipo hapo. Nashauri pata muda wa kupitia taratibu.” Kinny alibaki amekodoa
macho. Hakutegemea kusikia hivyo.
Mbawala anamtuma Fina/Tunda kwake? Tena na kumuelekeza kwa msaidizi wake! Kiroho kikamuuma kidogo Kinny. “Wamekutana wapi mpaka kumpa yote haya? Kwa nini asinitafute mimi mwenyewe?” Kinny akawaza huku akiumia.
Tunda akamsogezea tena karibu lile kabrasha. Akashtuka kidogo. “Daah! Siamini bwana. Kama utani umekamilisha hii dili!” “Hongera. Nimeipitia na
mimi, inaonekana ni kweli ni kazi kubwa umeipata.
Mambo yako yatakuwa safi.” Akaongeza Tunda taratibu, asijue maumivu ya Kinny. “Nilijua baada ya pale,
angenitumia mimi mwenyewe au hata kunitumia haya yote kwenye email yangu!”Akajikuta anaropoka kile kilichojaza moyo wake kwa kulalamika. Tunda hakujibu kitu. Akanyamaza
kimya. “Lakini hata hivi ni sawa tu,
nakushukuru sana.” Akajirudi kwa haraka. Juisi ikawa imeletwa, Tunda akachukua yake na kuanza
kuinywa taratibu tu.
Ungependa vile Tunda alivyoshika hiyo glasi na hivyo vidole. Akamuona anavuta pumzi kwa nguvu, akamwangalia.
“Na kuhusu sisi?” Tunda akakunja
uso taratibu. “Namaanisha mahusiano yetu.” “Nafikiri nilikueleza tukiwa Dodoma, Kinny. Au
unamaanisha nini?” “Lakini nimeomba msamaha Fina.” “Mbona nimekwambia
hakuna neno kabisa! Naomba uwe na amani
Kinny. Tushukuru Mungu kazi
uliyoniamini nayo nimeikamilisha.
Furahia wewe na mkeo.” Kinny akazidi kuishiwa nguvu.
“Basi naomba nikurudishie ile pesa uliyonirudishia
tulipokuwa hotelini Dodoma.” Tunda
akakunja uso. “Kwa nini!?” “Nahesabu ni
kama umeniziria.”
“Hata
kidogo. Basi labda kukupa amani, hesabu
hivi, mahusiano yetu ni ya kikazi.
Uliniazima nauli kwenda Dodoma kufanya
kazi. Nilifanya kazi yangu,
umeshanilipa kwa mara ya kwanza, unanimalizia
kwa kukubali kuwa garama za kazi yote
ilikuwa juu yangu isipokuwa malazi ya
siku moja. Wewe bosi wangu au kampuni
ya Kinny ndio
imegaramia. Basi. Rahisi kama hivyo.
Tunaachana kwa amani. Ukiwa na
kazi nyingine unayotaka nikufanyie,
nitafute. Rahisi hivyo na kuweka
tofauti zetu kando.” “Sasa hizo tofauti ndizo nataka tuzimalize.”
Kinny akaendelea.
“Tafadhali nisamehe Fina. Umekuwa mtu
mwema sana kwangu.
Umenifanyia jambo kubwa sana, ni
vile hufahamu tu. Hiyo tenda itabadili
maisha yangu na familia yangu. Kama
ulivyoona mwenyewe, inalipa pesa
nzuri tu. Nitapata nafasi ya kuwa na
watoto wangu hapa nchini. Yote ni
wewe umesaidia. Mbawala
alishanikatalia, akawa ananikwepa. Nisingependa unifanikishie hivi,
halafu nikageuka kukuumiza. Yani unaleta
mafanikio kwa garama ya kuumia!
Hapana Fina. Naomba nisamehe.
Tafadhali. Ulinipa wakati mzuri sana ambao nilihitaji kwa muda
mrefu. Nilikufurahia na nimependa
utulivu wako na natamani tuendelee kuwa pamoja.” Tunda akacheka kidogo na kuinama kama anayefikiria.
“Naomba niwe mkweli kwako Kinny.” “Karibu.”
Kinny
akajiweka sawa. “Wewe ni mume wa mtu na
baba wa watoto wawili. Hakuna namna yakuweka tofauti zako na zangu sawa. Hatuwezi kufikia sehemu tukawa ukurasa mmoja
kwa kuwa wewe ni mpitaji tu kwenye
maisha yangu. Na nasikitika kwenye huo
upande mwingine ilitokea nikaumia. Nahisi sio
wewe uliyeniumiza moja kwa moja ila
umenikumbusha tu mambo ya nyuma.
Na kwa kuwa muungwana ili tuachane
salama, naweza kusema hukukusudia.
Nina vidonda vyangu ambavyo
havijapona, na wewe ukatokea
ukakanyaga huko huko vilipo,
umenitonesha.” “Daah!” Kinny akasikika akisikitika.
“Kufupisha tu stori ndefu na tumalizane hapa ili
kila mtu aendelee na shuguli zake,
naomba rejea mazungumzo yetu
au kile nilichokwambia Dodoma. Tubakie kwenye maswala ya kikazi tu. Ukiona ipo
kazi unataka nikufanyie,
tukafikiana bei.” Hapo Tunda
akacheka kidogo, kuweka msisitizo na kumkumbusha anamdai. “Tafadhali usisite kunitafuta.
Lakini si haya mahusiano ya mapenzi ya
wizi. Mkeo anakuja, naamini utakuwa sawa
tu.” Chakula kikaja, Tunda akainamia
sahani yake. Kwa kumtizama tu,
alikuwa ameumia mpaka usoni. Ujanja wote
ulimwisha Kinny mtoto wa jiji.
Kukataliwa kubaya! Haswa na mrembo
kama Tunda ambaye alishamuonjesha penzi ambalo
alitaka kuliendeleza kwa wizi.
“Huyu ni Mbawala tu.” Kinny aliwaza akiwa mbele ya Tunda aliyekuwa anakula chakula kwa madaha. “Na watakuwa
wamekwenda kuonana tena Dodoma.
Jamaa amenipora mwanamke
wangu.”
Akachukia Kinny. “Chakula cha hapa
ni kizuri sana! Umeshawahi kula hapa?” Tunda akavunja ukimya. “Mara moja nafikiri. Wanampishi mzuri.”
Kinny akajibu, Tunda akaendelea kula. Vipande vidogo mdomoni, kutafuna taratibu kama hataki. “Nimeumia sana Fina.” Tunda akanyanyua uso kumtizama, hakujibu kitu. “Naomba leo nikulipe kwa
hundi. Sikuja na pesa yeyote, kwa
kuwa sikutegemea kama Mbawala atakutafuta
wewe na mkamalizana naye. Nilikuwa
nikisubiria mawasiliano yake kwa barua pepe. Nilipanga kuwa nikishapokea
ndipo nikutafute, nikulipe.” “Hamna neno.” Akajibu hivyo tu, Tunda
akarudi kuinamia sahani yake. Alijua fika Kinny ameumia kwa Mbawala kutomtafuta yeye na
kumsukumia kwa msaidizi wake. Ni kama
amemdharau. Tunda akaendelea kula.
Kinny akatoa hundi. Akaandika kiasi cha pesa kwa
malipo na kuweka saini. Jina akaacha
wazi, kitu kilichomfurahisha Tunda. “Nashukuru sana Fina. Naamini hiki kiasi ni sawa.” Bila
kuangalia, Tunda akashukuru. Kinny akamtizama kwa muda na kuondoka. Ndipo Tunda akavuta ile
hundi, akasoma na kucheka. “Bingooo!”
Akajipongeza moyoni akaendelea kula.
Tunda akajiangalia vile
alivyopendeza, amelala mchana! “Siwezi
kurudi nyumbani. Heri hata
nikangalie movie.” Akaendelea kula
taratibu huku akifikiria.
Tewele!
A |
lipokuwa akila simu kutoka kwa Tewele ikaingia. Tunda akacheka. “Upo?” Tunda akaanza. “Tokea uniache siku ile, nimekaa nakufikiria tu.” Tunda akacheka taratibu. “Unanifikiria kwa mema au mabaya?” “Natamani unishike tena Irene. Na hivi unatumia muda mfupi, nisaidie mama. Angalau unitulize. Sitakuweka sana.” “Mmmh!” Tunda akajidai kufikiria. Lakini alimpenda Tewele. Alikuwa anatimiza haja zake haraka sana, sio kama Mbawala. “Tafadhali Irene. Angalau akili itulie.” “Uko wapi na ulitaka tukutane wapi?” “Popote unapotaka wewe. Nitakulipia pesa ya usafiri.” "Basi tukutane pale pale kwa siku ile. Ila leo ujiandae.”Akamsikia anacheka.
“Nitakaa na wewe mpaka uridhike.” “Asante mama. Basi utanikuta hapo. Si unasogea sasa hivi?”
Akauliza Tewele. “Unajua mimi sipendi kuwekwa. Kwa hiyo uniambie tunakutana
baada ya muda gani?” “Mimi ndio natoka hapa ofisini.”
“Basi na mimi natafuta usafiri, nakuja. Lakini nafikiri ili wasijue tunapokwenda, nichukue nje ya Kanisa la
St.Peters. Nitamwambia anishushe pale.” Wakakubaliana
upande atakaokuwepo. Wakaagana.
Tunda akafurahi kupendeza kwake sio
bure. Akatoka hapo akiwa ameshiba, swafi, tayari kwa kazi.
Alipofika
pale walipokubaliana, akamkuta ameegesha gari anamsubiria. Tunda akacheka. “Kiu gani hii!”
Akajiuliza wakati anatembea taratibu
akimfuata. Akampigia simu. “Toka sasa kwenye
gari unipokee.”
Tewele akacheka. Nia ili amuone jinsi alivyopendeza. Akamuona kwa mbali anashuka. Tunda akakata simu huku akimfuata. Akamsogelea. “Umependeza. Geuka.” Akamtaka ageuke. “Mmmh!” Akamsikia akiguna wakati
anageuka taratibu mbele yake. Tunda
akacheka. “Leo Irene nipe kila kitu,
sio nusunusu.” “Ni wewe tu na muda wako. Usiku huu wote nakupa wewe.” Akastuka. “Sasa kama ni hivyo, kwa
nini tusitafute sehemu?”
“Sawa.”
Tunda akakubali bila kumzungusha.
“Basi tuongozane mpaka pale Moroco. Mimi nitachukua taksii mpaka
kwenye hoteli.” Tunda akamuelekeza sehemu ilipo hiyo hoteli ambayo alijua ipo salama kwao, kisha akaendelea. “Nitachukua chumba, halafu nitakwambia ni wapi nilipo, uje moja
kwa moja, usipite mapokezi
ukaonekana na watu
wanaokufahamu.” “Hapo utakuwa
umenisaidia mama.” Wakaingia ndani
ya gari.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Samahani bwana. Ilibidi tu kupokea. Huyu ni Mkurugenzi wetu. Msumbufu sana. Tunamwita mkoloni. Jeuri na majivuno kweli. Anataka anachoengea yeye ndio kiwe hivyo hivyo. Hashauriki.” “Pole. Anaitwa nani?” “Mihayo. Jamaa amesoma. Na..”
Kadiri alivyokuwa akimuelezea, Tunda
akajua lazima ni yeye tu. Akili
ilishavurugika. Chuki ikaibuka kali
sana. Akakumbuka vile alivyomuharibu sura yake. Tewele aliendelea
kuongea akimlalamikia kwa hili na lile, Tunda
kimya.
Wakafanya kama walivyokubaliana. Tunda akapata chumba kilichojificha, ndipo akampigia simu Tewele afike hapo. Alikuwa amemuacha kituo cha Moroco. Baada ya muda akafika hapo. Akaingia mpaka hapo chumbani.
“Acha nitumie choo kwanza.” “Huwezi kwenda na suruali
bwana. Njoo nikuvue.” Tewele akacheka huku akimsogelea, asijue nia ya Tunda. Aliona simu ipo mfuko wa nyuma wa suruali yake. Akamtoa ile suruali na chipu, kwa madaha yote huku akimpapasa,
Tewele akifurahia kushikwa na binti huyo mdogo, mrembo wa kuvutia. “Uwahi
huko chooni, maana ushanichanganya!” Tewele akakimbilia chooni huku anacheka. Bila kupoteza
muda, akaingia kwenye simu ya Teweele
kwa haraka sana. Moja kwa moja
kwenye namba ya mwisho iliyoingia. ‘Mihayo.’ Ilikuwa imeandikwa hivyo. “Ewaah!” Akafurahi kuipata ile namba
kwa haraka. Kwa kuokoa muda asije akakamatwa, akajitumia ile namba kwa ujumbe,
kwa kutumia simu ileile ya Tewele, kisha akafuta ule ujumbe aliojitumia namba.
Ile anamaliza tu, Tewele naye anatoka
chooni. Tunda akaruka kwa
haraka kama anayekwenda kumuwahi kumpokea kwa mahaba, kumbe ni mshtuko wa kukamatwa,
na simu akarusha pembeni. Uzuri aliitupia palepale kwenye kochi. Tewele hakuwa ameelewa alijua mambo ya mahaba.
Kwa kupaniki, Tunda alimfanyia mengi ambayo hata hakukusudia. Tewele alikuwa akigugumia na kufurahia kila kitu. Tunda alimzungusha hapo chumbani, uzuri Tewele mwenyewe hakuwa akiweza mengi. Mwili mkubwa, umri ulishaenda, basi, hata kabla ya lisaa kuisha akawa hoi. Amemaliza. “Utaniua Irene.” Tunda akacheka. “Tatizo ni lako. Mtamu, halafu unanukia vizuri.” “Pafyume ya paris hiyo.” “Ukienda uniletee na mimi.”
“Au
twende wote?” Tunda akaa kwa
haraka.
“Ufaransa?”
“Sasa je!
Fikiria kupata usiku kama huu kwa
uhuru. Mbali na
macho ya watu wanaotuwinda!
Tunakula vitu vyetu kwa nafasi bila
haraka, tena kwa kituo!” Tunda akacheka, asiamini. “Wewe andaa safari twende nikakubembeleze huko.” Tewele akacheka. “Sio sasa siku ifike,
unipe sababu?” “Ni lini?” “Aaah! Tatizo ni Mihayo. Anabana
kweli! Hali haikuwa hivi. Sasa hivi
anaogopa kutoa safari. Anasema viongozi
wote macho yapo bandari. Basi hakuna
safari. Ila ipo moja hiyo, nafikiri
ataiidhinisha tu. Ngoja tuendelee
kumlamba.” Tunda akazidi kumchukia mume wa shangazi yake.
Akafikiria kwa haraka. “Sasa na wewe lazima ujue kula na vipofu.” “Sio yule.”Akabisha Tewele. “Hakuna mtu asiyenunulika.
Kila mtu anao udhaifu wake Tewele.
Unatakiwa kuufahamu wake ndio uutumie.” “Mmmh!” Akaguna kama
anayemfikiria Mihayo. “Nakwambia ukweli.”
“Sio yule jamaa. Nakwambia ni mkoloni.” “Aliyekwambia
wakoloni hawanunuliki ni nani?”
“Kwa
njia gani?”Akauliza Tewele. “Kwanza lazima ujue ni
nini anapenda. Anakunywa wapi na
rafiki zake! Siku gani? Wewe unaweza kuingiaje
kwenye kundi lao la marafiki! Kisha na
wewe unajiwekea muda wa kwenda hapo
kunywa na unahakikisha wanakuona kama na
wewe upo hapo kwenye maeneo yao.
Usijikaribishe kwenye meza yao kwa
haraka au pupa mpaka wao wenyewe wa kukaribishe, huku ukichunguza aina
gani ya mazungumzo
wanazungumza. Kama ni michezo,
michezo gani! Mpira wa miguu, tenesi,
golf, ni nini! Wasomi na matajiri huwa
wanaunganishwa na vitu fulani ndio
maana wanaweza kuchukuliana.
Hawazungumzi kila kitu. Sasa kazi
yako kubwa ni kujua ni nini anapenda
na kinamfurahisha.” Tunda akaendelea.
“Basi na wewe unapata
nafasi ya kuwasoma taratibu. Jipitishe.
Hakikisha wanakutambua kuwa na wewe upo pale kwenye viwanja vya hadhi
yao, wasalimie na kuwapa ofa tu. Usikae.
Kumuonyesha upo, na mazingira anayofika
yeye na wewe upo. Na sio wakati wote
unamlilia shida. Muonyeshe unao uwezo. Heshima unayompa kazini sio kwa sababu ya dhiki, ni nidhamu ya kazi tu. Watu kama hao wana kiburi. Akishakuona hivyo na wala hukimbilii kwenye meza yao kutaka kukaa nao kama limbukeni, na upo sawa nao kwenye maisha, taratibu utajikuta unakaribishwa kwenye meza zao.” Tunda
akaendelea.
“Na ukishakaribishwa mara
moja kwenye meza yao, sio sasa
unazidisha pombe na kuongea kila kitu au
mambo wanayopinga wao, au kumzungumzia kiongozi fulani ambaye wao hawampendi mpaka uwakere! Hapana. Hapo tena ndio unakuwa mstaarabu na kumuonyesha unafahamu mambo
wanayoyapenda kama wao.” “Kama wanapenda kitu ambacho mimi sina hata ufahamu nacho?” Tewele
akauliza. “We Tewele!?”
Tunda
akavuta shuka akakaa huku amejifunika na
mshangao usoni. “Karine hii unauliza
unajuaje mambo! Kila kitu kipo
mtandaoni. Ndio maana nilikwambia
chunguza wanachopenda. Ukishakijua na
wewe kifanyie kazi. Hakikisha kama
ni mchezo unajua wachezaji wa mpaka wa kimataifa. Mjini hapa, unakula na watu kwa akili. Na ninakuhakikishia Tewele, ukiweza kuwepo kwenye meza yao, ukaongea mambo ya maana. Sio kujiliza shida. Ukafanikiwa kuongeza uthamani wako nje ya mambo ya kazi, tena kirafiki, hata ofisini atakuangalia kwa jicho la karibu.” Tewele akaonekana kufurahia hilo wazo, asijue Tunda
anaongea kwa jinsi anavyomfahamu huyo
mjomba wake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alishaishi naye, anamjua yeye na wanaomzunguka. Ile haiba yao ya kiburi na dharau kwa wengine wanao waona hawajafikia daraja lao. Aliwaona wakiwa wanakuja nyumbani kwake. Aina ya watu anaoweza kuwakaribisha au hata kuzungumza nao. Wote walikuwa wasomi sana. Watu
wa viwango vya
juu. Walioelimika na wenye
nyadhifa za juu. Tunda hakuwahi kuona
mtu wa hali ya kawaida, wala si chini,
wa kawaida tu, kufika pale kwa
shangazi yao. Kila aliyekaribishwa
pale, alikuwa na sifa fulani tena za
juu. Na ndivyo ilivyokuwa hata kwa binti
zao. Hawakuwa na marafiki wengi. Na mara nyingi aliwasikia wakilalamikia watu kuwa wanaongea vitu vya ajabu. Mazungumzo ya kijinga.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ule ushauri ukamwingia Tewele, na yeye akakaa “Hiyo akili.” “Jua sasa anapokunywa na wenzake.”
“Tena nasikia
wenzake watu wa totozi kweli.”
“Na yeye?”
Tunda akauliza akitaka kujua ya sirini. “Yeye simba
mwenda pole. Nasikia yupo makini
sana. Alishakuwa na mahusiano na mfanyakazi mmoja hivi, pale pale bandari. Walikuwa wasiri sana. Yaani mtu wa karibu wa yule dada ndio alikuja kutuambia, tena baadaye baada ya yule dada kuacha kazi pale. Lakini kwa kuwa watu wanamuogopa, ikaishia chini chini. Hakuna aliyejua kilichoendelea
baada ya yule dada kuondoka pale. Na aliondoka bila hata kuaga au kusema ni kwa nini anaacha kazi, wakati alikuwa msichana mdogo tu, halafu mzuri kweli! Tukashangaa anawezaje
kuacha kazi bandari! Lakini hakuna
aliyeuliza, sababu ya hofu. Hata huyo
dada aliyesema alikujaga kukanusha.
Nafikiri kwa hofu pia. Lakini nasikia ni
kweli.” Tunda akafurahi sana kupata hizo
habari.
“Si umeona? Hakuna asiye
na udhaifu?”
“Kweli
bwana.”Akakubali
Tewele. “Wapi anapokunywa na wenzake?” “Nasikia Lidazi.”
“Basi. Kumbe
umeshajua. Na kinywaji gani anapendelea?” “Hapo ndio sijui.” Yeye Tunda alijua.
Lakini mwiko kuropoka. “Hilo sio tatizo.
Jipitishe pitishe. Jenga mahusiano ya
zaidi. Na weka deni ambalo hatasahau
kulipa fadhila. Au hata fanya nyama
choma na wewe Tewele!” “Wapi sasa?” Tewele akauliza. “Si nyumbani kwako! Tafuta tu weekend moja, mkaribishe yeye na
mkewe na mtu mwingine muhimu. Sio walevi
unaojua sio wastaarabu. Mkaribishe
mapema kama hata week mbili kabla ya
siku unayotaka wafike kwako. Mtajie
mtu mkubwa wa sehemu fulani ambaye naye atakuwepo. Ataona umuhimu wa kuja. Halafu kwa mwanzoni, muwe tu wachache. Andaa mazingira mazuri na ya heshima. Na yeye atapata deni la kuja kukukaribisha siku moja. Na kazini sio tena kila ukimuona au ukiingia ofisini kwake unamkumbushia safari za kikazi!” Tewele akacheka.
“Kweli tena. Jipitishe au
hata ukimkuta sehemu rusha tu neno.
Mpe matokeo ya mpira ya siku
iliyopita. Kama anapenda mpira lakini.” Tunda alimjua mjomba wake mlevi wa mpira wa mguu. Alijua anachomshauri. “Na hapo sasa
sio tena na wewe uanze kujisahau na
kujigeuza kama ndio wewe mtangazaji wa hiyo
mechi wakati mpo kazini! Unaongea kuanzia kona walizopiga, makosa waliyofanya uwanjani,
yooote wakati ni muda wa kazi! Hapana
bwana.” Tewele akacheka sana.
“Kidogo tu, unapita kama
ndio salamu. Acha kujitetemesha
hovyo. Ndio maana anakuweka kwenye
kundi la wajinga wajinga. Na taratibu. Jiwekee kuwa ni malengo ya muda mrefu. Sio kila kitu kwa mara moja. Atakushtukia. Usipompata yeye kwa haraka, basi rafiki zake.” Tewele akafurahia
sana hilo wazo.
Akaonekana kuchangamka kweli
kweli. Tunda akawa anacheka.
Tewele aliondoka, akamuacha Tunda hapo chumbani na pesa nzuri tu japo sio nyingi sana. Lakini Tunda akajiambia hata hivyo hakutumia nguvu nyingi, inatosha. Aliwahi kuondoka,
akasema anawahi nyumbani. Tunda akabaki akimfikiria mjomba wake akiwa amejilaza palepale chumbani. “Mihayo!” Akawaza. “Hakika atalipa. Nitamlipa
kisasi, yeye na familia yake watajuta.” Tunda akaendelea kuwaza
wakati akiingalia ile namba yake ya
simu. “Hakika na mkewe atajuta
kila unyama alionitendea.
Nitahakikisha na yeye anaumia.” Roho ya chuki ikamwingia Tunda.
Akakumbuka
mahusiano ya wizi Tewele aliyoambiwa
alikuwa nayo huko kazini. “Kumbe na yeye yumo!” Akacheka vile
alivyo nyumbani, akijionyesha
baba mwenye maadili, “kumbe hovyoo!”
Tunda akafyoza kabisa akiwa amemdharau
kutoka moyoni na kudhamiria kuwalipa vibaya sana.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Nini Tunda
atafanya kwa familia ya Shangazi yake? Mikasa ipi inamsubiria mbeleni? Ameshapata
namba ya waziri Mbawala mwenyewe. Je, atamtafuta baba mtu baada ya kula kichwa
ya mtoto? Usikose muendelezo.
0 Comments:
Post a Comment