T |
unda
hakutembea hatua nyingi kutoka kwenye gari ya Kinny, simu yake ikaanza kuita. Akapokea. “Kesho
nina safari ya Dodoma. Naondoka na ndege ya mchana. Ni safari ya kibiashara. Naomba nisindikize.”
Tunda akacheka. “Acha kunicheka Fina!” “Unataka nikusindikize?” “Tafadhali sana.” “Saa ngapi?” “Naweza kukufuata kwako mchana wa saa sita.” “Hapana. Tukutane hapahapa.
Tena muda huo ndio nitakuwa nimemaliza
na mimi shuguli zangu.” “Sawa
Fina. Usinidanganye tafadhali. Ujue nakata tiketi ya watu wawili.” Kinny akabembeleza. “Siwezi kukupa
ahadi ya uongo.” “Basi nitafurahi nikikuona tena.” “Tunakaa siku ngapi?”Akauliza Tunda huku akitembea kutoka kwenye eneo hilo la Mlimani city. “Siku mbili, ya tatu tunarudi.
Nakutana na jamaa mmoja wa pale bungeni,
kisha tukifanikiwa, tunapumzika siku
moja, inayofuata tunarudi.” “Sawa.” Tunda alitamani kuruka juu kwa furaha. Hakutegemea kumpata Kinny kiurahisi hivyo.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alishushwa na taksii nje ya geti usiku huo, akaingia na kusalimiana na mlinzi aliyemkuta siku hiyo nyumbani kwake. Kampuni hiyo ya ulinzi ilikuwa ikibadilisha walinzi mara kwa mara ili mlinzi mmoja asije kufanya njama za kuiba kwa wateja wao. Akaingia ndani akiwa amejawa furaha. Moja kwa moja
kwenye chumba chake
chakuvalia, akaanza kujiandaa na
safari ya kwenda kumwingiza Kinny
kwenye mtego awe Sadiki.
Akaanza
kutafuta nguo zakuvaa kwa siku hizo
tatu ambazo watakuwa Dodoma.
Akaweka mbili zaidi kama akiba.
Kuanzia chupi mpaka nguo za kulalia,
alibeba mitego mitupu. Akawa anacheka mwenyewe huku akipanga mahesabu yake. Akaweka na viatu vya maana vinavyoendana na hizo nguo. Aliporidhika, ndipo akaenda chumbani kwake sasa.
Akiwa chumbani kwake akijiandaa kulala, akaanza kuwaza jinsi ya kufanya na ile gia aliyoingilia kwa Kinny,
yakumuuzia vinywaji. Tunda hakuwa na mtu yeyote
anayemfahamu ambaye anauza bia. Ule ulikuwa uongo kwa Kinny baada
yakubadili wazo la kuomba kazi pale
kwenye Club ya Kinny. Lakini hakuwa
akijua chochote juu ya bia. Alikuwa
akiona tu bia zikishushwa kwenye baa za
Sadiki. Hakuwa akiuliza wala kutaka
kujua zinapotoka na kwa bei gani! Sasa
anamalizaje hilo bila kuharibu mahusiano!
Ndilo likawa swali usiku huo. “Lazima
kutumia akili ya ziada.” Tunda
akawaza huku akicheka
na kujipongeza kuwa na akili ya
haraka yakufikiria.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Asubuhi
kabla ya safari ya Dodoma, Tunda aliamka
akabaki amejilaza kitandani
kwake. Wazo likamjia, lililomfanya
ajipongeze. Akacheka sana akiwa peke
yake. Akaanza kujiandaa sasa na safari
akiwa akili imetulia na anajua kitu chakufanya. Alijitengeneza
vizuri ndipo akatoka kurudi Mlimani
city ambapo walikubaliana na Kinny wakutane
hapo. Kabla dereva hajamwingiza ndani
kabisa pale Mlimani City, akamwambia
amsogeze kituo cha daladala, kisha
amsubirie mbele kidogo. Akafanya hivyo,
Tunda akashuka. Vijana waliokuwa wamesimama pale kituoni wote wakamgeukia. Wakabaki wamekodoa macho wakimwangalia kadiri
alipokuwa akiwasogelea taratibu. Hata
yeye mwenyewe Tunda
alijua amependeza.
“Samahani.” Akamwambia mmoja wao aliyeonekena amechangamka kidogo.
Akamuomba wasogee pembeni ili
wazungumze. Kaitwa na mrembo waliyekuwa
wote wamempokea kwa macho ya uchu tokea anashushwa kwenye hiyo gari safi ambayo ilikuwa kama yake kumbe Uber! Kwa haraka akasogea kama aliyewazidi wenzake bila swali. “Nina kazi ndogo tu, nataka unisaidie kaka yangu. Nitakulipa.”Akaanza Tunda taratibu. Akatoa miwani yake ya jua aliyokuwa ameivaa, akaishika mkononi na kumtizama yule kijana. “Bila shida.”Alikubali kwa haraka sana.
Tunda
akajua ameshamchanganywa kwa muonekano na sauti yake, akajua atafanya
chochote atakachomtuma, akamcheka
akilini mwake. Akamwambia kitu anachotaka afanye. Akampa maneno ya kuzungumza kwenye simu yake. Akamuuliza mara mbili tatu kama ameelewa huku na yeye akimuuliza maswali kutaka uhakika kama ameelewa sawasawa ili ajibu
kama alivyomfundisha, asiharibu. Darasa hilo liliendelea kwa muda mfupi tu, kijana akaonekana kuelewa kila alichofundishwa na Tunda. Alipojiridhisha naye, ndipo akampigia simu kijana anayehusika na manunuzi ya vinywaji pale kwenye club ya Kinny.
Alipojitambulisha Tunda kuwa ndiye Fina wa jana yake, yule mfanyakazi wa Kinny akakumbuka kwa haraka, kwani
alimwambia siku hiyo
angempigia. “Huyu ndio kiongozi wao. Hebu zungumza naye ili mpange.” Tunda akamkabidhi simu yule kijana na kikaratasi cha maswali ya kumuuliza yule
mfanyakazi wa Kinny.
Walishayapitia hayo maswali pamoja, yalikuwa mawili tu. Tunda
alikuwa ameshayaandaa tokea
nyumbani kwake. Juu ya bei na
usafiri. Naye yule kijana akachangamka
vizuri sana. Akaweka shoo ya nguvu hapo
kwenye simu akiuliza hayo maswali mawili
tu, lakini utafikiri ni kweli anao
huo mzigo. Kijana wa Kinny mwenyewe akashindwa biashara. Kijana wa Tunda alimwambia kwanza siku wanazotaka wao mzigo upelekwe kwenye
hiyo club yao sio siku zao za kuuza.
Wanakuwa busy kiwandani.
Pili, kuwapelekea vinywaji kule kwenye club yao sio bure, akamtajia bei ya usafiri. “Mbona sisi tunaletewa
mpaka hapa bure kabisa?”“Sasa hayo si ni
magari ya kiwandani Tajiri yangu? Hii biashara ya binafsi, kaka.” Yule kijana akajibu na kumfurahisha zaidi Tunda. Akamalizia kwa kumpa bei ya bia zenyewe sasa. Ilikuwa chini kidogo na ile bei ya yule kijana wa Kinny aliyomtajia Tunda jana wakiwa baa.
Yule
mfanyakazi wa Kinny
akashindwa. “Naona kama haitatulipa sana. Itaongeza tu usumbufu.” Tunda akachukua yeye simu sasa. Na yeye akaongeza njia ngumu. “Au labda
mzifuate wenyewe?” “Tatizo usafiri
dada yangu. Hata hivyo bei waliyotupa
haina tofauti kubwa sana na ya hawa wanayotuletea hapa. Kitakachoongezeka ni usumbufu tu kwetu.” “Ni kweli. Umefikiria vizuri
sana. Nitamwambia Kinny jinsi ulivyo na
akili nzuri ya kufikiria.” Akacheka kwa heshima, na kuagana na Tunda
“Mungu anipe nini mimi!” Tunda akajipongeza baada yakuona mipango yake imekaa na kwenda sawa. Hakuna wakumkamata. Akamlipa yule kijana aliyekutana naye palepale kwenye kituo nje ya Mlimani city, akamsaidia kuzungumza na kijana wa Kinny, aliporidhika malipo, Tunda akarudi kwenye ile gari, ili imuingize sasa ndani kumsubiria Kinny. Lengo lake likawa limetimia. Akacheka nafsini kwake. Akajipongeza kwa utapeli wake. “Nani wa kunikamata? Kijana hanijui, simu kutumia yangu, namba yakupiga baadaye akanushe niliyomfundisha ayaseme
pia hana. Na jina la aliyezungumza
naye pia hana! Mjini Shule.” Tunda akazidi kucheka nafsi kwake akijipongeza.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alingia ndani kabisa Mlimani City, akatafuta mgahawa mzuri, akakaa hapo. Hakuwa amepata kifungua kinywa. Njaa ilishaanza kumsumba. Na kwa kuwa alikuwa hali chakula usiku ili asinenepe zaidi, mara nyingi asubuhi ilikuwa lazima ale vizuri. Saa 11 jioni, ilikuwa mwisho wakuingiza kitu kizito tumboni kwake. Muhudumu akamletea kila kitu alichoagiza, akashukuru nakuanza kula taratibu bila haraka.
Saa sita kasoro, akaona simu ya Kinny
inaingia. Akacheka na kupokea. “Nimefika Fina.” “Tulikubaliana saa sita
kamili.”“Basi hamna tatizo. Nitasubiri mama. Utanikuta upande huu wa kuingilia.” Akamwelekeza alipoegesha
gari yake. Tunda akaelewa. “Sawa. Saa sita kamili
nitakuwa nimefika hapo. Sitakuweka.” “Nitashukuru.” Akajua wazi
ameshamkamata. Akacheka nafsini
mwake, akaendelea kula taratibu bila
haraka.
Alimsubirisha kwa robo saa ndipo akatoka. Akamgongea kioo. Alikuwa ameinamia simu yake. Akatoka kwa haraka akabaki ameduaa. Tunda akacheka kama
kumtoa kwenye ule mshangao. “Daah! Hakika Fina
wewe ni mzuri! Upo nadhifu!” “Asante Kinny. Na
wewe Umependeza.” Akawa muugwana akapokea sifa na kumsifu na
yeye. Wakaangaliana na kucheka. “Mbona mimi
nimekubali kushindwa!”
Tunda
akazidi kucheka, akakumbuka hali ya
Kinny jana kwenye gari. Kinny
akazunguka kwenda kumfungulia mlango na kumpokea mzigo. Akawa anamtizama wakati anaingia garini.
Hakika Tunda alipendeza na kuwaka kwenye hilo jua la saa sita. Alivaa suruali nyeupe, kiatu kirefu cha rangi ya kijani ambayo inaendana na aina ya blauzi aliyokuwa amevaa yenye mistari ya kijani kwa mbali kama vile viatu. Alishika pochi mbili. Moja kubwa, nzuri sana kwa kuitizama kwa macho. Ndio
iliyokuwa imebeba nguo zake za ziada na vitu vyakutumia safarini na pochi ndogo ya rangi ya dhahabu isiyong’aa sana.
Vyote vilionekana vizuri na vya
thamani. Ile suruali kule chini aliikunja pindo mbili, alikuwa amevaa cheni nzito ya dhahabu kwenye mguu mmoja. Sikioni pia alivaa hereni zakuning’inia kama cheni aliyovaa mkononi. Nywele alikuwa ameshonea wiving ya rangi ya gold kidogo iliyochanganywa na nyeusi. Fupi, iliyokatwa kote pembeni kasoro katikati.
Akaweka miwani ya jua. Usingechoka
kumtizama, na hata kama unampango wakumuhonga,
usingethubutu kumpa pesa chache.
Kinny akatoa gari pale Mlimani city, kuelekea uwanja wa ndege. “Sasa nani atakuja kuchukua gari yako?” “Huwa nikiwa nasafiri siku chache hivi, huwa naliacha tu palepale uwanjani. Naona inanipunguzia usumbufu. Wengine hatuna
madereva. Tunajiendesha wenyewe.”
“Kwa nini
usimuombe mkeo akulete?” Kinny
akacheka kidogo. “Mke wangu na watoto hawaishi hapa nchini. Wapo ughaibuni huko. Huku tunatafuta tu pesa.”
“Safi sana.” Tunda alijibu hivyo tu
kwa ufupi, hakutaka kuendeleza yale mazungumzo.
Akazungumzia maswala ya vinywaji, na ugumu aliokutana nao yule mfanyakazi wake. “Anaonekana ni kijana mwenye upeo mzuri wa kufikiria.” “Ndio maana huwa nampenda na kumuamini na maamuzi fulani fulani. Anajua kupima mambo. Maana
ingekuwa mwingine, angehadaika na bei, akasahau garama ya usafiri.”Kinny akaingia kwenye mstari wa Tunda, hilo akalifurahia kuwa wamerekebisha hapo, amepona. Wakazungumza mambo ya kawaida tu, mpaka wakaondoka jijini Dar kuelekea Dodoma.
Tunda & Kinny
jijini Dodoma.
“Twende
hotelini kwanza, tuvute muda mpaka saa
mbili ndio nakutana na jamaa.” Kinny
alimwambia Tunda mara walipotua uwanja
wa ndege wa jijini Dodoma. Bado ilikuwa mapema tu. “Kijana mwenyewe mdogo tu,
lakini amepewa majukumu
yanayomfanya anaringa kama mtoto wa
kike! Nambembeleza karibia nimlambe!” Tunda
akacheka. “Kwani unataka nini?”
“Yeye
ndiye anahusika na bajeti ya wa
bunge wakiwepo bungeni. Wanataka kuanzisha chakula cha mchana kwa wabunge wote kipindi cha bunge kikianza mpaka mwisho. Wametangaza hiyo tenda. Sasa yeye ndiye muhusika mkuu. Nilitaka nimuombe mimi hiyo kazi
yakulisha wabunge. Na
kutengeneza mazingira mazuri hata ya
kuwafanya wawe wote wanapata
kifungua kinywa hapohapo bungeni
muda wote wa bunge linapokuwa likiendelea.
Sasa upatikanaji wake ndio shida.” Kinny
akaendelea kama anayelalamika.
“Sasa ananizungusha, nakaribia kuchanganyikiwa. Ni hivyo tu wife naye anasisitiza. Anaona ikienda vizuri, tukafanikiwa hiyo kazi, anataka arudi nchini, aifanye yeye mwenyewe hiyo kazi ya kuwalisha hao waheshimiwa.” “Pole. Pengine safari hii atakubali.” Akaguna Kinny kama
asiyesadiki. “Pengine na wewe unamuendea
kibabe ndio maana anakuwekea
ngumu.” “Nilitakiwa nifanyaje?” “Kuwa kama mtu mwenye
shida, unayemuomba.” Tuna akatoa wazo. “Daah! Mimi nahisi nimefanya kila njia.”
Kwa mazungumzo
yake na Kinny kuanzia wanatoka Dar ampaka hapo, Tunda kwa haraka sana
alishajua hawezi kumfanya kuwa Sadiki
mwingine. Wakati wote
Kinny amekuwa akizungumzia familia yake. Mkewe ni kama ndiye anayeongoza mambo mengi ya familia hasa pesa. Swali likawa atanufaikaje naye? Hilo ndio likawa swali alilokuwa akiliwaza Tunda tokea yupo kwenye ndege, Kinny akiongelea mambo yake na familia yake.
Wazo likamjia wakiwa kwenye taksii hiyo ikiwapeleka hotelini. Uzuri Tunda alikuwa
mkimya. Ikamsaidia kufikiria
vizuri, wakati Kinny akiendelea kuzungumzia
mambo yake na kulalamika, yeye anafikiria.
Akamgeukia Kinny. “Nikikupatia mimi
hiyo kazi, utanilipa kiasi gani?” Kinny akabaki kama ameduaa
kidogo. “Nakuuliza Kinny? Tuna siku ya
leo, kesho na kesho kutwa. Kama unauhakika umetumia njia zote. Sasa hivi ongeza uthamani wako.” “Kwa kufanyaje!?” Kinny akakaa sawa wakati anauliza ili kumsikiliza Tunda aliyekuwa ametulia wakati wote.
Mtu ambaye
sio mzungumzaji, akitaka kuongea, lazima
utataka kumsikiliza tu. “Mpigie simu leo, mwambie una mtu muhimu sana unamiahadi naye leo jijini. Huwezi kuahirisha kwa kuwa yupo kwenye zihara hapa nchini na anaondoka kesho asubuhi sana. Usitoe maelezo mengi sana. Lakini mwambie umemtuma leo meneja masoko wako huku Dodoma ili kukuwakilisha kwenye miahadi yenu. Mwambie tunaweza kukutana saa mbili kamili usiku. Ila kama bado atakuhitaji wewe mwenyewe, basi mwambie utawahi ndege ya kwanza inayokuja huku Dodoma kesho ili mpate hata dakika chache za mazungumzo. Hivyo tu. Usiongeze neno wala kupunguza. Halafu uone kama sijakupatia mimi hiyo kazi. Labda iwe haipo.” Kinny akastaajabu sana.
“Yaani mpaka tu hapa,
mimi mwenyewe umeshanifanya
nikukubalie kwenda kukutana naye.”
Tunda akacheka. Na walikuwa wamefika hotelini. “Mama umejaliwa lugha
ya ushawishi! Halafu mwenyewe
taratibu, mpaka unamaliza, mtu anataka
aseme ndiyo tu!” Tunda alizidi kucheka
huku wakiingia ndani. “Lakini wewe unaonaje wazo langu?”
“Nakwambia mimi
mwenyewe ushanishawishi! Kabla
yeye hajasema “ndiyo’, mimi nishasema
ndiyo!” Tunda akacheka. “Lakini nakupa siku ya leo
tu, kesho naenda kupambana naye
mwenyewe. Asiniletee mchezo. Sina
ninaloongea na mke wangu ila hili tu!”
“Sawa. Lakini nikikufanikishia, usinisahau .” “Siwezi. Nakuhakikishia kama
ukinipatia hiyo tenda, nakupa pesa
bila maswali Fina. Ni kazi ya pesa
nyingi, ati! Kwanza hata mke wangu
ataniona wa maana.” Tunda akacheka
kidogo na kunyamaza.
Walipofika ndani, Tunda alikaa kwenye makochi akamuacha Kinny aende yeye mwenyewe mapokezi. Kinny akajiandikisha, akapewa funguo za chumba. Akarudi kumchukua Tunda ndipo wakaelekea chumbani. Walifika hapo hotelini ilishakuwa jioni. “Njaa inakuuma?” Tunda
akamuuliza. “Nilivyo na hamu uniguse na
hiyo mikono yako laini, chakula
kitasubiri tu.” Tunda alicheka sana. “Hutaki kuoga kwanza?”“Acha bwana Fina! Sasa
tumechafuka wapi wakati tumetoka kwenye
ndege na kuja hapa?”
“Mimi
nilikuonya mtindo wa kukariri Kinny.
Unapitwa na mengi!” “Halafu ukisemaga hivyo inakuwa kweli!” Tunda akaanza kucheka.
“Naomba tuanzie hapa
kidogo, halafu ndio tukaoge. Mwenzio
hali mbaya. Nikikuangalia hivyo!
Natamani tu unitulize kwanza. Nina siku...”
Tunda akamziba mdomo taratibu kwa
vidole vyake viwili. “Shhhhh!”
Taratibu Tunda akamtaka anyamaze. “Hutaki kelele eeh?” Kinny akauliza kwa
sauti ya chini ya kunong’ona. Tunda akacheka huku
akitingisha kichwa kukubali. Akamsukuma kitandani taratibu. Akamuwekea mto chini ya kichwa, kuwa ajiegemeze. Yaani alale chali. Alipolala akiwa anamtizama, Tunda akaanza kuvua nguo zake mbele yake taratibu bila haraka huku akimwangalia na
tabasamu usoni.
“Sasa na mimi si ni vue?” Kinny akauliza huku
akibabaika. “Shhhh!” Tunda akamnyamazisha tena.
Alianza kwa kutoa ile shati ya juu.
Akabakiwa na sidiria juu. Akachomoa
ule mkanda kiunoni akaurushia
kwenye kochi. Akaanza kushusha ile
suruali na tabasamu usoni. Kinny
akavuta pumzi kwa nguvu huku
akitazama kwa makini.
Chupi iliyokuwa imebaki hapo,
ikamfanya Kinny ajiweke sawa, amtizame
zaidi. Juu ya ile chupi kulikuwa na
cheni ya dhahabu iliyowaka zaidi sababu
ya kiuno cheusi cha Tunda. Kinny akalamba midomo. Tunda akacheka taratibu.
Akaanza
kushusha ile suruali akiwa bado
hajatoa viatu. “Nikusaidie?” Kinny
akauliza. Tunda akatingisha kichwa
kukataa huku akicheka. Akageuka,
akainama ili kuvua viatu. “Oooh my!” Kinny alisikika taratibu.
Tunda akacheka taratibu. Akatoa
viatu, akatoa na ile suruali. Akarudisha
viatu vyake miguuni taratibu na ile
cheni ya mguu ikabakia palepale.
Akaokota ile suruali. Akaikung’uta kidogo kama anayeitengeneza. Akaikunja
na kwenda kuiweka kwenye kochi lililokuwa na pochi yake, huku akiwa na chupi tu, na viatu vilivyokuwa vimemkaa vizuri mguuni. Virefu, mchongoko mbele. Kinny alibaki
akiangalia huku akivuta pumzi.
Bado
alikuwa na nguo zake vilevile
akisubiri kuona kitu Tunda atamfanyia.
Tunda akafungua pochi
yake, akachukua kitu ndani ya
hiyo pochi, akarudi na kupanda kitandani
vile vile. “Fina!” Akamwita taratibu.
“Ungeacha nikuvue mimi hiyo chupi.” Kinny aliongea taratibu
kwa sauti ya chini akionekana wazi
ameshalemewa. Tunda akacheka tu, na
kumkalia mapajani. Akanyanyua mkono
wa Kinny na kumshikisha kiunoni
kwenye kiungio cha chupi kama
anayemfanya ailegeze. Kinny akaelewa kwa
haraka, akavuta kwa makini. Chupi
yenyewe ilionekana nzuri yakuvutia,
hakutaka kuharibu. Kimkanda cha
pembeni kikaachia. Tunda akatoa
taratibu huku akimwangalia.
Alijinyanyua kidogo kumpisha aitoe
kabisa, kisha akaanza kumfanyia fujo
hapo kitandani na nguo zake vile vile,
hakumtoa.
Tunda alikuwa yupo kazini, anajua analolifanya
kwa hatua. Hakujichanganya na hakujisahau. Alijua yupo pale ili atumiwe mwili wake. Na yeye akakusudia kufanya kazi yake vizuri huku akijikinga. Alimchanganya Kinny mtoto wa jiji la maraha Dar, akabakia akiweweseka na nguo zake, nusu suruali. “Daah! Tumekubaliana tukae siku ngapi tena?” Tunda
akacheka huku akinyanyuka pale alipokua amemkalia. Akatoa viatu vyake taratibu bila haraka, akaelekea bafuni akiwa na ile cheni ya kiunoni na ya mguuni.
Kinny
akabaki akijipapasa shingoni, sikioni
kule Tunda alikokuwa akipitisha ulimi wake. Mwili ukazidi
kumsisimka. “Sasa, sasa hivi si
naruhusiwa kutoa nguo?”Akauliza Kinny
kwa tahadhari. “Huwezi kuoga na nguo.” Tunda akajibu akiingia
bafuni. Kama anayekimbizwa, akatoa nguo
haraka huku akizitupa kila mahali
akakimbilia bafuni kumfuata Tunda. Huko
nako Tunda akamfanyia
vihoja vya makusudi. “Kwani Fina wewe huna mifupa mama!?” Tunda akacheka sana. “Utanifanya nishindwe
kazi bwana! Na bora ningekubali lile
wazo lako la kwanza, la kuanza kuoga.” “Nilikwambia uache
kukariri.” Tunda
akamjibu taratibu huku akiendelea
kuoga.
“Kuanzia sasa hivi nitakuwa mtoto mzuri. Nafuata ushauri.” Tunda akamwangalia huku akioga. Akamvuta karibu
yake, Tunda akampa mgongo baada
yakumuona anataka kumbusu midomoni. Akajua
amenogewa. Akamkumbatia akiwa
amesimama nyuma yake. Akabaki
ametulia mgongoni mwake, amekumbatia
kiuno kilichobeba ile cheni.
Aliizungusha mara kadhaa, akahisi
amepotelea mawazoni. Tunda akatulia tu
huku maji yakiendelea kuwamwagikia. Walitoka
hapo, Kinny akiwa ameshachanganywa
na Tunda, hakuna aliloambiwa akakataa au
kupinga.
Akampigia simu huyo mtu ambaye Tunda alitaka akakutane naye yeye badala yake. Akakubali hiyo saa mbili kamili wakutane na huyo meneja masoko wake Kinny. Hapo hapo Tunda akachukua namba yake ya simu. “Anaitwa nani?” Tunda akauliza wakati anaingiza namba yake ya simu kwenye simu yake. “Mbawala.” Kinny akajibu. Tunda akaandika kwenye simu yake. Akamuona Kinny anasinzia. “Lala.” “Kweli? Sio ulitaka tukae wote mpaka uondoke? Maana muda umeisha.” “Usijali. Lala tu. Nitakuletea na chakula.” “Hapo utakuwa umenisaidia. Asante.” Hapo hapo akafunga macho na kulala.
Tunda kwa
Mbawala.
Tunda alifurahi sana kuua ndege wa wiwili kwa jiwe moja. Tumaini lakumfanya Kinny kama Sadiki, lilishaisha. Hakuacha kumtaja mkewe katika
kila jambo. “Huyu
tutasumbuana naye huyu. Naona
ameshikwa masikio na mkewe. Hana
analolifikiria au kulifanya bila mke
wake! Club yenyewe ya Dar,
ameongezewa mtaji na mkewe. Wote
tunalia shida! Hapana.” Tunda
alishawaza hilo. Kumpata Mbawala
ikawa faraja. Akakusudia huko
akafanye mawili kwa mpigo. Akajawa
hamasa ya namna yake. Akaamua
apendeze haswa. Kuuza kazi ya Kinny
ili aje amlipe, na kumnasa Mbawala.
Akavaa kigauni cha hawaida tu. Lakini kifupi na kilichanua chini. Rangi mbili, Gold/dhahabu isiyowaka ndiyo ilikuwa juu ambako ilikuwa kama shumizi, yaani vimikanda na katikati ya kiuno mistari niwili iliyomkaba haswa kiuno. Mistari ya hiyo rangi ya hiyo dhahabu ya juu na nyeusi. Chini ya kiuno pale kwenye kile kiungio cha dhahabu na nyeusi, kuliunganishwa muundo
wa mwamvuli, nyeusi tupu
iliyojimwaga haswa mpaka juu yamagoti
kidogo. Kiatu kirefu chakufunika,
mchongoko kilichokuwa kimemkaa vizuri
na kimeendana na pochi ndogo
aliyokuwa ameshika mkononi ya dhahabu. Kwa hiyo kiatu, pochi na ile gauni kwa juu, vyote viliendana. Alivaa hereni zile za mnyororo ndefu mpaka mabegani na cheni ya mkononi na mguu mmoja.
Basi. Tunda akacheka alipojitizama kwenye
kioo. Akajipulizia pafyumu tulivu.
Hakuwa akijipaka rangi usoni mwake
sababu ya rangi yake ya mwili.
Wakati wote
nyusi alizilaza tu na kuweka wanja
kidogo, pengine usingetambua, na
mafuta ya mdomo ya rangi ya
wekundu kwa mbali kama pinki.
Akajizungusha tena kwenye kioo mara
kadhaa, akiweka kichwa kulia na
kushoto. Akacheka. Akatoka taratibu
kama asiyetaka kumuamsha Kinny.
Akiwa
njiani akampigia simu
Mbawala. Ikaita mara tatu ikakatwa.
Akatuma ujumbe. ‘Naitwa Fina, tunamiahadi ya saa mbili kamili. Nipo
njiani. Sitaki kukupotezea muda wako,
nitafika kwa wakati.’ Akautuma
huo ujumbe. ‘Nipo hapa tokea dakika 10 zilizopita.’ Ujumbe huo ukarudi. Tunda akajua anakwenda kukutana
na kiburi. Akacheka, ‘Hakuna mwanaume
jeuri mbele ya mwanamke’. Akajiaminisha Tunda. Hakumjibu.
Walishafika kwenye huo mgahawa waliokuwa wamekubaliana. Ile sehemu tu yenyewe, akajua Kinny anamuheshimu
Mbawala kwa kukutana naye sehemu kama
ile. Tunda akakusudia kufanya ‘entrance’
ya nguvu. Kuwa kila mtu amwangalie kuanzia juu mpaka chini wakati anaingia pale. Atafanya nini! Akaanza kuwaza wakati anashuka kwenye taksii. Akatoa simu yake mlio kabisa. Akaweka ‘silence’. Mgahawa ulikuwa mtulivu.
Akaanza kuongea kama anayezungumza na mtu kwenye simu wakati anakaribia mlangoni kwa sauti yake tulivu isiyo ya fujo ila yakusikika kiasi. “No. I hope it
wont take long.” Tunda alisikika akizungumza na mtu kwenye simu akimwakikishia kuwa hiko kikao
anachokwenda kufanya, hakitachukua muda mrefu huku akiingia taratibu kwa sauti yake tulivu. “Noo!” Akacheka Tunda taratibu, simu sikioni. “I promise. Bye for now.” Tunda akaahidi huko
kwenye simu kisha akabonyeza simu yake kama aliyekata. Akawa amesimama katikati ya ule mgahawa.
“Sorry!” Akajifanya muungwana, akaomba msamaha wa
usumbufu, kinyenyekevu kwa watu aliowakuta pale ndani ya ule mgahawa waliokuwa
wametulia yeye akizungumza na simu wakati akiingia. Akawa kama amekumbuka kitu, akarudi nyuma mpaka pale alipompita mtu wakupokea wateja. “Naitwa Fina, nina miahadi
na Mbawala.”Akanong’ona. Akaona mtu anamfuata kwa haraka. “Ni mimi.” Wote yeye na muhudumu
wakageuka. “Ni mimi ndiye
Mbawala.” Akajitambulisha kwa
haraka kama aliyekwisha kubabaika tayari.
Hapakuwa
na watu wengi humo ndani na Tunda alishamuhisi kwani alikuwa amekaa peke yake kwenye meza, ila tu, alitaka ageuke wamuone na nyuma. Kwa jinsi alivyokuwa amependeza, hakutaka kufika na kukaa tu. Alitaka kila mtu amuone. Alivyomtulivu usoni, usingejua hila ya Tunda kichwani mwake. Hakika alikuwa amependeza. Kuanzia kichwa mpaka unyayo
yupo safi. Kingereza chenyewe alichokuwa akikiongea kwa
pozi kwenye simu kilikuwa kimetulia, hakusikika kuunga maneno kwa shida.
Kigauni kile kilifika sehemu ambazo
ungependa kuangalia zaidi. Mguu mweusi,
laini kwa kuutazama kwa macho,
mrefu, ulionyooka, umetulia kwenye
kiatu hicho cha juu kizuri. Akaning’iniza cheni nene. Mtaratibu usoni, na tabasamu
lenye kuonyesha meno machache meupe pee
na macho hayo, hakika utatamani asikae.
Huwezi kulaumu usumbufu
aliosababisha wakati anaingia. Utachukia
akikaa tena akafichwa na mtu mbele
yake.
Naitwa “Fina.” Tunda akamsogelea
Mbawala na kujitambulisha taratibu huku akimpa mkono ulionyoka tena uliokaza si mlegevu.
Kuashiria yupo kikazi. Mbawala akaupokea
mkono huku amekodoa macho usoni. “Naitwa Mbawala.” “Nimefurahi
kukufahamu. Nashukuru kwa muda wako.
Nakuahidi sitakuchukulia muda wako
mwingi.” “Karibu mezani. Nilikuwa nimekaa pale.”Akanyoosha mkono
huku akitangulia kuonyesha njia.
Tunda akamfuata.
“Karibu.”
Tunda
akakaa alipoonyeshwa, mbele yake. “Acha
tuagize hata vinywaji.” Tunda akamtizama
kama anayemshangaa kidogo. “Kama huna haraka lakini.” Akajihami. “Niliambiwa
wewe ni mtu unayethamini sana muda wako.” Akacheka kwa kujisuta
kidogo. “Sio hata weekend bwana! Leo
siku ya mapumziko. Naomba
tuzungumze wakati tunakula. Sijala siku
nzima. Naona hata macho yanaanza kuona yasiyokuwepo.” Tunda akatulia tu akimsikiliza. “Unakunywa nini?”
“Maji
tafadhali.” Mbawala akamshangaa kidogo. “Maji tu!?” “Maji yananitosha. Asante.” Tunda akajibu
na tabasamu. Muhudumu akaja, Mbawala akasisitiza kuwa lazima wote wale. Akamuagizia na
yeye Tunda, muhudumu
akaondoka.
“Unaishi hapahapa Dodoma?” Mbawala akaanzisha mazungumzo. “Hapana.
Nimekuja huku kwa ajili yako. Wewe mtu mkubwa
sana, bwana! Naona kukupata
inakuwa garama kweli!” Mbawala
akacheka sana. “Wanao kwambia hayo,
wanakuwa wananitafuta mida mibaya.
Ila mimi napatikanika sana tu.” “Basi
afadhali nimekupata siku
ya mapumziko. Naamini na mimi
utanipa sikio lako.”
Wakacheka
kidogo. “Naona safari za Dar
zitaanza kuwa nyingi.”
Tunda
akacheka kwa utulivu na kuuliza. “Kwani zilikuwa chache?” “Na fujo zile, najitahidi sana kuzipunguza.” “Kama mahitaji yote ukiyapata Dodoma, huna haja ya kufuata kelele za Dar. Huku ni patulivu.” “Ndio tatizo hilo.
Patulivu, lakini bado sijapata vitu nadhifu.” Tunda akacheka na kuinama kidogo.
“Ndio tatizo pekee kwangu kwenye huu mji mkuu.” “Fungua milango tukusogezee huduma huku. Mkikaribisha wawekezaji, mtapata huduma zote. Tatizo lenu mnabania.” Mbawala akacheka sana. “Inategemea na mwekezaji. Wengine viburi, hawana lugha ya biashara.” “Naelewa. Pole.” “Ndio majukumu hayo.”
“Ukubwa unakuja na majukumu, sio?” “Unakuwa jalala haswa!”
Mbawala akaafiki.
“Naomba
Mungu na mimi nipate nafasi kabla hilo
jalala halijajaa na kufukiwa.” “Usijali. Tutatengeneza mazingira mazuri ili na wewe
upate nafasi yako.” Tunda
akacheka taratibu huku akimtizama.
Alishamuona amelainika.
Chakula kikaletwa, Tunda akakila kwa kukidonoa donoa akiwa anatumia kisu na uma. Huyo kuku akamgeuza kulia na kushoto na uma wake huku akimsikiliza Mbawala akijigamba kwa hili na lile. Aliweka mdomoni vipande vidogo
sana vya nyama, na kutafuna taratibu
tena kwa muda mrefu. Mbawala alimaliza
chakula chake, Tunda hakuwa hata amefika
robo. Akaweka kisu na uma chini. “Ndio
tayari hivyo!?” “Inatosha. Imeshakuwa
usiku. Sipendi kulala na vyakula vingi
tumboni.”“Ndio maana
una mwili mzuri Fina.” Tunda
akacheka taratibu na kushukuru kwa sifa huku akisogeza ile sahani pembeni. “Asante.”
“Sasa maswala ya kikazi yakiisha, ndio basi tena?”
Tunda akatabasamu. “Inategemea tunaachana vipi.” Tunda akamjibu na macho yaliyomfanya Mbawala atulie
kidogo. “Naomba nikukaribishe
kwangu.” “Safari hii nipo
kikazi. Safari za matembezi hizo tuzipange baada ya leo.”
“Fina unamasharti?” “Hataa. Kawaida tu. Hatuwezi kuchanganya mambo Mbawala! Hili hatujamaliza,
tunarukia mengine!?”
“Nimekukaribisha
tu kwangu.” “Nimekusikia. Nikifika halafu
nikagoma kuondoka?” Mbawala akacheka sana.
“Hiyo itakuwa rehema.” Tunda akacheka kidogo.
“Naomba nikuache. Nina miahadi
mingine kabla ya saa tatu na nusu
usiku huu.” “Nahisi kama mimi muda wangu umepunjwa!” “Ni kutokana na nilivyoambiwa juu yako. Kuwa huwa hupendi kupotezewa muda, nikaweka miahadi ya
haraka. Tena nikiwa najua wala hutataka
kunisikiliza.” “Hapana bwana!
Wamekutisha tu. Sasa itabidi mniandalie
menu yenu. Mniambie mtaweza kuwalisha
nini. Nijue bei zenu. Kisha tujue kuanzia hapo.” “Naomba nikuombe kitu
Mbawala. Najua ni nje ya kazi. Ila naomba
msaada wako.” “Nini tena?” Mbawala akauliza.
“Najua sasa hivi umechoka.
Naomba nipe muda mfupi kesho.
Nikufuate popote, ili tuiandae hiyo menu
pamoja ambayo unafikiria wangependa.
Na bei
ambayo Mbawala ataikubali.” Mbawala akacheka sana. “Fina unaniibia bwana!”
“Nisaidie tafadhali. Angalau nipate tu mwanga. Lakini kama unaona ni kuvuka mipaka, basi. Tusichanganye mambo.” Tunda
akatingisha kibiriti. “Hapana. Hata
kidogo. Hamna shida. Kwani unafikiri
itachukua muda mrefu!” “Ehe!”
“Sio kitu
kirefu hata kidogo. Hata mimi mwenyewe
naweza nikaandika na kukutumia.”
“Kweli Mbawala!? Sitaki nikuchoshe kwa kukuongezea jukumu zito.”
Tunda aliongea kwa kubembeleza kama anayemuhurumia tena.
“Hata kidogo.
Ni nafasi nzuri, ningependa na nyinyi
mnufaike. Tena ikikaa
vizuri, tutaipitisha kwa
haraka tu.” “Nakushukuru sana Mbawala.
Hata sijui nikulipe nini?”
“Niahidi
kurudi huku kunitembelea.”
Tunda
akacheka sana. “Au ombi
zito?” “Hapana.
Linawezekana kabisa. Umekuwa
msaada mkubwa kwangu. Naomba
tupange, naweza kukukaribisha Dar, au mimi nikarudi kukutembelea.
Lakini naomba niwe
nimekukamilishia jukumu ulilonipa kwanza.” Tunda akamuwekea ngumu kiustarabu. Kwamba ni mpaka
amkamilishie haja yake. “Hilo mbona ni
kama limesha kwisha Fina!
Nakutengenezea kila kitu,
na kukuwekea mpaka bei.
Kitakachobakia ni kuweka tu kwenye
karatasi yenye logo yenu na muhuri,
basi. Na kama mtabadilisha, iwe kidogo.”
“Basi itabidi kuja kusherehekea hukuhuku.” “Naomba na mimi niwepo
kwenye hiyo sherehe.”
Tunda
akacheka tena. “Wewe ndio muhusika
mkubwa. Utakosaje tena?”
“Basi acha
nikaanze kazi. Naamini weekend ijayo
utakuwa mgeni wangu.” “Wema hauozi.” Akisisitiza, afanye
upande wake, atapewa tu penzi. Wakacheka
na kuagana Tunda akiwa amempa mawasiliano ya barua pepe ya Kinny. Kwamba
akimaliza atume huko.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alimwambia
dereva taksii ampitishe sehemu yenye
nyama choma nzuri, akanunua na kurudi
nayo hotelini. Kinny bado alikuwa
amelala. Tunda akamuamsha. “Kula kwanza
ndio urudi kulala.” “Nilikuwa na uchovu na ukame wa muda mrefu!”
Tunda akacheka. “Kweli. Sijapata muda kama huu kwa muda mrefu. Kwanza nilitoa akili kabisa kwenye mapenzi. Nilikuwa nakimbizana na biashara, bila kupumzika huku wife naye akipiga kelele kila siku!” “Pole. Kaa ule kwanza halafu nikupe habari njema.” Kinny akakaa kwa haraka.
“Haiwezekani! Usiniambie yule mpuuzi amekukubalia!” “Hajaishia hapo. Na amesema..”
Tunda
akamuelezea kila kitu kinachomuhusu yeye
kasoro kuja kukutana wao wawili tena. “Mpuuzi sana yule. Au una kimzizi wewe Fina!” Tunda alicheka sana. “Ungejua
jinsi nilivyosumbuka naye huyu mjinga,
usingeamini. Nimeshafanya safari
kama hizi zaidi ya mara mbili! Nakuja,
ananiambia hataweza kuniona, yupo
busy. Nikimpigia simu, ananijibu kwa
ujumbe kuwa atanitafuta. Ujue hapo ni
mpaka nimtafute tena na anaweza
asipokee au akapokea na kuniambia
tuonane siku ambayo ukifika hapa
anakwambia amepata safari ya kikazi
yupo nje ya Dodoma.” Tunda akazidi
kucheka.
“Kweli Fina. Nimefurahi sana.” “Sasa sio ufurahi, unisahau!”
“Sithubutu. Umeniokoa na kelele za mke wangu kuliko nitakavyokwambia! Tukikamilisha
tu, nakulipa, na yeye nampigia.
Nahisi atakusanya watoto kesho yake
arudi. Kashachoka kuishi huko.”
Tunda akanyamaza, hakuchangia. Hapo
Kinny akajishtukia kidogo. Akajirudi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kesho
yake asubuhi, Kinny alipoangalia barua
pepe ambayo Tunda alimpa Mbawala atume
hapo, akakuta ameshatuma.
Akamuamsha Tunda akiwa haamini. “Huyu
mjinga ametuma bwana! Ona.” Tunda akakaa
huku akivuta shuka asibakie mtupu. “Umemchanganya mpaka
ameweka na bei mbili mbili, kama
jinga! Ameandika hapa, isizidi hii ya
pili. Angalau iwe katikati. Bwana kaka
huyu umemchanganya Fina! Naona hata
ukimuomba gari yake, huyu atakupa tu.” Wakacheka.
Kinny akairekebisha haraka huku Tunda akiwa amejilaza tu hapo kitandani akihesabu pesa atakayomchomoa Kinny.
“Inabidi uende mapokezi ukaiprinti umpelekee.” “Mimi tena! Hapana Fina. Naweza nikaharibu mama. Tafadhali mrudishie wewe mwenyewe. Asije akaona hii sura yangu, akagairi.” Tunda akacheka. “Basi kaiprinti
halafu mimi nitampelekea.” Kinny akambusu nakutoka
hapo akikimbia.
Bahati yake mbaya, nzuri kwa Tunda akasahau simu yake. Tunda akakaa kwa haraka akaingia moja kwa moja kwenye
phonebook yake ili kuiba namba za simu
za watu. Alijua mtu kama Kinny, mtoto wa
jiji, ameishi nje ya nchi, lazima anao
watu wenye pesa. Akaanza kuperuzi
taratibu akisoma majina ya watu kwa
makini. Yale ya watu wakubwa
aliyoyasikia mtaani, alichukua namba
zao. Moja kwa moja akawa anahamishia
kwenye simu yake. Aliporidhika, akaweka
simu ya Kinny pembeni na kumpigia simu
Mbawala.
“Naomba nikushukuru kwa kuwa mwaminifu, Mbawala. Asante.” Hiyo sauti tu yenyewe, akafurahia. “Karibu mrembo. Unarudi lini
Dar?” “Leo jioni.” “Hatuonani?” “Lazima nikuage Mbawala.
Siwezi kuondoka kimya kimya.” “Nitashukuru.
Na leo nipo tu nyumbani.” “Ulitaka nije mpaka kwako!?” Tunda akashangaa kidogo. “Hamna neno. Karibu. Naishi
peke yangu na ni mazingira matulivu.
Niambie nini unapenda, nikutayarishie
ukifika ukute kipo tayari.” Tunda akacheka huku
akifikiria.
“Niambie chochote Fina, nitapika.” “Mimi sio mchaguzi Mbawala.
Nakula kila kitu. Ni surprise.” Mbawala akacheka kama aliyeridhaka. “Hapo umenipa
uhuru. Basi karibu.” “Nije saa ngapi?” “Muda
wowote hata sasa hivi.” Tunda akacheka taratibu kama anayefikiria kisha akafikia muafaka.
“Basi naomba iwe mida ya saa tano ili
angalau saa saba niweze kuondoka. Nijiandae kurudi Dar.” “Naona kama unanipa muda
mfupi!” Mbawala akalalamika kidogo.
“Huu ni mfupi
kwa kuwa umeingiliana na kazi. Nilikuruhusu
unitafute baada ya kukamilisha hili.” “Hapo sawa. Nitafanya juhudi
zote ili weekend ijayo uwepo huku tena.” Tunda akacheka akiashiria kukubalina naye. Baada
ya kumuelekeza nyumbani kwake
wakaagana kwa makubaliano akishindwa
kufika, basi ampe dereva taksii simu,
atamuelekeza. Tunda akajitayarisha
vizuri.
Aliporudi
Kinny akamtaka kimapenzi kabla
hajaondoka, Tunda akamwambia
anamuwahi Mbawala ili awahi kurudi,
warudi Dar kama alivyobadilisha. “Naona leo
tubaki hapa tukisherehekea.” Tunda akacheka huku akimalizia kujiandaa. “Ila sio ndio ukatumie
siku nzima na Mbawala, urudi hapa usiku.
Wakati mimi ndio nimekuleta huku.” Ile
kauli ilimuuma sana Tunda. Akamgeukia
kama aliyeishiwa nguvu kabisa. “Kwa nini
usimpelekee wewe mwenyewe tu?” Tunda akakaa kabisa kama aliyeishiwa nguvu. “Nakutania Fina. Naomba usikasirike tafadhali. Nimetania tu.” “Hapana. Sio hasira. Lakini naona kwa kuwa nimeshafanya kazi kubwa na amekubali. Naona sio mbaya ukamalizana naye mwenyewe.” Tunda
aliongea kinyonge huku akivua
viatu.
“Naomba nisamehe Fina!
Nimeropoka tu. Nahisi nimefurahia kupita
kiasi kazi kubwa uliyofanya.
Nimejisahau naongea na nani. Nishazoea
kuropoka kwa wale walevi wangu.
Tafadhali naomba unisamehe.” Tunda hakujibu, akavaa tena viatu vyake, akachukua
ile bahasha akatoka bila kujibu kitu.
Nyumbani Kwa Mbawala.
Mbawala alikuwa amejenga nyumba hapo jijini Dodoma.
Tunda alipofika nyumbani kwa Mbawala,
akajua ni kwanini alitaka aende nyumbani
kwake. Kama kujionyesha tu. Kijana huyo
mdogo, alijenga nyumba nzuri sana hapo
jijini. Ilikuwa na ramani nzuri, pazuri
na kweli palikuwa patulivu. “Karibu
sana Fina.”Akaenda kumpokea nje ya
geti baada ya kumpigia simu kumtaarifu
taksii imesimama kwenye hilo geti
jekundu kama alivyoelekeza. Mbawala
alimfungulia mlango. Tunda akashuka.
“Asante. Kweli hapa nipatulivu.” Tunda akasifia. “Nilikwambia mimi.” Wakacheka wakati
wanaingia ndani.
Palikuwa pananukia vizuri. “Ni nini hicho umepika kinanukia kuanzia mlangoni?” “Twende ukaone. Nimetengeneza brunch.” Tunda akacheka taratibu huku akisogelea lilipo
jiko. Ukutani akakumbana na picha
zilizomfanya atulie aangalie. “Kumbe
waziri Mbawala ni baba yako!?” Mbawala
akacheka. “Huoni tulivyofanana hivyo
vichwa?” “Sasa hivi ndio nikiwaangalia pamoja, mnafanana naye. Ila naona rangi ya mama.” “Ewaa. Rangi ya mama.”
Tunda akatizama picha nyingine, hapo
ukutani. Kulikuwa na picha amevaa joho halafu akaonekana mwanaume
mtumzima mwenye asili ya kizungu na yeye amevaa Joho la tofauti alikuwa akimkabidhi
yeye cheti.
“Naona umehitimu uzunguni!”
Mbawala
akacheka sana. “Mimi na dada yangu huyu
kwenye hii picha na wazazi, wote
tulisomea nje ya nchi. Lakini wote tulirudi nyumbani. Hapo ilikuwa mahafali ya shahada ya pili.” “Hongera sana. Nani sasa
mkubwa?” Taffy ndiye mkubwa. Tupo wawili tu.” “Safi sana.”Akasifia kidogo ndipo akaelekea jikoni. Akawa sasa ameelewa siri ya kiburi na mafanikio hayo ya huyo Mbawala aliye naye hapo.
Alipoingia jikoni akakuta amekaanga viazi alivyokata pande nne, pamoja na vitunguu, hoho za rangi tatu. Kijani, njano na nyekundu. Zote zimekatwa kwa muundo wa pembe nne tena kubwa kulingana kidogo na vile viazi. Vilitoa harufu kama kulikuwa na kitunguu
swaumu. Pembeni kulikaangwa mayai yaliyokuwa na Cheese katikati. Na firigisi zilizokuwa zimekaangwa vizuri, na kuwekwa kwenye bakuli
zuri pamoja na nyama za kuku
zakukaanga.
“Mpaka nimepatwa njaa!” Mbawala akalifurahia
hilo. “Basi chukua sahani, tuanze kula. Hata mimi bado sijapata kifungua kinywa.”
Wakakaa hapo
hapo mezani wakila na kuzungumza. Vikajaa
vicheko huku Tunda
akiendelea kumsoma taratibu kumjua
ni mtu wa namna gani. Hata
walipomaliza kula, walikaa tu hapo hapo
jikoni wakizungumza. Mbawala ndiye
alikuwa mzungumzaji mkubwa, Tunda
akimsikiliza na kumrushia maswali
machache tu kumuonyesha yupo naye kwenye
yale mazungumzo huku
kichwani akimpigia mahesabu.
Akaamua siku hiyo hatampa kitu, mpaka
siku atakayomlipia yeye mwenyewe
tiketi ya kurudi Dodoma.
Akamkabidhi zile karatasi za Kinny. Akamuuliza
lini ategemee kuidhinishwa. Mbawala akamwambia atajitahidi kuzungumza na mwenzake, ili aweke saini ya pili. Napo hapo akajinadi kuwa yeye ndio mwenye kauli ya mwisho, akaongea hili na lile. Ilimradi aonekane wa muhimu kwa Tunda aliyekuwa akimpigia mahesabu ni kiasi gani cha pesa atakacho mchomoa siku akirudi. Tunda alibaki kimya akimsikiliza tu.
Mwishoe
akaangalia muda kwenye simu yake,
na kumtumia ujumbe dereva taksii
kumtaka arudi pale kumchukua. “Nashukuru
sana kwa brunch. Naomba niondoke ili
niwahi ndege.” “Umeniahidi kurudi.” “Si tulisema weekend
ijayo?” “Unafikiri utaweza
kuja?” Mbawala akauliza kwa kubembeleza kidogo.
Kisha akaendelea. “Nitakutumia
tiketi na mimi mwenyewe nitakupokea
uwanja wa ndege.” Tunda akatoa
tabasamu huku akisimama.
“Nitakuona
jumamosi Mbawala. Nakushukuru
sana.” “Nilidhani unakuja ijumaa usiku, uondoke jumapili usiku!”
Tunda akatulia kidogo kama anayefikiria.
“Naomba nikujibu siku ya
jumatato. Kuna dili ya pesa nyingi
ijumaa usiku. Nitaangalia kama atakubali
tusogeze juma lijalo.” “Daah! Sitaki
nikuharibie bwana. Lakini ningependa
tupate hata siku mbili Fina. Naweza
hata kufidia hio pesa kama itabidi ili
tu nikupate kwa siku mbili.” Tunda
akacheka kidogo na kumsadiki. Maana
katika mazungumzo yake ya kujinadi,
alionyesha hana majukumu kabisa.
Pesa yake ni yake. Baba waziri, mama ana NGO yake mwenyewe tena nje
ya nchi, wamezaliwa wawili tu. Dada
Taffy naye msomi! Lazima pesa ipo.
“Nashukuru. Lakini miahadi yenyewe ni zaidi ya pesa ya siku moja.” Tunda akazungusha kiuungwana kidogo. “Kwa hiyo akikataa
tusogeze miahadi yetu, nitakujulisha ili
tupange wakati mwingine.”
“Yaani
tusogeze siku!? Heri hiyo siku moja
kuliko kukosa kabisa.” Wakasikia kengele
ya getini. Wakajua ni dereva taksi. “Naona amefika.
Tutawasiliana Mbawala. Asante
sana.” “Na mimi
nimefurahi umefika kwangu. Naamini
tutapata muda mzuri ukija.” “Naamini hivyo.” Tunda akambusu shavuni, akataka kutoka. Mbawala akamvuta mkono, Tunda akageuka. “Naomba nilipie garama za kuja na kuondoka hapa
kwangu.” Tunda akacheka.
“Huna sababu yakufanya
hivyo Mbawala!” “Wewe ni mgeni wangu Fina. Nilikualika mimi, sitaki safari yangu
ikugharimu bwana.” Tunda
akacheka sana. “Unanilipiza nini?” “Jana
ulinifundisha
tabia nzuri. Ukimwita mtu kwenye kikao,
ni kwa garama zako.”
“Sikumaanisha
unilipe bwana.”
Tunda
akakataa kiustarabu kumbe anashida na
kila shilingi inayokuja mbele yake. “Naomba unisubiri. Nilijiandaa.” Mbawala akaondoka pale na kurudi na habasha. Tunda akacheka huku akiipokea. “Asante.”
Akamtizama
na macho yake, Mbawala akatoa tabasamu
la kunogewa. Tunda akatoka huku akicheka taratibu.
Alipofika tu kwenye taksii akaanza kuhesabu zile pesa huku akicheka mwenyewe.
Hakuamini. “Hapa sijamvua nguo, nikimvua nguo atanipa kiasi
gani!?” Tunda akawaza huku dereva
taksii akiendesha kimya kimya. Akamuomba
wapitie sehemu mbili tatu,
ndipo akamuomba amrudishe hotelini.
Kwa Kinny tena!
Tunda alirudi hotelini akamkuta Kinny anamsubiri akiwa amejawa wasiwasi. “Bado umenikasirikia Fina?” “Hapana Kinny. Ila ningependa tuheshimiane. Mimi sio mtoto mdogo. Najua kitu gani nafanya.” “Nilikosa Fina.
Nisamehe mama. Tafadhali naomba yaishe.” “Yameisha. Na nimerudi na
habari njema zaidi.” Akamsimulia
walipofikia na Mbawala, hilo akaona
limemfurahisha zaidi. “Na mimi
nimekuandalia bahasha yako. Hii ni
kwa sasa. Ile tenda ikipita, nitakutafuta.” “Asante Kinny. Nashukuru.”
Tunda akapokea
na kuweka kwenye begi lake lakini akionekana amebadilika kabisa usoni. Ile furaha iliyokuwepo tokea wanafika, iliisha kabisa.
“Umenichukia Fina?” “Hapana.”
“Usinichukie
tafadhali. Naona kama tunaweza
kufanya mengi.”
Tunda
akacheka taratibu na kukaa mbele yake
akimtizama, kisha akatulia kama
anayefikiria kidogo, Kinny akajua
ameharibu kwa hakika. Fina huyu sio Fina
waliyekuwa naye jana na asubuhi hiyo
kabla hajaropoka. “Nafikiri mahusiano
yetu yabaki ya kikazi tu Kinny.” Tunda
akaanza taratibu tu na kuendelea. “Nimefurahi tumeweza kupata muda wa pamoja, na tenda yako naona ataipitisha bila shida. Sidhani kama Mbawala ni mtu kigeugeu. Kwa kumsikiliza tu, anaonekana anasimamia anachosema. Naamini
atakutafuta akupe majibu mazuri.” “Mbona kama unaniaga Fina?” Tunda akacheka
kinyonge kidogo.
“Nilipitia kukata tiketi
yangu ya ndege, naondoka muda mfupi sana
kuanzia sasa kurudi Dar. Naamini
tutaonana tena wakati mwingine.” Kinny akajirudisha kitandani kama aliyeishiwa nguvu kabisa. Tunda
akachukua vitu vyake,
akambusu shavuni, akatoka. Kinny
alipogeuka pembeni akakuta bahasha.
Akafungua ndani kwa haraka. Akakuta
pesa na kikaratasi
kidogo kimeandikwa, “Ni pesa ya
nauli uliyonigaramia kunileta huku
Dodoma. Asante.” Kinny akaumia sana.
Akahisi Tunda/Fina amemuona
ni mnyanyasaji. Akaogopa hata
kumpigia simu. Akarusha ile bahasha
mbali, ikagonga mlango na pesa zote zikamwagika chini sakafuni.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tunda aliondoka jijini Dododma akiwa amemuacha Kinny kitandani. Akiwa kwenye ndege akaanza kujifikiria. Akajichukia kidogo. Akaona Kinny amemdharau kupita kiasi. Lakini akajiambia hayo ni maisha, na lazima yaendelee tu. “Kwanza tusingeenda popote na Kinny! Mkewe amemjaa sana kichwani mwake.” Akawaza. Tunda hakutaka kuja kurudi chini. Nani anafuata baada ya Kinny kushindwa kuziba pengo la Sadiki? Jibu likawa Mbawala.
“Mbawala anaonekana anayo pesa
na nimtoaji. Sijamfanyia chochote, amenihonga na kunipa dili kubwa hivi!” Akawaza Tunda. “Na anapenda sifa, ndio maana amekazania jina la baba yake ili watu wajue kama ni mtoto wa waziri.” Akaendelea kukumbuka
mazungumzo yake akijisifia nchi
walizokwenda pamoja kama familia. Dada
yake ananyadhifa hii, mama yake ana
hili. Ilimradi tu kujigamba kwa
Tunda. Tunda akacheka. “Zitamtoka
huyu, mpaka achanganyikiwe.”Akajiambia Tunda akiwa kwenye ndege.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Juma hilo Tunda alilichukulia taratibu akijua akitengeneza kwa Mbawala, basi tenda ya Kinny itapita, Kinny atamlipa pesa zaidi. Bado hongo atakayomchomoa Mbawala
mwenyewe. Akaona ajipumzishe lakini bado akawa na wasiwasi. “Kweli Mbawala atamudu kuniweka mjini?” Akajiuliza Tunda. “Huyu ni kijana. Akianza
kunihonga mfululizo, atataka
kunimiliki. Mwishowe atataka nihamie
Dodoma. Kitafuata kutotumia
kondomu. Mwisho mtoto kama sio kuniua
kwa maradhi.” Hapo Tunda akastuka
na kukaa.
“No way. Hakuna kumtafuta Sadiki mwingine. Si mzee wala kijana. Atarudia maombi yaleyale kama Sadiki.
Kumzalia mtoto wa
kuunganisha undugu au ndoa kuwa
mke wa pili.”
Tunda akafyonza na kukusudia kutotafuta
mwanaume wa kumganda. Aliyapenda hayo
maisha yake matulivu ya kurudi nyumbani kwake
peke yake na kulala bila fujo baada ya
mahangaiko ya maisha. “Wote
wataniweka mjini. Wasijidai
wajanja.”
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tunda mikakati
mizito ili Maisha mazuri na matulivu yaendelee jijini. Atafanya nini? Usikose Muendelezo
kujua makubwa na mazito ya Tunda kwa wanaume wenye nazo kuanzia kichwani na
shahada zao mpaka mifukoni mwao.
0 Comments:
Post a Comment