Umekwisha Soma hadithi hii???
Maajabu ya Endles Love!
![]() |
Inawezekana ukawa umesoma makumi ya vitabu, mamia au hata maelfu, lakini kama hujasoma kile kiitwacho Endles Love “Upendo usio na kikomo” bado una deni.
Hiki ni kitabu cha pekee kinachompitisha msomaji katika maisha ya kawaida aliyowahi kupitia, anayopitia au hata yale atakayopitia mbeleni. Kinagusa maisha ya kimwili na yale ya kiroho ‘holistic’, lakini pia hakimuachi hewani, kila tatizo linapata ufumbuzi unamuwezesha mhusika kuendelea mbele.
Kitabu hiki kilichoandikwa na Naomi Mwakanyamale Ng’imba, kina kurasa karibu 300, lakini zinaonekana chache sana unapokisoma kutokana na mtririko wa matukio yenye kugusa hisia za kila mwanadamu. Ni kama maisha halisi yaliyohamishiwa kwenye kurasa za kitabu.
Miongoni mwa maajabu ya kitabu hiki ni jinsi kinavyotafsiri nguvu ya ajabu iliyopo katika ‘msamaha’. Lakini kikionesha jinsi upendo ulivyo na nguvu kushinda mauti. Mwisho wa kila tukio ni kuuelekeza moyo wa mwanadamu katika kumrejea muumba wake na kuishi maisha ya upendo, badala ya kujitesa kwa kuhesabu maovu ya nyuma.
Mmoja wa wanasaikolojia aliyekisoma kitabu cha Endles Love alisema: “Endles Love ni chuo cha maisha halisi ya mwanadamu, matukio yake kila mtu yanamgusa, alishayapitia au anayapitia, hakuna namna halisi ya kukichambua kwa uhalisia wake njia bora ni kila mtu kukisoma. Kinafunua siri kuwa maisha bila Mungu ni kama Pweza Jangawani, hata achanganye miguu kiasi gani ataishia kutimua vumbi, haendi popote.”
Wasiliana nami moja kwa moja ili kuweza kusoma simulizi hii na kuwa nayo kwenye viganja vyako, popote ulipo kwa
Whatapp namba +1205-767-8163
0 Comments:
Post a Comment