Jax aliumia sana. Alibaki pale akiwaza kwa muda na kuondoka. Akili zake zilikuwa zikizunguka ila akakusudia kumuonyesha dada yake yeye sio kama baba yake, na amekusudia kubadilika. Akaamua kwenda nyumbani kwa dada yake. Kwa kuwa ni yeye, mlinzi alimfungulia kwa haraka tu. Akaenda kuegesha gari kabisa na kuingia bila hodi. Dada yake akatoka chumbani. Akamsalimia, Nelly akabaki akimwangalia tu bila kuitika. Jax akaongeza. “Wewe funga tu mlango unapotaka kulala, mimi naingia kulala.” Nelly akabaki ameduaa. Kwamba usiku huo analala hapo kwake! Jax akaingia kwenye chumba chake ambacho hata Tino huwa anakitumia, kimya.
![]() |
Maisha ya Jax yakaanza hapo nyumbani kwa dada yake. Akarudi kuishi
na dada yake kama zamani. Nelly
hakumuuliza. Ila kumuona anatoka asubuhi, na kurudi nyumbani mapema tu
akiashiria hana pakwenda. Ila kumjali dada yake kukaongezeka mpaka Nelly akawa
anashangaa. Zawadi za hapa na pale hazikukoma. Na akiwepo naye nyumbani mara
amtengenezee chai ya jioni au kumtengenezea juisi kisha kumuwekea kabisa na
kumsogezea alipokaa. “Hii ina virutubisho vizuri na muhimu mwilini, unahitaji.”
Nelly akawa anajiangalizia tu na kunyamaza.
Maisha yakaendelea kwa ndugu
hao wawili. Wanaishi hapo wawili tu bila wenza ila ajira zao ndio zikawa ndoa.
Wote kujituma sana kazini. Na ukweli upande huo wa kazi walifanikiwa sana, ila
si kwenye mahusiano. Hata wao wenyewe wawili hawakuwa na muda wa pamoja wa
kufurahia kama ndugu. Wakiwa hapo kwenye nyumba hiyo kama hawaangalii taarifa
ya habari, basi kila mmoja macho kwenye kompyuta akifanya kazi za kiofisi. Siku
ikianza, wote barabarani kuwahi kazini. Magari yaliyoegeshwa hapo nje ya nyumba
ya Nelly, na jinsi wanavyovaa wakitoka hapo, ndipo utajua wamefanikiwa kifedha,
ila mbali na maisha ya kazini, hapakuwa na maisha mengine. Na hakuna aliyejua
kinachoendelea kwa mwenzie.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
B |
aada ya
maharusi hao watarajiwa kutengana na ndoa kushindikana, Jax akiwa kwa dada
yake, kwa upande wa Lara yeye maisha ya kaanza na kushika kasi huko kisiwani
Zanzibar akiwa hakuna anayejua alipo. Ila akafurahia kuishi asikojulikana
kashfa yake. Ile hali ikamsaidia kumuongezea ujasiri na kumtoa majonzi na
ikabidi afanye juhudi za makusudi kuchangamka ili kutoa maswali kwake ya moja
kwa moja. Akajulikana tu ni binti ambaye hajaolewa wala hana mchumba. Akakazana
kutumia dawa alizoandikiwa hospitalini alipokuwa na Jax, zakuongeza damu huku
akizingatia milo.
Haikuchukua muda mrefu kwa Lara kurudia hali yake ya zamani ila
safari hii sio na tabia za kisichana alizokuwa nazo. Lara alishajiona amekuwa
mtu mzima. Utoto uliisha siku anampoteza mtoto wake na Jax. Akarudia uzuri
wake, lakini mtulivu. Na kwa kuwa aliowakuta pale kazini ni watu wazima,
akakosa wasichana kama kina Suzy wakuzunguka nao kwenye starehe. Akajituliza.
Kazini, nyumbani kwake, basi. Hakutaka urafiki wa undani ambao itamlazimu
kueleza historia ya nyuma. Akakwepa ushoga.
Baada ya miezi mitatu kupita akiwa kazini siku ya jumamosi, waliingia wanaume wawili. Walionekana ni watu wazima kidogo. Lara aliona wakihudumiwa na mwenzao. Akaendelea na shuguli zake. Kukatokea kutoelewana kidogo na anayewahudumia wakaambiwa wasubiri. Akaitwa Lara. Lara akaenda pale. “Naomba uwasikilize wewe Lara. Naona mimi nikizungumza nao, hawanielewi.” Lara akawasalimia.
“Niwasaidie nini?” “Simu na laini yenye namba hizi. Ilikuwa simu
yangu, nimeibiwa.” Mmoja akaongea. “Hiyo ni rahisi tu. Naomba tuhamie pale
kwenye meza yangu.” Lara akawatoa hapo akijua waliposhindwana na muhudumu wa
kwanza.
Walikaa, Lara akaandika ile namba kwenye kompyuta yake likaja jina
kamili. Kabla hajamtajia, Lara akamwangalia. “Naomba kitambulisho chako chenye
jina kamili kama inavyoonekana wakati ukisajili hii namba.” “Ulisikia pale
alipokwambia kuwa ameibiwa mpaka waleti?” Mwenzie akauliza kwa ukali kidogo
kama asiyetaka kupotezewa muda zaidi. Lakini akashangaa muomba namba ambaye
ndio alikuwa mwenye kelele, amepoa. “Siwezi kujua kama wewe ndio...” Lara
akarudi kwenye kompyuta kutaka kusoma jina. “Jeremaya Kembo.” Akawahi huyo
muibiwa kabla Lara hajasoma jina lake kwenye hiyo kompyuta na kuongeza. “Lakini
wewe unaweza kuniita Jerry.” Lara na mwenzie aliyekuja naye na kujaribu
kumtetea, wakamgeukia. Mwenzie akashangaa kidogo.
“Niite tu Jerry.” Akaweka msisitizo akimtizama Lara kwa kutulia
kabisa kama siye yeye aliyekuwa akigomba mezani kwa mfanyakazi mwezie Lara.
Mwenzie akapigiwa simu, ikabidi kupokea na kuondoka. “Ninachotaka kusema ni
kuwa, nilazima kuwepo na kitambulisho kinacho...” “Nimeelewa kabisa. Kwanza ni
kwa ajili ya usalama wangu mimi mwenyewe na taarifa zilizopo kwenye hiyo simu
na laini yangu. Maana mwingine anaweza akawa mwizi tu, akaja hapa nakutaka laini
yangu mimi!” Gafla yeye akaonekana ndio anauelewa juu ya hilo kuliko hata Lara
mwenyewe, wakati ndio ulikuwa ugomvi wao na muhudumu wa kwanza waliyeshindwana
mpaka kuitwa Lara. Akajieleza hapo Lara akimsikiliza. “Uliniambia unaitwa nani
tena?” Ikaishia kutaka kujua jina lake. “Lara.” Lara akamtajia jina akicheka,
maana alianza na utundu maneno yakumfanya acheke.
Akatoka bosi wake akaonekana kumfahamu sana huyo mteja. Akamtamka kwa
heshima sana ‘Mr. Kembo’. Na kumpa mkono kinyenyekevu akamkaribisha ofisini
kwake. Akasimama na kuongozana na bosi wao ofisini kwake. Lara akajua ni mtu
mzito. Baada ya muda mfupi akaona bosi wake anampigia simu na kumuita ofisini
kwake. Lara akaenda kwa haraka. “Nimempa line yake lakini itabidi uongozane
naye hotelini kwake ukachukue vitambulisho vyake.” Lara akashangaa. “Si ulisema
umeibiwa waleti!?” “Huwa sitembei na hati ya kusafiria. Nacho si ni
kitambulisho? Bosi wako amekikubali, au wewe hukitaki?” Lara akababaika kidogo
akiwa na maswali kwa nini yeye mwenyewe asiende na kuleta! “Nimekuja na
usafiri, hatutachelewa.” Akaweka msisitizo, Lara akamwangalia bosi wake. Akaona
anamwangalia. “Sawa.” Wakatoka.
Walipanda kwenye gari nzuri sana mpaka Lara akashangaa. Ni kama
alishafahamu matajiri wa hapo mjini. Kembo hakuwa mmoja wao. Akatulia garini na
kupotelea mawazoni. Akamuona Jerry anamcheka, akageuka. “Sasa unanicheka nini!?”
“Bwana wewe ni muoga! Sasa hapo unaogopa nini?” “Mimi siogopi.” Lara akajibu
huku akijaribu kujiweka sawa. Yule aliyekuwa naye ndani akimtetea wakati
akiwahudumia alikuwa akiendesha, wao wakakaa nyuma. Lara aliingia hapo garini
na kupotelea mawazoni mpaka hapo anamsemesha.
“Umehamia lini huku Zanzibar?” Jerry akamuuliza kwa utulivu tu. “Sina
muda mrefu.” Lara akajibu bila kutoa maelezo mengi kisha na yeye akamuuliza.
“Kwa nini umeniuliza?” “Nakuona bado ni mgeni. Umeshapata wenyeji?” Lara
akasita kujibu. “Unapapenda huku?” “Sio pabaya.” “Umeshatembelea Bwejuu?”
Akamuuliza tena akicheka taratibu. “Hapana.” “Umeshapasikia lakini?” “Ndiyo.”
Lara akajibu kwa upole. “Ungetamani kwenda siku moja?” Lara akamtizama na
kunyamaza. Akageukia pembeni.
“Lara?” Akamuita tena. Lara akamgeukia. “Sijawahi kufikiria.” Lara
akajibu. Hapo ikabidi amtizame vizuri. Ni kweli tokea awe na Jax, Lara alikuwa
akitazama wanaume wote nakuwaona kama ndugu, kasoro Jax. Hata mtu alipoonyesha
nia ya mapenzi, hakuwa akielewa au hata hakutaka kufikiria mwanaume mwingine
upande wa mapenzi. Lakini hapo akajua huyo Jerry anarusha ndoano. Jerry
alimtizama kwa kutulia na tabasamu la kutongoza. Lara akatoa tabasamu na
kugeukia pembeni. Akamfikiria Jerry.
Alionekana ni mtu mzima, sio kijana. Lakini akamgundua sio wakawaida.
Pesa inamtindo wakunukia hata ikiwa haipo kwenye mfuko. Mwenye mafanikio na
aliyestaarabika haitaji kukwambia. Utaona tu. Lara akagundua pale yupo tajiri
na mfanyakazi. “Huwa mnafunga ofisi saa ngapi?” Jerry akamuuliza tena. “Siku za
jumamosi ni saa sita na nusu, lakini jumatatu mpaka ijumaa ni saa kumu jioni.
Jumapili mapumziko.” “Huwa unakwenda kupumzika wapi?” Akamuuliza tena. Lara
akiwa hamwangalii, ameinama akimjibu. “Bado sijaanza kutembea. Nilitaka kuzoea
kazi kwanza.” “Sasa umeshazoea?” Lara akatabasamu tu na kunyamaza akiwa
ameinama. Kisha akageukia pembeni. Yule dereva kimya.
Lara akashangaa gari inasimami mbele ya Verde hotel. Akashuka Jerry
akaenda kumfungulia mlango. “Nilifikiri nakusubiria hapahapa!” Lara akajihami.
“Ndani ya gari!?” Akamuuliza. Lara akajitizama. “Upo sawa. Twende. Tukikipata
utakihakiki kama jina ni langu na sura ni yangu, kisha tutashuka chini tena
kukinakili, ndipo uondoke na nakala yake. Twende.” Lara akashuka kwani safari
hii Jerry aliongea kikazi. “Asante.” Akashukuru Lara kiustaarabu baada ya Jerry
kumfungulia mlango na kuufunga. Dereva akaondoka. Lara na Jerry wakaingia
ndani.
Wakapanda kwenye lifti, Lara akifuata nyuma. Wakapandisha mpaka
gorofa ya pili tu, Jerry akaongoza njia mpaka chumbani kwake. Akafungua mlango
kwa kadi, mlango ukafunguka. “Karibu ndani.” “Asante.” Lara akashukuru na
kuingia mpaka ndani. Palikuwa pazuri sana. Safi. Kumepangiliwa vizuri. “Unaweza
kukaa tu.” Lara akaenda sehemu ya makochi, Jerry akaingia sehemu ambayo Lara
aliweza kuona kitanda. Akapotelea hapo, baada ya muda mfupi akarudi na hati ya
kusafiria na kumkabidhi. Lara akahisi mikono inaanza kutetemeka. Akafungua ili
kuhakiki kama ni yeye, akasoma jina na kumtizama sura. Jerry alikuwa ametulia
tu akimwangalia. “Naona sura ya hapa inafanana na wewe.” Lara akaongea
taratibu. “Basi kama umeridhika, twende tukakinakili pale mapokezi.” Lara
akasimama kwa haraka, na kwa hofu akamrudishia hati yake ya kuzaliwa kama sicho
kilichompeleka pale.
Kabla hajatoka, Jerry akamuita. “Lara!” Lara akageuka. “Hukunijibu
swali langu.” “Kama nimeshazoea kazi?” Lara akauliza. “Kumbe upo makini?” Lara
akacheka kwa hofu kidogo. “Nimeshazoea, lakini niliamua kutulia tu.” Ikawa kama
anajitetea. “Leo kuna simu muhimu sana nataka kuzungumza nayo ili kujua kama
nitaondoka hapa au leo nina baki. Ndio maana nilipoibiwa simu yangu
nilihangaika ili muweze kunirudishia line
yangu. Kama mambo yakienda sawa itanilazimu kuondoka na ndege ya mchana,
vinginevyo nitakuwepo mpaka jumatatu. Je, kama nitakuwepo ungependa kurudi kwa
chakula cha jioni?” “Hapana.” Lara akajibu bila hata kufikiria mara mbili.
Jerry akakunja uso. “Kwamba wewe huli?” “Kwamba sitaki kurudi hapa na
kula na wewe.” Lara akajibu bila hofu. “Kwa nini? Au umeshafikiria mbali na
ukajua nitakuwa nakutaka kimapenzi?” Jerry akamuuliza kwa kumsuta. “Naomba
niwahi kabla hatujafunga ofisi.” Lara akatoka. “Unarudije ofisini?” Jerry
akamfuata nyuma. “Nitajua nikishapata hiyo nakala.” Wakajikuta wamesimama
kwenye lifti. Akamsikia akicheka tena.
Lara akageuka. “Bwana usiwe unanicheka!” “Kwani una miaka mingapi
Lara?” “Sitaki.” Jerry akacheka zaidi. “Sasa unacheka nini!?” “Unavyoogopa!
Sasa hapo unakimbia unafikiri nitakubaka?” “Mimi sikujui.” “Kwa hiyo unafikiri
na mimi nitakubaka tu nikiwa sikufahamu? Hujui kubakwa pia ni bahati? Kwamba
aliyekubaka inamaana amekuamini.” Lara akamwangalia kwa mshangao.
“Kweli Lara! Sasa unafikiri mimi nitakuita hapa, nikiwa nimekuona tu
leo, halafu nikutake kimapenzi! Ukiniua kwa maradhi! Au kwa kuwa nimevutiwa na
wewe ndio unafikiri mimi ni malaya wakutupwa! Kila ninakoenda nakusanya
wasichana!” “Mimi sijui!” “Sasa si ungekuta nguo za kike chumbani kwangu au
mwanamke kabisa! Unafikiri kwa nini nilikukaribisha wewe mpaka chumbani?” “Mimi
sijui Jerry.” Lifti ikafunguka Lara akapanda kwa haraka. Jerry naye akaingia.
“Sasa unakimbilia wapi wakati hata hati yenyewe huna Lara!?
Utarudisha nini ofisini? Tulia bwana!” Jerry akaenda kusimama mbele yake.
“Pumua.” Lara akabaki akimtizama huku anarudi nyuma. Jerry akaanza kucheka
tena. “Ujue hapo ndio mwisho. Na hapa kwenye hii lifti kuna kamera. Siwezi
kukubaka Lara! Naomba vuta pumzi kwa nguvu, ili kutoa hiyo hofu iliyokuingia.”
“Mimi napumua vizuri tu na sina hofu.” “Sio kweli. Mpaka mabega yako
yanaonekana upo na tension. Yapo so stiff!” Lara akainama. “Mimi sio mtu
mbaya. Naomba tulia. Sitakufanya chochote kwa kuwa na mimi naheshimika sana
kwenye jamii. Siwezi kukubali msichana niliyekutana naye tu, akaniharibia
heshima. Ni baba na watoto pia. Ukipiga kelele ukisema nimekubaka, hudhani kuwa
nitapoteza kila kitu?” Kidogo Lara akafikiria na kutulia. Lifti ikafunguka
akatoka.
“Lara?” Jerry akamuita taratibu. “Upo sawa?” “Ndiyo.” Lara akajibu
wakiwa wamesimama pembeni ya lifti. “Upo sawa sababu upo hapa au kwa sababu
umenielewa?” “Nimekuelewa.” Akajibu taratibu. “Nashukuru. Basi twende tutoe
kopi, ili uwahi kazini. Na samahani kama nimevuka mipaka na nikakuudhi.” Jerry
akaongea akibembeleza. “Hamna kilichoniudhi.” “Basi twende.” Wakasogea
mapokezi. Wakapata huduma ya nakala, akamkabidhi. “Asante.” Lara akashukuru.
“Sasa yule dereva si wangu. Huwa namtumia tu nikifika hapa. Ni wa rafiki yangu.
Huwa namtumia ninapotaka kutoka tu, nikimaliza shughuli zangu namruhusu. Ni
sawa nikikuchukulia taksii itakayokurudisha ofisini?” “Nitashukuru.” Gafla
Jerry akawa wakubembeleza, Lara akapoa kabisa.
Wakatoka hapo ndani wakaenda pamoja mpaka nje. Akamtafutia taksii,
akasubiri akapanda tena kwa kumfungulia mlango. Ikamgusa Lara. “Nashukuru
Jerry. Uwe na wakati mzuri.” “Naomba nijulishe ukifikishwa salama. Au nitakuwa
nimezidisha?” “Hapana. Nitakujulisha.” Lara akatoa cheko la aibu na kuinama.
“Nimeshalipia, usilipe tena.” “Asante.” Akamfungia, dereva akaondoa gari. Lara
akabaki akimfikiria Jerry. Akacheka. Akakumbuka hiyo hali yakujaliwa. Akacheka
na kuinama peke yake.
Alifika ofisini mambo yakawa mengi akifunga week. Mpaka saa nane ndio
akatoka. Alipofika nyumbani na kutulia, ndipo akamkumbuka Jerry. Lakini
akagundua hakuchukua namba yake ofisini. Akajichukia kuona Jerry alikuwa
muungwana vile lakini ameshindwa kumjulisha! Akafikiria chakufanya, mwishoe
akaona akamtizame tu kama bado yupo pale hotelini.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Lara akaoga. Mtoto wa kike akajitengeneza kama enzi zake akiwa
anatoka. Mwenyewe alijua amependeza. Akarudi hotelini. Akafika mpaka ndani. Akataka
kumuulizia pale mapokezi, lakini akajiambia ni heri apitilize tu wasije kumzuia
na kama ana msichana, akamfumanie. Akapanda kwenye lifti mpaka gorofa ya pili
huku akijiambia endapo atagonga mlango usipofunguliwa, atajua hayupo, na
ataondoka. Akaanza kujishitukia akijiuliza kinachompeleka pale ni nini!
Akajisuta akiwa amekaribia mpaka mlangoni. Mwishoe akajiambia sio sawa. Aondoke
tu. Haraka sana akaondoka bila hata kugonga mlango.
Jerry.
B |
aada ya
jumamosi nyingine moja kupita, ya pili tokea akutane na Jerry, Lara akiwa
amekaa mezani kwake ana kazi, akashitukia Jerry amekaa mbele yake. “Jerry!”
“Nahisi kama nilikusoma kwa haraka Lara. Na katika kukusoma kwangu, uongo
haikuwa moja ya sifa nilizoziona unazo.” Jerry aliongea akisikika kulalamika.
“Sikukudanganya Jerry!” Akatoa simu yake. “Hii ni simu na line niliyonunua
hapahapa kwenu. Inaingia simu zote za watu waliowahi kunitafuta, na hakuna
aliyenilalamikia kwamba alinitafuta na kunikosa!” “Kwa sababu sikupiga, Jerry.”
“Sasa kwa nini uliniahidi kitu ambacho ulijua usingeweza kutimiza?” Lara na
Jerry waliendeleza mazungumzo hapo ofisini, Jerry akiwa amekaa kama mteja na
akizungumza kwa sauti ya chini tu.
“Siku ile niliporudi hapa, nikakuta nimepewa wateja wengi na bosi
alikuwa anawahi kuondoka. Akaniachia ofisi. Nimetoka hapa saa nane, nikiwa
nimesahau kuchukua namba yako ofisini kwa bosi. Kumbuka ulihudumiwa na Bosi, na
akawa amefunga.” Jerry akageuka kuangalia ofisi ya bosi wake Lara. Lara akajua
anachomaanisha. Kwamba mbona yeye anapaona pako wazi! Inamaana kumefungwa mpaka
sasa! Akarudisha macho kwa Lara.
“Siku ile alikuwa amefunga
Jerry. Na huwezi amini nilirudi mpaka pale hotelini.” “Lara!” “Sidanganyi
Jerry. Nilirudi.” “Niliondoka. Lakini ulishindwa vipi kunipigia hata jana!”
“Kumbuka uliniambia wewe ni mtu wa familia. Ningejuaje kama ni sawa kukupigia
tu?” Hapo akamuona Jerry ametulia.
“Nimerudi.” “Utakuwepo kwa siku ngapi?” “Inategemea. Sipo kikazi.”
Lara akamtizama kidogo na kurudisha macho kwenye kompyuta. Akamtolea kadi na
kumuwekea mbele yake. Lara akaivuta na kuisoma. “Nitakupigia. Safari hii
naahidi nitapiga.” Akaiweka kwenye pochi yake. “Nitakuwa hotelini nasubiria.”
“Unasubiria nini!?” Lara akawa kama hajaelewa. “Nasubiria simu yako au hukuwa ukimaanisha?”
“Nitapiga Jerry.” Hapo hapo akamtumia ujumbe na jina lake. ‘Lara’. Akautuma.
“Nimekutumia ujumbe. Ujue safari hii namaanisha.” Jerry akatabasamu na
kuangalia simu yake.
Akamuona anaandika kitu kwenye simu yake kisha akamwangalia. “Haya.
Nimeitunza. Na mimi naruhusiwa kupiga wakati gani?” “Wakati wowote ule.”
“Unamaanisha?” “Kabisa Jerry. Naishi peke yangu na sina mtu anayeangalia simu
yangu, ni mimi tu.” Hilo likamfurahisha Jerry. “Swali la mwisho kabla
sijaondoka.” Lara akamwangalia. “Itachukua muda gani kufikiwa ujumbe wangu?”
Lara akawa ameelewa. Akacheka kidogo. “Hakuna mtu mwingine Jerry. Hakuna
msururu wa wanaume wenye namba yangu.” “Asante.” Akashangaa anaondoka bila
yakuongeza neno. Inamaana ndicho alichomaanisha na amepata jibu alilotarajia.
Lara akacheka taratibu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Lara alitoka hapo ofisini akampigia mara alipofika tu nyumbani kwake.
“Ni mimi Lara.” Lara akajitambulisha. Akamsikia
akicheka. “Pole na kazi.” “Asante. Pole na wewe.”
“Nilikwambia kama nipo tu mapumzikoni? Sipo kikazi.” “Sasa unafanya nini kwenye
hayo mapumziko?” Lara akauliza. “Nakusikiliza
wewe.” Lara akacheka akishangaa. “Sikutanii
Lara. Hata ukinikaribisha nikutembelee kwako nitakuja tu.” Lara
akacheka. “Naishi uswahilini mwenzio. Chumba kimoja na
hakuna A/c feni la mezani.” “Kama wewe unaweza kuishi hapo, na mimi nitaweza kuishi
tu.” “Hutapaweza. Unataka tukale sehemu? Sijala mchana.” “Hapa wanavyakula
vizuri. Karibu.” “Asante.” “Kwa hiyo unakuja?” “Basi nioge kutoa jasho ndipo
nije.” “Ujue nakusubiri.” Lara akacheka na kukata simu. Akaanza
kujitayarisha.
Mida ya saa kumi akawa anagonga mlangoni kwa Jerry. Safari hii
ilikuwa gorofa ya tatu. Jerry akamfungulia na tabasamu kubwa. Alikuwa mtu
mzima, lakini alionekana anajipenda sana. Msafi kwa kumtizama, hata mwili wake
alionekana ana utunza vizuri. Hakuwa mnene kabisa. Akampisha mlangoni.
“Nimekuletea zawadi kutoka safari. Lakini sijui kama utapenda!” Lara akakunja
uso. “Mimi!?” “Nipo hapa na wewe Lara. Sizungumzi na mtu mwingine.” Lara
akacheka.
Jerry akaelekea ndani. Akamtolea mfuko. “Najua wewe ni mrefu futi.”
Akamtajia. “Niliangalia mkono wako nikakisia. Nafikiri sijakosea.” Lara
akashangaa sana. “Na harufu niliyoipata siku ile kutoka kwako, naamini kwa aina
hii ya parfume sijaenda mbali.” Lara akamwangalia na kufungua mfuko akiwa bado
na mshangao.
Akakuta pafyumu na saa nzuri sana ya mkononi. Akamwangalia tena.
“Hivi vitu ni vya thamani sana Jerry! Kwa nini umeninunulia mimi!?” “Nafikiri
nimevutiwa sana na wewe, Lara. Ndio maana nimerudi ili kukwambia. Halafu kama
utakubali, tuanzishe mahusiano.” Jerry alikwenda moja kwa moja kwenye pointi
mpaka Lara akabaki anamshangaa.
“Samahani Lara. Mimi nimuwazi sana. Halafu siishi hapa Zanzibar.
Kusema nitachukua mambo taratibu nijivute ndio baadaye sana nikwambie. Nikija
hapa nakuja sababu za kibiashara tu. Na pia sio kijana na sitarudi kuwa mtoto.
Sina muda wakupoteza. Nikishajua nataka kitu, kuwa situlii mpaka nikitafute na
kukipata.” Lara akabaki akimwangalia nakushindwa ajibu nini.
Jerry akakaa pembeni yake. “Lara?” “Uliniambia unafamilia Jerry! Mimi
naingilia wapi!? Sitaki kuwa mvunja ndoa.” “Usiwe na wasiwasi. Hutavunja ndoa
yangu na wala hutaingilia chochote kwenye ndoa yangu.” Lara akawa hajaelewa.
“Ndio itakuaje!?” “Nina watoto wawili wakubwa tu. Ni mapacha, wapo wakiishi na
mke wangu kwenye mji unaitwa Virginia. Mke wangu na watoto wanaishi huko. Na ni
vijana wakubwa tu, wanaingia chuo mwaka huu mwishoni.” Lara akajiweka sawa.
“Nilikuwa na mahusiano mengine. Lakini yale nilikuwa na mke wa mtu.
Tuka...” “Jamani Jerry wewe ni muwazi kupitiliza bwana!” Jerry akaanza kucheka.
“Nivumilie nimalize. Pagumu panakaribia kuisha.” Lara akamtizama. “Basi
napunguza ukali wa maelezo.” “Hapana. Lakini sijawahi kukutana na mtu kama wewe!”
Jerry akacheka. “Basi nimalizie kwa kusema niliachana naye. Amerudi kwa mumewe,
wakaamua kuongeza mtoto mwingine. Imeshapita miezi nane sasa tokea tuachane.”
“Sasa amepata mtoto?” “Sidhani. Maana mara ya mwisho nilimuona akiwa hana tumbo
na hiyo ni miezi mitatu iliyopita.” Lara akashangaa. “Sasa hukumuuliza?”
“Sikuona sababu kwakweli. Kwa kuwa hainihusu tena.” Lara akamtizama.
“Na sina UKIMWI.” Akaongeza na kuzidi kumshangaza Lara. “Ila tunaweza
kwenda kupima tena tukiwa pamoja ili ujiridhishe na mimi. Ila mimi nimeridhika
na wewe. Kwanza nimevutiwa na kila kitu chako. Nakutaka Lara. Na mimi huwa sio
mzuri wa jibu la hapana. Nitakung’ang’ania mpaka unikubali.” “Kwa hiyo mbali na
mimi, unawasichana wengine wangapi?” “Kwa kuniona hapa, ujue ni wewe peke yako
mbali na mke wangu. Kingine, mimi sio mtu wa wanawake wengi. Kwa hiyo usiwe na
wasiwasi. Mtakuwa wawili tu, na mke wangu. Ila ningependa kujua kama unakuwa na
mahusiano mengine. Mimi ni muoga sana wa magonjwa. Na sitaki kumua mke wangu
tukaacha watoto wetu.” Lara akahisi ni kama anasikiliza hadithi. Akaweka ule
mfuko chini.
Jerry akacheka na kusimama. “Nikuagizie chakula gani? Nataka tule
hapahapa chumbani tufahamiane zaidi.” “Hapana Jerry. Mimi sipo tayari kueleza
chochote kinachonihusu.” “Kwa nini!?” “Kwa sababu ya nyuma ni machungu matupu.
Na ndio maana nilikimbilia huku na nimebaki bila rafiki kwa kuwa sitaki
kuzungumzia maisha yangu ya nyuma.” Jerry akafikiria kidogo. “Mara ya mwisho
kupima UKIMWI ilikuwa lini na umejamiana mara ya mwisho lini?” Lara akamtizama
na kutingisha kichwa. “Naomba na hilo lisiwe siri Lara. Mengine ni sawa.”
“Naomba twende hospitalini tukapime upate majibu yako, tafadhali. Lakini si
kukueleza maisha yangu ya nyuma.” “Wazo zuri.” Kama utani, Lara akashangaa
anachukua waleti na kutorudi pale. “Twende.” Lara akacheka kama haamini
wakatoka.
“Unafikiri mimi nakutania? Nipo hapa kwa ajili yako Lara. Sipo
kikazi. Nimerudi juzi kutoka kwa familia yangu. Japo nilipeleka mzigo wa
biashara kule, nimerudi ndio nikakufuata. Nilikuwa nakifikiria hicho kiumbo
chako kila wakati!” Lara akacheka mpaka akainama. “Bwana Jerry!” “Nakwambia
ukweli. Sidanganyi. Unafikiri ingekuwa mtu mwingine angenitoa hapa kwenda
kupima UKIMWI kama sio kwamba nakutaka kwa hali na mali!” “Bwana Jerry!” Jerry
akazidi kumcheka Lara aliyekuwa amejificha uso wakiwa wamesimama kwenye lifti.
Akampitishia mikono kiunoni na kumvuta karibu. Lara akajisogeza karibu mpaka
mwilini mwake. Jerry akamkumbatia vizuri. Akashangaa Lara anatulia hapo. Kimya.
Akahisi analia. Akamchungulia pale kifuani, akagundua analia.
Jerry akamvuta pembeni. Akamkumbatia vizuri na kumbusu. “Naruhusiwa
kuuliza?” Lara akatingisha kichwa kukataa. “Okay. Basi tutasimama hapa mpaka
utulie. Au unataka turudi ndani?” “Twende
hospitalini. Mimi nipo sawa.” Lara akajaribu kujifuta machozi. “Hiyo ni
kazi yangu.” Akamfuta machozi kama mtoto, mpaka Lara akacheka. “Ujue mimi
mkubwa!” “Sio ukiwa na mimi. Ukiwa na mimi wewe ni babe wangu.” Lara akajisikia
vizuri. Akacheka kwa kudeka.
Walikwenda hospitalini. Wote wakatolewa damu. Wakakaa hapo
wakisubiri. “Ukikutwa umeathirika, nitasikitika!” Ilimbudi tu Lara acheke. “Kwa
nini?” “Ninakutamani sana. Sitaki maradhi yatutenganishe.” Lara akamwangalia na
kushindwa kuongea. Akaishia kucheka. “Mimi sina maradhi Jerry. Sijajaamiana
nafikiri zaidi ya mwaka sasa.” Jerry akatoa macho. “Hivyo ulivyo wewe!”
“Nikoje?” “Mrembo hivyo, hujapata wakukuganda kama mimi!?” “Sikutaka tu.” Lara
akajibu na kuinama. Jerry akajua kuna stori nzito hapo. “Basi nakushukuru kwa
kunipa mimi nafasi.” “Nani amekwambia kama nimekukubali?” Jerry akacheka
sana.
“Unacheka kwa sauti bwana Jerry, mpaka watu wanatugeukia sisi!”
“Mwenzio sina chakujificha. Sasa niambie nafanyaje ili nikupate Lara? Ila
nataka kukwambia utakayoyapata ukinikubali. Furaha. Kila ukiwa na mimi utakuwa
na wakati mzuri. Huo ni uhakika. Hata ukitaka usifanye kazi ila kutumia tu, ni
juu yako.” Lara akashangaa sana. “Sikutanii. Wewe ukitaka uwe na mimi kila
wakati, ruksa. Kasoro kwa familia yangu tu. Lakini kwengine hamna shida. Halafu
ujue nitakujali, sitakuumiza. Mimi ndivyo nilivyo. Acha nijisifie. Nimejaliwa
kupenda na kujali hasa nikipata mwanamke anayetaka kupendwa. Mengine utajionea.
Utashangaa wewe ndio unaning’ang’ania. Nipe usiku wa leo tu, uone kama kesho
utataka kuondoka.” “Nani amekwambia usiku wa leo nitalala na wewe!?” “Basi
naanza kukuomba Lara. Naomba usiku wa leo usiniache peke yangu. Nimekuja kote
huku kwa ajili yako, kweli utaniacha peke yangu!?” Lara akainama akiwa
ameshalainika.
“Lara?” “Mimi sikufahamu Jerry!” “Nakuruhusu uniulize chochote
unachotaka na nakuahidi sitakudanganya, ili tu unifahamu hivyo unavyotaka.”
Lara akamwangalia na kuinama tena. Akamshika shingo na kumwinua. Palepale
hospitalini akaanza kumbusu. Lara akanogewa na hilo busu. Jerry alijua kubusu!
Lara akajisogeza karibu akiwa ameshikwa vizuri, wamekaa tu wala
hawajakumbatiana. Akaendelea kumbusu mpaka akamuona amelainika palepale.
Akamuachia. Lara akajishitukia na kuinama. Akamvuta mkono. Akaubusu na
kuukumbatia. Wakatulia. Akamuona anamuegemea begani kama mtoto mkiwa
anayehitaji mapenzi. Jerry akamzungushia mikono na kumkumbatia vizuri.
Walitoka hapo na kurudi hotelini wote wakionekana hawana maambukizi
yeyote kwamba afya zao ni nzuri. Waliagiza chakula chumbani. Wakati wanakula
Jerry akaanza. “Unahisi nina miaka mingapi?” Lara akamwangalia. “Kisia tu.”
“Mwishoni mwa 40.” Lara akajibu, Jerry akacheka. “Nina miaka 55. Nilichelewa
kuoa na kuzaa sababu ya kutafuta pesa. Na sikutaka watoto wengi. Mmoja tu, ndio
maana mke wangu akahangaika kuzaa mapacha. Kwamba mara moja. Tunalea mara moja,
halafu basi.” Mpaka hapo Lara akajua anachotaka kumwambia. Akapoa.
“Nilikwambia mimi nimuwazi Lara. Nataka tukubaliane mapema na
unielewe ili kusijekuwa na kutokuelewana au kuumizana. Sitaki uje uumie. Sio
kutoka kwangu. Nina malengo ya pesa tu kwa sasa na nipo busy mno. Sina muda
wakulea. Na mimi kwangu mtoto sio kitu kidogo. Hao watoto wanaolelewa na mama
yao, wananigarimu sana. Muda na pesa, kwa sababu sitaki wakue bila mimi au
wahisi sikuwa na malengo wakati wanazaliwa. Inanilazimu niwepo kwenye maisha
yao kila wanaponihitaji. Katika uzima na ugonjwa. Najitahidi kuwepo kila wakati
wanaponihitaji kitu kinachonifanya niahirishe shuguli zangu nyingi. Ninachotaka
kusema ni kuwa..” “Hutaki kuzaa na mimi.” Lara akamalizia.
“Ukiiweka hivyo inakuwa chungu kidogo. Ila ni kwamba sina muda na
sitaki kuongeza mtoto mwingine hata kwa mke wangu. Na yeye kuna wakati
alijaribu sana kunishawishi tuongeze mtoto, lakini ilibidi kumuweka wazi. Kuwa
hataongeza na mimi. Mimi ni baba wa wawatoto wawili, basi. Sina nafasi ya
watoto wengine. Kwa yeyote yule.” Jerry akaweka msisitizo, kidogo ikamuumiza
Lara.
Jerry akaendelea. “Hata hao mapacha ilikuwa shuguli sana kukubali.
Nilitaka mtoto mmoja tu.” Lara akabaki ameinama. Akamkumbuka Jax na mtoto
waliyempoteza. Akakumbuka alivyokuwa tayari kuzaa na Jax aliyesema asingekuwa
na shida na kuzaa naye. Jerry amekuwa muwazi tokea mwanzo. Lara akawa
anajiuliza kama aondoke au la. Moyo ulishatibuka.
“Naomba usifikirie mbali wakati nipo hapa na wewe. Niulize chochote
Lara. Tafadhali usikate tamaa na kuniona mimi ni mbaya. Nina uhakika haukuwa na
mpango wa kuzaa na yeyote yule. Na ninauhakika unampango wa kuwa na familia
nzuri, na mimi nina familia yangu. Huoni kama nimekuwa mtu mzuri kwako,
sijakudanganya?” “Labda sijaelewa, niulize. Unachotaka kutoka kwangu ni nini?”
Lara akauliza taratibu tu.
“Kampani yako. Nakuhitaji kwenye maisha yangu. Mimi na wewe tu. Na
nimefurahi kujua kwa sasa huna mtu. Kwa hiyo tutakuwa huru kuwa popote
tutakapokubaliana kuwa bila kuongeza jukumu jingine la watoto. Utakapokuwa
tayari kuanzisha familia yako, uniambie tu, tutazungumza na kukubaliana.” Lara
akavuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha. “Sio ngumu Lara. Nakuahidi wakati mzuri.
Nakuhakikishia. Labda ushindwe mwenyewe. Huna haja yakuishi huku. Labda upende.
Wanachokulipa hapo, naweza kukupa kwa mwaka mzima. Ukaweka benki na kuendelea
kuwa na mimi tu. Hata ukitaka kufanya hiyo ndio kazi yako, sina shida.” Lara
akakunja uso.
“Labda niweke hivi, wanakulipa mshahara kiasi gani, kwa mwezi?” Lara
akainama. “Niambie tu, usione aibu.” Lara akamtajia. “Sasa hiyo zidisha kwa
mwaka, mara tatu, nitakupa uweke benki kwa kuwa na mimi tu. Ukichoka kukaa tu,
ukataka kazi, tutatafuta.” Jerry aliongea kirahisi mpaka akamshangaza Lara. “Na
kwa kuwa mimi nina akili ya biashara, ningekushauri ufungue kitu chako
ujiajiri.” Lara akahisi ni kama anamdanganya. Ila kwa nini! Jerry amekwenda
mpaka kutoa damu! Akanyanyua uso akaona anamwangalia.
“Kwa nini ufanye hivyo!?” Lara akamuuliza. “Labda ungeuliza hivi, kwa
nini nafanya hivyo kwako wewe. Si ndio swali lako?” Lara akabaki akimwangalia
kama anayetaka kumsoma. “Lara?” “Mimi naona unazidi kunichanganya Jerry!” Jerry
akaanza kucheka. “Usichanganyikiwe, wewe niulize tu. Na nimekusaidia kuweka
swali vizuri. Sasa ni hivi Lara. Kwa nini wewe, ni kwa sababu nimevutiwa na
wewe. Sitafuti mke wa kuoa wala kuzaa watoto. Hicho kipengele nimefunga.
Ninachotaka ni msichana mdogo, mzuri wa sura na umbile. Sasa vyote wewe unavyo
ndio nilipokuona, nikakutizama mpaka vidole vya mikono, nikajua ndio kitu
nataka.” Lara alichoka mpaka akabaki ameduaa. Jerry akazidi kucheka.
“Yaani wewe nimeshakupigia mahesabu yote ndio maana nikarudi. Maana
nilikuwa nakufikiria zile siku nitakazokuwa nikiamka pembeni yako!” Lara
akanyanyuka na chakula chake. Jerry akazidi kucheka. “Unaweza kujiuliza kwa
ninavyozunguka kote huko sijaona wasichana wengine?” Lara akasimama na
kumgeukia. “Nawaona lakini unakuta wanavimapungufu fulani fulani. Halafu
wamejaa mpaka wanakera! Hawapo kama hivyo wewe, mtulivu na unaunyenyekevu
fulani hivi. Hujikubuu! Sio lishangingi. Upo kitoto kitoto, unaweza kujaa
mkononi. Halafu mzuri. Mpaka midomo yako mitamu! Pale hospitalini nilikuwa
natamani nisiku..” Lara akaondoka. Jerry akazidi kucheka. “Sasa mbona unakimbia
sifa zako! Lara?” Lara akaenda chooni na chakula chake. Akamsikia akizidi
kucheka kule alipomuacha, yeye akaendelea kula huko chooni.
Mwishoe akamfuata. “Sasa kwa nini unakula huku chooni?” “Nakukimbia
Jerry.” Jerry alicheka mpaka akakaa chini kabisa. “Njoo ukae hapa ule. Mimi
nitanyamaza.” Lara akaenda kukaa pale pembeni yake. Lakini chini hapohapo chooni
wakiwa wamekaa sakafuni kabisa. Akaanza kula tena, kimya. Akala mpaka akamaliza
bila Jerry kuzungumza kitu.
Lara akamwangalia. “Sasa unafanya nini hapo?” “Nilikuahidi kuwa kimya
ili umalize kula. Na sitaki kukuacha peke yako, wewe ni mgeni wangu.” “Asante
kwa chakula.” “Umetosheka?” “Kabisa. Twende na wewe ukale.” “Mimi imeshatosha.
Nimekwambia miaka yangu. Nipo hivi nilivyo mpaka ukadhani ni mdogo kihivyo ni
kwa kutoa mlo wa usiku. Ndio maana unaniona hivi.” “Kweli una mwili mzuri!” “Na
mazoezi. Chakula kwangu ni kwa ajili yangu sio mimi kwa chakula. Si hata kitabu
cha Mungu kimeandika?” Lara akamtizama na kunyamaza.
“Umeamua nini?” “Juu yako?” Lara akamuuliza. Jerry akacheka. “Juu
yetu sio yangu mimi. Huhitaji muda mzuri na mtulivu?” “Nataka.” “Sasa kwa nini
unajifikiria wakati mimi nakuahidi wakati mzuri na ahadi nzuri kiasi hiki!
Hutakaa ukapata mwanaume kama mimi Lara. Mkweli na mwenye pesa!” Lara akacheka.
“Unafanya biashara gani?” “Una muda kiasi gani wakunisikiliza juu ya biashara
zangu?” Lara akacheka na kusimama kwenda kuosha mkono, Jerry akasimama na yeye.
Akamfuata pale kwenye sinki nyuma yake akaanza kumbusu shingoni. Huku
akimpapasa taratibu. Lara akajikausha mikono Jerry akiendelea kumbusu na
kumnusa shingoni. Lara akacheka. “Unanitekenya!” Akamsikia akicheka kidogo na
mikono ilishaingia ndani ya gauni kupitia chini akinyanyua gauni taratibu mpaka
mikono ikafika kiunoni na kurudi kwenye makalio huku midomo yake ikiwa shingoni
kwa nyuma mpaka pembeni akimbusu. Raha aliyokuwa akiisikia Lara, alitamani
kugeuka lakini Jerry alikuwa amesimama nyuma yake akiendelea kumpapasa kwa
shauku, hakutaka kumtoa hapo. Akahisi anamtoa nguo ya ndani huku mikono
ikimzunguka kama aliyekuwa akimuona kwa mikono na hisia. Jerry alikuwa amefunga
macho.
“Lara.” Akamsikia akimuita taratibu. Lara akatulia tu. Akamtoa nguo
zote akiwa vile vile amesimama nyuma yake, kisha akamnyanyua na kumuweka juu ya
sinki. “Nilijua tu siwezi kukosea. Upo vilevile kama nilivyokudhania.” Jerry
alikuwa akimwangalia pale alipomuweka. “God!
you are beautiful Lara!” Akamsifia kwa kumaanisha. Lara akacheka na
kujificha uso. Akamsikia akimbusu tumboni kwenye kitovu huku akipandisha juu
taratibu mpaka midomoni. Yeye bado alikuwa ana nguo zote.
Alimtoa hapo na kwenda kumlaza kitandani. Lara mwenyewe alijua Jerry
anamfurahia hatua kwa hatua. Ila aligundua amependa hips zake. Wakati mwingi
kwenye mapenzi alikuwa akimalizia mchezo akiwa amezikamata kwa nguvu huku
akivuta hisia. Alipokuwa anampakata huku mapenzi yakiendelea, midomo haikutoka
kwenye matiti na mikono kwenye hips zake ndipo alipokuwa akimaliza na kumuona
amefurahia zaidi. Na anapokuwa amemuinamisha, basi lazima atazishikilia hizo
hips za Lara kwa nguvu ndipo anamsikia mpaka akigugumia. Lara alijua ameupenda
mwili wake na kuufurahia, kitu kilichomuongezea ujasiri na yeye akatulia kufurahia
mapenzi hayo yenye ahadi ya utajiri tu.
Na kweli alipata usiku mzuri. Jerry alijua anachokifanya na hakuwa
mwenye papara. Alifanya naye mapenzi hatua kwa hatua. Mpaka wanamalizia penzi
la asubuhi kabla hawajatoka kitandani, Lara mwenyewe hakutaka kuondoka hapo.
“Jumapili huwa unafanya nini?” Jerry akamuuliza wakiwa bado wapo kitandani. “Napumzika, nafua na kufanya usafi
kwenye chumba changu. Ulitaka niondoke sasa hivi?” Jerry akamgeukia vizuri.
“Kwa haya unayonipa hapa, nishaanza kufikiria maisha bila wewe.” Lara
akajifunika mto na kumfinya. Jerry akacheka. “Upo kama nilivyokutarajia, ila na
zaidi. Mpaka naona shida kukuacha.” “Bwana Jerry!” Akamsikia akicheka. Lara
akatoka kwenye mto. “Tuondoke wote basi.” “Twende wapi?” “Tukaishi wote Dar.”
Lara akawa kama hamuelewi.
“Halafu kuja huku utakuwa ukinisindikiza kwenye biashara zangu. Nakuahidi hutapata shida na sitasubiri uniombe kitu. Nimejaliwa kujali.” “Wewe ni mtu wa namna gani!?” Jerry akacheka sana na kumvutia juu ya mwili wake, Lara akawa amemlalia. “Bora nijisifie mwenyewe maana hakuna atakayeweza kukueleza habari zangu vizuri isipokuwa mimi mwenyewe. Nitakupenda Lara, mpaka mwenyewe utashindwa kuniacha.” Lara alicheka sana mpaka akajificha shingoni kwake. Jerry akaanza kumpapasa.
“Unanifurahia?” Lara akakubali kwa kutingisha kichwa. “Sasa
kwa nini unasita kuchukua hatua nyingine? Au kwa kuwa sijaanza kwa
kukudanganya?” Lara akacheka na kutaka kutoka hapo mwilini, Jerry akamvuta.
Lara akamwangalia. “Una midomo mitamu, Lara! Nibusu tena.” Lara akachangamkia
penzi la mara ya pili asubuhi hiyo.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mpaka siku ya jumatatu Lara alishindwa kuondoka hapo. Alichofanya ni
kumtumia ujumbe bosi wake kumwambia anaumwa. Jerry alikuwa akicheka tu. “Na
kesho utamwambiaje?” “Utakuwa umeondoka Jerry, na kuniacha niendelee na shuguli
zangu.” Jerry akazidi kucheka. “Mimi nina mpango wakuendelea kupata raha mpaka
jioni ndipo niondoke hapa. Usinifukuze na kunipunja kwa kushindwa kuamua kwako.
Mimi nimeamua ni wewe. Raha unayonipa, nimeamua kuipokea wala sijivungi. Kwanza
kazi yenyewe wanakulipa mshahara mdogo! Sijui kwa nini unaing’ang’ania!” “Ukija
kunikimbia nitaishije?” “Ndio maana nakwambia nakulipa mshahara wako wa miaka
mitatu kabisa. Halafu unakuwa na kazi yakustarehe tu.” “Hivi wewe unamaanisha
kweli!?” Akatoka na kuelekea kwenye mkoba wake.
Akamuona anatoa kitabu cha hundi, akaandika na kumkabidhi. “Ukienda kuweka hii kwenye akaunti yako, inakuwa pesa.” “Jerry!” “Watu wanafanya kazi na kupata pesa, halafu hawajui kutumia pesa zao kuwapatia raha. Mimi nina pesa, wewe unacho ninachokitaka. Sasa kwa nini unashangaa! Nakutaka Lara.” Ikawa kama utani. Lara akakubali. Akaanzia benki. Akaweka ile hundi. Alipoona pesa imeingia kwenye akaunti yake, akaenda kuandika barua ya kuacha kazi, kisha akarudi hotelini kwa Jerry. Jerry akapiga simu kuongeza tiketi ya pili yakurudi jijini siku inayofuata.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kipi kitaendelea,
usikose muendelezo...
0 Comments:
Post a Comment