Akiwa ofisini, akapata ujumbe. ‘Unajua kama mkeo amegoma kufanya kliniki? Tokea mtoto alazwe, amegoma kwenda. Na leo ni siku yake, pia amegoma kutoka hapa. Mdogo wako alikuwa hapa kumuelezea umuhimu wa kliniki zake kwa kipindi hiki, pia amekataa kutoka hapa.’ Andy akavuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha. Ulikuwa ujumbe kutoka kwa mama mkwe wake.
Hata yeye alishasahau maswala ya kliniki. Alijua wazi kumtoa Mina pale haitakuwa kazi rahisi. Akafikiria kwa haraka. Alikuwa na mkutano dakika chache zifuatazo. Na ilikuwa muhimu. Akamjibu mama mkwe wake. ‘Nashukuru kwa taarifa. Muache, nitakuja baada ya lisaa.’ Akajibu hivyo na kuendelea kujiandaa na kikao.
~~~~~~~~~~~
Alipomaliza tu kikao akaaga sekretari wake na kutoka. Njiani akampigia simu Paul. “Nimezembea kliniki ya Mina.” “Mama yake aliniomba nizungumze naye. Nikamtafutia daktari palepale ambaye angeweza kumuona, lakini pia amekataa kwenda.” “Kwa muda huu tutakuwa tumechelewa?” “Acha nimpigie nitakujulisha.” “Nashukuru. Narudi hospitalini. Popote atakapokuwa, ukiniambia, nitampeleka mimi mwenyewe.” “Sawa.” Akaendelea kukanyaga mafuta mpaka hospitalini.
Kabla hajashuka garini Paul akampigia. “Anaweza kuwaona sasahivi.” “Nashukuru sana. Unaweza kuzungumza naye kama anaweza kumpokea kabisa kwa sasa, au tumeshachelewa?” “Kwamba ahame kliniki yake ya hapa?” “Unajua hawezi kutoka pale chumbani kwa muda mrefu. Ni bora ahamie tu hapahapa. Ili ikifika siku ya kujifungua kama yuko hapa, wajue jinsi ya kusaidia.” “Nitazungumza naye ili taarifa zake zihamishiwe kwake.” “Ni vipimo gani anatakiwa kwa ujauzito wake leo?” “Kwa kuwa anaanza, atataka kufanya kila kitu.” Akawa amemfikia mdogo wake. Wakakata simu na kuendelea kuzungumza.
Akamkabidhi kikopo kidogo cha mkojo, Andy akaelekea alipolazwa Ayvin. Akafika nakumkuta Mina amepiga magoti kitandani kwa mwanae, wazazi wake na mama Ron wamekaa kimya tu.
~~~~~~~~~~~
“Hilo shati jeupe baba!” Andy akacheka. “Nyinyi kwenu ni wasafi sana! Kwenu wote mpo wa safi, kila wakati!” “Baba yao huyo. Nilipata shida mwanzoni aliponioa, mpaka nikamzoea. Basi akaambukiza vijana wake wote utafikiri wanaambizana!” Mama Ruhinda akadakia. “Wanakuwa kile ulichowakuza wewe.” Mama Ron akaongea kama akimpongeza mama Ruhinda.
Hapo Andy kiatu cheusi kinang’aa, kama kioo! Suruali ndio nyeusi haswa, halafu shati jeupe, peee! Koti la suti na tai aliacha garini.
“Pole na kazi.” Baba yake akamwambia. “Asante. Si nyinyi bado mtakuwepo hapa?” “Sisi tupo.” “Na mimi sitoki mpaka Raza aje kunipokea.” “Basi natoka na Mina mara moja, hatutakawia.” Mina alishituka akageuka.
“Tunakwenda wapi tena!?” “Njoo hapa bafuni tuzungumze.” Akamnyooshea mkono kabisa kumsaidia kusimama. “Tunakwenda wapi?” “Nimepata daktari wa kukuangalia wewe na Ayvan.” Akaanza kulia. “Sisi wote ni wazima Andy!” “Hutaki kwenda kumuangalia na Ayvan?” Akamuuliza taratibu.
“Nataka, ila kaka yake mgonjwa, sitaki nimuache peke yake.” “Wazazi wapo, watakuwa naye kwa muda mfupi wakati tukiangalia hali ya mdogo wake. Nimeomba apimwe, na tumuone. Haitachukua muda mrefu.” “Kunakuwa na foleni kubwa!”“Nakuahidi hatutakaa sana. Daktari anakusubiria wewe tu. Njoo tuchukue kipimo cha kwanza." Akamshika mkono kumuongoza chooni.
“Nimekumiss Mina!” Wakamsikia akizungumza naye kwa upendo huku akifunga mlango wa upande wa bafu. “Na mimi nimekumiss Andy, sema mtoto anaumwa sana. Akili inakuwa kwake tu, nashindwa kufikiria kitu kingine. Ila unajua nakupenda.” “Najua Mina. Leo umemuombea?” “Kila saa naomba.” “Usilie sasa. Unaamini atapona?” Wakasikia kimya.
“Eti Mina?” “Nahisi nimeingiwa hofu Andy. Naomba huku nahisi pengine Mungu hajanisikia.” “Pole. Ila tufanye kile tunachoweza. Tuendelee kumsihi Mungu juu yake na ndugu zake. Unamuombea na Ayvan?” “Nasahau.” Huwa ni muwazi hivyohivyo.
Baada ya muda wakatoka. “Akibadilika hali, kwa namna yeyote ile, mnipigie. Au..” “Usiwe na wasiwasi mama, wewe ndio utakuwa wa kwanza.” “Asante baba. Na msije mkaondoka. Asije akamka akajikuta peke yake. Au mimi nibaki Andy, wewe peleka kipimo.” Hapo machozi mpaka kifuani, ashabadili mawazo.
“Kwa kuwa mtakuwa hapahapa, na sio mbali, akifungua tu macho, tutawapigia simu nyinyi wakwanza.” Baba yake mkwe akamuwahi. Andy akaongeza. “Yaani kabla hajaanza fujo zake pale kitandani, sisi tutakuwa tumeshafika hapa.” Kidogo akacheka. Akamwangalia pale kitandani, kisha akaanza kulia tena. Mikono kichwani. “Mungu wangu niamshie mwanangu jamani!” “Pole Mina. Pole mpenzi wangu, lakini naomba ukumbuke mambo mawili ya msingi.”
Akamgeuza kabisa amuangalie yeye. “Cha kwanza, hata kama Mungu ameshajibu, hataamka pale leo kwa sababu yupo kwenye nusu kaputi. Wamemlaza mpaka amalize dawa wanazompa, kisha wajiridhishe yupo sawa.” “Lakini kweli!” Akaongeza mama Ron, na kuendelea.
“Kwamba hata ukitoka hapa, huku nyuma hataamka.” “Kabisa mama. Na siku wanamuamsha, wote tutakuwa hapa. Hakuna atakayemuamsha bila wewe. Na pili, sasa hivi una Ayvan ambaye hana tegemeo jingine lolote isipokuwa wewe. Utakapopandishapressure, jua utamdhuru Ayvan. Na najua hutaki kumpoteza. Au hujali tena?” “Najali. Najali sana. Napenda wanangu wote. Sema sitaki kumpoteza hata mmoja. Twende tukamuangalie anaendeleaje. Nakuwa na hofu tu, najisahau. Ila na Ayvan namjali.”Wakatoka akijaribu kutulia, mumewe akimfuta machozi.
~~~~~~~~~~~
“Na Andy ndiye anayemuwezea Mina. Bila hivyo asingetoka hapa.” Mama Ruhinda akacheka taratibu kwa masikitiko. “Paul katumia akili yote ya kidaktari, nikaona amegonga mwamba, anamuitikia vizuri, ila hatoki. Na nikajua anamkubalia ili amuache, atoke, yeye abaki hapa. Nikasema nimtafute mumewe.” “Kumbe wewe ndiye uliyemuita Andy?!” “Ilibidi. Maana nilijua hatatoka hapa, na Paul ataendelea kupoteza muda, akirudi kumuulizia, jambo haliishi.” “Hii hali inatia wasiwasi sana.” Mzee Ruhinda akaongeza na kunyamaza.
~~~~~~~~~~~
Mina alikutwa na pressure ya juu, na hana maji ya kutosha mwilini. Mkojo ulikuwa mchafu. Wakaambiwa waongeze umakini kipindi hicho cha mwisho. Andy akaeleza wanakopitia. Paul alikuwa hapo akisikiliza kwa pembeni, akamtumia ujumbe huyo daktari kwa siri kuwa anahitaji kulala kabisa, amuandikie dawa ya usingizi ila asimwambie Mina mwenyewe. Kisha akamtumia huo ujumbe kaka yake hapohapo. Andy akasoma, Mina hajui.
Kwa hakika Andy akashukuru kuona mdogo wake amewaza sahihi kabisa. Ili kumtoa Mina magoti siku nzima. Akaambiwa aongeze kunywa maji lasivyo atawekewa dripu. Akakubali kuongeza kunywa maji. Maana ilikuwa kula yake ni mpaka Andy amsimamie, vinginevyo alikuwa anafunga kavu bila hata kunywa maji, na tumbo hilo kubwa lakujifungua.
Paul akatumia tena ujumbe watu wa familia kuwa Mina anapumzishwa, ila atakuwa chumbani kwa mtoto wake, watu wasiende jioni hiyo na asubuhi, ili alale kabisa. Andy akaona huo ujumbe kwenye kundi lao la familia, akajibu akimshukuru tena Paul, Mina asijue anaongelewa yeye kila kona.
~~~~~~~~~~~
Akaomba wazazi wake wakamchukue Ayvin shuleni na kuwa naye, akamruhusu Mama Ron aondoke. Akala vizuri na kumeza dawa asijue ni za usingizi. Akaanza kusinzia. “Njoo tuombe kwanza ndipo ujipumzishe.” Hilo akalifurahia. Akaongoza maombi yeye mwenyewe akilia, mpaka Andy akasema ‘Amina’, akamuweka kifuani hapo kochini, ambapo panageuka kitanda, haikuchukua muda, akapotelea usingizini kwa uchovu. Alilala asijue alipo.
Pumu Ilipopata Mkohozi
Kwa shuguli ndefu ya mapenzi siku ya jumapili, walilala na kuamka jioni wakabaki wakipapasana kitandani. Waliagiza chakula, wakala na kurudia mapenzi ya muda mrefu kila mmoja akitaka kumridhisha mwenzie wakiendelea kutoana upweke.
~~~~~~~~~~~
Usiku walilala kwa kuchelewa. Lakini Tuma akawa wakwanza kuamka. Japokuwa aliamkia chini ya kwapa la Jerry, akiwa amemuwekea mkono mwingine juu, alijua bado amelala kwa jinsi alivyokuwa akipata pumzi zake sawia. Akashindwa kutoka kitandani akimuhurumia asimuamshe.
Tuma akabaki akiwa hapo kitandani ametulia na kujawa furaha, bado haaminikinachomtokea, kama aliyeokota lulu usingizini, anaomba Mungu asiamke. Akabaki akiwaza vile maisha yake yatakavyojaa Jerry! Furaha ikazidi kuongezeka. Ila akakumbuka Jerry si mume, hayo yana mwisho. Akaanza kunyong’onyea alivyokumbuka kuna kutengana tena.
Akiwa amepotelea mawazoni akaona anavuta mkono wake kama anayetaka kugeuka. Akapata nafasi ya kutoka kitandani. “Mbona unaniacha sasa?” Akageuka. Jerry akamwangalia na kujinyanyua. “Umeota ndoto gani, mbona imekunyima raha?” “Hamna kitu. Wewe lala tu. Naenda kuoga.” “Njoo kwanza.” Akijua hayupo sawa akamtaka arudi kitandani. “Naenda kutumia choo. Nilibana mkojo sikutaka kukuamsha.” “Usioge bila mimi.” Tuma akacheka akijua anapenda kuchezewa huko bafuni maana ndio wimbo alikuwa akiimba jana siku nzima.
“Tuma! Usije nisahamu.” “Narudi.” Akaenda kutumia choo na kurudi. Akakaa pembezoni mwa kitanda.
“Niambie ni nini kimekunyima raha?” “Hamna, mbona..” Akataka kukataa ila akaona hamna sababu. “Ni nini?” “Tutarudia maisha yetu ya zamani Jerry! Hivi vyote leo ndio mwisho.” “Sio lazima leo ikawa mwisho.” Tuma akabaki akimwangalia.
“Umeniambia unanipenda Tuma. Si ndivyo?” “Lakini hatuwezi epuka uhalisia wa maisha!” “Ambao ni upi?” “Hatuwezi ishi hivi, hata kama umesema utakuja nioa, lakini kabla ya ndoa hatuwezi ishi pamoja, Jerry!” “Ndio nauliza kwa nini? Au unahofia Eli?” “Na yeye pia. Sio sawa aone nimehama nyumba kimyakimya. Kwanza mimi sijazoea.Sifanyagi hivyo.” Jerry akakunja uso kidogo akikumbuka kuelezwa habari zake na Mbaki. Akataka kumuuliza lakini akashindwa. Akaanza mara kadhaa, akashindwa.
Ila akaishia kumtaja Mbaki kwenye sentensi zake zilizoshindwa kukamilika, na Tuma akamuelewa. “Ndio maana Mbaki alinitafutia nyumba nzuri, yeye ndio alikuwa akija kulala kwangu, au tunasafiri. Sikutaka kuishi naye unyumba kabla ya ndoa au kuzaa naye kabla ya ndoa, na hayo nilimwambia tokea mwanzo. Na hapo ujue ni maisha niliishi naye kabla ya kuwa na Eli.” “Nimeelewa. Tutakuwa sawa Tuma. Naomba tusikaribishe wasiwasi wa kesho wakati ndio tumeianza siku ya leo. Mwenzio bado nakuhitaji.”
Akajisogeza na kumtoa shuka alilokuwa amejifunga mpaka juu ya matiti na kuanza kunyonya moja alilolifikia. Alilinyonya taratibu, mpaka Tuma akajilaza. Akamtoa chuka kwa juu na kuendelea kumnyonya akipapasa jingine huku akipikicha chuchu. Alikuja kugundua matiti ndio sehemu ya kwanza na kubwa inayomlainisha Tuma.
Akatoka kitandani na kumbeba eti mpaka bafuni. “Umenikata Jerry!” Akamcheka na kuanza kumkiss huku akimchezea mwili wake. Wakafanya romance hapo bafuni waking’ang’aniana kama wenye kiu! Katikati ya romance akaona anamchukua mkono, anamuweka kwenye kokwa zake. Akamcheka nafsi kwake akijua mchezo aliupenda, ashaanza kuzoea.
Akajituma mtoto wa kike. Lakini asubuhi hii hakutaka kupigia bao mdomoni, akamnyanyua na kumuinamisha. Akaanza kujiingizia huku akimchezea kisimi. Ukageuka uwanja wa mapenzi asubuhi hiyo ya saa nne.
Aluta kontinyua…
Huku kwa Sandra yeye akapata waraka wa majibu ya ule ukaguzi. Eti akaambiwa hali ya hilo jengo ni mbaya SANA. Hatari, mtu yeyote hawezi kuendelea kuwepo hapo. Wanatakiwa kutoka mara moja. “Sasa tunatoka bila hata notice!? Na mali zangu je?” “Umeona huu ufa hapa? Upo mpaka juu. Muda wowote hili paa linaweza shuka. Akaambiwa mengi ya kitaalamu na ya kuogopesha, mpaka akasalimu amri.
Wakati akiwaza wapi pakuhamisha mali zake. Maana alikuwa na magari hapo nje zaidi ya 10, ambayo ni ya watu japo anawadai, wasipo lipa ni yake. Asingeweza kukurupuka tu, lakini napo aliambiwa kesho yake watafika hapo kuanza ujenzi, ifikapo mwisho wa siku hiyo, wawe wameondoka.
Wakaachwa na sintofahamu ya hali ya juu! Lakini hilo jambo zima lilivyopelekwa mpaka kufika hapo, Rodrick akaona si jambo la kawaida. Akamfuata Sandra ofisini kwake. “Kwani mwenye hili jengo ni nani?” “Muhindi mmoja hivi lakini.…” Hapo akamuona anakunja uso kama anayejaribu kuvuta kumbukumbu baada ya kusita.
“Nini?” “Niliambiwa paliuzwa, kuna kampuni ilinunua. Sikufuatilia kwa sababu ni Jerry ndiye aliyekuwa akishugulikia maswala ya pango au tuseme hapa kwa jumla. Hata sijui alikuwa akilipa kodi kiasi gani! Halafu…” Ikawa kama anafunguka macho.
“Nini?” “Kwenye bajeti ya mwezi, sikumbuki kuona garama za malipo ya hapa!” Ndipo wakaanza kusaka sasa kujua kwa miaka yote hiyo kama 6 ni nani alinunua hapo! Wote macho kwenye komputa ya Sandra. Wakaanza kusaka. Kuperuzi nyuma kwenye barua pepe za miaka 6 hadi 10 iliyopita.
Ndipo wakakutana na barua pepe iliyomtaarifu hilo eneo kuuzwa kwa… “Hii ni kampuni ya JJ!” Rodrick alishituka sana alipoweza soma jina la kampuni waliyonunua hilo eneo. Ndio Sandra kuweka mikono kichwani. Kushakuchwa.
“Mungu wangu!” Akasikika Sandra. “Hakika nawashitaki na mimi! Hawawezi nichezea akili.” “Kwani mlikuwa mkimlipa kiasi gani?” Ikabidi Rodrick kumuuliza dada yake. Hakuwa na jibu lakini haraka sana akaenda kwenye ukurasa wa bajeti za hapo za kila mwezi alizokuwa akisimamia na kupanga huyohuyo Jerry.
Walisaka juu mpaka chini, hamna kitu. “Kwani wewe hukuwa ukihusika na bajeti kabisa?!” Rodrick akauliza akimshangaa dada yake maana ni kama gafla kila kitu ilikuwa ni Jerry! Yeye hana taarifa!
“Yeye ndiye aliyekuwa akipanga bajeti nzima, mimi naidhinisha.” “Sasa hiyo ya pango uliyokuwa ukiidhinisha iko wapi?” Sandra hajui, wote macho kwenye kurasa ya bajeti.
Miaka nenda, miaka rudi, hawakuona garama yeyote iliyoorodheshwa kulipia hapo. Sandra akashangaa sana, asielewe jambo kama hilo aliweza vipi kutojua!
“Kwamba yeye Jerry hakukwambia kama mlikuwa mkipanga hapa bure, HAMLIPII?!” Mdogo wake akamuuliza swali ambalo hakuwa na jibu nalo. Kwa ukweli alikuwa akimdharau SANA Jerry. Ilikuwa yeye ndio aongee, Jerry asikilize. Hakuwa hata akimtilia maanani anapozungumza jambo. Kwanza alikuwa akimkatisha kila anapozungumza, wazi kuonyesha hakuwa akimsikiliza tokea mwanzo au anazungumza ujinga. Jerry naye alipokuwa akikatishwa, ananyamaza tu. Haendelei kuzungumzia hilo jambo, kuepuka neno baya atakaloambiwa hata mbele za watu.
Sandra akabaki akivuta kumbukumbu bila kufanikiwa kupata kitu. Akajua inawezekana alishamwambia, LAKINI hakumtilia maanani, na pengine hata alimjibu hovyo.
Kwa hiyo wakati siku yake imeharibika, huku kwa Jerry yeye alikuwa akichezewa kokwa zake na kunyonywa! Wapo ulimwengu miwili tofauti. Yupo na Tuma wakitoana upweke. Na mbaya zaidi, hakuna jinsi ya kumfikia tena. Jerry aliyekuwa akimdharau, amegeuka mali hadimu. Huko aliko Jerry alikuwa akiomba ulimwengu mzima usimame, pasiwe jumanne anapotakiwa aanze majukumu mazito aliyoyaomba kwa kaka yake.
Pale Bahati Inapokuja Ila Kwa Kuchelewa
Walikuwa wakiangalia picha za shuguli ya siku iliyopita. “Umebahatika mama yangu.” “Katika umri huu! Na kule nilikopitishwa na baba yenu, halafu na haya anayonifanyia Jo, hakika hakuna jinsi nyingine ya kueleza ila kusema maombi ni akiba, Pam. Japokuwa nilipita pabaya sana, tena kwa muda mrefu, lakini nakumbuka maombi niliyokuwa nikiomba kabla ya kukutana na baba yenu, nahisi ni kama Mungu aliyaficha sehemu, ndio anayajibu sasa.” Akaendelea Dorothy, taratibu.
“Nilikuwa nikiomba! Aisee nilikuwa muombaji Pam.” “Bibi aliniambia ni kama ilikuwa huduma yako!” “Kabisa. Kufunga na kuomba lilikuwa jambo nasikia kiu nalo. Ikanisaidia kujitunza kwelikweli, ile yakutotaka kumkosea Mungu. Sasa nilipokuja kuangukia kwa baba yenu! Mpaka nikawa najiuliza, hivi huyu Mungu niliyekuwa nikimuomba yupo au la! Hapo nikayumba sana.”
“Maana yalikuwa ni maisha ambayo!” Akawaza. “Sijui niseme nini, ila jua ni maisha hata wanyama hawawezi ishi vile. Sasa nikabaki nikimshangaa Mungu niliyekuwa nikimuamini, halafu kuja kukutanishwa na mtu kama baba yako! Nikashangaa sana maana napo pia nilishaombea mwanaume atakayekuja kuwa mume wangu. Na alianza kwa heshima sana. Hakuwa mwehu vile, mpaka nyumbani wakaamini nimebahatika haswa.
“Ndio baadaye nishaingia kwenye ndoa, ndio sasa nikawa najiuliza, ‘kweli huyu mtu ndiye majibu ya maombi yangu kweli, kutoka kwa Mungu!?’ Hakika sikuwa nikiamini. Ile juhudi ya maombi na jibu lenyewe! Haviendani kabisa!”
“Alipozidi kunitesa na nikawa sina kimbilio, ananifungia, ndipo nikakumbuka tena faraja niliyokuwa niikiipata magotini. Nikarudia kuomba.” “Kwamba uliacha?” “Kabisa! Maana nilijiambia pengine Mungu hayupo, nazungumzaga peke yangu. Maana kama kweli nilikuwa nikiomba vile, nakuja kukutana na mtu kama yule! Sasa huyo Mungu ni Mungu gani! Basi nikarudi kuomba.”
“Japokuwa mambo yalizidi kuwa mabaya kwenye ile ndoa, lakini baada ya kurudia maisha ya maombi, nikawa na amani moyoni, nina nguvu ya kuendelea mpaka majirani walikuwa wanahisi nina tatizo la akili, sio mzima.”
“Kwa nini?” “Mwanaume analeta wanawake mpaka ndani, kitandani kwetu Pam! Tena si kwa kujificha ni kwa kuniambia nitoke, niwapishe! Halafu wakati mwingine ananipiga! Na mimi bado tu nipo! Kweli!?” Mpaka Pam machozi yalimtoka. “Pole mama. Sasa kwa nini na wewe ulibakia?”
“Hata sijui Pam! Sijui ilikuaje, ilikuwa kama kipindi ambacho na mimi akili ipo kwenye mshituko, sijui chakufanya! Nimepigwa na kibumbuwazi. Nimepoteza dira. Halafu nafikiri kuna upande fulani nilikuwa nikijiambia pengine ningekazana kwa hili na lile, angekuja badilika! Hata sijui!” Akawa kama anayejaribu kuvuta kumbukumbu za machungu.
“Halafu kumbuka nilishakuwa na nyinyi. Sikuweza kuwaacha. Kwanza alikuwa akinifungia, hataki hata nizungumze na majirani. Sasa useme ningetoroka, na nyinyi!?” Pam akazidi kuumia.
“Alikuwa mchoyo sana, yule wakuhesabu mpaka finyango! Kwanza pesa hatoi. Siku akitoa, hamtalala kwa amani. Masimango na kulalama. Wanawake anaoingiza hapo si mmoja wakueleweka kusema nikimuachia watoto, watakuja lelewa. Hapana. Maana kitendo cha kubadili vile wanawake inamaana na wenzangu walishamuona anamapungufuwakawa wanamkimbia.”
“Na kingine tena, ningewaacha na nani na yeye alikuwa mwajiriwa? Kutoka asubuhi kurudi jioni kama si usiku. Jumatatu mpaka ijumaa. Halafu hakuwa hata akiwajali! Nikashindwa kuondoka kabisa.”
“Lakini kitendo cha kuja kunirudisha kwetu, japo kilikuwa cha aibu na kibaya, mimi nilihisi Mungu amenijibu.” “Mmmh!” Pam akachoka kabisa.
“Kabisa Pam. Mungu anajibu kwa njia zake. Halafu kuja kukutana na Jo hivi!” “Bwana anakupenda Jo!” “Hakina ananipenda tena sio yakujisingizia, mpaka amewashangaza nyumbani. Babu yako anashangaa ule utayari wa kulipa mahari yote! Mpaka kaka akamwambia mahari huwa haimalizwi!” “Nakumbuka.” Wakaanza kucheka.
“Mill aliniambia anataka ndoa ya haraka.” “Ndivyo alivyoniambia na mimi. Sasa sijui ni kwa sababu anataka tukaishi naye!” “Sasa na wewe kwa nini hutaki kwenda kwake tena?” Akamuona kama anayefikiria.
“Lakini hata baba yako sikulala naye mpaka ndoa, Pam!” “Mama wewe!” “Hakika tena. Mimi vyahivyo siviwezi Pam.” “Na uzee huo mama wewe!?” “Najua havieleweki. Lakini naona kama…” Akasita. Kisha akafikiria.
“Nafikiri nimejiwekea tu mwenyewe. Japokuwa kwa upande mmoja najiambia mbona kwa baba yenu nilisubiria, na akaja kuniumiza! Lakini pia upande mwingine najiambia pengine kule kujinyima kwangu pengine Mungu amekuona, ndio ananilipa kupitia Jo!” Pam akapoa.
“Hata sijui! Lakini huko rohoni mwangu havijanikalia sawa. Kimwili natamani, lakini nahisi rohoni itanitesa sana kuja kuona nililala naye kabla ya ndoa. Hata yeye Jo nimemwambia. Inaweza isilete maana kwake, lakini kwangu imejengeka mpaka rohoni. SIWEZI Pam. Siwezi kulala hovyohovyo! Eti kesho niamkie kitandani kwa mwanaume asiye mume aliyehalalisha Mungu! Hakika hapana. Kama ataweza subiria mpaka ndoa, sawa, akishindwa basi.”
“Au ni ile siku ya kwanza ulipoenda kwake alikutisha?” “Pengine, lakini pia najiambia ukute Mungu aliniepushia ile siku nisijeanguka majaribuni. Hebu niambie ndio ningelala kwake, asubuhi inampata ile hali ya mkewe! Ningeumia zaidi, nakuona ni kama baba yako anarudishwa kwangu tena. Au aliyokuwa akiyasema kwangu ni sahihi, Jo amethibitisha mimi kweli ni takataka. Ingeniuma sana.” Pam akatulia akifikiria.
“Labda ndio maana anaharakisha maswala ya ndoa! Nasikia amemwambia Mill, atakayeweza kufika kwenye harusi yenu sawa, atakayeshindwa atamtumia picha. Hatasubiri.” “Kwamba hata hao wanae hatawasubiria tena?” “Alivyomwambia Mill, hatamsubiria mtu. Taratibu za kanisani zikikamilika tu, na tarehe iliyopangwa ikifika salama, yeye anaoa.” Akawa kama anaunganisha matukio.
“Ndio maana anamsumbua sana dada yake, kwenye maswala ya nguo yawe tayari kwa haraka! Dada yake alikuwa akiniambia lazima juma hili tuipate hiyo nguo, lasivyo Jo atarukwa akili. Anataka kila kitu kiwe tayari ibakie kusubiria tu siku yenyewe.”
~~~~~~~~~~~
“Hongera mama yangu.” “Na wewe hongera. Mill amenionyesha nyumba yenu.” Pam akaanza kucheka. “Huamini!” “Hata siamini mama! Ila anahangaika sana tuondoke nchini kabla siku za kujifungua. Sasa sijui!” “Ungemuacha aende kwanza Pam!” “Akipotea huko kama safari ile!” “Hawezi. Kwa jinsi nilivyozungumza na Jo, kurudi huko ni muhimu na itawasaidia wote. Anavyosema yule binti ya dada yake, kazi yake iliishia kwenye kukamilisha ule mkataba wa nyumba. Sasa kuanzia hapo, nyumba imeshakuwa yenu, hausiki tena. Inatakiwa sasa yeye mwenyewe aende.”
“Sasa Mill anataka kwenda na Shema! Kweli mama!” “Itaongeza uzito. Maana mwanao ni raia jina tu. Hata huko nchini kwao hajafika. Kule kuingia na kutokakutaongeza kitu hata kwenye mambo yako.” Akamshitukia.
“Mbona unazungumza na mimi kama uliyetumwa!” Mama yake akacheka. “Umetumwa na nani? Mill?” “Mill amezungumza sana na mimi. Ikabidi kwenda kuyathibitisha kwa Jo. Ndio akanieleza umuhimu wa Mill na Shema kuingia pamoja na kutoka. Shema aingie kwenye system zao, kuthibitisha kuwa yupo. Ameenda huko Marekani. Akakaa kwao hata kama ni kwa siku chache, na kurudi kwako. Jo ameniambia ni muhimu sana, maana uhamiaji wa huko wana sifa nyingi za utapeli za watu wa huku au wageni wengi wanaotaka kuhamia nchini kwao. Kuwaaminisha kwa vitendo pekee ndio itakayosaidia.” Pam akapoa.
“Tutakuwa wote Pam. Na Mill amesema hataacha safari hii ujifungue bila yeye. Popote utakapo kuwepo, siku ya kujifungua lazima awepo. Ameniambia safari hii hana sababu ya kutokurudi au hata kutafuta mwanamke huko. Ashapata uraia. Anayo familia. Hana sababu ya kutorudi kwako. Jipe muda wa kufikiria, uamue.” Pam akarudisha macho kwenye simu kuendelea kuangalia picha za shuguli ya mahari ya mama yake siku iliyopita, nyumbani kwa mjomba wake. Kilikuwa kitu kidogo, lakini nzuri sana.
~~~~~~~~~~~
Mill alimuona ametulia usiku huo. Hata alipokuwa akimpapasa na kujaribu kuzungumza na mwanae huko tumboni, Pam alikuwa kama hayupo hapo. Akavuta mto pembeni yake. “Unawaza nini?” “Ukiondoka na Shema, mtarudi lini?” Mill akatulia akifikiria.
“Kwanza niulize, umeridhia?” “Naona hakuna jinsi! Ila nimejawa hofu Mill!” “Hofu hapana. Maana sitakutelekeza Pam. Ila naelewa wasiwasi wako. Na ujue hiki ninachokifanya ni kwa manufaa yetu sisi wote wanne, mpaka huyo mtoto tumboni, kama familia.” Akaendelea taratibu, kama anayepasua jipu.
“Ile nyumba tumenunua ni jengo tu. Karibu sana watataka tuandikishe umeme kwa akaunti yenye maji yetu sisi wenyewe. Aliyetuuzia nyumba atafunga mkataba wa hivyo vitu muda si mrefu, kama bado. Hakuwezi kukabakia pale giza na pakame. Lakini nikienda mimi, tukafungua hivyo vyote kwa majina yetu mawili, na kuanza kulipia bills zetu za pale kwenye ile nyumba, itaonyesha sio usanii.”
“Pili, nimeshawekana sawa na Jo, nataka nikafungue kampuni ya nursing home, kwa majina yetu na Jo atakuwa mmoja wa washiriki kwenye bodi ya kampuni yetu na kuna madaktari alionipa na amesema alishawagusia. Lakini sasa itabidi niende nikakutane nao, nizungumze nao mimi mwenyewe kabla sijaendelea na chochote.”
“Kuna mambo ya kisheria nilazima mimi mwenyewe niwepo, kuweka saini na kuingia mkataba na watu huko. Nifungue ofisi kabisa na kuweka mambo sawa. Siwezi nikakamilisha kama nipo hapa.” “Ndio kwa muda gani?”
“Nitajitahidi tusikae sana.” “Mill! Mbona kama unajua ila hutaki kuniambia?” “Hutajifungua mimi nisiwepo Pam. Na sitakukimbia. Jua ni garama unayotakiwa kulipa kwa ajili ya watoto wetu, na mimi najiambia hivyohivyo. Napambana kwa ajili yenu. Tusaidiane tuweke hii familia pamoja, tena sehemu nzuri.” Hapo akawa amemfanya ajisikie anahusika, kuwa analo jukumu na yeye lakufanya.
“Sijui kama unanielewa?” “Naelewa.” “Haya maisha hapa ni mazuri na yanapumzisha sana. Sana tu. Kuingia hivi, na kutoka, rahisi sana. Lakini kwa jinsi ninavyokuona wewe, juhudi zako, na ni mke usiye na makuu, tunaweza tengeneza pesa hiyo! Watoto wetu wasiwahi pata shida. Tulipe tu garama kwa sasa, nikiamini itatulipa baadaye.”
“Na ujue kabisa, hata mimi sifurahii kuondoka na kukuacha, Pam. Natamani kama tungeweza tukaondoka wote, hili jambo liishe. Lakini haitakuwa rahisi. Hii ndio njia pekee ya kuwafunga wa Marekani mpaka watoe Visa yako.” Wakaendelea kuzungumza wakijipanga, mpaka Pam akaridhia kumtoa Shema. Kwamba safari hii Mill anaondoka na mpaka aliyemkuta naye! Alijawa na hofu ya kupotea kwake na mwanae, kama mara ya mwisho, lakini hakuwa na jinsi.
Lakini safari hii ataachwa pazuri. Nyumba nzuri na magari. Hatahangaika tena. Kampuni ya hapo nchini, ilikuwa kwa jina lake. Na Mill alihakikisha anafahamu kila kitu kinachoendelea kwenye hiyo kampuni akijua ipo siku atamuacha aiendeshe bila yeye.
~~~~~~~~~~~
Inaendelea…
0 Comments:
Post a Comment